WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA

Similar documents
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA III VI

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO

Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Ufanisi katika Ufundishaji kwenye Shule za Msingi na Sekondari nchini Tanzania

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

Kufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007

Songa kwenye kilele cha upeo. Masuala ya Msingi na Ujuzi juu ya Uendeshaji wa Serikali za Mitaa

KITEGO CHA MAREKEBISHO NA HAKI ZA MTOTO

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU

Elimu Ina Umuhimu gani katika Jamii? Kuelekea Elimu Sahihi

MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA PRO-ROUTES. Ombi kwa ajili ya fedha za umma wa mradi wa ziada

TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM)

Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA 2006/07

Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame M. Mbarawa (Mb.); Waheshimiwa Mawaziri na Wabunge wote mliohudhuria;

Dibaji ya Mwenyekiti wa Kamati ya Pamoja ya Uongozi

Nilikua na Ndoto ya Kumaliza Shule Changamoto za Elimu ya Sekondari Tanzania

Miradi na jamii. 3.1 Utangulizi

JAMHURI YA KENYA. Mkakati wa Ushirikiano MUKHTASARI FY Public Disclosure Authorized. Public Disclosure Authorized

KUHUSU AFRODAD. Dira ya AFRODAD. Dhamira ya AFRODAD. AFRODAD inalenga mchakato sawa na endelevu wa maendeleo kuelekea Afrika yenye mafanikio.

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA. Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo. TOLEO Na.

LUGHA YA KISWAHILI KATIKA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA ELIMU SHULE ZA SEKONDARI

KAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI TANZANIA

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Tufundishane! Mwalimu Bora In this issue: Issue 6, December Do you want to be in our next issue?

Ufundishaji wa lugha nyingine

UFUATILIAJI WA MIRADI NA TATHMINI

Kuuelewa Mchakato wa Bajeti Tanzania Mwongozo wa Asasi za Kiraia

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )

Information for assessors (do not distribute this page to participants):

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )

MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2017/18

In the matter of an Application by the KIGOMA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (KUWASA) For a Tariff and Charges Adjustment

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA MHESHIMIWA DKT

KUSHUKA KWA HADHI YA LUGHA ZA JAMII NCHINI TANZANIA YOHANA P. MSANJILA University of Dar es Salaam, Tanzania

RIPOTI YA WARSHA KUHUSU HABARI KWA AJILI YA UWAJIBIKAJI

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

MAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

Azimio lililopitishwa na Mkutano Mkuu tarehe 18 Desemba 2013 [juu ya taarifa ya Kamati ya Tatu (A/68/456/Add.2)]

Kutetea Haki za Binadamu

UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA)

5. Mheshimiwa Spika, Bunge lako Tukufu lilijadili kwa kina Miswada ifuatayo:

Human Rights Are Universal And Yet...

Shabaha ya Mazungumzo haya

UHUSIANO WA MIKAKATI YA UFUNDISHAJI WA FASIHI YA WATOTO YA KISWAHILI NA UMILISI WA KUSOMA KATIKA SHULE ZA MSINGI, KASARANI, KAUNTI YA NAIROBI, KENYA

Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali ya Madini Ukanda

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

Mwongozo wa Mwezeshaji

Elimu-Jumuishi Kwa Vitendo

Mwongozo wa Mafunzo Yaliyochanganywaya K4Health

TAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF) KUHUSU HAKI ZA WATOTO KATIKA KATIBA MPYA

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig

Elimukombozi, Lugha na Upashanaji Habari nchini Tanzania, katika Muktadha wa Utandawazi

NGUZO KUMI ZA KILIMO KWANZA

KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA

Programu ya Uendelezaji Mifumo ya Maji Vijijini (PUMMV) katika Tanzania. Modeli wa Ukodishaji Mradi

Kitabu Cha Mafunzo Ya Uongozi Kwa Wanawake

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

Kubadili Sheria Za Mbegu Na Ulinzi Wa Aina Za Mbegu Na Mimea Nchini Tanzania

Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara)

Elimu Bora, lakini... C HakiElimu Elimu bora, lakini...

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA FEDHA

Kiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika

Mwongozo wa Utekelezaji wa Njia za S5-UUE (KAIZEN)-UUU Tanzania

TANZANIA MARKETS PAN Sera zinazoboresha masoko

MAPENDEKEZO YA MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA TANZANIA

MWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI

SautiElimu. Sauti Yako Isikike

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA UCHUMI WA ZANZIBAR

USIMAMIZI MKUU WA UBORA WA MAHURUJI

ORDER NO BACKGROUND

Makala ya Mshiriki wa Mafunzo

MAADHIMISHO YA MIAKA 15 YA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

Mwongozo wa Kutathimini mifumo ya Ugawanaji wa faida na Mapato Katika Miradi ya Jamii ya MKUHUMI

In the matter of Application by the TANGA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (TANGA UWASA) For a Multi-Year Tariff Adjustment

RIPOTI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI

Mipango ya miradi katika udugu

Muhtasari wa taarifa ya warsha ya wataalamu juu ya mfumo wa habari kwa njia ya ramani (PGIS), Morogoro, Juni 30 - Julai 1, 2014

MITAZAMO KUHUSU KISWAHILI MIONGONI MWA WAZUNGUMZAJI WA KIJALUO: KIFANI CHA SHULE ZA MSINGI KATIKA KAUNTI YA MIGORI. OWALA JAEL AKINYI C50/75493/2012

JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Dodoma ambako kikao cha Bunge kinaendelea kuja kushiriki japo sehemu ya uzinduzi wa mkutano.

TAARIFA YA MWAKA YA UTENDAJI KAZI IDARA YA UTAWALA BORA 2013/2014

Mazoezi yaliyofanyika wakati wa warsha kuhusu Elimu-Jumuishi kwa Vitendo. Zanzibar, 7-10 Februari 2006

Afya Bora, Utu na Kinga. Ripoti ya Mashauriano ya Kiufundi Aprili 2009, Hammamet, Tunisia

Unyanyasaji wa Watoto & Kutelekezwa

HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE

Evaluation of Contextual Teaching of Kiswahili Proverbs in Secondary Schools in Kenya

Mwongozo wa Familia wa Kujifunza

Mwongozo kwa familia zinazofanya kazi pamoja kwa maisha endelevu. Nyenzo ya Mafunzo

TANZANIA TAARIFA YA MWISHO WA UTEKELEZAJI

Sera ya Faragha. Upeo. Aina za Data na Mbinu za Ukusanyaji

Transcription:

