Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi

Similar documents
MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2017/18

Songa kwenye kilele cha upeo. Masuala ya Msingi na Ujuzi juu ya Uendeshaji wa Serikali za Mitaa

TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM)

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU

KUHUSU AFRODAD. Dira ya AFRODAD. Dhamira ya AFRODAD. AFRODAD inalenga mchakato sawa na endelevu wa maendeleo kuelekea Afrika yenye mafanikio.

NGUZO KUMI ZA KILIMO KWANZA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

KAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI TANZANIA

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

MAADHIMISHO YA MIAKA 15 YA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

UFUATILIAJI WA MIRADI NA TATHMINI

JAMHURI YA KENYA. Mkakati wa Ushirikiano MUKHTASARI FY Public Disclosure Authorized. Public Disclosure Authorized

Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA 2006/07

In the matter of Application by the TANGA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (TANGA UWASA) For a Multi-Year Tariff Adjustment

Miradi na jamii. 3.1 Utangulizi

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU

Dibaji ya Mwenyekiti wa Kamati ya Pamoja ya Uongozi

Kuuelewa Mchakato wa Bajeti Tanzania Mwongozo wa Asasi za Kiraia

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Nilikua na Ndoto ya Kumaliza Shule Changamoto za Elimu ya Sekondari Tanzania

Ufanisi katika Ufundishaji kwenye Shule za Msingi na Sekondari nchini Tanzania

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA

SautiElimu. Sauti Yako Isikike

Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali ya Madini Ukanda

In the matter of an Application by the KIGOMA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (KUWASA) For a Tariff and Charges Adjustment

Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame M. Mbarawa (Mb.); Waheshimiwa Mawaziri na Wabunge wote mliohudhuria;

Elimu Bora, lakini... C HakiElimu Elimu bora, lakini...

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA. Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo. TOLEO Na.

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA MHESHIMIWA DKT

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Azimio lililopitishwa na Mkutano Mkuu tarehe 18 Desemba 2013 [juu ya taarifa ya Kamati ya Tatu (A/68/456/Add.2)]

Kufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007

TAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF) KUHUSU HAKI ZA WATOTO KATIKA KATIBA MPYA

Information for assessors (do not distribute this page to participants):

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, MHESHIMIWA DKT. PHILIP I. MPANGO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO

TANZANIA MARKETS PAN Sera zinazoboresha masoko

Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara)

5. Mheshimiwa Spika, Bunge lako Tukufu lilijadili kwa kina Miswada ifuatayo:

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA FEDHA

Programu ya Uendelezaji Mifumo ya Maji Vijijini (PUMMV) katika Tanzania. Modeli wa Ukodishaji Mradi

Mwongozo wa Utekelezaji wa Njia za S5-UUE (KAIZEN)-UUU Tanzania

ORDER NO BACKGROUND

RIPOTI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA NISHATI NA MADINI

Kimesanifiwa na:- E.D.Kissuu ECOMM TANZANIA S.L.P ,Dar es Salaam. Simu:

MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA PRO-ROUTES. Ombi kwa ajili ya fedha za umma wa mradi wa ziada

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TAARIFA YA MWAKA YA UTENDAJI KAZI IDARA YA UTAWALA BORA 2013/2014

Kubadili Sheria Za Mbegu Na Ulinzi Wa Aina Za Mbegu Na Mimea Nchini Tanzania

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

MAPENDEKEZO YA MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA TANZANIA

RIPOTI YA WARSHA KUHUSU HABARI KWA AJILI YA UWAJIBIKAJI

3. Mheshimiwa Spika, 4. Mheshimiwa Spika,

UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU VIKWAZO VYA KULINDA MAISHA KATIKA USAIDIZI WA KIMATAIFA WA AFYA KWA MSAADA WA KIMATAIFA UNAOFADHILIWA NA MAREKANI

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Draft 03 MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO MWENGE

KITEGO CHA MAREKEBISHO NA HAKI ZA MTOTO

Dodoma ambako kikao cha Bunge kinaendelea kuja kushiriki japo sehemu ya uzinduzi wa mkutano.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA III VI

Tufundishane! Mwalimu Bora In this issue: Issue 6, December Do you want to be in our next issue?

