Silaha Za Shetani. Ellis Forsman. Silaha Za Shetani (The Devices of Satan) 1

Similar documents
Watumishi Wa Kristo. Ellis P. Forsman. Watumishi Wa Kristo (Servants Of Christ) 1

"ATATOKEA MARA YA PILI, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu." Waebrania 9:28.

Nia Dhidi Ya Kristo Je Unamheshimu?

Agano Lililofunikwa Kwa Damu

MUNGU ALIUMBA ULIMWENGU 1 WETU NA VYOTE VILIVYO HAI

Kuwa Macho Na Mbwa Mwitu (Watch Out for Wolves)

Theolojia Ujumla. Mike Taylor Semester Munguishi Bible College

Kuiponya Picha Tuliyonayo Kuhusu Mungu

WAKOLOSAI MTAALA. B. Maoni: Tunapendekeza uwe na fafanuzi (commentary) yoyote yenye kushikilia mafundisho ya awali (conservative) katika Wakolosai.

Ushindi ndani ya Kristo W. W. PRESCOTT

walozaliwa, si kwa damu, wala mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, mbali kwa Mungu. Sisi sio tena binadamu wa kawaida tu kwa sababu sisi ni w

Mzabibu Na Matawi. (The Vine And The Branches) Ellis P. Forsman. Mzabibu Na Matawi (The Vine And The Branches) 1

MELKISEDECK LEON SHINE. katoliki.ackyshine.com

Kwa Nini Yesu Alikufa Msalabani?

GRACE COMMUNION INTERNATIONAL KANUNI YA IMANI

MUNGU ANADHIHIRISHWA KUPITIA KWA YESU KRISTO.

Maisha Ya Mkristo Ni Nini?

FORWARD BY DANIEL SZMIOT

Tazama Yuaja. Kuhusu Toleo Hili. Umuhimu wa Mafundisho ya Biblia. Nguvu katika neno la Mungu.

Maisha Yaliyojaa Maombi

JE, YAWEZEKANA KUISHI BILA KUTENDA DHAMBI?

B. Wanafunzi watapata ufahamu mkubwa wa kitabu hiki, na jinsi kinavyofundisha kuhusu kanisa.

Aina Tatu Za Ibada. Ellis Forsman. Aina Tatu Za Ibada (Three Kinds Of worship) 1

Inavyodaiwa na wanaochanganya Biblia. Ellis Forsman. Inavyodaiwa na Wanao changanya Biblia (Alleged Bible Contradictions) 1

WAFUNAJI WA NAFSI ABC By Vagn Rasmussen Translation by Lydia Madsen

Information for assessors (do not distribute this page to participants):

WEWE NI NANI? Toleo X Toleo Ukweli wa Injeli Toleo 23

Mafundisho Ya Msingi Wa Kikristo. Na Andrew Connally

Kifo Na Mbingu. (Death And Heaven) Ellis P. Forsman. Kifo Na Mbingu (Death And Heaven) 1

IMANI NA MATENDO ELLEN G. WHITE

Mukhtasari Wa Mabishano Kwa Na Dhidi Ya Vikombe Vingi Vya Ushirika

Tafuteni Kwanza Ufalme Wa Mungu

MSAMAHA NA UPATANISHO

Na Itafunika Wingi Wa Dhambi

Patanishwa, Hesabiwa Haki, Takaswa

Ndugu na dada zangu wapendwa,

BIBLICAL INSTRUCTION AND ENCOURAGEMENT FOR THE MAFUNDISHO YA BIBLIA NA HIMIZO KWA MISSION FIELD WORLDWIDE. KAZI YA KIMISHENI ULIMWENGUNI KOTE

NGUVU. Utangulizi. Yesu alisema,

Ndugu na dada zangu wapendwa,

VITAMBULISHO VITA NO DHA HIRI VYA KA NISA LA KWELI LA MUNGU ALIYE HAI

RISALA FUPI YA KUMUWEZESHA MTU KUPAMBANUA NI IPI DINI YA HAKI MWANDISHI: SALEH M. KYAMBO

Roho Mtakatifu Ni Nini?

