HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA,KWA WANANCHI, 30 SEPTEMBA, 2001
|
|
- George Newman
- 5 years ago
- Views:
Transcription
1 HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA,KWA WANANCHI, 30 SEPTEMBA, 2001 Leo napenda nizungumze nanyi, kwa lugha nyepesi iwezekanavyo, juu ya mahusiano tunayowania kuyarekebisha kati yetu, tukiwa miongoni mwa nchi maskini, na mataifa tajiri yenye viwanda. Mahusiano nitakayoyazungumzia leo si yale ya misaada. Maana, nikiwa Rais wenu nafedheheshwa sana kuona bajeti yetu ya taifa inategemea mno wahisani. Pamoja na jitihada zote za kuongeza makusanyo ya kodi, bado tunaweza kugharamia asilimia 58 tu ya bajeti yetu kutokana na mapato ya ndani. Kwa maneno mengine, kwa kila shilingi mia moja kwenye bajeti yetu ya sasa, ni shilingi 58 tu ndizo zetu; shilingi 42 kwa kila mia ni misaada na mikopo kutoka nje. Wahenga walituasa: Mtegemea cha ndugu hufa maskini. Kazi mliyonipa, Ndugu Wananchi, ni kuweka misingi ya kulitoa taifa letu katika aibu hii ya utegemezi uliokithiri, ili serikali za nje, au taasisi yoyote ya nje, ikituvunjia heshima ya utu wetu na uhuru wetu, tuweze kuwajibu bila wasiwasi kuwa: Msitubabaishe, hatuli kwenu! Ili tufikie lengo hilo, tunapaswa kukuza uwezo wetu wa kuendelea kwa kujitegemea kwa kuongeza uzalishaji wa bidhaa bora, kwa bei nafuu, na kuziuza ndani na nje ya nchi kwa gharama nafuu. Tutafanya hivyo pia kwa kutoa huduma bora zaidi, ikiwemo za utalii, fedha, bima, usafiri na mawasiliano, nazo kwa ufanisi na kwa bei nafuu. Hakuna njia nyingine ya mkato katika vita dhidi ya unyonge wa umaskini. Nasisitiza umuhimu wa ubora wa bidhaa na huduma, kwa gharama nafuu, kwa sababu katika dunia ya utandawazi shughuli zote hizo hufanyika katika mazingira ya ushindani mkubwa sana; ushindani wa ufanisi, ushindani wa ubora, na ushindani wa bei. Kilicho bora na nafuu huuzika kwa wepesi zaidi. Huu ni ukweli wa dunia ya leo na ijayo. Kuupuuza ukweli huo ni kujichimbia zaidi kwenye lindi la umaskini. Ushindani mkali katika biashara, uwekezaji na huduma ni sura moja tu kati ya sura nyingi za dunia ya utandawazi; dunia ambayo haiwezekani tena kujitenga nayo au kukwepa maingiliano na nchi nyingine. Sura nyingine, ambayo ni dhahiri, ni kuwa kwenye ushindani huo mwenye nguvu zaidi aghalabu ndiye hushinda. Ukweli huo unabadilika tu iwapo upo utaratibu wa kutoa upendeleo fulani kwa mnyonge, ili kumwezesha mnyonge huyo, kwa misaada halisi, naye ajenge uwezo wa ushindani wa haki. Kila nchi maskini ina wajibu wa kuwa na sera muafaka kwa maendeleo na kujenga mazingira ya kisera, kisheria, kiutawala na kiutekelezaji yatakayokuza uzalishaji, huduma na biashara. Lakini hiyo peke yake haitoshi. Bado katika maingiliano ya kibiashara na kiuchumi na nchi tajiri tunahitaji upendeleo, na misaada halisi ya kujenga uwezo wa uzalishaji na biashara katika uchumi wa soko na mazingira ya ushindani. Mimi binafsi, na serikali yenu kwa jumla, tumekuwa mstari wa mbele katika kujenga hoja hizo kwa niaba ya nchi yetu sisi wenyewe, na kwa niaba ya nchi zote maskini, nyingi zikiwa barani Afrika. Tumekuwa hodari wa kujenga na kutetea hoja hizi kiasi kwamba tunaalikwa huku na huko kufafanua mikakati tunayoiona inafaa ili kuleta ushindani wa haki, ushindani wenye utu, katika dunia ya leo na ijayo; ushindani unaohakikisha nchi maskini nazo zinafaidika kutokana na maingiliano ya kibiashara na
2 kiuchumi duniani, kwa namna ambayo bado tunakuwa na uchumi wa kitaifa, uchumi unaokua, uchumi unaoleta maendeleo ya wote na kupunguza umaskini. Mfumo wa maingiliano ya kiuchumi na kibiashara duniani ambao hatima yake ni kuongeza umaskini wa walio maskini, badala ya kupunguza pengo kati ya matajiri na maskini, ni mfumo ambao Tanzania imeupinga, na itaendelea kuupinga, kwa nguvu zake zote. Ni kwa msingi huo Tanzania iliteuliwa kuwa mratibu wa nchi maskini zenye uwakilishi mjini Geneva kwenye Shirika la Biashara Duniani, (WTO). Kwa wadhifa huo, tuliandaa Mkutano wa Mawaziri wa Biashara wa Nchi Maskini mjini Zanzibar, tarehe Julai mwaka huu. Nchi 45 kati ya 49 zilizoalikwa zilihudhuria mkutano huo, na kwa pamoja kupitisha Azimio la Zanzibar, pamoja na kukubaliana juu ya Ajenda ya Maendeleo na Malengo ya Majadiliano, kama maandalizi ya nchi maskini kwa ajili ya Mkutano wa Mawaziri wa Biashara Duniani utakaofanyika mjini Doha, nchini Qatar, mwezi Novemba mwaka huu. Kwa muda mrefu, nchi maskini zimejihisi kutosikilizwa vya kutosha katika majadiliano kuhusu mfumo wa biashara duniani, na ndio maana leo upo mfumo wenye madhara makubwa kwetu, mfumo ambao usipobadilishwa utatubakisha katika lindi la umaskini. Safari hii tunataka nchi tajiri zitusikilize vizuri zaidi, na kuzingatia hoja zetu, iwapo kweli wanaamini kuwa na sisi tunayo haki ya kunufaika na mfumo huo. Na kwa hili maneno yao hayatoshi; sasa tunataka vitendo. Maana, kama methali yetu isemavyo: Ada ya mja hunena, muungwana ni kitendo. Mojawapo ya mambo ambayo tunabishana sana na nchi tajiri ni juu ya umuhimu na uharaka wanaouona wao wa kuingiza mambo mapya kwenye makubaliano ya mfumo wa biashara duniani. Kimsingi sisi nchi maskini hatuoni mantiki ya kuongeza mambo mapya katika makubaliano yetu wakati ambapo yale tuliyokubaliana huko nyuma, hususan yale yenye maslahi kwa nchi maskini, bado hayajatekelezwa vya kutosha na nchi hizo tajiri. Aidha, nchi maskini zilitoa msimamo pale Zanzibar kuwa hazina uwezo wa kuingia kwenye majadiliano ya mambo mapya wakati ndio kwanza zinaanza kuelewa yale yaliyokubaliwa siku za nyuma. Hivyo, kwa maoni yetu, kinachohitajika hivi sasa si kukimbilia masuala na maeneo mapya, bali kusaidia nchi maskini kujenga uwezo wa kushiriki na kunufaika katika mfumo wa biashara uliopo duniani hivi sasa, kama wakubwa walivyotuahidi watafanya katika majadiliano na makubaliano ya awali. Mkutano wa Zanzibar, na mchango wa Tanzania, umesaidia kuelewesha wa nchi tajiri kuhusu hofu zetu za haki, na vipaumbele vyetu. Baada ya mkutano huo, Waziri wa Viwanda na Biashara wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alialikwa kwenye Mkutano wa Mashauriano wa Mawaziri wa Biashara kutoka nchi teule 18 duniani waliokutana Mexico tarehe 2 mwezi huu wa tisa. Tanzania ilialikwa kama mwakilishi wa nchi maskini, na kutokana na jukumu tulilochukua kuandaa mkutano wa Zanzibar. Itafanyika mikutano mingine ya maandalizi kabla ya mkutano wa Doha. Kote huko, Tanzania itakuwa mstari wa mbele kujenga hoja na kutetea maslahi ya nchi maskini kama yetu, ili hatimaye nasi tushiriki na kufaidika na mfumo wa biashara duniani, kwa manufaa ya wananchi wetu. Napenda muelewe kuwa kazi hii si nyepesi hata kidogo, maana tunataka kurekebisha mfumo ambao hivi sasa una manufaa kwa wakubwa, na wapiga kura wao.
