ORODHA YA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI SPIKA MHE. PANDU AMEIR KIFICHO. Rais.

Similar documents
Information for assessors (do not distribute this page to participants):

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

ORODHA YA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI SPIKA MHE. PANDU AMEIR KIFICHO. Rais.

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

ORODHA YA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI SPIKA MHE. PANDU AMEIR KIFICHO. Shughuli za Serikali/Jimbo la Mwanakwerekwe.

MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA PRO-ROUTES. Ombi kwa ajili ya fedha za umma wa mradi wa ziada

Human Rights Are Universal And Yet...

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU

In the matter of an Application by the KIGOMA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (KUWASA) For a Tariff and Charges Adjustment

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

April 14, 2016 COUNTY ASSEMBLY DEBATES 52

ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA UCHUMI WA ZANZIBAR

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA SABA. Kikao cha Thelathini na Tisa Tarehe 1 Juni, (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A

Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame M. Mbarawa (Mb.); Waheshimiwa Mawaziri na Wabunge wote mliohudhuria;

JAMHURI YA KENYA. Mkakati wa Ushirikiano MUKHTASARI FY Public Disclosure Authorized. Public Disclosure Authorized

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA NNE. Kikao cha Nane Tarehe 23 Juni, 2006

Dodoma ambako kikao cha Bunge kinaendelea kuja kushiriki japo sehemu ya uzinduzi wa mkutano.

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA,KWA WANANCHI, 30 SEPTEMBA, 2001

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO

3 FEBRUARI, 2015 BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA NANE. Kikao cha Saba - Tarehe 3 Februari, 2015

Miradi na jamii. 3.1 Utangulizi

MAADHIMISHO YA MIAKA 15 YA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

13 APRILI, 2012 BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA SABA. Kikao cha Nne Tarehe 13 Aprili, (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA SABA. Kikao cha Saba Tarehe 13 Aprili, (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA PILI. Kikao cha Nne - Tarehe 29 Januari, (Kikao Kilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

BUNGE LA TANZANIA MKUTANO WA NANE. Kikao cha Ishirini na Nane Tarehe 16 Julai, (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA MOJA. Kikao cha Hamsini na Tatu Tarehe 19 Juni, (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi)

TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM)

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA. Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo. TOLEO Na.

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

TANZANIA MARKETS PAN Sera zinazoboresha masoko

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA SITA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TISA. Kikao cha Pili - Tarehe 14 Aprili, 2010

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA KUMI NA MBILI TAREHE 22 JUNI, 2005

5. Mheshimiwa Spika, Bunge lako Tukufu lilijadili kwa kina Miswada ifuatayo:

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA SITA

UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA)

JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees

Pronunciation: Mä-hret Zäläke Ndal-ka-tscho Molla Mare Gebre-gzabiär 1/12

JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1

NGUZO KUMI ZA KILIMO KWANZA

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA MBILI. Kikao cha Tatu Tarehe 6 Septemba, (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A

2 FEBRUARI, 2015 BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA NANE. Kikao cha Sita - Tarehe 2 Februari, 2015

RIPOTI YA WARSHA KUHUSU HABARI KWA AJILI YA UWAJIBIKAJI

Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi

Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara)

In the matter of Application by the TANGA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (TANGA UWASA) For a Multi-Year Tariff Adjustment

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig

Programu ya Uendelezaji Mifumo ya Maji Vijijini (PUMMV) katika Tanzania. Modeli wa Ukodishaji Mradi

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara

HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE

Nilikua na Ndoto ya Kumaliza Shule Changamoto za Elimu ya Sekondari Tanzania

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level

MTIHANI WA MWIGO WILAYA YA BUTERE MUMIAS-2007 Hati ya kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya

TIST HABARI MOTO MOTO MAANDALIZI YA MWAKA 2000 Y2K PREPARATIONS SASA NI WAKATI WA KUANZA KUPANDA MBEGU ZAKO

United Pentecostal Church June 2017

Mhashamu Askofu Jude Thaddaeus Ruwa ichi, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania; Mwadhama Policarp Kardinali Pengo,

KUSHUKA KWA HADHI YA LUGHA ZA JAMII NCHINI TANZANIA YOHANA P. MSANJILA University of Dar es Salaam, Tanzania

Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA 2006/07

2

TIST HABARI MOTO MOTO

Kufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC)

March 14, 2018 PARLIAMENTARY DEBATES 1 NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL REPORT. Wednesday, 14 th March The House met at 9.30 a.m.

RIPOTI YA KAMATI TEULE YA KUCHUNGUZA UPOTEVU WA NYARAKA ULIOTOKEA KATIKA TAASISI YA NYARAKA NA KUMBUKUMBU ZA TAIFA ZANZIBAR.

28 JUNI, 2018 MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA MOJA. Kikao cha Hamsini na Tisa Tarehe 28 Juni, (Mkutano Ulianza Saa 3.

Kiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika

SautiElimu. Sauti Yako Isikike

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU

KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )

HAKI NA TARATIBU ZA AJIRA, KAZI NA HIFADHI YA JAMII

MWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI

Dibaji ya Mwenyekiti wa Kamati ya Pamoja ya Uongozi

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA MHESHIMIWA DKT

Kubadili Sheria Za Mbegu Na Ulinzi Wa Aina Za Mbegu Na Mimea Nchini Tanzania

Uzio wa pilipili unazuia tembo kuvamia mazao shambani! Jinsi ya kujenga na kudumisha uzio wa pilipili Tanzania

3. Mheshimiwa Spika, 4. Mheshimiwa Spika,

usudi la Maisha Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na kupishana usiku na mchana, kuna kweli ishara kwa wenye akili, ambaye mkumbuke-

KITEGO CHA MAREKEBISHO NA HAKI ZA MTOTO

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )

Mwongozo wa Kutathimini mifumo ya Ugawanaji wa faida na Mapato Katika Miradi ya Jamii ya MKUHUMI

Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali ya Madini Ukanda

MAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II

Ufunguo wa Kutaalamika Haraka

Azimio lililopitishwa na Mkutano Mkuu tarehe 18 Desemba 2013 [juu ya taarifa ya Kamati ya Tatu (A/68/456/Add.2)]

Elimukombozi, Lugha na Upashanaji Habari nchini Tanzania, katika Muktadha wa Utandawazi

Transcription:

ORODHA YA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI SPIKA MHE. PANDU AMEIR KIFICHO 1.Mhe. Kamal Basha Pandu 2.Mhe. Ali Mzee Ali 3.Mhe. Shamsi Vuai Nahodha Naibu Spika/Jimbo la Rahaleo. Mwenyekiti wa Baraza/Uteuzi wa Rais. MBM/Waziri Kiongozi/ Kiongozi wa Shughuli za Serikali/Jimbo la Mwanakwerekwe. 4.Mhe. Ali Juma Shamuhuna MBM/Naibu Waziri Kiongozi/Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo/ Jimbo la Donge. 5.Mhe. Abubakar Khamis Bakary Kiongozi wa Upinzani/ Waziri Kivuli Afisi ya Waziri Kiongozi/Jimbo la Mgogoni. 6.Mhe. Haji Omar Kheri Mnadhimu wa Upande wa Serikali/Jimbo la Tumbatu. 7.Mhe. Soud Yussuf Mgeni Mnadhimu wa Upande wa Upinzani/Jimbo la Wawi. 8.Mhe. Dr. Mwinyihaji Makame Mwadini 9.Mhe. Hamza Hassan Juma MBM/Waziri wa Nchi (AR) na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Anaeshughulikia Masuala ya Fedha na Uchumi/ Jimbo la Dimani. MBM/Waziri wa Nchi, Afisi ya Waziri Kiongozi/ Jimbo la Kwamtipura. 10.Mhe. Ramadhan Abdulla Shaaban MBM/Waziri wa Nchi (AR) Katiba na Utawala Bora/Uteuzi wa Rais. 1

11.Mhe. Suleiman Othman Nyanga MBM/Waziri wa Nchi (AR) Tawala za Mikoa na Vikosi Vya S.M.Z./Jimbo la Jang ombe. 12.Mhe. Br.Gen. Adam C. Mwakanjuki MBM/Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi/Uteuzi wa Rais. 13. Mhe. Machano Othman Said Waziri wa Nchi, (AR) Mawasiliano na Uchukuzi./Jimbo la Chumbuni. 14.Mhe. Samia Suluhu Hassan 15.Mhe. Burhan Saadat Haji 16.Mhe. Asha Abdalla Juma MBM/Waziri wa Utalii/Biashara na Uwekezaji/Nafasi za Wanawake. MBM/Waziri wa Kilimo, Mifugo na Mazingira/ Jimbo la Kikwajuni. MBM/Waziri wa Kazi Maendeleo ya Vijana,Wanawake na Watoto/ Uteuzi wa Rais. 17.Mhe. Haroun Ali Suleiman MBM/Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali/Jimbo la Makunduchi. 18.Mhe. Sultan Moh d Mugheiry 19.Mhe. Mansoor Yussuf Himid 20.Mhe. Zainab Omar Moh d 21.Mhe. Idi Pandu Hassan MBM/Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii/ Uteuzi wa Rais. MBM/Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi/Jimbo la Kiembesamaki. MBM/Waziri wa Nchi (AR) Kazi Maalum/ Nafasi za Wanawake. Mwanasheria Mkuu wa Serikali. 22. Mhe. Mahmoud Thabit Kombo Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo/Jimbo la Mpendae. 2

