TANZANIA MARKETS PAN Sera zinazoboresha masoko

Similar documents
NGUZO KUMI ZA KILIMO KWANZA

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA. Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo. TOLEO Na.

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA MHESHIMIWA DKT

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

Miradi na jamii. 3.1 Utangulizi

JAMHURI YA KENYA. Mkakati wa Ushirikiano MUKHTASARI FY Public Disclosure Authorized. Public Disclosure Authorized

MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA PRO-ROUTES. Ombi kwa ajili ya fedha za umma wa mradi wa ziada

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA FEDHA

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU

Kubadili Sheria Za Mbegu Na Ulinzi Wa Aina Za Mbegu Na Mimea Nchini Tanzania

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi

MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2017/18

TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM)

Programu ya Uendelezaji Mifumo ya Maji Vijijini (PUMMV) katika Tanzania. Modeli wa Ukodishaji Mradi

Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA 2006/07

In the matter of an Application by the KIGOMA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (KUWASA) For a Tariff and Charges Adjustment

Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali ya Madini Ukanda

UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA)

KUHUSU AFRODAD. Dira ya AFRODAD. Dhamira ya AFRODAD. AFRODAD inalenga mchakato sawa na endelevu wa maendeleo kuelekea Afrika yenye mafanikio.

ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA UCHUMI WA ZANZIBAR

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, MHESHIMIWA DKT. PHILIP I. MPANGO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

Taarifa Kuhusu Hali ya Uchumi wa Tanzania

In the matter of Application by the TANGA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (TANGA UWASA) For a Multi-Year Tariff Adjustment

Dodoma ambako kikao cha Bunge kinaendelea kuja kushiriki japo sehemu ya uzinduzi wa mkutano.

NGUO MPYA ZA UKOLONI. Mikataba ya Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Umoja wa Ulaya na Afrika. Agosti 2017

Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame M. Mbarawa (Mb.); Waheshimiwa Mawaziri na Wabunge wote mliohudhuria;

Information for assessors (do not distribute this page to participants):

MAADHIMISHO YA MIAKA 15 YA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU

KAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI TANZANIA

USIMAMIZI MKUU WA UBORA WA MAHURUJI

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA,KWA WANANCHI, 30 SEPTEMBA, 2001

Uhakika wa Mbegu kwa Uhakika wa Chakula MWONGOZO WA UZALISHAJI WA MBEGU ZA ASILI ZA MAHINDI

UFUATILIAJI WA MIRADI NA TATHMINI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu WEMA

Songa kwenye kilele cha upeo. Masuala ya Msingi na Ujuzi juu ya Uendeshaji wa Serikali za Mitaa

Mwongozo wa Kutathimini mifumo ya Ugawanaji wa faida na Mapato Katika Miradi ya Jamii ya MKUHUMI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Deputy Minister for Finance

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara

Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2013

Kuuelewa Mchakato wa Bajeti Tanzania Mwongozo wa Asasi za Kiraia

Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara)

HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE

HOTUBA YA WAZIRI WA KILIMO MHESHIMIWA MHANDISI DKT. CHARLES JOHN TIZEBA (MB) KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA YA WIZARA YA KILIMO KWA

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )

Kufanya Uwekezaji kuwa wa Manufaa kwa Afrika: Jibu la Mbunge kuhusu Unyakuzi wa Ardhi

Uwepo, Athari na Udhibiti wa Sumu-Suvu Kwenye Vyakula vya

MAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA NISHATI NA MADINI

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

3. Mheshimiwa Spika, 4. Mheshimiwa Spika,

HOTUBA YA WAZIRI WA KILIMO MIFUGO NA UVUVI MHESHIMIWA, ENG. DKT. CHARLES JOHN TIZEBA (MB.) KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA YA WIZARA

