KUHUSU AFRODAD. Dira ya AFRODAD. Dhamira ya AFRODAD. AFRODAD inalenga mchakato sawa na endelevu wa maendeleo kuelekea Afrika yenye mafanikio.

Similar documents
Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA PRO-ROUTES. Ombi kwa ajili ya fedha za umma wa mradi wa ziada

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2017/18

Azimio lililopitishwa na Mkutano Mkuu tarehe 18 Desemba 2013 [juu ya taarifa ya Kamati ya Tatu (A/68/456/Add.2)]

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

Miradi na jamii. 3.1 Utangulizi

Kuuelewa Mchakato wa Bajeti Tanzania Mwongozo wa Asasi za Kiraia

Songa kwenye kilele cha upeo. Masuala ya Msingi na Ujuzi juu ya Uendeshaji wa Serikali za Mitaa

Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

JAMHURI YA KENYA. Mkakati wa Ushirikiano MUKHTASARI FY Public Disclosure Authorized. Public Disclosure Authorized

MAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI

UFUATILIAJI WA MIRADI NA TATHMINI

MAADHIMISHO YA MIAKA 15 YA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali ya Madini Ukanda

Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA 2006/07

Dibaji ya Mwenyekiti wa Kamati ya Pamoja ya Uongozi

TAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF) KUHUSU HAKI ZA WATOTO KATIKA KATIBA MPYA

Kutetea Haki za Binadamu

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti

NGUZO KUMI ZA KILIMO KWANZA

Information for assessors (do not distribute this page to participants):

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

RIPOTI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU

TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM)

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU

RIPOTI YA WARSHA KUHUSU HABARI KWA AJILI YA UWAJIBIKAJI

TANZANIA TAARIFA YA MWISHO WA UTEKELEZAJI

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA MHESHIMIWA DKT

TANZANIA MARKETS PAN Sera zinazoboresha masoko

Programu ya Uendelezaji Mifumo ya Maji Vijijini (PUMMV) katika Tanzania. Modeli wa Ukodishaji Mradi

In the matter of an Application by the KIGOMA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (KUWASA) For a Tariff and Charges Adjustment

HAKI NA TARATIBU ZA AJIRA, KAZI NA HIFADHI YA JAMII

ORDER NO BACKGROUND

Kufanya Uwekezaji kuwa wa Manufaa kwa Afrika: Jibu la Mbunge kuhusu Unyakuzi wa Ardhi

Kubadili Sheria Za Mbegu Na Ulinzi Wa Aina Za Mbegu Na Mimea Nchini Tanzania

Mwongozo wa Kutathimini mifumo ya Ugawanaji wa faida na Mapato Katika Miradi ya Jamii ya MKUHUMI

KIMAZINGIRA NA KIJAMII NA MPANGO WA UDHIBITI

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )

MAPENDEKEZO YA MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA TANZANIA

UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU VIKWAZO VYA KULINDA MAISHA KATIKA USAIDIZI WA KIMATAIFA WA AFYA KWA MSAADA WA KIMATAIFA UNAOFADHILIWA NA MAREKANI

Govt increases vetting threshold of contracts

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

Mwongozo wa Utekelezaji wa Njia za S5-UUE (KAIZEN)-UUU Tanzania

TAARIFA YA MWAKA YA UTENDAJI KAZI IDARA YA UTAWALA BORA 2013/2014

Afya Bora, Utu na Kinga. Ripoti ya Mashauriano ya Kiufundi Aprili 2009, Hammamet, Tunisia

Sera ya Faragha. Upeo. Aina za Data na Mbinu za Ukusanyaji

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

USIMAMIZI MKUU WA UBORA WA MAHURUJI

Deputy Minister for Finance

Dodoma ambako kikao cha Bunge kinaendelea kuja kushiriki japo sehemu ya uzinduzi wa mkutano.

MWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI

KAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI TANZANIA

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, MHESHIMIWA DKT. PHILIP I. MPANGO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig

In the matter of Application by the TANGA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (TANGA UWASA) For a Multi-Year Tariff Adjustment

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA FEDHA

Afya Bora, Utu na Kinga. Ripoti ya Mashauriano ya Kiufundi Aprili 2009, Hammamet, Tunisia

HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE

AZAKI PIGA KURA UCHAGUZI MKUU TANZANIA OKTOBA. #TanzaniaTuitakayo OKTOBA 2015 ILANI YA UCHAGUZI YA AZAKI TANZANIA.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA. Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo. TOLEO Na.

ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA UCHUMI WA ZANZIBAR

Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara)

3. Mheshimiwa Spika, 4. Mheshimiwa Spika,

Mipango ya miradi katika udugu

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA

HISTORIA, MAENDELEO NA MABADILIKO YA KATIBA TANZANIA TANGU UHURU HADI MIAKA HAMSINI YA UHURU 9 DESEMBA 2011.

JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1

Waandishi: wa Toleo la 5. Scholastica Jullu Athanasia A. Soka Safina Hassan Mary Njau. Toleo la 5: 2008 ISBN

UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA)

Unyanyasaji wa Watoto & Kutelekezwa

Kimesanifiwa na:- E.D.Kissuu ECOMM TANZANIA S.L.P ,Dar es Salaam. Simu:

Taarifa Kuhusu Hali ya Uchumi wa Tanzania

Uzio wa pilipili unazuia tembo kuvamia mazao shambani! Jinsi ya kujenga na kudumisha uzio wa pilipili Tanzania

KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA

Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame M. Mbarawa (Mb.); Waheshimiwa Mawaziri na Wabunge wote mliohudhuria;

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II

Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2013

Kitabu Cha Mafunzo Ya Uongozi Kwa Wanawake

KUSHUKA KWA HADHI YA LUGHA ZA JAMII NCHINI TANZANIA YOHANA P. MSANJILA University of Dar es Salaam, Tanzania

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA,KWA WANANCHI, 30 SEPTEMBA, 2001

Kilimo cha kiekolojia cha Wakulima Wadogo Hufanikisha Haki za Mazingira

KITEGO CHA MAREKEBISHO NA HAKI ZA MTOTO

Na Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake Toleola4

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

International Labour Office. Kazi za Ndani Zenye Madhara kwa Watoto: Kijitabu cha Maelezo Mafupi

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO

ONDOA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA AFYA YA WATOTO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Kuwafikia waliotengwa

KIJARIDA JUU YA HAKI ZA RAIA KATIKA MFUMO JINAI

The Government is committed to improve marine transport and has a number

Summaries of GC Reports 2012, Vol. 2, Sec. 1, Swahili

Mwongozo wa Mwezeshaji

Transcription:

KUHUSU AFRODAD Dira ya AFRODAD AFRODAD inalenga mchakato sawa na endelevu wa maendeleo kuelekea Afrika yenye mafanikio. Dhamira ya AFRODAD Kupata sera zitakazorekebisha migogoro ya madeni ya Afrika kulingana na thamani ya mfumo wa haki za binadamu. Malengo ya AFRODAD ni pamoja na yafuatayo: 1. Kuongeza ufanisi na usimamizi wenye tija na matumizi ya rasilimali ya serikali za Afrika; 2. Kupata/kuleta mabadiliko katika dhana ya kimataifa ya kijamii na kiuchumi na mpangilio wa kidunia wa kisiasa kwenye mchakato wa maendeleo unaotambulisha mahitaji na matakwa ya watu wengi duniani; 3. Kuwezesha mazungumzo kati ya vyama vya kiraia na serikali kwenye masuala yanayohusiana na Madeni na maendeleo Afrika au sehemu nyingine.

MKATABA WA KUKOPA Kanuni na Miongozo ya Ukopaji huru wa fedha kwa nchi za Afrika Toleo Lililorekebishwa Hatimiliki 2013 AFRODAD Haki zote zimehifadhiwa ISBN 978-0-7974-4509-3 EAN 9780797445093

YALIYOMO DIBAJI 6 1. UZINGATIAJI WA BUSARA NA DESTURI ZA UKOPAJI NA USIMIMIAJI WA MADENI YA UMMA 8 2. UWEPO WA SHERIA NA KANUNI ZINAZOTABIRIKA 11 3. MIUNDO NA WAJIBU ZINAZORATIBIKA NA MADHUBUTI 13 4. UWEPO WA OFISI HURU YA USIMAMIZI WA MADENI 18 5. USHIRIKI WA UMMA, UJUMUISHWAJI NA KUWEKA TAARIFA HADHARANI 20 6. KUHESHIMU UBINADAMU NA HAKI ZA WATU ZA KIIKOLOJIA 23 7. KUHESHIMIANA NA USAWA KATIKA UBIA NA WAKOPESHAJI NA WAFADHILI WA KIMATAIFA 25 MAREJEO NA USOMAJI WA ZIADA 27

MKATABA WA KUKOPA DIBAJI Nchi za Kusini mwa jangwa la Sahara zinakabiliwa na changamoto kubwa katika michakato ya kuingia mikataba ya madeni na usimamizi wa madeni ya umma. Changamoto hizo zinatokana na vyanzo vya fedha za maendeleo, michakato ya kuidhinisha mikopo, hali na masharti ya mikopo, uchumi mkuu na sera za udhibiti, uwezo wa kitaasisi kwa ujumla, na uwezo wa nchi kukopesheka. Majeraha ya Migogoro ya madeni ya miaka ya 1970, 1980 na 1990 yanatokana na udhaifu wa michakato ya uingiaji wa mikataba ya mikopo na usimamizi wa madeni ya umma. Migogoro hii ya madeni ilichangia kwa kiasi kikubwa matatizo ya kiuchumi na kijamii katika nchi za Kusini mwa jangwa la Sahara kwa kuathiri uimara wa uchumi na uwezo wa kukopesheka kimataifa. Madeni ya muda mrefu yalidumaza uwekezaji, ukuaji wa uchumi na biashara. Kulipia madeni kuliyasonga matumizi ya serikali katika elimu, afya na mahitaji mengine ya kijamii katika nchi nyingi zilizokuwa zinadaiwa. 6

