KAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI TANZANIA

Similar documents
Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI Nchini Tanzania

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM)

Songa kwenye kilele cha upeo. Masuala ya Msingi na Ujuzi juu ya Uendeshaji wa Serikali za Mitaa

Information for assessors (do not distribute this page to participants):

Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi

Miradi na jamii. 3.1 Utangulizi

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA 2006/07

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )

MAADHIMISHO YA MIAKA 15 YA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )

MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2017/18

MWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI

UFUATILIAJI WA MIRADI NA TATHMINI

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig

Kuuelewa Mchakato wa Bajeti Tanzania Mwongozo wa Asasi za Kiraia

In the matter of an Application by the KIGOMA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (KUWASA) For a Tariff and Charges Adjustment

ORDER NO BACKGROUND

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

Dibaji ya Mwenyekiti wa Kamati ya Pamoja ya Uongozi

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA. Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo. TOLEO Na.

JAMHURI YA KENYA. Mkakati wa Ushirikiano MUKHTASARI FY Public Disclosure Authorized. Public Disclosure Authorized

TAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF) KUHUSU HAKI ZA WATOTO KATIKA KATIBA MPYA

MAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU

RIPOTI YA WARSHA KUHUSU HABARI KWA AJILI YA UWAJIBIKAJI

KUHUSU AFRODAD. Dira ya AFRODAD. Dhamira ya AFRODAD. AFRODAD inalenga mchakato sawa na endelevu wa maendeleo kuelekea Afrika yenye mafanikio.

HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA MHESHIMIWA DKT

TAARIFA YA MWAKA YA UTENDAJI KAZI IDARA YA UTAWALA BORA 2013/2014

Human Rights Are Universal And Yet...

Makala ya Mshiriki wa Mafunzo

Ufanisi katika Ufundishaji kwenye Shule za Msingi na Sekondari nchini Tanzania

Mwongozo wa Mwezeshaji

RIPOTI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI

Kimesanifiwa na:- E.D.Kissuu ECOMM TANZANIA S.L.P ,Dar es Salaam. Simu:

Mipango ya miradi katika udugu

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Kutetea Haki za Binadamu

Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara)

MAPENDEKEZO YA MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA TANZANIA

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

TANZANIA MARKETS PAN Sera zinazoboresha masoko

KUSHUKA KWA HADHI YA LUGHA ZA JAMII NCHINI TANZANIA YOHANA P. MSANJILA University of Dar es Salaam, Tanzania

NGUZO KUMI ZA KILIMO KWANZA

Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame M. Mbarawa (Mb.); Waheshimiwa Mawaziri na Wabunge wote mliohudhuria;

SautiElimu. Sauti Yako Isikike

Mwongozo wa Utekelezaji wa Njia za S5-UUE (KAIZEN)-UUU Tanzania

Kufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007

Kitabu Cha Mafunzo Ya Uongozi Kwa Wanawake

Sera ya Faragha. Upeo. Aina za Data na Mbinu za Ukusanyaji

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti

Unyanyasaji wa Watoto & Kutelekezwa

KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA

Vijana wanazungumza kuhusu ujinsia, maisha na uhusiano VIJANA WANAZUNGUMZA KUHUSU NGONO, MAISHA NA UHUSIANO. Training and Research Support Centre

In the matter of Application by the TANGA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (TANGA UWASA) For a Multi-Year Tariff Adjustment

Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali ya Madini Ukanda

Dodoma ambako kikao cha Bunge kinaendelea kuja kushiriki japo sehemu ya uzinduzi wa mkutano.

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA

MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA PRO-ROUTES. Ombi kwa ajili ya fedha za umma wa mradi wa ziada

Programu ya Uendelezaji Mifumo ya Maji Vijijini (PUMMV) katika Tanzania. Modeli wa Ukodishaji Mradi

UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU VIKWAZO VYA KULINDA MAISHA KATIKA USAIDIZI WA KIMATAIFA WA AFYA KWA MSAADA WA KIMATAIFA UNAOFADHILIWA NA MAREKANI

Ufundishaji wa lugha nyingine

Mwongozo wa Mafunzo Yaliyochanganywaya K4Health

Mwongozo wa Kutathimini mifumo ya Ugawanaji wa faida na Mapato Katika Miradi ya Jamii ya MKUHUMI

Azimio lililopitishwa na Mkutano Mkuu tarehe 18 Desemba 2013 [juu ya taarifa ya Kamati ya Tatu (A/68/456/Add.2)]

Afya Bora, Utu na Kinga. Ripoti ya Mashauriano ya Kiufundi Aprili 2009, Hammamet, Tunisia

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

KITEGO CHA MAREKEBISHO NA HAKI ZA MTOTO

Mwongozo kwa familia zinazofanya kazi pamoja kwa maisha endelevu. Nyenzo ya Mafunzo

Mazoezi yaliyofanyika wakati wa warsha kuhusu Elimu-Jumuishi kwa Vitendo. Zanzibar, 7-10 Februari 2006

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TANZANIA TAARIFA YA MWISHO WA UTEKELEZAJI

USIMAMIZI MKUU WA UBORA WA MAHURUJI

KUCHUNGUZA MASUALA YA KISIASA KATIKA RIWAYA ZA SHAABAN ROBERT: MFANO WA KUSADIKIKA NA KUFIKIRIKA

HUDUMA ZA AFYA KWA WOTE

Nilikua na Ndoto ya Kumaliza Shule Changamoto za Elimu ya Sekondari Tanzania

UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA)

HAKI NA TARATIBU ZA AJIRA, KAZI NA HIFADHI YA JAMII

Afya Bora, Utu na Kinga. Ripoti ya Mashauriano ya Kiufundi Aprili 2009, Hammamet, Tunisia

ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA UCHUMI WA ZANZIBAR

Shabaha ya Mazungumzo haya

Elimu Bora, lakini... C HakiElimu Elimu bora, lakini...

Mwongozo wa Jamii juu ya Afya ya Mazingira

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees

MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA. Kwa Wanaoanza

Govt increases vetting threshold of contracts

Draft 03 MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO MWENGE

Elimu-Jumuishi Kwa Vitendo

Transcription:

KAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI TANZANIA KAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI TANZANIA NI UFUMBUZI KATIKA KUSHIRIKISHA JAMII? NI UFUMBUZI KATIKA KUSHIRIKISHA JAMII? Februari, 2013 Februari, 2013

SHUKURANI Kwa niaba ya Idara ya VVU na UKIMWI ambayo iliendesha ufuatiliaji huu, ninapenda kuwashukuru kwa dhati wale wote walioshiriki katika kufanikisha ufuatiliaji huu. Kwanza ninamshukuru Mkurugenzi Mkuu wa Sikika Bw.Irenei Kiria kwa msaada mkubwa alioutoa katika kufanikisha ufuatiliaji huu. Ninawashukuru pia wanaidara wenzangu; Daniel Mugizi, Aisha Hamis na Norah Mchaki kwa kujituma bila kuchoka katika hatua zote za ufuatiliaji huu. Vilevile ninawashukuru kwa dhati wafanyakazi wa Sikika pamoja na Jason Lakin kutoka IBP kwa mchango mkubwa wa mawazo waliotupatia wakati wa mchakato wa kuandaa ripoti hii. Ninapenda pia kutambua mchango wa Dr Isangula Kahabi aliyepitia muswada wa ripoti hii, msaidizi wa Sikika, Bw. Frank Lymo ambaye pamoja na wasaidizi wengine walifanya kazi bila kuchoka wakati wa kukusanya na kuchambua data. Ninawashukuru kwa dhati pia viongozi wa wilaya za Kinondoni, Temeke, Ilala, Kibaha, Kondoa, na Mpwapwa; ikiwa ni pamoja na makatibu kata (KMK), makatibu wa vijiji (KWK) na maafisa maendeleo ya jamii (AMJ) kwa kutuunga mkono na kushirikiana nasi katika ufuatiliaji huu. Vilevile wajumbe wote wa KZU waliokubali kushiriki katika ufuatiliaji huu, tunawashukuru sana. Mwisho ninatoa shukurani kwa Dr P. P. Lipembe kwa kutafsiri ripoti hii. Tusekile Mwambetania Mkuu wa Idara ya VVU na UKIMWI Sikika Company Limited Hakimiliki 2013 Kampuni ya Sikika, Haki zote zimehifadhiwa Chapisho namba: 2, 2013. Tarehe ya kuchapishwa Februari 2013 Imeandaliwa na: Sikika, Idara ya VVU & UKIMWI Picha ya Mbele: Wajumbe wa Kamati za Kudhibiti UKIMWI Kondoa i

