Human Rights Are Universal And Yet...

Size: px
Start display at page:

Download "Human Rights Are Universal And Yet..."

Transcription

1 Human Rights Are Universal And Yet... Episode 05 Title : The right to education Author : Julien Adayé Editor : Aude Gensbittel Translator : Anne Thomas, Eric Ponda Proofreader: Pendo Paul Characters (sounds, clips) / Narrators Intro/Outro male around 30 english Narrator female around 30 english Pascal Monson male about 50 french Céline Allah female 20 french Pronunciation (German): [Ju-liE~ Adaïeh] (E~ = in, please ask a french native speaker) [Pas-kal MM~sM~] (M~ = on, please ask a french native speaker) [Celin Ala] 1

2 Intro: Hujambo na karibu katika sehemu ya tano kwenye mfululizo wa vipindi hivi vya Noa Bongo Jenga maisha yako kuhusu Haki za Binadamu. Haki za Binadamu ni kwa wote..ingawa " Uhuru wa binadamu ni haki ya kuzaliwa, na lazima kuwepo na usawa katika kudumisha hadhi na haki kwa wote, na hii ndio nguzo muhimu katika azimio hili la Umoja wa Mataifa, kwamba kila binadamu, ana uhuru na uwezo wa kutumia azimio hili kudai haki na uhuru kama inavyobainishwa kwenye azimio hilo. Haki hizi zimeangaziwa katika kifungu nambari 1 na 2 ambavyo ni msingi wa azimio hili. Kifungu nambari 26, kinaeleza kwamba kila binadamu ana haki ya kupata elimu bora. Hii ni mongoni mwa haki ambazo haziheshimiwi hasa miongoni mwa mataifa mengi barani Afrika. Je, nini kinaweza kufanya kuhakikisha haki ya elimu inaimarishwa na kudumishwa kwa wote? Julien Adayé [Ju-liE~ Adaïeh] amesafiri hadi nchini Côte D'Ivoire kuchunguza zaidi suala hili. 1. Narrator Kila mmoja ana haki ya kupata elimu bora. Kifungu nambari 26 katika azimio hili la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu, kinasema kuwa kila mmoja ana haki ya kupata elimu ya msingi. Lakini tatizo kubwa ni kwamba haki ya elimu bora haidumishwi au mara nyingi inapuuzwa katika mataifa mengi ulimwenguni, kwasababu ya kukosa ufahamu au ukosefu wa fedha. Na matokeo yake, idadi kubwa ya watu hawawezi kusoma na kuandika. Mfano nchini Côte D Ivoire, asilimia 51 ya idadi ya watu waliotimu miaka 15 na zaidi nchini humo hawajui kusoma na 2

3 kuandika. Watoto wengi wanakosa kwenda shule na kisha kujutia baadaye. Hali hii imemtokea Céline Allah [Celin Ala], msichana wa miaka 20 hivi: 2. O-Ton ALLAH CELINE (French) Nilizaliwa katika kambi moja huko msituni. Babangu aliniambia kuwa si lazima wasichana waende shule kwasababu ni rahisi kupata mume na kuolewa. Wakati huo tayari mamangu alikuwa ametengana na babangu. Ninahuzunika sana ninapowaona wasichana wengine wakienda shule. Mara nyingi unashindwa kujieleza kwa marafiki zako. Na hili ndilo jambo linalonitia machungu zaidi. 3. Narrator Céline hayuko peke yake. Takwimu zinaonyesha kuwa elimu ya msichana imepuuzwa zaidi kuliko ile ya mvulana. Jumla ya asilimia 40 ya wavulana nchini Côte D Ivoire, hawawezi kusoma na kuandika. Yapo mashirika mengi nchini humo ambayo yamejitolea kuhakikisha kuwa kiwango cha kutojua kusoma na kuandika, kinashuka nchini Cote D Ívoire. Shirika la ABC limekuwa likiendesha shughuli zake nchini humo kwa muda mrefu sana, na makao yake makuu yapo katikati mwa mji wa Cocody mashariki mwa mji mkuu Abidjan. Hapa tunakutana na Pascal Monson [Pas-kal Mo~so~], mshirikishi wa shirika la ABC na anatuelezea kuhusu taaluma yake: 4. O-Ton MONSON PASCAL Nimefanya kazi katika sekta hii ya elimu tangu mwaka wa 1983, nikiwa mfanyakazi serikalini. Nimefanya kazi hii kwa zaidi ya miaka 8 kabla ya serikali kunipeleka kufundisha shule ya msingi, ambako nilifunza kwa muda wa miaka miwili kisha kuhamishwa hadi shule ya sekondari jijini. 3

4 Siku moja nilipokuwa nikifundisha, nilikutana na mwanafunzi ambaye hakujua kusoma wala kuandika. Baada ya kujiunga na shule alitokwa na machozi ya furaha siku alipopata cheti kwa kufuzu mtihani wake wa mwisho. Na hii ilinipa msukumo wa kuendelea kuwasaidia watu kujua kusoma na kuandika, ili waweze kuwa watu wa kutegemewa katika jamii. 5. Narrator Kujua kusoma na kuandika, ni ufunguo wa maisha bora, kwani inatoa fursa kwa mtu kuendeleza taaluma unayopenda maishani na kuwa mtu wa kuheshimiwa katika jamii. Mfano kusoma barua na ujumbe mfupi wa simu ya mkononi, kwa wengi huwa ni kiyama. Licha ya matatizo yanayomkumba Celine anafahamu vyema teknolojia ya kisasa ya mawasiliano. Kama wasichana wengine wa rika lake, ana simu ya mkononi ingawa hajui kusoma wala kuandika. Je, huwa anaitumia vipi hasa anapopokea ujumbe kwenye simu yake? 6. O-Ton ALLAH CELINE (French) Siwezi kusoma wala kuandika ujumbe mimi husaidiwa na rafiki zangu. Ni jambo linalonisikitisha sana hasa wanaponisomea ujumbe kwenye simu yangu kutoka kwa mpenzi wangu, lakini nitafanyaje! Ilinibidi nimweleza mchumba wangu kwamba siwezi kusoma na kuandika. Na siku hizi yeye hunipigia simu tu. 7. Narrator Watu ambao hawawezi kusoma na kuandika hawataki kuonekana ni washamba. Wanataka kuwa na simu ya mkononi kama Céline, na kisha baadaye kujifunza pole pole namna ya kukitumia kifaa hicho. Mfano 4

