KILIMO CHA VITUNGUU MAJI NA VITUNGUU TWAUMU (SWAUMU)

Similar documents
pages/mkulima-mbunifu/

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees

2 Usimamizi wa Rutuba ya Udongo Tanzania Organic Agriculture Movement

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Uzalishaji wa mboga na matunda ni muhimu kwa afya na kipato

Ni kwa nini mkulima awe maskini?

Uhakika wa Mbegu kwa Uhakika wa Chakula MWONGOZO WA UZALISHAJI WA MBEGU ZA ASILI ZA MAHINDI

TIST HABARI MOTO MOTO

Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

KUZALISHA MBEGU YA MAHARAGE KIJITABU CHA KWANZA

MBINU ZA IPM KWENYE KILIMO CHA KAHAWA

Information for assessors (do not distribute this page to participants):

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

TIST HABARI MOTO MOTO. Benefits of Loan Repayment. Faida za ulipaji wa mikopo U OTESHAJI W A M ITI Y A M ATUNDA

4 WADUDU,MAGONJWA NA MAGUGU

Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI VIDOKEZO MUHIMU KATIKA UNUNUZI NA USALAMA WA CHAKULA

Shamba Darasa na Stadi za Maisha kwa Vijana (SDSMV) Tanzania. Kiongozi Cha Mwezeshaji. Jaap Van Pol na Francesca Dalla Valle

Uwepo, Athari na Udhibiti wa Sumu-Suvu Kwenye Vyakula vya

MTI KWA MATUMIZI YA KILA AINA HDRA

Utangulizi wa ugonjwa wa shinikizo la damu

TIST HABARI MOTO MOTO MAANDALIZI YA MWAKA 2000 Y2K PREPARATIONS SASA NI WAKATI WA KUANZA KUPANDA MBEGU ZAKO

MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA. Kwa Wanaoanza

Kilimo cha kiekolojia cha Wakulima Wadogo Hufanikisha Haki za Mazingira

Muongozo wa utatuzi. Kwa wasimamizi wa malaria RDTs 06/11/16. MALARIA Rapid Diagnostic Test

UMRI WA MAKAMO NA KUKOMA KWA HEDHI

Bustani 10,000 Katika Afrika. Alberto Prina

Human Rights Are Universal And Yet...

Hatari, Haki za Usalama katika Bahari 03

Teknolojia za Utayarishaji, Usindikaji na Matumizi ya Matunda na Mboga baada ya kuvuna

Uzio wa pilipili unazuia tembo kuvamia mazao shambani! Jinsi ya kujenga na kudumisha uzio wa pilipili Tanzania

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti

Vyote Unavyopaswa Kujua Kuhusu Viazi Vitamu

ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA UCHUMI WA ZANZIBAR

Muhtasari wa taarifa ya warsha ya wataalamu juu ya mfumo wa habari kwa njia ya ramani (PGIS), Morogoro, Juni 30 - Julai 1, 2014

Kuwa na Ukimwi ni kama vile kutakiwa kuendelea kuuzima moto unaoniunguza bila kukoma.

Upande 1.0 Bajeti yako

PYRINEX. 1 Liter INSECTICIDE

Mwongozo wa Kitaifa wa Ujumbe wa Uzazi wa Mpango

Wadudu na magonjwa ya mazao

Siku ya kwanza. Mguso wa ngozi-kwa-ngozi (Ulezi wa kangaruu) Mtoto wako anaweza kuhisi mdundo wa moyo wako

Kuwawezesha wasichana kwa kuboresha kujikubali na kujithamini Hivi Ndivyo Nilivyo

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

AMMA KWA AFRIKA RATIBA/ITIKADI. Ratiba Maalum ya Kutibu Magonjwa Maambukizi na Hususan Fikra Zinazoleta Pooza Mwili na Akili

Jamii. ,,,^mm^mmm-<^^^^ illli MA RH-EREN.CE CENTRE

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

Picha ni hati miliki ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Watoto(PCD), Imperial College London. Maelezo

Utunzaji, Uhifadhi na Usafirishaji Bora wa Maziwa

Kubadili Sheria Za Mbegu Na Ulinzi Wa Aina Za Mbegu Na Mimea Nchini Tanzania

UFUPISHO WA 35. Hali ya kiulimwengu ya Tekinolojia ya kibiashara/ugeuzi jeni na uboreshaji mazao: Clive James Chair, ISAAA Board of Directors

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig

KUPWA NA KUJAA KWA BAHARI. (TIDES AND TIME)

Pronunciation: Mä-hret Zäläke Ndal-ka-tscho Molla Mare Gebre-gzabiär 1/12

Mwongozo wa Jamii juu ya Afya ya Mazingira

5. Mheshimiwa Spika, Bunge lako Tukufu lilijadili kwa kina Miswada ifuatayo:

Wewe Maisha Yako Ndoto Zako. Kitabu cha Vijana Balehe

Vyote Unavyopaswa Kujua Kuhusu Viazi Vitamu

Kifaa Maalum cha Kutazamia Jua: Maelekezo ya kutumia

Uzazi wa Mpango. Uzazi wa Mpango. Kulinganisha Ufanisi wa Njia za Uzazi wa Mpango. iwe na ufanisi zaidi. Zenye ufanisi.

