Na Itafunika Wingi Wa Dhambi

Similar documents
Nia Dhidi Ya Kristo Je Unamheshimu?

Inavyodaiwa na wanaochanganya Biblia. Ellis Forsman. Inavyodaiwa na Wanao changanya Biblia (Alleged Bible Contradictions) 1

Agano Lililofunikwa Kwa Damu

Watumishi Wa Kristo. Ellis P. Forsman. Watumishi Wa Kristo (Servants Of Christ) 1

MUNGU ALIUMBA ULIMWENGU 1 WETU NA VYOTE VILIVYO HAI

"ATATOKEA MARA YA PILI, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu." Waebrania 9:28.

Kifo Na Mbingu. (Death And Heaven) Ellis P. Forsman. Kifo Na Mbingu (Death And Heaven) 1

Aina Tatu Za Ibada. Ellis Forsman. Aina Tatu Za Ibada (Three Kinds Of worship) 1

Ushindi ndani ya Kristo W. W. PRESCOTT

Patanishwa, Hesabiwa Haki, Takaswa

Kifo Na Mbingu (Death And Heaven)

Information for assessors (do not distribute this page to participants):

Mukhtasari Wa Mabishano Kwa Na Dhidi Ya Vikombe Vingi Vya Ushirika

Roho Mtakatifu Ni Nini?

walozaliwa, si kwa damu, wala mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, mbali kwa Mungu. Sisi sio tena binadamu wa kawaida tu kwa sababu sisi ni w

Tazama Yuaja. Kuhusu Toleo Hili. Umuhimu wa Mafundisho ya Biblia. Nguvu katika neno la Mungu.

MSAMAHA NA UPATANISHO

Kuiponya Picha Tuliyonayo Kuhusu Mungu

Silaha Za Shetani. Ellis Forsman. Silaha Za Shetani (The Devices of Satan) 1

MUNGU ANADHIHIRISHWA KUPITIA KWA YESU KRISTO.

KAMA MUNGU YU PAMOJA NASI, BASI YAKO WAPI MATENDO YAKE YA AJABU?

Maisha Ya Mkristo Ni Nini?

Theolojia Ujumla. Mike Taylor Semester Munguishi Bible College

MASWALI NA MAJIBU JUU YA KITABU CHA MWANZO

usudi la Maisha Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na kupishana usiku na mchana, kuna kweli ishara kwa wenye akili, ambaye mkumbuke-

WAFUNAJI WA NAFSI ABC By Vagn Rasmussen Translation by Lydia Madsen

Ndugu na dada zangu wapendwa,

BIBLICAL INSTRUCTION AND ENCOURAGEMENT FOR THE MAFUNDISHO YA BIBLIA NA HIMIZO KWA MISSION FIELD WORLDWIDE. KAZI YA KIMISHENI ULIMWENGUNI KOTE

UZAO WA NYOKA. 2 Basi, usiku huu, tuna malimbuko tu ya utukufu huo mkuu. 3 Kwa uchaji tunasimama kwa imani yetu katika Uwepo

Mzabibu Na Matawi. (The Vine And The Branches) Ellis P. Forsman. Mzabibu Na Matawi (The Vine And The Branches) 1

Ellen White, waasisi wa Kiadventista,na Sabato Lunar

JE, YAWEZEKANA KUISHI BILA KUTENDA DHAMBI?

Kwa Nini Yesu Alikufa Msalabani?

IMANI NA MATENDO ELLEN G. WHITE

WEWE NI NANI? Toleo X Toleo Ukweli wa Injeli Toleo 23

Mafundisho Ya Msingi Wa Kikristo. Na Andrew Connally

UTARATIBU WA KANISA. 2 Jambo la kwanza ninalotaka kusema ni kwamba mchungaji. 3 Sisi tunaamini katika Kanisa la kimitume, tukifundisha

RISALA FUPI YA KUMUWEZESHA MTU KUPAMBANUA NI IPI DINI YA HAKI MWANDISHI: SALEH M. KYAMBO

GRACE COMMUNION INTERNATIONAL KANUNI YA IMANI

WAKOLOSAI MTAALA. B. Maoni: Tunapendekeza uwe na fafanuzi (commentary) yoyote yenye kushikilia mafundisho ya awali (conservative) katika Wakolosai.

