HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE

Similar documents
GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

MAADHIMISHO YA MIAKA 15 YA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame M. Mbarawa (Mb.); Waheshimiwa Mawaziri na Wabunge wote mliohudhuria;

TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM)

JAMHURI YA KENYA. Mkakati wa Ushirikiano MUKHTASARI FY Public Disclosure Authorized. Public Disclosure Authorized

Dodoma ambako kikao cha Bunge kinaendelea kuja kushiriki japo sehemu ya uzinduzi wa mkutano.

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU

TANZANIA MARKETS PAN Sera zinazoboresha masoko

Information for assessors (do not distribute this page to participants):

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )

Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA 2006/07

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA. Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo. TOLEO Na.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali ya Madini Ukanda

Azimio lililopitishwa na Mkutano Mkuu tarehe 18 Desemba 2013 [juu ya taarifa ya Kamati ya Tatu (A/68/456/Add.2)]

Dibaji ya Mwenyekiti wa Kamati ya Pamoja ya Uongozi

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA PRO-ROUTES. Ombi kwa ajili ya fedha za umma wa mradi wa ziada

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA MHESHIMIWA DKT

HAKI NA TARATIBU ZA AJIRA, KAZI NA HIFADHI YA JAMII

Kutetea Haki za Binadamu

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA,KWA WANANCHI, 30 SEPTEMBA, 2001

KAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI TANZANIA

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA UCHUMI WA ZANZIBAR

Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara)

International Labour Office. Kazi za Ndani Zenye Madhara kwa Watoto: Kijitabu cha Maelezo Mafupi

MAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI

MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2017/18

Mhashamu Askofu Jude Thaddaeus Ruwa ichi, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania; Mwadhama Policarp Kardinali Pengo,

Afya Bora, Utu na Kinga. Ripoti ya Mashauriano ya Kiufundi Aprili 2009, Hammamet, Tunisia

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

Miradi na jamii. 3.1 Utangulizi

Kimesanifiwa na:- E.D.Kissuu ECOMM TANZANIA S.L.P ,Dar es Salaam. Simu:

Kubadili Sheria Za Mbegu Na Ulinzi Wa Aina Za Mbegu Na Mimea Nchini Tanzania

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA FEDHA

TAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF) KUHUSU HAKI ZA WATOTO KATIKA KATIBA MPYA

In the matter of an Application by the KIGOMA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (KUWASA) For a Tariff and Charges Adjustment

UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU VIKWAZO VYA KULINDA MAISHA KATIKA USAIDIZI WA KIMATAIFA WA AFYA KWA MSAADA WA KIMATAIFA UNAOFADHILIWA NA MAREKANI

Human Rights Are Universal And Yet...

Songa kwenye kilele cha upeo. Masuala ya Msingi na Ujuzi juu ya Uendeshaji wa Serikali za Mitaa

5. Mheshimiwa Spika, Bunge lako Tukufu lilijadili kwa kina Miswada ifuatayo:

TAARIFA YA MWAKA YA UTENDAJI KAZI IDARA YA UTAWALA BORA 2013/2014

NGUZO KUMI ZA KILIMO KWANZA

Afya Bora, Utu na Kinga. Ripoti ya Mashauriano ya Kiufundi Aprili 2009, Hammamet, Tunisia

HUDUMA ZA AFYA KWA WOTE

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, MHESHIMIWA DKT. PHILIP I. MPANGO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO

USIMAMIZI MKUU WA UBORA WA MAHURUJI

Mwongozo wa Utekelezaji wa Njia za S5-UUE (KAIZEN)-UUU Tanzania

Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi

KITEGO CHA MAREKEBISHO NA HAKI ZA MTOTO

MAPENDEKEZO YA MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA TANZANIA

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO

Utangulizi wa ugonjwa wa shinikizo la damu

Kufanya Uwekezaji kuwa wa Manufaa kwa Afrika: Jibu la Mbunge kuhusu Unyakuzi wa Ardhi

MWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA NISHATI NA MADINI

RIPOTI YA WARSHA KUHUSU HABARI KWA AJILI YA UWAJIBIKAJI

UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA)

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII

JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI

Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2013

Kilimo cha kiekolojia cha Wakulima Wadogo Hufanikisha Haki za Mazingira

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Deputy Minister for Finance

Kuwa na Ukimwi ni kama vile kutakiwa kuendelea kuuzima moto unaoniunguza bila kukoma.

