Human Rights Are Universal And Yet...

Similar documents
Information for assessors (do not distribute this page to participants):

Pronunciation: Mä-hret Zäläke Ndal-ka-tscho Molla Mare Gebre-gzabiär 1/12

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

JAMHURI YA KENYA. Mkakati wa Ushirikiano MUKHTASARI FY Public Disclosure Authorized. Public Disclosure Authorized

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA)

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

Deutsche Welle, Learning by Ear 2009 Seite 1 People Who Make A Difference Liberia: Anita Varney Health Facilitator, Fishtown/Liberia

SautiElimu. Sauti Yako Isikike

Kiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika

Kuwafikia waliotengwa

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

LBE 2009 Migration Episode 3: Living without documents

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

Elimukombozi, Lugha na Upashanaji Habari nchini Tanzania, katika Muktadha wa Utandawazi

Kufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007

Ufundishaji wa lugha nyingine

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig

Nilikua na Ndoto ya Kumaliza Shule Changamoto za Elimu ya Sekondari Tanzania

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II

ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA UCHUMI WA ZANZIBAR

Kutetea Haki za Binadamu

Tufundishane! Mwalimu Bora In this issue: Issue 6, December Do you want to be in our next issue?

LUGHA YA KISWAHILI KATIKA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA ELIMU SHULE ZA SEKONDARI

Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA

Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2013

KUWEZESHA MBINU ZA UZUIAJI MIMBA KATIKA SUHULA ZA AFYA: MASWALI 10 KWA VIKUNDI VYA JAMII KUZINGATIA

5. Mheshimiwa Spika, Bunge lako Tukufu lilijadili kwa kina Miswada ifuatayo:

MAADHIMISHO YA MIAKA 15 YA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU VIKWAZO VYA KULINDA MAISHA KATIKA USAIDIZI WA KIMATAIFA WA AFYA KWA MSAADA WA KIMATAIFA UNAOFADHILIWA NA MAREKANI

MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA. Kwa Wanaoanza

Elimu-Jumuishi Kwa Vitendo

Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame M. Mbarawa (Mb.); Waheshimiwa Mawaziri na Wabunge wote mliohudhuria;

Uzio wa pilipili unazuia tembo kuvamia mazao shambani! Jinsi ya kujenga na kudumisha uzio wa pilipili Tanzania

Ufanisi katika Ufundishaji kwenye Shule za Msingi na Sekondari nchini Tanzania

TAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF) KUHUSU HAKI ZA WATOTO KATIKA KATIBA MPYA

TANZANIA MARKETS PAN Sera zinazoboresha masoko

JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1

Dibaji ya Mwenyekiti wa Kamati ya Pamoja ya Uongozi

Utangulizi wa ugonjwa wa shinikizo la damu

Vijana wanazungumza kuhusu ujinsia, maisha na uhusiano VIJANA WANAZUNGUMZA KUHUSU NGONO, MAISHA NA UHUSIANO. Training and Research Support Centre

JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI

KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA

RIPOTI YA WARSHA KUHUSU HABARI KWA AJILI YA UWAJIBIKAJI

MAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI

Usimulizi wa Riwaya ya Nyongo Mkalia Ini E. S. MOHOCHI University of Egerton, Kenya

Kitabu Cha Mafunzo Ya Uongozi Kwa Wanawake

MACHAGUO YA UZAZI KUFIKIRIA KUWA MZAZI

Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara)

HAKI NA TARATIBU ZA AJIRA, KAZI NA HIFADHI YA JAMII

Ufunguo wa Kutaalamika Haraka

TIST HABARI MOTO MOTO MAANDALIZI YA MWAKA 2000 Y2K PREPARATIONS SASA NI WAKATI WA KUANZA KUPANDA MBEGU ZAKO

Kimesanifiwa na:- E.D.Kissuu ECOMM TANZANIA S.L.P ,Dar es Salaam. Simu:

ORODHA YA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI SPIKA MHE. PANDU AMEIR KIFICHO. Rais.

TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM)

Ndugu na dada zangu wapendwa,

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA. Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo. TOLEO Na.

HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE

Dodoma ambako kikao cha Bunge kinaendelea kuja kushiriki japo sehemu ya uzinduzi wa mkutano.

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

TATHMINI YA PAMOJA SHULE ZA UPILI ZA JIMBO LA MACHAKOS.

