Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

Similar documents
GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Taarifa Kuhusu Hali ya Uchumi wa Tanzania

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA MHESHIMIWA DKT

Information for assessors (do not distribute this page to participants):

TANZANIA MARKETS PAN Sera zinazoboresha masoko

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA FEDHA

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, MHESHIMIWA DKT. PHILIP I. MPANGO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO

JAMHURI YA KENYA. Mkakati wa Ushirikiano MUKHTASARI FY Public Disclosure Authorized. Public Disclosure Authorized

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU

In the matter of an Application by the KIGOMA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (KUWASA) For a Tariff and Charges Adjustment

KUHUSU AFRODAD. Dira ya AFRODAD. Dhamira ya AFRODAD. AFRODAD inalenga mchakato sawa na endelevu wa maendeleo kuelekea Afrika yenye mafanikio.

Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi

ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA UCHUMI WA ZANZIBAR

Kubadili Sheria Za Mbegu Na Ulinzi Wa Aina Za Mbegu Na Mimea Nchini Tanzania

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA,KWA WANANCHI, 30 SEPTEMBA, 2001

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

MAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

In the matter of Application by the TANGA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (TANGA UWASA) For a Multi-Year Tariff Adjustment

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

NGUZO KUMI ZA KILIMO KWANZA

MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2017/18

MAADHIMISHO YA MIAKA 15 YA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

Kuuelewa Mchakato wa Bajeti Tanzania Mwongozo wa Asasi za Kiraia

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali ya Madini Ukanda

ORDER NO BACKGROUND

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA. Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo. TOLEO Na.

Miradi na jamii. 3.1 Utangulizi

Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2013

Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara)

Dodoma ambako kikao cha Bunge kinaendelea kuja kushiriki japo sehemu ya uzinduzi wa mkutano.

TANZANIA TAARIFA YA MWISHO WA UTEKELEZAJI

RIPOTI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI

Programu ya Uendelezaji Mifumo ya Maji Vijijini (PUMMV) katika Tanzania. Modeli wa Ukodishaji Mradi

NGUO MPYA ZA UKOLONI. Mikataba ya Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Umoja wa Ulaya na Afrika. Agosti 2017

MAPENDEKEZO YA MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA TANZANIA

Kutetea Haki za Binadamu

Dibaji ya Mwenyekiti wa Kamati ya Pamoja ya Uongozi

UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA)

TANGA CEMENT PLC ANNUAL REPORT TAARIFA YA MWAKA.

Kiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika

UFUPISHO WA 35. Hali ya kiulimwengu ya Tekinolojia ya kibiashara/ugeuzi jeni na uboreshaji mazao: Clive James Chair, ISAAA Board of Directors

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig

MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA PRO-ROUTES. Ombi kwa ajili ya fedha za umma wa mradi wa ziada

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu WEMA

Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame M. Mbarawa (Mb.); Waheshimiwa Mawaziri na Wabunge wote mliohudhuria;

Human Rights Are Universal And Yet...

Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA 2006/07

5. Mheshimiwa Spika, Bunge lako Tukufu lilijadili kwa kina Miswada ifuatayo:

TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM)

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

TAARIFA YA MWAKA YA UTENDAJI KAZI IDARA YA UTAWALA BORA 2013/2014

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA, KWA WANANCHI, TAREHE 31 JULAI 2001

RIPOTI YA WARSHA KUHUSU HABARI KWA AJILI YA UWAJIBIKAJI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

MWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI

Summaries of GC Reports 2012, Vol. 2, Sec. 1, Swahili

UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU VIKWAZO VYA KULINDA MAISHA KATIKA USAIDIZI WA KIMATAIFA WA AFYA KWA MSAADA WA KIMATAIFA UNAOFADHILIWA NA MAREKANI

Sera ya Faragha. Upeo. Aina za Data na Mbinu za Ukusanyaji

KUSHUKA KWA HADHI YA LUGHA ZA JAMII NCHINI TANZANIA YOHANA P. MSANJILA University of Dar es Salaam, Tanzania

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees

Govt increases vetting threshold of contracts

HISTORIA, MAENDELEO NA MABADILIKO YA KATIBA TANZANIA TANGU UHURU HADI MIAKA HAMSINI YA UHURU 9 DESEMBA 2011.

