HISTORIA, MAENDELEO NA MABADILIKO YA KATIBA TANZANIA TANGU UHURU HADI MIAKA HAMSINI YA UHURU 9 DESEMBA 2011.

Similar documents
GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

MAPENDEKEZO YA MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA TANZANIA

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Information for assessors (do not distribute this page to participants):

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

Kimesanifiwa na:- E.D.Kissuu ECOMM TANZANIA S.L.P ,Dar es Salaam. Simu:

Kutetea Haki za Binadamu

TAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF) KUHUSU HAKI ZA WATOTO KATIKA KATIBA MPYA

MWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI

Songa kwenye kilele cha upeo. Masuala ya Msingi na Ujuzi juu ya Uendeshaji wa Serikali za Mitaa

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara

MAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

Kubadili Sheria Za Mbegu Na Ulinzi Wa Aina Za Mbegu Na Mimea Nchini Tanzania

MIONGOZO MIWILI KUPAA NA KUTUNGULIWA KWA AZIMIO LA ARUSHA

Azimio lililopitishwa na Mkutano Mkuu tarehe 18 Desemba 2013 [juu ya taarifa ya Kamati ya Tatu (A/68/456/Add.2)]

KUHUSU AFRODAD. Dira ya AFRODAD. Dhamira ya AFRODAD. AFRODAD inalenga mchakato sawa na endelevu wa maendeleo kuelekea Afrika yenye mafanikio.

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA,KWA WANANCHI, 30 SEPTEMBA, 2001

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1

Human Rights Are Universal And Yet...

JAMHURI YA KENYA. Mkakati wa Ushirikiano MUKHTASARI FY Public Disclosure Authorized. Public Disclosure Authorized

MAADHIMISHO YA MIAKA 15 YA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

Elimukombozi, Lugha na Upashanaji Habari nchini Tanzania, katika Muktadha wa Utandawazi

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE

In the matter of an Application by the KIGOMA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (KUWASA) For a Tariff and Charges Adjustment

KAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI TANZANIA

JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI

Na Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake Toleola4

Kiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika

K. M a r k s, F. E n g e l s

ORDER NO BACKGROUND

Miradi na jamii. 3.1 Utangulizi

Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame M. Mbarawa (Mb.); Waheshimiwa Mawaziri na Wabunge wote mliohudhuria;

AZAKI PIGA KURA UCHAGUZI MKUU TANZANIA OKTOBA. #TanzaniaTuitakayo OKTOBA 2015 ILANI YA UCHAGUZI YA AZAKI TANZANIA.

Waandishi: wa Toleo la 5. Scholastica Jullu Athanasia A. Soka Safina Hassan Mary Njau. Toleo la 5: 2008 ISBN

Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara)

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig

HAKI NA TARATIBU ZA AJIRA, KAZI NA HIFADHI YA JAMII

SautiElimu. Sauti Yako Isikike

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

NGUO MPYA ZA UKOLONI. Mikataba ya Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Umoja wa Ulaya na Afrika. Agosti 2017

Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi

Je! imezingatia maslahi ya mkulima mdogo?

Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA 2006/07

KIJARIDA JUU YA HAKI ZA RAIA KATIKA MFUMO JINAI

Dibaji ya Mwenyekiti wa Kamati ya Pamoja ya Uongozi

MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA PRO-ROUTES. Ombi kwa ajili ya fedha za umma wa mradi wa ziada

Mhashamu Askofu Jude Thaddaeus Ruwa ichi, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania; Mwadhama Policarp Kardinali Pengo,

Dodoma ambako kikao cha Bunge kinaendelea kuja kushiriki japo sehemu ya uzinduzi wa mkutano.

RIPOTI YA WARSHA KUHUSU HABARI KWA AJILI YA UWAJIBIKAJI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA. Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo. TOLEO Na.

5. Mheshimiwa Spika, Bunge lako Tukufu lilijadili kwa kina Miswada ifuatayo:

Kitabu Cha Mafunzo Ya Uongozi Kwa Wanawake

RIPOTI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI

Usimulizi wa Riwaya ya Nyongo Mkalia Ini E. S. MOHOCHI University of Egerton, Kenya

Kuuelewa Mchakato wa Bajeti Tanzania Mwongozo wa Asasi za Kiraia

KUSHUKA KWA HADHI YA LUGHA ZA JAMII NCHINI TANZANIA YOHANA P. MSANJILA University of Dar es Salaam, Tanzania

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU

LUGHA YA KISWAHILI KATIKA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA ELIMU SHULE ZA SEKONDARI

Shabaha ya Mazungumzo haya

Ellen White, waasisi wa Kiadventista,na Sabato Lunar

RIPOTI YA KAMATI TEULE YA KUCHUNGUZA UPOTEVU WA NYARAKA ULIOTOKEA KATIKA TAASISI YA NYARAKA NA KUMBUKUMBU ZA TAIFA ZANZIBAR.

TANZANIA TAARIFA YA MWISHO WA UTEKELEZAJI

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Spika,

ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA UCHUMI WA ZANZIBAR

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA MHESHIMIWA DKT

Elimu Ina Umuhimu gani katika Jamii? Kuelekea Elimu Sahihi

TAARIFA YA MWAKA YA UTENDAJI KAZI IDARA YA UTAWALA BORA 2013/2014

Pronunciation: Mä-hret Zäläke Ndal-ka-tscho Molla Mare Gebre-gzabiär 1/12

TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM)

Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2013

KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU

ORODHA YA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI SPIKA MHE. PANDU AMEIR KIFICHO. Rais.

wasiofaa. Naomba sana kila raia afanye bidii awezavyo kumkaribia Mwenyezi Mungu vile anavyoona inafaa, lakini asipitishe hukumu juu ya wengine.

MTIHANI WA MWIGO WILAYA YA BUTERE MUMIAS-2007 Hati ya kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya

KUCHUNGUZA MASUALA YA KISIASA KATIKA RIWAYA ZA SHAABAN ROBERT: MFANO WA KUSADIKIKA NA KUFIKIRIKA

KISWAHILI KARATASI YA 2 LUGHA

UNABII WA BIBLIA. CBM Publishing 32 Blenheim Road, Far Cotton Northampton, England. NN4 8NW

Mwongozo wa Utamaduni Toleo la Kwanza

Mukhtasari Wa Mabishano Kwa Na Dhidi Ya Vikombe Vingi Vya Ushirika

Mwongozo wa Kutathimini mifumo ya Ugawanaji wa faida na Mapato Katika Miradi ya Jamii ya MKUHUMI

Summaries of GC Reports 2012, Vol. 2, Sec. 1, Swahili

KITEGO CHA MAREKEBISHO NA HAKI ZA MTOTO

Ripoti hii ni kwa heshima ya wale wanaharakati wengi wa Tanzania ambao ndio binafsi wanaopitia hali iliyoangaziwa, na vilevile wale walioyapoteza

Kufanya Uwekezaji kuwa wa Manufaa kwa Afrika: Jibu la Mbunge kuhusu Unyakuzi wa Ardhi

Tora UTANGULIZI KWA TORA SOMO LA KWANZA

BUNGE LA TANZANIA MKUTANO WA NANE. Kikao cha Ishirini na Nane Tarehe 16 Julai, (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A

MUNGU ANADHIHIRISHWA KUPITIA KWA YESU KRISTO.

