Yaliyomo. Kuhusu kitabu hiki. Hautakuwa peke yako. Mfumo wa msaada ni wa manufaa sana wazazi wote wanahitaji!

Similar documents
Information for assessors (do not distribute this page to participants):

Mwongozo wa Familia wa Kujifunza

MACHAGUO YA UZAZI KUFIKIRIA KUWA MZAZI

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees

Kijitabu cha Maelezo cha Programu ya Famasia

Siku ya kwanza. Mguso wa ngozi-kwa-ngozi (Ulezi wa kangaruu) Mtoto wako anaweza kuhisi mdundo wa moyo wako

Utangulizi wa ugonjwa wa shinikizo la damu

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

Kuwawezesha wasichana kwa kuboresha kujikubali na kujithamini Hivi Ndivyo Nilivyo

Ufundishaji wa lugha nyingine

Vijana wanazungumza kuhusu ujinsia, maisha na uhusiano VIJANA WANAZUNGUMZA KUHUSU NGONO, MAISHA NA UHUSIANO. Training and Research Support Centre

Human Rights Are Universal And Yet...

JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI

Wewe Maisha Yako Ndoto Zako. Kitabu cha Vijana Balehe

MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA. Kwa Wanaoanza

KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA

Mwongozo wa Utamaduni Toleo la Kwanza

Mazoezi yaliyofanyika wakati wa warsha kuhusu Elimu-Jumuishi kwa Vitendo. Zanzibar, 7-10 Februari 2006

Kocha Mkuu. mabingwa. itakuwa INASTAHILI. Ili Kutoa mafunzo kwa wanafunzi wako kuwa. itakuwa ya kuumiza. Itachukua muda. Itahitaji moyo wa kujitoa.

Deutsche Welle, Learning by Ear 2009 Seite 1 People Who Make A Difference Liberia: Anita Varney Health Facilitator, Fishtown/Liberia

usudi la Maisha Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na kupishana usiku na mchana, kuna kweli ishara kwa wenye akili, ambaye mkumbuke-

Kufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig

Palliative Care Toolkit

UMRI WA MAKAMO NA KUKOMA KWA HEDHI

Hatari, Haki za Usalama katika Bahari 03

Elimukombozi, Lugha na Upashanaji Habari nchini Tanzania, katika Muktadha wa Utandawazi

Kiu Cha umtafuta Mungu

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

Ufunguo wa Kutaalamika Haraka

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO

Early Grade Reading Assessment for Kenya

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

Mwongozo kwa familia zinazofanya kazi pamoja kwa maisha endelevu. Nyenzo ya Mafunzo

Namba ya moduli 3 Kuangalia sanaa

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

Usimulizi wa Riwaya ya Nyongo Mkalia Ini E. S. MOHOCHI University of Egerton, Kenya

KUWEZESHA MBINU ZA UZUIAJI MIMBA KATIKA SUHULA ZA AFYA: MASWALI 10 KWA VIKUNDI VYA JAMII KUZINGATIA

Mwongozo wa Mwezeshaji

Mwongozo wa Mafunzo Yaliyochanganywaya K4Health

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

International Labour Office. Kazi za Ndani Zenye Madhara kwa Watoto: Kijitabu cha Maelezo Mafupi

Elimu Bora, lakini... C HakiElimu Elimu bora, lakini...

Elimu Ina Umuhimu gani katika Jamii? Kuelekea Elimu Sahihi

Upande 1.0 Bajeti yako

Makala ya Mshiriki wa Mafunzo

SautiElimu. Sauti Yako Isikike

JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II

Ellen White, waasisi wa Kiadventista,na Sabato Lunar

Sera ya Faragha. Upeo. Aina za Data na Mbinu za Ukusanyaji

Shabaha ya Mazungumzo haya

TAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF) KUHUSU HAKI ZA WATOTO KATIKA KATIBA MPYA

Juni 3-9 Pata Manufaa Kamili kwakusomabiblia

Miradi na jamii. 3.1 Utangulizi

KISWAHILI KARATASI YA 2 LUGHA

Adhabu ya jino kwa jino na Musitakabali wa imani zetu

Tufundishane! Mwalimu Bora In this issue: Issue 6, December Do you want to be in our next issue?

Kuwa na Ukimwi ni kama vile kutakiwa kuendelea kuuzima moto unaoniunguza bila kukoma.

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Pronunciation: Mä-hret Zäläke Ndal-ka-tscho Molla Mare Gebre-gzabiär 1/12

Elimu-Jumuishi Kwa Vitendo

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level

Kifaa Maalum cha Kutazamia Jua: Maelekezo ya kutumia

Theolojia Ujumla. Mike Taylor Semester Munguishi Bible College

Hakimiliki na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa TAFSIRI YA BIBLIA. Mwandishi. Jonathan M. Menn

Roho Mtakatifu Ni Nini?

