KITEGO CHA MAREKEBISHO NA HAKI ZA MTOTO

Similar documents
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

TAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF) KUHUSU HAKI ZA WATOTO KATIKA KATIBA MPYA

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig

TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM)

Information for assessors (do not distribute this page to participants):

JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

MAPENDEKEZO YA MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA TANZANIA

HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE

UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU VIKWAZO VYA KULINDA MAISHA KATIKA USAIDIZI WA KIMATAIFA WA AFYA KWA MSAADA WA KIMATAIFA UNAOFADHILIWA NA MAREKANI

Nilikua na Ndoto ya Kumaliza Shule Changamoto za Elimu ya Sekondari Tanzania

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi

KUHUSU AFRODAD. Dira ya AFRODAD. Dhamira ya AFRODAD. AFRODAD inalenga mchakato sawa na endelevu wa maendeleo kuelekea Afrika yenye mafanikio.

MWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI

4. Kanuni za Petroli (Ushiriki wa Watanzania) za mwaka 2017 zilianza kutumika rasmi tarehe 5 Novermba Shughuli za Petroli za kwanza ni

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara

HAKI NA TARATIBU ZA AJIRA, KAZI NA HIFADHI YA JAMII

Waandishi: wa Toleo la 5. Scholastica Jullu Athanasia A. Soka Safina Hassan Mary Njau. Toleo la 5: 2008 ISBN

Songa kwenye kilele cha upeo. Masuala ya Msingi na Ujuzi juu ya Uendeshaji wa Serikali za Mitaa

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA

MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA PRO-ROUTES. Ombi kwa ajili ya fedha za umma wa mradi wa ziada

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU

Azimio lililopitishwa na Mkutano Mkuu tarehe 18 Desemba 2013 [juu ya taarifa ya Kamati ya Tatu (A/68/456/Add.2)]

Afya Bora, Utu na Kinga. Ripoti ya Mashauriano ya Kiufundi Aprili 2009, Hammamet, Tunisia

Deputy Minister for Finance

Dibaji ya Mwenyekiti wa Kamati ya Pamoja ya Uongozi

Na Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake Toleola4

KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II

International Labour Office. Kazi za Ndani Zenye Madhara kwa Watoto: Kijitabu cha Maelezo Mafupi

Tufundishane! Mwalimu Bora In this issue: Issue 6, December Do you want to be in our next issue?

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI-TAMISEMI HALMASHAURI YA WILAYA BUMBULI

JAMHURI YA KENYA. Mkakati wa Ushirikiano MUKHTASARI FY Public Disclosure Authorized. Public Disclosure Authorized

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame M. Mbarawa (Mb.); Waheshimiwa Mawaziri na Wabunge wote mliohudhuria;

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU

HALMASHAURI YA WILAYA YA SUMBAWANGA

KAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI TANZANIA

Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara)

Afya Bora, Utu na Kinga. Ripoti ya Mashauriano ya Kiufundi Aprili 2009, Hammamet, Tunisia

HUDUMA ZA AFYA KWA WOTE

Ripoti hii ni kwa heshima ya wale wanaharakati wengi wa Tanzania ambao ndio binafsi wanaopitia hali iliyoangaziwa, na vilevile wale walioyapoteza

MAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI

Human Rights Are Universal And Yet...

Miradi na jamii. 3.1 Utangulizi

Mwongozo wa Utekelezaji wa Njia za S5-UUE (KAIZEN)-UUU Tanzania

Ufanisi katika Ufundishaji kwenye Shule za Msingi na Sekondari nchini Tanzania

Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI Nchini Tanzania

KIJARIDA JUU YA HAKI ZA RAIA KATIKA MFUMO JINAI

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

Kutetea Haki za Binadamu

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA

JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI

Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA 2006/07

RIPOTI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI

Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali ya Madini Ukanda

MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2017/18

RIPOTI YA WARSHA KUHUSU HABARI KWA AJILI YA UWAJIBIKAJI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Hatari, Haki za Usalama katika Bahari 03

Unyanyasaji wa Watoto & Kutelekezwa

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

KIMAZINGIRA NA KIJAMII NA MPANGO WA UDHIBITI

In the matter of Application by the TANGA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (TANGA UWASA) For a Multi-Year Tariff Adjustment

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees

SautiElimu. Sauti Yako Isikike

Makala ya Mshiriki wa Mafunzo

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. OFISI YA RAIS- TAMISEMI.