Early Grade Reading Assessment for Kenya

Kocha Mkuu. mabingwa. itakuwa INASTAHILI. Ili Kutoa mafunzo kwa wanafunzi wako kuwa. itakuwa ya kuumiza. Itachukua muda. Itahitaji moyo wa kujitoa.

Kijitabu cha Maelezo cha Programu ya Famasia

usudi la Maisha Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na kupishana usiku na mchana, kuna kweli ishara kwa wenye akili, ambaye mkumbuke-

Mazoezi yaliyofanyika wakati wa warsha kuhusu Elimu-Jumuishi kwa Vitendo. Zanzibar, 7-10 Februari 2006

March 14, 2018 PARLIAMENTARY DEBATES 1 NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL REPORT. Wednesday, 14 th March The House met at 9.30 a.m.

HALIYA VITABUVYA WATOTOKATIKA TANZANIA

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

Unyanyasaji wa Watoto & Kutelekezwa

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU

Azimio lililopitishwa na Mkutano Mkuu tarehe 18 Desemba 2013 [juu ya taarifa ya Kamati ya Tatu (A/68/456/Add.2)]

Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA 2006/07

Kiu Cha umtafuta Mungu

Mhashamu Askofu Jude Thaddaeus Ruwa ichi, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania; Mwadhama Policarp Kardinali Pengo,

Mwongozo wa Mafunzo Yaliyochanganywaya K4Health

Elimu Ina Umuhimu gani katika Jamii? Kuelekea Elimu Sahihi

KUSHUKA KWA HADHI YA LUGHA ZA JAMII NCHINI TANZANIA YOHANA P. MSANJILA University of Dar es Salaam, Tanzania

KITEGO CHA MAREKEBISHO NA HAKI ZA MTOTO

Mipango ya miradi katika udugu

UMRI WA MAKAMO NA KUKOMA KWA HEDHI

Kuwawezesha wasichana kwa kuboresha kujikubali na kujithamini Hivi Ndivyo Nilivyo

Mwongozo wa Utamaduni Toleo la Kwanza

April 14, 2016 COUNTY ASSEMBLY DEBATES 52

Yaliyomo. Kuhusu kitabu hiki. Hautakuwa peke yako. Mfumo wa msaada ni wa manufaa sana wazazi wote wanahitaji!

Summaries of GC Reports 2012, Vol. 2, Sec. 1, Swahili

HUDUMA ZA AFYA KWA WOTE

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA

Ellen White, waasisi wa Kiadventista,na Sabato Lunar

UHUSIANO WA MIKAKATI YA UFUNDISHAJI WA FASIHI YA WATOTO YA KISWAHILI NA UMILISI WA KUSOMA KATIKA SHULE ZA MSINGI, KASARANI, KAUNTI YA NAIROBI, KENYA

Mwongozo wa Kutathimini mifumo ya Ugawanaji wa faida na Mapato Katika Miradi ya Jamii ya MKUHUMI

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA,KWA WANANCHI, 30 SEPTEMBA, 2001

Transcription:

Human Rights Are Universal And Yet... Episode 05 Title : The right to education Author : Julien Adayé Editor : Aude Gensbittel Translator : Anne Thomas, Eric Ponda Proofreader: Pendo Paul Characters (sounds, clips) / Narrators Intro/Outro male around 30 english Narrator female around 30 english Pascal Monson male about 50 french Céline Allah female 20 french Pronunciation (German): [Ju-liE~ Adaïeh] (E~ = in, please ask a french native speaker) [Pas-kal MM~sM~] (M~ = on, please ask a french native speaker) [Celin Ala] 1