5 msichana huyu amevumbua mbinu ya kuhifadhi nambari za simu za watu ana kuwapa watu namba yake. 8. O-Ton ALLAH CELINE (French) Huwa naandika nambari hizi kwa karatasi au kadi ndogo zenye maelezo. Na ninazo nyingi kwenye mkoba wangu, huwa nazipeana kwa watu wanaponiuliza nambari zanhu za simu. Na kisha huwa nawapa simu yangu ili waweze kuandika nambari zao pia. 9. Narrator Shirika hili la ABC linadhamiria kuwapa elimu watu wasiojua kusoma na kuandika, ili kukabiliana na changamoto hizi. Ingawa halina darasa hata moja, limeweka mikakati ya kufanikisha azma hii. Anasema Pascal Monson [Pas-kal Mo~so~]. 10. O-Ton MONSON PASCAL (FRENCH) Tuko na wanafunzi 50, ambao wamejiunga na elimu ya watu wazima. Tunatoa huduma zetu kwa awamu tatu. awamu ya kwanza kuanzia saa nne hadi saa sita, ya pili saa tisa hadi kumi na moja jioni na ya mwisho saa kumi na mbili hadi saa mbili usiku. Masomo haya yamegawanywa katika vitengo vitatu, kitengo cha elimu ya msingi, kwa watu wasiojua kabisa kusoma na kuandika, kisha kitengo cha pili cha kundi la wanaoelewa kidogo kidogo yaani kuanzia mwaka mmoja hadi miaka miwili na kitengo cha tatu wale ambao wamejua kusoma na kuandikamwaka mmoja hadi miwili. 11. Narrator Mfumo huu wa elimu unaambatana na ule wa kitaifa nchini Cote D Ivoire ambapo wanafunzi wanaojiunga na masomo kwa mara ya kwanza 5

6 wanajifunza jinsi ya kusoma herufi na nambari, na kisha kuanza kusoma kuandika na kuhesabu. 12. ATMO : Literacy classes 13. Narrator Wanapokamilisha masomo hupewa vyeti vya kuhitimu elimu ya msingi. Mafunzo yanayotolewa na shirika la ABC humgharimu mtu kiasi cha faranga 2000 kila mwezi, kiasi sawa na shilingi elfu sita hivi. Kiwango hiki bado ni cha gharama ya juu sana hasa ikizingatiwa pato la mtu wa kawaida la faranga 500 kwa siku yaani chini ya shilingi elfu mbili nchini Cote D Ivoire. Kwa hivyo, si familia nyingi zinaweza kumudu gharama hii. Hata hivyo, lakini ili kuweza kuwasaidia watu wengi zaidi wanaotaka kujiunga na masomo, mashirika yasiyo ya kiserikali yameimarisha juhudi za kutafuta ufadhili kutoka nje. Wakati wa sherehe za kuadhimisha siku ya kujua kusoma na kuandika, wizara ya elimu nchini humo ilitangaza mipango ya kupunguza kiwango cha kutojua kusoma na kuandika kutoka asilimia 51 hadi asilimia 35 ifikapo mwaka 2020, na kwamba itashirikiana na mashirka mengine kutimiza lengo hili. Tayari mashirika yasiyo ya kiserikali yameimarisha juhudi za kuwahamasisha watu kuhusu umuhimu wa kujua kusoma na kuandika na hapa tena ni Pascal Monson [Pas-kal Mo~so~] : 14. O-Ton MONSON PASCAL (FRENCH) Hivi majuzi serikali ilitangaza kwamba kiwango cha kutojua kusoma na kuandika kimefikia asilimia 51- kiwango hiki kiko juu sana. Hii nikumaanisha kwamba nusu ya idadi ya watu nchini humu hawajui kusoma na kuandika. Na ndio sababu hivi majuzi serikali iliyaalika 6

7 mashirika yasiyo ya kiserikali kwenye warsha iliyokusudiwa kupigana na vita dhidi ya kutojua kusoma na kuandika. Tulihudhuria warsha hiyo na wizara ilionyesha moyo na kuahidi kuendelea kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali katika kupambana na vita hivi nchini Cote D Ivoire. 15. Narrator Matamshi haya ya Pascal Monson [Pas-kal Mo~so~] yanawiana na yale ya wizara ya elimu nchini humo. HUshirikiana katika kuhakikisha haki ya kujua kusoma na kuandika inatekelezwa. lakini mpango huu utaweza kufaya kazi vipi? 16. O-Ton MONSON PASCAL (FRENCH) Mfano iwapo shirika lisilo la kiserikali linataka kusaidia katika kuimarisha kiwango cha elimu, serikali huwa inasaidia kwa kufungua milango ya taasisi zake hasa katika sehemu ambazo miradi hiyo inatekelezwa, mfano katika shule za umma. Katika sehemu hizi Wizara ya Elimu inashirikiana kwa karibu na mashirika haya, kwa msaada unaohitajika 17. Narrator Pia wizara hutoa misada ya kifedha ili kufadhili elimu ya watu wazima mbali na kutoa kandarasi kwa mashirika haya. 18. O-Ton MONSON PASCAL (FRENCH) Pia shule nyingi za kibinafsi huwa tayari kusaidia katika kuimarisha elimu ya watu wazima nchini Côte d Ivoire. Kunapotokea kandarasi kubwa, wizara hiyo ya elimu huyaalika mashirika yasiyo ya kiserikali ili yaweze kutekeleza kandarasi hiyo na kulipwa faida kidogo. Pia, kuna kitengo maalum katika wizara hiyo kilichobuniwa kushughulikia elimu ya watu wazima nchini humo Côte D Ivoire. Kitengo hiki hushirikiana na mashirika yasiyo ya serikali kupunguza kiwango hiki ya kutojua kusoma 7

8 na kuandika. Ama kwa hakika kifungu nambari 26 kwenye azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu kinazingatiwa hapa nchini. 19. Narrator Céline pia anataka kuona kifungu hiki Cha 26 kinazingatiwa kikamilifu sio tu nchini Côte D Ivoire bali kote Barani Afrika. Pia mama huyu ana hamu sana ya kuendelea na elimu ya watu wazima lakini hawezi kugharamia masomo hayo na pia kupata muda wa kufanya kazi zake. Lengo kubwa ni kutoa hamasa kwa wazazi kutilia mkazo elimu ya watoto wao, kwani hangependa kuwaona watoto wengine katika hali hii. 20. O-Ton ALLAH CELINE Mtu ambaye hajui kusoma na kuandika ni kama kipofu. Huwa si rahisi kufahamu mambo maishani. Na mimi nisingependa kuona watoto wengine wakipata shida kama mimi. Ni mrembo ndio, lakini siwezi kujieleza, jambo linalonisikitisha sana. Nawahimiza wazazi kuwapeleka watoto wao shuleni. 21. Narrator Kwa kufanya hivyo, kunawapa nafasi nzuri ya kuwa na maisha bora. Kifungu cha 26 kwenye azimio hili kinasema kuwa, Elimu inafaa kudumishwa kwa wote kwa lengo la kustawisha maendeleo ya binadamu na kwa kuheshimu na kuzingatia misingi ya uhuru na haki za binadamu Outro Iwapo serikali ina nia njema na kwa ushirikiano wa mashirika yasiyo ya kiserikali, kila mmoja anaweza kupata elimu bora. Na kwa ripoti hii iliyotayarishwa na Julien Adayé, ndipo tunapokamilisha sehemu ya tano ya mfululizo wa vipindi vya Noa Bongo, Jenga maisha yako kuhusu haki za binadamu. Asante kwa kutusikiliza na endapo ungetaka 8