YALIYOMO Orodha ya Majedwali na Maumbo... iii Orodha ya Vifupisho... iv Muhtasari wa Utekelezaji... v Utangulizi... 1 Mbinu za Ufuatiliaji... 2 Muundo wa Ufuatiliaji... 2 Watoa Taarifa wa Ufuatiliaji... 2 Uteuzi wa Watoa Taarifa... 2 Ukusanyaji wa Taarifa... 2 Mazingatio ya Maadili ya Kiufuatiliaji... 2 Kuingiza na Kuchambua Taarifa... 3 Mipaka ya Ufuatiliaji... 3 Matokeo Na Mjadala... 4 Wajumbe wa Kamati... 4 Kiwango cha Elimu... 4 Mikutano... 5 Uhusiano Kati ya Halmashauri na KZU... 5 Uhusiano Kati ya KZU na Jamii... 6 Uwiano wa Kijinsia... 6 Miongozo ya Kamati za Kudhibiti UKIMWI... 6 Majukumu na Wajibu wa KZU... 7 Ushiriki wa Kamati Katika Kupanga... 8 Mbinu za Kubainisha WAVIU... 8 Hitimisho & Mapendekezo... 10 Marejeo... 11 Kiambatisho... 12 ii

ORODHA YA MAJEDWALI NA MAUMBO Jedwali 1 Viwango vya Elimu vya Wajumbe wa KZU Jedwali 2 Idadi ya wajumbe wa KZU waliothibitisha kupokea mrejesho kutoka halmashauri Jedwali 3 Idadi na asilimia ya wajumbe wa KZU wanaoshiriki katika kufanya mipango ya shughuli za Serikali za Mitaa Umbo 1 Asilimia ya KZU zilizokutana kila mwezi, zilizokutana angalao mara moja au hazikukutana kabisa. Idadi kubwa ya KZU hazijakutana kutoka zilipoundwa katika maeneo yao. Umbo 2 Idadi ya wajumbe wa KZU waliothibitisha kuwa walitoa mrejesho kwa jamii zao Umbo 3 Njia ambazo KZU hutumia kutambua mahitaji ya WAVIU iii

ORODHA YA VIFUPISHO AMJ IBP International Budget Patnership KWK Katibu wa Kijiji AMK Afisa Mtendaji wa Kata KZU Kamati za UKIMWI KZUK Kamati za UKIMWI za Kata KZUV Kamati za UKIMWI za Vijijni SPSS Kichanganua Takwimu za Sayansi Jamii TACAIDS Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania UKIMWI Upungufu wa Kinga Mwilini VVU Virusi vya UKIMWI WAVIU Wanaoishi na virusi vya UKIMWI iv

MUHTASARI WA UTEKELEZAJI Kamati za Kudhibiti UKIMWI (KZU) kwenye ngazi za kijiji/mtaa na kata ni njia mojawapo ya kuwahu-sisha wananchi katika kukabiliana na janga la VVU na UKIMWI. Miongozo ya kuunda KZU ilianzishwa mwaka 2003 kwa lengo la kuwawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika masuala ya VVU na UKIMWI katika ngazi ya jamii. Lengo la ufuatiliaji huu lilikuwa ni kubainisha iwapo KZU zinafanya kazi kikamilifu kutoa nafasi kwa wananchi kushiriki katika kupanga mipango na kufanya maamuzi kuhusu masuala ya VVU na UKIMWI. Mwaka 2011 Sikika iliendesha ufuatiliaji katika wilaya sita zilizomo katika eneo lake la kazi; wilaya hizo ni Kinondoni, Temeke, Ilala za jijini Dar es salaam; wilaya ya Kibaha katika mkoa wa Pwani; na wilaya za Mpwawa na Kondoa katika mkoa wa Dodoma. Ufuatiliaji wenyewe ulifanywa kwa madhumuni ya kufuatilia shughuli za KZU hususani mafanikio yake katika kufanikisha huduma za VVU na UKIMWI nchini, kubainisha changamoto zinazoikabili na hatimaye kubainisha njia za kuboresha utendaji kazi wake. Jumla ya wajumbe 78 wa KZU walisailiwa kwa kutumia dodoso elekezi katika kata 42. Katika mkoa wa Dodoma, wajumbe watatu wa KZU walijaza dodoso kwa kila kata. Kwa mikoa wa Dar es salaam na Pwani, wajumbe wawili wa KZU kutoka kila kata walijaza dodoso. Taarifa zilichanganuliwa kwa kutumia kichanganua takwimu za sayansi jamii (SPSS). Matokeo ya ufuatiliaji huu yalionesha kuwa; KZU zipo kinadharia tu katika muundo wa serikali za mitaa, na mara kwa mara hazifanyi kazi kulingana na malengo ya kuanzishwa kwake. Kimuundo, kamati zilikuwa na wajumbe wengi zaidi wanaume (asilimia 67) kuliko wanawake (asilimia 33), hali inayodhihirisha kuwa jitihada zaidi zinatakiwa kufanywa ili kukuza ushiriki wa wanawake katika KZU. Ilidhihirika pia kuwa kiasi cha asilimia 23 ya wajumbe waliohojiwa hawakuwa wanafahamu kazi na wajibu wao kama wajumbe wa KZU; jambo ambalo liliwafanya washindwe kutekeleza wajibu wao kikamilifu. Vilevile hata wale walioelewa wajibu wao, hawakuwa wakiutekeleza kikamilifu. Ilibainika vilevile kuwa baadhi ya miongozo inayohusu utendajikazi wa KZU haikufuatwa kikamilifu; Ilionekana vilevile kulikuwa na uhusiano dhaifu kati ya KZU, halmashauri na wananchi. Mara kwa mara halmashauri hazikutoa mrejesho kwa KZU kuhusu maamuzi yanayofanywa kwenye ngazi ya wilaya, hali kadhalika KZU hazikuwasilisha taarifa kwa wananchi. Zaidi ya hayo asilimia 81 ya wajumbe hawakuelewa lolote juu ya kupanga mipango na kuandaa bajeti, hii ilitokana zaidi na kutoshiriki kwao kwenye michakato husika. Zaidi ya hayo njia za kutambua mahitaji ya jamii, hasa watu wanaoishi na VVU (WAVIU) hazikuwa wazi. Kwa mujibu wa matokeo ya ufuatiliaji huu, Sikika inashauri yafuatavyo; taratibu za uundaji wa KZU zifuate miongozo iliyotolewa. Miongozo hiyo haina budi irekebishwe mara kwa mara ili kuhakiki mapungufu yaliyojitokeza; hususani suala la kubainisha mahitaji ya wananchi. Vilevile wajumbe wa KZU wanahitaji kupatiwa mafunzo juu ya namna ya kutekeleza wajibu na majukumu yao mara tu wanapochaguliwa na baada ya hapo. Kwa kufanya hivyo wajumbe wa KZU watakuwa na uwezo zaidi wa kuweka mipango na kuandaa bajeti katika ngazi ya jamii. Vilevile muundo wa KZU hapana budi utoe nafasi sawa ya kijinsia ili kuwawezesha wanawake wengi zaidi kushiriki kikamilifu katika kukabiliana na janga la VVU na UKIMWI. v

