Muongozo wa utatuzi. Kwa wasimamizi wa malaria RDTs 06/11/16. MALARIA Rapid Diagnostic Test

Similar documents
Information for assessors (do not distribute this page to participants):

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig

Mfumo na maelezo ya kina ya mpango wa kimataifa wa viwango vya chakula kwa wenye matatizo ya kumeza (IDDSI) Juni 2017

Kifaa Maalum cha Kutazamia Jua: Maelekezo ya kutumia

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

TIST HABARI MOTO MOTO

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Hatari, Haki za Usalama katika Bahari 03

Utangulizi wa ugonjwa wa shinikizo la damu

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA. Kwa Wanaoanza

Njia za upimaji wa mpango wa kimataifa wa viwango vya chakula kwa wenye matatizo ya kumeza (IDDSI) VYAKULA VINYWAJI VYA KAWAIDA

JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti

HALMASHAURI YA WILAYA YA SUMBAWANGA

Mwongozo wa Kitaifa wa Ujumbe wa Uzazi wa Mpango

KUWEZESHA MBINU ZA UZUIAJI MIMBA KATIKA SUHULA ZA AFYA: MASWALI 10 KWA VIKUNDI VYA JAMII KUZINGATIA

Njia Bora za Ukusanyaji na Upimaji Maziwa

ORDER NO BACKGROUND

Ni kwa nini mkulima awe maskini?

Njia bora za ukusanyaji na upimaji maziwa

KILIMO CHA VITUNGUU MAJI NA VITUNGUU TWAUMU (SWAUMU)

Miradi na jamii. 3.1 Utangulizi

Programu ya Uendelezaji Mifumo ya Maji Vijijini (PUMMV) katika Tanzania. Modeli wa Ukodishaji Mradi

Vijana wanazungumza kuhusu ujinsia, maisha na uhusiano VIJANA WANAZUNGUMZA KUHUSU NGONO, MAISHA NA UHUSIANO. Training and Research Support Centre

Uzio wa pilipili unazuia tembo kuvamia mazao shambani! Jinsi ya kujenga na kudumisha uzio wa pilipili Tanzania

Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Utunzaji, Uhifadhi na Usafirishaji Bora wa Maziwa

Human Rights Are Universal And Yet...

Sera ya Faragha. Upeo. Aina za Data na Mbinu za Ukusanyaji

Siku ya kwanza. Mguso wa ngozi-kwa-ngozi (Ulezi wa kangaruu) Mtoto wako anaweza kuhisi mdundo wa moyo wako

Upande 1.0 Bajeti yako

USIMAMIZI MKUU WA UBORA WA MAHURUJI

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

Kuwawezesha wasichana kwa kuboresha kujikubali na kujithamini Hivi Ndivyo Nilivyo

2 Usimamizi wa Rutuba ya Udongo Tanzania Organic Agriculture Movement

Mazoezi yaliyofanyika wakati wa warsha kuhusu Elimu-Jumuishi kwa Vitendo. Zanzibar, 7-10 Februari 2006

Uzalishaji wa mboga na matunda ni muhimu kwa afya na kipato

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

TIST HABARI MOTO MOTO. Benefits of Loan Repayment. Faida za ulipaji wa mikopo U OTESHAJI W A M ITI Y A M ATUNDA

MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA PRO-ROUTES. Ombi kwa ajili ya fedha za umma wa mradi wa ziada

Shamba Darasa na Stadi za Maisha kwa Vijana (SDSMV) Tanzania. Kiongozi Cha Mwezeshaji. Jaap Van Pol na Francesca Dalla Valle

KUZALISHA MBEGU YA MAHARAGE KIJITABU CHA KWANZA

KUHUSU AFRODAD. Dira ya AFRODAD. Dhamira ya AFRODAD. AFRODAD inalenga mchakato sawa na endelevu wa maendeleo kuelekea Afrika yenye mafanikio.

Early Grade Reading Assessment for Kenya

Bustani 10,000 Katika Afrika. Alberto Prina

PYRINEX. 1 Liter INSECTICIDE

AMMA KWA AFRIKA RATIBA/ITIKADI. Ratiba Maalum ya Kutibu Magonjwa Maambukizi na Hususan Fikra Zinazoleta Pooza Mwili na Akili

Hakimiliki na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa TAFSIRI YA BIBLIA. Mwandishi. Jonathan M. Menn

MUONGOZO WA UTUNZAJI WA URITHI WA UTAMADUNI 1 SECURITY AT MUSEUMS

UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU VIKWAZO VYA KULINDA MAISHA KATIKA USAIDIZI WA KIMATAIFA WA AFYA KWA MSAADA WA KIMATAIFA UNAOFADHILIWA NA MAREKANI

Mipango ya miradi katika udugu

MWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI

ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA UCHUMI WA ZANZIBAR

KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA

pages/mkulima-mbunifu/

International Labour Office. Kazi za Ndani Zenye Madhara kwa Watoto: Kijitabu cha Maelezo Mafupi

Tora UTANGULIZI KWA TORA SOMO LA KWANZA

UFUATILIAJI WA MIRADI NA TATHMINI

Kuuelewa Mchakato wa Bajeti Tanzania Mwongozo wa Asasi za Kiraia

HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE

Deputy Minister for Finance

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu WEMA

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO

Usimulizi wa Riwaya ya Nyongo Mkalia Ini E. S. MOHOCHI University of Egerton, Kenya

Mwongozo wa Mafunzo Yaliyochanganywaya K4Health

ONDOA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA AFYA YA WATOTO

Usindikaji bora wa maziwa

Mwongozo wa Mwezeshaji

Kuwa na Ukimwi ni kama vile kutakiwa kuendelea kuuzima moto unaoniunguza bila kukoma.

