IBADA NA UMOJA WA KANISA Na Mchg. Dkt. Msafiri Mbilu

Similar documents
Information for assessors (do not distribute this page to participants):

"ATATOKEA MARA YA PILI, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu." Waebrania 9:28.

Agano Lililofunikwa Kwa Damu

Ushindi ndani ya Kristo W. W. PRESCOTT

Theolojia Ujumla. Mike Taylor Semester Munguishi Bible College

Mukhtasari Wa Mabishano Kwa Na Dhidi Ya Vikombe Vingi Vya Ushirika

wasiofaa. Naomba sana kila raia afanye bidii awezavyo kumkaribia Mwenyezi Mungu vile anavyoona inafaa, lakini asipitishe hukumu juu ya wengine.

WAFUNAJI WA NAFSI ABC By Vagn Rasmussen Translation by Lydia Madsen

WEWE NI NANI? Toleo X Toleo Ukweli wa Injeli Toleo 23

MUNGU ANADHIHIRISHWA KUPITIA KWA YESU KRISTO.

Ellen White, waasisi wa Kiadventista,na Sabato Lunar

GRACE COMMUNION INTERNATIONAL KANUNI YA IMANI

usudi la Maisha Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na kupishana usiku na mchana, kuna kweli ishara kwa wenye akili, ambaye mkumbuke-

Ufunguo wa Kutaalamika Haraka

KANISA NA UAMSHO Na Mchg. Dkt. Faith Lugazia

MELKISEDECK LEON SHINE. katoliki.ackyshine.com

Ndugu na dada zangu wapendwa,

UTARATIBU WA KANISA. 2 Jambo la kwanza ninalotaka kusema ni kwamba mchungaji. 3 Sisi tunaamini katika Kanisa la kimitume, tukifundisha

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

Inavyodaiwa na wanaochanganya Biblia. Ellis Forsman. Inavyodaiwa na Wanao changanya Biblia (Alleged Bible Contradictions) 1

B. Wanafunzi watapata ufahamu mkubwa wa kitabu hiki, na jinsi kinavyofundisha kuhusu kanisa.

Roho Mtakatifu Ni Nini?

Mafundisho Ya Msingi Wa Kikristo. Na Andrew Connally

RISALA FUPI YA KUMUWEZESHA MTU KUPAMBANUA NI IPI DINI YA HAKI MWANDISHI: SALEH M. KYAMBO

Kiu Cha umtafuta Mungu

Nia Dhidi Ya Kristo Je Unamheshimu?

MUHTASARI WA SEMINA YA TAASISI YA BIBLIA NA UTUMISHI MOROGORO TAREHE 18/11/2014

walozaliwa, si kwa damu, wala mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, mbali kwa Mungu. Sisi sio tena binadamu wa kawaida tu kwa sababu sisi ni w

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees

Oktoba-Desemba

MIAKA 500 YA MATENGENEZO YA KANISA NA USHUHUDA WETU Na Askofu Dr. Abednego Keshomshahara

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Ndugu na dada zangu wapendwa,

Makasisi. Waingia Uislamu

BIBLICAL INSTRUCTION AND ENCOURAGEMENT FOR THE MAFUNDISHO YA BIBLIA NA HIMIZO KWA MISSION FIELD WORLDWIDE. KAZI YA KIMISHENI ULIMWENGUNI KOTE

Mzabibu Na Matawi. (The Vine And The Branches) Ellis P. Forsman. Mzabibu Na Matawi (The Vine And The Branches) 1

Kanuni. Muhimu za Kujifunza Biblia. Mchungaji Drue Freeman. Dan Hawkins & Joseph Brown. General Editors.

Kifo Na Mbingu. (Death And Heaven) Ellis P. Forsman. Kifo Na Mbingu (Death And Heaven) 1

Human Rights Are Universal And Yet...

Maisha Yaliyojaa Maombi

UNABII WA BIBLIA. CBM Publishing 32 Blenheim Road, Far Cotton Northampton, England. NN4 8NW

Adhabu ya jino kwa jino na Musitakabali wa imani zetu

WAKOLOSAI MTAALA. B. Maoni: Tunapendekeza uwe na fafanuzi (commentary) yoyote yenye kushikilia mafundisho ya awali (conservative) katika Wakolosai.

VITAMBULISHO VITA NO DHA HIRI VYA KA NISA LA KWELI LA MUNGU ALIYE HAI

MUNGU ALIUMBA ULIMWENGU 1 WETU NA VYOTE VILIVYO HAI

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

KWA NINI SISI SI MADHEHEBU?

