LEARNING BY EAR. Mihadarati na vileo Poromoko la jamii. Episode 6: Matokeo. AUTHOR: Chrispin Mwakideu. EDITOR: Andrea Schmidt, Aboubakary Liongo

Similar documents
Information for assessors (do not distribute this page to participants):

Human Rights Are Universal And Yet...

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

United Pentecostal Church June 2017

Ufunguo wa Kutaalamika Haraka

MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA. Kwa Wanaoanza

Roho Mtakatifu Ni Nini?

LBE 2009 Migration Episode 3: Living without documents

Deutsche Welle, Learning by Ear 2009 Seite 1 People Who Make A Difference Liberia: Anita Varney Health Facilitator, Fishtown/Liberia

MACHAGUO YA UZAZI KUFIKIRIA KUWA MZAZI

Kuzimu na Kurudi na Dr. Rawlings Documentary Video Transcript, TBN Films

walozaliwa, si kwa damu, wala mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, mbali kwa Mungu. Sisi sio tena binadamu wa kawaida tu kwa sababu sisi ni w

2

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti

usudi la Maisha Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na kupishana usiku na mchana, kuna kweli ishara kwa wenye akili, ambaye mkumbuke-

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

Utangulizi wa ugonjwa wa shinikizo la damu

LEARNING BY EAR MGENI KIZABIZABINA MSOALIKWA- VITA VYA FAMILIA MOJA DHIDI YA UGONJWA WA MALARIA

United Pentecostal Church April Kushangilia Kwa Sala

Ushindi ndani ya Kristo W. W. PRESCOTT

2

ULEMAVU BARANI AFRIKA EPISODE 4: '' ULEMAVU SIO KUTOWEZA'' SCENE TWO: AT OLUANDA S SCHOOL COMPOUND

Nia Dhidi Ya Kristo Je Unamheshimu?

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) VERBATIM REPORT OF

Early Grade Reading Assessment for Kenya

Kiu Cha umtafuta Mungu

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Adhabu ya jino kwa jino na Musitakabali wa imani zetu

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level

Mutugi Kamundi. Jemma Kahn. Kiswahili. Demane na pacha wake. Author - South African Folktale

Ndugu na dada zangu wapendwa,

Ndugu na dada zangu wapendwa,

YEHOVA-YIRE 1. 2 Baba yetu wa Mbinguni, tunakikaribia Kiti Chako cha. 3 Tunakushukuru kwa kutuzuru jana jioni. Tunaomba

Kuwa na Ukimwi ni kama vile kutakiwa kuendelea kuuzima moto unaoniunguza bila kukoma.

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC)

UMRI WA MAKAMO NA KUKOMA KWA HEDHI

KAMA MUNGU YU PAMOJA NASI, BASI YAKO WAPI MATENDO YAKE YA AJABU?

SwahiliWeb ELECTRONIC DEPOSITORY AND RESOURCE ARCHIVE.

IM ETUPASA KUTIMIZA HA KI YOTE

Mukhtasari Wa Mabishano Kwa Na Dhidi Ya Vikombe Vingi Vya Ushirika

Haja Ya Dini. Author(s): Publisher(s): Translator(s): Category: Topic Tags: Featured Category: Published on Al-Islam.org (

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

Ellen White, waasisi wa Kiadventista,na Sabato Lunar

Hatari, Haki za Usalama katika Bahari 03

Oktoba-Desemba

March 14, 2018 PARLIAMENTARY DEBATES 1 NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL REPORT. Wednesday, 14 th March The House met at 9.30 a.m.

Siku ya kwanza. Mguso wa ngozi-kwa-ngozi (Ulezi wa kangaruu) Mtoto wako anaweza kuhisi mdundo wa moyo wako

JE! MUNGU ANAMPA MWANAMKE HAKI YA KUTOA MIMBA IWAPO NI MHANGA WA UBAKAJI?

Pronunciation: Mä-hret Zäläke Ndal-ka-tscho Molla Mare Gebre-gzabiär 1/12

JE, YAWEZEKANA KUISHI BILA KUTENDA DHAMBI?

Inavyodaiwa na wanaochanganya Biblia. Ellis Forsman. Inavyodaiwa na Wanao changanya Biblia (Alleged Bible Contradictions) 1

Iliyoendelea sana. Kitengo cha 2. Kitabu cha mwanafunzi Iliyoendelea sana

"ATATOKEA MARA YA PILI, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu." Waebrania 9:28.

