Forum:MyElimu Home for Students to Share Knowledge Thread: Dunia Uwanja Wa Fujo

Similar documents
Information for assessors (do not distribute this page to participants):

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

Mbinu za Ujenzi wa Wahusika na Usawiri wa Sifa Zao: Uhakiki wa Riwaya ya Dunia Uwanja Wa Fujo ya E. Kezilahabi

Usimulizi wa Riwaya ya Nyongo Mkalia Ini E. S. MOHOCHI University of Egerton, Kenya

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

Hati ya Kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya.( K.C.S.E)

Human Rights Are Universal And Yet...

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level

MTIHANI WA MWIGO WILAYA YA BUTERE MUMIAS-2007 Hati ya kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya

Theolojia Ujumla. Mike Taylor Semester Munguishi Bible College

Mwongozo wa Utamaduni Toleo la Kwanza

KUCHUNGUZA UJINSIA NA MATUMIZI YA LUGHA KATIKA METHALI ZA WAKURYA

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

SANIFU KWA SHULE ZA SEKONDARI KITABU CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO

usudi la Maisha Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na kupishana usiku na mchana, kuna kweli ishara kwa wenye akili, ambaye mkumbuke-

JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1

"ATATOKEA MARA YA PILI, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu." Waebrania 9:28.

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Kiu Cha umtafuta Mungu

MUNGU ANADHIHIRISHWA KUPITIA KWA YESU KRISTO.

MACHAGUO YA UZAZI KUFIKIRIA KUWA MZAZI

# 18 Uponyaji Kutokana na Kukataliwa

Nordic Journal of African Studies 23(4): (2014)

N09/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q

Ufunguo wa Kutaalamika Haraka

UJAGINA WA MWANAMKE KATIKA PANGO

Mutugi Kamundi. Jemma Kahn. Kiswahili. Demane na pacha wake. Author - South African Folktale

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti

Adhabu ya jino kwa jino na Musitakabali wa imani zetu

JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI

SANIFU KWA SHULE ZA SEKONDARI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO

KUCHUNGUZA MCHOMOZO KATIKA FASIHI YA KISWAHILI: UTAFITI LINGANISHI WA USHAIRI KATIKA DIWANI YA USTADHI ANDANENGA

FANI KATIKA NYIMBO TEULE ZA ANASTACIA MUKABWA MBURU JAMES MUNGAI TASNIFU HII IMETOLEWA ILI KUTOSHELEZA BAADHI YA

Ushindi ndani ya Kristo W. W. PRESCOTT

Haja Ya Dini. Author(s): Publisher(s): Translator(s): Category: Topic Tags: Featured Category: Published on Al-Islam.org (

KUCHUNGUZA MASUALA YA KISIASA KATIKA RIWAYA ZA SHAABAN ROBERT: MFANO WA KUSADIKIKA NA KUFIKIRIKA

PDF created with pdffactory trial version

Tora UTANGULIZI KWA TORA SOMO LA KWANZA

UFASIHI SIMULIZI KATIKA RIWAYA ZA SHAABAN ROBERT: Mifano kutoka Adili na Nduguze na Wasifu wa Siti Binti Saad. Khatib Khamis Saleh

JAZANDA YA NJOZI KATIKA BAADHI YA MASHAIRI YA EUPHRASE KEZILAHABI (ONEIRIC IMAGES IN EUPHRASE KEZILAHABI S SELECTED POEMS) 1

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

K. M a r k s, F. E n g e l s

CHUO KIKUU CHA NAIROBI IDARA YA KISWAHILI MAMLAKA NA ITIKADI KATIKA NYIMBO TEULE ZA TAARAB

NAFASI YA MUZIKI ULIOPENDWA KATIKA FASIID YA KISWAHILI PAMELA M. Y NGUGI. Inkisiri. M a kala. AAP 64 (2000): Swahili Forum VII

Na Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake Toleola4

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

Kiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika

Hakimiliki na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa TAFSIRI YA BIBLIA. Mwandishi. Jonathan M. Menn

Ndugu na dada zangu wapendwa,

NAFASI YA MWANAMKE: JINSI INAVYOTETEWA KATIKA NYIMBO ZA TAARAB ZA ZANZIBAR ELIZABETH KANGOGO YEGO C50/68796/2011 IDARA YA ISIMU NA LUGHA

Tufundishane! Mwalimu Bora In this issue: Issue 6, December Do you want to be in our next issue?

UJASIRI WA YOHANA MBATIZAJI

Mafundisho Ya Msingi Wa Kikristo. Na Andrew Connally

Deutsche Welle, Learning by Ear 2009 Seite 1 People Who Make A Difference Liberia: Anita Varney Health Facilitator, Fishtown/Liberia

(Hati ya kuhitimu kisomo cha sekondari Kenya (K.C.S.E)

MITAZAMO KUHUSU KISWAHILI MIONGONI MWA WAZUNGUMZAJI WA KIJALUO: KIFANI CHA SHULE ZA MSINGI KATIKA KAUNTI YA MIGORI. OWALA JAEL AKINYI C50/75493/2012

UFAHAMU NAME INDEX SCHOOLDATE UFAHAMU

Uponyaji Wa Laana. (Kumb. 28:1-14).

MUNGU ALIUMBA ULIMWENGU 1 WETU NA VYOTE VILIVYO HAI

Shabaha ya Mazungumzo haya

TAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF) KUHUSU HAKI ZA WATOTO KATIKA KATIBA MPYA

Wanawake katika Uislamu

TASFIDA KAMA MKAKATI WA UPOLE: UWIANO WA TASFIDA ZA KISWAHILI NA EKEGUSII

Pronunciation: Mä-hret Zäläke Ndal-ka-tscho Molla Mare Gebre-gzabiär 1/12

Mwongozo kwa familia zinazofanya kazi pamoja kwa maisha endelevu. Nyenzo ya Mafunzo

KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA

MARUDIO K.C.S.E KNEC KISWAHILI KARATASI 102/2 MASWALI NA USAHIHISHO

wasiofaa. Naomba sana kila raia afanye bidii awezavyo kumkaribia Mwenyezi Mungu vile anavyoona inafaa, lakini asipitishe hukumu juu ya wengine.

Elimukombozi, Lugha na Upashanaji Habari nchini Tanzania, katika Muktadha wa Utandawazi

Kufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007

Roho Mtakatifu Ni Nini?

