Kiinimacho cha mahali: kiambishi tamati cha mahali -ni. Ridder Samsom na Thilo C Schadeberg Chuo Kikuu cha Leiden

Similar documents
Information for assessors (do not distribute this page to participants):

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

Ufunguo wa Kutaalamika Haraka

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Theolojia Ujumla. Mike Taylor Semester Munguishi Bible College

N09/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

ULINGANISHI WA KIISIMU KATI YA LAHAJA YA KIPEMBA NA KITUMBATU

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

Kifaa Maalum cha Kutazamia Jua: Maelekezo ya kutumia

ATHARI ZA KIMOFOFONOLOJIA ZA KIOLUSUBA KATIKA MATUMIZI YA KISWAHILI SANIFU KAMA LUGHA YA PILI

MAP ISI YA KISW AHILI

KENYA NATIONAL EXAMINATION COUNCIL REVISION MOCK EXAMS 2016 TOP NATIONAL SCHOOLS

Haja Ya Dini. Author(s): Publisher(s): Translator(s): Category: Topic Tags: Featured Category: Published on Al-Islam.org (

Usimulizi wa Riwaya ya Nyongo Mkalia Ini E. S. MOHOCHI University of Egerton, Kenya

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level

Mafundisho Ya Msingi Wa Kikristo. Na Andrew Connally

Tora UTANGULIZI KWA TORA SOMO LA KWANZA

Kiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika

UCHANGANUZI LINGANISHI WA SINTAKSIA YA SENTENSI SHARTI YA KISWAHILI SANIFU NA EKEGUSII CHUO KIKUU CHA NAIROBI

MTIHANI WA MWIGO WILAYA YA BUTERE MUMIAS-2007 Hati ya kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya

KUSHUKA KWA HADHI YA LUGHA ZA JAMII NCHINI TANZANIA YOHANA P. MSANJILA University of Dar es Salaam, Tanzania

MATATIZO YA MATUMIZI YA LUGHA KATIKA VYOMBO VYA HABARI: MIFANO KUTOKA KENYA 1 KITULA KINGE'I. 1. Utangulizi. AAP 64 (2000): Swahili Forum VII 45-56

Mukhtasari Wa Mabishano Kwa Na Dhidi Ya Vikombe Vingi Vya Ushirika

Hati ya Kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya.( K.C.S.E)

Mwongozo wa Utamaduni Toleo la Kwanza

Mutugi Kamundi. Jemma Kahn. Kiswahili. Demane na pacha wake. Author - South African Folktale

usudi la Maisha Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na kupishana usiku na mchana, kuna kweli ishara kwa wenye akili, ambaye mkumbuke-

TASFIDA KAMA MKAKATI WA UPOLE: UWIANO WA TASFIDA ZA KISWAHILI NA EKEGUSII

Msigano wa Majina ya Walemavu katika Jamii ya Wazungumzaji Kiswahili: Mifano kutoka Tanzania

K. M a r k s, F. E n g e l s

ATHARI ZA KIISIMU ZA LAHAJA YA KIMAKUNDUCHI KATIKAKISWAHILI SANIFU KINACHOTUMIKA SHULENI MAKUNDUCHI ZANZIBAR

Kiu Cha umtafuta Mungu

Adhabu ya jino kwa jino na Musitakabali wa imani zetu

UNABII WA BIBLIA. CBM Publishing 32 Blenheim Road, Far Cotton Northampton, England. NN4 8NW

Agano Lililofunikwa Kwa Damu

KUPWA NA KUJAA KWA BAHARI. (TIDES AND TIME)

CHUO KIKUU CHA NAIROBI

Roho Mtakatifu Ni Nini?

MADA MATUMIZI YA TAKRIRI NA SITIARI KATIKA UTENZI WA RASI LGHULI JUSTUS MAUNDU NDUMBU C50/65902/2011 CHUO KIKUU CHA NAIROBI IDARA YA ISIMU NA LUGHA

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees

ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA UCHUMI WA ZANZIBAR

KISWAHILI KARATASI YA 2 LUGHA

LUGHA YA KISWAHILI KATIKA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA ELIMU SHULE ZA SEKONDARI

Pronunciation: Mä-hret Zäläke Ndal-ka-tscho Molla Mare Gebre-gzabiär 1/12

MUNGU ANADHIHIRISHWA KUPITIA KWA YESU KRISTO.

MARUDIO K.C.S.E KNEC KISWAHILI KARATASI 102/2 MASWALI NA USAHIHISHO

Ellen White, waasisi wa Kiadventista,na Sabato Lunar

B. Wanafunzi watapata ufahamu mkubwa wa kitabu hiki, na jinsi kinavyofundisha kuhusu kanisa.

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC)

Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya Tanzania

JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI

2 LILE NENO LILILONENWA

2

Ufundishaji wa lugha nyingine

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

JE, YAWEZEKANA KUISHI BILA KUTENDA DHAMBI?

