Deutsche Welle, Learning by Ear 2009 Seite 1 People Who Make A Difference Liberia: Anita Varney Health Facilitator, Fishtown/Liberia

Similar documents
Information for assessors (do not distribute this page to participants):

Human Rights Are Universal And Yet...

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

LBE 2009 Migration Episode 3: Living without documents

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti

usudi la Maisha Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na kupishana usiku na mchana, kuna kweli ishara kwa wenye akili, ambaye mkumbuke-

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

Pronunciation: Mä-hret Zäläke Ndal-ka-tscho Molla Mare Gebre-gzabiär 1/12

Utangulizi wa ugonjwa wa shinikizo la damu

Ushindi ndani ya Kristo W. W. PRESCOTT

Ufunguo wa Kutaalamika Haraka

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level

Yaliyomo. Kuhusu kitabu hiki. Hautakuwa peke yako. Mfumo wa msaada ni wa manufaa sana wazazi wote wanahitaji!

MACHAGUO YA UZAZI KUFIKIRIA KUWA MZAZI

Kuwa na Ukimwi ni kama vile kutakiwa kuendelea kuuzima moto unaoniunguza bila kukoma.

Adhabu ya jino kwa jino na Musitakabali wa imani zetu

Vijana wanazungumza kuhusu ujinsia, maisha na uhusiano VIJANA WANAZUNGUMZA KUHUSU NGONO, MAISHA NA UHUSIANO. Training and Research Support Centre

Kiu Cha umtafuta Mungu

Mutugi Kamundi. Jemma Kahn. Kiswahili. Demane na pacha wake. Author - South African Folktale

United Pentecostal Church June 2017

Hatari, Haki za Usalama katika Bahari 03

TIST HABARI MOTO MOTO MAANDALIZI YA MWAKA 2000 Y2K PREPARATIONS SASA NI WAKATI WA KUANZA KUPANDA MBEGU ZAKO

Mwongozo wa Utamaduni Toleo la Kwanza

Ellen White, waasisi wa Kiadventista,na Sabato Lunar

WEWE NI NANI? Toleo X Toleo Ukweli wa Injeli Toleo 23

Wewe Maisha Yako Ndoto Zako. Kitabu cha Vijana Balehe

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

International Labour Office. Kazi za Ndani Zenye Madhara kwa Watoto: Kijitabu cha Maelezo Mafupi

Kuiponya Picha Tuliyonayo Kuhusu Mungu

Jamii. ,,,^mm^mmm-<^^^^ illli MA RH-EREN.CE CENTRE

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees

walozaliwa, si kwa damu, wala mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, mbali kwa Mungu. Sisi sio tena binadamu wa kawaida tu kwa sababu sisi ni w

wasiofaa. Naomba sana kila raia afanye bidii awezavyo kumkaribia Mwenyezi Mungu vile anavyoona inafaa, lakini asipitishe hukumu juu ya wengine.

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

JE! MUNGU ANAMPA MWANAMKE HAKI YA KUTOA MIMBA IWAPO NI MHANGA WA UBAKAJI?

KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA

K. M a r k s, F. E n g e l s

2

Kuwawezesha wasichana kwa kuboresha kujikubali na kujithamini Hivi Ndivyo Nilivyo

# 18 Uponyaji Kutokana na Kukataliwa

IM ETUPASA KUTIMIZA HA KI YOTE

TIST HABARI MOTO MOTO

Haja Ya Dini. Author(s): Publisher(s): Translator(s): Category: Topic Tags: Featured Category: Published on Al-Islam.org (

PDF created with pdffactory trial version

Ndugu na dada zangu wapendwa,

Roho Mtakatifu Ni Nini?

Elimukombozi, Lugha na Upashanaji Habari nchini Tanzania, katika Muktadha wa Utandawazi

Usimulizi wa Riwaya ya Nyongo Mkalia Ini E. S. MOHOCHI University of Egerton, Kenya

Kuzimu na Kurudi na Dr. Rawlings Documentary Video Transcript, TBN Films

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) VERBATIM REPORT OF

KUPWA NA KUJAA KWA BAHARI. (TIDES AND TIME)

Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI Nchini Tanzania

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

Kocha Mkuu. mabingwa. itakuwa INASTAHILI. Ili Kutoa mafunzo kwa wanafunzi wako kuwa. itakuwa ya kuumiza. Itachukua muda. Itahitaji moyo wa kujitoa.