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA 2007 i

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA i

Taasisi ya Elimu Tanzania, 2005 Toleo la 2013 ISBN978-9976 - 61-357 -2 Umebuniwa na kutayarishwa na: Taasisi ya Elimu Tanzania, S.L.P. 35094, Dar es Salaam, TANZANIA Simu: +255 22 2773005 Faksi: +255 22 2774420 Baruapepe: director.general@tie.go.tz Tovuti: www.tie.go.tz Umeidhinishwa na: Kamishna wa Elimu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, S.L.P. 9121, Dar es Salaam, TANZANIA. Simu.: 255-22 - 2122373 Faksi: 255-22 - 2113271 Baruapepe: ebhalalusesa@yahoo.co.uk Tovuti: www.moe.go.tz Kama una maoni kuhusu Mtaala huu, tafadhali wasiliana na Kamishna wa Elimu kupitia anuani iliyotajwa hapo juu. ii

YALIYOMO DIBAJI...v VIFUPISHO...vi ISTILAHI...vii UTANGULIZI... viii USULIviii 1.0 MUKTADHA WA SASA WA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI...1 1.1 Mahitaji ya Kijamii...1 1.2 Mahitaji ya Kiuchumi...1 2.0 MATAMKO YA SERA...2 2.1 Sera za Kimataifa...2 2.2 Sera za Kitaifa...2 3.0 DIRA, DHAMIRA, MALENGO NA UJUZI WA JUMLA WA ELIMU YA MSINGI...3 3.1 Dira...3 3.2 Dhamira...4 3.3 Malengo...4 3.4 Ujuzi wa Jumla wa Elimu ya Msingi...5 4.0 MUUNDO RASMI WA ELIMU...6 4.1 Miaka ya Kusoma...6 4.2 Muda wa kusoma...6 5.0 MUUNDO WA MAUDHUI, MAENEO NA MASOMO YA KUJIFUNZA...7 5.1 Maeneo na Masomo ya Kujifunza...7 5.2 Idadi ya Vipindi kwa kila Somo kwa Wiki...9 6.0 VIWANGO VYA RASILIMALI KATIKA UTEKELEZAJI WA MTAALA.9 6.1 Rasilimali Watu...9 6.2 Rasilimali Vitu...11 7.0 NJIA ZA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA...11 8.0 UPIMAJI WA MAENDELEO YA MWANAFUNZI...12 iii

8.1 Aina za Upimaji...12 8.2 Muundo wa Mtihani...14 9.0 TATHMINI YA MTAALA...16 9.1 Tathmini Endelezi...16 9.2 Tathmini Tamati...16 9.3 Malengo ya Tathmini ya Mtaala...17 REJEA...19 iv

DIBAJI Mitaala ya Elimu katika ngazi za Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Vyuo vya Ualimu imewekwa katika tovuti hii. Mitaala hii ni ile iliyoandaliwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi mwaka 2005 ambayo ilizingatia ufundishaji unaozingatia ujuzi na ujenzi wa maana badala ya ule wa awali unaozingatia maarifa. Mitaala hii imekuwa ikitumika kwa kipindi chote kuanzia mwaka 2005 hadi hivi sasa. Mitaala imeboreshwa kufuatia mchakato wa majadiliano katika vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vilivyofanyika mwezi Februari 2013, pamoja na maoni na hoja mbalimbali zilizotoka kwa wadau wa elimu. Pamoja na maboresho yaliyofanyika, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inaweka mitaala hii wazi kwa wadau wote wa elimu na jamii kwa ujumla ili kuendelea kupata maoni zaidi ya jinsi na namna ya kuiboresha mitaala hiyo. Aidha, katika kipindi hiki cha kukusanya maoni, mitaala hii itaendelea kutumika hadi hapo mchakato wa kuihuisha utakapokuwa umekamilika. Prof. E.P. Bhalalusesa KAMISHNA WA ELIMU WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI v

VIFUPISHO UNESCO Organization EK MKUKUTA MMEM TAMISEMI TEHAMA TET UKIMWI VVU WyEMU United Nations Educational Scientific and Cultural Elimu ya Kujitegemea Mpango wa Taifa wa Kuinua Uchumi na Kupunguza Umaskini Mpango wa Maendeleo wa Elimu ya Msingi Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Taasisi ya Elimu Tanzania Ukosefu wa Kinga Mwilini Virusi Vya Ukimwi Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi vi

ISTILAHI Haiba Masuala mtambuko Mbinu shirikishi Mchakato Maudhui Ujuzi Utandawazi Hali ya mtu inayofanya wengine wavutike naye kutokana na uzuri, heshima, tabia nzuri na mwenendo wake mzuri. Mambo ambayo yapo au hutokea katika jamii na huweza kuathiri mazingira, binadamu, wanyama na mimea. Masuala hayo ni kama vile VVU/UKIMWI, utumikishwaji wa watoto, usalama barabarani, uzazi salama, ukeketaji, elimu ya mazingira na mengineyo. Njia za kufundishia na kujifunzia ambazo humshirikisha mwanafunzi kikamilifu wakati wa ufundishaji/ujifunzaji. Mwenendo mzima wa namna ya kutenda jambo fulani kwa mfano, mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji. Majumuisho ya maarifa na stadi zinazotarajiwa kufundishwa katika somo. Uwezo au ustadi wa kufanya jambo fulani anaotazamiwa mwanafunzi kuuonyesha baada ya kufundishwa/kujifunza. Mfumo wa uchumi unaoruhusu biashara huria kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine bila kuzuizi cha kodi kwa kutumia mifumo ya kisasa ya mawasiliano ya haraka kama vile intaneti, barua pepe, simu za mkononi, za mezani na faksi. vii

UTANGULIZI USULI Mtaala ni mwongozo mpana unaoweka viwango vya utoaji elimu kwa kuzingatia maeneo yafuatayo: maudhui na ujuzi watakaojifunza wanafunzi yaani maarifa, stadi na mwelekeo, njia za kufundishia na kujifunzia zitakazotumika katika utekelezaji wa mtaala, vifaa vya kufundishia na kujifunzia vinavyohitajika, sifa za kitaaluma na kitaalamu za mwalimu atakayeuwezesha mtaala, miundo mbinu wezeshi katika utekelezaji wa mitaala, muda utakaotumika katika ufundishaji na ujifunzaji, upimaji, ufuatiliaji na tathmini ya mtaala. Kwa hiyo, mtaala katika mtazamo wa kisasa unaonekana kama ni kioo kinachoakisi falsafa na utamaduni wa jamii, vikiwemo vyanzo vya maarifa na malengo ya elimu ya nchi. Kioo hiki huonesha pia maarifa, stadi na mwelekeo anaotarajiwa kujenga mlengwa pamoja na njia za utahini, ufuatiliaji na tathmini. Mtaala wa Elimu ya msingi ni miongoni mwa miongozo sita (6) ya mitaala ya shule na vyuo iliyoboreshwa. Haya ni mafanikio yaliyotokana na ushirikiano wa kitaalamu na kitaaluma kati ya UNESCO, Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (WyEMU). TET inajivunia mafanikio hayo na inatarajia kuwa ushirikiano huu utakuwa endelevu ili kuinua ubora wa elimu nchini. SABABU ZA KUBORESHA MTAALA Mtaala huu wa Elimu ya Msingi uliboreshwa kwa kuzingatia Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995, Mpango wa kisekta wa Maendeleo ya Elimu wa 1999-2009, Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2025, Mpango wa Maendeleo wa Elimu ya Msingi (MMEM) 2000-2006, Mpango wa Taifa wa Kuinua Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUKUTA), mapendekezo ya tafiti anuai za kielimu hususani ripoti ya utafiti wa kuboresha elimu ya msingi Tanzania bara ya Agosti, 2004. Matokeo ya utafiti na maoni ya wadau yalidhihirisha umuhimu wa kuboresha mtaala uliokuwa ukitumika wa mwaka 1997. viii