23. Mhe. Mzee Ali Ussi Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi/Jimbo la Chaani. 24. Mhe. Khatib Suleiman Bakari Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Mazingira/Jimbo la Bububu. 25.Mhe. Khamis Jabir Makame Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali/Jimbo la Mtoni. 26.Mhe. Shawana Bukheti Hassan 27.Mhe. Tafana Kassim Mzee 28.Mhe. Omar Ali Shehe 29.Mhe. Zakiya Omar Juma 30.Mhe. Abass Juma Muhunzi 31.Mhe. Abdulla Juma Abdulla 32.Mhe. Haji Faki Shaali 33.Mhe. Mtumwa Kheir Mbarak Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii/Jimbo la Dole. Naibu Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi/Jimbo la Uzini. Waziri Kivuli Wizara ya Nchi, Afisi ya Waziri Kiongozi/Jimbo la Chake-Chake. Waziri Kivuli -Wizara ya Nchi (AR) na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi/Nafasi za Wanawake. Waziri Kivuli Wizara ya Nchi (AR) na MBLM Fedha na Uchumi/Jimbo la Chambani. Waziri Kivuli Wizara ya Nchi (AR) Tawala za Mikoa na Vikosi Vya SMZ/Jimbo la Chonga. Waziri Kivuli Wizara ya Nchi (AR) Katiba na Utawala Bora/Jimbo la Mkanyageni. Waziri Kivuli Wizara ya Nchi (AR) Kazi Maalum/Nafasi za Wanawake. 3

34.Mhe. Hamad Masoud Hamad Waziri Kivuli Wizara ya Maji,Ujenzi, Nishati na Ardhi/Jimbo la Ole. 35.Mhe. Said Ali Mbarouk Waziri Kivuli Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi/Jimbo la Gando. 36.Mhe. Rashid Seif Suleiman 37.Mhe. Mohamed Ali Salim Waziri Kivuli Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii/Jimbo la Ziwani. Waziri Kivuli Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali/Jimbo la Mkoani. 38.Mhe. Asaa Othman Hamad Waziri Kivuli Wizara ya Kilimo, Mifugo na Mazingira/Jimbo la Wete. 39.Mhe. Aziza Nabahan Suleiman Waziri Kivuli Wizara ya Kazi, Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto/Nafasi za Wanawake. 40.Mhe. Najma Khalfan Juma Waziri Kivuli Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo/Nafasi za Wanawake. 41.Mhe. Muhyddin Moh d Muhyddin Waziri Kivuli Wizara ya Utalii, Biashara na Uwekezaji/Jimbo la Mtambile. 42.Mhe. Abdulla Mwinyi Khamis Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja. 43.Mhe. Ali Abdalla Ali 44.Mhe. Ali Denge Makame 45.Mhe. Ali Haji Ali 46.Mhe. Ali Moh d Bakari Jimbo la Mfenesini. Jimbo la Amani. Jimbo la Mkwajuni. Jimbo la Tumbe. 4

47.Mhe. Ali Suleiman Ali 48.Mhe. Ame Mati Wadi 49.Mhe. Ame Ussi Juma 50.Mhe. Amina Iddi Mabrouk 51.Mhe. Anaclet Thobias Makungila 52.Mhe. Ashura Abeid Faraji 53.Mhe. Bihindi Hamad Khamis 54.Mhe. Dadi Faki Dadi 55.Mhe. Fatma Abdalla Tamim 56.Mhe. Fatma Abdulhabib Fereji 57.Mhe. Haji Mkema Haji 58.Mhe. Hasnuu Moh d Haji 59.Mhe. Hija Hassan Hija Jimbo la Kwahani. Jimbo la Matemwe. Jimbo la Nungwi. Nafasi za Wanawake. Jimbo la Fuoni. Nafasi za Wanawake. Nafasi za Wanawake. Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini, Pemba. Nafasi za Wanawake. Jimbo la Mji Mkongwe. Jimbo la Koani. Uteuzi wa Rais. Jimbo la Kiwani. 60.Mhe. Major Juma Kassim Tindwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini, Pemba. 61.Mhe. Makame Mshimba Mbarouk 62.Mhe. Mkongwe Nassor Juma 63.Mhe. Moh d Kombo Mkanga Jimbo la Kitope. Nafasi za Wanawake. Jimbo la Chwaka. 64.Mhe. Mustafa Moh d Ibrahim Mkuu wa Mkoa wa Kusini, Unguja. 65.Mhe. Mwanajuma Faki Mdachi 66.Mhe. Omar Ali Jadi Nafasi za Wanawake. Jimbo la Kojani. 5

67.Mhe. Pembe Juma Khamis 68.Mhe. Ramadhan Nyonje Pandu 69.Mhe. Raya Suleiman Hamad 70.Mhe. Said Khelef Ali 71.Mhe. Salim Abdulla Hamad 72.Mhe. Salmin Awadh Salmin 73.Mhe. Subeit Khamis Faki 74.Mhe. Suleiman Hemed Khamis 75.Mhe. Thuwaybah Edington Kissasi 76.Mhe. Zahra Ali Hamad Ndg. Ibrahim Mzee Ibrahim Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini, Unguja. Jimbo la Muyuni. Nafasi za Wanawake. Jimbo la Bumbwini. Jimbo la Mtambwe. Jimbo la Magomeni. Jimbo la Micheweni. Jimbo la Konde. Nafasi za Wanawake. Nafasi za Wanawake. Katibu wa Baraza la Wawakilishi 6

Kikao cha Nane Tarehe 3 April, 2009 (Kikao kilianza saa 3:00 asubuhi) DUA Mhe. Spika (Pandu Ameir Kificho) alisoma dua HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Mhe. Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi: Mhe. Spika, kwa ruhusa yako naomba kuwasilisha hati mezani inayohusu taarifa ya mapendekezo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuhusu ripoti ya Mshauri Mwelekezi juu ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia kwa Baraza hili tukufu. MASWALI NA MAJIBU Nam. 80 Bima ya Maisha kwa Wafanyakazi wa Serikali Mhe. Ame Ussi Juma Aliuliza:- Ili kumnusuru mfanyakazi na matatizo mbali mbali, ipo haja ya kuandaa utaratibu wa kuwakatia Bima ya Maisha wafanyakazi wa serikali, jambo ambalo litasaidia kujenga mapenzi ya kazi zao. (a) (b) Je, Mhe. Waziri wizara yako ina utaratibu gani wa kuwakatia Bima ya Maisha wafanyakazi wako? Kwa kuwa serikali inawathamini wafanyakazi wake, na kwa kuwa haijaandaa utaratibu wa kuwanusuru na maafa ya maisha yao kwa kuwakatia Bima ya Maisha, Je, wizara haioni haja ya kuanzisha utaratibu huu? Mhe. Waziri wa Nchi (AR) na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Anayeshughulikia Masuala ya Fedha na Uchumi Alijibu:- Mhe. Spika kwa idhini yako ninaomba kumjibu Mhe. Mwakilishi swali lake Nam. 80 lenye vifungu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mhe. Spika, Bima ya Maisha ni miongoni mwa mambo ambayo yamo ndani ya utaratibu wa kuendeleza hifadhi ya jamii. Hifadhi ya Jamii kwa mujibu wa tafsiri ya Shirika la 7

(b) Kazi Duniani (ILO) ni mpango wenye kusaidia jamii inapokabiliwa na matatizo ya kijamii na kiuchumi ambayo pamoja na mambo mengine husababishwa kwa kusita au kwa kupungua kwa kipato kwa sababu ya maradhi, kutokuwa na ajira, kupata ulemavu, uzee na hata mauti. Mhe. Spika, nakubaliana na maelezo ya Mhe. Mjumbe kuhusu umuhimu wa wafanyakazi kuwa na kinga ya maisha. Katika kulitekeleza suala hilo, ndio Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikaanzisha Mfuko wa Hifadhi ya Jamii chini ya Sheria Nam. 2 ya mwaka 2005 kama mpango wa lazima mandatory scheme kwa wafanyakazi wote. Hatua hii ya serikali imelenga kwa wafanyakazi kutoa kinga katika baadhi ya mambo niliyoyataja hapo juu. Pia Sheria Nam. 5 ya mwaka 2005 imeruhusu fidia kutolewa kwa wale watakaopata ajali kazini. Hata hivyo, serikali haikatazi kwa wafanyakazi mmoja mmoja na wananchi kwa ujumla kuwa na Bima za Maisha zinazotolewa na Mashirika ya Bima tuliyonayo nchini. Mhe. Said Ali Mbarouk: Nakushukuru Mhe. Spika, naomba nimuulize Mhe. Waziri swali la nyongeza. Kwa majibu wa swali hili Mhe. Waziri ameeleza kwamba suala la Bima ya Maisha linahusiana pia na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii. Je, utaratibu gani anaokusudia kuuchukua ili kuona kwamba wafanyakazi wanaojiunga na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii hapa Zanzibar basi moja kwa moja wanapata Bima ya Maisha katika suala hilo? Mhe. Waziri wa Nchi (AR) na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Anayeshughulikia Masuala ya Fedha na Uchumi: Mhe. Spika, nafikiri Mhe. Said Ali Mbarouk kanifahamu lakini kidogo kataka kuainisha vitu viwili ambavyo niseme ni kitu kimoja lakini hivi ni vitu viwili, Bima ya Maisha na hii nyengine ambayo ni Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa ujumla. Sasa hii hifadhi ya jamii kwa jumla ni inclusive Bima ya Maisha. Sasa huu Mfuko wa Hifadhi ya Jamiii una mpango wake kwa wafanyakazi kuwasaidia ile hakiba ya uzeeni. Lakini kwa Bima ya Maisha ni kama nilivyosema ni kitu kimoja wapo katika hiyo hifadhi ya jamii. Kwa hivyo, ni vitu viwili ambavyo mwisho nimesema serikali inaruhusu watu kujikatia hifadhi ya jamii individually. 8

