Msigano wa Majina ya Walemavu katika Jamii ya Wazungumzaji Kiswahili: Mifano kutoka Tanzania

Similar documents
UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

Information for assessors (do not distribute this page to participants):

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

LUGHA YA KISWAHILI KATIKA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA ELIMU SHULE ZA SEKONDARI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

Elimukombozi, Lugha na Upashanaji Habari nchini Tanzania, katika Muktadha wa Utandawazi

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Human Rights Are Universal And Yet...

Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara)

Ufunguo wa Kutaalamika Haraka

Ufanisi katika Ufundishaji kwenye Shule za Msingi na Sekondari nchini Tanzania

MAADHIMISHO YA MIAKA 15 YA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1

MITAZAMO KUHUSU KISWAHILI MIONGONI MWA WAZUNGUMZAJI WA KIJALUO: KIFANI CHA SHULE ZA MSINGI KATIKA KAUNTI YA MIGORI. OWALA JAEL AKINYI C50/75493/2012

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO

Kiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika

TAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF) KUHUSU HAKI ZA WATOTO KATIKA KATIBA MPYA

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II

Haja Ya Dini. Author(s): Publisher(s): Translator(s): Category: Topic Tags: Featured Category: Published on Al-Islam.org (

KUSHUKA KWA HADHI YA LUGHA ZA JAMII NCHINI TANZANIA YOHANA P. MSANJILA University of Dar es Salaam, Tanzania

MAPENDEKEZO YA MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA TANZANIA

KISWAHILI KARATASI YA 2 LUGHA

JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI

usudi la Maisha Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na kupishana usiku na mchana, kuna kweli ishara kwa wenye akili, ambaye mkumbuke-

N09/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q

Mukhtasari Wa Mabishano Kwa Na Dhidi Ya Vikombe Vingi Vya Ushirika

KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA

Elimu-Jumuishi Kwa Vitendo

MTIHANI WA MWIGO WILAYA YA BUTERE MUMIAS-2007 Hati ya kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya

Kiu Cha umtafuta Mungu

KENYA NATIONAL EXAMINATION COUNCIL REVISION MOCK EXAMS 2016 TOP NATIONAL SCHOOLS

Mwongozo wa Utamaduni Toleo la Kwanza

Azimio lililopitishwa na Mkutano Mkuu tarehe 18 Desemba 2013 [juu ya taarifa ya Kamati ya Tatu (A/68/456/Add.2)]

ATHARI ZA KIISIMU ZA LAHAJA YA KIMAKUNDUCHI KATIKAKISWAHILI SANIFU KINACHOTUMIKA SHULENI MAKUNDUCHI ZANZIBAR

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU

TASFIDA KAMA MKAKATI WA UPOLE: UWIANO WA TASFIDA ZA KISWAHILI NA EKEGUSII

Usimulizi wa Riwaya ya Nyongo Mkalia Ini E. S. MOHOCHI University of Egerton, Kenya

International Labour Office. Kazi za Ndani Zenye Madhara kwa Watoto: Kijitabu cha Maelezo Mafupi

Elimu Ina Umuhimu gani katika Jamii? Kuelekea Elimu Sahihi

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig

HAKI NA TARATIBU ZA AJIRA, KAZI NA HIFADHI YA JAMII

KUCHUNGUZA MASUALA YA KISIASA KATIKA RIWAYA ZA SHAABAN ROBERT: MFANO WA KUSADIKIKA NA KUFIKIRIKA

Tora UTANGULIZI KWA TORA SOMO LA KWANZA

Ufundishaji wa lugha nyingine

Mazoezi yaliyofanyika wakati wa warsha kuhusu Elimu-Jumuishi kwa Vitendo. Zanzibar, 7-10 Februari 2006

Theolojia Ujumla. Mike Taylor Semester Munguishi Bible College

Kutetea Haki za Binadamu

Mwongozo wa Kanisa la Waadventista wa Sabato

MAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI

Ellen White, waasisi wa Kiadventista,na Sabato Lunar

Pronunciation: Mä-hret Zäläke Ndal-ka-tscho Molla Mare Gebre-gzabiär 1/12

KAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI TANZANIA

Kufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007

UHUSIANO WA MIKAKATI YA UFUNDISHAJI WA FASIHI YA WATOTO YA KISWAHILI NA UMILISI WA KUSOMA KATIKA SHULE ZA MSINGI, KASARANI, KAUNTI YA NAIROBI, KENYA

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA

ETIMOLOJIA YA MAJINA YA MAHALI YA KASKAZINI PEMBA KUWA UTAMBULISHO WA UTAMADUNI WA WAPEMBA

JAMHURI YA KENYA. Mkakati wa Ushirikiano MUKHTASARI FY Public Disclosure Authorized. Public Disclosure Authorized

DHANA NA MATKTIZO YA TAFSIRI:

SautiElimu. Sauti Yako Isikike

Kimesanifiwa na:- E.D.Kissuu ECOMM TANZANIA S.L.P ,Dar es Salaam. Simu:

Shabaha ya Mazungumzo haya

Mhashamu Askofu Jude Thaddaeus Ruwa ichi, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania; Mwadhama Policarp Kardinali Pengo,

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA 2006/07

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level

Hati ya Kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya.( K.C.S.E)

Ushindi ndani ya Kristo W. W. PRESCOTT

Deutsche Welle, Learning by Ear 2009 Seite 1 People Who Make A Difference Liberia: Anita Varney Health Facilitator, Fishtown/Liberia

HISTORIA, MAENDELEO NA MABADILIKO YA KATIBA TANZANIA TANGU UHURU HADI MIAKA HAMSINI YA UHURU 9 DESEMBA 2011.