Nilikua na Ndoto ya Kumaliza Shule Changamoto za Elimu ya Sekondari Tanzania

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU

ONDOA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA AFYA YA WATOTO

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )

Mwongozo wa Kutathimini mifumo ya Ugawanaji wa faida na Mapato Katika Miradi ya Jamii ya MKUHUMI

Kufanya Uwekezaji kuwa wa Manufaa kwa Afrika: Jibu la Mbunge kuhusu Unyakuzi wa Ardhi

KIMAZINGIRA NA KIJAMII NA MPANGO WA UDHIBITI

Elimu Bora, lakini... C HakiElimu Elimu bora, lakini...

Deputy Minister for Finance

KAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI TANZANIA

Songa kwenye kilele cha upeo. Masuala ya Msingi na Ujuzi juu ya Uendeshaji wa Serikali za Mitaa

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA NISHATI NA MADINI

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

Ufanisi katika Ufundishaji kwenye Shule za Msingi na Sekondari nchini Tanzania

Pronunciation: Mä-hret Zäläke Ndal-ka-tscho Molla Mare Gebre-gzabiär 1/12

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )

Uhakika wa Mbegu kwa Uhakika wa Chakula MWONGOZO WA UZALISHAJI WA MBEGU ZA ASILI ZA MAHINDI

Mipango ya miradi katika udugu

Bustani 10,000 Katika Afrika. Alberto Prina

HAKI NA TARATIBU ZA AJIRA, KAZI NA HIFADHI YA JAMII

Elimukombozi, Lugha na Upashanaji Habari nchini Tanzania, katika Muktadha wa Utandawazi

Muhtasari wa taarifa ya warsha ya wataalamu juu ya mfumo wa habari kwa njia ya ramani (PGIS), Morogoro, Juni 30 - Julai 1, 2014

USIMAMIZI MKUU WA UBORA WA MAHURUJI

KUWEZESHA MBINU ZA UZUIAJI MIMBA KATIKA SUHULA ZA AFYA: MASWALI 10 KWA VIKUNDI VYA JAMII KUZINGATIA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TISA. Kikao cha Pili - Tarehe 14 Aprili, 2010

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA SITA

Kimesanifiwa na:- E.D.Kissuu ECOMM TANZANIA S.L.P ,Dar es Salaam. Simu:

HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE

muhtasari 37 brief 37 Kiwango cha kiutandawazi cha mazao ya kibiashara ya kibayoteki/ugeuzi jeni: 2007 Clive James Bordi ya wakurugenzi wa ISAAA

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara

The Government is committed to improve marine transport and has a number

Transcription:

Policy brief TZ.12/2010K Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada? 1. Utangulizi Kila mwaka Bunge la Tanzania hupitia na kuchanganua kwa makini bajeti ya Serikali. Misamaha ya kodi, kwa upande mwingine, haipati nafasi sawia ya kupitiwa Bungeni, hivyo kuifanya kuwa matumizi yaliyofichika (hidden expenditures). Misamaha ya kodi inahusisha kiasi kikubwa cha fedha. Mwaka 2009/10 peke yake, asilimia 2.3 ya pato la taifa au TZS 695 bilioni zilitolewa kama misamaha ya kodi. Ukubwa wa kiwango cha fedha kinachohusishwa kinaibua maswali kuhusu makusudi ya motisha hizi na iwapo kiwango kinachotumika kinafaa kutolewa. Je, inawezekana kuwa misamaha ya kodi ni mikubwa mno kwa nchi ambayo inakabiliwa na changamoto ya kukusanya fedha za kutosha kugharamia bajeti yake? Je, inawezekana kuwa Tanzania ingekuwa na unafuu kama misamaha inayotolewa ingepunguzwa na badala yake fedha zaidi kutumika kugharimia afya, maji na elimu? Na kwanini taarifa kuhusu nani anafaidika na misamaha hazipatikani kwa umma? Muhtasari huu hautoi msimamo kuhusu masuala haya. Badala yake kwa kuwasilisha mambo 9 kuhusu misamaha ya kodi Tanzania, unalenga kuchangia katika mjadala kuhusu iwapo hali iliyopo sasa ina manufaa. Uchambuzi huu unatokana na taarifa za mapato ya kodi zilizopatikana kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) 1. Unaonesha kuwa: Misamaha ya kodi imeongezeka kwa kiwango kikubwa katika sehemu ya pili wa muongo huu (2006-2010). Kama misamaha ya kodi ingetolewa kwa kiwango kinachoshabihiana na kile kinachotolewa na nchi ya Kenya (asilimia 1 ya pato la taifa) upungufu katika malengo ya ukusanyaji wa mapato ungeweza kuepukika. Muhtasari huu umeandaliwa na Uwazi-Twaweza, iliyopo Hivos Tanzania Uwazi, S.L.P 38342, Dar es Salaam, Tanzania. Simu +255 22 266 4301. Nukushi +255 22 266 4308. Barua pepe: info@uwazi.org. Tovuti: www.uwazi.org Kimetolewa Oktoba 2010 1