3 FEBRUARI, 2015 BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA NANE. Kikao cha Saba - Tarehe 3 Februari, 2015

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA SABA. Kikao cha Thelathini na Tisa Tarehe 1 Juni, (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A

Unyanyasaji wa Watoto & Kutelekezwa

Mwongozo wa Kanisa la Waadventista wa Sabato

Uzio wa pilipili unazuia tembo kuvamia mazao shambani! Jinsi ya kujenga na kudumisha uzio wa pilipili Tanzania

Transcription:

Saint Augustine University of Tanzania From the SelectedWorks of Daudi Mwita Nyamaka Mr. Winter December 9, 2011 HISTORIA, MAENDELEO NA MABADILIKO YA KATIBA TANZANIA TANGU UHURU HADI MIAKA HAMSINI YA UHURU 9 DESEMBA 2011. Daudi Mwita Nyamaka, Mr. Available at: https://works.bepress.com/dmnyamaka/2/

HISTORIA, MAENDELEO NA MABADILIKO YA KATIBA TANZANIA TANGU UHURU HADI MIAKA HAMSINI YA UHURU 9 DESEMBA 2011. Mada kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Tanzania Bara (Tanganyika) yaliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Kanda ya Ziwa na Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino cha Mwanza na Kufanyika katika ukumbi wa M13 SAUT tarehe 9 Dec 2011. Daudi Mwita Nyamaka-Mhadhiri Msaidizi SAUT, Mtafiti na Mchambuzi mambo ya Kikatiba. 1. UTANGULIZI Dunia ya leo imejikita zaidi katika demokrasia. Demokrasia kwa ufupi ni dhana inayolenga ushiriki wa wananchi katika kuweka misingi sahihi ya uendeshaji wa nchi wenyewe wao wakiwa ndio msingi wa mamlaka yote ya nchi na walio na uwezo wa mwisho wa kuipa serikali madaraka na mamlaka yake. Ushiriki wao huwa aidha wa moja kwa moja au wa uwakilishi. 1 Moja ya misingi mikuu inayolenga kukuza demokrasia ya namna hii ni Katiba ya Nchi. Katiba ni msingi mkuu wa uendeshji wa nchi, ukuaji wa demokrasia na utawala wa sheria. Yenyewe ndiyo sheria kuu na ambayo kwayo sheria zote nyinginezo hupata uhalali na hufungamana. 2 Katiba kama utaratibu muafaka wa jamii husika huweka bayana misingi ya utawala, vyombo vya utawala, na mgawanyo wa madaraka baina ya vyombo vikuu vya dola- yaani Bunge, Mahakama na Serikali (Watendaji wakuu) Kubwa zaidi, Katiba ndiyo inayoainisha nafasi waliyonayo wananchi katika kuweka utaratibu wa kuendesha nchi yao. 3 Kwa muda mrefu sasa, hasa baada ya mabadiliko ya sera za kiuchumi na kuanguka kwa mfumo wa chama kimoja na kuingia katika mfumo wa vyama vingi, umma wa Wa-tanzania umeghubikwa na hoja mbalimbali za msingi sana kuhusu mustakabali wa taifa letu la Tanzania. Moja ya hoja ambazo zimekamata sana fikra za 1 Taz. Ibara ya 1 ya Katiba ya Jamhuri ya Watu wa Kenya, 2010. 2 Taz. Ibara ya 2 (1-4), Ibid. 3 Taz. Ibara ya 105 Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 na Ibara 39 Katiba ya Zanzibari 1984 utaona mkanganyiko na hivyo kushindwa kuelewa ni ipi Katiba yenye nguvu kati hizi mbili. 1

wengi katika umma wa Watanzania ni suala la kuwepo kwa Katiba Mpya. Makongamano na warsha mbalimbali zimeitishwa kuijadili Katiba na madai mbalimbali yametolewa yakikosoa muundo wa Katiba iliyopo Tanzania, kulingana na mazingira tuliyonayo na hivyo kudai kuitishwa kwa kongamano la kikatiba nchini ili kuunda Katiba Mpya, na matunda yake imekuwa ni kutungwa kwa Sheria ya Marekebisho ya Katiba 2011 ambayo hata hivyo inalalamikiwa sana kwa kutungwa bila kuwapa watanzania nafasi ya kushiriki na pia kumrundikia Rais madaraka yote bila hata kuwashirikisha wapiga kura wake. 4 Ni jambo lisiloshaka kwamba, katika jamii tuliyo nayo hivi leo demokrasia na utawala wa kidemokrasia ni moja ya dhana muhimu sana zinazoleta mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi yoyote. Demokrasia na utawala wa kidemokrasia sio tu vichochezi vya maendeleo bali ni mihimili mikubwa ya kupambana na umaskini hasa katika nchi kama Tanzania na nyinginezo. Pasipokuwepo na demokrasia na utawala unaojali demokrasia na kanuni ambatanishi kama vile utawala wa sheria, heshima kwa haki za binadamu na utawala bora, uwezekano wa kupambana na umaskini na ufukara ni ndoto sana. Taifa lolote lisilojali demokrasia ya dhati huanguka ama hubaki maskini na tegemezi kwa vile huwa limeua fursa muhimu mbadala ambazo kama zingepewa nafasi, zingeleta matokeo chanya katika maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii. Maadili huporomoka katika jamii na uzalendo husikika tu kama hadithi miongoni mwa watu. Ubinafsi hutawala na hapo ndipo unaposikia chukua chako mapema, ama hata kwa wale wengine wanaopigana kwa hoja kuelekea Ikulu wanapopewa fursa tu ya kuteua wanachama wao kuwa wabunge viti maalumu huishia kuteuwa wapendwa wao, ama kweli tumethubutu, tumeweza na tunasonga mbele. Ili Taifa libadilike kiuchumi, kisiasa na kijamii ni lazima watu washirikishwe kikamilifu katika kuandaa mazingira ya mabadiliko hayo na hasa ushirikishwaji katika kuweka misingi imara ya mabadiliko yenye manufaa na yanayolenga mbali na upeo wa leo. Ushirikishwaji sahihi wa umma katika kuweka misingi ya kuiendesha jamii ndicho chanzo pekee cha kuimarisha demokrasia ya 4 Taz. Sehemu ya Tatu ambapo Rais anapewa mamlaka ya kuunda Tume kuchagua wanatume na kuwaandalia hadidu za rejea. Lakin ingekuwa busara kuwapa wananchi nafasi ya ya kuchagua wanatume kadhaa na kumpa Rais kuwathibitisha miongoni mwao na hata hadidu za rejea wapewe mamlaka watu wa Tume waaandae wenyewe. 2

