JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAGU

Similar documents
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI-TAMISEMI HALMASHAURI YA WILAYA BUMBULI

JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI-TAMISEMI

HALMASHAURI YA WILAYA YA SUMBAWANGA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. OFISI YA RAIS- TAMISEMI.

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA IRINGA SHULE YA SEKONDARI TOSAMAGANGA

Kumb.Na.BSS/A.6/33 Tarehe: 18 Juni 2018 YAH: MAAGIZO YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2018/2019

JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA

JAMHURI YA MUUNGANO IVA TANZANIA

2018/2019 OFISI YA RAIS-TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

YAH: MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI WERUWERU HALMASHAURI YA MOSHI MKOA WA KILIMANJARO MWAKA 2018

JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI HALMASHAURI YA MANISPAA YA MPANDA SHULE YA SEKONDARI RUNGWA

YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS - TAMISEMI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

YAH: MAAGIZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI KAREMA KIDATO CHA TANO MWAKA 2018

SHULE YA SEKONDARI KIBAHA S.L.P 30053, KIBAHA SIMU NA Kibaha

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MANISPAA YA BUKOBA.

Information for assessors (do not distribute this page to participants):

FOMU YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO

ARCHDIOCESE OF MWANZA

Kumb.Na.HVEMS/JI/BT/018 Novemba 17, YAH: MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE CHINI YA TAASISI YA ROCK MEMORIAL EDUCATION TRUST 2018

KAWAWA JKT HIGH SCHOOL PO.BOX 213 MAFINGA IRINGA PHONE MOBILE, , , ,

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1

NAFASI ZA MASOMO MASOMO YA ASUBUHI

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig

Nilikua na Ndoto ya Kumaliza Shule Changamoto za Elimu ya Sekondari Tanzania

KITEGO CHA MAREKEBISHO NA HAKI ZA MTOTO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO

Ufanisi katika Ufundishaji kwenye Shule za Msingi na Sekondari nchini Tanzania

SautiElimu. Sauti Yako Isikike

Mwongozo wa Familia wa Kujifunza

Human Rights Are Universal And Yet...

MWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI

Hatari, Haki za Usalama katika Bahari 03

MTIHANI WA MWIGO WILAYA YA BUTERE MUMIAS-2007 Hati ya kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya

UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU VIKWAZO VYA KULINDA MAISHA KATIKA USAIDIZI WA KIMATAIFA WA AFYA KWA MSAADA WA KIMATAIFA UNAOFADHILIWA NA MAREKANI

PDF created with pdffactory trial version

Tufundishane! Mwalimu Bora In this issue: Issue 6, December Do you want to be in our next issue?

Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi

KANUNI ZA MAADILI MWONGOZO WA WANAFUNZI

KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA

Uzio wa pilipili unazuia tembo kuvamia mazao shambani! Jinsi ya kujenga na kudumisha uzio wa pilipili Tanzania

KIJARIDA JUU YA HAKI ZA RAIA KATIKA MFUMO JINAI

JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI

SANIFU KWA SHULE ZA SEKONDARI KITABU CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO

Hati ya Kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya.( K.C.S.E)

Elimu-Jumuishi Kwa Vitendo

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees

Adhabu ya jino kwa jino na Musitakabali wa imani zetu

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level

MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA PRO-ROUTES. Ombi kwa ajili ya fedha za umma wa mradi wa ziada

Azimio lililopitishwa na Mkutano Mkuu tarehe 18 Desemba 2013 [juu ya taarifa ya Kamati ya Tatu (A/68/456/Add.2)]

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

Sera ya Faragha. Upeo. Aina za Data na Mbinu za Ukusanyaji

KAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI TANZANIA

Deutsche Welle, Learning by Ear 2009 Seite 1 People Who Make A Difference Liberia: Anita Varney Health Facilitator, Fishtown/Liberia

MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2017/18

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA

ORODHA YA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI SPIKA MHE. PANDU AMEIR KIFICHO. Rais.