Ndugu na dada zangu wapendwa,

Mipango ya miradi katika udugu

Kufunga Milango - Uponyaji Kutokana na Athari za Giza

Ushindi ndani ya Kristo W. W. PRESCOTT

United Pentecostal Church June 2017

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

MAFUNZO YA AFYA YA UZAZI: Nyongeza ya Mtalaa Kwa vijana

# 18 Uponyaji Kutokana na Kukataliwa

Kitabu Cha Mafunzo Ya Uongozi Kwa Wanawake

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara

Unyanyasaji wa Watoto & Kutelekezwa

Haja Ya Dini. Author(s): Publisher(s): Translator(s): Category: Topic Tags: Featured Category: Published on Al-Islam.org (

TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM)

Mwongozo wa Jamii juu ya Afya ya Mazingira

KITEGO CHA MAREKEBISHO NA HAKI ZA MTOTO

MSAMAHA NA UPATANISHO

Picha ni hati miliki ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Watoto(PCD), Imperial College London. Maelezo

Tora UTANGULIZI KWA TORA SOMO LA KWANZA

Jamii. ,,,^mm^mmm-<^^^^ illli MA RH-EREN.CE CENTRE

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2012

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

CGAP Smallholder Household Survey in Tanzania / Utafiti wa kaya ndogondogo Tanzania

TIST HABARI MOTO MOTO

Shamba Darasa na Stadi za Maisha kwa Vijana (SDSMV) Tanzania. Kiongozi Cha Mwezeshaji. Jaap Van Pol na Francesca Dalla Valle

Mukhtasari Wa Mabishano Kwa Na Dhidi Ya Vikombe Vingi Vya Ushirika

Iliyoendelea sana. Kitengo cha 2. Kitabu cha mwanafunzi Iliyoendelea sana

Maisha Yaliyojaa Maombi

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU

KENYA NATIONAL EXAMINATION COUNCIL REVISION MOCK EXAMS 2016 TOP NATIONAL SCHOOLS

Mwongozo wa Kitaifa wa Ujumbe wa Uzazi wa Mpango

Transcription:

Yaliyomo Kuhusu kitabu hiki Kuhusu kitabu hiki.........................................................1 Unapojisikia vibaya.........................................................2 Unapoanza kuwa mzima na ukiwa mzima..................................4 Kuendelea kuwapatia watoto mahitaji na hisia..............................6 Hisia kitu cha kushiriki na mtoto..........................................8 Miaka ifikapo 2 4........................................................ 10 Miaka 5 7 ifikapo........................................................ 11 Mpango wa matunzo..................................................... 12 Kujiandaa kabla........................................................... 13 Vidokezi kwa marafiki na familia......................................... 14 Vidokezi zaidi kwa patna.................................................. 16 Kwa maelezo zaidi na msaada...................... Ndani ya jalada la nyuma Folda la Mpango wangu wa matunzo.............. Ndani ya jalada la nyuma Shukurani Kijitabu hiki kimeandaliwa na Australian Infant Child Adolescent and Family Mental Health Association Ltd for the Australian Government Department of Health and Ageing Children Of Parents with a Mental Illness (COPMI) national initiative. Maelezo zaidi na msaada kuhusu COPMI national initiative inapatikana www.copmi.net.au Tunapenda kuwashukuru wazazi, waangalizi, watoto na wataalamu waliohusika kutengeneza kijitabu hiki. Published by the Australian Infant Child Adolescent and Family Mental Health Association Ltd (ABN 87 093 479 022) Designed, Illustrated and Produced by Motiv Brand Design AICAFMHA 2009 ISBN 0-9752124-5-1 Pia kinapatikana katika mfululizo: Family Talk The Best For Me and My Baby Kijitabu hiki ni kwa ajili ya watu wanaoishi na matatizo ya afya ya kiakili au ugonjwa wa akili, wenye watoto wa umri kati ya miaka 2 na 7. Pia ni kwa ajili ya mwenzako, familia na marafiki. Kina mawazo yanayosaidia kuhusu namna ya kuwa mzazi mzuri unayeweza kuwa wakati hauko vizuri kama ambavyo ungependa na namna kusaidia maendeleo ya ukuaji wa mtoto wako wakati wa miaka pekee ya mwanzo. Hautakuwa peke yako. Watu wengi wenye ugonjwa wa akili wanaokuza watoto hujisikia wapweke na tofauti na wazazi wengine. Baadhi huwa na woga kuomba msaada, hufikiria watapimwa bila usawa kwa matendo yao. Lakini, kuna wazazi zaidi wanaokuza watoto wakati wakiwa na matatizo ya kiakili bila wa watu wengi kufahamu na kuna watu na huduma za msaada. Hizi ni pamoja na wataalamu wa afya (Daktari wako wa kawaida, nesi wa afya za watoto, timu ya tiba ya magonjwa ya akili, huduma ya afya ya jamii namengineyo) na wafanyakazi wa awali wa watoto ( matunzo ya familia na wafanyakazi wa vituo vya kutunza watoto, shule za awali na watumishi wa shule za msingi)* Ndani ya jalada utapata namba za simu za huduma za kupiga na viunganishi vya mtandao. Mfumo wa msaada ni wa manufaa sana wazazi wote wanahitaji! Hii ni familia au marafiki, majirani, wafanyakazi wa jamii, vikundi vya msaada kwa wazazi na wazazi wengine unaokutana kupitia vikundi vya michezo vya watoto, vituo vya kutunza watoto, shule za awali na shuleni. * Zaidi ya kijitabu hiki (huitwa Kusaidia kuweka fumbo pamoja ) kwa ajili ya wafanyakazi wa awali wa watoto kinapatikana kwenye sehemu ya Wafanyakazi kwenye www.copmi.net.au 1