TIST HABARI MOTO MOTO MAANDALIZI YA MWAKA 2000 Y2K PREPARATIONS SASA NI WAKATI WA KUANZA KUPANDA MBEGU ZAKO

KAMA MUNGU YU PAMOJA NASI, BASI YAKO WAPI MATENDO YAKE YA AJABU?

Haja Ya Dini. Author(s): Publisher(s): Translator(s): Category: Topic Tags: Featured Category: Published on Al-Islam.org (

United Pentecostal Church June 2017

Tora UTANGULIZI KWA TORA SOMO LA KWANZA

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

IMANI NA MATENDO ELLEN G. WHITE

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

KITABU CHA KUONGOZA FAMILIA

Watumishi Wa Kristo. Ellis P. Forsman. Watumishi Wa Kristo (Servants Of Christ) 1

MWONGOZO WA NAMNA YA KUHAMASISHA MAOMBI YA MCHANA NA USIKU YA SIKU 10.

MAFUNDISHO YA UMISHENI

Draft 03 MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO MWENGE

Maisha Ya Mkristo Ni Nini?

JE, YAWEZEKANA KUISHI BILA KUTENDA DHAMBI?

Juni 3-9 Pata Manufaa Kamili kwakusomabiblia

MAHUBIRI TUNAYOWEZA KUONA

Mhashamu Askofu Jude Thaddaeus Ruwa ichi, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania; Mwadhama Policarp Kardinali Pengo,

Vol. 113, Namba 1, 2013 ISSN

NGUVU. Utangulizi. Yesu alisema,

maombi, kabla tu hatujalifungua Neno hili la Kiungu.

Mwongozo wa Kanisa la Waadventista wa Sabato

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

Kwa Kongamano Kuu 2016

MSAMAHA NA UPATANISHO

Sura ya 7 Kielelezo: Tumepatanishwa na Mungu na Wanadamu

YEHOVA-YIRE 1. 2 Baba yetu wa Mbinguni, tunakikaribia Kiti Chako cha. 3 Tunakushukuru kwa kutuzuru jana jioni. Tunaomba

UKUFUNZI WENYE NGUVU MMOJA-KWA-MMOJA

Aina Tatu Za Ibada. Ellis Forsman. Aina Tatu Za Ibada (Three Kinds Of worship) 1

ONYO LA MWISHO KWA DUNIA

Tumaini Kwa Afrika. Thomas Schirrmacher. Hoja 66. Dibaji na Prof. Mchungaji Dk. Thomas K. Johnson. Thomas Schirrmacher Tumaini Kwa Afrika TASCM RVB

FORWARD BY DANIEL SZMIOT

Kocha Mkuu. mabingwa. itakuwa INASTAHILI. Ili Kutoa mafunzo kwa wanafunzi wako kuwa. itakuwa ya kuumiza. Itachukua muda. Itahitaji moyo wa kujitoa.

Mipango ya miradi katika udugu

PDF created with pdffactory trial version

Tazama Yuaja. Kuhusu Toleo Hili. Umuhimu wa Mafundisho ya Biblia. Nguvu katika neno la Mungu.

Silaha Za Shetani. Ellis Forsman. Silaha Za Shetani (The Devices of Satan) 1

Hakimiliki na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa TAFSIRI YA BIBLIA. Mwandishi. Jonathan M. Menn

Kufunga Milango - Uponyaji Kutokana na Athari za Giza

Kuiponya Picha Tuliyonayo Kuhusu Mungu

JE! MUNGU ANAMPA MWANAMKE HAKI YA KUTOA MIMBA IWAPO NI MHANGA WA UBAKAJI?

KUTAMBUA SIKU YA KO NA UJUMBE WAKE

MASWALI NA MAJIBU JUU YA KITABU CHA MWANZO

IM ETUPASA KUTIMIZA HA KI YOTE

United Pentecostal Church April Kushangilia Kwa Sala

Uongozi Siri Na Larry Chkoreff. Version 1.2 Desemba 2010

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO

Kiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika

UZAO WA NYOKA. 2 Basi, usiku huu, tuna malimbuko tu ya utukufu huo mkuu. 3 Kwa uchaji tunasimama kwa imani yetu katika Uwepo

MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA. Kwa Wanaoanza

TIST HABARI MOTO MOTO. Benefits of Loan Repayment. Faida za ulipaji wa mikopo U OTESHAJI W A M ITI Y A M ATUNDA

Ndugu na dada zangu wapendwa,

Kifo Na Mbingu (Death And Heaven)

Transcription:

1 IBADA NA UMOJA WA KANISA Na Mchg. Dkt. Msafiri Mbilu SOMO LA I Kama kuna nyakati katika Historia ya Kanisa ambazo tunapaswa kuangalia kwa undani juu ya IBADA NA UMOJA WA KANISA, ni sasa. Sababu kubwa ni kwamba nyakati hizi kumekuwa na mafundisho mengi sana ambayo yanawachanganya Washarika wetu. Vikundi vingi vimeibuka vyenye mikazo ya washerehesha watu na wala siyo ibada mkazo uwe ni mafundisho ya Neno la Mungu. Ni lazima sisi tuwe na utaratibu wa kiibada unaofanana ili watu waweze kututambua kuwa sisi ni Walutheri wenye Umoja na tuliobobea katika mafundisho sahihi ya neno la Mungu. Kanisa letu lina mfumo ulio wazi na hivyo mfumo huu utumike kuweka UMOJA katika mambo ya Ibada. Kwa msingi wa Katiba yetu ya KKKT tunapaswa kuuenzi, kuulinda na kuuimarisha Umoja wetu. Waasisi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, ambao ni viongozi waliotutangulia walikuwa na maono makubwa juu ya Umoja wa Kanisa. Katika Kanuni ya IV ya Katiba yetu ya KKKT Kifungu F, juu ya Wajibu wa Kanisa Katiba inasema kuwa: Kanisa lina wajibu wa Kutengeneza na kusimamia taratibu za Ibada zitakazotumiwa katika Kanisa. Yapo mambo mengi sana yanayotuunganisha katika Umoja wetu mfano Mashule, Hospitali, Hotel, Chuo Kikuu na miradi mbalimbali, nk. Lakini sisi kama Kanisa na jamii ya Waaminio, kinacho tuunganisha zaidi na kuonyesha Umoja wetu ni Ibada. Ni katika Ibada ndipo utagundua kuwa hapa uko kwenye Kanisa la Kilutheri au Kanisa jingine. Mfano ukiingia kwenye Kanisa la RC pale mlangoni utakutana na chombo chenye maji ya Baraka. Huo ni utambulisho mkubwa kwamba sasa nimeingia kwenye Kanisa la RC. Ukiingia Makanisa mengine wanayojitambulisha kama Makanisa ya Uamsho utapiga makofi kwa kuimba mapambio hadi kiganja kipate moto. Ndiyo utambulisho wao. Sisi Walutheri nasi tunayo aina yetu ya kuabudu na hapo ndipo penye utambulisho wetu. Ibada ni njia moja inayoweza kuweka utambulisho wetu kwa wazi sana. Wataalamu wa mambo ya dini wanasema Kwa ujumla dini zote zinafanana kwa kuwa kila dini ina kusudi la kumwabudu Mungu wake, tofauti kubwa inayozifanya dini ziwe tofauti ni mtindo wa Ibada. Kwa maneno mengine hapa ni kwamba ni katika Ibada ndimo watu walimokubaliana namna ya kumwabudu Mungu wao. Sisi Wakristo tuko kwenye madhehebu mbalimbali. Kinachoweza kututambulisha au kutofautisha kati ya dhehebu moja na jingine ni ile namna ya kumwabudu Mungu. Tunashukuru katika KKKT tuna kitabu kimoja cha ibada tena chenye rangi moja. Kila unapopita utaweza kuwatambua Wakristo wa Kiliutheri. Ukipita mtaani popote ni rahisi kuwatambua Walutheri kwa kuwa Kitabu chao cha ibada kinafahamika. (Our Identity). Mbinu kubwa wakoloni waliyotumia ili kuweza kuwatawala Waafrika kwa urahisi, ni kuwajengea wazo la kudharau kile kilicho chao na kupenda cha kigeni. Wapo Wachungaji wa Kilutheri ambao katika nyakati hizi wameanza kudharau utambulisho wao katika ibada. Wamechotwa na vikundi vilivyoko huko mtaani na kuona kuwa labda ibada zao zinafaa zaidi. (Kanisa liweke utaratibu wa kuhakikisha kuwa Ibada yetu zinafanana na kufuatwa).