9 kukisikiliza tena kipindi hiki, tembelea mtandao wetu wa dw.de / lbe. Hadi wakati mwengine tutakapokutana tena kwa makala nyingine, kwaheri kwa sasa! 9

Information for assessors (do not distribute this page to participants):

Information for assessors (do not distribute this page to participants): R&P Cultural Orientation Model Assessment Written Version Swahili Information for assessors (do not distribute this page to participants): This written version of the Model Cultural Orientation (CO) Assessment

More information

Pronunciation: Mä-hret Zäläke Ndal-ka-tscho Molla Mare Gebre-gzabiär 1/12

Pronunciation: Mä-hret Zäläke Ndal-ka-tscho Molla Mare Gebre-gzabiär 1/12 Human Rights Are Universal And Yet... Episode 07 Title : The right to food drought and famine in Ethiopia Author : Tedla Getachew Editor : Aude Gensbittel, Pendo Paul Translator : Anne Thomas Proofreader:

More information

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013 www.xtremepapers.com UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level *9257224991* SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013 Additional Materials: Answer Booklet/Paper

More information

JAMHURI YA KENYA. Mkakati wa Ushirikiano MUKHTASARI FY Public Disclosure Authorized. Public Disclosure Authorized

JAMHURI YA KENYA. Mkakati wa Ushirikiano MUKHTASARI FY Public Disclosure Authorized. Public Disclosure Authorized horized Public Disclosure Authorized Public Disclosure Authorized Public Disclosure Authorized JAMHURI YA KENYA Mkakati wa Ushirikiano FY2014-2018 MUKHTASARI Mkakati wa Ushirikiano wa Jamhuri ya Kenya

More information

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti Mradi wa kujua kuhusu Pesa Aprili 2011 FLP - Swahili Mradi wa kujua kuhusu Pesa Ipindi vyetu vya maelezo vya bure, warsha na kozi hutoa fursa ya kujifunza kuhusu

More information

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu The Human Rights Centre Uganda Azimio la Mkutano Mkuu 53/144 (8 Machi 1999) Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu AZIMIO KUHUSU HAKI NA WAJIBU WA MTU BINAFSI, VIKUNDI NA JUMUIYA

More information

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani HakiElimu: Mfululizo wa Mada za Uchambuzi Namba. 2003.4S Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere 1 Rakesh

More information

UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA)

UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA) Empowered lives. Resilient nations. UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA) Kenya Miradi ya Equator Wanafijiji na Maendeleo Himili ya Jamii MIRADI YA UNDP EQUATOR Kote duniani, jamiii zinazidi kubuni

More information

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO UTANGULIZI International Montessori Teachers College (IMTC), ni chuo kilichoanzishwa hapa nchini Tanzania mwaka 2012 na kinatoa kozi ya kimataifa ya ualimu wa watoto wadogo (yaani child care and nursery

More information

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23) GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER (Made under Section 23) THE ELECTRICITY (STANDARDIZED SMALL POWER PROJECTS TARIFF) ORDER, 2015 Citation 1. This Order may be cited

More information

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU TANZANIA EDUCATION NETWORK / MTANDAO WA ELIMU TANZANIA () 1.0 USULI Tanzania, sawa na nchi nyingine, ilitia saini Malengo ya Maendeleo ya Milenia na Malengo ya

More information

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23) GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER (Made under Section 23) THE ELECTRICITY (STANDARDIZED SMALL POWER PROJECTS TARIFF) ORDER, 2016 citation 1. This Order may be cited

More information

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO MPANGO KAZI WA USHIRIKI WA MTOTO TANZANIA 2014-2019 JANUARI, 2014 Dibaji Kwa mujibu wa takwimu za Sensa ya Taifa ya Idadi

More information

Deutsche Welle, Learning by Ear 2009 Seite 1 People Who Make A Difference Liberia: Anita Varney Health Facilitator, Fishtown/Liberia

Deutsche Welle, Learning by Ear 2009 Seite 1 People Who Make A Difference Liberia: Anita Varney Health Facilitator, Fishtown/Liberia Deutsche Welle, Learning by Ear 2009 Seite 1 Title: Anita Varney Health Facilitator, Fishtown/Liberia Author: Stefanie Duckstein, HA Afrika/ Nahost Editor: Christine Harjes Translator: Tony Dunham Sound

More information

SautiElimu. Sauti Yako Isikike

SautiElimu. Sauti Yako Isikike SautiElimu Sauti Yako Isikike SautiElimu Sauti Yako Isikike Mtayarishaji : Godfrey Telli Mchangiaji : Robert Mihayo Mhariri : Rakesh Rajani Shukrani za dhati kwa timu ya waandaaji wa SautiElimu 1-10: Lilian

More information

Kiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika

Kiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika Kiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika Stephen N. Kamau Abstract It is a fact that in the recent past, globalization has gradually taken shape in Africa and as such the continent has no choice but to

More information

Kuwafikia waliotengwa

Kuwafikia waliotengwa Kuwafikia waliotengwa Kuwafikia waliotengwa Muhtasari Chapisho la UNESCO 2 M U H T A S A R I R I P O T I Y A U S I M A M I Z I W A K I M A T A I F A W A M R A D I W A E L I M U K W A W O T E 2 0 1 0 Ripoti

More information

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada? Policy brief TZ.12/2010K Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada? 1. Utangulizi Kila mwaka Bunge la Tanzania hupitia na kuchanganua kwa makini bajeti ya Serikali.