Ushindi ndani ya Kristo W. W. PRESCOTT

Elimukombozi, Lugha na Upashanaji Habari nchini Tanzania, katika Muktadha wa Utandawazi

KUTAMBUA SIKU YA KO NA UJUMBE WAKE

Uponyaji Wa Laana. (Kumb. 28:1-14).

ETIMOLOJIA YA MAJINA YA MAHALI YA KASKAZINI PEMBA KUWA UTAMBULISHO WA UTAMADUNI WA WAPEMBA

MAKALA: USHAIRI WA KISWAHILI KATIKA NJIA PANDA: KUTUMIA AU KUTOTUMIA METHALI

Hatari, Haki za Usalama katika Bahari 03

KUCHUNGUZA UJINSIA NA MATUMIZI YA LUGHA KATIKA METHALI ZA WAKURYA

KWA NINI SISI SI MADHEHEBU?

JAZANDA YA NJOZI KATIKA BAADHI YA MASHAIRI YA EUPHRASE KEZILAHABI (ONEIRIC IMAGES IN EUPHRASE KEZILAHABI S SELECTED POEMS) 1

PDF created with pdffactory trial version

Ndugu na dada zangu wapendwa,

2

DHANA NA MATKTIZO YA TAFSIRI:

Hakimiliki na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa TAFSIRI YA BIBLIA. Mwandishi. Jonathan M. Menn

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

V\ FANI KATIKA USHAIRI WA HASSAN MWALIMU MBEGA: UHAKIKI WA UPISHO WA UMALENGA NA DAFINA YA UMALENGA DONALD OMWOYO OSIEMO

Kifo Na Mbingu. (Death And Heaven) Ellis P. Forsman. Kifo Na Mbingu (Death And Heaven) 1

SANIFU KWA SHULE ZA SEKONDARI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO

Kufunga Milango - Uponyaji Kutokana na Athari za Giza

BIBLICAL INSTRUCTION AND ENCOURAGEMENT FOR THE MAFUNDISHO YA BIBLIA NA HIMIZO KWA MISSION FIELD WORLDWIDE. KAZI YA KIMISHENI ULIMWENGUNI KOTE

walozaliwa, si kwa damu, wala mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, mbali kwa Mungu. Sisi sio tena binadamu wa kawaida tu kwa sababu sisi ni w

KAMA MUNGU YU PAMOJA NASI, BASI YAKO WAPI MATENDO YAKE YA AJABU?

Sera ya Faragha. Upeo. Aina za Data na Mbinu za Ukusanyaji

MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA. Kwa Wanaoanza

KUCHUNGUZA MCHOMOZO KATIKA FASIHI YA KISWAHILI: UTAFITI LINGANISHI WA USHAIRI KATIKA DIWANI YA USTADHI ANDANENGA

WEWE NI NANI? Toleo X Toleo Ukweli wa Injeli Toleo 23

YEHOVA-YIRE 1. 2 Baba yetu wa Mbinguni, tunakikaribia Kiti Chako cha. 3 Tunakushukuru kwa kutuzuru jana jioni. Tunaomba

Human Rights Are Universal And Yet...

IM ETUPASA KUTIMIZA HA KI YOTE

"ATATOKEA MARA YA PILI, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu." Waebrania 9:28.

Maisha Yaliyojaa Maombi

MAANA HALISI IMAAN ( I )

Cambridge International Examinations Cambridge Ordinary Level

Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Oktoba-Desemba

UTARATIBU WA KANISA. 2 Jambo la kwanza ninalotaka kusema ni kwamba mchungaji. 3 Sisi tunaamini katika Kanisa la kimitume, tukifundisha

United Pentecostal Church June 2017

maombi, kabla tu hatujalifungua Neno hili la Kiungu.

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA,KWA WANANCHI, 30 SEPTEMBA, 2001

Transcription:

AAP 37 (1994). 127-JJB Kiinimacho cha mahali: kiambishi tamati cha mahali -ni Ridder Samsom na Thilo C Schadeberg Chuo Kikuu cha Leiden The locative suffix -ni n this article we discuss two hypotheses about the origin of the locative suffix -ni. The better known hypothesis (Raum 1909; Meinhof 1941142) assumes that the suffix -(i)ni developed out of a class 18 demonstrative, though the details of the assumed phonological changes have never been made clear. The competing hypothesis by Sacleux (1939) suggests that locative nouns with -ni started out as compounds with the noun ini 'liver'. We think that this second hypothesis is phonologically more plausible and that it also accounts for the specific link with the meaning of class 18 'inside'. Comparison of the spread of the!ocative suffix -(i)ni and of the word ini 'liver', together "'ith other historical considerations, point to Kiswahili (or Sabaki) as the most likely origin of this iocative suffix 1. Utangulizi Makala yetu inahusu asili na usambazaji wa kiambishi tamati cha mahali -ni.. Katika lugha karibu zote za Kibantu kuna ngeli tatu za mahali zenye viambishi hivi vitatu: pa, ku na mu. Katika lugha ya Kiswahili mofimu hizi zinatumika sana kama viwakilishi, kwa mfano katika viwakilishi vionyeshi hapa, huku, humu, tena katika viwakilishi vimilikishi, kwa mfano kwao.. Tunavikuta pia kama viambishi vya vitenzi, kwa mfimo hapapitiki, kumekucha, hamna.. Matumizi yake kama viambishi vya kijina yako katika vivumishi tu, kwa mfano pazuri. Lakini majina yenyewe, kwa kawaida, hayatokei pamoja na viambishi awali vya ngeli hizi, isipokuwa maneno machache ambayo bila shaka yameundwa hi vi hivi zamani, kwa mfano kuuke na kuume, kushoto, kuzimu na machache mengineyo..