Dibaji ya Mwenyekiti wa Kamati ya Pamoja ya Uongozi

Kilimo cha kiekolojia cha Wakulima Wadogo Hufanikisha Haki za Mazingira

Muhtasari wa taarifa ya warsha ya wataalamu juu ya mfumo wa habari kwa njia ya ramani (PGIS), Morogoro, Juni 30 - Julai 1, 2014

Azimio lililopitishwa na Mkutano Mkuu tarehe 18 Desemba 2013 [juu ya taarifa ya Kamati ya Tatu (A/68/456/Add.2)]

Govt increases vetting threshold of contracts

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II

RIPOTI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI

MAPENDEKEZO YA MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA TANZANIA

Uzio wa pilipili unazuia tembo kuvamia mazao shambani! Jinsi ya kujenga na kudumisha uzio wa pilipili Tanzania

2 Usimamizi wa Rutuba ya Udongo Tanzania Organic Agriculture Movement

Kutetea Haki za Binadamu

MWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

ORDER NO BACKGROUND

UTANGULIZI. 1. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako. 2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote nitumie fursa hii kuungana na

UFUPISHO WA 35. Hali ya kiulimwengu ya Tekinolojia ya kibiashara/ugeuzi jeni na uboreshaji mazao: Clive James Chair, ISAAA Board of Directors

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees

KIMAZINGIRA NA KIJAMII NA MPANGO WA UDHIBITI

UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU VIKWAZO VYA KULINDA MAISHA KATIKA USAIDIZI WA KIMATAIFA WA AFYA KWA MSAADA WA KIMATAIFA UNAOFADHILIWA NA MAREKANI

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti

Nilikua na Ndoto ya Kumaliza Shule Changamoto za Elimu ya Sekondari Tanzania

Pronunciation: Mä-hret Zäläke Ndal-ka-tscho Molla Mare Gebre-gzabiär 1/12

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO

HAKI NA TARATIBU ZA AJIRA, KAZI NA HIFADHI YA JAMII

TANZANIA TAARIFA YA MWISHO WA UTEKELEZAJI

RIPOTI YA WARSHA KUHUSU HABARI KWA AJILI YA UWAJIBIKAJI

5. Mheshimiwa Spika, Bunge lako Tukufu lilijadili kwa kina Miswada ifuatayo:

KUSHUKA KWA HADHI YA LUGHA ZA JAMII NCHINI TANZANIA YOHANA P. MSANJILA University of Dar es Salaam, Tanzania

Bustani 10,000 Katika Afrika. Alberto Prina

Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI Nchini Tanzania

muhtasari 37 brief 37 Kiwango cha kiutandawazi cha mazao ya kibiashara ya kibayoteki/ugeuzi jeni: 2007 Clive James Bordi ya wakurugenzi wa ISAAA

Kuwafikia waliotengwa

Upatikanaji wa Silaha Ndogo ndogo na Hisia za Usalama nchini Kenya: Ukadiriaji

International Labour Office. Kazi za Ndani Zenye Madhara kwa Watoto: Kijitabu cha Maelezo Mafupi

TAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF) KUHUSU HAKI ZA WATOTO KATIKA KATIBA MPYA

Ufanisi katika Ufundishaji kwenye Shule za Msingi na Sekondari nchini Tanzania

DIRA DHIMA. Kuendeleza, kuwezesha, kudhibiti na kusimamia matumizi endelevu ya Rasilimali za Nishati na Madini kwa manufaa ya Watanzania.

TANGA CEMENT PLC ANNUAL REPORT TAARIFA YA MWAKA.