Nam. 24 Mbinu za Uendeshaji Miradi ya Wananchi Mhe. Ali Denge Makame (Kny. Mhe. Anaclet Thobias Makungila) Aliuliza:- Mradi wa MACEMP umeanzishwa baina ya SMT na SMZ kwa madhumuni ya kuendeleza jitihada za serikali kutekeleza mkakati wa kukuza uchumi na kuwapunguzia umasikini wananchi wanaoishi ukanda wa pwani kwa kubuni njia mbali mbali za kutekeleza miradi yao walioianzisha. Je, mradi wa MACEMP umepata mafanikio au matatizo ani katika kuwapunguzia umasikini wananchi waishio ukanda wa pwani? Mhe. Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Mazingira - Alijibu:- Mhe. Spika, kwa ruhusa yako naomba kumjibu Mhe. Mwakilishi swali lake Nam. 24 lenye vifungu a na b kama ifuatavyo:- Mhe. Spika, mafanikio ya msingi yaliyopatikana katika mradi ndani ya Mradi wa MACEMP ni pamoja na uelewa wa jamii kwa asilimia 90 wanaoishi katika ukanda wa pwani juu ya kuhifadhi, kulinda, kutunza mazingira ya bahari na rasilimali zake zilizopo katika ufukwe na ardhini. Wananchi wamefaidika na miradi tofauti ambapo kwa kiasi kikubwa uendelezaji wa miradi hiyo utaweza kuwapunguzia umasikini. Jumla ya miradi 96 Pemba na miradi 76 Unguja yenye thamani ya Tshs.2,789,340,542/- ambapo zimetumika katika miradi ya uvuvi, ufugaji, kilimo cha mwani, miradi ya utengenezaji wa kamba ya usumba, majengo pamoja na vitendea kazi tofauti. Kwa upande wa matatizo ya Mradi wa MACEMP kwa kuwa umekuwa ni mkombozi wa wanavijiji waishio ukanda wa pwani, wizara yangu imekuwa ikipokea malalamiko tofauti ndani ya vijiji vya ukanda wa juu na hasa kilimo kwa kukosa kwao kuwa na fungu la kuwahudumia. Aidha, mahitaji yameongezeka na hivyo wizara iko katika harakati za kuzungumza na wahisani ili kuona jinsi ya kuweza kukidhi mahitaji ya nchi pamoja na vijiji vyake vyote. Mhe. Ali Suleiman Ali: Mhe. Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mhe. Naibu Waziri naomba kuuliza swali moja la nyongeza. Mhe. Spika, hivi sasa wananchi wa ukanda wa pwani wamefaidika sana na mradi huu wa MACEMP. Kwa asilimia kubwa wanahamasika katika utendaji wa kazi zao mbali mbali pamoja na kulinda mazingira yao. 9

Je, kwa kuwa hapa Zanzibar tuna Chuo Kikuu cha Sayansi Bahrini ambacho lengo lake kubwa ni kuielimisha jamii juu ya athari mbali mbali za matumbawe na mambo mengineyo ya baharini. Wizara ina mpango gani katika kushirikiana na chuo hicho juu ya kufanya tafiti mbali mbali ili kunusuru jamii ya matumbawe isipotee. Mhe. Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Mazingira: Mhe. Spika, wizara yangu haitaona tabu kushirikiana na chuo hicho. Nataka nimhakikishie kwamba, kwanza tunayo mashirikiano ya pamooja na pia tutaendelea kufanya mashirikiano ya pamoja ya ziada. Nam. 25 Kushuka kwa Uzalishaji wa Zao la Karafuu, Zanzibar Mhe. Salmin Awadh Salmin Aliuliza:- Pamoja na juhudi za serikali za kuanzisha Mpango wa Taifa wa Uimarishaji wa Mikarafuu, lakini bado inaonekana kwamba uzalishaji wa zao hilo unashuka siku hadi siku. (a) (b) Je, Mhe. Waziri kuna utafiti wowote uliofanywa kuhusu sababu zinazopelekea kushuka kwa uzalishaji wa karafuu hapa nchini? Je, serikali haijaona umuhimu wa kujua idadi ya mikarafuu inayozaa hapa nchini na taarifa zake zikatolewa katika kila mwaka hasa wakati wa vikao vya Bajeti.? Mhe. Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Mazingira Alijibu:- Mhe. Spika, kwa ruhusa yako naomba kumjibu Mhe. Mwakilishi swali lake Nam. 25 lenye vifungu a na b kama ifuatavyo:- Mhe. Spika, kabla ya kujibu swali hili napenda kutoa maelezo mafupi juu ya suala hili. Mhe.Spika, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Msaada wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), iliajiri taasisi ya utafiti ya mambo ya uchumi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kufanya utafiti wa mkakati wa kuendeleza zao la karafuu pamoja na mapitio ya wajibu wa ZSTC (The Zanzibar Clove Development Sterategy and Review of Function of ZSTC) ya mwaka 2004. 10

(a) Mhe. Spika, utafiti ule umefanyika na sababu zilizopelekea kushuka kwa uzalishaji wa karafuu hapa nchini ni hizi zifuatazo:- Maradhi Utunzaji mbaya wa mashamba Ukongwe wa miti na Mbinu dhaifu za uvunaji. Wizara yangu hapa inatoa wito kuyaweka mashamba yetu katika hali usafi. (b) Mhe. Spika, serikali inajua umuhimu wa kujua idadi ya mikarafuu inayozaa hapa nchini na taarifa zake hutolewa katika vikao vya bajeti kila mwaka. Kutokana na umuhimu huo, wizara yangu tayari imefanya tathmini ya gharama za kufanya utafiti huo na gharama zake ni jumla ya shs.353,957,530/-. Tayari zimeshawasilishwa Wizara ya Fedha na Uchumi kwa ajili ya kutafutiwa mfadhili tokea mwaka 2008. aidha wizara yangu imo mbioni kutafuta mfadhili wa kazi hiyo. Mhe. Subeit Khamis Faki: Nakushukuru sana Mhe. Spika, kwa kunipa nafasi ya kumuuliza Mhe. Naibu Waziri swali moja la nyongeza. Mhe. Waziri atakubaliana na mimi kwamba sababu moja inayosababisha zao la karafuu kushuka ni bei ndogo ya wakulima wanayopewa na inasababisha wananchi mashamba yao kutoyashughulikia kwa sababu wanaona bei wanayoipata ni ndogo. Je, atakubaliana na mimi kama ataongeza bei kila mmoja atalisafisha shamba lake kwa ajili ya kupata mazao zaidi. Mhe. Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Mazingira: Mhe. Spika, kwana nataka nimhakikishie kwamba bei ya karafuu haipangwi na Wizara ya Kilimo, bei hiyo inatokana na soko la dunia. Bahati nzuri au mbaya karafuu sasa hivi hatuzalishi sisi peke yetu visiwani, kuna na nchi nyengine ambazo zinazalisha karafuu. Lakini suala la kwamba wananchi wanashindwa kuyatengeneza mashamba yao kwa sababu hatujaongeza bei. Hili namuomba kupitia Baraza la Wawakilishi kama hiyo ndio dhana na sisi wenyewe tunaamini hivyo, basi tuwatake wananchi wetu wayasafishe mashamba yao na yawe endelevu kwa kipindi kijacho. Kwa sababu mambo haya yanakwenda na kurudi, kuna kipindi inapanda na kuna kipindi inashuka. Je, pale itapokuwa imepanda na mikarafuu tumeshaiangamiza tutategemea tupate kitu gani? Kwa hivyo, nawaomba wahamasishwe zaidi. 11

