UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO

Size: px
Start display at page:

Download "UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO"

Transcription

1 UTANGULIZI International Montessori Teachers College (IMTC), ni chuo kilichoanzishwa hapa nchini Tanzania mwaka 2012 na kinatoa kozi ya kimataifa ya ualimu wa watoto wadogo (yaani child care and nursery school teachers), kwa ngazi ya cheti na diploma. Chuo hiki kimeanzishwa hapa nchini, ili kukidhi hitaji la upatikanaji wa walezi wa watoto na waalimu bora wa elimu ya awali wenye viwango na ubora unaokubalika kitaifa na kimataifa. ANUANI NA MANDHARI YA CHUO Chuo kimejengwa katika eneo tulivu na salama lililopo katika kijiji cha Mapinga, jirani na Daraja linalotenganisha Mkoa wa Dar es salam na Wilaya ya Bagamoyo. Aidha, chuo kina mazingira yaliyoandaliwa maalumu ili kumwezesha mwalimu mtarajiwa kupata ujuzi unaoendana na aina ya ujuzi anaoupata chuoni na kazi atakayoifanya mara baada ya kuhitimu mafunzo yake. KUTAMBULIKA KWA CHUO CHA IMTC International Montessori Teachers College (IMTC), tunatambuliwa na kushirikiana na Serikali jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuhakikisha tunaandaa walezi wa watoto na walimu wa elimu ya awali wenye elimu, ujuzi na viwango vya kitaifa na kimataifa katika stadi za malezi na ufundishaji wa watoto. Pia, tunao usajili wa kudumu wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (National Council for Technical Education). Naomba yetu ya usajili ni NACTE No. REG/TLF/012. Usajili huo unatuwezesha kutoa mafunzo ya ngazi ya cheti na diploma kwa walezi na walimu wa elimu ya awali kuanzia ngazi ya NTA Level 4 hadi NTA Level 6. Pia, chuo hiki kimesajiliwa na kinashirikiana na Wizara ya afya na Ustawi wa jamii kutoa mafunzo ngazi ya cheti, kwa kozi ya huduma ya malezi ya watoto.

2 Kusajiliwa, kutambulika na kushirikiana na taasisi za Serikali zinazosimamia elimu na malezi ya watoto kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, kunamhakikishia mhitimu katika IMTC mambo makuu matatu kama ifuatavyo:- (a) Ubora wa elimu inayotolewa, (b) Uhakika wa nafasi ya ajira mara baada ya kuhitimu katika shule za Serikali au katika shule zinazomilikiwa na watu binafsi ama taasisi na mashirika, (c) Fursa na uhuru wa kujiendeleza kwenye chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali kwa ajili ya masomo ya digrii, nk. MIFUMO YA UFUNDISHAJI Tunao wakufunzi wa ngazi na viwango vya kimataifa, wanaotumia mbinu na stadi zinazomwezesha kila mwanachuo kujitambua, kujiamini na kujipatia ujuzi wa malezi na ufundishaji wa watoto wadogo. Aidha, ufundishaji wetu unazingatia nadharia na vitendo kama ifuatavyo:- (a) Mafunzo ya nadharia ya Darasani Ufundishaji wa nadharia unaambatana na utumiaji wa mifumbo mbalimbali ya teknolojia kama vile powerpoint, video na oudio. Aidha, walimu wanatumia mbinu shirikishi na mijadala ili kuhakikisha kila mwanafunzi anafikiwa, anajifunza na kufikia malengo. (b) Mafunzo kwa vitendo ya namna ya kutumia vifaa kufundisha watoto Tunalo darasa maalumu lenye vifaa mbalimbali, tunalolitumia kufundisha kwa vitendo. Lengo likiwa ni kumwezesha kila mwanafunzi kujua namna ya kutumia vifaa mbalimbali kulea na kufundisha watoto. Aidha, uwepo wa darasa hilo unatoa uhuru kwa mwanachuo kutumia muda wake wa ziada kufanya mazoezi kwa vitendo kadri anavyoweza ili kuhakikisha anatimiza malengo yake ya kujizoeza, kupata ujuzi na kufaulu vizuri majaribio ya kitaaluma. (c) Mafunzo kwa vitendo ya namna ya kutengeneza vifaa vya kufundishia watoto Chuo kinaendesha mafunzo kwa vitendo kwa kuwafundisha wanafunzi jinsi ya kutengeneza seti za vifaa mbalimbali vya

3 kufundishia watoto. Vifaa hivyo ambavyo vina thamani ya zaidi ya milioni tano, mwanachuo uondoka navyo mara baada ya kuhitimu mafunzo ili aweze kujiajiri au kuvitumia mara anapokuwa ameajiriwa. Vifaa hivyo vyenye thamani ya zaidi ya milioni tano vimegawanyika katika makundi yafuatayo:- (i) (ii) (iii) (iv) (v) (vi) (vii) (viii) Vifaa vya kumjenga mtoto ili aweze kujitegemea katika maisha yake Vifaa vya kutafiti na kuchochea ukuaji wa milango ya fahamu ya mtoto Vifaa vya kumfundisha mtoto stazi za lugha na mawasilino Vifaa vya kumfundisha mtoto stadi za Hisabati Vifaa vya kumfundisha mtoto stadi za jiografia Vifaa vya kumfundisha mtoto stadi kuhusu mazingira Vifaa vya kumfundisha mtoto stadi za sayansi Vifaa vya kumfundisha mtoto asili na utamaduni (d) Mazoezi kwa vitendo shuleni Chuo kinamiliki na kuendesha shule ya awali ambayo uwawezesha wanachuo kujifunza kwa vitendo tabia, mienendo na malezi ya watoto. Pia, kwa kushirikiana na shule za awali washirika, chuo uwapangia wanachuo kufanya mafunzo ya mazoezi kwa vitendo chini ya uangalizi maalumu. Mazoezi hayo uwawezesha wanachuo kuimarisha ujuzi wao kwa vitendo kuhusu malezi ya watoto, mfumo wa ufundishaji wa watoto wadogo, utaratibu wa uendeshaji wa vituo vya kulea watoto na shule za awali, n.k. Utaratibu huu wa mazoezi kwa vitendo kwa wanachuo, pia ufungua milango ya uhakika wa fursa za ajira mara baada ya kuhitimu. Kwa