3 Majadiliano haya yana sura ya uchumi, na yana sura ya kisiasa pia. Lakini ni kazi ambayo hatuna budi kuifanya. Bila hivyo nchi maskini kama yetu hazitainuka tena, hazitakuwa na uchumi wa kitaifa, hazitaendelea, na wala hazitashinda vita dhidi ya umaskini. Marekebisho haya ni kwa faida ya vizazi vijavyo vya nchi tajiri na nchi maskini. Maana, dunia ambayo siku hadi siku matajiri wanazidi kutajirika na maskini wanazidi kufukarika, daima haiwezi kutulia wala kuwa na amani. Pengine nitoe mifano ya jinsi ambavyo mfumo wa sasa unatukandamiza. Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo (UNCTAD) limethibitisha hivi karibuni kuwa sababu kubwa ya bara la Afrika kutofaidika na biashara duniani ni kwa vile asilimia 80 ya mauzo yetu nje yanatokana na mafuta yasiyosafishwa na bidhaa za kilimo na madini zisizosindikwa. Katika soko la dunia, wakubwa ndio hupanga bei watakayonunulia bidhaa zetu hizo zisizosindikwa; kisha ni wao pia wanaopanga bei watakayotuuzia sisi bidhaa za viwanda vyao. Matokeo yake leo unahitaji kuuza kahawa, pamba, au korosho nyingi zaidi, pengine hata mara mbili au tatu, kupata fedha za kutosha kuagizia trekta moja kuliko ilivyokuwa miaka 10 au 20 iliyopita. Kwa nchi kama yetu, ambapo kilimo ndicho uti wa mgongo wa uchumi, hakuna njia nyingine ya kukihusisha kilimo na maendeleo ya uchumi kwa ujumla ila kwa kuongeza uwezo wetu wa kusindika mazao ya kilimo ndani ya nchi. Tukifanya hivyo, kutakuwa na uhakika wa soko na bei ya mazao ya mkulima; viwanda vya mazao ya kilimo vitatoa ajira kwa wanachi, ambao mapato yao yatajenga uwezo wa kununua bidhaa za viwanda vingine, ambavyo navyo sasa vitaajiri zaidi; na tutauza nje bidhaa zilizoongezewa thamani. Ndugu zangu, ukinunua kikombe cha chai au kahawa kwenye nchi tajiri, sehemu ya bei unayolipa inayomfikia mkulima wa Tanzania ni ndogo mno; ni utani, kama si kebehi. Sehemu kubwa ya bei inatokana na uongezaji thamani wa bidhaa zetu ghafi katika viwanda vya nchi tajiri, ikiwemo mishahara minono kwa wafanyakazi wa nchi hizo. Nitoe mfano. Bei ya kikombe kimoja cha kahawa bora, kama tuzalishayo sisi Tanzania, kwenye mgahawa wenye hadhi katika nchi tajiri, ni wastani wa sh. 1,800/= (USD 2), yaani karibu mara mbili ya wastani wa mapato ya mkulima wa Tanzania kwa siku. Katika miaka 20 iliyopita, bei ya kahawa tunayouza nje imepungua kwa wastani wa asilimia 225; lakini bei ya kahawa ya unga (instant coffee) katika nchi zilizoendelea na zinazosindika kahawa yetu imeongezeka kwa asilimia 200!! Tunapigana na umaskini katika mfumo wa mahusiano ya kibiashara duniani ambao ndani yake upo utaratibu wa unyonyaji, kiasi kwamba unavyozidi kuzalisha ndivyo mapato yanavyopungua. Kama nchi tajiri wanataka na sisi tufaidike, ili tushinde umaskini, lazima pamoja na mambo mengine watusaidie, katika uchumi wa soko, kujenga uwezo wa kusindika mazao yetu, na kuyaongezea thamani ndani ya nchi zetu maskini. Hivi sasa bei anayolipwa mkulima wetu haina uhakika, lakini bei ya bidhaa wanazotuuzia wao zina uhakika. Wakulima wao wanahakikishiwa mapato yao na Serikali kwa njia ya ruzuku au fidia. Hivi sasa, kwa mwaka, nchi tajiri duniani hutumia dola za kimarekani zaidi ya bilioni 300 (sh.270 trilioni) kuwapa ruzuku wakulima wao, kiasi ambacho ni karibu sawa na pato la mataifa yote ya Afrika kusini mwa jangwa la Sahara. Lakini, kwa vile sisi Serikali zetu hazina uwezo wa kutoa fidia au ruzuku, wakulima wetu wanaachwa wategemee huruma ya wanunuzi wakubwa wa kimataifa. Tunaambiwa bei ya kahawa imeshuka duniani, lakini ukienda Ulaya bei ya kahawa dukani au kwenye mgahawa ni ile ile. Vivyo hivyo kwa korosho, nguo za pamba na kadhalika. Tunajadiliana na kujenga hoja ana kwa ana na nchi tajiri kuwa kama kweli zinaunga mkono vita vyetu dhidi ya umaskini, na kama zinataka na sisi tufaidike na
4 mfumo wa biashara duniani, lazima wasaidie kufidia hasara za wakulima wetu pale bei ya mazao yao inaposhuka ghafla kwenye soko la kimataifa. Lazima pia uwepo uwiano mzuri baina ya bei ya tunachouza sisi, na kile wanachotuuzia wao. Takwimu za Shirika la UNCTAD zinaonyesha kuwa uwiano huo ungekuwepo, katika miaka 20 iliyopita Afrika ingekuwa imeuza mara mbili ya thamani ya mauzo yetu katika biashara ya kimataifa hivi sasa, na kuongeza wastani wa kipato cha mwaka kwa kila Mwafrika kwa asilimia 50; yaani pale ambapo kipato hicho hivi sasa ni sh.200,000/=, kipato hicho kingekuwa sh.300,000/= kama uwiano wa bei za mauzo yetu na manunuzi yetu nje ungebakia kama ulivyokuwa mwaka Ni dhahiri basi kuwa kama kweli nchi tajiri zinataka tufanikiwe katika vita dhidi ya umaskini, lazima watusaidie tutendewe haki zaidi kwenye soko la kimataifa, na uwepo uwiano wa haki kati ya bei ya tunachouza sisi na bei ya wanachotuuzia wao. Mfumo unaofanya kile sisi tunachowauzia wao kiendelee kushuka bei, lakini kile wao wanachotuuzia sisi kiendelee kupanda bei, ni mfumo ambao hauwezi kutetewa, maana si wa haki hata kidogo, na kwa kweli ni wa unyonyaji. Kukosekana kwa uwiano huo kumesababisha nchi za Kiafrika kuwa na uwezo mdogo zaidi wa kuwekeza kwenye huduma muhimu za jamii, kama vile afya na elimu, na katika kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara. Kisha uduni wa elimu, na mazingira yasiyofaa ya uwekezaji na biashara, hutumika kama sababu ya kuzidi kukwepa bara la Afrika. Ukichanganya hasara itokanayo na