Kule kwetu Micheweni nafikiri sio mikarafuu mingi, kwa hivyo, naomba Mhe. Mjumbe asisikilize sana labda wale waheshimiwa wenye mikarafuu mingi zaidi watu wa Mkoani wahamasishe wananchi wao ili mashamba wazidi kuyalimia na kuyaweka katika hali ya uzuri na wizara uangu kupitia ZSTC tutaendelea kuliendeleza zao hili kwa sababu tunatoa miche mingi kila kipindi na tutaisimamia ipasavyo. Hilo nilikuwa naongeza nyongeza tu Mhe. Spika. Mhe. Ame Mati Wadi: Mhe. Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mhe. Naibu Waziri naomba kuuliza swali moja la nyongeza. Mhe. Waziri kwa muda mrefu serikali kwa jumla inahimiza kutunzwa mikarafuu. Lakini kutokana na wananchi vile hawasimamiwi vizuri maeneo walioko, hivi sasa kuna hujuma kubwa sana ya kukata mikarafuu na kuuza kuni hasa katika Mkoa wa Kaskazini, Wilaya ya Kaskazini B. ukipita maeneo ya Donge utaona kuni za mikarafuu mitupu. Hivyo, nani anapaswa kulishughulikia hili ili kuona mikarafuu inalindwa. Pili iko sheria ambayo inadhibiti kwamba kuni ya mkarafuu isionekane inauzwa kiholela. Mhe. Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Mazingira: Mhe. Spika, kwanza nataka nikubaliane kwamba kuna watu na sio Donge peke yake naweza kusema ni maeneo yote yenye mikarafuu wana tabia ya kuikata mikarafuu kwa ajili ya shughuli za mabekari na mambo mengine. Lakini ninalotaka kusema kuwa ni jukumu la nani? Hili ni jukumu la Wizara ya Kilimo, serikali kwa ujumla pamoja na yeye mwenyewe Mhe. Ame Mati. Anapoiona mikarafuu pale Donge imekatwa basi sio lazima amsubiri Mwakilishi wa pale Naibu Waziri Kiongozi, yeye pia ana haki ya kutoa taarifa kituo cha polisi pale pale alipoliona lile tukio na hatua zitachukuliwa za kisheria. Kwa hivyo, hatuna haja ya kusubiriana au labda ije Wizara ya Kilimo aikamate, sote tuna wajibu wa kukamata na kwa sababu hii ni mali yetu sote na serikali yetu sote na tumekuja humu kama ni serikali. Mhe. Spika, la pili naomba alirejee tena swali lake. Mhe. Ame Mati Wadi: Mhe. Spika, niliuliza kwamba iko sheria inayoilinda mikarafuu ili kuni zake zisikatwe ovyo? Mhe. Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Mazingira: Mhe. Spika, sheria ipo, sio mikarafuu tu, kwa miti yote iliyopo Zanzibar ina sheria zake. Na ndio maana tumeweka vibali maalum kama mkarafuu una tatizo basi unatakiwa ukatwe kwa utaratibu uliowekwa, yaani labda ni mbovu kabisa au unahatarisha 12

maisha ya mtu. Kwa hivyo, sheria ipo na inafanya kazi na ndio kama nilivyosema na yeye akiliona hilo kosa asisubiri kuja kuuliza ndani ya Baraza, tufanye kazi kwa pamoja na tulinde kwa pamoja. Ahsante Mhe. Spika. Mhe. Mohammed Ali Salim: Mhe. Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii ya kuuliza swali moja la nyongeza. (a) Mhe. Spika, naomba nimuulize Mhe. Naibu Waziri, kwa kuwa bei ya karafuu katika shoko la dunia huwa inateremka kila wakati. Kuna sababu zipi za msingi zao hili lisibinfsishwe? (b) Tumeambiwa kuwa bei ya karafuu inapatikana kutokana na bei soko la dunia. Je ni asilimia ngapi ya bei ya soko ya dunia anayopewa mkulima hapa? (c) Tumeambiwa upunguaji wa karafuu umesababishwa na moja katika sababu ya uchumaji mbaya wa karafuu. Naomba Mhe. Naibu Waziri anijulishe zamani zilikuwa zikichumwa vipi zikawa nyingi na sasa hivi zinachumwa vipi zikawa haba. Mhe. Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Mazingira: Mhe. Spika, naomba nianze kujibu kifungu (c) alichosema kwamba zamani karafuu zilikuwa zinachumwa vipi na sasa zinachumwa vipi. Wengi tuliyoondoka katika Kisiwa cha pili tulikuwa wachumaji wa karafuu. Nakumbuka hapa kulikuwa na nyimbo ya Bambuti alikuwa anaimba twendeni Pemba tukachume karafuu. Ni imani yangu kwamba na watu walikuwa wakitolewa Unguja wanakuja Pemba kuchuma karafuu. Sasa katika uvunaji ule wa zamani kwa sababu sitaki kusema labda enzi hizo za miaka ya 1919 au 1990, wenye mikarafuu yao walikuwa wakisikia kimedata kile kitawi tu, basi wanakushusha na wanakwambia basi. Lakini sasa hivi watu wameachia huria yale mashamba yao. Unaweza kumkuta mtu mmoja anaweza kuvuna mikarafuu zaidi ya sita anakwenda anakata matawi, kwa sababu ile hali ya kuisimamia ile mikarafuu yetu wenyewe sisi imepungua na ndio maana labda utakuta mkarafuu umevunwa mwaka huu mwakani uzazi wake unakuwa mdogo. Kwa sababu lazima kwanza mpaka uchipue matawi mengine. Kwa hivyo, ni tofauti kubwa kati ya uvunaji wa zamani na wa sasa. Labda lile la bei kupanda na kushuka ndio wanakuwa wanadharau lile zao lao. (a) Hili ni zao ambalo serikali bado inalitegemea. Kwa hivyo, serikali mpaka sasa hivi haijawa na mpango wa kulibinafsisha suala la karafuu na kuwaachia wananchi waliendeleze wenyewe. Hili litakuwa ni zao la taifa lenye kuleta kipato kwa taifa. Kwa hivyo, likipanda, likishuka lakini bado ni zao la taifa hatuna mpango wa kuwaachia watu binafsi walichukue. 13

(b) Asilimia inayopatikana, serikali inapata kiasi gani na wananchi wanapata kiasi gani. Hili kwa kweli nilikuwa sijajiandaa na nitalirejesha kwa maandishi kwa Mhe. Mwakilishi. Ahsante. Mhe. Waziri Kiongozi: Mhe. Spika, nakushukuru sana kwa kunipa fursa hii ya kutoa maelezo ya ziada pale alipomalizia Mhe. Naibu Waziri. Mhe. Mohammed Ali Salim ameuliza kwa nini bei ya karafuu sasa hivi inapanda, inashuka lakini serikali bado haijaamua kulibinafsisha zao la karafuu. Nafikiri nusu ya jibu amejijibu mwenyewe, kwa sababu serikali iliyo makini unapokuwa na zao kama hili ambalo bei yake haitabiriki sana, unapoamua kwa haraka kulibinafsisha itakapotokea bei imeanguka basi wananchi wanaweza wakafanya maamuzi mabaya ya kuanza kuikata hiyo mikarafuu yenyewe. Mifano ipo. Wale wanaokumbuka vizuri wakati wenzetu Tanzania Bara walipoanza kubinafsisha soka la kawaha na kadhalika, watu walianza kuikata mibuni hiyo kwa ajili ya kupanda viazi na kadhalika. Sasa huo ni mfano mmoja. Mfano mwengine ukatokea kwenye sehemu za Lindi, Mtwara. Tumeona kwamba mikorosho hali iliyoipata. Sasa wazo la kubinafsisha zao la karafuu linafikiriwa. Nakumbuka kuna taarifa hapa ya serikali ilishaletwa huko nyuma kama miaka mitatu iliyopita. Sasa wazo lipo, lakini unapotaka kufanya maamuzi magumu kwa zao ambalo tunalitegemea sana kama hili, maamuzi yako yanahitaji kufanyiwa kazi kwa umakini na tumesema tokea wakati huo mpaka leo tunaendelea kufanya utafiti wa kutosha. Kwa sababu sisi tayari tumeshaona wenzetu pale walipoanguka, sasa si vizuri na sisi kuelekea huko bali sisi tuendelee kufanya utafiti. Tukifikia mahala tukiridhika mara tu tutakapoanza kulibinafsisha soko lile basi tusije tukawaachia wakulima wa zao hili muhimu matatizo. Kwa sababu jambo lolote serikali ni kama mzazi vile, mtu yeyote akifanya kosa hata kama kosa lile linatokea na matendo yake mwenyewe basi mwisho wake lawama ataitupia serikali. Sisi ambao leo hapa tunaiharakisha serikali ifanye ubinafsishaji wa zao la karafuu likitokea jambo lolote hapa bei ikianguka sisi wenyewe tutabadilika na kuiuliza serikali kwamba hivyo nyinyi hamkujua? Hamkuwa makini? Sasa ili tusifike huko tukaanza kulaumiana hapo baadaye tunasema jambo hili kinadharia linaonekana ni zuri. Sisi serikali hatuna tatizo na jambo hili, lakini tunalosema tunahitaji kufanya utafiti wa kutosha kuhusu jambo hili ili wakati tutakapofanya maamuzi yetu basi yawe ya busara hata kama itatokea athari baadaye lakini athari yenyewe iwe ni ndogo ambayo tunaweza kuikabili. Mhe. Spika, nakushukuru. 14