V\ FANI KATIKA USHAIRI WA HASSAN MWALIMU MBEGA: UHAKIKI WA UPISHO WA UMALENGA NA DAFINA YA UMALENGA DONALD OMWOYO OSIEMO

KISWAHILI KARATASI YA 2 LUGHA

Usimulizi katika Utenzi wa Swifa ya Nguvumali

Kutetea Haki za Binadamu

MATATIZO YA MWANAMKE KATIKA KIDAGAA KIMEMWOZEA NA NYUSO ZA MWANAMKE. MONICA C RUTO

Elimu Ina Umuhimu gani katika Jamii? Kuelekea Elimu Sahihi

MADA MATUMIZI YA TAKRIRI NA SITIARI KATIKA UTENZI WA RASI LGHULI JUSTUS MAUNDU NDUMBU C50/65902/2011 CHUO KIKUU CHA NAIROBI IDARA YA ISIMU NA LUGHA

UTARATIBU WA KANISA. 2 Jambo la kwanza ninalotaka kusema ni kwamba mchungaji. 3 Sisi tunaamini katika Kanisa la kimitume, tukifundisha

Mukhtasari Wa Mabishano Kwa Na Dhidi Ya Vikombe Vingi Vya Ushirika

Upekee wa Utenzi wa Swifa ya Nguvumali: Utenzi wa Mpito, Mseto wa Imani za Jadi Na Usasa MWENDA MUKUTHURIA Egerton University, Kenya

Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara)

KUSHUKA KWA HADHI YA LUGHA ZA JAMII NCHINI TANZANIA YOHANA P. MSANJILA University of Dar es Salaam, Tanzania

Waandishi: wa Toleo la 5. Scholastica Jullu Athanasia A. Soka Safina Hassan Mary Njau. Toleo la 5: 2008 ISBN

SautiElimu. Sauti Yako Isikike

Hatari, Haki za Usalama katika Bahari 03

Kitabu Cha Mafunzo Ya Uongozi Kwa Wanawake

Elimu Bora, lakini... C HakiElimu Elimu bora, lakini...

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC)

JE, YAWEZEKANA KUISHI BILA KUTENDA DHAMBI?

Mhashamu Askofu Jude Thaddaeus Ruwa ichi, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania; Mwadhama Policarp Kardinali Pengo,

RISALA FUPI YA KUMUWEZESHA MTU KUPAMBANUA NI IPI DINI YA HAKI MWANDISHI: SALEH M. KYAMBO

LUGHA YA KISWAHILI KATIKA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA ELIMU SHULE ZA SEKONDARI

Yaliyomo. Kuhusu kitabu hiki. Hautakuwa peke yako. Mfumo wa msaada ni wa manufaa sana wazazi wote wanahitaji!

Kimesanifiwa na:- E.D.Kissuu ECOMM TANZANIA S.L.P ,Dar es Salaam. Simu:

MAKALA: USHAIRI WA KISWAHILI KATIKA NJIA PANDA: KUTUMIA AU KUTOTUMIA METHALI

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

KUCHUNGUZA UFASIHI SIMULIZI UNAOJITOKEZA NDANI YA HADITHI ZA KUSADIKIKA NA ADILI NA NDUGUZE

Transcription:

Forum:MyElimu Home for Students to Share Knowledge Thread: Dunia Uwanja Wa Fujo MwlMaeda - June 10, 2017, 9:19 am Dunia uwanja wa fujo ni riwaya iliyoandikwa na Euphrase Kezilahabi mwaka wa 1975. Ni riwaya ambayo inasawiri maisha ya wanadamu hususani waishio Afrika Mashariki, hasa hasa katika nchi ya Tanzania. â œdunia uwanja wa fujoâ inaelezea jinsi maisha yaliyopo duniani ni sawasawa na fujo, kwani kila mtu anayekuja duniani huleta fujo zake na baadaye kutoweka. Mwandishi anaelezea kwamba kila mtu anafanya fujo zake na kusababisha matatizo mbalimbali katika jamii yake kama vile mauaji, ukabila, umalaya, uchawi, ubakaji, ulevi wa kupindukia n.k. Hivyo basi mwandishi anaamini kwamba katika dunia kila mtu anakuja na fujo zake na kutoweka. Kwa mfano, mhusika Tumaini katika riwaya hii ameleta fujo zake kama vile umalaya, mauaji na mengine mengi na baadaye kutoweka. Mbinu za kifani katika riwaya hii Fani za kijadi ndizo zilizosababisha riwaya izalike. "Dunia ni uwanja wa fujoâ ni mojawapo ya riwaya zilizotokana na fani ya kijadi ambayo ni sira. Sira ni fani ya kijadi ambayo hujumuisha wasifu na tawasifu, yaani habari za maisha ya watu; kwa mfano mwandishi E. Kezilahabi katika riwaya yake hii amejaribu kumuonyesha mhusika Tumaini maisha aliyokuwa akiishi. Mfano uk. 11, â œalibatizwa, alikuwa mtoto wa mwalimu Kapingaâ â â. Vile vile Tumaini alikuwa mlevi, malaya, mfano uk. 73 â œmwenyewe kaingiaaaa, tajiri wetuuuâ. Hivyo basi riwaya hii inasadifu kuwa ni mojawapo ya riwaya za fani za kijadi ambayo hujumuisha wasifu wa mhusika Tumaini toka mwanzo hadi mwisho wa maisha yake. Muundo Muundo ni namna visa na matukio hufuatana kwa mtiririko. Hivyo tunaweza kusema pia muundo ni mfuatano wa masimulizi katika kazi ya fasihi. Katika riwaya hii mwandishi ametumia muundo wa rejea pamoja na changamano. Katika muundo wa rejea mwandishi anaanza kwa kuonyesha maisha ya Dennis pale alipowapokea wageni akina Tumaini na pia kurejelea kwa kuonyesha maisha ya Dennis pale tangu utoto wake (uk.66). Pia mwandishi ametumia muundo changamano au rukia ambapo visa vinakuwa vinarukiana: hii inajidhihirisha sehemu ya kwanza ambapo anatuonyesha nyumbani kwa Kasala ambaye anaishi kijijini Bugolola; kisa hakijaisha tunaona pia kisa cha Tumaini (uk.11) ambapo mwandishi anaonyesha alivyozaliwa na kubatizwa. Mwandishi pia ameigawa kazi yake katika sehemu kuu tatu na kila sehemu ameipa namba ili kusadifu yaliyomo katika kazi yake ya riwaya. Katika sehemu ya kwanza E. Kezilahabi amewachora wahusika kwa kuonyesha adha na matatizo mbalimbali yanayoikabili jamii ya Bugolola, kwa mfano ushirikina, umalaya na ulevi: mambo hayo yote ameyaonyesha katika namba 1, 2, 3, 4, 5. Pia katika sehemu ya pili tunamuona Tumaini akiwashawishi akina John na Anastasia kwenda nao mjini Dar es Salaam, lakini inakomea Shinyanga baada ya kukutana na dada ya Dennis, kitu kilichompelekea Tumaini na wenziwe kuanza maisha mapya mjini Shinyanga. Lakini katika maisha hayo Tumaini na John wanakuwa wenye kupenda pombe na ansa, kitu kilichopelekea kufilisika kwa Tumaini. Sehemu ya tatu inaonyesha baada ya Tumaini kuamua kufanya kazi alivyopata mafanikio makubwa, lakini mafanikio hayo yanaingia doa baada ya serikali kuingiza mfumo wa ujamaa, kitu kilichopelekea mali zote za Tumaini. Mwisho kabisa tunamuona akichukua jukumu la kumuua mkuu wa wilaya ya Shinyanga ambaye ndiye alikuwa msimamizi mkuu wa shughuli za ujamaa; kitendo hicho kinapelekea hukumu ya kifo kwa Tumaini (namba 12, 13, 14).

