If a tree falls - Deforestation in Africa"

Similar documents
Information for assessors (do not distribute this page to participants):

If a tree falls - The Rocket Stove"

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

Human Rights Are Universal And Yet...

MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA. Kwa Wanaoanza

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Deutsche Welle, Learning by Ear 2009 Seite 1 People Who Make A Difference Liberia: Anita Varney Health Facilitator, Fishtown/Liberia

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

Ufunguo wa Kutaalamika Haraka

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti

MTIHANI WA MWIGO WILAYA YA BUTERE MUMIAS-2007 Hati ya kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level

usudi la Maisha Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na kupishana usiku na mchana, kuna kweli ishara kwa wenye akili, ambaye mkumbuke-

2

LBE 2009 Migration Episode 3: Living without documents

Hatari, Haki za Usalama katika Bahari 03

walozaliwa, si kwa damu, wala mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, mbali kwa Mungu. Sisi sio tena binadamu wa kawaida tu kwa sababu sisi ni w

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA)

WEWE NI NANI? Toleo X Toleo Ukweli wa Injeli Toleo 23

Vijana wanazungumza kuhusu ujinsia, maisha na uhusiano VIJANA WANAZUNGUMZA KUHUSU NGONO, MAISHA NA UHUSIANO. Training and Research Support Centre

United Pentecostal Church April Kushangilia Kwa Sala

United Pentecostal Church June 2017

Theolojia Ujumla. Mike Taylor Semester Munguishi Bible College

Tora UTANGULIZI KWA TORA SOMO LA KWANZA

Kiu Cha umtafuta Mungu

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

April 14, 2016 COUNTY ASSEMBLY DEBATES 52

Ellen White, waasisi wa Kiadventista,na Sabato Lunar

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees

Ushindi ndani ya Kristo W. W. PRESCOTT

MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA PRO-ROUTES. Ombi kwa ajili ya fedha za umma wa mradi wa ziada

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA,KWA WANANCHI, 30 SEPTEMBA, 2001

Mwongozo wa Jamii juu ya Afya ya Mazingira

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC)

Kifo Na Mbingu. (Death And Heaven) Ellis P. Forsman. Kifo Na Mbingu (Death And Heaven) 1

JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI

2

JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

Kuwawezesha wasichana kwa kuboresha kujikubali na kujithamini Hivi Ndivyo Nilivyo

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

Elimukombozi, Lugha na Upashanaji Habari nchini Tanzania, katika Muktadha wa Utandawazi

TIST HABARI MOTO MOTO MAANDALIZI YA MWAKA 2000 Y2K PREPARATIONS SASA NI WAKATI WA KUANZA KUPANDA MBEGU ZAKO

JE, YAWEZEKANA KUISHI BILA KUTENDA DHAMBI?

MACHAGUO YA UZAZI KUFIKIRIA KUWA MZAZI

Miradi na jamii. 3.1 Utangulizi

Uponyaji Wa Laana. (Kumb. 28:1-14).

Utangulizi wa ugonjwa wa shinikizo la damu

Unyanyasaji wa Watoto & Kutelekezwa

Mutugi Kamundi. Jemma Kahn. Kiswahili. Demane na pacha wake. Author - South African Folktale

MUNGU ANADHIHIRISHWA KUPITIA KWA YESU KRISTO.

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC)

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) VERBATIM REPORT OF

Mipango ya miradi katika udugu

Iliyoendelea sana. Kitengo cha 2. Kitabu cha mwanafunzi Iliyoendelea sana

MAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI

SautiElimu. Sauti Yako Isikike

Adhabu ya jino kwa jino na Musitakabali wa imani zetu

TAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF) KUHUSU HAKI ZA WATOTO KATIKA KATIBA MPYA

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig

Mwongozo wa Utamaduni Toleo la Kwanza

Sera ya Faragha. Upeo. Aina za Data na Mbinu za Ukusanyaji

KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA

Usimulizi wa Riwaya ya Nyongo Mkalia Ini E. S. MOHOCHI University of Egerton, Kenya

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC)

N09/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q

International Labour Office. Kazi za Ndani Zenye Madhara kwa Watoto: Kijitabu cha Maelezo Mafupi

Roho Mtakatifu Ni Nini?