KUHUSU AFRODAD. Dira ya AFRODAD. Dhamira ya AFRODAD. AFRODAD inalenga mchakato sawa na endelevu wa maendeleo kuelekea Afrika yenye mafanikio.

RIPOTI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti

3. Mheshimiwa Spika, 4. Mheshimiwa Spika,

ONDOA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA AFYA YA WATOTO

Mwongozo wa Jamii juu ya Afya ya Mazingira

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA, KWA WANANCHI, TAREHE 31 JULAI 2001

In the matter of Application by the TANGA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (TANGA UWASA) For a Multi-Year Tariff Adjustment

HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA MHESHIMIWA

Kitabu Cha Mafunzo Ya Uongozi Kwa Wanawake

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Kiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika

Pronunciation: Mä-hret Zäläke Ndal-ka-tscho Molla Mare Gebre-gzabiär 1/12

Elimukombozi, Lugha na Upashanaji Habari nchini Tanzania, katika Muktadha wa Utandawazi

Taarifa Kuhusu Hali ya Uchumi wa Tanzania

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees

Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI Nchini Tanzania

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

Mwongozo wa Kutathimini mifumo ya Ugawanaji wa faida na Mapato Katika Miradi ya Jamii ya MKUHUMI

JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1

NGUO MPYA ZA UKOLONI. Mikataba ya Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Umoja wa Ulaya na Afrika. Agosti 2017

Sera ya Faragha. Upeo. Aina za Data na Mbinu za Ukusanyaji

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA

Kufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA SABA. Kikao cha Thelathini na Tisa Tarehe 1 Juni, (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

Summaries of GC Reports 2012, Vol. 2, Sec. 1, Swahili

Transcription:

HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE. JENISTA MHAGAMA (MB), KATIKA KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA AFYA NA USALAMA MAHALI PA KAZI DUNIANI DODOMA, 28 APRILI 2016 Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Kamishna wa Kazi Mtendaji Mkuu OSHA Mkurugenzi Mtendaji ATE Katibu Mkuu TUCTA Mkurugenzi wa ILO Wageni Waalikwa Waajiri na Wafanyakazi wote Mabibi na Mabwana Napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Mtendaji Mkuu wa OSHA na Wafanyakazi wote wa OSHA kwa kunikaribisha kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho haya ambayo waajiri na wafanyakazi wa Tanzania wanaungana na wengine duniani katika kuhimiza uboreshaji wa mazingira ya kazi ili kuzuia athari zinazoweza kutokea kwa sababu ya mazingira mabaya ya kazi. Napenda pia kutoa shukrani zangu za dhati kwa Wadau wote wakiwemo TUCTA, ATE, ILO, Washiriki wa Maonyesho, Washiriki wa Tuzo ya Afya na Usalama Mahala pa kazi na washiriki wengine wote kwa namna moja ama nyingine walivyoshiriki kikamilifu katika 1

