Agano Lililofunikwa Kwa Damu

Similar documents
"ATATOKEA MARA YA PILI, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu." Waebrania 9:28.

Nia Dhidi Ya Kristo Je Unamheshimu?

MUNGU ALIUMBA ULIMWENGU 1 WETU NA VYOTE VILIVYO HAI

Inavyodaiwa na wanaochanganya Biblia. Ellis Forsman. Inavyodaiwa na Wanao changanya Biblia (Alleged Bible Contradictions) 1

Ushindi ndani ya Kristo W. W. PRESCOTT

Kwa Nini Yesu Alikufa Msalabani?

Kifo Na Mbingu. (Death And Heaven) Ellis P. Forsman. Kifo Na Mbingu (Death And Heaven) 1

MUNGU ANADHIHIRISHWA KUPITIA KWA YESU KRISTO.

Mzabibu Na Matawi. (The Vine And The Branches) Ellis P. Forsman. Mzabibu Na Matawi (The Vine And The Branches) 1

Theolojia Ujumla. Mike Taylor Semester Munguishi Bible College

Watumishi Wa Kristo. Ellis P. Forsman. Watumishi Wa Kristo (Servants Of Christ) 1

Mafundisho Ya Msingi Wa Kikristo. Na Andrew Connally

WAKOLOSAI MTAALA. B. Maoni: Tunapendekeza uwe na fafanuzi (commentary) yoyote yenye kushikilia mafundisho ya awali (conservative) katika Wakolosai.

WAFUNAJI WA NAFSI ABC By Vagn Rasmussen Translation by Lydia Madsen

Information for assessors (do not distribute this page to participants):

BIBLICAL INSTRUCTION AND ENCOURAGEMENT FOR THE MAFUNDISHO YA BIBLIA NA HIMIZO KWA MISSION FIELD WORLDWIDE. KAZI YA KIMISHENI ULIMWENGUNI KOTE

B. Wanafunzi watapata ufahamu mkubwa wa kitabu hiki, na jinsi kinavyofundisha kuhusu kanisa.

GRACE COMMUNION INTERNATIONAL KANUNI YA IMANI

Kifo Na Mbingu (Death And Heaven)

Silaha Za Shetani. Ellis Forsman. Silaha Za Shetani (The Devices of Satan) 1

Patanishwa, Hesabiwa Haki, Takaswa

Adhabu ya jino kwa jino na Musitakabali wa imani zetu

JE, YAWEZEKANA KUISHI BILA KUTENDA DHAMBI?

Tazama Yuaja. Kuhusu Toleo Hili. Umuhimu wa Mafundisho ya Biblia. Nguvu katika neno la Mungu.

IMANI NA MATENDO ELLEN G. WHITE

Kiumbe Kipya Katika Kristo

WEWE NI NANI? Toleo X Toleo Ukweli wa Injeli Toleo 23

Aina Tatu Za Ibada. Ellis Forsman. Aina Tatu Za Ibada (Three Kinds Of worship) 1

Kanuni. Muhimu za Kujifunza Biblia. Mchungaji Drue Freeman. Dan Hawkins & Joseph Brown. General Editors.

walozaliwa, si kwa damu, wala mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, mbali kwa Mungu. Sisi sio tena binadamu wa kawaida tu kwa sababu sisi ni w

Ellen White, waasisi wa Kiadventista,na Sabato Lunar

MELKISEDECK LEON SHINE. katoliki.ackyshine.com

usudi la Maisha Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na kupishana usiku na mchana, kuna kweli ishara kwa wenye akili, ambaye mkumbuke-

Roho Mtakatifu Ni Nini?

Maisha Yaliyojaa Maombi

Ndugu na dada zangu wapendwa,

United Pentecostal Church June 2017

Maisha Ya Mkristo Ni Nini?

Mukhtasari Wa Mabishano Kwa Na Dhidi Ya Vikombe Vingi Vya Ushirika

PDF created with pdffactory trial version

ONYO LA MWISHO KWA DUNIA

Sura ya 7 Kielelezo: Tumepatanishwa na Mungu na Wanadamu

Ndugu na dada zangu wapendwa,

UJASIRI WA YOHANA MBATIZAJI

RISALA FUPI YA KUMUWEZESHA MTU KUPAMBANUA NI IPI DINI YA HAKI MWANDISHI: SALEH M. KYAMBO

UNABII WA BIBLIA. CBM Publishing 32 Blenheim Road, Far Cotton Northampton, England. NN4 8NW

FORWARD BY DANIEL SZMIOT

MASWALI NA MAJIBU JUU YA KITABU CHA MWANZO

KAMA MUNGU YU PAMOJA NASI, BASI YAKO WAPI MATENDO YAKE YA AJABU?