CGAP Smallholder Household Survey in Tanzania / Utafiti wa kaya ndogondogo Tanzania

Transcription:

TANZANIA MARKETS PAN Sera zinazoboresha masoko UPOTEVU WA MAZAO YA NAFAKA BAADA YA MAVUNO: CHANGAMOTO NA UBORESHAJI Usuli Kuna makubaliano ya jumla kwamba marekebisho ya sera zinazohusu sekta ya kilimo, hasa katika suala la kupunguza upotevu wa mazao aina ya nafaka, yapewe kipaumbele Utafiti uliofanyika huko nyuma, ulithibitisha kwamba kiasi kinachopotea tangu kuvuna hadi kuliwa, kinafikia asilimia 40. Upotevu huo hutegemea mazingira yaliyopo; kwa mfano: aina ya zao, mahali linapostawishwa, na kadhalika. Hata hivyo, hakuna takwimu sahihi zinazo onyesha kiasi cha upotevu huo 1. Takwimu zinazonukuliwa ni za kipindi cha mwaka 1950 hadi 1960 2. Upotevu au kuharibika kwa chakula kuna athari kubwa katika kipato na maisha ya wakulima. Kwa mfano, nafaka: Inakadiriwa kwamba kila mwaka hasara inayotokana na kuharibika kwa mazao ya nafaka barani Afrika, kusini mwa jangwa la Sahara, inafikia dola za Kimarekani bilioni 4 na hii ni sawa na asilimia 15 ya thamani ya mavuno hayo 3. Utafiti uliofanywa na Idara ya Uchumi ya Kilimo na Biashara, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, ulibaini takwimu zifuatazo (Jedwali 1) 4 : Sera na Hatua Zinazochukuliwa Kudhibiti Upotevu Kabla ya miaka ya 1970, Tanzania haikuwa na sera kuhusu hifadhi ya mazao ya chakula, mpaka alipotokea mdudu muharibifu sana wa mahindi Large Grain Borer katika miaka ya 1980. Mdudu huyo aliteketeza sana mahindi baada ya kuvunwa, na kuhatarisha hali ya usalama wa chakula nchini. Tatizo hili lilipelekea Serikali kulazimika kuagiza mahindi kutoka nchi jirani ili kufidia upungufu uliosababishwa na mdudu huyu. Jedwali 1: Wastani wa upotevu wa nafaka kuu 3 nchini Tanzania, kati ya 2003 na 2007 (kwa tani) RURAL LIVELIHOOD DEVELOPMENT PROGRAMME UZALISHAJI 2003 2004 2005 2006 2007 Mahindi Uzalishaji (tani) 3,343,758 3,218,541 3,472,885 3,302,057 3,593,659 Upotevu: 15.5% 518,282 498,874 538,297 511,819 557,017 Mpunga Uzalishaji (tani) 704,287 759,386 805,065 909,990 896,696 Upotevu: 10.7% 75,359 81,254 86,142 97,369 95,946 Mtama Uzalishaji (tani) 820,100 714,339 711,631 971,198 861,386 Upotevu: 12.5% 102,513 89,292 88,954 121,400 107,673 Supported by: 1 Tafiti elekezi - Daima 2 Chanzo: PMC, SUA, Usaili Julai 2012 3 Benki ya Maendeleo ya Afrika - ADB (Framework Paper: Programme for Post harvest Losses Reduction in Africa, 2010 2014) FAO/WB Workshop on Reducing PHL in grain supply chains in Africa: lessons learned and practical guidelines, FAO Hqrts. Rome, Italy, March 2010 4 Uzoefu wa Tanzania wa kuelimisha wakulima wadogo jinsi ya kuhifadhi mazao baada ya kuvunwa, Idara ya Uchumi na Biashara ya Kilimo SUA, Oktoba 2012 1

