102/3 KISWAHILI FASIHI KARATASI YA 3 JULAI/AGOSTI 2011 MUDA: 2 ½ Kiswahili Fasihi Hati ya Kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya.( K.C.S.E) MAAGIZO Jibu maswali manne pekee Swali la kwanza ni lazima Maswali hayo mengine matatu kutoka sehemu nne zilizobaki yaani, tamthilia,riwaya, Ushairi na fasihi simulizi. Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja. Karatasi hii ina kurasa 4 zilizopigwa chapa. Watahiniwa ni lazima waangalie kama kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo. Nyamira- 11 kidato cha nne 1
SEHEMU YA A: HADITHI FUPI MAYAI WAZIRI WA MARADHI: K.W Wamitila. 1. LAZIMA.. Ni. Nisubiri kidogo mpenzi.. naja hivi punde tuyamaliza uyasemayo. a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (ala 4) b) Anayosema mnenewa yanaashiria matatizo yanayomkumba. Jadili kwa kutoa mifano kitabuni manne ya matatizo hayo ambayo pia ni matatizo yanayoikumba jamii. (ala.8) c) Ni vipi matatizo hayo yanavyoweza kusuluhishwa? (ala.8) SEHEMU YA B : RIWAYA Jibu swali la 2 au la 3 S.A Mohamed : UTENGANO 2. Shoga Futoni ni Futoni kweli, mambo yake ni mfutofuto, hakuna mtaji mkubwa hata hivyo kwa mimi na wewe.... a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (ala.4) b) Eleza jinsi njia alizotumia kujipatia riziki mnenewa zilivyomtia mashakani (ala. 10) c) Eleza jinsi mnenewa hakubadilisha maisha yake. (ala.6) au 3. Huku ukitoa mifano onyesha jinsi mwandishi amefaulu katika matumizi ya mbinu zifuatazo za sanaa: (i) Rejea (ala.10) (ii) Sadfa (ala.10) SEHEMU YA V: USHAIRI 4. Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata. UTII Raia Mwema ni yule, aliyejaa utii, Si ubishi na kelele, akanywalo hasikii, Ni mwasi huyo jinale, achunguzwe kwa bidii, Uonapo uhalifu, usambe huuzuii, Ndio huo uvunjifu, kamawe huzingatii Mwananchi mwadilifu,hilo halikadirii Utii kama haupo,sheria haziagii Nyamira- 11 kidato cha nne 2
Maswali. Imani huwa haipo, na mema hayatujii Usalama hufa papo, mara nchi ikadhii Nia za watu watano, ambazo hazififii Uchao ni tangamano, si chusa hawachukii Hushinda kumi na tano, ambao hawatulii Raia asiyetii, ni fasidi wa nchiye. Kila raia nchini, ni ile au ni hii Ana hisa wastani,ingawa haitumii Hazuiliwi hanani,kusema hatumbukii. (a)taja sifa mbili za raia Mtiifa. (ala. 2) (b) Ni mambo gani ambayo hutokea wananchi wanapokosa utii? ( ala.2) (c) Eleza ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari ( ala 4) (d) Onyesha mbinu mbili zilizotumiwa ili kuonyesha uhuru wa mtunzi,kwa kutolea mifano.( ala.2) (e) Hili ni shairi la aina gani? Toa sababu. ( ala.2) (f) Eleza muundo wa shairi. (alam 4) (g) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi. (i) Mwasi (ii) haziagii (iii) Tangamano (v) hisa 5. Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata. Wana haramu Hebu nikuulize mama Afrika Kwa nini Mimba changa ukajichukulia Ya haramu sana ilotepetea Ukazaa wana walo jahilia Wasiojijua, wala yao njia? Kuzurura ukamalizikia Bila muruwa, heba kukupotea Ukawa ganda la kupita njia Usije maoni ya kuonelea? Kwa nini.. Ukazaa kizazi kilo kiwete Kilihasirika kwa wakati wote Kilichopagawa kwa kingi kite (ala.4) Nyamira- 11 kidato cha nne 3
Hata utu wake ukakipotea? Ah moyo waumia! Hupigwa na mshangao Niwafikiriapo Wale barobaro wanao Wasaliti wanati walo na vyeo Walomdhidi mama mzazi wao Kwa muradi wao. Lakini sijali Sijali kwani najua Siku moja itawadia Wanaharamu watajihalalia Kila cha haramu kukuondolea Na kukurakasa.. Mama wasikia? Hiyo siku ya siku itakapofika Kila la dhuluma litajikatika Na kila mahali utadhihirika Mwisho wa salata na uharamia. Mama wasikia? Maswali (a) mwandihsi analalamikia mambo yapi katika shairi hili? (b) Mwandishi ametumia mbinu gani katika kutumia maneno. Mama Afriaka? Neno hili ( ala.5) limetumika kumaanisha nini? ( ala. 4) (c) Andika ubeti wa nne katika lugha ya nathari. ( ala.4) (d) Eleza maana ya maneno yafuatatyo: ( ala 5) (i) jahilia (iii) Kilohasirika (v) Barobaro. (ii) Muruwa (iv) kite (e) Mtunzi anamaanisha nini anaposema, ukazaa kizazi kilo kiwete? ( ala. 2) SEHEMU YA C : THAMTHILIA KIFO KISIMANI: Kithaka wa Mberia 6. Huku ukitoa mifano jadili mambo mbalimbali yanayodhinirisha ubaya wa utawala wa Mtemi Bokono. ( ala. 20) Nyamira- 11 kidato cha nne 4
SEHEMU YA D: FASIHI SIMULIZI. 7. (a) Kwa kutoa mifano taja mambo yoyote manne yanayozua lakabu (ala.4) (b) Jadili kwa kutoa mifano, umuhimu wa lakabu (ala.8) (c)el eza sifa zozote nne za lakabu (ala.8) Nyamira- 11 kidato cha nne 5