128 RDDER SAMSOM AND THLO C SCHADEBERG Bali, tunapotaka kutaja mahali pa kitu fulani, kwa mhmo 'kwenye nyumba', hatuwezi kuongeza kiambishi awali cha mahali, lakini inatubidi kuongeza kiambishi tamati -ni, kwa mfano nyumbani. Jina pamoja na kiambishi tamati -ni likawa ni jina la ngeli ya 16 (nyumbanipale), au ya 17 (nyumbani kwetu), au ya 18 (nyumbani humu). 1 unajua kwamba, hii si hali ya Kibantu cha asili kwa sababu lugha nyingine, kwa kawaida, hutumika viambishi awali hi vi pamoja na majina, kwa mf~mo, Wagogo wangesema ha-nyumba, ku-nyumba, mu-nyumba.. Lugha zenye kiambishi tamati -ni ni chache, na zote ziko Afrika Mashariki na Afrika Kusini, na hasa haziko mbali na mwambao wa Bahari ya Hindi.. Lugha hizo zinaonyeshwa kwenye amam _. R. 1 Orodha hii inafuata tasnifu ya Claire Gregoire (1975, uk. 185-204) inayohusu ngeli za mahali katika lugha za Kibantu.. (Tumeiondoa lugha ya Kinyamwezi ambayo haitumii kiambishi tamati -ni isipokuwa katika maneno machache yaliyoazimiwa kutoka lugha ya Kiswahili. Tena tumeongeza lugha ya Kirangi) Katika baadhi ya lugha hizo kiambishi si -ni lakini -ini.. rabu i ya mwanzoni inasikika vivyo hivyo katika Kikikuyu, kwa mf'anopumba-im, na pengine katika Kizulu, kwa mfano ezulwini 'mbinguni' < iizulu; katika lugha nyingine (kwa mfano E.60, S..30, SAO) hujiunga na irabu itanguliayo; kwa mf~o Kisotho ya Kaskazini (S..32) tseleng 'njiani' < tsela; Kichaga (E62) mringeny 'majini' < mringa.. Kwa hiyo inakubalika kwamba mofimu hii mwanzoni ilikuwa ina umbo la -ini. Basi, swali ambalo tungependa kulijibu ni: Mofimu hii limetungwa vi pi, na wapi, na linl 2. Dhanio ia Raum-Meinhof Carl Meinhof, katika makala iliyotolewa 1942, alipendekeza kwamba asili ya kiambishi tamati -ni ni kiwakilishi kionyeshi cha ngeli ya 18 yenye umbo la imwi Anavyoona Meinhof, kiambishi awali mu- ikalainika, ikawa m- na baadaye ikatoweka kabisa.. Kwa hiyo, watu wakaanza kuongeza kiwakilishi kionyeshi chenye maana ya 'humu' au 'humo'.. Meinhof anadai pia kwamba umbo la mu inaweza kugeuka ni: badiliko lilo hilo limetokea katika mofimu ya nafsi ya pili (wingi) ambayo ni mu kama kiambishi cha kitenzi lakini inaonekana kama nyi au

KAMBSH TAMAn CffA MAHAL -N 129 ~._-- ---..... ji ' - ' ' ' ( ---- ~...,-~...,..-...... - 0 Ramani 1: Lugha zenye ki ambi shi tamat i cha mahali -ini ESO E.60 E70 F33 G.20 G36 GAO G.62 P30 Kikikuyu, Kikamba.,. Kichaga (Machame..) Kipokomo, Kitaita Kirangi Kipare, Kisambaa, Kibondei.. Kikami (si lazima) Kiswahili Kihehe (si lazima) Kimakua, Kilomwe s 20 S30 SAO s..so s 60 Kivenda Kisotho, Kitswana Kinguni (Kizulu, Kixhosa) Kitsonga Kitonga cha nhambane

