MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU

Similar documents
TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM)

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU

MAPENDEKEZO YA MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA TANZANIA

Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi

JAMHURI YA KENYA. Mkakati wa Ushirikiano MUKHTASARI FY Public Disclosure Authorized. Public Disclosure Authorized

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

Azimio lililopitishwa na Mkutano Mkuu tarehe 18 Desemba 2013 [juu ya taarifa ya Kamati ya Tatu (A/68/456/Add.2)]

Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA 2006/07

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

MAADHIMISHO YA MIAKA 15 YA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

Nilikua na Ndoto ya Kumaliza Shule Changamoto za Elimu ya Sekondari Tanzania

TANZANIA MARKETS PAN Sera zinazoboresha masoko

Songa kwenye kilele cha upeo. Masuala ya Msingi na Ujuzi juu ya Uendeshaji wa Serikali za Mitaa

NGUZO KUMI ZA KILIMO KWANZA

HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE

MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2017/18

KUHUSU AFRODAD. Dira ya AFRODAD. Dhamira ya AFRODAD. AFRODAD inalenga mchakato sawa na endelevu wa maendeleo kuelekea Afrika yenye mafanikio.

MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA PRO-ROUTES. Ombi kwa ajili ya fedha za umma wa mradi wa ziada

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA. Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo. TOLEO Na.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF) KUHUSU HAKI ZA WATOTO KATIKA KATIBA MPYA

Dodoma ambako kikao cha Bunge kinaendelea kuja kushiriki japo sehemu ya uzinduzi wa mkutano.

Dibaji ya Mwenyekiti wa Kamati ya Pamoja ya Uongozi

KAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI TANZANIA

Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara)

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )

KITEGO CHA MAREKEBISHO NA HAKI ZA MTOTO

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

Miradi na jamii. 3.1 Utangulizi

Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame M. Mbarawa (Mb.); Waheshimiwa Mawaziri na Wabunge wote mliohudhuria;

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA FEDHA

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO

Mwongozo wa Kutathimini mifumo ya Ugawanaji wa faida na Mapato Katika Miradi ya Jamii ya MKUHUMI

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA

Information for assessors (do not distribute this page to participants):

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA MHESHIMIWA DKT

AZAKI PIGA KURA UCHAGUZI MKUU TANZANIA OKTOBA. #TanzaniaTuitakayo OKTOBA 2015 ILANI YA UCHAGUZI YA AZAKI TANZANIA.

Kutetea Haki za Binadamu

MAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Afya Bora, Utu na Kinga. Ripoti ya Mashauriano ya Kiufundi Aprili 2009, Hammamet, Tunisia

Kubadili Sheria Za Mbegu Na Ulinzi Wa Aina Za Mbegu Na Mimea Nchini Tanzania

Unyanyasaji wa Watoto & Kutelekezwa

UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA)

MWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI

Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali ya Madini Ukanda

Kuuelewa Mchakato wa Bajeti Tanzania Mwongozo wa Asasi za Kiraia

Programu ya Uendelezaji Mifumo ya Maji Vijijini (PUMMV) katika Tanzania. Modeli wa Ukodishaji Mradi

TAARIFA YA MWAKA YA UTENDAJI KAZI IDARA YA UTAWALA BORA 2013/2014

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara

In the matter of an Application by the KIGOMA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (KUWASA) For a Tariff and Charges Adjustment

3. Mheshimiwa Spika, 4. Mheshimiwa Spika,

Kitabu Cha Mafunzo Ya Uongozi Kwa Wanawake

Afya Bora, Utu na Kinga. Ripoti ya Mashauriano ya Kiufundi Aprili 2009, Hammamet, Tunisia

HAKI NA TARATIBU ZA AJIRA, KAZI NA HIFADHI YA JAMII

KUSHUKA KWA HADHI YA LUGHA ZA JAMII NCHINI TANZANIA YOHANA P. MSANJILA University of Dar es Salaam, Tanzania

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA,KWA WANANCHI, 30 SEPTEMBA, 2001

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, MHESHIMIWA DKT. PHILIP I. MPANGO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

Kilimo cha kiekolojia cha Wakulima Wadogo Hufanikisha Haki za Mazingira

Shabaha ya Mazungumzo haya

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA III VI

JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

Mwongozo wa Utekelezaji wa Njia za S5-UUE (KAIZEN)-UUU Tanzania

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

UFUATILIAJI WA MIRADI NA TATHMINI

RIPOTI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

Human Rights Are Universal And Yet...

