SwahiliWeb ELECTRONIC DEPOSITORY AND RESOURCE ARCHIVE.

Size: px
Start display at page:

Download "SwahiliWeb ELECTRONIC DEPOSITORY AND RESOURCE ARCHIVE."

Transcription

1 SwahiliWeb ELECTRONIC DEPOSITORY AND RESOURCE ARCHIVE Archive: Pat Caplan Document: NEMA meeting (Swahili) File reference: SW/PC/13030 This document has been downloaded from the SwahiliWeb archive on the understanding that it is copyright under the laws of the United Kingdom and the Berne Convention, and that no further copying, storage or distribution, in any form or by any means, including electronically, is permitted except under the provisions of fair dealing. Copyright of all materials deposited with SwahiliWeb remains with the copyright holder. Those seeking copyright and associated permissions will be referred to the copyright holder.

2 Meeting to start NEMA political party, Kanga village 1994 part transcribed by Joseph Bwaithondi 2011 In the early 1990s, it was decided that Tanzania, hitherto a one-party state, should allow other political parties to run in elections. This meeting was convened by people from one of the new parties NEMA in Kanga village in It was recorded and a translation into English made directly from tape (qv). It was transcribed in SPEAKER: Kwa kawaida kwenye mikutano kuna lugha zetu tunaanzia, kwa mfano wakati ule wa TANU au CCM wao walikuwa wakisema kidumu chama cha Mapinduzi Kidumu watu wakiitikia Kidumu. Lakini katika mtiririko wa chama chetu hiki hatufanyi hivyo na sisi tuna sauti yetu. Watu wote nitawafundisha halafu tutaanza. Sasa sijuhi niwafundishe halafu tuanze? Mimi uwa nauliza au naanza NEMA mbele ninyi mtaitikia hivi Daima tutanema NEMA. (Kicheko toka kwa wajumbe) tunapofungua na tunapofunga tunafanya hivyo hivyo sawa? NEMA MBELE DAIMA TUTANEMA NEMA nyie ndio mtaitikia hivyo. Sasa tunaanza NEMA MBELE SPEAKER: Kwa kuanzia baada ya kufungua hiyo hadhara yenyewe tunakuja maana ya NEMA. NEMA ni kifupi cha maneno ya Kiingereza National Alliance For Mass Advancement. Kwa maana yake ni chama cha kuleta maendeleo wananchi kwa kuwa huko kote ni kugumu basi tunakatiza tunaita NEMA. Naona hapa tumeelewana hivi. Viongozi wake:- Viongozi wake sasa hivi ni wa muda mfupi. kutakuwa na Viongozi wake wa kudumu baada ya mzunguko mmoja. Viongozi wake ni Raisi Subira Kawambwa, huyu ndio raisi wake wa muda. Sio muda mrefu muda wake utapita. Halafu kuna kanda. Viongozi walioanzisha hii NEMA Tanzania waliigawanya kwa kanda. Kanda ya mashariki kuna kiongozi wetu Abubakari Malima. Naye ametoa salamu kwa wtu wa Mafya. yeye ni mzima akipata wasaa tu atakuja. Wapo viongozi wengine kama Dr. Dau, Prof. Isengo watu mbalimbali wengine toka Chuo kikuu. Lakini wa muhimi ni hawa wawili nilitaka kuwafahamisheni. Tatu, kuna kitu histori. Nataka kutoa historia fupi nikiwa naendelea na huu utaratibu wangu. Historia ina desturi ya kujirudia, inaweza kufanyika mwaka huu ikakaa halafu ikaja kufanyika mwaka mwingine japo ikipita miaka 20 au 50 au hata 100. Sasa kihistoria wakombozi wa Mafia ni watu wa Bweni na Kange. Mtakumbuka Athumani Waziri ni mtu wa hapa huyu ndio wa kwanza aliyejitolea muhanga kupanda Mashua kwenda kuitafuta TANU ilipo na akaileta kwa njia hii. Wakati wenzetu kule wana Congress na UPP. Historia ile ile inajirudia baada ya miaka 33 au 34 imeanza Bweni vile vile na Kange. Huku kwa wenetu vile vile kuna vyama vya siasa lakini nguvu yake ni ndogo, kwa sababu havuja kaa kikao hata kimoja. Kwa hiyo kaskazini huku kuna historia ya aina yake ambayo inatupeleka kule ili peke yake mie nalifurahia na linaleta fahari. SW/PC/ NEMA meeting (Sw)

3 Baada ya hpo nataka kuwaelezea jinsi mwenendo wa dunia unavyokwenda. Dunia inamwendo wake mwenyewe. Ilitoka kwenye ujima ikaingia kwenye utumwa. Ikatoka kwenye utumwa ikaingia kwenye vita kuu ya kwanza na yapili. Ikatoka katika vita ya 1 na 2 ikaingia kwenye vita baridi. Ikatoa kwenye vita baridi ikaingia kwneye mfumo wa vyama vingi vya siasa. Imetoka hapo sasa wengine tumeshaingia kwenye mazingira lakini kwa kuwa sisi tumekuwa tumechelewa ndio sasa tumeingi a hapa. Lakini nchi zilikuwa zimeendelea zimeshamaliza. uingereza kule wana vyama zaidi ya kimoja kwenye siasa kuna Labour, Lib-democrat na hicho ambach akitaki mabadiliko (conservative). Sasa nchi hii ya Tanzania tunao hiki kitu ni kigeni wakti wenzetu wameshasahau sie tunakiona ni kigeni. sasa kwa nini dunia inakwenda hivi? Dunia hii inakwenda hivi kwa sababu moja ni kumsaidia mtu ambaye maisha yake yapo chini. Lengo lake kuu ni kumuinua mtu hali yake. Kama si mfumo wa dunia kufanya hivi leo tusingekuwa na sauti kufanya hapa. Nakumba huko nyuma baada ya TANu kujitawala hukuthubutu mtu usimame kuongelea chama kingine cha siasa ungewekwa ndani. Lakini dunia ile ile baada ya kuona wanyonge wankandamizwa zaidi wakasema hapana tunafanya hivi. Na kweli chama tawala chcochote kinafuata masharti, kwa maaana tunaishukuru dunia kutusaidia sisi wanayanyonge kwa maana Tanzania tuko wengi. Sasa nakuja kwenye madhumuni ya NEMA. NEMA madhumuni yake makubwa ni kupata wanachama kwanza,kadi tunazo hizi nilichukua kadi 250 nikaona labda zitatosha kati ya vijiji 4 na 5 kumbe nilifanya makosa, zingine nimeziacha Kilindoni. Kilindoni peke yake imechukua kadi karibu 200. Sasa hizi ni kadi zetu tunachotaka na madhumuni yetu kupita sehemu hata sehemu ni kuongeza idadi ya wanachama. Na kila kadi moja ina shilingi 110 ikiwa malipia na ada yake kwa mwaka. Sasa tukishaongeza idadi ya wanachama nini chamwisho? Tukishaongeza idadi kubwa ya wanachama sasa tutakutaka wewe kupiga kura kwa upande wa NEMA. Nia yetu na dhamira yetu ni kuiangusaha CCM kwani imeshindwa imeshindwa kabisa kutuongoza katika nchi hii. Hatutaki kufanya fujo tutakwenda kwa utaratibu tuliopangia. Sasa kuishinda ccm chama tawala tunahitaji sisi wanyonge kuungana kupinga Yule tajiri anachosema. Sasa Kanga mmepata,bweni mmepata, Mlali mmepata sasa nakwenda Jimbo, Balemi. Mbunge wetu anatoka kwenye NEMA katika wilaya ya Mafia hii ndio kusudio letu kubwa. Pili raisi wetu kwenye nchi hii anatoka kwenye NEMA ndio dhamira yetu kwa sasa. Kwa hiyo wazee tukubaliane CCM imetupeleka mahali pabaya. Ubaya mkubwa uliofanywa na CCM ni kuwadanganya wananchi wake. Imetudanganya katika kipindi cha miaka 33, tukipata uhuru kodi inaondoka, elimu bure, tukipata uhuru matibabu bure. Kodi imerudi, elimu sio bure na madawa yanauzwa, bado wananchi tumekaa tu. Miongoni mwenu mmeshakata tama kadi ya CCM hamna na kadi nyinne hamna mmejikalia tu sasa si wakati wa kukaa tena huuwakti si wakukaa kimya. Utakapo kaa kimya CCm huna ya NEMa huna wewe ni mtu utakuwa dhalimu wa nafsi yako. Wakati umefika wananchi wa kuiambia ccm basihatuan uchanga. Wewe miaka 33 bado unasema nchi change bado? Hakuna kitu chochote tulichofanya kwa muda huu wote. Kwa upande wa chama hakuna. Kwa hiyo tunasema CCM imeshindwa na kama imeshindwa iondoke na itaondoka kwa kura kwakadi zenu. Ina mtindo CCM ianimba kwenye vyombo vya habari na vitabu, hili tuendelee nchi hii tunahitaji vitu 4 inasema watu ardhi, siasa safi na uongozi bora ndio tuaendelea. Sasa ardhi Tanzania ipo, watu tupo 27 milioni tumekwama hapa na SW/PC/ NEMA meeting (Sw)

