Siku ya kwanza. Mguso wa ngozi-kwa-ngozi (Ulezi wa kangaruu) Mtoto wako anaweza kuhisi mdundo wa moyo wako

Similar documents
Information for assessors (do not distribute this page to participants):

Utangulizi wa ugonjwa wa shinikizo la damu

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti

Yaliyomo. Kuhusu kitabu hiki. Hautakuwa peke yako. Mfumo wa msaada ni wa manufaa sana wazazi wote wanahitaji!

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees

PYRINEX. 1 Liter INSECTICIDE

TIST HABARI MOTO MOTO

Kijitabu cha Maelezo cha Programu ya Famasia

Kifaa Maalum cha Kutazamia Jua: Maelekezo ya kutumia

Picha ni hati miliki ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Watoto(PCD), Imperial College London. Maelezo

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA. Kwa Wanaoanza

UMRI WA MAKAMO NA KUKOMA KWA HEDHI

Wewe Maisha Yako Ndoto Zako. Kitabu cha Vijana Balehe

KUWEZESHA MBINU ZA UZUIAJI MIMBA KATIKA SUHULA ZA AFYA: MASWALI 10 KWA VIKUNDI VYA JAMII KUZINGATIA

Jamii. ,,,^mm^mmm-<^^^^ illli MA RH-EREN.CE CENTRE

AMMA KWA AFRIKA RATIBA/ITIKADI. Ratiba Maalum ya Kutibu Magonjwa Maambukizi na Hususan Fikra Zinazoleta Pooza Mwili na Akili

Vijana wanazungumza kuhusu ujinsia, maisha na uhusiano VIJANA WANAZUNGUMZA KUHUSU NGONO, MAISHA NA UHUSIANO. Training and Research Support Centre

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

Hatari, Haki za Usalama katika Bahari 03

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Upande 1.0 Bajeti yako

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig

Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI VIDOKEZO MUHIMU KATIKA UNUNUZI NA USALAMA WA CHAKULA

MACHAGUO YA UZAZI KUFIKIRIA KUWA MZAZI

KILIMO CHA VITUNGUU MAJI NA VITUNGUU TWAUMU (SWAUMU)

Uzazi wa Mpango. Uzazi wa Mpango. Kulinganisha Ufanisi wa Njia za Uzazi wa Mpango. iwe na ufanisi zaidi. Zenye ufanisi.

International Labour Office. Kazi za Ndani Zenye Madhara kwa Watoto: Kijitabu cha Maelezo Mafupi

Uzio wa pilipili unazuia tembo kuvamia mazao shambani! Jinsi ya kujenga na kudumisha uzio wa pilipili Tanzania

Kuwawezesha wasichana kwa kuboresha kujikubali na kujithamini Hivi Ndivyo Nilivyo

Ufunguo wa Kutaalamika Haraka

Njia Bora za Ukusanyaji na Upimaji Maziwa

KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Njia bora za ukusanyaji na upimaji maziwa

Kuwa na Ukimwi ni kama vile kutakiwa kuendelea kuuzima moto unaoniunguza bila kukoma.

Muongozo wa utatuzi. Kwa wasimamizi wa malaria RDTs 06/11/16. MALARIA Rapid Diagnostic Test

Deutsche Welle, Learning by Ear 2009 Seite 1 People Who Make A Difference Liberia: Anita Varney Health Facilitator, Fishtown/Liberia

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO

Mfumo na maelezo ya kina ya mpango wa kimataifa wa viwango vya chakula kwa wenye matatizo ya kumeza (IDDSI) Juni 2017

Utunzaji, Uhifadhi na Usafirishaji Bora wa Maziwa

Mwongozo wa Familia wa Kujifunza

Mwongozo wa Kitaifa wa Ujumbe wa Uzazi wa Mpango

MUONGOZO WA UTUNZAJI WA URITHI WA UTAMADUNI 1 SECURITY AT MUSEUMS

Palliative Care Toolkit

KUPWA NA KUJAA KWA BAHARI. (TIDES AND TIME)

Human Rights Are Universal And Yet...

Kocha Mkuu. mabingwa. itakuwa INASTAHILI. Ili Kutoa mafunzo kwa wanafunzi wako kuwa. itakuwa ya kuumiza. Itachukua muda. Itahitaji moyo wa kujitoa.

Makala ya Mshiriki wa Mafunzo

Ni kwa nini mkulima awe maskini?

