2.1.1 Kabla ya Ukoloni
|
|
- Claude McBride
- 5 years ago
- Views:
Transcription
1 2.1 Historia ya Tamthiliya ya Kiswahili Ukilinganishwa na tanzu nyingine za fasihi ya Kiswahili, utanzu wa tamthiliya ndio mchanga zaidi. Hata hivyo, chimbuko lake kwa upande wa sanaa-tendaji ni la kale mno. Chimbuko lake hasa ni katika fasihi simulizi ya Kiswahili katika mawasilianao ya moja kwa moja baina ya msimulizi wa ngano na hadhira, katika maigizo mbalimbali ya msimulizi wa ngano, katika ushirikiano wa moja kwa moja baina ya msimulizi na hadhira yake, katika majibizano ya kishairi yanayotokea katika hafla mbalimbali, katika nyimbo na ngoma za watoto na watu wazima, katika michezo ya sarakasi na kadhalika. Kwa hiyo, historia na maendeleo ya tamthiliya nchini Tanzania inaweza kuelezwa kwa kurejelea vipindi vitatu muhimu: Kabla ya Ukoloni, Kipindi cha Ukoloni na Kipindi cha Uhuru Kabla ya Ukoloni Tamthiliya zilizoandikwa ili ziigizwe jukwaani hazikuwepo kabla ya ukoloni. Mchezo wa kuigiza ulioandikwa ulikuja na wakoloni (Bertoncini, 1989). Aina za sanaa za maonyesho zilizokuwepo zilitofautiana na tamthiliya hii iliyoingizwa na tamaduni ngeni. Zilikuwepo tamthiliya zisizoandikwa, zilizogezwa au kufaraguzwa (improvised) kwa ajili ya kuonyeshwa kwenye shughuli maalumu, kwa mfano sherehe za jando na unyago, mazishi, kutawazwa kwa mtemi, arusi na michezo ya watoto. Tamthiliya hizo zilikuwa na sifa kadha za tamthiliya, yaani hadithi, vitendo, wahusika na waigizaji wao, na dialojia. Isitoshe, zilikuwa na sifa za Sanaa za Maonyesho kama vile: Dhana Inayotendeka, Uwanja Unaotendewa, Watendaji, Hadhira, Kusudio la Kisanaa, Muktadha wa Kisanaa na Ubunifu (Umithilishaji). Tamthiliya hizo hazikuwa na ploti ya ki-aristotle wala matini yaliyoandikwa. Hivyo hizi zilikuwa tamthiliya-simulizi Kipindi Cha Ukoloni ( ) Tamthiliya ilianza Tanzania wakati ukoloni ulipoingia hasa kuanzia miaka ya Ukoloni unahusu jamii mbili ambapo jamii moja yenye nguvu huitawala jamii nyingine. Katika hali kama hii, hutokea tamaduni mbili utamaduni unaokandamiza na ule unaokandamizwa. Katika kipindi hiki palikuwepo: Tamthiliya za Kizungu, Vichekesho na Tamthiliya ya Kiswahili. 1
2 Tamthiliya za Kizungu Tamthiliya za kizungu zilikusudiwa ama kuwaburudisha maofisa na walowezi (masetla) wa kizungu, au kufundisha Bibilia na imani ya Kikristo.Tamthiliya hizi ziliigizwa kuanzia miaka ya 1920, nyingi zilichezwa mashuleni. Shule ndio hasa zilitumika kuonyeshea tamthiliya zilizojaa ujumi, amali na itikadi ya Kibepari. Kwa sababu tamthiliya inahitaji kusomwa na kukaririwa kabla ya kuonyeshwa kwenye jukwaa, basi usomi ulikuwa kigezo kikubwa cha kufanikisha tamthiliya. Hali hii iliwafanya wala tu waliojua kusoma na kuandika Kiingereza waimudu fani hii. Hawa walipatikana shuleni tu ukiondoa wakoloni wenyewe. St. Joseph Convent School, hivi sasa Forodhani, ilianza kuonyesha tamthiliya za Kiingereza kuanzia Tamthiliya hizo ni kama vile The Sherrif s Kitchen, The Ugly Duckling ya Milne na The Birds of a Feather ya Francis. Nyingi katika tamthiliya hizi zilikuwa zile za wakati wa Victoria huko Uingereza ( ). Tamthiliya hizi zilijulikana kama Drawing Room Drama. Zilijishughulisha na masuala ya kinyumbani, yaani jinsi familia ya Kiingereza huishi, matazamio yake na mambo yafafanayo na hayo. Kwa kifupi, tamthiliya hizi zilitakiwa kuwa na ujumi-taaluma wa tamthiliya, yaani lugha na mtindo wa uonyeshaji uliotakiwa Uingereza wakati huo Four Wall-Bourgeois Theatre. Tamthiliya zote zilikuwa kwenye Kiingereza. Baadhi ya tamthiliya zilitokana na michezo iliyoandikwa na Waingereza, kwa mfano Shakespeare, na baadhi zilikuwa ni za dini ya Kikristo. Takriban tamthiliya zote za kipindi hiki zilikuwa ni za kibwanyenye, yaani zisizopingana na mfumo wa ubepari na ukoloni uliokuwepo. Tamthiliya chache mno zilitafsiriwa kwa Kiswahili, kwa mfano, tamthiliya ya Moliere, Le Medecin Malge Lui Tabibu Asiyependa Utabibu. Mbali na shule, zilianzishwa taasisi zingine zilizojishughulisha na tamthiliya. Hindu Volunteer Corps ambayo ilionyesha tamthiliya za Kihindi ilianzishwa mnamo Baadaye, vilianzishwa vikundi vya kuigiza tamthiliya za kizungu: Dar es Salaam players (Little Theatre, 1947) na Arusha Little Theatre, 1953 (Lihamba, 1985:38). Tamthiliya katika lugha ya Kiingereza ilizidi kushamiri baada ya kufanyika mkutano wa wakoloni wa Kiingereza huko Cambridge mwaka wa 1948 uliojulikana kama Cambridge Summer Conference. Mkutano huu uliongelea suala la kutumia maonyesho kama kipengengele kimoja cha kueneza utamaduni wa Kiingereza kwenye 2
