Karibu Katika Mazungumzo Kuhusu Mchakato wa Uhamasishaji Maendeleo ya Kanisa na Jamii CCMP/UMOJA Shabaha ya Mazungumzo haya Kuwafahamisha viongozi wa makanisa kuhusu Mchakato wa CCMP ambao umekuwa ukitumika kuliwezesha kanisa kutoa huduma kamilifu kwa binadamu Kuwafamisha viongozi wa makanisa vile Yesu alivyohudumu katika kumkomboa mwanadamu kiroho, kimwili na kiakili Kuleta mtazamo mpya katika huduma zetu CCMP ni Nini? CCMP yasimama kama Church and Community Mobilisation Process, (mchakato wa uhamasishaji Maendeleo ya Kanisa na Jamii) hii ni njia mojawapo inayotumika kuleta maendeleo katika jamii badala ya njia zile za kisekta zilizozoeleka ambayo inashabaha ya kumwezesha mtu au shirika kuondokana na umaskini wa kimawazo na ule wa kimwili akitumia raslimali zilizoko katika maeneo anamoishi. Ambapo;- UMOJA ni makala iliyoandaliwa kumwezesha mtu anayehamasisha atoe mafundisho hayo ya uhamasishaji 1
? kiakili Kiroho kijamii Kimwili Maskini ni mtu ambaye hana uwezo wakujiamulia mwenywe hali anayotaka katika maisha yake ya kiroho, kimwili, kijamii ama kiakili. Umaskini huu unaletelezwa na udhaifu wa kimwili, kipato duni, uhusiano mbovu kati yake na Mungu wake na majirani, ushawi mdogo kwa jamii yake, Conversation kutokuwa - Arusha na elimu nk Kanisa lipofahamu maana ya umaskini litahudumu kama Yesu alivyofanya Je huduma ya Yesu ililenga maeneo gani ya maisha ya binadamu? Soma Math 9:35 Maswali ya kujiuliza leo 1. Kanisa limekuwa na mtazamo gani wa huduma kwa leo? 2. Je makanisa yetu leo yanatoa huduma kamilifu kwa watu kama Yesu alivyofanya? Kama siyo 3. Basi ni ujumbe gani leo kanisa lapeleka kwa jamii? Kwa nini ujumbe wetu ni tofauti na ule Yesu alifanya? 4. Je ni mambo gani kanisa leo lapaswa kufanya ili kuhudumia jamii inayolizunguka kwa ukamilifu kama vile Yesu alifanya? 2
Kwa nini njia ya CCMP ni Muhimu kwa Kanisa? Muda mwingi makanisa yamekuwa yakielezea umuhimu wa kutoa huduma kamilifu kwa binadamu kwa nadharia tu. Utaskia wakiongelea habari ya kuwahudumia watu kiroho, kimwili, kiakili na kijamii. Uelewa huu umekuwa ni wa kinadharia pasipo kuelewa hasa maana halisi ya huduma kamilifu kuwa ni kitu gani! Hivyo kupitia mchakato wa CCMP huduma kamilifu imeeleweka wazi kwa wakristo na viongozi wao kama ifuatavyo;- Uelewa wa kawaida wa watu juu ya huduma kamilifu kwa binadamu umekuwa ni;- Upatikanaji wa;- chakula Makazi ya kujistili mavazi Afya njema Elimu Maji, nk. Ambapo mtazamo wa Mungu juu ya maisha ya Mwanadamu ni (Isaya 65:17-25) 3
Kwa hiyo malengo ya CCMP ni yapi? Kusudi la CCMP: - kujenga uwezo wa watu wachukue jukumu la kuamua hatima ya maisha wanayoyatamani wakihoji wanatoka wapi, wako wapi sasa, wakitazama kwa kina visababishi vya umaskini, raslimali walizopewa na Mungu katika mazingira yao, na kuzitumia kutekeleza shughuli zinazopelekea kubadili hali ya maisha yao ya baadaye 2King 7:3-6 Lengo la CCMP: - kuwezesha kanisa la Mtaaa kufanyika nuru na chumvi kwa jamii inayolizunguka kwa kuwakwamua wanajamii waondokane na umaskini Mat 5:13-16 Hatua za mchakato wa CCMP: - mchakato wa CCMP unahatua kuu tano kama inavyoelezwa katika Kitiini cha Umoja. Hatua ya kwanza inashughulika na kuamsha kanisa liwe na maono ya huduma kamilifu kwa binadamu, ya pili ni kuamsha jamii kujitambua hali yake ilivyo, hatua ya tatu ni kuota ndoto za mabadiliko wanayoyatamani na kuweka mipango ya namna ya kuyafikia matamanio yao, hatua ya nne ni kutekeleza mipango waliyojiwekea na mwisho kufanya tathimini kuona kama makusudio yao yamefikiwa. Kanisa linapopitia mchakato wa namna hii huanza kuajibika kwa hali yake na kuchukua jukumu la kuiongoza na kuihamaisha