kuhakikisha kuwa maadhimisho ya siku hii ya leo yanafanikiwa. Wadau wote hongereni sana kwa kazi nzuri. Aidha napenda kutoa pongezi za kipekee kwa washiriki wa maonyesho kwa kutuonyesha kazi nzuri mnazofanya katika kulinda afya na usalama wa wanyakazi na jamii kwa ujumla. Ndugu Wafanyakazi na Waajiri na wadau leo tumekutana hapa kuhitimisha madhimisho ya siku ya Afya na Usalama mahali pa kazi Duniani. Mwezi mzima wa Aprili umekuwa ni mwezi wa kufanya shughuli mbali mbali za kuongeza ufahamu wa masuala ya afya na usalama mahali pa kazi. Shughuli hizo zilikuwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya afya na usalama mahali pa kazi kwa wajasiliamali wadogo na kuendesha mikutano ya waajiri katika kanda zote sita. Aidha siku hii ni siku ya kufanya kampeni ya kimataifa ya kuboresha afya na usalama wa wafanyakazi inayolenga kuifanya kazi iwe ya hadhi na heshima kwa kuondoa hali zote hatarishi. Ndugu Wafanyakazi na Waajiri siku hii ilikuwa ni siku ya wafanyakazi ambayo ililenga kuwakumbuka wahanga wa ajali na magonjwa yanayotokea kazini iliyoanza kuadhimishwa mwaka 1996. Baadae Shirika la Kazi Duniani (ILO) likaona haitoshi kuadhimisha siku hii kwa ajili tu ya kuwakumbuka watu walioumia na kupoteza maisha wakiwa kazini bali pia kuna haja ya kufanya juhudi za makusudi ili kuzuia vihatarishi vinavyopelekea kuumia na kupoteza maisha kwa wafanyakazi wengine. Hivyo, kuanzia mwaka 2003 pamoja na kuwakumbuka wahanga wa ajali na magonjwa mahali pa 2

kazi pia kumekuwa na kampeni za kuzuia au kupunguza ajari na magonjwa hayo yasitokee. Katika kuzuia ajali na magonjwa ya kazi, maadhimisho ya siku hii sasa yana malengo yafuatayo: Kupanua uelewa kuhusu ukubwa na madhara ya ajali na magojwa yatokanayo na kazi miongoni mwa waajiri na wafanyakazi; Kuhamasisha namna ya kulinda afya na usalama wa wafanyakazi wakiwa kazini hasa tunapoelekea kuwa na uchumi wa Viwanda. Pia tutaendelea kusisitiza kuwa suala la Usalama na Afya Mahala pa kazi halina budi kuzingatia kanuni za kimataifa na Kuhamasisha mataifa wanachama wa umoja wa mataifa kujenga uwezo na utaalamu wa kuweka mifumo na sera zinazolenga kukinga wafanyakazi wakiwa kazini. Wafanyakazi na Waajiri, ajali na magonjwa yanatokea sehemu za kazi kwasababu ya kutoboresha mazingira ya kazi, yanasababisha hasara kubwa sana. Hasara hizo ni kama kuongezeka kwa gharama za matibabu,kupoteza baadhi ya viungo vya mwili, malipo ya fidia, uharibifu wa mali mbalimbali, kupotea kwa muda wa uzalishaji, kuingia katika gharama za kufundisha mfanyakazi mwingine iwapo aliyeumia hataweza tena kurudi kazini na kadhalika. Hasara hizo huongeza gharama za uzalishaji na husababisha kuongezeka kwa bei za bidhaa zinazozalishwa au huduma inayotolewa. Aidha hali hii husababisha kupunguza tija hali inayosababisha kudidimiza juhudi zetu katika mpango mzima wa kukuza uchumi na kuondoa umasikini. 3

Ndugu Wafanyakazi na Waajiri, kwa hali hiyo, sasa kuna haja ya kujenga utamaduni wa kuzuia ajali na magonjwa sehemu za kazi na huu ni vema ukawa ni mkakati ya kitaifa. Mkakati huu utaweka haki ya mazingira salama ya kazi kwa wafanyakazi, itakayoheshimiwa na watu wote katika ngazi zote kwa kushirikisha Serikali, Waajiri, Wafanyakazi na wadau wengine wakishirikiana wote kwa pomoja ili kuweka mazingira salama mahali pa kazi. Mkakati huo utaweka haki na wajibu wa kila mmoja wetu kuhakikisha kuwa msingi wa kuweka mazingira salama ya kazi ni kuzuia ajali Ndugu,Wafanyakazi Waajiri, na wananchi kwa ujumla, ukiuliza wafanyakazi sababu ya ajali kutokea wengi wao watajibu kuwa ajali ni matokeo ya mazingira mabaya Mahala pa kazi na ukiuliza waajiri wao watajibu kuwa ajali ni uzembe wa wafanyakazi. Hii ndio inadhihirisha kuwa wafanyakazi na waajiri hawajui kwa ufasaha ajali au hata magonjwa ya kazini yanasababishwa na nini. Lakini jambo ambalo linawezekana kusababisha ajali kwa kiwango kikubwa ni makosa ya kibinadamu. Na makosa mengi ya kibinadamu yanakuwa ni kwasababu ya kutokuwa na utamaduni wa kuzuia hizo ajali au magonjwa. Kujenga utamaduni wa kujikinga na madhara sehemu za kazi katika ngazi ya Taifa na hata katika sehemu za kazi ni muhimu sana ili kuboresha mazingira ya kazi. Uboreshaji wa mazingira ya kazi kunahitajika kuweka mifumo madhubuti ya afya na usalama mahali pa kazi ambayo ni kuweka sheria nzuri, kuimarisha ukaguzi, kutoa mafunzo kwa waajiri na wafanyakazi ikiwemo kutoa utalaamu. Ili 4