Rahisi. Kitabu cha mwanafunzi. Mabingwa kwa ajili ya tunda la Roho Mtakatifu. Rahisi

Ndugu na dada zangu wapendwa,

Miradi na jamii. 3.1 Utangulizi

pages/mkulima-mbunifu/

2 Usimamizi wa Rutuba ya Udongo Tanzania Organic Agriculture Movement

Mazoezi yaliyofanyika wakati wa warsha kuhusu Elimu-Jumuishi kwa Vitendo. Zanzibar, 7-10 Februari 2006

JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI

Tora UTANGULIZI KWA TORA SOMO LA KWANZA

Mutugi Kamundi. Jemma Kahn. Kiswahili. Demane na pacha wake. Author - South African Folktale

Kufunga Milango - Uponyaji Kutokana na Athari za Giza

Shabaha ya Mazungumzo haya

Usimulizi wa Riwaya ya Nyongo Mkalia Ini E. S. MOHOCHI University of Egerton, Kenya

Sera ya Faragha. Upeo. Aina za Data na Mbinu za Ukusanyaji

Mukhtasari Wa Mabishano Kwa Na Dhidi Ya Vikombe Vingi Vya Ushirika

Ufundishaji wa lugha nyingine

Mwongozo wa Mwezeshaji

United Pentecostal Church June 2017

TIST HABARI MOTO MOTO MAANDALIZI YA MWAKA 2000 Y2K PREPARATIONS SASA NI WAKATI WA KUANZA KUPANDA MBEGU ZAKO

Programu ya Uendelezaji Mifumo ya Maji Vijijini (PUMMV) katika Tanzania. Modeli wa Ukodishaji Mradi

Usindikaji bora wa maziwa

Rahisi. Mabingwa kwa ajili ya tunda la Roho Mtakatifu. Kitabu cha mwanafunzi. Rahisi

usudi la Maisha Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na kupishana usiku na mchana, kuna kweli ishara kwa wenye akili, ambaye mkumbuke-

Njia za upimaji wa mpango wa kimataifa wa viwango vya chakula kwa wenye matatizo ya kumeza (IDDSI) VYAKULA VINYWAJI VYA KAWAIDA

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level

LBE 2009 Migration Episode 3: Living without documents

Roho Mtakatifu Ni Nini?

Kiu Cha umtafuta Mungu

Ushindi ndani ya Kristo W. W. PRESCOTT

Mabingwa kwa ajili ya tunda la Roho Mtakatifu. Iliyoendelea sana. Kitabu cha mwanafunzi. Iliyoendelea sana

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

Uzalishaji wa mboga na matunda ni muhimu kwa afya na kipato

Juni 3-9 Pata Manufaa Kamili kwakusomabiblia

Mwongozo wa Utamaduni Toleo la Kwanza

CGAP Smallholder Household Survey in Tanzania / Utafiti wa kaya ndogondogo Tanzania

United Pentecostal Church April Kushangilia Kwa Sala

Iliyoendelea sana. Kitengo cha 2. Kitabu cha mwanafunzi Iliyoendelea sana

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2012

Early Grade Reading Assessment for Kenya

Shamba Darasa na Stadi za Maisha kwa Vijana (SDSMV) Tanzania. Kiongozi Cha Mwezeshaji. Jaap Van Pol na Francesca Dalla Valle

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

KUZALISHA MBEGU YA MAHARAGE KIJITABU CHA KWANZA

Mwongozo wa Jamii juu ya Afya ya Mazingira

Mwongozo wa Mafunzo Yaliyochanganywaya K4Health

KITABU CHA KUONGOZA FAMILIA

MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA PRO-ROUTES. Ombi kwa ajili ya fedha za umma wa mradi wa ziada

# 18 Uponyaji Kutokana na Kukataliwa

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU

Kufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007

Transcription:

Siku ya kwanza Baada tu ya mtoto kuzaliwa ni wakati wa kufurahia, lakini pia ni wa kuchosha. Kujua vitu vichache kuhusu kunyonyesha hufanya siku ya kwanza kuwa rahisi kidogo. Baada ya kujifungua Wakati mzuri wa kuanza kunyonyesha ni baada tu mtoto wako anapozaliwa. Mtoto wako huwa tahadhari baada ya kuzaliwa, na wakati anapowekwa kifuani, mtoto huenda akasongea kwenye titi lako na kuanza kunyonya. Usiwe na wasiwasi ikiwa huwezi kunyonyesha mtoto wako baada ya kujifungua. Watoto wengine hawapati ugumu wa kubebwa hata kama kunyonyesha kumecheleweshwa. Wataalamu wako wa huduma ya afya wanaweza kukusaidia kujenga na kutunza utoaji wa maziwa yako hadi uwe na nafasi ya lishe lishe maalum ya kwanza. Mguso wa ngozi-kwa-ngozi (Ulezi wa kangaruu) Wacha muuguzi wako amweke mtoto wako kwenye kifua chako na blanketi juu yenu wawili. Vuta mtoto karibu kwenye kifua kati ya matiti yako. Inapaswa, umwache mtoto hapo kwa angalau muda wa dakika 30 au hadi mtoto anyonye. Mguso wa ngozi-kwa-ngozi baada ya kujifungua una faida zifuatazo kwa mtoto: Wewe na mtoto wako mnapata kujuana Mtoto wako anaweza kuhisi mdundo wa moyo wako Kuwa karibu na mama ni pahali pazuri kwa mtoto wako ili aweze kuzoea mazingira yake mapya Halijoto ya ngozi iliyo thabiti, kiwango cha pigo la moyo, na shinikizo la damu Mtoto huenda asilie Dang a Mara tu mtoto anapozaliwa, na baada ya siku 3 hadi 4, matiti yako hutoa aina ya maziwa yanayoitwa dang a, ambayo ni mazito zaidi kuliko maziwa ya kawaida. Maziwa haya ya kwanza ya rangi ya manjano au dhahabu yana virutubishi vyote ambavyo mtoto wako mchanga anahitaji kwa siku za kwanza za maisha, kwa kiwango kamilifu. Yanasaidia kukinga mtoto wako kutokana na maambukizo, ambayo ndiyo maana ni vizuri kuanza kunyonyesha mapema iwezekanavyo. Usiwe na wasiwasi ikiwa inapoonekana kwamba mtoto wako anapata kiwango kidogo wakati wa lishe ya kwanza. Kabla ya maziwa yako kuongezeka (kawaida kati ya Na» Kuhakikishiwa ubora kwa pamoja na: Msaada wa moja kwa moja wa masaa ishirini na nne kwa wiki (24/7). Wauguzi na washauri wa unyonyeshaji wanapatikana. Piga simu kwa Feeding Expert (Mtaalamu wa Malisho): 1-800-986-8800.

o Mbinu na Vidokezo vya Kunyonyesha: Siku ya kwanza siku 3 hadi 4), mtoto wako anapokea kiwango kidogo cha dang a kutoka katika matiti-yako kiasi cha kijiko cha chai hadi kijiko kikubwa pekee yake kwenye kila lishe. Kiwango hiki kinatosha kumlisha mtoto wako. Kunyonyesha kila mara Nyonyesha kila mara siku chache za kwanza, kila saa 1-3 (mwanzo wa kipindi hadi mwanzo wa kipindi kingine) ili: Kusaidia kujenga utoaji wa maziwa vizuri Kumpa mtoto wako lishe, kingamwili, na faida kadhaa za afya Kusaidia mtoto wako kutoa choo cha kwanza (meconium) Kusaidia kupunguza uwezekano wa matiti yaliyojaa wakati maziwa yako yanapokuja kwa mara ya kwanza Jifunze kunyonyesha wakati usaidizi wa kitaalam unapatikana na kabla matiti hayajajaa Namna ya kuanza Ufunguo wa kunyonyesha vizuri ni kuweka titi lako vizuri na kinywa cha mtoto wako. Mkao mzuri unawezesha mtoto wako kukomeo kwenye titi. Tumia mto ili kusaidia kushikilia mwili wa mtoto wako. Utataka kunyonyesha mtoto mara kwa mara ili kuhifadhi utoaji wako. Inaweza kuchukua majaribio kadhaa kupata kumbeba vizuri. Ikiwa mtoto wako hajabebwa vizuri, anza tena. Na kama lishe ya kwanza hainyweki vizuri, pumzika! Wewe na mtoto wako ni wageni; kwa haya; uvumilivu unahitajika. Jaribu tena baada ya dakika 30 au zaidi. Ni sawa kuomba msaada: Na kumbuka kulala kidogo wakati mtoto anapolala! Baada ya kujifungua kwa njia ya upasuaji Kunyonyesha mapema na wakati mwingi hutoa faida nyingi kwako na mtoto wako baada ya kujifungua kwa njia ya upasuaji. Kunyonya kwa mtoto wako unasisimsha uterasi ya mama kupunguka kwa haraka na una harakisha kupona kwake. Kunyonyesha pia kunaleta hisia zako na mtoto wako karibu, ambako ni muhimu ikiwa mlitenganishwa baada ya kujifungua au ikiwa kujifungua kulitisha ajabu. 2011 Abbott Laboratories Inc. Januari 2011 73150 Swahili The First Days