Vijana wanazungumza kuhusu ujinsia, maisha na uhusiano VIJANA WANAZUNGUMZA KUHUSU NGONO, MAISHA NA UHUSIANO. Training and Research Support Centre

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC)

Elimukombozi, Lugha na Upashanaji Habari nchini Tanzania, katika Muktadha wa Utandawazi

KWA NINI SISI SI MADHEHEBU?

Kocha Mkuu. mabingwa. itakuwa INASTAHILI. Ili Kutoa mafunzo kwa wanafunzi wako kuwa. itakuwa ya kuumiza. Itachukua muda. Itahitaji moyo wa kujitoa.

JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1

April 14, 2016 COUNTY ASSEMBLY DEBATES 52

MASWALI NA MAJIBU JUU YA KITABU CHA MWANZO

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

MUNGU ALIUMBA ULIMWENGU 1 WETU NA VYOTE VILIVYO HAI

If a tree falls - Deforestation in Africa"

Kifo Na Mbingu. (Death And Heaven) Ellis P. Forsman. Kifo Na Mbingu (Death And Heaven) 1

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC)

Maisha Yaliyojaa Maombi

Kuwawezesha wasichana kwa kuboresha kujikubali na kujithamini Hivi Ndivyo Nilivyo

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC)

Tafuteni Kwanza Ufalme Wa Mungu

2 LILE NENO LILILONENWA

Kiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika

MAADHIMISHO YA MIAKA 15 YA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

wasiofaa. Naomba sana kila raia afanye bidii awezavyo kumkaribia Mwenyezi Mungu vile anavyoona inafaa, lakini asipitishe hukumu juu ya wengine.

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees

Yaliyomo. Kuhusu kitabu hiki. Hautakuwa peke yako. Mfumo wa msaada ni wa manufaa sana wazazi wote wanahitaji!

Makasisi. Waingia Uislamu

Juni 3-9 Pata Manufaa Kamili kwakusomabiblia

UTARATIBU WA KANISA. 2 Jambo la kwanza ninalotaka kusema ni kwamba mchungaji. 3 Sisi tunaamini katika Kanisa la kimitume, tukifundisha

Theolojia Ujumla. Mike Taylor Semester Munguishi Bible College

Mafundisho Ya Msingi Wa Kikristo. Na Andrew Connally

Agano Lililofunikwa Kwa Damu

KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA

TIST HABARI MOTO MOTO

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

KUTAMBUA SIKU YA KO NA UJUMBE WAKE

Makala ya Mshiriki wa Mafunzo

WEWE NI NANI? Toleo X Toleo Ukweli wa Injeli Toleo 23

Uongozi Siri Na Larry Chkoreff. Version 1.2 Desemba 2010

Wewe Maisha Yako Ndoto Zako. Kitabu cha Vijana Balehe

SautiElimu. Sauti Yako Isikike

Upande 1.0 Bajeti yako

maombi, kabla tu hatujalifungua Neno hili la Kiungu.

Tora UTANGULIZI KWA TORA SOMO LA KWANZA

N09/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q

Palliative Care Toolkit

December 19, 2017 MOMBASA COUNTY ASSEMBLY DEBATES 30

ORODHA YA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI SPIKA MHE. PANDU AMEIR KIFICHO. Rais.

MAANA HALISI IMAAN ( I )

Transcription:

LEARNING BY EAR Mihadarati na vileo Poromoko la jamii Episode 6: Matokeo AUTHOR: Chrispin Mwakideu EDITOR: Andrea Schmidt, Aboubakary Liongo PROOFREADER: Charlotte Collins List of characters by scene: SCENE ONE: AT THE POLICE STATION Beri (f, 45) Inspekta Tino (m, 40) SCENE TWO: MORNING AT CHUNGA SANA BUS STOP Jabali (m, 18) Chambo (m, 30) SCENE THREE: OKOSHO AND ZULA AT BAMJU'S Zula (m, 18) Okosho (m, 18) Bamju (m, 40) 1

SCENE FOUR: CHAMBO AND JABALI AT THE REHAB CENTRE Jabali (m, 18) Chambo (m, 30) Jane (f, 35) SCENE FIVE: AT THE POLICE STATION Beri (f, 45) MSIMULIZI (m/f) 2

