Draft 03 MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO MWENGE

Similar documents
GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Information for assessors (do not distribute this page to participants):

In the matter of an Application by the KIGOMA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (KUWASA) For a Tariff and Charges Adjustment

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

In the matter of Application by the TANGA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (TANGA UWASA) For a Multi-Year Tariff Adjustment

MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2017/18

MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA PRO-ROUTES. Ombi kwa ajili ya fedha za umma wa mradi wa ziada

TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM)

Miradi na jamii. 3.1 Utangulizi

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU

JAMHURI YA KENYA. Mkakati wa Ushirikiano MUKHTASARI FY Public Disclosure Authorized. Public Disclosure Authorized

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO

ORDER NO BACKGROUND

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame M. Mbarawa (Mb.); Waheshimiwa Mawaziri na Wabunge wote mliohudhuria;

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA NISHATI NA MADINI

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU

TANZANIA MARKETS PAN Sera zinazoboresha masoko

NGUZO KUMI ZA KILIMO KWANZA

Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA 2006/07

KAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI TANZANIA

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig

Dibaji ya Mwenyekiti wa Kamati ya Pamoja ya Uongozi

Songa kwenye kilele cha upeo. Masuala ya Msingi na Ujuzi juu ya Uendeshaji wa Serikali za Mitaa

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA MHESHIMIWA DKT

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE

MAADHIMISHO YA MIAKA 15 YA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II

3. Mheshimiwa Spika, 4. Mheshimiwa Spika,

Mwongozo wa Kanisa la Waadventista wa Sabato

Shabaha ya Mazungumzo haya

UFUATILIAJI WA MIRADI NA TATHMINI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA FEDHA

TAARIFA YA MWAKA YA UTENDAJI KAZI IDARA YA UTAWALA BORA 2013/2014

Programu ya Uendelezaji Mifumo ya Maji Vijijini (PUMMV) katika Tanzania. Modeli wa Ukodishaji Mradi

Mipango ya miradi katika udugu

Taarifa Kuhusu Hali ya Uchumi wa Tanzania

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees

KITEGO CHA MAREKEBISHO NA HAKI ZA MTOTO

Human Rights Are Universal And Yet...

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA

Azimio lililopitishwa na Mkutano Mkuu tarehe 18 Desemba 2013 [juu ya taarifa ya Kamati ya Tatu (A/68/456/Add.2)]

KIMAZINGIRA NA KIJAMII NA MPANGO WA UDHIBITI

MAPENDEKEZO YA MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA TANZANIA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA. Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo. TOLEO Na.

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

SautiElimu. Sauti Yako Isikike

Nilikua na Ndoto ya Kumaliza Shule Changamoto za Elimu ya Sekondari Tanzania

MAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI

ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA UCHUMI WA ZANZIBAR

Kimesanifiwa na:- E.D.Kissuu ECOMM TANZANIA S.L.P ,Dar es Salaam. Simu:

UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA)

Summaries of GC Reports 2012, Vol. 2, Sec. 1, Swahili

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

5. Mheshimiwa Spika, Bunge lako Tukufu lilijadili kwa kina Miswada ifuatayo:

Kitabu Cha Mafunzo Ya Uongozi Kwa Wanawake

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TIST HABARI MOTO MOTO

RIPOTI YA WARSHA KUHUSU HABARI KWA AJILI YA UWAJIBIKAJI

Tufundishane! Mwalimu Bora In this issue: Issue 6, December Do you want to be in our next issue?

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )

Ufanisi katika Ufundishaji kwenye Shule za Msingi na Sekondari nchini Tanzania

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )

KUHUSU AFRODAD. Dira ya AFRODAD. Dhamira ya AFRODAD. AFRODAD inalenga mchakato sawa na endelevu wa maendeleo kuelekea Afrika yenye mafanikio.

RIPOTI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI

Kuuelewa Mchakato wa Bajeti Tanzania Mwongozo wa Asasi za Kiraia

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

Kufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, MHESHIMIWA DKT. PHILIP I. MPANGO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA III VI

KUSHUKA KWA HADHI YA LUGHA ZA JAMII NCHINI TANZANIA YOHANA P. MSANJILA University of Dar es Salaam, Tanzania

Deputy Minister for Finance

Dodoma ambako kikao cha Bunge kinaendelea kuja kushiriki japo sehemu ya uzinduzi wa mkutano.