4 siasa safi na uongozi bora. Maana yake CCM kashindwa kututawala. Wananchi wakati umefika tunakuombeni sana mpokee NEMA mneemeke. Si jambo la uoga si jambo la wizi kusema mimi nitachukua kadi usiku mie nitachukua siku nyingine hapana mie kadi yangu ni hii natembea nayo. Tumetumia taratibu zote za serikali kuja hapa ndio maana tunavyombo vya dola hapa. Huyu ni dola katika kata yake ilikuwa vyombo vingine toka wilayani vifike lakinibahati mbaya vimekwama na usafiri nadhani safari nyingine vitakuwa vimefika. Maana hiki kikao ni cha kwanza hata kule wilayani wanadhani hawafanyi kitu kule kumbe tumekwisha anza. Taarifa zitakazo toka huku baada ya kikao hiki, tukija wakati mwingine nao watakuja. Sasa hivi ulimi CCM watatoa manake wataona kuna kazi. Kwa hiyo tunachokuombenimuiunge mkono NEMA. Bwenu mmepata Makada kuna vijana nimewachia 2 wanaendlea maana watu walinizunguka ikanibidi niacha kadi pale na niache na vijana na hapa Inshala naamini endapo mtanipokea nyingine naziacha hapa hapa. Nikifika kilindoni nitafanya mawasilianao na makada wangu na mimi mwenyewe nitakuwa nakuja mara kwa mara kuwasilaana. Wananchi sasa wakati umefika msingoje tu rehema kutoka Mbinguni iteremke. Hapana kwanza mjikaze nyie wenyewe mkibebwa mshike mbeleko. Kutakuwa na maswali baada ya hapa na mtapewa nafasi. Sera yako nini ndio CCM itawauliza. Maswali hayo nitaanza kuyajibu. Tunaema kama alivyosema yesu, ya kwamba nimekuja kuziendeleza amri za Musa na si kwamba kuzifuta. CCM kakwamba katika matibabu, elimu alipokwama katika kodi. Tumekuja kufuta kodi. Tumekua kuleta Elimu bure, hapa hapa Mafia Kilindoni watu wanshindwa kusoma. Miongoni mwenu mmeshashinda kuwasomesha watoto wenu kule. Kodi tunalipishwa kila siku. Mtoto shuleni anachangishwa mashuleni kila kukichwa. Wilaya hii ndio haijalipishwa matibabu ya hospitali, wilaya nyingine watu wamekufa dripu za kjongeza maji zipo ofisini na kaani yupo lakini mtu hana fedha ya kuinunua. Wameshakufa watu matumbo ya kuarisha kwa sababu hawana pesa Tanzania hii. Kwa hiyo mkisikia nyoka mwe msimuache apite shika kigongo. Manake akimaliza kule atakuja na huku. Haiwezakekani dawa ikauzwa hospitali ya Kilindoni hapa ikatolewa bure. CCM kazi yake kudanganya watu kuwa inauzwa Wilayani na huku msiwe na wasiwasi. Iuzwe wilayani hapa hisiuzwe haya maneno kweli yanaingia kwenye akili ya mtu? Ndio wanaanza kidogo kidogo kuingia huku vijijini. Kesho na kesho kutwa mtaanza kununua madawa. Kwa hiyo ili hatulikubali kwa vitendo. Chukueni kadi tukomeshe habari hizi. Kama hajachukua kadi zenu mmetukwamisha. Mmekwama nyinyi na sisi. Kinachofanya CCM hatukioni. Juzijuzi tulichangishwa pesa za kununua gari ya wagonjwa. Pesa hakuna nahakuna gari na kuna maelezo. Sasa hivi mwenyekiti wa wilaya hata posho hapewi na anakwenda kazini kwa miguu. Sasa ndugu zangu tumesema basi. Na kusema basi kwa kuchuka kadi na sio kwa kukaa kimya. Tumeichoka CCM tukueni kadi na sio kusema kimya kumya toeni shilingi 110 mchukue kadi na suku ya uchaguzi tunawaondosha. Asantenti kwa kumaliza nakaribisha maswahili. Ninaweka maneno yetu yale yale, NEMA mbele mnaitikia vile vile daima tutanema NEMA. SW/PC/ NEMA meeting (Sw)