5. Mheshimiwa Spika, Bunge lako Tukufu lilijadili kwa kina Miswada ifuatayo:

Elimu Ina Umuhimu gani katika Jamii? Kuelekea Elimu Sahihi

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA NISHATI NA MADINI

SautiElimu. Sauti Yako Isikike

MWONGOZO WA USHIRIKISHWAJI KATIKA KUPANGA MATUMIZI YA ARDHI WORLD BANK

In the matter of Application by the TANGA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (TANGA UWASA) For a Multi-Year Tariff Adjustment

RIPOTI YA WARSHA KUHUSU HABARI KWA AJILI YA UWAJIBIKAJI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

HUDUMA ZA AFYA KWA WOTE

UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU VIKWAZO VYA KULINDA MAISHA KATIKA USAIDIZI WA KIMATAIFA WA AFYA KWA MSAADA WA KIMATAIFA UNAOFADHILIWA NA MAREKANI

KIMAZINGIRA NA KIJAMII NA MPANGO WA UDHIBITI

Elimukombozi, Lugha na Upashanaji Habari nchini Tanzania, katika Muktadha wa Utandawazi

Uhakika wa Mbegu kwa Uhakika wa Chakula MWONGOZO WA UZALISHAJI WA MBEGU ZA ASILI ZA MAHINDI

Draft 03 MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO MWENGE

Kuwafikia waliotengwa

Ufanisi katika Ufundishaji kwenye Shule za Msingi na Sekondari nchini Tanzania

ONDOA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA AFYA YA WATOTO

Ripoti hii ni kwa heshima ya wale wanaharakati wengi wa Tanzania ambao ndio binafsi wanaopitia hali iliyoangaziwa, na vilevile wale walioyapoteza

Sera ya Faragha. Upeo. Aina za Data na Mbinu za Ukusanyaji

Taarifa Kuhusu Hali ya Uchumi wa Tanzania

Mwongozo kwa familia zinazofanya kazi pamoja kwa maisha endelevu. Nyenzo ya Mafunzo

Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI Nchini Tanzania

TANZANIA TAARIFA YA MWISHO WA UTEKELEZAJI

Mipango ya miradi katika udugu

Kufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007

Transcription:

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU NA WAJIBU WA Serikali za Mitaa

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU NA WAJIBU WA Serikali za Mitaa Kimetayarishwa na Kikundi Kazi cha Serikali za Mitaa cha Policy Forum Kimehaririwa na: Israel Ilunde na Habraham Shamumoyo Mchora Katuni: Regis Maro Kimechapishwa na Policy Forum Toleo la kwanza: Agosti, 2016 ISBN:978-9987-708-23-9 Kimesanifiwa na kupigwa chapa na: Colour Print Tanzania Limited

Yaliyomo VIFUPISHO... 4 DIBAJI... 5 UTANGULIZI... 6 LENGO NAMBA MOJA: Kutokomeza Umasikini wa Aina Zote Kila Mahali... 7 LENGO NAMBA MBILI: Kutokomeza Njaa, Kuwa na Uhakika wa Chakula, Lishe Bora na Kukuza Kilimo Endelevu... 7 LENGO NAMBA TATU: Kuhakikisha Afya Njema na Ustawiwa Watu wa Rika Zote... 8 LENGO NAMBA NNE: Kuhakikisha Elimu Bora, na yenye Usawa kwa Wote na Kutoa Fursa kwa Wote Kujiendeleza... 9 LENGO NAMBA TANO :Kuwepo na Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake na Wasichana Wote...11 LENGO NAMBA SITA: Kuhakikisha Upatikanaji na Usimamizi Endelevu wa Maji na Usafi kwa wote...12 LENGO NAMBA SABA: Nishati Mbadala kwa Gharama Nafuu...13 LENGO NAMBA KUMI NA MOJA:Kuweka Miji na Makazi ya Binadamu kuwa Jumuishi, Salama, Imara na Endelevu...14 LENGO NAMBA KUMI NA TANO: Kulinda Uhai Katika Ardhi na Baionuwai...15 LENGO NAMBA KUMI NA SITA: Kuendeleza Jamii Jumuishi na Yenye Amani kwa Ajili ya Maendeleo Endelevu, Kutoa Haki kwa Wote na Kujenga Taasisi Imara Zenye Kuwajibika katika Nyanja Zote...16 MAPENDEKEZO YETU...16 HITIMISHO...17 REJEA...18 3