JE! MUNGU ANAMPA MWANAMKE HAKI YA KUTOA MIMBA IWAPO NI MHANGA WA UBAKAJI?

VITAMBULISHO VITA NO DHA HIRI VYA KA NISA LA KWELI LA MUNGU ALIYE HAI

Maisha Yaliyojaa Maombi

Rahisi. Kitabu cha mwanafunzi. Mabingwa kwa ajili ya tunda la Roho Mtakatifu. Rahisi

Ndugu na dada zangu wapendwa,

MELKISEDECK LEON SHINE. katoliki.ackyshine.com

maombi, kabla tu hatujalifungua Neno hili la Kiungu.

YEHOVA-YIRE 1. 2 Baba yetu wa Mbinguni, tunakikaribia Kiti Chako cha. 3 Tunakushukuru kwa kutuzuru jana jioni. Tunaomba

2 LILE NENO LILILONENWA

FORWARD BY DANIEL SZMIOT

Mutugi Kamundi. Jemma Kahn. Kiswahili. Demane na pacha wake. Author - South African Folktale

LALA. Terry Warford. LALA (Sleep - Terry Warford) 1

KUTAMBUA SIKU YA KO NA UJUMBE WAKE

Tafuteni Kwanza Ufalme Wa Mungu

Kiumbe Kipya Katika Kristo

Uongozi Siri Na Larry Chkoreff. Version 1.2 Desemba 2010

United Pentecostal Church June 2017

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level

Uponyaji Wa Laana. (Kumb. 28:1-14).

NGUVU. Utangulizi. Yesu alisema,

Kiu Cha umtafuta Mungu

B. Wanafunzi watapata ufahamu mkubwa wa kitabu hiki, na jinsi kinavyofundisha kuhusu kanisa.

KWA NINI SISI SI MADHEHEBU?

Makasisi. Waingia Uislamu

Mabingwa kwa ajili ya tunda la Roho Mtakatifu. Iliyoendelea sana. Kitabu cha mwanafunzi. Iliyoendelea sana

IM ETUPASA KUTIMIZA HA KI YOTE

Adhabu ya jino kwa jino na Musitakabali wa imani zetu

H. M. Baagil, M. D. WAMY Studies on Islam

United Pentecostal Church April Kushangilia Kwa Sala

Rahisi. Mabingwa kwa ajili ya tunda la Roho Mtakatifu. Kitabu cha mwanafunzi. Rahisi

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

UKUFUNZI WENYE NGUVU MMOJA-KWA-MMOJA

Iliyoendelea sana. Kitengo cha 2. Kitabu cha mwanafunzi Iliyoendelea sana

Sura ya 7 Kielelezo: Tumepatanishwa na Mungu na Wanadamu

Mabingwa kwa ajili ya tunda la Roho Mtakatifu. Ngumu. Ngumu. Kitabu cha mwanafunzi

UNABII WA BIBLIA. CBM Publishing 32 Blenheim Road, Far Cotton Northampton, England. NN4 8NW

Ufunguo wa Kutaalamika Haraka

Kanuni. Muhimu za Kujifunza Biblia. Mchungaji Drue Freeman. Dan Hawkins & Joseph Brown. General Editors.

Oktoba-Desemba

ONYO LA MWISHO KWA DUNIA

UNABII WA HABARI ZA BIBLIA

Ndugu na dada zangu wapendwa,

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

UJASIRI WA YOHANA MBATIZAJI

Kuwa Macho Na Mbwa Mwitu (Watch Out for Wolves)

Tora UTANGULIZI KWA TORA SOMO LA KWANZA

MAFUNDISHO YA UMISHENI

Tumaini Kwa Afrika. Thomas Schirrmacher. Hoja 66. Dibaji na Prof. Mchungaji Dk. Thomas K. Johnson. Thomas Schirrmacher Tumaini Kwa Afrika TASCM RVB

# 18 Uponyaji Kutokana na Kukataliwa

MTIHANI WA MWIGO WILAYA YA BUTERE MUMIAS-2007 Hati ya kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya

MAHUBIRI TUNAYOWEZA KUONA

MWONGOZO WA NAMNA YA KUHAMASISHA MAOMBI YA MCHANA NA USIKU YA SIKU 10.

