Pronunciation: Mä-hret Zäläke Ndal-ka-tscho Molla Mare Gebre-gzabiär 1/12

Similar documents
Human Rights Are Universal And Yet...

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Information for assessors (do not distribute this page to participants):

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

JAMHURI YA KENYA. Mkakati wa Ushirikiano MUKHTASARI FY Public Disclosure Authorized. Public Disclosure Authorized

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA,KWA WANANCHI, 30 SEPTEMBA, 2001

Kiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2013

ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA UCHUMI WA ZANZIBAR

Kuwafikia waliotengwa

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

Taarifa Kuhusu Hali ya Uchumi wa Tanzania

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti

Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara)

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

Kutetea Haki za Binadamu

TAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF) KUHUSU HAKI ZA WATOTO KATIKA KATIBA MPYA

Utangulizi wa ugonjwa wa shinikizo la damu

MAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

Azimio lililopitishwa na Mkutano Mkuu tarehe 18 Desemba 2013 [juu ya taarifa ya Kamati ya Tatu (A/68/456/Add.2)]

Dodoma ambako kikao cha Bunge kinaendelea kuja kushiriki japo sehemu ya uzinduzi wa mkutano.

JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1

UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA)

Ufunguo wa Kutaalamika Haraka

JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

Deutsche Welle, Learning by Ear 2009 Seite 1 People Who Make A Difference Liberia: Anita Varney Health Facilitator, Fishtown/Liberia

NGUO MPYA ZA UKOLONI. Mikataba ya Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Umoja wa Ulaya na Afrika. Agosti 2017

Elimukombozi, Lugha na Upashanaji Habari nchini Tanzania, katika Muktadha wa Utandawazi

KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA

LBE 2009 Migration Episode 3: Living without documents

Kilimo cha kiekolojia cha Wakulima Wadogo Hufanikisha Haki za Mazingira

UFAHAMU NAME INDEX SCHOOLDATE UFAHAMU

Kubadili Sheria Za Mbegu Na Ulinzi Wa Aina Za Mbegu Na Mimea Nchini Tanzania

MACHAGUO YA UZAZI KUFIKIRIA KUWA MZAZI

HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE

MAADHIMISHO YA MIAKA 15 YA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees

Mukhtasari Wa Mabishano Kwa Na Dhidi Ya Vikombe Vingi Vya Ushirika

Usimulizi wa Riwaya ya Nyongo Mkalia Ini E. S. MOHOCHI University of Egerton, Kenya

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu WEMA

Ufundishaji wa lugha nyingine

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )

UFUPISHO WA 35. Hali ya kiulimwengu ya Tekinolojia ya kibiashara/ugeuzi jeni na uboreshaji mazao: Clive James Chair, ISAAA Board of Directors

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara

Dibaji ya Mwenyekiti wa Kamati ya Pamoja ya Uongozi

usudi la Maisha Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na kupishana usiku na mchana, kuna kweli ishara kwa wenye akili, ambaye mkumbuke-

Hatari, Haki za Usalama katika Bahari 03

K. M a r k s, F. E n g e l s

Kimesanifiwa na:- E.D.Kissuu ECOMM TANZANIA S.L.P ,Dar es Salaam. Simu:

MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA PRO-ROUTES. Ombi kwa ajili ya fedha za umma wa mradi wa ziada

UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU VIKWAZO VYA KULINDA MAISHA KATIKA USAIDIZI WA KIMATAIFA WA AFYA KWA MSAADA WA KIMATAIFA UNAOFADHILIWA NA MAREKANI

5. Mheshimiwa Spika, Bunge lako Tukufu lilijadili kwa kina Miswada ifuatayo:

HUDUMA ZA AFYA KWA WOTE

TANZANIA MARKETS PAN Sera zinazoboresha masoko

Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA 2006/07

Ufanisi katika Ufundishaji kwenye Shule za Msingi na Sekondari nchini Tanzania

Tanzania, sasa kondoo anayesubiri kuchinjwa

KUSHUKA KWA HADHI YA LUGHA ZA JAMII NCHINI TANZANIA YOHANA P. MSANJILA University of Dar es Salaam, Tanzania

Kiu Cha umtafuta Mungu

Kufanya Uwekezaji kuwa wa Manufaa kwa Afrika: Jibu la Mbunge kuhusu Unyakuzi wa Ardhi