5 Mtu2: Sasa viongozi waliopo itakuwaje? SPEAKER: Nilichosema chama kitatoa wagombea Ubunge na urahisi. Kwa mfano kma CCM itamtoa Kimbau kama mgombea ubunge sie yaye tutato mtu wetu wa kushindana na wa CCM na lazima ashinde. Na katika urahisi ni hivyo hivyo. Kama vyama vingine vitatoa wagombea basin a sisi tutatoa pia na atashinda. Mtu3: Kwanza nashukuru. Katika uliyeyaongelea ni mazuri kwanza kuhusu kodi kwa kweli imekuwa kali sana. Pili kuhusu dawa kama dawa inauzwa wilayani hata huku itafika kuuzwa tu kama NEMA hatashinda hii hali lazima itafika tu. Ni hivyo kama kuitia motisha hii NEMA Mtu4: Katibu mie nina ridhaa na maulizo kidogo. Leo mimi nimekaa bahari na chombo kidogo na misukosuko, lakini huku nilipotoka nikinoa nanga nakwenda kwengine. Ikiwa ninavyotaka hii NEMA kwa maneno yake Mazuri ya ufasaha kabisa. Kwa hiyo tuambia mema na sio tu kwamba nikinoa nagnga tu hapa kwenda huko nikakumbana na dhuruba nyingine. Na chombo kupausuka. Sasa kidogo ungezungumzia taratibu angalau tuzijue. SPEAKER: Taratibu kwa mtu kashaumwa na nyoka akiona unyasi anashituka. Mie nimeshaumwa na nyoka kwa miaka 33 sasa. Hakuna chochote nilichopata. Nimepiga kura mara 7 bial kupata maendeleo yoyote yale. Mpeni NEMA kipindi kimoja na mtaona mabadiliko. Mwenyekiti wa nyumba kumi atalipwa mshahara na sio kama wa CCM. Eti afanye kazi halafu akatafute shughuli zake nyingine. kama mtu haumlipi manake nini? Wakishafika watu 200 hapa Kanga mna haki ya kufungua Tawi. Mwenyekiti wetu mtamuona hapa hapa. Mtu5: NEMA ikafaulu kwetu jema na hisipofaulu sisi itakuwaje? Manke hii ndio siasa SPEAKER: NEMA haishindi kwa mabavu itashinda kwa kura. Demokrasi manake usawa na usawa manake ni uadilifu. Tutaishinda CCM kwa usawa wala hakuna mgogoro. Tukishindwa tutajipangwa kwa kipindi kingine na sio kwamba NEMA ndio itakuwa imekufa. Lakini nachosema NEMA haitashindwa, ila kwa kuwa umekuwa na wasiwasi tukishindwa tutaendlea na shuhuli zetu kama kawaida. Mtu6: Sasa nimesikia hivi vyam vingi wale wanao hama CCM wanachomewa nyumba zao sasa itakuwaje? SPEAKER: Wasi wasi ondoa. Serikali yetu inafanya kazi vizuri na ipo imara na wasi wasi huo indoa. NEMA wapo tofauti na CUF lengo letu ni kukiondoa chama tawala kwa hiyo wasiwasi huo ondoa. Mtu7: Je matatizo tuliokuwa nayo mtatuondolea SPEAKER: Nadhani wewe ni mswahili na maana ya neno NEMA unalielewa. Tunataka kuwaondolea matatizo mliyokuwa nayo. Tunachotaka mtuunge mkono tu tumalize kazi mnatuchelewesha. SW/PC/ NEMA meeting (Sw)

6 Watu wanacheka. SPEAKER: Kadi zipo imeandikwa NEMA na chini kuna ngano na vigogo vinashikana. Hata kama haujui kusoma wewe utelewa tu. Mtu8: Na chama hiki kimezaliwa lini SPEAKER:mwezi wa tano SW/PC/ NEMA meeting (Sw)

Information for assessors (do not distribute this page to participants):

Information for assessors (do not distribute this page to participants): R&P Cultural Orientation Model Assessment Written Version Swahili Information for assessors (do not distribute this page to participants): This written version of the Model Cultural Orientation (CO) Assessment

More information

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013 www.xtremepapers.com UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level *9257224991* SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013 Additional Materials: Answer Booklet/Paper

More information

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E) 102/3 KISWAHILI KARATASI YA 3 Fasihi Julai/Agosti 2013 MUDA : SAA 2 ½ Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E) Kiswahili Karatasi 3 Julai/ Agosti Muda: Saa 2 ½ MAAGIZO: Andika jina lako na nambari yako

More information

April 14, 2016 COUNTY ASSEMBLY DEBATES 52

April 14, 2016 COUNTY ASSEMBLY DEBATES 52 MOMBASA COUNTY ASSEMBLY HANSARD REPORT Thursday, 14 th April, 2016 The House met at 2.48pm. (Hon. Deputy Speaker (Mr. Mswabah Rashid) in the Chair) PRAYERS Hon. Deputy Speaker (Mr. Mswabah Rashid): Kindly

More information

usudi la Maisha Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na kupishana usiku na mchana, kuna kweli ishara kwa wenye akili, ambaye mkumbuke-

usudi la Maisha Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na kupishana usiku na mchana, kuna kweli ishara kwa wenye akili, ambaye mkumbuke- Kusudi la Maisha hawatakuambia nini walihitimisha kupitia uchunguzi au hoja ya uchambuzi. Katika hali nyingi, hakika wao kukuambia nini mtu mwingine alisema... Au wao watakuambia nini kawaida kudhaniwa

More information

2

2 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23 24 25 26 27 28 29 30 31 32 33 34 35 36 37 38 39 40 41 42 43 44 45 46 47 48 49 50 51 52 53 54 55 56 57 58 59 60 61 62 63 64 65 66 67 68 69 70 71

More information

2

2 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23 24 25 26 27 28 29 30 31 32 33 34 35 36 37 CKRC VERBATIM REPORT OF CONSTITUENCY PUBLIC HEARINGS, KALOLENI CONSTITUTENCY, HELD AT MARIAKANI SECONDARY

More information

ORODHA YA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI SPIKA MHE. PANDU AMEIR KIFICHO. Rais.

ORODHA YA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI SPIKA MHE. PANDU AMEIR KIFICHO. Rais. ORODHA YA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI SPIKA MHE. PANDU AMEIR KIFICHO 1.Mhe. Kamal Basha Pandu 2.Mhe. Ali Mzee Ali 3.Mhe. Shamsi Vuai Nahodha Naibu Spika/Jimbo la Rahaleo. Mwenyekiti wa Baraza/Uteuzi

More information

Roho Mtakatifu Ni Nini?

Roho Mtakatifu Ni Nini? Roho Mtakatifu Ni Nini? kwa ajili ya mkutano. Mkutano huu utakuwa tofauti, kidogo na ile ya kawaida tunayokuwa nayo hapa. Kwa kawaida, kila wakati tunapokuja pamoja hapa, ni mkutano kwa wa kwa ajili ya

More information

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) VERBATIM REPORT OF

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) VERBATIM REPORT OF CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) VERBATIM REPORT OF CONSTITUENCY PUBLIC HEARINGS, BARINGO NORTH CONSTITUENCY, HELD AT KABARTONJO CHIEFS OFFICE ON 3 rd JULY, 2002 CONSTITUENCY PUBLIC HEARINGS,

More information

Human Rights Are Universal And Yet...

Human Rights Are Universal And Yet... Human Rights Are Universal And Yet... Episode 05 Title : The right to education Author : Julien Adayé Editor : Aude Gensbittel Translator : Anne Thomas, Eric Ponda Proofreader: Pendo Paul Characters (sounds,

More information

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level * 899145 4 672* SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2010 Additional Materials: Answer Booklet/Paper READ

More information

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani HakiElimu: Mfululizo wa Mada za Uchambuzi Namba. 2003.4S Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere 1 Rakesh

More information

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23) GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER (Made under Section 23) THE ELECTRICITY (STANDARDIZED SMALL POWER PROJECTS TARIFF) ORDER, 2015 Citation 1. This Order may be cited

More information

Mukhtasari Wa Mabishano Kwa Na Dhidi Ya Vikombe Vingi Vya Ushirika

Mukhtasari Wa Mabishano Kwa Na Dhidi Ya Vikombe Vingi Vya Ushirika Mukhtasari Wa Mabishano Kwa Na Dhidi Ya Vikombe Vingi Vya Ushirika (A Summary Of Arguments For And Against Individual Communion Cups) Na J D Logan Communion Cups) 1 Mukhtasari Wa Mabishano Kwa Na Dhidi

More information

Ufunguo wa Kutaalamika Haraka

Ufunguo wa Kutaalamika Haraka 0 Ufunguo wa Kutaalamika Haraka Ufunguo wa Kutaalamika Haraka Kijitabu Kielelezo; Nakala ya Bila Malipo Yaliyomo 1 Yaliyomo Utangulizi...04 Habari Fupi Kuhusu...08 Fumbo la Ulimwengu wa Ng ambo ya Pili...11

More information

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC)