Vifupisho PF LGWG AZAKI YPC TNCHF HAFOTA M-WACOD ALAT UKIMWI SDGS FYDP II WHO UNICEF UNFPA Policy Forum Local Government Working Group Asasi za Kiraia Youth Partnership Countrywide Tanzania Network of Community Health Funds Habitat Forum Tanzania Mudugu Women and Community Development Association of Local Authorities of Tanzania Upungufu wa Kinga Mwilini Sustainable Development Goals Five Year Development Plan II World Health Organization United Nations Children s Emergency Fund United Nations Population Fund 4

DIBAJI Ndugu Msomaji, tunafurahi kwa mara nyingine kukuletea kitabu kipya kiitwacho Malengo ya Maendeleo Endelevu na Wajibu wa Serikali za Mitaa ikiwa ni mwendelezo wa mkakati wa Kikundi Kazi cha Serikali za Mitaa cha Jukwaa la Sera (PF-LGWG) kwa kuelimisha wananchi kuhusu sera za kitaifa na kimataifa zinazopaswa kutekelezwa na Serikali za Mitaa ili kuhamasisha ushiriki wa wananchi kwenye masuala ya umma na kukuza uwajibikaji katika jamii. Kitabu hiki kimetafsiri na kuchambua kwa lugha ya Kiswahili malengo 11 kati ya 17 ya Malengo Endelevu ya Dunia yaliyopitishwa na Umoja wa Mataifa Tarehe 25 Septemba, 2015. Madhumuni ya kitabu hiki ni kuongeza uelewa wa wananchi, mamlaka za Serikali za Mitaa, madiwani, wana AZAKI na wadau wengine kuhusu malengo tajwa ili kujua majukumu yao na kuwawezesha kuyatekeleza kwa vitendo kwenye ngazi husika. Aidha inatarajiwa kwamba yoyote atakayesoma kitabu hiki atapata uelewa wa majukumu yake na mamlaka anayoifanyia kazi hivyo kutimiza wajibu wake wa kuwatumikia wananchi kwa ufanisi na uadilifu. Uelewa wa wananchi juu ya tamko hili la kimataifa, utawawezesha kuchukua hatua za makusudi kupitia vikundi na majukwaa yao kutimiza wajibu wao na kufuatilia uwajibikaji wa serikali kwenye mikataba na makubaliano ya kimataifa hususani Malengo ya Maendeleo Endelevu. Uandishi wa kitabu hiki umekuwa ni ule wa kutafsiri kila lengo na kutoa ufafanuzi wa uhusiano wa lengo husika na wajibu au nafasi ya Serikali za Mitaa katika kuchangia kufikiwa kwa lengo husika. Kwa kiasi kikubwa kitabu kinaonesha hali halisi ya sasa katika ngazi za halmashauri zetu na kusisitiza umuhimu wa kila Serikali ya Mtaa kutafsiri lengo husika kwa muktadha wa eneo husika na kujiwekea viashiria vya ufanisi wakiwa wametenga rasilimali za kutosha. Tunatoa shukrani kwa wote walioshiriki kuandaa kitabu hiki kama ifuatavyo: Uongozi wa Jukwaa la Sera (PF) kwa kuwezesha gharama za chapisho, ndugu Israel Ilunde (YPC) kwa kuongoza kikosi kazi kuandaa na hatimaye kuhariri kitabu hiki, wajumbe mahiri kwenye kikosi kazi akiwemo; Kellen Mngoya (HAFOTA), Kidani Magwilla (TNCHF), Regina Katabi (M-WACOD), Aziza Bendera(YPC) na Nuru Ngailo (Sekretarieti ya PF) kwa kazi ya uandishi.tunamshukuru Ndugu Habraham Shamumoyo (Sekretarieti ya ALAT) kwa kushiriki kuhariri kitabu hiki. Tunawashukuru wafanyakazi wa Policy Forum, Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) na wadau wengine kwa kuratibu na kuhakikisha kitabu kinakamilika na kuwafikia walengwa. Israel Ilunde Mwenyekiti PF -LGWG 5