5. Mheshimiwa Spika, Bunge lako Tukufu lilijadili kwa kina Miswada ifuatayo:

Kijitabu cha Maelezo cha Programu ya Famasia

Early Grade Reading Assessment for Kenya

International Labour Office. Kazi za Ndani Zenye Madhara kwa Watoto: Kijitabu cha Maelezo Mafupi

MAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI

MAFUNZO YA AFYA YA UZAZI: Nyongeza ya Mtalaa Kwa vijana

Elimu Bora, lakini... C HakiElimu Elimu bora, lakini...

13 APRILI, 2012 BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA SABA. Kikao cha Nne Tarehe 13 Aprili, (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A

Mazoezi yaliyofanyika wakati wa warsha kuhusu Elimu-Jumuishi kwa Vitendo. Zanzibar, 7-10 Februari 2006

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

Vijana wanazungumza kuhusu ujinsia, maisha na uhusiano VIJANA WANAZUNGUMZA KUHUSU NGONO, MAISHA NA UHUSIANO. Training and Research Support Centre

4. Kanuni za Petroli (Ushiriki wa Watanzania) za mwaka 2017 zilianza kutumika rasmi tarehe 5 Novermba Shughuli za Petroli za kwanza ni

Upande 1.0 Bajeti yako

MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA. Kwa Wanaoanza

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

Kocha Mkuu. mabingwa. itakuwa INASTAHILI. Ili Kutoa mafunzo kwa wanafunzi wako kuwa. itakuwa ya kuumiza. Itachukua muda. Itahitaji moyo wa kujitoa.

Deputy Minister for Finance

LUGHA YA KISWAHILI KATIKA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA ELIMU SHULE ZA SEKONDARI

ORDER NO BACKGROUND

CGAP Smallholder Household Survey in Tanzania / Utafiti wa kaya ndogondogo Tanzania

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

TANZANIA MARKETS PAN Sera zinazoboresha masoko

RIPOTI YA WARSHA KUHUSU HABARI KWA AJILI YA UWAJIBIKAJI

Bustani 10,000 Katika Afrika. Alberto Prina

RIPOTI YA KAMATI TEULE YA KUCHUNGUZA UPOTEVU WA NYARAKA ULIOTOKEA KATIKA TAASISI YA NYARAKA NA KUMBUKUMBU ZA TAIFA ZANZIBAR.

Mhashamu Askofu Jude Thaddaeus Ruwa ichi, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania; Mwadhama Policarp Kardinali Pengo,

Elimu Ina Umuhimu gani katika Jamii? Kuelekea Elimu Sahihi

Kimesanifiwa na:- E.D.Kissuu ECOMM TANZANIA S.L.P ,Dar es Salaam. Simu:

Banana Investments Ltd

Kuwawezesha wasichana kwa kuboresha kujikubali na kujithamini Hivi Ndivyo Nilivyo

Transcription:

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAGU NAMBA ZA SIMU. MKUU WA SHULE: 0754 912 801 MAKAMU MKUU WA SHULE: 0765620813/0714556568 MATRON :0788070645 MTAALUMA: 0755 543 484. Email; magusecondary@yahoo.com SHULE YA SEKONDARI MAGU, S.L.P 186, MAGU. 10/06/2017. MAZAZI/MLEZI WA MWANAFUNZI S.L.P.. YAH: MAELEKEZO YA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO SHULE YA SEKONDARI MAGU HALMASHAURI YA MAGU MKOA WA MWANZA 2017. 1. Nafurahi kukutaarifu kuwa mwanao amechaguliwa kujiunga na kidato cha tano katika shule hii mwaka 2017/2018 tahasusi ya. Shule ya Sekondari ya Magu ipo umbali wa Km 2 magharibi mwa mji wa Magu. Usafiri wa mabasi kutoka mwanza mjini unapatikana katika kituo cha mabasi cha Buzuruga nauli ni Tsh. 3000/=. Kwa wanaotoka Musoma, shuka stend ya mabasi ya magu panda usafiri wa Pikipiki kwa nauli ya Tsh. 1000/= hadi shuleni. Muhula wa masomo unaanza tarehe 17/07/2017. Hivyo mwanafunzi anatakiwa kuripoti shuleni tarehe hiyo. Mwisho wa kuripoti ni tarehe 30/07/2017.