2 Siku hizi kutokana na shida kubwa ya ajira kazi ya Uchungaji imeingiliwa sana. Kila mtu anao uwezo wa kujiita Mchungaji bila mafundisho yoyote. Mfano Mchungaji Kweka wa Unga Ltd aliyekuwa mlinzi amekuwa mchungaji. Inasikitisha kuwa Wachungaji wetu wanaacha mapokeo yao wanawaiga watu hawa. Ibada zao hazina mfumo maalumu. Mfano Ndugu yangu mmoja alipata ajali akalazwa miezi 4 Bombo Hospital ametoka ananiambia nimeugua kwa muda mrefu sana sasa nimeamua kuwa Mchungaji. Mfano Gazeti moja limeandika MCHUNGAJI ABAKA kumbe ni Mchungaji wa Mbuzi. Siku hizi hata Waganga wa Kienyeji wameamua kuwa Wahubiri wa Injili huku wakiweka mikazo ile ile ya Waganga juu ya kupiga ramli, kuagua, kutafsiri matukio kadha wa kadha. Mfano Mhubiri kwenye Channel 10 alikuwa akihubiria watu na kuwaambia: Kama unayo majina ya wachawi unaofikiri wanakutesa, andika majina yao kisha yaweke kwenye bahasha pamoja na sadaka yako ya 20,000 ili usiku huu nikayashughulikie. Kama huna hela sasa tuma kwa M-Pesa namba 0769 000034. Huyu ni mganga wa kienyeji kaamua kuwa Mchungaji. Tena wanajiita watumishi ili kuweka tofauti kidogo ili tufanane wote. (Mf. Siku hizi sikubali kirahisi kuitwa Mtumishi). Siku hizi vikundi ni vingi sana, tena vingine vya kibiashara vyenye majina ya ajabu ajabu kama ifuatavyo: - Helicopter of Christ Church - The Devil s Hunter Ministry - Laboratory Church of God - The New Manchester United Church IBADA ZETU KKKT Liturgia ya KKKT Liturgia yetu ya KKKT iko kwenye Kitabu chetu cha nyimbo kiitwacho TUMWABUDU MUNGU WETU (TMW). Tunawashukuru wenzetu walioandaa kitabu hiki na sasa kinatumika katika Kanisa zima. Kitabu hiki ni kizuri na kinapaswa kufuatwa na wote ili kuimarisha na kudumisha umoja wetu. Kitabu hiki kina nyimbo 440. Mfano wa Nyimbo za Kuabudu - TMW 424 Nionapo amani kama shwari. TUANGALIE MATUMIZI HALISI YA KITABU HIKI Uk. 329 - Sala ya matayarisho: Bwana Yesu uishie mahali pa juu Uk. 330 - Sala ya kimya washarika wakisubiri ibada kuanza: Ee Mungu, Baba wa mbinguni, KUANZA IBADA Kuingia ibadani: - Mavazi ikiwemo kanzu yawe safi na kupigwa pasi - Mwendo wa kuingia Usikimbie - Tuingie kwa unyenyekevu - Tusiwe na haraka sana - Kuinama madhabahuni - Tusilipue mambo bora yaishe - Nyimbo ziandaliwe Mfano Usharika mmoja Mchungaji mvivu aliomba mtu achague wimbo Mama mmoja akachagua Nimechoka kabisa...

3 UANZISHWAJI WA IBADA Upigaji wa msalaba - Wapendwa katika Bwana: Tuanze ibada ya siku hii katika jina la Baba, na la +Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amen. - Msalaba ni katika Mwana - Baada ya kufungua ibada, kabla Washarika hawajakaa ifuate Zaburi ya siku. - Hapa tunatofautiana sana. Nikiwa kwenye usharika wenye kwaya nyingi nawapa nafasi hapa ya kuimba - Baada ya wimbo wa Kwaya tunaimba wimbo wa Kitabu. - Usianze Liturgia na wimbo wa Kwaya. UCHAGUZI WA NYIMBO Aanza ibada na wimbo unaolenga Majira ya mwaka wa Kanisa au tukio lililopo Wachungaji tumekuwa wavivu wa kuandaa nyimbo: Mchungaji ana wimbo wake mmoja tu haukosekani ibada zote: Bwana U sehemu yangu. Krismasi asubuhi watu wanatazamia waimbe tofauti yeye anaanzisha Bwana U sehemu yangu. Pasaka watu wanaguswa kuimba Yesu Amefufuka lakini wanaambiwa waimbe Bwana U sehemu yangu. Kwenye Mazishi kuna nyimbo zake kwa mfano TMW 154 Ninataka kuingia lakini wanaongozwa waimbe Bwana U sehemu yangu. Baada ya wimbo wa Kitabu inafuata Liturgia Uk. 331 Sala: Mungu wa Neema, umetupa akili ili tukujue wewe... Usharika usimame Liturjia Uk. 332 Bwana Mungu wetu yupo hapa... UNGAMO LA DHAMBI Lisemwe kwa usahihi: Tuseme Mungu Mwenyezi tusiseme Mungu mwenye enzi yote. Wenye enzi yote ni watawala wa dunia hii Obama, Museveni, Magufuli, nk. Ondoleo la dhambi MASOMO: Wale wanaosoma wafundishwe: - Nasoma somo la Waraka toka...waraka ni Paulo tu. - Injili ya Mathayo... - Kitabu cha Yeremia, nk. Anayesoma asikosee. Neno la Mungu lisomwe kwa usahihi. - (Mwanafunzi wangu akikosea namkata maksi kwenye continuous assessment). - Anayesoma aandaliwe mapema - Mfano pale Bukoba msomaji hutangazwa wiki moja kabla ili msomaji ajiandae. UKIRI WA IMANI Ndugu zangu siku zote tunasema tuungane na wakristo wenzetu ulimwengu mzima tukikiri imani ya Mitume. Lakini tunayokiri sisi siyo. Nimegundua kosa linaanzia kwenye mafundisho ya Kipa Imara. KKKT tuwe na utaratibu mmoja wa kukiri Imani ya Kikristo. Yapo makosa makuu mawili: Namwamini Mungu, Baba Mwenyezi. Siyo Mungu mwenye Enzi yote. Wenye enzi yote ni viongozi wa dunia hii. Lakini Mungu wetu ni MUNGU MWENYEZI.