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) VERBATIM REPORT OF MSAMBWENI CONSTITUENCY PUBLIC HEARINGS, DIANI SECONDARY SCHOOL 2 ON Monday, May 6, 2002 3 CONSTITUENCY PUBLIC HEARINGS, MSAMBWENI CONSTITUENCY

More information

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23) GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER (Made under Section 23) THE ELECTRICITY (STANDARDIZED SMALL POWER PROJECTS TARIFF) ORDER, 2016 citation 1. This Order may be cited

More information

wasiofaa. Naomba sana kila raia afanye bidii awezavyo kumkaribia Mwenyezi Mungu vile anavyoona inafaa, lakini asipitishe hukumu juu ya wengine.

wasiofaa. Naomba sana kila raia afanye bidii awezavyo kumkaribia Mwenyezi Mungu vile anavyoona inafaa, lakini asipitishe hukumu juu ya wengine. HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA, KWENYE IBADA YA KUWEKWA WAKFU NA KUINGIZWA KAZINI ASKOFU MARTIN FATAELI SHAO WA DAYOSISI YA KASKAZINI YA KANISA LA

More information

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC)

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) VERBATIM REPORT OF CONSTITUENCY PUBLIC HEARINGS, SIGOR CONSTITUENCY, AT KIBICHBICH D.O. S OFFICE 2 ON Monday 1 st July 2002 CONSTITUENCY PUBLIC HEARING SIGOR

More information

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania Nordic Journal of African Studies 16(1): 18 29 (2007) Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania ABSTRACT This paper has attempted

More information

JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1

JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1 The Human Rights Centre Uganda JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1 AZIMIO LA KIMATAIFA JUU YA HAKI ZA KIBINADAMU SURA YA NNE YA KATIBA YA JAMHURI YA UGANDA YA 1995: MASIMULIZI YALIYOFASIRIWA KWA URAHISI NA KUFUPISHWA

More information

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA,KWA WANANCHI, 30 SEPTEMBA, 2001

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA,KWA WANANCHI, 30 SEPTEMBA, 2001 HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA,KWA WANANCHI, 30 SEPTEMBA, 2001 Leo napenda nizungumze nanyi, kwa lugha nyepesi iwezekanavyo, juu ya mahusiano tunayowania

More information

"ATATOKEA MARA YA PILI, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu." Waebrania 9:28.

ATATOKEA MARA YA PILI, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu. Waebrania 9:28. KUJA KWA KRIST0 MARA YA PILI "ATATOKEA MARA YA PILI, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu." Waebrania 9:28. Mara nyingi sana kuja kwa Kristo mara ya pili huangaliwa tu kama fundisho la dini. Ni

More information

Ellen White, waasisi wa Kiadventista,na Sabato Lunar

Ellen White, waasisi wa Kiadventista,na Sabato Lunar Ellen White, waasisi wa Kiadventista,na Sabato Lunar Ukristo leo unadhihirisha waumini karibu bilioni mbili katika maelfu ya madhehebu tofauti na tofauti na madhehebu. Kati ya hizi, zaidi ya 500 madhehebu

More information

Theolojia Ujumla. Mike Taylor Semester Munguishi Bible College

Theolojia Ujumla. Mike Taylor Semester Munguishi Bible College Theolojia 1 Ujumla Mike Taylor Semester 1 2014-2015 Munguishi Bible College MIKE TAYLOR 2014 THEOLOJIA 1 i THEOLOJIA Utangulizi! 1 1. Kumfahamu Mungu katika Injili! 3 1.1. Mawazo Makuu 3 1.2. Maana ya

More information

KAMA MUNGU YU PAMOJA NASI, BASI YAKO WAPI MATENDO YAKE YA AJABU?

KAMA MUNGU YU PAMOJA NASI, BASI YAKO WAPI MATENDO YAKE YA AJABU? KAMA MUNGU YU PAMOJA NASI, BASI YAKO WAPI MATENDO YAKE YA AJABU?, Asante, Ndugu Neville, na habari za jioni, marafiki. Nimerudi tena. Sikupata ila masaa manne asubuhi ya leo. Hiyo ni aibu. Na baada ya

More information

MASWALI NA MAJIBU JUU YA KITABU CHA MWANZO

MASWALI NA MAJIBU JUU YA KITABU CHA MWANZO MASWALI NA MAJIBU JUU YA KITABU CHA MWANZO Sasa, kama ye yote ana swali lo lote wanalotaka kulileta,, basi, hebu yasogezeni tu juu hapa, acha mtoto fulani ayalete au vyo vyote mtakavyo. Au, labda, tukimaliza

More information

SautiElimu. Sauti Yako Isikike

SautiElimu. Sauti Yako Isikike SautiElimu Sauti Yako Isikike SautiElimu Sauti Yako Isikike Mtayarishaji : Godfrey Telli Mchangiaji : Robert Mihayo Mhariri : Rakesh Rajani Shukrani za dhati kwa timu ya waandaaji wa SautiElimu 1-10: Lilian

More information

March 14, 2018 PARLIAMENTARY DEBATES 1 NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL REPORT. Wednesday, 14 th March The House met at 9.30 a.m.

March 14, 2018 PARLIAMENTARY DEBATES 1 NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL REPORT. Wednesday, 14 th March The House met at 9.30 a.m. March 14, 2018 PARLIAMENTARY DEBATES 1 NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL REPORT Wednesday, 14 th March 2018 The House met at 9.30 a.m. [The Temporary Deputy Speaker (Hon. (Ms.) Mbalu) in the Chair] PRAYERS QUORUM

More information

Ushindi ndani ya Kristo W. W. PRESCOTT

Ushindi ndani ya Kristo W. W. PRESCOTT Ushindi ndani ya Kristo W. W. PRESCOTT 1 Ushindi Ndani ya Kristo Na W. W. Prescott Mfasiri: M. Mwamalumbili Victory in Christ - Kiswahili 2 Yaliyomo Alinipenda Mimi Aliishi kwa ajili Yangu Mimi Alikufa

More information

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC)

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) 2 3 CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) 4 VERBATIM REPORT OF 5 6 CONSTITUENCY PUBLIC HEARINGS, ORGANISED GROUPS EMBAKASI CONSTITUENCY, HELD AT DANDORA KINYAGO SHOOL (GITARI MARIGU) ON 28 TH

More information

Kiu Cha umtafuta Mungu

Kiu Cha umtafuta Mungu ZAIDI YA NAKALA MILLION 3 ZIMECHAPISHWA KATIKA LUGHA 59 KOTE DUNIANI K Kiu Cha umtafuta Mungu Huduma ya Daktari Richard A. Bennett ilianza katika mabaraza ya miji. Akiwa mwanafunzi chuoni, alikumbana na

More information

Deutsche Welle, Learning by Ear 2009 Seite 1 People Who Make A Difference Liberia: Anita Varney Health Facilitator, Fishtown/Liberia

Deutsche Welle, Learning by Ear 2009 Seite 1 People Who Make A Difference Liberia: Anita Varney Health Facilitator, Fishtown/Liberia Deutsche Welle, Learning by Ear 2009 Seite 1 Title: Anita Varney Health Facilitator, Fishtown/Liberia Author: Stefanie Duckstein, HA Afrika/ Nahost Editor: Christine Harjes Translator: Tony Dunham Sound

More information

KWA NINI SISI SI MADHEHEBU?