TANZANIA MARKETS PAN Sera zinazoboresha masoko

Njia Bora za Ukusanyaji na Upimaji Maziwa

muhtasari 37 brief 37 Kiwango cha kiutandawazi cha mazao ya kibiashara ya kibayoteki/ugeuzi jeni: 2007 Clive James Bordi ya wakurugenzi wa ISAAA

International Labour Office. Kazi za Ndani Zenye Madhara kwa Watoto: Kijitabu cha Maelezo Mafupi

Mukhtasari Wa Mabishano Kwa Na Dhidi Ya Vikombe Vingi Vya Ushirika

KUWEZESHA MBINU ZA UZUIAJI MIMBA KATIKA SUHULA ZA AFYA: MASWALI 10 KWA VIKUNDI VYA JAMII KUZINGATIA

Mfumo na maelezo ya kina ya mpango wa kimataifa wa viwango vya chakula kwa wenye matatizo ya kumeza (IDDSI) Juni 2017

MACHAGUO YA UZAZI KUFIKIRIA KUWA MZAZI

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA

Issue No.1 Morogoro school of journalism May Salma :Wanachuo lipeni ada kwa wakati

TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM)

Lesson 11 Weather and Seasons Hewa Majira

Miradi na jamii. 3.1 Utangulizi

Mwongozo huu wa ufugaji kuku wa Asilia umezinduliwa rasmi leo tarehe 1 Agosti 2009 wakati wa sikukuu ya Wakulima Tanzania mjini Mbeya

Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2013

Njia bora za ukusanyaji na upimaji maziwa

HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu WEMA

Njia za upimaji wa mpango wa kimataifa wa viwango vya chakula kwa wenye matatizo ya kumeza (IDDSI) VYAKULA VINYWAJI VYA KAWAIDA

Mwongozo wa Kutathimini mifumo ya Ugawanaji wa faida na Mapato Katika Miradi ya Jamii ya MKUHUMI

N09/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q

Ufunguo wa Kutaalamika Haraka

K. M a r k s, F. E n g e l s

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA, KWA WANANCHI, TAREHE 31 JULAI 2001

NGUO MPYA ZA UKOLONI. Mikataba ya Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Umoja wa Ulaya na Afrika. Agosti 2017

UNABII WA BIBLIA. CBM Publishing 32 Blenheim Road, Far Cotton Northampton, England. NN4 8NW

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU

Alama za maelezo. mastakimu. dimbwi. kidimbwi. mto. kijito. ndani mchangani / chini ya ardhi. mchana / usiku. mchana. usiku

Kijitabu cha Maelezo cha Programu ya Famasia

Mutugi Kamundi. Jemma Kahn. Kiswahili. Demane na pacha wake. Author - South African Folktale

ONDOA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA AFYA YA WATOTO

Yaliyomo. Kuhusu kitabu hiki. Hautakuwa peke yako. Mfumo wa msaada ni wa manufaa sana wazazi wote wanahitaji!

MTIHANI WA MWIGO WILAYA YA BUTERE MUMIAS-2007 Hati ya kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya

JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

Usimulizi wa Riwaya ya Nyongo Mkalia Ini E. S. MOHOCHI University of Egerton, Kenya

Dodoma ambako kikao cha Bunge kinaendelea kuja kushiriki japo sehemu ya uzinduzi wa mkutano.

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO

CGAP Smallholder Household Survey in Tanzania / Utafiti wa kaya ndogondogo Tanzania

MAADHIMISHO YA MIAKA 15 YA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

Programu ya Uendelezaji Mifumo ya Maji Vijijini (PUMMV) katika Tanzania. Modeli wa Ukodishaji Mradi

Transcription:

2016/2017 TEMBELEA ACKYSHINE.COM/SHOP KUPATA MAJARIDA MENGINE KILIMO CHA VITUNGUU MAJI NA VITUNGUU TWAUMU (SWAUMU) Kutoka ackyshine.com/shop Melkisedeck Shine

