KAWAWA JKT HIGH SCHOOL PO.BOX 213 MAFINGA IRINGA PHONE MOBILE,0762-785899, 0765 752082, 0758 767533, EMAIL: kawawa.highschool@yahoo.com Kumb Na. 841KJ/KAWSS/2540 6 Namba ya Fomu. Tarehe.. FOMU YA USAJILI WA MWANAFUNZI A. MAELEZO YA MTOTO 1. Jina kamili la mtoto 2. Tarehe ya kuzaliwa 3. Wilaya aliyozaliwa Mkoa wa 4. Raia wa 5. Jinsia ya 6. Shule ya msingi alikomaliza masomo Wilaya ya Mkoa wa 7. Mwaka aliomaliza masomo ya msingi 8. Dini B. MAELEZO YA MZAZI /MLEZI 1. Jina la Mzazi/Mlezi 2. Uraia wako 3. Anwani ya Mzazi/Mlezi 4. Kazi yako 5. Unakofanyia kazi 6. Namba ya simu ya nyumbani 7. Namba ya simu ya kazini 8. Uhusiano na Mtoto C. MAELEZO MUHIMU 1. Masomo yatakayotahiniwa ni kingereza, Hesabu na Maarifa 2. Gharama ya fomu hii ni Tshs 10,000/= (Elfu kumi tu) ambazo hazitarudishwa 3. Majibu ya watahiniwa waliochaguliwa yatapatikana kwenye kituo ulichochukulia fomu mara baada ya shule kufanya uchaguzi 4. Bandika picha ndogo ya mwanafunzi juu (passport size) Tarehe ya kufanya mtihani ni tarehe 27/10/18 D. VITUO VYA KUUZIA FOMU ZA KUFANYIA MTIHANI 1. Kawawa High school - Mafinga 2. Jitegemee High School - Dar es salaam 3. Wilolesi shule ya Msingi - Iringa Mjini 4. Azimio la shule ya Msingi - Makambako 5. Usangila - Mafinga sokoni (EE Sikaponda psc) Maj Mkuu wa Shule
WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA Simu 0655 540230 Kawawa (JKT) High School 0767 785899 Sanduku la Posta 213 Fax 0262 277 144 MAFINGA Tarehe Ndugu MAELEZO YA KUJIUNGA NA SHULE Nafurahi kukukaribisha kujiunga kidato cha kwanza katika shule ya Sekondari Kawawa (JKT) High school. Shule itafunguliwa rasmi tarehe 07 January 2019, mwisho wa kuripoti ni tarehe 14 Januari 2019. 1. UTANGULIZI a. Kawawa (JKT) High school ipo Mkoa wa Iringa Wilaya ya Mufindi katika Mji wa Mafinga. Shule imejengwa katika eneo la kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa Mafinga kilometa (6) toka Mjini Mafinga. b. Mji wa Mafinga upo katikati ya Makambako na Iringa Mjini na km 85 toka Makambako. c. Teremka kituo cha mabasi Mafinga Mjini ambapo ndio kituo kikuu. Kituoni hapo zipo taxi za kukodi. Ambapo karibu wote wanafahamu shule ilipo watakuleta bila wasiwasi wowote gharama za usafiri wa Taxi ni kati ya Tshs 8,000/= na Tshs 9,000/= kutegemea na bei ya mafuta ya magari. 2. USAFIRI KWA WATOKAO NJE YA MKOA a. Watokao Dar es salaam au Morogoro, watumie mabasi yaendayo Mbeya Njombe au Songea kama GALAXY, NYAGAWA, UPENDO SUPER FEO, HAPPY AFRICA, LUWINZO, ABOOD, NEW FORCE. b. Watokao Dodoma watumie mabasi ya ABOOD, ANAOTHER G, KIMBINYIKO, SHABIBY LINE, 3. HALI YA HEWA a. Hali ya hewa Mafinga ipo hivi :- i. Mwezi wa January March ni kipindi cha mvua za masika ambapo wanafunzi hulazimika kuwa na koti la mvua au mwamvuli. ii. Mwezi Aprili August au September ni kipindi cha baridi iii. Mwezi Septemba Octoba au Disemba ni kipindi cha joto na mvua za vuli ambazo huanza mwezi Octoba na Novemba. b. Kwa wanafunzi wenye matatizo ya kifua (Pumu) mahali hapa hapafai kwa yeye kusoma.