Mikao mbalimbali Mikao ya kunyonyesha Kishiko cha kulaza Kishiko cha kulaza cha katikati Kishiko cha kandanda Kulala chini Mikao ya kunyonyesha Utahitajika kupata mkao au mikao yenye starehe kwako wewe na mtoto wako. Wataalamu wengine wanapendekeza mikao ya kubadilishabadilisha. Kwa njia hiyo mtoto hatabebwa na kuweka shinikizo mahali pamoja kila wakati. Jaribu mikao hii na uone inayokufaa. Kishiko cha kulaza Keti kwenye kiti chenye starehe, na kwa usaidizi wa mkono wako na mgongo usiegemee juu ya mtoto wako. Tumia mto au blanketi laini iliyokunjwa, taulo, au vitu vingine laini kuegemeza mkono wako na kuleta mtoto wako kwa urefu wa titi lako. Akina mama wengine hupata kutumia stuli kuwa muhimu kuwasaidia kuweka mahitaji yao kwa kiwango sawa na mapaja yao. Weka mtoto wako akikuangalia katikati ya tumbo lako, tumbo kwa tumbo, na uso na magoti karibu. Weka kichwa cha mtoto kwenye mkunjo wa kiwiko, na mdomo wake mbele ya chuchu, na pania chini ya mkono wa mtoto wako ukizunguka kiuno chako, mbali ya njia. Vuruta mtoto wako kwenye titi wakati mdomo wake umefunguka, mbali kidogo na titi ili pua yake, shavu lake, na kidevu vyote vishike titi. Kishiko cha kulaza cha katikati Mkao huu ni mzuri kwa mama ambaowamekuwa ana shida ya kubeba mtoto na mwenye watoto wadogo au watoto waliozaliwa kabla ya wakati wao. Unaweza kuona kubebwa huko kuzuri kuliko mkao wa kishiko cha kulaza. Kwa mshiko huu, kaa vizuri, na mito ikiwa nyuma yako. Egemea nyuma kidogo ili usiiname juu ya mtoto. Shika mtoto wako katikati wa mwili wako, kwenye mkono kinyume na titi ambalo mtoto atanyonya. Shikilia shingo ya mtoto wako na kichwa na mkono huu kwa kuwa au mwili wake utaongezeka kwa urefu wa kigasha chako. Tumia mkono kwenye upande wa titi unaonyonyesha nao kushikilia titi. Weka kinywa chamtoto wako kwa kiwango cha chuchu yako, na mwili wake kwa upande wake, ukikuangalia. Vuta mtoto wako kwenye titi wakati mdomo wake umefunguka kabisa, mbali kidogo na titi ili pua yake, shavu lake, na kidevu vyote vishike titi. Na» Kuhakikishiwa ubora kwa pamoja na: Msaada wa moja kwa moja wa masaa ishirini na nne kwa wiki (24/7). Wauguzi na washauri wa unyonyeshaji wanapatikana. Piga simu kwa Feeding Expert (Mtaalamu wa Malisho): 1-800-986-8800.