SautiElimu. Sauti Yako Isikike

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )

Nilikua na Ndoto ya Kumaliza Shule Changamoto za Elimu ya Sekondari Tanzania

Upande 1.0 Bajeti yako

Haja Ya Dini. Author(s): Publisher(s): Translator(s): Category: Topic Tags: Featured Category: Published on Al-Islam.org (

Kufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007

In the matter of an Application by the KIGOMA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (KUWASA) For a Tariff and Charges Adjustment

TIST HABARI MOTO MOTO MAANDALIZI YA MWAKA 2000 Y2K PREPARATIONS SASA NI WAKATI WA KUANZA KUPANDA MBEGU ZAKO

Mwongozo wa Jamii juu ya Afya ya Mazingira

Kuwa na Ukimwi ni kama vile kutakiwa kuendelea kuuzima moto unaoniunguza bila kukoma.

Oktoba-Desemba

Summaries of GC Reports 2012, Vol. 2, Sec. 1, Swahili

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA. Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo. TOLEO Na.

Ripoti hii ni kwa heshima ya wale wanaharakati wengi wa Tanzania ambao ndio binafsi wanaopitia hali iliyoangaziwa, na vilevile wale walioyapoteza

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

Kitabu Cha Mafunzo Ya Uongozi Kwa Wanawake

HAKI NA TARATIBU ZA AJIRA, KAZI NA HIFADHI YA JAMII

TIST HABARI MOTO MOTO

MAPENDEKEZO YA MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA TANZANIA

N09/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q

RIPOTI YA WARSHA KUHUSU HABARI KWA AJILI YA UWAJIBIKAJI

2

Na Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake Toleola4

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO

Mhashamu Askofu Jude Thaddaeus Ruwa ichi, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania; Mwadhama Policarp Kardinali Pengo,

International Labour Office. Kazi za Ndani Zenye Madhara kwa Watoto: Kijitabu cha Maelezo Mafupi

muhtasari 37 brief 37 Kiwango cha kiutandawazi cha mazao ya kibiashara ya kibayoteki/ugeuzi jeni: 2007 Clive James Bordi ya wakurugenzi wa ISAAA

March 14, 2018 PARLIAMENTARY DEBATES 1 NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL REPORT. Wednesday, 14 th March The House met at 9.30 a.m.

UNABII WA BIBLIA. CBM Publishing 32 Blenheim Road, Far Cotton Northampton, England. NN4 8NW

Bustani 10,000 Katika Afrika. Alberto Prina

Miradi na jamii. 3.1 Utangulizi

"ATATOKEA MARA YA PILI, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu." Waebrania 9:28.

Kijitabu cha Maelezo cha Programu ya Famasia

Transcription:

Human Rights Are Universal And Yet... Episode 07 Title : The right to food drought and famine in Ethiopia Author : Tedla Getachew Editor : Aude Gensbittel, Pendo Paul Translator : Anne Thomas Proofreader: Pendo Paul Kisuaheli: Eric Ponda Characters (sounds, clips) / narrators Intro/Outro male around 30 english Narrator male around 30 english Mihret Zeleke female 28 french Endalkachew male 40 amharic Molla (NGO) Mare female 35 amharic Gebregziabher Blen Abera female 25 amharic (taxi passenger) Rebecca Iyob female 30 french (Journalist) Judith Schuler female 35 french Pronunciation: Mä-hret Zäläke Ndal-ka-tscho Molla Mare Gebre-gzabiär 1/12

