Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI Nchini Tanzania

Similar documents
KAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI TANZANIA

TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM)

Information for assessors (do not distribute this page to participants):

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Miradi na jamii. 3.1 Utangulizi

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA 2006/07

MAADHIMISHO YA MIAKA 15 YA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA. Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo. TOLEO Na.

Songa kwenye kilele cha upeo. Masuala ya Msingi na Ujuzi juu ya Uendeshaji wa Serikali za Mitaa

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2017/18

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara)

TANZANIA MARKETS PAN Sera zinazoboresha masoko

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig

MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA PRO-ROUTES. Ombi kwa ajili ya fedha za umma wa mradi wa ziada

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU

Ufanisi katika Ufundishaji kwenye Shule za Msingi na Sekondari nchini Tanzania

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II

In the matter of Application by the TANGA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (TANGA UWASA) For a Multi-Year Tariff Adjustment

JAMHURI YA KENYA. Mkakati wa Ushirikiano MUKHTASARI FY Public Disclosure Authorized. Public Disclosure Authorized

In the matter of an Application by the KIGOMA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (KUWASA) For a Tariff and Charges Adjustment

JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI

MAPENDEKEZO YA MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA TANZANIA

HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE

Makala ya Mshiriki wa Mafunzo

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

ORDER NO BACKGROUND

Dibaji ya Mwenyekiti wa Kamati ya Pamoja ya Uongozi

Mwongozo wa Mwezeshaji

KITEGO CHA MAREKEBISHO NA HAKI ZA MTOTO

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU

Kuuelewa Mchakato wa Bajeti Tanzania Mwongozo wa Asasi za Kiraia

Afya Bora, Utu na Kinga. Ripoti ya Mashauriano ya Kiufundi Aprili 2009, Hammamet, Tunisia

UFUATILIAJI WA MIRADI NA TATHMINI

UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU VIKWAZO VYA KULINDA MAISHA KATIKA USAIDIZI WA KIMATAIFA WA AFYA KWA MSAADA WA KIMATAIFA UNAOFADHILIWA NA MAREKANI

HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA MHESHIMIWA

TAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF) KUHUSU HAKI ZA WATOTO KATIKA KATIBA MPYA

ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA UCHUMI WA ZANZIBAR

Mwongozo wa Utekelezaji wa Njia za S5-UUE (KAIZEN)-UUU Tanzania

Afya Bora, Utu na Kinga. Ripoti ya Mashauriano ya Kiufundi Aprili 2009, Hammamet, Tunisia

International Labour Office. Kazi za Ndani Zenye Madhara kwa Watoto: Kijitabu cha Maelezo Mafupi

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA MHESHIMIWA DKT

Human Rights Are Universal And Yet...

Programu ya Uendelezaji Mifumo ya Maji Vijijini (PUMMV) katika Tanzania. Modeli wa Ukodishaji Mradi

RIPOTI YA WARSHA KUHUSU HABARI KWA AJILI YA UWAJIBIKAJI

Sera ya Faragha. Upeo. Aina za Data na Mbinu za Ukusanyaji

KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA

MAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI

MWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI

HUDUMA ZA AFYA KWA WOTE

Kuwa na Ukimwi ni kama vile kutakiwa kuendelea kuuzima moto unaoniunguza bila kukoma.

Nilikua na Ndoto ya Kumaliza Shule Changamoto za Elimu ya Sekondari Tanzania

KUHUSU AFRODAD. Dira ya AFRODAD. Dhamira ya AFRODAD. AFRODAD inalenga mchakato sawa na endelevu wa maendeleo kuelekea Afrika yenye mafanikio.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Mipango ya miradi katika udugu

TAARIFA YA MWAKA YA UTENDAJI KAZI IDARA YA UTAWALA BORA 2013/2014

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

NGUZO KUMI ZA KILIMO KWANZA

KUWEZESHA MBINU ZA UZUIAJI MIMBA KATIKA SUHULA ZA AFYA: MASWALI 10 KWA VIKUNDI VYA JAMII KUZINGATIA

Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali ya Madini Ukanda

MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA. Kwa Wanaoanza

SautiElimu. Sauti Yako Isikike

Govt increases vetting threshold of contracts

UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA)

TANZANIA TAARIFA YA MWISHO WA UTEKELEZAJI

Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame M. Mbarawa (Mb.); Waheshimiwa Mawaziri na Wabunge wote mliohudhuria;

Azimio lililopitishwa na Mkutano Mkuu tarehe 18 Desemba 2013 [juu ya taarifa ya Kamati ya Tatu (A/68/456/Add.2)]

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA NISHATI NA MADINI

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara

Unyanyasaji wa Watoto & Kutelekezwa

HAKI NA TARATIBU ZA AJIRA, KAZI NA HIFADHI YA JAMII

USIMAMIZI MKUU WA UBORA WA MAHURUJI

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, MHESHIMIWA DKT. PHILIP I. MPANGO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO

Ripoti hii ni kwa heshima ya wale wanaharakati wengi wa Tanzania ambao ndio binafsi wanaopitia hali iliyoangaziwa, na vilevile wale walioyapoteza

Kutetea Haki za Binadamu

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

Kufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO

5. Mheshimiwa Spika, Bunge lako Tukufu lilijadili kwa kina Miswada ifuatayo:

Kijitabu cha Maelezo cha Programu ya Famasia

Dodoma ambako kikao cha Bunge kinaendelea kuja kushiriki japo sehemu ya uzinduzi wa mkutano.

Kubadili Sheria Za Mbegu Na Ulinzi Wa Aina Za Mbegu Na Mimea Nchini Tanzania

RIPOTI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA FEDHA

KUSHUKA KWA HADHI YA LUGHA ZA JAMII NCHINI TANZANIA YOHANA P. MSANJILA University of Dar es Salaam, Tanzania

Utangulizi wa ugonjwa wa shinikizo la damu

Mwongozo wa Kutathimini mifumo ya Ugawanaji wa faida na Mapato Katika Miradi ya Jamii ya MKUHUMI

Transcription:

Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI Nchini Tanzania

2 Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013

Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI Dar es salaam, Dodoma na Pwani 2013 Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013 i

Yaliyomo ORODHA YA VIFUPISHO iii SHUKURANI iv MUHTASARI WA UTEKELEZAJI v 1 UTANGULIZI 1 2 MBINU ZA UFUATILIAJI 3 i Muundo wa Ufuatiliaji 3 ii Watoa taarifa wa Ufuatiliaji 3 iii Uteuzi wa watoa taarifa 3 iv Ukusanyaji wa taarifa 4 v Mazingatio ya Maadili ya Kiutafiti 4 vi Kuingiza na Kuchambua taarifa 4 vii Mipaka ya Ufuatiliaji 5 3 MATOKEO NA MJADALA 6 i Ngazi za kupatia huduma 7 ii Uwiano wa Kijinsia 8 iii Umri wa washiriki 10 iv Viwango vya elimu 11 v Faragha na Ukarimu kwenye Vituo vya Huduma 12 a. Kiwango cha faragha 12 b. Ukarimu 13 vi Dawa na vifaa tiba 13 a. Upatikanaji wa Dawa za kupunguza makali ya VVU 13 b. Huduma ya Mashine za kuhesabu CD4 13 c. Upatikanaji wa Kondomu katika vituo vya huduma za afya 15 vii Idadi ya Watoa huduma (Rasilimali watu) 15 viii Taarifa Kuhusu VIRUSI na UKIMWI kwenye Vituo vya 16 Huduma za Afya ii Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013

4 HITIMISHO 17 5 MAPENDEKEZO 18 6 MAREJEO 20 Viambatanisho Kiambatanisho na: 1: Upatikanaji wa mashine za CD4 21 Kiambatanisho na: 2: Hojaji 25 Kiambatanisho na: 3: Utambulisho kwa msailiwa 31 Kiambatanisho na: 4: Fomu ya ridhaa ya msailiwa 33 Orodha ya Vifupisho AMJ AMT ARVs HWN SPSS TACAIDS UKIMWI URT VMM VVU WAVIU Afisa Maendeleo wa Jamii Afisa Mtendaji wa Kata Dawa za Kupunguza makali ya VVU Huduma za Wagonjwa Nyumbani Kichanganua Takwimu za Sayansi Jamii Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania Upungufu wa Kinga Mwilini Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Vituo vya Matunzo na Matibabu Virusi vya UKIMWI Wanaoishi na virusi vya UKIMWI Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013 iii