4 sababu waajiri na wamiliki wa shule upata fursa za kujua uwezo wa waajiriwa watarajiwa kabla ya kuingia katika soko la ajira. Pia, sifa na uwezo wa kila mwanachuo wa kumudu majukumu yake utambulika na kujulikana. UTARATIBU WA KUJIUNGA IMTC Mtu yeyote anayetaka kujiunga na International Montessori Teachers College (IMTC), anatakiwa kufika chuoni ili aweze:- (a) Kupata maelezo, kujionea na kujiridhisha (b) Kuchukua fomu ya maombi, kuijaza na kuirejesha kwa wakati (fomu inapatikana chuoni tu) (c) Kufanya mahojiano na majaribio ya kupima uwezo wa uelewa na mapenzi kwa watoto (d) Kukamilisha taratibu za kiutawala VIGEZO MUHIMU VINAVYOHITAJIKA Vigezo muhimu vinavyozingatiwa ili uchaguliwe kujiunga na International Montessori Teachers College (IMTC), ni:- (a) Kuwa mhitimu wa elimu ya sekondari, kidato cha nne au zaidi, (b) Mtu yeyote mwenye elimu ngazi ya cheti au zaidi (cheti kilichotolewa na taasisi au chuo kinachomilikiwa na Serikali au chuo kilichosajiliwa na kutambuliwa na Serikali), (c) Au mwenye cheti cha kuhitimu mafunzo ya malezi ya watoto kinachotolewa na Idara ya Ustawi wa Jamii, (d) Mwenye wito wa kulea na kufundisha watoto, (e) Kwa wanafunzi wa kigeni:-

5 Chuo chetu ni cha viwango vya kimataifa, hivyo kinatoa fursa kwa raia wa kigeni kujiunga na kozi zinazotolewa. Utaratibu wa kujiunga kwa raia wa kigeni umefafanuliwa katika kurasa za website yetu. Hata hivyo, ni muhimu pia kufahamu kwamba mhitimu katika chuo chetu anakuwa na misingi ya viwango, vigezo na uwezo wa kufanya kazi katika nyanja aliyoisomea popote duniani. KOZI ZITOLEWAZO Chuo kinatoa kozi za ualimu wa watoto wadogo kama ifuatavyo: 1. Diploma ya ualimu na malezi ya watoto Kozi hii ni ya muda wa miaka miwili (2), na ina masomo yafuatayo:- Child Development Teaching Methodology School Management Safety And First Aid Communication skills Education philosophy General knowledge Nutrition Mathematics Arts and raft Language- English and Kiswahili Leadership Health Civics Moja ya faida za kusoma kozi hii ni kuwezeshwa kuwa na ujuzi kamili wa kutengeneza vifaa vya kulea na kufundishia watoto. Pia mwanachuo akihitimu umilikishwa na kuruhusiwa kuondoka na vifaa vyote alivyovitengeneza wakati wa mafunzo. 2. Cheti cha ualimu na malezi ya watoto Kozi hii ni ya muda wa mwaka mmoja (1), na ina masomo yafuatayo:- Child Development

6 Safety And First Aid Communication skills Education philosophy Montessori philosophy General knowledge Health & Nutrition Arts and raft Language- English and Kiswahili Civics Kozi hii haiambatani na utengenezaji wa vifaa vya kulea na kufundisha watoto. MFUMO WA KUPIMA UWEZO NA UELEWA - MITIHANI Mitihani ya kupima uelewa na ujuzi ni asilimia 100%. Asilimia hizi hupatikana kwa njia mbili, nazo ni jumla ya mazoezi na majaribio yote ya nadharia na vitendo ni 80% na mtihani wa mwisho wa mwaka ukamilisha alama 20% ili kutimia 100% UJUZI MWINGINE UNAOTOLEWA CHUONI Mafunzo ya ICT Chuo kinatoa mafunzo ya matumizi ya kompyuta bure kwa kila mwanachuo. Mafunzo haya yanalenga kumpa ujuzi wa ziada na kumwandaa mwanachuo kutumia ICT katika mfumo wa ufundishaji na kujifunza. Aidha, utaratibu huu unamwezesha mwanachuo kuwa ni mlezi na mwalimu anayekwenda kwa wakati kwa kuzingatia mifumo ya kisasa ya elimu, habari na mawasiliano. Pia, mfumo huu unatoa fursa kwa kila mwanachuo kutumia rasilimali hizo kutafuta taarifa mbalimbali zinazohusiana na masomo yake. Ujasiliamali na stadi za maisha Kwa kuzingatia mahitaji ya ajira na kujiajiri, chuo kinaendesha mafunzo maalumu yanayomjengea uwezo mwanachuo ili aweze kujiajiri mara baada ya kuhitimu. Utaratibu huu maalumu unamwezesha mwanachuo kujitambua,

7 kujiamini na kutumia fursa za ujuzi anaopewa ili kuwa chachu ya mabadiliko katika mfumo wa maisha yenye changamoto ya kukosekana kwa ajira. Aidha, mfumo wetu wa ufundishaji ni wa aina ya pekee na unazingatia mbinu ya elimu ya kujitegemea. Pia unamjenga na kumwezesha mwanachuo kuwa na ujuzi wa kutengeneza vifaa vya kufundishia ambavyo ni nyezo na mtaji wa kuweza kumudu kuanzisha kituo kwa ajili ya kutoa elimu ya awali kwa watoto. Vile vile mwanachuo anapewa mafunzo maalumu yanayomwezesha kutoa huduma ya ushauri nasaha kwa watoto na wazazi kuhusu ustawi na maendeleo ya watoto. Mafunzo ya upigaji picha kwa njia ya video Kila mwachuo anafundishwa ujuzi wa kutumia vifaa vya kisasa ili kuchukua na kuhifadhi kumbukumbu za watoto kwa njia ya picha, video na sauti. Utaratibu huu unazingatia ukweli kwamba, kila aliyefanikiwa hapa duniani amepitia katika mikono ya walezi na walimu walipo katika shule hasa za awali, ingawa kumbukumbu za walio wengi hazikuwekwa au kuhifadhiwa. Hivyo ili kukidhi hitaji hilo la kuweka kumbukumbu za watoto, chuo kimejenga studio za kisasa zenye vifaa vinavyotambulika kwa ubora ulimwenguni kwa lengo la kufanikisha utoaji wa ujuzi huo na kumwandaa mwanachuo kuweza kuchukua na kuhifadhi kumbukumbu za matukio muhimu ya watoto wanaopita mikononi mwake katika mchakato mzima wa malezi. Matuki hayo ni kama vile kumbukumbu za siku za kuzaliwa za watoto wa shule yake, kumbukumbu za mahafali, n.k Sanaa na ubunifu Moja ya misingi na aiba ya mlezi na mwalimu wa watoto wadogo, ni kuwa na vipaji vya ubunifu na sanaa. Ubunifu katika ufundishaji wa watoto unaoambatana na michezo na sanaa mbalimbali, urahisisha mfumo wa uamishaji wa maarifa na ujuzi kutoka kwa mwalimu kwenda kwa watoto. Hivyo, mkakati wa IMTC ni pamoja na kumwandaa mwanachuo kutumia michezo, sanaa na ubunifu katika kulea na kuwafundisha watoto. Lakini pia