MUUNDO WA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI Mtaala huu una sehemu kuu nane (8). Sehemu ya kwanza inahusu muktadha wa sasa wa mtaala wa Elimu ya Msingi unaozingatia mahitaji ya kijamii na kiuchumi. Sehemu saba zinazofuatia katika mtaala huu zinaelezea masuala ya kimtaala yanayopaswa kutekelezwa ili kufikia lengo la kukidhi mahitaji ya kijamii na kiuchumi. Mtaala wa shule za msingi utatekelezwa kwa ufanisi kwa kufuata mwongozo unaobainisha masuala muhimu ya kielimu, ikiwa ni pamoja na matamko ya sera ya elimu yanayoeleza malengo ya Elimu Tanzania. Ieleweke wazi kuwa kuna malengo makuu ya kitaifa yanayotazamiwa kufikiwa pamoja na ujuzi wa jumla unaokusudiwa kujengwa kwa mwanafunzi katika ngazi ya Elimu ya Msingi. Katika mtaala huu yafuatayo yameelezwa kwa ufasaha: Muundo wa elimu nchini pamoja na maudhui, masomo na maeneo ya kujifunza. Mwongozo umebainisha pia viwango vya rasilimali vinavyohitajika katika utekelezaji wa mtaala, njia za kufundishia na kujifunzia, taratibu za upimaji wa mwanafunzi na tathmini ya mtaala. ix

1.0 MUKTADHA WA SASA WA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI Madhumuni ya elimu ya msingi ni kujenga misingi ya kielimu, kijamii na kiutamaduni. Elimu hii inakusudiwa kumwezesha kila mwanafunzi kupata maarifa, mwelekeo, ujuzi na stadi za msingi za kusoma, kuandika, kuhesabu, kubaini na kutambua changamoto zilizopo katika mazingira na mbinu za kukabiliana nazo. Maendeleo makubwa na ya haraka katika sayansi na teknolojia, na hasa teknolojia ya kupashana habari yamesababisha mabadiliko makubwa ya uendeshaji wa shughuli za kiuchumi na kijamii katika kila nchi. Hivyo mtaala wa Elimu ya Msingi umezingatia mahitaji haya. 1.1 Mahitaji ya Kijamii Tanzania Bara ina jumla ya watu zaidi ya milioni arobaini na tatu wanaotoka katika makabila mbalimbali ambao wameunda taifa moja linalotumia Kiswahili kama lugha ya mawasiliano inayowaunganisha watu hao katika shughuli zao za kila siku za maendeleo. Mtaala wa elimu ya msingi umezingatia mahitaji ya kijamii kwa kutumia lugha ya Kiswahili inayoeleweka na inayotumiwa na watu walio wengi. Aidha, mtaala umehusisha masuala ya utandawazi, teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA), elimu ya jinsia, utawala bora, stadi za maisha, ushauri na unasihi pamoja na huduma za faraja kwa wanaoishi na virusi vya UKIMWI. 1.2 Mahitaji ya Kiuchumi Mtaala wa elimu ya msingi umehusisha masuala ya ujasiriamali, stadi za kazi pamoja na sayansi na teknolojia ili kumwezesha mlengwa kujitegemea zaidi yeye mwenyewe kwa jitihada zake za kutambua na kutumia rasilimali zilizopo kupata mahitaji yake ya msingi ili kuwa na maendeleo endelevu yenye ufanisi katika jamii. Aidha, elimu itakayotolewa itaunganisha nadharia na vitendo ili kuleta tija. 1

2.0 MATAMKO YA SERA Katika uandaaji wa mtaala huu, sera mbalimbali za kimataifa na za kitaifa zimezingatiwa ili kumwandaa kikamilifu mwanafunzi aweze kupata elimu bora. Sera zilizozingatiwa ni sera za Kimataifa na Kitaifa:- 2.1 Sera za Kimataifa Sera za kimataifa zilizozingatiwa ni pamoja na Sera ya Haki za Mtoto ya mwaka 1989, Sera ya Elimu kwa Wote ya mwaka 1990 na Malengo ya Maendeleo ya Milenia ya mwaka 2002. 2.2 Sera za Kitaifa Mtaala wa Elimu ya Msingi unaelekeza kutekeleza malengo ya elimu yanayotokana na sera ya Elimu ya mwaka 1995 ambayo imeeleza kuwa lengo kuu la Elimu ya Msingi ni kumpa mwanafunzi Elimu na Stadi bora zitakazokuwa msingi wa Elimu na Mafunzo katika ngazi za juu na kumuandaa kuingia katika ulimwengu wa kazi. Mtaala huu pia umeandaliwa kukidhi mahitaji ya Mpango wa Kisekta wa Maendeleo ya Elimu wa mwaka 1999-2009, Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2025, Mpango wa Maendeleo wa Elimu ya Msingi Awamu ya Kwanza (MMEM I) 2000-2006, Program ya maendeleo ya kisekta na Mpango wa Taifa wa Kuinua Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUKUTA). 2.2.1 Mpango wa Kisekta wa Maendeleo ya Elimu (1999-2009) Mpango wa Kisekta wa Maendeleo ya Elimu wa mwaka 1999-2009 umeandaliwa chini ya sera ya Elimu na Mafunzo (1995) kwa madhumuni ya kukuza ushiriki wa wadau katika elimu, kuimarisha uwazi miongoni mwa watendaji, matumizi bora ya rasilimali, uwekaji na usimamizi wa mipango, tathmini na utekelezaji wa malengo ya sekta ndogo za elimu; yaani msingi, sekondari, ualimu na elimu ya ufundi. 2.2.2 Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2025 Dira ya Maendeleo ya Tanzania kufikia mwaka 2025 imelenga kukuza maendeleo ya jamii, hususani kutoa elimu bora kwa lengo la kuendeleza 2