MIAKA 500 YA MATENGENEZO YA KANISA NA USHUHUDA WETU Na Askofu Dr. Abednego Keshomshahara

Kocha Mkuu. mabingwa. itakuwa INASTAHILI. Ili Kutoa mafunzo kwa wanafunzi wako kuwa. itakuwa ya kuumiza. Itachukua muda. Itahitaji moyo wa kujitoa.

Mwongozo wa Kanisa la Waadventista wa Sabato

Kuzimu na Kurudi na Dr. Rawlings Documentary Video Transcript, TBN Films

Mabingwa kwa ajili ya tunda la Roho Mtakatifu. Iliyoendelea sana. Iliyoendelea sana. Kitabu cha mwanafunzi

Mwabudu Yehova, Mfalme wa Umilele. Miaka 100 ya Utawala wa Ufalme Inakuhusuje? UKURASA WA 12 NYIMBO: 97, 101. Kufanya Maamuzi ya Hekima Ukiwa Kijana

Pasaka Na Meza Ya Bwana Sehemu Ya 1

Kwa Kongamano Kuu 2016

Transcription:

Na Itafunika Wingi Wa Dhambi na Ellis Forsman Na Itafunika Wingi Wa Dhambi (And Shall Hide A Multitude Of Sins) 1

Na Itafunika Wingi Wa Dhambi na Ellis Forsman Oktoba 10, 2011 Na Itafunika Wingi Wa Dhambi (And Shall Hide A Multitude Of Sins) 2

Na Itafunika Wingi Wa Dhambi Yakobo 5:19-20 Yak. 5:19-20, Ndugu zangu ikiwa mtu wa kwenu amepotelewa mbali na kweli, na mtu mwingine akamrejeza; jueni ya kuwa yeye amrejezaye mwenye dhambi hata atoke katika njia ya upotevu, ataokoa roho na mauti, na kufunika wingi wa dhambi. Yakobo anatuambia ya kuwa mtu anayemwokoa mwenye dhambi katika upotevu wa njia yake, anaokoa nafsi na kufunika wingi wa dhambi. Hili linapaswa kuwa swala la umuhimu kwetu sisi sote, maana sisi sote ni wenye dhambi. Rum. 3:23, Kwa maana wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu. Zaidi sana dhambi huleta mauti ya milele. (Yakobo 5:19-20 hapo juu). Katika mtazamo wa hili, ni lazima tufurahi kwa dhambi zetu kufunikwa. Dhambi zetu zinawezaje kufichwa? Hebu na tujifunze hili, tukitazama kile ambacho hakitatufunika dhambi zetu na kile kitakachofunika dhambi zetu. Mwanadamu anajaribu kufunika dhambi zake kwa ualisia wa kuzificha Adam na Eva walijaribu kuzifunika dhambi zao kwa kuzificha kutoka katika uso wa Mungu. Mwanzo 3:8, Kisha wakasikia sauti ya BWANA Mungu ikitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, BWANA Mungu asiwaone. Haikuwasaidia, na pia haitatusaidia. Akani alijaribu hili. Yosh. 7:11, Israeli wamefanya dhambi naam wamelivunja agano langu nililowaagiza, naam; naam wametwaa baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu; tena wameiba, tena wameficha na kuvitia pamoja na vitu vyao wenyewe. Yosh. 7:21, Nilipoona katika nyara joho nzuri ya Babeli, na shekeli mia mbili za fedha, na kabari ya dhahabu, uzani wake shekel hamsini basi nalivitamani nikavitwaa, tazama vimefichwa mchangani katikati ya hema yangu,, na ile fedha chini yake. Na Itafunika Wingi Wa Dhambi (And Shall Hide A Multitude Of Sins) 3