HOJA ZA KAMATI Kamati ya Maendeleo ya Wanawake na Ustawi wa Jamii (Majadiliano yanaendelea) Mhe. Spika: Waheshimiwa Wajumbe tuliachia jana kwamba tumalize majadiliano kwa kuwasikiliza waheshimiwa wawili waliyoomba na baadaye twende kwa Waheshimiwa Mawaziri. Naomba sasa nimkaribishe Mhe. Haji Mkema Haji. Mhe. Haji Mkema Haji: Mhe. Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii kuchangia Ripoti ya Kamati ya Maendeleo ya Wanawake na Ustawi wa Jamii ambayo imewasilishwa jana katika Baraza hili. Mhe. Spika, nachukua nafasi hii kwanza kuwapongeza sana Wajumbe wote wa Kamati hii kwa kazi nzuri waliyoifanya. Lakini pia taarifa yao imekuwa safi ambayo imeeleza shughuli mbali mbali zilizofanywa na wizara hizi nne walizokabidhiwa, yaani Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Wizara Kazi, Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto. Mimi nina maoni yafuatayo:- Nikija katika Wizara ya Habari katika ukurasa wa 25 wa ripoti hii kifungu cha 14.5 kumeelezwa mafanikio kamati iliyoyaona juu ya ujenzi wa studio ya redio ya jamii huko Micheweni. Hii ni hatua nzuri itasaidia sana rediao hii kutoa taaluma katika eneo hilo. Nafikiri hii inakwenda sambamba na ule mpango wa kuondoa umasikini. Kwa sababu redio ni chombo cha taaluma ndugu zetu wa Micheweni watapata taaluma mbali mbali za kimaisha, kazi pamoja na uhai wao. Kwa hivyo, naipongeza serikali. Lakini wakati tunajenga studio mpya je, hali za studio zetu nyengine vipi hizi? Mhe. Spika, hali za studio zetu ni mbaya sana, mitambo imechakaa na matangazo wananchi hawayapati vyema. Sasa ningeiomba serikali ikaitizama sana idara hii ili tupate mitambo mipya. Mhe. Spika, kipindi kilichopita mimi nilikuwemo kwenye kamati hii, tuliona matatizo ya mitambo yetu ya Medium Wave hapo Chumbuni. Sasa sijui ni kiasi gani jitihada za serikali zimefanikiwa kuweza kurejesha tena mitambo ile ili wananchi wakaweza kupata redio yetu kikamilifu. Sasa hivi tunatumia Short 15

Wave pamoja na Redio ya FM ili kupata matangazo yetu. Lakini mtambo huu wa Medium Wave ndio hasa unaotoa taarifa au matangazo ya uhakika kwa visiwa vyetu hivi. Mhe. Spika, ningeuliza jitihada za kurejesha mtambo huu zimefikia vipi? Mhe. Spika, vile vile katika kifungu 14.3 ripoti hii kamati imeona kazi za upelekaji umeme Uwanja wa Gombani. Bado lakini matarajio wamekubaliana lakini hatujaelezwa ni lini hasa shughuli hii itafanywa. Nakumbuka hata na sisi tulipokuwepo kwenye kamati hii maneno haya haya tuliambiwa. Sasa mimi ninakuwa na wasi wasi umeme huu sijui tutangoja huo wa kutoka Pangani ndio unaotaka kuletwa Gombani au vipi ili hizi taa ziweze kuwekwa pale katika kiwanja chetu. Nina wasi wasi na hizo taa nazo zitaota kutu hata huo umeme utapokuja kutiwa taa ziwe hazifai tupate hasara tena ya kuzitafuta taa zitazoweza kulingana na wakati huo. Mhe. Spika, Shirika la Umeme ni letu wenyewe basi tufanye jitihada kuharakisha huu umeme, kama si huu tunaoungojea kutoka Pangani tulionao, basi iharakizwe umeme ufike taa hizi zitiwe katika uwanja huu ili uweze kutumika kama ilivyokusudiwa. Mhe. Spika, kamati katika kifungu cha 14.4 imeshauri idara kufanya jitihada ili kurejesha hadhi ya studio zetu za redio pamoja na TV. Mhe. Spika, nitofautiane na kamati hapa, kuiambia idara tunaionea nafikiri wangeiambia serikali. Maana yake jitihada za wizara mimi naamini zipo. Kwa sababu mafundi wetu wanajitahidi sana katika mitambo hiyo hiyo mibovu na tunapata matangazo. Lakini nafikiri mambo yamezidi kimo, hivi sasa lazima serikali iingilie ihakikishe inatoa fedha kununua mitambo mingine. Kwa hivyo, nafikiri Mwenyekiti wa Kamati atakapokuja hapa anieleze sio waitupie kazi hii idara au wizara. Hapa waziri uwezo wake umeshafika kwa sababu yeye ni kuwatumia mafundi wake kurekebisha, kufanya ukarabati na kazi hiyo inafanywa kwa miaka mingi. Sasa tunataka mitambo mipya katika redio na TV. Sasa kamati ushauri ndio lakini imeelekeza sipo. Kamati ielekeze mashauri haya kwa serikali kutoa fedha za kununulia mitambo ili hadhi ya vyombo vyetu iweze kurejea. Mhe. Spika, katika ukurasa wa 128 pameelezwa hatua za magofu, maendeleo ya magofu chini ya mradi wa MACEMP. Mhe. Spika, kazi hii kweli inakwenda vizuri na imefika pahala inaridhisha. Lakini kwenye mradi huu mbali ya kuwa ukarabati haya magofu, lakini kulikuwa na kazi nyengine muhimu zaidi ya upimaji wa maeneo ya magofu ya historia pamoja na kuwekewa uzio. Je, katika hili wizara imefanikiwa kiasi gani? Maana yake mradi huu umeingiza mambo hayo kukarabati, kupimwa na kuwekewa uzio maeneo hayo. 16

Mhe. Spika, kazi hizo ndio ilikuwa za mwanzo. Hivi sasa maeneo mengi ya kihistoria yanavamiwa na mtu kuondoka inakuwa vigumu. Itafika pahala hizi pesa tulizopewa tutashindwa kuzitumia na fedha tunazihitaji. Sasa ikiwa pesa unazosaidiwa huzitumii wale waliotusaidia watatuona hatuna shida na tutakosa misaada. Kwa sababu hao hao wanaosaidia kwenye MACEMP ndio wanaosaidia kwenye shughuli nyengine za kilimo, ufugaji na taaluma. Wakiona fedha tunazirejesha watatuona ni wazembe wa kuzitumia pesa na mwanya huu utatukosesha misaada katika njia nyengine. Mhe. Spika, ningependa kujua katika hatua hii ya kuendeleza magofu, zile hatua za upimaji na kuweka uzio maeneo yote ya historia ambayo fedha za MACEMP zimetajwa yamefikiwa katika kiwango gani. Mhe. Spika, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ukurasa wa 130 wenzetu hawa walipata fursa ya kupewa taarifa juu ya namna ya wizara inavyopanua fursa za upatikanaji wa elimu katika ngazi zote. Mhe. Spika, naipongeza wizara na jinsi inavyofanya mimi nakubaliana nao nina ushahidi wa kutosha kwa kazi hii wanayoifanya. Mhe. Spika, katika matokeo ya mtihani wa mwaka huu Jimbo langu la Koani limebahatika skuli za sekondari 3, Kikungwi ninakoishi, Uzi na Jumbi zimefunguliwa sekondari, haya ni mafanikio. Kwa hivyo, mimi naishukuru serikali na iendeleze juu ya hivyo. Lakini kupanua fursa za elimu ni pana kabisa. Kwanza elimu haiwezi kupatikana bila ya walimu, mazingira yao, pamoja na hao wanafunzi. Mhe.Spika, nashukuru wanafunzi wapo na tunazaa, naiambia serikali wanafunzi watakuwepo wa kutosha, malighafi hiyo itakuwepo ya kutosha. Lakini sasa kuna shida ya mapungufu ya walimu hasa wale wa masomo ya sayansi. Kwenye skuli zetu hizi anaweza kuwepo mwalimu mmoja tu wa hesabu, au wa physics mmoja, wa biology mmoja, waliobakia wote wa dini, Kiswahili, historia na Kiarabu. Mhe. Spika, bado tupo katika hali mbaya. Katika kupanua fursa hizi bado Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali bado inayo kazi kubwa na ijitahidi ilenge tupate walimu wa sayansi wa kutosha hizi fursa ziweze kutumika vizuri. Kuna maeneo yametokea matokeo mabaya siwezi kusema pengine nikawalaumu wanafunzi. Lakini anakuwepo mwalimu mmoja wa masomo hayo kwa muda wote na wanafunzi waliowazidi kimo. Kwa hivyo, mbali na sababu ambazo zitajulikana, lakini ukosefu wa walimu mahsusi katika masomo haya nalo limechangia wanafunzi wetu kufanya vibaya katika baadhi ya skuli. 17