c. Kutokana na hali ya hewa ya Mafinga ugonjwa wa malaria upo kwa kiasi kidogo na mara nyingi wale wanaotoka sehemu za joto huja nao. Dawa za magonjwa ya kawaida hutolewa shuleni na Daktari au Nesi wa shule kwa wale wanaohitaji vipimo hupimwa katika hospitali kubwa ya Jeshi ambayo pia ina wodi ya kulaza wagonjwa. 4. MALIPO YA ADA Malipo ya ada kwa mwaka yatakuwa kama ifuatavyo:- a. Kwa mwanafunzi wa Bweni ni Tshs 1,500,000/= (milioni moja laki tano tu kwa mwaka ) Mzazi/Mlezi anaweza kulipa zote kwa mara moja au kwa awamu mbili kama ifuatavyo:- i. Muhula wa kwanza Tshs 800,000/= ii. Muhula wa pili Tshs 700,000/= b. Kwa mwanafunzi wa kutwa ni Tshs 700,000/= (Laki saba) Mzazi/Mlezi anaweza kulipa zote kwa mara moja au kwa awamu mbili kama ifuatavyo:- i. Muhula wa kwanza Tshs 350,000/= ii. Muhula wa pili Tshs 350,000/= NB: Malipo ya ada yalipwe Bank zifuatazo:- NMB 60203500075 AU CRDB 0150350159601 ( Kawawa Sec School) Baada ya kulipia BANK hakikisha UNALETA PAY IN SLIP YA BANK HUSIKA Shuleni ndani ya mwezi huo huo. Pia inasisitizwa mwanafunzi yeyote hatapokelewa shuleni bila kuwa na ada kamili iliyoainishwa hapo juu. 5. GHARAMA ZINGINE a. Gharama za Mitihani na majaribio mbalimbali kwa mwaka Tshs 40,000/= i. Muhula wa kwanza Tshs 20,000/= ii. Muhula wa pili Tshs 20,000/= b. Gharama za Matibabu Tshs 20,000/= kwa mwaka c. Gharama ya Kitambulisho Tshs 5,000/= d. Fedha za tahadhari (Caution money) Tshs 50,000/= endapo haitatumika kufidia uharibifu mwanafunzi atarejeshewa fedha hizo. a. Michango hii iwekwe kwenye akaunti ya benki ya NMB NO 60210021453 KAWAWA REMEDIAL ACCOUNT. b. Kumbuka kutochanganya akaunti inayotumika kulipa Ada, Michango mingine, usichanganye.
6. SARE ZA SHULE (a) Ili mwanafunzi awe nadhifu na mwenye kupendeza, sare zao zitashonwa shuleni kwa gharama ya Tshs 110,000/= ambazo fedha hizo mwanafunzi atakuja nazo wakati wa kusajiliwa, sare hizo ni (included). i. Wasichana: Sketi 2, Mashati 2, ya mikono mirefu, Tai, (njano) Sweta, Tshirt na Nembo ya shule ii. Wavulana: suruali 2, Mashati 2 ya mikono mirefu Tai, ( kijani) Sweta, Tshirt na nembo ya Shule. (b) Gauni na Track suit (Shamba dress) Tshs 60,000/= kwa Bweni tu, fedha ambazo mwanafunzi atakuja nazo wakati wa kusajiliwa. ( pesa hizo ziletwe taslimu shuleni) Wanafunzi hawaruhusiwi kuja na nguo za nyumbani ambazo si za heshima. Hatakiwi kabisa mfano suruali za mtepeto, vizibau (carwash) sketi fupi, nguo zinazoonyesha maumbile, blauzi fupi zinazoonyesha tumbo au vitovu nje. NB Nguo zitakazokamatwa ambazo zimekatazwa zitachomwa moto hadharani na shule haitawajibika kulipa chochote. 7. TAALUMA a. Wastani utakaomruhusu mwanafunzi kuingia kidato kingine ni 41% mwanafunzi ambaye hatafikisha kiwango hicho hataruhusiwa kuingia kidato kingine kinachofuata, atalazimika kurudia darasa. b. Masomo yanayofundishwa shuleni ni :- CIVICS, KISWAHILI, BASIC MATHEMATICS, ENGLISH LANGUAGE, FRENCH, PHYSICS, BIOLOGY, HISTORY, GEOGRAPHY, CHEMISTRY, KOMPYUTA, NA LITERATURE IN ENGLISH (c) VIFAA VYA DARASANI KWA WOTE 1. Madaftari makubwa saba (07) (counter book) 2. Madaftari madogo kumi (10) 3. Kamusi ya kingereza 4. Picha ndogo nne passport size 5. Kalamu ya wino, penseli na rula (d) Inashauriwa kila mwanafunzi awe na vitabu vyake binafsi aweze kujisomea muda wote. Ili kufikia lengo hili shule imeruhusu mawakala wa