UTANGULIZI Wanazuoni na wachambuzi wengi wanakiri kwamba Malengo ya Milenia yalikuwa yameandaliwa bila ushiriki mpana wa wadau na kuwaacha wengi nyuma na yalikuwa hayatekelezeki kirahisi kwa kukosa malengo mahsusi na viashiria vya mafanikio. Kutokana na uzoefu huo uandalizi wa Malengo ya Maendeleo Endelevu yaliyopitishwa na Umoja wa Mataifa Septemba, 2015 ulizingatia umuhimu wa kuwashirikisha wadau mbali mbali na kusisitiza haja kuweka mkakati wa utekelezaji na raslimali za kutosha na serikali kuu na Serikali za Mitaa duniani kote. Malengo haya ambayo kwa idadi ni 17, yameshirikisha watu kutoka nchi zilizoendelea na zinazoendelea na ndipo makubaliano yakawekwa na viongozi kutia saini. Kwa kuwa hadi sasa takribani watu milioni 8 bado wanaishi kwenye dimbwi la umasikini; lishe duni, njaa, kutegemea kilimo cha mvua huku wakitegemewa kuilisha dunia kwa asilimia 80. Kwa hali hiyo, upo umuhimu wa kuwekeza kwa wakulima wadogo wadogo hususani vijana na wanawake ili kuhakikisha usalama wa chakula na ajira kwa watu masikini. Jambo la kusikitisha ni kwamba watoto wa kike na wa kiume wapatao milioni 6 hufa kila mwaka kabla ya miaka mitano wakati mazingira yakidorora na nishati kutia shaka. Hizi ndizo changamoto za dhahiri ambazo Malengo ya Maendeleo Endelevu yanajaribu kujielekeza ili kuwa na dunia iliyosawa na haki. Hakuna atakayeachwa nyuma ni kauli mbiu ya wazi inayoweka msingi wa Malengo ya Maendeleo Endelevu ikidhamiria kuleta matokeo chanya kwa watu wote. Kitabu hiki kilichopo mikononi mwako kimeandikwa kwa lugha rahisi ili upate kuyaelewa maudhui ya baadhi ya malengo hayo. Hapa tumefafanua malengo kumi na moja kati ya kumi na saba ambayo yanagusa shughuli za Serikali za Mitaa moja kwa moja na kazi za Policy Forum. Malengo yenyewe ni; Lengo la kwanza, la pili, la tatu, la nne, la tano, la sita, la saba, la kumi na moja, la kumi na tano, la kumi na sita na la kumi na saba. Fuatana nasi uelimike na uvumbue fursa za kijamii, kiuchumi na kisiasa kwa maendeleo yako na ustawi wa jamii. 6

LENGO NAMBA MOJA - Kutokomeza Umasikini wa Aina Zote Kila Mahali Lengo hili linahusu kuongeza kipato cha watu waishio kwenye umaskini na kuhakikisha wanapata huduma za msingi na kumlinda kila mtu kuepukana na majanga. Hivyo basi, Serikali za Mitaa zina jukumu la kuhakikisha kwamba, ifikapo 2030:- Zinatokomeza umasikini uliokithiri kwa watu wote, wanaoishi kwa kipato chini ya dola za kimarekani 1.25 kwa siku. Kiasi cha watu wanaume, wanawake, na watoto, wa kila umri wanaoishi katika hali ya umasikini kinapungua japo kwa nusu. Watu wote, wanawake na wanaume, hasa maskini, wana haki sawa za kiuchumi na upatikanaji wa huduma za msingi, umiliki wa ardhi na mali nyinginezo,mirathi, maliasili, teknolojia inayofaa, huduma za kifedha na mikopo. Zinawatambua wananchi wanaoishi katika hali ya umasikini, ili kuelekeza rasilimali na huduma kwa wananchi hao kwa ajili ya kuwasaidia kuepuka hali hiyo. Zinajenga uwezo wa watu maskini ili kuwaimarisha na kurekebisha hali yao ya umaskini ili kuwaondoa katika mazingira yaliyo duni na majanga. LENGO NAMBA MBILI - Kutokomeza Njaa, Kuwa na Uhakika wa Chakula, Lishe Bora na Kukuza Kilimo Endelevu Lengo hili linabainisha kwamba njaa ni tatizo linalotakiwa kuondolewa kwa kushughulikiwa kikamilifu ili kuhakikisha kila kaya ama binadamu anafurahia maisha kwa kuwa na uhakika wa kupata chakula cha kutosha, salama na chenye virutubishi sahihi hasa kwa maskini, watu waishio kwenye mazingira hatarishi, watoto wachanga, wazee, wasichana, mama wajawazito na wanaonyonyesha. Kilimo ni lazima kiboreshwe, kikuzwe na kiwe endelevu ili ifikapo 2030 tatizo la njaa liwe limekwisha. Hivyo basi Serikali za Mitaa zinatakiwa kufanya yafuatayo;- 7