Shukurani Kwa niaba ya Idara ya VVU na UKIMWI ambayo iliendesha ufuatiliaji huu, ninapenda kuwashukuru kwa dhati wale wote walioshiriki katika kufanikisha zoezi hili. Ninapenda kuwashukuru wafanyakazi wa Sikika kwa mchango wao wa mawazo wakati wa kuandaa ripoti hii. Shukurani za dhati ninazitoa kwa wanaidara wa VVU na UKIMWI; Tusekile Mwambetania, Daniel Mugizi, Aisha Hamis na Norah Mchaki kwa kujituma bila kuchoka katika hatua zote za ufuatiliaji huu. Ninapenda pia kutambua mchango wa Gertrude Mugizi aliyepitia muswada wa ripoti hii, msaidizi wa Sikika, Bw. Frank Lyimo ambaye pamoja na wasaidizi wengine walifanya kazi bila kuchoka wakati wa kukusanya na kuchambua data. Ninawashukuru kwa dhati pia wale wote wanaoishi na virusi vya UKIMWI (WAVIU) katika wilaya za Kinondoni, Temeke, Ilala, Kibaha, Kondoa, na Mpwapwa; kwa kukubali kushiriki katika utafiti huu. Ninawashukuru vilevile watoa huduma wote wa wilaya hizi kwa kutuunga mkono na kushirikiana nasi katika zoezi hili. Mwisho ninatoa shukurani kwa Dr P. P. Lipembe kwa kuihariri na kutafsiri ripoti hii. Irenei Kiria Mkurugenzi Mtendaji Sikika Hakimiliki 2013 Sikika Company Limited, Haki zote zimehifadhiwa. Kimechapishwa 2013 Imetayarishwa na: Idara ya VVU na UKIMWI, Sikika iv Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013

Muhtasari wa Utekelezaji Sekta ya afya na UKIMWI inakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zinasababisha upatikanaji wa huduma kuwa wa matatizo. Huduma za VVU na UKIMWI nchini hutolewa katika Vituo vya Matunzo na Matibabu (VMM) ambapo watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI (WAVIU) hupatiwa huduma mbalimbali. Huduma hizi ni pamoja na; elimu ya kinga, maambukizi mapya, ufuatiliaji wa maendeleo, dawa (dawa za kupunguza makali ya VVU (ARVs) dawa za kutibu magonjwa nyemelezi n.k.) pamoja na ugawaji wa kondomu. Mojawapo ya malengo ya Sikika ni kuhakikisha kuwa huduma za VVU na UKIMWI, dawa pamoja na taarifa zinawafikia wananchi wote. Sikika ilifanya ufuatiliaji kwa lengo la kutathmini hali ya upatikanaji wa huduma za VVU na UKIMWI. Matokeo ya ufuatiliaji huu yanatarajiwa kusaidia kuhimiza serikali kuongeza upatikanaji wa huduma za VVU na UKIMWI ikiwemo dawa, vifaa na elimu katika vituo vya huduma za afya vya umma ambazo zitafikiwa kwa urahisi na watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI (WAVIU). Taarifa za ufuatiliaji huu zilikusanywa kwa njia ya hojaji zilizojibiwa na watumia huduma wanaoishi na virusi vya UKIMWI (WAVIU). Kundi hili lilitumika ili kupata uzoefu wao, hususani juu ya matatizo wanayopata na jinsi wanavyoweza kukabiliana na ugonjwa huo. Jumla ya kata 45 kutoka wilaya za Kinondoni, Ilala na Temeke za mkoa wa Dar es salaam; Kibaha katika mkoa wa Pwani; pamoja na wilaya za Kondoa na Mpwapwa katika mkoa wa Dodoma zilihusishwa katika ufuatiliaji huu ambapo kiasi cha WAVIU 20 kutoka kila kata waliteuliwa kwa usaili; hivyo jumla ya WAVIU 743 walisailiwa. Kabla ya kuanza usaili, washiriki waliarifiwa kuhusu kuzingatiwa kwa kanuni za usiri na kutakiwa kuthibitisha ridhaa ya ushiriki wao kwa maandishi. Sambamba na hilo, pia washiriki walielezwa juu ya hiari yao kujitoa kwenye utafiti wakati wowote walipopenda kufanya hivyo. Matokeo yanaonesha kuwa idadi kubwa ya washiriki wa ufuatiliaji huu (72%) walikuwa ni wanawake. Walipoulizwa kuhusu mahali pa kupatia huduma na matibabu ya VVU na UKIMWI, wengi wa washiriki (58%) walieleza kupatiwa Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013 v

huduma na matibabu kutoka kwenye zahanati; wakati 26% ya washiriki walipata huduma yao kwenye vituo vya afya; na idadi ya wanaopata huduma katika hospitali za wilaya ni 16%. Hii inadhihirisha kuwa zahanati ni sehemu ambazo hufikiwa kwa urahisi zaidi na watumiaji. Halikadhalika, ilibainishwa kuwa uchache wa watoa huduma, kutokupatikana kwa taarifa kuhusu mipango, bajeti na mapato; na matumizi ya vituo kwa wananchi (zaidi ya 90% ya washiriki) pamoja na uhaba wa mashine za CD4 ni changamoto katika vituo vya kutolea huduma za VVU na UKIMWI. Vilevile, ukosefu wa faragha (au usiri) katika vyumba vya ushauri nasaha ni tatizo kwani wagonjwa hupaswa kuchangia chumba na watu wengine wakati wa kupatiwa ushauri nasaha. Hata hivyo, matokeo yanadhihirisha kuwa katika vituo vingi vya matibabu na matunzo (asilimia 95%); upatikanaji wa dawa za kupunguza makali ya VVU (ARVs) unaridhisha. Kulingana na matokeo haya, Sikika inashauri kuwa zahanati ziboreshwe ili zitoe huduma za VVU na UKIMWI ambazo hazitolewi kwa sasa, kama zinavyotolewa katika vituo vya matunzo na matibabu (VMM). Hii ni kwa sababu idadi kubwa ya WAVIU, hasa wale wanaoishi vijijini wanatumia zahanati kupata huduma za afya. Faragha katika vyumba vya ushauri nasaha hapana budi izingatiwe ili kuimarisha dhana ya usiri. Vilevile ununuzi na matengenezo ya kipimo cha CD4 vipewe kipaumbele katika mipango na bajeti, kwa kuwa huduma hii ni muhimu sana kwa WAVIU ingawa ni WAVIU wachache sana hufikiwa na huduma hii. Mipango na bajeti ya Tume ya Utumishi wa Umma ilenge katika kuajiri na kuwaendeleza watumishi wa afya; kwani watumishi wachache waliopo, wameelemewa na kazi. vi Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013

1. Utangulizi Ili kuweza kutoa huduma za afya zilizo bora hapana budi kuwashirikisha watumiaji wa huduma hizo katika mchakato wa uboreshaji wake. Pamoja na mchango muhimu wa madaktari, manesi na wafanyakazi wengine katika kutoa huduma za afya, ni muhimu watumiaji wa huduma wakashirikishwa ili kuongeza ubora na kuhakikisha kuwa huduma hizo zinawanufaisha walengwa. Kwa mujibu wa UNAIDS, ushirikishwaji wa WAVIU wenyewe katika kuandaa na kutekeleza programu za VVU na UKIMWI ni njia muhimu ya kudumisha programu hizo. Izingatiwe kuwa WAVIU ndio wanaoishi na ugonjwa huo na hapana shaka wanaelewa mikakati inayoweza kutumika katika kudhibiti ugonjwa huo (UNAIDS, 2007). Matatizo yanayohusu upatikanaji wa huduma za afya pamoja na VVU na UKIMWI nchini, bado ni kiwazo katika kufikia afya bora hususan, kwa WAVIU. Moja ya malengo ya Sikika ni kuhimiza upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na taarifa kuhusu VVU na UKIMWI kwa wananchi. Katika shughuli ya ufuatiliaji wa utoaji huduma za afya uliofanyika kwa mwaka mzima wa 2011, katika wilaya za Ilala, Temeke, Kinondoni, Kibaha, Mpwapwa na Kondoa changamoto mbalimbali juu ya upatikanaji wa huduma za afya zilibainika. Kwa mujibu wa ripoti ya Sikika juu ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba ya mwaka 2011, imebainika kuwa uhaba wa dawa muhimu na vifaa tiba limekuwa ni tatizo la muda mrefu kwenye vituo vya huduma za afya. Kutokana na sababu hii, Sikika ilifanya ufuatiliaji ili kubaini jinsi wananchi, hasa WAVIU wanavyotathmini hali ya huduma za afya nchini. Madhumuni ya ufuatiliaji huu yalikuwa ni kubaini upatikanaji wa huduma za VVU na UKIMWI nchini. Matokeo yake yataiwezesha Sikika kutambua maeneo muhimu ya kushughulikiwa ili kuimarisha huduma za afya, na kwa namna moja ama nyingine kuliwezesha shirika kuchangia katika kuhimiza serikali kuimarisha upatikanaji wa dawa na vifaa vya kutolea huduma za VVU na UKIMWI katika vituo vya huduma za afya ambavyo vitafikiwa kwa urahisi na WAVIU. Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013 1