Uongozi Siri Na Larry Chkoreff. Version 1.2 Desemba 2010

United Pentecostal Church June 2017

maombi, kabla tu hatujalifungua Neno hili la Kiungu.

UTARATIBU WA KANISA. 2 Jambo la kwanza ninalotaka kusema ni kwamba mchungaji. 3 Sisi tunaamini katika Kanisa la kimitume, tukifundisha

Ellen White, waasisi wa Kiadventista,na Sabato Lunar

Ndugu na dada zangu wapendwa,

Kifo Na Mbingu (Death And Heaven)

UKUFUNZI WENYE NGUVU MMOJA-KWA-MMOJA

KAMA MUNGU YU PAMOJA NASI, BASI YAKO WAPI MATENDO YAKE YA AJABU?

usudi la Maisha Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na kupishana usiku na mchana, kuna kweli ishara kwa wenye akili, ambaye mkumbuke-

Tumaini Kwa Afrika. Thomas Schirrmacher. Hoja 66. Dibaji na Prof. Mchungaji Dk. Thomas K. Johnson. Thomas Schirrmacher Tumaini Kwa Afrika TASCM RVB

ONYO LA MWISHO KWA DUNIA

UJASIRI WA YOHANA MBATIZAJI

Kanuni. Muhimu za Kujifunza Biblia. Mchungaji Drue Freeman. Dan Hawkins & Joseph Brown. General Editors.

Mabingwa kwa ajili ya tunda la Roho Mtakatifu. Iliyoendelea sana. Kitabu cha mwanafunzi. Iliyoendelea sana

LALA. Terry Warford. LALA (Sleep - Terry Warford) 1

Ufunguo wa Kutaalamika Haraka

Oktoba-Desemba

Sura ya 7 Kielelezo: Tumepatanishwa na Mungu na Wanadamu

PDF created with pdffactory trial version

Kiumbe Kipya Katika Kristo

JE! MUNGU ANAMPA MWANAMKE HAKI YA KUTOA MIMBA IWAPO NI MHANGA WA UBAKAJI?

UNABII WA BIBLIA. CBM Publishing 32 Blenheim Road, Far Cotton Northampton, England. NN4 8NW

MWONGOZO WA NAMNA YA KUHAMASISHA MAOMBI YA MCHANA NA USIKU YA SIKU 10.

Kufunga Milango - Uponyaji Kutokana na Athari za Giza

Kiu Cha umtafuta Mungu

Rahisi. Mabingwa kwa ajili ya tunda la Roho Mtakatifu. Kitabu cha mwanafunzi. Rahisi

UZAO WA NYOKA. 2 Basi, usiku huu, tuna malimbuko tu ya utukufu huo mkuu. 3 Kwa uchaji tunasimama kwa imani yetu katika Uwepo

Adhabu ya jino kwa jino na Musitakabali wa imani zetu

MAFUNDISHO YA UMISHENI

MASWALI NA MAJIBU JUU YA KITABU CHA MWANZO

YEHOVA-YIRE 1. 2 Baba yetu wa Mbinguni, tunakikaribia Kiti Chako cha. 3 Tunakushukuru kwa kutuzuru jana jioni. Tunaomba

Uponyaji Wa Laana. (Kumb. 28:1-14).

Juni 3-9 Pata Manufaa Kamili kwakusomabiblia

Kwa Kongamano Kuu 2016

United Pentecostal Church April Kushangilia Kwa Sala

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

MAHUBIRI TUNAYOWEZA KUONA

Rahisi. Kitabu cha mwanafunzi. Mabingwa kwa ajili ya tunda la Roho Mtakatifu. Rahisi

Mabingwa kwa ajili ya tunda la Roho Mtakatifu. Iliyoendelea sana. Iliyoendelea sana. Kitabu cha mwanafunzi

2 LILE NENO LILILONENWA

KWA NINI SISI SI MADHEHEBU?