Tanzanian Markets-PAN Policy Brief no 3-KSW / 2013 Usalama wa chakula, ni suala linalopewa kipaumbele na Serikali ya Tanzania. Kwa sababu hii, Serikali iliandaa mikakati na programu ambazo zilizaa Mkakati wa Kuendeleza Sekta ya Kilimo (Agricultural Sector Development Strategy - ASDS). ASDS inasisitiza sera muafaka na mikakati inayolenga kuchochea wadau kutoka sekta ya umma na binafsi kuwekeza kwenye kilimo. Kama uwekezaji makini utafanyika katika ngazi zote kwenye mlolongo wa thamani: Kuhifadhi kusindika kufunga kupakia kusafirisha na kuuza, kiwango cha upotevu / uharibifu wa mazao kitapungua sana. Hata hivyo, hakuna kumbukumbu zinazotaja sera inayohusu suala la kudhibiti upotevu wa mazao baada ya kuvunwa. Juhudi za Serikali kwa kiasi kikubwa zililenga katika ujenzi wa maghala. Tangu miaka ya 1970, Serikali kwa kushirikiana na taasisi za Umoja wa Mataifa: FAO/UNDP, pamoja na wabia wengine, ilichukua hatua mahususi za kushughulikia tatizo hili. Kwa upande mwingine Sasakawa Global 2000 katumia mkakati fungamanishi (integrated) wa kukabiliana na changamoto hii, ikiwa ni pamoja na: kuelimisha wakulima na wauza pembejeo jinsi ya kudhibiti upotevu wa mazao baada ya kuvunwa, pamoja na kujenga maghala bora. Kwa sasa Tanzania ina maghala 1,260. Idadi hii ni ndogo mno ukiilinganisha na mahitaji halisi ya takribani vijiji 11,000 vilivyopo. Mbali na hili, kuna matatizo mengine: Mosi, maghala mengi hayawafai wakulima kwa sababu ya kuwa mbali. Pili, baadhi ya maghala ni mabovu kwa kuachwa kwa muda mrefu bila kukarabatiwa. Tatu, maghala mengine ama yamekodishwa kwa wafanya-biashara binafsi, au yanatumiwa kwa shughuli nyingine tofauti na kuhifadhi mazao. kuwa tani 3,897,500 kwa mwaka) teknolojia zinazotumiwa wakati wa kuvuna na kusindika ni duni sana. Hali hii husababisha upotevu wa mavuno unaokisiwa kuwa tani 1,559,000 kila mwaka. Tafsiri ya takwimu hizi ni upotevu wa takribani asilimia 40 baada ya mavuno. Kwa kawaida, wakulima wanafahamu ukubwa wa tatizo la upotevu / uharibifu wa mazao (rejea Jedwali 1). Kujenga maghala ya kuhifadhia mazao peke yake hakutoshi kudhibiti uharibifu huo. Uharibifu na upotevu wa mavuno hutokea tangu hatua ya kuvuna hadi kuandaliwa kuliwa. Kwa hiyo, hata maamuzi na vitendo kadha wa kadha baada ya kuvuna, huchangia upotevu wa mazao. Kwa sababu hii, msisitizo uwekwe kwenye huduma kamilishi bila kuangalia kitu kimoja tu. Hata hivyo, ilibainika kwamba kiasi kikubwa cha upotevu husababishwa na: ukaushaji usioridhisha, shambulio la wadudu, na panya. Kwa hiyo, inabidi kuwa na mtazamo mpana katika suala hili - yaani mlolongo mzima wa thamani. Lengo ni kupunguza upotevu / uharibifu katika hatua zote: kuvuna kusafirisha kusindika - kuhifadhi kupeleka sokoni. Matokeo ya Utafiti Je, takwimu za upotevu / uharibifu wa mazao zinatufundisha nini? Takwimu za utafiti huu zinatufundisha kwamba licha ya ongezeko la uzalishaji wa nafaka kitaifa (unaokadiriwa Jedwali 1: muhtasari wa sababu za upotevu wa mazao Sababu za upotevu Kiwango cha utambuzi wa wakulima Uharibifu utokanao na shambulio la wadudu na panya Asilimia 35 wanatambua Upotevu wakati wa kusafirisha kutoka shambani hadi nyumbani Asilimia 16 wanatambua Uzembe wakati wa kupima mazao na kuyafungasha Asilimia 12 wanatambua Ukaushaji wa mavuno usioridhisha Asilimia 9 wanatambua Ucheleweshaji wa kuuza mazao (soko lisilotabirika) Wanaotambua ni chini ya asilimia 5 Upotevu wakati wa kusindika mazao Wanaotambua ni chini ya asilimia 5 Punje kuvunjika-vunjika (hasa mchele) Wanaotambua ni chini ya asilimia 5 2