Mungu alichukizwa na kabila lote la Israeli kwa sababu Akani alichukua nyara joho za Yeriko. Familia yake yote iliangamia kwa sababu ya kile alichokifanya. Kuficha hakukumsaidia. Juhudi hii ya kuficha dhambi haikuwapitisha hawa. Hii ni sawa pia leo. Watu hunyatia na kufanya hili na lile na kujaribu kuficha dhambi zao. Haiwezi kufanyika. Unaweza kuhakiki kuwa dhambi zako zitakuumbua. Hes. 32:23, Lakini kama hamtaki kufanya neno hilo; ninyi mmefanya dhambi mbele za BWANA, nanyi jueni ya kwamba hiyo dhambi yenu itawapata hapana budi. Wengine hujaribu kuficha dhambia zao kwa kuzikubali, na kuomba msamaha kwa kugeuzia lawama kwa wengine Adamu na Eva walijaribu hilo pia. Mwanzo 3:12-13, Adamu akasema huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala. BWANA Mungu akamwambia mwanamke nini hili ulilofanya? Mwanamke akasema nyoka alinidanganya nikala. Lakini hii ilikuwa na uhusiano gani na kosa lao? Haruni ndugu yake Musa, alijaribu mfumo huu wa kuficha dhambi zake. Kutoka 32:1-22, Hata watu walipoona ya kuwa Musa amekawia kushuka katika mlima, wakakusanyana wakamwendea Haruni wakamwambia haya katufanyizie miungu itakayokwenda mbele yetu, kwa maana Musa huyo aliyetutoa katika nchi ya Misri hatujui yaliyompata. Haruni akawaambia zivunjeni pete za dhahabu zilizo katika masikio ya wake zenu, na wana wenu, na binti zenu mkaniletee. Watu wote wakazivunja pete za dhahabu zilizo katika masikio yao wakamletea Haruni. Akaipokea mikononi mwao akaitengeneza kwa patasi akaifanya iwe sanamu wa ndama kwa kuiyeyusha, nao wakasema hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli iliyokutoa katika nchi ya Misri. Naye Haruni alipoona jambo hili, akajenga madhabahu mbele yake, Haruni akatangaza akasema, kesho itakuwa sikukuu kwa BWANA. Wakaondoka asubuhi na mapema wakatoa dhabihu, wakaleta sadaka za amani, watu wakaketi kula na kunywa, wakaondoka wacheze. BWANA akamwambia Musa haya shuka, kwa maana watu wako uliowatoa katika nchi ya Misri wamejiharibu nafsi zao; wamepotoka upesi kuiacha ile njia niliyowaamuru, wamejifanyizia ndama ya kuyeyusha wakaiabudu na kuitolea dhabihu, waksema hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli iliyokutoa katika nchi ya Misri. Tena BWANA akamwambia Musa mimi nimewaona watu hawa na tazama ni watu wenye shingo ngumu basi sasa niache ili hasira zangu ziwake juu yao, niwaangamize nami nitakufanya wewe uwe Na Itafunika Wingi Wa Dhambi (And Shall Hide A Multitude Of Sins) 4