kukosekana kwa uwiano mzuri wa kibiashara, tatizo la madeni, na mambo mengine, utagundua kuwa badala ya mataifa tajiri kuisaidia Afrika, bara letu maskini ndilo linapeleka nje fedha nyingi zaidi kuliko zinazoingia. Inakadiriwa kuwa kwa kila shilingi 100 za fedha halisi zilizoingia barani Afrika kutoka nje tangu mwaka 1980, shilingi 106 zilitoka nje; shilingi 51 kutokana na uwiano mbaya wa biashara, shilingi 25 kutokana na ulipaji wa madeni na faida ya wawekezaji kutoka nje, na shilingi 30 kutokana na sababu nyinginezo zitumiwazo kutoa fedha nje. Matokeo yake tukipata sh.100, tunalipa sh.106. Tutaendelea kweli hivyo? Tunawahoji wakubwa: hawaoni ukweli huo? Ndugu Wanachi, Hatulalamiki tu. Nchi nyingi barani Afrika zimejitahidi sana kuzingatia ushauri wa wakubwa, ikiwemo kwa kulegeza masharti ya biashara na kufungua milango ya uwekezaji na biashara. Wakubwa walituahidi kuwa tukifanya hivyo watatusaidia, na pia tutafaidika na mfumo huo mpya wa biashara duniani. Lakini ukweli ni kuwa nyingi ya ahadi zao hazijatekelezwa, au ukipewa kwa mkono mmoja utanyang anywa kwa mkono mwingine. Ninyi Watanzania wenzangu mlishuhudia sakata la minofu ya samaki kutoka Ziwa Victoria ambapo kwa miezi 11 tulizuiwa kuuza barani Ulaya kwa kudhaniwa tu kuwa samaki wetu wana sumu, jambo ambalo lilikuja kuthibitika kuwa si kweli, lakini baada ya kutuletea hasara kubwa sana. Kwa vile minofu hiyo ndiyo zao letu kuu hivi sasa tuuzalo katika masoko ya Ulaya, kwa kipindi tulichozuiwa kuuza hasara tuliyopata inakadiriwa kufika Sh 24 bilioni fedha za kigeni, licha ya maelfu ya familia zinategemea biashara ya samaki hao kukosa mapato kwa kipindi hicho. Ukweli ni kuwa pamoja na ahadi nyingi za wakubwa, bado bidhaa za nchi maskini, ikiwemo zitokanazo na kilimo, hasa zilizosindikwa kama vile nguo na viatu, bado zinawekewa vizingiti vingi sana kuingia kwenye masoko ya wakubwa. Na haya si maneno yangu tu; wenyewe pia wanakiri hivyo. Katika mkutano wa kila mwaka wa mataifa makubwa (G8) uliofanyika mjini Genoa, Italia, mwezi Julai mwaka huu, ilitolewa taarifa kuhusu fursa na hatari za soko la utandawazi kwa nchi maskini. Taarifa hiyo iliandaliwa kwa pamoja na Benki ya Dunia,
5 Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), na Benki za Maendeleo za Kanda za Afrika, Asia, Ulaya, na Marekani. Napenda ninukuu taarifa hiyo ilivyosema kuhusu hali ngumu inayolikabili bara la Afrika. Ibara ya 26 ya taarifa hiyo inasema ifuatavyo: Isitoshe, Afrika inakabiliwa na ulindwaji wa hali ya juu sana wa masoko ya nchi tajiri (Afrika) inapotaka kuuza katika masoko hayo... Iwapo vikwazo viwekwavyo kwa bidhaa za Afrika katika masoko ya Kanada, Jumuiya ya Ulaya, Japan na Marekani vingefutwa, mauzo nje ya bara la Afrika ya bidhaa ambazo hazitokani na mafuta yangeongezeka kwa asilimia 14. Inakadiriwa pia kuwa, Afrika ingeruhusiwa kuuza bidhaa za kilimo kwa wingi zaidi kwenye soko la nchi hizo tajiri, mapato halisi barani Afrika yangeongezeka kwa USD 6 (Sh.5,400) kwa kila mtu Kwa hiyo, ni muhimu sana kwa nchi tajiri kupunguza kinga waliyojiwekea dhidi ya bidhaa za Afrika, hasa bidhaa za kilimo, ili kusaidia uchumi wa nchi za Kiafrika ukue kwa namna itakayosaidia kupunguza umaskini Tunafurahi wakubwa wanakiri hivyo; tunachodai na kushinikiza sasa ni kuwa watekeleze kwa vitendo ahadi zao za kurekebisha hali hiyo. Tulijifunza tangu enzi za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere, kuwa chimbuko la sera ya nje ni sera za ndani. Sera za usawa ndani ya nchi zinatusukuma kutafuta usawa katika mahusiano na nchi za nje. Aidha, utekelezaji wa sera ya nje hupata nguvu kwa wanaozisimamia kujua Watanzania wote ni wamoja, na wanaunga mkono yale wanayoyalenga katika sera yetu ya nje. Nimewaelezeni leo sehemu au sura moja tu ya sera yetu ya nje, nayo ni kutafuta haki, usawa na manufaa katika dunia ya utandawazi, na biashara za ushindani mkali kimataifa. Tunahitaji sana mitaji kutoka nje ya nchi; lakini mwisho wake lazima tuwe bado na uchumi wa taifa, na kuwa na haki ya kubuni na kutekeleza sera ya taifa ya uchumi na maendeleo. Tunajua hatuwezi kuendelea, na kushinda vita dhidi ya umaskini, bila uwekezaji mitaji wenye ufanisi, na kushiriki kikamilifu kwenye biashara ya nje. Lakini tunajua pia kuwa mfumo wa biashara uliopo hauna maslahi ya kutosha kwetu, na hauwezi kutusaidia kupiga vita umaskini. Na kweli tusipoangalia unaweza kutuzidishia umaskini. Tunaomba wananchi mtuelewe tunapoongoza mapambano ya nchi maskini kudai haki, maslahi na usawa zaidi katika mahusiano ya kibiashara na kiuchumi na nchi tajiri zenye viwanda. Kama nilivyosema, kazi hiyo ni ngumu, maana tunataka kubadili mfumo ambao ulivyo sasa unafaidisha wakubwa. Lakini baadhi yao wameonyesha nia njema, na kama nchi maskini tukisimama pamoja, kama tulivyofanya Zanzibar, wakubwa hao watatusikiliza, maana hoja zenyewe ni wazi, wenyewe wanazikiri, wanachohitaji ni msukumo na utashi wa kisiasa kutekeleza. Ni wajibu wetu kuchochea utashi wao huo kwa kujenga na kutetea hoja zetu. Sisi ndani ya nchi tumeazimia kwa dhati kupiga vita umaskini. Lakini ili tufanikiwe utashi huo wa ndani ya nchi lazima uungwe mkono na utashi nje ya nchi. Sera nzuri ndani ya nchi lazima ziungwe mkono na sera nzuri nje ya nchi. Na mazingira mazuri ndani ya nchi yanahitaji mazingira bora kwenye nchi tajiri vile vile ndipo tufanikiwe.