Wakati unapojisikia vibaya Kuangalia mahusiano yako na mtoto wako unapojisikia vibaya. Kama unahitaji kuwa mbali nao itasaidia kama ukituma ujumbe mfupi, picha au kupiga simu au kuwatembelea kwa muda mfupi. Utajitahidi kwa taratibu kuwa na muda na mtoto wako wakati ukiwa unapata nafuu. Mtoto wako atafarijika kama wewe utaweza kufanya vitu ulivyokuwa unafanya pamoja naye. 2 Wazazi wote huona kukuza watoto wadogo ni changamoto lakini unapojisikia vibaya hufanya mambo kuwa magumu zaidi. Ni muhimu kwa wewe kusisitiza kuwa mzima. Mara nyingine inabidi kuwa mbali na mtoto wako - kwa masaa machache kila siku au kwa siku kadhaa- kukuwezesha wewe kupumzika au kupata msaada kwa afya yako. Kuomba msaada ni hatua ya kuridhisha. Watoto wadogo huhitaji watu pamoja nao watakaofanya vitu kwa namna waliyoizoea, hii husaidia kuwa na utulivu. Mara nyingine hii ni vigumu kama unajisikia kuwa mbali nao, woga au mwenye huzuni. Ni SAWA kuomba msaada kwa mtu mwingine anayefahamika na kuaminika vizuri kwa mtoto wako, aweze kuwapa muda mwingi na usikivu wanaohitaji. Msaada kama huu unaweza kutoka kwa rafiki au mwenzako, babu na bibi au mzazi wa kufikia au mfanyakazi wa watoto, mhudumu wa kituo cha mafunzo cha familia au mwalimu. Omba mtu unayemwamini akusaidie kuandaa mpango wa matunzo (kurasa wa 12) kuwezesha mtoto wako kupata matunzo yake ya kawaida. Watoto hujifunza mpangilio wa maisha na kujihusisha na watu wengine kutokana na mahusiano waliyokuwa nayo na watu wazima waliowakuza wakiwa na umri mdogo. Uendelezaji mpangilio huu wa maisha hauwezi kuwekwa pembeni wakati wewe ukiwa unapata msaada lakini bahati nzuri watajifunza kutoka kwa wengine pamoja na wewe. Hii haitawazuia wao kukupenda wewe. Huwezi kujisikia vibaya muda wote, na wewe utabaki kuwa mzazi wa mtoto wako hata kama ukiwa unajisikia vizuri au sivyo. Ninadhamiria kufanya naye vitu vidogo vya pekee kila siku mara nyingine hupendelea kukumbatiwa, saa nyingine hadithi au mchezo wa haraka. Kama unapata shida na mahusiano na mtoto wako zungumza na mfanyakazi wa afya wanaweza kukonyesha vidokezi, mfano kujifunza kucheka na kuonyesha mvuto na vitu anayofanya mtoto wako katika muda mfupi. Kujibu maswali mtoto wako anayoweza kuuliza kuhusu ugonjwa au matibabu yako. Watoto huweza kufahamu ishara kutoka kwa wengine kama matukio ya wakati huu yamekatazwa. Ni vizuri ugonjwa wako ukazungumziwa kwa uhuru na kwa maneno rahisi. Mtoto wako anatakiwa kujisikia sawa kuuliza maswali. ( angalia zaidi kurasa za 9 na 10 huhusu hili). Kwa maelezo na msaada, piga simu Lifeline 131 114 (Masaa 24 ya ushauri kwa njia ya simu) Au msaada wa wazazi... ACT... (02) 6287 3833 Tas...1800 808 178 NSW - Karitane Care Line...1300 227 464 - Tresillian...1800 637 357 - Parentline...1300 1300 52 Vic...13 22 89 SA...1300 364 100 Qld & NT...1300 301 300 WA...1800 654 432 or (08) 9272 1466 3