Mhe. Spika, naiomba wizara ilione hilo hasa katika skuli zetu za Wilaya ya Kati. Sababu kubwa ambayo imefanya wanafunzi wetu kufanya vibaya ni ukosefu wa walimu wa masomo muhimu hasa yale ya sayansi. Lakini pia walimu wenyewe kuwa katika mazingira magumu. Mhe. Spika, walimu wengi wanatoka mijini hawafiki katika vituo vyao vya kusomesha kwa wakati. Kama vimepangwa vipindi mwalimu asomeshe saa 2:00 mpaka saa 3:00, mwalimu anaingia saa 4:00 vipindi vile vimeshampita. Kwa hivyo, kunakuwa na upungufu wa masaa ya wanafunzi kupata taaluma nayo pia inasababisha. Kwa sababu kiwango cha elimu walichotakiwa wapate hakikufika. Sasa nawaomba wenzetu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali wangeorodhesha wakachukua data za walimu wote wanaokaa mjini wakafanya utaratibu wa usafiri wa pamoja, ili walimu wetu wawe na uhakika wa usafiri na kuweza kufika kwa wakati. Mhe. Spika, katika ukurasa wa 132 kuna mradi unaoendelea wa Vyuo Vikuu ambapo kimetajwa Chuo cha SUZA. Mhe. Spika, hivi sasa kuna ujenzi wa chuo hicho na station yake kubwa itakuwa pale Tunguu katika Jimbo la Koani ambalo mimi ninawakilisha. Sasa nimuulize Mwenyekiti wa Kamati, ule ujenzi umeshaanza, sijui mikataba wameiona wenzetu wanakamati? Mkandarasi aliyewekwa ni madhubuti? Ana uwezo? Taratibu zote zile za mikataba zimetimizwa maana yake ule ni mradi mkubwa. Lakini juu ya hayo Mhe. Spika, kwa sababu mimi ndio njia yangu kila siku nina wasi wasi na mkandarasi yule kama kweli ana uwezo wa kukamilisha ujenzi huo kwa wakati. Kwa sababu kwanza mjenzi kama yule utaona kwenye vifaa vyake vya kufanyia kazi ni hafifu tena duni. Halafu kasi za ufanyaji wa kazi ni ndogo, hii inatimia wiki ya tatu hakuna kazi zinazofanywa baada ya kuchimba misingi imefukiwa nusu na sasa hivi mvua zinakuja mtu hana vifaa nina wasi wasi. Sasa sijui wizara kwa kiasi gani inafuatilia mradi huu ili uende kwa mujibu wa mikataba na uweze kufanikiwa kwa wakati. Mhe. Spika, mtu ukitafunwa na nyoka ukiona unyasi hushtuka. Kampuni kama hizi nyingi zimeshatutia mashaka, uwanja wa ndege tunao mpaka leo wametutia kisirani. Imeletwa kampuni hapo zaidi ya miaka miwili haijafanya lolote baadae serikali imevunjiana mkataba kutafuta mkandarasi mwengine mpaka hivi leo hapajafanyika lolote. Kwa hivyo, natoa indhari juu ya huyu mkandarasi ambaye anajenga majengo ya vyuo vikuu Tunguu afuatiliwe ahimizwe tuhakikishe anakwenda kwa mujibu wa kazi tunayoitaka lakini na kwa wakati ambao tumempangia. 18

Mhe. Spika, ukurasa wa 141 kuna Bodi ya Sensa kazi ambazo zimefanywa nashukuru. Lakini bodi hii lazima iwe makini kuhakikisha maadili ya Mzanzibari yanalindwa kuhusiana na vipindi pamoja na nyimbo ambazo zinaimbwa kwenye vyombo vya habari, lakini hata katika mashughuli pamoja na hadhara. Bado Mhe. Spika, nyimbo za ovyo ovyo zinaendelea kuimbwa bila ya mpango. Jana nimeisikia nyimbo inaimbwa mpaka kati kati inasema Mzee Juma mbona kunlala? Senlala nautia kasi. Hivyo kweli nyimbo hiyo wenzetu bodi wameisikia? Hii nyimbo kweli ina maadili ya Mzanzibari? Sasa kama uko na mwanao anasikia mambo haya ya kutia kasi itakuwaje? Mhe. Spika, naomba Bodi ya Sensa iwe makini katika nyimbo kama hizi. Japo utakuja kuona yale maneno kweli hamna tusi. Lakini je, ule mpangilio, mantiki yake bado kabisa haipo katika mambo ya Kizanzibari. Nyimbo kama hizi zifutwe katika mambo ya hadhara pamoja na vyombo vyetu. Mhe. Spika, ukurasa wa 136 kifungu 7.1.4 Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Kufanya uzinduzi wa Road map ya kusaidia kupunguza vifo vya mama na watoto. Mhe. Spika, mradi huu ni mzuri, lakini ili kufikiwa mambo hayo basi vituo vyetu viwe na fursa ya kutosha. Kwa sababu mbiu ya mradi huu inasema watu wote wakazalie kwenye vituo vya afya. Lakini vituo vya afya bado havijafikia hatua hiyo ya kila mtu akazalie kule kutokana na mazingira ya usafiri pamoja na hali. Mhe. Spika, unampeleka kituoni mzazi, basi awepo mkunga, lakini vituo vya afya vingi havina nyumba ya mkunga karibu. Kwa mfano Jimbo la Chonga, kituo kiliopo pale unamtoa mtu Kuyuni au Ngwachani kuja kituo cha Chonga hata ukifika mashaka. Mkunga anakaa Pujini, Mkuu wa Kituo mwenye ufunguo yupo Kipapo. Sasa muda huu wa kukaa huyu mama atasalimika ni hatari. Halafu kama anashindwa panatakiwa sasa hivi umsafirishe na halikadhalika. Mhe. Spika, vituo vyetu vingi bado vinakuwa na matatizo ya kumwezesha mama kuzalia kituoni na akaweza kusalimika kwa mfano Ukongoroni, Uzi na kwengineko. Mhe. Spika, pia vituo vya Wilaya ya Kati vingi haviko katika hali nzuri bado vipo katika grade ya chini. Vile vile sehemu ya martenity ward juzi tulikuwa na semina hapa, basi yale maombi serikali isikie sio waziri, malipo yale yaondolewe. Hivyo kweli Mhe. Waziri wa Fedha hana fedha za kuendesha wodi moja kwa kuweka vitu muhimu kwa wodi ile ya wazazi? Nafikiri hiyo ipo. Mhe. Spika, hili tumelisema mapeme tunataka kwenye bajeti tuone kuna reform katika wodi ya wazazi, la si hivyo Pentagon ipo itahakikisha bajeti hiyo hatuikubali. 19

Tunahitaji kuona kinamama wanaokwenda wodi ya wazazi wanapata huduma bila ya usumbufu na kwa unafuu. Mwenye kufunga kidonda muache achangie, anayekohoa hawezi atakwenda kutafuta mpambawake, mwenye kamasi anaweza kutafuta mchofu, lakini mzazi lazima aende pale ili aweze kujifungua salama. Mhe. Spika, ni lazima yawekwe mazingira ambayo mtu yeyote wa kimasikini aweze kujifungulia pale bila ya usumbufu. Mhe. Spika, naomba kumalizia na Wizara ya Kazi, Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto kuhusu ufinyu wa bajeti. Naomba hili lizingatiwe kwa sababu pale ndio tanuri la wadau ambao wanataka kupunguziwa umasikini, vijana, watoto na wanawake lakini bajeti ni ndogo. Mhe. Spika, kilio hiki naomba serikali isikie kwa sababu hii ni ripoti ya kamati hatuzungumzi na wizara, tunakwambia wewe Spika ili serikali ijue. Mhe. Spika, naunga mkono ripoti hii. Ahsante. Mhe. Salim Abdalla Hamad: Mhe. Spika, nashukuru kwa kupata nafasi hii ya kutoa mchango wangu katika hotuba iliyotolewa na Kamati ya Maendeleo ya Wanawake na Ustawi wa Jamii. Mhe. Spika, kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu na mimi kunijaalia katika kipindi hiki kuwemo katika kamati hii. Mimi kwa jina lake nilifikiri ina kazi ndogo tu kumbe ni kamati yenye kazi nzito. Isipokuwa masikitiko yangu ni kuwa haya maendeleo ya wanawake hayakupewa mkazo sana katika kamati, lakini inafanya kazi ngumu katika wizara zote katika hali sawa sawa. Kwa hivyo, naomba izidishiwe wakati na ipangiwe mipango ili iweze kweli kushughulikia maendeleo ya wanawake. Mhe. Spika, nahisi leo wakati ni mali sana kwa hivyo nitajitahidi kutumia wakati mchache. Naomba moja kwa moja nisizungumze kama ilivyo katika taarifa iliyomo katika kitabu chetu, lakini kutokana na niliyoyaona tu katika kutembea kwangu. Mhe. Spika, kwanza nianze na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali. Wizara hii ndio wizara pekee ambayo inatupa wananchi kwenye fani za masomo mbali mbali na wananchi hao ndio wanaolitumikia taifa hili katika shughuli kadhaa. Elimu ikikua kimaumbile na maendeleo ya nchi yatakua kwa sababu wataalam wa kila fani watakuwepo. Elimu ikidumaa takriban na maendeleo yetu huwa yanadumaa na mwisho wake ndio huhitaji wasaidizi kutoka nchi za nje kwa zile sehemu ambazo hatuna uwezo nazo kuzihudumia. Mhe. Spika, mimi katika kutembelea wizara hii na kufuatilia baadhi ya mambo nimeona kwanza mfumo wa wizara ni mzuri wa kuwasomesha watoto mpaka darasa la 12. Naupongeza huu mtindo unaoendelea kwa kila skuli yenye darasa la 10 ikipasisha zaidi ya wanafunzi 20 kama mazingira yanaruhusu wanafungua darasa la 11 na 12. Lakini elimu kwa kuhesabu mabanda haiendi sambamba 20

