TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU

Similar documents
Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA MHESHIMIWA DKT

JAMHURI YA KENYA. Mkakati wa Ushirikiano MUKHTASARI FY Public Disclosure Authorized. Public Disclosure Authorized

MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2017/18

MAADHIMISHO YA MIAKA 15 YA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

Information for assessors (do not distribute this page to participants):

Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA 2006/07

Dibaji ya Mwenyekiti wa Kamati ya Pamoja ya Uongozi

TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM)

ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA UCHUMI WA ZANZIBAR

Nilikua na Ndoto ya Kumaliza Shule Changamoto za Elimu ya Sekondari Tanzania

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

Kuuelewa Mchakato wa Bajeti Tanzania Mwongozo wa Asasi za Kiraia

Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara)

In the matter of an Application by the KIGOMA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (KUWASA) For a Tariff and Charges Adjustment

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA FEDHA

Kuwafikia waliotengwa

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA,KWA WANANCHI, 30 SEPTEMBA, 2001

Taarifa Kuhusu Hali ya Uchumi wa Tanzania

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO

5. Mheshimiwa Spika, Bunge lako Tukufu lilijadili kwa kina Miswada ifuatayo:

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA. Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo. TOLEO Na.

Dodoma ambako kikao cha Bunge kinaendelea kuja kushiriki japo sehemu ya uzinduzi wa mkutano.

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, MHESHIMIWA DKT. PHILIP I. MPANGO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

Human Rights Are Universal And Yet...

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA PRO-ROUTES. Ombi kwa ajili ya fedha za umma wa mradi wa ziada

NGUZO KUMI ZA KILIMO KWANZA

Azimio lililopitishwa na Mkutano Mkuu tarehe 18 Desemba 2013 [juu ya taarifa ya Kamati ya Tatu (A/68/456/Add.2)]

Ufanisi katika Ufundishaji kwenye Shule za Msingi na Sekondari nchini Tanzania

Miradi na jamii. 3.1 Utangulizi

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

TANZANIA MARKETS PAN Sera zinazoboresha masoko

Kubadili Sheria Za Mbegu Na Ulinzi Wa Aina Za Mbegu Na Mimea Nchini Tanzania

KUHUSU AFRODAD. Dira ya AFRODAD. Dhamira ya AFRODAD. AFRODAD inalenga mchakato sawa na endelevu wa maendeleo kuelekea Afrika yenye mafanikio.

Songa kwenye kilele cha upeo. Masuala ya Msingi na Ujuzi juu ya Uendeshaji wa Serikali za Mitaa

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA NISHATI NA MADINI

TANZANIA TAARIFA YA MWISHO WA UTEKELEZAJI

Programu ya Uendelezaji Mifumo ya Maji Vijijini (PUMMV) katika Tanzania. Modeli wa Ukodishaji Mradi

Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2013

TAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF) KUHUSU HAKI ZA WATOTO KATIKA KATIBA MPYA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II

KAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI TANZANIA

MAPENDEKEZO YA MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA TANZANIA

KUSHUKA KWA HADHI YA LUGHA ZA JAMII NCHINI TANZANIA YOHANA P. MSANJILA University of Dar es Salaam, Tanzania

3. Mheshimiwa Spika, 4. Mheshimiwa Spika,

TAARIFA YA MWAKA YA UTENDAJI KAZI IDARA YA UTAWALA BORA 2013/2014

In the matter of Application by the TANGA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (TANGA UWASA) For a Multi-Year Tariff Adjustment

ORDER NO BACKGROUND

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

KIMAZINGIRA NA KIJAMII NA MPANGO WA UDHIBITI

Pronunciation: Mä-hret Zäläke Ndal-ka-tscho Molla Mare Gebre-gzabiär 1/12

Mwongozo wa Kutathimini mifumo ya Ugawanaji wa faida na Mapato Katika Miradi ya Jamii ya MKUHUMI

UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA)

Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali ya Madini Ukanda

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

LUGHA YA KISWAHILI KATIKA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA ELIMU SHULE ZA SEKONDARI

KITEGO CHA MAREKEBISHO NA HAKI ZA MTOTO

Kufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007

Elimukombozi, Lugha na Upashanaji Habari nchini Tanzania, katika Muktadha wa Utandawazi