taifa kuu. Musa akamsihi sana BWANA Mungu wake, na kusema BWANA kwa nini hasira zako kuwaka juu ya watu wako uliowaleta kutoka katika nchi ya Misri kwa uweza mkuu na kwa mkono wenye nguvu? Kwa nini Wamisri kunena amewatoa kwa kuwatenda uovu, ili apate kuwaua milimani na kuwaondoa watoke juu ya uso wan chi? Geka katika hasira yako kali, ughairi uovu huu ulio nao juu ya watu wako. Mkumbuke Ibrahimu na Isaka na Israeli watumishi wako ambao uliwaapia kwa nafsi yako, na kuwaambia nitazidisha kizazi chenu mfano wa nyota za mbinguni tena nchi hii yote niliyoinena nitakipa kizazi chenu nao watairithi milele. Na BWANA akaughairi ule uovu aliosema ya kwamba atawatenda watu wake. Basi Musa akageuka akashuka katika mlima na zile mbao mbili za mawe mikononi mwake, mbao zilizoandikwa pande zote mbili, upande huu na upande huu ziliandikwa. Na zile mbao zilikuwa kazi ya Mungu nayo maandiko yalikuwa maandiko ya Mungu, yaliyochorwa katika zile mbao. Na Yoshua aliposikia kelele za watu walipokuwa wakipiga kelele, akamwambia Musa kuna kelele ya vita maragoni. Akasema hiyo si sauti ya watu wapigao kalele kwa sababu ya kushinda vitani, wala si sauti ya watu wapigao kelele kwa sababu ya kushindwa, bali kelele za watu waimbao ndizo ninazizisikia mimi. Hata alipoyakaribia marago akaiona ile ndama na ile michezo. Hasiza ya Musa ikawaka, akazitupa zile mbao mikononi mwake, akazivunja chini yam lima. Akaitwaa ile ndama waliyoifanya akaichoma moto, akaisaga hata ikawa mavumbi, akainyunyiza juu ya maji akawanywesha wana wa Israeli. Akamwambia Haruni watu hawa wamekufanyani hata ukaleta dhambi hii kuu juu yao? Haruni akasema hasira ya bwana wangu isiwake, wewe unawajua watu hawa ya kuwa wamejielekeza kwa wabaya. Haruni hakuona weupe wo wote kwa sababu ya kilio cha watu. Bado alikuwa na hati. Watu wanajaribu kujipatia udhuru kwa njia kama hiyo leo. Wansema, marafiki zangu si Wakristo, na sitaki kuwaudhi. Lakini hiyo inahusianaje na hatia? Wengine wanajaribu kuficha dhambi zao kwa kuwatesa wanaojaribu kuwarekebisha. Wakorintho ni mfano mzuri wa hii. 2 Kor. 10:9-10, Nisije nikaonekana kana kwamba nataka kuwaogofya kwa nyaraka zangu. Maana wasema nyaraka zake ni nzito, hodari; bali akiwapo mwenyewe mwilini ni dhaifu na maneno yake si kitu. 2 Kor. 11:6-8, lakini nijapokuwa mimi ni mtu asiyeweza kunena hii si hali yangu katika elimu; ila katika kila neno nimedhihirishwa kwenu. Na Itafunika Wingi Wa Dhambi (And Shall Hide A Multitude Of Sins) 5

Tendo kama hilo linaweza kuzua moshi na kuficha hatia katika macho ya baadhi, lakini haiwezi kufunika dhambi. Ujumbe kutoka kwa manabii wa Biblia: Ujumbe wa Nuhu kuanzia hatua za kuingia katika Safina haikuwa, Haikuwa kwamba ni jambo zuri linalo kwenda kukutokea. Yeremia hakuwekwa katika tundu la simba kwa kuwaambia watu, Niko sawa., Nanyi mko Sawa.! Danieli hakuwekwa katika tundu la simba kwa kuwaambia watu, Uwezekano wa kufikiria kunaweza kuhamisha milima! Yohana mbatizaji hakulazimishwa kuhubiri katika nyika na ghafla akakatwa kichwa kwa sababu alihubiri, Tabasamu, Mungu anakupenda! Manabii wawili wa dhiki hawatauawa kwa sababu ya kuhubiri, Mungu yuko katika mbingu yake, na yote ni sawa katika dunia! Badala yake, ujumbe wa hawa watu wote wa Mungu ulikuwa ni nini? Dhairi, neno moja, Tubu! Wengine wanajaribu kuficha dhambi zao kwa kusubiri muda wa kuzisuluhisha Kaka yake Yusufu alitarajia kwamba hii ingewasaidia; lakini wakakuta kwamba dhambi zao hazikufichwa hata kwa mpito wa muda. Mwanzo 42:21-23, Wakaambiana kweli sisi tulimkosa ndugu yetu, kwa kuwa tuliona shida ya roho yake, alipotusihi wala hatukusikia kwa hiyo shida hii imetupata. Reubeni akajibu, akawaambia sikuwaambia, nikisema msimkose kijana? Wala hamkusikia kwa hiyo damu yake inatakwa tena. Wala hamkujua ya kwamba Yusufu anawasikia, kwa sababu alikuwapo mkalimani kati yao. Wanadamu wanadhamira potofu wa muda na ambacho hakitafanyika na kinachofanyika. 2 Pet. 3:3-4, Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku ya mwisho watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao tama zao wenyewe, na kusema iko wapi ahadi ile ya kuja kwake? Kwa maana tangu hapo babu zetu walipolala, vitu vyote vinakaa katika hali iyo hiyo tangu mwanzo wa kuumbwa. Na Itafunika Wingi Wa Dhambi (And Shall Hide A Multitude Of Sins) 6