Kanuni na Miongozo ya Ukopaji huru wa fedha kwa nchi za Afrika Mkataba huu wa Kukopa una Kanuni na Miongozo ya Ukopaji huru wa fedha. Unataka kutoa mwongozo na kujulisha ukopaji huru kwa lengo la kuchangia uboreshaji wa utawala dhaifu wa sasa, michakato ya kitaasisi na kisheria ya mikataba ya mikopo na usimamizi wa deni la umma. Kwahiyo, AFRODAD inazihimiza nchi zote zinazokopa hasa zile zilizopo Kusini mwa jangwa la Sahara kufuata kanuni na miongozo, ili kuhakikisha ufanisi na utumiaji wenye tija wa rasilimali madeni na vifaa, kuzuia kujirudia kwa migogoro ya madeni na kuzifanya serikali kuwajibika kwa wananchi wao. Mkataba huu una kanuni na miongozo saba pana zifuatazo: 1. Uzingatiaji wa busara na desturi za ukopaji na usimimiaji wa madeni ya umma 2. Uwepo wa sheria na kanuni zinazotabirika 3. Miundo na wajibu zinazoratibika na madhubuti 4. Uwepo wa ofisi huru ya usimamizi wa madeni 5. Ushiriki wa umma, ujumuishwaji na kuweka taarifa hadharani 6. Kuheshimu ubinadamu na haki za watu za kiikolojia 7. Kuheshimiana na usawa katika ubia na wakopeshaji na wafadhili wa kimataifa 7

MKATABA WA KUKOPA 1 UZINGATIAJI WA BUSARA NA DESTURI ZA UKOPAJI NA USIMIMIAJI WA MADENI YA UMMA 1.1 Msaada wa Kisiasa: Serikali za Kitaifa zinahitaji kutumia busara na kuupatia msaada umuhimu wa kisiasa ukopaji na usimamizi wa madeni ya umma ili kuhakikisha uendelevu wa madeni. 1.2 Mazingira Imara ya Kiuchumi: Serikali za Kitaifa lazima:- 1.2.1 Zihakikishe kuwa mkakati wa madeni ya Umma unaendana na sera kuu ya uchumi kwa kuhakikisha kwamba kiwango cha ukuaji wa thamani ya sasa ya deni jipya linalotolewa ni sawa au ni pungufu ya kiwango cha ukuaji wa mauzo ya nje ya nchi, kwa ajili ya uendelevu wa deni la nje. 1.2.2 Angalia kama mkopo mpya wa mradi unaendana na sera ya maendeleo ya uchumi kwa ujumla kabla ya kuidhinishwa. 8

Kanuni na Miongozo ya Ukopaji huru wa fedha kwa nchi za Afrika 1.2.3 Kuhakikisha kuwa mkopo ni kwa ajili ya sekta zilizo kipaumbele na lazima kuimarisha uwezo wa sekta ya Umma hasa katika usimamizi wa uwekezaji wa umma ili kuongeza thamani ya fedha kwenye miradi inayofadhiliwa na mkopo. 1.2.4 Kuhakikisha uthabiti wa uchumi mkuu, uendelevu wa fedha, viwango vya chini vya riba, na usimamiaji wa viwango vya athari za ukopeshaji taasisi huru. 1.3 Vifungu vya Katiba: Serikali lazima zianzishe mifumo sahihi na yenye nguvu kisheria na miundo itakayowajibika kuratibu na kusimamia madeni ya Umma. 1.4 Ridhaa ya Umma na Uwazi: Serikali lazima zichukue hatua za Kisheria kuhakikisha kwamba ukopaji wote wa Umma na usimamizi wa madeni unapata idhini ya Bunge na Umma kwa ujumla. 1.5 Kujenga Uwezo: Serikali ni lazima zihakikishe kuwa nchi zao zina uwezo wa kina, endelevu na wa muda mrefu wa kusimamia madeni. Hii ni pamoja na: 9

MKATABA WA KUKOPA 1.5.1 Kuwa na fungu la zana za usimamizi wa madeni: Kumbukumbu sahihi na rekodi za kisasa za madeni yote na madeni yote ya nje yaliyohakikiwa wazi wazi, ratiba ya majukumu ya malipo ya madeni ikiwa ni pamoja na masuala ya dharura; uwezo wa kukadiria athari za maamuzi ya kukopa ya taasisi nyingi za ndani kwenye wasifu mzima wa deni la nchi; bajeti ya Taifa na uwiano wa malipo. 1.5.2 Kuhakikisha kwamba wafanyakazi wote wa Umma wanaoshughulika na kuingia mikataba ya mikopo na usimamizi wa deni la Umma wanalenga katika ufanisi wa kazi na majukumu yao: 1.5.2.1 Hakikisha mafunzo zaidi kwa walioshika ofisi zinazohusika kwenye mikataba ya mikopo na usimamizi wa deni la Umma wakaguzi wa hesabu, wahasibu, wachumi na wanasheria. 1.5.2.2 Hakikisha kwamba wafanyakazi wenye uzoefu na motisha wanabakia na kupatiwa msaada wa miundombinu muhimu, teknolojia na rasilimali fedha. 1.5.2.3 Hamasisha ushirikishaji wa wataalamu wa nje ili kujenga ujuzi wa rasilimali watu waliopo inavyotakiwa au hitajika. 1.5.2.4 Hamasisha kaguzi za pamoja na Taasisi nyingine kubwa za Ukaguzi zilizoendelea. 10