Azimio lililopitishwa na Mkutano Mkuu tarehe 18 Desemba 2013 [juu ya taarifa ya Kamati ya Tatu (A/68/456/Add.2)]

Mwongozo wa Familia wa Kujifunza

Ufanisi katika Ufundishaji kwenye Shule za Msingi na Sekondari nchini Tanzania

Ufundishaji wa lugha nyingine

Mwongozo wa Jamii juu ya Afya ya Mazingira

Mwongozo wa Utamaduni Toleo la Kwanza

UMRI WA MAKAMO NA KUKOMA KWA HEDHI

TANZANIA TAARIFA YA MWISHO WA UTEKELEZAJI

Kitabu Cha Mafunzo Ya Uongozi Kwa Wanawake

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

CGAP Smallholder Household Survey in Tanzania / Utafiti wa kaya ndogondogo Tanzania

Mwongozo wa Utekelezaji wa Njia za S5-UUE (KAIZEN)-UUU Tanzania

RIPOTI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI

MAADHIMISHO YA MIAKA 15 YA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

N09/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q

JAMHURI YA KENYA. Mkakati wa Ushirikiano MUKHTASARI FY Public Disclosure Authorized. Public Disclosure Authorized

RIPOTI YA WARSHA KUHUSU HABARI KWA AJILI YA UWAJIBIKAJI

Uhakika wa Mbegu kwa Uhakika wa Chakula MWONGOZO WA UZALISHAJI WA MBEGU ZA ASILI ZA MAHINDI

Yaliyomo. Kuhusu kitabu hiki. Hautakuwa peke yako. Mfumo wa msaada ni wa manufaa sana wazazi wote wanahitaji!

Uwepo, Athari na Udhibiti wa Sumu-Suvu Kwenye Vyakula vya

KUPWA NA KUJAA KWA BAHARI. (TIDES AND TIME)

Kutetea Haki za Binadamu

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara

Kufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007

Transcription:

Muongozo wa utatuzi Kwa wasimamizi wa malaria RDTs MALARIA Rapid Diagnostic Test Device Umetengenezwa na FIND kwa kushirikiana na Johns Hopkins Bloomberg Shule ya Afya ya Jamii (JHSPH), ubia wa malaria (Malaria Consortium) na Shirika la kimataifa la huduma kwa Umma (Population Services International) kwa msaada wa fedha kutoka UNITAD. Baadhi ya michoro inatokana na vielelezo ainasafu (generic materials) vilivyopo kupitia; http://www.finddx.org/ implementation-tools/#malaria 06/11/16

Yaliyomo Sehemu ya 1: Utatuzi wa majibu ya RDT yasiyo ya kawaida...3 Sehemu ya 2: Utatuzi wa masuala ya vifaa ambata kwenye kit...13 Sehemu ya 3: Utatuzi wa masuala ya vifaa vya kuhamisha damu...16 Sehemu ya 4: Maelekezo ya kutatua matatizo...28 Utangulizi Mapendekezo ya kiutendaji kwa ajili ya kutatua matatizo yanayoweza kutokea wakati unatumia vipimo vya haraka vya uchunguzi wa malaria (Malaria RDTs), na unatoa maelekezo rahisi ya jinsi ya kufanya endapo matatizo hayataweza kutatuliwa. Mwongozo umesanifiwa kama kifaa saidizi kwa ajili ya mafunzo na usimamizi, utumike na wasimamizi ambao wanasimamia kazi za watumiaji wa RDT, katika mazingira ya huduma za afya ambapo RDTs zinatumika. Orodha ya matatizo imechaguliwa kutokana na uzoefu mkubwa kutoka katika nyanja mbalimbali za utafiti pamoja na mpango wa upimaji wa Lot za mrdt, hata hivyo haukujitosheleza kwa kina. Mapendekezo yoyote kwajili yamaboresho na ripoti zozote za matatizo ambazo hazijaainishwa kwenye muongozo huu, tafadhali zipelekwe kwa info@finddx.org Nukuu zinazopendekezwa: FIND, JHSPH, MC na PSI, 2015, Geneva, Switzerland. Muongozo wa utatuzi kwa wasimamizi wa malaria RDT. FIND 2015 haki zote zimehifadhiwa. Nyaraka hii ni huru kuiangalia, kudondoa, kunakili au kutafsiri, sehemu au yote endapo chanzo Msaada wa kutengeneza muongozo huu wa mafunzo umetolewa na UNITAD. Maoni yaliyotolewa ni jukumu pekee la waandishi na sio lazima kuwa yanatokana na sera za mashirika yanayotoa msaada wa kifedha. Shukrani: Shukrani za pekee kwa watu wote walioandika, kupitia na kurekebisha yaliyomo katika uchapishaji huu: Anderson Chinorumba (WHO), Cristina Lussiana (PSI), Daniel Kyabanyinze (FIND), Jane Cunningham (WHO), Kurt Mulholland (URC, Vielelezo), Mario Cabera (Mbunifu wa kitabu na vielelezo vya ziada), Sandra Incardona (FIND), Steve Harvey (JHSPH), (wengine watakaoongezwa) 2 Muongozo wa usuluhisho