More information

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E) 102/3 KISWAHILI KARATASI YA 3 Fasihi Julai/Agosti 2013 MUDA : SAA 2 ½ Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E) Kiswahili Karatasi 3 Julai/ Agosti Muda: Saa 2 ½ MAAGIZO: Andika jina lako na nambari yako

More information

LBE 2009 Migration Episode 3: Living without documents

LBE 2009 Migration Episode 3: Living without documents LBE 2009 Migration Episode 3: Living without documents Author: Marta Barroso Editor: Thomas Mösch Characters: Narrator 1: female Narrator 2: male Inserts (English): male, (42) Voice ( Passport, please!,

More information

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania Nordic Journal of African Studies 16(1): 18 29 (2007) Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania ABSTRACT This paper has attempted

More information

Elimukombozi, Lugha na Upashanaji Habari nchini Tanzania, katika Muktadha wa Utandawazi

Elimukombozi, Lugha na Upashanaji Habari nchini Tanzania, katika Muktadha wa Utandawazi Elimukombozi, Lugha na Upashanaji Habari nchini Tanzania, katika Muktadha wa Utandawazi Martha Qorro 1 1.0 Utangulizi Elimu ni suala la jamii ambalo mipango na taratibu zake zinahitaji kushirikisha wadau

More information

Kufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007

Kufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007 Kufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007 1. Utangulizi Changamoto kuu iliyopo kuhusiana na Elimu ya msingi nchini Tanzania kwa sasa ni namna

More information

Ufundishaji wa lugha nyingine

Ufundishaji wa lugha nyingine CHUO CHA ELIMU CHA KIMATAIFA OFISI YA ELIMU YA KIMATAIFA Ufundishaji wa lugha nyingine Na Elizabeth B. Bernhardt ELIMU MAZOEA KITABU NA. 20 1 Chuo cha Elimu cha Kimataifa (The International Academy of

More information

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig KITINI CHA JINSI YA KUTUMIA MFUMO WA SIMU YA KIGANJANI KATI YA BARAZA LA FAMASI NA WAMILIKI WA MADUKA NA WATAALAMU WA DAWA YALIYOMO UTANGULIZI... 3 SEHEMU YA KWANZA: MALIPO YA KUHUISHA VIBALI... 4 1.1

More information

Nilikua na Ndoto ya Kumaliza Shule Changamoto za Elimu ya Sekondari Tanzania

Nilikua na Ndoto ya Kumaliza Shule Changamoto za Elimu ya Sekondari Tanzania Nilikua na Ndoto ya Kumaliza Shule Changamoto za Elimu ya Sekondari Tanzania Kwa toleo neno la waraka huu, tafadhali email:crd@hrw.org FEBRUARI 2017 ISBN: 978-1-6231-34464 Nilikua na Ndoto ya Kumaliza

More information

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA

More information

ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA UCHUMI WA ZANZIBAR

ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA UCHUMI WA ZANZIBAR ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA UCHUMI WA ZANZIBAR MUHTASARI WA RIPOTI YA YA MWISHO. JULY 2012 for Page i Muhtasari Utafiti huu wa athari za Mabadiliko ya Tabianchi kwa uchumi Zanzibar umetoa tathmini

More information

Kutetea Haki za Binadamu

Kutetea Haki za Binadamu Kutetea Haki za Binadamu Kitabu cha Marejeo kwa watetezi wa Haki za Binadamu Toleo la pili i Kutetea Haki za Binadamu: Kitabu cha Marejeo kwa watetezi wa Haki za Binadamu (Toleo la pili) 2012 East and

More information

Tufundishane! Mwalimu Bora In this issue: Issue 6, December Do you want to be in our next issue?

Tufundishane! Mwalimu Bora In this issue: Issue 6, December Do you want to be in our next issue? Tufundishane! Let s teach each other! This newsletter is published by The Foundation for Tomorrow and is meant to be a venue for teachers and schools to share and learn from each other s best practices.

More information

LUGHA YA KISWAHILI KATIKA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA ELIMU SHULE ZA SEKONDARI

LUGHA YA KISWAHILI KATIKA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA ELIMU SHULE ZA SEKONDARI LUGHA YA KISWAHILI KATIKA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA ELIMU SHULE ZA SEKONDARI SIKOMBE YIZUKANJI YORADI TASNIFU YA KISWAHILI KWA MINAJILI YA KUTUNUKIWA SHAHADA YA UZAMILI (MA. KISWAHILI) KITIVO CHA SANAA

More information

Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi

Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi HakiElimu: Mfululizo wa Mada za Uchambuzi Namba. 2003. 6S Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari

More information

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA 2007 i WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA

More information

Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2013

Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2013 W N S E Muhtasari Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2013 Kuinuka kwa Nchi za Kusini: Maendeleo ya Binadamu katika Ulimwengu Anuwai Empowered lives. Hati ya kunakili 2013 na Mradi wa Maendeleo ya Umoja wa

More information

KUWEZESHA MBINU ZA UZUIAJI MIMBA KATIKA SUHULA ZA AFYA: MASWALI 10 KWA VIKUNDI VYA JAMII KUZINGATIA

KUWEZESHA MBINU ZA UZUIAJI MIMBA KATIKA SUHULA ZA AFYA: MASWALI 10 KWA VIKUNDI VYA JAMII KUZINGATIA KUWEZESHA MBINU ZA UZUIAJI MIMBA KATIKA SUHULA ZA AFYA: MASWALI 10 KWA VIKUNDI VYA JAMII KUZINGATIA Toleo la kwanza 2012 Mwandishi: USAID DELIVER PROJECT Wachangiaji: Gary Steele, John Snow, Inc. and Judith

More information

5. Mheshimiwa Spika, Bunge lako Tukufu lilijadili kwa kina Miswada ifuatayo:

5. Mheshimiwa Spika, Bunge lako Tukufu lilijadili kwa kina Miswada ifuatayo: HOTUBA YA MHESHIMIWA MIZENGO PETER PINDA (MB), WAZIRI MKUU, WAKATI WA KUTOA HOJA YA KUAHIRISHA MKUTANO WA KUMI NA MBILI WA BUNGE DODOMA TAREHE 29 AGOSTI 2008 UTANGULIZI 1. Mheshimiwa Spika, leo ni takriban

More information

MAADHIMISHO YA MIAKA 15 YA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

MAADHIMISHO YA MIAKA 15 YA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY HABARI ISSN 1821-5335 Makala Maalum Miaka 15 ya Foundation for Civil Society MAADHIMISHO YA MIAKA 15 YA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY Uwezeshaji wa moja ya sekta madhubuti za asasi za kiraia barani Afrika

More information

UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU VIKWAZO VYA KULINDA MAISHA KATIKA USAIDIZI WA KIMATAIFA WA AFYA KWA MSAADA WA KIMATAIFA UNAOFADHILIWA NA MAREKANI

UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU VIKWAZO VYA KULINDA MAISHA KATIKA USAIDIZI WA KIMATAIFA WA AFYA KWA MSAADA WA KIMATAIFA UNAOFADHILIWA NA MAREKANI UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU VIKWAZO VYA KULINDA MAISHA KATIKA USAIDIZI WA KIMATAIFA WA AFYA KWA MSAADA WA KIMATAIFA UNAOFADHILIWA NA 30 SEPTEMBA, 2017 UTANGULIZI Tarehe 23 Januari, 2017, Rais Donald Trump

More information

MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA. Kwa Wanaoanza

MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA. Kwa Wanaoanza 1 Matumizi bora ya Facebook kwa Biashara MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA Kwa Wanaoanza For IT Services & Web Solutions Web: Email: info@dudumizi.com Phone: 0768816728 2 Matumizi bora ya Facebook kwa

More information

Elimu-Jumuishi Kwa Vitendo

Elimu-Jumuishi Kwa Vitendo Elimu-Jumuishi Kwa Vitendo Taarifa ya Warsha Kuhusu Elimu-Jumuishi Iliyofanyika Zanzibar, 7-10 Februari 2006 Kujifunza hakuna mwisho. Kazi ya vikundi imenipa fursa ya kujieleza bila kuhofia kuwa ningekosea.