kweli na kijito cha haki, uhuru na usawa katika jamii. Katika hali hiyo, ndipo dhana ya kuwa mamlaka yote iko kwa umma na kwamba serikali itapata mamlaka yake toka kwa huo umma huleta maana. 5 Ni hakika na dhahiri sikuzote kuwa, Wananchi ndio wenye nchi. Hata hivyo, kama misingi ya wananchi kuwa na nchi haikutokana na ridhaa yao, mara zote msemo huo hubadilika na kuwa watawala ndio wenye nchi na wala nchi na wananchi sio wenye nchi na wala si wala nchi. 6 Ili wananchi wawe ndio wenye nchi na wenye mamlaka ya mwisho juu ya mustakabali wa mambo yahusuyo nchi na rasilimali zake, utashi wa kisiasa na uchumi, basi ni lazima uwepo mfumo imara uliotokana na ridhaa yao na unaoweka bayana kanuni na taratibu za msingi na za kidemokrasia kuhusu hatima au mustakabali wa taifa lao na maendeleo yao kwa ujumla. Msingi huo mkuu wa mfumo huo muafaka si mwingine bali ni Katiba ya nchi. Kukosekana kwa katiba yenye ridhaa halisi ndicho chanzo kikubwa cha kuparanganyika kwa jamii na kudumaa kwa maendeleo na ustawi wao hasa katika nchi nyingi za dunia ya tatu na hasa Afrika. Tukitii misingi hii ya ushirikishwaji na kujenga maadili katika jamii, basi ndipo twaweza kujinadi kwa kauli mbiu tumethubutu, tumeweza na tunasonga mbele. Kwa nini basi yahitajiwa Katiba madhubuti katika nchi? Kwa uchache, ziko sababu takribani nne ambazo twaweza kuzibainisha hapa kwa nini Katiba yoyote ya nchi lazima iwe madhubuti na imara. Hata hivyo, umadhubuti wa Katiba hutokana na ridhaa ya wananchi yaani yenyewe lazima itokane na matakwa yao. Sababu ya kwanza ni kwamba Katiba itokanayo na umma hutoa uthibitisho na uhakikisho kwa umma kuwa, sura na utaratibu wa uundwaji wa serikali utatokana na namna au utaratibu ule ambao wao (umma) wameukubali na kuridhia kitaifa yaani Katiba. Katiba ndiyo inayoweka bayana mihimili ya utawala wa dola na kwamba mihimili hiyo hujitegemea yenyewe. 7 5 Taz. Ibara ya 8 ya Katiba ya Tanzania, 1977. Taz See also, Makaramba, (op. cit. note 1at p. x. 6 Taz. Nyamaka, D. Mwita, Social Contract Theory of John Locke (1632-1704), in the Contemporary World; SAUT LAW JOURNAL, VOL 1 NO 1 2011, PP 49-60 7 Taz. Ibara ya 3 ya Katiba ya Jamhuri ya Watu wa Kenya, Serikali yoyote itakayo ingia madarakani kinyume na misingin ya Katiba ni batili. Kununua kura, kuiba kura na mengine vyote ni ubatili mtupu na ulaghai kwa wananchi. 3

Pili, uwepo wa katiba madhubuti itokanayo na umma ni kiashiria kwa wananchi kuwa utawala wa sheria na heshima kwa binadamu na misingi yote ya haki italindwa na kuhifadhiwa ndani ya Katiba na kwa mujibu wa Katiba hiyo serikali itatekeleza wajibu wake. Kwa hali hiyo, ni mwiko kwa serikali kutumia madaraka yake isivyo halali na au kwa mabavu na pia haitaweza kamwe kufanya maamuzi kandamizi au kutunga sheria au sera yoyote kandamizi na inayokiuka misingi ya haki kama ilivyobainishwa ndani ya Katiba. Kufanya hivyo kutakuwa kukiuka matakwa ya wananchi (umma) ambao kwao mamlaka ya mwisho ya utawala wa nchi hukaa. Tatu, Kama sheria mama (grundnorm or the basic law) Katiba iliyo madhubuti hutoa hakikisho kwa umma kwamba, sheria zote, maelekezo yote yenye nguvu ya kisheria na kiutawala, sera zote na kanuni zozote zile, lazima zifungamane na kupata uhalali wake kutokana na Katiba waliyoiridhia wananchi wenyewe. 8 Kwa hali hiyo Katiba hutoa hakikisho la jamii huru na vilevile huihakikishia jamii hiyo uhuru, uwiano na fursa sawa katika shughuli zozote zile, ziwe za kiuchumi, kijamii au kisiasa. Hivyo, Katiba huweka mazingira yenye kanuni na taratibu sawia kuhusu ukuaji na ustawi wa jamii husika. Taratibu kama za uchaguzi huru na wa haki unaojali uwazi na unaotoa mwanya wa asiyeridhika kuwasilisha hoja zake mbele ya chombo huru cha utoaji haki (yaani mahakama) bila kikwazo chochote au gharama kubwa, ni sehemu muhimu ya Katiba iliyo madhubuti. 9 Nne, Katiba iliyo madhubuti huwa ni msingi mkubwa wa utawala bora, na unao zingatia uwazi, uwajibikaji na utawala wa sheria, dhana ambazo kwa pamoja ni misingi mikubwa ya demokrasia na maendeleo ya nchi. 10 Kwa sababu hizo, uwepo wa Katiba madhubuti itokanayo na ridhaa ya wananchi wote na inayotoa uhakikisho wa mazingira ya uwanja wenye uwiano sawa 8 Taz. Ibara ya 2 (4) Katiba ya Jamhuri ya Watu wa Kenya 2010 na Ibara 64 (5) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 4 Katiba ya Zanzibari, 1984, Ibara ya 2 Katiba ya Ghana, sehemu ya kwanza Katiba ya Uganda Ibara 2. 9 Katiba iliyo madhubuti na imara hutokana na watu wenyewe. Taz. Nyamaka, D. Mwita, Processes and Institutions of Constitution-making with Refernce to Tanzania; SAUT LAW JOURNAL VOL 1 NO 2, 2011. 10 Tazama kitabu kilichoandikwa na John Hatchard, Muna Ndulo & Peter Slinn, Comparative Constitutionalism and Good Governance in the Commonwealth: An Eastern and Southern African Perspective - (Frontmatter)- Available from http://assets.cambridge.org/97805215/84647/frontmatter/9780521584647_frontmatter.pdf (As accessed on 31 st July 2008). 4

na wa ushindani, ni hatua muhimu sana katika ukuaji wa demokrasia ya kweli hasa katika zama hizi za mfumo wa vyama vingi Tanzania. Tunaposherehekea miaka hamsini ya uhuru wa Tanzania Bara hatuna budi kuitazama historia ya Katiba, tulivyoanza toka mikononi mwa wakoloni, tulipo tunapoelekea na sababu sababishi kwa Katiba mbalimbali katika vipindi tofauti toka uhuru mpaka sasa. 2 HISTORIA NA MFULULIZO WA MATUKIO MBALIMBALI YALIYOPELEKEA KUUNDWA KWA KATIBA NCHINI TANZANIA TANGU UHURU HADI SASA Ni jambo murua kuweka bayana kwamba, maendeleo ya kikatiba katika nchi ya Tanzania yametokana na mabadiliko mbalimbali yaliyokuwa yakitokea katika nchi, na hivyo kusababisha kuundwa (enactment) au kurekebishwa (amendment) kwa muundo wa Katiba katika wakati husika. Vipo, kwa uchache, vipindi vikuu vitano vilivyoambatana na kuundwa kwa katiba mpya kabisa nchini na vipindi kumi na nne vya kufanyia tu marekebisho Katiba iliyopo.leo tunapoadhimisha miaka hamsini ya uhuru wa Tanganyika tupo katika kipindi cha sita kuelekea kuunda Katiba mpya. Vipindi hivi vya kihistoria viliashiria mabadiliko ya msingi na ya kina sana ya muundo wa katiba ya nchi kwa vile mabadiliko hayo, yaliingia chini na ndani kabisa ya mizizi ya Taifa na mustakabali wake. Matukio ya msingi yaliyopelekea kuwepo kwa mazingira yaliyohitaji mabadiliko ya kikatiba na hivyo kujenga vipindi hivyo vya kihistoria ni kama yanavyoelezwa hapa chini: i) Katiba ya Tanganyika 1961 Kupatikana kwa Uhuru wa Tanganyika -1961-1962. Tunapoizungmzia Katiba hii hatuna budi kukumbuka Azimio la Tabora (Busara) 1958 ambapo wazalendo watanganyika walimuunga mkono Mwalimu Nyerere kutumia busara na si nguvu kudai Uhuru wa Tanganyika. Historia inatuambia wakoloni walimshitaki Mwalimu Nyerere kwa kile walichokiita kuwa ni Uchochezi na kutakiwa kulipa faini shilingi elfu tatu ama kenda jela miezi sita, lakini wazalendo walichanga na kumnusuru Mwalimu Nyerere kwenda jela, mbio na harakati za busara zikasonga mbele hata kuleta uhuru tarehe 9 Disemba 1961. Tukio hili la uhuru 5