130 RDDER SAMSOM AND THLO C. SCHADE1JERG ni ikitumiwa kama kiwakilishi nafsi huru, yaani ninyi. Kwa kweli, dhanio hilo limeshapendekezwa katika sarufi ya Kichaga iliyotolewa 1909.. Mwandikaji Raum anasema (uk.. 58): "Die Ortssilbe mu hat sich im Motschi nur als Suffix am Nomen erhalten als Lokativsilbe fli. Der Wechsel im Nasal ist in der unbetonten Endsilbe begreiflich; er hatte zur weiteren Folge den Umlaut von u in i." Gregoire anaona hoja nne zinazoweza kuimarisha dhanio la Raum-Meinhof: Kwanza, si kitu cha kigeni kuturnia kiwakilishi kionyeshi cha mahali pamqja na jina ili kuimarisha maana ya mahali.. Hii inatokea katika baadhi ya lugha za Ki bantu za Afrika Mashariki. Ya pili, eneo la -ini na eneo ambalo kiambishi awali mu- hulainika yanafanana. Ya tatu, katika lugha ya Kigusii (E.42) kuna kihusishi 1m1 yenye maana ya 'katika' inayofuata jina.. Gregoire anafikiri kwamba labda neno hilo (au neno kama hilo) ni asili ya kiambishi tarnati -ni.. Ya nne, inaonekana kwamba kiambishi tarnati -ni kina uhusiano maalum na ngeli ya 18 yenye maana ya undani.. Uhusiano huu unaonekana katika neno la zarnani sana ndani ambalo ni la ngeli 18 (neno nda yenye maana ya 'tumbo' limetoweka katika lugha ya Kiswahili); lakini hapana neno kama hili kutokana na ngeli ya 16 au 17.. Tena, katika lugha ya Kitonga cha nhambane (S.. 62, Msumbiji) vipo viwakilishi vionyeshi vya ngeli za 16 na 18, lakini kile cha ngeli ya 16 hakiwezi kutumika pamoja najina lenye kiambishi cha mahali -nl. Hoja tatu za kwanza hazina nguvu sana. Hoja ya kwanza inaonyesha kwamba muundo huo unawezekana, lakini haionyeshi zaidi.. Hoja ya pili ina tatizo fulani.. Kuna baadhi ya lugha ambazo huturnia -ni badala ya kiambishi awali cha rnahali mu-, lakini viambishi vyenye umbo ilo hilo vya ngeli za 1 na za 3 bado vipo katika lugha hizo bila kulainika. Hoja ya tatu, pia, haitusaidii sana: ingawa asili ya neno hilo mi haijulikani hakuna sababu yoyote kufikiri kwamba inatokana na kiwakilishi kionyeshi cha ngeli ya 18. nayobaki ni hoja ya ya mwisho, yaani maana ya -ni si mahali popote lakini hasa undani.. Upande mwingine kuna sababu ya kupinga dhanio la Raum-Meinhof. natubidi kusisitiza kwamba kiwakilishi cha mahali cha Kiherero imwi 'humu', ambacho Meinhof alifikiri kwamba ni asili ya -(i)ni, hakijulikani katika maenezi la kiambishi tamati cha mahali -ni; tena kanuni za kubadilisha imwi ikawe ini si wazi kabisa.

KAMBSH TAMAT CHA MAHA -N 129 --.--... -.... /,_ \ ' ' ( ------... '....--... ' "..._,... ' ( Ramani 1: Lugha zenye ki ambi shi tamat i eh a mahal i -ini ESO E.60 E70 F33 G.20 G.36 GAO G.62 P30 Kikikuyu, Kikamba. Kichaga (Machame... ) Kipokomo, Kitaita. Kirangi Kipare, Kisambaa, Kibondei. Kikami (si lazima) Kiswahili Kihehe (si lazima) Kimakua, Kilomwe S.20 S30 SAO S50 s 60 Kivenda Kisotho, Kitswana Kinguni (Kizulu, Kixhosa) Kitsonga Kitonga cha nhambane

130 RDDER SAMSOM AND THLO C SCHADEBERG ni ikitumiwa kama kiwakilishi nafsi hum, yaani ninyi.. Kwa kweli, dhanio hila limeshapendekezwa katika sarufi ya Kichaga iliyotolewa 1909.. Mwandikaji Raum anasema (uk.. 58): "Die Ortssilbe mu hat sich im Motschi nur als Suffix am Nomen erhalten als Lokativsilbe fli. Der Wechsel im Nasal ist in der unbetonten Endsilbe begreiflich; er hatte zur weiteren Folge den Umlaut von u in i." Grt!goire anaona hoja nne zinazoweza kuimarisha dhanio la Raum-Meinhof: KwarJZa, si kitu cha kigeni kuturnia kiwakilishi kionyeshi cha rnahali pam~ja na jina ili kuimarisha maana ya mahali. Hii inatokea katika baadhi ya lugha za Kibantu za Afrika Mashariki.. Ya pili, eneo la -ini na eneo ambalo kiambishi awali mu- hulainika yanahmana. Ya tatu, katika lugha ya Kigusii (E42) kuna kihusishi mi yenye maana ya 'katika' inayofuata jina. Gregoire anafikiri kwamba labda neno hilo (au neno karna hila) ni asili ya kiambishi tarnati -ni. Ya nne, inaanekana kwamba kiambishi tamati -ni kina uhusiana maalum na ngeli ya 18 yenye maana ya undani.. Uhusiana huu unaanekana katika nena la zarnani sana ndani ambalo ni la ngeli 18 (neno nda yenye maana ya 'tumba' limetaweka katika lugha ya Kiswahili); lakini hapana neno kama hili kutakana na ngeli ya 16 au 17. Tena, katika lugha ya Kitanga cha nhambane (S.. 62, Msumbiji) vipo viwakilishi vionyeshi vya ngeli za 16 na 18, lakini kile cha ngeli ya 16 hakiwezi kutumika parnoja najina lenye kiambishi cha mahali -ni.. Hoja tatu za kwanza hazina nguvu sana. H~ja ya kwanza inaonyesha kwamba muundo hua unawezekana, lakini haionyeshi zaidi.. Hoja ya pili ina tatiza fulani.. Kuna baadhi ya lugha ambazo huturnia -ni badala ya kiarnbishi awali cha rnahali mu-, lakini viambishi vyenye umbo lilo hila vya ngeli za 1 na za 3 bado vipo katika lugha hiza bila kulainika. Haja ya tatu, pia, haitusaidii sana: ingawa asili ya nena hila mi haijulikani hakuna sababu yoyate kufikiri kwamba inatakana na kiwakilishi kianyeshi cha ngeli ya 18.. nayobaki ni haja ya ya mwisha, yaani maana ya -ni si mahali popote lakini hasa undani Upande mwingine kuna sababu ya kupinga dhania la Raum-Meinhof.. natubidi kusisitiza kwamba kiwakilishi cha mahali cha Kiherera imwi 'humu', ambacha Meinhof alifikiri kwamba ni asili ya -(i)ni, hakijulikani katika maenezi la kiambishi tarnati cha mahali -ni; tena kanuni za kubadilisha imwi ikawe ini si wazi kabisa.