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

Sera ya Faragha. Upeo. Aina za Data na Mbinu za Ukusanyaji

Mhashamu Askofu Jude Thaddaeus Ruwa ichi, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania; Mwadhama Policarp Kardinali Pengo,

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

Kutetea Haki za Binadamu

MWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI

Mwongozo wa Kutathimini mifumo ya Ugawanaji wa faida na Mapato Katika Miradi ya Jamii ya MKUHUMI

MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA. Kwa Wanaoanza

Unyanyasaji wa Watoto & Kutelekezwa

TIST HABARI MOTO MOTO MAANDALIZI YA MWAKA 2000 Y2K PREPARATIONS SASA NI WAKATI WA KUANZA KUPANDA MBEGU ZAKO

TAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF) KUHUSU HAKI ZA WATOTO KATIKA KATIBA MPYA

Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara)

TANGA CEMENT PLC ANNUAL REPORT TAARIFA YA MWAKA.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI-TAMISEMI HALMASHAURI YA WILAYA BUMBULI

IBADA NA UMOJA WA KANISA Na Mchg. Dkt. Msafiri Mbilu

Mwongozo wa Jamii juu ya Afya ya Mazingira

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Uzio wa pilipili unazuia tembo kuvamia mazao shambani! Jinsi ya kujenga na kudumisha uzio wa pilipili Tanzania

Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali ya Madini Ukanda

HOTUBA YA WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA MHESHIMIWA DKT

Mwongozo wa Utekelezaji wa Njia za S5-UUE (KAIZEN)-UUU Tanzania

GRACE COMMUNION INTERNATIONAL KANUNI YA IMANI

Transcription:

MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO MWENGE MPANGO MKAKATI WA MIAKA MITANO WA MAENDELEO YA KANISA 2013-2017 i

YALIYOMO 1. UTANGULIZI... 1 1.1 Lengo kuu... 1 1.2 Historia kwa ufupi... 1 1.3 Malengo ya mkakati... 2 Rasilimali za Kiroho... 4 1.3.2 Rasilimali Watu... 5 1.3.3 Rasilimali Fedha... 6 1.3.4 Rasilimali Miongozo... 6 1.3.5 Mradi wa kusambaza kitabu cha Pambano Kuu... 7 1.3.6 Miradi mikuu ya ujenzi... 7 2. DHIMA, DIRA, NA KAULI MBIU... 8 2.1 Dhima (Mission)... 8 2.2 Dira (Vision)... 8 2.3 Kauli mbiu (Mission Statement)... 8 3. MPANGO MKAKATI WA MIAKA MITANO KUANZIA 2013-2017... 8 3.1 Mfumo wa uongozi... 8 3.2 Idadi ya washiriki na Makisio ya ukuaji wa kanisa kuanzia 2005-2020... 9 3.3 Mambo muhimu (Key issues)... 10 3.4 Mikakati ya kukabili changamoto zilizoainishwa... 11 4. MAENEO YA UTEKELEZAJI KIMKAKATI... 11 4.1 Uwakili... 11 4.2 Huduma za Kanisa... 12 4.3 Elimu... 12 4.4 Vijana... 12 4.5 Shule ya Sabato... 12 4.6 Huduma za watoto... 13 4.7 Afya... 13 4.8 Kwaya za Kanisa na vikundi vya uimbaji... 13 4.9 Ofisi ya Karani wa Kanisa... 13 4.10 Mawasiliano... 14 4.11 MIUNDO MBINU (Majengo ya kanisa, vyoo, viwanja)... 14 4.11.1 Hali ilivyo sasa... 14 ii

4.11.2 Maboresho ya Miundombinu (Majengo, Viwanja)... 14 4.11.3 Uboreshaji wa mandhari ya eneo na Jengo la Kanisa (Mwenge)... 14... 15 4.11.3.1 Faida na Hasara za mapendekezo ya upanuzi wajengo la kanisa la sasa... 15 4.11.4 Ujenzi wa Jengo la matumizi anuai... 16 4.11.5 Majengo Kanisa Makundini... 16 4.11.6 Ukarabati wa nyumba ya mchungaji... 17 4.11.7 Ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi makao mapya ya ETC... 17 5. MIKAKATI YA KUPATA FEDHA KWAAJILI YA MIRADI YA MAJENGO... 17 5.1. Kuanzisha mfuko maalum wa maendeleo ya kanisa... 17 5.2 Kikosi kazi cha watu 100-200... 18 5.3 Washiriki wote wa kanisa kuhusishwa... 18 5.4 Changizo kutoka watu wa nje ya kanisa kwa njia ya harambee... 18 6. RAMANI YA UTEKELEZAJI... 19 6.1 Ramani yaa kila mwaka ya utekelezaji wa mpango mkakati... 19 6.2 Ramani ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi kwa mwaka 2013... 21 7. BAJETI YA UTEKELEZAJI MPANGO MKAKATI... 23 8. VIELELEZO NA VIAMBATANISHI... 26 8.1 Ramani ya upanuzi wa Kanisa (Sehemu za office... 26 8.2 Picha au mtazamo wa kisanifu katika picha za pande tatu (3D Views photos)... 28 iii