Sehemu ya 1: Utatuzi wa majibu ya RDT yasiyo ya kawaida Kwaajili ya wasimamizi wanaosimamia watumiaji wa malaria RDT 3

Vipimo batili Matatizo ya Muundo Hakuna mstari wa udhibiti wala wa kipimo. Mstari wa udhibiti hakuna, lakini mstari wa kipimo upo na unaonekana. Stripu ya RDT ipo mahali pasiposahihi au umesogea mfano: umesogea kulia au kushoto au umesogea juu kiasi kwamba hauonekani kwenye shimo la sampuli. Majibu ya RDT ni batili Majibu ya RDT ni batili RDT haifai kutumika RDT nyingine ifunguliwe rudia kipimo. Kama tatizo litaendelea, fuata maelekezo sehemu ya 4. RDT nyingine ifunguliwe rudia kipimo. Kama tatizo litaendelea, fuatilia maelekezo sehemu ya 4. 4 Muongozo wa usuluhisho

Wekundu kwenye dirisha la kusomea majibu Wekundu mwepesi. Mistari ya kipimo na udhibitii ipo na inaonekana. Wekundu mwepesi. Mstari wa udhibiti upo. Mstari wa kipimo hakuna lakini haujafichwa na wekundu. Wekundu mzito. Mstari wa udhibiti upo na unaonekana, lakini mstari wa kipimo umefichwa na wekundu. Majibu chanya ya RDT Majibu hasi ya RDT Majibu ya kipimo sio ya uhakika RDT nyingine ifunguliwe na kipimo kirudiwe. Kama tatizo litaendelea, fuata maelekezo sehemu ya 4. Kwaajili ya wasimamizi wanaosimamia watumiaji wa malaria RDT 5

Kutotakata kikamilifu (Doa jekundu) Doa jekundu lisilozuia mistari ya kipimo na udhibiti. Mistari yote ya udhibiti ya kipimo ipo na inaonekana. Doa jekundu lisilozuia mistari ya kipimo na udhibiti. Mstari wa udhibiti unaonekana lakini mstari wa kipimo haupo. Doa jekundu lipo sehemu ambapo mstari wa kipimo unatakuwa kuwepo. Mstari wa udhibiti unaonekana lakini uwepo au kutokuwepo kwa mstari wa kipimo haujulikani. Majibu Chanya ya RDT Majibu hasi ya RDT Majibu ya kipimo sio ya uhakika RDT nyingine ifunguliwe na kipimo kirudiwe. Kama tatizo litaendelea, fuata maelekezo sehemu ya 4. 6 Muongozo wa usuluhisho

Kushindikana kutiririka Damu na buffer havikufika hadi mwisho wa stripu. Mstari wa kipimo upo na unaonekana lakini hakuna mstari wa udhibiti. Damu na bafa havikufika urefu wa stripu. Hakuna mstari wa udhibiti na hakuna mstarii wa kipimo. MAJIBU YA RDT NI BATILI MAJIBU YA RDT NI BATILI RDT nyingine inatakiwa ifunguliwe na kipimo kirudiwe. Kama tatizo likiendelea, fuata maelekezo sehemu ya 4. RDT nyingine inatakiwa ifunguliwe na kipimo kirudiwe. Kama tatizo likiendelea, fuata maelekezo sehemu ya 4. Kwaajili ya wasimamizi wanaosimamia watumiaji wa malaria RDT 7

Mstari wa kipimo umesambaa Mstari wa kipimo hafifu -umevunjika Mstari wa kipimo ni mpana kuliko mstari wa udhibiti, bila kuwa na mipaka ya uhakika. Mstari wa kipimo unaonekana lakini haujakamilika (umevunjika). Mistari ya kipimo upo hata kama ni mipana/ haina mipaka ya uhakika=> Majibu chanya ya RDT. Upo hata kama haijakamilika => Majibu ya RDT ni chanya. 8 Muongozo wa usuluhisho