3 makoloni. Kwa hiyo, matombola, brass bendi na tamthiliya vikatiliwa mkazo. Matokeo ya mkutano huu kwenye makoloni ikawa ni uanzishwaji wa mashindano ya tamthiliya shuleni. Mnamo mwaka wa 1957, Baraza la Kiingereza (British Council) lilianzisha mashindano ya uigizaji wa tamthiliya za Kiingereza nchini Tanzania, yaliyoitwa School Drama Competition. Tamthiliya zote zilibidi kuwa kwenye lugha fasaha ya Kiingereza. Mashindano hayo yaliendelea hadi 1963, yalipoanza kusimamiwa na Youth Drama Association. Kuanzia wakati huo, tamthliya za Kiswahili zilianza kuhusishwa katika mashindano hayo, na hivyo kuchochea utuzi wa tamthiliya katika lugha hiyo. Vichekesho Vichekesho 1 ni aina ya tamthiliya-gezwa (zilizotungwa papo kwa hapo bila kuandikwa). Zilianza miaka ya 1920 kwa lengo la kuburudisha wenyeji. Tamthiliya hizo kwa kawaida zilikuwa na vituko vya kuchekesha na ziliwasuta watu waliofikiriwa kuwa washamba, wajinga au wasiostaarabika. Tamthiliya hizo zilimwonyesha mhusika anayetoka shamba na kwenda kuzuzuka mjini. Vichekesho viliendelea hata baada ya uhuru (na bado vipo) ila dhamira zake zilibailika. Tamthiliya-Andishi ya Kiswahili Tangu 1920 mpaka 1960 mambo yaliyowakabili wakabili wanaotawaliwa (Waafrika) yalikuwa ardhi, ukabila na kujipatia uhuru. Hata hivyo, tamthiliya zilizoandikwa wakati huu na waafrika hazikujishughulisha na mambo haya matatu. Katika kipindi hiki, kabla ya kuchapishwa vitabu vyote, ilibidi vipitiwe kwenye Kamati ya Lugha ya Makoloni ya Afrika Mashariki. Hiki kilikuwa chombo cha mtawala cha kusimamia ukuzaji wa lugha ya Kiswahili. Kutokana na hali hii, maandishi yoyote yale ambayo ni kinyume na ukoloni hayangeweza kuchapishwa. Tamthiliya za wakati huu zilihusu mambo ambayo kwa kiasi fulani yalisababishwa na tabaka tawala lakini hayakuchambuliwa kwa kina 1 Katika Muktadha huu dhana hii imetumiwa kwa maana ya Pop-Comedy yaani komedia pendwa au futuhi pendwa. 3
4 kuweza kutoa mwanga wa kuyatatua. Tamthiliya hizi zililenga kwenye masuala yanayohusu rushwa, mapenzi, ukabila na migongano ya utamaduni. Iwapo tamthiliya hizi zingegusia uondoaji wa ukabila, basi zingeweza kuchangia kuleta umoja ambao ungetumika kunyakua ardhi ambayo ilikuwa imechukuwa na mkoloni na hatimaye kuleta vuguvugu la kumtoa kabisa mkoloni. Tamthiliya za kiswahili zilizoandikwa kwanza kabla ya kuigizwa jukwaani zimeanza kutokea miaka ya Tamthiliya za mwanzo zilikuwa za kidini km. Imekwisha (Frank, C The Highway Press, Nairobi). Tamthiliya nyingi za kidini ziliandikwa na kuigizwa tu shuleni na makanisani, lakini hazikuchapishwa vitabu. Tamthiliya za mwanzo zisizokuwa za kidini zilianza kutungwa kati ya 1952 na Shughuli za tamthiliya wakati huo wa Hali ya Hatari 2 zilisimamiwa na Graham Hyslop, mwingereza aliyekuwa katika utumishi wa serikali ya kikoloni Kenya. Hyslop alianzisha kikundi cha maigizo kwa ajili ya askari mwaka wa 1944, na miaka ya 1950 alianza kutunga michezo ambayo iliigizwa na kikundi chake. Michezo yake ya kwanza katika Kiswahili ni Afadhali Mchawi (EALB, 1957) na Mgeni Karibu (EALB, 1957). Michezo hiyo iliigizwa kati ya 1954 na Tamthiliya ya Afadhali Mchawi (Hyslop, 1957) iligusia mgogoro unaoletwa na mahari, mila na umamboleo. Baadaye Hyslop alianza kuzunguka katika shule na vyuo mbalimbali nchini Kenya akifundisha muziki na uigizaji. Miongoni mwa wanafunzi wa mwanzo wa Hyslop waliokuwa wakisoma Alliance High School ni Henry Kuria, Kimani Nyoike, Gerishom Ngugi na B.M. Kurutu. Tamthiliya ya Kuria, Nakupenda Lakini (EALB, 1957) iliigizwa kwa mara ya kwanza mwaka Tamthiliya ya Nyoike, Maisha ni Nini? iliigizwa mwaka Tamthiliya ya Gerishon Ngugi, Nimelogwa Nisiwe na Mpenzi (EALB, 1961) iliigizwa mwaka 1956 na ya Kurutu, Atakiwa na Polisi mwaka Kwa jumla, hadi tulipopata uhuru, tamthiliya zote za Kiswahili zilizochapishwa zilikuwa zimeandikwa na Wakenya. Watanzania hawakujitokeza katika uwanja huu hadi baada ya uhuru Kipindi cha Uhuru Tanzania kuwa jamhuri mwaka wa 1962 kuliashiria mambo mapya kwenye tamthiliya. Kwanza usomi ulipiga hatua kutokana na siasa 2 Wakati wa vita vya Mau Mau nchini Kenya. 4
5 mpya ya wananchi kujitawala wenyewe. Chuo Kikuu cha kwanza nchini kilianzishwa Serikali pia ilianzisha Wizara ya Utamaduni wa Taifa mwaka wa Katika kipindi hiki cha uhuru palikuwepo: Tamthiliya za Kizungu, Vichekesho na Tamthiliya ya Kiswahili. Tamthiliya ya Kizungu Tamthiliya ya kizungu iliendelea kuigizwa hata baada ya uhuru, hasa mashuleni na katika kumbi maalumu za maonyesho kama Little Theatres. Hata hivyo, umaarufu wake ulipungua kiasi, hususan upande wa Tanzania. Baadhi ya tamtiliya muhimu za kizungu zilianza kutafsiriwa na kuigizwa kwa lugha ya Kiswahili ili zieleweke zaidi na wananchi km. tafsiri za J.K. Nyerere za Shakespeare, Juliasi Kaisari (OUP, 1964) na Mabepari wa Venisi (OUP, 1969); tafsiri za S.S. Mushi za michezo ya Shakespeare ya Makbeth (TPH, 1968) na Tufani (TPH, 1969); Moliere, Mchuuzi Muungwana (A. Morrison, EALB 1961) na Mnafiki (L. Taguaba, TPH 1973); Sophocles, Mfalme Edipode (S.S. Mushi OUP, 1971); Gogol, Mkaguzi Mkuu wa Serikali (C. Mwakasaka, HEB 1979), nk. Licha ya tamthiliya za kizungu, kadhalika tamthiliya za Kiafrika zilizoandikwa kwa lugha za kigeni na lugha nyingine za kiafrika, zilifasiriwa kwa Kiswahili km. Mtawa Mweusi (Ngugi wa Thiong o, HEB, 1978); Soyinka W. Masaibu ya Ndugu Jero (Mf. A.S. Yahya OUP 1974); O. Ijimere, Kifungo cha Obatala (HEB, 1978); Ngugi wa Thing o na Ngugi Mirii, Nitaolewa Nikipenda (HEB, 1982); M. Mulokozi (1968), The Tragedy of Mkwawa (Mf. Kahingi, 1970). Vichekesho Baada ya uhuru vichekesho vilichua sura tofauti kidogo. Badala ya kuwasuta washamba vilianza kuwasuta wazungu weusi, yaani waafrika wanaoringia elimu au vyeo na kudharau utamaduni wao (Darlite 2/2: ). Vipengele kama matendo, maonyesho na maongezi vilitumiwa katika uundaji wa vichekesho hivi. Baadhi ya vichekesho, hasa vinavyoonyeshwa kwenye mabaa na sehemu nyingine za burudani na starehe, hujaribu kuzungumzia matatizo ya watu wa kawaida, km. matatizo ya familia, ukosefu wa kazi, ukimwi, uhalifu, udanganyifu wa waganga wa jadi, nk. Vipo pia vichekesho vya kisiasa vyenye kuzungumzia kadhia za kisiasa, ubinafsi wa viongozi, matatizo yanayokumba watu vijijini, mijini, nk. 5