Early Grade Reading Assessment for Kenya

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC)

LEARNING BY EAR MGENI KIZABIZABINA MSOALIKWA- VITA VYA FAMILIA MOJA DHIDI YA UGONJWA WA MALARIA

Kufunga Milango - Uponyaji Kutokana na Athari za Giza

JAZANDA YA NJOZI KATIKA BAADHI YA MASHAIRI YA EUPHRASE KEZILAHABI (ONEIRIC IMAGES IN EUPHRASE KEZILAHABI S SELECTED POEMS) 1

Ndugu na dada zangu wapendwa,

Mazoezi yaliyofanyika wakati wa warsha kuhusu Elimu-Jumuishi kwa Vitendo. Zanzibar, 7-10 Februari 2006

Pronunciation: Mä-hret Zäläke Ndal-ka-tscho Molla Mare Gebre-gzabiär 1/12

"ATATOKEA MARA YA PILI, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu." Waebrania 9:28.

PDF created with pdffactory trial version

MSAMAHA NA UPATANISHO

Shabaha ya Mazungumzo haya

Kufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007

Kuiponya Picha Tuliyonayo Kuhusu Mungu

ORODHA YA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI SPIKA MHE. PANDU AMEIR KIFICHO. Rais.

Kifo Na Mbingu (Death And Heaven)

Kutetea Haki za Binadamu

# 18 Uponyaji Kutokana na Kukataliwa

2 LILE NENO LILILONENWA

MWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI

Kitabu Cha Mafunzo Ya Uongozi Kwa Wanawake

Ni kwa nini mkulima awe maskini?

Ufundishaji wa lugha nyingine

UMRI WA MAKAMO NA KUKOMA KWA HEDHI

UFAHAMU NAME INDEX SCHOOLDATE UFAHAMU

KAMA MUNGU YU PAMOJA NASI, BASI YAKO WAPI MATENDO YAKE YA AJABU?

Wewe Maisha Yako Ndoto Zako. Kitabu cha Vijana Balehe

Kifaa Maalum cha Kutazamia Jua: Maelekezo ya kutumia

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

Kijitabu cha Maelezo cha Programu ya Famasia

Transcription:

LEARNING BY EAR If a tree falls - Deforestation in Africa" EPISODE EIGHT: "FARM is born" AUTHOR: Romie Singh EDITORS: Thomas Mösch, Jan-Philipp Scholz PROOFREADING: Natalie Glanville-Wallis List of characters EPISODE EIGHT: Narrator SCENE 1 Isi (m, 18) SCENE 2 Isi (m, 18) Mother (f, 36) SCENE 3 Talib (m, 20) Chika (f, 18) SCENE 4 Akiki (f, 7) Chief (m, 36) Sesi (f, 18) SCENE 5 Chika (f, 18) "Themba" (f, 30) Talib (m, 20) Chief (m, 40) Mulogo (m, 20) Mother (f, 36) Group of Men/Women SCENE 6 Akiki (f, 7) Isi (m, 18) Sesi (f, 18) 1

INTRO Karibu kwenye Noa Bongo Jenga Maisha Yako na katika kipindi cha nane cha mchezo wetu mpya kuhusu uharibifu wa misitu. Kisa hiki kinaendelea kwenye mazingira ya vita vya wenyewe kwa wenyewe na kinaonyesha jinsi uharibifu wa misitu- ukataji wa miti na maeneo ya nyasi- ulivyotatiza maisha ya vijijini na kusababisha mzozo kati ya jamii mbili za wakulima. Sasa jamii hizo mbili zinajipata pamoja kwenye kambi ya wakimbizi ya Dovani na zimeanza kutafuta ufumbuzi sawa kwa matatizo ya siku za usoni. Katika kipindi cha leo, jamii mbili zilizo na mzozo zinatafuta njia za kulima kwa kuzingatia hali ya mazingira na pia kupika kwa kutumia kuni chache. Wakati huo huo Isi anaogopa kwamba huenda hali yake yeye kuzaliwa pacha imesababisha laana katika famila yake. Episode EIGHT: FARM is Born. 2