2. Mambo muhimu ya kuzingatia 2.1 sare ya shule:- a) Sare ya Shule hii ni:- i. shati mbili TETRON rangi nyeupe mikono mirefu ambazo hazibani mwili na ziwe na mfuko mmoja tu kushoto. ( zitavaliwa kwa kuchomekewa) ii. kwa wavulana:- suruali mbili rangi ya DARK BLUE zenye malinda mawili ya cross pembeni, mfuko mmoja nyuma upande wa kulia na upana chini ya miguu iwe inchi 17 ( isiwe modo) iii. kwa wasichana;- sketi mbili za rangi ya DARK BLUE upana wa malinda ya sketi uwe kati ya Inchi 1 ½ na 2 zenye mikanda ( belt ) ndogo. ( belt pana haikubaliki) urefu kwenda chini iguse kifundo cha miguu. Au sentimeta 10 kutoka kwenye unyayo wa miguu. iv. Kwa wasicha wa kislamu wanaweza kushona blauzi ya mikono mirefu rangi nyeupe mbili, rangi ya njano moja, kijuba rangi nyeupe mbili na rangi ya njano moja. b) Sale ya michezo ni jezi na tracker rangi NYEKUNDU. c) Viatu vya shule ni vya ngozi rangi nyeusi vyenye kisigino kifupi vya kufunga gidamu yaani kamba ( boots na raba nyeusi haziruhusiwi) d) Soksi jozi mbili nyeupe zisizo na mapambo yoyote wala maandishi e) Mkanda mweusi wa ngozi wa kuvalia suruali kwa wavulana. f) Tai mbili ya blue yenye michilizi myeupe ( punda milia) 2.2 Ada na michangoa ya shule. a) Ada ya shule kwa mwaka ni Tsh. 70,000/= au 35,000/= kwa muhula, mzazi unaweza kulipa ada ya mwaka au kwa muhula mmoja. Fedha hizo zilipwe kwenye akaunti ya shule No. 31201200067 Magu Secondary School recurrent Account, Bank ya NMB tafadhali andika jina la mwanafunzi kwenye Bank pay in slip. b) Michango inayotakiwa kulipwa na kila mzazi ni i. Ukarabati wa samani 15000/= ii. Kitambulisho na picha 6000/= iii. Taaluma 20,000/= iv. Wapishi, walinzi na vibarua wengine 30,000/= v. Nembo ya Shule 2,000/= vi. Huduma ya kwanza na Bima ya afya 10,000/= vii. Tahadhari 5,000/= ( haitarejeshwa) Michango hii ilipwe kwenye account No. 312025000187 jina la account ni Magu Sekondari Elimu ya kujitegemea Bank ya NMB.

c) Mahitaji muhimu ambayo mwanafunzi anapaswa kuleta shuleni i. Ream moja ya karatasi kwa mwaka ( aina ya double A) ii. Vitabu vya masomo ya tahasusi ( angalia kwenye orodha ya vitabu kulingana na tahasusi husika ) iii. Dissecting kit kwa wanafunzi wa somo la Biology iv. Scientific calculate function 991 ( kwa tahasusi za sayansi) v. Godoro (Ft. 3x6 upana) vi. Mashuka rangi ya pink pair 2, foronya rangi ya pink pair 1 vii. Chandarua rangi ya blue 1 viii. Taa ya solata itatumika pale umeme unapokatika. ix. Blaketi 1 kwa wale tu wenye matatizo ya kiafya. x. Vyombo vya chakula:- sahani, bakuli, kijiko na kikombe. xi. Ndoo mbili ndogo zenye mifuniko xii. Vifaa vya usafi:- i. PCB Mopa, Mfagio mlaini ( soft broom) na chelewa ii. PCM Mopa, Mfagio mlaini ( soft broom ) na chelewa iii. CBG Kwanja, reki na chelewa iv. HKL Reki, Mfagio mgumu ( hard broom) na chelewa. d) T.shirt rangi ya njano muundo wa kola zenye visikizo nzito jozi mbili e) Sweta rangi ya Blue moja. f) Nguo za kushindia ( shamba dress ) ni:- i. Wasichana gauni mshono wa solo ndefu, isiyobana mikono mifupi pia mikono mirefu kwa wasichana wa kiislam rangi ya Blue Bahari kitambaa kiwe kizito ( jozi 2) ii. Wavulana suruali nyeusi isiyobana jozi mbili. N.B. kwa wanaotoka mbali, vifaa vyote vinapatikana Mwanza na Magu Mjini pia tai, tishet na sweta zinapatikana kwenye duka la shule hivyo unashauriwa kama vitu hivyo ni vigumu kuvipata katika mazingira uliopo waweza kuja kununulia maeneo haya.