Matatizo yanayoweza kutokea Wekundu kwenye dirisha la kusomea majibu au kutotakata kabisa Visababishi wezekana Damu nyingi kupita kias Buffer kidogo Kusoma kabla ya muda kutimu Damu na buffer kushindwa kutiririka Damu haitoshi Utoaji wa damu wa polepole mno (kuganda kwa damu) au mabaki ya pamba Majibu hasi potofu Damu kidogo Buffer nyingi kupita kiasi Kusoma majibu kabla ya muda Kwaajili ya wasimamizi wanaosimamia watumiaji wa malaria RDT 9

kidole cha 4 cha mkono wa kushoto wa mgonjwa. Safisha kidole kwa pamba ya alkoholi, acha kidole kikauke kabla ya ku to b o a la damu kwenye tundu lililoandikwa h e r u fi A m g o n j w a k u p a t a t o n e l a d a m u. U s i r u h u s u n c h a y a s i n d a n o i g u s e kitu chochote kabla ya kutoboa kidole cha mgonjwa l a v i f a a v y a n c h a k a l i c. Desiccant sachet kwenye boksi la vifaa vya ncha kali mara tu utakapomaliza kutoboa kidole. Usiweke chini sindano kabla hujaitupa duara lililoandikwa herufi B h e s a b u k w a u s a h i h i nambari ya matone la damu kuongeza bafa Usisome kipimo kabla ya dakika 1 5 m a r a b a a d a y a k u o n g e z a b a f a. Unaweza kupata majibu potofu) Vidokezo vichache kwa ajili ya kutatua matatizo (1/3) Utaratibu sahihi wa RDT Angalia tena maelezo katika muongozo wa utendaji wa kazi (job aid): - Kiasi cha damu? - Kiasi cha buffer? - Muda wa kusoma? 5. Fungua pamba ya alkoholi, shikilia 9. T u m i a t u b u y a k a p i l a r i k u w e k a t o n e 1 4. H o w t o r e a d t h e t e s t r e s u l t s : 6. Fungua sindano. Toboa kidole cha 1 0. Tupa tubu ya kapilari kwenye boksi 7. Tupa sindano 1 1. Ongeza bafa kwenye tundu la 8. T u m i a t u b u y a k a p i l a r i k u c h u k u a t o n e 1 2. Subiri dakika 15 baada ya 1 3. S o m a m a j i b u y a k i p i m o ( A n g a l i z o : Uchukuaji sahihi na kiasi sahihi cha damu Safisha kidole vizuri, hakikisha hakuna mabaki ya alkoholi wala pamba Utumiaji sahihi wa kifaa cha kuhamisha damu Damu kidogo mno Damu kidogo mno Kiwango sahihi cha damu kiwango sahihi cha damu Damu nyingi mno Damu nyingi 10 Muongozo wa usuluhisho

Vidokezo vichache kwa ajili ya kutatua matatizo (2/3) Kiasi sahihi cha buffer Kwa kitabakero, buffer iko kwenye sehemu au juu ya sehemu yenye mshale mwekundu; kwa kichupa, hesabu kwa usahihi idadi ya matone kama ilivyoainishwa kwenye maagizo ya mtengenezaji. Hesabu kwa usahihi nambari ya matone Muda sahihi wa kusoma na kutafsiri mistari ya kipimo Subiri muda sahihi ufike kabla ya kusoma majibu ya kipimo (kati ya dakika 15-20) kulingana na maagizo ya mtengenezaji. Hata mstari uliofifia ni majibu chanya ya kipimo ili mradi mstari wa udhibiti upo. Kwaajili ya wasimamizi wanaosimamia watumiaji wa malaria RDT 11

Vidokezo vichache kwa ajili ya kutatua matatizo (3/3) Utafsiri sahihi wa dalili Angalia kwa dhati muongozo wa huduma za mgonjwa, 1 tafsiri majibu ya kipimo kutokana na historia na dalili za mgonjwa. 1 Chati tiriri hii ni kwaajili ya kuonyesha mfano tu, miongozo ya kitaifa ya matibabu/kutibu ugonjwa inatakiwa kufuatwa. Hali nzuri ya ubora wa hadubini (Kama imefanyika kwa mgonjwa huyo huyo) Kama hadubini ilitumika kuangalia kipimo cha mgonjwa huyo huyo, hakiki ubora wake (uwezo, kuaminika n.k kwa hadubini) na tafsiri tofauti za vipimo kwa kuzingatia mazingira hayo. 12 Muongozo wa usuluhisho

Sehemu ya 2: Utatuzi wa masuala ya vifaa ambata kwenye kit Kwaajili ya wasimamizi wanaosimamia watumiaji wa malaria RDT 13