Tumaini Kwa Afrika. Thomas Schirrmacher. Hoja 66. Dibaji na Prof. Mchungaji Dk. Thomas K. Johnson. Thomas Schirrmacher Tumaini Kwa Afrika TASCM RVB

UKUFUNZI WENYE NGUVU MMOJA-KWA-MMOJA

UTARATIBU WA KANISA. 2 Jambo la kwanza ninalotaka kusema ni kwamba mchungaji. 3 Sisi tunaamini katika Kanisa la kimitume, tukifundisha

Kiu Cha umtafuta Mungu

Uongozi Siri Na Larry Chkoreff. Version 1.2 Desemba 2010

Pasaka Na Meza Ya Bwana Sehemu Ya 1

NGUVU. Utangulizi. Yesu alisema,

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

Na Itafunika Wingi Wa Dhambi

YEHOVA-YIRE 1. 2 Baba yetu wa Mbinguni, tunakikaribia Kiti Chako cha. 3 Tunakushukuru kwa kutuzuru jana jioni. Tunaomba

VITAMBULISHO VITA NO DHA HIRI VYA KA NISA LA KWELI LA MUNGU ALIYE HAI

MSAMAHA NA UPATANISHO

maombi, kabla tu hatujalifungua Neno hili la Kiungu.

Oktoba-Desemba

Tora UTANGULIZI KWA TORA SOMO LA KWANZA

Tafuteni Kwanza Ufalme Wa Mungu

Kwa Kongamano Kuu 2016

LALA. Terry Warford. LALA (Sleep - Terry Warford) 1

JE! MUNGU ANAMPA MWANAMKE HAKI YA KUTOA MIMBA IWAPO NI MHANGA WA UBAKAJI?

Uponyaji Wa Laana. (Kumb. 28:1-14).

Kuiponya Picha Tuliyonayo Kuhusu Mungu

KUTAMBUA SIKU YA KO NA UJUMBE WAKE

UZAO WA NYOKA. 2 Basi, usiku huu, tuna malimbuko tu ya utukufu huo mkuu. 3 Kwa uchaji tunasimama kwa imani yetu katika Uwepo

KWA NINI SISI SI MADHEHEBU?

Hakimiliki na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa TAFSIRI YA BIBLIA. Mwandishi. Jonathan M. Menn

Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya Tanzania

United Pentecostal Church April Kushangilia Kwa Sala

MWONGOZO WA NAMNA YA KUHAMASISHA MAOMBI YA MCHANA NA USIKU YA SIKU 10.

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

# 18 Uponyaji Kutokana na Kukataliwa

2 LILE NENO LILILONENWA

IM ETUPASA KUTIMIZA HA KI YOTE

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

Juni 3-9 Pata Manufaa Kamili kwakusomabiblia

MTIHANI WA MWIGO WILAYA YA BUTERE MUMIAS-2007 Hati ya kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya

Ndugu na dada zangu wapendwa,

Kuwa Macho Na Mbwa Mwitu (Watch Out for Wolves)

UNABII WA HABARI ZA BIBLIA

Mwabudu Yehova, Mfalme wa Umilele. Miaka 100 ya Utawala wa Ufalme Inakuhusuje? UKURASA WA 12 NYIMBO: 97, 101. Kufanya Maamuzi ya Hekima Ukiwa Kijana

Haja Ya Dini. Author(s): Publisher(s): Translator(s): Category: Topic Tags: Featured Category: Published on Al-Islam.org (

Makasisi. Waingia Uislamu

H. M. Baagil, M. D. WAMY Studies on Islam

Ufunguo wa Kutaalamika Haraka

Mabingwa kwa ajili ya tunda la Roho Mtakatifu. Iliyoendelea sana. Iliyoendelea sana. Kitabu cha mwanafunzi

Mwongozo wa Kanisa la Waadventista wa Sabato

MAFUNDISHO YA UMISHENI

Rahisi. Mabingwa kwa ajili ya tunda la Roho Mtakatifu. Kitabu cha mwanafunzi. Rahisi

MAHUBIRI TUNAYOWEZA KUONA

Rahisi. Kitabu cha mwanafunzi. Mabingwa kwa ajili ya tunda la Roho Mtakatifu. Rahisi