4 - I BELIEVE IN GOD, FATHER ALMIGHTY, - Ich glaube an Gott, den Vater, den Allmächtigen, den Schöpfer des Himmels und der Erde. - Credo in Deum Patrem omnipotentem, Creatorem caeli et terrae. - Almighty: the one who has power to do everything. Even beyond death. Ushirika wa watakatifu. Siyo usharika wa watakatifu. Tunaongeza vitu vidogo vidogo kwenye Ibada zetu na hivyo tunapobadili hata mambo makubwa ya Imani hatujui. Mfano: Ubarikiwe na Bwana wetu Yesu Kristo wa Nazareti aliye hai. Mfano: Salamu ya Kristmas: - Wengine wanasema Yesu amezaliwaaa. - Yesu Amefufuka Amefufuka kweli Haleluya apologetic. Kuwahakikishia watu kuwa kweli Amefufuka. MATANGAZO Baada ya ukiri ni wimbo na Matangazo. Wachungaji wa KKKT matangazo yamekuwa mengi mno. Nilialikwa usharika mmoja ibada ni tatu na matangazo yalikuwa 20. SALA YA BWANA...bali utuokoe kutoka uovu. Liturjia Uk. 355 Mt. 6:13 - Alla rusai hemas apo tou Ponerou. Amen. - But rescue us from evil. - Bali utuokoe kutoka uovu. SOMO LA II MAHUBIRI Baada ya Matangazo yanafuata mahubiri ya NENO LA MUNGU. Kilele cha ibada ya Kilutheri Mimbarani ambapo neno la Mungu linahubiriwa kwa usahihi wake. Martin Luther alijitahidi kusimama katika NENO akikaza kuwa ni katika Neno lililohubiriwa kwa usahihi wake ndipo watu watatambua wokovu wao unaopatikana kwa imani. Ili neno liweze kuwafikia watu sawasawa tunapaswa kuzingatia mambo muhimu katika ibada zetu. a) Kipindi cha Mahubiri kipewe muda wa kutosha katika ibada zetu. Katika ibada nyingi siku hizi Matangazo yamepewa muda mrefu zaidi kuliko mahubiri. Mfano nilialikwa usharika mmoja kuna ibada tatu lakini matangazo yalikuwa 28. Pendekezo: Tuwe na Newsletter ya Usharika (Gemeinde Brief) hata ikitoka mara moja kwa mwezi ili kuweka yale matangazo muhimu. Washarika wakishazoea kusoma matangazo kwenye notice board watajijengea utamaduni mzuri kuliko kuweka matangazo mengi. Uwepo wimbo wa Mahubiri. Tusianze mahubiri kwa pambio. Kulinda umoja na mapokeo yetu. Mahubiri yaandaliwe vizuri. Tena yaandikwe kwa ufasaha. Mhubiri mzuri ni yule anayeandika mahubiri yake. Usiandike outline tu andika hubiri zima neno kwa neno. Kisha soma ulichoandika. Mfano Mhubiri ambaye hajaandaa mahubiri yake utamgundua tu. - Bwana asifiwe ni nyingi hata mahali pasipo stahili.