MIAKA 500 YA MATENGENEZO YA KANISA NA USHUHUDA WETU Na Askofu Dr. Abednego Keshomshahara

KUTAMBUA SIKU YA KO NA UJUMBE WAKE

Haja Ya Dini. Author(s): Publisher(s): Translator(s): Category: Topic Tags: Featured Category: Published on Al-Islam.org (

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

Makasisi. Waingia Uislamu

Mabingwa kwa ajili ya tunda la Roho Mtakatifu. Ngumu. Ngumu. Kitabu cha mwanafunzi

Human Rights Are Universal And Yet...

# 18 Uponyaji Kutokana na Kukataliwa

Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya Tanzania

IM ETUPASA KUTIMIZA HA KI YOTE

Mwongozo wa Kanisa la Waadventista wa Sabato

KITABU CHA KUONGOZA FAMILIA

UNABII WA HABARI ZA BIBLIA

Kocha Mkuu. mabingwa. itakuwa INASTAHILI. Ili Kutoa mafunzo kwa wanafunzi wako kuwa. itakuwa ya kuumiza. Itachukua muda. Itahitaji moyo wa kujitoa.

Mwabudu Yehova, Mfalme wa Umilele. Miaka 100 ya Utawala wa Ufalme Inakuhusuje? UKURASA WA 12 NYIMBO: 97, 101. Kufanya Maamuzi ya Hekima Ukiwa Kijana

wasiofaa. Naomba sana kila raia afanye bidii awezavyo kumkaribia Mwenyezi Mungu vile anavyoona inafaa, lakini asipitishe hukumu juu ya wengine.

Transcription:

Silaha Za Shetani na Ellis Forsman Silaha Za Shetani (The Devices of Satan) 1

Silaha Za Shetani na Ellis Forsman Oktoba 15, 2012 Silaha Za Shetani (The Devices of Satan) 2

Silaha Za Shetani 2 Kor. 2:11 Paulo alipoandika barua yake ya pili kwa Wakorintho, alizungumzia uwezo wa Shetani kuweza kuchukua nafasi kwao. 2 Kor. 2:11, Shetani asije akapata kushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake. Aliwapasha habari Wakristo, hataivyo, hatupaswi kuwa katika nafasi ya kukutwa pabaya. Nafasi ya Shetani inategemea juu ya mmoja kukataa silaha zake. Lakini kama tukiwa tunafahamu mbinu ambazo Shetani anatumia kuwaongoza watu upotevuni, tunaweza kumshinda kwa mafanikio! Baadhi Ya Silaha Za Shetani ni zipi? Tunawezaje kujikinga dhidi yao? Katika somo hili tutajaribu kuyajibu maswali haya. Tunaanza na kutambua silaha za Shetani ambazo Paulo anaelezea baadaye katika waraka huu. Zinatia upofu akili za watu Ukiangalia hili neno silaha za shetani Kuna wengine ambao mungu wa dunia hii amewatia upofu. 2 Kor. 4:3-4, Lakini ikiwa Injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea; ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu. Roho alionya kwamba hili linapaswa kufanywa kupitia mafundisho ya mashetani. 1 Tim. 4:1-3, Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga nimani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe; waki wazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakulaambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli. Silaha Za Shetani (The Devices of Satan) 3

Leo hii, akili nyingi zimetiwa upofu katika kweli Kwa mafundisho ya WASIO MWAMINI MUNGU wanaamini kwamba hakuna Mungu. Kwa mafundisho ya MABADILIKO kimsingi sisi ni wanyama. Kwa mafundisho ya KIBINADAMU mwanadamu ndiye kipimo cha vitu vyote. Wale waliotiwa upofu wanabanwa katika kupokea ukweli. Kinga yetu bora dhidi yake Hakika ni kosa, kuhusisha vita kwa mawazo ya binadamu. 2 Kor. 10:3-5, Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili. (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zinauwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;) tukiangusha mawazo ya kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo; Silaha yetu kuu ni UKWELI, ambayo inaweza kushinda mabishano ya uongo na kuwaweka huru wale waliotiwa upofu katika utumwa. Yoh. 8:32, Nanyi mtaifahamu kweli, nayo kweli itawaweka huru. Hivyo, hitaji la kujadili, ili kuangusha chini mabishano. 2 Kor. 10:5, Tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo. Zingatia mfano wa Paulo, aliye shiriki mawazo yake na wengine. Mdo. 17:2-3, Na Paulo kama ilvyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo akahojiana nao kwa maneno ya maandiko sabato tatu, akiyafunua na kuwaeleza ya kwamba ilimpasa Kristo kuteswa na kufufuka katika wafu; na ya kwamba Yesu huyu ninayewapasha ninyi habari zake ndiye Kristo. Mdo. 19:8-9, Akaingia ndani ya sinagogi akanena kwa ushujaa kwa muda wa miezi mitatu, akihojiana na watu na kuwavuta katika mambo ya ufalme wa Mungu. Lakini wengine walikaidi, wakakataa kuamini wakiitukana ile Njia mbele ya mkutano; basi akaondoka akawaacha, akawatenga wanafunzi, akahojiana na watu kila siku katika darasa la mtu mmoja, jina lake Tirano. Silaha Za Shetani (The Devices of Satan) 4