Kufunga Milango - Uponyaji Kutokana na Athari za Giza

IBADA NA UMOJA WA KANISA Na Mchg. Dkt. Msafiri Mbilu

Transcription:

Agano Lililofunikwa Kwa Damu na Ellis Forsman Agano Lililofunikwa Kwa Damu (The Blood-Sealed Covenant) 1

Agano Lililofunikwa Kwa Damu na Ellis Forsman Oktoba 14, 2012 Agano Lililofunikwa Kwa Damu (The Blood-Sealed Covenant) 2

Agano Lililofunikwa Kwa Damu Ebr. 9: Somo la Kuzingatia leo ni Agano Lililofunikwa Kwa Damu. Je unakumbukwa kwamba katika kila nyakati iwe nyakati za Agano la Kale na Agano Jipya, kumekuwa na umuhimu uliyoshikanishwa katika damu na Mungu katika mpango wake wa wokovu? Iwe wakati wa Mababu (kwanzia na Adamu), wakati wa Musa (kwanzia kutolewa kwa Sheria ya Musa), au wakati wa Wakristo wa Agano Jipya, Mungu wetu kila mara amekuwa akitumia damu katika mpango wake unaookoa. Bila kujali dhihaka ya mwanadamu wa leo ya kile kinachoitwa dini ya damu, mfumo mwingi wa Biblia unazunguka matumizi ya damu. Kwa wakati huu ningekupendekezea uzingatie mafundisho ya Neno la Mungu kuhusu Agano Lililofunikwa kwa Damu. Dhambi na damu Ukweli unafahamika zaidi kwa mwanadamu ni dhambi! Kila kaburi ulilowahi kusimama pembeni yake, kila chozi ambalo limewahi kuteremka shavuni kwako, kila ugonjwa ulilowahi kupitia zimetokea kwa sababu ya dhambi; kama siyo moja kwa moja, lililetwa kwa sababu ya dhambi ya kwanza katika Bustani ya Edeni. Tunapofikiria ukweli kwamba ni damu pekee ya Kristo inayoweza kuondoa dhambi, basi inakuwa vyema kwamba somo hili ni la muhimu sana. Dhabihu za damu katika wakati wa Mababu Wakati wa Mababu, ukianzia kwa Adamu na Eva ukishuka chini hadi katika kutolewa Sheria ya Musa, damu iliyotolewa dhabihu ya wanyama ilihitajika na Mungu. Katika Familia ya kwanza, ndugu wawili, Kaini na Abili, walitoa dhabihu kwa Mungu. Kwa ushahidi, tunaweza kuona kwamba dhabihu ya damu iliamuriwa na Mungu. Mwanzo 4:2-5, Akaongeza akamzaa ndugu yake Habili. Habili alikuwa mchunga kondoo, na Kaini alikuwa mkulima ardhi. Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa BWANA. Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na Agano Lililofunikwa Kwa Damu (The Blood-Sealed Covenant) 3

sehemu zilizonona za wanyama. BWANA akamtakabali Habili na sadaka yake; bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana. Ebr. 11:4, Kwa imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo ijapokuwa amekufa, angali akinena. Ukweli ni kwamba sadaka ya Habili ilifanywa kwa imani, inaonyesha kwamba Mungu aliagiza aina ya dhabihu aliyopenda. Rum. 10:17, Basi imani chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Mungu. Hivyo basi, Habili alitoa sadaka yake kulingana na maagizo ya Mungu, siyo mapenzi yake binafsi au mawazo yake. Kwa vile sadaka ya Kaini ilikataliwa, na kwa agizo la hitaji la Mungu kwa ajili ya agano la damu katika nyakati zingine, ni wazi kwamba damu ya wanyama iliyotolewa dhabihu tu ndiyo ambayo Mungu aliwaambia. Tunaokolewa kwa damu Pasaka Dhabihu kwa Mungu zilizofanywa na wana wa Israeli na kusheherekea Pasaka ni mifano ya umuhimu wa damu. Sura ya 12 ya kitabu cha Kutoka inafunua hadithi dhabihu zilizotelewa pamoja na kuanzishwa kwa Pasaka. Sikukuu hii ilianzishwa katika kilele cha kuondoka kwa Waisraeli katika utumwa wa Kimisri katika karne zote, kwa ukumbusho wa tukio la uhuru. Katika usiku huo wa maajabu, Waisraeli walipaswa kuchukua damu ya mwanakondoo na kuipaka katika miimo ya milango ambayo Pasaka iliandaliwa. Mungu aliahidi kwamba atakapoona damu malaika wa kifo atapita juu ya nyumba hizo. Atawaokoa na kifo. Malaika wa kifo alifanya kama ilivyoahidiwa, akipiga tu Wamisri wasiotahiriwa ambao hawakujikinga kwa damu. Damu ya utii ilimaanisha wokovu. Pasipo damu katika miimo ya milango, kifo kilikuwa ni lazima; pasipo kutii, kifo kilikuwa ni lazima. Kuja kwa mara ya Mwisho Kuna ulinganifu kati ya tukio hili na siku ya kuja kwake Bwana nyakati za mwisho, atakapotokea kwa mara nyingine kama malaika wa kisasi kuwaadhibu wale ambao hawajaitii injili, na ambao hawajakingwa na damu ya Mwana Kondoo wa uzima. Agano Lililofunikwa Kwa Damu (The Blood-Sealed Covenant) 4