kufanikiwa katika hili waajiri na wafanyakazi kwa pamoja ni lazima wachukulie kwamba suala la afya na usalama mahali pa kazi ni sehemu ya mipango na mikakati ya uzalishaji au utoaji huduma. Ndugu,Wafanyakazi na Waajiri, ndugu wananchi sambamba na hilo mnamo mwezi June 2006 Shirika la kazi Duniani (ILO) lilipitisha mkataba mpya wa kimataifa unaoitwa Promotional Framework for Occupational Safety and Health Convention (No. 187). Mkataba huo lengo lake ni kuweka msisitizo katika kutekeleza mikataba mingine iliyotangulia ambayo yote kwa pamoja ni kuendelea kuboresha mazingiara ya kazi ili kuzuia ajali, magonjwa yatokanayo na kazi na vifo katika nchi wanachama wake. Katika kufanya hivyo msisitizo umewekwa katika mambo matatu makubwa. Mambo hayo kwanza ni kuwa na Sera ya Taifa ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi; pili kuweka mifumo imara ya utekelezaji wa sera hiyo kama vile Sheria na Mamlaka zinazopaswa kutekeleza sera hiyo; na tatu kuweka Mikakati Madhubuti ya utekelezaji. Kwetu sisi Tanzania, wakati tunajiandaa kuridhia mkataba huo tayari tumeishaanza utekelezaji wa baadhi ya mambo kama sehemu ya maandalizi. Mfano Sera ya Taifa ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi imeishapitishwa katika vyombo vyote vya Serikali na hivi sasa Serikali inaandaa mkakati wa utekelezaji. Marekebisho ya Sheria ya Usalama na Afya mahali pa kazi nayo yamefikia hatua nzuri. Tuna imani kuwa mkataba huo mara utakaporidhiwa utekelezaji wake utakuwa rahisi, na magonjwa katika sehemu za kazi yatapungua kwa kiasi kikubwa. 5

Ndugu Wafanyakazi na Waajiri, ningependa kuchukua fursa hii kuwataka waajiri kwa kushirikiana na wafanyakazi na taasisi mbali mabli za umma na binafsi kuhakikisha kuwa mifumo na sera thabiti ya kusimamia afya na usalama mahali pa kazi inawekwa sehemu zao za kazi ili kuzuia magonjwa yanayotokea Mahala pa kazi. Ndugu Wafanyakazi na Waajiri katika kufanya maadhimisho haya, Shirika la Kazi Duniani (ILO) linatoa kauli mbiu ya kila mwaka ambayo inakuwa ni kwa dunia nzima. Mwaka huu tunapo adhimisha siku hii kauli mbiu ya mwaka huu duniani kote ni Msongo wa Mawazo Sehemu za Kazi: Ni Changa Moto kwa Wote (Workplace Stress: A Collective Challenge). Siku hizi duniani kote wafanyakazi wanakumbana na mabadiliko sehemu za kazi pamoja na mahusiano mapya sehemu za kazi. Hii ni pamoja na ushindani wa kibiashara, wateja kutarajia au kuhitaji bidhaa au huduma bora zaidi kwa wakati na kwa bei nafuu. Hii imepelekea waajiri kuhitaji wafanyakazi wao wafanye kazi kwa bidii zaidi kwa masaa mengi na kwa weledi ili kukidhi mahitaji ya wateja wao. Aidha mdololo wa uchumi umesababisha waajiri wapunguze uzalishaji na kupunguza idadi ya wafanyakazi. Nafasi za ajira zimekuwa finyu, wafanyakazi wamekuwa na wasiwasi wa kupoteza kazi na wengine tayari wamepunguzwa kazi. Matokeo hayo yote ni kuwepo na vihatarishi vya kisaikolojia vinavyosababisha msongo wa mawazo mahali pa kazi miongoni mwa wafanyakazi. 6