SautiElimu. Sauti Yako Isikike

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI-TAMISEMI HALMASHAURI YA WILAYA BUMBULI

UMRI WA MAKAMO NA KUKOMA KWA HEDHI

Kiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2012

Siku ya kwanza. Mguso wa ngozi-kwa-ngozi (Ulezi wa kangaruu) Mtoto wako anaweza kuhisi mdundo wa moyo wako

JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1

"ATATOKEA MARA YA PILI, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu." Waebrania 9:28.

United Pentecostal Church April Kushangilia Kwa Sala

Kijitabu cha Maelezo cha Programu ya Famasia

Kitabu Cha Mafunzo Ya Uongozi Kwa Wanawake

Mwabudu Yehova, Mfalme wa Umilele. Miaka 100 ya Utawala wa Ufalme Inakuhusuje? UKURASA WA 12 NYIMBO: 97, 101. Kufanya Maamuzi ya Hekima Ukiwa Kijana

Na Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake Toleola4

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA,KWA WANANCHI, 30 SEPTEMBA, 2001

YEHOVA-YIRE 1. 2 Baba yetu wa Mbinguni, tunakikaribia Kiti Chako cha. 3 Tunakushukuru kwa kutuzuru jana jioni. Tunaomba

Mafundisho Ya Msingi Wa Kikristo. Na Andrew Connally

Mwongozo wa Familia wa Kujifunza

MUNGU ALIUMBA ULIMWENGU 1 WETU NA VYOTE VILIVYO HAI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA

AMMA KWA AFRIKA RATIBA/ITIKADI. Ratiba Maalum ya Kutibu Magonjwa Maambukizi na Hususan Fikra Zinazoleta Pooza Mwili na Akili

Kifo Na Mbingu. (Death And Heaven) Ellis P. Forsman. Kifo Na Mbingu (Death And Heaven) 1

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC)

JAZANDA YA NJOZI KATIKA BAADHI YA MASHAIRI YA EUPHRASE KEZILAHABI (ONEIRIC IMAGES IN EUPHRASE KEZILAHABI S SELECTED POEMS) 1

Mukhtasari Wa Mabishano Kwa Na Dhidi Ya Vikombe Vingi Vya Ushirika

Tora UTANGULIZI KWA TORA SOMO LA KWANZA

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

UFAHAMU NAME INDEX SCHOOLDATE UFAHAMU

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC)

MASWALI NA MAJIBU JUU YA KITABU CHA MWANZO

Kufunga Milango - Uponyaji Kutokana na Athari za Giza

Uongozi Siri Na Larry Chkoreff. Version 1.2 Desemba 2010

Oktoba-Desemba

KANISA NA UAMSHO Na Mchg. Dkt. Faith Lugazia

TAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF) KUHUSU HAKI ZA WATOTO KATIKA KATIBA MPYA

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

KUWEZESHA MBINU ZA UZUIAJI MIMBA KATIKA SUHULA ZA AFYA: MASWALI 10 KWA VIKUNDI VYA JAMII KUZINGATIA

Ufundishaji wa lugha nyingine

IMANI NA MATENDO ELLEN G. WHITE

2

Uponyaji Wa Laana. (Kumb. 28:1-14).

MWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI

BIBLICAL INSTRUCTION AND ENCOURAGEMENT FOR THE MAFUNDISHO YA BIBLIA NA HIMIZO KWA MISSION FIELD WORLDWIDE. KAZI YA KIMISHENI ULIMWENGUNI KOTE

ORODHA YA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI SPIKA MHE. PANDU AMEIR KIFICHO. Rais.