Katika 2 Thes. 1:7-9, Biblia inatuonya kwamba wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake katika mwali wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu, na wao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu; watakaoadhibiwa kwa maangamizi ya milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake; Leo, sawa na jinsi ilivyokuwa katika Agano la Kale, yuko katika damu ya agano iliyofunikwa! Ukweli wa Injili Kuhusu kifo, maziko na ufufuo wa Kristo unaanzisha msingi wa Injili, uwezo wa Mungu uuletao wokovu. Ukweli kuhusu Mwana wa Mungu lazima iaminiwe na tuyatii maagizo yake, kama damu iokoayo inaweza kusaidia nafsi za wanadamu. Marko 16:16, Aaminiye na kubatizwa ataokoka asiyeamini atahukumiwa. Nisawa na kuwa hakungekuwa na sababu ya kibinadamu, ao maantinki ya mwanadamu, iliyohushishwa katika damu juu ya miimo ya milango katika kula Pasaka na kutolewa kwao kutoka kwa malaika wa kifo, hivyo, kwa wengi, inaweza kuonekana kwamba hakuna dalili ya imani, toba, kukiri, ubatizo, na ondoleo la dhambi zetu leo. Hataivyo, katika maswala yote, haijalishi kwamba ama tunaelewa au hapana hekima ya mapenzi ya Mungu; afadhali, tukubali ukweli kwamba Mungu amenena na ni jukumu letu kuamini na kutii! Tunaweza kufahamu kwa yetu ni agano lililofunikwa kwa damu, pia, na kwamba Mungu atatunza ahadi zake kwetu sisi sawa na jinsi alivyofanya na Israeli, kama tukimtii. Kipindi cha Musa na damu Hebu kidogo tuangalie Kipindi cha Musa. Tunakuta ndani yake, pia, kwamba Mungu alihitaji damu iliyohusisha damu. Agano Jipya, katika kuangalia nyuma katika Agano la Kale, inaweka wazi: Ebr, 9:18-22, Kwa hiyo hata lile la kwanza halikuanzwa pasipo damu. Maana kila amri ilipokuwa imekwisha kunenwa na Mungu kwa hao watu wote, kama ilivyoamuru sheria, aliitwaa damu ya ndama na ya mbuzi, pamoja na maji na sufu nyekundu na hisopo akakinyunyizia kitabu chenyewe na watu wote, akisema hii ni damu ya agano mliloamuriwa na Mungu. Na ile hema yote nayo na vyombo vyote vya ibada alivinyunyizia damu vivyo hivyo. Na katika torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo. Agano Lililofunikwa Kwa Damu (The Blood-Sealed Covenant) 5