Blen Abera Rebka E-yiob Tedla Geta-tscho Intro : Hujambo na karibu katika awamu ya saba kwenye mfululizo wa vipindi hivi vya Noa Bongo Jenga Maisha yako kuhusu haki za binadamu. Maada kuu ikiwa ni Haki za binadamu ni kwa wote, ingawa... "Uhuru wa binadamu ni haki ya kuzaliwa, na kwamba hadhi na haki za kila mmoja zinafaa kuheshimiwa pasi na kubaguliwa. Na hii ndio nguzo muhimu katika azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu. Kwamba kila binadamu pasi na kubaguliwa anaweza kutumia sheria hii kudai haki na uhuru wake kama inavyoelezwa kwenye azimio hili la Umoja wa Mataifa. Haya yanaelezwa katika kifungu cha kwanza na cha pili ambavyo ni msingi wa azimio hili. Katika kifungu cha 25 kwenye azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu, kinaeleza kwamba, kila mtu ana haki ya kuishi maisha mazuri, ikiwa ni pamoja na haki ya afya nzuri na familia yake, na haki ya chakula. Lakini kinyume kabisa cha hayo, katika sehemu nyingi za ulimwengu hasa barani Afrika, baa la njaa limekuwa jambo la kawaida hasa katika sehemu zinazokumbwa na hali ngumu ya ukame. Mfano ni nchi ya Ethiopia ambako Tedla Getachew (Tedla Geta-tscho) anaangazia tatizo hili: 1. SFX : noise cafeteria (Alliance Ethio-Française ) 2/12

2. Narrator Tunakuana na mwanamke wa makamu, wa rika la miaka thelathini hivi, anambembeleza mtoto aliyefunikwa kwa blanketi na kuacha kichwa chake tu. Hali yake taabani kwa jinsi alivyodhooika kiafya, thibitisho kwamba anapitia hali ngumu ya maisha. Jina lake ni Mehret Zeleke (Mä-hret Zäläke) Anaketi kwenye ubao wa mgahawa wa Ethio-French Alliance uliopo mjini Addis Ababa. Mama huyu anakiri kwamba maisha si rahisi kwake: 3. O-Ton 1/ Mehret Zeleke (French) : Ni kweli maisha ni magumu hasa tunapoelekea mwishoni mwa mwezi! Na tatizo hili linazidi unapokuwa na mtoto mchanga- Mimi hufanya kazi, kama mwalimu wa kujiajiri mwenyewe. Natumia ujuzi wangu wa lugha ya Kifaransa kufundisha katika shule za binafsi utanisaidia, lakini kwa hakika gharama ya maisha imepanda sana maisha yamekuwa magumu! KW begin 4. NARRATOR Kupanda kwa gharama za maisha ni tatizo kubwa hasa wakati huu. Kama ilivyo katika maitaifa mengi Barani Afrika, uchumi wa Ethiopia unategemea kilimo ambacho huchangia hadi asilimia 90 ya mauzo ya kigeni na kubuni asilimia 80 ya nafasi za kazi nchini humo. Hivyo ni nguzo ya shughuli za kiuchumi nchini humo, mbali na kwamba sekta hii ya kilimo inategemea na Wa-Ethiopia wengi kwa chakula. Wakati kunapokuwa na ukame, sekta yote ya uchumi hutikisika. Bidhaa za kimsingi kama vile nafaka huwa adimu, hivyo kusababisha 3/12

mfumuko wa bei, na tatizo la ukosefu wa ajira kutokana na kuyumba kwa uchumi. 5. ATMO City 6. Narrator Hapa mjini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, uhaba wa chakula ni dhahiri kuliko sehemu nyingine za taifa. Lakini unapomsikiliza Mehret Zeleke (Mä-hret Zäläke), taarifa za vyombo vya habari huwa hazielezei ukweli halisi wa maisha hapa mjini. Licha ya kwamba anaishi mjini, hali ya maisha ni ngumu na haina tofauti na ilivyo katika sehemu za mashambani. 7. O-Ton 2 / Mehret (French) Nimeshuhudia watoto wakianguka na kuzimia wanapokuwa wakielekea shuleni..mara nyingine watoto wanakuja kuniombaa niwanunulie angalau mkate, huwa hawataki pesa wanataka chakula, na sio eti ni watoto omba omba la hasha, wanachotaka ni chakula tu. Kunafamilia ambazo haziwezi kumudu chakula mara tatu kwa siku, hazina chakula cha kutosha kabisa! Baa la njaa ni dhahiri kama inavyoangaziwa kwenye vyombo vya habari. Si rahisi kufahamu hali halisi kwasababu naishi mjini, lakini ukweli kiwango cha umaskini kinazidi kupanda. KW end 8. Atmo Office 9. Narrator 4/12