Kuongeza uzalishaji katika kilimo na kipato mara dufu kwa wazalishaji wadogo wa chakula hasa wanawake, wafugaji, wavuvi, wakulima ikiwemo utafutaji na usawa katika kupata ardhi yenye miliki salama. Kuongeza ajira kwenye kilimo,upatikanaji wa rasilimali na stadi mbalimbali katika kukuza kilimo na uzalishaji,huduma za kifedha/mitaji,masoko,thamani ya mazao ghafi na kuwa na mfumo endelevu wa uzalishaji wa mazao ya chakula. Kuimarisha ardhi na kurutubisha udongo, kuongeza uwezo wa watu kukabili mabadiliko ya tabia nchi na majanga mbalimbali kama mafuriko,ukame, ndege waharibifu na kadhalika. LENGO NAMBA TATU - Kuhakikisha Afya Njema na Ustawiwa Watu wa Rika Zote Lengo hili linahusu kuwezesha watu kuishi maisha yenye afya bora na hivyo kuongeza umri wa kuishi kwa watu wa rika zote ifikapo 2030. Hivyo basi Serikali za Mitaa zinatakiwa kufanya yafuatayo;- Kupunguza vifo vya mama wajawazito chini ya 398 kati ya 100,000 kila mwaka. Kupunguza vifo vya watoto wanaozaliwa na walio chini ya miaka 5. Vifo 51 kwa vizazi hai 1000 kwa watoto wa kiume na vifo 41 kwa vizazi hai 1000 kwa watoto wa kike. Kutokomeza maambukizi ya UKIMWI, kifua kikuu, na magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza kama vile malaria, kisukari, shinikizo la damu, vikope, nimonia, na magonjwa yatokanayo na maji kama; kuhara damu, kichocho, kipindupindu, homa ya matumbo pia magonjwa mengine yanayoambukiza kama magonjwa ya zinaa. Kupunguza vifo na ulemavu unaosababishwa na ajali za barabarani ifikapo 2020. 8

Kuweka katika mikakati mbalimbali taarifa sahihi, elimu na stadi za huduma ya afya ya uzazi kwa wananchi kwa ajili ya utekelezaji. Kupunguza magonjwa na vifo vitokanavyo na uchafuzi wa mazingira yanayotokana na madawa yenye sumu yanayoingia kwenye hewa safi,maji na udongo vitu ambavyo vinatumiwa na binadamu kwa ajili ya ustawi wa maisha yao. Kwa ujumla lengo hili linahitaji uwepo wa mikakati endelevu,programu maalum, rasilimali na usimamizi makini kutoka ngazi ya Taifa kwa kushirikiana na Serikali za Mitaa ili liweze kutimia na kuleta matokeo yanayotarajiwa ifikapo 2030. LENGO NAMBA NNE - Kuhakikisha Elimu Bora, Yenye Usawa na Kutoa Fursa kwa Wote Kujiendeleza Lengo hili linasisitiza kuwezesha kila mtu kusoma, kujifunza na kuhakikisha kwamba binadamu wote wanafikia vipawa vyao kikamilifu. Vilevile, Serikali za Mitaa zina nafasi ya kuhamasisha elimu ya ufundi stadi katika mikakati ya maendeleo ya kiuchumi na kuhakikisha mafunzo yanaleta tija katika soko la ajira. 9