Kanuni na Miongozo ya Ukopaji huru wa fedha kwa nchi za Afrika 2 UWEPO WA SHERIA NA KANUNI ZINAZOTABIRIKA 2.1 Mfumo wa Sheria: Mikataba yote ya mikopo ya Umma na sheria na kanuni za usimamizi wa madeni lazima zifungamane na vifungu vya katiba na sehemu nyingine halisi za sheria zinazofafanua jinsi gani mikopo ya Umma ipatikane, itumike na kulipwa. 2.1.1 Mfumo wa Sheria lazima pia utoe muda maalum ambamo maombi ya mkopo yatafanyika na kuidhinishwa ili kuepuka kupunguza kasi ya michakato ya uidhinishaji ili kuhakikisha utekelezaji kwa wakati na ufuatiliaji wenye ufanisi. 2.1.2 Mikataba mipya ya mikopo itakuwa ndani ya muktadha wa mkakati mzima wa deni la serikali na kulingana na programu/mipango ya maendeleo ya Taifa. Mipango ya kukopa ya serikali inabidi kuendana na uendelezaji wa muda mrefu wa deni. 2.2 Mamlaka ya Kukopa: Mfumo wa Kisheria lazima uweke wazi ni nani mwenye mamlaka ya kukopa kwa niaba ya serikali. 11

MKATABA WA KUKOPA 2.2.1 Kuna haja ya kuwa na miongozo iliyowazi ya kisheria/kikatiba kuhusu majukumu na uwajibikaji kati ya wakala wa serikali wanaohusika kwenye usimamizi wa madeni, hasa kwa upande wa Wizara ya Fedha, Benki Kuu na wakala tofauti au yeyote wa usimamizi wa madeni na majukumu ya wafanyakazi yaliyoainishwa vizuri ikiwa ni pamoja na sera bayana za udhibiti na ufuatiliaji na mipangilio ya utoaji taarifa. 2.3Kiwango cha juu cha Kukopa: Inabidi ziwepo sheria, kanuni na sera ambazo zitaainisha mipaka ya ukopaji wa madeni ya Umma ya nje. Hii lazima ilandane na uchambuzi endelevu wa deni la nchi. 2.4 Idhini ya Kukopa: Muhimili wa kutunga sheria wa serikali Bunge litaidhinisha mikopo kabla mikataba haijasainiwa. Hii itawezesha na kuhakikisha kwamba mchakato wa mkataba wa mkopo ilifanyika kulingana na miongozo na sheria zilizowekwa, na inaweza kulipwa katika bajeti ya Taifa. 2.5 Mchakato wa Kuidhinisha: Sera ya Kukopa ambayo inaainisha taratibu za kuidhinisha, muundo wa kamati ya majadiliano na maandalizi ya majadiliano lazima zianzishwe. 12

Kanuni na Miongozo ya Ukopaji huru wa fedha kwa nchi za Afrika 3 MIUNDO NA WAJIBU ZINAZORATIBIKA NA MADHUBUTI 3.1 Muundo wa Taasisi, Uratibu na Mawasiliano: Serikali zitaanzisha Ofisi ya Usimamizi wa Madeni ya Taifa (OUMT) kuhakisha uratibu na mawasiliano mazuri kati ya wadau mbalimbali kwenye kuingia mikataba ya mikopo na taratibu za usimamizi wa madeni. 3.2 Wizara ya Fedha: Wizara husika (mf. Wizara ya Fedha) itawasilisha mahitaji ya serikali kukopa kwa ajili ya idhini bungeni ili kupitishwa kama inavyotakiwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za nchi. 3.2.1 Wizara ya Fedha: Itasimamia fedha za nchi ili kuhakikisha kuwa uwajibikaji kamili unafanyika kwa Bunge na kwamba udhibiti wake wa fedha unaimarishwa. 3.2.2 Wizara husika: Wizara husika zita: 3.2.2.1 Toa taarifa za mara kwa mara za maendeleo ya programu zote zinazofadhiliwa na mikopo ya nje/ miradi kwa Wizara ya Fedha. 13