Mashirika ya kijamii yanafanya juhudi za kupunguza kiwango cha umaskini nchini humo. Shirika la kupigania haki za binadamu nchini humo, linakusudia kuhakikisha kuwa haki za binadamu zinaheshimiwa hasa kwa kuzingatia kifungu nambari 25 kwenye azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya chakula kwa wote. Baraza la mashirika ya kutetea haki za binadamu lina makao yake mjini Addis Ababa. Wakati raia wanapokabiliwa na tisho la njaa, kutokana na kipindi kirefu cha msimu wa ukame, kama inavyotokea mara kwa mara nchini Ethiopia, shirika hilo huwa na uwezo mdogo sana wa kushughulikia tatizo hilo. Kulingana na mkuu wa shirika hilo, Endalkevhew Molla (Ndal-ka-tscho Molla), hali hii pia inasababishwa na ukosefu wa pesa na ufahamu miongoni mwa raia wake kuhusu haki zao. 10. O-Ton / Endalkachew Molla (Amharic) KW begin Tunapozungumzia haki ya kuishi maisha bora, sio tu mashirika au taasisi yaayopaswa kulaumiwa kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake. Ni vyema kuangalia maisha kwa jumla kuhusu masuala ya ajira na chakula. Kwa ufupi tunazungumiza haki ya kimsingi kwenye azimio la kimataifa kuhusu haki za binadamu. Kwa hakika tunazingatia na kufuata maadili ya kimsingi kwenye azimio hili, na tunaihimiza serikali ya Ethiopia ambayo imetia sahihi azimio hili la kimataifa, kuheshimu na kutekeleza haki zote zilizomo kwenye azimio hili pasi na kusita au kujikokota. KW end Kwa upande wetu, kwasababu ya uwezo wetu finyu, tunashirikiana na mashirika mengine ya kanda hii inayokumba na ukame, kutuletea ripoti 5/12

kuhusu visa vya ukiuka wa haki zao. Kawaida huwa tunawasilisha ripoti hizi kwa taaisisi husika, lakini tatizo ni kwamba, wengi hawafahamu haki zao, na hata kwa wale wanaofahamu, huwa si rahisi kujitokeza. Hii inamaanisha hatuwezi kupata picha halisi ya tatizo hili. Hata ikiwa watu wanafahamu haki zao kuhusu chakula, na haki ya kukingwa dhidi ya athari za ukame, hakumaanishi moja kwa moja wanadai haki hizo, iwe ni kupitia shirika letu au njia nyinginezo zile. Na hii inatokana na ukosefu wa elimu au kiwango cha chini cha ufahamu. Inadhihirisha kwamba kuna upungufu lakini si eti tatizo hilo halipo! 11. Narrator Mara kwa mara nchi ya Ethiopia hukumbwa na baa la nja. Kunako miaka ya sabini baa la njaa liliikumba nchi hiyo, na kisha baadaye kuanzia mwaka wa 1982 hadi 84 kukatokea baa la njaa ambalo halijawahi kushuhudiwa katika kanda hii. Watu wengi waliathirika na maelfu na wengine kupoteza maisha. Baa la njaa huzungumziwa tu wakati hali ya ukame inapokumba eneo fulani la nchi. Lakini ukweli ni kwamba utapia mlo una athari kubwa zaidi kwani hutokana na ukosefu wa lishe bora, pale mtu anapokuwa na kiwango cha chini ya kalori 1200 kwa siku, kuliko kile kinachohitajika cha kalori 2400 kwa siku. Hali hii inapotokea na kuendelea, hapo mtu anaanza kudhoofika kiafya na hata kupoteza maisha. Eneo zima la upembe mwa Afrika limo hatarini mwa kukumbwa na baa la njaa la mara kwa mara. Nchini Ethiopia, mamilioni ya watu wanahitaji msaaada wa chakula. Mara kwa mara serikali ikishirikiana na mashirika ya kijamii, hugawa chakula cha misaada katika sehemu zinazoathirika, lakini hii huwa ni hatua tu ya kutibu ugonjwa na wala sio chanzo cha ugonjwa huo. Mojawapo ya chanzo cha tatizo la njaa ni ongezeko la idadi ya watu. Idadi ya watu inaongezeka kwa 6/12