8 unamjengea mwalimu na mlezi mtarajiwa uwezo wa stadi za kutambua vipaji vya watoto na mbinu za kuviendeleza. Huduma ya kwanza na usalama wa watoto Moja ya mafunzo yanatolewa katika mtaala wa masomo ni suala la ulinzi wa watoto, huduma ya kwanza na uokoaji. Mafunzo hayo humjengea mwanachuo stadi za tahadhari. Lakini pia umjengea uwezo wa kiufahamu wa hatua za kuchukua katika kukabiliana na ajali au majanga mbalimbali. ADA International Montessori Teachers College (IMTC), kwa kutambua mahitaji ya jamii kulingana na kipato cha Watanzania walio wengi, tumeweka utaratibu wa ulipaji wa ada unaozingatia uwezo wa kila mwanafunzi. Hivyo, ulipaji wa ada kidogo kidogo unajadiliwa na kuruhusiwa. HUDUMA NYINGINE MUHIMU ZINAZOTOLEWA NA CHUO Chuo kinamiliki hosteli nzuri yenye hadhi iliyojengwa katika mazingira ya chuo na huduma hii hutolewa bure kwa kila mwanachuo. Aidha, mazingira ya vyumba vya kulala ni mazuri na yenye vitanda na magodoro na huduma nyingine muhimu kama vile:- Maji safi na salama Umeme wa uhakika Ulinzi Viwanja vya michezo Chakula, nk.

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA 2007 i WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA

More information

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA

More information

Information for assessors (do not distribute this page to participants):

Information for assessors (do not distribute this page to participants): R&P Cultural Orientation Model Assessment Written Version Swahili Information for assessors (do not distribute this page to participants): This written version of the Model Cultural Orientation (CO) Assessment

More information

Kufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007

Kufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007 Kufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007 1. Utangulizi Changamoto kuu iliyopo kuhusiana na Elimu ya msingi nchini Tanzania kwa sasa ni namna

More information

KITEGO CHA MAREKEBISHO NA HAKI ZA MTOTO

KITEGO CHA MAREKEBISHO NA HAKI ZA MTOTO KITEGO CHA MAREKEBISHO NA HAKI ZA MTOTO Mwaka 2009 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha sheria mpya ya Mtoto ambayo ni sehemu ya juhudi za serikali za kuhakikisha kuwa haki na ustawi wa

More information

Tufundishane! Mwalimu Bora In this issue: Issue 6, December Do you want to be in our next issue?

Tufundishane! Mwalimu Bora In this issue: Issue 6, December Do you want to be in our next issue? Tufundishane! Let s teach each other! This newsletter is published by The Foundation for Tomorrow and is meant to be a venue for teachers and schools to share and learn from each other s best practices.

More information

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23) GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER (Made under Section 23) THE ELECTRICITY (STANDARDIZED SMALL POWER PROJECTS TARIFF) ORDER, 2016 citation 1. This Order may be cited

More information

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO MPANGO KAZI WA USHIRIKI WA MTOTO TANZANIA 2014-2019 JANUARI, 2014 Dibaji Kwa mujibu wa takwimu za Sensa ya Taifa ya Idadi

More information

Nilikua na Ndoto ya Kumaliza Shule Changamoto za Elimu ya Sekondari Tanzania

Nilikua na Ndoto ya Kumaliza Shule Changamoto za Elimu ya Sekondari Tanzania Nilikua na Ndoto ya Kumaliza Shule Changamoto za Elimu ya Sekondari Tanzania Kwa toleo neno la waraka huu, tafadhali email:crd@hrw.org FEBRUARI 2017 ISBN: 978-1-6231-34464 Nilikua na Ndoto ya Kumaliza

More information

Ufanisi katika Ufundishaji kwenye Shule za Msingi na Sekondari nchini Tanzania

Ufanisi katika Ufundishaji kwenye Shule za Msingi na Sekondari nchini Tanzania Ufanisi katika Ufundishaji kwenye Shule za Msingi na Sekondari nchini Tanzania Desemba 2014 1 Shukurani Ripoti hii iliandikwa na Dk. Mkumbo. Ushauri wa kitaalamu ulitolewa na Elizabeth Missokia na Godfrey

More information

Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi

Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi HakiElimu: Mfululizo wa Mada za Uchambuzi Namba. 2003. 6S Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari

More information

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA III VI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA III VI JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA III VI JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA

More information

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23) GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER (Made under Section 23) THE ELECTRICITY (STANDARDIZED SMALL POWER PROJECTS TARIFF) ORDER, 2015 Citation 1. This Order may be cited

More information

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani HakiElimu: Mfululizo wa Mada za Uchambuzi Namba. 2003.4S Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere 1 Rakesh

More information

TANZANIA MARKETS PAN Sera zinazoboresha masoko

TANZANIA MARKETS PAN Sera zinazoboresha masoko TANZANIA MARKETS PAN Sera zinazoboresha masoko UPOTEVU WA MAZAO YA NAFAKA BAADA YA MAVUNO: CHANGAMOTO NA UBORESHAJI Usuli Kuna makubaliano ya jumla kwamba marekebisho ya sera zinazohusu sekta ya kilimo,

More information

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU TANZANIA EDUCATION NETWORK / MTANDAO WA ELIMU TANZANIA () 1.0 USULI Tanzania, sawa na nchi nyingine, ilitia saini Malengo ya Maendeleo ya Milenia na Malengo ya

More information

Dibaji ya Mwenyekiti wa Kamati ya Pamoja ya Uongozi

Dibaji ya Mwenyekiti wa Kamati ya Pamoja ya Uongozi Dibaji ya Mwenyekiti wa Kamati ya Pamoja ya Uongozi Mwaka wa nne wa utekelezaji wa Mpango wa Msaada wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDAP 2011-2016) nchini Tanzania ulikuwa na mafanikio makubwa lakini

More information

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig KITINI CHA JINSI YA KUTUMIA MFUMO WA SIMU YA KIGANJANI KATI YA BARAZA LA FAMASI NA WAMILIKI WA MADUKA NA WATAALAMU WA DAWA YALIYOMO UTANGULIZI... 3 SEHEMU YA KWANZA: MALIPO YA KUHUISHA VIBALI... 4 1.1

More information

TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM)

TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM) TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM) 2007-2017 TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM) 2007-2017 Kimetolewa na Sikika (Zamani YAV) S.L.P 12183 Dar Es Salaam