INTRO: Nakusalimu nikikukaribisha tena katika Noa bongo! Jenga maisha yako. Hiki kikiwa ni kipindi cha sita katika tamthilia inayoendelea kuhusu mihadarati na vileo kwa jina Poromoko la jamii. Kipindi kilichopita tuliona wanawake wa Chunga Sana wakiandamana kulalamika juu ya waume zao, ambao pombe haramu ilikwisha wafanya geu geu. Inspekta Tino alipigwa na mshangao mkuu, pale mkubwa wake Beri alipojiunga na waandamaji hao. Baadaye, Puyanga alitiwa mbaroni na mke wake Beri kwa mashtaka ya kujihusisha na biashara ya mihadarati. Jabali akajitolea kumsaidia Chambo katika kazi yake ya Youth watch inayoelimisha vijana kuepuka mihadarati na pia kuwashauri waathirika wa madawa haramu na vileo. Kwengineko, rafiki wa Jabali, Zula na Okosho wameanza kuishi maisha ya hali ya juu. Lakini hii itaendelea kwa muda gani? Tutambue yote katika kipindi cha leo, kiitwacho Matokeo. Tunaanza na simu ya dharura kutoka kwa Bamju ambaye hakuwa na habari Puyanga kakamatwa na polisi. SCENE ONE: AT THE POLICE STATION 1. BERI: (tough and firm voice) Inspekta Tino! Una hakika Bidhaa zote za Puyanga uko nazo? 2. INSP. TINO: Ndio, mkubwa. Inaonekana mumewako ni tajiri sana lakini njia za kupata hiyo mali ndiyo hazijulikani. 3. BERI: Tafadhali, Inspekta, wacha kumuita mumewangu. Kwa sasa yeye ni mshukiwa. 4. SFX: MOBILE PHONE RINGING 3

5. BERI: (hurriedly) Hiyo ni simu yake! Ninajuwa mlio wake. Hebu angalia nani anapiga, lakini usijibu. 6. INSP. TINO: Bamju anapiga! Nilikwambiaje nilijuwa anahusika na madawa ya kulevya. Nimejaribu sana kumkamata. Tufanyeje? 7. BERI: Kata simu. Ni muhimu tufikirie kidogo jinsi ya kutatua kesi hii. 8. INSP. TINO: Pole sana kwa haya, Beri. Wewe ni kielelezo kizuri cha kikosi cha polisi. Nakuvulia kofia afande. 9. BERI: Ah, wacha kunihurumia! Kazi iko uko nje, kuna haja ya kwenda na kuzuia watu wasiuze madawa ya kulevya ili kuharibu maisha ya wananchi. 10. SFX: SAME MOBILE PHONE RINGING AGAIN 11. INSP. TINO: Bamju tena. Inaonekana hana subira mwenzetu. 12. MSIMULIZI: Kweli, sio subira tu, bali wasiwasi pia uliomwingia Bamju. Alihitaji madawa ya kulevya zaidi kwani biashara inanawiri akashindwa kwanini hampati Puyanga? Kwengineko, asubui hiyo, katika kituo cha basi cha Chunga Sana, Jabali alimpata Chambo akiwa anamsubiri. 4

SCENE TWO: MORNING AT CHUNGA SANA BUS STOP 13. SFX: BUS STOP AMBIENCE, MORNING 14. CHAMBO: Yani siku yako ya kwanza, na umechelewa kazini 15. JABALI: Kumradhi. Habari za asubui. 16. CHAMBO: Za kwangu njema. Una hakika uko tayari? Nakuahidi haitakuwa kazi rahisi. 17. JABALI: Niko tayari. Leo nitafanya nini? 18. CHAMBO: Nina kipindi cha ushauri leo katika kituo cha kubadili tabia na waathiriwa wa mihadarati, kisha mkutano wa viongozi wa kituo hicho, alafu baadaye mihangaiko yangu ya kawaida. 19. JABALI: (takes a deep breath) Sawa. Twende kazi! 20. MSIMULIZI: Ingawa juhudi nyingi zimefanywa, walakin Afrika ingali nyuma kwa masuala ya waathiriwa wa mihadarati na jinsi ya kuwasaidia. bado tunahitaji wataalamu wa ushauri, vifaa, matibabu na huduma ili kumudu idadi ya waathiriwa hawa. Hata Chambo ana mafunzo kidogo. Lakini kwanza, tuone jinsi Okosho na Zula watakavyozichukuwa habari mbaya. 5