Transcription:

Deutsche Welle, Learning by Ear 2009 Seite 1 Title: Anita Varney Health Facilitator, Fishtown/Liberia Author: Stefanie Duckstein, HA Afrika/ Nahost Editor: Christine Harjes Translator: Tony Dunham Sound Clips in DALET: Learning by Ear: LbE_PEO_Liberia_Varney Characters Narrator: Male voice Voice Over: Anita Varney, 36 INTRO Hujambo na karibu kwenye makala ya Noa Bongo Jenga Maisha Yako juu ya Watu Wanaoleta Maendeleo katika jamii. Leo hii tunakutana na Anita. Yeye ni muhudumu wa afya katika eneo la kijijini kwenye nchi moja ya Afrika Magharibi. Kwa hivyo tunakwenda moja kwa moja hadi mji mdogo wa Fishtown, nchini Liberia. 1. SFX: Women s Workshop Ab: 0:48: Anita: kina mama oh kina mama. (Clapping hands) Umeme, Umeme. Ni maambukizi ya ugonjwa wa zinaa. Gonorrhoea. All: Gonorrhoea. Anita: Syphilis. All: Syphilis Anita: Mnamalizia wenyewe Vizuri! Mchana wa leo wanaburudika juu ya kilima kimoja kati ya vilima vitatu vinavyounganisha kijiji cha Fishtown. Majina ya magonjwa ya kuambukiza kutokana na ngono yanatajwa mle ndani ya chumba huku sauti hizo zikisika hadi nje uwanjani. Anita hatulii mguu mmoja huku mwingine kule, na anajaribu licha ya joto kali kuwatuliza wanawake wale 30 ili wamsikilize.

Deutsche Welle, Learning by Ear 2009 Seite 2 2. SFX: Women s Workshop Anita anaashiria kwa kidole chake, picha za sehemu za siri zilizoathirika. Wanawake wanajisogezasogeza kwenye viti vyao huku wakiguna kwa sauti za chini. Mada ya warsha ya leo ni magonjwa ya zinaa. Sio mada ya kupendeza sana, kwa mujibu wa Anita Kwa hivyo usipowachangamsha, watachoka. 3. SFX: Women s Workshop Anita Yawasese Varney, urefu wake ni kama mita moja na sentimita themanini hivi, ni mrefu kuliko wanawake wote hapo. Hata mwili wake ni mkubwa kuliko wengine. Anapenda kuvaa viatu vya spoti na suruali ya jeans inayombana, wakati wote simu yake ya mkononi huwa inaning inia kwenye mkanda wake. Anita ana miaka 36, yeye ni mkunga na mshauri wa maswala ya afya wa shirika la Medica Mondiale, shirika la Kijerumani la kutetea haki za wanawake. Shirika hili lilijenga ofisi yake ndogo katika kijiji cha Fishtown. Wanawake na wasichana hukabiliwa na hali ngumu nchini mwao, anasema Anita huku akiwapa mikono na kuagana na wasichana wanaoondoka. 4. Sound Clip Anita, Eng. Wanaawake wa Afrika tunapenda kuamini kuwa wanawake ni kama vitu tu katika nyumba zao. Yaani wao wameumbwa kusema ndio Bwana kila wakati kwa waume zao. Hawana haki ya kutoa mapendekezo. Kwa sababu wanaume wanajiona kuwa wao ndio majogoo, wanaofaa kuwika. Wanatawala nyumba zao, mpaka maisha ya wake zao. Kwa mujibu wa Anita, jambo hilo halifai kukubalika. Anatingisha kichwa chake na kuweka mikono yake kiunoni.