Unapoendelea vizuri na unapokuwa vizuri Kusaidia maendeleo ya watoto wako Ni kawaida kwa mzazi kuwa na wasiwasi kuhusu maendeleo ya watoto wao - kuna mitandao na watu wanapatikana kukusaidia kujifunza kuhusu maendeleo ya mtoto wako ( mfano. www.raisingchildren.net.au, www. cyh.com, child health services, child care workers and teachers). Hisia za watoto za kujithamini huendelezwa tunapowasifia na kutambua kwa vitu wanavyofanya. Haimaanishi kuwasifia kila wakati - wafahamishe kuwa unapendelea vitu wanavyofanya kwa kutoa mawazo yako kuhusu michezo au matendo hayo (mfano. Ninakuona hapo unatengeneza mji mkubwa na hizo bloku ). Kuwa mwangalifu usijaribu kulipizia muda ambao ulikuwa hujisikii vizuri (mfano kwa zawadi) hii itamchanganya mtoto. Ni muhimu kurudia kwa haraka mwenendo na desturi za familia.confusing. Wakati huo Ilikuwa ni ngumu sana kuvumilia anapolia. Hakuna njia moja ya kukuza mtoto. Ingawa, watoto wote huhitaji chakula, wema, malazi na usalama na mazingira ya kuchangamsha. Muhimu wanahitaji angalau mtu mzima mmoja ambaye anaweza akaanzisha mahusiano nao na kuwatimizia mahitaji ya moyo na maendeleo. Unahitaji kuwaruhusu ili wakusaidie kwa muda lakini wakati unaendelea vizuri unaweza ukarudia na majukmu ambayo wengine wamekuwa wakikusaidia. Kujihusisha tena baada ya ugonjwa huchukua muda kidogo lakini taratibu jaribu kupata furaha katika mahusiano yenu kwa kufanya vitu vidogo na rahisi pamoja ambavyo mtoto wako anapendelea (mfano. mchezo wa kuzunguka na mtoto wako katika mduara huku umemshikilia mikono, kumsogelea kwa karibu/kumkumbatia, hadithi kabla ya kulala). Kuwa karibu na mwangalizi wa kawaida wa mtoto wako inakupa mapumziko wewe wakati mtoto wako anapata mwendelezo wa mambo aliyozoea. Wafahamishe watoto wako kuwa si lazima kukutafuta wewe - kutegemea wewe kuwaangalia wao. Ni kawaida kwa watoto kutaka kusaidia inapotokea mtu katika familia hajisikii vizuri au hana furaha. Ni vema kuwa na msaada kutoka kwa watoto katika kushiriki kazi lakini kuwa mwangalifu wanapotaka kuwa kama mzazi au kuchukua nafasi ya mwangalizi. Nilistuka kidogo mtoto wangu wa kiume aliposisitiza kuwa mbwa kwa siku nzima- ilikuwa kitu cha ajabu. Watu wa kituo cha watoto walishauri kuwa ilikuwa ni kitu cha kawaida katika umri huu. Watoto wadogo hunufaika kutokana na kusomewa, na kufanya vitu na watu wazima. Badilishana na mtoto wako katika kuchagua michezo mtakayofurahia pamoja. Nikiwa nahitaji muda wa kupumzika, ninamwambia afikirie ni vitu gani angependa tufanye pamoja au kusoma pamoja baadaye nikiwa tayari kuwa na muda wa pekee na binti yangu. Anapoendelea kupata nafuu itakusumbua sana pale mtoto anapolia na kuhamaki. Ni muhimu kwako kujisikia unazimudu hisia zako mwenyewe kabla ya kumsaidia mtoto wako kuendeleza ujuzi wa kutulia mwenyewe pale anapoudhika. (mfano. kuzungumza kwa sauti ya utaratibu, kumshikilia mtoto ambaye ameshindikana). Kama huwezi kumudu mahitaji ya mtoto wako kwa muda, jaribu kumtafuta mtu anayeweza kumwangalia mtoto wakati wewe unapumzika. Pata msaada kwa mfanyakazi wa afya. 4 5