SCENE THREE: OKOSHO AND ZULA AT BAMJU'S 21. SFX: HEAVY BANGING ON A TABLE (studio) 22. OKOSHO: (furious) Unamaanisha nini, humpati muuzaji? Twahitaji mali, tena sasa hivi! 23. BAMJU: ( calm but threatening) Kijana, chunga mdomo wako! Nilikwambia, sijui ni kwanini hachukui simu yangu. Nimejaribu mara mia moja na moja. 24. ZULA: (speaking sluggishly he is high ) Aah labda labda Labda amekufa. Unajuwa, kama kama... katika sinema, mameni. 25. OKOSHO: (suddenly begging) Tafadhali. Twahitaji bidhaa, Bamju. Tafadhali tusaidie. Hauoni twateseka? Hatuwezi kufanya chochote bila dozi yetu ya kila siku. Tafadhali tusaidie, tafadhali. (almost in tears) 26. (ZULA is heard snoring) 27. BAMJU: (angrily) Nje! Tokeni nje, nyote wawili! Bure sana, makabeji ya bei duni. Kazi kwisha. Nyinyi tayari mumekuwa waathiriwa. Niliwaonya heroini sio ubani wa kutafuna. Nje! 28. OKOSHO: Tafadhali Tafadhali, Bamju! 6

29. ZULA: (as if in a dream, still sluggish) Okosho, Nini... kuna nini tena kilichotokea mameni? 30. BAMJU: Hakuna kilichotokea! Au kitakachotokea. Na sitaki kuwaona tena hapa kwangu. Mumenielewa? 31. SFX: DOOR OPENED, THEN CLOSED AND LOCKED; NOISE OF TOWN IN BACKGROUND 32. OKOSHO: (thinking aloud) Hapana, haiwezakani nakumbuka... Bamju akisema kuna wauzaji unga wengine hapa Chunga Sana. Ni lazima tuwatafute watuuzie dozi yetu. Lakini pesa je? Tutapataje kama hatuna kazi? Hmm nishajua. twenzetu, mameni Zula, tukachape kazi. 33. MSIMULIZI: Moja ya matokeo ya utumizi wa mihadarati na vileo, ni kwamba humgeuza mtu kuwa mhalifu. Tayari tunaona dalili hizi kwa Okosho na Zula ambao washaathiriwa na madawa. Watafanya nini ili kujipatia dose yao? Zidi kusikiliza. Si mbali sana na hapo, Jabali na Chambo walifika kwenye kituo cha kurekebisha waathiriwa, yaani rehab centre. Jabali alistaajabu kuona mtu wa kwanza aliyekuwa mwanamke kwa jina, Jane. Jane alikuwa na miaka thelathini hivi, na Jabali hakuelewa kivipi mrembo kama huyu kuishia mahala kama hapa. 7

SCENE FOUR: CHAMBO AND JABALI AT THE REHAB CENTRE 34. SFX: 3 WOODEN CHAIRS BEING PULLED ACROSS THE FLOOR. 35. CHAMBO: Habari, Jane. Nafurahi kukuona tena hii asubui. 36. JANE: Mzuri sana, Chambo. Ni nani huyu kijana mzuri? Ni kakako? 37. CHAMBO: Hapana. Ni mfanyakazi mwenzangu. Unaonaje kama akijiunga nasi? 38. JANE: Hamna tatizo. Angalau tupumue kwa kuona sura mpya. 39. CHAMBO: Vyema basi! Sawa, endelea basi, mweleze wewe ni nani. Kwa maana naona tayari damu zenu zimepatana. 40. JABALI: (clears throat) Kwa majina naitwa... ni Jabali. Nashukuru kukujua! 41. JANE: Ni vyema kukujua, Jabali. 42. CHAMBO: Sawa. Sasa, tuanze basi? Jane, mbona usimueleze basi kwanini uko hapa. 8

43. JANE: Niko hapa kwa sababu nahitaji msaada. Nimeathiriwa na nikotini. Nikotini inapatikana katika bidhaa zote za tumbaku, nilianza kuvuta sigara tangu nikiwa shule ya upili. Nilipohitimu nilikuwa navuta paketi nzima kwa siku, baada ya hapo ndipo nikawa siwezi tena bila sigara. Majuzi nilianza kupata madhara katika afya yangu, na nilipochunguzwa na daktari, akanishauri niache sigara. Sio rahisi, lakini kwa ushauri wa Chambo naona maendeleo. 44. CHAMBO: Sasa unajisikiaje? 45. JANE: Kichwa bado kinaniuma. Tamaa inapunguwa, lakini mwili bado unataka sigara. 46. CHAMBO: Jane, unaendelea vyema. Kumbuka, hamu ikikujia, ndio unafanyaje 47. JANE: najikumbusha tena na tena, kwanini nahitaji kuacha. 48. CHAMBO: Na unakumbuka sababu hizo, Jane? Kweli? 49. JANE: (worried) Naweza kujikumbusha kwa kusoma karatasi pale nilipoziandika? 50. CHAMBO: Bila shaka! 51. SFX: PAPER TAKEN OUT OF A POCKET (studio) 9