wa Tanganyika liliweka mazingira ya kipindi cha mpito kutokana na mabadiliko ya kiutawala toka kwa Wakoloni Waingereza kwenda kwa Wazalendo wa Tanganyika hasa kupitia tamko rasmi la serikali ya kikoloni -Tanganyika Constitution Order in Council of 1960 11, ambalo ndilo lililoidhinisha kuwepo kwa serikali huru ya Tanganyika na Katiba yake (the Independence Constitution) 12 mnamo mwezi Disemba, 1961.Kwa jinsi hiyo, kupatikana kwa uhuru wa Tanganyika mwaka 1961 kulileta fursa ya kipekee ya mabadiliko ya baadae ya katiba, hasa kutokana na ulazima wa kuweka mambo na hatima ya Taifa huru la Tanganyika chini ya utawala huru wa Watanganyika. Hata hivyo, umuhimu wa mabadiliko ya kikatiba baada ya uhuru haukuwa umefichika. Kwa wakati ule, katiba iliyoleta uhuru (yaani the Independence Constitution) 13 ilikuwa na muundo uliofuata mfumo wa Kiingereza (Westminster). Katika mfumo huu Malkia wa Uingereza (au mfalme) bado anabakia mtawala ila si mtendaji mkuu. Waziri mkuu ndiye anayeunda serikali na kuwa mtendaji mkuu. Kwa hali hiyo Tanganyika ilikuwa bado na kivuli cha Malkia kwa mbali. Kwa upande wa siasa za vyama, kimsingi, katiba hii ya kwanza ya Tanganyika ilikuwa ni ya vyama vingi. Hata hivyo, kwa vile Katiba hii ilitengenezwa na kupewa Tanganyika chini ya Serikali ya Malkia wa Uingereza enzi hizo, wataalamu wa mambo ya katiba wanatanabaisha kwamba, katiba hii, ilikuwa ni ya namna tu ya kuleta makubaliano au maridhiano kati ya wakoloni na wazalendo wa Kitanganyika lengo hasa likiwa ni kutoa hakikisho la kuwepo dola huru la Tanganyika. 14 Chini ya Katiba hii ya uhuru, dhana kubwa ya bunge kuwa chombo chenye mamlaka ya juu (supremacy of the parliament) ilijikita ndani yake pamoja na ile ya kuhakikisha kuwepo kwa uhuru wa mahakama (independence of the judiciary.) 15 Uwepo wa dhana hizi muhimu katika katiba ya uhuru lilikuwa jambo lisiloepukika hasa kutokana na msisimko mkubwa 11 Taz. Government Notice No. 415 of 1/12/61. 12 Taz. S.I. 1961, No. 2274 13 ibid 14 Taz. Fimbo, G.M. Towards Separation of Powers in a New Democracy : Tanzania, (1995) 22 (1&2) The African Review, pp.16-31 15 Taz Makaramba, (op. cit. note 1) 6

ambao wapigania uhuru walikuwa nao na hivyo serikali ya kikoloni isingependa kuona mabadiliko yatakayo leta madhara hasa kwa maslahi yao baada ya uhuru. Maslahi yoyote yanalindwa dhidi ya ukandamizi wa serikali kama bunge na mahakama zikiwa huru na zikitenda kazi zake ipasavyo. Hivyo serikali ya kikoloni ililiona jambo hilo na kuliweka ndani ya katiba hata kama wao hawakuwatendea hivyo Watanganyika kipindi cha ukoloni. ii) Katiba ya Jamhuri ya Tanganyika 1962 Kipindi cha pili kilicholeta mazingira mbadala yaliyohitaji mabadiliko ya katiba Tanzania (Tanganyika) kilikuja mwaka 1962. Mwaka mmoja tu baada ya uhuru kulitokea mabadiliko ya msingi sana ya kiserikali na utawala kwa ujumla. Tanganyika ilikuwa Jamhuri inayojitawala yenyewe na hivyo kuondokana na mfumo wa Katiba yenye mfumo wa kikoloni (Westminister). Badala ya kuendelea kuwa na Malkia pamoja na Waziri mkuu (ambaye ndiye mtendaji mkuu na kiongozi wa serikali), Tanganyika iliachana na mfumo huo na kuamua kujiingiza katika mfumo wa U-rais, huku rais akiwa ndiye mkuu wa nchi na mwenye madaraka ya kuteua serikali na vyombo vinginevyo. Hivyo, kunako mwaka 1962, Tanganyika ilibadilisha Katiba ya kwanza na kuunda Katiba mpya ya Jamhuri ya Tanganyika (The Republican Constitution, 1962). 16 Kwa hali hiyo, Malkia wa Uingereza hakuwa tena na fursa ya kuongoza dola huru la Tanganyika kupitia mlango wa nyuma. Yamkini kubadili katiba ilikuwa ni moja ya njia za kuudhihirishia ulimwengu kuwa Tanganyika huru yapaswa na yaweza kujitawala yenyewe. Hivyo tangu mwaka 1962, Tanganyika ikawa inafuata mfumo wa utawala wa U-rais, Rais akiwa amechaguliwa na umma. Ni muhimu pia kuweka bayana kwamba, kuundwa kwa katiba mpya ya Jamhuri Tanganyika mwaka 1962 kulikuwa ni mwanzo wa kulimbikiza madaraka mengi kwa rais wa Jamhuri. Kwa mfano, licha ya kuwa mkuu wa nchi, rais ndiye aliyekuwa mkuu wa serikali na ndiye aliyeunda serikali. Ndiye aliyekuwa amiri jeshi mkuu, mteua mawaziri 16 Ibid. Tazama pia McAuslan, W.B., The Republican Constitution of Tanganyika, (1964) 13 International & Comparative Law Quarterly, 502-573 7

pamoja na wakuu wengine wa ngazi ya juu serikalini. Kulingana na msomi mmoja wa mambo ya Katiba, Profesa Okoth-Ogendo, kwa nchi nyingi za kiafrika, mara baada ya uhuru hali iligeuka na mazingira yote yakageuka kuelekea uanzishwaji wa dola la ki-rais ( imperial presidency ). 17 Ni muhimu pia tuweke bayana kwamba utaratibu mzima wa kuibadilisha Katiba ya Uhuru na kuanzisha katiba mpya ya Jamhuri ya Tanganyika haikufuata taratibu za kikawaida za kuunda katiba yaani ushirikishi wa umma. Hakukuwepo na mkutano au kongamano la katiba. Kilichofanyika ni kwamba, Bunge ndilo lililotumiwa hasa baada ya kujivika kilemba cha Bunge la Katiba (a constituent Assembly) 18 na hivyo kupitia mbinu hii likajipatia mamlaka ya kutunga Katiba mpya ya Jamhuri ya Tanganyika. 19 Wabunge 71 wa TANU walijigeuza na kuwa bunge maalumu la kutunga Katiba, na hivyo wananchi wa kawaida hawakushirikishwa moja kwa moja. iii) Katiba ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibari 1964 Jambo la tatu lililopelekea kipindi kingine muhimu cha mabadiliko ya hali ya kisiasa na kiutawala na ambayo yaliathiri mfumo mzima na hata katiba ya nchi ni Muungano wa Jamhuri ya watu wa Tanganyika na ile ya watu wa Zanzibar mwaka 1964. 20 Mnamo mwaka 1963 Zanzibar ilipata uhuru toka kwa mwingereza lakini bado Sultani alibaki kuwa mtawala na hivyo kupelekea mapinduzi ya kuuondoa utawala wa Sultani Zanzibari. Mara baada ya mapinduzi hapakuwa tena na Katiba Zanzibari badala yake nchi iliongozwa kwa Amri za Rais (Presidential Decrees). 21 Kwa utashi wa viongozi wa Tanganyika na Zanzibari na kwa masilahi ya mataifa haya mawili hasa ulinzi, inavyosemekena, ilionekana ni muhimu 17 Taz. Okoth-Ogendo, H.W.O Constitutions Without Constitutionalism: Reflections on an African Political Paradox in Shivji, I.G., (ed.) State and Constitutionalism: An African Debate on Democracy, Human Rights & Constitutionalism Series, No.1, Southern African Political Economy Series (SAPES) Trust, Harare, Zimbabwe, 1991. 18 Tazama Sheria ya Bunge la Katiba Namba 66 ya Mwaka 1962 19 Taz. Makaramba, (op. cit note 1) 20 Taz. Sheria Namba 22 ya Mwaka 1964 (the Union of Zanzibar and Tanganyika Law, 1964) 21 Tanz. Nyamaka, D. Mwita, Processes and Institutions of Constitution-making with Refernce to Tanzania, op cit. 8