Kutambua mahitaji na hisia za watoto wako. Watoto ni wachunguzi sana wa hali za wazazi wao wanapopata nafuu. Wengine hutaka kuonyesha tabia nzuri au kuwa kimya au wachangamfu au kuwa na msaada mwingi kupunguza wazazi wao kujisikia vibaya tena. Jaribu kuwasaidia kuelewa kuwa furaha au afya yako sio jukumu lao. Katika mazungumzo, jaribu kumsikiliza sana mtoto wako, jaribu kuelewa mawazo na mitazamo yake na kuonyesha kukubali hisia na maoni yake. Watoto wengine wanafanya vitu kutokana na hasira au kuchanganyikiwa na tabia ambazo huzipendi. Jaribu kuongea nao kuhusu kitu kinachosababisha tabia hiyo au kuitaja hiyo tabia ( mfano unaonekana kukasirika sana leo - kuna kitu gani?. Jisamehe wewe: Sio kila muda ni lazima Hata kwa wazazi ambao ni makini na wenye kujitolea sana kuna baadhi ya siku huwa wanataka zipite. Katika siku kama hizi, kumbuka sio kila muda ni lazima. Huna haja ya kutumia vizuri kila kitu au nafasi unayopata. Sio kila mazingira yatakuwezesha kutimiza malengo au kutoyatimiza kabisa. Wewe ni binadamu - sio mara zote unaweza kuwapatia watoto wako usikivu wanaohitaji. Hii haimanishi binti yako hatakuwa na uhodari au afya au imara kama wewe ungekuwa sawa! Mahusiano na maelewano kati yenu yanatakiwa sana, ukiondoa mambo mabaya sana katika maisha, ni vitu vinayotokea kwa muda mrefu ndiyo vyenye madhara lakini sio matukio yanayotokea mara moja moja. nafika au haufiki muhimu watoto wao. Kutoka mtandao wa Raising Children: www.raisingchildren.net.au Watoto wana njia tofauti za kuwasiliana kuhusu mahitaji na hisia zao na ni ngumu kuzitambua ishara za watoto. Chukua muda kumsikiliza na kuangalia sura ya mtoto, sauti na ishara. Weka muda katika siku ( mfano, vipindi ya dakika 5-10) ambao unaweza kuwa makini kuzisoma ishara au alama za mtoto wako na kuzikidhi - anaweza akataka uangalizi wako, au kukumbatiwa au kuachwa peke yake. Kama una mtoto mdogo zaidi ya mmoja inasaidia ukipata muda wa kuwasikiliza kila mmoja peke yake. Unaweza kuhitaji msaada kuitikia ishara za watoto kwasababu ni rahisi kuzisoma bila usahihi wakati wakijaribu kukufurahisha wewe au wakionyesha tabia ambayo wanafikiri itakusaidia wewe kupata nafuu. Mfanyakazi wa awali wa watoto a mfanyakazi wa afya wanaweza kukusaidia wewe kwa hili. Kama kuna mabadiliko katika maisha ya mtoto wako ( mfano. kama unahitaji kuwa mbali naye, au kama kuna mtu mwingine anakusaidia nyumbani) utaona kuwa tabia ya mtoto wako imerudi nyuma kwa muda au wamepoteza ujuzi waliojifunza (mfano. kutumia choo). Hii itabadilika bila ya wewe kufanya chochote mara mtoto wako anapoanza kujiamini tena. Mjulishe mwalimu wa mtoto wako au mfanyakazi wa watoto kuhusu mazingira yako wanaweza kukupa msaada wa ziada kama inabidi. Pia unaweza kuzungumza nao kuhusu wasiwasi wako kuhusu tabia ya mtoto wako. Mara nyingine wazazi huona ni ngumu kuwa na mapenzi na watoto wao. Zungumza na mfanyakazi wako wa afya kama hii inatokea kwako. 6 7

Hisia - ni tendo la kumshirikisha mtoto wako. Unafikiri watoto wanajisikiaje? Kwanini unafikiri wanajisikia hivyo? Furaha Kushangaa Woga Huzuni Hasira Shauku Chora picha konyesha unavyojisikia sasa hivi. Watoto wa miaka miwili wanaweza kutambua uso wa furaha au huzuni lakini watoto wakifika miaka nane wengi wanaweza kujua hisia zote katika kurasa hizi. Unaweza kupata orodha ya vitabu vya watoto vinavyoweza kukusaidia kuongelea hisia au ugonjwa wa akili katika sehemu ya rasilimali ya www.copmi.net.au 8 9