KJAMBSH TAMAT CHA MAHAL -N 131 3. Dhanio la Sacleux Chmles Sacleux ametoa maoni tofauti juu ya asili ya kimnbishi tmnati -ni. Katika Kmnusi yake mamufu (1939) anasema kuwa kimnbishi tmnati hicho kinatokana na neno ini ambalo tafsiri yake kwa Kifm ansa ni 'foie, pmtie intime'. Haelezi zaidi ila katika lahaja moja ya Kiteita, yaani Kidavida, watu husema nyumbeni kufuatana na msinyao wa nyumba na ini: nyumba- ini. Sacleux hakutoa sababu nyengine au maelezo zaidi nao wataalamu wengine wa lugha za Kibantu hawajapata kuangalia fikra hiyo.. Basi nasi tujmibu kukadiria uwezekano wa fikra hiyo kuwa kimnbishi tmnati -ini inatokana na jina ini lenye maana ya 'kinofu chekundu cha ndani ya mwili kilichojaa dmnu na kinachotoa nyongo kusaidia kuyeyusha chakula tumboni' (A. S. Nabhany, Kando ya Kiswahili, muswada).. Maenezi ya shina ini: Rmnani 2 inaonyesha lugha zilizo na neno ini!en ye maana tuliyotaja hapo juu.. Katika lugha nyengine tunayakuta mashina mbalimbali kwa maana ya 'ini' kmna vile: -llma, mnbalo lina maana ya 'moyo' kwa lugha nyengine.. Mashina mengine tupatayo ni -toga, hasa katika lugha za eneo la P, na -bmd! katika lugha za eneo la S.. Basi tukitazama maenezi haya, tunaona maenezi hayo hasa ni katika lugha za Kisabaki, na lugha chache nyengine huko na huko katika Kenya, Tanzania na Uganda.. Mojawapo ya lugha hizi iwe asili ya kimnbishi tmnati -ini. Maana ya neno ini: Tukichambua maana na matumizi ya neno ini kwa Kiswahili, tunaona mambo mawili: (1) Neno la ini au zaidi maini hutumika tu kwa maana ya 'kiungo cha ndani'.. (2) Mnymnbuliko wa jina ini katika ngeli ya 7, yaani kiini, unatumika kwa maana yafuatayo: Sacleux (1939) anaeleza kuwa maana yake hasa ni coeur d'une chose, 'moyo wa kitu', ambayo ni hasa sehemu ya ndani iliyo muhimu kuliko zote.. Kwa mfano kiini cha karafuu ni kama 'chembe' au 'punje' ya karafuu. Neno la kiini pia hutumika kwa njia ya sitiari, naye Sacleux anatoa mfano huo: Pate ndiyo kiini cha ungwana, yaani kisiwa cha Pate kiwe chanzo au asili ya ustaarabu. Mifano mingine ni kiini chajicho kwa 'mboni' (Sacleux