kuungana na kuwa nchi moja. Muungano huu ulipelekea kufanyiwa marekebisho makubwa Katiba iliyokuwepo Tanganyika (yaani ile ya 1962) na kupatikana kwa kile kinachojulikana kama sheria ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (the Acts of the Union, 1964 22 ) ambayo imejumuisha pia jedwali la mkataba wa Muungano au kwa lugha nyingine (Articles of Union). Kulingana maoni ya wataalam na wazamivu wa sheria jedwali hili lina nguvu ya kikatiba. 23 Sehemu ya VII ya mkataba huu wa Tanganyika na Zanzibar, na ambao uliridhiwa na mabunge ya pande zote mbili, ilimtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, akiisha kubaliana na Makamu wa Rais katika jambo hilo la kuunganisha nchi hizi husika, kufanya mambo mawili makubwa na ya muhimu sana. Mambo hayo yalikuwa:- I) Kuteua Tume ya Katiba (Constitutional Commission) ambayo itakuwa na jukumu la kutoa mapendekezo ya muundo wa katiba mpya ya Jamhuri ya muungano na; II) Kuitisha Bunge la Katiba (a Constituent Assembly) litakalokuwa na wawakilishi toka pande zote mbili za Muungano na ambao watakutana ndani ya mwaka mmoja wa kuanza kwa muungano, ili kujadili mapendekezo husika na kuipitisha Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano. Hii ilitazamiwa kuwa katiba ya muda ambayo iliweka utaratibu wa kuandaa Katiba ya kudumu kwa kuunda tume kuhakikisha ushiriki wa wananchi unakuwepo. Tume hii ilikuwa chini mheshimiwa Rashidi Mfaume Kawawa. Hata hivyo, kipindi hiki mahususi cha uteuzi wa Tume ndani ya mwaka mmoja kama kilivyo elezwa katika sehemu ya VII ya mkataba wa Muungano (Articles of Union) kilifanyiwa marekebisho mwaka 1965 kufuatia sheria ya Bunge la Katiba 24 na 22 Namba. 22 ya mwaka 1964 23 See Shivji, I.G. The Legal Foundation of the Union in Tanzania s Union and Zanzibar Constitutions, Professorial inaugural Lecture, DUP, Dar-es-Salaam, 1990. See also Kabudi, P.J.A.M., International Law Examination of the Union of Tanganyika and Zanzibar: A Federal or Unitary State? L.L.M. Dissertation, University of Dar-es-Salaam (1986) (mimeo) See also section 1 of the the Constituent Assembly Act, 1965, Act. No. 18 of 1965 24 Taz. Kifungu cha 2 cha sheria ya Bunge la Katiba (the Constituent Assembly Act), 1965, Act. Namba 18 of 1965 9

kumfanya Rais, akiwa amekubaliana na Makamu wake ambaye ndiye Rais wa Zanzibar, ateue Tume na kuitisha Bunge la Katiba pale anapoona ni wakati muafaka. Kwa kuzingatia utaratibu huu uliooneshwa hapo juu, ni dhahiri kuwa, mchakato mzima wa kuipata katiba hata kipindi hiki cha Muungano bado haukufuata misingi ile halisi ya ushirikishwaji umma, jambo ambalo limerithiwa mpaka leo. Kwa mfano, badala ya kuitishwa kwa mkutano wa, au Kongamano la Katiba (a constitutional conference), hekima ya wakati ule ilielekeza Rais wa Muungano avishwe madaraka ya kuteua Tume ya Katiba itakayoleta mapendekezo mezani na aitishe Bunge la Katiba litakalo yapitia na kutunga Katiba ya Muungano. Hata hivyo sharti lilitaka amshirikishe makamu wake ambaye alikuwa Rais wa Zanzibar. Ili kuyafungamanisha haya yote sawa sawa na Mkataba wa Muungano (the Acts of the Union), iliyokuwa Katiba ya Tangnyika ya mwaka 1962 ilibadilishwa na kuitwa katiba ya muda (the Interim Constitution of the United Republic of Tanganyika and Zanzibar, 1964). 25 Jina la dola mpya nalo lilibadilishwa mara baada ya Muungano na kuitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 26 Katiba hii ilianzishwa kwa tamko la Rais na kuridhiwa na bunge la Tanganyika na Baraza la Wawakilishi Zanzibari. iv) Katiba ya Muda 1965 Baada ya kupitishwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na Katiba ya Tanganyika kufanyiwa marekebisho kukidhi haja ya sura mpya ya dola, mnamo mwaka 1965 Katiba ya Muda ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (The Interim Constitution of Tanzania) ilipitishwa. 27 Kupitishwa kwa Katiba hii ya mpito ya mwaka 1965 kulileta sura mpya ya mambo katika siasa za Tanzania. Kwanza, Katiba hii ambayo ilipitishwa na Bunge la Katiba, ilileta mabadiliko ya kipekee katika nyanja ya siasa za nchi na uendeshwaji wa shughuli zote za kisiasa Tanzania, nchi ambayo ndiyo kwanza tu ilikuwa ikilea mfumo mchanga wa demokrasia ya vyama vingi. Pili, mabadiliko haya ya kipekee yalilenga kusimika mfumo tofauti kabisa wa kisiasa na 25 Tz. Sheria No. 22 ya 1964; pia taz. Makaramba, (op. cit. note 1) 26 Tz. Sheria Namba 61 ya mwaka 1964 27 Tz. Sheria Namba 43 ya Mwaka 1965 kama ilivyorekebshwa na sheria Namba 21 na Namba 45 zote za mwaka 1965 10