1.MUSIC UP Scene 1 2.ISI NARRATOR: Wiki hii imekuwa na vituko vyake. Ilianza na taharuki pale Akiki alipokimbia kutoka kambini. Nilikisia kuwa ni kwa sababu ya ndoto aliyoota kwamba dadake alikuwa amejificha kwenye mti kijiji kwao. Lakini alivyojua mti wa kwenda kutafuta mpaka sasa ni kitendawili. Yeye na Sesi walirudi salama katika kambi ya Dovani. Lakini Sesi angali katika mshtuko. Nimejaribu kumuimbia lakini wapi! Hawezi kuzungumza au tuseme anakataa kuzungumzia-sijui ni vipi. Hajanizungumzia. Ninaogopa asijekuwa na taarifa zisizopendeza. 3.MUSIC UP 3

Scene 2 4. SFX Morning ambience. In the kitchen. Sound of stove, fire crackling 5.ISI: Ma? Unafikiri mambo mabaya hutokea kutokana na walivyofanya mababu zetu? Au wazazi wetu? 6.MOTHER: Unazungumzia nini? Hatujafanya jambo lolote baya sisi. 7.ISI: Ninafikiria tu Ma, wala usinikasirikie, mimi na Kato ni mapacha. Nyumbani kwetu watu walisema kwamba mapacha wana nguvu za ziada, kwamba tunaweza kuleta bahati au mkosi kulingana na nyota za wazazi wetu. Sijapata kuelewa hayo. 8.MOTHER: Mapacha wanapendeza, Isingoma. Wewe na Katu si nuksi. Mmetuletea raha maishani mwetu. 9.ISI: Lakini, labda tunaadhibiwa. Pengine ni lazima Kato ateseke kwa kuwa baba yetu alisababisha mzozo miongoni mwa watu wetu. Aliwapatia wauza mbao msitu wetu. Waliiangamiza miti yetu kwa hivyo sisi lazima tulipe. 4

10.MOTHER: Babako alikuwa akijaribu kuwatajirisha watu wetu alipoafikia huo uamuzi. Hakutaka kujitajirisha binafsi. Lakini alihadaiwa na kampuni ya BigWood. Hana uzoefu wa mas-ala ya mikataba na makubaliano. 11.ISI: Alikosea tu? 12.MOTHER: Naam. Babako ni binadamu. Mababu zetu hawatuadhibu. Tunajiadhibu sisi wenyewe! Kweli Isi. Nakwambia kweli, umasikini na vita ndivyo vinavyotutatiza; si wewe, si Kato wala si babako. 13.MUSIC UP 5

Scene 3 14. SFX: Office sounds / Machine noise of fax. 15.TALIB: Aaah! Hii pepesi (fax) imeingia Chika. Kutoka makao makuu ya Saidia Afrika. 16.CHIKA: Ehe! Inasema nini? 17.TALIB: (trying to understand the print) Um unaweza kuisoma? Macho yako yanaangaza zaidi ya yangu! 18.CHIKA: Balaa hii. Si macho yako Talib! Mtambo wetu wa kuchapishia ndo umekwisha wino! Lakini..eem...Acha nitizame. Ukurasa wa mwanzo unaonyesha kwamba ni hati ya mafunzo ya nyanjani. 19.CHIKA: (Reading slowly) Lengo: Kuanzisha usimamizi wa misitu unaoongozwa na jamii. 20.TALIB: Naam, nimekuwa nikisubiri ujumbe huu! Tunahitaji taarifa hizi kuwafunza watu ambao wamekuwa wakipigania haki za malisho pamoja na misitu. 6