Govt increases vetting threshold of contracts

Mwongozo wa Kutathimini mifumo ya Ugawanaji wa faida na Mapato Katika Miradi ya Jamii ya MKUHUMI

TANZANIA TAARIFA YA MWISHO WA UTEKELEZAJI

HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE

UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA)

Deputy Minister for Finance

Elimu-Jumuishi Kwa Vitendo

MWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI

Kutetea Haki za Binadamu

Unyanyasaji wa Watoto & Kutelekezwa

KIMAZINGIRA NA KIJAMII NA MPANGO WA UDHIBITI

ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA UCHUMI WA ZANZIBAR

HAKI NA TARATIBU ZA AJIRA, KAZI NA HIFADHI YA JAMII

Taarifa Kuhusu Hali ya Uchumi wa Tanzania

Kuwafikia waliotengwa

Kitabu Cha Mafunzo Ya Uongozi Kwa Wanawake

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA,KWA WANANCHI, 30 SEPTEMBA, 2001

LUGHA YA KISWAHILI KATIKA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA ELIMU SHULE ZA SEKONDARI

HUDUMA ZA AFYA KWA WOTE

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA PILI. Kikao cha Nne - Tarehe 29 Januari, (Kikao Kilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A

Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI Nchini Tanzania

Elimu Ina Umuhimu gani katika Jamii? Kuelekea Elimu Sahihi

HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA MHESHIMIWA

KUSHUKA KWA HADHI YA LUGHA ZA JAMII NCHINI TANZANIA YOHANA P. MSANJILA University of Dar es Salaam, Tanzania

Mipango ya miradi katika udugu

Elimukombozi, Lugha na Upashanaji Habari nchini Tanzania, katika Muktadha wa Utandawazi

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA SABA. Kikao cha Thelathini na Tisa Tarehe 1 Juni, (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A

Afya Bora, Utu na Kinga. Ripoti ya Mashauriano ya Kiufundi Aprili 2009, Hammamet, Tunisia

Human Rights Are Universal And Yet...

Transcription:

Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi HakiElimu: Mfululizo wa Mada za Uchambuzi Namba. 2003. 6S

Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari 1 Rakesh Rajani na George Omondi 2 Utangulizi Serikali ya Tanzania imetambua umuhimu wa kuwekeza kwa watu wake kwa nia ya kupambana na magonjwa, umaskini na ujinga. Tangu mwaka 1995, kumekuwa na mfululizo wa mageuzi kushughulikia tatizo linalokwamisha elimu. Hali ya miundo mbinu haijafanyiwa marekebisho na kumekuwepo na upungufu wa mahitaji muhimu. Wanafunzi wengi wanasoma ndani ya madarasa yaliyojaa na yenye upungufu wa madawati, wanafunzi ishirini hata zaidi wanalazimika kuchangia kitabu kimoja. Walimu hawalipwi vizuri na hawajaandaliwa vyema kwa usimamizi na ubora wa majukumu wanayoyafanya. Kanuni za ufundishaji darasani na mahusiano ya mwalimu na mwanafunzi ni ya kiburi na ukatili badala ya kuwa ya kuheshimiana na kujaliana. Umaskini uliokithiri na madeni umekwamisha uwezo wa Serikali kutoa rasilimali husika katika elimu na kutoa uwezo wa kaya kuendana na ongezeko la gharama za elimu. Changamoto nyingine ni UKIMWI ambao umepunguza uwezo wa wananchi na kubebesha mzigo mkubwa unaoongeza umaskini na kuzidisha kutoendelea. Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) 2002-2006 (URT 2001a) una mkakati wa kupambana na tatizo hili. Unakusudia kutoa nafasi kwa watanzania wote kupata elimu bora kama nyenzo ya Tanzania kupambana na umaskini. Elimu ni sekta iliyopewa kipaumbele na inachukuliwa kuwa ni kiini cha maendeleo katika sera ya kuondoa umaskini (PRS, URT 2000). Sambamba na dira ya 2025, elimu inayosisitizwa si yoyote ile. Bali ni: Elimu ichukuliwe kama mkakati kwa kuweka mageuzi ya kifikra na kuunda taifa lililoelimika vizuri, lenye maarifa ya kutosha yanayohitajika katika kutatua kwa ufanisi na kiushindani changamoto ya maendeleo inayoikabili nchi. Kutokana na hilo, mfumo wa elimu hauna budi kupangwa upya na kubadilishwa kwa ubora unaolenga katika kukuza ubunifu na utatuzi wa matatizo. (Dira 2025 ukurasa 19, kama ilivyonukuliwa na URT 2001a) Nguzo za upatikanaji, usawa na ubora kwa watoto wote ndiyo misingi ya MMEM (ukurasa 2). Inaendana na makubaliano ya Tanzania katika mikataba ya kimataifa kuhusu Haki ya Mtoto na Elimu kwa Wote. Muhimu zaidi ni kuwa MMEM imetilia mkazo masuala ya utawala; hasa katika mfumo wa uboreshaji wa mabaraza ya ngazi za chini, kama ilivyo katika mageuzi ya Serikali za Mitaa (URT 1998). Msisitizo uko katika uwazi, demokrasia, ushiriki katika maamuzi na uwajibikaji. Vilevile MMEM inasisitizia lengo la Serikali kujenga mtazamo wa sekta pana zaidi, kwa maana ya kuwa juhudi yote ya Serikali juu ya elimu ya msingi na misaada ya wafadhili inaandaliwa kupitia MMEM badala ya kuwa na mitazamo tofauti ambayo haitaleta maendeleo sawia na yenye gharama kuiendesha. 1 Muhtasari huu umeandaliwa kusaidia Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi kufahamika kwa upana zaidi kwa wanaojishughulisha na maswala ya maendeleo, watetezi, wahamasishaji na umma kwa ujumla.tunaamini utachangia katika kuibua mijadala kuhusu mwelekeo wa elimu ya msingi na mafanikio yaliyopatikana mpaka sasa, kwa sababu mijadala ya namna hiyo ni muhimu kwa demokrasia na maendeleo. Mada hii ya Uchambuzi ilichapishwa kwa mara ya mwanza na HakiElimu katika lugha ya Kiingereza mwaka 2003 2 Rakesh Rajani ni Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu. George Omondi ni mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 1