52. JANE: (calmer, reading from paper) Sababu ya kwanza: nawacha sigara kwa sababu zinahatarisha afya yangu na sitaki kufa kwa ajili ya nikotini. Pili, Naepuka sigara kwa sababu hazinidhuru mimi pekee, bali wote walio karibu yangu. Tatu,nawacha uvutaji kwa sababu ni ghali na siwezi matumizi haya. Nne 53. MSIMULIZI: Jane akiendelea kunukuu sababu zake za kuacha uvutaji sigara. Jabali alitulia tuli, akimtazama, akamsikiliza, na kupendezwa mno na motisha alokuwa nayo Jane. Bamju, upande mwengine, alifikia pomoni.. kwa hivyo alifanya lile wengi wetu siku hizi hufanya wakati simu unayopiga haishikwi. SCENE FIVE: AT THE POLICE STATION 54. SFX: SMS RINGTONE AS WHEN A TEXT MESSAGE ARRIVES 55. BERI: (excited) Shabash! Subira huvuta heri. Sasa, Bw. Bamju, umetuma ujumbe gani kwa mume wangu? 56. SFX: BEEP TONE AS WHEN ONE OPENS A TEXT MESSAGE 1

57. BERI: (reads out) Bosi, kunaendelea nini? Najaaribu kukupigia sikupati. Mzigo wa leo sijaupata. Wafanyikazi wawili tayari nimewaachisha kazi. Au nikauchukuwe mzigo mwenyewe? Nasubiri unitume. Bamju. (thinking aloud) Hmm ndiyo sababu Puyanga anajiona ni mkurugenzi hata nyumbani. Hata hivyo nifanyeje sasa? Hmm 58. SFX: BEEPS AS WHEN ONE TYPES A TEXT MESSAGE. 59. BERI: (talking as she types) Pole. Nimeshikika. Ndio,nenda kachukuwe mzigo mwenyewe. Unakujuwa kweli huko mzigo uliko? Puyanga (Pause) Tuma ujumbe! Tafadhali 60. SFX: BEEP TONE AS WHEN MESSAGE IS SENT. 61. BERI: Pole mumewangu, imenibidi nidanganye kidogo. Lakini la kuwa umeshikika kidogo si uongo. Sasa, wacha tuone kama Bamju ni mjinga kama ninavyodhania. 62. MSIMULIZI: Bamju alifurahia ujumbe kutoka kwa Puyanga, bila kujuwa ujumbe ule ulitoka kwa Beri, kule kituo cha polisi alikozuiwa Puyanga. Alimtumia ujumbe haraka Puyanga - na Beri karibu azirai. 63. SFX: SMS TONE AS WHEN A TEXT MESSAGE ARRIVES 11

64. BERI: (impressed) Lahaula! Haraka jinsi hiyo... Wacha tuone... (reads text out again) Nashukuru kujuwa uko sawa. Ndio, nakumbuka ukinieleza mzigo uko kwa (sound of shocked disbelief) Mjumbe wetu (mbunge wa eneo letu), Mheshimiwa Kizito. Kama kuna mabadiliko yeyote nieleze. Shukran Bosi tuko pamoja. OUTRO: Mshangao, hofu, kutoamini: Beri alihisi hisia hizi zote, na zaidi. Ngazi hii inaelekea wapi? Hakupoteza hata dakika moja, kwani alishafahamu kitu muhimu sana, lakini atachukua hatua gani? Atamgeukia nani, ikiwa waheshimiwa na wakuu wa serikali wanahusika katika hazma hii? Na je Okosho na Zula wanapanga nini ili kujipatia dozi yao? Bado Chambo na Jabali wako kule kwenye kituo cha kurekebisha waathiriwa madawa ya kulevya na kuna mengi yanayowangoja. Yote haya na mengine, ni katika kipindi kijacho. Kusikiliza tena hiki kipindi, au vingine vilivyorushwa hewani, tembelea tovuti zetu za www.dw.de/lbe Hadi wakati mwingine, kwaheri. 1