Adhabu ya jino kwa jino na Musitakabali wa imani zetu

Mafundisho Ya Msingi Wa Kikristo. Na Andrew Connally

MARUDIO K.C.S.E KNEC KISWAHILI KARATASI 102/2 MASWALI NA USAHIHISHO

Yaliyomo. Kuhusu kitabu hiki. Hautakuwa peke yako. Mfumo wa msaada ni wa manufaa sana wazazi wote wanahitaji!

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA SABA. Kikao cha Thelathini na Tisa Tarehe 1 Juni, (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A

Utangulizi wa ugonjwa wa shinikizo la damu

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA. Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo. TOLEO Na.

Mwongozo wa Familia wa Kujifunza

2

Dibaji ya Mwenyekiti wa Kamati ya Pamoja ya Uongozi

JE, YAWEZEKANA KUISHI BILA KUTENDA DHAMBI?

UJAGINA WA MWANAMKE KATIKA PANGO

KITEGO CHA MAREKEBISHO NA HAKI ZA MTOTO

Evaluation of Contextual Teaching of Kiswahili Proverbs in Secondary Schools in Kenya

UFAHAMU NAME INDEX SCHOOLDATE UFAHAMU

WEWE NI NANI? Toleo X Toleo Ukweli wa Injeli Toleo 23

MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA. Kwa Wanaoanza

TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM)

Kubadili Sheria Za Mbegu Na Ulinzi Wa Aina Za Mbegu Na Mimea Nchini Tanzania

Watumishi Wa Kristo. Ellis P. Forsman. Watumishi Wa Kristo (Servants Of Christ) 1

MIONGOZO MIWILI KUPAA NA KUTUNGULIWA KWA AZIMIO LA ARUSHA

Sera ya Faragha. Upeo. Aina za Data na Mbinu za Ukusanyaji

MUNGU ANADHIHIRISHWA KUPITIA KWA YESU KRISTO.

ATHARI ZA KIMOFOFONOLOJIA ZA KIOLUSUBA KATIKA MATUMIZI YA KISWAHILI SANIFU KAMA LUGHA YA PILI

ULINGANISHI WA KIISIMU KATI YA LAHAJA YA KIPEMBA NA KITUMBATU

ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA UCHUMI WA ZANZIBAR

Transcription:

1

78 Kioo cha Lugha JZ. 11 Msigano wa Majina ya Walemavu katika Jamii ya Wazungumzaji Kiswahili: Mifano kutoka Tanzania Elizabeth G. Mahenge Ikisiri Walemavu wamekuwa wakilalamikia matumizi ya majina yanayowarejelea katika jamii ya wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili. Jambo hili nililigundua wakati nilipokuwa ninafuatilia vipindi vya walemavu katika runinga na redio nchini Tanzania. Majina kama vile kilema, kiwete, kipofu, zeruzeru, asiyesikia na mengineyo ni baadhi ya majina ambayo wazungumzaji wamekuwa wakiyatumia kwa muda mrefu (yaani tangu zamani za kale) lakini kwa upande mwingine wanaoitwa majina hayo wamekuwa wakiyakataa. Makala haya yanachunguza msigano wa majina wanayoitwa walemavu nchini Tanzania. Vilevile, makala yatazungumzia vikwazo mbalimbali wanavyokutana navyo walemavu katika mawasiliano. Mambo haya yana umuhimu mkubwa wa kuzungumziwa katika makala haya kwani lengo kuu la kuwepo kwa lugha katika jamii ni mawasiliano. Pia makala haya yatatoa mapendekezo mbalimbali kuhusiana na mambo ambayo yameshughulikiwa katika utafiti huu. 1.0 Utangulizi Ulemavu ni hali ya kupoteza kiungo au kuwa na kikwazo cha kushindwa kujishughulisha na maisha ya kawaida sawia na watu wengine (ILO, 2007). Kikwazo hicho kinaweza kuwa ni kutokana na hali ya mwili, akili au sababu za kijamii ambazo kwa pamoja zinasababisha kushindwa kujumuika na wengine. Makala haya yamelenga kuchunguza msigano wa majina yanayotumika kuwaita walemavu katika jamii ya Watanzania. Katika kulifikia lengo hili tutapitia maana ya ulemavu, historia ya walemavu nchini Tanzania na maana ya lugha. Kwa kuwa lengo kuu la lugha ni mawasiliano makala haya pia yataongelea vikwazo vinavyojitokeza katika kufanya mawasiliano na watu wenye ulemavu. Utafiti huu ulifanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako mwandishi wa kazi hii alikuwa akisoma darasa moja na baadhi ya walemavu waliotafitiwa. Sampuli ya utafiti huu ilijumuisha walemavu wa ngozi wawili (2), walemavu wa viungo watatu (3) na wasioona kumi (10). Jumla ya wahojiwa walikuwa kumi na tano (15). Wanawake walikuwa wanane (8) na wanaume walikuwa saba (7). Umri wao ni kati ya miaka 20 hadi 35. Wanafunzi hawa walikuwa wakisoma shahada mbalimbali kama vile Elimu, Sosholojia na Sheria mnamo mwaka 2002-2006. 2.0 Maana ya Ulemavu Kwa mujibu wa asasi, wataalamu na jamii kwa ujumla inaonekana kuwa kumekuwapo na tofauti ya maana katika istilahi ulemavu. Miongoni mwa fasili hizo ni ile inayosema kwamba ulemavu ni hali ya kupoteza kiungo au kuwa na kikwazo cha kushindwa kujishughulisha na maisha ya kawaida sawia na watu