walengwa katika ubunifu, ugunduzi au uvumbuzi, maarifa na stadi mbalimbali, kutoa wataalamu wenye uwezo wa kutatua matatizo ya jamii nchini, utumiaji wa sayansi na teknolojia na utoaji wa elimu kwa vitendo katika ngazi zote za elimu na kuwa na jamii iliyoelimika vyema ifikapo mwaka 2025. 2.2.3 Mpango wa Maendeleo wa Elimu ya Msingi (2000-2006) Mpango wa Maendeleo wa Elimu ya Msingi (MMEM) 2000-2006 ulilenga katika kuwa na mtaala bora wenye muundo unaotekelezeka na kukidhi mahitaji ya wadau wa elimu ikiwa ni pamoja na kuufanya umlenge mwanafunzi zaidi, kujenga ujuzi badala ya maudhui, kuingiza masuala mtambuko na stadi za maisha katika mtaala, kuboresha ufundishaji kwa walimu na ujifunzaji wa wanafunzi, kuboresha upimaji na ufuatiliaji wa maendeleo ya mwanafunzi ili kuhakikisha kwamba wanafunzi wanapata elimu iliyo bora wakati wote. 2.2.4 Mkakati wa Taifa wa Kuinua Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUKUTA) Mwongozo huu pia umezingatia malengo yaliyomo katika Mkakati wa Taifa wa Kuinua Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUKUTA) ambao umelenga kuwa na mtaala wa elimu ya msingi utakaowapa walengwa maarifa, stadi na mielekeo chanya ya kushiriki vyema katika kujiletea maendeleo yao wenyewe. Hali hiyo italeta tija kwa mtu binafsi na kwa taifa kwa ujumla na hivyo kupunguza umaskini. Kwa mujibu wa sera ya elimu, lugha rasmi ya kufundishia Elimu ya Msingi itakuwa ni Kiswahili na lugha ya Kiingereza itafundishwa kama somo la lazima. Kwa shule zinazotumia Kiingereza kama lugha ya kufundishia, somo la Kiswahili litafundishwa kama somo la lazima. 3.0 DIRA, DHAMIRA, MALENGO NA UJUZI WA JUMLA WA ELIMU YA MSINGI 3.1 Dira Elimu ya msingi inalenga kuwa na mtanzania aliyeelimika na mwenye 3

maarifa, stadi na mwelekeo madhubuti na aliye mahiri katika kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika maisha yake ya kila siku. 3.2 Dhamira Kutoa fursa ya elimu bora kwa usawa na kwa wananchi wote na kuhakikisha kuwepo kwa mazingira bora yanayomjali mwanafunzi katika ujifunzaji wenye ujenzi wa ujuzi. 3.3 Malengo 3.3.1 Malengo ya Elimu Nchini Tanzania Elimu itolewayo ni ya kurithisha maarifa stadi na mielekeo bora kutoka kwa vizazi vilivyopita hadi vizazi vya wakati huu na vijavyo. Hivyo yafuatayo ndio malengo ya elimu nchini:- a) Kuelekeza na kukuza maendeleo, kuboresha haiba ya wananchi wa Tanzania, rasilimali zao na matumizi bora ya rasilimali hizo katika kuleta maendeleo ya mtu binafsi na ya kitaifa. b) Kukuza tabia ya kuthamini utamaduni, mila na desturi za watu wa Tanzania. c) Kukuza upatikanaji wa fursa za kusoma, kuandika na kuhesabu na matumizi sahihi ya maarifa na stadi za kijamii, kisayansi, kiufundi, kiteknolojia, kitaalamu na aina nyingine za maarifa na ujuzi, kwa ajili ya maendeleo na kuboresha hali ya mtu na jamii. d) Kukuza na kuendeleza kujiamini, kudadisi, weledi na kuheshimu utu wa mtu na haki za binadamu na kuwa tayari kufanya kazi kwa kujiendeleza na kwa maendeleo ya taifa. e) Kuwezesha na kupanua mawanda ya kujipatia maarifa, kuboresha na kukuza stadi za kiakili, ki-vitendo, uzalishaji na nyinginezo zitakiwazo katika kukidhi mabadiliko ya mahitaji ki-uchumi. f) Kumwezesha kila raia kuelewa misingi ya Katiba ya nchi pamoja na kuthamini haki za binadamu na uraia, wajibu na majukumu yanayoendana nayo. g) Kukuza utashi wa kupenda na kuheshimu kazi za kujiajiri na kuajiriwa na kuboresha utendaji kazi katika sekta za uzalishaji na huduma. 4

h) Kujenga misingi ya maadili yanayokubalika kitaifa na ushirikiano wa kitaifa na kimataifa, amani na sheria kwa njia ya kujifunza. i) Kuwezesha kuwapo kwa matumizi sahihi, usimamizi na utunzaji wa mazingira. 3.3.2 Malengo ya Jumla ya Elimu ya Msingi Elimu ya Msingi ina madhumuni ya kuwapatia walengwa maarifa, stadi na mielekeo inayohitajika kwa maendeleo ya watanzania katika ulimwengu wa sasa. Yafuatayo ndio malengo ya Elimu ya Msingi:- a) Kumwezesha kila mwanafunzi kuelewa na kuthamini utu wake, kujipatia maarifa, kuheshimu na kuthamini asili ya utamaduni wetu, mila na desturi za jamii, pamoja na umoja wa Kitaifa, utambulisho, maadili na kujiamini. b) Kutoa fursa ya kumwezesha kila mwanafunzi kupata maarifa, kuthamini na kutumia kikamilifu lugha ya Kiswahili na kuiheshimu kwa kuwa ni alama ya umoja, utambulisho na heshima ya taifa. c) Kumwezesha kila mwanafunzi kufahamu misingi ya Katiba ya nchi pamoja na kuheshimu haki za binadamu na za uraia, wajibu na majukumu ya kila raia. d) Kumwezesha kila mwanafunzi kupata zana za msingi za kujifunzia kusoma na kuandika, mawasiliano, kuhesabu na kutatua matatizo pamoja na misingi ya kujifunza maarifa mchanganyiko, ujuzi na mwelekeo unaohitajika ili kumudu maisha na maendeleo kwa kadri ya uwezo wake. e) Kumpa mwanafunzi misingi ya kujitegemea, kujiendeleza na kujiamini f) Kumuandaa mwanafunzi kwa ajili ya ngazi ya pili ya elimu yaani elimu ya sekondari, ufundi stadi na elimu endelezi. g) Kumuandaa mwanafunzi kuingia katika ulimwengu wa kazi. 3.4 Ujuzi wa Jumla wa Elimu ya Msingi Elimu ya msingi inatazamiwa kumpatia mlengwa ujuzi wa: a) Kuthamini mila, desturi na utamaduni pamoja na umoja wa kitaifa na kuwa na maadili mema na kujitambua yeye mwenyewe, b) Kuchunguza, kuchambua na kutafsiri mambo; 5