o Mbinu na Vidokezo vya Kunyonyesha: Mikao mbalimbali Kishiko cha kandanda Mkao huu ni mzuri kwa wamama wenye matiti makubwa, kwa wale waliojifungua kwa njia ya upasuaji, walio na shida ya kuwabeba watoto wao, au wamama walio na watoto wadogo au waliozaliwa kabla ya wakati wao. Mshiko huu pia unaweza kukuwezesha kuwa na mkono uliowazi, au kukuwezesha kunyonyesha watoto wawili wakati mmoja. Manufaa ya mshiko huu ni kuwa unaweza kuona jinsi ulivyowabeba. Kaakwenye kiti chenye starehe, na kwa usaidizi wa mkono wako na mgongo usiegemee juu ya mtoto. Tumia mto au blanketi laini iliyokunjwa, taulo, au vitu vingine kushikilia mkono wako. Tumia mto au blanketi laini iliyokunjwa, taulo, au vitu vingine kando yako kushikilia kiwiko chako na nyuma ya mtoto. Weka kichwa cha mtoto wako kwenye kitanga cha mkono, kiwango cha titi lako, na pania mtoto wako kwenye upande wa kiuno chako, ukimlaza chini ya mkono wako. Shikilia chini ya kichwa cha mtoto wako kati ya kidole cha gumba na kidole cha kwanza. Weka blanketi laini kati ya mkono wako na kichwa cha mtoto wako ili kuwa nyororo, ikiwa unafikiria hatakuwa sawa. Vuta mtoto wako kwenye titi wakati mdomo wake umefunguka kabisa, mbali kidogo na titi ili pua lake, shavu lake, na kidevu vyote vishike titi. Ikiwa mtoto wako ana shida ya gesi, unaweza kubadilisha shiko hilo ili mtoto wako aketi wima, ili kuwacha njia kidogo ya hewa ndani ya tumbo lake. Kulala chini Ni nzuri kwa lishe ya usiku na wakati ambapo kukaa si sawa. Lala kwenye upande wako, ukitumia mto kushikilia kichwa chako na shingo, na nyingine kwa mgongo wako ikihitajika; au lala kwa upande wako na mkono mmoja umekunjwa chini ya kichwa na mkono mwingine ukishikilia titi lako. Mlaze mtoto wako karibu na wewe kwenye kitanda chako, ili kinywa akekiwe kinyume na chuchu, na uweke blanketi iliyokunjwa, taulo, au kitambaa kilicho laini nyuma ya mgongo wa mtoto wako. Shikilia chini ya kichwa cha mtoto wako kati ya kidole cha gumba na kidole cha kwanza. Vuta mtoto wako kwenye titi wakati mdomo wake umefunguka kabisa, kidogo na titi ili pua lake, shavu lake, na kidevu vyote vishike titi. Ikiwa utahitaji kubadilisha matiti, shika mtoto wako karibu na mwili wako na sokota kwenye mgongo wako, halafu kwenye upande mwingine. Haijalishi ni mkao upi unaochagua, jambo la muhimu kukumbuka ni kwamba mdomo wa mtoto wako unapaswa kuwa kwa kiwango sawa na chuchu yako. Kichwa chake chapaswa kuwa kwenye laini sambamba na tumbo lake-ukikuangalia-usibadilishwe upande mwingine. Kumbuka ikiwa kichwa cha mtoto wako kimebadilishwa upande mwingine, ni vigumu kwake kumeza. (Jionee: Pindua kichwa chako na umeze. Halafu angalia mbele na umeze tena. Gundua tofauti?) Pia, ikiwa kichwa cha mtoto wako kimepinduliwa, inakuwa vigumu kwa mtoto wako kupata chuchu vizuri na titi kwenye mdomo wake. 2011 Abbott Laboratories Inc. Januari 2011 73153 Swahili Positions

Mambo ya Msingi Inapofika wakati wa kumlisha mtoto wako, ni vigumu kushinda manufaa ya maziwa ya titi. Maziwa ya titi: Yana viungo sawavya virutubishi vya kumsaidia mtoto wako kupigana na maambukizo na magonjwa ya kawaida ya watoto Ni ya manufaa, hupatikana kila mara, na inatolewa kwa halijoto iliyo sawa husaidia uterasi ya mama kurudi kwenye hali yake kabla-kuwa mja mzito Inapunguza hatari ya mama kupata saratani ya titi Huokoa pesa Kujifunza kunyonyesha Wanawake wengi wajawazito wanahamu ya kujua kama watafaulu katika unyonyeshaji na ikiwa watatoa maziwa ya kutosha. Kwa akina mama-kwanza, unyonyeshaji ni ustadi wa kujifunza. Utataka kujifunza mengi kama uwezavyo na kuomba usaidizi wakati unapohitaji. Vyanzo vizuri vinajumuisha daktari wako, mkunga, muuguzi au wataalamu wengine wa huduma ya afya, mshauri wa unyonyeshaji, na ligi ya La Leche, kama vile vipindi vya unyonyeshaji kazini, ambayo hutoa msaada ili kukusaidia kuendelea kunyonyesha kwa muda mrefu inavyo wezekana. Vidokezo vifuatavyo vitakusaidia kuwa tayari kunyonyesha na kukusaidia kujibu baadhi ya maswali ambayo huenda ukawa nayo. Mwanzo mzuri baada ya kujifungua Pumzika: Lala sana jinsi uwezavyo. Jipe muda wa kupona. Usijaribu kufanya mengi mapema. Lala kidogo kila siku, na lala wakati mtoto wako anapolala. Furahia wageni, lakini kumbuka unahitaji kupumzika unavyoweza katika wiki chache za kwanza. Mpangilio wa kunyonyesha: Lisha mtoto wako kila saa 1-3 wakati wa siku chache za kwanza (mwanzo wa kipindi hadi mwanzo wa kipindi kingine). Hii itasaidia kusisimsha utoaji wa maziwa, na kupunguza au kuzuia uvimbe mara tu maziwa yanapokuja. Na» Kuhakikishiwa ubora kwa pamoja na: Msaada wa moja kwa moja wa masaa ishirini na nne kwa wiki (24/7). Wauguzi na washauri wa unyonyeshaji wanapatikana. Piga simu kwa Feeding Expert (Mtaalamu wa Malisho): 1-800-986-8800.