Misingi Mikuu ya MMEM Watu wengi wanafikiri MMEM inahusu ujenzi wa madarasa na kuandikisha wanafunzi tu. MMEM ina nguzo kuu nne: kuongeza uandikishaji, kuinua ubora wa elimu, kujenga uwezo na kuboresha nyenzo za kifedha na watu pamoja na kuzibadili taasisi. MMEM inatambua wazi kuwa mambo yote manne ni muhimu na yanaingiliana na budi yafanikishwe kwa pamoja. 1. Upanuzi wa Kuandikisha MMEM inakusudia watoto wote wenye kati ya miaka 7 12 wawe wameandikishwa darasa la kwanza kufikia Septemba 1, 2004. Idadi ya wanaoandikishwa kila mwaka inatazamiwa kuongezeka kwa asilimia 50 kufikia milioni 1.6 kwa kila mwaka kati ya 2004 hadi 2006, kabla ya kudhibitiwa tena kufikia wastani wa milioni moja (angalia jedwali). Hii itawawezesha watoto wote waliokwama nje ya shule kupata elimu rasmi, hata hivyo baadhi ya wachache walio na umri mkubwa watapatiwa elimu maalum. Mbinu kuu zitakazotumika kuongeza uandikishaji ni kama ifuatavyo: Kuondoa ada: Kuondoa ada na michango mingine ya lazima kuanzia Januari 2002 ili kusiwe na mtoto anayenyimwa elimu (ukurasa 5). Kuajiri na kuwapa motisha walimu: Kuajiri, kutoa mafunzo na kusambaza walimu wa kutosha wa shule za msingi kwa namna ambayo itatosheleza ongezeko kubwa la uandikishaji na kuhakikisha kunakuwepo na mgawanyo sawa na wenye uwiano wa kijinsia wa walimu waliopata mafunzo (ukurasa 6). Marupurupu yatolewe kwa walimu wanaofanya kazi katika maeneo magumu kuhakikisha wapo wa kutosha. Kuwapatia nyumba na ajira inayokidhi mahitaji ndiyo mikakati muhimu. Kujenga madarasa na nyumba za walimu: Kujenga madarasa mengine mapya (pamoja na vyoo na maji), kuwapatia nyumba walimu kama kivutio cha usambazwaji kwa kutoa kipaumbele kwa walimu wa kike katika maeneo yaliyo mbali sana na yale ya vijijini na kuwapatia nyumba asilimia 30 ya walimu wapya kwa mwaka (Ukurasa 7). Jedwali: Malengo ya Uandikishaji ya MMEM 2002-2006 (kurasa 5-7) Mwaka Nafasi Darasa la 1 Walimu waajiriwa wapya Ujenzi wa madarasa mapya 2002 1,500,000 9,047 13,868 2003 1,600,000 11,651 13,396 2004 1,640,969 10,563 14,203 2005 1,041,880 7,286 6,794 2006 1,065,843 7,249 5,832 Jumla 6,848,692 45,796 54,093 2. Kuinua Ubora MMEM inakusudia kufufua na kuboresha elimu ya msingi, kwa kuangalia sehemu tatu muhimu: a) kuboresha mbinu na njia za walimu za ufundishaji b) kuhakikisha upatikanaji wa vifaa bora vya kufundishia na kujifunzia, na c) kuhakikisha ubora unadhibitiwa (ukurasa 9). Kimsingi sehemu hizi ni: 2