Hasabu 32:23, Lakini kama hamtaki kufanya neno hilo, ninyi mmefanya dhambi mbele za BWANA nanyi jueni ya kwamba hiyo dhambi yenu itawapata, hapana budi. Ufu. 20:13, Bahari itawatoa wafu waliokuwamo ndani yake, na mauti na kuzimu zitawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. Dhambi hizo zilibebwa kwa muda mrefu. Wakati haufuti dhambi, lakini toba na kukiri zinafuta dhambi. Wengine hujaribu kuficha dhambia zao kwa kusema uongo na kuzikataa dhambi zao Sara alisema uongo ili kuficha shauku na uoga wake. Mwanzo 18:1-15, BWANA akamtokea Ibrahimu karibu na mialoni ya Mamre, alipokuwa ameketi mlangoni pa hema yake mchana wakati wa hari. Akainua macho yake akaona na tazama watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema akainama mpaka nchi, akasema Bwana wangu kama nimeona fadhili machoni pako nakuomba usinipite sasa mimi mtumwa wako. Na yaletwe basi maji kidogo mkanawe miguu, mkapumzike chini ya mti huu. Nami nitaleta chakula kidogo mkaburudishe moyo baadaye mwendelee iwapo mmemjia mtumwa wenu. Wakasema haya fanya kama ulivyosema. Basi Ibrahimu akaenda hima hemani kwa Sara, akasema imiza vipimo vitatu vya unga safi, uukande ufanye mikate. Ibrahimu akapiga mbio kwenda kundini, akaleta ndama wa ng ombe aliye laini, nzuri akampa mtumishi, naye akahimiza kuiandaa. Akatwaa siagi na maziwa, na ndama aliyoiandaa, akawaandikia mbele yao akasimama karibu nao chini ya mti nao wakala. Wakamwambia yu wapi Sara mkeo? Akasema yumo hemani. Akamwambia hakika nitakurudia wakati huu huu mwakani, na tazama Sara mkeo atapata mwana wa kiume. Sara akasikia mlangoni pa hema iliyokuwa nyuma yake. Basi Ibrahimu na Sara walikuwa wazee na umri wao mkubwa, na Sara alikuwa amekoma katika desturi ya wanawake. Kwa hiyo Sara akacheka moyoni mwake, akisema niwapo mkongwe, nitapata furaha na bwana wangu mzee? BWANA akamwambia Ibrahimu mbona Sara amecheka akisema, mimi kweli nitazaa mwana nami ni mzee? Kuna neno gani lililo gumu la kumshinda BWANA? Kwa muhula wake nitakurudia, wakti huu huu mwakani, na Sara atapata mwana wa kiume. Akakana Sara akisema sikucheka, maana aliogopa naye akasema, sivyo umecheka. Na Itafunika Wingi Wa Dhambi (And Shall Hide A Multitude Of Sins) 7

Haikufanya kazi. Hii yaweza kuwa mfumo uliozoeleka unaotumika leo. Haiwezi kufanya kazi. Kusema uongo ili kuficha dhambia zake ilimshusha chini Rais (Nixon) Kuna njia moja hakika na kweli ya kuficha dhambi zako Yak. 5:19-20, Ndugu zangu ikiwa mtu wa kwenu amepotelewa mbali na kweli, na mtu mwingine akamrejeza; jueni ya kuwa yeye amrejezaye mwenye dhambi hata atoke katika njia ya upotevu, ataokoa roho na mauti, na kufunika wingi wa dhambi. Mwenye dhambi aliyekengeuka lazima aongolewe Lazima asikie. Rum. 10:17-18, Basi imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa neno la Kristo. Lakini nasema je wao hawakusikia? Naam, wamesikia sauti yao imeenea duniani mwote, na maneno yao hata miisho ya ulimwengu. Lazima aamini. Mdo. 16:30-31, Kisha akawaleta nje akasema Bwana zangu yanipasa nifanye nini nipate kuokoka? Wakamwambia mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako. Lazima atubu. Mdo. 17:30, Basi zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hazioni, bali sasa anawaagiza watu wote wa kila mahali watubu. Lazima akiri. Rum. 10:9-10, Kwa sababu ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. Lazima abatizwe. 1 Pet. 3:21, Mfano wa mambo hayo ni ubatizo unaowaokoa pia siku hizi; siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu ladhamiri safi mbele za Mungu. Mkristo anayepotea lazima pia aongolewe Lazima atubu. Mdo. 8:18-22, Hata Simoni alipoona ya kuwa watu wanapewa Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono ya mitume, akataka kuwapa fedha akisema, nipeni na mimi uwezo huu ili kila mtu nitakayemwekea mikono yangu, apokee Roho Mtakatifu. Lakini Petro akamwambia, Fedha yako na ipotelee mbali pamoja na wewe kwa kuwa umedhania ya kuwa karama ya Mungu yapatikana kwa mali. Huna fungu wala huna sehemu katika jambo hili, kwa kuwa moyo wako si mnyofu mbele za Mungu. Basi tubia uovu wako huu ukamwombe Bwana, ili kama yamkini usamehewe fikira hii ya moyo wako. Na Itafunika Wingi Wa Dhambi (And Shall Hide A Multitude Of Sins) 8