1. UTANGULIZI Mpango ni mfumo wa kimaandishi unaoonesha kazi zinazotakiwa kufanywa na hatua mbalimbali za kufikia malengo yaliyowekwa kwa muda maalumu. Mpango mkakati husaidia ufanisi katika utekelezaji na kuweka mpangilio mzuri wa matumizi ya rasilimali. Pia husaidia kuratibu kazi zote ili kufikia malengo kwa kuweka vipaumbele. Ni muhimu sana kuwa na mpango mkakati kwa kuwa utatupatia mwelekeo wa ni wapi tunataka kwenda na tutafika kwa namna gani. Shughuli mbalimbali na maeneo ya kimkakati huwekwa bayana, hii inasaidia kufahamu nyenzo na raslimali zinazohitajika na namna ya kuzipata. Ugawaji wa majukumu na dhamana miongoni mwa viongozi au washiriki ni moja ya faida za kuwa na mpango kazi. Mipango mkakati huwezesha kufanya tathmini kuona kama malengo na mipango tuliyojiwekea imefanikiwa au haikufanikiwa kama ilivyopangwa. Kanisa la Mwenge limekuwa na mipango ya muda mfupi mfupi hususani kila mwaka, hali ambayo haiwezi kutoa dira endelevu kwa kanisa. Hivyo mpango huu ni hatua muhimu katika kulipatia kanisa dira ya kuliongoza katika mipango mbalimbali bila kujali mabadiliko ya uongozi yanayofanyika kila mwaka. Hii italiwezesha kanisa kuwa na mipango endelevu itakayokuwa ikitekelezwa na kila uongozi unapoingia madarakani wakati wa uhai wa mpango husika. 1.1 Lengo kuu Lengo kuu la mpango mkakati huu ni kuliongoza katika uendeshaji wa majukumu yake makubwa ambayo ni: malezi ya washiriki kiroho, uinjilisti, uwakili na majengo kwa kuweka malengo mahususi na namna ya kufikia malengo hayo ifikapo mwaka 2017. 1.2 Historia kwa ufupi Kanisa la Waadventista wa Sabato Mwenge ni miongoni mwa makanisa mengi ya waadventista wa Sabato Tanzania ambalo liko katika eneo la Mwenge, kando kidogo mwa barabara mpya ya Bagamoyo, likipapakana na zahanati ya Mwenge kijijini wilaya ya Kinondoni, Jijini Dar es Salaam. Kanisa lilianza mwaka 1967 likiwa ni tawi la Shule ya Sabato Lugalo Sergeant Mess. Tawi liliendelea hadi mwaka 1980 lilipopewa hadhi ya kuwa Kundi la Shule ya Sabato. Kutokana na matatizo yaliyojitokeza ya kutokuwa na uhuru wa kuingia eneo la jeshi kufanya ibada, mwaka 1981 likawa ni kundi la Kanisa la Magomeni na kuendelea kukua hadi Juni mwaka 1985 lilipotengwa rasmi kwa kupewa hadhi ya kuwa Kanisa kamili na hivyo kutambuliwa rasmi kuwa miongoni mwa makanisa mahalia ya Waadventista wa Sabato ulimwenguni. Kanisa liliendelea kukua kwa kuanzisha makundi ambayo nayo yalitengwa kuwa makanisa. Makanisa ambayo ni zao la Mwenge ni pamoja na Ushindi, Bagamoyo, Lugalo, Tegeta, Mbezi Beach, Mbezi juu, Kerege na Bunju. Kwa sasa Kanisa lina makundi 7 ambayo ni: Bumafa, Chivilikiti, Mabwepande, Zinga, Amani, Kimele na Vikawe; pia kuna tawi moja la shule ya Sabato katika shule ya sekondari ya Lord Barden. Hadi kutengwa kuwa Kanisa, Kanisa halikuwa na nyumba ya kuabudia, hivyo juhudi zilifanyika za kutafuta kiwanja na 1