Misamaha ya kodi inayotolewa na Mamlaka ya Mapato (TRA) katika visiwa vya Zanzibar ni mara mbili ya misamaha ya kodi inayotolewa Tanzania bara. Misamaha ya kodi inawanufaisha zaidi wawekezaji wakubwa wenye vyeti vya kupatiwa motisha kutoka katika Kituo cha Uwekezaji Tanzania (Tanzania Investment Centre) na Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (Zanzibar Investment Promotion Authority). 2. Sababu za kutolewa kwa misamaha ya kodi Misamaha ya kodi hutolewa kwa sababu mbalimbali. Nchini Tanzania, misamaha ya kodi hutolewa kwa sababu zifuatazo: Pale ambapo kutokana na asili ya ugeni au nafasi rasmi inayoambatana na matumizi ya bidhaa husika, bidhaa hiyo inakuwa hairuhusiwi kutozwa kodi kwa mfano matumizi ndani ya ndege zinazosafiri kwenda nchi za nje, au bidhaa zinazotumika jeshini na katika misioni za kidiplomasia. Pale ambapo shughuli zinazofanywa na baadhi ya mashirika hazizalishi faida lakini zina mchango muhimu kwa jamii ambao serikali pengine isingeweza kuufanikisha. Kigezo hiki kinatumika kutoa misamaha ya kodi kwa taasisi zinazotoa misaada ikiwa ni pamoja na mashirika ya dini. Pale ambapo matumizi ya bidhaa fulani yana faida kwa jamii. Kwa mfano: baadhi ya dawa za binadamu na mifugo zina msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (Value Added Tax au VAT), kama ilivyo kwa magari ya zimamoto. Kutotoza bidhaa kama hizi kodi kunaongeza matumizi yake, na kuleta manufaa zaidi kwa mchango wake chanya kwa jamii Sababu nyingine ya misamaha ya kodi ni kuchochea ukuaji wa uchumi. Misamaha hii kwa kawaida inategemewa kuongeza uwekezaji, ajira, ukuaji wa pato na hivyo kuleta mapato zaidi ya kodi katika muda mrefu. Makundi ya makampuni yanayopewa aina mbalimbali za misamaha ya kodi kama vile katika kodi inayotozwa faida za mashirika/makampuni, na kupunguziwa ushuru wa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje yanaangukia katika kundi hili. Mfano wa wazi zaidi wa makampuni haya ni makampuni yalioanzishwa chini ya sheria ya maeneo ya usindikaji kwa ajili ya mauzo nje ya nchi [The Export Processing Zones Authority (EPZA) Act], makampuni ya uchimbaji madini na makampuni mengine yenye vyeti vya kupewa motisha kutoka TIC na ZIPA. 3. Mambo tisa kuhusu misamaha ya kodi Tanzania Jambo la kwanza: Kiasi kikubwa cha mapato hakikusanywi Kiasi cha pesa ambazo Tanzania inatoa kama misamaha ya kodi ni kikubwa lakini kimeongezeka zaidi katikati ya muongo huu. Katika kilele cha ukuaji wake, misamaha ya 2