o Mbinu na Vidokezo vya Kunyonyesha: Mambo ya Msingi Eneo: Weka mtoto wako karibu na wewe ili kuzuia kusonga sana. Pia, weka nepi, vifaa vya kubadilisha, maji au maji ya matunda yaliyo baridi, na kumbwe au vitafunio karibu na wewe. Akina mama wengine hufurahia kunywa maji baridi kidogo au maji ya matunda wanapolisha watoto wao, na wengine hupenda kusikiza muziki wa kutuliza, au yote hayo. Faraja: Hakikisha kuwa wewe na mtoto wako mko sawa kabisa wakati wa kunyonyesha, kwa kutumia mito au mkono wa kiti kushikilia uzito wa mtoto wako. Akina mama wengine hutumia blanketi iliyokunjwa, taulo, au vitu vingine laini, badala ya mito. Akina mama wengine wanapata kwamba kuweka kitu chini ya miguu husaidia kushikilia mtoto vizuri kwa kuinua eneo la paja. Msaada wa kunyonyesha: Uliza mtu akusaidie kushikilia mtoto wako na kuweka mtoto katika hali nzuri ya kubebwa, haswa wakati unajifunza kunyonyesha kwa mara ya kwanza. Akina mama wengi hufaidika kutokana na usaidizi wa mkufunzi, mtu aliye na ujuzi wa kunyonyesha, kama vile mshauri wa unyonyeshaji, daktari wa watoto, au muuguzi. Wakati wote omba usaidizi ikiwa unahitaji msaada au usaidizi wa kunyonyesha, au unahisi uchungu wakati unaponyonyesha. Mtandao wa Msaada: Kila mtu anataka kusaidia baada ya mtoto kuja. Omba usaidizi hadi daktari wako akueleze kwamba ni sawa kurudi kwa utaratibu wa kawaida. Uliza familia, marafiki, na majirani kusaidia kutayarisha au kuchukua chakula, kusafisha, kuosha nguo, vyombo, au kazi nyingine za nyumbani, kuangalia watoto wale wakubwa wengine, na kutekeleza kazi ndogo ndogo. Kumbuka, ni sawa kuomba msaada! Dawa nyingine, vitamini, na nyongeza nyingine: Wasiliana na daktari wako, mkunga, au mshauri wa unyonyeshaji ikiwa unachukua aina yoyote ya dawa, vitamini, au dawa za ziada za mitishamba, hata dawa zisizoagizwa za kuumwa na kichwa au mafua, kwa sababu dawa nyingi hupitia katika maziwa ya mama, ijapokuwa kwa kiasi kidogo. Zuia kileo na punguza kafeni. Lishe ya mama: Maziwa ya mama ndiyo ambayo mtoto wako anahitaji katika miezi 4 hadi 6 ya kwanza ya maisha yake, lakini unahitaji kuendelea kula lishe bora. Kumbuka kile unachokula au kunywa huenda ikaathiri wewe na mtoto wako. Wakati wa kunyonyesha, hakikisha kuchukua kalori 500/kwa siku zaidi ya vile ulivyokuwa kabla ya kuwa mjamzito (Kaloro 2500/kwa siku kwa wanawake wengi), chukua kiongeza kalisi na kaa na maji ya kutosha kwa kuknywa bilauri 8 za maji/kwa siku. Sidiria ya kunyonyesha na pedi ya matiti: Chagua sidiria za kunyonyesha zilizo sawa na zinazotoshea vyema, zinazoshikilia vizuri, lakini hazikazi kwamba zinasaki kwenye matiti au mgongo. Viumiko vya titi vya pamba ni vizuri kuliko vile vya sanisi, kwa sababu vinawezesha usambazaji wa hewa kwenye chuchu. Pedi za titi wakati mwingine ni muhimu kuwa nazo, kama vile nguo zinazo rahisisha kunyonyesha (mashati yanayoweza kufunguka au kuvutwa ni mazuri). 2011 Abbott Laboratories Inc. Januari 2011 73149 Swahili Basics