c) Kusoma, kuandika, kuhesabu, kubuni na kuwasiliana kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza d) Kutumia stadi za kazi ili kumwezesha kuingia katika ulimwengu wa kazi na ujasiriamali ; e) Kutumia Kiswahili kwa ufasaha na kuiheshimu lugha ya Kiswahili ambayo ni alama ya umoja wa taifa, alama ya kujitambulisha na kujiamini. f) Kufanya majaribio rahisi ya kisayansi; g) Kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano kwa ufanisi, h) Kujitegemea, kujiendeleza na kujiamini pamoja na kutatua matatizo katika maisha ya kila siku ; 4.0 MUUNDO RASMI WA ELIMU Muundo wa elimu rasmi utakuwa ni 2-7-4-2-3+ yaani miaka miwili (2) ya elimu ya awali, miaka saba (7) ya elimu ya msingi, miaka mine (4) ya elimu ya sekondari ngazi ya kawaida, miaka miwili (2) ya ngazi ya juu ya sekondari na miaka isiyopungua mitatu (3) ya elimu ya chuo kikuu. 4.1 Miaka ya Kusoma Elimu ya msingi itakuwa ni ya miaka saba na ya lazima kwa uandikishwaji na mahudhurio. Mwishoni mwa ngazi hii wanafunzi wanaweza kuendelea na elimu ya sekondari, mafunzo ya ufundi stadi au kuingia kwenye ulimwengu wa kazi. Umri wa kuanza shule kwa wanafunzi ni miaka saba (7). Mwaka wa masomo utakuwa na siku 194, ambazo zitagawanywa katika mihula miwili itakayokuwa na majuma 21 kila mmoja. 4.2 Muda wa kusoma Muda wa kusoma au kujifunza ni saa tatu na nusu (3½) kila siku kwa darasa la I na la II. Kwa darasa la III hadi la VII muda wa kusoma utakuwa ni saa 6 kwa siku. Aidha, wanafunzi wasioona katika darasa la I na II wana vipindi vingi zaidi ili waweze kujifunza stadi za kusoma na kuandika katika breili. 6

5.0 MUUNDO WA MAUDHUI, MAENEO NA MASOMO YA KUJIFUNZA Muundo wa maudhui, maeneo na masomo ya kujifunza yatatofautiana kutoka darasa moja hadi lingine kulingana na makuzi ya mtoto. Maudhui ya mtaala huu yamejikita katika ujifunzaji unaolenga ujenzi wa ujuzi. 5.1 Maeneo na Masomo ya Kujifunza Kutakuwa na maeneo makuu sita (6) ya kujifunza katika elimu ya msingi ambayo mwanafunzi atatakiwa kujifunza maeneo yote. Maeneo hayo ni:- (a) Lugha Eneo hili linahusisha masomo ya Kiswahili, English na French. Umuhimu wa lugha ni kuwaandaa walengwa wenye ujuzi wa kusikiliza, kusoma, kuzungumza na kuandika kwa ufasaha pamoja na kuelewa na kujieleza kwa kutumia lugha inayojumuisha alama na maneno. Pia huwezesha walengwa kuwasiliana katika shughuli za kila siku katika muktadha na mazingira mbalimbali. (b) Sayansi ya Jamii Hili ni eneo linalohusisha masomo ya Historia, Jiografia na Uraia. Umuhimu wa eneo hili ni kuwawezesha walengwa kuelewa na kuthamini haki za binadamu na umuhimu wake, kuelewa historia ya jamii na kutekeleza wajibu wao katika jamii na nchi zilizo jirani na kuchangia katika maendeleo. Huwawezesha walengwa pia kuelewa, kuthamini na kuendeleza utamaduni unaofaa katika jamii na kutambua tamaduni za jamii nyingine zinazofaa. Kuelewa mazingira anamoishi, kuyatunza, kuyahifadhi na kuyatumia katika njia endelevu, kutambua na kushiriki katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi, kijamii na kisiasa. (c) Sayansi na Teknolojia Hili ni eneo linalohusisha masomo ya sayansi na TEHAMA ambayo umuhimu wake ni kuwapatia walengwa ujuzi wa kupenda na kutumia misingi ya sayansi na teknolojia katika maisha ya kila siku. 7

Huwawezesha walengwa kutambua mbinu mbalimbali za kutafuta na kupata habari kwa kutumia teknolojia za kiasili na za kisasa, kutambua misingi ya sayansi na kutumia teknolojia kutatua matatizo binafsi na ya jamii, kubuni na kutumia ugunduzi wa kisayansi katika hali endelevu na kutambua hatua za mchakato wa uchunguzi wa kisayansi. (d) Stadi za Maisha Eneo hili linahusisha masomo ya Stadi za Kazi, na Haiba na Michezo. Umuhimu wa masomo hayo ni kuwawezesha walengwa kujenga misingi ya stadi za kazi mbalimbali, zikiwemo za kilimo, ufugaji, uvuvi, ufundi na usanii ili kujiendeleza katika maisha yao. Humwezesha mlengwa kuzingatia amali na maadili ya jamii, kuepuka vishawishi na vitendo vinavyoweza kuhatarisha maisha. (e) Maadili na Masuala ya Kiroho Hili ni eneo linalohusika na somo la dini ambalo umuhimu wake ni kumuwezesha mlengwa kuishi kwa kuzingatia maadili mema katika maisha yake, kuishi kwa kuzingatia misingi ya dini yake akionesha upendo, uadilifu na kudumisha amani ndani ya jamii wakati wote na mahali popote. Kumcha Mungu kwa mujibu wa kanuni na taratibu za madhehebu ya dini yake. Kujenga tabia ya uvumilivu na kuheshimu tofauti za kiimani na za kiitikadi wakati wote na mahali popote. (f) Hisabati Hili ni eneo muhimu ambalo huwawezesha walengwa kupata ujuzi wa kuhesabu, kusoma na kuandika namba, kufanya matendo ya Hisabati ya kujumlisha, kutoa, kuzidisha na kugawanya. Huwawezesha pia kuweza kuchora, kuwasilisha na kutafsiri data, takwimu na grafu. Kufumbua mafumbo kwa kukokotoa, kukadiria, kupanga, kuorodhesha, kufafanua, kuwianisha na kurahisisha. Kupima, kuunda na kutengeneza violwa na modeli sahili. Kutumia maarifa, mantiki na stadi za kihisabati katika maendeleo yake na jamii. 8

5.2 Idadi ya Vipindi kwa kila Somo kwa Wiki Kipindi kitakuwa cha dakika 30 katika darasa la I na la II, hivyo kuwa na vipindi 32 kwa wiki. Kwa darasa la III hadi la VII kipindi kitakuwa cha dakika 40, hivyo kufanya jumla ya vipindi 42 kwa wiki. Jedwali Na.1 linaonesha masomo na idadi ya vipindi kwa kila darasa kwa wiki. Jedwali Na 1: Masomo na Idadi ya Vipindi kwa kila Darasa kwa Wiki SOMO Darasa I II IDADI YA VIPINDI Darasa III IV Darasa V -VII Kiswahili 6 7 7 English 7 7 7 Hisabati 7 7 7 Sayansi 2 4 4 Jografia - 3 3 Historia - 2 2 Uraia - 2 2 Stadi za Kazi 3 2 2 Haiba na Michezo 2 2 2 TEHAMA 1 2 2 Dini 2 2 2 French 2 2 2 Jumla 32 42 42 Tanbihi: Masomo ya Hisabati, Kiswahili na English yamepewa vipindi vingi ili kuendana na msisitizo wa elimu ya msingi ambao ni kumpa mlengwa stadi za kudumu za kusoma, kuandika na kuhesabu. 6.0 VIWANGO VYA RASILIMALI KATIKA UTEKELEZAJI WA MTAALA 6.1 Rasilimali Watu 6.1.1 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Elimu ya Msingi Mwalimu mkuu wa shule ya elimu ya msingi anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo: 9