3

Tanzanian Markets-PAN Policy Brief no 3-KSW / 2013 Sababu za Kutotumia Maghala Yaliyopo Wakulima wengi wanasema kikwazo ni gharama kubwa ya kukodi mahali pa kuhifadhia mazao. Gharama hiyo hupunguza sana faida ya mauzo, hasa mkulima asipohakikishiwa kiasi atakachotozwa kwa huduma ya ghala. Mbali na hili, kuna mambo mengine yanayochangia wakulima kusita kutumia maghala: 1. Ufahamu mdogo kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mazao ghalani. 2. Usimamizi usioridhisha wa maghala yaliyopo. 3. Utendaji usio makini. 2. Wawekezaji wanatatizwa na gharama kubwa ya kujenga maghala, kukosekana au urasimu katika kupata sehemu muafaka za kujenga maghala, faida ndogo baada ya kuwekeza, uhaba wa wajenzi makini wa maghala, na kadhalika. Upotevu na uharibifu wa mazao yakiwa ghalani husababishwa na: Wadudu na panya (46%). Wizi (20%). Unyevu (18%). Magunia mabovu (13.9%). Kutokuwa na bima (13.9%). Uhaba wa viuatilifu (13.9%). Hali mbovu ya barabara, uhaba wa maghala, ukubwa wa gharama ya kuyatumia, umbali wa kuyafikia (wastani wa umbali ni kilomita 15), na adha ya kufikisha mazao kwenye hifadhi, vyote hivi husababisha wakulima wasite kutumia maghala. Hivyo kuendelea na utamaduni wa kutumia vifaa vya kijadi. Mara nyingi vifaa hivyo havitoshelezi mahitaji ya kisasa. Ukosefu wa motisha ya kuwekeza kwenye ujenzi wa maghala. Ingawa utafiti uliofanyika haukugundua sababu zilizo wazi kuhusu uwekezaji mdogo kwenye ujenzi wa maghala ya kuhifadhia mazao, kuna viashirio vya kukwama kwa uwekezaji. Kukwama huko kunaweza kuwekwa katika makundi mawili. Wakulima wenye kiasi fulani cha ziada ya mavuno, na wanapenda kihifadhiwe kwenye ghala la jumuia. Wawekezaji (taasisi, wachuuzi wa mazao, wafanya biashara yingine, nakadhalika) ambao lengo lao ni kuwekeza fedha zao, na kupata faida. Hawa wote wakumbana na changamoto za kujenga majengo ya kuhifadhia mazao ya kilimo, pamoja na kutumia teknolojia nyingine za kudhibiti uharibifu wa mazao. 1. Wakulima wengi hawana uelewa wa kutosha kuhusu faida za kujenga na kutumia maghala. Baadhi ya changamoto zinazowakabili ni: Kukosekana kwa miundombinu mizuri sehemu za vijijini, uchache wa mazao ya kuhifadhiwa, ufinyu wa fedha za kuwekeza, ugumu wa kupata mikopo kutoka kwenye taasisi za fedha, kutokuwepo huduma ya bima ya mazao, Serikali kusita kusaidia katika ujenzi wa maghala, na kadhalika. Mpango wa Miaka 5 wa Kuendeleza Juhudi za Kuhifadhi Mazao Mpango huu ambao utadumu kwa miaka mitano, 2011/12 2015/16, unalenga kuboresha maeneo yafuatayo: Kufanikisha uhusiano na ushirikiano katika kupanga na kutekeleza mipango ya kiuchumi. Kuongeza kiwango cha ubia kati ya sekta ya umma na binafsi katika kuwekeza kwenye huduma za kiuchumi na kijamii. Kujenga uwezo wa taasisi wa kutoa huduma, zikijumuisha Serikali za Mitaa. Kuongeza ukuaji wa sekta ya kilimo, kutoka ya sasa ambayo ni asilimia 4.2% hadi 6.2%. Kuboresha upatikanaji wa taarifa za soko la mazao ya kilimo. Kuboresha / kupanua usindikaji wa mazao na kuongeza thamani yake. Kuhakikisha upatikanaji na utumiaji wa zana bora za kilimo, na kuhimiza matumizi ya zana kubwa kubwa. Kuimarisha / kupanua elimu ya taaluma ya kilimo, na huduma za ugani. Kuimarisha utaratibu wa kupata taarifa za utafiti na kuzifikisha kwa wakulima ili wazitumie. Aidha, kuna haja ya kuweka utaratibu wa kufuatilia ili kuhakikisha malengo yaliyowekwa yanafikiwa. Kwa kufanikisha hili, ni budi Serikali iwe makini katika kuamua kipi kipewe kipaumbele katika mkakati wa kupunguza upotevu / uharibifu wa mazao. Tukifanikisha hili, soko litakuwa na chakula cha kutosha, pia wazalishaji na walaji watanufaika. 4