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA

UFUATILIAJI WA MIRADI NA TATHMINI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame M. Mbarawa (Mb.); Waheshimiwa Mawaziri na Wabunge wote mliohudhuria;

HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara

Summaries of GC Reports 2012, Vol. 2, Sec. 1, Swahili

HAKI NA TARATIBU ZA AJIRA, KAZI NA HIFADHI YA JAMII

SautiElimu. Sauti Yako Isikike

Govt increases vetting threshold of contracts

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu WEMA

TIST HABARI MOTO MOTO MAANDALIZI YA MWAKA 2000 Y2K PREPARATIONS SASA NI WAKATI WA KUANZA KUPANDA MBEGU ZAKO

Uhakika wa Mbegu kwa Uhakika wa Chakula MWONGOZO WA UZALISHAJI WA MBEGU ZA ASILI ZA MAHINDI

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA SABA. Kikao cha Thelathini na Tisa Tarehe 1 Juni, (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A

Elimu-Jumuishi Kwa Vitendo

UTANGULIZI. 1. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako. 2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote nitumie fursa hii kuungana na

RIPOTI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI

UFUPISHO WA 35. Hali ya kiulimwengu ya Tekinolojia ya kibiashara/ugeuzi jeni na uboreshaji mazao: Clive James Chair, ISAAA Board of Directors

Kufanya Uwekezaji kuwa wa Manufaa kwa Afrika: Jibu la Mbunge kuhusu Unyakuzi wa Ardhi

Draft 03 MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO MWENGE

Kiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika

Unyanyasaji wa Watoto & Kutelekezwa

RIPOTI YA WARSHA KUHUSU HABARI KWA AJILI YA UWAJIBIKAJI

Deputy Minister for Finance

MWONGOZO WA USHIRIKISHWAJI KATIKA KUPANGA MATUMIZI YA ARDHI WORLD BANK

UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU VIKWAZO VYA KULINDA MAISHA KATIKA USAIDIZI WA KIMATAIFA WA AFYA KWA MSAADA WA KIMATAIFA UNAOFADHILIWA NA MAREKANI

Kutetea Haki za Binadamu

MWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

Transcription:

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU TANZANIA EDUCATION NETWORK / MTANDAO WA ELIMU TANZANIA ()