Wenye miaka 2-4 Wenye miaka 5 7 (utakuta mifano zaidi kwenye mtandao COPMI sehemu ya Wazazi na Familia www.copmi.net.au). Waangalizi hasa wa mtoto (mfano mfanyakazi wa watoto, babu, bibi, waangalizi wa kufikia) wanaweza kufahamu lugha unayoitumia kuelezea ugonjwa au dalili za ugonjwa ili kuhakikisha mtoto anapata ujumbe sahihi. Kama kila mtu anaweka siri, mtoto atafikiri haruhusiwi kuzungumzia juu ya wasiwasi na mambo husika- kuwa wazi humsaidia mtoto kuuliza maswali kuhusu mambo yanayotokea na kumuandaa kufahamu mambo mengine magumu kadiri anavyozidi kukua. Angalia na watoto wako kuhusu wanavyojisikia na kama kuna mabadiliko ya utaratibu. Kuwa wazi kuzungumza kuhusu ugonjwa wako - kuwa na nafasi ya kuwasikiliza wanapotaka kuzungumza. Usiwaongezee mizigo ya wasiwasi wako Ni vizri kuzungumza mambo haya na marafiki, familia au mfanyakazi wa afya. Mara nyingine mtoto wako anaweza kutaka au kupenda kuongea na mtu mwingine zaidi ya wewe kuhusu wasiwasi wao - ni kawaida katika ukuaji. Wafahamishe kuwa wewe uko sawa kuhusu hili ili wasijisikie kufanya hivyo kutakuudhi wewe. Wahamasishe watoto wako kupenda maisha ya shuleni na kufanya mambo yao wenyewe. Usiache uangalizi wa mtoto wako kwa watu wengi. Ni muhimu kuwa na waangalizi wale wale na wachache wenye kufahamika kukusaidia wewe kujisikia na amani na kuhamasisha maendeleo yao. 10 Wahamasishe wakueleze jinsi wanavyojisikia kuhusu kitu kilichotokea. Watoto wa umri huu huunganisha kila kitu na wao kwa namna fulani ili kujaribu kufahamu kama wameelewa na pia kuondoa kitu wasichokielewa. Kwa mfano mtoto anaweza kufikiri kuwa mbali na wazazi ni adhabu au umbali wa kimawazo na mzazi wake (kwasababu ya ugonjwa au dawa) humaanisha kuwa mzazi hampendi. Tafuta maneno unayokuwa sawa nayo kuongelea kama familia kuzungumzia kuhusu ugonjwa wako na yatumie kama lugha ya kawaida. Baadhi ya familia huzumza kuhusu mzazi kuwa na mawazo yaliyovurugika wakiwa hawajisikii vizuri au wanahitaji siku ya utulivu na ukimya.wengine hutumia mifano ya kitabia katika hadithi za kitabu cha Winnie the Pooh wanaoitwa Eeyore and Tigger kuelezea namna mzazi anayojisikia Kwa kawaida watoto huelewa mambo mengi kuliko uzungumzaji. Wanajua kama kuna kitu kibaya kwahiyo inasaidia kuzungumza nao kitu kilichotokea. Weka maelezo mafupi na ya ukweli - kuchora au picha husaidia. Waulize wanavyofikiria kuhusu kilichotokea. Kundi la umri huu ( miaka 5- ) huelewa maelezo lakini hutumia maneno wahayosikia kutoka kwa watu wazima bila ya kuelewa maana yake. Elewa ufahamu wa mtoto wako wa maelezo, maneno na mazingira (mfano Je neno hili. lina maana gani? ). Weka maneno yasiyoeleweka kwa usahihi. Katika hatua hii watoto wanaweza kujua kwa taratibu mawazo ya watu wengine lakini bado hufikiria wao ndio wanaosababisha mambo kutokana na tabia mbaya, kufikiri au kutaka vitu (mfano wao ndio wamesababisha ugonjwa wa mzazi). Hujifunza kusoma, watoto wengine huanza kupenda maelezo yaliyoandikwa (mfano vitabu vya hadithi, mitandao ya watoto). Ili kufahamu mambo mengi juu ya mahitaji ya watoto katika makundi tofati ya umri zungumza na mfanyakazi wa afya au mfanyakazi wa awali wa watoto au angalia mitandao iliyoorodheshwa ndani ya jalada. 11