KILIMO CHA VITUNGUU (VITUNGUU MAJI) Vitunguu ni zao la mbogamboga na hulimwa kwa ajili ya balbu zake ambazo hutumika kama kiungo cha chakula. Vitunguu vina matumizi mengi sana na vina madini joto, chuma, vitamin A, vitamin B, vitamin C na vitamin E. Vitunguu hulimwa na hukubali zaidi nyanda za baridi. Nyanda zenye joto vitunguu hulimwa pia. Vitunguu vinaweza kulimwa mwaka mzima endapo maji yanapatikana. Aina za vitunguu vinavyolimwa tanzania Red Creole Bombay Red Hybrid F1 Hali ya hewa Joto linatakiwa sana kwa ajili ya ukuaji wa balbu ila joto likizidi vitunguu hukomaa mapema kabla balbu hazijafikia ukubwa unaostahili, hivyo mkulima anaweza kupata mazao kidogo. Udongo Vitunguu huweza kupandwa kwenye udongo wowote wenye rutuba, usiotuamisha maji na usionata sana. Hufanya vizuri kwenye udongo wenye asidi kidogo japo udongo wenye alkali kidogo sio mbaya sana. Kwenye udongo wenye mchanga mchanga umwagiliaji ni lazima. Udongo mzuri sana kwa ustawi wa vitunguu ni tifutifu-kichanga. Mbolea Epuka matumizi ya mbolea mbichi isioiva vizuri kwani husababisha vitunguu kuwa na shingo pana sana majani hukua sana badala ya balbu. Tembelea ackyshine.com/shop Kupata majarida mengine KILIMO CHA VITUNGUU (VITUNGUU MAJI) 2

Umwagiliaji [KILIMO CHA VITUNGUU MAJI NA VITUNGUU TWAUMU Umwagiliaji ni muhimu sana hasa wakati wa kuanza kutengeneza balbu. Unyevu uliozidi ni hatari sana kipindi cha ukuaji. Kitalu cha vitunguu Ni muhimu kumwagilia maji ya kutosha siku kumi za mwanzo tangu kusia mbegu kitaluni. Vitunguu hukaa kitaluni kwa wiki 6-8 na miche ifikiapo upana wa penseli na urefu wa sm 15 ni tayari kwa kuhamishia shambani/bustanini. Upandaji Kabla ya kupanda udongo ni lazima utifuliwe vizuri na reki kuondoa mabaki ya mimea na mawe ama Vipande vikubwa vya udongo. Matuta yawe na upana wa mita moja. Vitunguu hupandwa kwa mstari mojakwamoja ama kutokea kitaluni. Pia huweza kupandwa kwa mstari pacha. Vitunguu hupandwa sm 10-15 kutoka mmea hadi mmea na sm 10-15 kutoka mstari hadi mstari, kama inavyoonekana kwenye mchoro hapa chini. Pia epuka kupanda vitunguu mahali palipopandwa mboga jamii ya vitunguu siku za nyuma. Mfano Vitunguu saumu na vitunguu majani. Utunzaji wa shamba Kutandazia shamba na majani yaliyooza vizuri ama mabua inashauriwa ili kuongeza ruba ya ardhi, zuia magonjwa yatokanayo na udongo na magugu. Kupanda vitunguu kwenye matuta yaliyoinuka ni muhimu sana kuzuiya utuamishaji wa maji na mlipuko wa magojwa ya miche. Kungoa magugu na uvunaji ufanywe kwa mkono. Vitunguu hufanya vizuri kama shamba litawekewa mbolea ya samadi ama mboji ilioiva vizuri. Kiasi cha tani 25-40 kwa heka kinashauriwa. Hii ni sawa na kilo 7.5-12 kwa tuta lenye urefu wa mita 3 na upana wa mita 1. Tembelea ackyshine.com/shop Kupata majarida mengine KILIMO CHA VITUNGUU (VITUNGUU MAJI) 3