Msuko Mbunda Msokile (1992:206) anasema kuwa msuko ni mtiririko au mfuatano wa matukio yanayosimuliwa kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Hali hii huandamana na uchaguzi au mpangilio na ufundi wa kusimulia matukio yaliyoungwa vyema katika kazi ya sanaa ya kubuni itumiayo lugha. Lakini si tofauti na ule ufafanuzi huu si tofauti na ule unaofafanua muundo, kwani nao ni mtiririko wa matukio jinsi jinsi yanavyopangwa kiufundi kutoka mwanzo wa simulizi hadi mwisho. Pesa za urithi alizoachiwa Tuamini pamoja na malezi mabaya kutoka kwa wazazi wake ndio zinakuwa usababishi wa utonvu wa nidhamu wa Tumaini katika kijiji chao cha Bugolola, mambo hayo ya uonvu wa nidhamu ni kama vile;- mlevi, Malaya, kutofanya kazi, pia alitumia ovyo mali alizoachiwa. Mfano katika (uk.15) â œtunamuona mama yake Tumaini akimkabithi Tumaini funguo ya kufungua sanduku la marehemu baba yake ammbalo lilikuwa limebeba urithi wake. Tumaini baada ya kupewa pesa za urithi hapa ndio tunaona mshitikizo kwani kwani pesa za urihi zilimsababisha kuamua kuacha shule na kuanza kuzitumia pea hizo ovyo kama vile ukahaba umalaya, ulevi, na mengineyo. (Uk. 16, 17). Pia katika riwaya hii msuko unaendea kuonekana pale ambapo Tumaini, John, na Anastazia walipofika Mwanza na kufanya maamuzi ya kuelekea Daes saalam baada ya kuona eneo la Mwanza haitawafaa kwa kuanza maisha mapya kwani palikuwa karibu mno na kijini kwao, sababu nyingine ilikuwa Akina Tumaini hawahuondoka kijijini kwao kwa wema. Safari yao ya kuelekea Dar es saalam inafikia kikomo pale ambapo walipofika Shinyanga na kukutana na Dennis ambaye aliwasihi wasitishe safali yao ili aambatane nao wakapajue kwake na kumpasha habari juu ya mambo yaliyokuwa yakiendelea kijijini kwao Mugele (uk.55-72). Hali ya kuahilisha safari ya kuelekea Shinyanga ilisababisha akina Tumaini kuanza maisha mapya mjini Shinyanga na kwa vile Tumaini alikuwa na pesa nyingi za urithi alianza maisha ya anasa hali hiyo ilipelekea kuishiwa Tumaini kipato na kumpelekea Tumaini kutafuta kazi ya ulinzi ambayo alisaidiwa na Dennis katika kuipata ajija hiyo(uk.114). Lakini pindi alipoanza kazi hiyo alijikuta akichukiawa na watu mbalimbali kutokana na kazi yake ya kuchunguza watu sili zao na kuzilipotisha serikarini. Kzi hiyo ilisababisha hata baadhi ya watu kumkimbia Tumaini mahali alipotia mguu wake. Mfano pindi alipofika baa wateteja walikunjwa haraka haraka na kukimbia hali hiyo ilisababisha wenye biashara zao kumchukia Tumaini na ikafikia hatua ya kumtafutia Tumaini wajambazi wa kumuadabisha Tumaini. Baada ya Tumaini kutafutiwa majambazi na kuwa ameadabishwa hali hiyo inatumika kama usababishi wa Tumaini kuichukia kazi yake na kuamua kutafuta kazi nyingine ya kujiajili yeye mwenyewe, kazi yenyewe ilikuwa ni kazi ya ukulima japo alianza kama mkulima mdogo lakini baadae akajikuta akipata maendeleo makubwa katika kazi yake mfano alinunua shamba kubwa na alitumia Trekta katika shuguli zake za kilimo. lakini ngombe wa maskini hazai serikali ikapitisha mfumo wa ujamaa ambapo ilidai hakuna umiliki binafsi na mali zote ni za ni za umma hali hiyo ilisababisha kumuingiza tumaini matatani kwa hakukubaliana na hali hiyo na kupelekea kufanya tukio la mauaji ambapo alimuua mkuu wa wilaya ambaye ndiye alikuwa ni kiongozi wa ujamaa (uk.114), Kitendo hicho kilitumika kama usababishi kwa Tumaini kuwekwa chini ulinzi wa polisi na hatimaye kuhukumiwa kunyongwa (Uk.131). Mtindo Mtindo ni jinsi msanii anavyotumia ufundi, umahiri na hisia zake katika kutenda au kueleza jambo fulani. katika riyawa hii kuna mitindo mbalimbali ambayo mwandishi ameitumia ni kama vile; VIPENGELE VYA MTINDO VILIVYOTUMIKA KATIKA RIWAYA HII; Monolojia [Masimulizi] kwa kiasi kikubwa mwandishi ametumia lugha ya masimulizi katika kuelezea visa/matukio, sifa na tabia za wahusika katika kuikamilisha kazi yake. MTINDO WA BARUA Mwandishi pia ametumia mtindo wa barua, m kwa mfano katika uk.68 mwandishi ametumia mtindo wa barua tunaona Vera akimwandikia Denis barua, pia uk.105 mwandishi ametumia mtindo huu wa barua, Tunamuona Tumaini akimuandikia Joku barua vilevile katika uk.110 â œtunamuona Denis akipokea barua kutoka kwa Veraâ, uk.123 â œbibi Kimalio alimuandikia barua denisâ. HOTUBA Mwandishi katika kazi yake hii ya riwaya ya â œdunia ni uwanja wa fujoâ ametumia mtindo wa hotuba. Kwa mfano katika uk. (115-117) mtindo wa hotuba umetumika na hotuba