Vihatarishi vya kisaikolojia sehemu za kazi ni muingiliano wa mazingira ya kazi, maudhui ya kazi, hali ya sehemu ya kazi, uwezo wa wafanyakazi kufanya kazi, utamaduni wa watu katika sehemu husika na mtizamo wa jamii ambayo inaweza kuathiri afya, utendaji wa kazi na kulidhika na kazi (job satisfaction). Mfano wa vihatarishi ni kama vile mazingira ya kazi kuwa hatarishi, kuwepo na michakato ya kazi (work procedures) zisizoshirikishi, kazi nyingi au ndogo kuliko uwezo wa wafanyakazi wenyewe, usalama wa ajira kuwa mdogo, muingiliano kati ya masuala ya kazini na nyumbani nk. Vihatarishi vinaweza kusababisha madhara ya kiafya kama vile magojwa ya moyo na damu, magonjwa na mifupa na misuri, msongo wa mawazo na hata kufikia hatua ya kuua mtu au kujiua. Inaweza pia kusababisha kubadili tabia ya maisha mfano kuvuta sigara kupita kiasi, unywaji wa pombe au Ulevi wa kupindukia, kula hovyo bila kufuata misingi ya kiafya, kukosa usingizi wa kutosha nk. Vihatarishi hivyo pia vinaweza kuhusishwa na kuongezeka kwa wafanyakazi kutohudhuria kazini au wafanyakazi wengine kuja kazini wakiwa na matatizo ya kiafya, wafanyakazi kukosa morali ya kufanya kazi na kujituma kwa bidii, wafanyakazi kuacha kazi au kutamani kuacha kazi, wafanyakazi kukosa umakini na ufanisi katika kazi nk. Vitu vyote hivyo vina fanya kampuni husika kukosa ushindani wa kibiashara na kampuni nyingine na kushuka kwa tija katika kampuni husika. Sehemu ya kazi huwa ya mashaka na hali ya kutojiamini kazini miongoni mwa wafanyakazi. 7

Ndugu,Wafanyakazi na Waajiri napenda kutoa wito kwa waajiri kwa kushirikiana na wafanyakazi kufanya juhudi za pamoja ili kuondoa hivyo vihatarishi vya kisaikologia. Upande wetu sisi serikali kwa kupitia OSHA tutakuwa tayari kutoa msaada na ushauri wa kiufundi wa namna ya kupunguza au kumaliza vihatarishi hivyo. Ndugu, Wafanyakazi, Waajiri na wadau tunapokutana kama hivi sio vibaya tukakumbushana masuala ya VVU na Ukimwi kwa kuwa mpaka sasa hakuna tiba pamoja na kuwa yapo madawa yanayo punguza makali ya virusi na kuongeza maisha ya waathirika. Wafanyakazi ndio wako katika hatari kubwa ya kupata maambukizo. Kwa hiyo kama lilivyo kwa ajali na magonjwa yanayotokana na kazi ni lazima tujenge utamaduni wa kuendeleza mapambano ya kutatua matatizo yanayo tufanya tusifikie lengo letu. Matatizo hayo ni kama vile kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu ukimwi, kuwepo ukimya mkubwa, unyanyapaa, kuendekeza ngono zembe, rushwa ya ngono sehemu za kazi, na vitendo visivyo vya haki kwa waathirika wa ukimwi. Kama ilivyo katika mtizamo wa Dunia kwa sasa ni lazima tufanye mambo matatu ambayo ni kutokomeza maambukizo mapya ya VVU, kumaliza kabisa vifo vinavyotokana na UKIMWI na kuondoa kabisa ubaguzi na unyanyapaa. Serikali ya Tanzania imepitisha Sera ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI ya mwaka 2012 na Mkakati wa Tatu wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI (2013 2017) ambapo lengo ni katika kinga na matibabu ya VVU. Mkakati wa Tatu wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI, ni 8