Msigano wa Majina ya Walemavu katika Jamii ya Wazungumzaji Kiswahili 79 wengine (ILO, 2007). Pia inafafanuliwa kuwa ulemavu ni kupoteza au kuwa na kikwazo cha kushindwa kupata fursa katika jamii sawasawa na watu wengine kutokana na hali ya kimaumbile, kiakili au sababu za kijamii (United Republic of Tanzania, 2010:2). Vivyo hivyo, inaelezwa kuwa ulemavu ni hali ya kupoteza au kuwa na kikwazo cha kushindwa kujishughulisha na maisha ya kawaida sawia na watu wengine kutokana na hali ya mwili, akili, au sababu za kijamii (Wizara ya Kazi, Maendeleo ya Vijana na Michezo, 2004). Swali la kujiuliza hapa ni je, ulemavu ni hali ya kupoteza? Kupoteza nini? Ukiachilia mbali fasili za ulemavu kwa mujibu wa asasi hizi chache, hatuna budi pia kupitia fasili ya dhana hii kwa mujibu wa watu wenye ulemavu wenyewe. Mathalani, Rutachwamagyo (2008:23) anaelezea kuwa ulemavu ni hali ya jamii kutotoa fursa au haki kwa mtu aliye na kilema ili ajumuike katika shughuli za kijamii kwa usawa. Vilevile, inafafanuliwa kuwa kwa kawaida ulemavu huwa ni wa fikra na mielekeo hasi; si wa maumbile (Apalei, 2010:76). Kwa mujibu wa Apalei (keshatajwa), mtu ambaye hana kasoro za kimaumbile anaweza kuwa mlemavu kutokana na mitazamo hasi waliyonayo wanajamii na mtu mwenye kasoro za kimaumbile akawa si mlemavu. Kamusi pia ni chanzo muhimu cha fasili ya maneno mbalimbali, kwa mfano Kamusi ya Kiswahili Sanifu inamwelezea mlemavu kuwa ni mtu aliye na kiungo cha mwili chenye hitilafu ; ni hali ya kulemaa (TUKI 2000:433). Kutokana na fasili hizi, makala haya yanaona kuwa tunapozungumzia watu wenye mahitaji maalumu au walemavu (kama ambavyo majina haya mawili yatatumika kuwarejelea) ni pamoja na wasioona, viziwi, bubu, bubuviziwi, bubuviziwiwasioona, walemavu wa viungo na albino. 3.0 Historia ya Walemavu Nchini Tanzania Tangu mwaka 1961, serikali kupitia Idara ya Ustawi wa Jamii imekuwa ikitoa huduma kwa watu wenye ulemavu bila kuwa na sera. Sera ya Taifa ya Watu Wenye Ulemavu ijulikanayo kama National Policy on Disability imetungwa mwaka 2004. Vilevile, Tamko la Haki za Watu wenye Ulemavu linalojulikana kama UN Declarations of Human Rights for People With Disabilities limetolewa mwaka 1975. Pia Tanzania iliridhia makubaliano kuhusu fursa na haki sawa kwa watu wenye ulemavu ambao unajulikana kama Standard Rules of the Equalization of Opportunities for Persons with Disability mwaka 1993 (URT, 2004). Kwa muktadha wa Bara la Afrika, Tanzania ni mwanachama na imesaini mkataba

80 Kioo cha Lugha JZ. 11 wa malengo ya utekelezaji wa haki za watu wenye ulemavu ambao unajulikana kama Plan of Action for the African decade of Persons with Disabilities mwaka 1999 2009. Pia Tanzania ni mwanachama wa taasisi ya Kiafrika inayojishughulisha na kuwawezesha walemavu kuishi baada ya kupata ajali. Tanzania ilijiunga na taasisi hii ya African Rehabilitation Institute mwaka 1985 (URT, 2004). Mwaka 2001 Tanzania iliingia mapatano ya kimataifa kuhusu ulinzi na uendelezaji wa haki na utu wa watu wenye ulemavu yanayojulikana kama Comprehensive and Integral International Convention on Protection and Promotion of Rights and Dignity of Person with Disabilities (URT, 2004). Kwa kipindi chote hicho, serikali imekuwa ikiwahudumia walemavu kupitia sera, miongozo, mapatano na mikataba. Mwaka 2010 ndipo sheria ya watu wenye ulemavu iitwayo Persons with Disability Act ilipopitishwa rasmi (URT, 2010). Kwa hiyo, sasa hivi kuna nguvu ya kisheria katika kudai haki za walemavu. Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu Zanzibar, na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kwa kushirikiana na Vyuo Vikuu Tanzania, mwaka 2008 waliendesha sensa ya watu wenye ulemavu na kubaini kuwa ni asilimia 8% ya Watanzania wana ulemavu (Mwakyusa, 2008). Vilevile, Shirika la Afya Duniani linakadiria kuwa katika kila jumuiya, asilimia 10% ya watu wake wana aina fulani ya ulemavu wa kimwili na kiakili (Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, h.t:3). Takwimu hizi zinaweza kuongezeka kwa kuwa kuna walemavu wanaofichwa majumbani na hivyo kutokuhesabiwa (Mahenge, 2011). Kutokana na utafiti huo wa Wizara ya Afya na wadau wake, ilibainika kuwa, viwango vya ulemavu ni vikubwa vijijini kuliko mijini. Pia kiwango cha ulemavu ni kikubwa Tanzania Bara kuliko Tanzania Visiwani. Hali hii ni kutokana na kwamba Tanzania bara ni kubwa kijiografia na ina idadi kubwa ya watu ukilinganisha na Tanzania Visiwani. Ulemavu wa macho unaonekana kuongoza kwa idadi kubwa ukifuatiwa na matatizo ya kutembea, uziwi na kadhalika (URT, 2004: iii). Kwa hiyo, idadi ya watu wenye ulemavu nchini Tanzania ni kubwa na hivyo kundi hili linahitaji kufanyiwa tafiti mbalimbali. Mojawapo ya tafiti hizo ni huu wa kuchunguza namna lugha ya Kiswahili inavyowarejelea watu hawa kwa kuwa wamekuwa wakilalamikia matumizi ya lugha hii. Je lugha ni nini? 4.0 Fasili ya Lugha Kwa mujibu wa Besha, Lugha inachukuliwa kama tabia ya kawaida ya mwanadamu, na kwa sababu ya ukawaida huo, si mara nyingi wanadamu wakakaa na kujiuliza kitu hiki (lugha) kikoje (Besha, 2007:1). Nao Massamba na wenzake (1999:1) wanaelezea kuwa, Wataalamu wengi wa isimu na lugha wanaelekea kukubaliana kwamba lugha ni mfumo wa sauti nasibu ambazo hutumiwa na jamii kwa madhumuni ya mawasiliano kati yao. Si hivyo tu, bali Kamusi ya Kiswahili