Katika kipindi cha Musa, damu iliyofunikwa agano la Mungu lililovuviwa. Hema pamoja na vyombo vyake vyote vya huduma vilisafishwa kwa damu. Kulikuwa na dhabihu za mara kwa mara ambazo zilikuwa zinatolewa kila mara, kulingana na vifungu saba za kwanza vya Mambo ya Walawi. Damu chini ya Sheria ya Kale, Ukumbusho Damu yote ile ya wanyama wa dhabihu wa wakati wa Agano la Kale isingeweza kuondoa dhambi za watu, hataivyo. Agano Jipya linafunua kwamba zilikuwa tu kivuli cha damu hiyo yenye nguvu ya Mwana Kondoo wa Mungu, ambayo ingekuja baadaye. Damu ya Kristo, Mwana Kondoo wa Mungu, ingeweza kwa hakika na kusafisha dhambi za wanadamu kabisa. Ebr. 10:1-4, Basi torati kwa kuwa ni kivuli cha mema yatakayokuwa wala si sura yenyewe ya mambo hayo, kwa dhabihu zile zile wanazozitoa kila mwaka daima, haiwezi wakati wowote kuwa kamilisha wakaribiao. Kama ndivyo, je! Dhabihu hazingekoma kutolewa; kwa maana waabuduo wakiisha kusafishwa mara moja, wasingejiona tena kuwa na dhambi? Lakini katika dhabihu hizo liko kumbukumbu la dhambi kila mwaka. Maana haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi. Dhambi kwa hakika isingeweza kuondolewa kupitia damu ya wanyama chini ya Agano la Kale. Bali kwa dhabihu zile, zilizoamriwa na Mungu, kulikuwa na kumbukumbu ya iliyofanywa kwa ajili ya dhambi kila mwaka. Wanyama wenye damu waliotolewa dhabihu ya nyakati hizo isingeweza kusafisha watu na dhambi zao. Zilikuwa ni kivuli iliyowaongoza watu katika damu ya Kristo, kama ilivyofunuliwa katika Agano Jipya, ambayo kwa hakika uondoa dhambi ya mtu. Gal. 3:24-27, Hivyo torati imekuwa kiongozi kutuleta kwa Kristo, ili tuhesabiwe haki kwa imani. Lakini iwapo imani imekuja, hatupo tena chini ya kiongozi. Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu. Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo Yesu mmemvaa Kristo. Damu katika Wakati wa Wakristo Leo tunaishi katika Wakati wa Kristo. Agano Jipya linaongelea damu ya Kristo kama dhabihu yetu. Agano Lililofunikwa Kwa Damu (The Blood-Sealed Covenant) 6

Ebr. 10:19-20, Basi ndugu kwa kuwa tunaujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu, njia ile aliyotuanzia iliyo mpya iliyo hai, ipitayo katika pazia, yaani mwili wake; Njia hii mpya, kwa njia ya damu ya Kristo, ilitabiriwa na waandishi wa Agano la Kale, ambao Mtume Petro ameandika: 1 Pet. 1:10-11, Katika habari ya wokovu huo manabii walitafuta-tafuta na kuchunguza chunguza, ambao walitabiri habari ya neema itakayowafikia ninyi. Wakatafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakao kuwako baada ya hayo. Nabii Isayaalikuwa mmoja kati ya hao aliyeongea kwa uwazi kuhusu kifo kijacho na kuinuliwa kwa Masihi. Isa. 53:4-6, Hakika ameyachukua masikitiko yetu, amejitwika huzuni zetu; lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, amepigwa na Mungu na kuteswa. Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu; adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. Sisi sote kama kondoo tumepotea; kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; na BWANA ameweka juu yake maovu yetu sisi sote. Katika mistari ya 10-12 ya kifungu hiki cha unabii, nabii anahitimisha: Isa. 53:10-12, Lakini BWANA aliridhika kumchbua; amemhuzunisha; utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi, ataona uzao wake ataishi siku nyingi, na mapenzi ya BWANA yatafanikiwa mkononi mwake; ataona mazao ya taabu ya nafsi yake, na kuridhika. Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye haki atawafanya wengi kuwa wenye haki; naye atayachukua maovu yao. Kwa hiyo nitamgawia sehemu pamoja na wakuu, naye atagawanya nyara pamoja nao walio hodari; kwa sababu alimwaga nafsi yake hata kufa, akahesabiwa pamoja na hao makosa. Walakini alichukua dhambi za watu wengi, na kuwaombea wakosaji. Karibia kila nabii wa wakati wa Agano la Kale alisema kuja kwa Mwana Kondoo wa Mungu. Nabii wa mwisho, Yohana Mbatizaji, alitangaza kuhusu Kristo: Yoh. 1:29-34, Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema tazama Mwana Kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu! Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba yuaja mtu nyuma yangu ambaye amekuwa mbele yangu. Wala mimi sikumjua lakini kusudi adhihirishwe kwa Israeli ndiyo maana mimi nalikuja nikibatiza kwa maji.tena Yohana akashuhudia akisema, nimemwona Roho akishuka kama hua kutoka mbinguni naye akakaa juu yake. Wala mimi sikumjua; lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyo aliniambia huyo Agano Lililofunikwa Kwa Damu (The Blood-Sealed Covenant) 7