UTANGULIZI Ushirikishaji wa jamii katika mchakato wa kufanya maamuzi kuhusu kupanga mipango, kuandaa bajeti na kutekeleza shughuli za VVU na UKIMWI ni suala muhimu sana katika harakati za kupambana na janga la VVU na UKIMWI. Ushirikishaji wa jamii katika kubainisha matatizo, kuweka vipaumbele na kutoa suluhisho lenye kuzingatia uhalisia wa jamii husika ni muhimu katika kukabiliana na VVU na UKIMWI. Israel (Isangula, 2012, uk. 15) amebainisha kuwa utumiaji wa mipango jamii shirikishi ni msingi wa mafanikio ya mpango husika. Wananchi wana mchango mahususi katika kuandaa mipango kulingana na vipaumbele vya jamii husika (Bassler, Brasier, Fogle, na Taverno, 2008). Hata hivyo ni dhahiri kuwa uhusishaji wa jamii katika kubuni, kuandaa na kutekeleza mipango kuhusu shughuli za VVU na UKIMWI hazijaenea sana nchini Tanzania. Shirika la Sikika linajihusisha na watumiaji huduma, watoa huduma na waandaaji sera za kufuatilia uwajibikaji wa jamii katika sekta ya afya na UKIMWI. Sikika lina wajibu wa kuhimiza ushirikiwa jamii katika kupanga, kuandaa bajeti na kutekeleza mipango. Vilevile Sikika linahusika katika kufuatilia na kuchambua bajeti za sekta ya afya na VVU/UKIMWI katika ngazi ya mitaa na serikali kuu. Katika utekelezaji wa shughuli zake za kawaida kwenye jamii, Sikika ilibaini kuwa wananchi hawakuwa wakihusishwa kikamilifu katika kupanga na kutekeleza mipango inayohusu masuala yanayoathiri maisha yao, kama vile afya na VVU na UKIMWI. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (2008) ilibaini ushirikishaji ha ifu kama ilivyoelezwa katika waraka wa serikali; Mara nyingi walengwa a maandalizi ya mipango,w otakahcm akitak u ilimakik wihsisuhawahkwa umiliki na mvuto kwa wananchi (uk. 27). hali inayopelekea kukosekana Kutokana na ushirikishaji ha ifu wa jamii katika masuala ya VVU na UKIMWI, serikali ya Muungano wa Tanzania imechukua hatua mbalimbali, ikiwamo ile ya kuanzisha Kamati za Kudhibiti UKIMWI (KZU). Miongozo ya uundaji wa KZU ilizinduliwa mwaka 2003 kwa lengo la kuweka msingi madhubuti wa kukabiliana na VVU na UKIMWI na kuchangia katika kuandaa shughuli za VVU na UKIMWI katika ngazi ya jamii. Miongozo ya KZU inazielekeza kamati hizo kuzihusisha jamii katika mchakato wa maandalizi mipango inayohusu kukabiliana na janga la VVU na UKIMWI, kuongeza uelewa na kutunza taarifa kuhusu shughuli za VVU na UKIMWI (Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 2003). Pamoja na kuanzisha KZU, serikali pia imetenga kasma ndani ya bajeti yake kwa lengo la kuimarisha KZU katika ngazi za kijiji/mtaa na kata. Hata hivyo, licha ya juhudi zilizofanywa katika kuongeza kiwango cha uhusishaji wa jamii katika maandalizi ya mipango kuhusu masuala yanayowahusu, bado kuna dalili ndogo za mafanikio ya juhudi hizi kutoka kwa jamii. Kutokana na hali hiyo, Sikika iliamua kufanya ufuatiliaji ili kujua hali ya KZU, ukilenga hasa hali ya utendaji kazi wake hususani ushiriki wa jamii. Lengo likiwa ni kuongeza uwezo wa kupambana, kutekeleza na hatimaye kuimarisha huduma zinazohusu VVU na UKIMWI nchini Tanzania. Katika ripoti hii tunaeleza matokeo ya ufuatiliaji na kushauri njia za kuboresha huduma hizo. Taarifa hii imegawanyika katika sehemu tano, Sehemu ya kwanza inatoa utangulizi wa ufuatiliaji; sehemu ya pili inaelezea njia zilizotumika katika kufanya ufuatiliaji huu na mipaka ya ufuatiliaji wenyewe. Sehemu ya tatu, inaelezea matokeo ya ufuatiliaji na kujadili kwa undani udhaifu uliobainika juu ya utendajikazi wa KZU. Sehemu ya nne, inatoa uchambuzi kwa ufupi kabla ya kuhitimisha na kutoa mapendekezo; sehemu ya tano, inatoa mapendekezo juu ya hatua za kufuata ili kurekebisha matatizo yaliyobainishwa. 1

MBINU ZA UFUATILIAJI MUUNDO WA UFUATILIAJI Ufuatiliaji huu ulikuwa ni wa kiufafanuzi, taarifa zilikusanywa kwa kutumia njia ya dodoso zilizojibiwa na wajumbe wa Kamati za Kudhibiti UKIMWI katika ngazi kijiji/mtaa na kata. WATOA TAARIFA Z A UFUATILIAJI Watoa taarifa za ufuatiliaji walikuwa ni wajumbe wa Kamati za Kudhibiti UKIMWI kutoka katika wilaya sita zilizo katika eneo la mradi wa Sikika. Wilaya hizo ni za Kinondoni, Ilala, na Temeke katika mkoa wa Dar Es Salaam, Kibaha katika mkoa wa Pwani, na wilaya za Kondoa and Mpwapwa katika mkoa wa Dodoma. Kwa mujibu wa miongozo iliyotolewa, wenyeviti wa kijiji/mtaa au diwani moja kwa moja huwa ndio wenyeviti wa KZU wa kijiji/mtaa na kata husika. Kwa mujibu wa miongozo, watendaji wa kijiji/mtaa na watendaji kata huwa ndio makatibu wa KZU. Eneo husika la ufuatiliaji wa Sikika liliteuliwa kutokana na sababu za kimiundombinu na kifedha ukilinganisha na maeneo mengine ambayo hayahusiki na shughuli za Sikika. UTEUZI WA WATOA TAARIFA Wajumbe wa kamati kwenye ngazi za vijiji/mitaa na kata walibainishwa kwa msaada kutoka kwa maafisa watendaji wa kata. Kata 10 ziliteuliwa katika kila wilaya za Kinondoni, Ilala, na Temeke pia kata 5 ziliteuliwa kutoka kila wilaya za Kibaha, Kondoa na Mpwapwa, hivyo kufanya jumla ya kata 45 ambako watoa taarifa walihusishwa. Wajumbe wawili wa KZU waliteuliwa kutoka kila kata ya mikoa ya Dar es salaam na Pwani, mmoja kutoka ngazi ya kata na mmoja wa ngazi ya kijiji/mtaa. Kutoka mkoa wa Dodoma walichaguliwa wajumbe watatu wa KZU. Idadi tarajiwa ya washiriki ilikuwa wajumbe 100, lakini ni wajumbe 78 tu walioweza kupatikana. Zifuatazo ni sababu zilizofanya kata zilizopo mkoa wa Dodoma kutoa washiriki watatu tofauti na mkoa wa Dar es salaam ambazo washiriki wawili walihusishwa kutoka katika kila kata; Dodoma ni eneo jipya la mradi wa Sikika na pia kata zinazohusika na mradi zimetengana sana. Kwa hiyo idadi kubwa zaidi ya watoa taarifa ilihitajiwa kwa kuwa wahusika hao watakuwa na maoni tofauti kwa sababu ya umbali na tofauti ya maeneo wanayoishi. Sababu nyingine ni kuwa, kwa vile hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Sikika kufanya ufuatiliaji katika mkoa wa Dodoma, ilikuwa muhimu kuhusisha watu wengi zaidi kutoka katika kila kata; kwa kufanya hivyo ilitarajiwa kuwa taarifa zitakazokusanywa zitakuwa na upeo mpana wa uzoefu na maoni ya watu. UKUSANYAJI WA TAARIFA Taarifa za ufuatiliaji zilikusanywa kwa kutumia njia ya dodoso. Jaribio la wajumbe 10 wa KZU ambao walichaguliwa kwa nasibu na ambao sifa zao zililingana na wahusika halisi na ambao hawakushiriki katika ufuatiliaji huu. Jaribio la dodoso lilifanywa kabla ya kuanza kwa ufuatiliaji wenyewe, lengo likiwa kutambua muda utakaotumika katika kuendesha usaili na pia kutambua usahihi wa maswali. Baada ya kufanya jaribio la dodoso, marekebisho kidogo yalifanywa kwa kuondoa baadhi ya maswali yaliyojirudia. MAZINGATIO YA MAADILI YA KIUFUATILIAJI Washiriki walikubali kushiriki katika ufuatiliaji kwa hiari yao. Hili lilitekelezwa kama ifuatavyo; kabla ya kutoa dodoso, mtafiti alielezea lengo na sababu ya ufuatiliaji na kuwathibitishia washiriki usiri wa taarifa zitakazotolewa na kuwa walikuwa huru kutoshiriki katika zoezi bila madhara yoyote kwao. 2