kama mabanda yale hayakufanyiwa matayarisho ya kina ili elimu inayopatikana katika mabanda yale iwe ni elimu sahihi. Kwa bahati mbaya nimetembelea skuli nyingi tu ambazo zina mpaka madarasa ya 12, nililogundua nyengine zina walimu wa kutosha, nyengine zina upungufu mkubwa wa walimu, lakini kwa jumla jumla sikupata kuona katika hizo skuli nilizotembelea skuli moja iliyokuwa idadi ya walimu inakidhi haja ya mahitajio ya taaluma kwa wanafunzi waliopo na hasa kwa upande wa sayansi. Mhe. Spika, kufungua darasa la 11 na 12 kwa vile yameenea katika visiwa vyetu matayarisho yake ni makubwa. Lakini kwa walimu waliomo katika shehia ile au shehia mbili za eneo lile palipokuwa na skuli kwa kuweza kuimanage skuli ile ni tabu kubwa. Pia kuwatoa walimu kutoka sehemu za mbali kuwaleta katika baadhi ya skuli haiwezekani kwa sababu ya kutokuwepo nyumba za kulala walimu. Kwa hivyo, ushauri wangu kwa wizara ni kuwa waendelee na mtindo huu, lakini watilie maanani upatikanaji wa walimu wanaoweza kuya-handle yale madarasa, ili taaluma inayohitajika ipatikane kwa manufaa ya nchi yetu na fedha inayotumika isiwe ya kufuta jasho. La pili Mhe. Spika, unapoingia katika elimu ya sekondari kuna masomo yamepangwa maalum ambayo ni masomo ya sayansi na hasa kwa kuwa tunayoyachukua sana ni biology, chemistry, physics na hesabu tunaingiza humo humo. Lakini ukiangalia matokeo ya mitihani ya kitaifa yanayotolewa kila mwaka ya darasa la 12, masomo haya ya sayansi wanafunzi wanafeli vibaya sana. Hata wale wenye uwezo wa kujiendeleza kwa kutumia fedha yao mfukoni baada ya kutofanikiwa kuendelea na masomo huwa wanachukua masomo ya art. Kwa hivyo, nchi yetu ina upungufu wa wataalam wa sayansi kwa maana hiyo tunajitoa katika ule ulimwengu wa sayansi na teknolojia. Ushauri wangu. Kama Mhe. Waziri anavyojitahidi kutafuta misaada mbali mbali kwa majengo na kadhalika, pia aone kuwa kila panapofunguliwa darasa la 10, vifaa vya sayansi husika viwepo, walimu wenye uwezo wawepo na ufuatiliaji uwe wa kutosha kuonekana kuwa hizi practical zinafanyika ili wanafunzi waweze kumudu masomo yao. Mhe. Spika, maabara ni jambo muhimu na nafikiri Mhe. Waziri atakubaliana na mimi kwamba skuli nyingi ambazo zina mpaka darasa la 12 ama zina store tu za kuweka vifaa vya maabara, lakini nyengine hazina kabisa. Si majengo mengi ni machache sana hasa siku hizi isipokuwa yale ya zamani utakapokwenda ukakuta laboratory, wanafunzi wanakuja wanafanya practical kadhaa. 21

Sasa mtihani unapokuja haulizwi kuwa ulikuwa ukifanya practical huko kwenye skuli yako au la, hii ndio sababu wanafunzi wetu huwa wanafeli sana katika masomo ya sayansi na hasa hivi sasa ilipoondolewa ile alternative practical ikawa wanafunzi wanafanya practical zao wenyewe. Kwa hivyo, naishauri wizara iangalie kwamba umuhimu sio kufika madarasa ya juu, umuhimu ni kupata elimu inayolingana na yale madarasa tujitahidi. Mhe. Spika, jengine unajua tumeongeza maskuli na wanafunzi wanapasi wengi na wengine wanakuwa na vipaji maalum wanapelekwa katika maskuli maalum na ni haki yao kufanyiwa hivyo. Lakini skuli zile hapo zamani zilijengwa katika haja ya wakati ule bahati mbaya hivi sasa skuli nyingi sana kama mfano Fidel Castro mabweni yaliyopo hayatoshelezi, matokeo yake unapoingia katika bweni utakuta magodoro yapo chini wanafunzi wanalala watatu katika godoro moja na kadhalika. Mpaka hivi juzi sikufanya utafiti lakini kulisababisha upande wa wanawake kukatokea maradhi ya kuambukiza ya ngozi. Kwa hivyo, ushauri wangu kwa wizara ni kwamba wakati wanajitahidi na nashukuru wapenda maendeleo wanasaidia sana Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ifanye mkakati maalum wa kuongeza mabweni haya ya kulalia wanafunzi katika zile skuli ambazo zinapelekwa wanafunzi wenye vipaji maalum, kwa vile idadi imeongezeka ina maana na makaazi ni lazima yaongezeke. Mhe. Spika, la mwisho kwa upande wa elimu, hatuwezi tukaikuza elimu mpaka tuone kwamba inatolewa ipasavyo. Watu wanaohusika na kuonesha kwamba elimu inatolewa ipasavyo baina ya skuli na skuli ni wakaguzi. Huu mtindo ambao mimi siko pamoja nao wa wizara hivi wanaofanya wa mwalim mkuu mwenye dhamana kuifanyia ukaguzi skuli yake anayofundisha, mimi huu napingana nao moja kwa moja na nitaupiga vita mpaka nihakikishe umeondoka. Kwa sababu nimefanya utafiti, mwalimu mkuu ndio kama anajikagua mwenyewe na anajua akipeleka taarifa iliyokuwa si nzuri kama anajipeleka yeye mwenyewe. Kwa hivyo, hufanya mambo ambayo sio kutokana na hali halisi ilivyo, lakini wizara kwa sababu ni mwalimu mkuu huonekana kuwa ile ndio ripoti sahihi na mwisho wake unapokuja mtihani utaona matokeo ya wanafunzi ni kinyume na ile taarifa inayopelekwa. Mhe. Spika, naishauri wizara irudie ule mtindo wa zamani wa kuweka wakaguzi maalum kwa vipindi maalum tena kwa siri wa kwenda kukagua skuli bila ya anayekaguliwa kujua kwamba leo mkaguzi anakuja. Mtindo ule ni nzuri sana kwa sababu wakati wote mwalimu anakuwa katika suspension na anaifanya kazi yake vilivyo. Nasikititika sana na Afisi yangu ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba tulipokwenda tukawakuta wakaguzi wamo katika ofisi wamekaa na hawafanyi kazi kukagua hizo skuli. Nasikia huwa 22

wanapitia pitia na wao, lakini kwa sababu hawana usafiri wamekaa tu ofisini. Kwa jumla pengine inaweza ikawa ndio sababu katika mtihani huu uliopita Zanzibar kwa matokeo ya jumla ikawa si mazuri. Walioangalia taarifa nafikiri Mhe. Haji Faki Shaali aliwahi kufanya hivyo nasikia skuli ya Uondwe ni ya tatu katika walimu wazuri. Mhe. Spika, sasa nizungumzie Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo. Mhe. Spika, hili kama ingekuwa wakati unaruhusu ningelizungumza kwa urefu, lakini kidogo tu niingie kwenye michezo. Mhe. Spika, tulikwenda kuangalia kiwanja cha Amani na tumekishuhudia kipo katika matengenezo makubwa sana. Kwa mimi mwenyewe binafsi kwa matengenezo ninavyoyaona na kasi inayokwenda pamoja na hili suala la ucheleweshaji wa vifaa, kiwanja kile kitachukua muda mrefu sana, kwa sababu matengenezo ni makubwa, lakini kasi ya utengenezaji ni ndogo sana. Mhe. Spika, nahofia isije ikawa kama kiwanja cha ndege dakika za mwisho tukafukuza wale waliotufanyia kazi yaani PRISMO. Hata hivyo, wakati kiwanja cha Amani ndio kiwanja chetu kikubwa tunachokitegema, kinaendelea kutengenezwa na kinatakiwa kufanyiwa extension kwa michezo chungu nzima, hii isiwe sababu ya kiwango chetu cha michezo kuteremka. Kwa hivyo, ushauri wangu ningeiomba wizara husika kwa kushirikia na serikali kikamilifu, ili kuona kuwa kutengenezwa kwa Kiwanja cha Amani si sababu ya kuteremka kiwango cha michezo yetu. Kwanza ukiacha Kiwanja cha Amani, kule Pemba kuna kiwanja kizuri cha Gombani. Kwa hivyo, naomba tuitumie hii fursa sasa hivi, wakati hichi kinatengenezwa basi na kile kifanyiwe matengenezo ya haraka, wala hakina matengenezo makubwa ya hivyo, ili kiweze kutumika hasa kwa kusaidia hizi timu za taifa. Kwa sababu timu inayotoka nje ikaja kuchezeshwa katika uwanja wa Mau na vile ulivyo, uwanja uliojaa mabango ya ZANTEL tu, itakuwa kama tunaizalilisha nchi. Hicho kiwanja cha Gombani ni kizuri tu, tujiharakishe kutia hayo mataa, kukifanyia matengenezo madogo, ili kiweze kutumika na heshima yetu ibakie pale pale, wala isijulikane kuwa tuna pengo hilo. Vile vile shughuli nyingi za michezo siku hizi zinaendeshwa katika kiwanja chetu cha Mau ambacho waheshimiwa tunakijua. Safari hii tulikuwa tukakikaguwe, lakini bahati mbaya mvua haikuturuhusu. Niliwahi kwenda kuangalia baadhi ya mechi, kwa ile hadhi iliyo, basi si kiwanja cha kuchezea timu za taifa ni udhalilishaji mkubwa wa nchi yetu katika wakati huu. Mhe. Spika, ushauri wangu kikafanyiwe matengenezo, vile vikuta anagalau vitiwe viraka, isiwe huyu kakaa hapa na yule kakaa kule, ni aibu moja kwa 23