132 RJDDER SAMSOM AND THLO C. SCHADEBERG anatoa kiini cheusi na kiini cheupe), kiini cha yai, na hilo neno pacha tulilotumia katika jina la makala yetu kiini macho (ingawa hapo Krapf 1882 anatoa asili tafimti kabisa: kilimato < killamato!). Sacleux anatoflmtisha kati ya kiini cha mti na moyo wa mti, kwa maana ya kuwa kiini cha mti ni undani wa mti ulio mgumu sana, nao moyo wa mti ndani yake iwe laini. Kwajumla tunaweza kukubali kuwa maana ya 'undani' au 'ndani ya' yangefaa kama asili ya kiambishi cha mahali -ini.. Maana hayo zaidi yangeambatana na ngeli ya mu-, ngeli ya 18.. Mifano rnichache ya Kiswahili cha zamani inaonyesha muungano huu wa kiambishi tamati cha mahali -ni na ngeli ya 18. Katika tasnifu yake (1979) Bi Miehe anataja mifano hiyo ya kiunganishi cha ngeli 18 kilichounganishwa na majina yaliyo na kiambishi tamati -ni; ndani na chini (Jini kwa Kimvita).. Katika Utendi wa "Das Geheimnis der Geheimnisse" (Dammann 1940:222, ubeti 71) kuna sehemu hii: na m;jani mwa kijambaa tja hoyo mbwa Juhaa aso?uu, asofaa mjokozwa ni azizi Und chinnen in dem Tuch jenes unwissenden Hundes, der weder Schaden noch Nutzen aufweist, der von den Machtigen verstoben wird, Mfimo mwengine unatokana na "Utendi wa Fatuma" (Dammann 1940: 116, ubeti 213): na waku.teneo kwake Jini mwa arishi yake shani Jao liwatike wq,the pia kwa a]aa Auch zu denen, welche sich versammelt haben unter seinem oberen Thron, ist ihre Herrlichkeit gekommen, zu ihnen alien in Eile.. Kiswahili cha siku hizi pia kinaonyesha uwezekano wa kuunganishwa kwa njia hiyo, kwa mfano: miongoni mwa..., kusini (au kaskazini) mwa.... Maana hayo ya 'kiungo cha ndani' kuwa asili ya maana ya 'ndani ya' au 'undani' na mwishowe kwa mahali, si ajabu. Walivyoeleza Heine, Claudi na Htinnemeyer (1991) mara nyingi viungo vya mwili hutokea kama dhana za mahali, ingawa kwa maana ya 'katika' hasa maneno kama 'tumbo' huturniwa, kama vile hilo neno la Kiswahili ndani < *nda-ni. Hata hivyo, neno lenye maana

KAMBSH TAMAT CHA MAHAL -N 133 ya '(ma)ini' limepata maana ya 'ndani (ya)' katika lugha ya Kingbandi (Aflika ya Kati); mabadiliko hayo hayo ya maana yametokea katika baadhi ya lugha za visiwa vya Pasifiki (Heine et al 1993: 140)* K wa kweli tumetafuta sana kupata matumizi mengine ya neno la Kiswahili ini au maini ambayo yawe tamathali, yaani si maana halisi tu. Hatukupata, ila msemo maneno ya kukata ini (Ndalu na King' ei 1988:65) au maneno yake yalinikata maini (Sauda Barwany, mawasiliano ya kibiniafsi) tu.. Maana yake ni kufuatana na Ndalu na King'ei 1988: "maneno ya kumkera na kumuudhi mtu"; kufuatana na S.. Barwany maana ni 'maneno yanamwumiza huyo mtu'.. Tena katika methali au rnisemo rningine hatukupata.. Scheven 1981 naye pia hana kiungo cha maini katika orodha yake.. Ukiuliza "Hii ndiyo nini?", mtu anaweza akakujibu "Maini, moja lako m(lja la Salirnini".. Basi, hatuna misemo zaidi.. Pengine hii inathibitisha kuwa kwa Kiswahili maana yenye sitiari au maana tamathali zaidi yanatolewa na maneno kama moyo au mtima nalo hilo neno (ma)ini limepata hasa maana ya kiungo halisi na baadaye maana ya mahali. Kuunganisha kwa maneno: kiwa tunakubaliana na fikra ya Sacleux kuhusu asili ya hiyo -ini ya mahali, inatulazimu tuthibitishe uwezekano wa kuunganisha kwa maneno mawili yawe neno pacha: neno la kwanza liwejina lolote, neno la pili ni ini.. Kwa kweli kwa Kiswahili si rahisi kuunganisha majina mawili ilivyo katika lugha nyingine.. Y ako maneno ambayo yameundwa kutokana na maneno mawili kwa kupoteza kiunganishi -a katikati, kama vile gari (la) moshi, maji (ya) moto, msu (wa) meno.. Hapo jina la pili hueleza kitu kuhusu jina la kwanza: msumeno si meno ya msu, lakini ni msu wenye meno; majimoto si moto wa maji, bali ni maji yenye moto; garimoshi si moshi la gari, lakini ni gari lenye moshi.. Kufuatana na msingi huu tunaweza tukasema nyumba ini si ini la nyumba, yaani ndani ya nyumba, lakini nyumba yenye ini.. Mfano kama huu wa kuwa kiangama ni jina linalotokea baada yajina la kwanza, tunakuta pia katika lugha ya Kiilwana: nyuuba mibeeni, yaani 'katika nyumba' (tafsiri halisi: nyumba rnimbani; D. Nurse, mawasiliano ya binafsi)..