Deutsche Welle, Learning by Ear 2009 Seite 3 5. Sound Clip Anita Ndio maana tunapambana. Tunajaribu kueneza elimu juu ya haki za binadamu ili kuwafanya wanawake wakubalike katika jamii kama wenza na sio wake tu wa kupigwapigwa au kutumiwa vibaya nyumbani, yaani kuwa kama vitu mbele ya waume zao na sio watu. Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Liberia vilichukua miaka 14 hadi kumalizika. Kwa mujibu wa Medica Mondiale wanawake wawili kati ya wanawake watatu walibakwa. Wakiwemo watoto wadogo na wanawake wazee. Wengi kati ya wanawake hao walitekwa nyara na kulazimishwa kuwa wanajeshi au kufanya kazi ya ukahaba. Hata baada ya vita kumalizika hapo mwaka 2003, visa vya utumiaji nguvu havikuishia hapo. Anita anasema kuwa ipo haja ya kusisitiza heshima miongoni mwa wanaume na wanawake na hatua hiyo ifuatiliwe polepole, hatua kwa hatua. 6. Sound Clip: Anita Ni mapambano: wanaume wanapata hofu iwapo wanawake watachukua madaraka, wanafikiri labda watanyag anywa kabisa ufalme wao. Kwa hiyo kuna mvutano mkubwa kati ya wanaume na wanawake. Lakini lazima wakubali vita hivyo, taratibu tumeanza kuona matunda. Wanaume wameanza kukubali kuwa wanawake ni wenzi wao na wana uwezo wa kutoa michango yenye faida iwapo watapewa nafasi. 7. SFX: Road Fishtown Waliberia wanapenda kusema kuwa hakuna chochote cha maana katika kijiji cha Fishtown, wanatania kwamba hakuna hata samaki kama jina la mji huo linavyomaanisha kwa lugha ya kimombo. Hata wale wanaoishi huko nao husema hivyo hivyo. Lakini hiyo yote sio kweli. Wenyeji wa huko wameuchimba mji huo mdogo katika eneo la Kusini mashariki mwa Liberia kutoka kwenye msitu mnene. Barabara ya udongo inagawa eneo hilo kati ya magharibi

Deutsche Welle, Learning by Ear 2009 Seite 4 na mashariki. Siku ya soko ambayo ni kila siku ya Alhamisi, mirundo ya samaki waliokaushwa huuzwa. Si hayo tu, mji mdogo wa Fishtown una ukumbi, kiwanja cha mpira, kituo cha polisi na pia maduka machache bila kusahau vilima vitatu vinavyokamilisha mpaka wa mji huo mdogo. 8. Sound Clip: Anita Oh Kilima,... ninakizungumzia kilima hiki huku nakipanda. Kwa hiyo pumzi zinaniishia. Tafadhali. (Laughs). Anita anapanda kilima kuelekea nyumbani kwa Luise Kwe. Jezi ya rangi ya manjano imeanikwa juani. Mjukuu wa Luise anachapa maji ndani ya beseni la plastiki. Luise anatuashiria tuingie ndani ya chumba chenye kuta ambazo zimejengwa kwa kutumia vifaa vya ujenzi vya kale. Kwa haraka anatafuta kitabu chake cha kumbukumbu ambacho amenakili kila mtoto aliyezaliwa na safari alizofanya majumbani. 9. SFX: Luise house Luise ni mmoja kati ya wakunga wengi wa kienyeji. Alijifunza kazi hiyo ya kuwasaidia akinamama wajawazito wakati wanapojifungua kutoka kwa mama yake na pia kutoka kwenye kozi moja ya Anita ambayo alihudhuria. Luise amesaidia kuwaleta watoto wengi wa Liberia duniani katika umri wake wa miaka 62. Anita hufika iwapo kuna matatizo na Luise anapokuwa hajui la kufanya. Ni jana tu anasema Luise huku uso wake ukionyesha woga, Ni jana tu alilazimika kumpeleka jirani yake kliniki. Alipatwa na maumivu makali. Anita anafuatilia kwa makini shughuli za Luise, hutaka