Silaha zingine inahusisha TABIA INAYOFANANA NA YA KRISTO ambazo zinauwezo katika Mungu Upole na ukarimu wa Kristo. 2 Kor. 10:1-4, basi mimi Paulo mwenyewe nawasihi kwa upole na utaratibu wa Kristo; mimi niliye mnyenyekevu nikiwa pamoja nanyi, basi nisipo kuwapo ni mwenye ujasiri kwenu; naama, naomba kwamba nikiwapo, nisiwe na ujasiri kwa uthabiti ambao nahesabu kuwa nao juu ya wale wanaodhania kuwa sisi tunaenda kwa jinsi ya mwili. Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vitu kwa jinsi ya mwili; (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zinauwezo katika Mungu hatakuangusha ngome;) Tukiwa na subira na unyenyekevu katika kuwaonya wengine. 2 Tim. 2:24-26, Tena haimpasi mtumwa wa Bwana kuwa mgomvi; bali kuwa mwanana kwa watu wote, awezaye kufundisha, mvumilivu; akiwaonya kwa upole wao washindanao naye, ili kama ikiwezekana Mungu awape kutubu na kuijua kweli; wapate tena fahamu zao na kutoka katika mtego wa Ibilisi, ambao hao wametegwa naye, hata kuyafanya mapenzi yake. Efe. 4:15, Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa Kristo. Tunaweza kuzishinda silaha hizi za shetani! Silaha nyingine za Shetani ni ku Kuwapata watu wamejinasa katika mambo ya dunia Ukizingatia hili silaha ya Shetani Ninazungumzia vitu vile vilivyoongelewa katika: 1 Yoh. 2:15-17, Msiipende dunia wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia kumpenda Baba hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. Na dunia inapita pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu milele. Tamaa ya mwili. Tamaa ya macho. Kiburi cha uzima. Silaha Za Shetani (The Devices of Satan) 5

Shetani alitumia mbinu hizi dhidi ya HAWA. Mwanzo 3:6, Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe naye akala. Alichokiona kilikuwa kizuri (tamaa ya mwili). Kilikuwa kinapendeza macho (tamaa ya mwili). Kilikuwa kinatamanika kwa maarifa (kiburi cha uzima). Shetani pia alizijaribu mbinu hizi katika kumjaribu Yesu. Mat. 4:1-11, Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi. Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa. Mjaribu akamwijia akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate. Naye akajibu akisema, Imeandikwa, mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu. Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu, akamwambia Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; na mikononi mwao watakuchukua; usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. Yesu akamwambia, Tena imeandikwa Usimjaribu Bwana Mungu wako. Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake, akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia. Ndipo Yesu alipomwambia, nenda zako Shetani; kwa maana imeandikwa msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye pekee yake. Kisha Ibilisi akamwacha; na tazama wakaja malaika wakamtumikia. amuru kwamba mawe haya yawe mikate (kiburi cha uzima). Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini (kiburi cha uzima). Haya yote nitakupa, kama (tamaa ya macho). Leo, shetani anatumia mbinu hizi kwa kisasi, akijaribu watu kupitia Ufisadi (tamaa ya mwili). Mambo ya kimwili (tamaa ya macho). Kiburi (kiburi cha uzima). Kinga yetu bora dhidi yake Tujae sisi wenyewe na Neno la Mungu! Hivi ndivyo Yesu alivyoshinda majaribu yaliyoletwa kwake na shetani. Silaha Za Shetani (The Devices of Satan) 6