kodi iliongezeka takribani mara mbili ndani ya mwaka mmoja, ikipanda kutoka TZS 459 bilioni mwaka 2004/05 hadi TZS 772 bilioni mwaka 2005/06. Mwaka 2009/10 misamaha ya kodi ilifikia TZS 695 bilioni. Kiasi hiki ni zaidi ya nusu ya TZS 1.3 trilioni ambayo Serikali inapanga kukopa kutoka taasisi za fedha za nchi za nje kwa ajili ya kugharimia ujenzi wa miundo mbinu mwaka 2010/11. Kama kiasi hiki cha fedha kingekusanywa, kingewezesha rasilimali kwa ajili ya elimu kuongezwa kwa zaidi ya asilimia 40 au kingefanikisha kupatikana kwa asilimia 72 zaidi ya rasilimali kwa ajili ya afya mwaka 2009/10. Kielelezo na. 1: Misamaha ya kodi Tanzania, mwaka wa fedha 2000-2010 3 Chanzo cha data: Ripoti za mapato ya Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Jambo la pili: Tanzania inatoa misamaha ya kodi zaidi ikilinganishwa na majirani zake Kiwango cha misamaha ya kodi zinazotolewa na Tanzania ni kikubwa. Hii inaonekana wazi kwa kulinganisha kiwango cha misamaha ya kodi kinachotolewa Tanzania na kile kinachotolewa Uganda na Kenya. Nchini Tanzania kati ya miaka ya 2005/06 na 2007/08 misamaha ya kodi ilikadiriwa kuwa wastani wa asilimia 3.9 ya pato la taifa. Mwaka 2008/09 misamaha ya kodi ilikuwa asilimia 2.8 ya pato la taifa na mwaka 2009/10 asilimia 2.3. Ukilinganisha na Kenya na Uganda misamaha ilifikia asilimia 1 na 0.4 ya pato la taifa la kila nchi husika 4 kwa mtiririko huo. Kama Tanzania ingerekebisha viwango vya misamaha ya kodi ili kulingana na kiwango kilichofikiwa na Kenya, zaidi ya TZS 600 bilioni zingeokolewa kwa mwaka 2007/08 peke yake. Ukubwa wa kiwango cha misamaha inayotolewa unaweza kuelezewa kwa kukilinganisha na malengo ya ukusanyaji wa mapato ya kodi ambayo Tanzania inashindwa kuyafikia. Katika mwaka 2008/09 na 2009/10 Serikali haikutimiza lengo lake la mapato kwa wastani wa TZS 453 bilioni kila mwaka. Katika kipindi hicho hicho, misamaha ya kodi iliyotolewa ilifikia wastani wa TZS 724 bilioni kwa mwaka. Kama misamaha ya kodi ingetolewa katika kiwango kinachofanana na kiwango cha misamaha ya kodi inayotolewa Kenya, TZS bilioni 484 zingeokolewa mwaka 2008/09 na TZS bilioni 302 mwaka 2009/10. Kwa maneno mengine, upungufu katika ukusanyaji wa mapato ungepunguzwa kwa kiasi kikubwa. 3

Kielelezo na.2: Lengo la mapato ambalo halikufikiwa na misamaha iliyotolewa 2008/9-2009/10 Chanzo : Ripoti za mapato ya kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Jambo la tatu: Chini ya Rais Kikwete misamaha ya kodi imeongezeka kwa kasi Ukuaji mkubwa wa misamaha ya kodi umetokea katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Katika kipindi cha miaka mitano (2006-2010) ya Rais Kikwete, misamaha ya kodi ilikuwa asilimia 1 ya pato la taifa (au asilimia 40) zaidi ya misamaha iliyotolewa wakati wa kipindi cha pili cha uongozi wa Rais Mkapa (2001-2005). Kielelezo na 3: Misamaha ya kodi wakati wa awamu ya kwanza ya Rais Kikwete na wakati wa awamu ya pili ya Rais Mkapa 4 Chanzo: Ripoti za mapato ya kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Jambo la nne: Wawekezaji wakubwa wa kimataifa wananufaika zaidi na misamaha ya kodi Ripoti ya mapato ya kodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inaonesha kuwa bidhaa na taasisi mbali mbali zinapata misamaha ya kodi. Makundi matatu yanapata misamaha mingi zaidi. Haya ni makampuni yenye vyeti vya kupatiwa motisha vinavyotolewa chini ya Sheria yauwekezaji Tanzania na Sheria ya Kuendeleza na Kulinda Uwekezaji Zanzibar; walipaji wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) chini ya vifungu na 220, 223 na 224; na makampuni ya madini chini ya Sheria ya Madini. Chini kabisa katika orodha ni walengwa wa manunuzi ya bidhaa katika maduka yasiyotozwa ushuru, pamoja na misamaha itolewayo kwa taasisi za dini. Misamaha mingi itolewayo kwa kupitia vituo vya kukuza uwekezaji pamoja na ile itolewayo kwa makampuni ya uchimbaji madini inanufaisha makampuni makubwa ya kimataifa. Kielelezo na. 4: Misamaha iliyotolewa 2008/09-2009/10, kwa makundi ya wapokeaji Chanzo: Ripoti za mapato ya kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Jambo la tano: Misamaha kwa bidhaa kutoka nje inachukua asilimia 75 ya misamaha yote Misamaha ya kodi inayotolewa kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inaweza kuwekwa katika makundi makuu mawili: Misamaha inayohusiana na uagizaji wa bidhaa nje ya nchi (ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa) na misamaha inayotolewa chini ya vipengele vya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT). Katika miaka miwili iliyopita, sehemu kubwa ya misamaha ya kodi iliyotolewa ilihusisha ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazoagizwa toka nje ya nchi. Kwa upande mwingine misamaha ya Kodi ya Ongezengo la Thamani (VAT) na misamaha ya kodi inayotolewa kwa bidhaa zinazouzwa kwenye maduka yasiyotozwa ushuru kwa pamoja yanachukua asilimia 25 ya misamaha yote iliyotolewa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita. 5