Hali kadhalika, Serikali za Mitaa zifanye utambuzi ili kuyafikia makundi yalio pembezoni na yaliyo katika mazingira hatarishi ili kuhakikisha wanapewa nafasi ya kupata elimu na mafunzo yanayokidhi mahitaji yao. Kwa sasa, changamoto zilizopo kama vile upungufu wa walimu, vifaa vya kufundishia na kujifunzia yapatiwe suluhisho la kudumu. Hivyo basi, Serikali za Mitaa zina jukumu la kutekeleza yafuatayo ifikapo 2030; Kuhakikisha kuwa wasichana na wavulana wote wanahitimu elimu ya msingi na sekondari; bure, yenye ubora na usawa unaoleta tija. Kuongeza mahudhurio ya wanafunzi shuleni. Kuhakikisha kuwa wasichana na wavulana wote wana fursa sawa ya kupata elimu bora ya awali ili iwaandae kwa elimu ya msingi. Kuhakikisha fursa sawa kwa wanawake na wanaume ili wapate elimu ya juu, mafunzo na ufundi stadi kwa gharama nafuu. Kuongeza idadi ya vijana na watu wazima wenye ujuzi pamoja na ufundi stadi kwa ajili ya ajira, kazi zenye heshima na ujasiriamali. Kuondoa matabaka ya kijinsia ndani ya elimu na kuhakikisha upatikanaji wa elimu katika ngazi zote ikiwemo mafunzo ya ufundi stadi kwa ajili ya watu wanaoishi katika maeneo hatarishi hususani, wenye ulemavu na watoto. 10

LENGO NAMBA TANO - Kuwepo na Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake na Wasichana Wote Lengo hili linakusudia kutokomeza ukatili na ubaguzi dhidi ya wanawake na wasichana na kuhakikisha wanapata fursa sawa katika umiliki wa rasilimali na nyanja zote za kimaisha. Kwa kuwa ndio kundi lililonyimwa fursa kwa muda mrefu. Pamoja na mambo mengine ili kufanikisha lengo hili ifikapo 2030 Serikali za Mitaa zinatakiwa kuondoa aina zote za ukatili na ubaguzi dhidi ya wanawake na wasichana, pamoja na;- Kuwa mfano wa kuigwa katika kuleta usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake kupata huduma za kijamii bila kubaguliwa. Kutoa kipaumbele; kutambua na kutatua matendo hatarishi na ukatili unaowakabili wanawake, kwa kutoa huduma stahiki kwa walioathirika na ukatili huo, na kutoa fursa za uongozi, umiliki ardhi utakaopelekea kuondoa mawazo mgando dhidi ya usawa wa kijinsia. 11

Kujumuisha masuala ya kijinsia katika shughuli za Serikali za Mitaa ili kukabiliana na vikwazo vinavyowakabili wanawake. Kuimarisha na kusimamia sheria na sera stahiki zinazoinua usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake na wasichana katika nyanja zote, kuondoa matendo hatarishi kama ndoa za utotoni na ukeketaji. LENGO NAMBA SITA Kuhakikisha Upatikanaji na Usimamizi Endelevu wa Maji na Usafi kwa Wote. Lengo hili linadhamiria upatikanaji wa maji safi na salama kwa ujumla ifikapo 2030. Changamoto iliyopo mijini ni kukosekana kwa huduma za maji safi kwenye makazi holela ama kwa gharama kubwa na kukosekana kwa udhibiti wa gharama za maji kutoka kwa wauzaji binafsi. Kwa maeneo ya vijijini hata kama maji yanapatikana bure inabidi utembee mwendo mrefu ili kuyapata yaweza kuwa sio salama. 12