6 Baadhi ya vichekesho vya redio Tanzania, km. Mahoka (kipindi kilichoanza mwaka 1974) na Pwagu na Pwaguzi (kilianza mwaka 1978), hukejeli na kukemea tabia mbovu za baadhi ya watu, wakiwemo viongozi wa kiasa. Siku hizi vichekesho hutangazwa na vituo vya redio na televisheni, na huonyeshwa mijini kwenye kumbi za starehe. Tamthiliya-Andishi ya Kiswahili Baada ya uhuru utunzi wa tamthiliya ulipamba moto zaidi, hasa upande wa Tanzania. Uhuru uliwafanya waandishi wa tamthiliya kuandika mambo ambayo wasingeweza kuyaandika hapo awali. Waandishi walitumia tamthiliya kuelezea matatizo yanayokabili jamii. Mashindano ya utunzi na uigizaji yaliyoendeshwa na Youth Drama Association nchini Tanzania yaliwawezesha watunzi chipukizi kujitokeza, akiwemo Ebrahim Hussein ambaye tamthiliya yake ya kwanza, Wakati Ukuta (EAPH,1969) ilishinda tuzo katika mashindano hayo. Wengine walikuwa Uhinga na Katalambula ambao walitunga tamthiliya za Kiswahili zilizoonyesha maadili katika jamii. Wakati huo pia ndipo walipoanza kutokea watunzi waliohitimu fani ya sanaa za maonyesho katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam km. E. Hussein, P. Muhando, N. Ngahyoma na G. Uhinga. Kwa mujibu wa Mulama (1983) watunzi walianza kuifungamanisha tamthiya na mahitaji ya nchi ya Tanzania. Uzukaji wa tamthiliya ukaambatana na hali maalumu za kiuchumi na kijamii. 6
NAFASI YA MUZIKI ULIOPENDWA KATIKA FASIID YA KISWAHILI PAMELA M. Y NGUGI. Inkisiri. M a kala. AAP 64 (2000): Swahili Forum VII
AAP 64 (2000): Swahili Forum VII 145-152 NAFASI YA MUZIKI ULIOPENDWA KATIKA FASIID YA KISWAHILI PAMELA M. Y NGUGI Inkisiri Nyimbo, kama tanzu ya fasihi yeyote ile zina majukumu mbalimbali ambayo hutekeleza
More informationInformation for assessors (do not distribute this page to participants):
R&P Cultural Orientation Model Assessment Written Version Swahili Information for assessors (do not distribute this page to participants): This written version of the Model Cultural Orientation (CO) Assessment
More informationKUMBUKIZI YA MAREHEMU MWALIMU EDWIN SEMZABA
SWAHILI FORUM 23 (2016): 144-153 KUMBUKIZI YA MAREHEMU MWALIMU EDWIN SEMZABA ELIZABETH MAHENGE & EMMANUEL MBOGO Wasifu wa Marehemu hadi kufika chuoni Mwalimu Edwin Charles Semzaba alizaliwa Muheza tarehe
More informationUtumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania
Nordic Journal of African Studies 16(1): 18 29 (2007) Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania ABSTRACT This paper has attempted
More informationHuman Rights Are Universal And Yet...
Human Rights Are Universal And Yet... Episode 05 Title : The right to education Author : Julien Adayé Editor : Aude Gensbittel Translator : Anne Thomas, Eric Ponda Proofreader: Pendo Paul Characters (sounds,
More informationK. M a r k s, F. E n g e l s
W a (any a kazi wa nchi zote, unganeni! K. M a r k s, F. E n g e l s Maelezo ya chama cha kikomunist Idara ya Maendcleo Moscow Tafsiri hii ya "Maelezo ya Chama cha Kikomunist" inatokana na maandishi
More informationLUGHA YA KISWAHILI KATIKA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA ELIMU SHULE ZA SEKONDARI
LUGHA YA KISWAHILI KATIKA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA ELIMU SHULE ZA SEKONDARI SIKOMBE YIZUKANJI YORADI TASNIFU YA KISWAHILI KWA MINAJILI YA KUTUNUKIWA SHAHADA YA UZAMILI (MA. KISWAHILI) KITIVO CHA SANAA
More informationHati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)
102/3 KISWAHILI KARATASI YA 3 Fasihi Julai/Agosti 2013 MUDA : SAA 2 ½ Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E) Kiswahili Karatasi 3 Julai/ Agosti Muda: Saa 2 ½ MAAGIZO: Andika jina lako na nambari yako
More informationElimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani
Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani HakiElimu: Mfululizo wa Mada za Uchambuzi Namba. 2003.4S Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere 1 Rakesh
More informationHALIYA VITABUVYA WATOTOKATIKA TANZANIA
AAP 68 (2001)- Swahi1i Fomm Vill 171-183 HALIYA VITABUVYA WATOTOKATIKA TANZANIA J S. MADUMULLA Whither is fled the visionary gleam Where is it now, the glory and the dream Wapi kimekimbilia, kianga cha
More informationUFASIHI SIMULIZI KATIKA RIWAYA ZA SHAABAN ROBERT: Mifano kutoka Adili na Nduguze na Wasifu wa Siti Binti Saad. Khatib Khamis Saleh
UFASIHI SIMULIZI KATIKA RIWAYA ZA SHAABAN ROBERT: Mifano kutoka Adili na Nduguze na Wasifu wa Siti Binti Saad Khatib Khamis Saleh Tasinifu ya Uzamili Katika Kiswahili Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Septemba,
More informationElimukombozi, Lugha na Upashanaji Habari nchini Tanzania, katika Muktadha wa Utandawazi
Elimukombozi, Lugha na Upashanaji Habari nchini Tanzania, katika Muktadha wa Utandawazi Martha Qorro 1 1.0 Utangulizi Elimu ni suala la jamii ambalo mipango na taratibu zake zinahitaji kushirikisha wadau
More informationGOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)
GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER (Made under Section 23) THE ELECTRICITY (STANDARDIZED SMALL POWER PROJECTS TARIFF) ORDER, 2016 citation 1. This Order may be cited
More informationHISTORIA, MAENDELEO NA MABADILIKO YA KATIBA TANZANIA TANGU UHURU HADI MIAKA HAMSINI YA UHURU 9 DESEMBA 2011.