5 - Mpe jirani yako mkono mwambie Mungu anakupenda. Kupeana mikono mara 25 katika ibada ni kuonyesha kuwa huna cha kuwaambia watu. Tuwe na muda mzuri wa kujiandaa kabla ya mahubiri. - Usiandalie mimbarani. - Tuwe na muda wa kusoma vitabu mbalimbali vya mafafanuzi ya Neno la Mungu. - Ni muhimu kutoa kidogo mafafanuzi ya somo ili washarika waelewe. Eleza kidogo mazingira ya somo kwa wakati ule (e.g. Mwana mpotevu alilisha nguruwe Wayahudi walimtazamaje mtu aliyelisha nguruwe wakati ule). - Exegesis (mafafanuzi) ya somo ni muhimu sana. Usilichukue somo na kuliingiza moja kwa moja katika maisha ya kawaida. Lijengee misingi. - Wahubiri wengi wanakuwa na mahubiri yao tayari kabla hata ya kusoma Neno la Mungu. Hivyo wamebaki kuhubiri ndoto zao badala ya Neno la Mungu. Mfano mhubiri mmoja alisoma Isaya 6:1 Katika mwaka ule aliokufa mfalme Uzia nalimwona Bwana. Kwa kuwa hajui mazingira ya somo akaanza kuhubiri: Isaya alimwona Bwana kwa kuwa Uzia alikufa. Ukitaka kumuona Bwana sharti uruhusu uzia uliye naye afe. b) Kama hujajiandaa sawasawa usiongoze ibada. Waachie wengine waongoze kuliko kuleta vituko kwenye ibada. Mfano Bwana harusi kwenye ibada ya mazishi alisema pokea pete hii... c) Tuwe makini kukaribisha wahubiri kwenye sharika zetu. Kama nilivyotangulia kusema, siku hizi kutokana na tatizo la ajira, watu wengi wamejifanya kuwa na kipawa cha kuhubiri wakijiita watumishi. Wanafanya mawasiliano na wazee wa Kanisa au washarika ili waweze kuja kuongoza semina kwenye sharika zetu. Na kuleta mafundisho yanayowachanganya watu. Askofu/ Mchungaji ndiye mwenye Dayosisi/ usharika wake/ mimbara /madhabahu. Awe makini katika kualika wahubiri. Ushauri kwa KKKT. Wahubiri waonyeshe vyeti kutoka vyuo vinavyotambulika. Rwanda wamefaulu. Mchungaji azungukie sharika kujua mambo yanayofanyika na tuwe waangalifu kufahamu yanayofanywa na Wainjilisti. Zifanyike semina za mara kwa mara katika Sharika na Jimbo Kanisa letu lina mfumo, hivyo ni vizuri kuona jinsi gani ya kudhibiti mafundisho kuanzia kwenye Dayosisi, Majimbo, Sharika na Mitaa. Wapo Wainjilisti wanafanya yao huko bila Mchungaji wa Usharika kujua. Wachungaji tuwe na ziara za kushtukiza mitaani. Maaskofu tuwe na ziara za kushtukiza kwenye sharika na mitaa. Tutajionea mambo. MWISHO Tuwe makini na mambo mapya yanayojitokeza. Tusiige kila kitu: - Wengine akibatiza mtoto anampakata ndipo ambatize. Hili siyo sahihi, mtoto analetwa na mdhamini. Hivyo mdhamini amshike mtoto Mchungaji ambatize. - Wengine wakifunga ndoa wanawafunga maarusi stola. Lengo ni ili kuimarisha ndoa na kuweka alama kuwa alichokiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe. It sounds good lakini siamini kuwa stola ndiyo inayofunga ndoa hasa. - Wengine wanaambiwa wakitoa sadaka waguse madhabahu maana ndiyo kuugusa moyo wa Mungu. Imeongeza mapato. Meza ya Bwana iandaliwe vizuri. Siyo kukunjakunja vitambaa.