moja. Zile taa mbili tatu ziliomo nafikiri hazihitaji gharama kubwa sana ziwashwe, angalau kionekane hiki ni kiwanja kinatumika kwa shughuli za michezo. Mwisho Mhe. Spika, kwa sababu ya wakati kama nilivyosema, naomba nizungumze kidogo kwenye Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. Mhe. Spika, hii ni wizara tegemezi inayotulindia maisha yetu, kwa matibabu na kinga. Kwanza natanguliza maneno yangu kuwa kutokana na kazi yake ilivyo na nilivyoiona, kumbe ni kiasi Mhe. Waziri akonde, ni mtu anayetaka kufanya kazi kweli kweli kwa ajili ya kuisaidia jamii, lakini kumbe mfuko wake ni mdogo sana. Kwa hivyo, Mhe. Spika, kwa nguvu zote naomba hii wizara iangaliwe katika bajeti kwa kupewa fedha ya kutosha, ili iweze kumudu shughuli zake. Tumekwenda tumemshauri mambo mengi kwa kumsaidia, kwa vituo vya afya vile vilioko mashamba, ambako madaktari hawawezi wakafika wanaostahiki kwa hadhi ya vile vituo vilivyo, kutokana na kuwa hakuna nyumba za kulala. Pamoja na kuwa kajitahidi kujenga nyumba 20 Pemba na 20 Unguja, lakini bado mahitaji ni makubwa pamoja na mambo mengine. Kwa hivyo, nahisi mimi ili tufanikiwe bajeti ya Wizara ya Afya ipewe kipaumbele. Mhe. Spika, jambo jengine ni kwamba mpaka hivi sasa kuna sehemu watu wana matatizo sana ya matibabu, tena sana, kiasi ambacho mpaka wananchi wenyewe wamejitolea kujenga vituo hivi vya afya, lakini kwa sababu ya uwezo hawajui waelekee wapi tena. Wengine wamejenga msingi nakadhalika. Katika watu waliojitahidi kufanya hivyo ni wananchi wa jimbo langu, katika kile kijiji cha Bwagamoyo katikati ya Jimbo la Mtambwe, mahali ambapo ndio tunapopita na wagonjwa, siku nyengine tukawahifadhi kwa haja za dharura tunapotaka kuwapeleka hospitali ambako ni mbali sana. Sasa Mhe. Spika, mimi naomba rasmi. Leo naseme hivi kwa sababu wale wananchi jimboni wasikie kuwa hili suala ninalishughulikia. Fedha nyingi wameshatumia wananchi, nguvu nyingi wameshatumia wananchi na wameshauriana na serikali, wamepimiwa tayari wameshapata hatimiliki ya lile eneo, ni mali ya kituo cha afya kinachojengwa na hawana zaidi ya kufanya kuliko hapo. Kwa hivyo, naiomba wizara kwanza waje waangalie ile kazi waliyoifanya wananchi, pia imefika pahala wasaidiwe ili na wananchi wangu angalau wapunguwe vile kufa njiani kwa kuwapeleka hospitali ambako ni mbali, iwe Wete au Chake Chake. Mhe. Spika, kwa hayo machache nakushukuru, naomba kukaa kitako. 24

Mhe. Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii: Mhe. Spika, kwanza nakushukuru kwa kunipa nafasi hii, nakwenda moja kwa moja kuipongeza kamati kwa kazi nzuri sana wanayoifanya kwenye wizara yangu. Kamati hii wanatushauri vizuri, maoni yao mazuri na wanapotutembelea kweli wanatushauri. Kwa sababu hata juzi tulivyokwenda kwa Mkemia Mkuu wa Serikali, Mhe. Ali Mzee alitusaidia sana Wizara ya Afya kwa kutoa ufafanuzi, na alidhihirisha kwamba kweli yeye ni Professor. Kwa hivyo, nawapongeza wote wanakamati. Pili, Mwenyekiti wa kamati hii, Mhe. Ali Suleiman Ali katika ripoti yako uliyosoma, mambo yote uliyoeleza sisi Wizara ya Afya tunayachukua na tutayafanyia kazi. Kwa hivyo, kwa hilo Mhe. Mwenyekiti usiwe na wasi wasi kwa changamoto, maoni na ushauri yote mliyoyasema sisi Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii tutayafanyia kazi. Mhe. Spika, sasa nakwenda moja kwa moja kwa Mhe. Moh d Ali Salim. Yeye anataka kujua kwamba madai ya fidia ya watu 355 walioanguka mikarafuu na gharama malipo yote ni milioni 43. Je, unajua habari hii? Na kama unajua, basi isiwe mtenda wema kijuki, lakini mwisho sijafahamu amemalizia nini. Kwa hivyo, Mhe. Spika, napenda kumfahamisha Mhe. Mjumbe kwamba sisi Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kazi yetu ni kwamba aliyeanguka mkarafuu tunampokea, tunamtibu, tunafanya makisio yake na tukisha tunapeleka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, baadae mambo yate yanapelekwa ZSTC kwa malipo. Sio Wizara ya Afya inayofanya malipo. Wizara ya Afya inafanya makisio na kumtibu, gharama zote ni juu ya ZSTC kwa malipo. Kwa hivyo, wenyewe wananisikia na waharakishe kuwalipa hao watu 355. Mhe. Ali Abdalla Ali wa Jimbo la Mfenesini. Kwanza ametupa pongezi kwa nyumba ya daktari katika jimbo lake. Tumezipokea. Pili, akataka kujua je, Wizara ya Afya mmejitayarisha vipi kwa wananchi hao wanaogongwa na kuumia vichwa. Katika jimbo lake kuna wananchi wake wawili wamegonjgwa na gari na wameumia vichwa, mmoja yuko ICU na mmoja alipelekwa Muhimbili, lakini amefariki. Je, Wizara ya Afya mmejitayarisha vipi? Wizara ya Afya tumejitayarisha vizuri sana. Kwanza hivi sasa tumenunua vifaa vya kisasa na kuanzia jana inafungwa mashine ya X-Ray ya kisasa, pia inafungwa mashine ya CT Scan. Nimeambiwa na mafundi CT Scan hii inayofungwa katika Bara la Afrika ni 3 tu. Moja iko Afrika ya Kusini, moja iko Nairobi na moja ndio hii iko hapa Zanzibar. Mhe. Spika, na hii X-Ray inayofungwa ni ya aina yake. Ile ya zamani itatumika, lakini hii ni ya aina yake, ukipimwa huku mambo yote yanaonekana 25

kule. Gharama zilizotumika ni dola 800,000 za Kimarekani. Fundi kutoka Nairobi Kenya yupo na wengine watakuja. Kwa hivyo, ikimalizika atakayeumia kichwa mara moja itaonekana tatizo liko wapi, haitokuwa tena kupelekwa Dar es Salaam. Daktari tunao wa kutosha, tuna Wazanzibari waliosomea, tuna Wacuba na tunao Wachina. Sasa hivi tumempeleka Radio Grapher mmoja anachukua specialist yuko Nairobi anachukua degree ya pili, kwa hivyo na yeye atarudi hivi karibuni sana, anaitwa Dk. Salim akirudi na yeye wataungana. Tumewapeleka juzi wafanyakazi wetu Afrika ya Kusini, Nairobi kuchukua mafunzo hayo hayo. Kwa hivyo, tumo katika matayarisho, tunataka wananchi wetu wasipate tabu, wasihangaike, yatakapotokea mambo kama haya basi watibiwe hapa hapa. Hilo ni jibu la Mhe. Ali Abdalla Ali. Halafu ametaka kujua nyumba za wazee Sebleni ni mbovu, je vipi hizi habari. Nilieleza vya kutosha kwamba nyumba za Sebleni tuliwapeleka DANIDA pale wakenda kuangalia, wakenda Pemba Limbani na wakenda Gombani. Lakini walichosema kama watasaidia basi nyumba ya Limbani, kwa sababu nyumba za Sebleni zina gharama kubwa sana, zinatakiwa milioni 800 kufanyiwa matengenezo, ili zirejee katika hali yake ile ile ya zamani. Lakini hatujazitupa. Mhe. Spika, kwa upande wa serikali nyumba mbili zilikuwa haziwaki taa, tumezitengeneza na sasa hivi taa zinawaka. Koridoo ilikuwa hali mbaya na tumeifanyia ukarabati kidogo. Huo ndio uwezo wetu na bado tumo katika mipango ya kufanya nyumba ya Sebleni kuitia katika mradi wa maendeleo ili ipate fedha na kuweza kufanyiwa matengenezo. Jitihada bado tunazifanya na tunazishughulikia. Mhe. Ame Mati Wadi wa Jimbo la Matemwe, ametusifu sana kuwa tumefanya vizuri kwenye Kituo cha Afya cha Mkia wa Ng ombe. Kile ni kituo cha kisasa kabisa, tulipata ushirikiano na ndugu zetu wa Korea ndio waliokijenga Kituo cha Afya cha Mkia wa Ng ombe. Pia alitaka kujua kuhusu Kituo cha Afya cha Makangale. Kituo hiki pia ni kizuri na ni cha kisasa na kimeshamalizika kinafanya kazi. Vile vile aliwapongeza Mhe. Mwakilishi na Mhe. Mbunge kwa usafiri wao. Hata mimi nawapongeza waheshimiwa hawa kwa msaada wao mzuri. Napenda kumhakikishia Mhe. Mwakilishi, najua ananidai milioni moja pale. Kwa hivyo, tutawalipa wale wananchi wa Mkia wa Ng ombe. Kuhusu uhaba wa madaktari. Mhe. Spika, tutajaribu kulitatua tatizo hili. Mhe. Spika, halafu nakuja kwa Mhe Rashid Seif wa Jimbo la Ziwani, yeye ametaka kujua kwa nini hizi ambulance hazihudumii wagonjwa. Mhe. 26