1.0 USULI Tanzania, sawa na nchi nyingine, ilitia saini Malengo ya Maendeleo ya Milenia na Malengo ya Elimu kwa Wote - yaliyoridhiwa mwaka 2000 na kutekelezwa hadi mwaka 2015. Ajenda ya sasa ya maendeleo ya nchi huongozwa na nyaraka nyingi zikiwemo Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), Ajenda ya Elimu 2030 na Mkakati wa Elimu wa Bara la Afrika (CESA). Serikali imepiga hatua kubwa katika kutimiza malengo ya kitaifa ndani ya muktadha wa malengo ya dunia/bara na hadi sasa imeonesha kuwa na msimamo thabiti wa kutekeleza malengo mapya kwa kuandaa Mpango wa Kuendeleza Sekta ya Elimu. (ESDP 2016/17-2021/22). Mpango huu unajenga juu ya jitihada za awali katika kutekeleza mpango wa elimu ya msingi bila malipo hapa Tanzania - unaoongozwa na Mkakati wa Elimu Jumuishi Kitaifa (2009-2017) na unaambatana na SDG4&5 ya elimu bora jumuishi ya haki sawa inayohimiza fursa za watu wote kuendelea kujifunza maisha yao yote. Lengo madhubuti la serikali la kuwezesha elimu jumuishi lilidhihirishwa na utoaji wa Tshs bilioni 16 kwa watoto wenye mahitaji maalum mwaka 2016. Kwa hiyo, haishangazi kwamba Tanzania imesifiwa kama nchi mojawapo iliyofanikisha malengo ya MDG na EFA katika miaka 15 iliyopita. Maendeleo yaliyopatikana yamethibitishwa kwa ongezeko la idadi ya wanafunzi kujiandikisha kutokana na kuondolewa kwa ada mwaka 2001. Kiwango cha Uandikishaji wa Jumla Shuleni (GER) kiliongezeka kufikia 85.6%, wakati kujiandikisha kwa ujumla ilifikia watoto 8,639,202 (ESA, 2016). Kwa mujibu wa ESA, GER kitapanda kufikia 100% kadiri watoto wanavyoongezeka kuandikishwa: 11,476,803 mwaka 2024. Hii inakadiriwa kuwa ongezeko la 30.5% katika miaka 10. Wakati wa kutathmini maendeleo hadi sasa, wadau wa elimu kutoka serikalini na Asasi za Kiraia walikutana kuanzia tarehe 15-16 Mei 2017 huko Blue Pearl Hotel Dar es Salaam na kutafakari kwa kina maendeleo pamoja na changamoto zilizopo katika sekta ya elimu. Yafuatayo ni mapendekezo ya sera yanayotokana na mkutano huu na yanawasilishwa kwa serikali ili wayazingatie - kufikia elimu jumuishi kwa wote kwa misingi ya haki sawa kwa muda mfupi zaidi. Changamoto zilizotambuliwa za sekta ya elimu zinazohitaji kufikiriwa kwa kina - wakati wa kusonga mbele - ni pamoja na yafuatayo: 10% ya Watoto wenye Mahitaji Maalum ya Elimu (CSEN) wako shuleni hapa Tanzania. Hii ina maana kwamba watoto walio wengi wameachwa nyuma. Zana za Kufundishia na za Kujifunzia hazitoshi kwa kikundi hiki cha watoto pamoja na kukosekana kwa walimu wenye stadi na taaluma maalum za kuwafundisha Watoto wenye Mahitaji Maalum ya Elimu. Kwa hiyo, Watoto wenye Mahitaji Maalum ya Elimu wako miongoni mwa kundi kubwa la watoto wanaofanya vibaya katika masomo yao, wanaokaa shuleni muda mrefu kuliko inavyotegemewa au kuacha shule kabisa. Hii inamaanisha pia kwamba Mkakati Jumuishi Kitaifa (NIS, 2009 2017) unapaswa kupitiwa kwa kina ili kulenga kwa makusudi wanaostahili

kunufaika na pia kuendana zaidi na hali halisi. Miundombinu ya shule haitoshi - Uwiano kati ya Wanafunzi na Darasa (PCR) ni 1:80, Choo na wanafunzi ni 1:55 kwa wastani, badala ya 1:22.5 ambacho ni kiwango tarajiwa na dawati/wanafunzi ni: 1:4.3 badala ya 1:3, ambacho ndicho kiwango. Kwa hiyo matokeo ya mafunzo huathirika. Usawa kijinsia ni 50% (2016) kwenye shule za msingi jambo ambalo linamaanisha kwamba Tanzania iko mbali na kufikia usawa kijinsia - kwa kuwa malengo kitaifa na kidunia hayajafikiwa tangu 2005. Kuondolewa kwa ada ni mpango mzuri ambao uliwawezesha wazazi kubeba gharama zingine za moja kwa moja za elimu ya msingi. Wazazi walichangia chakula shuleni na pia walilipia gharama za mitihani ya mwezi na maandalizi ya mitihani ya mwisho. Lakini gharama hizi zimekuwa mzigo mzito mno kwa wazazi jambo ambalo limesababisha watoto wa kaya maskini kuacha shule. Ruzuku ya $10 kwa kila mtoto iliyoanzishwa mwaka 2001 sasa haitoshi kutokana na kupungua kwa thamani ya shilingi baada ya miaka yote hii. Wakati, mwaka 2001, dola moja ilikuwa sawa na Tshs 10,000 Tanzania, leo dola ni sawa na Tshs 2,200. Kiuhalisia, imekuwa sawa na $5 ukizingatia kwamba mtoto hapokei hizi $10 moja kwa moja. Ingawa Sera ya Elimu ya Awali ipo, mafanikio ya sera hii ni madogo sana. Elimu ya Awali ilijumuishwa moja kwa moja katika elimu ya msingi (2014) lakini shule nyingi hazina madarasa mazuri ya elimu ya awali. Sekta ya shule za awali hazina walimu wenye stadi wa kutosha wa kuweza kuwapatia watoto taarifa sahihi. Bado kuna watoto zaidi ya milioni 3 ambao hawapo shuleni na ushahidi mwingine huonesha kwamba idadi hii huongezeka kutokana na watoto wanaoacha shule. 2.0 MASUALA YA SERA Wadau wa Baraza la Kitaifa la Sera walitambua kuwepo kwa hali inayoweza kufanikisha SDG 4 hapa Tanzania. Kuwepo kwa sera ya elimu bila malipo (Sera ya Elimu na Mafunzo, 2014) kwa muda wa miaka 11, Mkakati Jumuishi wa Kitaifa na sera ya jinsia n.k. huthibitisha msimamo imara wa Tanzania kutekeleza SDG 4 na 5, Ajenda ya Elimu 2030 na Mkakati wa Elimu wa Bara la Afrika (CESA). Hali hii hutoa fursa zaidi kwa kuharakisha mafanikio katika sekta ya elimu Tanzania kwa kulenga hasa ujumuishi na haki sawa katika sekta. Kutenga na kuwekea vipaumbele kwa Elimu ya Awali, elimu ya wasichana, watoto wenye mahitaji maalum na watoto nje ya shule itasaidia kukabiliana na ukosefu wa haki sawa pamoja na kupunguza umaskini. Miradi ya kijamii katika sekta ya elimu Tanzania inaweza kufikiriwa upya ili kuhakikisha kwamba mkakati wa lishe kitaifa, ruzuku za shule na miradi mengine inayolenga mahitaji katika jamii, inalenga pia kupunguza mzigo wa wazazi ili kushughulikia vizuri zaidi maslahi ya kikundi lengwa. Sera na mfumo kisheria unaoambatana na sera vitasaidia kuonesha njia vizuri zaidi na pia kutenga fedha za kutosha kwa ajili ya miradi ya kijamii katika sekta ya elimu.