21.CHIKA: 22.TALIB: Kama hao wanaoishi katika kambi hii wanaotoka wilaya za Banega na Abanto! Ndo hivyo. Usimamizi wa misitu utakaohusisha jamii. Hatua hiyo inahakikisha kwamba kila upande unahusishwa vilivyo, hasa wanawake, watwae umilisi wa rasilimali zao na kutafuta mbinu mwafaka za kuzisimamia,- maanake misitu, mimea na maji. Ni jambo la mashinani. Endelea! Inasema nini? 23.CHIKA: (Reading slowly and clearly) Sehemu ya Kwanza: Jinsi ya kubuni shirika pana la kijamii linalohusisha watu wengi kusimamia misitu; Sehemu ya Pili: Jinsi ya kuwatambua watumizi wote wa misitu na vipi wanavyotumia hiyo misitu. Sehemu ya Tatu: Jinsi ya kuandaa ramani za misitu, kutathmini rasilimali; Sehemu ya Nne: Jinsi ya kujadiliana mikataba na utekelezaji wa mipango muhimu. 24.SFX FAX MACHINE STOPS 25.TALIB: 26.CHIKA: Looo. Kurasa kumi na tano! Kuna mambo mengi sana hapo ya mtu kuelewa, Chika! Lakini kabla hatujawafahamisha wengine, tunahitajika kwanza kusoma. Loo! Nina furaha si haba,talib! Njoo! Tuanze! 27.MUSIC UP 7

Scene 4 27a. SFX Daytime ambience inside 28.AKIKI: Sesi? Umeamka? 29.SESI: (breathes more heavily in response) 30.AKIKI: Chifu Apaloo amekuja kukutembelea kukujulia hali. 31.SESI: (breathes louder) 32.CHIEF APALOO: (gently)hujambo mjukuu wangu. Mama Kipko ameniomba nije kwa kuwa mimi nawe ni wa jamii moja. Anadhani huenda hilo litasaidia. Sijaja kufanya lolote jingine! Nataka kuongea nawe tu. Na wewe Akiki pia! Lala kando ya Sesi. Ningependa kuwaambia jambo la kuvutia kuhusu msitu wa Abanto. Ebu fikirieni hiyo miti. Mikubwa na mirefu. Kwa juu matawi na majani yake utadhani ni paa la nyumba. Kila kitu kimewekwa sawa. Katika hali yake ya kiasili. 33.SESI GIVES A BIG SIGH 8

34.AKIKI: (softly) Sawa Sesi! Tulia! 35.CHIEF APALOO: Huo mti ambao Akiki alikupata ndani, ungalipo kwa sababu hata mimi kuna wakati nilijificha ndani! Kama ulivyofanya! 36.SESI (gives an approving grunt) Hmmm 37.CHIEF APALOO: Nilikuwa nikilala kwenye mti kama kawaida yangu wakati wauza mbao walipofika mahali hapo. Nikawasikia wakiulizana ni nani angepanda juu na kuukata mti huo. 38.AKIKI: Walikuwa wakitaka kuukata mti huo mkubwa hivyo kwa mikono? 39.CHIEF: Naam! Wajinga hao. Tena bila ya idhini. Walikuwa na mnunuzi mjini aliyetaka mti huo akautengezee ngoma. Lakini na mimi pia nilikuwa na ngoma yangu ndogo ambayo niliibeba kila wakati. 40.SFX AFRICAN DRUMMING 9

41.CHIEF APALOO: Nilianza kupiga ngoma na kutoa sauti za ajabu ajabu kama vile pepo. Wooooooooo. 42.AKIKI: (laughing) Hiyo haishtuwi hata kidogo! 43.CHIEF APALOO: Inashtua, hasa ukiwa katika msitu wenye giza! Nadhani walifikira kwamba ni pepo aliyekuwa ndani ya mti. Sijapata kuona watu waoga jinsi hiyo. Walitimua mbio za ajabu! 44.SESI: Happy whimpering sound 45.CHIEF APALOO: Aaha! Sesi! Nakuona unatabasamu! Unaipenda taswira hiyo pia! Kuna hadithi nyingi zaidi kama hiyo. Ninaondoka! Lakini waonaje nikija kukutembelea tena? 466.AKIKI: (softly) Kwa hisani yako Chifu, tutembelee tena! 47.MUSIC UP 10

Scene 5 48. SFX Day time ambience outside 49.FADE IN MEN AND WOMEN S VOICES 50.CHIKA: Kwa hivyo hili ni wazo pana. Kama nilivyosema, hili si tena kundi la wanawake tu. Ni shirika la kijamii lililo na wanachama waliochaguliwa kuendesha kamati kadha wa kadha ambazo mtahitajika kubuni. Kusimamia msitu si jambo dogo ati. Naam Themba? 51.THEMBA: Unataka tusajili shirika la kijamii na tulifanye kuwa rasmi? Na liwe na jina zuri, sawa? 52.TALIB: Wazo zuri hilo! Na? Fikira zozote? 53.THEMBA: (saying each letter) F A R M. Maanake Farm kwa maana ya Forest and Rural Management. 54.CHIKA: Themba! Jina zuri hiyo! Kunaye anapinga? 55.MEN/WOMEN APPROVE: Nalipenda sana! Wazo zuri! Hongera Themba! 11