Awe amehitimu Kidato cha nne katika shule ya sekondari inayotambulika serikalini kwa kiwango cha Daraja la III au zaidi. Awe amehitimu mafunzo ya ualimu Ngazi ya stashahada au zaidi, katika Chuo cha Ualimu kinachotambulika serikalini. Awe na uzoefu wa kufundisha elimu ya msingi usiopungua muda wa miaka 5. 6.1.2 Mwalimu wa Shule ya Elimu ya Msingi Mwalimu atakayefundisha shule ya zifuatazo: elimu ya msingi anatakiwa kuwa na sifa Awe amehitimu Kidato cha nne katika shule ya sekondari inayotambulika serikalini kwa kiwango cha Daraja la III. Awe amehitimu mafunzo ya ualimu Ngazi ya Cheti au zaidi, katika Chuo cha Ualimu kinachotambulika serikalini. 6.1.3 Idadi ya Vipindi na Uwiano wa Mwalimu na Wanafunzi Darasa la elimu ya msingi litakuwa na wanafunzi 40 na uwiano wa mwalimu na wanafunzi utakuwa ni 1:40. Mwalimu atapaswa kufundisha vipindi kati ya 28 hadi 32 katika ngazi ya shule ya msingi kwa wiki. 6.1.4 Wakaguzi wa Shule Ukaguzi wa utekelezaji wa mtaala utafanywa na idara ya ukaguzi wa shule kuanzia ngazi ya wizara hadi halmashauri za wilaya. Kazi kubwa ya wakaguzi wa shule itakuwa ni kuhakikisha viwango vya ubora vya elimu ya msingi katika utekelezaji wa mtaala vinazingatiwa kikamilifu. Wakaguzi wa shule watatoa taarifa ya utekelezaji wa mtaala mara kwa mara na taarifa hiyo itatumika katika kuboresha mtaala. Vile vile, usimamizi wa utekelezaji wa mtaala utafanywa kuanzia ngazi ya wizara hadi 10

shule. Msimamizi wa ngazi ya shule ni mwalimu mkuu, ngazi ya kata ni mratibu elimu kata (MEK), ngazi ya Wilaya ni Afisa elimu wilaya, ngazi ya Mkoa ni Afisa elimu mkoa na ngazi ya wizara ni Mkurugenzi wa Idara ya Elimu ya Msingi. Idara ya Ukaguzi itashirikiana na Wizara ya Elimu katika ngazi zote ili kuwe na ufanisi katika kukagua na kusimamia masuala yote ya elimu. 6.2 Rasilimali Vitu 6.2.1 Vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia Mihtasari, miongozo, vitabu, na zana za kufundishia na kujifunzia ni vya muhimu katika utekelezaji wa mtaala wa elimu ya msingi ili kukidhi malengo ya elimu yanayotarajiwa. Vitabu vya kiada na ziada vitakavyotumika ni vile vilivyopendekezwa na kupitishwa na kamati ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inayosimamia udhibiti wa vifaa vya elimu. Mihtasari na miongozo ya masomo itakayotumika ni ile itakayoandaliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania na kuidhinishwa na wizara inayohusika na elimu. Katika kila muhtasari wa somo kutakuwa na orodha ya vifaa na zana za kufundishia na kujifunzia zilizopendekezwa. 6.2.2 Samani na Majengo Majengo na samani yanatakiwa yazingatie walengwa wa aina zote wakiwemo wasichana, wavulana na wote wenye mahitaji maalum. Madarasa na majengo mengine kama vile maktaba yajengwe kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa na Wizara inayohusika na Elimu. 7.0 NJIA ZA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA Njia zitakazotumika katika mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji ni njia shirikishi zinazomjali zaidi mwanafunzi katika kuwezesha kufikiwa kikamilifu kwa malengo ya mada au somo husika. Njia hizo ni nyenzo kuu na muhimu katika kufanikisha ujifunzaji fanisi, 11

mchakato ambao mwanafunzi hupata fursa ya kutenda, kufikiri peke yake, kujadili na wenzake katika vikundi na darasa zima, kushiriki na wenzake katika kufikiri na kutenda, kubuni, kuchunguza na kufikia mwafaka. Katika mchakato huo, mwalimu (mwezeshaji) huhakikisha kuwa fursa za kutenda na kushiriki kwa wanafunzi huwa sawa kwa jinsia zote, na fursa hizo hutumika katika kukuza vipaji vya kila mmoja. Mwalimu atumie mbinu zinazomshirikisha mwanafunzi zaidi wakati wa ufundishaji na ujifunzaji. 8.0 UPIMAJI WA MAENDELEO YA MWANAFUNZI Mwalimu atalazimika kupima maendeleo ya mwanafunzi wakati na baada ya tendo la ufundishaji na ujifunzaji. Upimaji unamwezesha mwalimu kupata data na kufahamu uwezo wa stadi, maarifa na mwelekeo aliofikia mwanafunzi. Upimaji pia unamwezesha mwalimu kujua ni kwa kiwango gani mwanafunzi amefikia malengo mahususi ya mada mbalimbali alizojifunza. 8.1 Aina za Upimaji Tathmini ya maendeleo ya mwanafunzi itazingatia aina mbili za upimaji. Aina hizo ni upimaji endelezi na upimaji tamati. (a) Upimaji Endelezi Upimaji endelezi utafanyika kila mara wakati mwalimu anaendelea kufundisha ili kubaini kama wanafunzi wamemudu kipengele fulani katika mada husika kabla ya kufundisha kipengele kinachofuata. Zana zitakazotumika katika upimaji huu ni mazoezi, majaribio, kazi mradi, maswali dodoso, maswali ya ana kwa ana, mazoezi kwa mwanafunzi mmoja mmoja, mazoezi kwa vitendo na mkoba wa kazi. Mwalimu atalazimika kuwapima wanafunzi kwa kuwapa mazoezi mbalimbali kwa kuzingatia zana za upimaji zilizopendekezwa katika kiwango cha elimu ya msingi. Aidha, mwalimu atalazimika kurekodi alama watakazopata wanafunzi kwa kufuata utaratibu uliooneshwa katika jedwali namba 2 kwa ajili ya kujumlishwa na alama za upimaji tamati. 12