Vifaa vya ziada: Jinsi ya kutumia maelekezo, matatizo yanayoweza kutokea na mapendekezo (1/2) Pamba ya alkoholi Fungua pakiti ya pamba ya alkoholi muda mfupi kabla ya matumizi. Futa kidole cha mgonjwa na acha kikauke kwa upepo. Usipulize kidole na usitumie kitambaa au kipande cha karatasi kukausha kwasababu umaweza kuchafua kidole. Kama pamba ya alkoholi imekauka: tumia pamba nyingine ya alkoholi. Kama hali hiyo ikijirudia, mtaarifu msimamizi au mhusika (maelezo Zaidi yapo sehemu ya 4). Kifaa chenye ncha kali (Lancet) Fig. 1 14 Muongozo wa usuluhisho Fungua pakiti ya kifaa cha ncha kali muda mfupi kabla ya matumizi. Toboa kidole ch mgonjwa na futa tone la kwanza la damu. Ruhusu kidole kikauke kabisa (alkoholi inaweza kuingiliana na kipimo). Tupa kifaa cha ncha kali kwenye boksi la taka za ncha kali mara tu unapomaliza kumtoboa mgonjwa. Kama tone la damu ni dogo mno: muambie mgonjwa asugue mikono pamoja ili kuwezesha damu kutembea. Polepole kamua kidole kwa kukisukuma kuelekea kwenye sehemu ya juu ya kidole ili kutengeneza tone kubwa. Toboa kwa hali ya haraka (kutoboa kidogo tu kunatoa matone madogo), kwenye upande wa kidole (kama inavyoonyeshwa kwenye picha 1). Kamua polepole kidole kutengeneza tone kubwa la damu.

Vifaa vya ziada: Jinsi ya kutumia maelekezo, matatizo yanayoweza kutokea na mapendekezo (2/2) Chupa ya bafa Kichupa kidogo cha bafa Kwa chupa na vichupa vidogo vya bafa Chupa inatakiwa kuwa na kiasi cha kutosha kwaajili ya vipimo vyote katika boksi. Rangi inatakiwa iwe thabiti (Kama inaweza kuonekana kwa mfano kwenye chupa yenye uwazi). Kabla ya kufungua kichupa kidogo, gonga kuhakikisha bafa yote imetulia. Kichupa kidogo kinatakiwa kiwe na bafa ya kutosha kwaajili ya kipimo kimoja. Rangi na kiasi vinatakiwa viwe thabiti kwa vichupa vidogo vyote. Shikilia chupa/kichupa kidogo wima, kamua polepole na taratibu ili kuwezesha matone kudondoka kwa uhuru, hesabu namba kamili ya matone kama inavyopendekezwa katika upimaji. Kama kuna kiasi kisichotosheleza au utupu katika chupa au vichupa vidogo, au kama rangi ya bafa si ya kawaida (Utafauti kati ya chupa au vichupa vidogo kutoka kwenye loti moja ya RDT): Tumia chupa nyingine au kichupa kidogo kingine kutoka katika loti nyingine (Hata kama ni toleo au bidhaa ya aina moja), au kutoka kwenye bidhaa ya RDT nyingine (hata kama ni RDT kwaajili ya malaria, au RDT kutoka kwa mtengenezaji huyo huyo), na usitumie maji kamwe. Katika hali yoyote; fuata maelekezo katika sehemu namba 4. Kwaajili ya wasimamizi wanaosimamia watumiaji wa malaria RDT 15

Sehemu ya 3: Utatuzi wa masuala ya vifaa vya kuhamisha damu 16 Muongozo wa usuluhisho

Vifaa vya kuhamisha damu: Maelezo jinsi ya kutumia (Maelekezo ya kina na mapendekezo katika kurasa 18-27) Taratibu bonyeza kifaa kabla ya kugusa tone la damu, kisha chukua damu mpaka juu kwenye alama (ya kwanza) kwa kuachia presha taratibu na polepole. Kifyonza sanifu mrija kifyonza kinachobonyezeka Wakati wa kuchukua damu usiachie presha kwa ghafla mno na usinyanyue kifaa kwani unaweza kusababisha matone ya hewa kuingia. Gusa tone la damu kwa ncha ya lupu na acha lupu ijae damu kikamilifu. tubu ya kapilari Hakikisha kiasi kizuri cha tone la damu na mgusano mzuri na uwazi wa chini wa lupu kuijaza. Shikilia tubu ya kapilari wima, weka ncha ya tubu ya kapilari kwenye tone la damu na acha ipande mpaka kwenye alama. Lupu Usisogeze kifaa na usikinyanyue wakati wa kuchota damu, kisha kinyanyue mara tu damu itakapofika kwenye alama. Appuyez sur la goutte de sang avec la pointe de la coupe et laissez la coupe se remplir complètement avec le sang. kikombe mgeuzo Usigandamize kikombe kwenye kidole ila gusa tone la damu taratibu. Acha ijae bila kukisogeza au kukinyanyua. Kwaajili ya wasimamizi wanaosimamia watumiaji wa malaria RDT 17