Angalia jinsi alivyojibu kila jaribu kwa kusema Imeandikwa. Mat. 4:4, Naye akajibu akisema imeandikwa mtu hataishi kwa mkate tu ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu. Mat. 4:7, Yesu akamwambia tena imeandikwa usimjaribu Bwana Mungu wako. Mat. 4:10, Ndipo Yesu alipomwambia, nenda zako shetani; kwa maana imeandikwa msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye pekee yake. Jenga upendo wenye nguvu kwa Baba! Maana upendo huo haushikamani na upendo wa dunia. 1 Yoh. 2:15, Msiipende dunia wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia kumpenda Baba hakumo ndani yake. Mtu hawezi kuwa rafiki wa dunia na aulinde urafiki na Mungu. Yak. 4:4, Enyi wazinzi hamjui ya kumba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu. Kwa kujaa wenyewe na Neno la Mungu na kuwa na nguvu katika upendo wetu kwake, tutajitoa kwake kikamilifu na kuwa tayari kumshinda shetani, tukimsababisha akimbie! Yak. 4:7, Basi mtiini Mungu Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. Vile vile, tusifikiri shetani atajiuzulu kirahisi; kuna silaha zingine juu ya ukosi wake, pamoja na Kuwatesa wale wanaojaribu kutenda haki Ukizingatia silaha hii ya shetani Petro alionya kwamba shetani anatafuta kuwa meza Wakristo kupitia mateso. 1 Pet. 5:8-9, Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye huzunguka zunguka, akitafuta mtu ammeze. Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kuwa mateso yale yale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani. Paulo aliogopa mateso yaliyoletwa kwake na shetani kwamba yangeweza kuwatesa pia Wathesalonike na wakajiuzulu. 1 Thes. 3:1-5, Basi kwa hiyo tulipokuwa hatuwezi kuvumilia zaidi, tuliona vyema kuachwa Athene pake yetu. Tukamtuma Timotheo ndugu yetu, mtumishi wa Mungu katika Injili ya Kristo, ili kuwafanya ninyi imara Silaha Za Shetani (The Devices of Satan) 7

na kuwafariji kwa habari ya imani yenu; mtu asifadhaishwe na dhiki hizi; maana ninyi wenyewe mnajua ya kuwa twawekewa hizo. Kwa kuwa tulipokuwapo kwenu tulitangulia kuwaambia kwamba tutapata dhiki, kama ilivyotukia nanyi mwajua. Kwa hiyo mimi nami nilipokuwa siwezi kuvumilia tena, nalituma mtu ili niijue imani yenu, asije yule mjaribu akawajaribu, na taabu yetu ikawa haina faida. Hata leo, Shetani anawatesa Wakristo! Zingine kiualisi, kupitia mateso makuu ya Wakristo. Zingine kupitia msukumo wa kijamii ambayo mara nyingi hutenda kazi sawasawa. Msukumo. Kuzomewa. Utenganifu. Kinga yetu bora dhidi yake Kuhimiza kila mmoja! Hiki ndicho Petro alichagua kufanya. 1 Pet. 5:8-10, Mwe na kiasi na kukesha kwa kuwa mshiataki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye huzunguka zunguka, akitafuta mtu ammeze. Nanyi mpingeni huyo mkiwa dhabiti katika imani mkijua ya kuwa mateso yale yale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani. Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, na kuwathibitisha na kuwatia nguvu. Paulo alimtuma Timotheo afanye ivyo hivyo. 1 Thes. 3:2-3, Tukamtuma Timotheo ndugu yetu, mtumishi wa Mungu katika Injili ya Kristo ili kuwafanya ninyi imara na kuwafariji kwa habari ya imani yenu; mtu asifadhaishwe na dhiki hizi; maana ninyi wenyewe mnajua ya kuwa twawekewa hizo. Jenga tabia njema: Furahi! Ukijua kwamba majaribu yanaweza kutufanya imara. Yak. 1:2-4, Ndugu zangu hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mabali mabali; mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno. Silaha Za Shetani (The Devices of Satan) 8