6 Mkereketwa mmoja wa maendeleo aliwahi kulinganisha mahusiano ya kiuchumi na kibiashara duniani na mchezo wa bao. Ili mchezo wa bao uendelee lazima hata yule mchezaji asiye mahiri sana naye ale kete kiasi fulani. Iwapo bingwa atakula kete zote peke yake, huo utakuwa mwisho wa mchezo. Tanzania, kwa niaba ya nchi 49 maskini duniani, ianawasihi wakubwa wakubali kuendeleza mchezo kwa kuhakikisha na sisi wadogo tunafaidika. Kwa pamoja, nchi maskini na nchi tajiri, tunaweza kukubaliana juu ya mfumo bora zaidi wa uchumi na biashara duniani wenye maslahi kwa washiriki wote. Tukiwa waratibu wa mtazamo wa nchi maskini, tutaendelea kupigania mfumo huo. Ninachoomba kutoka kwenu, wananchi, ni uelewa wenu wa hali halisi ilivyo, na kuunga mkono harakati za Serikali yenu za kurekebisha hali ilivyo sasa. Tukijua mko pamoja nasi, tutakusanya nguvu za kimataifa tukiwa kifua mbele. Mungu ibariki Afrika Mungu ibariki Tanzania Ahsanteni kwa kunisikiliza. 1. G8 Genoa Summit, A Globalized Market Opportunities and Risks for the Poor : Global Poverty Report, July 2001
Information for assessors (do not distribute this page to participants):
R&P Cultural Orientation Model Assessment Written Version Swahili Information for assessors (do not distribute this page to participants): This written version of the Model Cultural Orientation (CO) Assessment
More informationDodoma ambako kikao cha Bunge kinaendelea kuja kushiriki japo sehemu ya uzinduzi wa mkutano.
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. PHILIP I. MPANGO (MB) WAKATI WA UFUNGUZI WA MKUTANO WA KIMATAIFA WA KUJADILI MATUMIZI YA TAKWIMU ZA UMASKINI NA NAMNA BORA YA KUPIMA HALI YA UMASKINI AFRIKA,
More informationHOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA, KWA WANANCHI, TAREHE 31 JULAI 2001
HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA, KWA WANANCHI, TAREHE 31 JULAI 2001 Leo napenda nizungumze nanyi kuhusu umuhimu wa kuweka akiba, na umuhimu wa kulipa
More informationGOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)
GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER (Made under Section 23) THE ELECTRICITY (STANDARDIZED SMALL POWER PROJECTS TARIFF) ORDER, 2016 citation 1. This Order may be cited
More informationTaarifa Kuhusu Hali ya Uchumi wa Tanzania
Taarifa Kuhusu Hali ya Uchumi wa Tanzania Benki Kuu ya Tanzania Septemba 2016 YALIYOMO 1.0 HALI YA UCHUMI WA TANZANIA... 3 1.1 UKUAJI WA UCHUMI... 3 1.2 MATAZAMIO YA UKUAJI WA UCHUMI MWAKA 2016... 4 1.3
More informationGOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)
GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER (Made under Section 23) THE ELECTRICITY (STANDARDIZED SMALL POWER PROJECTS TARIFF) ORDER, 2015 Citation 1. This Order may be cited
More informationTANZANIA MARKETS PAN Sera zinazoboresha masoko
TANZANIA MARKETS PAN Sera zinazoboresha masoko UPOTEVU WA MAZAO YA NAFAKA BAADA YA MAVUNO: CHANGAMOTO NA UBORESHAJI Usuli Kuna makubaliano ya jumla kwamba marekebisho ya sera zinazohusu sekta ya kilimo,
More informationNGUO MPYA ZA UKOLONI. Mikataba ya Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Umoja wa Ulaya na Afrika. Agosti 2017
TAARIFA Agosti 2017 NGUO MPYA ZA UKOLONI Mikataba ya Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Umoja wa Ulaya na Afrika Jumuiya ya Jamii ya 2007: Wajumbe wanaadhamana Nairobi dhidi ya EPAs. SwissInfo Tangu mwaka
More informationTAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU
TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU TANZANIA EDUCATION NETWORK / MTANDAO WA ELIMU TANZANIA () 1.0 USULI Tanzania, sawa na nchi nyingine, ilitia saini Malengo ya Maendeleo ya Milenia na Malengo ya
More informationMisamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?
Policy brief TZ.12/2010K Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada? 1. Utangulizi Kila mwaka Bunge la Tanzania hupitia na kuchanganua kwa makini bajeti ya Serikali.
More informationHOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, MHESHIMIWA DKT. PHILIP I. MPANGO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, MHESHIMIWA DKT. PHILIP I. MPANGO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA 2018/19 1 I. UTANGULIZI 1. Mheshimiwa
More informationJAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA FEDHA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA FEDHA HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA, MHESHIMIWA MUSTAFA HAIDI MKULO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA
More informationAzimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu
The Human Rights Centre Uganda Azimio la Mkutano Mkuu 53/144 (8 Machi 1999) Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu AZIMIO KUHUSU HAKI NA WAJIBU WA MTU BINAFSI, VIKUNDI NA JUMUIYA
More informationMheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame M. Mbarawa (Mb.); Waheshimiwa Mawaziri na Wabunge wote mliohudhuria;
HOTUBA YA BALOZI MHANDISI JOHN W.H. KIJAZI, KATIBU MKUU KIONGOZI, WAKATI WA UFUNGUZI WA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAHANDISI KWA MWAKA 2017, UKUMBI WA JAKAYA KIKWETE, DODOMA, SEPTEMBA 7, 2017 Mheshimiwa Waziri
More informationJAMHURI YA KENYA. Mkakati wa Ushirikiano MUKHTASARI FY Public Disclosure Authorized. Public Disclosure Authorized
horized Public Disclosure Authorized Public Disclosure Authorized Public Disclosure Authorized JAMHURI YA KENYA Mkakati wa Ushirikiano FY2014-2018 MUKHTASARI Mkakati wa Ushirikiano wa Jamhuri ya Kenya
More informationKubadili Sheria Za Mbegu Na Ulinzi Wa Aina Za Mbegu Na Mimea Nchini Tanzania
Kubadili Sheria Za Mbegu Na Ulinzi Wa Aina Za Mbegu Na Mimea Nchini Tanzania Athari Zake Kwa Mifumo Ya Mbegu Inayosimamiwa Na Wakulima Na Kwa Wakulima Wadogo April 2016 CONTENTS UTANGULIZI 3 MAELEZO YA
More informationHOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA MHESHIMIWA DKT
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA MHESHIMIWA DKT. WILLIAM AUGUSTAO MGIMWA (MB) AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA 2013/2014 I. UTANGULIZI 1. Mheshimiwa
More informationIn the matter of an Application by the KIGOMA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (KUWASA) For a Tariff and Charges Adjustment
In the matter of an Application by the KIGOMA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (KUWASA) For a Tariff and Charges Adjustment Background 1. On 17 th May 2011 KUWASA submitted an application for
More informationElimukombozi, Lugha na Upashanaji Habari nchini Tanzania, katika Muktadha wa Utandawazi
Elimukombozi, Lugha na Upashanaji Habari nchini Tanzania, katika Muktadha wa Utandawazi Martha Qorro 1 1.0 Utangulizi Elimu ni suala la jamii ambalo mipango na taratibu zake zinahitaji kushirikisha wadau
More informationHOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE
HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE. JENISTA MHAGAMA (MB), KATIKA KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA AFYA NA USALAMA MAHALI PA KAZI DUNIANI DODOMA, 28 APRILI
More informationJAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA. Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo. TOLEO Na.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo TOLEO Na. 1, Desemba, 2012 Yaliyomo Orodha ya Vifupisho -------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------3
More informationUKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA)
Empowered lives. Resilient nations. UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA) Kenya Miradi ya Equator Wanafijiji na Maendeleo Himili ya Jamii MIRADI YA UNDP EQUATOR Kote duniani, jamiii zinazidi kubuni
More informationElimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani
Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani HakiElimu: Mfululizo wa Mada za Uchambuzi Namba. 2003.4S Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere 1 Rakesh
More informationMwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara
Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara Umetayarishwa na Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania kwa Kushirikiana na Idara ya Maendeleo
More informationJAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, MHESHIMIWA DKT. PHILIP I. MPANGO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA
More informationJAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO MPANGO KAZI WA USHIRIKI WA MTOTO TANZANIA 2014-2019 JANUARI, 2014 Dibaji Kwa mujibu wa takwimu za Sensa ya Taifa ya Idadi
More informationRipoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara)
Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara) Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara) Hakimiliki Shirika la Kazi Duniani 2010 Toleo la kwanza 2010 Machapisho ya Ofisi
More informationMAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI
MAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI MAKUBALIANO YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI Paris, 20 Oktoba 2005 Kongamano Kuu la Umoja wa Mataifa linalohusisha
More informationMAADHIMISHO YA MIAKA 15 YA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY
HABARI ISSN 1821-5335 Makala Maalum Miaka 15 ya Foundation for Civil Society MAADHIMISHO YA MIAKA 15 YA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY Uwezeshaji wa moja ya sekta madhubuti za asasi za kiraia barani Afrika
More informationKiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika
Kiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika Stephen N. Kamau Abstract It is a fact that in the recent past, globalization has gradually taken shape in Africa and as such the continent has no choice but to
More information5. Mheshimiwa Spika, Bunge lako Tukufu lilijadili kwa kina Miswada ifuatayo:
HOTUBA YA MHESHIMIWA MIZENGO PETER PINDA (MB), WAZIRI MKUU, WAKATI WA KUTOA HOJA YA KUAHIRISHA MKUTANO WA KUMI NA MBILI WA BUNGE DODOMA TAREHE 29 AGOSTI 2008 UTANGULIZI 1. Mheshimiwa Spika, leo ni takriban
More informationUNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013
www.xtremepapers.com UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level *9257224991* SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013 Additional Materials: Answer Booklet/Paper
More informationMALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU
MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU NA WAJIBU WA Serikali za Mitaa MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU NA WAJIBU WA Serikali za Mitaa Kimetayarishwa na Kikundi Kazi cha Serikali za Mitaa cha Policy Forum Kimehaririwa
More informationHuman Rights Are Universal And Yet...
Human Rights Are Universal And Yet... Episode 05 Title : The right to education Author : Julien Adayé Editor : Aude Gensbittel Translator : Anne Thomas, Eric Ponda Proofreader: Pendo Paul Characters (sounds,
More informationUTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO
UTANGULIZI International Montessori Teachers College (IMTC), ni chuo kilichoanzishwa hapa nchini Tanzania mwaka 2012 na kinatoa kozi ya kimataifa ya ualimu wa watoto wadogo (yaani child care and nursery
More informationUtumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania
Nordic Journal of African Studies 16(1): 18 29 (2007) Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania ABSTRACT This paper has attempted
More informationKUSHUKA KWA HADHI YA LUGHA ZA JAMII NCHINI TANZANIA YOHANA P. MSANJILA University of Dar es Salaam, Tanzania
Nordic Journal of African Studies 12(3): 296 309 (2003) KUSHUKA KWA HADHI YA LUGHA ZA JAMII NCHINI TANZANIA YOHANA P. MSANJILA University of Dar es Salaam, Tanzania ABSTRACT Lugha za jamii hapa nchini
More informationUFUPISHO WA 35. Hali ya kiulimwengu ya Tekinolojia ya kibiashara/ugeuzi jeni na uboreshaji mazao: Clive James Chair, ISAAA Board of Directors
I S A A A Huduma ya kinimataifa ya upataji na utumizi wa kiteknolojia ya kuboresha kilimo MUHTASARI WA KIUTEKELEZAJI UFUPISHO WA 35 Hali ya kiulimwengu ya Tekinolojia ya kibiashara/ugeuzi jeni na uboreshaji
More informationMWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2017/18
MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2017/18 WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO NOVEMBA, 2016 ISBN 978-9987 - 829-02 - 9 ii YALIYOMO 1.0 UTANGULIZI... 1 2.0 MABORESHO YA MFUMO WA KIBAJETI... 2
More informationRipoti ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA 2006/07
Mwongozo wa Lugha Rahisi wa Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA 2006/07 Mwongozo huu Umeandaliwa na Hakikazi Catalyst kwa niaba ya Wizara ya Fedha na Uchumi. Desemba 2007 Dibaji Ripoti ya Mwaka ya
More informationMpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi
Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi HakiElimu: Mfululizo wa Mada za Uchambuzi Namba. 2003. 6S Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari
More informationKutetea Haki za Binadamu
Kutetea Haki za Binadamu Kitabu cha Marejeo kwa watetezi wa Haki za Binadamu Toleo la pili i Kutetea Haki za Binadamu: Kitabu cha Marejeo kwa watetezi wa Haki za Binadamu (Toleo la pili) 2012 East and
More informationRipoti ya Maendeleo ya Binadamu 2013
W N S E Muhtasari Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2013 Kuinuka kwa Nchi za Kusini: Maendeleo ya Binadamu katika Ulimwengu Anuwai Empowered lives. Hati ya kunakili 2013 na Mradi wa Maendeleo ya Umoja wa
More informationPronunciation: Mä-hret Zäläke Ndal-ka-tscho Molla Mare Gebre-gzabiär 1/12
Human Rights Are Universal And Yet... Episode 07 Title : The right to food drought and famine in Ethiopia Author : Tedla Getachew Editor : Aude Gensbittel, Pendo Paul Translator : Anne Thomas Proofreader:
More informationKUHUSU AFRODAD. Dira ya AFRODAD. Dhamira ya AFRODAD. AFRODAD inalenga mchakato sawa na endelevu wa maendeleo kuelekea Afrika yenye mafanikio.