Tanzania inatoa fursa kwa utoaji wa elimu bora jumuishi bila malipo iwapo fursa zote za kugharamia elimu jumuishi zimetafutwa na kutumika hasa na msimamo imara zaidi kutetea misingi ya haki sawa na utawala bora. Hatua zinazochukuliwa kuziba mianya ya kukwepa kodi, rushwa na ubadhirifu wa fedha za umma zinatoa fursa nzuri zaidi za kufanikisha SDG 4 na 5. Uwajibikaji endelevu na hatua za kinidhamu dhidi ya watumishi wa umma wasio weledi na hatua za kupunguza matumizi zitasaidia kuhakikisha uwezo wa kugharamia elimu jumuishi na hakisawa Tanzania. 3.0 MAPENDEKEZO YA SERA Baraza la siku mbili la serikali na asasi za kiraia kuhusu sera ya elimu lilikubaliana kwa sauti moja kuhusu maeneo muhimu kadhaa ya elimu yanayotakiwa kupewa kipaumbele. Baraza lina imani madhubuti kwamba maeneo haya yakitekelezwa kikamilifu, sekta ya elimu ya Tanzania itashuhudia kuboreshwa sana. 1. Kubuni vyanzo mbadala nchini ya kugharamia sekta ya elimu Asilimia fulani ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (k.m. 5%) itolewe kwa sekta ya elimu. Fedha zinaweza kuwekwa kwenye mfuko maalum wa elimu na kutunzwa na msimamizi wa mfuko huo. Kisha msimamizi ataomba idhini ya bunge kugawa fedha hizo kwa utoaji wa pembejeo za shule na rasilimali katika sekta ndogo za elimu hapa Tanzania. Baraza lilivutiwa sana na mfano wa aina hii kutoka Ghana. Inapendekezwa kwamba pesa zinazotokana na kampuni za mawasiliano (Vodacom, Airtel, Tigo, Zantel na TTCL) zigawiwe moja kwa moja kwenye sekta ya elimu. Pesa hizi ziwekwe kwenye mfuko usioingilika ili kuhakikisha pesa hazigawiwi vibaya. Ilipendekezwa kwamba Mrabaha ya Madini na Gesi igawiwe zaidi kwa sekta ya elimu. Mantiki ya pendekezo hili ni kwamba, kwa kuwa madini (extractives) ni rasilimali isiyoweza kurejeshwa, njia bora ya kuwekeza hizi pesa ni kuwekeza katika mustakabali wa Tanzania - watoto wetu. Inapendekezwa zaidi kwamba angalau 30% ya Mfuko wa Kuendeleza Jimbo itengwe na kulengwa kugharamia elimu katika maeneo kadhaa. Aidha baraza lilipendekeza kwamba asilimia fulani kutoka sekta ya utalii (k.m. 10%) irudishwe kwenye maeneo ya utalii - vijiji kwa ajili ya kuwekezwa kwenye sekta ya elimu. Wadau wa serikali na asasi za kiraia walipendekeza pia ongezeko la bajeti ya elimu hadi kufikia lengo la kimataifa la kutenga 20% ya bajeti ya nchi kwa ajili ya elimu ili kuzidisha fursa ya kusoma kwa wote nchini Tanzania. Aidha ilifahamishwa na kupendekezwa kwamba kijiji cha Kikanda Wilayani Kilwa, katika mwaka uliopita, kupitia kwa sheria ndogo ya marejesho 20% iliyopitishwa kuhusu makusanyo ya mazao ya kijiji kama vile ufuta, mapato kutoka kwenye kijiji yalifikia takriban Tshs milioni mia mbili. Iwapo kiasi hicho kilielekezwa kugharamia elimu kitaleta mabadiliko makubwa katika shule ya