MKATABA WA KUKOPA 3.2.2.2 Shiriki katika majadiliano na mashauriano yote ya mikataba yote ya mkopo kwa ajili ya miradi na programu chini ya mamlaka yao. 3.2.2.3 Tekeleza, fuatilia na tathmini miradi na programu zote kwenye mamlaka yao kwa kushirikiana kwa karibu na wafadhili, Wizara ya Fedha, asasi za kiraia na walengwa. 3.3 Uangalizi wa Bunge: Bunge litasimamia jukumu muhimu la kuhakikisha uwajibkaji katika kuingia mikataba na michakato ya usimamizi wa madeni. 3.3.1 Bunge madhubuti na linalowajibika hukabiliana na athari za ukopaji uliokithiri kwa kushinikiza mifumo ya uwajibikaji wa serikali na uchunguzi wa kisheria, na kuishinikiza serikali kuboresha utendaji wa kifedha na kibajeti. 3.3.2 Mwanasheria Mkuu: Mwanasheria Mkuu wa Serikali atatoa ushauri wa kisheria wakati mchakato wa mkataba wa mkopo ili kuhakikisha kwamba unaenda sambamba na sheria za nchi. 3.4 Ukopaji wa Makampuni ya Umma: Serikali lazima ianzishe utaratibu na vigezo kwa ajili ya kutoa dhamana kwa makampuni ya Umma. Hii ni muhimu kwasababu endapo makampuni ya Umma yatashindwa kulipa riba na gharama za madeni, serikali itatakiwa kulipa. 14

Kanuni na Miongozo ya Ukopaji huru wa fedha kwa nchi za Afrika 3.5 Jukumu la Benki Kuu: Benki Kuu itapaswa kufanya kazi kama mshauri wa kifedha wa serikali kwenye masuala ya mikataba ya mikopo na kusimamia madeni. 3.5.1 Sheria ya nchi inatakiwa ionyeshe wazi madaraka ya Benki Kuu, uhusiano wake na Wizara ya Fedha, uhuru wake, uwajibikaji wake kwa Bunge na Taifa, tahadhari lazima ichukuliwe ili kuepuka udhalimu/matumizi mabaya ya madaraka kama hayo. 3.5.2 Benki Kuu inatakiwa kudumisha mfumo salama na madhubuti wa malipo na ulipaji. 3.5.3 Benki Kuu itapaswa kupata maelezo yote ya mali fedha za serikali na taasisis zake kutoka kwenye taasisi za fedha na kuziwasilisha kwenye Ofisi ya Madeni na Wizara ya Fedha. 3.5.4 Benki Kuu itapaswa kuwezesha ulipaji wa madeni kwa kufuata ushauri wa Ofisi ya Usimamizi wa Madeni. 3.6 Mkaguzi Mkuu wa Hesabu: Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa hesabu itawajibika kukagua taarifa za madeni ya umma zilizowekwa wazi kwenye taarifa za fedha za serikali au nyaraka nyingine ambazo kiasi cha deni la Umma limeonyeshwa na kuhakikisha kuwa kiasi kimeonyeshwa/wakilishwa katika misingi sahihi. 15

MKATABA WA KUKOPA 3.6.1 Mkaguzi Mkuu wa Hesabu lazima awezeshwe vizuri na aripoti kwa wakati kuhusu akaunti ya umma ya nchi. 3.6.2 Mkaguzi Mkuu wa Hesabu atafanya uchambuzi huru na kuhakikisha kwamba taarifa zinawekwa bayana kwa umma na bodi muhimu au makundi ili kuwezesha usimamizi wa madeni ulioboreshwa na uelewa wa athari za kujifunga kifedha za sasa na za baadaye. Mkaguzi Mkuu wa Hesabu lazima afanye kaguzi kuhakikisha ufuatiliaji wa vigezo vya biashara za kifedha vilivyowekwa kwenye usimamizi wa madeni. 3.7 Mhasibu Mkuu: Ofisi ya Mhasibu Mkuu itatoa miongozo na taratibu kwa ajili ya usimamizi wa fedha za umma. Ofisi ya Mhasibu Mkuu inapaswa kuweka mfumo wa jumla wa udhibiti na utumiaji wa rasilimali za umma. 3.8 Taasisi za Fedha za Kimataifa/wakopeshaji: Taasisi za fedha za Kimataifa kwa kutumia Miongozo ya Usimamiaji wa Madeni ya Umma ya Kundi la IMF/ Benki ya Dunia lazima ziwezeshe ushauri wa kitaalamu kwa nchi, mara kwa mara kusisitiza haja ya madeni endelevu na kuwezesha utekelezaji wenye ufanisi wa mipango ya uchumi. 16

Kanuni na Miongozo ya Ukopaji huru wa fedha kwa nchi za Afrika 3.8.1 Uwezo wa ufadhili wa ndani: Taasisi za Fedha za Kimataifa zisaidie katika kujenga na kuimarisha uwezo wa ndani wa kufanya tafiti ambazo zitaarifu mchakato wa kutengeneza sera. 17