haraka nchini Ethiopia, ambapo sasa inafikia watoto sita kwa kila mwanamke mmoja. Na kiwango hiki ni cha juu sana! 12. SFX : ATMO : traffic 13. Narrator Tuko katikati mwa mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa. Mji huu wenye idadi ya mamilioni ya watu, una nafasi nzuri ya mtu kujiendeleza. Mji huu mkuu wa kiuchumi na kiutawala, huwavutia watu wengi wanaohamia hapa kutoka sehemu za mashambani kutafuta maisha bora. Ukweli wa mambo ni kwamba idadi ya watu maskini inazidi kuongezeka katika barabara za mji huu wa Addis Ababa. (Oton 14 and 15 follow on from each other like vox pops) 14. Oton Mare Gebregziabher (Amharic) Woman Nilihamia mjini kutoka Gondar, jimbo lililoko eneo la kati mwa nchi, yapata miaka minne hiv iliyopitata. Nimekutana na wazee ambao hawana watoto wala watu wakuwategemea, na wanaishi tu katika barabara za mji huu. Kawaida wazee hawa hukusanyika nje ya makanisa kuomba misaada, na wale ambao hawajiwezi kabisa mwishowe hufariki katika barabara hizi. 15. Oton Blen Abera ( Amharic ) Woman Ni kweli, wazee kwa vijana, waliosoma na wale ambao hawajasoma, wote hukusanyika nje ya makanisa. Nimewahi kuwaona, wengine wakiishia kurandaranda mitaani wakiombaomba. 7/12

16. Narrator Kulingana na wasichana hawa, idadi ya watu wanaohitaji misaada inazidi kuongezeka katika barabara za mji huo mkuu. Lakini je, hii inatokana na ukosefu wa fedha au baa la njaa? Tatizo hili linashuhudiwa katika miji mingi kote ulimwenguni hasa Barani Afrika Rebecca Iyob (Rebka E-yiob) ni mwandishi wa habari na ana maoni tofauti: 17. O-Ton Rebecca Iyob (French) Mimi husafiri sana. Mwezi uliopita nilikuwa nchini Niger, kisha nikapitia Burkina Faso, na naweza kusema kuwa hapa kiwango cha umaskini si cha juu sana. Nimesafiri nchini Djibouti na hali ya umaskini nchini humo ni ya kiwango cha juu sana. Hivyo nikilinganisha na mataifa mengine huwezi kusema idadi ya watu wanaorandaranda mitani ni kubwa kushinda nchi nyingine Ni kweli kuna tatizo la umaskini, lakini wengi wao wanafamilia. Nadhani watu wengi nchini Ethiopia wanaweza kujimudu kwa chakula. 18. ATMO MARKET 19. Narrator Shughuli za kibiashara huwa zinaendelea kama kawaida katika masoko mengi mjini Addisa Ababa. Hata ingawa bei zimepanda maradufu katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, wakazi hao hawawezi kukosa chakula chao maarufu "injera." Hizi ni aina za chapati zinazotengenezwa kutokana na unga unaofanana na mtama, ambao una protini nyingi. Kwa wakati huu, kilo 50 za unga huo, kiasi kinachoweza kulisha familia ya watu watatu kwa miezi mitatu, 8/12

hugharimu takriban birr 1400 sawa na euro 63. Hiki ni kiwango sawa na mshahara wa mfanyakazi wa kawaida wa serikali. KW begin Mara nyingi wale wanaofanya kazi katika sekta ya jua kali, mara nyingi hupokea kiasi cha kati ya Birr 30 na 40 sawa na euro 1.5 hadi 2, ambacho hakiwezi kutosheleza mahitaji yao. Mfanyakazi mwenye ujuzi, mara nyingi hulipwa hadi birr 50 sawa na 2uro 2.5. Kawaida bei za vyakula huwa juu sana, ambapo lita moja ya mafuta, inaweza kuuzwa hadi kiasi sawa na kodi ya chumba kimoja cha kulala. KW end Kulingana na ripoti ya hivi punde ya Benki ya Dunia, asilimia 40 ya idadi ya watu sawa na zaidi ya watu milioni 30, ni maskini nchini Ethiopia. Wengi wao hulala njaa kutokana na uhaba wa chakula, ambao huikumba nchi hiyo mara kwa mara. Na hali hii huwa mbaya wakati kiwango cha chakula cha misaada kinapopungua kutoka shirika la Mpango wa chakula Duniani (WFP), linaloshughulikia tatizo hili nchini humo, anasema mkuu wa shirika hilo nchini Ethiopia Judith Schuler, 20. Oton Judith Schuler (French) Kidogo hali hiyo imeimarika. Tulikuwa na mavuno mazuri sana msimu huu. Lakini tunagawa chakula cha msaada katika sehemu ambazo bado zinakumbwa na uhaba wa chakula, ingawa hatujapata ripoti kamili ya 9/12