Rum. 5:3-4, Wala si hivyo tu ila na mfurahi katika dhiki pia; mkijua ya kuwa dhiki kazi yake ni kuleta saburi; na kazi ya saburi ni uthabiti ni uthabiti wa moyo; na kazi ya uthabiti wa moyo ni tumaini; Mkijua ya kuwa wale wanaovumilia ubarikiwa na Mungu. 1 Pet. 4:12-14, Wapenzi msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho. Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe. Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni heri yenu; kwa kuwa Roho wa utukufu na wa Mungu anawakalia. Mat. 5:10-12, Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; maana ufalme wa mbinguni ni wao. Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu. Furahini na kushangilia; kwa kuwa dhawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu. Jiingize mwenyewe kwa Mungu katika kufanya mema. 1 Pet. 4:19, Mkaribishane ninyi kwa ninyi, pasipo kunung unika; Mungu ni Muumbaji mwaminifu. Anazingatia mateso yetu, na siku moja atawalipa wale wanaotusumbua (pamoja na Shetani mwenyewe!), na kutupatia pumziko. 2 Thes. 1:4-8, Hata na sisi wenyewe twaona fahari juu yenu katika makanisa ya Mungu kwa ajili ya saburi yenu, na imani mlio nayo katika adha zenu zote na dhiki mnazostahimili. Ndiyo ishara hasa ya hukumu iliyo haki ya Mungu, ili mhesabiwe kuwa mwastahili kuuingia ufalme wa Mungu, ambao kwa ajili yake mnateswa. Kwa kuwa ni haki mbele za Mungu kuwalipa mateso wale wawatesao ninyi; na kuwalipa ninyi mteswao raha pamoja na sisi; wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake katika mwali wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu na wao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu; Ufu. 20:10, Na yule ibilisi mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele. Kuna silaha nyingine ya Shetani, ambazo maranyingi huwa na madhara ya kuuwa Silaha Za Shetani (The Devices of Satan) 9

Kuwafanya watu wafurahie urafiki wa uovu Ukizingatia hili silaha ya Shetani Mazungumzo yasiyo sahihi inaweza kuzuia juhudi za mtu katika kutenda mema. 1 Kor. 15:33, Msidanganyike mazungumzo mabaya huaribu tabia njema. Amnoni aliongozwa vibaya na mshauri wa rafiki, yake Yonadabu. 2 Sam. 13:1, Ikawa baada ya hayo, Absalomu mwana wa Daudi, alikuwa na umbu mzuri, jina lake akiitwa Tamari, naye Amnoni mwana wa Daudi akampenda. Leo, Wakristo wengi wanabanwa katika ukuaji wao wa kiroho Kwa urafiki wanaotunza. Kwa shughuli ambazo rafiki hao wanahusika nazo. Kinga yetu bora dhidi yake Kutambua hatari ya marafiki wasio sahihi. Mith. 13:20, Enenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima; bali rafiki wa wapumbavu ataumia. Shika ushauri ambao Paulo aliwapa Wakorintho: 2 Kor. 6:14-16, Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? Tena pana patano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. 2 Kor. 6:17-18, Kwa hiyo tokeni kati yao, mkatengwe nao, asema Bwana, msiguse kitu kilicho kichafu, nami nitawakaribisha. Nitakuwa Baba kwenu, nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike, asema Bwana Mwenyezi. Silaha Za Shetani (The Devices of Satan) 10