Intro: Hujambo na karibu katika sehemu ya tano kwenye mfululizo wa vipindi hivi vya Noa Bongo Jenga maisha yako kuhusu Haki za Binadamu. Haki za Binadamu ni kwa wote..ingawa " Uhuru wa binadamu ni haki ya kuzaliwa, na lazima kuwepo na usawa katika kudumisha hadhi na haki kwa wote, na hii ndio nguzo muhimu katika azimio hili la Umoja wa Mataifa, kwamba kila binadamu, ana uhuru na uwezo wa kutumia azimio hili kudai haki na uhuru kama inavyobainishwa kwenye azimio hilo. Haki hizi zimeangaziwa katika kifungu nambari 1 na 2 ambavyo ni msingi wa azimio hili. Kifungu nambari 26, kinaeleza kwamba kila binadamu ana haki ya kupata elimu bora. Hii ni mongoni mwa haki ambazo haziheshimiwi hasa miongoni mwa mataifa mengi barani Afrika. Je, nini kinaweza kufanya kuhakikisha haki ya elimu inaimarishwa na kudumishwa kwa wote? Julien Adayé [Ju-liE~ Adaïeh] amesafiri hadi nchini Côte D'Ivoire kuchunguza zaidi suala hili. 1. Narrator Kila mmoja ana haki ya kupata elimu bora. Kifungu nambari 26 katika azimio hili la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu, kinasema kuwa kila mmoja ana haki ya kupata elimu ya msingi. Lakini tatizo kubwa ni kwamba haki ya elimu bora haidumishwi au mara nyingi inapuuzwa katika mataifa mengi ulimwenguni, kwasababu ya kukosa ufahamu au ukosefu wa fedha. Na matokeo yake, idadi kubwa ya watu hawawezi kusoma na kuandika. Mfano nchini Côte D Ivoire, asilimia 51 ya idadi ya watu waliotimu miaka 15 na zaidi nchini humo hawajui kusoma na 2

kuandika. Watoto wengi wanakosa kwenda shule na kisha kujutia baadaye. Hali hii imemtokea Céline Allah [Celin Ala], msichana wa miaka 20 hivi: 2. O-Ton ALLAH CELINE (French) Nilizaliwa katika kambi moja huko msituni. Babangu aliniambia kuwa si lazima wasichana waende shule kwasababu ni rahisi kupata mume na kuolewa. Wakati huo tayari mamangu alikuwa ametengana na babangu. Ninahuzunika sana ninapowaona wasichana wengine wakienda shule. Mara nyingi unashindwa kujieleza kwa marafiki zako. Na hili ndilo jambo linalonitia machungu zaidi. 3. Narrator Céline hayuko peke yake. Takwimu zinaonyesha kuwa elimu ya msichana imepuuzwa zaidi kuliko ile ya mvulana. Jumla ya asilimia 40 ya wavulana nchini Côte D Ivoire, hawawezi kusoma na kuandika. Yapo mashirika mengi nchini humo ambayo yamejitolea kuhakikisha kuwa kiwango cha kutojua kusoma na kuandika, kinashuka nchini Cote D Ívoire. Shirika la ABC limekuwa likiendesha shughuli zake nchini humo kwa muda mrefu sana, na makao yake makuu yapo katikati mwa mji wa Cocody mashariki mwa mji mkuu Abidjan. Hapa tunakutana na Pascal Monson [Pas-kal Mo~so~], mshirikishi wa shirika la ABC na anatuelezea kuhusu taaluma yake: 4. O-Ton MONSON PASCAL Nimefanya kazi katika sekta hii ya elimu tangu mwaka wa 1983, nikiwa mfanyakazi serikalini. Nimefanya kazi hii kwa zaidi ya miaka 8 kabla ya serikali kunipeleka kufundisha shule ya msingi, ambako nilifunza kwa muda wa miaka miwili kisha kuhamishwa hadi shule ya sekondari jijini. 3

Siku moja nilipokuwa nikifundisha, nilikutana na mwanafunzi ambaye hakujua kusoma wala kuandika. Baada ya kujiunga na shule alitokwa na machozi ya furaha siku alipopata cheti kwa kufuzu mtihani wake wa mwisho. Na hii ilinipa msukumo wa kuendelea kuwasaidia watu kujua kusoma na kuandika, ili waweze kuwa watu wa kutegemewa katika jamii. 5. Narrator Kujua kusoma na kuandika, ni ufunguo wa maisha bora, kwani inatoa fursa kwa mtu kuendeleza taaluma unayopenda maishani na kuwa mtu wa kuheshimiwa katika jamii. Mfano kusoma barua na ujumbe mfupi wa simu ya mkononi, kwa wengi huwa ni kiyama. Licha ya matatizo yanayomkumba Celine anafahamu vyema teknolojia ya kisasa ya mawasiliano. Kama wasichana wengine wa rika lake, ana simu ya mkononi ingawa hajui kusoma wala kuandika. Je, huwa anaitumia vipi hasa anapopokea ujumbe kwenye simu yake? 6. O-Ton ALLAH CELINE (French) Siwezi kusoma wala kuandika ujumbe mimi husaidiwa na rafiki zangu. Ni jambo linalonisikitisha sana hasa wanaponisomea ujumbe kwenye simu yangu kutoka kwa mpenzi wangu, lakini nitafanyaje! Ilinibidi nimweleza mchumba wangu kwamba siwezi kusoma na kuandika. Na siku hizi yeye hunipigia simu tu. 7. Narrator Watu ambao hawawezi kusoma na kuandika hawataki kuonekana ni washamba. Wanataka kuwa na simu ya mkononi kama Céline, na kisha baadaye kujifunza pole pole namna ya kukitumia kifaa hicho. Mfano 4