Kabla ya kuanza usaili, wachunguzi walijitambulisha na kueleza lengo la ufuatiliaji.washiriki walithibitishiwa pia kuwa taarifa zitakazokusanywa zitakuwa ni kwa madhumuni ya ufuatiliaji peke yake na kuahidiwa kuwa watajulishwa matokeo ya ufuatiliaji huo. KUINGIZA NA KUCHAMBUA TAARIFA Kiongozi chenye vigezo vya maswali kiliandaliwa baada ya kuandika maswali ya dodoso na kutumika katika uchanganuzi wa taarifa. Kiongozi hiki kilijaribishwa baada ya jaribio la dodoso ili kuona kama kilifaa kwa uchanganuzi wa taarifa. Baada ya ukusanyaji taarifa, maswali yaliyo wazi yalipewa alama kulingana na hoja zilizojitokeza. Uhariri wa taarifa na utoaji alama ulifanywa kutokana na majibu ya washiriki. Baadaye taarifa zilizopangwa kwenye makundi zilichanganuliwa kwa kutumia kichanganua takwimu za sayansi jamii (SPSS). Ili kuhakikisha kuwa uchanganuzi wa taarifa ulifanywa kwa usahihi, taarifa zilihakikiwa kwa kusahihisha dosari zilizojitokeza katika uingizaji wake na hatimaye majibu yake kupimwa kulingana na miongozo ya uanzishaji wa KZU. MIPAKA YA UFUATILIAJI Matokeo haya yanahusu wilaya sita zilizotajwa awali; kwa hiyo ni dhahiri kuwa hayawezi kuwa kiwakilisho cha hali ilivyo katika wilaya nyinginezo nchini. Hata hivyo, yale yaliyodhihirika katika ufuatiliaji huu yanaweza kulinganishwa na hali ilivyo katika wilaya nyingine zenye hali zinazofanana na zile zilizobainishwa katika ufuatiliaji huu, na hivyo kuwa kigezo cha kuanzia katika kutatua matatizo nchini. 3

MATOKEO NA MJADALA WAJUMBE WA KAMATI Ufuatiliaji ulichunguza taratibu zinazoongoza jinsi wajumbe wa KZU wanavyochaguliwa. Ingawa mwongozo wa uundaji wa KZU hauelezei taratibu za namna wajumbe wa kamati wanavyochaguliwa, bali unafafanua muundo wake unavyotakiwa kuwa na makundi ya watu wanaotakiwa kuwakilisha kamati mbalimbali. Hivyo ilibainika kuwa mwongozo wenyewe ulikuwa na mapungufu, jambo lililothibitisha umuhimu wa kufanyiwa marekebisho. Licha ya kwamba miongozo imeweka wazi ni nani wanaweza kuwa wajumbe wa kamati, ufuatiliaji huu ulibaini kuwa miongozo hiyo haikuwa inafuatwa sawasawa; hii inathibitishwa na ukweli kuwa kamati zilizohusika katika ufuatiliaji huu hazikukidhi kuwa kiwakilishi halisi cha makundi mbalimbali yaliyomo katika jamii husika. Ufuatiliaji ulibaini kuwa zaidi ya nusu ya washiriki (asilimia 64) walikuwa wajumbe kwa kuteuliwa na viongozi wa jamii. Kiasi cha asilimia 19 ya washiriki walikuwa wajumbe kutokana na nyadhifa walizokuwa nazo katika jamii, kama vile katibu wa kijiji (KWK), A isa Mtendaji wa kata (AMK) au diwani. Kwa mujibu wa miongozo watumishi wanaoshikilia nyadhifa hizi wanatakiwa kuwa sehemu ya kamati. Ilibainika kuwa kati ya wajumbe 78 waliohojiwa, ni asilimia 17 tu ndio waliochaguliwa na wananchi. Sikika inaamini kuwa ili wajumbe wa kamati waweze kuwakilisha jamii husika, hakuna budi wachaguliwe na wananchi wenyewe. Hii ni mahsusi kwa wale wanaowakilisha moja kwa moja makundi ya watu katika jamii; kama vile vijana, WAVIU, viongozi wa dini nk. Wawakilishi wa kuchaguliwa wanafaa zaidi katika kuwasilisha matakwa, maoni na vipaumbele vya wahusika kwenye mikutano na kutetea maslahi ya makundi yao, na kwa kufanya hivyo huwa ni wawakilishi tegemeo la jamii zao. Hivyo, ni muhimu kwa wawakilishi wa watu kuwa ni wale ambao wanaaminika na waliochaguliwa na wananchi wenyewe. KIWANGO CHA ELIMU Kiwango cha elimu cha washiriki kilichunguzwa pia ili kubainisha jinsi kinavyoathiri namna wajumbe wanavyoendesha shughuli za kamati. Baadhi ya majukumu ya wajumbe wa KZU ni; kuandaa ripoti, kuchambua sera na mipango mkakati na kutoa mrejesho kwa jamii. Ilibainika kuwa wajumbe wenye viwango vya juu vya elimu (kiwango cha sekondari na elimu ya juu) walionyesha upeo mkubwa zaidi wa uelewa wa mambo haya kuliko wale waliokuwa na kiwango cha chini. Kwa mfano, wajumbe walipotakiwa kuelezea jambo kwa undani, wale wenye elimu ya sekondari na elimu ya juu, walijibu maswali na kujieleza kwa ufasaha zaidi ukilinganisha na wajumbe wenye elimu ya msingi na wale wasiosoma kabisa. Ilidhihirika vilevile kuwa baadhi ya wajumbe wa kamati hawakujua kusoma, ingawa hawa walikuwa ni wachache, lakini wangeweza kuleta utata katika uendeshaji wa shughuli za kamati. Kati ya washiriki waliohojiwa, wengi wao (52%) wana elimu ya msingi, huku 24% ya washiriki wana elimu ya sekondari na 18% ya washiriki wana elimu ya juu kama jedwali1 hapo chini linavyoonesha. Jinsia Hakusoma Elimu ya Msingi Kiwango cha Elimu Elimu ya sekondari Elimu ya sekondari ya Juu Elimu ya Juu Wanaume 2 23 16 1 10 52 Wanawake 0 18 3 1 4 26 Jumla 2 41 19 2 14 78 Jumla Jedwali I: Viwango vya Elimu vya Wajumbe wa KZU 4