jamii ijiletee mabadiliko kwa kutumia raslimali walizopewa na Mungu ili kukidhi mahitaji yao. Mbinu zipi hutumika katika kuhamasisha jamii na kanisa? Njia kuu zinazotumika kuhamasisha kanisa na jamii hasa hasa ni njia shirikishi na uwezeshaji;- Mitaala ya Biblia hasa hasa hii hutumika kanisani kama vile mitaala ya Msingi, mitaala ya raslimali, mitaala ya kujenga mahusiano nk, (Mat 5:13-16; 2king 4:1-7; Mat 4:12-13,23-25; 9:35-38;) Mbinu zakujieleza na uchambuzi wa taarifa na takwimu, e.g. Mtiririko wa matukio, ramani, ramani ya raslimali, siku ya kawaida, jinsia, maigizo, nyimbo, kalenda ya majira ya mwaka, uchambuzi wa taasis, majedwali, madodoso, mikutano ya hadhara, maswali ya uchambuzi, nk Kupatia mafunzo na mbinu za kuwezesha kanisa/jamii timu yawawezeshaji iliyochanguliwa na dayosisi; hawa ndio wahamasishaji wa maendeleo hasa katika kanisa na jamii wakiwezesha watu kujikwamua kimaisha Waajibikaji wakuu katika kufanikisha mchakato huu ni nani? Uongozi wenye maono yenye huduma kamilifu Wawezeshaji wenye uelewa na ujuzi juu ya huduma kamilifu na CCMP Kanisa la mtaa na jamii ( wanufaikaji na watekelezaji wa mpango wa huduma kamilifu 4
Mihimili au nguzo za CCMP Mabadiliko ya jumla ya maisha ya watu Badiliko la maisha ya mtu kiroho na kimwili Badiliko la utu wa mtu siyo vitu vya juu juu tu Badiliko la kimtazamo au fikra Mungu anayatazamaje maisha yake, uhusiano wake na wengine pia nafsi yake mwenyewe Uhusiano mwema unaotenda kazi Suala la mahusiano bora katika mchakato huu ndio kiini cha mabadiliko halisia yaletayo tija Uhusiano mwema na Mungu. Uhusiano mwema na watu wengine. Uhusiano mwema na mazingira anapoishi ama anamoishi Endelevu Mabadiliko ya muda mrefu. Maendeleo yanayomilkiwa na watu wenyewe, maendeleo yanayoendeshwa na jamii husika. Maendeleo yanayozingatia manufaa kwa vizazi vijavyo. 5
Kujenga uwezo wa watu Watu wajigundulie wenyewe Watu wachukue jukumu la kubadilisha hali ya maisha yao wenyewe. Watu wawe na sauti wakitoa mawazo yao kwa uhuru Watu waamue juu ya hatima ya maisha yao wenyewe. Siyo kuwapunguzia maumivu, bali kuwaachilia!!! (not relief, but realize) Unasisitiza juu ya Mchakato badala ya matokeo Mabadiliko ya watu badala ya vitu. Kuambatana na watu sio kuwaendesha (kuwatumia) katika safari yao ya mabadiliko licha yakuwa itachukua muda mrefu. Kutembea katika mwendo ambao jamii inauweza. Hatua kwa hatua tembea ili wajigundulie. Siyo vitu, bali mabadiliko ya maisha ya watu kwanza Wafikie utambuzi wa fursa walizopewa na mwenyezi Mungu Watambue mabadiliko wanayoweza kuyafikia. Wachukue hatua za utekelezaji ili kusababisha mabadiliko wanayoyatamani yawepo. Wafurahie na kushangilia mafanikio wanayoyapata (wamtukuze Mungu). 6
Kanisa la mtaa kuleta mabadiliko ya maisha ya watu mahali lilipo Kanisa la mtaa kama wakala ama chombo cha Mungu cha kusababisha mabadiliko chanya katika maisha ya watu. Kanisa la mtaa likiwasha moto na kuchochea maendeleo kwa jamii inayolizunguka ile kuleta mabadiliko ya hali ya maisha. Mkristo mmoja mmoja akitekeleza wajibu wake katika kuiwezesha jamii kuwa na maendeleo chanya ya kimaisha Wawezeshaji Mahiri Waliobadilika ili kuwa mawakala wa kubadilisha wengine Wawezeshaji waliofunzwa vyema na wanamzigo wa kuleta mabadiliko kamilifu kwa watu. Wawezeshaji waliobadilishwa na mafunzo na wanashauku ya kuona mabadiliko hayo yanatokea katika maisha ya watu wengine. Wawezeshaji walio na uwezo wa kuzalisha wawezeshaji wengine (2 Tim 2:2). Manufaa yanayoletwa na mchakato wa CCMP 7
Manufaa yanayoletwa na mchakato wa CCMP Manufaa yanayoletwa na mchakato wa CCMP MWISHO Maswali na Majibu Asante kwa kunisikiliza 8