Msigano wa Majina ya Walemavu katika Jamii ya Wazungumzaji Kiswahili 81 Sanifu nayo inafasili kuwa, Lugha ni mpangilio wa sauti na maneno unaoleta maana na ambao hutumiwa na watu ili kuwasiliana (TUKI, 2000: 211). Ukiziangalia fasili hizi za lugha utaona kuwa zinabagua lugha ya alama ambayo ni njia ya mawasiliano kwa baadhi ya walemavu kama vile viziwi, bubuviziwi, na bubuviziwiwasioona. Kuhusiana na lugha ya alama, Muzale (2004: i) anaeleza kuwa lugha hii ilichipuka nchini Tanzania baada ya viziwi kuanza kukaa pamoja na kulazimika kuwasiliana, hasa katika shule maalumu za viziwi. Lugha ya alama ni miongoni mwa lugha inayotumiwa na watu wenye ulemavu kama vile viziwi, bubuviziwi, na bubuviziwiwasioona. Kwa hiyo, kuna haja ya kuijumuisha kwenye orodha ya lugha na kutambuliwa rasmi nchini Tanzania. Hivyo, kwa maana pana, tunaweza kusema kuwa, lugha ni njia inayowezesha watu wa kundi fulani kuwasiliana ama kwa maandishi, sauti, alama, ishara, na lugha ya alama mguso. Kama lugha ni njia ya mawasiliano miongoni mwa wanajamii, je ni kwa kiasi gani lugha hiyo inatumika kuwarejelea walemavu? Katika sehemu ya 6.0 tutawasilisha majina ya walemavu kama wanavyoitwa katika jamii ya wazungumzaji wa Kiswahili nchini Tanzania na pia tutaonesha majina ambayo yanapendekezwa na walemavu wenyewe. Kabla hatujafika kwenye kiini cha makala yetu hatuna budi kueleza japo kwa ufupi vikwazo wanavyokutana navyo watu wenye ulemavu. Kwa kufanya hivi itatusaidia kupata mwanga kuhusu walemavu na suala zima la mawasiliano katika jamii. 5.0 Vikwazo Wanavyokutana navyo Walemavu katika Mawasiliano Watu wenye ulemavu wanakabiliwa na vikwazo mbalimbali kutokana na changamoto kadha za miili yao. Kwa mfano, mlemavu ambaye ni bubukiziwiasiyeona anakabiliwa na vikwazo vingi kwa pamoja. Kwanza, ni bubu hivyo anashindwa kuzungumza. Pili, ni kiziwi hivyo anashindwa kusikia sauti, na tatu haoni kwa hiyo anashindwa kuona. Mlemavu huyu anahitaji lugha ya alama ya kupapasa pamoja na maandishi ya nukta nundu ili aweze kuwasiliana na wanaoona au na watu wenye hali kama ya kwake. Kwa upande mwingine, mlemavu wa viungo ambaye hana miguu hushindwa kupanda ngazi katika majengo. Mlemavu huyu anahitaji njia isiyo na ngazi au lifti ili aweze kufika ghorofani (labda ni ofisini, hospitalini au shuleni) ili kuwasiliana na wanajamii wenzake au kupata huduma mbalimbali.