Ufuatiliaji huu ulilenga kuchunguza mambo muhimu, kama vile; upatikanaji wa dawa na vifaa vinavyohusiana na VVU na UKIMWI, faragha na hali ya huduma inayotolewa na watoa huduma, huduma za maabara, utoshelevu wa idadi ya watoa huduma, na upatikanaji wa taarifa kuhusu VVU na UKIMWI katika vituo vya huduma za afya. Ripoti hii ina sura tano; sura ya kwanza ni ya utangulizi na sura ya pili inaelezea mbinu zilizotumika katika kufanya ufuatiliaji. Sura ya tatu inalezea matokeo ya ufuatiliaji kwa kuzingatia maoni ya washiriki juu ya uwepo na upatikanaji wa huduma za VVU na UKIMWI. Sura ya nne inatoa hitimisho la ufuatiliaji; na sura ya tano inaelezea mapendekezo juu ya hatua za kufanya ili kukabiliana na changamoto zilizobainishwa. 2 Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013

2. Mbinu za Ufuatiliaji i Muundo wa Ufuatiliaji Ufuatiliaji huu ulikuwa ni wa kiufafanuzi ambao ulizingatia maelezo yaliyotolewa na washiriki bila kuhusisha namna yoyote ya ushawishi ambao matokeo yake yatakuwa daima wazi kwa swali na tafsiri tofauti. ii Watoa taarifa wa Utafiti Watoa taarifa katika ufuatiliaji huu walikuwa ni WAVIU waliohudhuria kwenye vituo vya huduma za afya vilivyomo katika wilaya sita za mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Dodoma, ambazo ni; Kinondoni, Ilala, na Temeke za mkoa wa Dar es Salaam, wilaya ya Kibaha katika mkoa wa Pwani, pamoja na wilaya za Kondoa na Mpwapwa katika mkoa wa Dodoma. Uteuzi wa maeneo husika ya ufuatiliaji wa Sikika ulifanywa kwa kuzingatia hali za miundombinu na kifedha ukilinganisha na maeneo mengine ambayo hayahusiki na shughuli za Sikika. iii Uteuzi wa watoa taarifa Watoa taarifa wa ufuatiliaji waliteuliwa kwa utaratibu wa bahati nasibu. Washiriki hao waliteuliwa kutoka jumla ya kata 45; ambapo kata 10 ziliteuliwa kutoka wilaya za Kinondoni, Ilala, na Temeke Kibaha, na pia kata 5 ziliteuliwa kutoka wilaya za Kondoa na Mpwapwa. Watu 20 wanaoishi na virusi vya UKIMWI (WAVIU) ambao walihudhuria katika vituo vya matunzo na matibabu (VMM) waliteuliwa kwa utaratibu wa bahati nasibu kwa ajili ya kusailiwa. Wasaili ambao pia walikuwa WAVIU waliteuliwa kwa utaratibu ufuatao; kwa mikoa ya Dar es salaam na Pwani washiriki ambao ni WAVIU, waliteuliwa kutoka orodha iliyoandaliwa na Afisa Mtendaji wa kata (AMK) pamoja na maafisa maendeleo wa jamii (OMJ). Kwa mkoa wa Dodoma mhusika mkuu wa vituo vya afya alisaidia kupatikana kwa WAVIU 20 kwa ajili ya kutoa taarifa. Kwa kuwa ufuatiliaji huu ulihusisha watu wazima pekee, watu walio chini ya umri wa miaka 18 hawakuhusishwa. Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013 3

iv Ukusanyaji wa taarifa Taarifa za ufuatiliaji zilikusanywa kwa kutumia dodoso. Kutokana na hali ya kiwango cha elimu ya watoa taarifa, dodoso zilijazwa na wahojiwa. Jaribisho la dodoso lilifanywa kwa washiriki (WAVIU) 20 ambao hawakushiriki ufuatiliaji halisi. Jaribisho hilo lilifanywa kabla ya ufuatiliaji halisi kwa lengo la kuthibitisha usahihi wa taarifa tulizokusudia kupata. Sikika ilitumia jaribisho hili kama hatua ya awali kubainisha makosa yaliyomo katika dodoso na kuyarekebisha kabla ya kuanza ukusanyaji wa taarifa. v Mazingatio ya Maadili ya Kiutafiti Kibali cha kufanya ufuatiliaji huu kilitolewa na mganga mkuu wa wilaya husika. Usaili ulifanywa mahali penye utulivu kwa wasailiwa na pia mazingira ya faragha yalizingatiwa. Kabla ya kuanza kwa usaili, washiriki wote walieleweshwa malengo ya ufuatiliaji na baadaye kujaza kibali cha kukubali. Washiriki vilevile walifahamishwa juu ya usiri wa taarifa wanazozitoa na uhuru wa wao kujitoa kwenye ufuatiliaji iwapo wangependa kufanya hivyo; na kwamba kufanya hivyo kusingekuwa na madhara kwao. Washiriki walielezwa pia taarifa watakazozitoa na kukusanywa ni kwa madhumini ya ufuatiliaji tu. Ili kuwalinda washiriki kutokana na madhara yanayoweza kutokana na majibu watakayotoa, majina yao hayakuwekwa bayana. Washiriki walithibitishiwa pia kuwa mwisho wa utafiti watajulishwa juu ya matokeo ya utafiti kupitia kata zao. vi Kuingiza na Kuchambua data Kiongozi chenye vigezo vya maswali kiliandaliwa baada ya kuandika maswali ya dodoso na kutumika katika uchanganuzi wa taarifa. Kiongozi hiki kilijaribishwa baada ya jaribisho la dodoso ili kuona kama litafaa kwa uchanganuzi wa taarifa. Baada ya ukusanyaji wa taarifa, maswali wazi yalipewa alama kulingana na hoja zilizojitokeza. Uhariri wa 4 Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013

taarifa na utoaji alama ulifanywa kutokana na majibu ya washiriki. Baadaye taarifa zilizopangwa kwenye makundi zilichanganuliwa kwa kutumia kichanganua takwimu za sayansi jamii (SPSS). Ili kuhahakikisha kuwa uchanganuzi wa taarifa ulifanywa kwa usahihi, taarifa zilihakikiwa kwa kusahihisha dosari zilizojitokeza katika uingizaji wake. vii Mipaka ya Ufuatiliaji Matokeo haya yanahusu wilaya sita ambako Sikika inafanya shughuli zake; kwa hiyo ni dhahiri kuwa hayawezi kuwa kiwakilisho cha hali ilivyo katika wilaya zote nchini. Hata hivyo, uzoefu wa WAVIU katika wilaya hizo unaweza kulinganishwa na vile ilivyo katika wilaya nyingine zenye hali zinazofanana na zile zilizobainishwa katika matokeo ya ufuatiliaji huu, na hivyo kuwa kigezo cha kuanzia katika kuimarisha muitikio wa kitaifa katika kukabili tatizo hili nchini. Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013 5

3. Matokeo na Mjadala Huduma za VVU na UKIMWI nchini kwa kawaida hutolewa na kupitia vituo vya matunzo na matibabu (VMM), ambako WAVIU hupatiwa dawa za kupunguza makali ya VVU (ARVs). Huduma nyingine zinazotolewa ni pamoja na; ushauri nasaha, matibabu ya magonjwa nyemelezi, elimu ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI, maelezo kuhusu maendeleo ya ugonjwa na namna ya kuudhibiti, kuzuia maambukizo ya kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, huduma za wagonjwa nyumbani (HWN), uzazi wa mpango, shughuli za kijamii na msaada wa kisheria. Huduma za VVU na UKIMWI hupatikana katika vituo mbalimbali kama vile hospitali za wilaya, vituo vya afya na zahanati. Kukua kwa janga la VVU na UKIMWI nchini kunaonesha ulazima wa huduma hizi kuenezwa nchini kote; vijijini na mijini na katika vituo vya huduma za afya vya ngazi zote; ili kuhakikisha kuwa huduma zinawafikia wale wote wanaozihitaji (URT, 2009). Taarifa zilizokusanywa kutoka kwa washiriki zilihusisha mambo yafuatayo; sifa za kijamii, ambapo washiriki walitakiwa waeleze ngazi za vituo wanavyohudhuria; kama vile zahanati, kituo cha afya, au hospitali ya wilaya; jinsia ya washiriki, mahali wanapoishi, umri wao, na viwango vyao vya elimu. Taarifa hizi zilikuwa muhimu kwa vile lengo lilikuwa ni kutambua namna vipengele hivi vinavyoweza kuathiri uwepo na upatikanaji wa huduma za VVU na UKIMWI. Washiriki walikuwa wakipatiwa matibabu kwa kipindi cha kati ya mwaka mmoja na miaka mitatu. Matokeo ya ufuatiliaji yanaonesha kuwa katika vituo vilivyotembelewa kumekuwa na mafanikio katika upatikanaji wa dawa za ARV na uanzishwaji wa vituo vya ushauri nasaha na kupima kwa hiari (VNH) pamoja na VMM. Hata hivyo, imedhihirika kuwa kumekuwa na changamoto mbalimbali juu ya upatikanaji wa huduma za matibabu zinazowakabili wasailiwa kwa wakati wote waliokuwa wakitumia vituo hivyo. 6 Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013