Deutsche Welle, Learning by Ear 2009 Seite 5 kujua juu ya afya ya mama mja mzito na vipimo vya mimba pamoja na hali ya mtoto aliye tumboni kwa jumla. 10. Sound Clip Anita: Kufanya kazi ya kutoa huduma kwa jamii, sio kwamba wewe uko juu na jamii iako chini yako, hapana ni lazima ujumuike pamoja na watu, ni muhimu kukubali hali yao ya maisha ndio na wao watakukubali. Lakini ukijaribu kujifanya kuwa wewe ni tafauti, au wewe ni mtaalamu ama mtu mashuhuri basi hautakubalika hata kidogo. Na ujumbe unaojaribu kuufikisha kwa jamii hautafika kamwe. Kwa hivyo ukikuta wao wanakaa chini kwenye sakafu basi na wewe kaa nao, hata ukiletewa kiti kataa ili kuwaonyesha kuwa wewe na wao mko sawa. Sio jambo rahisi, anasema Anita, huku akijitoa ukope kwenye jicho lake. 11. Sound Clip Anita Kwangu mimi hii ni changamoto kubwa katika kazi yangu ya kutoa ushauri katika maswala ya afya na vilevile kama mwanamke niliyeolewa. Nina mume na nina watoto watatu. Mume wangu yuko Monrovia. Anaishi na watoto wetu kule. Shida niliyo nayo ni kuwa mume wangu analalamika saa zote: anasema lazima uje nyumbani ulee watoto hakuna mtu anayewapa malezi ya mama, watoto wanahitaji kuonyeshwa upendo, wanakuhitaji. Huwezi kuwageuzia mgongo na kujali kazi yako tu.yaani analalamika wakati wote. Inabidi nimueleweshe ili niweze kuendelea na kazi yangu. Wakati hamu kubwa ya kumuona mumewe na watoto wao, Joel, Francis na Franita ikimjia, yeye hutumia usafiri wa kawaida kwa siku mbili hadi katika mji mkuu wa Monrovia. Maisha ni mazuri kule. Huduma za afya ni bora, watu wanajihusisha na mambo mengi. Kuna hata sinema mjini Monrovia. Lakini hayo si muhimu kwake kwani mawazo yake hufikiri tu juu ya mji mdogo wa Fishtown na kukumbuka kuwa wakati ule anahitajika zaidi. 12. Sound Clip Anita

Deutsche Welle, Learning by Ear 2009 Seite 6 Kutokea mwanzo mimi sikuwa muhudumu wa afya. Nilikuwa Anita tu kutoka shule ya upili. Nilikuwa nina ndoto hii ambayo nilitaka niitimize. Shabaha yoyote uliyonayo maishani unaweza kuitekeleza, inategemea na wewe mwenyewe tu, bidii yako na uvumilivu. Kwa hivyo Anita niko sawa na mwanamke mwingine yeyote anayeweza kutimiza lengo lake maishani. Ninawahimiza wanawake; wanaweza kabisa kufikia malengo yao na kuwa msaada mkubwa katika maisha ya watu wanaohitaji msaada huo. Na hilo ndilo jambo la muhimu. Ukimsaidia mtu maisha yako hayatakuwa kazi bure. Nina amini hilo sana. 13. SFX Anita walking 14. SFX thunder storm Upepo unatetemesha mabati. Kutoka mashariki msimu wa mvua umeanza. Anita anaelekea katika hospitali ya mji wa Fishtown. Wizara ya afya ya Liberia ina nyumba yenye vyumba vitatu vidogo vya wagonjwa, maabara na chumba cha kujifungulia kina mama wajawazito, nyumba hiyo imepakwa rangi ya kijani na nyeupe. Nyumba hiyo ni hospitalli. Friji la kuwekea dawa linafanya kazi kwa nguvu ya jenereta inayonguruma kwa sauti kubwa. Anita anapita kati ya kundi la wasichana. Nguo zao zimetunishwa na matumbo yao ya duara. Anita anageuka na kusimama mbele ya kundi hilo halafu anateremsha mabega yake. 15. Sound Clip Anita Habari za asubuhi nyote. Saa tatu 3:00 Na leo hii tutazungumza juu ya: Kuwatunza watoto wetu, wote: kuwatunza watoto wetu. Kwa maelezo ya kina yanayoeleweka, Anita anatilia mkazo umuhimu wa chakula chenye vitamini za kutosha. Matunda mengi, mboga na maji safi ya kunywa. Wanawake wanafuatilia maelezo yake kwa shauku.