Kumudu majukumu ya kamati huweza kuwa ni changamoto kwa mtu mwenye uelewa mdogo juu ya masuala haya au asiyeweza kusoma na kuandika. Hivyo uwezo mkubwa wa kuelewa mambo, ujuzi na uzoefu alionao mtu ni baadhi ya sifa muhimu ambazo wanakamati wanatakiwa kuwa nazo. Maelezo haya ni kielelezo kuwa kiwango cha elimu kitazamwe kama sifa mojawapo ya msingi kwa mtu kuwa mjumbe wa kamati. Ufuatiliaji zaidi ufanywe ili kubaini kwa kiasi gani utendaji wa wajumbe wa KZU unaathiriwa na kiwango chao cha elimu. MIKUTANO Kwa mujibu wa miongozo ya KZU, kamati zinatakiwa kufanya mikutano mara moja kila mwezi (Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 2003). Wakati wa mikutano wajumbe wanapaswa kujadili na kutoa maamuzi kuhusu mikakati ya kuimarisha shughuli za VVU na UKIMWI kwenye ngazi za kata na kijiji/mtaa. Matokeo ya ufuatiliaji yanaonyesha kuwa kati ya wajumbe 78 waliohojiwa, asilimia 35 walifanya mikutano kila mwezi, wakati asilimia 65 hawakufanya. Kwa vile miongozo inaagiza kuwa kamati zifanye mikutano kila mwezi ili kujadili masuala ya VVU na UKIMWI, ni lazima kamati zifuate agizo hili, na zitoe sababu na maelezo pale zisipokutana kama ilivyoelekezwa, bila kufanya hivyo utendaji kazi wao utatiliwa mashaka. Asilimia ya KZU zilizokutana kila mwezi 35% 65% Hapana Kwa vile miongozo ya KZU inawataka wajumbe washiriki katika kupanga mipango; inatazamiwa kuwa wajumbe wa kamati watakuwa wanaelewa majukumu yao na jinsi ya kuyatekeleza. Lakini walipoulizwa kama wanaifahamu mipango na bajeti za UKIMWI, ni wajumbe 15 tu kati ya 78 waliosema wanaifahamu, ambayo ni takribani 19% tu ya wajumbe wote. Pamoja na kiwango kisichoridhisha cha uelewa wa wajumbe wa KZU juu ya wajibu wao katika mchakato wa kuandaa bajeti; tatizo jingine linatokana na mwongozo wenyewe kushindwa kuweka wazi ukomo wa wajumbe kushiriki katika mchakato mzima wa maandalizi ya bajeti; licha ya kwamba wameruhusiwa kuandaa na kufuatilia utekelezaji wa mipango. Ndio Umbo la 1: Asilimia ya KZU zilizokutana kila mwezi, zilizokutana angalao mara moja au hazikukutana kabisa. Idadi kubwa ya KZU hazijakutana kutoka zilipoundwa katika maeneo yao. UHUSIANO KATI YA HALMASHAURI NA KZU Ilitazamiwa kuwa halmashauri na KZU katika ngazi za kijiji/mtaa na kata ziwe na uhusiano imara wa kiutendaji na kufahamishana juu ya utekelezaji na usimamizi wa shughuli. Wajumbe walipoulizwa kama kamati zao zilipata mrejesho kutoka halmashauri kuhusu utekelezaji wa shughuli za UKIMWI, ni asilimia 17 tu ya wajumbe walithibitisha kupata mrejesho, wakati idadi kubwa (asilimia 83) ya wajumbe hawakuwa wamepata mrejesho kutoka halmashauri, kama inavyoonyeshwa katika jedwali na: 2 Mrejesho Idadi ya washiriki Asilimia Ndiyo 13 17 Hapana 65 83 Jumla 78 100 Jedwali 2: Idadi ya wajumbe wa KZU waliothibitisha kupokea mrejesho kutoka halmashauri Kuwepo na uhusiano kati ya serikali na wadau wake ni muhimu katika kushughulikia masuala yanayohusu VVU na UKIMWI. Mitandao na mahusiano ya kiutendaji kati ya serikali na wadau inatakiwa ianzishwe ili kuimarisha ushiriki na kufanikisha malengo yaliyowekwa(tacaids, 2010). Kwa mujibu wa matokeo ya ufuatiliaji yaliyoelezwa hapo juu, hakuna dalili kuwa haya yanatendeka 5

UHUSIANO KATI YA KZU NA JAMII KZU zina wajibu wa kuzihusisha na kufanya kazi pamoja na jamii na wadau wengine ili kuimarisha shughuli za utoaji wa huduma za VVU na UKIMWI (Jamhuri ya Muungano wa Tanzania). Wajumbe walipoulizwa iwapo wanawapa wananchi wa maeneo yao taarifa za mipango, bajeti na ripoti za utekelezaji, idadi kubwa ya wajumbe (asilimia 65) walieleza kuwa hawakuwa wanatoa mrejesho kwa jamii, wakati huohuo asilimia 35 walithibitisha kuwa walikuwa wakitoa mrejesho kwenye jamii. Washiriki waliokuwa wakitoa mrejesho walieleza kuwa walifanya hivyo kwa kutumia njia za. mikutano ya kamati na mikutano ya hadhara, na vilevile mikutano ya Idadi ya Wajumbe wa KZU wanaotoa mrejesho kuelezea UKIMWI. Kwa upande mwingine wajumbe wasiotoa mrejesho walieleza kuwa walifanya hivyo kwa sababu viongozi wao hawakujua kuwa walikuwa 51 wanajibika kutoa mrejesho kwa jamii, hivyo hawakuitisha mikutano, au Hapana hawakushirikishwa katika jambo hilo. 27 Ndiyo Ilielezwa vilevile kuwa serikali haikuwa imetenga fedha kwa ajili ya shughuli hizo. Kutoa mrejesho na mawasiliano kwa jamii kunaimarisha 0 10 20 30 40 50 60 zaidi ushiriki wa wananchi. Ni muhimu kuhakikisha kuwa wananchi wanahusishwa katika michakato ya Umbo la 2: Idadi ya wajumbe wa KZU waliothibitisha kuwa walitoa kufanya maamuzi mrejesho kwa jamii zao UWIANO WA KIJINSIA Dhana ya uwiano wa kijinsia ina maana ya kuzingatia kuwa wanawake na wanaume wana mahitaji na vipaumbele tofauti, wanakabiliwa na changamoto tofauti na vilevile wana matarajio tofauti hususan mchango wao katika maendeleo (SDC, 2003). Ilibainika kuwa kati ya wajumbe 78 wa KZU waliohojiwa, idadi kubwa (asilimia 67) walikuwa ni wanaume kuliko wanawake ambao walikuwa (asilimia 33) Ufuatiliaji ulibaini kuwa wajumbe wengi walikuwa wameteuliwa au kuwa wajumbe kutokana na nyadhifa walizokuwa nazo katika jamii kama vile KWK, AMK na kadhalika, na wengi wao walikuwa wanaume. Muongozo wa kuunda Kamati za Kudhibiti UKIMWI umebainisha kanuni zinazoagiza kuhusishwa kwa wanawake kama vile WAVIU, vijana, na watu mashuhuri; makundi ambayo kwa kawaida yamekuwa hayana wawakilishi wanawake. Iwapo nchi inataka kuhakikisha kuwa kunakuwapo na ushiriki wa usawa na wa maana kutoka kwa makundi yote, hapana budi juhudi za makusudi zifanyike katika kuwawezesha wanawake ili waweze kuchukua nafasi nyingi zaidi za uongozi. Juhudi hizi zinaweza kuwa ni pamoja na kuzitaka kamati zote kutenga nafasi sawa kwa wanaume na wanawake lakini pia kuhakikisha kuwa kuna ushiriki imara wa wanawake. Ufuatiliaji umeonyesha kuwa ushiriki wa wanawake ni mdogo. MIONGOZO YA KAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI Miongozo ya uundaji wa Kamati za Kudhibiti UKIMWI katika ngazi ya jamii ilianzishwa nchini Tanzania mwaka 2003. Miongozo hiyo iliundwa kwa mujibu wa sheria Na 22 ya mwaka 2001 na sheria Na 7 na 8 za Sheria za Serikali za Mitaa za mwaka 1982. Miongozo hii ililenga Serikali za Mitaa kutokana na ukweli kuwa janga la ugonjwa huu lilionekana kuathiri zaidi ngazi hii. Kuanzishwa kwa miongozo kwa ajili ya serikali za mitaa kulikuwa na lengo la kuzipa serikali hizo wajibu wa kupambana na janga hili. Miongozo ya KZU inaelezea taratibu za utekelezaji wa shughuli za kupambana na UKIMWI katika ngazi ya serikali za mitaa; hata hivyo kuna udhaifu katika baadhi ya vipengele vya miongozo hiyo: Miongozo inataja watu wanaoweza kuwa wajumbe wa kamati kutoka ngazi ya kijiji hadi halmashauri lakini haielezei namna wajumbe hao watakavyochaguliwa na watakuwa kwenye madaraka kwa muda gani. 6