MKATABA WA KUKOPA 4 UWEPO WA OFISI HURU YA USIMAMIZI WA MADENI 4.1 Mfumo wa Usimamizi wa Madeni: Kwa madhumuni ya kuwa na mfumo mzuri wa uratibu wa mikataba ya mikopo na usimamizi wa madeni serikali inabidi ianzishe Ofisi ya Usimamizi wa Madeni. Shughuli za Usimamizi wa Madeni lazima ziwekwe chini ya Ofisi moja ya Usimamizi wa Madeni yenye majukumu ya nyuma, kati na ya mbele ya kiofisi. Wakati ofisi ya mbele itashughulika na sera za madeni, sera za kukopa, taratibu na mbinu za kujadiliana, uelewa wa kitaaluma, ofisi ya kati itajikita kwenye kitengo cha uchambuzi/upembuzi na athari, umuhimu wa mkopo uliopendekezwa wakati ofisi ya nyuma itajishughulisha na utunzaji wa takwimu, ukuaji wa mikopo, uthibitishaji wa taarifa za madeni, misaada na masharti. 4.2 Uratibu wa Madeni yote: Ofisi ya Usimamizi wa Madeni inaiwezesha nchi kuunganisha, kupanga na kuimarisha shughuli zote za usimamizi wa madeni kwenye chombo kimoja maalumu kilicho huru. Hii inaruhusu mpangilio mzuri wa udhibiti na inaondoa mwingiliano na kujirudia kunakohusiana na ushirikishwaji wa mawakala wengi, na ambapo usambaaji wa habari ni dhaifu na unaratibiwa vibaya. 18

Kanuni na Miongozo ya Ukopaji huru wa fedha kwa nchi za Afrika 4.3 Mfumo wa Taarifa za Usimamizi wa Madeni: Shughuli na jukumu la Ofisi ya Usimamizi wa Madeni vinapaswa kuwa vimeandikwa vizuri na kuwekwa kwenye nyaraka, ikiwa na kitabu cha muongozo, ikiwa ni pamoja na program muhimu za usimamizi za komputa. 4.4 Uwepo wa huduma za Kitaalamu: Ofisi huru ya Usimamizi wa madeni ya umma (DMOs) itoe faida za kipekee za kiutawala na utumishi na ubadilikaji ambao sio wa kawaida kwa ofisi/vitengo vya usimamizi wa madeni ambavyo vimeingizwa kwenye wizara za fedha na/benki Kuu. 4.5 Aina ya Ofisi ya Usimamizi wa Madeni: Jukumu la Ofisi ya Madeni linategemeana na shughuli zake za usimamizi wa madeni, kama majukumu inayopangiwa na sheria na taratibu, kwenye mkakati inayochagua kuufuata na kwenye njia ilizowekewa kuyafikia malengo yake. Ili kuhakikisha kwamba michakato ya usimamizi wa madeni, kama vile ulipaji wa madeni inafanyika kwa ufanisi zaidi; wajibu na majukumu lazima yawe wazi na taarifa za madeni lazima ziwe zimeimarishwa. 19

MKATABA WA KUKOPA 5 USHIRIKI WA UMMA, UJUMUISHWAJI NA KUWEKA TAARIFA HADHARANI 5.1 Umiliki na Uwajibikaji: Umiliki wa Kitaifa ni muhimu kwa mafanikio ya miradi yote ya maendeleo inayofadhiliwa kwa mikopo na ruzuku. Watu, ambao wanapaswa kuwa walengwa wa mwisho wa mikopo iliyochukuliwa kwa jina lao, lazima wawe na haki ya kushiriki katika mchakato wa kufanya maamuzi ya yanayohusu kukopa kwa umma. Hili lifanyike kupitia uwakilishi wa bunge, ushiriki wa raia wa moja kwa moja au ushiriki wa raia kupitia asasi za kiraia au uwakilishaji. Asasi za kiraia, hasa waangalizi na makundi yenye maslahi, yanapaswa kutambuliwa kama njia za kuimarisha umiliki wa fedha za umma na uwajibikaji. 5.2 Uwazi na ushirikishaji wa wananchi kikamilifu: Mchakato wa mkataba wa mkopo lazima uwe wa uwazi na shirikishi, ukiwashirikisha wananchi na jamii zinazoathirika kwa kuwapa taarifa na muda wa kutosha kujadili uchukuaji wa mkopo, ikiwa ni pamoja na kusudi na masharti ya mkopo kwa mujibu wa katiba ya nchi. 20

Kanuni na Miongozo ya Ukopaji huru wa fedha kwa nchi za Afrika 5.3 Kutambuliwa asasi za Kiraia Kisheria na Kitaasisi: Serikali zilizokubaliana na Mkataba huu zianzishe mabaraza na taratibu ambazo wananchi kwa kupitia hayo mabaraza na hizo taratibu wanaweza kujadili na kushawishi mapendekezo ya sera za kiuchumi kuimarisha umiliki wa umma wa mikakati ya uchumi na madeni. Sheria za serikali lazima zionyeshe wazi kwamba hii asasi ya kiraia ita: 5.3.1 Kuwa na jukumu la kushauri katika mchakato wa mkataba wa mkopo na usimamizi wa madeni ikifanya kama wataalamu ikifanya kazi kwa karibu na wanaoongoza majadiliano na serikali kwa kushawishi maamuzi ya kisera, kwa kutoa ushauri wa kisheria, kitaalamu au kiufundi. 5.3.2 Fanya tafiti na uhamasishaji wakati wa kutengeneza mapendekezo ya mradi/programu na kwenye hatua za majadiliano ya makubaliano ya mkopo. 5.3.3 Fuatilia miradi na mipango ya maendeleo, ikiwa ni pamoja na namna inavyofadhiliwa. Hii inaruhusu asasi za kiraia kufuatilia matokeo ya miradi na programu zinazofadhiliwa na mikopo, pamoja na fedha zilizotolewa kama matokeo ya mipango ya msamaha wa madeni. 21