Serikali za Mitaa zinapaswa kutekeleza yafuatayo;- Kuongeza upatikanaji wa maji safi ya kunywa na yenye gharama nafuu kwa wote. Kuhakikisha uwepo wa usafi kwa makundi ya wanawake, wasichana na wale waishio katika mazingira hatarishi. Kupunguza uchafuzi wa mazingira, kemikali zenye sumu na upotevu wa maji na kuboresha maji taka yatumike tena. Kuwezesha ushiriki na ushirikishwaji wa jamii katika usimamizi wa maji na usafi. Kuongeza ufanisi katika upatikanaji wa maji. Kulinda vyanzo vya maji na kuhifadhi maji kwa kuhusianisha ulinzi na uhifadhi wa milima, misitu, ardhi oevu, mito, maziwa na viumbe waishio kwenye maji ifikapo 2020. LENGO NAMBA SABA - Nishati Mbadala kwa Gharama Nafuu Lengo hili linadhamiria kuhakikisha kila mtu ana uwezo wa kufikiwa/ kupata nishati mbadala kwa gharama nafuu. Baada ya uvumbuzi wa kiasi kikubwa cha gesi nchini, Tanzania ipo katika nafasi nzuri ya kufikia lengo hili. Serikali za Mitaa zinapaswa kujumuisha katika mikakati yao matumizi ya nishati mbadala. Na pia, zina nafasi nzuri kutambua mapungufu katika upatikanaji wa nishati mbadala kwa makundi yaliyo pembezoni na mazingira hatarishi. Pia, Serikali za Mitaa zina jukumu la kuchangia utumiaji mzuri wa nishati hiyo kwa kuwekeza katika ujenzi wa majengo yatumiayo nishati mbadala na vyanzo vya nishati uoto kwa majengo ya umma. Kupitia jitihada tajwa hapo juu, Serikali za Mitaa zitapunguza gharama za matumizi ya nishati itokanayo na misitu. 13

LENGO NAMBA KUMI NA MOJA - Kuweka Miji na Makazi ya Binadamu Kuwa Jumuishi, Salama, Imara na Endelevu. Lengo hili linawataka mameya wa miji na Serikali za Majiji kutekeleza majukumu yao katika kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu; ikiwa ni pamoja na kuleta maendeleo endelevu kuanzia ngazi ya Mtaa hadi Jiji/Miji kwa kuhamasisha ushiriki wa wananchi. Linasisitiza pia, Serikali kuzuia ujenzi holela na kuweka mipango miji na utaratibu wa upatikanaji wa soko la viwanja na nyumba hasa kwa watu wa kipato cha chini ili makazi yao yawe na huduma zote muhimu kwa binadamu, mfumo wa usafiri kwa umma wenye kuzingatia mahitaji maalum kwa watu wenye ulemavu, wazee na watoto. Vilevile kuzuia ujenzi wa makazi kwenye maeneo hatarishi na yale ambayo tayari watu wanaishi, wahusika wapatiwe mahali salama kwa ajili ya makazi. Kuweka mipango mikakati ya kuendeleza huduma za msingi vijijini ili kuwepo uwiano kati ya Miji na Vijiji. 14

Serikali za Mitaa kwa kushirikiana na Serikali Kuu zina wajibu wa kutambua urithi wa asili na utamaduni na kuhifadhi kwa ajili ya vizazi vijavyo mfano; mapango,wanyama,majengo ya kale nk. LENGO NAMBA KUMI NA TANO - Kulinda Uhai Katika Ardhi na Baionuwai Lengo hili linakusudia kulinda maliasili na wanyama pori. Serikali za Mitaa kama watoa huduma wana nafasi kubwa ya kubadili tabia za wanajamii kwa kuwahamasisha kushiriki kulinda,na kusimamia maliasili na makazi. Pia, katika mipango miji na mkakati wa maendeleo Serikali za Mitaa zinajukumu la kuhakikisha ulinzi wa maliasili. LENGO NAMBA KUMI NA SITA - Kuendeleza Jamii Jumuishi na Yenye Amani kwa Ajili ya Maendeleo Endelevu, Kutoa Haki kwa Wote na Kujenga Taasisi Imara Zenye Kuwajibika katika Nyanja Zote Lengo hili linadhamiria kudumisha usalama wa raia wake na kuhakikisha Serikali inafanya kazi kwa ufanisi na kwa haki. Kupitia lengo hili Serikali za Mitaa zinajukumu la kuwa na ufanisi zaidi na kuwajibika kwa wananchi wake kwa kupambana na rushwa na kuongeza uhuru wa wananchi kupata taarifa. 15