More information

Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame M. Mbarawa (Mb.); Waheshimiwa Mawaziri na Wabunge wote mliohudhuria;

Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame M. Mbarawa (Mb.); Waheshimiwa Mawaziri na Wabunge wote mliohudhuria; HOTUBA YA BALOZI MHANDISI JOHN W.H. KIJAZI, KATIBU MKUU KIONGOZI, WAKATI WA UFUNGUZI WA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAHANDISI KWA MWAKA 2017, UKUMBI WA JAKAYA KIKWETE, DODOMA, SEPTEMBA 7, 2017 Mheshimiwa Waziri

More information

Uzio wa pilipili unazuia tembo kuvamia mazao shambani! Jinsi ya kujenga na kudumisha uzio wa pilipili Tanzania

Uzio wa pilipili unazuia tembo kuvamia mazao shambani! Jinsi ya kujenga na kudumisha uzio wa pilipili Tanzania Uzio wa pilipili unazuia tembo kuvamia mazao shambani! Jinsi ya kujenga na kudumisha uzio wa pilipili Tanzania Jinsi ya kujenga na kudumisha uzio wapilipili Tanzania Wildlife Division, Tanzania Wildlife

More information

Ufanisi katika Ufundishaji kwenye Shule za Msingi na Sekondari nchini Tanzania

Ufanisi katika Ufundishaji kwenye Shule za Msingi na Sekondari nchini Tanzania Ufanisi katika Ufundishaji kwenye Shule za Msingi na Sekondari nchini Tanzania Desemba 2014 1 Shukurani Ripoti hii iliandikwa na Dk. Mkumbo. Ushauri wa kitaalamu ulitolewa na Elizabeth Missokia na Godfrey

More information

TAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF) KUHUSU HAKI ZA WATOTO KATIKA KATIBA MPYA

TAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF) KUHUSU HAKI ZA WATOTO KATIKA KATIBA MPYA TAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF) KUHUSU HAKI ZA WATOTO KATIKA KATIBA MPYA Marekebisho ya 23 January 2013 YALIYOMO KURASA TAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF)... 0 KUHUSU HAKI ZA WATOTO... 0

More information

TANZANIA MARKETS PAN Sera zinazoboresha masoko

TANZANIA MARKETS PAN Sera zinazoboresha masoko TANZANIA MARKETS PAN Sera zinazoboresha masoko UPOTEVU WA MAZAO YA NAFAKA BAADA YA MAVUNO: CHANGAMOTO NA UBORESHAJI Usuli Kuna makubaliano ya jumla kwamba marekebisho ya sera zinazohusu sekta ya kilimo,

More information

JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1

JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1 The Human Rights Centre Uganda JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1 AZIMIO LA KIMATAIFA JUU YA HAKI ZA KIBINADAMU SURA YA NNE YA KATIBA YA JAMHURI YA UGANDA YA 1995: MASIMULIZI YALIYOFASIRIWA KWA URAHISI NA KUFUPISHWA

More information

Dibaji ya Mwenyekiti wa Kamati ya Pamoja ya Uongozi

Dibaji ya Mwenyekiti wa Kamati ya Pamoja ya Uongozi Dibaji ya Mwenyekiti wa Kamati ya Pamoja ya Uongozi Mwaka wa nne wa utekelezaji wa Mpango wa Msaada wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDAP 2011-2016) nchini Tanzania ulikuwa na mafanikio makubwa lakini

More information

Utangulizi wa ugonjwa wa shinikizo la damu

Utangulizi wa ugonjwa wa shinikizo la damu Utangulizi wa ugonjwa wa shinikizo la damu BLOOD PRESSURE UK Shinikizo la damu ndicho chanzo kikubwa cha ulemavu na vifo vya mapema kule Uingereza, kupitia kiharusi, mshtuko wa moyo na maradhi ya moyo.

More information

Vijana wanazungumza kuhusu ujinsia, maisha na uhusiano VIJANA WANAZUNGUMZA KUHUSU NGONO, MAISHA NA UHUSIANO. Training and Research Support Centre

Vijana wanazungumza kuhusu ujinsia, maisha na uhusiano VIJANA WANAZUNGUMZA KUHUSU NGONO, MAISHA NA UHUSIANO. Training and Research Support Centre Shangazi Stella Vijana wanazungumza kuhusu ujinsia, maisha na uhusiano VIJANA WANAZUNGUMZA KUHUSU NGONO, MAISHA NA UHUSIANO Training and Research Support Centre Zimbabwe Shangazi Stella Kiongozi cha Mwezeshaji

More information

JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI

JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI Mwongozo huu utatumika kama njia ya kuwafunza watafiti watakaohusika na utafiti unaohusu binadamu. Muongozo huu utatumika

More information

KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA

KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA KUWEZESHA Radio za kijamii Kutumia Tehama Mwongozo huu umeandaliwa ili kuvipa

More information

RIPOTI YA WARSHA KUHUSU HABARI KWA AJILI YA UWAJIBIKAJI

RIPOTI YA WARSHA KUHUSU HABARI KWA AJILI YA UWAJIBIKAJI International Records Management Trust RIPOTI YA WARSHA KUHUSU HABARI KWA AJILI YA UWAJIBIKAJI ukumbi wa British Council Tanzania Auditorium Machi 27-28, 2000 Dar es Salaam, Tanzania warsha imeandaliwa

More information

MAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI

MAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI MAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI MAKUBALIANO YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI Paris, 20 Oktoba 2005 Kongamano Kuu la Umoja wa Mataifa linalohusisha

More information

Usimulizi wa Riwaya ya Nyongo Mkalia Ini E. S. MOHOCHI University of Egerton, Kenya

Usimulizi wa Riwaya ya Nyongo Mkalia Ini E. S. MOHOCHI University of Egerton, Kenya Nordic Journal of African Studies 9(2): 49-59 (2000) Usimulizi wa Riwaya ya Nyongo Mkalia Ini E. S. MOHOCHI University of Egerton, Kenya UTANGULIZI Tukichunguza hazina ya uhakiki uliofanywa katika taaluma

More information

Kitabu Cha Mafunzo Ya Uongozi Kwa Wanawake

Kitabu Cha Mafunzo Ya Uongozi Kwa Wanawake Uongozi Bora Kitabu Cha Mafunzo Ya Uongozi Kwa Wanawake UONGOZI BORA Uongozi ni uwezo wa kubuni na kuyaweka maono katika vitendo. -Mshiriki katika Semina ya Mafunzo Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya

More information

MACHAGUO YA UZAZI KUFIKIRIA KUWA MZAZI

MACHAGUO YA UZAZI KUFIKIRIA KUWA MZAZI This booklet on Becoming a Parent was developed by the Tanzania Home Economics Association with support from Our Bodies Ourselves. Other booklets and more information on the project are available at. MACHAGUO

More information

Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara)

Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara) Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara) Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara) Hakimiliki Shirika la Kazi Duniani 2010 Toleo la kwanza 2010 Machapisho ya Ofisi

More information

HAKI NA TARATIBU ZA AJIRA, KAZI NA HIFADHI YA JAMII

HAKI NA TARATIBU ZA AJIRA, KAZI NA HIFADHI YA JAMII HAKI NA TARATIBU ZA AJIRA, KAZI NA HIFADHI YA JAMII SHERIA KATIKA LUGHA RAHISI KIMETOLEWA NA CHAMA CHA WANASHERIA TANZANIA BARA (TANGANYIKA LAW SOCIETY) KWA UFADHILI WA TAASISI YA LEGAL SERVICE FACILITY

More information

Ufunguo wa Kutaalamika Haraka

Ufunguo wa Kutaalamika Haraka 0 Ufunguo wa Kutaalamika Haraka Ufunguo wa Kutaalamika Haraka Kijitabu Kielelezo; Nakala ya Bila Malipo Yaliyomo 1 Yaliyomo Utangulizi...04 Habari Fupi Kuhusu...08 Fumbo la Ulimwengu wa Ng ambo ya Pili...11

More information

TIST HABARI MOTO MOTO MAANDALIZI YA MWAKA 2000 Y2K PREPARATIONS SASA NI WAKATI WA KUANZA KUPANDA MBEGU ZAKO

TIST HABARI MOTO MOTO MAANDALIZI YA MWAKA 2000 Y2K PREPARATIONS SASA NI WAKATI WA KUANZA KUPANDA MBEGU ZAKO TIST HABARI MOTO MOTO Tel. 026-2322246 P.O.BOX 53 MPWAPWA E-Mail tist@twiga.com 01 October 2000 Y2K PREPARATIONS Holes and Seedlings made ready for the year 2000 programme By Gayo Mhila The process of

More information

Kimesanifiwa na:- E.D.Kissuu ECOMM TANZANIA S.L.P ,Dar es Salaam. Simu:

Kimesanifiwa na:- E.D.Kissuu ECOMM TANZANIA S.L.P ,Dar es Salaam. Simu: Kimesanifiwa na:- E.D.Kissuu ECOMM TANZANIA S.L.P. 21425,Dar es Salaam. Simu: +255 713 607 207 edkissuu@gmail.com Katuni zimechorwa na: Adam Lutta Babatau Inc. Box 13565 Dar es salaam, Simu:+255 713 474200

More information

ORODHA YA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI SPIKA MHE. PANDU AMEIR KIFICHO. Rais.

ORODHA YA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI SPIKA MHE. PANDU AMEIR KIFICHO. Rais. ORODHA YA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI SPIKA MHE. PANDU AMEIR KIFICHO 1.Mhe. Kamal Basha Pandu 2.Mhe. Ali Mzee Ali 3.Mhe. Shamsi Vuai Nahodha Naibu Spika/Jimbo la Rahaleo. Mwenyekiti wa Baraza/Uteuzi

More information

TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM)

TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM) TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM) 2007-2017 TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM) 2007-2017 Kimetolewa na Sikika (Zamani YAV) S.L.P 12183 Dar Es Salaam

More information

Ndugu na dada zangu wapendwa,

Ndugu na dada zangu wapendwa, UJUMBE WA URAIS WA KWANZA, MEI 2014 Na Rais Thomas S. Monson Upendo Asili ya Injili Hakika hatuwezi kumpenda Mungu kama hatuwapendi wasafiri wenzetu katika safari hii ya maisha duniani. ninafurahia mawazo

More information

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA. Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo. TOLEO Na.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA. Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo. TOLEO Na. JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo TOLEO Na. 1, Desemba, 2012 Yaliyomo Orodha ya Vifupisho -------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------3

More information

HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE

HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE. JENISTA MHAGAMA (MB), KATIKA KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA AFYA NA USALAMA MAHALI PA KAZI DUNIANI DODOMA, 28 APRILI

More information

Dodoma ambako kikao cha Bunge kinaendelea kuja kushiriki japo sehemu ya uzinduzi wa mkutano.

Dodoma ambako kikao cha Bunge kinaendelea kuja kushiriki japo sehemu ya uzinduzi wa mkutano. HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. PHILIP I. MPANGO (MB) WAKATI WA UFUNGUZI WA MKUTANO WA KIMATAIFA WA KUJADILI MATUMIZI YA TAKWIMU ZA UMASKINI NA NAMNA BORA YA KUPIMA HALI YA UMASKINI AFRIKA,

More information

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora K I T A B U C H A M B I N U B O R A C H A T O A U k u r a s a 1 TANZANIA OSAKA ALUMNI Kitabu cha Mbinu Bora Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa P.O. Box 1923, Dodoma. Novemba, 2012

More information

TATHMINI YA PAMOJA SHULE ZA UPILI ZA JIMBO LA MACHAKOS.

TATHMINI YA PAMOJA SHULE ZA UPILI ZA JIMBO LA MACHAKOS. www.eeducationgroup.com JINA NAMBA YAKO...... SAHIHI YA MTAHINIWA... TAREHE:...... 102/1 KISWAHILI KARATASI YA 1 INSHA MUDA :SAA 1 ¾ TATHMINI YA PAMOJA SHULE ZA UPILI ZA JIMBO LA MACHAKOS. Hati ya kuhitimu

More information

Early Grade Reading Assessment for Kenya

Early Grade Reading Assessment for Kenya EDDATA II Early Grade Reading Assessment for Kenya Baseline Instruments: Kiswahili and English EdData II Technical and Managerial Assistance, Task Number 4 Contract Number EHC-E-01-04-00004-00 Strategic

More information

Kocha Mkuu. mabingwa. itakuwa INASTAHILI. Ili Kutoa mafunzo kwa wanafunzi wako kuwa. itakuwa ya kuumiza. Itachukua muda. Itahitaji moyo wa kujitoa.