82 Kioo cha Lugha JZ. 11 Mlemavu wa macho aina hii ya ulemavu inategemea kama ni asiyeona kabisa au anayeona kidogo (mwenye uoni hafifu). Mlemavu asiyeona kabisa anakabiliwa na kikwazo cha kukosekana kwa maandishi ya breili na mashine zake. Kikwazo hiki kinamfanya ashindwe kusoma maandishi yasiyo na nundu kwa kuwa, ili aweze kuwasiliana anahitaji maandishi ya aina hiyo. Mlemavu wa macho ambaye anaona kidogo (mwenye uoni hafifu), anahitaji maandishi yaliyokuzwa kidogo. Mathalani, watu wenye ulemavu wa ngozi wanakabiliwa na tatizo hili. Hawaoni maandishi ya kawaida kama vile fonti 12 au chini ya hapo na badala yake wanahitaji maandishi yanayotumia fonti kubwa zaidi. Mlemavu ambaye ni bubu ana mahitaji tofauti na mlemavu ambaye ni bubukiziwi. Bubu ana uwezo wa kusikia kinachozungumzwa ila hawezi kuzungumza. Kwa hiyo, huyu anaweza kuwasiliana kwa vitendo na maandishi na kwa kutoa sauti fulani inayoashiria kuzungumza. Lakini kwa mlemavu ambaye ni bubukiziwi yeye anahitaji lugha ya alama ili aweze kuwasiliana. Kwa hiyo, mlemavu huyu anakabiliwa na kikwazo cha kukosekana vitabu vilivyo katika lugha ya alama pamoja na wakalimani wa lugha ya alama, kitu ambacho kinamfanya ashindwe kuwasiliana kwa njia ya kusikia sauti. Kwa hiyo, vyote hivyo kwa pamoja ni vikwazo kwa mlemavu katika suala la mawasiliano na/au ujifunzaji. Kila mlemavu ana changamoto zake ambazo ni tofauti na za mwingine. 6.0 Msigano wa Majina ya Walemavu katika Jamii ya Watanzania Kama tulivyokwisha sema toka awali, kwamba kumekuwapo na msigano wa majina wanayoitwa watu wenye ulemavu katika jamii ya Watanzania, majina hayo kwa mujibu wa maelezo yao, yanaonekana kuwadhalilisha. Majina haya ni kama vile kiwete, kilema, kipofu, zeruzeru na taahira kama tulivyoyataja mwanzoni mwa makala haya. Majina haya yanasababisha watu wenye ulemavu wajisikie vibaya (kufedheheshwa). Kutokana na hali hiyo, tulilazimika kufanya utafiti huu mdogo. Utafiti huu unatokana na kutoridhishwa kwa walemavu na majina yanayotumika kuwarejelea. Majina hayo yanaakisi ulemavu wao kama ni wa viungo, macho, akili na masikio. Hata hivyo, utafiti wetu umegundua kuwa walemavu wenye tatizo la uziwi hawana malalamiko kuhusiana na kuitwa kiziwi au viziwi. Wao hawajisikii kudhalilishwa wanapoitwa hivyo (taarifa hii ni kwa mujibu wa mazungumzo ya mtafiti na mwalimu Malise wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, 2010, yaliyofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika semina ya Lugha ya Alama ya Tanzania - LOT). Kuwapo kwa msigano kati ya majina wanayoitwa walemavu ni suala lililokuwapo kwa muda sasa katika jamii ya wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili. Kuwaita majina hayo ambayo hawayataki hakutokani na makusudi au kukosekana kwa

Msigano wa Majina ya Walemavu katika Jamii ya Wazungumzaji Kiswahili 83 majina mwafaka, la hasha! Bali ni kutokana na mazoea ambayo jamii imejijengea ya kuwaita kwa namna hiyo. Yaani kuwaita kwa kurejelea hali ya viungo vyao au maumbile yao. Utafiti wetu umegundua kuwa kuelimika miongoni mwa walemavu kumewasaidia kuchunguza majina yao haya na kuyaona kuwa yanawanyanyapaa na kuwadhalilisha. Ninataja kuelimika kwa kuwa hoja hii iliibuliwa na wanavyuo walemavu pamoja na walemavu wasomi ambao ni wanaharakati kama vile Kaganzi Rutachwamagyo ambaye aliwahi kuwa mkurugenzi wa Information Centre on Disability (ICD) na wengineo. Hoja yao kuu kuhusu udhalilishaji wa majina hayo ilikuwa ni matumizi ya ngeli ya kitu au vitu (KI/VI) badala ya ngeli ya viumbe hai (M/WA). Katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mnamo mwaka 2002-2006 kulikuwa na wanafunzi wenye ulemavu wapatao wanne ambao nilisoma nao shahada ya ualimu na somo la kufundishia likiwa ni Kiswahili. Wanafunzi hawa ndio walionifanya nianze kufanya utafiti ili kuona kwa nini wanakataa kuitwa hivyo tulivyozoea kuwaita. Hebu tujiulize, kuna tofauti gani kati ya ngeli ya KI/VI na M/WA? Ngeli ya KI/VI inahusisha vitu visivyo na uhai ambavyo huanza na kiambishi ki katika umoja na vi katika wingi. Nomino kama vile kiti-viti, kisu-visu, kioo-vioo na kiatu-viatu zinaingia katika ngeli hii. Kwa hiyo, kumwita mtu kilema-vilema, kipofu-vipofu na kiwete-viwete ni kumdhalilisha na kumfanya ajisikie vibaya kutokana na kulinganishwa na kitu. Kuhusiana na jina kiwete, mmoja wa watafitiwa wetu anaeleza kuwa jina hili ni la kudhalilisha hata wewe mwenyewe ukifikiria kwenye akili yako sawa hata kama unaonekana vile lakini ukiangalia kwa undani ni kama linakudhalilisha lile jina [.] hivi sasa sisi tumezoea kuita mlemavu wa viungo. Kwa upande wa jina kipofu, walemavu waliohojiwa na mtafiti wanaeleza kuwa jina hili linadhalilisha. Pia watu wazima huwa wana kejeli zao. Mtu anaweza kukukebehi tu na kusema: kwani wewe kipofu. Kwa hiyo unafanya rejea ya mtu mwingine kwa mambo mabaya.. Jina sahihi ambalo halidhalilishi ni asiyeona. Hali hii ya kupinga kuitwa majina haya imejitokeza pia kwa jina zeruzeru. Utafiti wetu umebaini kuwa jina hili katika baadhi ya tamaduni za Kiafrika linamaanisha mtoto wa shetani. Hivyo, watu wengine hudhani moja kwa moja kuwa zeruzeru ni mtoto wa shetani...jamii haina budi kuachana na jina zeruzeru na badala yake kutumia jina albino.