6 Wachungaji ndio wanaotoa sakramenti USHAURI Tuwe waangalifu kufuatilia kazi zinazofanywa na Wainjilisti na Walimu wa Mitaa huko sharikani. Sharika nyingine ni kubwa sana lakini tujenge mfumo wa kudhibiti. Wainjilisti wapewe semina za mara kwa mara. Wachungaji wapewe semina mara kwa mara. Baada ya Mkutano huu. Kwenye Dayosisi zetu. Katika mpango Mkakati wa Kanisa (strategic plan) jambo la semina lipewe kipau mbele. Ili Liturgia na nyimbo ziimbwe vizuri tuwe na utaratibu wa kuajiri wana muziki katika sharika zetu. Baadhi ya Dayosisi zimeanza, Dodoma na Mashariki na Pwani baadhi ya wana Muziki wamepata ajira. Hii itasaidia ibada zetu ziwe na vinanda vya kuongoza nyimbo. Dayosisi zitume walimu kusoma Muziki kwenye chuo chetu Kikuu cha Makumira. Kozi ni nzuri sana. Tuone jinsi ya kufanya Ibada zinazogusa watu wa makundi yote mfano Walemavu mbalimbali wenye ulemavu wa kusikia, kuona, kutembea na ulemavu mwingine. SOMO LA III UTUNZAJI WA KAZI ZA UMOJA ITIKIO LA IBADA ZETU Katika kipindi kilichopita tumezungumza kuwa kilele cha Ibada zetu za Kilutheri ni mimbarani ambapo Neno la Mungu linahubiriwa kwa usahihi wake. Baada ya NENO Wakristo wanapewa nafasi ya kumshukuru Mungu wao kwa matoleo yao kama itikio lao kwa Mungu. Wakristo wafundishwe kwa kina jinsi ya kumtolea Mungu sadaka zao maana Kanisa linahitaji fedha ili kuweza kujiendesha na kutimiza malengo yake. Mtume Paulo anafundisha akisema katika 2Kor. 9:6-7 Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu. Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu. Nawapongeza Wachungaji wote wa KKKT jinsi walivyofaulu kufundisha Wakristo jinsi ya kumtolea Mungu. UKUBWA WA KKKT Kanisa lilipoanza mwaka 1963 likiwa na jumla ya washarika 500,000. Leo hii KKKT ina Washarika Milioni 6.5. Hii ni idadi kubwa sana. Fungamano la Makanisa ya Kilutheri Duniani ina jumla ya Makanisa ya Kilutheri wanachama 145 katika nchi 78 Duniani. Jumla ya Walutheri wote duniani ni Milioni 70/ 74. Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania ni kanisa la pili kwa ukubwa Duniani kwa kuwa na Wakristo Milioni 6.5. Ni Kanisa la pili Afrika pia. Kanisa la kwanza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu ni Kanisa la Mekane Yesus, Ethiopia lina Washarika 7.9. Kanisa la tatu kwa ukubwa ni Kanisa la Sweden lina Washarika 6.3. Picha hii inaonyesha wazi kuwa KKKT ni Kanisa lenye nguvu kubwa sana duniani. Nina hakika Mkuu wetu wa Kanisa au Katibu Mkuu akisimama mahali anaonekana kama mwakilishi wa Kanisa kubwa sana Duniani. Mfano Wakati wa Tamko la Maskofu juu ya Ushoga tuliitwa maeneo mbalimbali kuhojiwa tuseme neno kule Ujerumani.

7 KAZI YA SADAKA Kazi kubwa ya sadaka ni kutunza kazi zote za Kanisa kama vile ujenzi wa makanisa, mishahara ya watumishi, kusaidia wanyonge (kazi za Diakonia) na kazi nyinginezo. Kazi kubwa ya sadaka ndugu zangu Wachungaji ni kutunza kazi za UMOJA wetu wa KKKT. Haitoshi kama tunatoa sadaka zetu huko sharikani lakini hatutunzi kazi za UMOJA. KAZI ZA UMOJA Kazi za UMOJA siyo za kubuni bali zinaonekana wazi katika Dhamira na Taswira ya Kanisa letu. Angaliz Katiba yetu ya KKKT uk. v. TASWIRA (VISION) Ushirika wa watu wenye upendo, amani na furaha waliobarikiwa kiroho na kimwili, wenye matumaini ya kuurithi uzima wa milele kwa njia ya Yesu Kristo DHAMIRA Kuwafanya watu wote wamjue Yesu Kristo ili wawe na uzima tele, kwa kuwahubiria Habari Njema kwa maneno na matendo, kwa kuzingatia Neno la Mungu kama lilivyo katika Biblia na misingi ya mafundisho ya Kilutheri kwa kuongozwa na Katiba ya KKKT. Hizo baraka za kiroho na kimwili ndizo zinazotusukuma kutimiza malengo tuliyojiwekea katika dhamira yetu, kuwafanya watu wote wamjue Yesu Kristo ili wawe na uzima tele, kwa kuwahubiria Habari Njema kwa maneno na matendo. Ni kwa msingi huu ndiyo maana kanisa limejikita sana katika kazi mbalimbali: Kazi za Misioni na Uinjilisti zipo misioni za ndani na nje. Radio Sauti ya Injili Moshi Shule ya Viziwi Mwanga Shule ya Viziwi Njombe Lutheran Junior Seminari Morogoro Kutunza Kazi za Ofisi Kuu Kazi hizi zote zinatunzwa na sadaka zetu. Tunazo sadaka za aina 3 ambazo hizo ndizo zinazotunza KAZI ZA UMOJA: ambazo ni 2%, Sadaka ya Siku ya KKKT na Sadaka ya Misioni na Uinjilisti. Swali la msingi: Je Wachungaji tunahamasisha washarika wetu kutoa kwa moyo kwa ajili ya kazi za Umoja? Naomba tuangalie siku ya KKKT. Kama kila msharika angehamasishwa kutoa kwa moyo tungekusanya fedha nyingi sana ambazo zingetosha sana katika utendaji wa kazi zetu. Tuko Waluthreri Milioni 6.5. Kama nusu ya washarika hawa kila mmoja angetoa Tsh. 1,000 tu, tungekusanya Sh. Bilioni 3.2. Badala yake kwa miaka minne (2012-2015) sadaka ya KKKT tumekusanya kwa jumla watu wote milioni 6.5 tumekusanya milioni 170. Maana yake kila mwaka tumetoa milioni 42,500,000. Maana yake kila msharika kwenye ile siku ya KKKT ametoa Sh. 6.50. kwa miaka minne hakuna msharika aliyefikisha Sh. 50. Hivi tuko serious na kazi za umoja? Mahali pengine hata sikukuu ya KKKT haiadhimishwi japo iko kwenye Kalenda. Mahali pengine hata ile barua ya salamu za Mkuu wa Kanisa haisomwi. Patano la KKKT ni kwamba siku hii kusiwe na sadaka nyingine yoyote. Lakini mahali pengine sadaka hii imewekwa kuwa ya tatu au ya nne.