KWA NINI SISI SI MADHEHEBU? KWA NINI SISI SI MADHEHEBU? Nimejaliwa kurudi mimbarani tena baada ya kama,, nadhani, karibu kutokuwepo kwa muda wa miezi mitatu. Kindi wamekuwa na wakati mgumu, na mimi pia. Loo, nimeburudika, hata hivyo,

More information

Ndugu na dada zangu wapendwa,

Ndugu na dada zangu wapendwa, UJUMBE WA URAIS WA KWANZA, MEI 2014 Na Rais Thomas S. Monson Upendo Asili ya Injili Hakika hatuwezi kumpenda Mungu kama hatuwapendi wasafiri wenzetu katika safari hii ya maisha duniani. ninafurahia mawazo

More information

Haja Ya Dini. Author(s): Publisher(s): Translator(s): Category: Topic Tags: Featured Category: Published on Al-Islam.org (

Haja Ya Dini. Author(s): Publisher(s): Translator(s): Category: Topic Tags: Featured Category: Published on Al-Islam.org ( Published on Al-Islam.org (https://www.al-islam.org) Home > Haja Ya Dini Haja Ya Dini Author(s): Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi [3] Publisher(s): Bilal Muslim Mission of Tanzania [4] Katika kijitabu

More information

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC)

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) Verbatim Report Of CONSTITUENCY PUBLIC HEARINGS, GANZE CONSTITUENCY, HELD AT GODOMA SECONDARY SCHOOL 2 ON Friday, 3 rd May 2002 VERBATIM REPORT OF CONSTITUENCY

More information

Adhabu ya jino kwa jino na Musitakabali wa imani zetu

Adhabu ya jino kwa jino na Musitakabali wa imani zetu Adhabu ya jino kwa jino na Musitakabali wa imani zetu Nabii Musa alipotoka mlima Sinai kupewa amri kumi za Mungu zilizoko kwenye kitabu cha Kutoka 20:1 17, Mungu alimpa na sharia zingine ambazo lengo lake

More information

LBE 2009 Migration Episode 3: Living without documents

LBE 2009 Migration Episode 3: Living without documents LBE 2009 Migration Episode 3: Living without documents Author: Marta Barroso Editor: Thomas Mösch Characters: Narrator 1: female Narrator 2: male Inserts (English): male, (42) Voice ( Passport, please!,

More information

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu The Human Rights Centre Uganda Azimio la Mkutano Mkuu 53/144 (8 Machi 1999) Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu AZIMIO KUHUSU HAKI NA WAJIBU WA MTU BINAFSI, VIKUNDI NA JUMUIYA

More information

United Pentecostal Church June 2017

United Pentecostal Church June 2017 Kwa Nini Tusali? Jarida la Maombi ya Wanawake Kimataifa "Chagua" Ladies Prayer International kwa Facebook United Pentecostal Church June 2017 Tuko na wafuasi Facebook katika Marekani, Hong Kong, Philippines,

More information

UTARATIBU WA KANISA. 2 Jambo la kwanza ninalotaka kusema ni kwamba mchungaji. 3 Sisi tunaamini katika Kanisa la kimitume, tukifundisha

UTARATIBU WA KANISA. 2 Jambo la kwanza ninalotaka kusema ni kwamba mchungaji. 3 Sisi tunaamini katika Kanisa la kimitume, tukifundisha UTARATIBU WA KANISA Tumemaliza hivi punde ule mkutano mkubwa wa siku, tano usiku kwenye Maskani, ambapo, kwa neema ya Mungu na kwa msaada Wake, nimejaribu sana, kwa Maandiko, kuliweka Kanisa la Bwana Yesu

More information

Ndugu na dada zangu wapendwa,

Ndugu na dada zangu wapendwa, UJUMBE WA URAIS WA KWANZA, NOVEMBA 2011 Na Rais Thomas S. Monson Simama Pahali Patakatifu Mawasiliano na Baba yetu aliye Mbinguni pamoja na maombi yetu Kwake na maongozi Yake kwetu ni muhimu ili tuweze

More information

walozaliwa, si kwa damu, wala mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, mbali kwa Mungu. Sisi sio tena binadamu wa kawaida tu kwa sababu sisi ni w

walozaliwa, si kwa damu, wala mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, mbali kwa Mungu. Sisi sio tena binadamu wa kawaida tu kwa sababu sisi ni w MAMLAKA Tunamshukuru Bwana kwa vile alivyo na yale aliyoyatenda. Tukiweza tu kumfikiria hata tukiwa na mahitaji mbalimbali, yeye atatutimizia. Tusiwatazame watu, tusijitazame sisi wenyewe, tumtazame Mungu

More information

Maisha Yaliyojaa Maombi

Maisha Yaliyojaa Maombi (A Prayer-Filled Life) na Terry Warford (A Prayer-Filled Life) 1 (A Prayer-Filled Life) na Terry Warford Nov 5, 2011 (A Prayer-Filled Life) 2 Sura ya nne nay a tano ya kitabu cha Ufunuo ni vifungu vinavyovutia.

More information

K. M a r k s, F. E n g e l s

K. M a r k s, F. E n g e l s W a (any a kazi wa nchi zote, unganeni! K. M a r k s, F. E n g e l s Maelezo ya chama cha kikomunist Idara ya Maendcleo Moscow Tafsiri hii ya "Maelezo ya Chama cha Kikomunist" inatokana na maandishi

More information

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA SABA. Kikao cha Thelathini na Tisa Tarehe 1 Juni, (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA SABA. Kikao cha Thelathini na Tisa Tarehe 1 Juni, (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa Tarehe 1 Juni, 2017 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA:

More information

TIST HABARI MOTO MOTO MAANDALIZI YA MWAKA 2000 Y2K PREPARATIONS SASA NI WAKATI WA KUANZA KUPANDA MBEGU ZAKO

TIST HABARI MOTO MOTO MAANDALIZI YA MWAKA 2000 Y2K PREPARATIONS SASA NI WAKATI WA KUANZA KUPANDA MBEGU ZAKO TIST HABARI MOTO MOTO Tel. 026-2322246 P.O.BOX 53 MPWAPWA E-Mail tist@twiga.com 01 October 2000 Y2K PREPARATIONS Holes and Seedlings made ready for the year 2000 programme By Gayo Mhila The process of

More information

MIONGOZO MIWILI KUPAA NA KUTUNGULIWA KWA AZIMIO LA ARUSHA

MIONGOZO MIWILI KUPAA NA KUTUNGULIWA KWA AZIMIO LA ARUSHA KIGODA CHA TAALUMA CHA MWALIMU NYERERE MIONGOZO MIWILI KUPAA NA KUTUNGULIWA KWA AZIMIO LA ARUSHA Yamekusanywa na kuhaririwa na: Bashiru Ally Saida Yahya-Othman Issa Shivji CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

More information

Kuzimu na Kurudi na Dr. Rawlings Documentary Video Transcript, TBN Films

Kuzimu na Kurudi na Dr. Rawlings Documentary Video Transcript, TBN Films Kuzimu na Kurudi na Dr. Rawlings Documentary Video Transcript, TBN Films (Mathayo7:13-14) 13 Ingieni kwa kupitia mlango mwembamba. Kwa maana njia inayoongoza kwenye maangamizi ni pana, na mlango wa kuingilia

More information

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti Mradi wa kujua kuhusu Pesa Aprili 2011 FLP - Swahili Mradi wa kujua kuhusu Pesa Ipindi vyetu vya maelezo vya bure, warsha na kozi hutoa fursa ya kujifunza kuhusu