i Ngazi za kupatia huduma Kama inavyooneshwa katika umbo namba 1, idadi kubwa (58%) ya wasailiwa walipata huduma kutoka katika zahanati ukilinganisha na 26% waliohudhuria kwenye vituo vya afya na 16% katika hospitali za wilaya. Kwa mujibu wa maelezo ya washiriki, sababu ya hali hii ni kuwa zahanati zinafikika kwa urahisi na wananchi kuliko ilivyo kwa vituo vya afya na hospitali za wilaya. Huduma hizi za kinga na matibabu zinatolewa katika VMM ambavyo hupatikana katika vituo vya afya pamoja na hospitali za wilaya ambazo mara nyigi ziko mbali na wananchi. Huduma hizi hujumuisha utolewaji wa dawa za kupunguza makali ya VVU, dawa za magonjwa nyemelezi, na vipimo vya maabara (k.m. kuhesabu CD4 na huduma za kinga); ingawa siyo VMM zote, hasa zile zilizo kwenye vituo vya afya, zinazotoa huduma za kuhesabu CD4. Kutokuwepo kwa huduma za matunzo na matibabu katika ngazi ya zahanati kuna athari kubwa kwa WAVIU kwani mara nyingine WAVIU hulazimika kusafiri mwendo mrefu kwa lengo la kutafuta huduma za kinga na matibabu hususan kipimo cha CD4, bila kuwa na uhakika wa kuipata huduma hiyo. Vilevile washiriki wengi walieleza kuwa hawakuwa na vipato vya kutosha kuwawezesha kumudu gharama za safari za kwenda kwenye vituo hivyo. Kufahamu idadi ya CD4 ni jambo muhimu kwa WAVIU kwa sababu huwezesha kufahamu hali ya ugonjwa na maendeleo ya matumizi ya ARV. Umbo la 1: Ngazi ya vituo vya huduma za afya vilivyotumiwa na WAVIU. Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013 7

Matokeo haya yanadhihirisha kuwa, ingawa huduma za VVU na UKIMWI zinapaswa kuwa za bure, lakini ni dhahiri kuwa kuna gharama zilizojificha ambazo watumia huduma hulazimika kuzigharamia. Inaeleweka wazi kuwa sekta ya afya na UKIMWI hutegemea sana msaada kutoka kwa wafadhili. Kwa mujibu wa taarifa za Tume ya Kudhibiti UKIMWI nchini, zaidi ya asilimia 90 ya fedha kwa ajili ya kudhibiti UKIMWI hutoka kwa wafadhili. Ili kurekebisha tatizo hili, sekta hii iko katika mchakato wa kuanzisha Mfuko wa Taifa wa UKIMWI ambao utakuwa na jukumu la kukusanya fedha kutoka vyanzo vya ndani ya nchi kwa ajili ya shughuli za VVU na UKIMWI. Hivyo kuna umuhimu wa kuongeza kasi ya kuanzisha mfuko huo na serikali iangalie uwezekano wa kutumia sehemu ya rasilimali za mfuko huo katika kuziboresha zahanati ili ziweze kutoa huduma za VVU na UKIMWI na hivyo kuimarisha upatikanaji wa huduma bora za VVU na UKIMWI katika maeneo ya vijijini. ii. Uwiano wa Kijinsia Matokeo yanaonesha kuwa katika wilaya zilikofanyika ufuatiliaji, idadi kubwa (72%) ya wasailiwa walikuwa ni wanawake. Matokeo haya yanashabihiana na yale ya ripoti kuhusu Mwelekeo wa VVU na UKIMWI na Malaria ya mwaka 2007/08 ambayo yalionesha kuwa wanawake wanajitokeza zaidi kupima VVU na UKIMWI kuliko wanaume, kwa tofauti ya 90% na 80%. Vilevile taarifa ya serikali (URT) ya mwaka 2010 inaeleza kuwa wanaume hawakuwa tayari kupima VVU na kupata ushauri nasaha. Hii inaweza kumaanisha kwamba wanawake wanauelewa zaidi kuhusu VVU na UKIMWI ikilinganishwa na wanaume; hivyo wengi wao wanahudhuria vituo vya huduma za VVU na UKIMWI kujua hali zao. Vilevile kwa mujibu wa ripoti ya Mkakati wa Taifa wa Kinga Dhidi ya Virusi vya UKIMWI wa mwaka 2009-2012, wanawake wengi zaidi wameambukizwa VVU na UKIMWI kuliko wanaume kutokana na sababu za unyonge wa kiuchumi na kijamii. Unyonge huu hufanya wanawake kushindwa kufanya maamuzi kuhusu ngono salama kwa sababu ya nafasi yao katika jamii, vilevile maumbile ya kibailojia ya wanawake yanawafanya waambukizwe kwa urahisi kuliko wanaume, matatizo ya ubakaji na ngono za kulazimishwa yanawafanya wanawake wawe katika hatari zaidi ya 8 Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013

kuambukizwa VVU na UKIMWI. Wanawake hawawezi kufanya maamuzi juu ya matumizi ya kondomu kwa sababu katika baadhi ya tamaduni kufanya hivyo ni mwiko, isitoshe kondomu za kike ni ghali, hivyo kufanya wanawake wengi kushindwa kumudu gharama zake (Actionaid/ACORD/Save the Children, 2002; Isangula, 2012). Hapana budi ufuatiliaji zaidi ufanywe nchini ili kubaini sababu zinazowafanya wanawake wengi zaidi wahudhurie huduma za VVU na UKIMWI kuliko wanaume, hasa katika maeneo ya vijijini. Programu ya Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) ilieleza kuwa wanawake waliathirika zaidi kutokana na gharama fichika ambazo wanapaswa kulipa wakati wa kupata huduma. Wanatumia muda mwingi kusafiri na kusubiri kupata huduma, muda ambao wangeweza kuutumia kwa shughuli nyingine za kuzalisha mali, kama vile kuhudumia familia zao au kazi za shambani. Vilevile gharama ya kusafiri wao pamoja na wanao wahudumia ni gharama nyingine zinazo wakabili wanawake. Uwezekano wa wanawake kupata matibabu ni mdogo kwa sababu hawawezi kuondoka kwenda kufuata matibabu, na kuacha familia zao peke yao. Isitoshe wengi wao hawawezi hata kumudu gharama za nauli ya basi ya kwenda viliko vituo vya Matunzo na Matibabu (VMM) (Tanzania Gender Networking Program, 2011; UNAIDS/ UNFPA/ UNIFEM, 2004). Ushiriki wa wanawake katika kutetea huduma bora za VVU na UKIMWI ni jambo muhimu. Hapo awali wanawake hawakuwa na sauti katika masuala haya, hivyo jitihada za kuwashirikisha zitawapa sauti na uwezo wa kuchukua hatua. Wanawake ndio wanaohusika katika kutoa huduma za matunzo majumbani, wanawahudumia watoto yatima, wanalima mashamba na kufanya kazi za kuajiriwa ili kuhudumia familia zao. Mara nyingi, wanawake ndio wenye kubeba jukumu la kuhudumia wagonjwa majumbani. Zaidi ya hayo, wanawake hufanya kazi zote za nyumbani, kama vile kufanya usafi, kufua; mara kwa mara wanawake husafiri umbali mrefu kwenda kuchota maji (UNAIDS/UNFPA/UNIFEM, 2004; Isangula, 2012). Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013 9