SHERIA ZA SHULE. 1. Mwanafunzi lazima awe na hekima, utii kwa walimu, viongozi, watu wazima na wageni na kati yao wenyewe 2. Ni wajibu wa Mwanafunzi kutunza mali za shule. 3. Wanafunzi hawaruhusiwi kuvuta sigara, kunywa pombe, kunywa vidonge vya kulevya au kuvuta bangi pamoja na wizi. 4. Wanafunzi hawaruhusiwi kufika nyumbani kwa walimu bila ruhusa na nje ya mipaka ya shule wakati wa masomo. 5. Ni marufuku kuingia nyumba za starehe kama vile baa ya pombe, dansini, na nyumba za kulala wageni ( Guest House). 6. Ni wajibu wa wanafunzi kuona kuwa viwanja vya shule, madarasa na vyumba vingine vimewekwa katika hali ya usafi 7. Matusi ya kusema au kuandika na ugomvi ni marufuku. 8. Mwanafunzi lazima ahudhurie vipindi vya dini yake kila siku. 9. Ni mwiko kwa wanafunzi kujiunga na vikundi vyenye tabia mbaya shuleni au nje ya shule 10. Kila mwanafunzi anapaswa kuwahi shuleni saa 1:00 Asubuhi kuhudhuria vipindi vyote vya masomo na kufanya kazi zote anazopewa na mwalimu 11. Ni wajibu wa kila mwanafunzi kushiriki kikamilifu katika mipango yote ya shule ya Elimu ya kujitegemea. Uvivu au utoro ni makosa makubwa. 12. Ni marufuku kupokea wageni. Wageni wapitie kwa mkuu wa shule. 13. Wanafunzi hawaruhusiwi kutoka nje ya shule mara waingiapo bila ruhusa ya uongozi wa shule 14. Ni marufuku kuzagaa kwenye baraza la shule au nje ya madarasa wakati wa vipindi 15. Mwanafunzi haruhusiwi kujipikia au kuchemsha chochote awapo shuleni. 16. Ni marufuku kujiungaishia au kuunganisha umeme katika maeneo yote ya shule UTARATIBU UNAOPASWA KUFUATWA NA MWANAFUNZI ANAPOKUWA SHULENI. 1. Kuhudhuria roll call kila saa 11 ½ jioni 2. Atawajibika kutunza mali na vifaa mahali anapoishi. Uharibifu ukitokea utawajibika. 3. Kushiriki mchaka mchaka saa 12:00 12:30 Asubuhi. 4. Atapaswa kuhudhuria muda wa maandalizi binafsi darasani ( preparation time) saa 2:00 usiku 5:00 usiku. 5. Atapaswa kuwa bwenini baada ya preparation time 6. Wanafunzi wawapo bwenini baada ya preparation time taa zitazimwa. 7. Mwanafunzi awapo shuleni na hata kama ataomba ruhusa kwenda nje ya maeneo ya shule atapaswa kuvaa sare ya shule muda wote. Hivyo kwa sababu hiyo anaruhusiwa kushona sale ya ziada.