More information

Agano Lililofunikwa Kwa Damu

Agano Lililofunikwa Kwa Damu Agano Lililofunikwa Kwa Damu na Ellis Forsman Agano Lililofunikwa Kwa Damu (The Blood-Sealed Covenant) 1 Agano Lililofunikwa Kwa Damu na Ellis Forsman Oktoba 14, 2012 Agano Lililofunikwa Kwa Damu (The

More information

Kimesanifiwa na:- E.D.Kissuu ECOMM TANZANIA S.L.P ,Dar es Salaam. Simu:

Kimesanifiwa na:- E.D.Kissuu ECOMM TANZANIA S.L.P ,Dar es Salaam. Simu: Kimesanifiwa na:- E.D.Kissuu ECOMM TANZANIA S.L.P. 21425,Dar es Salaam. Simu: +255 713 607 207 edkissuu@gmail.com Katuni zimechorwa na: Adam Lutta Babatau Inc. Box 13565 Dar es salaam, Simu:+255 713 474200

More information

Tafuteni Kwanza Ufalme Wa Mungu

Tafuteni Kwanza Ufalme Wa Mungu Tafuteni Kwanza Ufalme Wa Mungu na Ellis P. Forsman God) 1 Tafuteni Kwanza Ufalme Wa Mungu na Ellis P. Forsman Oktoba 7, 2011 God) 2 Tafuteni Kwanza Ufalme Wa Mungu Mat. 6:24-34 Yesu alitoa maelezo haya

More information

Kifo Na Mbingu. (Death And Heaven) Ellis P. Forsman. Kifo Na Mbingu (Death And Heaven) 1

Kifo Na Mbingu. (Death And Heaven) Ellis P. Forsman. Kifo Na Mbingu (Death And Heaven) 1 Kifo Na Mbingu (Death And Heaven) Na Ellis P. Forsman Kifo Na Mbingu (Death And Heaven) 1 Kifo Na Mbingu (Death And Heaven) Na Ellis P. Forsman Oktoba 11, 2011 Kifo Na Mbingu (Death And Heaven) 2 Kifo

More information

maombi, kabla tu hatujalifungua Neno hili la Kiungu.

maombi, kabla tu hatujalifungua Neno hili la Kiungu. ALAMA YA MNYAMA Sasa, kesho usiku Daima tunaonyesha jambo moja,, Bwana Yesu Kristo, ni hivyo tu, na lo lote ambalo ni mapenzi Yake ya Kiungu kwetu kufanya. Lakini kama ni mapenzi Yake ya Kiungu kesho usiku,

More information

WEWE NI NANI? Toleo X Toleo Ukweli wa Injeli Toleo 23

WEWE NI NANI? Toleo X Toleo Ukweli wa Injeli Toleo 23 Toleo X Toleo 23 WEWE NI NANI? (Habari ifuatayo ni hadithi ya mambo ambayo yamenakiliwa katika Matendo 19:10-20 SUV). Paulo mtume wa Yesu Kristo alihubiri katika mji wa Efeso kwa miaka miwili. Katika muda

More information

HISTORIA, MAENDELEO NA MABADILIKO YA KATIBA TANZANIA TANGU UHURU HADI MIAKA HAMSINI YA UHURU 9 DESEMBA 2011.

HISTORIA, MAENDELEO NA MABADILIKO YA KATIBA TANZANIA TANGU UHURU HADI MIAKA HAMSINI YA UHURU 9 DESEMBA 2011. Saint Augustine University of Tanzania From the SelectedWorks of Daudi Mwita Nyamaka Mr. Winter December 9, 2011 HISTORIA, MAENDELEO NA MABADILIKO YA KATIBA TANZANIA TANGU UHURU HADI MIAKA HAMSINI YA UHURU

More information

Nia Dhidi Ya Kristo Je Unamheshimu?

Nia Dhidi Ya Kristo Je Unamheshimu? Nia Dhidi Ya Kristo Je Unamheshimu? (Attitude Towards Christ Do you Honor Him?) Na Ellis P. Forsman (4-Attitude Towards Christ - Do you Honor Him) 1 Nia Dhidi Ya Kristo Je Unamheshimu? (Attitude Towards

More information

MSAMAHA NA UPATANISHO

MSAMAHA NA UPATANISHO Hakimiliki 2007-2017 na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa. MSAMAHA NA UPATANISHO na Jonathan M. Menn B.A., Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison, 1974 J.D., Cornell Law School, 1977 M.Div., Trinity Evangelical

More information

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA, KWA WANANCHI, TAREHE 31 JULAI 2001

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA, KWA WANANCHI, TAREHE 31 JULAI 2001 HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA, KWA WANANCHI, TAREHE 31 JULAI 2001 Leo napenda nizungumze nanyi kuhusu umuhimu wa kuweka akiba, na umuhimu wa kulipa

More information

Waandishi: wa Toleo la 5. Scholastica Jullu Athanasia A. Soka Safina Hassan Mary Njau. Toleo la 5: 2008 ISBN

Waandishi: wa Toleo la 5. Scholastica Jullu Athanasia A. Soka Safina Hassan Mary Njau. Toleo la 5: 2008 ISBN KIONGOZI CHA SHERIA Hakimiliki 2008 Kimetolewa na: Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC) Waandishi: wa Toleo la 5 Scholastica Jullu Athanasia A. Soka Safina Hassan Mary Njau Toleo la 5: 2008 ISBN

More information

ORODHA YA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI SPIKA MHE. PANDU AMEIR KIFICHO. Rais.

ORODHA YA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI SPIKA MHE. PANDU AMEIR KIFICHO. Rais. ORODHA YA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI SPIKA MHE. PANDU AMEIR KIFICHO 1.Mhe. Kamal Basha Pandu 2.Mhe. Ali Mzee Ali 3.Mhe. Shamsi Vuai Nahodha Naibu Spika/Jimbo la Rahaleo. Mwenyekiti wa Baraza/Uteuzi

More information

December 19, 2017 MOMBASA COUNTY ASSEMBLY DEBATES 30

December 19, 2017 MOMBASA COUNTY ASSEMBLY DEBATES 30 MOMBASA COUNTY ASSEMBLY HANSARD REPORT Tuesday, 19 th December, 2017 The House met at 3:07p.m. (Mr. Speaker (Hon. Aharub Ebrahim Khatri) in the Chair) PRAYERS Mr. Speaker (Hon. Khatri): Members you may

More information

Tora UTANGULIZI KWA TORA SOMO LA KWANZA

Tora UTANGULIZI KWA TORA SOMO LA KWANZA SOMO LA KWANZA UTANGULIZI KWA TORA For videos, study guides and other resources, visit Third Millennium Ministries at thirdmill.org. 2014 nathird Millennium Ministries Haki zote zimehifadhiwa. Hakuna sehemu

More information

Kifo Na Mbingu (Death And Heaven)

Kifo Na Mbingu (Death And Heaven) Kifo Na Mbingu (Death And Heaven) Na Ellis P. Forsman The Rapture And Millennialism 1 Kifo Na Mbingu Na Ellis P. Forsman Octoba 11, 2011 The Rapture And Millennialism 2 Kifo Na Mbingu Heb. 9:27 Ili kufika

More information

Uongozi Siri Na Larry Chkoreff. Version 1.2 Desemba 2010

Uongozi Siri Na Larry Chkoreff. Version 1.2 Desemba 2010 Uongozi Siri Na Larry Chkoreff Version 1.2 Desemba 2010 Kimetafsiriwa na kuchapishwa na: Cistern Materials Translation & Publishing Center, Nairobi, Kenya Barua pepe: info@cisternmaterialscenter.com www.cisternmaterialscenter.com