56.CHIKA: FARM! Barabara! Tutakapokuwa tayari tutajiandikisha kwa jina FARM na hapo tutaweza kujadiliana kuhusu Mkataba wa Usimamizi wa Misitu. Mkataba huu ni muhimu. Unatufanya sisi kuwa washirika wenza kisheria na makundi mengi yanayomiliki misitu hata na serikali! Sote tutashiriki kwenye utaratibu wa kidemokrasia wa kuamua jinsi ya kutumia rasilimali za misitu bila kuharibu mazingira. 57.EXCITED VOICES 58.TALIB: Nadhani kwanza, tuangazie washikadau hao- watu wanaotumia misitu au bidhaa zinazotoka msituni. 59. VOICES OF APPROVAL 60.CHIKA: Hili ni jedwali lenu mjaze. Katika kisanduku cha upande wa kulia, tafadhalini jazeni majina ya makundi hayo kutegemea ukubwa wayo. Kwa hivyo "Mshikadau wa kwanza litakuwa kundi kubwa linalotumia msitu kila mara. 61.CHIEF APALOO: Tuseme ni wanaoishi wakidunduliza bidhaa za msituni- wanaokwenda kutafuta kuni. 12

62.MULOGO: Wanaotegemea asali kutoka mwituni. 63.CHIKA: Na pia waganga wa miti shamba. 64.TALIB: 65.MOTHER: 66.TALIB: Barabara! Jazeni shughuli zao kwenye kisanduku kinachofuata. Na kisha, kwenye kisanduku cha kulia tuorodheshe bidhaa tunazopata, siyo? Naam. Kwa hivyo kwa kipato cha mshikau wa kwanza tuna kuni, asali, dawa na uuzaji wa miti shamba. 67.CHIEF APALOO: Na kisha mshikadau wa pili ni kundi kubwa la pili linalofaidika na rasilimali ya misitu. 68.MOTHER: Wachungaji, nadhani walio na mifugo. 69.MULOGO: 70.CHIKA: Na mshikadau wa tatu pengine ni wapasuaji mbao- wakati miti. Sawa. Naam! Tafadhali mshirikiane kwenye makundi na mkubaliane mnachojaza. Tutakutana baada ya nusu saa ili tubadilishane mawazo. 71.MUSIC UP 13

Scene 6 72. SFX Night time ambience outside 73.AKIKI: Mwambie kitendawili hicho, Isi. Ni kizuri sana. 74.ISI: Mwambiye wewe mwenyewe Akiki! 75.AKIKI: Sawa. Sikiza Sesi! Mti unapoanguka msituni, na hakuna mtu karibu wa kusikia, je mti huo hutoa sauti yoyote? 76.ISI: (gently) Unafikiri nini jawabu yake, Sesi? 77.SESI MAKES A HAPPIER SOUNDING NOISE 78.AKIKI: (happy) Oh Isi, Ameshaaanza! Amerejewa na sauti yake! Atakuwa na uwezo wa kuzungumza hivi karibuni. 79.ISI: (worried) Lakini atasema nini pindi akipata sauti! 80. MUSIC UP 14

OUTRO. Ni hayo tuliyokuandalia kwa leo katika kipindi cha Noa Bongo Jenga Maisha Yako kiitwacho Mti unapoanguka..., kilichoandikwa na Romie Singh, kinachoshughulikia suala la uharibifu wa misitu. Jamii zinaunda shirika la usimamizi wa misitu, lakini Isingoma atapata amani? Usikose kujiunga nasi katika kipindi cha tisa upate kujua mambo yatakavyokuwa. Kumbuka, ukitaka kusikiliza tena kipindi hiki au kuwaarifu marafiki zako tafadhali tembelea wavuti www.dw-world.de/lbe Kwaheri kwa sasa! END OF EPISODE 8 15