Saint Augustine University of Tanzania From the SelectedWorks of Daudi Mwita Nyamaka Mr. Winter December 9, 2011 HISTORIA, MAENDELEO NA MABADILIKO YA KATIBA TANZANIA TANGU UHURU HADI MIAKA HAMSINI YA UHURU
More informationHati ya Kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya.( K.C.S.E)
102/3 KISWAHILI FASIHI KARATASI YA 3 JULAI/AGOSTI 2011 MUDA: 2 ½ Kiswahili Fasihi Hati ya Kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya.( K.C.S.E) MAAGIZO Jibu maswali manne pekee Swali la kwanza ni lazima Maswali
More informationKUSHUKA KWA HADHI YA LUGHA ZA JAMII NCHINI TANZANIA YOHANA P. MSANJILA University of Dar es Salaam, Tanzania
Nordic Journal of African Studies 12(3): 296 309 (2003) KUSHUKA KWA HADHI YA LUGHA ZA JAMII NCHINI TANZANIA YOHANA P. MSANJILA University of Dar es Salaam, Tanzania ABSTRACT Lugha za jamii hapa nchini
More informationUHUSIANO WA MIKAKATI YA UFUNDISHAJI WA FASIHI YA WATOTO YA KISWAHILI NA UMILISI WA KUSOMA KATIKA SHULE ZA MSINGI, KASARANI, KAUNTI YA NAIROBI, KENYA
UHUSIANO WA MIKAKATI YA UFUNDISHAJI WA FASIHI YA WATOTO YA KISWAHILI NA UMILISI WA KUSOMA KATIKA SHULE ZA MSINGI, KASARANI, KAUNTI YA NAIROBI, KENYA NA SELINA RHOBI CHACHA E55/23475/11 TASNIFU HII IMEWASILISHWA
More informationKUCHUNGUZA UFASIHI SIMULIZI UNAOJITOKEZA NDANI YA HADITHI ZA KUSADIKIKA NA ADILI NA NDUGUZE
KUCHUNGUZA UFASIHI SIMULIZI UNAOJITOKEZA NDANI YA HADITHI ZA KUSADIKIKA NA ADILI NA NDUGUZE MUHAMMED ALI SALIM TASINIFU ILIYOWASILISHWA KWA AJILI YA KUTIMIZA SEHEMU YA MASHARTI YA KUTUNIKIWA SHAHADA YA
More informationMIONGOZO MIWILI KUPAA NA KUTUNGULIWA KWA AZIMIO LA ARUSHA
KIGODA CHA TAALUMA CHA MWALIMU NYERERE MIONGOZO MIWILI KUPAA NA KUTUNGULIWA KWA AZIMIO LA ARUSHA Yamekusanywa na kuhaririwa na: Bashiru Ally Saida Yahya-Othman Issa Shivji CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
More informationKUCHUNGUZA MASUALA YA KISIASA KATIKA RIWAYA ZA SHAABAN ROBERT: MFANO WA KUSADIKIKA NA KUFIKIRIKA
KUCHUNGUZA MASUALA YA KISIASA KATIKA RIWAYA ZA SHAABAN ROBERT: MFANO WA KUSADIKIKA NA KUFIKIRIKA BIBIANA MASSAWE AMBROSE TASINIFU ILIYOWASILISHWA KWA AJILI YA KUTIMIZA SHARTI PEKEE LA KUTUNUKIWA DIGRII
More informationMhashamu Askofu Jude Thaddaeus Ruwa ichi, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania; Mwadhama Policarp Kardinali Pengo,
HOTUBA YA MHESHIMIWA MIZENGO P. PINDA (MB), WAZIRI MKUU, KWENYE SHEREHE YA KUADHIMISHA MIAKA HAMSINI YA BARAZA LA MAASKOFU KATOLIKI TANZANIA, TAREHE 08 JUNI 2008, MSIMBAZI CENTRE, DAR ES SALAAM Mhashamu
More informationKiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika
Kiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika Stephen N. Kamau Abstract It is a fact that in the recent past, globalization has gradually taken shape in Africa and as such the continent has no choice but to
More informationKENYA NATIONAL EXAMINATION COUNCIL REVISION MOCK EXAMS 2016 TOP NATIONAL SCHOOLS
KENYA NATIONAL EXAMINATION COUNCIL REVISION MOCK EXAMS 2016 TOP NATIONAL SCHOOLS ALLIANCE BOYS HIGH SCHOOL KISWAHILI KARATASI YA 2 SCHOOLS NET KENYA Osiligi House, Opposite KCB, Ground Floor Off Magadi
More informationMAKALA: USHAIRI WA KISWAHILI KATIKA NJIA PANDA: KUTUMIA AU KUTOTUMIA METHALI
MAKALA: USHAIRI WA KISWAHILI KATIKA NJIA PANDA: KUTUMIA AU KUTOTUMIA METHALI Na Joseph Nyehita Maitaria Mwanafunzi wa Ph.D Idara ya Kiswahili na Lugha za Kiafrika Chuo Kikuu cha Kenyatta Ikisiri Makala
More informationUsimulizi wa Riwaya ya Nyongo Mkalia Ini E. S. MOHOCHI University of Egerton, Kenya
Nordic Journal of African Studies 9(2): 49-59 (2000) Usimulizi wa Riwaya ya Nyongo Mkalia Ini E. S. MOHOCHI University of Egerton, Kenya UTANGULIZI Tukichunguza hazina ya uhakiki uliofanywa katika taaluma
More informationUJAGINA WA MWANAMKE KATIKA PANGO
UJAGINA WA MWANAMKE KATIKA PANGO NA MUNIU GEORGE GITHUCI C50/65581/2011 TASNIFU HII IMETOLEWA ILI KUTOSHELEZA BAADHI YA MAHITAJI YA SHAHADA YA UZAMILI KATIKA CHUO KIKUU CHA NAIROBI IDARA YA KISWAHILI NOVEMBER
More informationMisamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?
Policy brief TZ.12/2010K Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada? 1. Utangulizi Kila mwaka Bunge la Tanzania hupitia na kuchanganua kwa makini bajeti ya Serikali.
More informationAzimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu
The Human Rights Centre Uganda Azimio la Mkutano Mkuu 53/144 (8 Machi 1999) Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu AZIMIO KUHUSU HAKI NA WAJIBU WA MTU BINAFSI, VIKUNDI NA JUMUIYA
More informationTANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora
K I T A B U C H A M B I N U B O R A C H A T O A U k u r a s a 1 TANZANIA OSAKA ALUMNI Kitabu cha Mbinu Bora Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa P.O. Box 1923, Dodoma. Novemba, 2012
More informationKimesanifiwa na:- E.D.Kissuu ECOMM TANZANIA S.L.P ,Dar es Salaam. Simu:
Kimesanifiwa na:- E.D.Kissuu ECOMM TANZANIA S.L.P. 21425,Dar es Salaam. Simu: +255 713 607 207 edkissuu@gmail.com Katuni zimechorwa na: Adam Lutta Babatau Inc. Box 13565 Dar es salaam, Simu:+255 713 474200
More informationUfanisi katika Ufundishaji kwenye Shule za Msingi na Sekondari nchini Tanzania
Ufanisi katika Ufundishaji kwenye Shule za Msingi na Sekondari nchini Tanzania Desemba 2014 1 Shukurani Ripoti hii iliandikwa na Dk. Mkumbo. Ushauri wa kitaalamu ulitolewa na Elizabeth Missokia na Godfrey
More informationGOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)
GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER (Made under Section 23) THE ELECTRICITY (STANDARDIZED SMALL POWER PROJECTS TARIFF) ORDER, 2015 Citation 1. This Order may be cited
More informationTAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF) KUHUSU HAKI ZA WATOTO KATIKA KATIBA MPYA
TAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF) KUHUSU HAKI ZA WATOTO KATIKA KATIBA MPYA Marekebisho ya 23 January 2013 YALIYOMO KURASA TAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF)... 0 KUHUSU HAKI ZA WATOTO... 0
More informationFANI KATIKA NYIMBO TEULE ZA ANASTACIA MUKABWA MBURU JAMES MUNGAI TASNIFU HII IMETOLEWA ILI KUTOSHELEZA BAADHI YA
FANI KATIKA NYIMBO TEULE ZA ANASTACIA MUKABWA MBURU JAMES MUNGAI TASNIFU HII IMETOLEWA ILI KUTOSHELEZA BAADHI YA MAHITAJI YA SHAHADA YA UZAMILI (M.A.) KATIKA IDARA YA KISWAHILI CHUO KIKUU CHA NAIROBI 2014
More informationMheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame M. Mbarawa (Mb.); Waheshimiwa Mawaziri na Wabunge wote mliohudhuria;
HOTUBA YA BALOZI MHANDISI JOHN W.H. KIJAZI, KATIBU MKUU KIONGOZI, WAKATI WA UFUNGUZI WA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAHANDISI KWA MWAKA 2017, UKUMBI WA JAKAYA KIKWETE, DODOMA, SEPTEMBA 7, 2017 Mheshimiwa Waziri
More informationJAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO MPANGO KAZI WA USHIRIKI WA MTOTO TANZANIA 2014-2019 JANUARI, 2014 Dibaji Kwa mujibu wa takwimu za Sensa ya Taifa ya Idadi
More informationNadharia za Uhakiki kama Mchakato wa Kutaalamisha Usomaji wa Fasihi
Journal of Linguistics and Language in Education Vol 8, Number 1 (2014): 37-48 Nadharia za Uhakiki kama Mchakato wa Kutaalamisha Usomaji wa Fasihi Richard M. Wafula * Ikisiri Utunzi na uhakiki wa fasihi
More informationMwongozo wa Utamaduni Toleo la Kwanza
Mwongozo wa Utamaduni Toleo la Kwanza Kubadilishana Tamaduni za Kijerumani na za Kitanzania Limeandaliwa na Anna Hoppenau, Johannes Hahn, Oliva Lyimo na Lisa Bendiek German-Tanzanian Partnership (DTP)
More informationRipoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara)
Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara) Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara) Hakimiliki Shirika la Kazi Duniani 2010 Toleo la kwanza 2010 Machapisho ya Ofisi
More informationRIPOTI YA KAMATI TEULE YA KUCHUNGUZA UPOTEVU WA NYARAKA ULIOTOKEA KATIKA TAASISI YA NYARAKA NA KUMBUKUMBU ZA TAIFA ZANZIBAR.
RIPOTI YA KAMATI TEULE YA KUCHUNGUZA UPOTEVU WA NYARAKA ULIOTOKEA KATIKA TAASISI YA NYARAKA NA KUMBUKUMBU ZA TAIFA ZANZIBAR. SEHEMU YA KWANZA 1.0 UTANGULIZI. Kamati Teule ya Kuchunguza Upotevu wa Nyaraka
More informationMWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI
MWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI 2012 MWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI 2012 Kitabu hiki kimetayarishwa na Shirika la Equality for Growth (EfG) Equality
More informationEvaluation of Contextual Teaching of Kiswahili Proverbs in Secondary Schools in Kenya
Evaluation of Contextual Teaching of Kiswahili Proverbs in Secondary Schools in Kenya Oduori T. Wamubi Prof. Simala, K. Inyani Profesa Mshiriki Masinde Muliro University of Science and Technology Prof.