8 Tungejitoa kwa moyo na kukusanya Bilioni tatu tungetekeleza majukumu yetu kwa wepesi sana. ASILIMIA 2% Makusanyo ya 2% yanatisha. Zipo Dayosisi hazipeleki kwa wakati. Haipelekwi kwa ukamilifu wake. Ukiangalia kwa ujumla wake mapato yamepanda sana katika sharika zetu. Asilimia 2 nayo inapaswa kupanda. SADAKA YA MISIONI NA UINJILISTI Kwa miaka minne hata milioni 40 hazijafika. Tumekusanya milioni 37 ni sawa na Sh. 9,250,000 kwa mwaka kwa Wakristo milioni 6.5. Lazima tuseme kitu kwenye Mkutano huu. Kutoa ni sehemu ya kutimiza UWAKILI wetu. Tumekabidhiwa vitu tutoe. Hata kama ni kidogo. Mfano Wachungaji tuwe waaminifu. Uaminifu uwepo hata katika kusimamia vifaa vya mashule kama sahani kwenye vituo, nk. Nilishuhudia Mwnj. Lutindi Mental Hospital amechukua shuka na kuliweka nyumbani kwake. Kazi zinazotuhitaji ni nyingi katika UMOJA wetu. Kazi ya Misioni na Uinjilisti itakwendaje? Tunatakiwa kuimarisha mawasiliano. Tena ni agizo la Mkutano Mkuu wa KKKT mwaka jana pale Makumira kuwa: Halmashauri Kuu ya Kanisa iliagizwa kuboresha, kuimarisha na kupanua mawasiliano machapisho, magazeti, radio, televisheni. Vyombo hivi vitumike kueneza ufalme wa Mungu. Je tutawezaje kuimarisha mawasiliano bila fedha? Wakati wa kuimarisha umoja wa Kanisa ni sasa. Dayosisi zote za KKKT wahakikishe wanatekeleza maazimio yanayotolewa na kushiriki kikamilifu katika Kazi za Umoja ikiwemo michango na sadaka zote. Halmashauri Kuu iliagizwa kuhakikisha mambo yanayohusu Kazi za Umoja yanaheshimiwe na Dayosisi zote. Asilimia mbili (2%) kwa KKKT ziwe zinawasilishwa kama inavyotakiwa na bila kukosa. Ukipita kwenye vituo vyetu vya kazi za UMOJA utaona hitaji kubwa la mshikamano wetu. Mfano Lutheran Junior Seminary Morogoro inahitaji kufanyiwa ukarabati wa kina. Tutaweza endapo tutajitoa kwa moyo katika sadaka zetu. Ofisi Kuu inafanya kazi zake kwa kuwa na nakisi kila mwaka kwa kuwa mapato hayatoshi. Tujitoe kwa moyo katika kuupenda UMOJA wetu huu. Yesu alituagiza tuwe na UMOJA. Kila Mchungaji akakumbukewajibu wake wa kulitunza Kanisa. Tuondoke na hamasa mpya ya kutekeleza majukumu yetu na kuweka kwenye Kalenda zetu kuingia kwa upya katika mwaka unaokuja. MUNGU ATUBARIKI KATIKA KUIPENDA, KUITUNZA NA KUIKUZA KKKT. Mada imetolewa na: Na Mchg. Dkt. Msafiri Mbilu, Mkurugenzi Tawi la Tanga Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU). Andiko kwa ajili ya Mkutano wa Wachungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), 24-29 Septemba, 2016.