ambaye utamwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu. Nami nimeona, tena nimeshuhudia kwa kuwa Huyu ni Mwana wa Mungu. Kifo Na Kuinuliwa Kwa Kristo Yesu Kristo, ambaye Yohana amemzungumzia, aliishi miongoni mwa wanadamu wa dunia hii kwa miaka thelathini kabla hajapelekwa gerezani ghafla na kuawa. Aliacha utukufu wa mbinguni ili aje duniani na kufanya kazi yake ya kipekee. Mtume Paulo aliwahimiza Wakristo: Fil. 2:5-11, Iweni na iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu akatwaa namna ya mtumwa akawa anamfano wa wanadamu; tena alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam mauti ya msalaba. Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba. Ndiyo, Yesu Kristo alikuja ulimwenguni humu kama zawadi ya upendo wa Mungu, kujitoa yeye mwenyewe katika nafasi yetu kwa ajili ya dhambi zetu! Wazo hili lazima lisaidie kila mmoja wetu.! Paulo, katika kulinganisha Agano la Kale na Agano Jipya, anasema: Ebr. 9:13-14, Kwa maana ikiwa damu ya mbuzi na mafahali na majivu ya ndama ya ng ombe waliyonyunyiziwa wenye uchafu hutakasa hata kuusafisha mwili; basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo machafu mpate kumwabudu Mungu aliye hai? Hakika, hakuna shaka kuhusu uwezo wa kusafisha na kutakasa wa damu ya Kristo. Nafsi ya mwanadamu inasafishwa na kutakaswa ili kwamba aweze kumtumikia Mungu aliye hai! Dhabihu Moja ya mwisho Umuhimu ujao wa dhabihu ya Kristo ilikuwa ni hitimisho yake. Paulo aliandika kuhusu Agano la Kale ya Musa, akisema: Agano Lililofunikwa Kwa Damu (The Blood-Sealed Covenant) 8

Ebr. 10:9-12, Ndipo aliposema, tazama nimekuja niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza, ili kusudi alisimamishe la pili. Katika mapenzi hayo mmepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu. Na kila kuhani hisimama kila siku akifanya ibada na kutoa dhabihu zile zile mara nyingi; ambazo haziwezi kabisa kuondoa dhambi. Lakini huyu alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele aliketi mkono wa kuume wa Mungu; Ndiyo, dhabihu ya damu ya Kristo ili kuwa ni dhabihu ya mara moja kwa yote. Haipaswi kurudiwa marazote, kama ilivyokuwa katika dhabihu ya wakati wa Agano la Kale. Mwandishi aliyevuviwa anathibitisha: Ebr. 10:14, Maana kwa toleo moja amekamilisha hata milele hao wanaotakaswa. Kuhani Mkuu Juu Ya Nyumba Ya Mungu Katika sura ya 10 ya kitabu cha Waebrania, Paulo anaongelea kuhani mkuu juu ya nyumba ya Mangu. Ujasiri na ukarimu wetu dhidi ya Mungu unaonekana kwa ukweli kwamba Yesu anahudumu kwa mamlaka na uwezo wa nyumba ya Mungu kama Kuhani Mkuu. Kuhani Mkuu wa Agano la Kale alikuwa ni mtu pekee ambaye angeweza kuingia patakatifu pa patakatifu katika uwepo wa Mungu. Leo, Yesu ndiye Kuhani wetu Mkuu, akifanya kazi katika uwepo wa Mungu. 1 Pet. 2:5, Ninyi nanyi kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani matakatifu mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo. Ebr. 2:17, Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake. Ebr. 8:1, Basi, katika hayo tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunaye kuhani mkuu wa namna hii, aliye keti mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni, Ebr. 4:14-15, Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu. Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi Agano Lililofunikwa Kwa Damu (The Blood-Sealed Covenant) 9

katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi. Hitimisho Tumaini yetu yote ya umilele unategemea juu ya damu inayotakasa ya Yesu Kristo, Mwana Kondoo wa Mungu! Dhambi inaweza kutia doa na kuchafua nafsi zetu, lakini damu ya Kristo itatusafisha kutoka katika uchafu huo. Isa. 1:18-19, Haya, njooni tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapo kuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu. Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;. Agano Lililofunikwa Kwa Damu (The Blood-Sealed Covenant) 10

Agano Lililofunikwa Kwa Damu (The Blood-Sealed Covenant) 11

Agano Lililofunikwa Kwa Damu (The Blood-Sealed Covenant) 12