3. Mheshimiwa Spika, 4. Mheshimiwa Spika,

Mwongozo wa Kutathimini mifumo ya Ugawanaji wa faida na Mapato Katika Miradi ya Jamii ya MKUHUMI

SUALA NYETI NI VURUGU Mashambulizi dhidi ya Wana LGBT katika Pwani ya Kenya H U M A N R I G H T S W A T C H

Programu ya Uendelezaji Mifumo ya Maji Vijijini (PUMMV) katika Tanzania. Modeli wa Ukodishaji Mradi

MAADHIMISHO YA MIAKA 15 YA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

Mwongozo wa Mwezeshaji

Mhashamu Askofu Jude Thaddaeus Ruwa ichi, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania; Mwadhama Policarp Kardinali Pengo,

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MANISPAA YA BUKOBA.

Kimesanifiwa na:- E.D.Kissuu ECOMM TANZANIA S.L.P ,Dar es Salaam. Simu:

Elimu-Jumuishi Kwa Vitendo

Kuuelewa Mchakato wa Bajeti Tanzania Mwongozo wa Asasi za Kiraia

TANZANIA MARKETS PAN Sera zinazoboresha masoko

Mazoezi yaliyofanyika wakati wa warsha kuhusu Elimu-Jumuishi kwa Vitendo. Zanzibar, 7-10 Februari 2006

TAARIFA YA MWAKA YA UTENDAJI KAZI IDARA YA UTAWALA BORA 2013/2014

5. Mheshimiwa Spika, Bunge lako Tukufu lilijadili kwa kina Miswada ifuatayo:

Kijitabu cha Maelezo cha Programu ya Famasia

NGUZO KUMI ZA KILIMO KWANZA

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA IRINGA SHULE YA SEKONDARI TOSAMAGANGA

YAH: MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI WERUWERU HALMASHAURI YA MOSHI MKOA WA KILIMANJARO MWAKA 2018

Yaliyomo. Kuhusu kitabu hiki. Hautakuwa peke yako. Mfumo wa msaada ni wa manufaa sana wazazi wote wanahitaji!

Palliative Care Toolkit

HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA MHESHIMIWA

Draft 03 MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO MWENGE

Bustani 10,000 Katika Afrika. Alberto Prina

RIPOTI YA KAMATI TEULE YA KUCHUNGUZA UPOTEVU WA NYARAKA ULIOTOKEA KATIKA TAASISI YA NYARAKA NA KUMBUKUMBU ZA TAIFA ZANZIBAR.

Transcription:

KITEGO CHA MAREKEBISHO NA HAKI ZA MTOTO Mwaka 2009 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha sheria mpya ya Mtoto ambayo ni sehemu ya juhudi za serikali za kuhakikisha kuwa haki na ustawi wa watoto unazingatiwa katika kila nyanja ya kijamii na kwamba msuala ya mtoto yanapewa kipaumbele. Sheria hii imelenga kuimarisha ulinzi, matunzo na haki za watoto Tanzania Bara. Sheria hii imeainisha haki ya mtoto kulelewa na Wazazi, haki ya kupewa jina kuwa na utaifa, haki ya kupata mahitaji ya msingi kama chakula, malazi, mavazi, matibabu, chanjo, elimu, pamoja na haki ya kucheza na kuburudika. Sheria hii imelenga kutekeleza mkataba wa kimataifa wa Haki za mtoto. {The UN Convention on the Rights of the Child (CRC)} ambao Tanzania imeridhia miaka 19 iliyopita na Mkataba wa Afrika wa Haki na Ustawi wa Mtoto.{The African Charter on The Rights and Welfare of The Child] Sheria hii imelenga kumlinda mtoto dhidi ya changamoto mbalimbali anazokutana nazo kama Ubaguzi, unyanyasaji na ukatili dhidi ya watoto. Sheria hii pia imeweka mfumo utakaohakikisha kuwa watoto wanapata haki zao za kisheria aidha wawe wamekinzana na sheria, wameingia kwenye mfumo wa sheria au wameshuhudia vitendo ambavyo wanajikuta wameingia kwenye mfumo wa sheria kama mashuhuda wa vitendo vya jinai,mirathi na kadhalika. Kabla ya sheria hii kupitishwa watoto wengi wa kitanzania walikuwa wanakutana na changamoto mbalimbali katika maisha yao ya kila siku kwa sababu ya kukosa sheria maalumu inayoelekeza haki zao na jinsi ya kuzipata hasa pale haki hizo zinapokiukwa.