84 Kioo cha Lugha JZ. 11 Kwa mujibu wa mazungumzo na walemavu hao, wanapendekeza ngeli ya viumbe hai ndiyo itumike kuwarejelea. Ngeli hii ya M/WA inahusisha viumbe hai ambao ni pamoja na wanyama, wadudu, ndege, na kadhalika. Binadamu ni kiumbe hai, ni mnyama, kwa hiyo jina linalomtambulisha mtu linapatikana katika ngeli hii ukiachilia mbali nomino zinazoanza na ki/vi kama vile kijana/vijana; kiongozi/viongozi; na kingunge/vingunge kwani majina haya hayaashirii dosari za kimwili. Kuna majina kama vile mtu-watu, mtoto-watoto, mzee-wazee, mjombawajomba, na kadhalika. Ngeli hii ndiyo inayotambulisha watu kwa hiyo walemavu nao ni watu. Kwa mantiki hiyo, majina yanayorejelea ulemavu yanatakiwa yatokane na ngeli hii. Ndiyo maana tuna majina na vitenzi mbadala kama vile mlemavu/walemavu; asiyeona/wasioona; mwenye umbile fupi/wenye maumbile mafupi, na kadhalika. Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977), haki za binadamu ni pamoja na: haki ya usawa, kuishi, kupata elimu, kujumuika, kwenda kokote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kushiriki katika jamii, kupata taarifa, usawa wa kutambuliwa kama mtu mbele ya sheria, kuheshimiwa, kutokubaguliwa, uhuru wa kujieleza, uhuru wa kutoa mawazo, ajira, kuwa na familia, kupiga kura, na uhuru wa kuabudu dini unayoipenda. Sababu ya makala haya kuihusisha Katiba ya nchi yetu ni kutaka kupata msingi wa kisheria kuhusu haki ya kuheshimiwa ambayo walemavu wanaona inakiukwa. Majina wanayoitwa walemavu nchini Tanzania yanakiuka haki ya kuheshimiwa. Jambo hili ni kinyume cha sheria na Katiba ya nchi. Katiba inamtaka kila mtu aheshimiwe utu wake kwa kuwa watu wote wako sawa mbele ya sheria. Je, ni kweli walemavu wanavunjiwa heshima na watumiaji wa lugha ya Kiswahili? Madai haya ya kutoheshimiwa yanathibitishwa pia na kitabu kinachoitwa Maadili kuhusu Ulemavu kilichoandikwa na ICD na kuchapishwa mwaka 2002 kwa msaada wa Ubalozi wa Ufini nchini Tanzania. Kitabu hiki kinaonesha majina yenye kejeli ambayo wanaitwa watu wenye ulemavu na ambayo yanawadhalilisha. Mwandishi wa kitabu hiki anasema hivi: Majina yenye kejeli ni udhalilishaji wa utu wa mhusika hivyo kuwa chanzo cha kumtenga na kumsababishia sononi. Mpe haki ya kuchagua jinsi anavyotaka aitwe (ICD, 2002:1). Nukuu hii inaelezea majina wanayoitwa walemavu ambayo ni: kipofu, zeruzeru, kiziwi, kichaa, zezeta, taahira, mbilikimo, kilema, kiwete, na asiyejiweza kuwa yanawakejeli na kuwafanya wajisikie kudhalilishwa utu wao. Majina hayo yanamfanya mlemavu ajisikie kutengwa na jamii yake na kumsababishia sononeko moyoni. Kwa hiyo, inashauriwa kuwa watu wasio na ulemavu wakubali mabadiliko. Wakubali kuwaita walemavu majina mazuri

Msigano wa Majina ya Walemavu katika Jamii ya Wazungumzaji Kiswahili 85 ambayo walemavu wanayataka. Mathalani, Kamusi ya Kiswahili Sanifu (TUKI, 2000) inafasili baadhi ya majina hayo ya walemavu kama ifuatavyo: Kilema: i. ni kasoro iliyoko kwenye kiungo au viungo vya mwili ; uatilifu. ii. mtu mwenye upungufu wa kiungo kama vile kiwete (TUKI, 2000: 169). Kiwete: ni mtu aliyelemaa miguu yote miwili (TUKI, 2000: 187). Kipofu: ni mtu asiyeona kutokana na kuugua, ajali, au kuzaliwa hivyo Zeruzeru: (TUKI, 2000:176). ni mtu ambaye nywele na ngozi yake imekosa rangi yake kamili na badala yake kuwa nyeupe sana na ambaye macho yake hayawezi kuvumilia mwangaza mwingi; albino (TUKI, 2000: 467). Hizo ndizo maana za majina hayo yanavyoelezwa kwenye kamusi. Maana hizo au majina hayo ndiyo yanayoibusha msigano. Ni msigano kwa kuwa, wanajamii ambao ni wazungumzaji wa Kiswahili, ambao sio walemavu, wanayatumia majina hayo kuwarejelea watu wenye ulemavu. Na kwa upande mwingine, walemavu wanayakataa majina hayo na kudai kuwa yanawadhalilisha. Badala yake, walemavu wana fasili yao kuhusu ulemavu na vilevile wana majina yao mbadala ambayo wanataka warejelewe kwayo, kama inavyopendekezwa hapa chini: 7.0 Watu wenye Ulemavu Wanapendekeza Waitweje? Pendekezo la kubadilisha majina hayo yenye dharau na kebehi linatolewa katika kitabu cha Maadili kuhusu Walemavu (ICD, 2002:1) na pia watafitiwa wa utafiti wetu. Majina hayo ndiyo wanayoyapendekeza walemavu wa Tanzania kupitia Kituo cha Habari Kuhusu Ulemavu. Majina hayo ni: asiyeona, albino, kiziwi, mwenye ugonjwa wa akili, mwenye ulemavu wa akili, mwenye umbile fupi, mlemavu, mlemavu wa viungo, na mtu mwenye ulemavu (ICD, 2002:1). Tutazame orodha ya majina hapa chini ambapo katika upande wa kushoto, kuna majina ambayo walemavu hawayapendi na upande wa kulia kuna majina ambayo walemavu wanapenda warejelewe: Badala ya Kuita Kipofu... Zeruzeru, mlemavu wa ngozi... Asiyesikia... Ita Hivi asiyeona albino kiziwi