Kuongeza uwezo na mbinu za walimu darasani: Walimu watasaidiwa kuweza kufundisha kwa namna ya usomi na umahiri, inayowapa mazingira mazuri watoto na kuzingatia jinsia (ukurasa 9) na kutumia njia zinazozingatia ujenzi wa ujuzi wa kudumu, tukizingatia ugonjwa wa UKIMWI (ukurasa 10). Kiasi cha dola 40 (takriban shilingi 40,000/=) kitatengwa kwa kila mwalimu kila mwaka, kwa maendeleo na mafunzo (ukurasa 10). Kuongeza vifaa vya kufundishia na kujifunzia katika ngazi ya shule: MMEM itatengeneza mazingira ya shule yanayofaa kwa kujifunzia (ukurasa 11). Kila mwanafunzi, kufika mwaka 2006, atakuwa na kitabu chake cha kiada. Muhimu zaidi ili kuanzisha pato la uhakika kwa matumizi mengine ya lazima nje ya mshahara, ruzuku ya uendeshaji ya dola 10 (takriban shilingi 10,000/-) kwa kila mwanafunzi aliyeandikishwa itaanzishwa nchi nzima kuanzia Januari, 2002 (ukurasa 11). Kwa kuanzia dola 4 zitapelekwa kwenye halmashauri za wilaya kwa ununuzi wa vitabu na vifaa vyingine vya elimu (ukurasa 11), baadae hizi nazo zitapelekwa moja kwa moja mashuleni, kulingana na mfumo wa uboreshaji wa Serikali za Mitaa ruzuku ya uendeshaji itapelekwa mashuleni ambao wataamua njia bora ya kuzitumia (Ukurasa 11). Kuwawezesha viongozi kuwasaidia walimu: Viongozi wa elimu (wakaguzi, wakufunzi, walimu wakuu n.k.) watapewa mafunzo ya kuwawezesha kutoa msaada ufaao kwa walimu, badala ya mtindo wa kutoa amri na maelekezo (ukurasa 9). 3. Kujenga Uwezo MMEM ina lengo la kujenga uwezo na umahiri wa watumishi wa ngazi zote, kwa ajili ya kufanikisha ubora, kugawa madaraka, ushiriki wa umma na kuwezesha jamii. Programu ina sehemu nne: Kufundisha na kuwapa motisha walimu: Mitaala ya ufundishaji walimu itaangaliwa upya kuona kama inakidhi mbinu za ufundishaji. Serikali itatoa mafunzo kwa kundi kubwa la walimu wapya, wanaokisiwa kufikia 46,000 katika kipindi cha miaka mitano ya MMEM. Maslahi mazuri ya kazi na vigezo vya utoaji huduma vitatolewa kwa walimu vikwazo vya kifedha kutatuliwa kwa walimu watakaoajiriwa (ukurasa 12). Kujenga uwezo wa usimamizi wa shule: Mafunzo ya usimamizi yatatolewa kwa walimu wakuu, kamati za shule, maofisa elimu wa kata na watumishi wengine ili kuongeza ubora, uwajibikaji, ufanisi na kufanikisha ushiriki wa jamii, uwiano wa jinsia na uwezo wa kupambana na athari za VVU/UKIMWI. Kufanikisha haya watumishi na wadau wote wanaosimamia MMEM watapatiwa taarifa za msingi na miongozo juu ya MMEM pamoja na mafunzo ya utendaji (ukurasa 13). Msisitizo mkubwa uko kwenye kamati za shule, ambazo zitapewa mafunzo juu ya majukumu mapya, pamoja na ruzuku ya dola 500 (takriban shilingi 500,000/-) kwa kila shule (ukurasa 13). Kuimarisha usimamizi wa fedha: Usimamizi wa fedha utaimarishwa kuanzia ngazi ya taifa hadi shule, hususan uwajibikaji wa matumizi ya ruzuku ya uendeshaji, ya maendeleo na ya uwezeshaji. Lengo kubwa ni kujenga uwezo wa kutayarisha taratibu, vitabu vya mahesabu na mafunzo kwa kuwezesha kuorodhesha, kuripoti na kukagua matumizi ya fedha za MMEM. Kanuni ya uwajibikaji na uwazi juu ya matumizi ya fedha za umma itasisitizwa na taarifa juu ya matumizi ya fedha za MMEM zitatolewa kwa ngazi zote za mfumo wa elimu, wakiwemo wazazi na jumuiya (ukurasa 14). 3