MAKOSA YATAKAYOSABABISHA MWANAFUNZI KUFUKUZWA SHULE. i) Wizi ii) Kutohudhuria masomo kwa zaidi ya siku 90 bila taarifa/ utoro iii) Kugoma na kuhamasisha mgomo iv) Kutoa lugha chafu kwa wanafunzi wenzake, walimu/ walezi na jamii kwa ujumla. v) Kupigana mwanafunzi kwa mwanafunzi, kumpiga mwalimu au mtu yeyote Yule. vi) Kusuka nywele kwa mtindo usio kubalika. Wanafunzi wote wanatakiwa kuwa na nywele fupi wakati wote wawapo shuleni. vii) Kufuga ndevu viii) Ulevi au unywaji wa pombe na matumizi ya madawa ya kulevya. ix) Uvutaji wa sigara. x) Uasherati, uhusiano wa jinsia moja, kuoa au kuolewa. xi) Kupata ujauzito au kutoa mimba. xii) Kushiriki matendo ya uhalifu, siasa na matendo yoyote yale yanayovunja sheria za nchi. xiii) Kusababisha mimba au kumpa mimba msichana. xiv) Kutembelea majumba ya starehe na nyumba za kulala wageni. xv) Kumiliki, kukutwa au kutumia simu ya mkononi katika mazingira ya shule. xvi) Kudharau Bendera ya ya Taifa xvi) Kufanya jaribio lolote la kujiua, au kutishia kujiua kama kunywa sumu n.k. xvii)uharibifu wa mali ya Umma kwa makusudi. VIAMBATISHO NA FOMU MUHIMU. a) Fomu ya Uchunguzi wa Afya ( Medical Examination Form) ambayo itajazwa na Mganga Mkuu wa hospitali ya Serikali. b) Fomu ya maelezo binafsi kuhusu historia ya mwanafunzi/ mkataba wa kutoshiriki katika mgomo, fujo na makosa ya jinai. c) Fomu ya mzazi kukiri kukubaliana na sheria, kanunni kulipa ada, michango na maelekezo mengine yatakayotolewa na shule. d) Picha nne (4) za wazazi na Ndugu wa karibu wa mwanafunzi wanaoweza kumtembelea mwanafunzi shuleni pamoja na namba zao za simu. Tafadhali soma kwa makini maelezo/maagizo haya na kuyatekeleza kikamilifu. KARIBUNI SANA KATIKA SHULE HII YA MAGU SAHAN J. BILAAZAH MKUU WA SHULE

FOMU NA PICHA ZA WAZAZI NA NDUGU WA KARIBU WA MWANAFUNZI WANAOWEZA KUMTEMBELEA MWANAFUNZI SHULENI PAMOJA NA NAMBA ZAO ZA SIMU. NA. JINA LA NDUGU MAHUSIANO NA. YA SIMU PICHA 1. 2. 3. 4.

FOMU YA MZAZI KUKIRI KUKUBALIANA NA SHERIA, KANUNI, KULIPA ADA, MICHANGO NA MAELEKEZO MENGINE YATAKAYOTOLEWA NA SHULE. Mimi ( jina la mwanafunzi ) nimesoma, nimeelewa na ninakubaliana na maagizo yote yanayoelekezwa katika barua ya maelezo niliyopewa na shule hii. Ninaahidi kwamba nitafuata sheria zote za shule na kutimiza wajibu wangu katika muda wote nitakapokuwa mwanafunzi wa shule hii. Sitajihusisha na mgomo wala kuchochea mgomo, makosa ya jinai au kujihusisha na vitendo vinavyohatarisha amani ya shule hii. Kwa jinsi hiyo uongozi wa shule uchukue hatua ya kuniondoa au kunisimamisha masomo au adhabu yoyote pale nitakapokwenda kinyume na maagizo, kanuni na sheria za shule. Ninaahidi pia kuwa nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu. Sahihi ya Mwanafunzi.. Jina la mwanafunzi. Tarehe Sahihi ya Mzazi / Mlezi Jina la Mzazi / Mlezi. Namba ya simu.. Tarehe