za msingi Wajibu wa wazazi na walezi katika kuhakikisha watoto wanapata haki zao Mikataba ya kimataifa na Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 zimeweka bayana wajibu wa wazazi na walezi ili kufanikisha utekelezaji wa haki za mototo kama ifuatavyo: Wazazi na walezi wana wajibu mkubwa wa kuhakikisha kwamba watoto wanapelekwa kwenye chanjo, wanapatiwa huduma za afya, wanaandikishwa na kwenda shule, wanafuatiliwa maendeleo yao shuleni, wanasikilizwa na kupewa miongozo na matunzo Jamii inatakiwa iwe bega kwa bega katika kufanikisha wajibu huu kwa kuhakikisha haki za mtoto zinalindwa na kuchukua hatua pale ambapo watoto wanaonekana kunyimwa haki zao. Wazazi, walezi na jamii wana wajibu wa kuhakikisha kwamba watoto wote, wakiwemo wale walio katika mkinzano na sheria wanafurahia haki zao na kutekeleza wajibu wao kikamilifu. Wazazi, walezi na jamii wana wajibu wa kuhakikisha kwamba wanawaongoza watoto katika kutekeleza wajibu wao kikamilifu Watoto waishio mitaani Sababu zinazopelekea watoto kuishi mitaani ni pamoja na: Kukosa haki za msingi chakula, malazi, mavazi, ulinzi na elimu, upendo, matibabu n.k. Wazazi kutengana Kufiwa na mzazi mmoja au wote wawili Kukosa mahitaji ya kisaikolojia na kijamii ukiwemo upendo kutoka kwa wazazi, walezi na jami kwa ujumla Ugomvi katika familia. Migogoro katika ndoa Vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi ya watoto. Ukeketwaji wa wanawake.

Kipato duni katika familia. Wazazi/ walezi walezi Utumikishwaji wa watoto. Kubaguliwa. Shinikizo la rika Kunyanganywa mali za wazazi wao. Matatizo yanayowakabili watoto waishio mitaani ni pamoja na Kubakwa/kulawitiwa Kuiga tabia zisizokubalika katika jamii mfano uhalifu, wizi, ukahaba, utumiaji wa madawa ya kulevya lugha ya kutusi n.k. Kuathiriwa na madhara yatokanayo na hali ya hewa kama jua kali, baridi, kali, kunyeshewa mvua n.k. Kukosa elimu Msongo Kukosa usalama Kuvurugikiwa maono au kuchanganyikiwa Kukosa mavazi, malazi, upendo, elimu, chakula, matibabu n.k. Kujaribu kujiua Kubaguliwa na jamii Kuambukizwa kirahisi magonjwa ya zinaa vikiwemo virudi vya UKIMWI Kupata mamba zisizotarajiwa na katika umri mdogo Kufantyishwa kazi zinazozidi umri na uwezo wao Idadi kubwa ya watoto waishio mitaani wanadai kuwa wamelazimika kuishi mitaani kutokana na mazingira yanayowazunguka. mfano, baadhi kutoa sababu mbalimbali zikiwemo za kukosa wazazi/walezi, unyanyasaji na ukatili wa wazazi/walezi, umaskini wa kukithiri katika familia zao, shinikizo la rika n.k. Mbinu za kuwalinda watoto wanaokinzana na sheria, watoto waishio mitaani na watukutu ni pamoja na:-

Kuwapatia makazi na malazi yanayostahili Kutokuwapa kazi ngumu kuliko umri na uwezo wao. Kuwakinga dhidi ya magonjwa Kuwapatia mavazi Kuhakikisha wanapata huduma za afya pale wanapohitaji. Kutowatendea vitendo vya kikatili mfano adhabu za kinyama kama kuwachoma miili yao, kuwaninginiza kwenye kamba, kuwalaza nje, kuwanyima chakula n.k. Kuwaandikisha shule na kufuatilia maendeleo yao shuleni. Kuwapatia maadili ya dini Kuwapatia fursa ya kucheza. Kuwapa mahitaji ya kisaikolojia na kijamii ukiwemo upendo, kuwajali, kuwasikiliza, kuwapongeza, kuwasifu, kuwapa taarifa zinazowahusu, kuwashauri, kuwapa nafasi ya kushiriki katika mambo mbali mbali katika jamii. Kuwafundisha stadi za maisha. Kujenga uhuru wa mawasiliano baina ya mzazi/mlezi na mtoto kumwezesha motto kuwa na uhuru wa kujieleza na kutoa taarifa ya vitendo vinavyokiuka haki za watoto. Kuziba mianya ya unyanyasaji wa watoto Mzazi/mlezi kutoa taarifa sahihi kwa mtoto ambazo zitamlinda motto na mambo ya udanganyifu au kumwongoza kwenye mitego ya hatari. Kujenga mahusiano yenye kuaminiana baina ya mlezi na mtoto Mzazi/mlezi kutoa muda maalumu na kwa wakati muafaka wa kuwasiliana na watoto. Mzazi/mlezi kuwa tayari kumsikiliza mtoto wakati wote ili apate uhuru wa kujieleza wakati wowote na kumwamini anapozungumza. Usajili wa Vituo vya watoto wnaoishi mitaani