86 Kioo cha Lugha JZ. 11 Kichaa... mwenye ugonjwa wa akili Zezeta, taahira... mwenye ulemavu wa akili Kifafa... mwenye kifafa Mbilikimo... mwenye umbile fupi Kilema... mlemavu Kiwete... mlemavu wa viungo Asiyejiweza... mtu mwenye ulemavu Katika orodha hiyo, neno asiyejiweza halimaanishi maskini bali wanaolitumia wanamaanisha mtu ambaye ana ulemavu, yaani anayehitaji msaada fulani ili aweze kutenda jambo fulani. Mathalani, mlemavu wa miguu ambaye hawezi kutembea huenda anahitaji kubebwa kama njia ya kujongea; ama la anatumia kitimwendo au baiskeli ya magurudumu kwa hiyo anahitaji kusukumwa. Umaskini sio ulemavu. 8.0 Hitimisho Makala yameona kuwa maana ya ulemavu inatofautiana kimtazamo baina ya watu wenye ulemavu na wale wasio na ulemavu. Utafiti umebaini na kuthibitisha kuwa kuna msigano wa majina waitwayo walemavu katika jamii ya wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili nchini Tanzania. Hakuna budi wadau husika wa mambo ya lugha wakiwemo wataalamu wa Kiswahili na watunzi wa kamusi, kukaa pamoja na watu wenye ulemavu mbalimbali ili kuzungumza na kuafikiana namna wanavyotaka kutambuliwa katika jamii. Ikifikia hatua hiyo, tupate Kamusi ya Kiswahili Sanifu ambayo imezingatia mahitaji maalumu ya watu wenye ulemavu. Kamusi ambayo ni jumuishi na itakayowafanya wazungumzaji wote wa Kiswahili wajisikie vizuri kuhusiana na lugha yao. Halikadhalika, jamii haina budi kubadili namna ya kuwaita walemavu hao. Vilevile, kwa kuzingatia haki za binadamu hasa kipengele cha kuheshimiwa, wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili hawana budi kuwaheshimu walemavu kwa kuwa ni haki ya msingi ya kila raia wa Tanzania kuheshimiwa. Lugha ya kebehi, dharau na inayolenga dosari za kimaumbile za watu wenye ulemavu iepukwe kwa nguvu zote. Nikisema hivi ninamaanisha kuwa, watu wenye ulemavu wana majina yao waliyopewa na wazazi wao, tusiwape majina kwa kurejelea hitilafu za miili yao. Mathalani, kama mtu ambaye si mlemavu lakini ana dosari ya kukojoa kitandani akiwa usingizini, atajisikiaje akiitwa kikojozi mbele ya wanajamii, watoto wake, au watu wake anaowaheshimu? Bila shaka mtu huyu atajisikia vibaya na huenda akaonyesha mrejesho hasi kutokana na kuitwa hivyo. Wito wa makala haya ni kuhimiza mabadiliko katika jamii hususan matumizi ya lugha inayotumika kuwarejelea watu wenye ulemavu.

Msigano wa Majina ya Walemavu katika Jamii ya Wazungumzaji Kiswahili 87 Marejeo Besha, M. R. (2007). Utangulizi wa Lugha na Isimu. Dar es Salaam: Macmillan Aidan Limited. CCBRT, (2010), Persons With Disability Act. Dar es Salaam: Mpiga Chapa wa Serikali. ICD, (2002). Maadili kuhusu Ulemavu. Dar es Salaam: Ubalozi wa Ufini Tanzania. ILO, (2007). Kufanikisha Fursa Sawa za Ajira kwa Watu wenye Ulemavu kupitia Sheria: Mwongozo, Dar es Salaam. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wizara ya Ajira, Maendeleo ya Vijana na Michezo, Sera ya Taifa Kuhusu Ulemavu. Mpiga Chapa wa Serikali : Dar es Salaam. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, (h.t:), Mwongozo Kuhusu Watumishi Wenye Ulemavu. Mpiga Chapa wa Serikali : Dar es Salaam. Mahenge, E. (2010). Baadhi ya Changamoto Zinazowakabili Walemavu wa Tanzania, (haijachapishwa. Iliwasilishwa kwenye Tamasha la Sauti za Kiswahili lililoandaliwa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Mwaka 2010 katika Hoteli ya Elephant Dar es salaam). Mahenge, E. (2011) Walemavu wa Tanzania. Carolina: North Carolina Co Ltd. Muzale, H. T. R. (2004). Kamusi ya Lugha ya Alama ya Tanzania (LAT). Dar es Salaam: TUKI. Mwakyusa, D. (2008). Jamhuri ya Muungano wa Tanzania: Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Taarifa ya Mheshimiwa Profesa David Homeli Mwakyusa (MB), Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii kwa vyombo vya habari kuhusu matokeo ya awali ya utafiti uliofanyika mwaka 2008 juu ya watu wenye ulemavu Tanzania. Massamba, D.P.B, Kihore, Y.M, Hokororo, J.I. (1999). Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu (SAMIKISA). Dar es Salaam: TUKI. United Republic of Tanzania (URT): Ministry of Labour, Youth Development and Sports. (2004). National Policy on Disability, Dar es Salaam. United Republic of Tanzania. (1977). The Constitution of United Republic of Tanzania. Dar es Salaam. United Republic of Tanzania. (2010). Persons With Disability Act. www.ccbrt.or.tz/.../summary of Persons with Disabilities Act 201.