ilikuwa ya kusisitiza Azimio la Arusha ambalo lililenga hatua ya siasa ya ujamaa nakujitegemea ambayo ilitaka watu wote wamiliki mali na uchumi kwa pamoja bila kujali mwenye nacho na asiye ncho. NYIMBO Ni mtindo mmoja wapo aliotumia mwandishi aliotumia mwandishi wa riwa hii. Kwa mfano uk.10 mwandishi ametumia wimbo ulioimbwa na mpiga zeze. â œwanaume Bugolola Mchana hawajambo Usiku hawana tendoâ Mwandishi pia ametumia wimbo kwa mtindo wa shairi katika kazi yake hii kwa mfano katika uk.13 tunona Tumaini akiandika shairi ambalo lilisomwa na mwalimu darasani kama ifuatavyo. â œyeh, Nitaoa msichana Msichana mwenye shingo Shingo shingo kama la mbuni..â Mwandishi ametumia wimbo wa maungunzo, mwandishi katika mtindo wa mazungumzo ametumia nafsi zote tatu yaani nafsi ya nafsi ya kwanza, nafsi ya pili, nafsi ya tatu katika kazi yake yake hii ya Dunia uwanja wa fujoâ kwa mfano. - Uk. 13 tuaona nafsi ya kwanza umoja â œnitaoa msichanaâ na - uk.27 tunaona nafsi ya kwanza wingi. â œhata sisi,â pia - Pia nafsi ya pili katika riwaya hii imetumika kwa mfano uk.36 â œâ wewe kasala Pia nafsi ya tatu katika riwaya hii tunaona katika uk.35 â œâ.yeye alisema kwa machozi MATUMIZI YA LUGHA Lugha ni muhimu katika kazi ya fasihi. Posipo lugha hakuna riwaya. Mwandishi wa riwaya hii â œdunia ni uwanja wa fujoâ ametumia lugha sanifu iliyosheheni taswira, mkoto, misemo, methali, tamathali za semi, nahau, lugha za kigeni, na mbinu zingine, za kisanaa kama ifuatavyo:- Lugha sanifu ni moja wapo ya ambayo mwandishi ametumia toka mwanzo hadi mwisho. Lugha iliyotumika ni Kiswahili sanifu. Pia mwandishi ametumia lugha isiyo sanifu kwa kiasi kidogo. Kwa mfano katika uk. 5, Mwandishi anasema â œâ. Batoto bamenisosondogorasondogola na chichwa, bengine bamenikorokorakorokora na kuchaâ. Uk. 30 â œâ. Vizuri walilia kwa sauti za kutisha, yuhuu. Huba, huba, huba. Wotha,wothaâ LUGHA YA KIGENI Imetumiwa na E. Kezilahabi katika riwaya yake hii. Lugha ya kigeni aliyotumia ni Kiingereza kwa mfano:- - â œafricans royal barâ (uk. 62). - â œsnow capâ (uk.62) - â œyou are too optimistic about life and you are too pessimisticâ (uk.65, 66). - â œwelcome backâ (uk.88). - â œsecurity (uk.89 na 90). MCHANGANYO NDIMI Ni matumizi ya lugha ambayo mwandishi ametumia katika riwaya hii. Mchanganyo ndimu ni ile hali mtu kuongea kwa kutumia lugha zaidi ya mbili. - Mfano. (Uk. 41) â œmimi â naturalistâ. LUGHA ZA MATUSI Ni Mbinu nyingine ilizotumiwa na mwandishi katika riwaya hii ni lugha za matusi kwa mfano. - â œwashenzini ninyiâ.(uk.12). - â œkumbe bado washenziâ (uk.50). - â œyule mshenzi amekwendaâ (uk.93) - â œnimemfukuza mbwa tumaini (uk.109). - â œkwanza wewe bwege. (uk.121). -â œâ. Alidakia na kusema unyokonyoko (uk.122). TAMATHALI ZA SEMI Ni maneno yanayotumiwa yanayotumiwa na wasanii Ili kutia nguvu katika kazi hiyo. Hivyo tamathali za semi zinazotumika katika riwaya hii ni pamoja na : TASHIBIHA/MSHABAHA Ni maneno ambayo hutumia kulinganisha kitu na kitu na kitu kingine kwa kutumia maneno kama vile â œmithili, sawa, kamaâ mfano:- - â œmiaka ni kama kunguniâ (uk.6). - â œbaba yako atakuwa mkali kama sambaâ (uk.6). - â œmapenzi ni kama mpunga mototo wanguâ (uk.14). - â œlakini mimi ninaumwa ninaumwa kama panya.â (uk.17). - â œsi tutakufa kama mbwaâ. (uk.19). - â œkukaa kama watakatifuâ. (uk.19.) - â œaliyekunyata nyumbani kwake kwa uoga kama panya aliyesikia mlio wa pakaâ. (uk.130). SITIARI Ni tamathali za semi ambazo ulinganisha vitu vizuri kwa kutumia viunganishi au linganishi.mfano â œniâ :- - â œwatoto wote yatima ni watoto wanguâ. (uk.15). - â œhuyo ni