Kukagua vituo vya kulelea watoto wanaoishi mitaani kabla ya kusajiliwa Kutoa leseni kwa vituo vyenye sifa vya kupata usajili Kukagua huduma zinazotolewa kwa watoto walio katika vituo vya watoto wanaoishi mitaani. Leseni Leseni leseni inayotolewa kuendesha vituo vya watoto wanaoishi mitaani inatakiwa itumike kwa kipindi cha miaka 2 tu na mtoa huduma atatakiwa aombe lesseni upya baada ya muda huo kwisha. Angalizo Vituo vinavyolelea watoto wanaoishi mitaani vinatakiwa kuhakikisha kwamba, mtoto anatakiwa akae kituoni kwa kipindi kifupi sana wakati tatizo lake linashughulikiwa ufumbuzi aweze kuunganishwa na familia anayotoka na kituo siyo mahala pa kudumu Nani mwenye sifa yakuanzisha na kuendesha vituo vya kulelea watoto wanaoishi mitaani? Ni mdau yeyote wa watoto mwenye nia ya dhati ya kuwasaidia watoto na ambaye yuko tayari kufuata kanuni na miongozo ya utoaji wa huduma hiyo kwa mujibu wa sheria. Uanzishaji wa vituo vya kulelea watoto wanaoishi mitaani unafanyika chini ya sheria ya mtoto ya mwaka 2009 Angalizo Vituo vya kulelea watoto wanaoishi mitaani vinatakiwa vilee watoto kwa kipindi kifupi wakati tatizo la mtoto linatafutiwa ufumbuzi ili aweze kuunganishwa

na familia yake. Ieleweke kwamba mahali salama na sahihi pa malezi ya mtoto ni katika familia au katika jamii anamotoka.vituo ni sehemu za dharura tu. Hatua za kushughulikia Leseni (i) Mwombaji atatakiwa kujaza fomu ya maombi ya leseni iitwayo P.W.F.1 kwa ajili ya kuanzisha Makao ya watoto. Fomu hii ataipata katika ofisi ya Ustawi wa Jamii katika Halmashauri ya Jiji, manispaa, Mji au Wilaya (ii) Mwombaji atawasilisha fomu iliyokamilika kujazwa kwa Ofisa wa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Jiji, Manispaa, Mji au Wilaya. Fomu itaambatishwa na barua ya utambulisho kutoka Ofisi ya Mtendaji wa Kata, nakala ya Katiba iliyoidhinishwa na aidha kabidhi Wasii Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto au Wizara ya Mambo ya Ndani, pamoja na nakala ya hati ya usajili. (iii) Ofisaustawi wa Jamii atafanya usaili wa kijamii kwa mwombaji wakati wa kuwasilisha maombi ya kuanzisha makao. (iv) Ofisaustawi wa Jamii mara baada ya kufanya usaili kwa mwombaji atafanya uchunguzi wa kijamii utakaojumuisha kutembelea majengo, wadhamini na watu wengine muhimu ili kukusanya taarifa zinazotakiwa. (v) Ofisa Ustawi wa Jamii atatayarisha ripoti ya uhakiki wa kijamii. (vi) Ofisa wa Afya wa Halmashauri ya Jiji, Manispaa na Mji au Wilaya atakagua mazingira na kumshauri mwombaji iwapo kutahitajika marekebisho yoyote. (vii) Ofisa wa Afya ataandika taarifa ya ukaguzi wa mazingira na kuiwasilisha kwa Ofisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Jiji, Manispaa, Mji au Wilaya. (viii) Ofisaustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Jiji, Manispaa, Mji au Wilaya atawasilisha fomu ya maombi (fomu Na. P.W.F.1), taarifa ya usaili, taaifa ya uchunguzi wa kijamii na taarifa ya ukaguzi wa kiafya wa