KUHUSU AFRODAD Dira ya AFRODAD AFRODAD inalenga mchakato sawa na endelevu wa maendeleo kuelekea Afrika yenye mafanikio. Dhamira ya AFRODAD Kupata sera zitakazorekebisha migogoro ya madeni ya Afrika kulingana
More informationTAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF) KUHUSU HAKI ZA WATOTO KATIKA KATIBA MPYA
TAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF) KUHUSU HAKI ZA WATOTO KATIKA KATIBA MPYA Marekebisho ya 23 January 2013 YALIYOMO KURASA TAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF)... 0 KUHUSU HAKI ZA WATOTO... 0
More informationNGUZO KUMI ZA KILIMO KWANZA
NGUZO KUMI ZA KWANZA (MFUMO WA UTEKELEZAJI) NGUZO YA 1 DIRA YA TAIFA YA KWANZA 1.1 Kupitisha Dira ya KWANZA SHUGHULI MAJUKUMU MUDA MHUSIKA MKUU 1. AZIMIO LA KWANZA 2. mpango wa utekelezaji wa KWANZA 3.
More informationATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA UCHUMI WA ZANZIBAR
ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA UCHUMI WA ZANZIBAR MUHTASARI WA RIPOTI YA YA MWISHO. JULY 2012 for Page i Muhtasari Utafiti huu wa athari za Mabadiliko ya Tabianchi kwa uchumi Zanzibar umetoa tathmini
More informationMradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali ya Madini Ukanda
WARAKA WA TAARIFA YA MRADI (PID) HATUA YA TATHMINI TAARIFA NA..: AB4376 Jina la Mradi Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali ya Madini Ukanda AFRIKA Sekta Madini na Uchimbaji mwingine (100%) Namba ya
More informationUfunguo wa Kutaalamika Haraka
0 Ufunguo wa Kutaalamika Haraka Ufunguo wa Kutaalamika Haraka Kijitabu Kielelezo; Nakala ya Bila Malipo Yaliyomo 1 Yaliyomo Utangulizi...04 Habari Fupi Kuhusu...08 Fumbo la Ulimwengu wa Ng ambo ya Pili...11
More informationKilimo cha kiekolojia cha Wakulima Wadogo Hufanikisha Haki za Mazingira
Kilimo cha kiekolojia cha Wakulima Wadogo Hufanikisha Haki za Mazingira Kilimo cha kiekolojia cha Wakulima Wadogo Hufanikisha Haki za Mazingira Kiongozi hiki kimeandaliwa kikiwa ni sehemu ya mradi wa
More informationAzimio lililopitishwa na Mkutano Mkuu tarehe 18 Desemba 2013 [juu ya taarifa ya Kamati ya Tatu (A/68/456/Add.2)]
This unofficial translation is provided by the International Service for Human Rights Umoja wa Mataifa A/AZI/68/ Ugaw Jumla Mkutano Mkuu 30 Januari 2014 Kikao cha Sitini na Nane Dondoo ya Ajenda 69(b)
More informationJUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1
The Human Rights Centre Uganda JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1 AZIMIO LA KIMATAIFA JUU YA HAKI ZA KIBINADAMU SURA YA NNE YA KATIBA YA JAMHURI YA UGANDA YA 1995: MASIMULIZI YALIYOFASIRIWA KWA URAHISI NA KUFUPISHWA
More informationTANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora
K I T A B U C H A M B I N U B O R A C H A T O A U k u r a s a 1 TANZANIA OSAKA ALUMNI Kitabu cha Mbinu Bora Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa P.O. Box 1923, Dodoma. Novemba, 2012
More informationJHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI
JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI Mwongozo huu utatumika kama njia ya kuwafunza watafiti watakaohusika na utafiti unaohusu binadamu. Muongozo huu utatumika
More informationKitabu Cha Mafunzo Ya Uongozi Kwa Wanawake
Uongozi Bora Kitabu Cha Mafunzo Ya Uongozi Kwa Wanawake UONGOZI BORA Uongozi ni uwezo wa kubuni na kuyaweka maono katika vitendo. -Mshiriki katika Semina ya Mafunzo Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya
More informationKufanya Uwekezaji kuwa wa Manufaa kwa Afrika: Jibu la Mbunge kuhusu Unyakuzi wa Ardhi
PAN AFRICAN PARLIAMENT PARLEMENT PANAFRICAIN البرلمان PAN- PARLAMENTO األفريقي AFRICANO Kufanya Uwekezaji kuwa wa Manufaa kwa Afrika: Jibu la Mbunge kuhusu Unyakuzi wa Ardhi Julai 21 22, 2011 Bunge la
More informationDibaji ya Mwenyekiti wa Kamati ya Pamoja ya Uongozi
Dibaji ya Mwenyekiti wa Kamati ya Pamoja ya Uongozi Mwaka wa nne wa utekelezaji wa Mpango wa Msaada wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDAP 2011-2016) nchini Tanzania ulikuwa na mafanikio makubwa lakini
More informationMhashamu Askofu Jude Thaddaeus Ruwa ichi, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania; Mwadhama Policarp Kardinali Pengo,
HOTUBA YA MHESHIMIWA MIZENGO P. PINDA (MB), WAZIRI MKUU, KWENYE SHEREHE YA KUADHIMISHA MIAKA HAMSINI YA BARAZA LA MAASKOFU KATOLIKI TANZANIA, TAREHE 08 JUNI 2008, MSIMBAZI CENTRE, DAR ES SALAAM Mhashamu
More informationMIONGOZO MIWILI KUPAA NA KUTUNGULIWA KWA AZIMIO LA ARUSHA
KIGODA CHA TAALUMA CHA MWALIMU NYERERE MIONGOZO MIWILI KUPAA NA KUTUNGULIWA KWA AZIMIO LA ARUSHA Yamekusanywa na kuhaririwa na: Bashiru Ally Saida Yahya-Othman Issa Shivji CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
More informationKimesanifiwa na:- E.D.Kissuu ECOMM TANZANIA S.L.P ,Dar es Salaam. Simu:
Kimesanifiwa na:- E.D.Kissuu ECOMM TANZANIA S.L.P. 21425,Dar es Salaam. Simu: +255 713 607 207 edkissuu@gmail.com Katuni zimechorwa na: Adam Lutta Babatau Inc. Box 13565 Dar es salaam, Simu:+255 713 474200
More informationK. M a r k s, F. E n g e l s
W a (any a kazi wa nchi zote, unganeni! K. M a r k s, F. E n g e l s Maelezo ya chama cha kikomunist Idara ya Maendcleo Moscow Tafsiri hii ya "Maelezo ya Chama cha Kikomunist" inatokana na maandishi
More informationMAPENDEKEZO YA MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA TANZANIA
MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA MAPENDEKEZO YA MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA TANZANIA KUHUSU JINSI YA KUINGIZA MASUALA YA USAWA WA JINSIA KATIKA RASIMU YA PILI YA KATIBA YA TANZANIA KWA NINI MISINGI YA USAWA
More informationJe! imezingatia maslahi ya mkulima mdogo?