msichana huyu amevumbua mbinu ya kuhifadhi nambari za simu za watu ana kuwapa watu namba yake. 8. O-Ton ALLAH CELINE (French) Huwa naandika nambari hizi kwa karatasi au kadi ndogo zenye maelezo. Na ninazo nyingi kwenye mkoba wangu, huwa nazipeana kwa watu wanaponiuliza nambari zanhu za simu. Na kisha huwa nawapa simu yangu ili waweze kuandika nambari zao pia. 9. Narrator Shirika hili la ABC linadhamiria kuwapa elimu watu wasiojua kusoma na kuandika, ili kukabiliana na changamoto hizi. Ingawa halina darasa hata moja, limeweka mikakati ya kufanikisha azma hii. Anasema Pascal Monson [Pas-kal Mo~so~]. 10. O-Ton MONSON PASCAL (FRENCH) Tuko na wanafunzi 50, ambao wamejiunga na elimu ya watu wazima. Tunatoa huduma zetu kwa awamu tatu. awamu ya kwanza kuanzia saa nne hadi saa sita, ya pili saa tisa hadi kumi na moja jioni na ya mwisho saa kumi na mbili hadi saa mbili usiku. Masomo haya yamegawanywa katika vitengo vitatu, kitengo cha elimu ya msingi, kwa watu wasiojua kabisa kusoma na kuandika, kisha kitengo cha pili cha kundi la wanaoelewa kidogo kidogo yaani kuanzia mwaka mmoja hadi miaka miwili na kitengo cha tatu wale ambao wamejua kusoma na kuandikamwaka mmoja hadi miwili. 11. Narrator Mfumo huu wa elimu unaambatana na ule wa kitaifa nchini Cote D Ivoire ambapo wanafunzi wanaojiunga na masomo kwa mara ya kwanza 5

wanajifunza jinsi ya kusoma herufi na nambari, na kisha kuanza kusoma kuandika na kuhesabu. 12. ATMO : Literacy classes 13. Narrator Wanapokamilisha masomo hupewa vyeti vya kuhitimu elimu ya msingi. Mafunzo yanayotolewa na shirika la ABC humgharimu mtu kiasi cha faranga 2000 kila mwezi, kiasi sawa na shilingi elfu sita hivi. Kiwango hiki bado ni cha gharama ya juu sana hasa ikizingatiwa pato la mtu wa kawaida la faranga 500 kwa siku yaani chini ya shilingi elfu mbili nchini Cote D Ivoire. Kwa hivyo, si familia nyingi zinaweza kumudu gharama hii. Hata hivyo, lakini ili kuweza kuwasaidia watu wengi zaidi wanaotaka kujiunga na masomo, mashirika yasiyo ya kiserikali yameimarisha juhudi za kutafuta ufadhili kutoka nje. Wakati wa sherehe za kuadhimisha siku ya kujua kusoma na kuandika, wizara ya elimu nchini humo ilitangaza mipango ya kupunguza kiwango cha kutojua kusoma na kuandika kutoka asilimia 51 hadi asilimia 35 ifikapo mwaka 2020, na kwamba itashirikiana na mashirka mengine kutimiza lengo hili. Tayari mashirika yasiyo ya kiserikali yameimarisha juhudi za kuwahamasisha watu kuhusu umuhimu wa kujua kusoma na kuandika na hapa tena ni Pascal Monson [Pas-kal Mo~so~] : 14. O-Ton MONSON PASCAL (FRENCH) Hivi majuzi serikali ilitangaza kwamba kiwango cha kutojua kusoma na kuandika kimefikia asilimia 51- kiwango hiki kiko juu sana. Hii nikumaanisha kwamba nusu ya idadi ya watu nchini humu hawajui kusoma na kuandika. Na ndio sababu hivi majuzi serikali iliyaalika 6