Tubu ya kapilari (1/2) Kutoboa kidole Kupata tone kubwa zuri: kabla ya kutoboa, kanda kidole ili kusisimua mzunguko wa damu. Toboa kidole cha mgonjwa kwa haraka na uthabiti. Taratibu kamua kidole kupata damu ya kutosha. Kuchukua damu Hakikisha kiasi kizuri cha tone kipo kwenye kidole kabla ya kuchukua damu. Weka ncha ya tubu ya kapilari juu ya tone la damu kwa kukishikilia wima. Acha damu ipande moja kwa moja mpaka ifike kwenye alama. Angalizo: Usichukue damu mara mbili kwa kutumia kifaa kimoja endapo uchukuaji damu utashindikana; ni lazima utumie kifaa kipya. Kuhamisha Wakati wa kuhamisha kutoka kwenye kidole kwenda kwenye RDTs, usifanye mahangaiko yoyote ya ghafla na usiguse kitu chochote kwa kutumia kifaa cha kuhamisha damu (chochote kati ya hivyo kinaweza kusababisha kumwagika kwa damu kutoka kwenye kifaa). 18 Muongozo wa usuluhisho

Tubu ya kapilari (2/2) Kuweka damu Ongeza damu kwenye shimo la sampuli ya RDT kwa kushikilia tubu ya kapilari wima. Ncha ya tubu inahitajika kugusana vizuri na stripu ya RDT mpaka kiasi chote cha damu kitakapochotewa kwenye pedi ya RDT. Matatizo yanayoweza kutokea Kuna matone ya hewa kwenye kifaa. Ni vigumu kupata damu sahihi kufika kwenye alama. Suluhisho Wakati wa kuchota damu kwenye kifaa, usikisogeze au kukinyanyua, kwani hii inaweza kusababisha hewa kuingia. Weka kifaa wima, kigusane na damu, bila kukandamiza kwenye kidole: damu itaenda polepole kupanda juu kwasababu ya msukumo wa kapilari. Mara tu damu ifikapo kwenye alama, nyanyua kifaa: hii itasaidia kuzuia damu isizidi juu ya alama. Kwaajili ya wasimamizi wanaosimamia watumiaji wa malaria RDT 19

Kifyonza (1/2) Kutoboa kidole Kupata tone kubwa zuri: kabla ya kutoboa, kanda kidole ili kusisimua mzunguko wa damu. Toboa kidole cha mgonjwa kwa haraka na uthabiti. Taratibu kamua kidole kupata damu ya kutosha. Kuchukua damu Hakikisha kiasi kizuri cha tone kipo kwenye kidole kabla ya kuchukua damu. Taratibu bonyeza balbu, kisha taratibu weka ncha yake kwenye tone la damu (usikandamize kwenye kidole). Taratibu na polepole achia presha kwenye balbu kuchota damu mpaka ifike kwenye alama, kisha nyanyua kifyonza na hamisha. Angalizo: usichukue camu mara mbili kwa kutumia kifaa kimoja cha kuhamisha endapo kuchukua damu kukishindikana: ni lazima utumie kipya. Kuhamisha Wakati wa kuhamisha kutoka kwenye kidole kwenda kwenye RDTs, usifanye mihangaiko ya aina yoyote kwa ghafla na usiguse kitu chochote kwa kutumia kifaa cha kuhamisha (chochote kati ya hivi kinaweza kusababisha kumwagika kwa damu kutoka kwenye kifaa). 20 Muongozo wa usuluhisho

Kifyonza (2/2) Kuweka damu Ongeza damu kwenye shimo la sampuli ya RDT kwa kushikilia kifyonza wima. Ncha ya kifyonza inahitaji kugusana na stripu ya RDT. Taratibu bonyeza balbu ya kifyonza mpaka kiasi chote cha damu kimechotewa kwenye RDT. Matatizo yanayoweza kutokea Kuna matone ya hewa kwenye kifaa. Ni vigumu kupata damu sahihi mpaka kwenye alama. Damu inabaki imekwama kwenye kifyonza. Suluhisho Wakati wa kuchota damu, weka kifaa vizuri kiguse damu na usikinyanyue kwani inaweza kusababisha matone ya hewa kuingia. Mara tu damu inapofika kwenye alama, nyanyua kifaa: hii itazuia kuchota damu zaidi ya kwenye alama. Usibonyeze balbu ya kifyonza kwa nguvu mno na usiachie kwa ghafla mno wakati wa kuchota damu kwani inaweza kutengeneza mfyonzo wa nguvu wa damu na itabaki imekwama kwenye kifyonza. Kwaajili ya wasimamizi wanaosimamia watumiaji wa malaria RDT 21

Kufyoza kinachobonyezeka (1/2) Kutoboa kidole Kupata tone zuri kubwa: kabla ya kutoboa, kanda kidole kusisimua mzunguko wa damu. Toboa kidole cha mgonjwa haraka na kwa uthabiti. Taratibu kamua kidole kupata damu ya kutosha. Kuchukua damu Hakikisha kiasi kizuri cha tone kipo kwenye kidole kabla ya kuchukua damu. Taratibu kamua balbu ya kifyoza, kisha taratibu weka ncha kwenye tone la damu (usigandamize kwenye kidole). Taratibu na polepole achia presha kwenye balbu ili kuchota damu mpaka ifikapo kwenye alam ya kwanza kisha nyanyua kifyonza kwaajili ya kuhamisha. Angalizo: Usichote damu mara mbili kwa kutumia kifaa kimoja endapo uchukuaji utashindikana: unatakiwa kutumia kifaa kipya. Kuahamisha Wakati wa kuhamisha kutoka kwenye kidole kwenda kwenye RDT, usifanye mahangaiko ya aina yoyote ya ghafla na usiguse kitu chochote na kifaa cha kuhamishia (chochote kati ya hivi vinaweza kusababisha kumwagika kwa damu kutoka kwenye kifaa. 22 Muongozo wa usuluhisho