134 RDDER SAMSOM AND THLO C SCHADEBERG,~,. ' ' ' " ' t t"".,..j'-"" '.,,.<~' Ramani 2: Lugha zenye neno ini Lugha zote za Sabaki, yaani lahaja mbalimbali ya Kiswahili, lahaja za Mijikenda, lahaja za Kipokomo, lahaja za Kikomoro - isipokuwa lugha ya Kiilwana Kikiyuyu (ESl) iini (lugha nyingine za kundi la Kenya ya Kati zinatumia neno m lima) Kinyankore (El3) ekine Kihaya (E.22) ine Lumasaba (E.31) khiini Kilugulu (0.35) kini Kisambaa (0.23).. Kizaramo (0.33) ini

KAMBSH TAMAT CHA MAHAL -N 135 4. Chanzo na usambazaji Tukubali kwanza kwamba kiambishi tamati -ini katika lugha zote zionyeshwazo kwenye Ramani 1 kina asili moja. Ni wazi kwamba lugha hizo si tawi moja la lugha za Kibantu; kwa hiyo tukubali tena kwamba kiambishi hicho kimesambaa kutoka lugha mqja.. Kuna lugha moja tu ambayo imeenea kaditi ya kutosha ya kuwa chombo cha kusambaza kwa mofimu hii: lugha ya Kiswahili.. Tena tunajua kwamba Kiswahili kilikuwa na kiambishi hicho tangu zamani sana.. Tunataja majina ya miji miwili tu: ~ji wa "Quelimani", yaani kilimani, huko Msumbiji; tena mji mkuu wa Visiwa vya Komoro, "Moroni", yaani motoni.. (Angalia kwamba shina la jina la mji na wa jina la visiwa ni ule ule moro au moto; ku-moro ni ngeli ya 17 ya Kibantu cha kawaida, moro-ni ni namna ya Kiswahili ya kutaja mahali. Kuna mlima mrefu wa volkeno huko katika kisiwa cha Ngazija.) Kusema kwamba Kiswahili kimekuwa chombo cha kueneza kiambishi tamati cha mahali -ini si kusema kwamba Kiswahi!i kilikuwa lugha ya kutunga mofimu hiyo.. Tungeweza kubuni mfululizo wa matukio ufuatao: Kiambishi -ini kilitokea kwanza katika lugha fulani, baadaye Kiswahili kilikopa mofimu hiyo, baadaye lugha nyingine ziliikopa kutoka kwa Kiswahili.. Tunapotaka kuona lugha zipi zingeweza kuwa asili ya kiambishi tamati -ini inatubidi kutafuta lugha ambazo zina kiambishi hicho pamoja na neno ini. Sasa, tukilinganisha orodha ya lugha yenye kiambishi tamati -ini (taz.. Ramani 1) na lugha zenye neno ini (taz.. Ramani 2) tunatambua kwamba zipo lugha chache tu ambazo zingeweze kuwa asili ya kiambishi tamati -ini. Hizo ni: lugha za Sabaki o Kikikuyu Kisambaa Tunachagua lugha za Sabaki - au pengine lugha ya Sabaki ya asili - kwa sababu mbili.. Ya kwanza, inaelekea kwamba neno ini si ya zamani sana katika lugha za Kikikuyu na Kisambaa.. Kikikuyu ni lugha ya pekee katika tawi la lugha za Kenya ya Kati yenye neno ini, na lugha ya Kisambaa pia ni lugha ya pekee katika tawi lake la "Seuta" ambayo ina neno ini. Sababu ya pili inatokana na umbo.. Kwa Kikikuyu, irabu ya mwisho ya neno ini si sawa na irabu ya mwisho ya kiambishi tamati -im. Angalia kwamba lugha ya pekee katika kundi la Sabaki ambayo imehifadhi irabu saba ya Kibantu cha asili