Kocha Mkuu. mabingwa. itakuwa INASTAHILI. Ili Kutoa mafunzo kwa wanafunzi wako kuwa. itakuwa ya kuumiza. Itachukua muda. Itahitaji moyo wa kujitoa. Ili Kutoa mafunzo kwa wanafunzi wako kuwa mabingwa itakuwa ya kuumiza. Itachukua muda. Itahitaji moyo wa kujitoa. Mkuu Inahitaji dhabihu. Unahitaji kujisukuma hadi mwisho wako. Lakini nakupa ahadi hii,

More information

Kijitabu cha Maelezo cha Programu ya Famasia

Kijitabu cha Maelezo cha Programu ya Famasia IDARA YA KUFIKIA HUDUMA ZA AFYA VERMONT Kijitabu cha Maelezo cha Programu ya Famasia GreenMountainCare MIASHA YENYE AFYA BORA ZAIDI Jedwali la Yaliyomo Jedwali la Yaliyomo... 2 Karibu kwenye Programu ya

More information

usudi la Maisha Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na kupishana usiku na mchana, kuna kweli ishara kwa wenye akili, ambaye mkumbuke-

usudi la Maisha Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na kupishana usiku na mchana, kuna kweli ishara kwa wenye akili, ambaye mkumbuke- Kusudi la Maisha hawatakuambia nini walihitimisha kupitia uchunguzi au hoja ya uchambuzi. Katika hali nyingi, hakika wao kukuambia nini mtu mwingine alisema... Au wao watakuambia nini kawaida kudhaniwa

More information

Mazoezi yaliyofanyika wakati wa warsha kuhusu Elimu-Jumuishi kwa Vitendo. Zanzibar, 7-10 Februari 2006

Mazoezi yaliyofanyika wakati wa warsha kuhusu Elimu-Jumuishi kwa Vitendo. Zanzibar, 7-10 Februari 2006 Mazoezi yaliyofanyika wakati wa warsha kuhusu Elimu-Jumuishi kwa Vitendo Zanzibar, 7-10 Februari 2006 Imechapishwa na: The Atlas Alliance Schweigaardsgt 12 SLP 9218 Grønland 0134 Oslo, Norway Simu: +47

More information

March 14, 2018 PARLIAMENTARY DEBATES 1 NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL REPORT. Wednesday, 14 th March The House met at 9.30 a.m.

March 14, 2018 PARLIAMENTARY DEBATES 1 NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL REPORT. Wednesday, 14 th March The House met at 9.30 a.m. March 14, 2018 PARLIAMENTARY DEBATES 1 NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL REPORT Wednesday, 14 th March 2018 The House met at 9.30 a.m. [The Temporary Deputy Speaker (Hon. (Ms.) Mbalu) in the Chair] PRAYERS QUORUM

More information

HALIYA VITABUVYA WATOTOKATIKA TANZANIA

HALIYA VITABUVYA WATOTOKATIKA TANZANIA AAP 68 (2001)- Swahi1i Fomm Vill 171-183 HALIYA VITABUVYA WATOTOKATIKA TANZANIA J S. MADUMULLA Whither is fled the visionary gleam Where is it now, the glory and the dream Wapi kimekimbilia, kianga cha

More information

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH Eneo La Huduma: Huduma Ya Ushirika Wa Biashara Kichwa: Sera Ya Mipango Ya Msaada Wa Kifedha SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH Tarehe Kupitishwa: 09/20/2013 Tarehe Ya Ufanisi: 09/20/2013 1/1/2017

More information

Unyanyasaji wa Watoto & Kutelekezwa

Unyanyasaji wa Watoto & Kutelekezwa Child Abuse & Neglect 43(2015)8 21 Orodha Yaliyomo inapatikana katika ScienceDirect Unyanyasaji wa Watoto & Kutelekezwa Nakala ya Utafiti Mbinu za kuimarisha mifumo ya ulinzi wa mtoto kuanzia chini kwenda

More information

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU NA WAJIBU WA Serikali za Mitaa MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU NA WAJIBU WA Serikali za Mitaa Kimetayarishwa na Kikundi Kazi cha Serikali za Mitaa cha Policy Forum Kimehaririwa

More information

Azimio lililopitishwa na Mkutano Mkuu tarehe 18 Desemba 2013 [juu ya taarifa ya Kamati ya Tatu (A/68/456/Add.2)]

Azimio lililopitishwa na Mkutano Mkuu tarehe 18 Desemba 2013 [juu ya taarifa ya Kamati ya Tatu (A/68/456/Add.2)] This unofficial translation is provided by the International Service for Human Rights Umoja wa Mataifa A/AZI/68/ Ugaw Jumla Mkutano Mkuu 30 Januari 2014 Kikao cha Sitini na Nane Dondoo ya Ajenda 69(b)

More information

Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA 2006/07

Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA 2006/07 Mwongozo wa Lugha Rahisi wa Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA 2006/07 Mwongozo huu Umeandaliwa na Hakikazi Catalyst kwa niaba ya Wizara ya Fedha na Uchumi. Desemba 2007 Dibaji Ripoti ya Mwaka ya

More information

Kiu Cha umtafuta Mungu

Kiu Cha umtafuta Mungu ZAIDI YA NAKALA MILLION 3 ZIMECHAPISHWA KATIKA LUGHA 59 KOTE DUNIANI K Kiu Cha umtafuta Mungu Huduma ya Daktari Richard A. Bennett ilianza katika mabaraza ya miji. Akiwa mwanafunzi chuoni, alikumbana na

More information

Mhashamu Askofu Jude Thaddaeus Ruwa ichi, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania; Mwadhama Policarp Kardinali Pengo,

Mhashamu Askofu Jude Thaddaeus Ruwa ichi, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania; Mwadhama Policarp Kardinali Pengo, HOTUBA YA MHESHIMIWA MIZENGO P. PINDA (MB), WAZIRI MKUU, KWENYE SHEREHE YA KUADHIMISHA MIAKA HAMSINI YA BARAZA LA MAASKOFU KATOLIKI TANZANIA, TAREHE 08 JUNI 2008, MSIMBAZI CENTRE, DAR ES SALAAM Mhashamu

More information

Mwongozo wa Mafunzo Yaliyochanganywaya K4Health

Mwongozo wa Mafunzo Yaliyochanganywaya K4Health Mwongozo wa Mafunzo Yaliyochanganywaya K4Health Wasiojua kusoma na kuandika katika karne ya 21 hawatakuwa wale wasiojua kusoma na kuandika lakini wale ambao hawawezi kujifunza, kutojifunza na kujifunza

More information

Elimu Ina Umuhimu gani katika Jamii? Kuelekea Elimu Sahihi

Elimu Ina Umuhimu gani katika Jamii? Kuelekea Elimu Sahihi Elimu Ina Umuhimu gani katika Jamii? Kuelekea Elimu Sahihi Gervas Zombwe 1 1. Utangulizi Katika mazingira ya kawaida kabisa ndani ya jamii yetu, Imezoeleka kusikia au kuona watu wakioanisha dhana ya elimu

More information

KUSHUKA KWA HADHI YA LUGHA ZA JAMII NCHINI TANZANIA YOHANA P. MSANJILA University of Dar es Salaam, Tanzania

KUSHUKA KWA HADHI YA LUGHA ZA JAMII NCHINI TANZANIA YOHANA P. MSANJILA University of Dar es Salaam, Tanzania Nordic Journal of African Studies 12(3): 296 309 (2003) KUSHUKA KWA HADHI YA LUGHA ZA JAMII NCHINI TANZANIA YOHANA P. MSANJILA University of Dar es Salaam, Tanzania ABSTRACT Lugha za jamii hapa nchini