Matokeo yanaonesha kuwa wanawake wengi zaidi walishiriki katika zoezi la ufuatiliaji kuliko wanaume. Lakini Sikika inafahamu kuwa ili kupata mafanikio katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI hapana budi wanaume na wanawake washiriki kwa kiwango kinacholingana katika mapambano hayo, kwa sababu kila kundi linakabiliwa na matatizo tofauti katika harakati za kinga, matibabu na ushawishi. Changamoto iliyopo kwa sasa ni namna ya kuwashirikisha wanaume, kwa sababu ni muhimu wanaume na wanawake kwa pamoja wachangie taarifa zitakazosaidia katika kuboresha huduma za VVU na UKIMWI. iii. Umri wa washiriki Katika ufuatiliaji huu Sikika ilitaka pia kubaini umri wa wananchi wanaopata huduma za VVU na UKIMWI katika vituo vya huduma za afya. Ilibainika kuwa idadi kubwa ya watu waliosailiwa walikuwa na umri wa miaka kati ya 30 na 44. Umri huu uko katika kundi la watu walioathirika zaidi na janga la VVU na UKIMWI nchini, yaani kati ya miaka 15 na 49 (URT, 2008). Umbo la 2: Umri wa washiriki 10 Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013

Matokeo haya yanaonesha kuwa ushiriki wa vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 24 na ule wa kati ya miaka 25 na 29 ulikuwa mdogo kuliko makundi mengine wakati wa ufuatiliaji huu. Hii ni pamoja na kuelewa kwamba watu walioathirika zaidi na janga la VVU na UKIMWI wako katika umri wa kati ya miaka 15 na 49. Hata hivyo ufuatiliaji huu haukuangalia kwa undani sababu za kuwepo kwa hali hii. iv. Viwango vya elimu Ufuatiliaji ulibaini kuwa asilimia 70 ya washiriki walikuwa wamehitimu kiwango cha elimu ya msingi tu, idadi ambayo ni sawa na watu 7 kati ya kila watu 10. Kundi la pili kwa ukubwa lilikuwa ni la watu ambao hawakusoma kabisa. Elimu ni kigezo kinachoweza kuathiri upatikanaji wa huduma za VVU na UKIMWI na kiwango cha elimu alichonacho mtu kinaweza kuathiri uwezo wake wa kuelewa na kuchambua masuala ya VVU na UKIMWI kama vile bajeti, sera na mipango; hivyo kuwawezesha kudai haki zao na kuwawajibisha viongozi wao. Kwa mujibu wa Mboera na wengine, (2005), kiwango kidogo cha elimu ni moja ya mambo yanayokwamisha utoaji wa habari za afya. Vikwazo vingine ni pamoja na mila, ufukara na upungufu wa wahudumu kwa uchache. Hivyo kwa mujibu wa matokeo ya ufuatiliaji huu, tunashauri wadau wahahakishe kuwa nyenzo za kutolea taarifa, uhamasishaji na ushawishi ziwe rahisi iwezekanavyo ili ziweze kueleweka na watu wengi. Hali hii itawezesha huduma za VVU na UKIMWI ziweze kupatikana kwa urahisi. Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013 11

Umbo na. 3: Asilimia ya washiriki kulingana na kiwango cha elimu Kwa mujibu wa matokeo ya Ufuatiliaji huu, inaonesha kuna uhusiano kati ya kiwango cha elimu na viwango vya kuenea kwa VVU na UKIMWI kwani imedhihirika (Rejea Umbo na. 3 hapo juu) kwamba jinsi kiwango cha elimu kinavyoongezeka ndivyo idadi ya WAVIU inavyopungua. Idadi kubwa ya washiriki (70%) walikuwa na kiwango cha elimu ya msingi wakifuatiwa na wale wasiosoma (18%) huku asilimia 12 wakiwa ni wale wenye elimu ya sekondari na kuendelea. v. Faragha na Ukarimu kwenye Vituo vya Huduma a. Kiwango cha faragha Kuhusu hali ya faragha katika vituo husika vya huduma ya afya, kiasi cha 85% ya washiriki walieleza kuwa waliridhika na hali iliyopo. Hata hivyo hoja zinazopingana zilitolewa na asilimia iliyobakia ya washiriki ambao hawakuridhika; baadhi walieleza kuwa wagonjwa zaidi ya mmoja walitumia chumba kimoja wakati wa kupatiwa ushauri nasaha, wakati jambo hili lilipaswa kuwa ni la faragha. Hali iliyopo ni aidha mtoa ushauri nasaha kutumia chumba wakati ambapo mshauri mwingine akiwemo ndani na mteja mwingine; au chumba cha kutolea ushauri nasaha kutumika kwa shughuli nyingine, kama vile kuhifadhi vitu, hivyo huwa kinatumika kwa shughuli nyingine wakati ushauri nasaha ukiwa unaendelea. Kwa mujibu wa Miongozo ya Kitaifa ya uendeshaji wa kliniki za VVU na UKIMWI (National Guidelines for the Clinical 12 Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013

Management of HIV&AIDS, 2005; 2009; 2012), kila KMM hutakiwa kutenga chumba cha faragha cha kutolea ushauri nasaha pamoja na kuwa na mtoa ushauri nasaha. b. Ukarimu Matokeo ya ufuatiliaji yanaonesha kuwa 89% ya washiriki waliridhika na hali ya ukarimu wa wahudumu. Hii inadhihirisha kuwa wahudumu katika maeneo ambako ufuatiliaji ulifanyika walijitahidi kutoa huduma kwa kiwango cha juu. Malalamiko pekee yaliyotolewa yalihusu unyanyapaa na kutolewa lugha chafu na baadhi ya wahudumu. vi Dawa na vifaa tiba a. Upatikanaji wa Dawa za Kupunguza makali ya VVU Hojaji la Sikika liliuliza kutaka kujua hali ya upatikanaji wa ARV katika vituo vya huduma vilivyopo ndani ya kata zilizoteuliwa, ambapo ilibainika kuwa kiasi cha 95% ya washiriki walieleza kuwa hawajawahi kukosa ARV pale walipozihitaji kwenye vituo vya afya. Asilimia 5 ya washiriki walieleza kuwa kuna wakati wamewahi kukosa kupatiwa ARV, lakini walithibitisha kuwa hiyo hutokea mara chache. Kwa mujibu wa usaili huu, washiriki hawakuona upungufu wa ARV kwani walizipata dawa hizo kama walivyoandikiwa. b. Huduma ya Mashine za kuhesabu CD4 Uwepo na upatikanaji wa huduma ya mashine za kuhesabu CD4 ulibainika kuwa ni changamoto kubwa katika wilaya zote zilizotembelewa. Kipimo cha kuhesabu CD4 ni kitu cha lazima kwa wagonjwa wanaopatiwa ARV. Kiwango cha CD4 humsaidia mtoa huduma kufuatilia maendeleo ya mgonjwa ili kufanya uamuzi juu ya aina ya ARV inayomfaa mgonjwa huyo. Vilevile idadi ya CD4 ni mwongozo unaoelekeza aina ya matibabu sahihi ya ARV yanayomfaa mgonjwa husika. Idadi ya CD4 vilevile husaidia kufanya uamuzi juu ya umuhimu wa kutibu magonjwa nyemelezi iwapo itabainika kuwa Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013 13

kiasi cha CD4 kipo chini ya kiwango kinachokubalika. Kwa mujibu wa miongozo ya kitaifa, VMM vina wajibu wa kutoa huduma za VVU na UKIMWI, ikiwamo pia ya kuhesabu CD4 (NACP, 2012). Wahudumu wa afya walieleza kuwa iwapo kituo hakina kipimo cha kuhesabia CD4, sampuli ya damu ya mgonjwa huchukuliwa na kupelekwa kwenye hospitali ya wilaya au mkoa kwa kufanyiwa kipimo hicho. Utaratibu huu haukuwa unafuatwa katika baadhi ya vituo vya afya vilivyotembelewa. WAVIU walieleza kuwa hulazimika kutembea umbali mrefu ili kufuata huduma ya kuhesabu CD4, kwa wale ambao hawawezi kumudu gharama za usafiri, hulazimika kuendelea kutumia dawa za ARV bila kufanyiwa kipimo cha kuhesabu CD4. Kutokana na ripoti ya Sikika (2013) kuhusu Maoni ya Wahudumu wa Afya Kuhusu Upatikanaji wa Huduma za Virusi na UKIMWI Nchini Tanzania kati ya vituo 56 vya afya vilivyotembelewa, 68% vilitoa huduma za matunzo na matibabu (VMM), huku mashine za kuhesabu CD4 zilikuwepo katika vituo 13 tu ambayo ni sawa na 23%. Kati ya mashine hizo 13, ni 38% tu zilikuwa zinafanyakazi (rejea umbo namba nne hapo chini). Tatizo hili hapana budi lipatiwe ufumbuzi kwa kuwa hesabu ya CD4 ni kipimo muhimu kinachoelekeza aina ya matibabu dhidi ya virusi ambayo mgonjwa anastahili kupatiwa. Kwa sababu hiyo ubainishaji makini wa hesabu ya CD4 ni jambo linalotakiwa kupewa kipaumbele. Hivyo, ni lazima kuwepo na mipango na utekelezaji thabiti pamoja na fedha za kutosha ili kuimarisha huduma za maabara. 14 Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013