More information

UNABII WA BIBLIA. CBM Publishing 32 Blenheim Road, Far Cotton Northampton, England. NN4 8NW

UNABII WA BIBLIA. CBM Publishing 32 Blenheim Road, Far Cotton Northampton, England. NN4 8NW Kama unataka kujifunza zaidi njia ya Mkristo wa kweli anavyopaswa kuishi, basi ni lazima ujifunze Biblia. Ili kukusaidia; Kanise la Christadelphian Bible Mission limechapisha kijitabu kuhusu mafunzo ya

More information

YEHOVA-YIRE 1. 2 Baba yetu wa Mbinguni, tunakikaribia Kiti Chako cha. 3 Tunakushukuru kwa kutuzuru jana jioni. Tunaomba

YEHOVA-YIRE 1. 2 Baba yetu wa Mbinguni, tunakikaribia Kiti Chako cha. 3 Tunakushukuru kwa kutuzuru jana jioni. Tunaomba YEHOVA-YIRE 1 Na tuendelee kusimama tu kwa muda kidogo wakati, tumeinamisha vichwa vyetu kwa maombi. Tunapoinamisha vichwa vyetu, sijui ni wangapi usiku huu wangetaka kukumbukwa katika maombi, una jambo

More information

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO Tel. +255748-537720/632013, P.O.BOX 6049 MOROGORO E-Mail info@ tist.org April 2004 Take care of your seedlings This year, thousands of seedlings have been planted in the TIST

More information

MTIHANI WA MWIGO WILAYA YA BUTERE MUMIAS-2007 Hati ya kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya

MTIHANI WA MWIGO WILAYA YA BUTERE MUMIAS-2007 Hati ya kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya Jina Nambari.. Shule... 102/3 KISWAHILI FASIHI KARATASI YA 3 JULAI / AGOSTI. 2007 MUDA: SAA 2 ½ MTIHANI WA MWIGO WILAYA YA BUTERE MUMIAS-2007 Hati ya kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya 102/3 KISWAHILI FASIHI

More information

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) VERBATIM REPORT OF CONSTITUENCY PUBLIC HEARINGS, BARINGO EAST CONSTITUENCY, HELD AT KOLLOWA

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) VERBATIM REPORT OF CONSTITUENCY PUBLIC HEARINGS, BARINGO EAST CONSTITUENCY, HELD AT KOLLOWA CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) VERBATIM REPORT OF CONSTITUENCY PUBLIC HEARINGS, BARINGO EAST CONSTITUENCY, HELD AT KOLLOWA ON 3 RD JULY 2002 2 CONSTITUENCY PUBLIC HEARINGS, BARINGO EAST

More information

KISWAHILI KARATASI YA 2 LUGHA

KISWAHILI KARATASI YA 2 LUGHA KISWAHILI KARATASI YA 2 LUGHA Maagizo (a) Andika jina lako na namba yako katika nafasi ulizoachiwa hapo juu. (b) Tia sahihi yako na tarehe ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu. (c) Jibu maswali

More information

Inavyodaiwa na wanaochanganya Biblia. Ellis Forsman. Inavyodaiwa na Wanao changanya Biblia (Alleged Bible Contradictions) 1

Inavyodaiwa na wanaochanganya Biblia. Ellis Forsman. Inavyodaiwa na Wanao changanya Biblia (Alleged Bible Contradictions) 1 Inavyodaiwa na wanaochanganya Biblia na Ellis Forsman Inavyodaiwa na Wanao changanya Biblia (Alleged Bible Contradictions) 1 Inavyodaiwa na wanaochanganya Biblia na Ellis Forsman Oktoba 8, 2011 Inavyodaiwa

More information

MUNGU ANADHIHIRISHWA KUPITIA KWA YESU KRISTO.

MUNGU ANADHIHIRISHWA KUPITIA KWA YESU KRISTO. MUNGU ANADHIHIRISHWA KUPITIA KWA YESU KRISTO. MUHTASARI WA UTANGULIZI WA THIOLOGIA YA USHIRIKA WA NAFSI TATU ZA UUNGU. GRACE COMMUNION INTERNATIONAL LIVING AND SHARING THE GOSPEL MUNGU ANADHIHIRISHWA NA

More information

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara Umetayarishwa na Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania kwa Kushirikiana na Idara ya Maendeleo

More information

MUNGU ALIUMBA ULIMWENGU 1 WETU NA VYOTE VILIVYO HAI

MUNGU ALIUMBA ULIMWENGU 1 WETU NA VYOTE VILIVYO HAI MUNGU ALIUMBA ULIMWENGU 1 WETU NA VYOTE VILIVYO HAI Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. Mwanzo 1:1 Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi. Wakolosai

More information

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora K I T A B U C H A M B I N U B O R A C H A T O A U k u r a s a 1 TANZANIA OSAKA ALUMNI Kitabu cha Mbinu Bora Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa P.O. Box 1923, Dodoma. Novemba, 2012

More information

Mhashamu Askofu Jude Thaddaeus Ruwa ichi, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania; Mwadhama Policarp Kardinali Pengo,

Mhashamu Askofu Jude Thaddaeus Ruwa ichi, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania; Mwadhama Policarp Kardinali Pengo, HOTUBA YA MHESHIMIWA MIZENGO P. PINDA (MB), WAZIRI MKUU, KWENYE SHEREHE YA KUADHIMISHA MIAKA HAMSINI YA BARAZA LA MAASKOFU KATOLIKI TANZANIA, TAREHE 08 JUNI 2008, MSIMBAZI CENTRE, DAR ES SALAAM Mhashamu

More information

Tanzania, sasa kondoo anayesubiri kuchinjwa

Tanzania, sasa kondoo anayesubiri kuchinjwa facebook: annuurpapers@yahoo.com Sauti ya Waislamu AHLU SUNNA WAL JAMAA HAJJ AND UMRA TRUST (9) UOMBEZI WA MTUME(SAW) ISSN 0856-3861 Na. 1176 RAJAB 1436, IJUMAA, MEI 8-14, 2015 BEI TShs 800/=, Kshs 50/=

More information

JE! MUNGU ANAMPA MWANAMKE HAKI YA KUTOA MIMBA IWAPO NI MHANGA WA UBAKAJI?

JE! MUNGU ANAMPA MWANAMKE HAKI YA KUTOA MIMBA IWAPO NI MHANGA WA UBAKAJI? Jarida la Dunia Yerusalemu Mpya Mchungaji Tony Alamo Makanisa Ulimwenguni Kote Taifa la Kikristo la Alamo Mchungaji Tony na Susan Alamo, Okestra, na kwaya katika kipindi chao cha kimataifa cha televisheni.