kiuchumi Tanzania, kinyume na matarajio ya awali kipindi cha mwanzoni cha uhuru. Kwa mujibu wa Katiba hii ya mpito ya mwaka 1965, na kwa mara ya kwanza kabisa katika historia ya Tanzania huru, vyama vyote vya siasa isipokuwa tu vile vilivyokuwa madarakani Tanzania Bara yaani (Tanganyika African National Union (TANU)) na Tanzania Visiwani (Afro-Shirazi Party (ASP)) vilisitishwa. Lengo hasa lilikuwa kuleta mfumo wa chama kimoja katika Jamhuri nzima ya Muungano wa Tanzania, azma ambayo waasisi wa Taifa la Tanganyika na Chama cha TANU walikuwa nayo tangu mwaka 1962. Kwa mtindo huo, bila kujadili mabadiliko mengineyo kama yale ya kuanzishwa kwa Azimio la Arusha na Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea mwaka 1967, mnamo mwaka ule wa 1975, Vyama vya TANU na ASP vilijikita ndani ya Katiba kwa mstari wa mbele na mamlaka yote. Dhana ya bunge kushika hatamu ya juu (supremay of parliarment) iligeuzwa na kumezwa na dhana mpya ya Chama kushika hatamu (party supremacy). 28 Kwa hali hiyo, vyombo vinginevyo vyovyote viliwajibika kwa chama tawala na matakwa yake. Katiba hii ilitokana na mchakato wa tume ya Rais ya Katiba iliyokusanya maoni kwa baadhi ya wananchi. Katiba hii ilitamka bayana chama kushika hatamu ya uongozi na nchi ambapo halmshauri kuu ya TANU (NEC) ikawa na nguvu kuliko bunge na hata katiba yenyewe. Lakini pia mambo ya muungano yakaanza kuongezeka na uhuru (autonomy) ya serikali ya Zanzibar ukaghubikwa na utata na kuwa moja ya kero za muungano hata leo. v) Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 Kuunganika kwa Chama cha TANU na ASP mwaka 1977 tarehe 5 ya mwezi Februari na kuzaliwa chama kipya cha CCM (Chama Cha Mapinduzi), hili lilikuwa tukio jingine la kipekee sana lililokamilisha ustadi wa wakongwe wa siasa za Tanzania na ambalo liliweka mazingira mapya ya kisiasa na kiuchumi yaliyohitaji Katiba mpya. Hivyo mnamo mwaka huo wa 1977, 28 Taz. Kifungu cha 3(3) na (4) cha sheria Namba 8 ya Mwaka 1975 11

miaka 12 baada ya kupitishwa kwa Katiba ya Muda ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1965, ilipitishwa katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 ambayo ndiyo iliyopo hadi sasa, japo imeshafanyiwa marekebisho ya msingi kumi na nne mpaka leo tunapoadhimisha miaka hamsini ya uhuru wa Tanzania Bara. Ndani ya Katiba hii, mtizamo na sura ya kisiasa iliyokuwa imejengwa kwa miaka 12 na Katiba ile ya muda ya mwaka 1965 uliendelezwa na chama kipya cha Mapinduzi (CCM) kilijikuta kama chama pekee na kilichoshika hatamu Tanzania Bara na Visiwani. Katiba hii ilipatikana kutokana na tume ya Rais iliyokuwa na wajumbe 20, kwa idadi sawa toka pande zote za muungano ikiongozwa na Sheikh Thabit Kombo akisaidiwa na Pius Msekwa kama katibu wa tume hii ya Rais. Hata hivyo tume hii ni ileile iliyotunga katiba ya CCM. Katiba hii ilipitishwa ndani ya masaa matatu na bunge maalumu lililoteuliwa na Rais kutokana na bunge la kawaida. Pamoja na kupatikana kwa Katiba yenye chama kimoja tu Bara na Visiwani, tabia ile iliyorithiwa tangu mwanzo wa mabadiliko ya Katiba miaka ya nyuma haikufichwa bali iliwekewa mazingira mazuri zaidi na yaliyowaondoa wengi katika ushiriki. Kwa wakati huo, kwa mfano, Kamati ya Chama ambayo ilikuwa imehusika katika jukumu la kuandaa na kuwasilisha mapendekezo ya kuwepo kwa Chama kimoja tu kwa pande zote za Muungano ndiyo iliyogeuzwa kwa maagizo ya Kamati Kuu ya Chama (National Executive Committee (NEC)) kufanyika kuwa Tume ya Katiba (Constitutional Commission) na kutakiwa kuandaa na kuwasilisha mapendekezo ya Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ripoti ya mapendekezo hayo yaliwasilishwa kwa Kamati Kuu ya Chama (NEC) na sio Bunge kwa vile chama ndicho kilicho kuwa na maamuzi ya mwisho. Ndipo baadae, NEC ikaliagiza baraza la mawaziri (cabinet) kuandaa rasimu ya muswada ambao ungewasilishwa kwa Bunge la Katiba (constituent assembly) kuhusu kutungwa kwa Katiba Mpya. Muswada huo ukapitishwa moja kwa moja Bungeni na Katiba mpya ikapatikana mwaka 1977. Mfumo wa chama kimoja ukazidi kujikita na dhana yake ya Chama 12

kushika hatamu ikaneemeka zaidi. Kwa hali hii ni dhahiri kuwa hata Katiba tuliyo nayo hivi leo haikuwashirikisha wananchi wote kwani si wote waliokuwa wanachama wa chama tawala. Hivyo utaratibu wa kutunga Katiba mpya kwa kuitisha kongamano la Katiba (constitutional conference) haujawahi kufanyika wala kuwa sehemu ya desturi nchini Tanzania hadi leo. 3 MABADILIKO NA MABORESHO KATIKA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 1977 (AMENDMENTS). I. Mabadiliko ya Kwanza 1979 Mabadiliko ya kwanza katika Katiba ya mwaka 1977 yalifanyika mwaka 1979 yakilenga hasa kwa ukuu kuanzishwa kwa mahakama ya rufani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye mamlaka katika pande zote za Muungano. Hii ilichangiwa pia na kuanguka kwa jumuiya ya Afrika Mashariki ya 1967 hivyo mifumo yote ikiwemo ya kimahakama kurudi kwa dola husika. II. Mabadiliko ya Pili ya 1980 Mabadiliko ya pili yalifanyika mwaka 1980 yakilenga kutatua kero mbalimbali za Muungano hasa kwa upande wa Zanzibar. Hata hivyo mabadiliko haya hayakutatua kero hizo kama ilivyotarajiwa. III. Mabadiliko ya Tatu 1980 Mwaka huo huo yalikuja tena mabadiliko mengine, yawezekena hii ilitokana na ubovu wa Katiba ama uchanga wa Taifa na ukuaji wake uliohitaji mtazamo shirikishi kwa watu wa Tanzania, na hilo halikufanyika ipasavyo. Katiba iliyoshirkisha watu huwa madhubuti na imara yenye kuhimiri mabadiliko ya kiuchumi, siasa na jamii maana hulenga vizazi vyote. IV. Mabadiliko ya Nne 1982 13

Mabadiliko ya nne ya Katiba ya 1977 yalikusudia kuboresha taratibu za kuteua wakuu wa mikoa na wilaya, hata hivyo mabadiliko haya hayakuweka bayana uwajibikaji wa wakuu hawa. V. Mabadiliko ya Tano 1984 Mabadiliko ya tano yalifuatia mahitaji ya watanzania kuwepo na ustawi na uangalizi wa haki za binadamu katika Katiba na hivyo kuingiza tamko la haki za binadamu katika Katiba. Sehemu ya tatu ya Katiba hii inajumuisha tamko la haki za binadamu. VI. Mabadiliko ya Sita 1990 Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilianzishwa na mabadiliko haya ya mwaka 1990 yakiwa ni mabadiliko ya sita katika Katiba ya mwaka 1977. Kabla ya tume hii masuala ya uchaguzi yalikuwa chini ya uangalizi wa Chama (CCM). Lengo la kuanzisha tume ilikuwa kusimamia uchaguzi mkuu wa vyama vingi wa 1995. VII. Mabadiliko ya Saba 1990 Ndani ya mwaka huu yalikuja mabadiliko mengine tena yakilenga kuweka utaratibu wa kuwa na mgombea mmoja wa urais upande wa Zanzibar kuundoa utaratibu wa awali ambao ulilalamikiwa. VIII. Mabadiliko ya Nane 1992 Mantiki ya mabadiliko ya mwaka 1992 ilikuwa ni kuruhusu tena mfumo wa vyama vingi nchini. Hii ilitokana na mwelekeo wa magharibi na msukumo wa wakubwa wa dunia waliotaka demokrasia ijikite katika vyama vingi vya siasa. Hata mfumo wa Bunge pia ulibadilika kwa kuruhusu viti maalumu kwa wanawake kwa asilimia 15 na viti vitano kwa baraza la wawakilishi ndani ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. IX. Mabadiliko ya Tisa 1992 Muda mfupi tu mara baada ya mabadiliko ya nane, yalitokea tena mabadilko ya tisa yakirekebisha taratibu za chaguzi za Rais wa Muungano, tamko kwamba Rais 14