MKATABA WA KUKOPA 5.3.4 Hamasisha umma na ongeza ufahamu juu ya masuala ya mikopo, ruzuku na masuala ya fedha za maendeleo. 5.4 Utoaji wa taarifa kwa umma: Sheria ya Serikali ya Fedha za Umma na uwajibikaji ieleze bayana kuwa taarifa za matumizi ya fedha za mikopo ziwekwe wazi kwa umma, hasa makundi ya kiraia, yenye nia ya kufuatilia mikopo na ruzuku za serikali. Mkataba wa mkopo uwekwe wazi kwa umma na usambazwe kwa wadau mbalimbali kwa kutumia njia sahihi za mawasiliano na zinazopatikana chini. Hii inaweza kuwa kupitia kwa wabunge, matangazo kwa njia ya tovuti, vyombo vya habari vya taifa, radio na/au televisheni. 5.5 Lugha: Mkataba upatikane kwa lugha kuu za Taifa (ikiwa ni pamoja na lugha za jumuiya zilizoathirika). Matoleo yote mawili toleo kuu na lililotafsiriwa yawe na uhalali sawa mahakamani. 22

Kanuni na Miongozo ya Ukopaji huru wa fedha kwa nchi za Afrika 6 KUHESHIMU BINADAMU NA HAKI ZA WATU ZA KIIKOLOJIA 6.1 Haki ya Umma ya Maendeleo endelevu: Sambamba na mkataba wa Afrika Haki za Binadamu serikali zihakikishe kuwa wananchi wanayo haki ya kupata kikamilifu haki yao ya maendeleo endelevu kutoka kwenye rasilimali madeni. Haki ya maendeleo na uchumi zisitengwe na haki za kijamii, kisiasa na kitamaduni. 6.2 Kukabili madhara ya Kukopa: Serikali ihakikishe kwamba madhara ya kukopa na athari zozote za utekelezaji wa miradi ya maendeleo vinapunguzwa mpaka kiwango cha chini kwa watu wa kawaida hasa makundi maalumu kama vile wanawake na watoto. Miradi inayofadhiliwa kwa madeni lazima isikiuke haki za binadamu na wala isichangie ukiukwaji wa haki za binadamu. Haki hizi zimebainishwa kwenye Mikataba na makubaliano yanayotambulika kimataifa ya Haki za Binadamu ambayo wakopaji au wakopeshaji wamesaini. 23

MKATABA WA KUKOPA 6.3 Uhamishaji: Miradi mikubwa ya maendeleo kwa hali yoyote ile lazima iepuke kuwa chanzo cha uhamishaji wa wazawa, masikini wa vijijini na wale wa kwenye makazi duni mijini kwenye ardhi yao, chanzo cha kipato na jamii. Iwapo miradi ya maendeleo kwa sababu yoyote itasababisha uhamishaji wa watu kutoka kwenye makazi yao fidia stahili itatolewa kwa jamii zilizoathiriwa. 6.4 Uharibifu wa Mazingira: Ukopaji wowote wa Umma ni lazima usikubali miradi inayokiuka viwango vya chini vinavyokubalika kimataifa vya utunzaji/ulinzi wa jamii, kazi na mazingira. 24

Kanuni na Miongozo ya Ukopaji huru wa fedha kwa nchi za Afrika 7 KUHESHIMIANA NA USAWA KATIKA UBIA NA WAKOPESHAJI NA WAFADHILI WA KIMATAIFA 7.1 Kuheshimiana: Serikali zitahakikisha kuwa uingiaji wa mikataba ya mikopo na masuala ya usimamizi wa madeni na wakopeshaji yanafanyika kwa kuheshimiana na utu. Kanuni za msingi za Ufanisi wa Msaada kwenye Azimio la Paris ya mwaka 2005, Ajenda ya Accra ya mwaka 2008 na Ushirikiano wa Busan kwa Ushirikiano Madhubuti wa Maendeleo ya mwaka 2011 lazima zitumike kuhakikisha usawa katika ushirikiano kati ya wafadhili na mataifa yanayokopa. 7.2 Kukataa Masharti: Nchi wanachama wa Mkataba huu lazima wakatae utumiaji wa masharti wa wafadhili na taasisi za fedha za kimataifa wanapokopa fedha. Hii huwasababishia kuwajibika kwa wakopeshaji na sio kwa wananchi wao. 25