(b) Upimaji Tamati Baraza la Mitihani la Tanzania litahusika na upimaji huu ambao utafanyika mwishoni mwa darasa la 7. Mtihani wa taifa utatungwa na kuratibiwa na Baraza la Mitihani. Upimaji utafanyika katika kila somo kama ilivyooneshwa katika jedwali Jedwali Na.2 Utaratibu wa Utahini katika Upimaji Endelezi na Tamati Eneo la Somo Zana za Upimaji Endelezi Upimaji Na. Kujifunzia Upimaji Fadaa Alama Tamati Drs I-IV Drs V- VII (BMT) 1. Lugha Kiswahili Majaribio 4 3 15 English French Maswali ya ana kwa ana 2 2 10 Mitihani ya 8 5 10 muhula Mkoba wa kazi 1 1 05 50 Kazi mradi 1 1 05 Mazoezi ya - 2 05 mwanafunzi mmoja mmoja Jumla 50 50 2 Hisabati Hisabati Majaribio 4 3 15 Mazoezi ya 2 2 15 50 mwanafunzi mmoja mmoja Mitihani ya 8 5 10 muhula Mkoba wa kazi - 1 05 Kazi mradi - 1 05 Jumla 50 50 3 Sayansi na Sayansi Majaribio 2 4 15 50 Teknolojia Mazoezi ya 2 2 15 mwanafunzi 13

Eneo la Somo Zana za Upimaji Endelezi Upimaji Na. Kujifunzia Upimaji Fadaa Alama Tamati Drs I-IV Drs V- VII (BMT) mmoja mmoja Mitihani ya 8 5 10 muhula Mkoba wa kazi 1 2 05 Kazi mradi - 1 05 Jumla 50 50 4 Maarifa Jiografia Wasilisho - 2 15 50 Uraia Historia darasani Majaribio 2 4 15 Mitihani ya 8 5 10 Muhula Mkoba wa kazi - 2 05 Kazi mradi 1 1 05 Jumla 50 50 5. Stadi za Stadi za Majaribio 2 4 15 maisha kazi Haiba na Michezo Mazoezi kwa 2 2 15 50 vitendo Mitihani ya 8 5 10 Muhula Mkoba wa Kazi 1 2 05 Kazi Mradi 1 1 05 Jumla 50 50 8.2 Muundo wa Mtihani Mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi utahusisha jumla ya masomo sita (6) kwa shule ambazo hazifundishi somo la French na saba (7) kwa shule zinazofundisha somo la French. Mitihani itagawanyika katika makundi makuu 14

matano (5), kama ifuatavyo: a) Masomo ya Lugha Kundi la lugha litahusisha masomo ya Kiswahili, English na French. Masomo ya Kiswahili na English yatatahiniwa kwa wanafunzi wote wakati somo la French litatahiniwa kwa wanafunzi ambao shule zao zinalifundisha. b) Somo la Hisabati Somo hili litatahiniwa kwa wanafunzi wote. c) Masomo ya Sayansi na Stadi za Kazi Kundi hili litahusisha masomo mawili ambayo ni Sayansi na Stadi za Kazi. d) Somo la Maarifa Kundi hili litahusisha masomo ya Uraia, Jiografia, Historia na Haiba na Michezo e) Somo la TEHAMA Katika upimaji tamati, masomo yafuatayo ni lazima yatahiniwe kwa wanafunzi wote; English, Kiswahili, Hisabati, Sayansi, Stadi za Kazi, TEHAMA, na Maarifa (Historia, Uraia, Jiografia na Haiba na Michezo). Somo la French litatahiniwa kama somo chaguzi kwa baadhi ya wanafunzi wa shule zinazofundisha somo hilo. Masomo hayo yatatahiniwa kwa muda wa siku tatu (3) na muda wa kutahini kila somo ni saa mbili (2). Kila mtihani utagawanyika katika sehemu mbili A na B kama inavyooneshwa katika jedwali ukurasa unaofuata. Jedwali Na. 3: Masomo yatakayotahiniwa na Muda wa Kutahini Na. KUNDI 1 Lugha MASOMO IDADI YA SEKSHENI MUDA YATAKAYOHUSIKA MASWALI Kiswahili 25 2 Saa 2 English 25 2 Saa 2 French (chaguzi) 25 2 Saa 2 2 Hisabati Hisabati 25 2 Saa 2 Sayansi na Stadi Sayansi na 3 25 2 Saa 2 za Kazi Stadi za Kazi 15

4 Maarifa Historia, Jiografia, Uraia na Haiba na Michezo 25 2 Saa 2 5 TEHAMA TEHAMA 25 2 Saa 2 9.0 TATHMINI YA MTAALA Katika elimu ya msingi, tathmini itafanyika ili kupima ubora au udhaifu wa mtaala kwa madhumuni ya kuuboresha au kuurekebisha ili kukidhi mahitaji ya taifa na wadau wa elimu nchini hususani wanafunzi. Kutakuwa na aina mbili za tathmini ya mtaala ambazo ni tathmini endelezi na tathmini tamati. 9.1 Tathmini Endelezi Tathmini endelezi inafanyika wakati wa utekelezaji wa mtaala. Lengo kuu ni kubaini mafanikio, matatizo na mapungufu yanayojitokeza ili kuyafanyia marekebisho. Kwa hiyo, ni ufuatiliaji wa mara kwa mara ili kujua kama mtaala unatekelezwa kama ulivyokusudiwa. Jedwali Na. 4: Ngazi za Tathmini Endelezi na Wahusika Ngazi Wahusika 1. Shule/Kata/Tarafa Walimu, Kamati za shule, Waratibu Elimu Kata 2. Wilaya/Mkoa/Kanda Maafisa Elimu katika wilaya/mkoa/kanda, Wakaguzi, Asasi zisizo za serikali, Mashirika ya Dini, Jumuiya za Wazazi na wamiliki Binafsi wa Shule. 3. Taifa WyEMU, TET, Asasi zisizo za serikali, Mashirika ya Kimataifa na Watafiti mbalimbali. 9.2 Tathmini Tamati Tathmini tamati hufanywa mwishoni mwa muda wa kozi au mafunzo au programu. Kwa kawaida kuna kipindi au mzunguko wa muda maalum wa 16