Kuboresha usimamizi wa taarifa za elimu: Usimamizi wa taarifa za elimu (EMIS) utaangaliwa upya na wasimamizi kupewa mafunzo, kuhakikisha wanawasilisha taarifa sahihi kwa wadau wote kwa wakati (ukurasa 14). 4. Muundo wa Taasisi Sehemu ya nne ya MMEM ni kujenga uwezo wa taasisi katika mfumo wote wa elimu, kwa kuwezesha demokrasia, mgawanyo wa madaraka, uwajibikaji, ushiriki mkubwa wa umma na kutoa madaraka ya usimamizi wa fedha kwa shule. Hii itaendana na kuongeza ruzuku kwa ngazi ya shule. Jambo la msingi ni kuhakikisha taarifa kuhusu MMEM zinawafikia kwa wakati wadau wote wakiwemo wanafunzi, wazazi, walimu, na wasimamizi wa elimu nchi nzima. Kiambatanisho cha Uimarishaji wa Taasisi (URT 2001b) kimeeleza kwa ufasaha yote kuhusu MMEM. Kinaelezea wajibu wa kila wizara na mamlaka za Serikali za Mitaa, kama halmashauri, ngazi ya kata na kamati za shule. Mambo yaliyotiliwa mkazo katika muundo wa taasisi ni haya yafuatayo: Kamati ya kuratibu: Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP) ni kamati inayoongozwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu ina jukumu la kuratibu MMEM. Katika ngazi hii Kamati Maendeleo ya Elimu ya Msingi (BEDC) itasimamia maendeleo ya programu za elimu, mipango na kukagua mipango yote sambamba na sera za Serikali (ukurasa 20). Kamati ya Maendeleo ya Elimu ya Msingi ina uwakilishi mpana, unaojumuisha wajumbe kutoka serikali, mashirika ya hiari na yasiyo ya serikali, chama cha walimu na wafadhili. Ofisi ya Rais -Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ina jukumu la kuhakikisha utoaji wa uhakika wa elimu ya msingi unaofanywa na mamlaka za Serikali za Mitaa, kutoa uongozi wa kimkakati na kujenga uwezo sambamba na kanuni za uboreshaji wa Serikali za Mitaa. Kazi ya Wizara ya Elimu na Utamaduni ni kuandaa mipango shirikishi, kutoa sera na kanuni na kuweka uthibitisho wa viwango bora. Wizara zote mbili zina majukumu ya kutathmini, kukusanya na kusambaza taarifa kwa wadau wote. Kamati za shule: Kamati za shule ni kiungo muhimu sana katika mfumo wa MMEM. Kisheria kila shule inatakiwa kuwa na kamati ya shule. Kazi zake kuu ni uandaaji wa mipango, bajeti na utekelezaji wa miradi katika njia inayowashirikisha wanafunzi, wazazi, watumishi na wadau wengine. Pia kamati ina uwezo wa kukadiria matumizi ya ruzuku ya maendeleo na uwezeshaji pamoja na kufuatilia matumizi yake na kutoa taarifa. Kamati inatakiwa kufanya shughuli zake kidemokrasia kwa kujali maslahi ya umma. Ushiriki wa jumuiya na uwajibikaji ni muhimu na uonekane kupitia wanaounda kamati za shule. Halmashauri za Wanafunzi na Mabaraza ya Shule: Chini ya MMEM wanafunzi wana nafasi muhimu katika usimamizi wa shule, katika utekelezaji wa MMEM. Halmashauri ya wanafunzi itakayokuwa na wajumbe wawili kuanzia darasa la 3-7 (na 2 hadi 4 kutoka vikundi maalum kama wanafunzi wenye ulemavu), itakutana mara moja kila mwezi kuongelea maslahi ya wanafunzi. Kutoka halmashauri yao wanafunzi wawili (wakike na wakiume) watachaguliwa kidemokrasia na wenzao kuwawakilisha katika kamati ya shule. Mwalimu atahudhuria mkutano wa Baraza la wanafunzi kama mwangalizi tu, kuwezesha kuendeleza uwezo na kupeana taarifa. Anapaswa kuepuka kutawala mkutano (kiambatanisho 6). Ngazi ya Kijiji/Mtaa: Kazi kubwa ya halmashauri ya Kijiji/Mtaa ni pamoja na uangalizi wa jumla wa kamati ya shule na kuhimiza utoaji wa taarifa za elimu kwa umma. Vile vile kuhimiza wazazi na walezi kuwaandikisha watoto na kutoa michango ya hiari, na 4