Kielelezo na. 5: Aina ya misamaha ya kodi kwa uwiano wake 2009-10 Chanzo: Ripoti za mapato ya Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Jambo la sita: Zanzibar inatoa mara mbili ya misamaha ukilinganisha na Bara Misamaha ya kodi inatolewa pande zote mbili za Muungano. Kama kielelezo na 6.1 na 6.2 vinavyoonesha, misamaha ya kodi imeongezeka pande zote mbili za Muungano. Hata hivyo, kama sehemu ya mapato, misamaha ya kodi imeongezeka kwa kasi zaidi Zanzibar. Katika kipindi cha 2006-2010, misamaha ya kodi iliyotolewa na Mamlaka ya Mapato (TRA) upande wa Zanzibar ilikuwa karibu asilimia 46 ya mapato yaliyokusanywa ukilinganisha na asilimia 26 katika kipindi cha 2001-2005. Kwa upande mwingine misamaha iliyotolewa na Mamlaka hiyo kwa upande wa Tanzania bara ilikuwa karibu asilimia 23-24 ya mapato yaliyokusanywa katika kipindi hicho chote. Kielelezo na 6.1: Kodi zilizokusanywa na misamaha iliyotolewa: Tanzania Bara 6 Chanzo: Ripoti za mapato ya kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Kielelezo na 6.2: Kodi iliyokusanywa na misamaha iliyotolewa Zanzibar Chanzo: Ripoti za mapato ya kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Jambo la saba: Misamaha ya kodi imeanza kupungua Serikali kupitia Wizara ya Fedha imeonesha kuwa ingependa kupunguza misamaha ya kodi. Kwa hakika misamaha ya kodi imeshuka kutoka kilele cha TZS 840 bilioni (au asilimia 4.3 ya pato la taifa) mwaka 2006/07 hadi TZS 695 bilioni au asilimia 2.3 ya pato la taifa mwaka 2009/10. Japokuwa haya ni maendeleo chanya, ikiwa katika kiwango cha asilimia 2.3 ya pato la taifa misamaha ya kodi inayotolewa na Tanzania imeendelea kubakia kuwa zaidi ya kati ya mara 2 na 6 ya ile ya Kenya na Uganda. Kielelezo na.7: Misamaha ya kodi kama asilimia ya pato la taifa Chanzo: Ripoti za mapato ya kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). 7