Miongozo haielezei masharti kuhusu umri au kiwango cha elimu anachotakiwa kuwa nacho mjumbe. Miongozo imeelezea kwa jumla tu wajibu na majukumu ya kamati bila kuweka wazi kazi mahsusi ya kila kamati katika ngazi husika. Mathalan, majukumu na wajibu wa kamati katika ngazi ya kijiji ni sawa na yale ya kamati kwenye ngazi ya halmashauri. Miongozo imebainisha pia jinsi mratibu wa shughuli za UKIMWI atakavyochaguliwa, pamoja na maelekezo mengine kama vile wajibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya, mji halmashauri au jiji. Wajumbe wa kila kamati husika wanatakiwa kuhusishwa katika mchakato wa kuandaa bajeti. Ingawa kifurushi cha taratibu za kufanya mipango ya VVUna UKIMWI kilitolewa kusaidia ngazi za mtaa katika kupanga na tayari baadhi ya mamlaka za mitaa zimeshaanza kukitumia; lakini mwongozo huo wa KZU hauelezei waziwazi jukumu hili wala kuelekeza utekelezaji wake Tatizo kubwa kuhusu miongozo hii ni kuwa imeandikwa kwa lugha ya Kiingereza wakati idadi kubwa ya watekelezaji wake wanaweza kuzungumza na kusoma Kiswahili pekee. MAJUKUMU NA WAJIBU WA KZU Ili KZU ziweze kutekeleza kazi zake kikamilifu, hapana budi wajumbe wote wayafahamu majukumu na wajibu wao. Kinyume chake, matokeo yameonyesha kuwa kiasi cha 23% ya wajumbe waliohojiwa hawakuwa wanaelewa wajibu walio nao kama wajumbe wa kamati. Cha kushangaza zaidi ni kuwa wajumbe waliokiri awali kuyaelewa majukumu yao, walipotakiwa kuyataja, walitaja shughuli ambazo hazikuelezwa kwenye miongozo ya Kamati za Kudhibiti UKIMWI.Kwa upande mwingine, yasiyo ya msingi wakiacha kuelezea yale ya msingi. Ilidhihirika pia kuwa baadhi ya majukumu ambayo yalitajwa na wahusika, na ambayo yalikuwamo katika mwongozo, hayakuwa yakitekelezwa na wajumbe. Wakati mwingine hata kama wajumbe walielewa nini cha kufanya kama wajumbe, hawakutekeleza wajibu huo, likiwemo jukumu la kuwatambua WAVIU, kufanya mikutano na jamii; kupanga mipango na kusimamia utekelezaji wake. Matokeo ya ufuatiliaji yamebaini kuwa kuna udhaifu katika mfumo wa ufuatiliaji wa kamati na wahusika hawawajibishwi wanapokosa kutekeleza majukumu yao. Hatua za marekebisho inabidi ziandaliwe, ikiwamo kutoa mafunzo ya awali kwa wajumbe kuhusu namna ya kutekeleza shughuli za KZU, na namna ya kuwaadhibu wale wasiotekeleza majukumu yao kikamilifu. Hii itahakikisha kuwa kamati zinatekeleza wajibu wao kikamilifu na hivyo kuhakikisha kuwa sauti za wananchi zinasikika na kuchangia mawazo juu ya hatua za kufanya katika kupanga shughuli serikali za mitaa/vijiji. Yafuatayo ni majukumu ya KZU yaliyomo katika miongozo ya uanzishaji wa Kamati za Kudhibiti UKIMWI katika ngazi ya jamii (Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2003, uk. 7). a. Kuwaleta pamoja wadau mbalimbali katika maeneo husika ili kuongeza mchango wa mawazo na mikakati, uongozi, kuhifadhi taarifa na utekelezaji wa kazi za TACAIDS. b. Kusimamia mchakato wa uanzishaji wa kamati zote zinazosimamia kudhibiti UKIMWI. c. Kupendekeza na kuchambua mipango kuhusu VVU na UKIMWI na utekelezaji wake na kuiwasilisha katika ngazi husika. d. Kutathmini hali ya UKIMWI katika eneo husika i. Idadi ya walioambukizwa, wagonjwa, yatima na wajane ii. Kiasi cha maambukizi. iii. Mazingira yanayosababisha maambukizi iv. Uelewa wa watu kuhusu masuala ya UKIMWI e. Kutathmini shughuli za wadau kuhusu masuala ya UKIMWI i. Mashirika yasiyo ya kiserikali (uwezo na matazamio yao) ii. Mashirika ya dini (uwezo na matazamio yao) iii. Mashirika ya serikali (uwezo na matazamio yao) baadhi ya wajumbe waliweza tu kutaja majukumu machache 7

f. Kwa kushirikiana na na wananchi na wadau wengine, kuandaa mipango inayohusu; i. Namna ya kupambana na maambukizi ya UKIMWI ii. Kuongeza uelewa wa watu kuhusu masuala ya UKIMWI iii. Kukusanya na kuweka kumbukumbu kuhusu; hali ya maambukizi ya UKIMWI, hali ya kipato cha waathirika wa UKIMWI. g. Kuweka kumbukumbu, kufuatilia na kutathmini hali ya utekelezaji wa mipango ya shughuli za UKIMWI. h. Kutafuta vifaa vya kufanyia kazi i. Kutoa ushauri kuhusu sera au sheria ndogondogo juu ya namna ya kudhibiti UKIMWI. Majukumu ya KZU yaliyoorodheshwa hapo juu ni thabiti, hivyo utekelezaji wake unahitaji watu kuwa na kiwango cha kufaa cha elimu, lakini kama ilivyoelezewa katika kipengele cha kiwango cha elimu, baadhi ya wajumbe wa KZU wana viwango vya chini vya elimu huku baadhi yao wakiwa hawajui kusoma wala kuandika. Vilevile, KZU katika ngazi za kijiji na kata hazipatiwi msaada wa fedha, pia wajumbe hawajapatiwa maelekezo kuhusu jinsi ya kutekeleza shughuli za UKIMWI. Iwapo serikali inataka KZU ziweze kutekeleza majukumu yake kwa ukamilifu, ni muhimu kamati hizi ziwezeshwe kwa kupatiwa msaada wa fedha na maelekezo ya namna ya kutekeleza majukumu yao, wenye kujituma na wenye uelewa mzuri wa mambo. Hii ina maana kuwa ni muhimu kwa kila mjumbe USHIRIKI WA KAMATI KATIKA KUPANGA Kifurushi mahsusi cha mipango ya VVU na Idadi ya UKIMWI kiliandaliwa kama nyenzo ya kuwasaidia watendaji katika ngazi ya jamii katika Ushiriki washiriki Asilimia kupanga mipango. Maudhui ya kifurushi hiki Ndiyo 15 19 ni rahisi kutumia na kinaziwezesha serikali Hapana 63 81 za mitaa kuandaa mipango kulingana na hali Jumla 78 100 halisi za maeneo husika. Hata hivyo, jukumu la kufanya mipango halikuelezwa vizuri katika Jedwali 3: Idadi na asilimia ya wajumbe wa KZU miongozo ya KZU (angalia c,f na g hapo juu). wanaoshiriki katika kufanya mipango ya shughuli za Walipotakiwa kueleza iwapo wanao uelewa serikali ya mitaa wowote kuhusu namna ya kupanga mipango katika masuala ya VVU na UKIMWI katika maeneo yao, 19% ya wahusika walijibu ndiyo na asilimia 81 walijibu hapana. (tazama Jedwali 3). Washiriki waliojibu hapana walieleza kuwa hawakushiriki shwa wakati wa kupanga na kuandaa bajeti; walikuwa bado wageni kwenye kamati; walichaguliwa kuwa wajumbe baada ya mchakato wa kupanga na kuandaa bajeti kuwa umeshapita; hawakuwa wameelezwa kuhusu mchakato wa maandalizi ya mipango; walidhani kuwa kupanga mipango na kuandaa bajeti ni wajibu wa halmashauri; hawakuwa wamefundishwa jinsi ya kuandaa mipango na bajeti; hapakuwa na fedha kwa ajili ya shughuli hiyo; hawakuwa wamefanya mikutano ya kamati hivyo kushindwa kuendesha shughuli hizo; kukosekana mawasiliano kati ya kamati na serikali; na kukosekana kwa majengo ya ofisi na vitendea kazi. Ni dhahiri kuwa sababu zote zilizotolewa zinaweza kuzuilika na zingeweza kurekebishwa iwapo maafisa husika wangejishughulisha zaidi, wangetekeleza wajibu wao vizuri na kama wangezingatia mambo haya kwa makini. MBINU ZA KUBAINISHA MAHITAJI YA WAVIU Baadhi ya majukumu ya kamati ni pamoja na kutathmini hali ya UKIMWI katika jamii na kukusanya taarifa kutoka kwa wananchi na wadau. Walipotakiwa kueleza ni njia zipi wanazitumia katika kukusanya taarifa juu ya mahitaji ya WAVIU, washiriki walitoa majibu mbalimbali kama inavyoonyeshwa kwenye (umbo na: 3) hapa chini. Wengi wao (wajumbe 31 kati ya 78 ) walieleza kuwa walipata taarifa kutoka kwa watoa huduma majumbani. Njia ambayo haikutumika sana (ilitajwa na wajumbe 3 kati ya 78) ni ile ya kupitia kwa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs). Kiasi cha wajumbe 20 kati ya wajumbe 78 walijibu kuwa hawakuwa na njia maalumu ya kukusanya taarifa hizo. 8