Kumbeba Mafunzo ya kunyonyesha yanahitaji muda na mazoezi kwako wewe na mtoto wako. Kuweka mtoto katika mkao unaofaa Weka uso wa mtoto wako na mwili ukikuangalia, na kichwa cha mtoto katika kiwango cha titi lako. Ikiwa unaweza kuchora laini sambamba kutoka kwa bega la mtoto wako hadi kiuno, basi umemweka mtoto wako katika mkao unaofaa. Hakikisha kwamba wewe na mtoto wako mko sawa kabisa, ukitumia mito au mkono wa kiti kuegemeza uzito wa mtoto wako. Kuweka titi katika mkao unaofaa Kwa uangalifu inua na shikilia titi lako polepole kwa kuweka vidole vyako chini ya titi lako na kidole cha gumba juu ya titi, mbali na areola (sehemu nyeusi inayozunguka chuchu lako). Fikiria kuweka titi lako na mkono wako katika umbo la C au U. Hakikisha kwamba vidole chini ya titi lako havigusi areola. Kumpa mtoto titi Kwa upole gusa mdomo wa chini wa mtoto wako kwenye shavu na chuchu lako katika mwendo wa chini au na kidole chako hadi mdomo wa mtoto wako ufunguke kabisa. Ikiwa kinywa cha mtoto wako hautafunguka kabisa, rudia kugusa hadi ufunguke. Kisha vuta mtoto wako haraka kwenye titi lako, ili pua ya mtoto wako, shavu na kidevu vyote vishike titi lako kidogo. Ikiwa matundu ya pua ya mtoto wako yamefungana,vuta makalio ya mtoto wako juu na karibu na wewe, ili kichwa cha mtoto wako kisonge nyuma kidogo. Mtoto wako anahitaji kunyonya zaidi ya chuchu moja. Mtoto wako anahitaji kuingiza angalau 1 ya aerola, na mdomo ukiwa juu ya mifuko ya maziwa katika eneo 1-1½ nyuma ya chuchu. Kwa njia hii, mtoto wako atapata maziwa mengi na utakuwa na uwezekano mdogo wa kupata kidonda kwenye chuchu. Mtoto wako anapoanza kunyonya kwa mara ya kwanza, utahisi mwasho wa kuvutwa kwa nguvu. Unapaswa kusikiza sauti ya mtoto wako anapomeza. Ikiwa utasikia sauti ya mwaliko (ulimi wa mtoto wako juu ya paa la mdomo wake) hii huenda ikamaanisha kwamba mtoto wako hajabebwa vizuri. Dalili zingine za kubebwa vibaya ni-uchungu katika chuchu au kufinywa. Na» Kuhakikishiwa ubora kwa pamoja na: Msaada wa moja kwa moja wa masaa ishirini na nne kwa wiki (24/7). Wauguzi na washauri wa unyonyeshaji wanapatikana. Piga simu kwa Feeding Expert (Mtaalamu wa Malisho): 1-800-986-8800.

o Mbinu na Vidokezo vya Kunyonyesha: Kumbeba Kubadilisha matiti Badilisha upande unaoanza kunyonyesha nao, kwa sababu mtoto wako ananyonya vizuri kwenye titi la kwanza ulilotumia. Ikiwa mtoto wako hanyonyi titi la pili au ananyonya kabisa titi la pili, anza kumnyonyesha titi hilo katika lishe inayofuata. Kumtoa mtoto kwenye titi Ikiwa ni lazima kumbadilisha mtoto wako wakati wa lishe au kupata kubebwa vizuri, kwa upole ingiza kidole kimoja ndani ya mdomo wa mtoto wako ili kukatiza uvutaji. Hii inasaidia kuzuia uharibifu wa chuchu na areola. Usivunjike moyo, mwanzo huenda ikachukua majaribio kadhaa kupata jinsi ya kumbeba-vyema. Njia nyingine mbili za kukatiza ufyonzajiinajumuisha kuvuta kidevu cha mtoto wako kwa upole au kufinya kwenye sehemu ya titi lako karibu na mdomo wa mtoto wako. 2011 Abbott Laboratories Inc. Januari 2011 73152 Swahili Latching On