baba yakoâ (uk.12). - â œujamaa ni mzuriâ. (uk.112). Takriri ni tamathali za semi ambayo neon hujirudiarudia kwa lengo la kusisitiza jambo Fulani. Takriri ni matumizi ya lugha ambayo msanii ametumia katika riwaya hii, mfano wa takriri:- - â œmauti, mautiâ. (uk.17). - â œhe! Hee! Hee!â (uk.18) - â œkasala, kasala, ngoja nije!â (uk.22) - â œyuhu! Yuhu!â (uk.27) - â œhaa! Haa! Haa! (uk.42) - â œmsiue, msiue!â (uk.44) TASHIHISI Ni tamathali za semi ambazo vitu ambavyo si viumbe hai hupewa hadhi ya kutenda kama binadamu. Mfano:- - â œmwezi uliona nyota ziliona hata jua liliona.â (uk.12) - â œtumaini alisikia sauti kama ya ndege akiimba kwa huzuni.â (uk.19) - â œkila jiwe walilokalia liliwaambia â œsamahani umekalia bega languâ. (uk.32) TANAKALI SAUTI Ni tamathali ya semi ambayo uigaji wa sauti za asili. Mfano Katika riwaya hii tanakari sauti alizotumia msanii ni kama ifuatavyo:- â œboooouuu! (uk.130) TAFSIDA Ni tamathali za semi ambazo kwazo matumizi zake ni za adabu. Mfano : â œkazi kutembeza kengele zako kwenye mabaa.â Uk.121. - â œtumaini alikuwa akishika mahali pabayaâ. Uk.53. METHALI Usemi wa kisanii wa kimapokea unaofikiriwa na jamii kuwa kweli na unaotumiwa kufumbia au kutolea mifano na huwa unabeba maana pana kuliko maneno yenyewe yanayotumiwa. Kwa mfano:- - â œwema wa mtu hujulikana siku ya mazishi yake.â (Uk.13) - â œugonjwa haufichwi. Afichae ugonjwa ndio hufa.â (Uk.29) - â œkweli wajinga ndio waalimu wa kuwafunza welevu. (uk.78) - â œukishikwa shikamana.â (Uk.102) MISEMO Ni mafungu ya maneno yanayotumiwa na jamii ya watu wa lugha hiyo kwa namna maalumu ili kutoa mafunzo, maadili na kuihadharisha jamii. Misemo ni maneno ambayo jamii huyatumia kutokana na uzoefu katika maisha. Kwa mfano: - â œponda mali kifo chaja.â (Uk.10) - â œulimwengu hauna mwema.â (Uk.103) - â œmapenzi yao sasa yalikuwa yamekwisha pata kovuâ. (Uk.108) - â œnilitaka uniondoe kwenye mdomo wa samba.â (Uk.24) NAHAU Haya ni mafungu ya maneno yenye maana maalumu ambayo haitokani na maneno ya kawaida yaliyopo kwenye maneno hayo. Nahau za lugha yoyote hutumiwa zaidi na jamii yenye asili ya lugha hiyo. Kwa mfano:- - â œamezunguka mbuyu - amekula rushwaâ. (uk.25 - â œunamvika kilemba cha ukokoâ. (Uk.71) Tanakali sauti - â œbooouuu!â MJALIZO Katika tamathali hii sentensi huwa ni mfuatano tu wa maneno yasiyo na viungo vyovyote. Mfano:- - â œwenye mashoka! wenye mikuki na miundu! Wenye pinde na wenye mapanga walianza kulifyeka lile chakaâ. (Uk.27) WAHUSIKA Wahusika ni watu au viumbe waliokusudiwa wawakilishe tabia za watu katika kazi za fasihi. Wahusika wa fasihi ni wa aina kuu tatu,wahusika kazi ya fasihi wanaweza kuwa wahusika wakuu, wahusika wadigo, na ewahusika wajenzi.wahusika huonyesha dhana mbili muhimu katika maisha ya watu yaani wema na mabaya pia wahusika humaanisha tabia maalumu iliyokusudiwa na jamii. Katika riwaya ya â œdunia uwanja Fujoâ wahusika wake ni mhusika mkuu, whusika wadogo, na wahusika wajenzi kama alivyoainisha Catherine Ndugo (1991) na Wangali Mwai(1991).ika riwaya hii mwandishi ametumia wahusika wa aina tatu kwa kutumia kigezo cha Catherine na Wangeri Mwai(1991) Kama wahusika wakuu, wadogo, na wajenzi kama ifuatavyo:- MHUSIKA MKUU Mhusika mkuu; huyu ni yule anejitokeza kila mara katika kazi za fasihi tangu mwanzo hadi mwisho. Maudhui ya kazi ya fasihi huwa yanamzungukia na hata kutolewa na mhusika mkuu zaidi ya wahusika wengine. TUMAINI Huyu Ndio mhusika mkuu katika riwaya hii kwani maudhui na dhamira zimejengwa juu yake. Pia tunaona wahusika wajenzi akina John, Anastazia, Dc, na mgeni kutoka Dar es saalam dhamira wanazozitenda zinamgusia mhusika mkuu ambaye ni Tumaini. Jina Tumaini ni jina ambalo

amepewa na mzazi wake mzee Kapinga ambaye alikuwa mwalimu. Jina Tumaini linasadifu matumaini ya wazazi wake, pia alikuwa ni mototo pekee wa kiume katika familia ya mwalimu Kapinga pia walikuwa na matumaini pindi atakapomaliza shule ndio atakuwa msaada wao katika familia na pindi watakapokuwa wazeeka.mambo hayo yanapatikana katika (uk.11). inasema â œâ Naam Tumaini alikuwa motto wa watu hawa. Tumaini kama jina lenyewe lionyeshavyo alikukuwa peke yake katika tumbo la mama yakeâ..â WASIFU WA TUMAINI - Alikuwa ni motto wa Kapinga. (uk.9) - Alikuwa Malaya (uk.8, 24) - Alikuwa mlevi (uk.94) - Mchapa kazi (uk. 114) - Mtumia Pesa vibaya (uk. 55) - Alikuwa muuaji. (uk.128) - Alikuwa na mapenzi ya dhati kwa mkewe (uk.128) Alikuwa na matusi (uk. 12) WAHUSIKA WADOGO WADOGO Hawa ni wahusika ambao hawajitokezi mara kwa mara katika kazi ya fasihi ndio ambao husimamia dhamira ndogo ndogo Katika riwaya hii ya â œdunia uwanja wa fujoâ wahusika wadogo wadogo waliojitokeza ni kama ifuatavyo:- 1. KAPINGA. SIFA ZA KAPINGA - Baba yake na Tumini. (uk.9) - Alikuwa mwalimu. (uk.9) - Alikuwa na malezi mabaya kwa mwanae. (uk.12) - Alikuwa ni Mume wa miango. (uk.9) - Alikuwa ni mbinafsi. (uk.15) - Alikuwa hapendi kushilikiana katika jamii. (uk. 12). 2. KASALA SIFA ZA KASALA - Ni mwanakijiji wa Bugolola. (uk. 1). - Mtoto wa Mugala. (uk. 2). - Baba yake na Misana. (uk. 2). - Mume wake na Mugele. (uk. 2). - Mtu mwema. (uk. 4). - Kiasi Fulani alikuwa ni mvivu.(uk.6) 3. MUNGERE SIFA ZA MUNGERE;- - Mke wa Kasala (uk.2). - Mama yake na Misana (uk.2). - Mwanakijiji wa Bugolola (uk.2). - Mtu mwema na mchapa kazi. (uk. 4). 4. MISANA. SIFA MISANA;- - Mtoto wa Kasala (uk.2). - Alikuwa mtundu. (uk.3). - Mtoto wa Mungere (uk.2). - Mdogo wao na akina Dennis, Leonila, Aulelia. (Uk.5). 5. MUGALA - mwananchi wa Bugolola. Uk.3 - Mchawi. Uk.3 na 7. - Ni mama yake na Kasala. uk.2 - Ni mjane uk.4. - Mtu mwenye hasila uk.22 - Alikuwa na malezi mabaya kwa wajukuu zake uk.19 6. LEONILA - Alikuwa dada yake Dennis na Misana. - Alikuwa ni motto wa Kasala Mungere. - Alikuwa ni mpenzi wa Tumaini uk. 8 na 24. 6. BENADETA - Mke wa pili wa Dennis uk. 121 - Mtu mwenye chuki uk. 120 - Alikuwa na dharau na mwenye matusi. uk 121 7. CHRISTINA - Alikuwa kahaba. Uk.96 - Alikuwa mlevi uk.94 - Alikuwa mlagai uk.95 - Hana mapenzi ya dhati uk.96 - Alikuwa anapenda sana pesa. Uk. 94 8. MAKOROBOI - Alikuwa jambazi uk.96 - Alikuwa mkatil na mwenye kisasi uk.96 - Anapenda pesa. Uk.96 WAHUSIKA WAJENZI Ni wahusika ambao maudhui yao na dhamira wanazozitenda zinamsaidia mhusika mkuu katika dhamira azitendazo. Mara nyingi wahusika wajenzi wanakazi ya kunjenga au kumsaidia mhusika mkuu katika dhamira zake. Katika riwaya hii wahusika wajenzi ni kama ifuatavyo: 1. JOHN JOHN Ni mhusika mjenzi kwani dhamira alizobeba na nafasi alizotumiwa na mwandishi ni kwa lengo la kumjenga mhusika mkuu tumaini. Pia tunaona John na Tumaini walikuwa na mahusiano na ushirikiano tangu wakiwa kijijini Bugolola mpaka waliposafiri kuelekea mjini Shinyanga. -Alikuwa mlevi uk.62 -Alikuwa Malaya uk.62 na 66. -Alikuwa mvivu uk. -Ana mapenzi ya dhati uk.97 2. ANASTAZIA Anastazia pia huyu ni mhusika mjenzi kwani alikubali kuambatana na Tumaini kijijini kwenda Mwanza halafu mjini Arusha. Pia uhusiano wao ulidumu na kupelekea kuoana na Tumaini. WASIFU WA ANASTAZIA NI KAMA IFUATAVYO:- - Alikuwa na mapenzi ya dhati. Uk.57, 97, & 99. - Alikuwa mke wa Tumaini. Uk. 61 - Mtu mwenye huruma uk.99 - Mtu mvumilivu. Uk.89 3. DENNIS Ni mmoja wapo wa wahusika wajenzi kwani ndio anaemjenga mhusika Tumaini kwa