Kufyoza kinachobonyezeka (2/2) Kuweka damu Ongeza damu kwenye shimo la sampuli ya RDT kwa kushikilia kifyonza wima. Ncha ya kifyonza inahitajika kugusana na stripu ya RDT. Taratibu kamua balbu ya kifyonza mpaka kiasi chote cha damu kitakapo chotewa kwenye RDT. Matatizo yanayoweza kutokea Kuna matone ya hewa kwenye kifaa. Ni vigumu kupata damu sahihi mpaka kwenye alama ya kwanza. Damu inabaki imekwama kwenye kifyoza. Suluhisho Wakati wa kuchota damu, weka kifaa kigusane vizuri na damu na usikinyanyue kwani kinaweza kuruhusu matone ya hewa kuingia. Mara tu damu inapofika kwenye alama ya kwanza nyanyua kifaa: hii itaepusha kuchota damu Zaidi ya kwenye alama. Usibonyeze balbu ya kifyonza kwanguvu mno na usiachie kwa ghafla mno wakati wa kuchota damu, kwani inaweza kuleta mfyonzo wa nguvu wa damu hivyo itabaki imekwama kwenye kifyoza. Kwaajili ya wasimamizi wanaosimamia watumiaji wa malaria RDT 23

Lupu (1/2) Kutoboa kidole Kupata tone kubwa zuri: kabla ya kutoboa, kanda kidole kusisimua mzunguko wa damu. Toboa kidole cha mgonjwa kwa haraka na kwa uthabiti. Polepole kamua kidole kupata damu ya kutosha. Kuchukua damu Hakikisha kiasi kizuri cha tone lipo kwenye kidole kabla ya kuchukua damu. Shikilia kidole cha mgonjwa wakati tone la damu likiangalia chini, kisha gusa tone la damu kwa ncha ya lupu na acha lupu ijae damu. Nyanyua kifaa mara tu lupu itakapokuwa imekamilika kujaa damu. Angalizo: Usichukue damu mara mbili ka kutumia kifaa kimoja cha kuhamishia damu endapo uchukuaji ulishindikana: ni lazima utumie kifaa kipya. Kuhamisha Wakati wa kuhamisha kutoka kwenye kidole kwenda kwenye RDTs, usifanye mihangaiko yoyote na usiguse kitu chochote kwa kutumia kifa cha kuhamisha (chochote kati ya hivi kinaweza kusababisha kumwagika kwa damu kutoka kwenye kifaa). 24 Muongozo wa usuluhisho

Lupu (2/2) Kuweka damu Ongeza damu kwenye shimo la sampuli ya RDT kwa kushikilia kifaa katika pembe kama ilivyoonyeshwa kwenye picha na polepole gandamiza lupu kwenye stripu. Endeleza mgusano mpaka kiasi chote cha damu kimechotwa. Matatizo yanayoweza kutokea Ni vigumu kujaza damu kwenye lupu kikamilifu. Ni vigumu kuachia kiasi chote cha samu kwenye RDT. Suluhisho Kwa kuchukua damu, hakikisha unatone kubwa la damu na kuna mguso mzuri kati ya tone na sehemu ya mwishoni ya lupu. Wakati wa kuchota damu, usisogeze kifaa na usikinyanyue mpaka lupu itakapojaa damu kikamilifu. Kwa kuweka damu, upande ulioko wazi wa ncha ya lupu inahitaji kugusa pedi ya sampuli ya RDT. Usisogeze kifaa mpaka pale damu itakapokuwa imefyonzwa na pedi ya RDT. Kwaajili ya wasimamizi wanaosimamia watumiaji wa malaria RDT 25

Kikombe Mgeuzo (1/2) Kutoboa kidole Kupata tone kubwa zuri: kabla ya kutoboa, kanda kidole kusisimua mzunguko wa damu. Toboa kidole cha mgonjwa kwa haraka na kwa uthabiti. Polepole kamua kidole kupata damu ya kutosha. Kuchukua damu Hakikisha tone la kiasi kizuri liko kwenye kidole kabla ya kuchukua damu. Weka ncha ya kifaa cha kikombe mgeuzo kwenye tone la damu, kwa kushikilia wima kikombe mgeuzo. Damu itafyonzwa moja kwa moja. Nyanyua kikombe pale tu kimeshajaa damu. Angalizo: Usichukue damu mara mbili kwa kutumia kifaa kimoja cha kuhamisha damu iwapo uchukuaji umeshindikana: unatakiwa utumie kipya. Kuhamisha Wakati wa kuhamisha kutoka kwenye kidole kwenda kwenye RDT, usifanye mahangaiko yoyote ya ghafla na usiguse kitu chochote kwa kutumia kifaa cha kuhamisha (Vyovyote kati ya hivi vinaweza kusababisha umwagikaji wa damu kutoka kwenye kifaa). 26 Muongozo wa usuluhisho