muhimu kushughulikia makundi muhimu ya watu walio hatarini kuambukizwa VVU badala ya wananchi kwa jumla, na wafanyakazi ni moja kati ya makundi muhimu sana. Ndugu Wafanyakazi na Waajiri, Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kufufua upya uchumi wa viwanda. Katika kufufua uchumi huyo kutakuwepo na uwekezaji mkubwa katika viwanda na ajira nyingi zitapatikana ambazo zitafanya Wantazania wengi zaidi kuajiriwa. Pia katika mnyororo mzima wa thamani ya ufufuaji wa viwanda hivyo, zitakuwepo shughuli mbali mbali kama vile usafirishaji, ongezeko la kilimo cha mazao ghafi, ukuaji wa sekta ya utoaji huduma nk. Aidha katika siku za karibuni tumeshuhudia jinsi sekta ya ujenzi inavyokua kwa haraka na kuongezeka kwa majengo makubwa nchini hasa katika majiji ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, na Mbeya. Tumeona katika kipindi cha takribani miaka kumi iliyopita kumekuwa na ongezeko kubwa la uwekezaji katika migodi ya madini mbalimbali kama vile dhahabu, uraniamu, madini ya vito n.k. Nchi yetu pia imegundua gesi asilia, uchimbaji wa gesi hiyo umeanza na utafiti zaidi unaendelea. Pia inawezekana tukagundua mafuta ya petrol kwa kuwa dalili zipo kubwa. Swali la kujiuliza ni kuwa ni gharama gani tutakazolipa kwa ongezeko la uwekezaji huo? Jibu lake ni rahisi. Katika uwekezaji huo kuna na kutakuwepo na ongezeko kubwa la vihatarishi. Wafanyakazi watakao jihusisha na shughuli zote hizo watakabiliwa na vihatarishi vya afya na usalama vya aina mbalimbali kulingana na shughuli watakazokuwa wanazifanya. 9

Hali hiyo itasababisha ajali na magonjwa yatokanayo na kazi kwa wafanyakazi wetu na kuingia gharama mbalimbali iwapo hatutaanza kujiwekea tahadhari endelevu. Kwa upande wetu sisi Serikali tumejipanga kukabiliana na vihatarishi hivyo. Kwa hiyo ningependa kutoa wito kwa wadau wote watuunge mkono ili tuweze kupambana na vihatairishi hivyo. Sisi kama Serikali tutatoa miongozo mbalimbali ya namna ya kukabiliana na vihatarishi hivyo na tutawaomba wadau wafuate miongozo hiyo. Serikali pia inathamini juhudi za makampuni ya umma na binafsi au waajiri kwa ujumla kwa kushirikiana na wafaanyakazi wanaojituma katika kuboresha mazingira ya kazi wao wenyewe bila kusukumwa. Hivyo kwa kupitia Wakala wa Usalama na Afya mahali pa Kazi (OSHA), Serikali imeanzisha tuzo maalumu kwa watu watakao kuwa wanaonyesha juhudi katika kuboresha mazingira ya kazi kwa kuweka mifumo ya afya na usalama kazini iliyoimara. Napenda kuchukua furusa hii kuzipongeza kampuni zilizofanikiwa kupata tuzo mwaka huu. Mwisho ningependa kusisitiza kuwa, serikali kamwe haitapuuza suala la Usalama na Afya Mahala pa Kazi na hivyo itaendelea kushirikiana na wadau wote ili kupunguza au hata ikiwezekana kuondoa kabisa vifo, ajali, magonjwa na madhara yatokanayo na kazi. Baada ya kusema hayo napenda kuwashukuru wote mlioshiriki kikamilifu katika maadhimisho haya. ASANTENI KWA KUNISIKILIZA. 10