Umbo na. 4: Vituo vya afya vyenye VMM na mashine za kuhesabu CD4 nzima c. Upatikanaji wa Kondomu katika vituo vya huduma za afya Kwa ujumla 77% ya washiriki walieleza kuwa kondomu zinapatikana kwenye vituo vya huduma za afya. Kwa mujibu wa matokeo ya ufuatiliaji huu, 60% ya washiriki walieleza kuwa wanachukua kondomu hizo. Kuchukuliwa kwa kondomu ni hatua ya mwanzo ya kuzitumia. Hivyo, kwa matokeo haya, Sikika inazishauri taasisi zinazohusika na uhamasishaji ziongeze juhudi za kushawishi watu watumie kondomu baada ya kuzichukua. vii. Idadi ya Watoa huduma (Rasilimali watu) Washiriki waliulizwa mtazamo wao juu ya idadi ya wahudumu wa afya katika VMM kama inakidhi mahitaji ya kituo. Malalamiko makubwa yaliyotolewa na washiriki katika vituo vyote ni kuwa idadi ya wagonjwa ilikuwa kubwa ikilinganishwa na ile ya madaktari na wahudumu, hali ambayo ilisababisha misururu mirefu na muda mrefu wa wagonjwa kusubiria huduma. Kati ya washiriki waliosailiwa, kiasi cha 55% walisema kuwa idadi ya wahudumu katika vituo vya matunzo na matibabu ilikuwa ya kutosha. Kiasi cha 59% ya Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013 15

wasailiwa walieleza kuwa kulikuwa na idadi ya kutosha ya wafanyakazi wa maabara. Walipoulizwa ni muda gani wanatumia kungoja kabla ya kupata huduma za maabara, wengi wa washiriki (kiasi cha 72% ya wasailiwa) walieleza kuwa hutumia wastani wa saa 1 mpaka 5. Katika wilaya ya Mpwapwa 31% ya wasailiwa walitumia wastani wa saa 3 kwenye maabara. Katika wilaya ya Kibaha, kiasi cha 45% ya wasailiwa walitumia kati ya saa 4 na 5 kwenye maabara. Wahudumu wa afya watanufaika iwapo idadi yao itaongezwa, kwani kwa kufanya hivi wataweza kutoa huduma bora zaidi na kuwapunguzia kazi hao wachache waliopo. viii Taarifa Kuhusu VVU na UKIMWI kwenye Vituo vya Huduma za Afya Kati ya washiriki waliosailiwa, zaidi ya 90% walieleza kuwa hakukuwa na taarifa zilizotolewa juu ya mipango, mapato au matumizi kuhusu VVU na UKIMWI. Hata hivyo, 56% ya washiriki walieleza kuwa taarifa nyingine zilikuwepo kwenye vituo vya afya; kama vile kuhusu lishe bora, kujikinga na kifua kikuu, na matumizi ya kondomu. Vituo vya afya vina uhaba wa elimu ya afya, taarifa na mawasiliano licha ya ukweli kwamba mambo hayo yana umuhimu mkubwa katika kudhibiti na kuzuia kuenea kwa magonjwa (Mboera et al, 2005). Kwa kawaida mahali maalumu pa kuweka matangazo ya taarifa ni sehemu ya mapokezi. Mahali pengine ni katika chumba cha mshauri. Wilayani Mpwapwa tulibaini kuwa vituo vya huduma havikuwa na ubao wa matangazo kwa kipindi cha ufuatiliaji. Hata hivyo katika kata nyingine zote, vituo vya afya vilikuwa na mbao za matangazo. 16 Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013

4. HITIMISHO Ufuatiliaji huu unaonesha matatizo wayapatayo WAVIU kuhusu huduma za afya ambazo zinatakiwa kushughulikiwa ipasavyo. Tunatarajia kuwa hii itasaidia kuimarisha juhudi za kuboresha huduma za VVU na UKIMWI nchini Tanzania. Matokeo ya ufuatiliaji yanaonesha kuwa idadi kubwa ya wasailiwa hupata huduma za afya kwenye zahanati pamoja na kwamba vituo hivyo havina huduma za kutosha za VVU na UKIMWI. Idadi kubwa ya washiriki walikuwa wanawake kuliko wanaume, hii inaweza kutafsiriwa kuwa wanawake wengi zaidi wanaelewa hali yao ya VVU kuliko wanaume. Kiasi cha 70% cha washiriki wamemaliza elimu ya msingi. Upatikanaji wa huduma za maabara umekuwa ni tatizo kubwa kwa WAVIU, ambao hudai kuwa hawapati vipimo wanavyohitaji kutokana na kukosekana kwa mashine au mashine kuwa mbovu. Tatizo la kukosekana kwa mashine za kuhesabu CD4 ndilo lililotajwa na washiriki kuwa ni tatizo kubwa zaidi. Juhudi za kuzuia maambukizi zinaathiriwa na kukosekana kwa huduma bora za maabara kunasababisha kushindwa kutambua maambukizi mapya ya VVU. Hali ya usiri ni jambo muhimu sana kwa WAVIU kwa kuwa huwapunguzia wasiwasi wa kunyanyapaliwa na huwapa wagonjwa utulivu na hali ya kujiamini kutokana na kupata huduma ya afya katika hali ya faragha. Uhaba wa vyumba vya kutolea ushauri nasaha unafanya kukosekana kwa hali ya usiri. Uchache wa wahudumu wa afya pia ni tatizo kwa wananchi. Wakati wa Ufuatiliaji tulishuhudia watu wengi waliokuwa wanangoja vipimo vya maabara, na wananchi walilalamikia tatizo la kukosekana kwa madaktari na manesi wa kutosha kuwahudumia. Hili ni tatizo katika sekta yote ya afya, lakini kwa mujibu wa ufuatiliaji huu, ni tatizo linalowaathiri zaidi WAVIU. Imedhihirika kuwa ingawa wananchi wanapata habari za kutosha kuhusu matumizi bora ya ARV na dawa za kudhibiti janga la VVU na UKIMWI, ni dhahiri pia kuwa hawapati taarifa za kutosha kuhusu namna serikali inavyoshiriki katika kupambana na UKIMWI kupitia mipango, bajeti na machapisho ya serikali. Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013 17

5. MAPENDEKEZO Washiriki wengi walipata huduma kutoka kwenye zahanati badala ya vituo vya huduma ya afya au hospitali za wilaya kutokana na umbali, hii ni pamoja na kwamba zahanati zinatoa baadhi tu ya huduma zinazohitajiwa na WAVIU. Tunashauri mamlaka za wilaya husika ziandae mipango na kutenga bajeti za kuanzisha VMM katika zahanati ili WAVIU wasilazimike kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za VVU na UKIMWI kwenye vituo vya afya na hospitali na wilaya. Ukosefu wa faragha katika vyumba vya kutolea ushauri nasaha kunapunguza hali ya usiri. Miongozo ya Kitaifa Kuhusu Matibabu ya VVU na UKIMWI ni lazima izingatiwe, hii inaelekeza kuwa kila VMM sharti iwe na chumba cha faragha pamoja na mshauri nasaha. Juhudi inatakiwa ifanyike ili kuhakikisha kuwa vyumba vya kutolea ushauri nasaha vinakuwa na faragha ya kutosha ili kuimarisha hali ya usiri. Inashauriwa serikali kwa kupitia halmashauri husika ziimarishe hali ya vyumba vilivyopo vya ushauri nasaha, pia ihakikishe kuwa inatenga vyumba mahsusi kwa ajili ya kufanyia ushauri nasaha. Upungufu wa mashine za kuhesabu CD4 ni tatizo lililobainishwa kwa wingi na watumia huduma. Huduma ya kuhesabu CD4 imekuwa hairidhishi kutokana na kukosekana kwa mashine hizo au kuwa mbovu. Tunashauri serikali kwa kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, hasa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI, itoe kipaumbele kwa mipango na bajeti za taifa inayohusu ununuzi na kufanyia matengenezo mashine za kuhesabu CD4. Kununua mashine mpya za kuhesabu CD4 na kuzifanyia matengenezo zile zilizopo kutarahisisha upatikanaji wa huduma hii kwa WAVIU wengi zaidi. Ofisi ya Rais ya Utumishi na Manejimenti ihakikishe kuwa inaongeza idadi ya watumishi katika vituo vya afya ili kukidhi mahitaji ya WAVIU na kuimarisha utoaji wa huduma muhimu. Izingatiwe kuwa ajira ya watumishi wapya wa afya lazima ipewe kipaumbele kwa kuwa ni tatizo mtambuka linalomuathiri kila mwananchi wa Tanzania na si kwa WAVIU pekee. 18 Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013