More informationMbinu za Ujenzi wa Wahusika na Usawiri wa Sifa Zao: Uhakiki wa Riwaya ya Dunia Uwanja Wa Fujo ya E. Kezilahabi
38 MULIKA NA. 34 Mbinu za Ujenzi wa Wahusika na Usawiri wa Sifa Zao: Uhakiki wa Riwaya ya Dunia Uwanja Wa Fujo ya E. Kezilahabi Leonard Flavian Ilomo Ikisiri Kipengele cha wahusika ni muhimu katika kuunda
More informationUTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO
UTANGULIZI International Montessori Teachers College (IMTC), ni chuo kilichoanzishwa hapa nchini Tanzania mwaka 2012 na kinatoa kozi ya kimataifa ya ualimu wa watoto wadogo (yaani child care and nursery
More informationN09/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q
N09/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q 88092387 SWAHILI B HIGHER LEVEL PAPER 1 SOUAHÉLI B NIVEAU SUPÉRIEUR ÉPREUVE 1 SUAHILI B NIVEL SUPERIOR PRUEBA 1 Tuesday 3 November 2009 (morning) Mardi 3 novembre 2009 (matin)
More informationHOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA,KWA WANANCHI, 30 SEPTEMBA, 2001
HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA,KWA WANANCHI, 30 SEPTEMBA, 2001 Leo napenda nizungumze nanyi, kwa lugha nyepesi iwezekanavyo, juu ya mahusiano tunayowania
More informationUNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013
www.xtremepapers.com UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level *9257224991* SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013 Additional Materials: Answer Booklet/Paper
More informationNGUO MPYA ZA UKOLONI. Mikataba ya Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Umoja wa Ulaya na Afrika. Agosti 2017
TAARIFA Agosti 2017 NGUO MPYA ZA UKOLONI Mikataba ya Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Umoja wa Ulaya na Afrika Jumuiya ya Jamii ya 2007: Wajumbe wanaadhamana Nairobi dhidi ya EPAs. SwissInfo Tangu mwaka
More informationForum:MyElimu Home for Students to Share Knowledge Thread: Dunia Uwanja Wa Fujo
Forum:MyElimu Home for Students to Share Knowledge Thread: Dunia Uwanja Wa Fujo MwlMaeda - June 10, 2017, 9:19 am Dunia uwanja wa fujo ni riwaya iliyoandikwa na Euphrase Kezilahabi mwaka wa 1975. Ni riwaya
More informationHaja Ya Dini. Author(s): Publisher(s): Translator(s): Category: Topic Tags: Featured Category: Published on Al-Islam.org (
Published on Al-Islam.org (https://www.al-islam.org) Home > Haja Ya Dini Haja Ya Dini Author(s): Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi [3] Publisher(s): Bilal Muslim Mission of Tanzania [4] Katika kijitabu
More informationKUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA
KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA KUWEZESHA Radio za kijamii Kutumia Tehama Mwongozo huu umeandaliwa ili kuvipa
More informationMATATIZO YA MATUMIZI YA LUGHA KATIKA VYOMBO VYA HABARI: MIFANO KUTOKA KENYA 1 KITULA KINGE'I. 1. Utangulizi. AAP 64 (2000): Swahili Forum VII 45-56
AAP 64 (2000): Swahili Forum VII 45-56 MATATIZO YA MATUMIZI YA LUGHA KATIKA VYOMBO VYA HABARI: MIFANO KUTOKA KENYA 1 KITULA KINGE'I 1. Utangulizi Mwandishi mawufu wa fasihi bwani Afiika, Chinua Achebe
More informationAzimio lililopitishwa na Mkutano Mkuu tarehe 18 Desemba 2013 [juu ya taarifa ya Kamati ya Tatu (A/68/456/Add.2)]
This unofficial translation is provided by the International Service for Human Rights Umoja wa Mataifa A/AZI/68/ Ugaw Jumla Mkutano Mkuu 30 Januari 2014 Kikao cha Sitini na Nane Dondoo ya Ajenda 69(b)
More informationSautiElimu. Sauti Yako Isikike
SautiElimu Sauti Yako Isikike SautiElimu Sauti Yako Isikike Mtayarishaji : Godfrey Telli Mchangiaji : Robert Mihayo Mhariri : Rakesh Rajani Shukrani za dhati kwa timu ya waandaaji wa SautiElimu 1-10: Lilian
More informationJAZANDA YA NJOZI KATIKA BAADHI YA MASHAIRI YA EUPHRASE KEZILAHABI (ONEIRIC IMAGES IN EUPHRASE KEZILAHABI S SELECTED POEMS) 1
SWAHILI FORUM 11 (2004): 69-73 JAZANDA YA NJOZI KATIKA BAADHI YA MASHAIRI YA EUPHRASE KEZILAHABI (ONEIRIC IMAGES IN EUPHRASE KEZILAHABI S SELECTED POEMS) 1 GRAZIELLA ACQUAVIVA This article is based upon
More informationDHANA NA MATKTIZO YA TAFSIRI:
BCStf GFBMAEA COLLECT!*# DHANA NA MATKTIZO YA TAFSIRI: TATHMINI YA RISASI ZIANZAPO KUCHANUA. OMONDI L F. O S A N O Tasnifu hii imetolewa ili kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya M.A. katika Chuo
More informationTora UTANGULIZI KWA TORA SOMO LA KWANZA
SOMO LA KWANZA UTANGULIZI KWA TORA For videos, study guides and other resources, visit Third Millennium Ministries at thirdmill.org. 2014 nathird Millennium Ministries Haki zote zimehifadhiwa. Hakuna sehemu
More informationMAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI
MAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI MAKUBALIANO YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI Paris, 20 Oktoba 2005 Kongamano Kuu la Umoja wa Mataifa linalohusisha
More informationElimu Ina Umuhimu gani katika Jamii? Kuelekea Elimu Sahihi
Elimu Ina Umuhimu gani katika Jamii? Kuelekea Elimu Sahihi Gervas Zombwe 1 1. Utangulizi Katika mazingira ya kawaida kabisa ndani ya jamii yetu, Imezoeleka kusikia au kuona watu wakioanisha dhana ya elimu
More informationATHARI ZA KIISIMU ZA LAHAJA YA KIMAKUNDUCHI KATIKAKISWAHILI SANIFU KINACHOTUMIKA SHULENI MAKUNDUCHI ZANZIBAR
ATHARI ZA KIISIMU ZA LAHAJA YA KIMAKUNDUCHI KATIKAKISWAHILI SANIFU KINACHOTUMIKA SHULENI MAKUNDUCHI ZANZIBAR SALEH ABDELSALAM MOHAMMED SALEH TASINIFU ILIYOWASILISHWA KWA AJILI YA KUKAMILISHA MASHARTI YA
More informationKuchanganya Maarifa Ya Kimila Na Ya Kisayansi Kwa Mwamko Wa Mazingira
Mradi wa Usimamizi wa Rufiji. Usimamizi wa na Uhifadhi wa Viumbe hai Anuai kwenye Misitu, Maeneo ya Miti, na Ardhi Owevu ya Delta na Uwanda wa Mafuriko wa Rufiji 1. Kuchanganya Maarifa Ya Kimila Na Ya
More informationHOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE
HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE. JENISTA MHAGAMA (MB), KATIKA KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA AFYA NA USALAMA MAHALI PA KAZI DUNIANI DODOMA, 28 APRILI
More informationNAFASI YA MWANAMKE: JINSI INAVYOTETEWA KATIKA NYIMBO ZA TAARAB ZA ZANZIBAR ELIZABETH KANGOGO YEGO C50/68796/2011 IDARA YA ISIMU NA LUGHA
NAFASI YA MWANAMKE: JINSI INAVYOTETEWA KATIKA NYIMBO ZA TAARAB ZA ZANZIBAR ELIZABETH KANGOGO YEGO C50/68796/2011 IDARA YA ISIMU NA LUGHA CHUO KIKUU CHA NAIROBI TASNIFU HII IMETOLEWA ILI KUTOSHELEZA BAADHI
More informationJAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA III VI
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA III VI JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA
More informationATHARI ZA KIMOFOFONOLOJIA ZA KIOLUSUBA KATIKA MATUMIZI YA KISWAHILI SANIFU KAMA LUGHA YA PILI
ATHARI ZA KIMOFOFONOLOJIA ZA KIOLUSUBA KATIKA MATUMIZI YA KISWAHILI SANIFU KAMA LUGHA YA PILI MEROLYNE ACHIENG OTIENDE Tasnifu hii imewasilishwa kwa ajili ya kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya
More informationTASFIDA KAMA MKAKATI WA UPOLE: UWIANO WA TASFIDA ZA KISWAHILI NA EKEGUSII
TASFIDA KAMA MKAKATI WA UPOLE: UWIANO WA TASFIDA ZA KISWAHILI NA EKEGUSII NA FLORAH N. OMOSA C50/84117/2012 TASNIFU HII IMETOLEWA KWA MADHUMUNI YA KUTOSHELEZA BAADHI YA MAHITAJIYA SHAHADA YA UZAMILI KATIKA
More informationMukhtasari Wa Mabishano Kwa Na Dhidi Ya Vikombe Vingi Vya Ushirika
Mukhtasari Wa Mabishano Kwa Na Dhidi Ya Vikombe Vingi Vya Ushirika (A Summary Of Arguments For And Against Individual Communion Cups) Na J D Logan Communion Cups) 1 Mukhtasari Wa Mabishano Kwa Na Dhidi
More informationKocha Mkuu. mabingwa. itakuwa INASTAHILI. Ili Kutoa mafunzo kwa wanafunzi wako kuwa. itakuwa ya kuumiza. Itachukua muda. Itahitaji moyo wa kujitoa.