kiasi kikubwa akiwa mjini Shinyanga. Pia TUMAINI ALIKUWA NA SIFA ZIFUATAZO -Ni mtu mwenye mapenzi ya dhati. Uk.59 -Alikuwa ni mototo wa Kasala. Uk 3 - Alikuwa ni mtumishi wa serikalini MAUDHUI katika kazi ya fasihi ni jumla ya mawazo yote yanayozungumzwa pamoja na mtazamo wa mwandishi juu ya mawazo hayo. Maudhui hujumuisha mawazo pamoja na mafunzo mbalimbali yaliyomsukuma msanii hadi akatunga na kusanii kazi fulani ya kifasihi. Vipengele vya maudhui ni pamoja na dhamira, migogoro, falsafa ujumbe na msimamo. Katika riwaya hii Dunia uwanja wa fujo mwandishi amejitahidi kwa kiasi kikubwa kuonyesha maudhi mbalimbali katika kazi yake kupitia vipengel;e mbalimbali kama vile Dhamira, migogoro, ujumbe, falsafa, mtazamo itikadi hii yote ni kwa lengo kuu la la kuelimisha jamii kuhusu mambo mbalimbali yanayotukia katika jamii hiyo. Dhamira; hili ni wazo kuu au mawazo mbalimbali yanayojitokeza katika kazi ya fasihi. Senkoro anataadharisha maana hii isichanganywe na maudhui kwani dhamira ni sehemu tu ya maudhui na aghalabu dhamira kuu ndio hujenga kiini cha kazi ya fasihi. Dhamira zimegawanyika katika makundi mawili, kuna dhamira kuu na dhamira ndogondogo. Dhamira kuu ni wazo kuu linalojitokeza katika kazi ya fasihi, dhamira kuu katika riwaya hii ni matatizo na mikinzano ya kijamii, kiuchumi, na kisiasa, sasa tuangalie ni kwa jinsi gani mwandishi ameijadili dhamira hii; Matatizo na mikinzano ya kijamii, kiuchumi, na kisiasa, Katika riwaya hii â œdunia uwanja wa fujoâ kwa kiasi kikubwa riwaya hii imejikita katika dhamira hii ambapo ameonyesha matatizo na mikinzano kiuchumi na kijamii ambayo jamii ya kitanzania iliyoandikiwa hukabiliwa nayo. Ili kuijenga dhamira hii mwandishi amewatumia wahusika kama vile Tumaini, John,Anastazia, Kapinga, Dennis ili kuiunda dhamira yake kuu katika riwaya hii. Tukianza na Tumaini mwandishi amemuonyesha kuwa ni mhusika ambaye anapinga sera za kijamaa ya siasa ya ujamaa iliyoanzishwa na serikari nchi nzima hali hiyo inaleta ukinzani kwa tabaka lenye mali kwani hawakuwa tayari kuachia mali zao kwa umma. Hali hii inadhihilisha pale Tumaini alipoamua kupingana na hali hiyo ya kunyanganywa mali zake na kupelekea kumuua mkuu wa wilaya, ambaye alikuwa ndio kiongozi mkuu katika mkoa Shinyanga katika shughuli za kusimamia sera hiyo ya ujamaa'.(uk.127) Hali hiyo ni mfano tosha kudhihilisha kuwa dhamira kuu katika riwaya hii ni'matatizo na mikinzano ya kijamii, kiuchumi, na kisiasa. Dhamira ndogo ndogo.haya ni mawazo yanayojitokeza ili kujenga dhamira kuu. Dhamira ndogondogo zinazojitokeza katika riwaya hii ni; MAPENZI NA NDOA. Mwandishi E. Kezilahabi amejadili suala la mapenzi na ndoa katika pande mbili tofauti, kwanza ameonesha mapenzi ya dhati na mapenzi ya ulaghai lakini pia ameonesha ndoa za dhati na ndoa za ulaghai. tukianza na mapenzi ya dhati, mapenzi ya dhati yanajitokeza kwa: a) MAPENZI YA DHATI KWA TUMAINI NA MKEWE ANASTAZIA Mwandishi ameonesha mapenzi ya dhati aliyokuwa nayo Tumaini kwa mke wake, Mwandishi anathibisha hili pale anapoamua kutoroka na Anstazia na kuelekea mjini Shinyanga ambako walianza maisha mapya pia tunaona jinsi gani wawili hawa walivyojaliana hata katika kipindi cha matatizo. Mfano Anastazia alionyesha mapenzi ya kweli pale alipompelekea Tumaini chakula na kumfaliji kuwa atapona, pindi Tumaini alipopigwa na akina makoloboi. Uk.97 Mapenzi ya dhati aliyokuwa nayo kwa mke wake pia yanajidhihirisha pindi mke wake huyo alipokubali kuishi na Tumaini japo alikuwa ni mhuni na mlevi pia ha baada ya Tumaini kupigwa na kualibiwa sura Anastazia alindelea kuafiki kuishi na na Mumewe Tumini, hii ni kwa kuwa alikuwa akimpenda. Mwandishi anathibitisha hili katika. [Uk 64] 2. Ulevi. Mwandishi E, Kezilahabi hakuwa nyuma kujadili suala la ulevi na athari zake kwa binadamu na jamii kwa ujumla, katika riwaya yake hii amemtumia muhusika Tumaini pamoja na John kuelezea dhamira hii. Tukianza na Tumaini, mwandishi anamwonesha Tumaini akianza tabia ya ulevi wa