anaweza kuondolewa kwa kura ya Bunge kwa kukosa imani nae na kuanzisha nafasi ya Waziri Mkuu kikatiba. X. Mabadiliko ya Kumi 1993 Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliyoanzishwa katika mabadiliko ya sita ya mwaka 1990 ilipewa mamlaka kikatiba kusimamia chaguzi za madiwani na hivyo chaguzi hizo kufanyika pamoja na uchaguzi mkuu wa Rais na Wabunge. XI. Mabadiliko ya Kumi na Moja 1994 Mabadiliko haya yalileta utaratibu wa kuwa na mgombea mwenza kwa nafasi ya Urais ambaye huwa makamu wa Rais mara baada kushinda uchaguzi mkuu. Na kwa mantiki hii basi mabadiliko haya yaliweka ukomo kwa Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano. XII. Mabadiliko ya Kumi na Mbili 1995 Kiapo kwa Rais, makamu wake, Waziri Mkuu na Rais wa Zanzibar kuulinda Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kiliwekwa na mabadilko haya. Na ukomo wa Rais kuwa vipindi viwili tu ulianzishwa na mabadilko haya. XIII. Mabadiliko ya Kumi na Tatu 2000 Hapa mfumo wa kumpata mshindi katika kinyang anyiro cha Urais kwa kupata kura nyingi zaidi ya wapinzani wake. Kabla ya mabadiliko haya Rais alipatikana kwa kupata walau asilimia 51 ya kura zote. Kadhalika Rais alipewa mamlaka kikatiba kuteua watu kumi kuwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kadhalika Viti maalumu vya wanawake bungeni viliongezwa kufika asilimia 20. XIV. Mabadiliko ya Kumi na Nne 2005 Hapa viti maalumu vya wanawake bungeni viliongezwa tena mpaka asilimia 30. Lakini pia uhuru wa kuabudu, uhuru wa kushiriki na watu wengine, uhuru wa maoni na kujieleza viliwekwa bayana na kuondoa vizuizi vyote (clawback clauses) 15

vilivyokuwepo kwenye Katiba. Kadhalika wabunge wa viti maalumu waliteuliwa sasa kwa uwiano wa ushindi wa kila chama majimboni. 4 CHANGAMOTO KUU KUELEKEA KATIBA MPYA TANZANIA a) Umiliki wa Katiba Katika kutizama dhana ya umiliki wa Katiba kama tulivyoona hapo juu, ili kupata uhalali wa Katiba [Legitimacy of Constitution] ni lazima Wananchi wawe wamiliki wa Katiba hiyo. Swali la msingi linaloibuka ni kuhusu jinsi Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 ilivyotungwa na ikiwa wananchi wa Tanzania walishirikishwa katika kuitunga. Kisha ni vema kutizama ikiwa wananchi wanaifahamu Katiba yao. Jambo lingine la msingi ambalo husahaulika mara kwa mara ni kuhusu nafasi ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 katika Muungano. b) Umiliki wa Taifa Leo tarehe 9 desemba 2011 tunapoadhimisha miaka hamsini ya uhuru wa Tanganyika, kaulimbiu ni tumeweza, tumethubutu na tunasongambele. Yamkini kauli mbiu hii inatazama lami toka mtwara mpaka mwanza bila kufikiri ni maliasili kiasi gani tumezigawa bure ama kwa bei ya kutupa kwa wawekezaji toka nje na zingetumika ipasavyo na kiuzalendo kwa masilahi ya taifa basi tungeweza, tungethubutu na tungesongambele kutoa huduma za jamii kama afya, elimu, maji nishati na hata miundombinu kwa kila mtanzania na hivyo kauli mbiu hii ingeakisi uhalisia na kupanda mbegu ya uzalendo kwa vizazi vya Tanzania. Uzalendo wa kweli na wa dhati huzaliwa, hujengwa na kudumishwa pale ambapo kuna heshima katika misingi ya usawa na wananchi kuwa na nafasi katika kumiliki raslimali za nchi. Swali linalozuka mara nyingi hutokana na wananchi kuhoji mara kwa mara serikali ni nini? ile inayoitwa mali ya umma kwa kawaida huwa ni ya nani? Ikiwa wawakilishi wa wananchi [Bunge] hawana ruhusa ya kuona [mathalan] 16

mikataba ya nchi na wawekezaji, mfano mikataba ya madini, n.k swali linabaki je, Umma ni nani? Matabaka yanayojengeka katika jamii kutokana na mfumo mpya wa elimu unaoifanya elimu kuwa bidhaa badala ya haki ya msingi; afya na huduma za kijamii nazo kukosa udhibiti wa kutosha huku walio wengi wakikosa huduma muhimu na wachache kufaidi yote haya ni mazingira ya kuua na kudidimiza uzalendo katika taifa. c) Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Katika kipengele hiki kumekuwa na utata mkubwa zaidi. Kumekuwa na hoja nyingi na maswali mengi ambayo hayajajibiwa. Kuhusu Bunge la Muungano kutunga sheria zisizokuwa na nguvu Zanzibar, kuhusu wabunge toka Zanzibar kushiriki katika kutunga sheria zinazohausu mambo yasiyo ya muungano, n.k. Pili maswali mengine yamehoji Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo haina mamlaka ya kisheria kufanya shughuli zake Zanzibar hata kama ni kuhusu suala la Muungano, na nafasi ya Mahakama ya Rufani hasa baada ya Mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar ya 1984 yaliyofanywa na Baraza la wawakililishi Mwaka 2010. Sura nzima ya Nne ya Katiba ya Sasa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepitwa na wakati na inapaswa kufanyiwa marekebisho makubwa ikiwa ni pamoja na kutambua nafasi ya Makamu wa Kwanza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar. 29 d) Ushiriki wa Wananchi Katika Uongozi wa Nchi Miongoni mwa changamoto nyingine za msingi ni suala zima la ushiriki wa wananchi katika uongozi wa nchi. Hii ni pamoja na kuhoji usahihi wa mfumo mzima wa uchaguzi, uhuru wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, na mamlaka ya Mahakama katika kuhoji na kuamua kuhusu matokeo ya uchaguzi wa Rais. Hoja ya ushiriki ikienda mbali zaidi inahoji ikiwa kweli kuna demokrasia kwa kuwanyima wananchi nafasi ya kuchaguliwa ikiwa hawapendelei kujiunga na chama fulani cha siasa. Suala la Mgombea huru nalo limetia dosari hata Uhuru wa Mahakama pale ambapo Mahakama ya Rufani ilipoacha kutumia mamlaka 29 Taz. Ibara ya 39 Katiba ya Zanzibari, 1984 17