Ili Kutoa mafunzo kwa wanafunzi wako kuwa mabingwa itakuwa ya kuumiza. Itachukua muda. Itahitaji moyo wa kujitoa. Mkuu Inahitaji dhabihu. Unahitaji kujisukuma hadi mwisho wako. Lakini nakupa ahadi hii,
More informationNa Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake Toleola4
;II. -~ ~.! ~ l Na Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake Toleola4 ~n.~ SURA YA KWANZA SHERIA YA ARDHI 1 UTANGULIZI Sura hii itaiangalia ARDHI na umuhimu wake katika maisha ya binadamu. Ardhi ni rasilimali
More informationCHUO KIKUU CHA NAIROBI IDARA YA KISWAHILI MAMLAKA NA ITIKADI KATIKA NYIMBO TEULE ZA TAARAB
CHUO KIKUU CHA NAIROBI IDARA YA KISWAHILI MAMLAKA NA ITIKADI KATIKA NYIMBO TEULE ZA TAARAB TASNIFU HII IMETOLEWA ILI KUTOSHELEZA BAADHI YA MAHITAJI YA SHAHADA YA UZAMILI KATIKA CHUO KIKUU CHA NAIROBI NOVEMBA
More informationKufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007
Kufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007 1. Utangulizi Changamoto kuu iliyopo kuhusiana na Elimu ya msingi nchini Tanzania kwa sasa ni namna
More informationKAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI TANZANIA
KAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI TANZANIA KAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI TANZANIA NI UFUMBUZI KATIKA KUSHIRIKISHA JAMII? NI UFUMBUZI KATIKA KUSHIRIKISHA JAMII? Februari, 2013 Februari, 2013 SHUKURANI
More informationKutetea Haki za Binadamu
Kutetea Haki za Binadamu Kitabu cha Marejeo kwa watetezi wa Haki za Binadamu Toleo la pili i Kutetea Haki za Binadamu: Kitabu cha Marejeo kwa watetezi wa Haki za Binadamu (Toleo la pili) 2012 East and
More informationUKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA)
Empowered lives. Resilient nations. UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA) Kenya Miradi ya Equator Wanafijiji na Maendeleo Himili ya Jamii MIRADI YA UNDP EQUATOR Kote duniani, jamiii zinazidi kubuni
More informationSANIFU KWA SHULE ZA SEKONDARI KITABU CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO
KISWAHILI SANIFU KWA SHULE ZA SEKONDARI KITABU CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO KITABU CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO YALIYOMO UTANGULIZI v MPANGILIO WA MASOMO YA KISWAHILI: KIDATO CHA TANO 1 FUNZO: Fasihi (Ukurasa
More informationApril 14, 2016 COUNTY ASSEMBLY DEBATES 52
MOMBASA COUNTY ASSEMBLY HANSARD REPORT Thursday, 14 th April, 2016 The House met at 2.48pm. (Hon. Deputy Speaker (Mr. Mswabah Rashid) in the Chair) PRAYERS Hon. Deputy Speaker (Mr. Mswabah Rashid): Kindly
More informationMARUDIO K.C.S.E KNEC KISWAHILI KARATASI 102/2 MASWALI NA USAHIHISHO
102 1B KISWAHILI KARATASI 1B OCT/ NOV 1995 2 ½ HOURS Jibu maswali yote MARUDIO K.C.S.E KNEC 1995 2010 KISWAHILI KARATASI 102/2 MASWALI NA USAHIHISHO 1. UFAHAMU Soma Makala yatuatayo kisha ujibu maswali
More informationWaandishi: wa Toleo la 5. Scholastica Jullu Athanasia A. Soka Safina Hassan Mary Njau. Toleo la 5: 2008 ISBN
KIONGOZI CHA SHERIA Hakimiliki 2008 Kimetolewa na: Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC) Waandishi: wa Toleo la 5 Scholastica Jullu Athanasia A. Soka Safina Hassan Mary Njau Toleo la 5: 2008 ISBN
More informationKISWAHILI KARATASI YA 2 LUGHA
KISWAHILI KARATASI YA 2 LUGHA Maagizo (a) Andika jina lako na namba yako katika nafasi ulizoachiwa hapo juu. (b) Tia sahihi yako na tarehe ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu. (c) Jibu maswali
More informationJumuiya ya Waislamu Waahmadiyya Tanzania
na Hadhrat Mirza Ghulam Ahmad wa Qadian Masihi Mauʻudi na Imam Mahdi as Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya Tanzania HOTUBA YA SIALKOT Tafsiri ya Kiswahili ya: Lecture Sialkot (Urdu) Imeelezwa na: Hadhrat
More informationHatari, Haki za Usalama katika Bahari 03
Hatari, Haki za Usalama katika Bahari 03 AEG swahili Bahari ya Aegean Brosha ya maelezo hii ni kwa watu wanaofikiria kuvuka bahari ya Aegean kati ya Ugiriki na Uturuki.Kuvuka kihramu ni uhalifu katika
More informationTIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees
TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO Tel. +255748-537720/632013, P.O.BOX 6049 MOROGORO E-Mail info@ tist.org April 2004 Take care of your seedlings This year, thousands of seedlings have been planted in the TIST
More informationUNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level
UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level * 899145 4 672* SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2010 Additional Materials: Answer Booklet/Paper READ
More informationUfundishaji wa lugha nyingine
CHUO CHA ELIMU CHA KIMATAIFA OFISI YA ELIMU YA KIMATAIFA Ufundishaji wa lugha nyingine Na Elizabeth B. Bernhardt ELIMU MAZOEA KITABU NA. 20 1 Chuo cha Elimu cha Kimataifa (The International Academy of
More informationPronunciation: Mä-hret Zäläke Ndal-ka-tscho Molla Mare Gebre-gzabiär 1/12
Human Rights Are Universal And Yet... Episode 07 Title : The right to food drought and famine in Ethiopia Author : Tedla Getachew Editor : Aude Gensbittel, Pendo Paul Translator : Anne Thomas Proofreader:
More informationUtangulizi wa ugonjwa wa shinikizo la damu
Utangulizi wa ugonjwa wa shinikizo la damu BLOOD PRESSURE UK Shinikizo la damu ndicho chanzo kikubwa cha ulemavu na vifo vya mapema kule Uingereza, kupitia kiharusi, mshtuko wa moyo na maradhi ya moyo.