More information

KITEGO CHA MAREKEBISHO NA HAKI ZA MTOTO

KITEGO CHA MAREKEBISHO NA HAKI ZA MTOTO KITEGO CHA MAREKEBISHO NA HAKI ZA MTOTO Mwaka 2009 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha sheria mpya ya Mtoto ambayo ni sehemu ya juhudi za serikali za kuhakikisha kuwa haki na ustawi wa

More information

Mipango ya miradi katika udugu

Mipango ya miradi katika udugu Partnerschaftlich Projekte planen Mipango ya miradi katika udugu 2 Dibaji... 3 Utangulizi... 4 I. Nafasi ya (Wajibu wa) Fedha katika Udugu: Mtazamo wa Ki-indonesi... 5 II. Namna UEM Inavyowezesha Miradi

More information

UMRI WA MAKAMO NA KUKOMA KWA HEDHI

UMRI WA MAKAMO NA KUKOMA KWA HEDHI This booklet on menopause was developed by the Tanzania Home Economics Association with support from Our Bodies Ourselves. Other booklets and more information on the project are available at http://www.ourbodiesourselves.org/tanzania.

More information

Kuwawezesha wasichana kwa kuboresha kujikubali na kujithamini Hivi Ndivyo Nilivyo

Kuwawezesha wasichana kwa kuboresha kujikubali na kujithamini Hivi Ndivyo Nilivyo Kuwawezesha wasichana kwa kuboresha kujikubali na kujithamini Hivi Ndivyo Nilivyo Mazoezi ya wenye umri wa miaka 11-14 Hivi Ndivyo Nilivyo kwa wenye umri wa miaka 11-14 Kuhusu Hivi Ndivyo Nilivyo Ikiwa

More information

Mwongozo wa Utamaduni Toleo la Kwanza

Mwongozo wa Utamaduni Toleo la Kwanza Mwongozo wa Utamaduni Toleo la Kwanza Kubadilishana Tamaduni za Kijerumani na za Kitanzania Limeandaliwa na Anna Hoppenau, Johannes Hahn, Oliva Lyimo na Lisa Bendiek German-Tanzanian Partnership (DTP)

More information

April 14, 2016 COUNTY ASSEMBLY DEBATES 52

April 14, 2016 COUNTY ASSEMBLY DEBATES 52 MOMBASA COUNTY ASSEMBLY HANSARD REPORT Thursday, 14 th April, 2016 The House met at 2.48pm. (Hon. Deputy Speaker (Mr. Mswabah Rashid) in the Chair) PRAYERS Hon. Deputy Speaker (Mr. Mswabah Rashid): Kindly

More information

Yaliyomo. Kuhusu kitabu hiki. Hautakuwa peke yako. Mfumo wa msaada ni wa manufaa sana wazazi wote wanahitaji!

Yaliyomo. Kuhusu kitabu hiki. Hautakuwa peke yako. Mfumo wa msaada ni wa manufaa sana wazazi wote wanahitaji! Yaliyomo Kuhusu kitabu hiki Kuhusu kitabu hiki.........................................................1 Unapojisikia vibaya.........................................................2 Unapoanza kuwa mzima

More information

Summaries of GC Reports 2012, Vol. 2, Sec. 1, Swahili

Summaries of GC Reports 2012, Vol. 2, Sec. 1, Swahili Summaries of GC Reports 2012, Vol. 2, Sec. 1, Swahili 1. 2-Muhtasari wa Ukurasa wa Ripoti ya Miaka minne ya Bodi Kuu ya Kanisa & Jamii............................... 2 2. Kamati ya Kawaida ya Malipo ya

More information

HUDUMA ZA AFYA KWA WOTE

HUDUMA ZA AFYA KWA WOTE SAUTIZETU HUDUMA ZA AFYA KWA WOTE 01 SAUTIZETU HUDUMA ZA AFYA KWA WOTE SAUTI ZETU Huduma za Afya kwa wote THE OPEN SOCIETY INITIATIVE FOR EASTERN AFRICA (OSIEA) (JAMII WAZI YA MPANGO WA AFRIKA MASHARIKI)

More information

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA SIMU NA: (027) 2642082 TANGA (OFISI) 0784 889 099 TANGA (NYUMBANI) Tovuti: www.tangaschool.sc.tz Barua pepe: tangaschool@yahoo.com JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI HALMASHAURI YA

More information

Ellen White, waasisi wa Kiadventista,na Sabato Lunar

Ellen White, waasisi wa Kiadventista,na Sabato Lunar Ellen White, waasisi wa Kiadventista,na Sabato Lunar Ukristo leo unadhihirisha waumini karibu bilioni mbili katika maelfu ya madhehebu tofauti na tofauti na madhehebu. Kati ya hizi, zaidi ya 500 madhehebu

More information

UHUSIANO WA MIKAKATI YA UFUNDISHAJI WA FASIHI YA WATOTO YA KISWAHILI NA UMILISI WA KUSOMA KATIKA SHULE ZA MSINGI, KASARANI, KAUNTI YA NAIROBI, KENYA

UHUSIANO WA MIKAKATI YA UFUNDISHAJI WA FASIHI YA WATOTO YA KISWAHILI NA UMILISI WA KUSOMA KATIKA SHULE ZA MSINGI, KASARANI, KAUNTI YA NAIROBI, KENYA UHUSIANO WA MIKAKATI YA UFUNDISHAJI WA FASIHI YA WATOTO YA KISWAHILI NA UMILISI WA KUSOMA KATIKA SHULE ZA MSINGI, KASARANI, KAUNTI YA NAIROBI, KENYA NA SELINA RHOBI CHACHA E55/23475/11 TASNIFU HII IMEWASILISHWA

More information

Mwongozo wa Kutathimini mifumo ya Ugawanaji wa faida na Mapato Katika Miradi ya Jamii ya MKUHUMI

Mwongozo wa Kutathimini mifumo ya Ugawanaji wa faida na Mapato Katika Miradi ya Jamii ya MKUHUMI David M. Mwayafu, Richard Kimbowa, Kristy Graham Mwongozo wa Kutathimini mifumo ya Ugawanaji wa faida na Mapato Katika Miradi ya Jamii ya MKUHUMI Na: David M. Mwayafu, Richard Kimbowa (Uganda Coalition

More information

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA,KWA WANANCHI, 30 SEPTEMBA, 2001

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA,KWA WANANCHI, 30 SEPTEMBA, 2001 HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA,KWA WANANCHI, 30 SEPTEMBA, 2001 Leo napenda nizungumze nanyi, kwa lugha nyepesi iwezekanavyo, juu ya mahusiano tunayowania

More information