msingi ya kijiji. Sheria ndogo kama hii inaweza kupitishwa katika vijiji vyote vya Tanzania na kwa kila zao kijijini ili kuimarisha ubora wa elimu. Tanzania inapoteza mapato makubwa sana kupitia kwenye kodi, kama ilivyooneshwa katika taarifa yenye kichwa: The One Billion Dollar Question Revisited: How Much is Tanzania Now Losing in Potential Tax Revenues Second edition, May 2017. Utafiti huu ulifadhiliwa na Interfaith Standing Committee on Economic Justice and the Integrity of Creation (ISCEJIC: TEC, BAKWATA and CCT) na kuandikwa na Mark Curtis (www.curtisresearch. org) pamoja na Profesa Prosper Ngowi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Dar es Salaam. Utafiti huu mpya unaonesha kwamba Tanzania inaendelea kupoteza rasilimali nyingi sana kila mwaka - na hali hii inazidi kuongezeka. Utafiti unakadiria kwamba Tanzania sasa hupoteza takriban $1.83 bilioni (Tshs. 4.09 trilioni) kwa mwaka kutokana na misamaha ya kodi, utoroshaji haramu wa fedha, kushindwa kulipisha kodi sekta isiyo rasmi na aina zingine za kukwepa kodi. Huenda nchi inapoteza $1.3 bilioni (TShs 2.9 trilioni) zaidi kutokana na ufisadi katika bajeti ya kitaifa, jambo ambalo linachepua rasilimali ambayo ingegharamia huduma muhimu za umma. Iwapo hizi $1.83 bilioni zilizopotea zingetumika kugharamia huduma za jamii zingeweza: i - Kuongeza mara tatu bajeti nzima ya afya ya serikali, au ii - Kuongeza bajeti ya serikali ya elimu karibu mara mbili. Aidha tafiti na taarifa mbalimbali zilionesha kwamba sekta isiyo rasmi ni ya kwanza kusababisha kupoteza mapato ya serikali, kushinda hata sekta ya madini. Hii itaongeza wigo wa kodi ya TRA ambayo sasa inasemekana kuwa chini ya milioni tatu TSH. Kwa hiyo, ni muhimu sana kurasimisha yote yasiyo rasmi na 20% ya yaliyokusanywa yaelekezwe kwenye elimu. 2. Vipaumbele katika kugharamia sekta ya elimu: Baraza kuhusu sera ya elimu lilikubaliana kwa kauli moja kwamba Serikali ya Tanzania haina budi kuwekeza zaidi katika sekta ya elimu - kama sekta nambari moja - na kutekeleza kikamilifu Sera ya Elimu bila Malipo ili kusawazisha fursa kielimu kwa watoto wote Tanzania. Kugharamia elimu zaidi kutokana na vyanzo vya ndani ya nchi, hivyo kutokana na mapendekezo hapo juu kunalenga pia kutokomeza ukosefu wa usawa Tanzania kwa kutumia fedha za elimu kwa watoto walio pembezoni - wakiwemo wasichana, watoto wenye mahitaji maalum na watoto nje ya shule - ili kuiwezesha Tanzania kutokomeza umaskini hivi karibuni na kupata jamii yenye usawa zaidi. Mgao maalum, mahsusi, uliotengwa na kuwekwa kwenye mfuko usioingilika