More informationMITAZAMO KUHUSU KISWAHILI MIONGONI MWA WAZUNGUMZAJI WA KIJALUO: KIFANI CHA SHULE ZA MSINGI KATIKA KAUNTI YA MIGORI. OWALA JAEL AKINYI C50/75493/2012
MITAZAMO KUHUSU KISWAHILI MIONGONI MWA WAZUNGUMZAJI WA KIJALUO: KIFANI CHA SHULE ZA MSINGI KATIKA KAUNTI YA MIGORI. OWALA JAEL AKINYI C50/75493/2012 TASNIFU HII IMEWASILISHWA KUTOSHELEZA BAADHI YA MAHITAJI
More informationKUCHUNGUZA UJINSIA NA MATUMIZI YA LUGHA KATIKA METHALI ZA WAKURYA
i KUCHUNGUZA UJINSIA NA MATUMIZI YA LUGHA KATIKA METHALI ZA WAKURYA TIMANYWA FELICIAN TASINIFU INAYOWAKILISHWA KWA AJILI YA KUTIMIZA SEHEMU YA SHARTI PEKEE LA KUTUNUKIWA SHAHADA YA UZAMILI (M.A. KISWAHILI)
More informationDeutsche Welle, Learning by Ear 2009 Seite 1 People Who Make A Difference Liberia: Anita Varney Health Facilitator, Fishtown/Liberia
Deutsche Welle, Learning by Ear 2009 Seite 1 Title: Anita Varney Health Facilitator, Fishtown/Liberia Author: Stefanie Duckstein, HA Afrika/ Nahost Editor: Christine Harjes Translator: Tony Dunham Sound
More informationKUCHUNGUZA DHAMIRA ZA NYIMBO ZA UGANGA KATIKA JAMII ZA WASWAHILI WILAYA YA MKOANI KUSINI PEMBA
KUCHUNGUZA DHAMIRA ZA NYIMBO ZA UGANGA KATIKA JAMII ZA WASWAHILI WILAYA YA MKOANI KUSINI PEMBA MUSSA YUSSUF ALI TASNIFU ILIYOWASILISHWA IKIWA NI SEHEMU YA MASHARTI YA KUPATIWA SHAHADA YA UZAMILI YA KISWAHILI
More informationUCHANGANUZI WA NOMINO-MKOPO ZA KIGIRYAMA KUTOKA KIINGEREZA NANCY JUMWA NGOWA
UCHANGANUZI WA NOMINO-MKOPO ZA KIGIRYAMA KUTOKA KIINGEREZA NANCY JUMWA NGOWA TASNIFU ILIYOWASILISHWA ILI KUTIMIZA MAHITAJI YA SHAHADA YA UZAMIFU YA CHUO KIKUU CHA PWANI. MEI, 2015 i UNGAMO Tasnifu hii
More informationWIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA 2007 i WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA
More informationMazoezi yaliyofanyika wakati wa warsha kuhusu Elimu-Jumuishi kwa Vitendo. Zanzibar, 7-10 Februari 2006
Mazoezi yaliyofanyika wakati wa warsha kuhusu Elimu-Jumuishi kwa Vitendo Zanzibar, 7-10 Februari 2006 Imechapishwa na: The Atlas Alliance Schweigaardsgt 12 SLP 9218 Grønland 0134 Oslo, Norway Simu: +47
More informationVijana wanazungumza kuhusu ujinsia, maisha na uhusiano VIJANA WANAZUNGUMZA KUHUSU NGONO, MAISHA NA UHUSIANO. Training and Research Support Centre
Shangazi Stella Vijana wanazungumza kuhusu ujinsia, maisha na uhusiano VIJANA WANAZUNGUMZA KUHUSU NGONO, MAISHA NA UHUSIANO Training and Research Support Centre Zimbabwe Shangazi Stella Kiongozi cha Mwezeshaji
More informationUpekee wa Utenzi wa Swifa ya Nguvumali: Utenzi wa Mpito, Mseto wa Imani za Jadi Na Usasa MWENDA MUKUTHURIA Egerton University, Kenya
Nordic Journal of African Studies 16(3): 298 319 (2007) Upekee wa Utenzi wa Swifa ya Nguvumali: Utenzi wa Mpito, Mseto wa Imani za Jadi Na Usasa MWENDA MUKUTHURIA Egerton University, Kenya ABSTRACT Nguvumali
More informationVITENDO USEMI NA ULINGANIFU WA MAANA KATIKA TAFSIRI: MIFANO KUTOKA TAFSIRI ZA KAZI MBILI TEULE ZA BARBARA KIMENYE
VITENDO USEMI NA ULINGANIFU WA MAANA KATIKA TAFSIRI: MIFANO KUTOKA TAFSIRI ZA KAZI MBILI TEULE ZA BARBARA KIMENYE NAHASHON AKUNGAH NYANGERI Tasnifu hii imetolewa madhumuni ya kutosheleza baadhi ya mahitaji
More informationKitabu Cha Mafunzo Ya Uongozi Kwa Wanawake
Uongozi Bora Kitabu Cha Mafunzo Ya Uongozi Kwa Wanawake UONGOZI BORA Uongozi ni uwezo wa kubuni na kuyaweka maono katika vitendo. -Mshiriki katika Semina ya Mafunzo Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya
More informationLBE 2009 Migration Episode 3: Living without documents
LBE 2009 Migration Episode 3: Living without documents Author: Marta Barroso Editor: Thomas Mösch Characters: Narrator 1: female Narrator 2: male Inserts (English): male, (42) Voice ( Passport, please!,
More informationMAP ISI YA KISW AHILI
AAP 42 (1995). 104-112 MAP ISI YA KISW AHILI ARMED SHEIKH NABHANY Resumee: Kiswahili, one among the Bantu languages, was formetly called Kingozi, the Waswahili (as they were called by the visiting Arabs)
More informationULINGANISHI WA KIISIMU KATI YA LAHAJA YA KIPEMBA NA KITUMBATU
ULINGANISHI WA KIISIMU KATI YA LAHAJA YA KIPEMBA NA KITUMBATU BAKARI K. BAKARI TASNIFU ILIYOWASILISHWA KWA AJILI YA KUTIMIZA SHARTI LA SHAHADA YA UMAHIRI YA KISWAHILI (M.A KISWAHILI) i UTHIBITISHO Aliyetia
More information