Kikombe Mgeuzo (2/2) Kuweka damu Ongeza damu kwenye shimo la sampuli ya RDT kwa kushikilia kikombe mgeuzo wima. Sehemu ya chini ya kikombe inahitaji kugusana vizuri na stripu ya RDT. Subiri mpaka Kiasi chote cha damu kimechotwa na kuwekwa kwenye stripu. Matatizo yanayoweza kutokea Ni vigumu kujaza kabisa damu kwenye kikombe. Suluhisho Kwa kuchukua damu, hakikisha unapata tone kubwa la damu. Kikombe kiwekwe polepole juu ya tone la damu na sio kugandamiza kwenye kidole lasi hivyo haitajaa damu na kiasi hakitakuwa sahihi. Ni vigumu kuachia kiasi chote cha damu kwenye RDT. Kwa damu iliyowekwa, Shikilia kifaa wima: Kama upande mmoja tu wa kikombe unagusa pedi ya RDT, damu haitatolewa vizuri. Kwaajili ya wasimamizi wanaosimamia watumiaji wa malaria RDT 27

Sehemu ya 4: Maelekezo ya kutatua matatizo 28 Muongozo wa usuluhisho

Kama tatizo linatokea kwa kesi chache Chache inamaanisha chini ya 10% ya kesi (mfano; vipimo au vifaa vya ziada chini ya vitatu vinamatatizo, kutoka boksi namba 25) Msimamizi atumie muongozo wa usuluhisho kutambua na kutatua matatizo kwa kushirikiana na mtumiaji wa RDT Msimamizi afanye mafunzo rejea, kulenga vyanzo vya matatizo na kusisitiza hatua muhimu za upimaji kwa RDT Mhakikishie mtumiaji wa RDT kuwa matatizo kama ya vipimo batili, kitengelenyuma chenye rangi nyekundu iliyo hafifu, n.k yanaweza kutokea mara chache Angalizo: Matizo ya chupa/vichupa vidogo vya bafa (mfano; kuwa kappa au kuwa na kiasi kisicho cha kutosha) inatakiwa kila wakati zitolewe ripoti kwa mhusika mteule wa kuwasiliana nae (Angalia ukurasa unaofuata). Kwaajili ya wasimamizi wanaosimamia watumiaji wa malaria RDT 29

Kama tatizo litaendelea au ni muhimu au linajirudia mara kwa mara Mara kwa mara inamaanisha zaidi ya 10% ya kesi (mfano vipimo/vifaa vya ziada vitatu au Zaidi venye matatizo, kutoka boksi namba 25) Mtiririko wa hatua Jaza fomu ya ripoti kwa kushirikiana na mtumiaji wa RDT Nani wa kuripoti kwake Jina: Cheo: Nambari ya simu: Piga picha na kusanya sampuli za RDT au vifaa vya ziada venye matatizo Jina: Cheo: Nambari ya simu: Ripoti matatizo kwa mratibu wa utambuzi au mzibiti ubora (QA/QC) Kama umeelekezwa fanya utafiti wa matatizo yanayofanana na ya watumiaji wengine wa RDT Jina: Cheo: Nambari ya simu: Jina: Cheo: Nambari ya simu: 30 Muongozo wa usuluhisho

Karatasi ya hesabu ya kurekodi matatizo Tarehe ya leo Jina la sehemu au mlango/utambulisho Jina la bidhaa ya RDT Nambari ya bechi la RDT Hatua iliyochukuliwa 1 2 3 4 5 6 7 Matatizo yameripotiwa kwa; (Jina), wakati: (Tarehe) Kwaajili ya wasimamizi wanaosimamia watumiaji wa malaria RDT 31

Karatasi ya hesabu ya kurekodi matatizo Tarehe ya leo Jina la sehemu au mlango/utambulisho Jina la bidhaa ya RDT Nambari ya bechi la RDT Hatua iliyochukuliwa 1 2 3 4 5 6 7 Matatizo yameripotiwa kwa; (Jina), wakati: (Tarehe) 32 Muongozo wa usuluhisho

Karatasi ya hesabu ya kurekodi matatizo Tarehe ya leo Jina la sehemu au mlango/utambulisho Jina la bidhaa ya RDT Nambari ya bechi la RDT Hatua iliyochukuliwa 1 2 3 4 5 6 7 Matatizo yameripotiwa kwa; (Jina), wakati: (Tarehe) Kwaajili ya wasimamizi wanaosimamia watumiaji wa malaria RDT 33

MALARIA RDT Muongozo wa usuluhisho Kwaajili ya wasimamizi wanaosimamia watumiaji wa malaria RDTs http://www.finddx.org/implementation-tools/#malaria