maeneo ya mazingira kwa Kamishna wa Ustawi wa Jamii kwa hatua zaidi. Muda wa kushughulikia maombi na utoaji wa Leseni Muda wa kushughulikia maombi ya leseni ya kuendeshea Makao ya Watoto waishio mitaani katika ngazi ya Jiji, manispaa, mji na halmashauri ya wilaya utakuwa ndani ya siku 60 ikiwa muombaji atakuwa amekidhi matakwa ya sheria; na utaratibu wa kuidhinishwa na kutolewa kwa leseni utakuwa ndani ya siku 45 kuanzia tarehe ya kupokea maombi katika ofisi ya Kamishna wa Ustawi wa Jamii. Masharti ya kuanzisha Makao ya Watoto waishiomitaani (i) (ii) (iii) (iv) (v) (vi) Mwombaji lazima awe na majengo imara na ya kudumu yaliyokusudiwa kuanzishwa makao ya watoto. Mwombaji lazima awe na hati ya kumiliki eneo yalipo majengo. Iwapo majengo ni ya kupanga mwombaji atalazimika kuwa na mkataba unaotoa muda wa mwaka mmoja kwa kutoa notisi iwapo mkataba utaisha. Majengo lazima yawe ya kudumu, bora na yenye hewa ya kutosha na yasiyo na vikwazo kwa watoto wenye ulemavu. Mwombaji sharti awe na rasilimali ya fedha inayoaminika na endelevu. Mwombaji hana budi kuwa na watumishi wa kutosha wenye staid za kusimamia na kuendesha makao ya watoto zikiwemo: Mawasiliano na watoto Stadi za Unasihi Stadi za Usaili Stadi za Kusimamia/uongozi Stadi za kuandika taarifa

(vii) Utabibu Asasi yoyote inayotaka kuanzisha Makao ya watoto inatakiwa kuwasilisha nakala ya hati ya usajili pamoja na katiba ya shirika \asasi vilivyoidhinishwa na aidha Kabidhi Wasihi Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na watoto au Wizara ya Mambo ya Ndani ambapo miongoni mwa mambo mengine madhumuni yake hayana budi yawe kuanzisha na kuendesha makao ya watoto. Mahali pa Makao ya Watoto a) Makao ya watoto shartiyawekwe katika eneo ambalo ni rahisi kupatiwa huduma muhimu na lisiloruhusu watoto kuwa katika athari mbaya na mienendo mibaya kutoka kwa jamii inayowazunguka, kwa mfano maeneo yaliyo karibu na vilabu vya pombe, vituo vya umeme, petroli, na gereji lazima kuwe na ukaguzi wa vifaa vya umeme vinavyoweza kuhatarisha usalama wa watoto (ii) Maeneo yasiwe na maafa yoyote yawe ya kibinadamu au ya asili (iv) Mahali pa majengo hapana budi kutajwa kwa uwazi wakati wa kuomba leseni (v) Iwapo kutafanyika upanuzi, marekebisho, ujenzi wa jengo jipya baada ya kupata leseni mwentye kleseni atamwarifu Kamishna kwa ajili ya ukaguzi na idhini ya kufanya hivyo. 6.0. USIMAMIZI WA MAKAO YA WATOTO Makao ya Watoto lazima yaajiri wafanyakazi wa kutosha na wenye sifa za lazima katika makundi yafuatayo: 6.1. Ofisa Mfawidhi Sifa (i) Lazima awe na shahada au stashahada ya juu katika taaluma ya Ustawi wa jamii

(ii) Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka 2 katika fani inayohusika. 6.1 Ofisa Mfawidhi Msaidizi Sifa (i) Lazima awe na Stashahada au Stashahada katika fani ya Usatwi wa jamii (ii) Uzoefu wa kazi usiopungua miaka miwili katika fani inayohusika. 6.1. Mlezi wa Watoto Sifa (i) Lazima awe amefaulu vizuri kidato cha Nne. (ii) Lazima awe na cheti katika fani ya ustawi wa jamii au mafunzo ya malezi ya watoto 6.1. Muuguzi wa Afya. Sifa (i) Lazima awe na cheti katika Tiba. 6.1. Wahudumu Kila Makao ya Watoto sharti yaweze kuajiri wahudumu kama viel wafagiaji, wapishi, watunza bustani, kutegemea na mahitaji Kwa mawasiliano Kamishna wa Ustawi wa Jamii S.L.P 1949 DAR ES SALAAM.