Jambo la tisa: Misamaha kwa mashirika yasiyo ya kiserikali na wawekezaji wakubwa imepungua; lakini imeongezeka kwa miradi ya wafadhili na taasisi za Serikali Kati ya mwaka 2008/09 na 2009/10 kiwango cha misamaha iliyotolewa kilipungua kutoka TZS 752 bilioni hadi TZS 695 bilioni. Jedwali namba 1 hapo chini linaonesha badiliko la kiasi cha misamaha iliyotolewa katika miaka miwili iliyopita. Linaonesha kuwa punguzo kubwa lilihusisha ushuru unaotozwa bidhaa kutoka nje na lilihusu zaidi makampuni yenye vyeti vya kupatiwa motisha kutoka TIC and ZIPA. Hii inafuatiwa na punguzo la misamaha kwa mashirika yasiyo ya kiserikali, na makampuni na watu binafsi. Wakati huo huo, misamaha mingi zaidi ilitolewa kwa miradi ya wafadhili na taasisi za serikali. Kwa upande wa mapato ya ndani, misamaha chini ya kipengele cha 3 cha VAT (3rd Schedule) pia imeongezeka kwa kiasi kikubwa. Jedwali na.1: Misamaha ya kodi, kwa makundi yake 2008/09 and 2009/10 2008/09 2009/10 Badiliko 2009-2010 Kitengo cha Ushuru wa Forodha Badiliko halisi (TZS Milioni) % Badiliko TIC & ZIPA 380,090.5 272,971.3 (107,119.2) -28.2 Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) 37,237.8 21,503.0 (15,734.8) -42.3 Makampuni na watu binafsi 51,233.4 35,639.7 (15,593.7) -30.4 Uchimbaji Madini 59,140.7 49,588.7 (9,551.9) -16.2 Taasisi za dini 408.0 260.3 (147.7) -36.2 Mashirika ya Umma 7,125.6 7,046.1 (79.5) -1.1 Jumuiya za Biashara za kikanda 3.0 - n/a n/a Taasisi za Serikali 21,617.3 52,481.6 30,864.3 142.8 Miradi ya wafadhili 21,552.7 72,257.8 50,705.1 235.3 Jumla ndogo 578,408.9 Idara ya Mapato ya Ndani.(3 rd Schedule) 511,748.5 (66,657.4) -11.5 VAT 220 13,249.6 217.0 (13,032.5) -98.4 Misamaha kwenye maduka yasiyotozwa kodi 3,892.4 2,691.6 (1,200.8) -30.8 Misamaha chini ya VAT 223/224 156,847.9 180,192.6 23,344.6 14.9 Jumla Ndogo 173,989.9 183,101.2 9,111.3 5.2 Jumla kuu 752,398.8 694,849.7 (57,546.1) -7.6 Chanzo: Ripoti za mapato ya kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). 8

4. Ikishaidhinishwa, ni vigumu kuondoa misamaha ya kodi Misamaha ya kodi ni upendeleo uliopitishwa kisheria. Hii inamaanisha kuwa kabla misamaha haijaruhusiwa kutolewa, sheria inahitajika kuainisha ni aina gani ya watu, mashirika ama bidhaa zisamehewe kodi. Mara sheria inapopitishwa na kuanza kutekelezwa ni vigumu kuuondoa upendeleo huu kwani wahusika wanaweza kutoa hoja za ushawishi ili ziendelee kuwepo. Jitihada za kuondoa misamaha ya kodi zilizofanywa na Serikali ya Tanzania hivi karibuni zimeonesha ni jinsi gani kuna ugumu katika kuondoa misamaha ya kodi iliyokwisha pitishwa kisheria: Mwaka 2009/10 jaribio la kuondoa msamaha maalum wa Kodi ya Ongezeko la Thamani(VAT) kwa taasisi zinazotoa misaada, mashirika ya dini na mashirika yasiyo ya kiserikali, kwa kigezo kwamba ilikuwa inatumiwa vibaya na baadhi ya walengwa, lilipingwa vikali na viongozi wa dini jambo ambalo lilipelekea kilio kikubwa kupitia vyombo vya habari na hatimaye kukataliwa kupitishwa na Bunge. Mwaka 2009/10 Serikali ilifanya mabadiliko katika sheria ya kodi ili kufuta kipengele kinachoruhusu utaratibu wa kuainisha baadhi ya bidhaa zinazodhamiriwa kutumika katika uwekezaji kama zilizodhaniwa kuwa bidhaa za mtaji (deemed capital goods) kwa lengo la kutaka misamaha ya kodi. Mwaka 2010/11 kipengele hicho kilirejeshwa. Mwaka 2009/10, Serikali ilifanya mabadiliko katika sheria ya kodi ili kurekebisha Tangazo la Serikali (Government Notice) Namba 99 la 2005 lililoidhinisha msamaha wa kodi kwa sehemu ya mafuta yanayoagizwa na makampuni ya uchimbaji madini. Hata hivyo, Serikali bado ilitakiwa kuingia katika mazungumzo na baadhi ya wawekezaji kabla sheria iliyorekebishwa haijaanza kutumika kwao kwani makubaliano waliyoingia na Serikali katika mikataba ya maendeleo ya uchimbaji madini ilikuwa na vipengele maalum vinavyowapa haki ya kupewa misamaha hiyo. Kesi hizi zinaonesha kwamba njia ya busara kwa Tanzania kuzuia kiwango kikubwa cha ukuaji wa misamaha ya kodi ni kuwa makini zaidi katika kuidhinisha misamaha hii. Na pale misamaha inapotolewa, iwe inatolewa kwa vipindi vya muda maalum pasipo nafasi ya nyongeza ya kipindi kingine. 9