More information

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu The Human Rights Centre Uganda Azimio la Mkutano Mkuu 53/144 (8 Machi 1999) Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu AZIMIO KUHUSU HAKI NA WAJIBU WA MTU BINAFSI, VIKUNDI NA JUMUIYA

More information

Elimu Ina Umuhimu gani katika Jamii? Kuelekea Elimu Sahihi

Elimu Ina Umuhimu gani katika Jamii? Kuelekea Elimu Sahihi Elimu Ina Umuhimu gani katika Jamii? Kuelekea Elimu Sahihi Gervas Zombwe 1 1. Utangulizi Katika mazingira ya kawaida kabisa ndani ya jamii yetu, Imezoeleka kusikia au kuona watu wakioanisha dhana ya elimu

More information

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA. Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo. TOLEO Na.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA. Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo. TOLEO Na. JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo TOLEO Na. 1, Desemba, 2012 Yaliyomo Orodha ya Vifupisho -------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------3

More information

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU NA WAJIBU WA Serikali za Mitaa MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU NA WAJIBU WA Serikali za Mitaa Kimetayarishwa na Kikundi Kazi cha Serikali za Mitaa cha Policy Forum Kimehaririwa

More information

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA SIMU NA: (027) 2642082 TANGA (OFISI) 0784 889 099 TANGA (NYUMBANI) Tovuti: www.tangaschool.sc.tz Barua pepe: tangaschool@yahoo.com JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI HALMASHAURI YA

More information

Elimu-Jumuishi Kwa Vitendo

Elimu-Jumuishi Kwa Vitendo Elimu-Jumuishi Kwa Vitendo Taarifa ya Warsha Kuhusu Elimu-Jumuishi Iliyofanyika Zanzibar, 7-10 Februari 2006 Kujifunza hakuna mwisho. Kazi ya vikundi imenipa fursa ya kujieleza bila kuhofia kuwa ningekosea.

More information

JAMHURI YA KENYA. Mkakati wa Ushirikiano MUKHTASARI FY Public Disclosure Authorized. Public Disclosure Authorized

JAMHURI YA KENYA. Mkakati wa Ushirikiano MUKHTASARI FY Public Disclosure Authorized. Public Disclosure Authorized horized Public Disclosure Authorized Public Disclosure Authorized Public Disclosure Authorized JAMHURI YA KENYA Mkakati wa Ushirikiano FY2014-2018 MUKHTASARI Mkakati wa Ushirikiano wa Jamhuri ya Kenya

More information

Songa kwenye kilele cha upeo. Masuala ya Msingi na Ujuzi juu ya Uendeshaji wa Serikali za Mitaa

Songa kwenye kilele cha upeo. Masuala ya Msingi na Ujuzi juu ya Uendeshaji wa Serikali za Mitaa Songa kwenye kilele cha upeo Masuala ya Msingi na Ujuzi juu ya Uendeshaji wa Serikali za Mitaa Masuala ya Msingi na Ujuzi juu ya Uendeshaji wa Serikali za Mitaa United Republic of Tanzania Photos provided

More information

Ufundishaji wa lugha nyingine

Ufundishaji wa lugha nyingine CHUO CHA ELIMU CHA KIMATAIFA OFISI YA ELIMU YA KIMATAIFA Ufundishaji wa lugha nyingine Na Elizabeth B. Bernhardt ELIMU MAZOEA KITABU NA. 20 1 Chuo cha Elimu cha Kimataifa (The International Academy of

More information

5. Mheshimiwa Spika, Bunge lako Tukufu lilijadili kwa kina Miswada ifuatayo:

5. Mheshimiwa Spika, Bunge lako Tukufu lilijadili kwa kina Miswada ifuatayo: HOTUBA YA MHESHIMIWA MIZENGO PETER PINDA (MB), WAZIRI MKUU, WAKATI WA KUTOA HOJA YA KUAHIRISHA MKUTANO WA KUMI NA MBILI WA BUNGE DODOMA TAREHE 29 AGOSTI 2008 UTANGULIZI 1. Mheshimiwa Spika, leo ni takriban

More information

Mwongozo wa Mwezeshaji

Mwongozo wa Mwezeshaji JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII Ushauri Nasaha na Upimaji wa VVU kwa Hiari Mwongozo wa Mwezeshaji Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI Machi 2010 Kimetafsiriwa kutoka lugha

More information

FOMU YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO

FOMU YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO FOMU YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO SEHEMU A (TAARIFA ZA MWANAFUNZI) Picha ya mwanafunzi na aje na picha tatu Jina kamili (majina matatu). Tarehe ya kuzaliwa.. Uraia.. Jinsia Anuani ya mwanafunzi... Shule

More information

Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame M. Mbarawa (Mb.); Waheshimiwa Mawaziri na Wabunge wote mliohudhuria;

Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame M. Mbarawa (Mb.); Waheshimiwa Mawaziri na Wabunge wote mliohudhuria; HOTUBA YA BALOZI MHANDISI JOHN W.H. KIJAZI, KATIBU MKUU KIONGOZI, WAKATI WA UFUNGUZI WA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAHANDISI KWA MWAKA 2017, UKUMBI WA JAKAYA KIKWETE, DODOMA, SEPTEMBA 7, 2017 Mheshimiwa Waziri

More information

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada? Policy brief TZ.12/2010K Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada? 1. Utangulizi Kila mwaka Bunge la Tanzania hupitia na kuchanganua kwa makini bajeti ya Serikali.

More information

LUGHA YA KISWAHILI KATIKA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA ELIMU SHULE ZA SEKONDARI

LUGHA YA KISWAHILI KATIKA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA ELIMU SHULE ZA SEKONDARI LUGHA YA KISWAHILI KATIKA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA ELIMU SHULE ZA SEKONDARI SIKOMBE YIZUKANJI YORADI TASNIFU YA KISWAHILI KWA MINAJILI YA KUTUNUKIWA SHAHADA YA UZAMILI (MA. KISWAHILI) KITIVO CHA SANAA

More information

Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara)

Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara) Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara) Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara) Hakimiliki Shirika la Kazi Duniani 2010 Toleo la kwanza 2010 Machapisho ya Ofisi

More information

Makala ya Mshiriki wa Mafunzo

Makala ya Mshiriki wa Mafunzo JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII Ushauri Nasaha na Upimaji wa VVU kwa Hiari Makala ya Mshiriki wa Mafunzo Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI Machi 2010 Kimetafsiriwa kutoka

More information

NGUZO KUMI ZA KILIMO KWANZA

NGUZO KUMI ZA KILIMO KWANZA NGUZO KUMI ZA KWANZA (MFUMO WA UTEKELEZAJI) NGUZO YA 1 DIRA YA TAIFA YA KWANZA 1.1 Kupitisha Dira ya KWANZA SHUGHULI MAJUKUMU MUDA MHUSIKA MKUU 1. AZIMIO LA KWANZA 2. mpango wa utekelezaji wa KWANZA 3.