unahitajika ili kushughulikia ukosefu wa usawa na ujumuishi katika sekta ya elimu. 3. Uwazi na Uwajibikaji katika Utoaji wa Elimu: Kuweka vipaumbele vya kugharamika ndani ya sekta ya elimu - kama ilivyooneshwa hapo juu - kuambatane na kufuatilia utoaji halisi wa fedha na matumizi ya rasilimali kwenye ngazi ya wilaya na shule. Uanikaji hadharani wa utoaji wa fedha utawezesha wakala zenye mamlaka na asasi za kiraia kufuatilia matumizi na usimamizi wa fedha hizo. Ushiriki wa jamii katika elimu unaweza kuboreshwa iwapo Kamati za Usimamizi wa Shule zinaimarishwa ili kuwa sehemu ya kusimamia na kufuatilia matumizi ya ruzuku na pembejeo na rasilimali kwenye ngazi ya jumuiya ya shule. Baraza lilipongeza uamuzi wa serikali wa kuondoa watumishi hewa na hivyo kuandaa fursa za kuajiri walimu stahiki. Aidha baraza lilihimiza serikali kuendelea kupambana na ukwepaji wa kodi na ubadhirifu wa fedha za umma na kuelekeza fedha zote zinazookolewa kugharamia huduma za jamii, hasa elimu. 4. Mipango ya Jamii ndani ya Sekta ya Elimu Programu ya taifa ya lishe shuleni ipangwe upya ili kuongeza fedha za kuwalisha watoto ili kuhakikisha ubora na uthabiti wa chakula kinachotolewa na pia kuwa kiungo kati ya lishe ya watoto na sekta ya kilimo. Inapendekezwa kwamba mazao ya shamba yanunuliwe na serikali kutoka kwa wakulima na kutumika kuwalisha watoto. Hii itasaidia pia kuwamotisha wakulima kuzalisha zaidi na kupunguza umaskini unaoambatana na kilimo cha kijungujiko. Inapendekezwa kwamba ruzuku ya shule igawiwe kwa namna ya kupambana kikamilifu na ukosefu wa usawa katika sekta ya elimu. Kwanza itolewe ruzuku ya msingi (kwa mfano $1,000 kwa mwaka) kwa kila shule kila mwaka. Hatua ya pili iwe ni kupeleka shuleni ruzuku kwa kila mtoto ($10 kwa kila mtoto) (kila muhula) kuhakikisha kwamba wasimamizi wa shule wana rasilimali na uwezo wa kuitumia kwa unyumbufu kukabiliana na mahitaji mahsusi ya wasichana maskini (kwa mfano pedi za wasichana, sare, vitabu n.k.), watoto yatima, watoto wenye mahitaji maalum n.k. Hitimisho Baraza lilihitimisha kwa kusema kwamba vipaumbele na madai ya sera hapo juu ni mageuzi kwa elimu Tanzania katika muktadha ya mifumo ya elimu kitaifa na kidunia, vikiwemo SDG 4 na 5, Ajenda ya elimu 2030, Mkakati wa Elimu wa Bara la Afrika (CESA) n.k. Kwa kweli, iwapo mpango unafuatwa kwa umakini, Tanzania inaweza kuwa miongoni mwa nchi za kwanza za Afrika chini ya Sahara, si tu kufikia elimu jumuishi bora kwa wote lakini pia kutoa fursa zenye uhakika za mafunzo ya stadi na kujiajiri kwa ajili ya vijana wake.