88 Kioo cha Lugha JZ. 11 Rutachwamagyo, K. (2000). Dhana ya Elimu Jumuishi: Ulemavu na Haki ya Elimu nchini Tanzania. Dar es Salaam. TUKI (2000) Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Dar es Salaam: TUKI.

Msigano wa Majina ya Walemavu katika Jamii ya Wazungumzaji Kiswahili 89 Baadhi ya Mahojiano kati ya Mtafiti na Watu wenye Ulemavu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Swali: Ninapenda kufahamu maana ya mlemavu kwa mtazamo wako. Jibu: Mtu mwenye ulemavu ni binadamu yeyote wa kawaida kama ulivyo wewe au kama mtu mwingine ambaye wewe unamfahamu. Lakini mpaka aitwe mwenye ulemavu ana kasoro zinazomfanya aonekane yuko tofauti na mwenzake kimtazamo, kimwili au kiakili na vinginevyo ambavyo tutazungumza huko mbele. Swali: Ulemavu ni nini? Jibu: Ni ile hali ya mtu kutomudu kufanya kitu kwa uwezo wake yeye mwenyewe. Mathalani, mtu amekatika mikono miwili hawezi kulima huyu ni mwenye ulemavu. Kule kukatika mikono yake ndicho kilema chake kwa hiyo, kile kikwazo chake mimi naweza kukiita kilema chake. Lakini kuna baadhi ya watu wamekuwa wakiwaita watu kilema. Mimi binafsi siwezi kumwita mtu kilema ila nitamwita mlemavu. Kilema ni ile hali inayomfanya aonekane vile kuwa na mapungufu fulani: kile ndicho kilema chake. Swali: Nimesikia kuwa baadhi ya majina wanayoitwa watu wenye ulemavu, wenyewe hawayapendi, majina kama kilema, kiwete, zeruzeru, kipofu, kiziwi. Wewe unasemaje? Jibu: Haya majina ya watu wenye ulemavu mzizi wake ni wa kizamani. Baadhi ya majina haya mzizi wake unatokana na mila na desturi kutoka maeneo mbalimbali ya Watanzania na Waafrika pengine hata Wazungu. Mkifanya utafiti mtabaini labda walivyokuwa wanawaita watu wenye ulemavu [...] Kwa hiyo naweza nikakubali baadhi ya majina hayo lakini kuna mengine naweza nikatoa hoja Kwa mfano neno kiziwi. Sina tatizo na neno kiziwi lakini nina tatizo na mtu anayeendelea kusema kwamba yule mtu hasikii. Kwa sababu mtu asiyesikia katika jadi yetu ni mkaidi, mwenye kiburi, maringo, majivuno, juha [ ] Swali: Vipi kuhusu jina kiwete? Jibu: Jina hili ni la kudhalilisha, hata wewe mwenyewe ukifikiria kwenye akili yako sawa, hata kama unaonekana vile, lakini ukiangalia kwa undani ni kama linakudhalilisha lile jina [.] hivi sasa sisi tumezoea kuita mlemavu wa viungo [ ] Swali: Kuna tofauti gani kati ya zeruzeru na albino? Jibu: Jina hili albino lina asili ya nchi za Kigiriki. Neno ambalo

90 Swali: Jibu: Kioo cha Lugha JZ. 11 linamaanisha kwenye tamaduni zao `nyeupe au yenye rangi nyeupe. Albino ni binadamu aliyekosa seli za kutengeneza rangi katika mwili wake kutokana na sababu za kibiolojia. Hapa Tanzania tulikuwa tunaita zeruzeru. Lakini wanaharakati walikaa wakatafakari nakuona jina hili linatumika kama kejeli. Jina hili katika baadhi ya tamaduni zetu linamaanisha mtoto wa shetani. Jina hili la zeruzeru linadhalilisha na watu wengine wanakwenda moja kwa moja na kusema kuwa zeruzeru ni mtoto wa shetani. Kwa hiyo, mtu mwenye ulemavu akapewa upendo na jamii inashawishiwa ikubali kuachana na jina zeruzeru [ ] Jina kipofu nalo unalizungumziaje? Jina hili linadhalilisha. Na pia watu wazima huwa wana kejeli zao. Mtu anaweza kukukebehi tu na kusema: kwani wewe kipofu. Kwa hiyo unafanya rejea mtu mwingine kwa mambo mabaya [ ]. Jina sahihi ambalo halidhalilishi ni asiyeona.