Njia zinazotumiwa na KZU kubainisha mahitaji ya WAVIU Hakuna njia zinazotumika 20 Huduma za majumbani 31 Mikutano ya Azaki 3 Mikutano ya KZU 16 Mikutano ya kata/kijiji 8 0 5 10 15 20 25 30 35 Umbo la 3: Njia ambazo KZU hutumia kutambua mahitaji ya WAVIU Mahitaji pamoja na vipaumbele vya WAVIU ni mambo yanayozingatiwa katika kuendesha programu za VVU na UKIMWI. Iwapo mipango na shughuli za VVU na UKIMWI haikuzingatia mahitaji na vipaumbele ikia lengo la kitaifa juu ya VVU na UKIMWI, ambalo linasema Huduma bora ili kupunguza maambukizi ya VVU na UKIMWI, kama ilivyoelezwa kwenye Kifurushi Mahsusi cha Mipango kuhusu VVU na UKIMWI (uk. 12). Matokeo yanadhihirisha zaidi kuwa kamati zinatumia watu wengine kama vyanzo vya kupata taarifa za badala ya kupata taarifa hizo kutoka kwa WAVIU wenyewe. Ni muhimu maoni ya WAVIU na mahitaji yao yakasikilizwa kulingana na uzoefu wao wenyewe. Asilimia 26 ya washiriki hawakuwa na njia yoyote ya kutambua WAVIU, hali inayoonyesha kuwa mipango yao haizingatii mahitaji na vipaumbele vya WAVIU. Kukosekana kwa njia za kubaini masuala ya WAVIU kunamaanisha kuwa mipango husika haizingatii mahitaji na vipaumbele vya WAVIU, jambo hili lirekebishwe mara moja. 9

HITIMISHO NA MAPENDEKEZO HITIMISHO Matokeo ya ufuatiliaji uliofanywa na Sikika yamebainisha changamoto mbalimbali zinazozikabili KZU kwenye ngazi za kata, kijiji/mtaa. Changamoto mojawapo ni ile inayohusu miongozo ya kuunda KZU. Miongozo hiyo ilionekana kukosa maelezo muhimu kuhusu namna KZU zinavyotakiwa kufanya kazi. Kukosekana kwa uwiano wa kijinsia ni jambo mojawapo linalopaswa kuchunguzwa kwa makini iwapo nchi inataka kuimarisha ushiriki wa wananchi. Viwango vya chini vya elimu na hali ya wajumbe kutopatiwa mwongozo kuhusu utekelezaji wa majukumu yao ni baadhi ya changamoto zinazotakiwa kushughulikiwa kikamilifu kwa sababu hayo ndiyo masuala ya msingi katika uendeshaji wa kamati. Tatizo lingine linahusu ushiriki usioridhisha wa kamati katika kupanga mipango na kuandaa bajeti pamoja na ushirikiano hafifu kati ya kamati, halmashauri na wananchi katika kubadilishana taarifa. Ili Tanzania iweze kupata mafanikio katika kukabiliana na VVU na UKIMWI hapana budi ifanye bidii katika kuimarisha KZU ili ziweze kufanya kazi vizuri zaidi. Wazo la kuanzisha KZU ni zuri, hata hivyo, pasipo kuimarisha mikakati ya utekelezaji inayolenga kutatua matatizo yanayozikabili KZU na jamii, kamati hizi zitashindwa kufanya kazi na hivyo kushindwa kupambana na UKIMWI. KZU zilianzishwa kwa lengo la kuzihusisha jamii katika kukabiliana na UKIMWI na pia kuunganisha serikali za mitaa/vijiji na serikali kuu katika mchakato wa kufanya maamuzi. Mkakati huu wa kutoka chini kwenda juu ulitazamiwa kuwa ungefaa katika harakati za kutekeleza programu za VIRUSI na UKIMWI. Ni muhimu kuimarisha dhana ya ushirikishaji katika kufanya maamuzi, kupanga mipango na katika utekelezaji wake. Kwa kufanya hiyo serikali za mitaa zitaweza kutoa mchango zaidi katika harakati za taifa dhidi ya janga la UKIMWI. MAPENDEKEZO Matokeo ya ufuatiliaji yameonyesha kuwa kuna matatizo mengi yanayozikabili KZU. Kwa kuanzia, miongozo yenyewe ambayo ndio inayoongoza utendaji wa KZU imeonekana kuwa na udhaifu mwingi. Ikizingatiwa kuwa KZU zilianzishwa kwa lengo la kuzishirikisha ngazi za chini kuchukua majukumu katika mapambano dhidi ya UKIMWI, juhudi kubwa zinapaswa kufanywa ili kuimarisha KZU kama inavyoelekezwa katika mapendekezo yafuatayo: 1. Miongozo ya kuanzisha Kamati za Kudhibiti UKIMWI kwenye ngazi ya serikali ya mitaa hapana budi iangaliwe upya na Ofisi ya Waziri Mkuu-mamlaka ya Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ili kurekebisha maelezo kuhusu taratibu za kuchagua wajumbe, kama vile, sifa za kielimu anazotakiwa kuwa nazo mjumbe. Vilevile taratibu za mawasiliano na mrejesho kati ya wananchi na KZU na baina ya KZU na halmashauri hapana budi zielezwe vizuri. Hii itaziwezesha KZU kufanya kazi vizuri zaidi na hivyo kuchangia zaidi taarifa zitakazo tumiwa na serikali za mitaa katika kupanga shughuli za VVU na UKIMWI katika bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu-mamlaka ya serikali za mitaa (TAMISEMI) 2. Wanawake hapana budi watiwe moyo wa kuwa wajumbe wa kamati na kugombea uongozi, na hasa kuchukua nafasi za uongozi ambazo kulingana na miongozo ya kitaifa zimetengwa mahsusi kwa ajili ya wanawake. Hii itaongeza zaidi ushiriki wao katika kufanya maamuzi na hivyo kuwezesha kutekelezwa kwa mipango ya VVU na UKIMWI yenye uwiano wa kijinsia, kwa sababu mahitaji ya wanawake na wanaume kuhusu VVU na UKIMWI yanatofautiana. Vilevile hii inatazamiwa kuwa itafanya muundo wa KZU kuwa na uwiano zaidi wa kijinsia kuliko ilivyo sasa ambapo nafasi nyingi zimeshikwa na wanaume. 3. Sifa za kielimu, hasa zile zinazomwesha mtu kuweka kumbukumbu, kuchambua, kupanga mipango, kutathmini shughuli na pia kushauri kuhusu sera na sheria ndogondogo juu ya jinsi ya kudhibiti VVU na UKIMWI hapana budi zizingatiwe katika kuchagua wagombea kuwa wajumbe wa kamati. Hii ina 10