2 Kor. 7:1, Basi wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu. Mwisho, hebu tuangalie silaha moja zaidi ya Shetani Inawavunja watu moyo kupitia waenda kanisa wasiofanana na Kristo Kuzingatia hii silaha ya Shetani Hii inafanana na kuhusika kwa Paulo katika kifungu chetu. 2 Kor. 2:6-11, Yamtosha mtu wa namna hii adhabu ile aliyopewa na walio wengi; hata kinyume cha hayo, ni afadhali mmsamehe na kumfariji, mtu kama huyo asije akamezwa katika huzuni yake ipitayo kiasi. Kwa hito nawasihi kumthibitishia upendo wenu. Maana naliandika kwa sababu hii pia, ili nipate bayana kwenu kwamba mmekuwa wenye kutii katika mambo yote. Lakini kama mkimsamehe mtu neno lo lote, nami nimemsamehe mtu neno lo lote, nimemsamehe kwa ajili yenu mbele za Kristo, Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake. Ndugu aliyetenda dhambi aliadabishwa, na akatubu. Hitaji sasa lilikuwa la kanisa kuthibitisha upendo wao na msamaha. Lasivyo, shetani anaweza kuchukua nafasi katika hali hii. Kulishinda kanisa kwa kutokupenda kwao kutokusamehe. Kumshinda ndugu mdhaifu kwa kumezwa kwake katika huzuni kama msamaha haukutolewa na kusanyiko. Leo, shetani wakati mwingine anapata nafsi kwa silaha hii. Wakristo ambao hawapendi wenzao, hawana huruma, na hawasamei wanakuwa kikwazo kwa wengine. Wakristo wanaopenda, wakarimu, katika huduma zao na kujitoa kwao kwa Mungu, wanathamani ya mvuto kwa Wakristo wapya. Kinga yetu bora dhidi yake Kuweka imani yetu kamili kwa Bwana, sio kwa wandugu. 2 Tim. 4:16-18, Katika jawabu langu la kwanza hakuna mtu aliyesimama upande wangu, bali wote waliniacha naomba wasihesabiwe hatia kwa jambo hilo. Lakini Bwana alisimama pamoja nami akanitia nguvu, ili kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu hata Silaha Za Shetani (The Devices of Satan) 11

wasikie Mataifa yote; nami nikaokolewa katika kinywa cha simba. Bwana ataniokoa na kila neno baya, na kunihifadhi hata nifike ufalme wake wa mbinguni. Utukufu una yeye milele na milele. Amina. Hii sio kupendekeza kwamba ndugu hawawezi kuaminiwa. Lakini ndugu wanashindwa, Bwana hashindwi! Kumbuka, kwamba siyo ndugu wote walio na mfano thabiti. 3 Yoh. 1:9-12, Naliliandikia kanisa neno, lakini Diotrefe, apendaye kuwa wa kwanza kati yao, hatukubali. Kwa hiyo nikija nitayakumbuka matendo yake atendayo, atoavyo upuzi juu yetu kwa maneno maovu; wala hatoshwi na hayo, ila yeye mwenyewe hawakaribishi hao ndugu na wale watakao kuwakaribisha, huwazuia na kuwatoa katika kanisa. Mpenzi, usiuige ubaya, bali uige wema. Yeye atendaye mema ni wa Mungu, bali yeye atendaye mabaya hakumwona Mungu. Demetrio ameshuhudiwa na watu wote, tena na ile kweli yenyewe. Nasi pia twashuhudia nawe wajua ya kwamba ushuhuda wetu ni kweli. Hitimisho Hii siyo orodha inayotisha, bali ni chembe chembe ya Silaha za Shetani. Maandiko kimsingi inafunua mengi zaidi kuhusu jinsi Mdanganyifu Mkuu atendavyo kazi. Ninaamini somo hili limekuwa dhahiri kuonyesha silaha za shetani, hataivyo Adui wetu hakika ananguvu. Ugumu wa silaha zake unatufanya tukae pembeni. Kama hatuweki bidii, hakika atatusumbua! Kumbuka, kwamba, maneno haya muhimu ya mtume Paulo Efe. 6:10-13, Hatimaye mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu war oho. Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote kusimama. Silaha Za Shetani (The Devices of Satan) 12

Silaha Za Shetani (The Devices of Satan) 13

Silaha Za Shetani (The Devices of Satan) 14

Silaha Za Shetani (The Devices of Satan) 15

Silaha Za Shetani (The Devices of Satan) 16