vitabu kufungua duka la vitabu na kuviuza kwa bei ya punguzo kati ya 12,500/= hadi 30,000/=. (e) Mwanafunzi anatakiwa kuwa na sanduku la la Posta kwa ajili ya kutumiwa maendeleo ya kitaaluma ya mtoto wake. 8. KWA MWANAFUNZI WA BWENI ANALAZIMIKA KUJA SHULENI NA VIFAA KWA MATUMIZI AMBAVYO NI:- i. Godoro la sponchi upana wa futi 2 ½ kwa urefu wa futi sita ii. Blanketi mbili iii. Mashuka mawili rangi ya pinki iv. Chandarua v. Koti la mvua au mwavuli vi. Sanduku la bati na kufuli lake Masanduku ya aina nyingine hayafai kwa mazingira ya shule (kufuli solex) vii. Ndoo ya maji viii. Vyombo vya chakula sahani, Bakuli, kijiko, na kikombe. Hivi hupatikana pia katika duka la shule. ix. Nguo za michezo raba. Bukta, fulana, sock, au track suit n.k x. Fedha za matumizi na nauli ya kurudia nyumbani wakati shule inapofungwa zitawasilishwa kwa mhasibu wa shule na hazitatolewa kwa mwanafunzi kwa shida yoyote. Fedha hizi hukusanywa mapema ili kupata fursa ya kukodi mabasi kuwarudisha wanafunzi majumbani wakati wa likizo shule itakapofungwa. Maelezo kuhusu viwango vya nauli atapata toka kwa mhasibu. Kwa vile hubadilika kutokana na bei za mafuta au leseni za magari kupanda. 9. UPIMAJI WA AFYA Kila mzazi atalazimika kupima afya ya mtoto wake ili kujua kama ataweza kusoma katika mazingira ambayo ni ya baridi. Imeambatanishwa fomu ya kupeleka kwa daktari ambayo inatakiwa kujazwa baada ya mtoto kupimwa. Inashauriwa kwa watoto wa kike wapimwe kwa uangalifu mkubwa ili kuwa na uhakika na afya zao. NB (i) Gharama za upimaji ni za mzazi mwenyewe (ii) Inashauriwa kupima katika hospitali ya Wilaya, Mikoa au hospitali binafsi zinazotambulika. 10. MUDA WA KUPOKEA WANAFUNZI Muda wa kupokea wanafunzi ni kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 11:00 jioni. Mwanafunzi au mzazi atakayefika zaidi ya muda huo atalazimika kulala mafinga mjini na kuripoti shuleni siku inayofuata ndani ya masaa yaliyoelekezwa hapo juu.
11. TABIA YA MTOTO Kwa mtoto yeyote mwenye matatizo ya nidhamu kwao, ingefaa mazazi aeleze kiundani ili matatizo yaeleweke kwa nia ya kumsaidia mtoto katika kumrekebisha. 12. KUTOKUWA NA SIMU Kutokana na maagizo ya Wizara ya Elimu mwanafunzi haruhusiwi kuwa na simu katika kipindi chote awapo shuleni, Akibainika kuwa nayo atanyang`anywa na kupewa adhabu kali. 13. NIDHAMU Maendeleo na matunda mazuri ya mtu yeyote yatapatikana baada ya nidhamu kupewa kipaumbele, nidhamu ikiwepo pamoja na jitihada. Mafanikio ni dhahiri yatapatikana. Wanafunzi wote wanapaswa kuishi maisha ya nidhamu siku zote ili waweze kufanikiwa vema katika masomo na maisha yao. Wizara ya Elimu imeainisha badhi ya makosa ambayo mwanafunzi akiyatenda anaweza kufukuzwa shule, kushitakiwa mahakamani au adhabu zote kwa pamoja kwa maana hiyo mwanafunzi anapaswa kuwa mwangalifu ili asipatikane na hatia katika makosa yafuayayo. i. Wizi ii. Uasherati, ubakaji na ushoga iii. Ulevi na matumizi ya madawa ya kulevya iv. Uvutaji wa bangi au sigara v. Makosa ya jinai vi. Kupigana au kupiga vii. Kuharibu kwa makusudi mali ya umma viii. Kudharau Bendera ya Taifa ix. Kupata mimba au kusababisha mimba x. Kuoa au kuolewa xi. Kukataa adhabu kwa makusudi xii. Kutoa mimba xiii. Kwenda nje ya eneo la shule bila ruhusa xiv. Utoro na uzembe wa kutofuata ratiba ya shule xv. Kuchelewa kufika shule wakati wa kufungua shule xvi. Kwenda kinyume na sheria za shule (EE Sikaponda psc) Maj Nkuu wa Shule
SHULE YA SEKONDARI KAWAWA (JKT) Sanduku la Posta 213, MAFINGA Simu: 0762785899 0713 821742 Fax: 026 277 2144 Daktari, Hospitali ya. Sanduku la Posta.. FOMU YA UPIMAJI WA AFYA YA MWANAFUNZI Tafadhali husika na kichwa cha habari hapo juu Unaombwa kupima afya ya mwanafunzi aitwaye wa kidato cha..mwaka.. ili kufahamu afya yake na kama anaweza kusoma katika mazingira yetu ya baridi. Wako katika Elimu. (EE Sikaponda, psc) Maj Mkuu wa shule IJAZWE NA DAKTARI Mimi Dr.... wa Hospitali ya..... iliyopo.nimempima mwanafunzi hapo juu na kugundua anayo/hana matatizo ya afya. Maoni na mapendekezo ya Daktari.. Sahihi na muhuri