Toleo NO. 044 Januari Machi 2014 Bei Shs. 500/= ISSN 0856-5937 Rasimu ya katiba mpya: Je! imezingatia maslahi ya mkulima mdogo? Yaliyomo Uk. 9 Uk. 11 Uk. 13 MVIWATA yapata wawakilishi wawili ndani ya Bunge
More informationTANGA CEMENT PLC ANNUAL REPORT TAARIFA YA MWAKA.
TANGA CEMENT PLC 2016 ANNUAL REPORT TAARIFA YA MWAKA www.simbacement.co.tz ANNUAL REPORT 2016 ANNUAL REPORT2016 TAARIFA YA MWAKA 2016 TAARIFA YA MWAKA 2016 02 ANNUAL REPORT 2016 Chairperson s Statement
More informationJifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti
Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti Mradi wa kujua kuhusu Pesa Aprili 2011 FLP - Swahili Mradi wa kujua kuhusu Pesa Ipindi vyetu vya maelezo vya bure, warsha na kozi hutoa fursa ya kujifunza kuhusu
More informationRIPOTI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA TAIFA YA UKAGUZI RIPOTI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI KUHUSU UKAGUZI WA MASHIRIKA YA UMMA KWA MWAKA WA FEDHA 2009/2010 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu
More informationMKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA PRO-ROUTES. Ombi kwa ajili ya fedha za umma wa mradi wa ziada
Public Disclosure Authorized Public Disclosure Authorized Public Disclosure Authorized Public Disclosure Authorized Résumé non technique Version Swahili MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA
More informationHAKI NA TARATIBU ZA AJIRA, KAZI NA HIFADHI YA JAMII
HAKI NA TARATIBU ZA AJIRA, KAZI NA HIFADHI YA JAMII SHERIA KATIKA LUGHA RAHISI KIMETOLEWA NA CHAMA CHA WANASHERIA TANZANIA BARA (TANGANYIKA LAW SOCIETY) KWA UFADHILI WA TAASISI YA LEGAL SERVICE FACILITY
More informationMWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI
MWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI 2012 MWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI 2012 Kitabu hiki kimetayarishwa na Shirika la Equality for Growth (EfG) Equality
More informationJAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. PHILIP I. MPANGO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA FEDHA
More informationSERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH
Eneo La Huduma: Huduma Ya Ushirika Wa Biashara Kichwa: Sera Ya Mipango Ya Msaada Wa Kifedha SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH Tarehe Kupitishwa: 09/20/2013 Tarehe Ya Ufanisi: 09/20/2013 1/1/2017
More informationUhakika wa Mbegu kwa Uhakika wa Chakula MWONGOZO WA UZALISHAJI WA MBEGU ZA ASILI ZA MAHINDI
Uhakika wa Mbegu kwa Uhakika wa Chakula MWONGOZO WA UZALISHAJI WA MBEGU ZA ASILI ZA MAHINDI b Uhakika wa Mbegu kwa Uhakika wa Chakula MWONGOZO WA UZALISHAJI WA MBEGU ZA ASILI ZA MAHINDI 1 Mwongozo wa Uzalishaji
More informationmuhtasari 37 brief 37 Kiwango cha kiutandawazi cha mazao ya kibiashara ya kibayoteki/ugeuzi jeni: 2007 Clive James Bordi ya wakurugenzi wa ISAAA
i s a a a Huduma ya Kimataifa ya Upataji na Utumizi wa Tekinolojia ya Kuboresha Kilimo muhtasari 37 brief 37 Kiwango cha kiutandawazi cha mazao ya kibiashara ya kibayoteki/ugeuzi jeni: 2007 Na Clive James
More informationKuwafikia waliotengwa
Kuwafikia waliotengwa Kuwafikia waliotengwa Muhtasari Chapisho la UNESCO 2 M U H T A S A R I R I P O T I Y A U S I M A M I Z I W A K I M A T A I F A W A M R A D I W A E L I M U K W A W O T E 2 0 1 0 Ripoti
More informationMiradi na jamii. 3.1 Utangulizi
3.1 Utangulizi Miradi na jamii Lengo la sura hii ni mapitio ya mazingira pana ambayo chini ya ardhi kwa ajili ya maendeleo vijijini upatikanaji wa maji inafaa. majadiliano wakapanga meneja, au kiongozi
More informationHati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)
102/3 KISWAHILI KARATASI YA 3 Fasihi Julai/Agosti 2013 MUDA : SAA 2 ½ Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E) Kiswahili Karatasi 3 Julai/ Agosti Muda: Saa 2 ½ MAAGIZO: Andika jina lako na nambari yako
More informationHISTORIA, MAENDELEO NA MABADILIKO YA KATIBA TANZANIA TANGU UHURU HADI MIAKA HAMSINI YA UHURU 9 DESEMBA 2011.