Utoaji wa taarifa, kama vile bajeti za vituo vya afya pamoja na sera kama vile za VVU na UKIMWI na zile za Sheria za UKIMWI haujazingatiwa. Tunashauri serikali ipitishe sera kutaka nakala za machapisho haya yatolewe kwa wahudumu. Kama hazikuwekwa kwenye mbao za matangazo, basi ziwekwe kwenye sehemu ya mapokezi za vituo vya afya au kwenye vyumba vya ushauri nasaha kwa wagonjwa wa VVU na UKIMWI. Taarifa nyingine zinazoweza kuwekwa kwenye sehemu ya mapokezi na vyumba vya ushauri nasaha ni pamoja na zile zinazohusu sera na sheria kuhusu VVU na UKIMWI. Kwa kuzingatia kuwa watumiaji wengi wa huduma za afya wana kiwango cha chini cha elimu, serikali ihakikishe kuwa inaandaa machapisho ambayo yanaweza kueleweka kwa urahisi kwa watumiaji. Mfano mzuri ni chapisho kuhusu sheria ya UKIMWI ya mwaka 2008 ambalo liliandaliwa na Sikika na kudhaminiwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. Hii itasaidia WAVIU kujua hatua zinazofanywa na serikali katika kuwasaidia, hivyo kujenga imani baina ya WAVIU kuwa serikali inawajali; kwa namna hiyo wao wenyewe watapata motisha ya kubuni hatua za kufanya ili kuongeza juhudi hizo. Machapisho haya yanatakiwa yatolewe kwa wananchi na ikiwezekana yapatikane kwa urahisi kwenye vituo vya Matunzo na Matibabu, kwani hapa ndipo WAVIU na wadau wengine wataweza kuwa na nafasi ya kupata machapisho haya. Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013 19

6. MAREJELEO Isangula, K.G. (2012). Improving women and family s health through integrated microfinance, health Education and promotion in rural areas. Journal of sustainable development. Vol 5 (5): 76-89. URL: http://dx.doi. org/10.5539/jsd.v5n5p76. Mboera et al. (2005). Research on knowledge systems: Determination of strategies for successful improvement of gaps for health knowledge in Tanzania. NIMR, Dar es Salaam. PEPFAR. (). PEPFAR country operational plan executive summary. PEPFAR Sikika. (2011). Medicines and medical supplies availability report. Using absorbent gauze availability survey as an entry point. A case of 71 districts and 30 health facilities across mainland Tanzania. Dar es Salaam URT. (2004). Operational plan for the national laboratory system to support HIV&AIDS care & treatment. MoHSW. URT. (2005). National guideline for the clinical management of HIV&AIDS control program. URT. (2009). National guideline for the clinical management of HIV&AIDS control program. URT. (2012). National guideline for the clinical management of HIV&AIDS control program. URT. (2008). Tanzania HIV&AIDS and Malaria indicator survey 2007-08. Government of Tanzania URT. (2009). National health laboratory strategic plan 2009-2015. MoHSW. URT. (2010). Gender operational plan for HIV response in mainland Tanzania (2010-2012). TACAIDS. URT. (n.d.). National mutisectoral HIV prevention strategy (2009-2012). TACAIDS URT. (n.d). National guideline for quality improvement of HIV&AIDS services. NACP 20 Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013

VIAMBATANISHO Kiambatanisho na: 1: Upatikanaji wa Mashine za CD4 Wilaya Kata Vituo vya afya CTCs Mashine za kuhesabu CD4 Ufanyaji kazi wa mashine Kinondoni Goba Goba hakuna Hakuna Hakuna mashine Kawe Kawe ipo Hakuna Hakuna mashine Kijitonyama Mwege ipo Hakuna Hakuna mashine Kijitonyama Kijitonyama ipo Hakuna Hakuna mashine Kimara Kimara ipo Hakuna Hakuna mashine Magomeni Magomeni hakuna Hakuna Hakuna mashine Mbezi Mbezi ipo Hakuna Hakuna mashine Mbezi Mpiji hakuna Hakuna Hakuna mashine Mwananyamala Mwananyamala ipo Ipo Haifanyi kazi Sinza Palestina ipo Ipo Inafanya kazi Tandale Tandale ipo Ipo Inafanya kazi Temeke Azimio Majimatitu ipo Hakuna Hakuna mashine Azimio Tambuka Reli ipo Hakuna Hakuna mashine Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013 21

Charambe Charambe ipo Hakuna Hakuna mashine Kigamboni Kigamboni ipo Hakuna Hakuna mashine Vijimbeni ipo Ipo Haifanyi kazi Mbagala Roundtable ipo Hakuna Hakuna mashine Mbagala Mbagala ipo Hakuna Hakuna mashine Mbagala kuu Mbagala Rangitatu ipo Ipo Haifanyi kazi Mji mwema Mji Mwema hakuna Hakuna Hakuna mashine Mji Mwema hakuna Hakuna Hakuna mashine Temeke Temeke ipo Ipo Hakuna mashine Toa ngoma Mzinga hakuna Hakuna Hakuna mashine Toangoma hakuna Hakuna Hakuna mashine Yombo vituka Malawi ipo Hakuna Hakuna mashine Ilala Ilala Amana ipo Ipo Haifanyi kazi Ilala Magereza ipo Hakuna Hakuna mashine Mchikichini Mnazi Mmoja ipo Ipo Inafanya kazi Buguruni Buguruni ipo Ipo Haifanyi kazi 22 Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013

Vingunguti Vingunguti hakuna Hakuna Hakuna mashine Kiwalani Kiwalani ipo Hakuna Hakuna mashine Chanika Chanika ipo Hakuna Hakuna mashine Kitunda Kitunda ipo Hakuna Hakuna mashine Tabata Tabata ipo Hakuna Hakuna mashine Segerea Segerea ipo Hakuna Hakuna mashine Kibaha Mlandizi Mlandizi ipo Ipo Inafanya kazi Kwala Kwala ipo Hakuna Hakuna mashine Magindu Magindu ipo Ipo Haifanyi kazi Magindu Gwata hakuna Hakuna Hakuna mashine Magindu Gumba hakuna Hakuna Hakuna mashine Magindu Lukenge hakuna Hakuna Hakuna mashine Ruvu Ruvu ipo Hakuna Hakuna mashine Ruvu Kikongo ipo Hakuna Hakuna mashine Soga Soga Hakuna Hakuna mashine Mpwapwa Mpwapwa Mjini Mpwapwa Mjini ipo Ipo Haifanyi kazi Kibakwe Kibakwe hakuna Hakuna Hakuna mashine Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013 23

Rudi Rudi hakuna Hakuna Hakuna mashine Pwaga Pwaga hakuna Hakuna Hakuna mashine Mima Mima hakuna Hakuna Hakuna mashine Kondoa Busi Busi ipo Hakuna Hakuna mashine Kondoa Town Kondoa Town ipo Ipo Inafanya kazi Hamai Hamai ipo Hakuna Hakuna mashine Kwa Mtoro Kwa Mtoro Ipo Hakuna Hakuna mashine Makorongo Makorongo Hakuna Hakuna Hakuna mashine 24 Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013

Kiambatanisho Na: 2: Hojaji DODOSO LA KUTATHIMINI UPATIKANAJI WA HUDUMA ZA VVU NA UKIMWI KWA WANANCHI Utangulizi Sikika ni shirika lisilo la kiserikali linalofanya kazi ya kuimarisha ushiriki wa jamii na kukuza uwazi na uwajibikaji katika kupanga na kutekeleza mikakati yote ya afya na UKIMWI ndani ya mifumo ya afya ya nchi katika ngazi zote kwa lengo la kuboresha huduma hizo. Dhumuni kuu la zoezi hili ni kutathmini hali ya upatikanaji wa rasilimali za kutolea huduma za VVU na UKIMWI zikiwemo dawa na vifaa na kuangalia kama rasilimali hizo zinawafikia wananchi (WAVIU) kama watumiaji wa mwisho wa huduma hizo. Matokeo ya zoezi hili yatatumika katika kuimarisha majadiliano na serikali juu ya uboreshaji wa huduma za VVU na Ukimwi kwa wananchi. Tarehe: Muda wa kuanza :... 1 Taarifa za jumla 1.1 Ngazi ya kituo ulichotembelea ( ) Hospitali ya Wilaya ( ) Kituo cha afya ( ) Zahanati ( ) Nyingine (Taja)... 1.2 Jina la kituo. 1.3 Mkoa Wilaya Kata 2 Taarifa za Msahiliwa 2.1 Jinsia : 1. Me ( ) 2. Ke ( ) 2.2 Umri wa Mhojiwa ( ) 18 24 ( ) 25 29 ( ) 30-34 ( ) 35-39 ( ) 40-44 ( ) 45-49 ( ) Miaka 50 na kuendelea Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013 25