136 RDDER SAMSOM AND TH/LO C SCHADEBERG ni Kiilwana; katika lugha hiyo kiambishi tamati cha mahali lina iiabu i mwishoni, kwa mfano nyuubeeni 'nyumbani' (D.. Nurse, mawasiliano ya binafsi).. Tena, lugha za kundi la Kisotho/Kitswana (S30) zimehifadhi irabu saba vilevile, na iko wazi kwamba kiambishi tamati chao cha mahali -) kinatokana na *-ini yenye irabu i mwishoni.. Kwa hiyo tunafikiri kwamba asili hasa ya kiambishi cha mahali ni Kiswahili Pendekezo hilo lina matatizo matatu.. Shida ya kwanza ni ukubwa wa eneo la kiambishi hicho -ini. Shida hii inahusu hasa lugha za Afrika Kusini.. Tunajua kwamba Waswahili wa zamani wamefika mpaka Msumbiji wa kati, yaani mpaka mdomo wa mto wa Zambezi, lakini hatuna ushahidi kwamba wamesafiri na kufimya biashara kusini zaidi Hata hivyo, kuna maneno kama imali 'fedha' katika lugha ya Kizulu ambayo inaonyesha kwamba mawasiliano yalikuwepo. Shida ya pili inahusu maana. Tumeona kwamba maana ya kiambishi tamati -ini inafanana na maana ya ngeli ya 18 mu-.. Dhanio la Sacleux inaeleza vizmi ulingano huo: Maana ya neno ini inataja 'kiini' cha kitu.. Kwa bahati mbaya, ulingano huo hauonekani wazi katika lugha ya Kiswahili ya siku hizi, lakini upo katika lugha ya Kitonga ambayo ni mbali sana ya Uswahilini.. natubidi tuseme kwamba kiambishi tamati kilikuwa na maana ya undani chanzoni wakati wa kutawanyika, lakini baadaye maana hii ilipanuka katika lugha ya Kiswahili na lugha nyingine za Sabaki mpaka ikawa na maana ya mahali popote au kokote.. Mifano tuliyoitajajuu kama miongoni mwa na chini mwa (kutokana na Kiswahili cha zamani) yangeweza kuimarisha dhanio hilo. Shida la tatu linahusu umbo la kiambishi.. Shida hilo linafanana na swali kuhusu maana: Umbo la kiambishi lilikuwa -ini kwa asili, lakini katika lugha ya Kiswahili ni -ni hila irabu mwanzoni.. Tukifuata Sacleux tumeshafahamu asili ya ile irabu i: ilikuwa ni kiambishi awali cha ngeli ya 5.. Wakati lugha nyingine zilipokopa mofimu hiyo umbo lake lazima lilikuwa bado -ini. Basi, kufuata kanuni za fonolojia ya Kiswahili tungetarajia kwamba tungesikia **nyumbeni badala ya nyumbani; linganisha irabu e katika hali ya kuamuru kwa wingi piteni. Lakini kama irabu ya mwisho wa kitenzi si a hatusikii dalili ya i, kwa mfano jaribuni.. Kwa hiyo tunapendekeza kwamba umbo la kiambishi tamati cha mahali limesawazishwa likawa -ni baada yajina lolote yenye irabu yoyote mwishoni.

KAMBSH/ TAMAT CHA MAHAL -N 137 Basi, ingawa hatuna hakika kamili juu ya asili ya kiambishi tamati cha mahali -ini inatuelekea kwamba kuna hoja za kutosha kuunga mkono na dhanio la Sacleux kuliko dhanio la Raum-Meinhof. * Tunamshukuru Bi G.. Scheckenbach (Bayreuth) ambaye anatukumbusha kwamba katika lugha ya Kikinga (G.. 65), neno unt1ma '(ma)ini' likiturnika kwa njia ya sitiari lina maana ya mahali panapokaa hisia za binadamu kama hofu na woga. Marejeo Dammann, Emst. 1940.. Dichtungen in der Lamu-Mundart des Suaheli. (Abhandlungen aus dem Gebiet der Auslandskunde der Hansischen Universitat, 51.) Hamburg: Friederichsen, de Gruyter & Co. Gregoire, Claire.. 1975. Les locatifs en bantou. (Annales, 83.. ) Tervuren: Musee royal de ' Afrique Centrale.. Heine, Bernd, Ulrike Claudi na Friederike Htinnemeyer.. 1991.. Grammaticalization.: a conceptual framework. Chicago: The University of Chicago Press.. Heine, Bernd, Tom Gtildemann, Christa Kilian-Hatz, Donald A. Lessau, Heinz Roberg, Mathias Schladt and Thomas Stolz.. 1993.. Conceptual shift; a lexicon of grammaticalization processes in African languages.. (Afrikanistische Arbeitspapiere, 34/35.) Cologne: nstitut ftir Afrikanistik, Universitat zu Koln. Krapf, Ludwig.. 1882. A dictionary of the Suahili language. London.. (Reprint Gregg Press1964, Ridgewood, New Jersey.) Meinhof, CarL 1941142.. Entstehung und Gebrauch der Lokativendung in Bantusprachen.. Zeitschrift fur Eingeborenen-Sprachen 32: 161-164.. Miehe, Gudrun.. 1979.. Die Sprache der tilteren Swahili-Dichtung (Phonologie und Morphologie). (Marburger Studien zur Afdka- und Asienkunde, A18) Berlin: Dietrich Reimer..

138 RDDER SAMSOM AND THLO C SCHADEBERG Ndalu, Ahmed, na Kitula G. King'ei.. 1988; 1991. Kamusi ya semi za Kiswahili.. Nairobi: Heinemann Kenya. Nurse, Derek, na Thomas l. Hinnebusch.. 1993.. Swahili and Sabaki: a linguistic hi.story. Berkeley and Los Angeles: University of California Press.. Raum, l. 1909.. Versuch einer Grammatik der Dschaggasprache (Moschi Dialekt).. (Archiv fiir das Studium deutscher Kolonialsprachen, 1 L) Berlin: Georg Reimer.. Sacleux, Ch. 1939.. Dictionnaire swahili-franfais. Paris: nstitut d'ethnologie.. Scheven, Albert. 198L Swahili proverbs: Nia zikiwa moja, kilicho mbali huja.. Washington, D. C.: University Press of America.