mashirika yasiyo ya kiserikali kwenye warsha iliyokusudiwa kupigana na vita dhidi ya kutojua kusoma na kuandika. Tulihudhuria warsha hiyo na wizara ilionyesha moyo na kuahidi kuendelea kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali katika kupambana na vita hivi nchini Cote D Ivoire. 15. Narrator Matamshi haya ya Pascal Monson [Pas-kal Mo~so~] yanawiana na yale ya wizara ya elimu nchini humo. HUshirikiana katika kuhakikisha haki ya kujua kusoma na kuandika inatekelezwa. lakini mpango huu utaweza kufaya kazi vipi? 16. O-Ton MONSON PASCAL (FRENCH) Mfano iwapo shirika lisilo la kiserikali linataka kusaidia katika kuimarisha kiwango cha elimu, serikali huwa inasaidia kwa kufungua milango ya taasisi zake hasa katika sehemu ambazo miradi hiyo inatekelezwa, mfano katika shule za umma. Katika sehemu hizi Wizara ya Elimu inashirikiana kwa karibu na mashirika haya, kwa msaada unaohitajika 17. Narrator Pia wizara hutoa misada ya kifedha ili kufadhili elimu ya watu wazima mbali na kutoa kandarasi kwa mashirika haya. 18. O-Ton MONSON PASCAL (FRENCH) Pia shule nyingi za kibinafsi huwa tayari kusaidia katika kuimarisha elimu ya watu wazima nchini Côte d Ivoire. Kunapotokea kandarasi kubwa, wizara hiyo ya elimu huyaalika mashirika yasiyo ya kiserikali ili yaweze kutekeleza kandarasi hiyo na kulipwa faida kidogo. Pia, kuna kitengo maalum katika wizara hiyo kilichobuniwa kushughulikia elimu ya watu wazima nchini humo Côte D Ivoire. Kitengo hiki hushirikiana na mashirika yasiyo ya serikali kupunguza kiwango hiki ya kutojua kusoma 7

na kuandika. Ama kwa hakika kifungu nambari 26 kwenye azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu kinazingatiwa hapa nchini. 19. Narrator Céline pia anataka kuona kifungu hiki Cha 26 kinazingatiwa kikamilifu sio tu nchini Côte D Ivoire bali kote Barani Afrika. Pia mama huyu ana hamu sana ya kuendelea na elimu ya watu wazima lakini hawezi kugharamia masomo hayo na pia kupata muda wa kufanya kazi zake. Lengo kubwa ni kutoa hamasa kwa wazazi kutilia mkazo elimu ya watoto wao, kwani hangependa kuwaona watoto wengine katika hali hii. 20. O-Ton ALLAH CELINE Mtu ambaye hajui kusoma na kuandika ni kama kipofu. Huwa si rahisi kufahamu mambo maishani. Na mimi nisingependa kuona watoto wengine wakipata shida kama mimi. Ni mrembo ndio, lakini siwezi kujieleza, jambo linalonisikitisha sana. Nawahimiza wazazi kuwapeleka watoto wao shuleni. 21. Narrator Kwa kufanya hivyo, kunawapa nafasi nzuri ya kuwa na maisha bora. Kifungu cha 26 kwenye azimio hili kinasema kuwa, Elimu inafaa kudumishwa kwa wote kwa lengo la kustawisha maendeleo ya binadamu na kwa kuheshimu na kuzingatia misingi ya uhuru na haki za binadamu Outro Iwapo serikali ina nia njema na kwa ushirikiano wa mashirika yasiyo ya kiserikali, kila mmoja anaweza kupata elimu bora. Na kwa ripoti hii iliyotayarishwa na Julien Adayé, ndipo tunapokamilisha sehemu ya tano ya mfululizo wa vipindi vya Noa Bongo, Jenga maisha yako kuhusu haki za binadamu. Asante kwa kutusikiliza na endapo ungetaka 8

kukisikiliza tena kipindi hiki, tembelea mtandao wetu wa dw.de / lbe. Hadi wakati mwengine tutakapokutana tena kwa makala nyingine, kwaheri kwa sasa! 9