Uvunaji Vitunguu huvunwa kuanzia siku 90-150 tangu kusia mbegu. Dalili za kukomaa ni kuanguka kwa majani. Vitunguu huvunwa kwa kuvuta kwa mkono na kuhifadhiwa siku kadhaa shambani vikiwa vimefunikwa na majani. Baada ya hapo majani hukatwa na balbu hupakiwa kwa ajili ya kuhifadhi kusubiria bei nzuri. Vitunguu huweza kuhifadhiwa hadi miezi 9 tangu vivunwe bila kuharibika. Vitunguu vihifadhiwe kwenye nyuzijoto chini ya 4.4 C ama juu ya nyuzijoto 25 C ili visiharibike. KILIMO CHA VITUNGUU TWAUMU (SWAUMU) Vitunguu twaumu viungo vinavyopendwa na watu wengi hasa kwa harufu yake nzuri Kwenye chakula na uwezo wake wa kuondoa harufu mbaya Kwenye chakula (shombo). Vile vile vitunguu twaumu vinatumika kama tiba mbadala ya maradhi mbalimbali. Jinsi ya kulima vitunguu twaumu Aina nyingi za vitunguu twaumu vitakuwa kama vinatoa mbegu kwenye mmea ingawa kuna nadharia nyingi lakini inashauriwa kukata hizi mbegu chini kabisa kwa kisu kikali na kisafi, usikate mapema mara baada ya kutokeza bali subiri mpaka mmea unapoanza kama kujikunja ndipo ukate. Mbegu hizi kwa kawaida zikipandwa kwa msimu wa kwanza zitazaa kitunguu kimoja tu cha duara lakini chenyewe ukikipanda tena kwenye mzunguko wa pili kitazaa vitunguu vingi kama kawaida. Mahitaji ya udongo Vitunguu twaumu vinahimili aina nyingi za udongo, ila vinastawi zaidi katika udongo usiotuamisha maji kabisa na wenye mbolea asili, kama mbolea si ya kutosha kwenye udongo, tumia samadi iliyokwisha oza vizuri usitoe samadi bandani na kuipeleka shambani moja kwa moja kwenye shamba la vitunguu thwaumu, labda kama utaliacha shamba bila kulimwa kwa zaidi ya miezi 6, pia unaweza kutumia mbolea za viwandani kama ammonium nitrate, Tembelea ackyshine.com/shop Kupata majarida mengine KILIMO CHA VITUNGUU TWAUMU (SWAUMU) 4

ammonium sulphate, urea n.k wakati wa kupanda na kila baada ya wiki 4 6 mara mbili zaidi Kupanda Kipindi kizuri kwa upandaji ni kipindi ambacho hakuna joto. Uotaji mzuri hutegemea pia namna vitunguu thwaumu vilivyo hifadhiwa kabla ya kupandwa, kama vilihifadhiwa sehemu zenye joto na hewa finyu uotaji wake utakuwa duni na dhaifu. Unachukua kitunguu twaumu na kutenganisha vitunguu kimoja kimoja (bulbs) na kuchagua vile vikubwa maana hivi ndivyo vitakavyo kupa mazao mengi na bora, nafasi kati ya kitunguu na kitunguu ni sentimeta 10 na kati ya mistari ni sentimeta 30. Baada ya kupanda pandishia udongo na uukandamize kuhakikisha kwamba kimekaa vizuri na hakiwezi kuathiriwa na mvua au maji wakati wa kumwagilia ili kisikae upande au kungolewa kabisa. Palizi Ungoleaji wa magugu na majani ni muhimu muda wote ili kuondoa kugombea rutuba, hewa na maji shambani, kwa wenye mashamba makubwa wanaweza kutumia dawa za kemikali kama ROUNDUP na nyinginezo ili kudhibiti magugu. Umwagiliaji Kwa kipindi chenye upungufu wa mvua au ni kipindi cha kiangazi ni vizuri ukamwagilia vitunguu twaumu ni asubuhi na sio jioni au mchana, hii inasaidia vitunguu twaumu kujijengea uwezo wa kupambana na magonjwa, baada ya mizi miwili unaweza kupunguza umwagiliajai huku ukiangalia kwa kuchimba kidogo kama vitunguu twaumu vimezaliana vya kutosha na kuanza kukomaa, ukiona vimekomaa acha kabisa kumwagilia ili visioze Magonjwa Magonjwa kama botrytis (kuoza shingo) blue mould na fusarium (kuoza kwa vitunguu) husababisha hasara kubwa kama hayatadhibitiwa kwa kutumia viuatilifu mara unapoona dalili, pia magonjwa kama white rot huchukua zaidi ya miaka 20 kuondoka kama yatavamia shamba lako, inashauriwa kufanya mabadiliko ya zao kila baada ya miaka mitano kwa kupanda mazao mengine yasiyo jamii moja kama vitunguu maji, unaweza kupanda maharage, mahindi, karoti na kabichi katika mzunguko huo. Pia magonjwa kama kutu ya majani husababisha na unyevu Tembelea ackyshine.com/shop Kupata majarida mengine KILIMO CHA VITUNGUU TWAUMU (SWAUMU) 5

mwingi hasa kama mimea itakuwa kwenye udongo unaotuamisha maji au mimea kumwagiliwa jioni au usiku. Kudhibiti magonjwa Tumia viuatilifu vinavyotakiwa kwa ugonjwa husika na pia kumbuka kumwagilia asubuhi tu Ili kudhibiti ugonjwa huu wa kutu mimea ingolewe na ichomwe au utumie viuatilifu vya kuulia fangasi wa mimea. Copyright All Rights Reserved, Ackyshine. 2016. Tembelea ackyshine.com/shop Kupata majarida mengine 6