More information

Miradi na jamii. 3.1 Utangulizi

Miradi na jamii. 3.1 Utangulizi 3.1 Utangulizi Miradi na jamii Lengo la sura hii ni mapitio ya mazingira pana ambayo chini ya ardhi kwa ajili ya maendeleo vijijini upatikanaji wa maji inafaa. majadiliano wakapanga meneja, au kiongozi

More information

KUSHUKA KWA HADHI YA LUGHA ZA JAMII NCHINI TANZANIA YOHANA P. MSANJILA University of Dar es Salaam, Tanzania

KUSHUKA KWA HADHI YA LUGHA ZA JAMII NCHINI TANZANIA YOHANA P. MSANJILA University of Dar es Salaam, Tanzania Nordic Journal of African Studies 12(3): 296 309 (2003) KUSHUKA KWA HADHI YA LUGHA ZA JAMII NCHINI TANZANIA YOHANA P. MSANJILA University of Dar es Salaam, Tanzania ABSTRACT Lugha za jamii hapa nchini

More information

MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA PRO-ROUTES. Ombi kwa ajili ya fedha za umma wa mradi wa ziada

MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA PRO-ROUTES. Ombi kwa ajili ya fedha za umma wa mradi wa ziada Public Disclosure Authorized Public Disclosure Authorized Public Disclosure Authorized Public Disclosure Authorized Résumé non technique Version Swahili MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA

More information

HALMASHAURI YA WILAYA YA SUMBAWANGA

HALMASHAURI YA WILAYA YA SUMBAWANGA HALMASHAURI YA WILAYA YA SUMBAWANGA E- mail: uchilesekondari@yahoo.com P.O. BOX 582 Mob: +255 (0) 752 476 389 SUMBAWANGA KUMB. NA. USS/JOINING/F.V/03 10 Juni 2017...... YAH: MAAGIZO YA KUJIUNGA NA KIDATO

More information

SautiElimu. Sauti Yako Isikike

SautiElimu. Sauti Yako Isikike SautiElimu Sauti Yako Isikike SautiElimu Sauti Yako Isikike Mtayarishaji : Godfrey Telli Mchangiaji : Robert Mihayo Mhariri : Rakesh Rajani Shukrani za dhati kwa timu ya waandaaji wa SautiElimu 1-10: Lilian

More information

Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA 2006/07

Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA 2006/07 Mwongozo wa Lugha Rahisi wa Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA 2006/07 Mwongozo huu Umeandaliwa na Hakikazi Catalyst kwa niaba ya Wizara ya Fedha na Uchumi. Desemba 2007 Dibaji Ripoti ya Mwaka ya

More information

Human Rights Are Universal And Yet...

Human Rights Are Universal And Yet... Human Rights Are Universal And Yet... Episode 05 Title : The right to education Author : Julien Adayé Editor : Aude Gensbittel Translator : Anne Thomas, Eric Ponda Proofreader: Pendo Paul Characters (sounds,

More information

Sera ya Faragha. Upeo. Aina za Data na Mbinu za Ukusanyaji

Sera ya Faragha. Upeo. Aina za Data na Mbinu za Ukusanyaji Sera ya Faragha Katika Sera hii ya Faragha ( Sera ), sisi, Qualcomm Incorporated na makampuni yetu tanzu (kwa pamoja sisi au yetu ), tunatoa maelezo kuhusu jinsi tunavyokusanya, kutumia, kuchakata, na

More information

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA HOTUBA YA WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO MHESHIMIWA SOPHIA M. SIMBA (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2013/14 DODOMA Mei,

More information

Mwongozo wa Utekelezaji wa Njia za S5-UUE (KAIZEN)-UUU Tanzania

Mwongozo wa Utekelezaji wa Njia za S5-UUE (KAIZEN)-UUU Tanzania Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Mwongozo wa Utekelezaji wa Njia za S5-UUE (KAIZEN)-UUU Tanzania Msingi wa Programu zote za Uimarishaji Ubora Toleo la 1 kwa Lugha ya Kiswahili

More information

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu WEMA

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu WEMA Maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu WEMA TWN Third World Network 1. WEMA ni nini? Mahindi yanayotumia maji kwa ufanisi yajulikanayo kwa kingereza kama Water Efficient Maize for Africa (WEMA) ni mpango

More information

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara Umetayarishwa na Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania kwa Kushirikiana na Idara ya Maendeleo

More information

Mazoezi yaliyofanyika wakati wa warsha kuhusu Elimu-Jumuishi kwa Vitendo. Zanzibar, 7-10 Februari 2006

Mazoezi yaliyofanyika wakati wa warsha kuhusu Elimu-Jumuishi kwa Vitendo. Zanzibar, 7-10 Februari 2006 Mazoezi yaliyofanyika wakati wa warsha kuhusu Elimu-Jumuishi kwa Vitendo Zanzibar, 7-10 Februari 2006 Imechapishwa na: The Atlas Alliance Schweigaardsgt 12 SLP 9218 Grønland 0134 Oslo, Norway Simu: +47

More information

UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU VIKWAZO VYA KULINDA MAISHA KATIKA USAIDIZI WA KIMATAIFA WA AFYA KWA MSAADA WA KIMATAIFA UNAOFADHILIWA NA MAREKANI

UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU VIKWAZO VYA KULINDA MAISHA KATIKA USAIDIZI WA KIMATAIFA WA AFYA KWA MSAADA WA KIMATAIFA UNAOFADHILIWA NA MAREKANI UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU VIKWAZO VYA KULINDA MAISHA KATIKA USAIDIZI WA KIMATAIFA WA AFYA KWA MSAADA WA KIMATAIFA UNAOFADHILIWA NA 30 SEPTEMBA, 2017 UTANGULIZI Tarehe 23 Januari, 2017, Rais Donald Trump

More information

MAPENDEKEZO YA MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA TANZANIA

MAPENDEKEZO YA MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA TANZANIA MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA MAPENDEKEZO YA MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA TANZANIA KUHUSU JINSI YA KUINGIZA MASUALA YA USAWA WA JINSIA KATIKA RASIMU YA PILI YA KATIBA YA TANZANIA KWA NINI MISINGI YA USAWA

More information

4. Kanuni za Petroli (Ushiriki wa Watanzania) za mwaka 2017 zilianza kutumika rasmi tarehe 5 Novermba Shughuli za Petroli za kwanza ni