kufanya tathmini tamati ya mtaala. Tathmini tamati kwa Elimu ya Msingi inapaswa kufanyika baada ya miaka saba kwa kuwa ndiyo mzunguko wa ngazi hii ya elimu. Kwa utaratibu huu tathmini tamati itafanywa siyo chini ya miaka saba (7) tangu kuanza utekelezaji wa mtaala ulioboreshwa au kurekebishwa. Kwa maana hiyo, tathmini tamati inabidi ifanywe kabla ya kurekebisha mitaala. Umuhimu wa tathmini tamati ni: a) Kuonyesha kiasi mafanikio yaliyofikiwa kufuatana na malengo yaliyokusudiwa kufikiwa. b) Kuwezesha kuamua kama malengo ya masomo yanafaa au hayafai. c) Kuamua kama ufundishaji ni bora au duni. d) Kubaini mambo yanayofanikisha au kuathiri utekelezaji. e) Kuibua maoni ya wadau kuhusu ubora au udhaifu wa mitaala. Wakati mwingine tathmini tamati inaweza kufanyika kabla ya miaka saba (7) kukamilika kwa upande wa ngazi ya Elimu ya Msingi. Hii hutokana na sababu zifuatazo: a) Kiwango cha elimu kinaposhuka na jamii kuleta malalamiko mengi. b) Haja ya kuingiza katika mtaala maarifa na stadi mpya kwa mfano: mabadiliko ya sayansi na teknolojia, utandawazi, masuala mtambuko kama elimu ya mazingira, stadi za maisha, elimu ya VVU/UKIMWI au hoja ya kuanzisha somo au masomo mapya. c) Haja ya kufanya marekebisho katika maudhui. Kwa mfano: Kuondoa maudhui yaliyopitwa na wakati au yasiyo sahihi, kuondoa mada ngumu na zisizo za lazima au kuhamisha mada kutoka darasa moja hadi lingine au kurekebisha mpangilio wa mada katika mihtasari. d) Haja ya kuboresha mbinu za kufundishia na kujifunzia, upimaji na ufuatiliaji. e) Mabadiliko ya sera ya elimu na mafunzo. 9.3 Malengo ya Tathmini ya Mtaala Lengo la tathmini ni kuhakiki mtaala unaotumika kwa madhumuni ya 17

kuuboresha au kuurekebisha. Tathmini huangalia mambo yote yaliyo katika mtaala ikiwemo malengo yaliyokusudiwa, maudhui, njia za kufundishia na kujifunzia, upatikanaji wa vifaa na zana za upimaji wa maendeleo ya wanafunzi, uwezo wa walimu katika kufundisha na mazingira ya kufundishia na kujifunzia. Kwa kifupi, tathmini inaangalia kama mtaala unatekelezeka. Malengo ya tathmini ya mtaala ni pamoja na: a) Kujua ubora na mapungufu ya mtaala na kiwango cha maarifa, stadi na mwelekeo waliopata wanafunzi. b) Kuona kama malengo yaliyokusudiwa yamefikiwa. c) Kujua ubora wa njia za kufundishia na kujifunzia zinazotumika. d) Kuona kama vifaa vya kufundishia na kujifunzia vinapatikana na vinatumika ipasavyo. e) Kuona kiwango cha ushiriki wa mwanafunzi akiwa ndani na nje ya darasa. f) Kuona kiwango cha ushirikishwaji cha jamii katika utekelezaji wa mtaala. g) Kuona kama mtaala unakidhi mahitaji ya wadau wa elimu. h) Kuangalia utoshelevu wa vitabu, vifaa na zana za kufundishia na kujifunzia. i) Kuona kama kuna mazingira yanayomjali mwanafunzi shuleni, ikiwa ni pamoja na wale wenye mahitaji maalum. Mazingira hayo ni kama utoshelevu wa vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo, ofisi, samani, kuwepo maua na miti ya mapambo, viwanja vya michezo na huduma za kijamii. j) Kuangalia matatizo ya utawala na uendeshaji wa shughuli za kielimu katika ngazi mbalimbali wakati wa utekelezaji na ufuatiliaji wa mtaala. k) Kupima jitihada zinazofanywa kuwezesha na kuboresha walimu kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa mitaala. l) Kuangalia mambo mengine nje na ndani ya shule yanayoathiri utekelezaji wa mtaala. 18

REJEA Bajumuzi J. (2002). Performance of the Visually Impaired Pupils in Tanzania, Dar es Salaam. (Unpublished Document). Barnes, D (1982). Practical Curriculum Study. Routledge and Kegan Paul: London. Institute of Curriculum Development (ICD): (1990). A Summary Report on BaselineSurvey on Primary, Secondary and Teacher Education Curriculum Reform intanzania Mainland. Dar Es salaam. (Unpublished Document). Kirk S. A et. al. (2003 ). Educating Exceptional Children, 10 th Edition. Houghton Mifflin Co. Boston. Ministry of Education and Culture (MOEC). (1995) Education and Training Policy. MOEC Dar es Salaam. MOEC. (2001). A Baseline Survey on Knowledge, Attitudes and Practices (KAP) in Tanzania Mainland. UNFPA: Dar es Salaam. Njabili F. A. (1993). Practical Guide for Classroom Measurement and Testing. The Basic Essentials: Mture Publishers: Dar es Salaam. Morsh C. J. (1977 ). Planning Management and Ideology: Key Concepts for Undestanding Curriculum. Falmer Press. UK. Taasisi ya Elimu Tanzania (TET). (2004). Ripoti ya Utafiti wa Kuboresha Mtaala wa Elimu ya Msingi. TET. Dar Es salaam (Kisawidi: Rekebisho la Kwanza); Agosti 2004. Taasisi ya Elimu Tanzania (TET). (1999). Ripoti ya Ufuati liaji wa Muundo Mpya wa Masomo katika Shule za Msingi Tanzania Bara. TET: Dar es Salaam. ( Andiko Lisilochapishwa). 19

Taasisi ya Elimu Tanzania (TET). (2003). Ripoti ya Warsha ya Kudurusu Mada za Elimu Dhidi ya Ukimwi katika Masomo Chukuzi kwa Shule za Msingi na Sekondari. TET. Dar Es Salaam. Taasisi ya Elimu Tanzania (TET). (2004). NCDF: A Guide to Innovative Teaching and Learning. Dar Es salaam. (Unpulished Document). Tanzania Institute of Education. (TIE). (2004). National Curriculum Development Framework (NCDF): Core Document. Dar Es salaam. (Unpublished Document) Tanzania Institute of Education (TIE). (2004). NCDF. A Guide to Assessment and Examination. Dar Es salaam, (Unpublished Document). Tanzania Institute of Education (TIE). (2004). NCDF. A Curr iculum Guide to Primary Education. Dar Es salaam. (Unpublished Document). UNICEF. (2004). Report on Baseline Survey on Gender. Sexuality. HIV/AIDS and Life Skills in Basic Education in Tanzania Mainland. Dar Es salaam. (Unpublished Document). UNICEF. (20 03) The State of the World s Children. Division of Communication. New York. United Republic of Tanzania (URT). (2003). Education Sector Development Plan: Primary Education Development Plan: Designs for the Improvement of Quality of Primary Education. MOEC: Dar es Salaam, April 2003. (Unpublished Document) URT. (2001). Education Sector Development Plan: Primary Education Development Programme (2002-2006), Basic Education Development Committee (BEDC), July 2001 (Unpublished Document) 20