More information

Kiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika

Kiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika Kiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika Stephen N. Kamau Abstract It is a fact that in the recent past, globalization has gradually taken shape in Africa and as such the continent has no choice but to

More information

Vijana wanazungumza kuhusu ujinsia, maisha na uhusiano VIJANA WANAZUNGUMZA KUHUSU NGONO, MAISHA NA UHUSIANO. Training and Research Support Centre

Vijana wanazungumza kuhusu ujinsia, maisha na uhusiano VIJANA WANAZUNGUMZA KUHUSU NGONO, MAISHA NA UHUSIANO. Training and Research Support Centre Shangazi Stella Vijana wanazungumza kuhusu ujinsia, maisha na uhusiano VIJANA WANAZUNGUMZA KUHUSU NGONO, MAISHA NA UHUSIANO Training and Research Support Centre Zimbabwe Shangazi Stella Kiongozi cha Mwezeshaji

More information

Watumishi Wa Kristo. Ellis P. Forsman. Watumishi Wa Kristo (Servants Of Christ) 1

Watumishi Wa Kristo. Ellis P. Forsman. Watumishi Wa Kristo (Servants Of Christ) 1 Watumishi Wa Kristo na Ellis P. Forsman Watumishi Wa Kristo (Servants Of Christ) 1 Watumishi Wa Kristo na Ellis P. Forsman Oktoba 14, 2011 Watumishi Wa Kristo (Servants Of Christ) 2 Sisi ni watumishi Watumishi

More information

Makasisi. Waingia Uislamu

Makasisi. Waingia Uislamu 1 Makasisi Waingia Uislamu 2 KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU MAKASISI WAINGIA UISLAMU Yaliyomo 1. KASISI YUSUFU ESTES ALIYEKUWA MFANYABIASHARA WA KIKRISTO & MUHUBIRI (USA)...

More information

LALA. Terry Warford. LALA (Sleep - Terry Warford) 1

LALA. Terry Warford. LALA (Sleep - Terry Warford) 1 LALA na Terry Warford LALA (Sleep - Terry Warford) 1 LALA na Terry Warford Novemba 6, 2011 LALA (Sleep - Terry Warford) 2 LALA Kulala ni sehemu muhimu katika maisha yetu ya kila siku, tukiipa akili zetu

More information

TIST HABARI MOTO MOTO. Benefits of Loan Repayment. Faida za ulipaji wa mikopo U OTESHAJI W A M ITI Y A M ATUNDA

TIST HABARI MOTO MOTO. Benefits of Loan Repayment. Faida za ulipaji wa mikopo U OTESHAJI W A M ITI Y A M ATUNDA TIST HABARI MOTO MOTO Tel. 026-2322246, P.O.BOX 53 MPWAPWA E-Mail tist@ twiga.com 01 June 2001 Benefits of Loan Repayment As the date of repayment nears, 15 June, groups are busy preparing crops, digging

More information

Mwongozo wa Familia wa Kujifunza

Mwongozo wa Familia wa Kujifunza Shule za umma za kata ya Fayette 1 Mwongozo wa Familia wa Kujifunza Muhtasari wa yale watoto wanastahili kufahamu na kuweza kufanya na njia za familia kuongeza masomo nyumbani. Tunaamini familia ni wenzetu.

More information

Oktoba-Desemba

Oktoba-Desemba Oktoba-Desemba 2014 1 Habari za Unabii wa Biblia 8 13 24 Katika toleo hili: 25 28 33 3 MwanaFiladelfia wa Karne ya 21 ni nani? Je, Yesu alifundisha kwamba kungekuwepo na tofauti kubwa baina ya Wakristo

More information

Aina Tatu Za Ibada. Ellis Forsman. Aina Tatu Za Ibada (Three Kinds Of worship) 1

Aina Tatu Za Ibada. Ellis Forsman. Aina Tatu Za Ibada (Three Kinds Of worship) 1 Aina Tatu Za Ibada na Ellis Forsman Aina Tatu Za Ibada (Three Kinds Of worship) 1 Aina Tatu Za Ibada na Ellis Forsman Octoba 15, 2011 Aina Tatu Za Ibada (Three Kinds Of worship) 2 Aina Tatu Za Ibada Yoh.

More information

RISALA FUPI YA KUMUWEZESHA MTU KUPAMBANUA NI IPI DINI YA HAKI MWANDISHI: SALEH M. KYAMBO

RISALA FUPI YA KUMUWEZESHA MTU KUPAMBANUA NI IPI DINI YA HAKI MWANDISHI: SALEH M. KYAMBO RISALA FUPI YA KUMUWEZESHA MTU KUPAMBANUA NI IPI DINI YA HAKI MWANDISHI: SALEH M. KYAMBO 1 RISALA FUPI copyright Hidaya Creativity, publishing Department. P.O. BOX 44799, 00100, GPO, NAIROBI-KENYA. Haki

More information

JE, YAWEZEKANA KUISHI BILA KUTENDA DHAMBI?

JE, YAWEZEKANA KUISHI BILA KUTENDA DHAMBI? JE, YAWEZEKANA KUISHI BILA KUTENDA DHAMBI? JOE CREWS 1 JE, YAWEZEKANA KUISHI BILA KUTENDA DHAMBI? Na Joe Crews (Hotuba Na. 16 ya Mambo ya Kweli Yanayoshangaza) Mfasiri: M. Mwamalumbili Is It Possible To

More information

Kocha Mkuu. mabingwa. itakuwa INASTAHILI. Ili Kutoa mafunzo kwa wanafunzi wako kuwa. itakuwa ya kuumiza. Itachukua muda. Itahitaji moyo wa kujitoa.

Kocha Mkuu. mabingwa. itakuwa INASTAHILI. Ili Kutoa mafunzo kwa wanafunzi wako kuwa. itakuwa ya kuumiza. Itachukua muda. Itahitaji moyo wa kujitoa. Ili Kutoa mafunzo kwa wanafunzi wako kuwa mabingwa itakuwa ya kuumiza. Itachukua muda. Itahitaji moyo wa kujitoa. Mkuu Inahitaji dhabihu. Unahitaji kujisukuma hadi mwisho wako. Lakini nakupa ahadi hii,

More information

IM ETUPASA KUTIMIZA HA KI YOTE

IM ETUPASA KUTIMIZA HA KI YOTE IM ETUPASA KUTIMIZA HA KI YOTE Daima ni majaliwa kuja kwenye nyumba ya Bwana., Kamwe, maishani mwangu, sijaona wakati mmoja nilijutia kuja kwenye nyumba Yake. Ni ninii Lakini ninadhani asubuhi ya leo ndio

More information

Piganieni haki zenu Bungeni

Piganieni haki zenu Bungeni Mpenzi msomaji ANNUUR linapatikana kwa Shs 800/= tu Sauti ya Waislamu AHLU SUNNA WAL JAMAA HAJJ AND UMRA TRUST ISSN 0856-3861 Na. 1167 JAMADIUL AWWAL 1436, IJUMAA, MACHI 6-12, 2015 BEI TShs 800/=, Kshs

More information

IMANI NA MATENDO ELLEN G. WHITE

IMANI NA MATENDO ELLEN G. WHITE IMANI NA MATENDO ELLEN G. WHITE IMANI NA MATENDO IMANI NA MATENDO Hotuba na Makala za Ellen G. White Masomo kutoka katika Hotuba zake Kumi na Tisa zilizotolewa Nzima au kwa Sehemu kuanzia mwaka 1881

More information

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada? Policy brief TZ.12/2010K Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada? 1. Utangulizi Kila mwaka Bunge la Tanzania hupitia na kuchanganua kwa makini bajeti ya Serikali.

More information

2 FEBRUARI, 2015 BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA NANE. Kikao cha Sita - Tarehe 2 Februari, 2015

2 FEBRUARI, 2015 BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA NANE. Kikao cha Sita - Tarehe 2 Februari, 2015 BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA NANE Kikao cha Sita - Tarehe 2 Februari, 2015 (Mkutano Ulianza Saa tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa

More information

2 LILE NENO LILILONENWA

2 LILE NENO LILILONENWA MAJINA YA MA KUFURU Asante, Ndugu Neville. Jambo hili lilikuwa kwa namna, fulani la la kustaajabisha kwangu. Sikutegemewa kuwepo hapa leo; bali usiku wa leo ni usiku wa Ushirika, nami nami niliona ningeshuka

More information