pombe kali baada ya kufiwa na wazazi wake kijijini Bugololola hata alipoamia mkoani Shinyanga aliendelea na tabia hiyo ya ulevi wa pombe, Mwandishi hakuishia hapo tu bali ameonesha na athari za tabia hiyo ya ulevi kama vile kupelekea kufilisika kwa tumaini kama mwandishi anavyothibitisha (Uk 94 &95) 3. MALEZI KWA WATOTO. Hii ni dhamira nyingine inayojitokeza katika riwaya hii, Mwandishi amemtumia muhusika Tumaini kuilezea dhamira hii, tunamwona Tumaini akipata malezi mabaya kutoka kwa wazazi wake kitu kilichopelekea kuyahalibu maisha ya Tumaini na kumfanya aache shule, awe mlevi, pamija na mengine mengi. Mfano Siku moja Tumaini alimchoma mlezi wake jichoni. Yule kijana alimpiga Tumaini kidogo, Tumaini alikimbia kwenda kushtaki kwa mama yake. â œmama Mpishi amenipiga!â Kwa nini umempiga mtoto wangu!â Mugaya alifoka.â Hali hii inaeleza jinsi Tumaini alivyo lelewa vibaya na kudekezwa na wazazi wake; uk 11 USHIRIKINA NA UCHAWI Ni hali ya kuamini nguvu za giza, ni jambo ambalo lina sababisha jamii nyingi kugawanyika na kukosa amani. Kwani mwandishi anadhihirisha hili anaposema; â œvizuu walilia kwa sauti ya kutisha : yuhu!yuu! huba!â uk. 30. â œtena alikuwa akilala ndani ya nyumba yako! Ndio maana mama yako alikuwa mchawiâ uk. 36. Suala la ushirikina katika jamii inayotuzunguka ni janga ambalo kila siku linahatarisha maisha ya watu hususani wazee wenye macho mekundu wako hatiani kupoteza maisha yao katika baadhi ya maeneo mfano mkoa wa Shinyanga na Simiu,hivyo dhamira hii haijapitwa na wakati. UNAFIKI. Hii ni dhamira pia inayojitokeza katika riwaya hii, katika kuijadili dhamira hii Mwandishi amemtumia mke wa Dennis kama mtu mnafiki kwani alijifanya anampenda mmewe kumbe alikuwa na uhusia mwamume mwingine ambaye ni John rafiki y yake na Dennis. Mwandishi anadhihilisha hali hiyo akionyesha katika kitabu chake kwamba; â œheshima yangu imekwishapotea John ukiniacha hivihivi nitaona aibu sana!â uk72. Tukigeukia katika uhalisia, tabia hii ya unafiki imeshamiri katika jamii zetu, unaweza ukawa na rafiki au ndugu ambaye akawa mnafiki kwako. Jamii inatakiwa kuondokana na tabia hii kwa haifai kabisa. NAFASI YA MWANAMKE. Katika riwaya hii mwanamke amechorwa katika pande mbili, amechorwa katika upande hasi lakini pia mwanamke amechorwa katika upande chanya, upande hasi mwanamke amechorwa kama kiumbe duni na dhaifu wakati katika upande chanya amechorwa kama mtu jasiri, mchapa kazi, mwenye upendo. n.k. Sasa hebu tuangalie nafasi ya mwanamke katika jamii kama alivyochorwa katika riwaya hii tukianza na upande hasi; Katika riwaya hii mwanamke amechorwa kama kiumbe duni, dhaifu, katika nafasi mwanamke amechorwa kama; A) CHOMBO CHA STAREHE. Mwandishi amemchora mwanamke kama chombo cha starehe anayeweza kutumiwa kuwastarehesha wanaume ili mradi kufurahisha nafsi zao, hili linathibitishwa na Mwandishi katika riwaya hii akimtumia muhusika Christina kama chombo cha starehe, ambaye alionekana kujirahisishwa kwa wanaume ili mladi apate fedha. Mfano;uk 95 & 96. â œsijaona mwanaume mwoga kama wewe! Kristina alisema. Tumaini alilala kitandani. Kristina alizima taaâ uk.96 Hata katika jamii yetu inayotuzunguka wanawake kwa kujijua au kutojua wamekuwa wakifanywa kama chombo cha starehe kuwastarehesha wanaume, jamii inatakiwa kubadilika na kuondokana na dhana hii kwani mwanamke pia anastahiri heshima katika jamii. B) MTU ASIYE NA MAAMUZI KATIKA JAMII Mwandishi amemchora mwanamke kama mtu asiye na maamuzi katika jamii yake, kwa mfano anamtumia muhusika ambaye alikuwa nini mama yake Tumaini kushindwa kufanya maamuzi juu mali alizoziacha kama urithi wa Tumaini japo hakupenda kumuachia mtoto wao fedha nyingi(alijua zitamuangamiza mwanae) lakini alishindwa kubatilisha kutokana na maamuzi yaliyoachwa na