Mpango wa matunzo Panga kabla Wazazi wengi huona ni manufaa kutengeneza mpango wa matunzo wa familia yao na ndugu wengine wa familia au marafiki (na watoto kama ni wakubwa vyakutosha). Mpango husaidia wote kufahamu vitu ambayo ungependa vifanyike endapo wewe utaugua tena na kushindwa kwa muda kuangalia mtoto wako. Mpango huu huwapa uhakika watoto pamoja na watu wazima wahaohusika zaidi na maisha ya mtoto. Utapata mifano ya mpango wa matunzo kwenye www.copmi.net.au katika sehemu ya rasilimali au kwa kuuliza mfanyakazi wa afya, mfanyakazi wa watoto au mfanyakazi katika shule anayosoma mtoto wako anaweza kukusaidia. Inaweza kuwa msaada kuandika mpangilio au utaratibu wa kawaida wa mtoto na familia. Inakuwa vizuri vitendo vya kawaida vya watoto wadogo kuendelea wakati mahusiano na mzazi yametenganishwa. Tumia kipande cha Mpango wa matunzo kinachokatwa na orodha ya usahihi nyuma ya kijitabu hiki ili kukusanya maelezo. Tunza mahali ambapo mtoto wako na wengine ambao wanamwangalia mtoto wanafahamu. Ni matumaini kuwa mtoto wako, wewe na wengine watafurahia matendo kwenye jalada la mpango wa matunzo. Panga kabla mahitaji yako binafsi pamoja na mtoto wako. Inasaidia kupanga kabla katika siku ambazo wewe unahitaji kupumzika zaidi, kwa mfano: Kuwa na chakula rahisi cha kuandaa kama supu, vijipande vya samaki, maharage ya kopo au mboga za majani za kwenye friza. Panga viti vya ndani ili iwe rahisi kumwangalia mtoto wako akiwa anacheza wakati wewe umepumzika kwenye kochi kama inabidi. Weka baadhi ya DVD anazopenda mtoto wako. Panga uangalizi wa mtoto mara kwa mara ili wewe upumzike, upate huduma ya afya au uweze kufanya kitu chako mwenyewe. Kuandaa mpango wa matunzo wa familia unasaidia sana kuweza kongelea baadhi ya vitu. 12 13

Ushauri kwa familia na marafiki 14 Mtu wa kuaminika aliye na mahusiano mazuri na mtoto wako ni tegemeo lao, hasa kama mtoto haelewi au anaogopa, anahitaji kuwa na muda mbali na mzazi au akiwa na maswali. Wafahamishe watoto kuwa wanaweza kukuuliza wewe maswali yeyote yanayohusu tabia ya mzazi wao, ugonjwa na au matibabu. Usifanye kuwa jambo la mwiko. Watoto wadogo hawahitaji majibu ya kina lakini inakusaidia wewe ukisikiliza maswali yao kufahamu jinsi wanavyochukulia ugonjwa huo na namna unavyowadhuru (kwa mfano Unafikiria kitu gani kinatokea? ). Kuwapa watoto majibu mafupi na rahisi ya maswali yao inawasaidia kuondoa nafasi katika ufahamu wao. Au sivyo mara nyingi huendelea kuotea maelezo ambayo huwatisha zaidi ukilinganisha na ukweli. Watoto wadogo hupendelea kuwa na mtu wa kumwambia habari zote mpya - mtu ambaye anayejihusisha na siku yao ilivyokuwa. Anayecheza nao na kuhamasisha furaha katika maisha yao. Tafuta msaada kwa ajili yako, hasa kama unatoa msaada wa muda kwa mtoto ( kwa mfano, piga simu Carers Advisory Service 1800 242 636). Mara nyingine mzazi akiwa na tatizo la akili, tabia zao huwachanganya na kuwaogopesha watoto. Mzazi mkorofi, asiyetulia, mwenye hasira anaweza kuogopesha na kumchanganya mtoto na ni vizuri kumlinda mtoto na tabia za ugonjwa wa akili. Uso mtupu au uliokosa hisia pia unaweza kumchanganya au kutishia amani ya mtoto. Unaweza kumsaidia mtoto kwa kumuondoa taratibu kutoka kwenye mazingira haya ya kutisha, mbembeleze na kuwa wazi na maswali atakayokuwa nayo khusu tabia ya mzazi wake. Kama mzazi anashindwa kuonyesha tabia ya kueleweka kwa mtoto, mueleze mtoto kuwa mzazi anajitahidi kwa wakati huo lakini tabia hiyo ya isiyofahamika ni sababu ya ugonjwa wa mzazi na sio jinsi wanavyojisikia juu ya mtoto wao. Muulize mtoto anajisikia vipi na mfahamishe kuwa ni sawa kuwa na huzuni, au hasira au kuwa na hisia nyingine. Zungumzia kuhusu hisia kama kielelezo cha mfano kwa mtoto (mfano. Najisikia huzuni wakati.. au Nimesikitika asubuhi hii wakati.. Tumia picha au hadithi za vitabuni zilizotajwa ukurasa wa 9 na 10. Mtu wa maktaba au mfanyakazi wa awali wa watoto anaweza kukusaidia kuchagua vitabu vya watoto vinavyoelezea hisia. Hakikisha watoto wakubwa wanajua namba ya Kids Help Line (1800 55 1800) na wakati gani wanaweza kupiga. Itasaidia kuhifadhi hii namba na namba nyingine muhimu kwa ajili ya watoto kwenye simu ya nyumbani. Kumsaidia mzazi anapoendelea kwa taratibu kuchukua nafasi zao za malezi. Kama umekuwa unafanya kazi ambazo mzazi alikuwa anazifanya, kuwa mwangalifu na maelewano yanayotakiwa kufanyika mzazi anapoendelea vizuri - Punguza hatua bila kuondoka kabisa. Wasisitize watoto wafahamu umuhimu wa nafasi ya mzazi katika familia. Jitolee kumsindikiza mzazi kwenye vituo vya awali vya watoto au kituo cha familia na uwe tayari kuzungumza na mwangalizi wa mtoto au mkurugenzi wa kituo khusu mahitaji ya mtoto na hali halisi ya familia. Ugonjwa wowote huongeza matatizo katika mahusiano ya familia. Epuka kuchukua upande kati yao. Kuwa makini na mahitaji ya mtoto ni msaada mkubwa. 15