4. Kanuni za Petroli (Ushiriki wa Watanzania) za mwaka 2017 zilianza kutumika rasmi tarehe 5 Novermba Shughuli za Petroli za kwanza ni MWONGOZO WA JINSI YA KUWASILISHA MAOMBI YA KUWEKWA KWENYE KANZIDATA YA WATANZANIA WENYE UWEZO WA KUUZA BIDHAA AU KUTOA HUDUMA (LSSP) KWENYE SHUGHULI ZA MAFUTA NA GESI ASILIA NCHINI Utangulizi 1. Mamlaka

More information

Programu ya Uendelezaji Mifumo ya Maji Vijijini (PUMMV) katika Tanzania. Modeli wa Ukodishaji Mradi

Programu ya Uendelezaji Mifumo ya Maji Vijijini (PUMMV) katika Tanzania. Modeli wa Ukodishaji Mradi Programu ya Uendelezaji Mifumo ya Maji Vijijini (PUMMV) katika Tanzania Modeli wa Ukodishaji Mradi Programu ya Uendelezaji Mifumo ya Maji Vijijini (PUMMV) Programu ya Uendelezaji Mifumo ya Maji Vijijini

More information

MITAZAMO KUHUSU KISWAHILI MIONGONI MWA WAZUNGUMZAJI WA KIJALUO: KIFANI CHA SHULE ZA MSINGI KATIKA KAUNTI YA MIGORI. OWALA JAEL AKINYI C50/75493/2012

MITAZAMO KUHUSU KISWAHILI MIONGONI MWA WAZUNGUMZAJI WA KIJALUO: KIFANI CHA SHULE ZA MSINGI KATIKA KAUNTI YA MIGORI. OWALA JAEL AKINYI C50/75493/2012 MITAZAMO KUHUSU KISWAHILI MIONGONI MWA WAZUNGUMZAJI WA KIJALUO: KIFANI CHA SHULE ZA MSINGI KATIKA KAUNTI YA MIGORI. OWALA JAEL AKINYI C50/75493/2012 TASNIFU HII IMEWASILISHWA KUTOSHELEZA BAADHI YA MAHITAJI

More information

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH Eneo La Huduma: Huduma Ya Ushirika Wa Biashara Kichwa: Sera Ya Mipango Ya Msaada Wa Kifedha SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH Tarehe Kupitishwa: 09/20/2013 Tarehe Ya Ufanisi: 09/20/2013 1/1/2017

More information

Draft 03 MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO MWENGE

Draft 03 MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO MWENGE MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO MWENGE MPANGO MKAKATI WA MIAKA MITANO WA MAENDELEO YA KANISA 2013-2017 i YALIYOMO 1. UTANGULIZI... 1 1.1 Lengo kuu... 1 1.2 Historia kwa ufupi... 1 1.3 Malengo ya

More information

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013 www.xtremepapers.com UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level *9257224991* SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013 Additional Materials: Answer Booklet/Paper

More information

UHUSIANO WA MIKAKATI YA UFUNDISHAJI WA FASIHI YA WATOTO YA KISWAHILI NA UMILISI WA KUSOMA KATIKA SHULE ZA MSINGI, KASARANI, KAUNTI YA NAIROBI, KENYA

UHUSIANO WA MIKAKATI YA UFUNDISHAJI WA FASIHI YA WATOTO YA KISWAHILI NA UMILISI WA KUSOMA KATIKA SHULE ZA MSINGI, KASARANI, KAUNTI YA NAIROBI, KENYA UHUSIANO WA MIKAKATI YA UFUNDISHAJI WA FASIHI YA WATOTO YA KISWAHILI NA UMILISI WA KUSOMA KATIKA SHULE ZA MSINGI, KASARANI, KAUNTI YA NAIROBI, KENYA NA SELINA RHOBI CHACHA E55/23475/11 TASNIFU HII IMEWASILISHWA

More information

MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2017/18

MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2017/18 MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2017/18 WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO NOVEMBA, 2016 ISBN 978-9987 - 829-02 - 9 ii YALIYOMO 1.0 UTANGULIZI... 1 2.0 MABORESHO YA MFUMO WA KIBAJETI... 2

More information

Kutetea Haki za Binadamu

Kutetea Haki za Binadamu Kutetea Haki za Binadamu Kitabu cha Marejeo kwa watetezi wa Haki za Binadamu Toleo la pili i Kutetea Haki za Binadamu: Kitabu cha Marejeo kwa watetezi wa Haki za Binadamu (Toleo la pili) 2012 East and

More information

KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA

KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA KUWEZESHA Radio za kijamii Kutumia Tehama Mwongozo huu umeandaliwa ili kuvipa

More information

RIPOTI YA WARSHA KUHUSU HABARI KWA AJILI YA UWAJIBIKAJI

RIPOTI YA WARSHA KUHUSU HABARI KWA AJILI YA UWAJIBIKAJI International Records Management Trust RIPOTI YA WARSHA KUHUSU HABARI KWA AJILI YA UWAJIBIKAJI ukumbi wa British Council Tanzania Auditorium Machi 27-28, 2000 Dar es Salaam, Tanzania warsha imeandaliwa

More information

Kitabu Cha Mafunzo Ya Uongozi Kwa Wanawake

Kitabu Cha Mafunzo Ya Uongozi Kwa Wanawake Uongozi Bora Kitabu Cha Mafunzo Ya Uongozi Kwa Wanawake UONGOZI BORA Uongozi ni uwezo wa kubuni na kuyaweka maono katika vitendo. -Mshiriki katika Semina ya Mafunzo Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya

More information

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO Tel. +255748-537720/632013, P.O.BOX 6049 MOROGORO E-Mail info@ tist.org April 2004 Take care of your seedlings This year, thousands of seedlings have been planted in the TIST

More information

3. Mheshimiwa Spika, 4. Mheshimiwa Spika,

3. Mheshimiwa Spika, 4. Mheshimiwa Spika, HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI, MHESHIMIWA JOHN POMBE MAGUFULI, (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2007/08 UTANGULIZI 1. Mheshimiwa

More information

UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA)

UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA) Empowered lives. Resilient nations. UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA) Kenya Miradi ya Equator Wanafijiji na Maendeleo Himili ya Jamii MIRADI YA UNDP EQUATOR Kote duniani, jamiii zinazidi kubuni

More information

KAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI TANZANIA

KAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI TANZANIA KAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI TANZANIA KAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI TANZANIA NI UFUMBUZI KATIKA KUSHIRIKISHA JAMII? NI UFUMBUZI KATIKA KUSHIRIKISHA JAMII? Februari, 2013 Februari, 2013 SHUKURANI

More information

Kumb.Na.BSS/A.6/33 Tarehe: 18 Juni 2018 YAH: MAAGIZO YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2018/2019