kuzishirikisha asasi zisizo za serikali (AZISE) na mashirika ya jumuiya kutoa ushirikiano katika MMEM Ngazi ya Kata: Kata ndiyo kiungo muhimu kati ya shule/jumuiya na ngazi ya wilaya. Kamati ya maendeleo ya kata ndiyo yenye jukumu la kuangalia utekelezaji wa shughuli zote za MMEM katika kata, pamoja na kuhamasisha AZISE na mashirika ya jumuiya kuiunga mkono. Mratibu wa elimu wa kata anatakiwa kuhakikisha watoto wote waliofikia umri wa kwenda shule wanaandikishwa na kutoa taarifa za elimu kwa wadau wote katika kata. Pia anatakiwa kusaidia kutambua maeneo muhimu kwa maendeleo ya shule. Mamlaka za Serikali za Mitaa: Mamlaka za Serikali za Mitaa, ambazo ni pamoja na Afisa Elimu wa Wilaya, zina jukumu la kusimamia utekelezaji wa mipango yote katika ngazi ya wilaya. Chini ya MMEM, serikali za mitaa zitajitoa katika shughuli za kiutendaji moja kwa moja na badala yake kutoa msaada wa kitaalamu na mipangilio kwa kamati za shule na halmashauri za vijiji. Kazi zao ni kutayarisha mipango ya maendeleo shirikishi, kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa MMEM, kusambaza fedha na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa kamati za shule na kuwasilisha taarifa muhimu kwa wadau. Mamlaka za serikali za mitaa zinatakiwa kushirikisha AZISE na mashirika ya jumuiya katika shughuli hii. Wafadhili na AZISE: MMEM inatoa nafasi kwa ushiriki wa wafadhili na AZISE katika masuala ya elimu nchini. Mtindo uliokuwepo wa kila mfadhili kuchagua mradi wake na kusababisha mgawanyiko unapaswa kuachwa. Wafadhili wanatakiwa kuongeza nguvu katika kuendeleza mipango ya Serikali na mifumo yake. Misaada ya wafadhili itaunganishwa katika bajeti ya Serikali au makusanyo mengine ya ufadhili na mapitio ya matumizi ya umma. Serikali inaridhishwa na ushiriki mashirika ya hiari zikiwemo Azise na mashirika ya kijamii. Kazi yao kubwa ni kushiriki kikamilifu katika kupanga mipango, utekelezaji, ufuatiliaji na kukagua mipango ya utoaji elimu katika ngazi zote. AZISE zinatakiwa kuchangia utaalamu, ujuzi na rasilimali kuboresha elimu ya msingi, na kushughulika na uchambuzi wa sera na utetezi. Wawakilishi wa AZISE na wafadhili ni wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Elimu ya Msingi (BEDC). Bajeti Mgao kwa elimu ya msingi hauna budi kuongezwa kwa kiwango cha kuridhisha, kujumuisha malengo ya MMEM ya upatikanaji, kujenga uwezo na majukumu ya kiutawala. Matumizi makubwa yakiwa mishahara ya walimu, mafunzo kwa walimu, na ruzuku ya uendeshaji, maendeleo na kujenga uwezo. Jumla ya mkadirio wa bajeti wa MMEM (kwa mabilioni ya shilingi) kwa kiwango cha 2001/2 (ukurasa 3) ni: 2002 2003 2004 2005 2006 Jumla (miaka 5) 299.5 323.0 364.4 344.6 356.4 1,687.9 Gharama halisi bado kuainishwa kwa mpango mzima wa MMEM na inaweza kupelekea tarakimu hizi kubadilika. Serikali ipo tayari kuwekeza asilimia 25 ya matumizi yake ya kawaida kwa sekta ya elimu. Kati ya hizi asilimia 62 itapelekwa kwenye elimu ya msingi. Makusanyo mazuri ya kodi yamaanishe rasilimali zaidi inawekezwa kwenye elimu. Licha ya haya pengo kubwa kifedha linatarajiwa kati ya rasilimali iliyopo na ile inayohitajika. Serikali itafanya majadiliano kupata msaada mkubwa zaidi wa kifedha kutoka kwa wafadhili 5

kufidia mapungufu ya bajeti. Hii ni kutokana na ahadi ya mashirika ya kimataifa na nchi matajiri katika mkutano wa Dakar wa 2000 ulioazimia kuwa hakuna nchi yenye mpango mzuri wa kuendeleza elimu itashindwa kufanya hivyo, kutokana na upungufu wa rasilimali. Marejeo United Republic of Tanzania URT (2001a) Primary Education Development Plan 2002-2006 (PEDP), Dar es Salaam URT (2001b) PEDP Strengtherning Institutional Arrangements Annex, Dar es Salaam URT (2000) Poverty Reduction Strategy, Dar es Salaam URT (1998) Policy Paper on Local Government Reform, President s Office Regional Administration and Local Government, Dar es Salaam 6