maana kuwa miongozo iliyopo ya KZU hapana budi ifanyiwe marekebisho ili kuweka kipengele cha elimu kitakachowalazimu wajumbe kuwa na ujuzi wa uchambuzi ili waweze kutekeleza wajibu wao kwa ufanisi zaidi. 4. Wajumbe wa KZU hapana budi wapatiwe mwongozo sahihi na ufafanuzi wa kutosha kuhusu majukumu na wajibu wao kama yalivyoelekezwa katika miongozo; ili kuwawezesha kutekeleza shughuli zao kwa ufanisi zaidi. Hii inalazimu kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu-mamlaka ya serikali za mitaa (TAMISEMI) kutenga bajeti kwa shughuli hizi na kutoa uangalizi wa mara kwa mara kwa siku zijazo. Kutokana na hayo uwezo wa wajumbe wa KZU katika kupanga mipango na kuandaa bajeti utaongezeka na hivyo kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kupanga mipango na kuandaa bajeti katika ngazi za jamii. 5. Njia za mawasiliano ziimarishwe kati ya KZU katika ngazi za jamii na halmashauri, na pia kati ya KZU za kijiji/kata na wananchi. Hii ifuatiwe na mamlaka za serikali ya mitaa (LGAs), KZU, na TACAIDS ambayo ni mamlaka kuu inayosimamia shughuli za VIRUSI nchini Tanzania. 6. Miongozo ya KZU ieleze waziwazi hatua za uwajibishaji zitakazotumika kuwawajibisha viongozi watakaoshindwa kutekeleza majukumu yao kama inavyotarajiwa. Hii ni pamoja na kuzipa KZU zenyewe mamlaka ya kuwawajibisha viongozi. 7. Fedha zitolewe ili kulipia shughuli, kama vile mafunzo, kuandaa mikutano ya mara kwa mara, na kufanikisha mawasiliano na wananchi na halmashauri ili kuhakikisha kuwa KZU zinafanya kazi. 8. Miongozo ya KZU iandikwe kwa lugha ya Kiswahili badala ya Kiingereza pekee, hii ni kwa sababu Kiswahili ndiyo lugha ya taifa na inazungumzwa na kueleweka na idadi kubwa ya watu nchini Tanzania. MAREJE0 Bassler, A., Brasier, K., Fogle, N., and Taverno, R., (2008). Developing Effective Citizen Engagement: A How-To Guide for Community Leaders. Pennsylvania State University Cooperative Extension Isangula, K.G. (2012). Improving women and family s health through integrated microfinance, health Education and promotion in rural areas. Journal of Sustainable Development, 5(5), 76-89. Retrieved from http://dx.doi.org/10.5539/jsd.v5n5p76. Oxfam GB Tanzania. (2009). Picture this. A Tanzania without poverty. Together everything is possible. Dar es salaam. Oxfam GB Tanzania. SDC. (2003). Gender in practice. A tool-kit for SDC and its partners. SDC TACAIDS. (2010). Gender operational for HIV response in mainland Tanzania (2010-2012). Dar es salaam,tanzania. TACAIDS. (n.d). Essential HIV&AIDS planning package. Tanzania: Division of national response. Dar Es Salaam, Tanzania. United Republic of Tanzania President s Office. (2003). Guidelines for forming AIDS committees at local level. Tanzania. United Republic of Tanzania. (2008). Technical Review of Council Health Service Boards and Health Facility Governing Committees in Tanzania. Tanzania. United Republic of Tanzania. (2010). Gender operational plan for HIV response in mainland Tanzania. Tanzania. 11

KIAMBATISHO DODOSO LA KUTATHMINI USHIRIKI WA KAMATI ZA UKIMWI KATIKA KUPANGA NA KUTEKELEZA SHUGHULI KUHUSU VVU/UKIMWI Jina la msaili Tarehe ya usaili.mkoa. Wilaya Kata. 1.0 TAARIFA ZA JUMLA ZA MSAILIWA 1.1 Jinsia: 1. Me ( ) 2. Ke ( ) 1.2 Kiwango cha elimu; ( ) Hakusoma ( ) Elimu ya msingi ( ) Elimu sekondari ya kawaida ( ) Elimu ya sekondari ya juu ( ) Elimu ya juu 1.3 Nafasi katika kamati... 1.4 Ulichaguliwaje kushika nafasiya ujumbe uliyonayo?... 2.0 TAARIFA YA KAMATI 2.1 Ngazi ya kamati (weka alama ya tiki) i. Wilaya ( ) ii. Kata ( ) iii. Mtaa ( ) 2.2 (a) Kamati yako ina wajumbe wangapi?... Eleza ni kundi gani wanaliwakilisha i.... iv... ii.... v.... iii.... vi.... (a) Kamati inakutana mara ngapi?... (b) Kamati ilikutana kwa mara ya mwisho lini?... 3.0 TAARIFA KUHUSU UELEWA WA WAJUMBE WA KAMATI KUHUSU MAJUKUMU NA 12

WAJIBU WA KAMATI ZAO. 3.1 Je kama mjumbe, unauelewa wajibu wako? a. Ndiyo ( ) b. Hapana ( ) (b) Kama jibu lako ni Ndiyo, tafadhali ueleze. i.... iv... ii.... v.... iii.... vi.... (c) Iwapo jibu lako ni Hapana, tafadhali eleza kwa nini hufahamu majukumu ya kamati yako. 4.0 USHIRIKI WA WAJUMBE KATIKA KUPANGA MIPANGO NA KUANDAA BAJETI KUHUSU VVU&UKIMWI 4.1 Kama mjumbe wa kamati, unaelewa juu ya mpango wa bajeti kuhusu VVU&UKIMWI? A. Ndiyo ( ) b. Hapana ( ) 4.2 (a) Je umewahi kushiriki katika kuandaa bajeti kwenye ngazi ya mtaa/kata/wilaya? a. Ndiyo ( ) b. Hapana ( ) (c) Kama jibu ni Hapana, tafadhali eleza kwa nini hukushirikishwa katika maandalizi. 4.3 Unatumia njia gani kutambua mahitaji ya jamii hasa WAVIU 5.0 KUFUATILIA UWAJIBIKAJI KATIKA JAMII 5.1 Je kamati yako inafuatilia shughuli zinazoendeshwa kuhusu VVU&UKIMWI? Ndiyo ( ) Hapana ( ) Sijui ( ) (b) Fafanua jibu lako 5.2 Je kamati yako inapata mrejesho kutoka manispaa kuhusiana na bajeti na shughuli zinazotekelezwa kuhusu VVU&UKIMWI a. Ndiyo ( ) b. Hapana ( ) 5.4 (a) Je kamati yako inatoa ripoti kwa jamii kuhusu mipango, bajeti ya VVU&UKIMWI na utekelezaji wa shughuli? Ndiyo ( ) Hapana ( ) (b) Kama Ndiyo, tafadhali eleza njia inayotumika kuwasilisha ripoti. (c) Kama Hapana, eleza kwa nini?... 5.5 Je ni kwa namna gani serikali / wilaya / TACAIDS zinawasadieni katika kutekeleza majukumu yenu? 13

Sikika inafanya kazi kuhakikisha usawa katika upatikanaji Sikika inafanya wa huduma kazi kuhakikisha bora za afya, usawa kwa katika upatikanaji kutathimini wa mifumo huduma ya uwajibakaji bora za afya, katika kwa ngazi kutathimini zote za serikali. mifumo ya uwajibakaji katika ngazi zote za serikali. Nyumba Na. 69 Eneo Ada Estate, Kinondoni Barabara ya Tunisia Mtaa wa Waverley S.L.P 12183 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 26 663 55/57 SMS: 0688 493 882 Faksi: +255 22 26 680 15 Barua pepe: info@sikika.or.tz Blog: www.sikika-tz.blogspot.com Facebook: Blog: www.sikika-tz.blogspot.com Sikika Tanzania Facebook: Sikika Tanzania Nyumba Na. 340 Mtaa wa Kilimani S.L.P 1970 Dodoma, Tanzania Simu: 026 23 21307 Faksi: 026 23 21316