Ushauri zaidi kwa mwenzako Kwa maelezo zaidi na msaada Uzazi ni mgumu kwa familia na ugonjwa wa akili pia - pata msaada kama unadhani mwenzako anapata shida sana. Kama kuna wasiwasi mwingi katika nyumba, ni rahisi kwa watoto wadogo kutambua. Usidhani mkiwa mnagombana wakati watoto wamelala au kwenye chumba kingine basi wanakuwa wamelindwa. Uliza kwa mfanyakazi wa afya au mfanyakazi anayehusika na ukuaji wa watoto kuhusu huduma hizi na maelezo katika eneo lako unaloishi ( mfano huduma za wanawake au familia na vituo vya huduma za jamii), au piga namba za simu zilizoandikwa mwishoni kwa msaada. Child Care Hotline................................................ 1800 670 305 (Kwa maelezo na ushauri hiari wa kutunza watoto katika eneo unaloishi) Carers Advisory Service (Counselling and Support)................... 1800 242 636 (Au wasiliana na Carer Association wa Jimbo au eneo la Nchi) Lifeline................................................................ 131 114 (Kwa masaa 24-ya huduma ya wasaha kwa simu na rufaa kwa huduma zingine za msaada) Lifeline s Just Ask.................................................. 1300 131 114 (Kwa maelezo kuhusu huduma za afya ya akili na rasilimali zaidi ya afya ya akili) SANE Australia Helpline.......................................... 1800 187 263 (Información y derivación a servicios de ayuda) Relationships Australia............................................ 1300 364 277 (Kwa maelezo na ushauri huhusu mahusiano kati ya watu) Mensline....................................................... 1300 78 99 78 (Kwa wanaume wanaohangaika kwenye mahusiano na familia) Parent Helplines ACT..........................(02) 6287 3833 Tas....... 1800 808 178 NSW Karitane Care Line...... 1300 227 464 Vic............13 22 89 Tresillian............... 1800 637 357 SA....... 1300 364 100 Parentline.............. 1300 1300 52 WA...... (08) 9272 1466 Qld y NT...................... 1300 30 1300 or 1800 654 432 16 Nilishangaa alipotuuliza kwanini tunachukiana - nilidhani tumeweka matatizo yetu mbali na yeye. Kuachana, Kutengana au Familia zilizomchanganyiko? Unaweza kupata usaidizi kutoka kwa wazazi au kukuza mtoto wako kama mzazi pekee mfano wasiliana na Relationships Australia, simu 1300 364 277, au Mensline, simu 1300 78 99 78, wasaidizi waliopo eneo lako Parent Helpline, au tembelea mtandaoni Raising Children Network parent forum section angalia ndani ya jalada la mwisho kwa maelezo zaidi. Huduma kutoka kwa Carers Advisory Service wanatoa ushauri nasaa na msaada kwa watu wanaotunza mwenzi wako, simu 1800 242 636. Ilikuwa vigumu kwa mara ya kwanza kukubali msaada lakini sijui ningefanya nini kama rafiki wa mke wangu alipokubali kumpeleka mtoto wetu wa msichana kituo cha watoto kila asubuhi, kama baba asinge shirikiana nasi na kama wifi yangu asingetuletea chakula. Useful web address (kumbuka: intaneti inapatikana katika librari ya eneo unaloishi) Raising Children Network www.raisingchildren.net.au Child and Youth Health www.cyh.com Children of Parents With A Mental Illness (COPMI) www.copmi.net.au Mental Health and Well-being www.mentalhealth.gov.au Families where a Parent has a Mental Illness (FaPMI) (Formerly VicChamps) www.easternhealth.org.au/champs/ Multicultural Mental Health Australia www.mmha.org.au My Child www.mychild.gov.au Attachment Resources www.attachmentresources.com.au SANE www.sane.org Carers Australia www.carersaustralia.com.au Relationships Australia Online Counselling www.relationships.com.au 17