kiwango cha msaada unaohitajika baada ya mavuno haya. Inasadikika kwamba idadi ya watu wanaohitaji chakula cha msaada imepungua kutoka watu milioni 4.5 hadi milioni 3.2. Kwa hakika haya ni mafanikio makubwa. Kawaida huwa tunasambaza chakula cha msaada kwa watu milioni 2.4 huku mashirika mengine ya kijamii yakikuhudumia sehemu nyingine zinazokumbwa na uhaba wa chakula. Sehemu zote ninazokumba na uhaba wa chakula bado zinaendelea kupokea misaada ingawa kiwango hicho kimepungua ikilinganishwa na mwaka uliopita. 21. Narrator Misaada ya dharura huwa inakusudiwa kupunguza tatizo, lakini je, ndilo suluhisho kwa tatizo lenyewe? Wakati baa la njaa linapokumba sehemu moja ya ulimwengu, idadi kuwa ya watu huathirika na pia kubadili mtazamo wao kuhusu tatizo hilo. 22. Musique : We are the world (archivnr. 4007823) from 3 09 (let the chorus about 10 then fade under the next text) 23. Narrator Mfano ni ilivyotokea mwaka wa 1985- wakati kulipotokea baa la njaa ambalo halijawahi kushuhudiwa nchini Ethiopia. Tatizo hili lilisababisha mwanamuziki mashuhuri nchini Uingereza Bob Geldon kuwakusanya waimbaji wengine mashuhuri barani Ulaya, ili kuisaidia Ethiopia. Miezi miwili baadaye, waimbaji mashuhuri nchini Marekani pia wakaiga mfano huo na kutunga wimbo uliovuma sana kuisaidia Ethiopia. Wimbo huu uliweza kukusanya zaidi ya dola milioni 60 kuwasaidia watu waliokuwa wanakufa njaa nchini humo. 10/12

Lakini mbali na kiu ya kuwasaidia watu wanaokabiliwa na njaa, je, viongozi wa kisiasa wanachangia vipi kuhakikisha haki ya kupata chakula inatekelezwa?, hasa ikizingatiwa kwamba watu wengi wanaishi maisha ya kifukara barani Afrika? Ama kwa hakika kuzungumzia haki hii kwa mtu ambaye hajui atakula nini kesho ni kama kitendendawili. Lakini ndio hali halisi anayozungumziwa Mehret Zeleke (Mä-hret Zäläke): 24. O-Ton Mehret Zekele (French) Kusema hivyo ni kama kejeli..! Siwezi kusema kwamba tuna haki au hatuna haki. Nafahamu kwamba nchi hii imo mbioni katika ustawi wa maendeleo lakini juhudi zaidi zinahitajika. 25. Narrator Wakati huo huo, Mehret lazima andelee kushughulikia maisha ya mtoto wake. Outro Vipindi virefu vya ukame ni tukio linaloshuhudiwa katika mataifa mengi ya ulimwengu kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Hata hivyo, lakini kiwango cha athari zake hutofautiana miongoni mwa mataifa haya. Lakini athari hizi zinazidi pale mshikamano wa nchi unapoyumbishwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe au kuongezeka kwa idadi ya watu. Hivyo, mabadiliko ya kinadharia miongoni mwa jamii katika kudumisha haki za kimsingi, ndilo linaloweza kuwa suluhisho pekee la kudumu. Hadi hapo tunafika mwisho wa kipindi cha leo cha Noa Bongo Jenga Maisha yako. Asante kwa kusikiliza ripoti hii ambayo imeandikwa na Tedla Getachew ikiwa ni sehemu ya mfululizo wa vipindi kuhusu haki za binadamu. Endapo 11/12

ungependa kukisikiliza tena kipindi hiki, tembelea mtandao wetu wa dw.de/lbe. Hadi mwakati mwengine, kwaheri kwa sasa! 12/12