Saint Augustine University of Tanzania From the SelectedWorks of Daudi Mwita Nyamaka Mr. Winter December 9, 2011 HISTORIA, MAENDELEO NA MABADILIKO YA KATIBA TANZANIA TANGU UHURU HADI MIAKA HAMSINI YA UHURU
More informationProgramu ya Uendelezaji Mifumo ya Maji Vijijini (PUMMV) katika Tanzania. Modeli wa Ukodishaji Mradi
Programu ya Uendelezaji Mifumo ya Maji Vijijini (PUMMV) katika Tanzania Modeli wa Ukodishaji Mradi Programu ya Uendelezaji Mifumo ya Maji Vijijini (PUMMV) Programu ya Uendelezaji Mifumo ya Maji Vijijini
More informationBUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA SABA. Kikao cha Thelathini na Tisa Tarehe 1 Juni, (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A
BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa Tarehe 1 Juni, 2017 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA:
More informationSautiElimu. Sauti Yako Isikike
SautiElimu Sauti Yako Isikike SautiElimu Sauti Yako Isikike Mtayarishaji : Godfrey Telli Mchangiaji : Robert Mihayo Mhariri : Rakesh Rajani Shukrani za dhati kwa timu ya waandaaji wa SautiElimu 1-10: Lilian
More informationUNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU VIKWAZO VYA KULINDA MAISHA KATIKA USAIDIZI WA KIMATAIFA WA AFYA KWA MSAADA WA KIMATAIFA UNAOFADHILIWA NA MAREKANI
UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU VIKWAZO VYA KULINDA MAISHA KATIKA USAIDIZI WA KIMATAIFA WA AFYA KWA MSAADA WA KIMATAIFA UNAOFADHILIWA NA 30 SEPTEMBA, 2017 UTANGULIZI Tarehe 23 Januari, 2017, Rais Donald Trump
More informationUSIMAMIZI MKUU WA UBORA WA MAHURUJI
USIMAMIZI MKUU WA UBORA WA MAHURUJI MWONGOZO KWA WAFANYABIASHARA WADOGO NA WA WASTANI WANAOUZA BIDHAA NJE YA NCHI TOLEO LA PILI Geneva 2011 ii IKISIRI YA HUDUMA YA HABARI ZA BIASHARA ID=42653 2011 F-09.03
More informationSera ya Faragha. Upeo. Aina za Data na Mbinu za Ukusanyaji
Sera ya Faragha Katika Sera hii ya Faragha ( Sera ), sisi, Qualcomm Incorporated na makampuni yetu tanzu (kwa pamoja sisi au yetu ), tunatoa maelezo kuhusu jinsi tunavyokusanya, kutumia, kuchakata, na
More informationTAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM)
TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM) 2007-2017 TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM) 2007-2017 Kimetolewa na Sikika (Zamani YAV) S.L.P 12183 Dar Es Salaam
More informationApril 14, 2016 COUNTY ASSEMBLY DEBATES 52
MOMBASA COUNTY ASSEMBLY HANSARD REPORT Thursday, 14 th April, 2016 The House met at 2.48pm. (Hon. Deputy Speaker (Mr. Mswabah Rashid) in the Chair) PRAYERS Hon. Deputy Speaker (Mr. Mswabah Rashid): Kindly
More informationKUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA
KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA KUWEZESHA Radio za kijamii Kutumia Tehama Mwongozo huu umeandaliwa ili kuvipa
More informationKAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI TANZANIA
KAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI TANZANIA KAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI TANZANIA NI UFUMBUZI KATIKA KUSHIRIKISHA JAMII? NI UFUMBUZI KATIKA KUSHIRIKISHA JAMII? Februari, 2013 Februari, 2013 SHUKURANI
More informationUNABII WA BIBLIA. CBM Publishing 32 Blenheim Road, Far Cotton Northampton, England. NN4 8NW
Kama unataka kujifunza zaidi njia ya Mkristo wa kweli anavyopaswa kuishi, basi ni lazima ujifunze Biblia. Ili kukusaidia; Kanise la Christadelphian Bible Mission limechapisha kijitabu kuhusu mafunzo ya
More informationHii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA SITA
Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA SITA Kikao cha Ishirini na Mbili Tarehe 6 Julai, 2009 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika
More informationMKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA WAZIRI MKUU MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI (2008 2012) Dar es Salaam Oktoba 2007 YALIYOMO ORODHA YA VIFUPISHO DIBAJI SHUKRANI MUHTASARI RASMI SURA
More informationBUNGE LA TANZANIA MKUTANO WA NANE. Kikao cha Ishirini na Nane Tarehe 16 Julai, (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A
Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA MKUTANO WA NANE Kikao cha Ishirini na Nane Tarehe 16 Julai, 2012 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma
More informationwasiofaa. Naomba sana kila raia afanye bidii awezavyo kumkaribia Mwenyezi Mungu vile anavyoona inafaa, lakini asipitishe hukumu juu ya wengine.
HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA, KWENYE IBADA YA KUWEKWA WAKFU NA KUINGIZWA KAZINI ASKOFU MARTIN FATAELI SHAO WA DAYOSISI YA KASKAZINI YA KANISA LA
More informationKuuelewa Mchakato wa Bajeti Tanzania Mwongozo wa Asasi za Kiraia
Kuuelewa Mchakato wa Bajeti Tanzania Mwongozo wa Asasi za Kiraia HakiElimu & Policy Forum KUUELEWA MCHAKATO.indd a 1/20/10 11:00:56 AM KUUELEWA MCHAKATO.indd b 1/20/10 11:00:57 AM Kuuelewa Mchakato wa
More informationShabaha ya Mazungumzo haya
Karibu Katika Mazungumzo Kuhusu Mchakato wa Uhamasishaji Maendeleo ya Kanisa na Jamii CCMP/UMOJA Shabaha ya Mazungumzo haya Kuwafahamisha viongozi wa makanisa kuhusu Mchakato wa CCMP ambao umekuwa ukitumika
More informationUnited Pentecostal Church June 2017
Kwa Nini Tusali? Jarida la Maombi ya Wanawake Kimataifa "Chagua" Ladies Prayer International kwa Facebook United Pentecostal Church June 2017 Tuko na wafuasi Facebook katika Marekani, Hong Kong, Philippines,
More informationTIST HABARI MOTO MOTO
TIST HABARI MOTO MOTO Tel. +255784-537720/+255717-062960/+255782-250947, P.O.BOX 6049 MOROGORO E-Mail info@tist.org May 2010 Cash Payments for Trees Clean Air Action has developed a way to pay the groups
More informationMaswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu WEMA
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu WEMA TWN Third World Network 1. WEMA ni nini? Mahindi yanayotumia maji kwa ufanisi yajulikanayo kwa kingereza kama Water Efficient Maize for Africa (WEMA) ni mpango
More informationMKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA WAZIRI MKUU MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI (2008 2012) TOLEO LA PILI Dar es Salaam, Oktoba, 2007 i ii JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA WAZIRI
More informationUsimulizi wa Riwaya ya Nyongo Mkalia Ini E. S. MOHOCHI University of Egerton, Kenya
Nordic Journal of African Studies 9(2): 49-59 (2000) Usimulizi wa Riwaya ya Nyongo Mkalia Ini E. S. MOHOCHI University of Egerton, Kenya UTANGULIZI Tukichunguza hazina ya uhakiki uliofanywa katika taaluma
More information