Kumb.Na.BSS/A.6/33 Tarehe: 18 Juni 2018 YAH: MAAGIZO YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2018/2019 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Shule ya Sekondari Bagamoyo Simu ya mkononi: +255 769 397 926 : +255 658

More information

Mwongozo wa Mafunzo Yaliyochanganywaya K4Health

Mwongozo wa Mafunzo Yaliyochanganywaya K4Health Mwongozo wa Mafunzo Yaliyochanganywaya K4Health Wasiojua kusoma na kuandika katika karne ya 21 hawatakuwa wale wasiojua kusoma na kuandika lakini wale ambao hawawezi kujifunza, kutojifunza na kujifunza

More information

MAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI

MAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI MAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI MAKUBALIANO YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI Paris, 20 Oktoba 2005 Kongamano Kuu la Umoja wa Mataifa linalohusisha

More information

Azimio lililopitishwa na Mkutano Mkuu tarehe 18 Desemba 2013 [juu ya taarifa ya Kamati ya Tatu (A/68/456/Add.2)]

Azimio lililopitishwa na Mkutano Mkuu tarehe 18 Desemba 2013 [juu ya taarifa ya Kamati ya Tatu (A/68/456/Add.2)] This unofficial translation is provided by the International Service for Human Rights Umoja wa Mataifa A/AZI/68/ Ugaw Jumla Mkutano Mkuu 30 Januari 2014 Kikao cha Sitini na Nane Dondoo ya Ajenda 69(b)

More information

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI-TAMISEMI HALMASHAURI YA WILAYA BUMBULI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI-TAMISEMI HALMASHAURI YA WILAYA BUMBULI JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI-TAMISEMI HALMASHAURI YA WILAYA BUMBULI NAMBA ZA SIMU: Mkuu Wa Shule: 0784524029 / 0766805826. Makamu Mkuu Wa Shule: 0714356735 / 0767356735. SHULE YA SEKONDARI

More information

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, MHESHIMIWA DKT. PHILIP I. MPANGO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, MHESHIMIWA DKT. PHILIP I. MPANGO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, MHESHIMIWA DKT. PHILIP I. MPANGO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA 2018/19 1 I. UTANGULIZI 1. Mheshimiwa

More information

YAH: MAAGIZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI KAREMA KIDATO CHA TANO MWAKA 2018

YAH: MAAGIZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI KAREMA KIDATO CHA TANO MWAKA 2018 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA SHULE YA SEKONDARI KAREMA Namba za simu: Mkuu wa shule: 0763414888/0784244108

More information

Elimukombozi, Lugha na Upashanaji Habari nchini Tanzania, katika Muktadha wa Utandawazi

Elimukombozi, Lugha na Upashanaji Habari nchini Tanzania, katika Muktadha wa Utandawazi Elimukombozi, Lugha na Upashanaji Habari nchini Tanzania, katika Muktadha wa Utandawazi Martha Qorro 1 1.0 Utangulizi Elimu ni suala la jamii ambalo mipango na taratibu zake zinahitaji kushirikisha wadau

More information

Kumb.Na.HVEMS/JI/BT/018 Novemba 17, YAH: MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE CHINI YA TAASISI YA ROCK MEMORIAL EDUCATION TRUST 2018

Kumb.Na.HVEMS/JI/BT/018 Novemba 17, YAH: MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE CHINI YA TAASISI YA ROCK MEMORIAL EDUCATION TRUST 2018 Hills View Catholic Diocese of Tanga Magunga District Hospital Road Mob:+255-784808420, +255 718 661681, +255 714901004 www.rmet.ac.tz, email: saroce2013@gmail.com KOROGWE, TANZANIA Kumb.Na.HVEMS/JI/BT/018

More information

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora K I T A B U C H A M B I N U B O R A C H A T O A U k u r a s a 1 TANZANIA OSAKA ALUMNI Kitabu cha Mbinu Bora Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa P.O. Box 1923, Dodoma. Novemba, 2012

More information

HAKI NA TARATIBU ZA AJIRA, KAZI NA HIFADHI YA JAMII

HAKI NA TARATIBU ZA AJIRA, KAZI NA HIFADHI YA JAMII HAKI NA TARATIBU ZA AJIRA, KAZI NA HIFADHI YA JAMII SHERIA KATIKA LUGHA RAHISI KIMETOLEWA NA CHAMA CHA WANASHERIA TANZANIA BARA (TANGANYIKA LAW SOCIETY) KWA UFADHILI WA TAASISI YA LEGAL SERVICE FACILITY

More information

TAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF) KUHUSU HAKI ZA WATOTO KATIKA KATIBA MPYA

TAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF) KUHUSU HAKI ZA WATOTO KATIKA KATIBA MPYA TAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF) KUHUSU HAKI ZA WATOTO KATIKA KATIBA MPYA Marekebisho ya 23 January 2013 YALIYOMO KURASA TAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF)... 0 KUHUSU HAKI ZA WATOTO... 0

More information

Bustani 10,000 Katika Afrika. Alberto Prina

Bustani 10,000 Katika Afrika. Alberto Prina Bustani 10,000 Katika Afrika Alberto Prina K i j i t a b u Timu ya wahariri: Abderrahmane Amajou, Typhaine Briand, Roba Bulga Jilo, Davide Dotta, Emanuele Dughera, Michela Lenta, Velia Lucidi, Irene Marocco,

More information

Kimesanifiwa na:- E.D.Kissuu ECOMM TANZANIA S.L.P ,Dar es Salaam. Simu:

Kimesanifiwa na:- E.D.Kissuu ECOMM TANZANIA S.L.P ,Dar es Salaam. Simu: Kimesanifiwa na:- E.D.Kissuu ECOMM TANZANIA S.L.P. 21425,Dar es Salaam. Simu: +255 713 607 207 edkissuu@gmail.com Katuni zimechorwa na: Adam Lutta Babatau Inc. Box 13565 Dar es salaam, Simu:+255 713 474200

More information

ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA UCHUMI WA ZANZIBAR

ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA UCHUMI WA ZANZIBAR ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA UCHUMI WA ZANZIBAR MUHTASARI WA RIPOTI YA YA MWISHO. JULY 2012 for Page i Muhtasari Utafiti huu wa athari za Mabadiliko ya Tabianchi kwa uchumi Zanzibar umetoa tathmini

More information

Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali ya Madini Ukanda

Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali ya Madini Ukanda WARAKA WA TAARIFA YA MRADI (PID) HATUA YA TATHMINI TAARIFA NA..: AB4376 Jina la Mradi Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali ya Madini Ukanda AFRIKA Sekta Madini na Uchimbaji mwingine (100%) Namba ya

More information

Mwongozo wa Familia wa Kujifunza

Mwongozo wa Familia wa Kujifunza Shule za umma za kata ya Fayette 1 Mwongozo wa Familia wa Kujifunza Muhtasari wa yale watoto wanastahili kufahamu na kuweza kufanya na njia za familia kuongeza masomo nyumbani. Tunaamini familia ni wenzetu.