yake kisheria ya kutafsiri sheria na badala yake kuliachia Bunge. Katiba hii tuliyonayo haitoi nafasi ya jinsi ya kuiwajibisha Mahakama pale inapoacha kutumia mamlaka iliyopewa. e) Uhusiano Kati ya Dola na Mwananchi Mwananchi wa kawaida hujiuliza mara kwa mara je ni nini wajibu wa polisi na Askari mgambo? Je haki ni nini na mahakama ni chombo cha namna gani? Maswali yote haya yana mwelekeo wa kuashiria kwamba wananchi wanahoji imani yao kwa vyombo vya utendaji haki. Kwa sababu hiyo tatizo la wananchi kujichukulia sheria mikononi linaendelea kuwepo kutokana na [pamoja na sababu nyingine] wananchi kutokuwa na imani na vyombo vya utoaji haki. Katiba haijaweza kutoa majibu kuhusu hali ya uadui/uhasama unaoendelea kujengeka kati ya vyombo vya dola na raia. 30 f) Haki za Binadamu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kwa mara ya kwanza ilitoa ulinzi kwa baadhi ya haki za binadamu mwaka 1984 na zikaanza rasmi kutekelezwa mwaka 1988. Hata hivyo, haki za binadamu katika Katiba bado hazina ulinzi wa utosha. Kwa upande wa Zanzibar Kwa Mfano, Baraza la Wawakilishi kwa sasa haliwezi kubadili kifungu chochote cha haki za binadamu mpaka tu pale amabapo ridhaa ya wananchi kupitia kura ya maoni itakuwa imepatikana. Pamoja na kuwepo kwa ibara zinazotoa ulinzi kwa haki za binadamu, Katiba ya Tanzania bado ni dhaifu katika kuzilinda, na wakati mwingine katiba hiyo hiyo ina ibara zinazopingana. Ibara ya 30 ya Katiba inaruhusu uvunjaji wa Haki uendelee hata baada ya hukumu ya mahakama hadi pale bunge litakapokuwa limetunga sheria husika au muda utakaokuwa umetolewa na Mahakama. g) Dira/Lengo Mahususi la Taifa 30 Mwaka 2009 LHRC ilitoa taarifa kuhusu Askari Polisi aliyeuliwa na wananchi wenye hasira kali! Wanachi kuvamia vituo vya polis, wananchi kuchoma mahakama n.k 18

Ibara ya 3 ya Katiba inasema kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa isiyokuwa na dini, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi. Lengo la Ibara hii ilikuwa ni kutoa taswira na mwelekeo wa Taifa la Tanzania. Hata hivyo mwelekeo huu ni potofu kutokana na sera kinyume za ubinafsishaji na mfumo wa soko huria. Kwa sasa swali linalojengeka ni kuhusu mustakabali wa taifa la Tanzania, je ni wapi tunataka kwenda kama taifa? Kukosekana kwa lengo Mahususi au Dira ya Taifa kunasababibishwa na Katiba iliyopo. Ibara ya 9 inasisitiza utekelezaji wa misingi ya kijamaa ambayo ni kuweka njia kuu zote za uchumi mikononi mwa umma, pia ibara ndogo ya (c) inasema kuwa shughuli za serikali zinatekelezwa kwa njia ambazo zitahakikisha kwamba utajiri wa taifa unaendelezwa, unahifadhiwa, na unatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa ujumla na pia kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine, haya yote yamepuuzwa na kuifanya Katiba iliyopo kuonekana kuwa imepitwa na wakati, bado haitoi jibu la swali linaloulizwa sasa, Je, ni nini dira ya Taifa la Tanzania? 5 HITIMISHO NA MTAZAMO WA MBELE Kama tulivyotanabaisha hapo juu, kwa muda wa zaidi ya miongo miwili sasa, na zaidi baada ya kuanzishwa mfumo wa demokrasia ya vyama vingi Tanzania mwaka 1992, kumekuwepo kilio cha wengi kuhusu Katiba mpya. Kilio hiki kimejikita katika msingi wa hoja mbalimbali za msingi na hasa ile inayolenga kuwa uhalali wa Katiba kama sheria mama ni lazima utokane na ridhaa ya wananchi au Umma. 31 Kwa maneno mengine, kama alivyowahi kusema Jaji Mwalusanya, msingi na chanzo kikuu cha katiba ni watu. 32 Hata hivyo, kama maneno haya yatatizamwa katika nuru ya historia ya Katiba Tanzania kama tulivyo fanya hapo juu, itabainika wazi kuwa, Katiba tuliyonayo hivi sasa haikutokana na watu (umma) wa Watanzania na hivyo si Katiba ya Watu (Umma). 33 Hii ni kutokana na ukweli kuwa Katiba hii imetokana na mapendekezo ya Kamati Kuu ya Chama kilichokuwa kimeshika hatamu zote za kisiasa na ambacho si kila mwananchi alikuwa 31 Taz. Mwalusanya, J. Conditions for the Functioning of a Democratic Constitution, in Mtaki, C.K & Okema, M., Constitutional Reforms and Democratic Governance in Tanzania, Friedrich Naumann Stiftung, pp.21-36, at 22 32 Ibid 33 Ibid 19

mwanachama wake. Mapendekezo hayo ndiyo yaliyowasilishwa bungeni na bunge likiwa limekaa kama bunge la Katiba kuyapitisha. 34 Hakukuwepo na kongamano lolote la Katiba. Tunapoadhimisha miaka hamsini ya uhuru ikiambatana na mchakato wa kuelekea katiba mpya tuyatafakari haya na kujipanga sawa tusivae viatu vya mkoloni ama maoni ya chama kimoja kama ilivyowahi tokea na kuminya uhalali wa katiba yetu. Mwisho, tusisahau ya kwamba katiba ni maridhiano ya kitaifa juu ya mustakabali wa Taifa la leo na la kesho yafikiwayo na wananchi wenyewe kwa hiari bila shuruti ama ushawishi, na hivyo Katiba ni watu, ni ya watu na si ya mtawala ama mali ya watawala. Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania, Mungu libariki jiji lako SAUT... MAREJEO MBALIMBALI i) ARD, Inc. Report, Democracy and Governance Assessment of Tanzania Transitions from the Single-Party State A Report submitted to the United States Agency for International Development, (2003) ii) Fimbo, G.M. Towards Separation of Powers in a New Democracy : Tanzania, (1995) 22 (1&2) The African Review, pp.16-31 iii) iv) Fombad, C.M., Challenges to Constitutionalism and Constitutional Rights in Africa and the Enabling Role of Political Parties: Lessons and Perspectives from Southern Africa (2007) 55 American Journal of Comparative Law Kabudi, P.J.A.M., International Law Examination of the Union of Tanganyika and Zanzibar: A Federal or Unitary State? L.L.M. Dissertation, University of Dar-es-Salaam (1986) (mimeo) v) Okoth-Ogendo, H.W.O Constitutions Without Constitutionalism: Reflections on an African Political Paradox in Shivji, I.G., (ed.) State and Constitutionalism: An African Debate on Democracy, Human Rights & Constitutionalism Series, No.1, Southern African Political Economy Series (SAPES) Trust, Harare, Zimbabwe, 1991. vi) Makaramba, V.R., A new Constitutional Order for Tanzania? Why and How, Friedrich Ebert Stiftung/ Tanganyika Law Society, (1997) 34 Ibid 20

vii) Mwalusanya, J. Conditions for the Functioning of a Democratic Constitution, in Mtaki, C.K & Okema, M., Constitutional Reforms and Democratic Governance in Tanzania, Friedrich Naumann Stiftung viii) McAuslan, W.B., The Republican Constitution of Tanganyika, (1964) 13 International & Comparative Law Quarterly, 502-573. ix) Rev. Christopher Mitikila v. Attorney General, [1995]TLR 31 x) Shivji, I.G. Constitutional Limits of Parliamentary Powers The Tanzania Lawyer (Special edition) October, (2003) xi) xii) Shivji, I.G. The Legal Foundation of the Union in Tanzania s Union and Zanzibar Constitutions, Professorial inaugural Lecture, DUP, Dar-es- Salaam, 1990. Jjuuko, F. na Muriuki, G., Shirikisho Ndani ya Shirikisho: Uzoefu wa Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki. Taarifa ya Ujumbe wa Kituo cha Katiba Nchini Tanzania kutafuta ukweli wa Mambo., Kampala, 2010. 21