Tanzanian Markets-PAN Policy Brief no 3-KSW / 2013 Serikali inajitahidi kuweka mazingira muafaka kwa uwekezaji katika uzalishaji wa chakula na kupunguza upotevu wa mavuno. Motisha za Kuchochea Sekta Binafsi Iwekeze Katika Ujenzi wa Maghala Kati ya aina sita za motisha, ziko tatu ambazo zimepandishwa hadhi kutokana na mchango wake wa kuchochea sekta binafsi iwekeze kwenye ujenzi wa maghala. Motisha hizo ni: 1. Uwepo na ufikiwaji wa masoko ambayo yanaaminiwa / yanategemewa. 2. Uwepo wa miundombinu muhimu kwa ajili ya usafirishaji, yenye ubora unaokubalika. 3. Uwepo wa taratibu za kutoa muamana au ruzuku kwa ujenzi wa maghala, ikiwa ni hakikisho la kumudu gharama za ujenzi mkubwa. Juhudi za Kuongeza Thamani ya Bidhaa ili Kupunguza Uharibifu Mbinu mojawapo ya kuongeza thamani ya mazao ni kuhimiza wakulima wazingatie ufanisi katika hatua zote za kuyashughulikia. Hii ni pamoja na usindikaji hatua ya kwanza, na ya pili. Usindikaji unaweza kufanywa kwa kiwango cha chini kabisa kwa ajili ya bidhaa vya walaji wa karibu. Baadhi ya mazao ambayo huzidi soko la ndani, huuzwa nje bila kusindikwa kwa bei nafuu. Kusindika mazao ya chakula (kuyaongezea thamani), wakulima hupata faida zifuatazo: Kupunguza kwa kiasi kikubwa uwezekano wa kuharibika. Wakulima kuongeza uelewa wa mantiki ya kusindika, kugredi, na kufikia viwango. Wazalishaji, wasindikaji, na walaji kupata fursa ya kufahamu matumizi ya teknolojia za kisasa katika kusindika mazao, na kupunguza upotevu / uharibifu. Serikali inaweza kusaidia kuweka mazingira mazuri ya kuwezesha wananchi waanzishe viwanda vidogo vya kusindika mazao kusudi thamani yake iongezeke. Baadhi ya vitu vya kusindika mazao vinavyotakiwa katika ngazi ya kijiji, ni: Upatikanaji kwa urahisi wa vifaa muhimu kwa usindikaji. Uwezo wa kikundi husika wa kusindika mazao, kusimamia biashara na wahudumu. Uelewa kuhusu uhakiki wa bidhaa, hati ya ubora, na mchakato wa kusanifisha. Mambo mengine yaliyotajwa ni : mazingira muafaka ya kufanya biashara, ushuru wa forodha wa upendeleo, na sera nzuri. Kwa hiyo, Serikali iangalie jinsi ya kuboresha mazingira kusudi Sekta binafsi ishawishike kuwekeza kwenye ujenzi wa maghala. Kipengele cha kutoa motisha kiingizwe kwenye mpango-mkakati wa kuendeleza sekta ya kilimo. Mikakati Inayopendekezwa Kupunguza Upotevu / Uharibifu wa Mazao Mikakati ya Uendeshaji Suluhisho la kupunguza upotevu / uharibifu wa mazao ya wakulima wadogo, pamoja na wadau wengine, linaweza kuwekwa katika makundi matano: 1. Maswala yanayohusu hifadhi : ujenzi na usimamizi wa maghala, pamoja na hifadhi katika ngazi ya kaya, usindikaji wa kutumia vifaa vya kisasa, kupunguza gharama za vifaa, na kudhibiti ubora wa mazao. 2. Uelimishaji na upatikanaji wa taarifa kuhusu ustadi wa kuvuna na kusimamia mchakato wa kuhifadhi mavuno. Kwa mfano: kutumia viuatilifu, na kudhibiti upotevu usiohusiana na suala la hifadhi ghalani. 3. Kuweka utaratibu kuunganisha wakulima na masoko, kutangaza bei za mazao, kuzingatia kanuni, na kuingilia kati mambo yakienda kombo. 4. Masuala ya ufanisi katika utendaji, ikihusisha kuboresha miundombinu pamoja na vyombo vya usafiri, kupima uzito na ujazo, na kuweka viwango vya ubora. 5. Kujenga uwezo wa vikundi au vyama vya wakulima wa kufahamu changamoto za upotevu wa mazao, kusimamia fedha, haki na wajibu wakati wa kuingia mikataba ya kibiashara. 5