mumewe.mfano anaonyesha; â œni vizuri zaidi mtoto kurithi vitu kama hivyo, licha ya hekima na kumrithisha mototo pesa ni ni kunvisha taji la uovu.â Baba yako alikataa kabisa; na kwa kuwa nilishindwa mawazo ya baba yako alipokuwa bado mzima, siwezi sasa kugeuza tamshi lake.â uk15 Hata katika jamii yetu, inawachukulia wanawake kama watu wasio na maamuzi katika familia na pindi inapotokea kufiwa na waume zao huwa wanapata shida na manyanyaso kutoka kwa ndugu wa mwanaume kama vile kufukuzwa kwenye nyumba, kunyang'anywa watoto na mali nyingine alizoshirikiana kuzichuma na mumewe. jamii inatakiwa kumpa nafasi mwanamke na itambue kuwa ana haki sawa kama mwanaume. MWANAMKE AMECHORWA KAMA MSALITI. Hii ni nafasi nyingine ambayo mwandishi amemchora mwanamke, kwa mfano tunaona mke wa Dennis kama mtu mnafiki kwani alijifanya anampenda mmewe kumbe alikuwa na uhusia mwamume mwingine ambaye ni John rafiki y yake na Dennis. Mwandishi anadhihilisha hali hiyo akionyesha katika kitabu chake kwamba; â œheshima yangu imekwishapotea John ukiniacha hivihivi nitaona aibu sana!â uk72. Migogoro ni mivutano na misuguano mbalimbali katika kazi za fasihi. Migogoro inaweza kuwa kati ya wahusika, familia zao, matabaka yao, au hata katika nyadhifa mbalimbali. Vilevile migogoro yaweza kuwa ya kiuchumi, kijamii, mogogoro ya nafsi, na migogoro ya kisiasa ambayo hujitokeza katika mitazamo tofauti kulingana na mtiririko wa visa na matukio yanavyopangwa na mwandishi. Kwa kuanza Mgogoro wa nafsi tunamuona Tumaini akipatwa mgogo nafsi pindi alipofiwa na wazazi wake na baadae kug unduli kuwa walikuwa wamechuliwa ka vizuu na bibi ake na Leonila pia mgogoro nafsi wa pili ni pale ambapo leonila ankataliwa kuolewa na Tumaini anajikuta akiingia katika lindi la mgogoro nafsi. Pia Leonila anjikuta akiingia katika mgogo wa nafsi pindi pindi wazazi wake walipomwandalia mazingila ya kuolewa na tembo uk.15 &39 Mgogoro kati ya mtu na mtu; Hapa tunaona mgogoro kati ya Anastazia pamoja na wazazi wake, Dennis na John, Dennis na Benadeta, Tumaini na Serikali,Kasala na mama yake.mfano. uk.22,23,&128. -â œkumtunza mzee ni mzigo lakini inabibi uuchukue kwa fulahaâ uk.23 -â œbaba nihurumie! Lakini Kasala aliendelea kumpiga. Bibi wameniua kwa sababu yako!â uk.22. UJUMBE/MAFUNZO Ujumbe; mwandishi anapoandika kazi yake huwa na ujumbe ambao hutaka uifikie jamii aliyoikusudia. Ujumbe katika kazi fasihi ni mafunzo mbalimbali ambayo hupatikana baada ya kusoma kazi ya fasihi. Katika kazi ya fasihi dhamira kuu hubeba ujumbe wa msingi na dhamira ndogondogo hubeba ujumbe ambao husaidia kuujenga au kuupa uzito zaidi ujumbe wa msingi. Baadhi ya ujumbe unaopatikana katika riwaya hii ni pamoja na;- Kikulacho kinguoni mwako, Huu ni ujumbe ama funzo tunalolipata baada ya kusoma riwaya hii, ujumbe huu tunaupata kupitia muhusika mama Resi pindi kwani alijifanya anampenda mmewe kumbe alikuwa na uhusia mwamume mwingine ambaye ni John rafiki yyake na Dennis.uk.72 Majuto ni mjukuu, Ujumbe huu unajitokeza pia katika riwaya hii, mwandishi anamtumia muhusika Tumaini pale alipoendekeza starehe zilimsababisha aingie kwenye mtego wa majambazi wa kupigwa na kuhalibiwa sura yake. uk.98 Elimu ni ufunguo wa maisha, Mwandishi anatupa ujumbe mwingine kuwa, ili mtu aweze kufanikiwa hana budi kushikiria na kuizingatia elimu kwani elimu ni ufunguo wa maisha, ujumbe huu katika riwaya hii unajitokeza kwa muhusika Dennis ambaye alipata kazi nzuri sababu alikuwa amekwenda shule na kupata elimu ya kutosha. â œnyumba ya Dennis ilikuwa ni kubwa sana. Ilikuwa na vyumba saba bila kuhesabu jiko lililokuwa mumo humo ndaniâ uk.60 Mpende akupendaye asiyekupenda achana nae, katika riwaya hii anaipa ujumbe jamii yake kuwa penda pale unapopendwa na si kumng'ang'ania tu mtu kwa kuwa moyo wako unataka tu kuwa naye, ujumbe huu tunaupata kupitia kwa muhusika Denni alipogundua kuwa mke wake alikuwa na mapenzi ya uongo aliamua kuachana nae.

â œdennis alipofika nyumbani alipiga kerere nimemfukuza mbwa,tumainiâ uk.109 MSIMAMO Msimamo; katika kazi ya fasihi, mawazo, mafunzo na falsafa ya msanii hubainisha msimamo wake kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii. Msimamo ni ile hali ya mwandishi kuamua kufuata na kushikilia jambo fulani. Jambo hili huweza kukataliwa na wengi lakini akalishikilia tu. Msimamo ndio huweza kuwatofautisha wasanii wawili au zaidi wanaoandika kuhusu mazingira yanayofanana. Hivyo basi mwandishi anamsimamo kwamba mambo yote yanayotendeka katika ulingu huu ni sasawa na fujo tupu, kwani hata kama utajitahidi vipi kupambana na shida za ulimwengu huu matatizo yataendelea kukukabili mpaka umauti utakapokufikia. Jina na jalada la kitabu, Tukianza na jina la kitabu, jina la kitabu ni â œdunia uwanja wa fujoâ linasadifu yale yaliyomo ndani ya kitabu kwani tangu mwanzo wa riwaya hii kuna matukio au fujo mbalimbali ambazo zimejitokeza fujo hizo ni kama vile umalaya, ulevi, uchawi pamoja na mengineyo mengi. Mfano suala la uchawi lidhihilika pale katika uk.36 unasema â œtena alikuwa akilala ndani ya nyumba yako! Ndio maana mama yako alikuwa mchawiâ uk. 36. FALSAFA YA MWANDISHI. Kulingana na Mbunda Msokile yeye anasema kuwa Falsafa ni wazo ambalo mtu anaamimini lina ukweli Fulani unaotawala maisha yake pamoja na maisha ya jamii. Hivyo basi katika riwaya hii anaamini kuwa katika riwaya yake ya â œdunia ni uwanja wa fujoâ Kwamba maisha hayana raha wala maana isipokuwa dunia ni uwanja wa fuzo. KUFAULU KWA MWANDISHI Mwandishi wa riwaya hii amefaru kwa kiasi kikubwa kuibua dhamira dhamira mbalimbali katika jamii. Kwani dhamira hizo zimeonekana kuwa ni kikingamizi kikubwa cha katika maendeleo ya jamii. Mfano suala la uchawi na ushilikina, malezi mabaya, ukale na usasa. Pia mwandishi amefaulu katika suala zima la lugha kwani ametumia lugha lahisi na inayoeleweka kwa msomaji yeyote hata kama si msomi mkubwa.