2.3 Kata unayotoka... 2.4 Hali ya ndoa ( ) Oa/ Olewa ( ) Achika ( ) Mjane ( ) Mgane ( ) Mseja Nyingine (taja)... 2.5 Je, una watu wanaokutegemea? Ndio ( ) Hapana ( ) Kama ndiyo, taja idadi... 2.6 Kiwango cha Elimu; ( ) Darasa la nne ( ) Darasa la saba ( ) Kidato cha nne ( ) Kidato cha sita ( ) Ufundi/Cheti ( ) Shahada/Diploma ( ) Stashahada/Degree Nyingine( Taja )... 3.0 Hali ya Upatikanaji wa huduma za VVU na UKIMWI 3.1 Je, umekuwa ukipata huduma za VVU na UKIMWI katika kituo hiki kwa muda gani? 3.2 Je, unaelezeaje huduma ya ushauri nasaha inayotolewa katika kituo hiki? ( ) Nzuri ( ) Nzuri kiasi ( ) Hairidhishi Fafanua jibu lako Faragha/usiri - elezea 26 Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013

Ukarimu Usikilizwaji 3.3 Je, unaelezeaje huduma inayotolewa katika maabara? ( ) Nzuri ( ) Nzuri kiasi ( ) Hairidhishi Fafanua jibu lako Faragha/usiri - elezea... Ukarimu Majibu kwa kila maswali unayouliza/ usikilizwaji Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013 27

Maelekezo kwa kila unachofanyiwa 3.4 (a) Je, idadi ya watoa huduma za VVU na UKIMWI katika kituo hiki inakidhi mahitaji halisi ya kituo? Ndio ( ) Hapana ( ) (b)fafanua jibu lako hapo juu 4. Upatikanaji wa dawa za Kupunguza makali ya VVU na UKIMWI (ARVs) 4.1 Je, unaelezeaje hali ya upatikanaji wa dawa za kupunguza makali ya VVU na UKIMWI hapa kituoni? (muda/mahitaji ya wagonjwa)... 4.2 Je,umewahi kuhitaji dawa za kupunguza makali ukakosa? Ndio ( ) Hapana ( ) 4.3 Kama ndio, ni mara ngapi umewahi kukosa?... 28 Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013

4.4 Je, ulichukua hatua gani baada ya kukosa dawa hizo? 4.5 (a) Je, unapata maelekezo sahihi ya jinsi ya kutumia dawa za kupunguza makali ya UKIMWI kutoka kwa mhudumu wa afya? Ndio ( ) Hapana ( ) 4.6 (b) Tafadhali fafanua jibu lako.... 5. Hatua za Kukinga uenezi wa maambukizi 5.1 (a) Je, mipira ya kiume na kike (kondom) huwa inapatikana katika kituo hiki? Ndio ( ) Hapana ( ) (b) Kama ndio, je huwa unachukua? -------------------------------------- Ndio ( ) Hapana ( ) ( c ) Kama hapana, kwanini huchukui 5.2 Je, umewahi kupata huduma ya dawa za magonjwa nyemelezi katika kituo hiki? Ndio ( ) Hapana ( ) Sijui ( ) Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013 29

Fafanua jibu lako... 6 Uwazi wa taarifa za VVU na UKIMWI 6.1 (a) Je, taarifa zifuatazo zinapatikana hapa kituoni kwa ajili ya matumizi ya watumiaji wa huduma? Tiki zinazopatikana ( ) Mipango ya UKIMWI ( ) bajeti ya UKIMWI ( ) mapato na matumizi ( ) sera na sheria ya UKIMWI ( )Machapisho mengine ya UKIMWI (Taja)... 6.1 (b) Kama zipo, zinapatikana mahali gani? ( ) Mapokezi ( ) Chumba cha ushauri nasaha ( ) Maabara ( ) Kwa daktari 7 Maoni ya Msahiliwa juu ya huduma inayotolewa Je, una maoni yeyote kuhusu uboreshaji wa huduma za afya katika kituo chako?... Muda wa kumaliza:.. Jina la Msahili 30 Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013

Kiambatanisho 3 UTAMBULISHO KWA MSAHILIWA Mimi... ni mkazi wa.. na ni mtumiaji wa huduma za VVU na UKIMWI katika kituo cha.. kilichopo ndani ya kata ya... na Wilaya ya...... kwa takribani... Nashiriki katika kufanya tathmini juu ya utolewaji wa huduma za VVU na UKIMWI katika vituo vya huduma vilivyopo katika kata yetu ya Tathmini hii inaendeshwa na Sikika ambalo ni shirika lisilo la kiserikali linalofanya kazi ya kuimarisha ushiriki wa jamii na kukuza uwazi na uwajibikaji katika kupanga na kutekeleza mikakati yote ya afya na UKIMWI ndani ya mifumo ya afya ya nchi katika ngazi zote kwa lengo la kuboresha huduma hizo. Dhumuni kuu la zoezi hili ni kutathmini hali ya upatikanaji wa rasilimali za kutolea huduma za VVU na UKIMWI zikiwemo dawa na vifaa na kuangalia kama rasilimali hizo zinawafikia wananchi (WAVIU) kama watumiaji wa mwisho wa huduma hizo. Ushiriki wako ni wa hiari na hautawekwa wazi; pia unaweza kujitoa katika zoezi hili wakati wowote ule. Hakutokuwa na malipo yoyote yatakayotolewa kwa washiriki; ila tunaamini ushiriki na mchango wako utazingatiwa na matokeo ya uchambuzi wa tathmini hii yanategemewa kusaidia kuboresha huduma za VVU na UKIMWI hasa upatikanaji wa dawa na vifaa kwa wakati na kulingana na mahitaji ya watumia huduma,kuboresha maadili, uwazi na uwajibikaji kwa watoa huduma. Vilevile zoezi hili litaboresha ushiriki wa jamii katika mipango na usimamizi wa huduma za VVU na UKIMWI. Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013 31

Hivyo, ushiriki wako katika zoezi hili ni kwa kutoa taarifa zenye ukweli ili kufanikisha lengo la tathmini. MUHIMU: Msahiliwa ni lazima awe ni mtumiaji wa huduma katika kituo kinachotoa huduma za VVU na UKIMWI cha serikali. 32 Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013

Kiambatanisho 4 FOMU YA RIDHAA YA MSAHILIWA Mimi. mkazi wa... na ni mtumiaji wa huduma katika kituo cha... kilichopo ndani ya kata ya... na Wilaya ya... nimekubali kwa hiari yangu kutoa maelezo ya afya yangu na kituo ninachochukulia dawa zinazozuia makali ya UKIMWI (ARVs). Nimefafanuliwa na kuelewa vizuri dhumuni na umuhimu wa kutoa taarifa hizi, na kwamba taarifa hizi zitatumika kwa ajili ya kuboresha huduma za afya na UKIMWI Tanzania. Pia naelewa kuwa ushiriki wangu hautowekwa wazi ila taarifa nitakazozitoa zitatumika kwa madhumuni ya uboreshaji wa huduma za afya na UKIMWI na si vinginevyo. Sahihi:...... Tarehe:.. Jina la Msahili:... Sahihi:... Tarehe:.. Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013 33

34 Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013

Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI 2013 35

Sikika inafanyakazi kuhakikisha usawa na upatikanaji wa huduma bora za afya, kwa kutathmini mifumo ya afya na uwajibikaji katika ngazi zote za serikali Nyumba Na. 69 Eneo Ada Estate, Kinondoni Barabara ya Tunisia Mtaa wa Waverley S.L.P 12183 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 26 663 55/57 SMS: 0688 493 882 Faksi: +255 22 26 680 15 Barua pepe: info@sikika.or.tz Tovuti: www.sikika.or.tz Blog: www.sikika-sikika.blogspot.com Twitter: @sikika1 Facebook: Sikika Tanzania Nyumba Na. 340 Mtaa wa Kilimani S.L.P 1970 Dodoma, Tanzania Simu: 026 23 21307 Faksi: 026 23 21316