More information

International Labour Office. Kazi za Ndani Zenye Madhara kwa Watoto: Kijitabu cha Maelezo Mafupi

International Labour Office. Kazi za Ndani Zenye Madhara kwa Watoto: Kijitabu cha Maelezo Mafupi International Labour Office Kazi za Ndani Zenye Madhara kwa Watoto: Kijitabu cha Maelezo Mafupi 1 Hakimiliki Shirika la Kazi Duniani 2007 Kimechapwa mara ya kwanza 2007 Machapisho ya Ofisi ya Shirika la

More information

Evaluation of Contextual Teaching of Kiswahili Proverbs in Secondary Schools in Kenya

Evaluation of Contextual Teaching of Kiswahili Proverbs in Secondary Schools in Kenya Evaluation of Contextual Teaching of Kiswahili Proverbs in Secondary Schools in Kenya Oduori T. Wamubi Prof. Simala, K. Inyani Profesa Mshiriki Masinde Muliro University of Science and Technology Prof.

More information

Vyote Unavyopaswa Kujua Kuhusu Viazi Vitamu

Vyote Unavyopaswa Kujua Kuhusu Viazi Vitamu Vyote Unavyopaswa Kujua Kuhusu Viazi Vitamu Kitabu cha Mafunzo Kwa Wakufunzi cha mradi wa Kuwafikia Wadau wa Mabadiliko JUZUU YA 7 Mada ya 13: Kutumia Kitabu cha Kozi ya Mafunzo Kwa Wakufunzi Kuhusu Vyote

More information

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MANISPAA YA BUKOBA.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MANISPAA YA BUKOBA. JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MANISPAA YA BUKOBA. SHULE YA SEKONDARI KAHORORO, S. L. P 198, BUKOBA. Tarehe 14/5/2018 MKOA WA KAGERA

More information

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania Nordic Journal of African Studies 16(1): 18 29 (2007) Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania ABSTRACT This paper has attempted

More information

MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA. Kwa Wanaoanza

MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA. Kwa Wanaoanza 1 Matumizi bora ya Facebook kwa Biashara MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA Kwa Wanaoanza For IT Services & Web Solutions Web: Email: info@dudumizi.com Phone: 0768816728 2 Matumizi bora ya Facebook kwa

More information

KUHUSU AFRODAD. Dira ya AFRODAD. Dhamira ya AFRODAD. AFRODAD inalenga mchakato sawa na endelevu wa maendeleo kuelekea Afrika yenye mafanikio.

KUHUSU AFRODAD. Dira ya AFRODAD. Dhamira ya AFRODAD. AFRODAD inalenga mchakato sawa na endelevu wa maendeleo kuelekea Afrika yenye mafanikio. KUHUSU AFRODAD Dira ya AFRODAD AFRODAD inalenga mchakato sawa na endelevu wa maendeleo kuelekea Afrika yenye mafanikio. Dhamira ya AFRODAD Kupata sera zitakazorekebisha migogoro ya madeni ya Afrika kulingana

More information

Yaliyomo. Kuhusu kitabu hiki. Hautakuwa peke yako. Mfumo wa msaada ni wa manufaa sana wazazi wote wanahitaji!

Yaliyomo. Kuhusu kitabu hiki. Hautakuwa peke yako. Mfumo wa msaada ni wa manufaa sana wazazi wote wanahitaji! Yaliyomo Kuhusu kitabu hiki Kuhusu kitabu hiki.........................................................1 Unapojisikia vibaya.........................................................2 Unapoanza kuwa mzima

More information

USIMAMIZI MKUU WA UBORA WA MAHURUJI

USIMAMIZI MKUU WA UBORA WA MAHURUJI USIMAMIZI MKUU WA UBORA WA MAHURUJI MWONGOZO KWA WAFANYABIASHARA WADOGO NA WA WASTANI WANAOUZA BIDHAA NJE YA NCHI TOLEO LA PILI Geneva 2011 ii IKISIRI YA HUDUMA YA HABARI ZA BIASHARA ID=42653 2011 F-09.03

More information

JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI

JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI Mwongozo huu utatumika kama njia ya kuwafunza watafiti watakaohusika na utafiti unaohusu binadamu. Muongozo huu utatumika

More information

Kubadili Sheria Za Mbegu Na Ulinzi Wa Aina Za Mbegu Na Mimea Nchini Tanzania

Kubadili Sheria Za Mbegu Na Ulinzi Wa Aina Za Mbegu Na Mimea Nchini Tanzania Kubadili Sheria Za Mbegu Na Ulinzi Wa Aina Za Mbegu Na Mimea Nchini Tanzania Athari Zake Kwa Mifumo Ya Mbegu Inayosimamiwa Na Wakulima Na Kwa Wakulima Wadogo April 2016 CONTENTS UTANGULIZI 3 MAELEZO YA

More information

HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE

HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE. JENISTA MHAGAMA (MB), KATIKA KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA AFYA NA USALAMA MAHALI PA KAZI DUNIANI DODOMA, 28 APRILI

More information

Mwongozo wa Kutathimini mifumo ya Ugawanaji wa faida na Mapato Katika Miradi ya Jamii ya MKUHUMI

Mwongozo wa Kutathimini mifumo ya Ugawanaji wa faida na Mapato Katika Miradi ya Jamii ya MKUHUMI David M. Mwayafu, Richard Kimbowa, Kristy Graham Mwongozo wa Kutathimini mifumo ya Ugawanaji wa faida na Mapato Katika Miradi ya Jamii ya MKUHUMI Na: David M. Mwayafu, Richard Kimbowa (Uganda Coalition

More information

BUNGE LA TANZANIA MKUTANO WA NANE. Kikao cha Ishirini na Nane Tarehe 16 Julai, (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A

BUNGE LA TANZANIA MKUTANO WA NANE. Kikao cha Ishirini na Nane Tarehe 16 Julai, (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA MKUTANO WA NANE Kikao cha Ishirini na Nane Tarehe 16 Julai, 2012 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma

More information

NAFASI ZA MASOMO MASOMO YA ASUBUHI

NAFASI ZA MASOMO MASOMO YA ASUBUHI NAFASI ZA MASOMO Shule yetu, iliyoanza mwaka 1974, inazingatia taaluma na maadili kwa kufuata sera ya elimu ya Kanisa Katoliki. Ni ya mchepuo wa biashara. Inapokea wanafunzi wa kike na wa kiume, wa kutwa

More information