5. Hitimisho Sababu mojawapo ya Tanzania kuwa na utegemezi mkubwa wa misaada toka kwa wahisani na kushindwa kuwekeza kwa haraka zaidi katika maendeleo yake ni ukusanyaji mdogo wa mapato yatokanayo na kodi. Taarifa hii imeonesha kuwa misamaha ya kodi Tanzania (Bara na Zanzibar) ni mikubwa ukilinganisha na ile ya jirani zake, Kenya na Uganda na kwa kiasi kikubwa inawafaidisha wawekezaji wakubwa wenye vyeti vya kupatiwa motisha kutoka vituo vya kukuza uwekezaji. Kujenga uwezo wa kujitegemea katika rasilimali ni kipaumbele cha Serikali na kinaweza kufanikishwa kwa kuhakikisha misamaha ya kodi inatolewa kwa uangalifu zaidi. Hili linaweza kufanikishwa kwa: Kupitia upya, sheria mbalimbali zinazotoa misamaha ya kodi; Kuhakikisha misamaha mipya inatolewa kwa umakini mkubwa zaidi, na kuitoa kwa vipindi maalum vilivyofungwa pasipo uwezekano wa nyongeza; na, Kuboresha utekelezaji wake. Zaidi ya hayo ni vigumu kwa wakati huu kusema ni kwa kiasi gani viwango vikubwa vya misamaha inayotolewa vinawafaidisha wananchi. Kwa kuwa na uwazi zaidi, kwa mfano, kwa kuweka bayana taarifa kuhusu makampuni yanayopokea misamaha ya kodi na viwango vya msamaha kwenye mtandao, uchambuzi kama huu unawezekana. Taarifa hizi kwa sasa hazipatikani kwa ukamilifu kwa umma, pamoja na kwamba misamaha ya kodi ni sawa tu na aina nyingine ya matumizi ya serikali. Kama ilivyo kwa matumizi ya afya, maji au elimu, inatakiwa misamaha ya kodi ipitiwe na kuchanganuliwa na Bunge, pamoja na walipa kodi. 10

Rejea Policy Forum (2009), How Much Revenue Are We Losing? Issue brief no. 3.09. Accessed in July 2010 from http://www.policyforum-tz.org/files/howmuchrevenuearewelosing. pdf The Citizen, 4 July 2010. Investor Dispels Fears about Mining Law. Accessed in July 2010 from http://thecitizen.co.tz/sunday-citizen/41-sunday-citizen-business/2797-investordispels-fears-about-mining-law.html AllAfrica.com, 15 June 2009. Tanzania: Country Cuts VAT to 18 Percent. Accessed in July 2010 from http://allafrica.com/stories/200906150870.html Reuters, 24 April 2010. Tanzania increases royalties in new mining law. Accessed July 2010 from http://www.reuters.com/article/iduslde63n04720100424 AllAfrica.com, 25 March 2010. Tanzania: Investors in Dar Transport to Enjoy Tax Exemptions. Accessed July 2010 from http://allafrica.com/stories/201003250228.html AllAfrica.com, 27 November 2009. Tanzania: Tax Waivers Set to Eat Up Sh3 Trillion. Accessed July 2010 from http://allafrica.com/stories/200911270656.html Vidokezo Vielelezo vyote vimetokana na taarifa zilizopatikana kutoka katika ripoti za mapato za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), 1997/98-2009/10. 2 Orodha ya misamaha yote ya kodi inapatikana kwenye tovuti ya Wizara ya Fedha Tanzania (http://www.mof.go.tz/) 3 Data zote zimewasilishwa katika mwaka wa fedha. Kwa mfano, 2005 ina maana ya mwaka wa fedha 2004/05 4 Maliyamkono T, Mason H., Ndunguru, A., Osoro N. E., & Ryder, A., (2009). Why Pay Tax? Dar es Salaam, Tema Publishers and Siyaya Publishing (Pty) Ltd. 11

12