MKATABA WA KUKOPA 7.3 Kuheshimu na Kuwezesha Taasisi za ndani: Wafadhili na Wakopeshaji wote wanapaswa kuvipatia vyombo vya uangalizi vya serikali na mabunge msaada wa kifedha na kitaalamu kuviwezesha kushiriki kikamilifu katika kujadili na kufuatilia mikopo ya nje. 7.4 Usuluhishi wa Haki na Uwazi: Mkataba wa mkopo lazima uwe na kifungu kwa ajili ya utaratibu wa usuluhishi huru na wazi iwapo kutakuwa na ugumu katika ulipaji au mgogoro (kwa ombi la mkopaji au mkopeshaji). Kutakuwa na usubirishaji wa ulipaji wa deni wakati majadiliano yakiendelea. Mkopaji asifunguliwe kesi mahakamani wakati majadiliano yanaendelea. Wakopaji na Wakopeshaji lazima wakubaliane na uamuzi wa msuluhishi huru na kuna haki ya kukata rufaa. 26

Kanuni na Miongozo ya Ukopaji huru wa fedha kwa nchi za Afrika Marejeo na Usomaji na Ziada 1. AFRODAD (2007) The Loan Contraction Process in Africa: Making Loans Work for the Poor: The Case of DRC, Study Report 2. AFRODAD (2007) The Loan Contraction Process in Africa: Making Loans Work for the Poor: The Case of Malawi, Study Report 3. AFRODAD (2007) The Loan Contraction Process in Africa: Making Loans Work for the Poor: The Case of Tanzania, Study Report 4. AFRODAD (2007) The Loan Contraction Process in Africa: Making Loans Work for the Poor: The Case of Mozambique, Study Report 5. Borresen P and Pascal E.C (2001); Role and organization of a debt office, Proceedings of the second inter-regional debt management conference, United Nations Conference on Trade and Development, pp 33-53. 6. Chadambuka. Z.T. (2009) A Critical Review of the Legal Framework of the Public Loan Contraction and Debt Management System in Zimbabwe. ZIMCODD, Harare. 7. Mutasa, C. (2007) Operationalizing debt sustainability in UNCTAD (2007) Proceedings of the Fifth Inter-regional Debt Management Conference, UN, Geneva. 27

MKATABA WA KUKOPA 8. De Renzio, P and Krafchik, W. (2007) Lessons from the field: The impact of Civil Society Budget Analysis and Advocacy in Six Countries, A Practitioners Guide, International Budget Project, Washington D.C. International Budget Project. 9. Fyson, S (2009) Sending in the Consultants: development agencies, the private sector and the reform of public finance in low-income countries, International Journal of Public Policy, Vol.4 n. ½. 10. Krafchik, W (2003) What role can Civil Society and Parliament Play in Strengthening the External Auditing Function? International Budget Project, Washington D.C. International Budget Project. 11. Maruping. A.M. (2003) Public Debt Sustainability and the development of domestic markets in UNCTAD (2003) Proceedings of the Fifth Inter-regional Debt Management Conference and WADMO conference, UN, Geneva. 12. MEFMI (2004) Towards an Effective national debt management strategy in Tanzania, Workshop on Debt Management, Dar es Salaam, United Republic of Tanzania. 13. MEFMI (2005) MEFMI, Public Debt Management Procedures Manual vol 1. Sable Press (PVT) Ltd, Harare. 14. Meja, V. (2008) The Public Loan Contraction Process-A key to Debt Management and Economic Governance, AFRODAD. Harare. 15. Overseas Development Institute (2007) Reforming public financial management when the politics aren t right: A proposal, Opinion Paper 89, London. 28

Kanuni na Miongozo ya Ukopaji huru wa fedha kwa nchi za Afrika 16. UNCTAD (2007) Proceedings of the Fifth Inter-regional Debt Management Conference, UN, Geneva. 17. UNCTAD (2003) Proceedings of the Fifth Inter-regional Debt Management Conference and WADMO conference, UN, Geneva. 18. United Republic of Tanzania (2004) Governments Loans, Guarantees and Grants Act, 1974 and Amendments 2004 19. UNITAR (2002) Institutional Framework for Public Sector Borrowing, UNITAR Training Programmes in the Legal Aspects and Financial Management, Document No.17. Geneva. 29

MKATABA WA KUKOPA KWA TAARIFA ZAIDI WASILIANA NA African Forum and Network on Debt and Development (AFRODAD) 31 Atkinson Drive, Hillside S.L.P. CY1517, Causeway Harare, Zimbabwe Simu: +263 4 778531/6 Nukushi: +263 4 747878 Tovuti: www.afrodad.org Barua pepe: afrodad@afrodad.co.zw 30

Kanuni na Miongozo ya Ukopaji huru wa fedha kwa nchi za Afrika 31

African Forum and Network on Debt and Development 31 Atkinson Drive, Hillside S.L.P. CY1517, Causeway Harare, Zimbabwe Simu: +263 4 778531/6 Nukushi: +263 4 747878 Tovuti: www.afrodad.org