Pia, kuongeza jitihada za kufanya maamuzi shirikishi ikiwemo ushiriki wa wananchi kwenye mipango na bajeti ili waweze kuwajibika zaidi. Pamoja na mambo mengine, Serikali za Mitaa zinatakiwa; kupunguza aina zote za ukatili na vifo kila sehemu, kujenga taasisi zenye uwazi, ufanisi na za kuwajibika katika nyanja zote. LENGO NAMBA KUMI NA SABA Kuendeleza Ubia katika Ngazi Zote. Ngazi ya Kimataifa, Kitaifa na Ngazi ya Serikali za Mitaa Lengo hili ni muhimu sana katika kungenga ushirikiano wa Serikali za Mitaa kimataifa, kikanda na kitaifa kwa lengo la kupata rasilimali, teknolojia na maarifa ya kutekeleza malengo yote endelevu. Ugatuzi wa madaraka na utoaji wa fursa za ushirikiano wa kimaendeleo ngazi ya Serikali za Mitaa ni jambo la muhimu na la msingi sana kwa ajili ya kuharakisha mafanikio ya Serikali za Mitaa na kufanikisha kutimia kwa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) ifikapo 2030 MAPENDEKEZO YETU Pamoja na kwamba Malengo ya Maendeleo Endelevu yamezingatiwa katika mpango wa maendeleo wa miaka mitano 16

(FYDP II), Serikali za Mitaa zijumuishe maudhui ya SDGs kwenye mipango yao. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania igatue madaraka kwa Serikali za Mitaa ipasavyo ili kuzipa uhuru Serikali za Mitaa kufanya maamuzi na kujipangia mipango ya maendeleo wenyewe na kunufaika na makusanyo ya mapato. Serikali za Mitaa zipewe mamlaka ya kuajiri ili kuimarisha uwajibikaji katika ngazi husika. Serikali za Mitaa zipewe vyanzo vya mapato vyenye uhakika na ruzuku ya kutosha na kwa wakati kutoka hazina kuu. HITIMISHO Kitabu hiki kimetafsiri na kuchambua kwa lugha ya Kiswahili malengo 11 kati ya 17 ya Malengo Endelevu ya Dunia yaliyopitishwa na Umoja wa Mataifa tarehe 25 Septemba, 2015. Bila shaka ndugu msomaji utakuwa umeongeza uelewa wako na kujikumbusha au kutambua majukumu yako kama mwananchi, au kama Mheshimiwa Diwani au mtumishi wa Serikali ya Mtaa au kama mmoja wa wana AZAKI na pengine ni mdau wa maendeleo kutoka sekta binafsi au jamii ya kimatafa. Bila shaka sasa utakubaliana nasi kuwa uelewa wa wananchi juu ya tamko hili la kimataifa, utawawezesha wananchi kuchukua hatua za makusudi kupitia vikundi na majukwaa yao kutimiza wajibu wao wa kufuatilia uwajibikaji wa Serikali kwenye mikataba na makubaliano ya kimataifa hususani Malengo haya ya Maendeleo Endelevu. Kwa kuwa uandishi wa kitabu hiki umekuwa ni ule wa kutafsiri kila lengo na kutoa ufafanuzi wa uhusiano wa lengo husika na wajibu au nafasi ya Serikali za Mitaa katika kuchangia kufikiwa kwa lengo husika, sisi tunaamini kwamba kila Serikali ya Mtaa itachukua hatua ya kujielekeza kwenye kila lengo husika kwa kuzingatia mazingira na muktadha wa eneo husika na kujiwekea viashiria vya ufanisi wakiwa wametenga rasilimali za kutosha ili kufanikisha kila lengo katika ngazi yao ikiwa ni sehemu ya juhudi za kufanikisha malengo yote 17 kitaifa. Malengo yote yanawezekana - chukua hatua na timiza wajibu wako sasa. 17

REJEA WHO, UNICEF, UNFPA, World Bank and the United Nations Population Division, Trend in Maternal Mortality: 1990 to 2015. Geneva, World Health Organization,2015), Mortality and Health - National bureau of statistics and Ministry of finance and office of chief government staticians, Ministry of State, President s office, State house and good governance 2015), Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, (Toleo la mwaka 2005), Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya), Sura ya 287 (Toleo la mwaka 2014), Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji), Sura ya 288 (Toleo la mwaka 2014). 18

19

Policy Forum S.L.P 38486, Dar es Salaam Simu: +255 22 2780200/255 782317434 Baruapepe: info@policyforum.or.tz Tovuti: www.policyforum.or.tz