Wiki za kwanza Kunyonyesha ni chaguo la kawaida kwako na mtoto wako, kunakotoa thamani nzuri ya kuunganisha, kama vile faida nyingi za utendajii kwa mama na mtoto. Unyonyeshaji mara kwa mara Mtoto wako anapo komaa, maziwa ya matiti pia hukomaa. Baada ya mtoto wako kuzaliwa, maziwa ya kwanza kutoka yanaitwa dang a. Maziwa haya ya kwanza ya rangi ya manjano, dhahabu yana kinga mwili na wingi wa chakula kamili kwa mtoto aliyezaliwa. Kati ya siku chache, dang a, itabadilishwa na maziwa ya matiti yaliyokomaa. Lishe ya kila mara itasaidia kutoa usumbufu unaokuja wakati mwingine na hisia ya kwanza ya kujawa na maziwa. Kila mama anataka kujua jinsi mtoto anahitaji kula na kwa muda gani. Haya ndiyo unayohitajika kujua: Mtoto wako atahitajika kunyonya kila saa 1-3, angalau mara 9-12 kwa muda wa saa 24 kwa dakika 10 au zaidi Kunyonyesha zaidi ya dakika 30 hakupendekezwi, kwa kuwa unaweza kusababisha kidonda kwenye chuchu Wacha mtoto wako, si saa, kuamua lishe itachukua muda gani Utoaji-na-Mahitaji Utoaji wa maziwa ya matiti ni kuhusu Mahitaji-na-Utoaji, vile mtoto anavyonyonya, ndivyo maziwa yatakavyotoka. Ikiwa unanyonyesha mara kwa mara au saa umepungua, matiti yatapunguza kiwango cha utoaji wa maziwa. Fuata maoni haya: Ruhusu mtoto wako angalau kunyonya titi moja wakati wa kila lishe Toa titi jingine baada mtoto wako kumaliza titi la kwanza Ikiwa mtoto wako hatunzi titi la pili au hanyonyi kabisa titi la pili, anza kunyonyesha titi hilo katika lishe inayofuata (titi lililo tupu linaweza kuhisika kuwa laini na tupu) Zingatia kuambatanisha pini ya usalama au kamba ya sidiria kama kumbusho la titi utakaloanza nalo kwenye lishe itakayofuata Mtoto wako ataduwaa na kutosheka baada ya kunyonya, lakini hakikisha kumpigia simu daktari wako au mshauri wa kunyonyesha ikiwa una wasiwasi Na» Kuhakikishiwa ubora kwa pamoja na: Msaada wa moja kwa moja wa masaa ishirini na nne kwa wiki (24/7). Wauguzi na washauri wa unyonyeshaji wanapatikana. Piga simu kwa Feeding Expert (Mtaalamu wa Malisho): 1-800-986-8800.

o Mbinu na Vidokezo vya Kunyonyesha: Wiki za kwanza Kumwamsha mtoto ili ale Kila mtoto amezaliwa na tabia yake na hitaji la kulala. Watoto wengi watalala kwa saa 18-22 katika siku ya 2-3 za kwanza baada ya kuzaliwa. Wakati wa wiki chache za kwanza, mtoto wako atahitaji kuamshwa ili kula. Watoto wengine watalala badala ya kula wakati wa wiki chache za kwanza. Hivi ni vidokezo kadhaa vya kuamsha na kunyonyesha mtoto wako: Amsha mtoto wako wakati wa mchana kwa lishe ikiwa saa 3 zimepita tangu lishe ya mwisho au ikiwa matiti yako yamejaa vibaya Hakikisha mtoto wako ameamka kabisa kabla ya kumtunza kwa kumnyonyesha mtoto aliyeamka nusu anaweza kurudi kulala wakati wa kunyonyesha; ongea na; papasa, fungua, au vua mtoto wako nguo ili kumsaidia kuamka, ukimwezesha dakika 5-10 kabla ya lishe ili kuhakikisha kuwa mtoto wako ameamka kabisa Kumbuka kwamba watoto wachanga huwa hawalali usiku wote Pumzika kwa kulala kidogo wakati mtoto wako anapolala Uzani wa mtoto Mara tu utoaji wa maziwa unapoimarishwa, mtoto wako anapaswa kuongeza aunsi 2/3 kwa siku kwa miezi 3 ya kwanza. Watoto wengi wachanga hupoteza uzito mdogo katika siku za kwanza baada ya kuzaliwa. Watoto wachanga huanza kuongeza uzito baada ya wiki ya kwanza. Baada ya wiki 2, watoto wengi wanarudi kwa uzito wao wa kuzaliwa. Nepi ya mtoto Baada ya siku nne, mtoto wako hatapitisha tena meconium (choo cha kijani kibichi au cheusi, kizito). Badala yake, mtoto wako atakuwa na mienendo ya uchengelele, angalau mara tatu kwa siku. AAP inapendekeza angalau napi chepechepe sita kwa siku baada ya siku ya 5. Wakati wa mwezi wa kwanza, mtoto wako anapaswa kuchepechepe angalau napi sita kwa siku na kuendelea kuwa na mienendo ya uchengelele wa mara 2-5. Mkojo wa mtoto wako unapaswa kuonekana safi. 2011 Abbott Laboratories Inc. Januari 2011 73151 Swahili The First Weeks