6

Tanzanian Markets-PAN Policy Brief no 3-KSW / 2013 Mikakati ya Kisera 1. Kutunga sera rafiki za kuvutia ushiriki wa sekta binafsi kusudi iwekeze zaidi katika ujenzi wa maghala, mathalan: kusitisha ulipaji wa kodi kwa vifaa vya ujenzi, wakulima wadogo kuhakikishiwa upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kazi hii 5. 2. Kuweka mazingira mazuri ya kufanikisha ushirikiano wa Sekta ya Umma na Binafsi, utakaosisitiza wajibu wa sekta binafsi katika mradi huu. Lengo ni kuhakikisha jamii husika inafaidika. 3. Serikali iwekeze zaidi kwenye sekta ya kilimo kwa lengo la kuboresha miundombinu ya vijijini, kwa mfano: barabara, maghala ya kisasa, nakadhalika 6 4. Kuboresha huduma za ugani ili kukuza elimu ya wakulima ya kutumia teknolojia za kisasa katika kudhibiti upotevu wa mazao, na kujenga uwezo wa watendaji wanaosimamia miradi ya kifedha (kwa mfano SACCOS ), na ustadi katika ujasiriamali. Mapendekezo Serikali Kufanikisha Dhima ya Sekta Binafsi Sekta binafsi inaweza kutimiza wajibu wake kwenye maeneo mengi katika mlolongo wa uzalishaji, ikiwemo kudhibiti upotevu / uharibifu wa mazao katika mlolongo wa thamani: kukusanya mavuno, kugredi, kupakia, kusafirisha, kuhifadhi kwenye stoo, kusindika, na kuuza. Serikali inao wajibu mkubwa wa kuweka mazingira muafaka ili sekta binafsi itimize majukumu yake. Mazingira mazuri ni pamoja na: kuwepo miundombinu mizuri, na kuhakikisha sheria na kanuni zinazotawala ubia zinafuatwa. Ili kufanikisha suala hili, hatua zifuatazo zinapendekezwa: Kundaa sera na mkakati-kamilifu kuhusu suala hili kwa kuzingatia umuhimu wa kila eneo kwenye mlolongo wa thamani. Hii itatoa nafasi ya kujadili vipengele vyote, wala siyo tu usalama wa chakula ( bali pia masuala ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni). Kuimarisha mshikamano wa ubia kati ya sekta ya umma na binafsi kwa kuweka mazingira mazuri ya kuwezesha sekta binafsi kujikita katika kudhibiti upotevu wa mazao. Hii ni pamoja na kutimiza kanuni, maelekezo, majukumu na wajibu. Mwishowe, jamii husika itanufaika. Kutoa motisha kwa sekta binafsi ili iwekeze kwenye programu hii. Kwa mfano: kuondoa ushuru kwa vifaa vya ujenzi wa maghala, kusindika mazao, na matumizi mengine ya