PHYSICS BOOKS ANASHAURIWA KUJA NA VITABU KIMOJA WAPO KATI YA:- Principles of physics class xi and xii by chand Thom Duhcan ABC modern physics 1, 2 Rodger Muncuster Duncan T, Advanced physics 5 th Edition Nelkon M & Pauker, Advanced level physics 7 th Edition Wilson Bufa,College physics,4 th edition Serway R.,Physics for scientists & engeers 3 rd edition Neamen D,Electronics circuit analysis and design SEARS &ZEMANSKY S, University physics with morden physics 13 th edition ADVANCED MATHEMATICS BOOKS C.J.TRANTER L.BOSTOCK, Pure mathematics Tanzania institute of education(tie), Advanced mathematics form five Tanzania institute of education(tie), Advanced mathematics form six J.K. Bckhouse et.pure mathematics 1 J.K. Bckhouse et.pure mathematics 2 S.CHAND S,Mathematics for; - Class xi - Class xii volume 1 - Class xii volume 2 SADRAL, Understanding mathematics BIOLOGY BOOKS COMPREHENSIVE BIOLOGY BIOLOGICAL SCIENCE UNDERSTANDING BIOLOGY FUNCTIONAL BIOLOGY CHAND

CHEMISTRY BOOKS CHAND XI, XII A-LEVEL CHEMISTRY RAMSDEN 4 th edition CONCEPTUAL CHEMISTRY ORGANIC CHEMISTRY PART 1, 2 IN ORGANIC CHEMISTRY FOR A-LEVEL PART 1, 2 SOIL CHEMISTRY PHYSICAL CHEMISTRY A-LEVEL HISTORY BOOKS A MAJOR EVENTS IN WORLD HISTORY PAPER 1 AND 2. MASTERING HISTORY PAPER 1 AND PAPER 2 HISTORY OF AFRICA LANGUAGE 2 BOOKS THE BEAUTIFUL ONE ARE NOT YET BORN I WILL MARRY WHEN I WANT BETRAYAL IN THE CITY A MAN OF THE PEOPLE LANGUAGE 01 BOOKS ADVANCED LEVEL ENGLISH A PRACTICAL APPROACH KISWAHILI 2 BOOKS VUTA NI KUVUTE MFADHILI KWENYE UKINGO WA THIMU NGUZO MAMA GEOGRAPHY BOOKS AN INTEGRATED REGIONAL STUDY ON HUMAN AND ECONOMIC GEOGRAPHY AFRICA IN DIAGRAMS- By Bunnet

TAARIFA MUHIMU KWA MWANAFUNZI. 1. Jina lako ( jina hili ni lazima lifanane na jina ulilokuwa unatumia kidato cha nne ) 2. BABA: i) Jina la baba yako. ii) Yu Hai.. iii) Kama amefariki lini. iv) Anuani yake.. (namba za simu).. v) Kazi na cheo chake. vi) Dini ya baba yako 3. MAMA: i) Jina la baba yako. ii) Yu Hai.. iii) Kama amefariki lini. iv) Anuani yake.. (namba za simu).. v) Kazi na cheo chake. 4. MLEZI. (i). unaye mlezi? ( mlezi ni mtu asiye mzazi wako) anayekutunza na kukuhudumia kwa chakula, malazi n.k (ii). Ndiyo/ Hapana. a) Jina la mlezi huyu ni.. b) Uhusiano wako na mlezi ( mjomba, kaka, rafiki, shangazi n.k). c) Anuani ya mlezi wako ni.. d) Kazi ya mlezi wako ni.. 5. i) Jina la mtu anayepelekewa ripoti zako za shule kama si baba au mama au mlezi wako ni nani.. anuani yake ni. Sahihi ya Mwanafunzi. Tafadhali ambatanisha nakala ya - Results slip ya kidato cha nne - Cheti cha kuzaliwa.

MINISTRY OF EDUCATION SCIENCE AND TECHNOLOGY ( To be completed by a Medical Officer) SHULE YA SEKONDARI MAGU, S.L.P 186, MAGU. REQUEST FOR MEDICAL EXAMINATION. Pupil s full name.. Age Blood count ( red and white.. Stool... Urine.. Syphilis Test.. T.B.Test. Eye Test.. Ears. Chest Spleen. Abdomen. ANY ADDITIONAL INFORMATION e.g Physical defects, Chronic or Family Diseases, etc. Signature.. Designation.. Station. Date.