Lazima kutubu na kuomba msamaha. Yakobo 5:16, Maana hapo malipo wivu na ugomvi ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya. 1 Yoh. 1:9, Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote. Pasipo kuzikiri dhambi zetu, hakuna ondoleo la dhambi. Kama ndugu akitenda dhambi dhidi ya mwingine, kwanza wanatakiwa kulifanyia kazi wao binafsi. Kama hiyo haiwekani, mashahidi wawili au watatu wanaletwa ili kulisuluisha. Kama isipowezekana, swala hilo upelekwa mbele ya kanisa. Dhambi ya siri hufanywa kuwa ya wazi. Huko Delta, Colorado, mwaka mmoja, swali liliulizwa, Je! Kukiri kunatakiwa kuwe kwa wazi. Kulikuwa na mjadala kuhusu swala hili, na watu wengi wakadhani kwamba hata dhambi ikijulikana kwa kiasi gani, ndivyo kukiri nayo inavyopaswa kuwa. Kama kuna dhambi ya siri kati ya wawili, wawili hao wanapaswa kukiri wao kwa wao. Kama dhambi ni dhidi ya Mungu, Yesu Kristo au kanisa, na kwa ujumla dhambi hiyo ikajulikana, basi dhambi hiyo itakuwa ya hadhara, na kukiri kunatakiwa kufanyike hadharani. Kama hakuna toba pamoja na kukubali kosa, hakuwezi kukawa na msamaha. Ninasoma sehemu ambapo miaka michache iliyopita, mwuaji alishawishika na kuwekwa katika kutubu. Baada ya kukaa miaka kadhaa gerezani, alikuwa anafikia wakati ambapo angeachiwa mapema kwa msamaha. Kaka yake alianza kutafuta ni jinsi gani kuachiwa huru huku kutakavyokuwa. Katika kumtembelea kaka yake gerezani, alimwuliza, Utafanya nini kama ukiachiwa huru kutoka gerezani? Kaka yake akajibu, Jambo la kwanza ni kumpiga hakimu Aliyenihukumu, na kumwua; na jambo la pili ni kumpiga shahidi mkuu, na kumwua. Kaka yake akaamka, na kuondoka kwa sababu ya kauli hiyo. Akawaambia wakuu wa gereza kwamba kaka yake afungwe maisha gerezani bila kuachiwa mapema. Alilipa deni la kutokiri. Siku moja wenye dhambi wa dunia hii watalipa deni kamili ya dhambi zao kama hawakuzitubia dhambi hizo. Hii ndiyo njia pekee ambayo dhambi hufunikwa. Na Itafunika Wingi Wa Dhambi (And Shall Hide A Multitude Of Sins) 9

Hitimisho Je! Unataka kuokolewa? Kwa nini unasubiri? Na Itafunika Wingi Wa Dhambi (And Shall Hide A Multitude Of Sins) 10

Na Itafunika Wingi Wa Dhambi (And Shall Hide A Multitude Of Sins) 11

Na Itafunika Wingi Wa Dhambi (And Shall Hide A Multitude Of Sins) 12