kiteknolojia; kutoa ardhi kwa ajili ya shughuli hii. Kuongeza bajeti kwa ajili ya sekta ya kilimo hadi asilimia 10% kulingana na azimio la Maputo (CAADP). Pamoja na fedha za kuendesha shughuli nyingine muhimu, kwa mfano: kuelimisha wakulima na kuimarisha huduma za ugani (zinazojumuisha: kilimo cha mkataba, wakulima wa pembezoni mwa mashamba makubwa out growers, kuimarisha usindikaji na hifadhi ya chakula, kuongeza thamani ya mazao, na biashara yake). Kuongeza uelewa wa wakulima kuhusu mbinu za kilimo bora, hifadhi ya mazao, kugredi na kufungasha. Kuweka mazingira mazuri ya kufanya sekta binafsi ishawishike kuongeza thamani ya mazao ya kilimo kwa kuzingatia sheria na kanuni zilizopo, kuboresha miundombinu za vijijini, na kuongeza msaada katika ujenzi wa maghala. Kuzingatia sera za fedha, na kutumia kwa busara mafungu yanayotengwa na Serikali kila mwaka. Kuboresha mfumo wa sasa wa vocha za kilimo, na kuangalia uwezekano wa kuanzisha benki za nafaka, na kupanua mfumo wa stakabadhi ghalani. Kuanzisha kitengo kitakachoshughulikia suala la kudhibiti upotevu / uharibifu wa mazao. Hii ni pamoja na: kudhibiti upotevu kwa gharama nafuu, kupata aina za mbegu zenye uathirikaji mdogo, kusimamia mpangilio wa kuhifadhi mazao ghalani na kuhakiki viwango vya ubora, kupanga daraja za mavuno na kujenga vituo vya kuyakusanyia, na kutumia vyombo vya habari kutoa taarifa za kitafiti kwa faida ya wakulima. Kuanzisha vituo vya kufundishia utaalamu wa kudhibiti upotevu / uharibifu wa mazao ngazi ya kijiji, kama mfano wa kuigwa. Hii ni pamoja na: ukaguzi wa mara kwa mara, teknolojia ya kufukiza, namna ya kupunguza gharama, nakadhalika. Kuhakikisha magari yanayotumiwa kusafisha mazao ya chakula yana leseni -hai. 5 Uzoefu wa Tanzania wa kuelimisha wakulima wadogo jinsi ya kuhifadhi mazao baada ya kuvunwa, idara ya Uchumi Kilimo na Biashara SUA, Oktoba, 2012 6 Kwa mujibu wa CAADP, serikali za Bara la Afrika zilijipa sharti la kutenga asilimia 10% ya bajeti ya mwaka kwa ajili ya sekta ya kilimo. Serikali ya Tanzania, Kama zilivyo nchi nyingine nyingi, haijatimiza sharti hili. Inawajibika kutimiza lengo hili 7

Tanzanian Markets-PAN Policy Brief no 1 / 2013 RURAL LIVELIHOOD DEVELOPMENT PROGRAMME Supported by: 8