Deutsche Welle, Learning by Ear 2009 Seite 7 16. SFX: Training at Clinic Baada ya kipindi cha chini ya dakika 30, tayari Anita anakimbilia miadi yake inayofuata. Katika chumba cha mwisho ndani ya kliniki hiyo Martha anatandika shuka nzuri za rangi, amechoka lakini ana furaha. Alijifungua jana usiku. Mtoto wake wa saba. Ijapokuwa hii ndio mimba yake ya kwanza yeye kujifungua katika kliniki. 17. SFX: Anita talking to mother Akiwa njiani kuelekea nyumbani, Anita pia anahisi uchovu kidogo. Tabu za wanawake nchini mwake huwa zinamuangukia yeye mara nyingine yeye husema hivyo. Inawabidi kupambana na mambo mengi tofauti. Chakula mara nyingi kinakuwa ni cha aina moja hakuna mabadiliko,maji ya kunywa si safi. Lakini baya zaidi ni manyanyaso ya kimwili. Ubakaji ndani ya familia unafanyika kila mara. Shirika la Medica Mondiale limempa mafunzo ya kukabiliana na hayo yote kiakili ili aweze kuwasaidia wanawake ambao wana matatizo kutokana na dhulma na mateso yaliyowafika. Lakini sio kazi rahisi hata kidogo. 18. Sound Clip Anita Hmm. Whoa. Mara nyingine unakabiliwa na ugumu hasa pale unapokumbana na kisa ambacho hata binadamu yeyote hangeweza kudhani kuwa kisa kama hicho kinaweza kutokea. Kwa mfano itokee mwanamume amembaka mtoto mdogo. Kesi kama hizo huwa zinaniletea bughdha kubwa. Ninajaribu kutambua njia zikazonipa utulivu. Mojawapo ni kukubali kuwa mambo kama hayo hutokea. Ni sehemu ya maisha. Kilichofanyika huwezi kukibadili. Kwa hivyo cha muhimu ni kukubali hoja halafu kuifanyia kazi. Kwa sababu ukiendelea kukana, mambo hayo huwezi kuyaelewa na kukubali jinsi...

Deutsche Welle, Learning by Ear 2009 Seite 8 Shirika la Kijerumani la Medica Mondiale linafanya kazi inayoonekana. Muasisi wake, Monika Hauser, alitunukiwa tuzo ya Muongozo wa Maisha - (the Right Livelihood Award) mwaka 2008. Na hivyo basi Anita alipata fursa ya kupaa angani hadi nchini Sweden kuhudhuria sherehe za kupokea tuzo hiyo katika mji wa Stockholm. Ilikuwa ni mara yake kwanza kulikanyaga bara Ulaya. Anita anayapiga mapaja yake kwa makofi. Anacheka kila anapokumbuka sherehe hizo. 19. Sound Clip Anita Nilivaa vazi langu la Kiafrika, kandambili za Kiafrika na nywele zangu nilizitengeneza pia mtindo wa Kiafrika. Nilipendeza sana hata wenyeji wa huko walipendezwa na mavazi yangu kwa sababu si kawaida wao kuona vazi kama lile. Wengi walinifuata na kutaka kupiga picha nami, walikuwa wakisema :Naweza kupiga picha na wewe yaani umependeza sana. Oh. Mungu wangu. (Laughs). Na urefu wangu huu, nilikuwa nawaangalia wote vichwani. Nywele zangu ziliwaziba wale waliokuwa wamekaa nyuma yangu wakati wa sherehe, Jamaa mmoja alikuja na kuniambia nakupongeza kwa kupendeza lakini nashukuru sikuwa nimekaa nyuma yako kwa sababu nisingeweza kuona chochote. (Laughs) OUTRO Je umeifurahia hadithi hii? Iwapo ungependa kutoa maoni yako, soma zaidi kuhusu mada hii au sikiliza tena hadithi hii ya Anita kwenye mtandao. Anuani yetu ni: www.dw-world.de/lbe Asante sana kwa kutusikiliza, ni matumaini yangu kuwa utajiunga nasi tena wakati ujao katika hadithi nyingine mpya kwenye makala haya ya Noa Bongo Jenga Maisha Yako, kuhusu Watu Wanaoleta Mabadiliko. Hadi wakati huo, Kwaheri! END