hatimaye kiwanja kilipatikana eneo la Mwenge na ujenzi kuanza rasmi mwaka 1989; jengo la Kanisa kwa wakati huo lilisanifiwa kuwa na uwezo wa kuchukua waumini 900 wakiwa wamekaa, ujenzi uliendelea hadi mwaka 2000 ulipokamilika. Baada ya shughuli za ujenzi kukamilika, utaratibu wa kuliweka wakfu ulifanyika. Tarehe 22-12-2002 jengo la kanisa liliwekwa wakfu rasmi; huduma hiyo ilifanywa na Mchungaji Dr. Herry Mhando. Idadi ya washiriki imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka licha ya washiriki wengine kuhamia makanisa mengine, idadi ya washiriki hadi kufikia Juni mwaka 2012 ilikuwa ni 2,330. 1.3 Malengo ya mkakati Kwa kipindi cha kuanzia 2013 2017 kanisa linaazimia kuwa na maeneo makuu ya kimkakati yafuatayo: A: Rasilimali za kiroho B: Rasilimali watu Lengo #1: Kuongeza washiriki kwa 100% ifikapo 2017 Lengo #2: Makundi yaliyopo sasa kuwa makanisa ifikapo 2017 (Zinga, Mabwepande, Kimele, na Bumafa) Lengo #3: Kuimarisha na kuyawezesha makundi kujitegemea ifikapo mwaka 2017 au baadaya 2017 Lengo #4: Kuwa na 60% ya washiriki wanaosoma Biblia, Lesoni ifikapo 2017 Lengo #5: Kuhakikisha kuwa 70% ya washiriki wana ufahamu mpana kuhusiana na mtindo na mwenendo wa maisha ya ki-adventista katika nyanja za afya, elimu, vyakula na vinywaji, na maburudisho. Lengo #1: Kuelimisha Wainjilisti Walei 15 wanaoweza kutumwa kama wainjilisti ifikapo mwaka 2017. Lengo #2: Kusomesha wanafunzi wawili elimu ya uchungaji ifikapo mwaka 2017 Lengo #3: Kuhakikisha kuwa asilimia tisini (90%) ya wahubiri wawe na elimu ya homilia ifikapo mwaka 2017 C: Rasilimali fedha Lengo #1: Kuhakikisha idadi ya washiriki wanaorudisha zaka na wanaotoa kwa mpango inaongezeka mara tatu zaidi ya miaka ya nyuma ifikapo 2017 Lengo #2: Kuwezesha asilimia sabini (70% ) ya washiriki wasio na ajira na wale wenye kupenda kujianjiri na kuanzisha biashara wawe na elimu ya ujasiriamali ya ujasiliamali ifikapo 2017. 2

D: Rasilimali miongozo Lengo: Kuhakikisha kuwa 100% ya washiriki wanafundishwa na kuelewa misingi 28 ya kanisa; waumini na viongozi wawe wamefundishwa kufuata sera na taratibu za kanisa, na washiriki wawe ameelimishwa kuhusu utumiaji wa maandishi ya Roho ya unabii ifikapo 2017. E: Mradi wa kusambaza kitabu cha Pambano Kuu Lengo: Kuhakikisha vitabu 20,000 vinanunuliwa na kusambazwa. F: Miradi mikuu ya ujenzi Lengo #1: Kufanya ukarabati mkubwa wa jengo la kanisa na kukamilisha ujenzi wa majengo ya ibada makundini. Lengo #2: Kukarabati nyumba ya mchungaji Lengo #3: Ujenzi wa nyumba ya mkurugenzi makao mapya ya ETC. Lengo #4: Ujenzi wa Jengo la Ustawi wa Jamii Kwa kila eneo la kimkakati malengo mahsusi yameainishwa katika jedwali hapa chini. 3

Rasilimali za Kiroho MPANGO MKAKATI MHUSIKA MUDA Lengo 1: Semina za uinjilisti kwa washiriki kanisani na makundini - Mzee wa kanisa Kuongeza washiriki kwa 100% mara moja kila robo -Mkuu wa ifikapo 2017 Unijilisti kwa njia ya machapisho ikihusisha masomo kwa njia huduma za kanisa ya sauti ya unabii, vitabu, vijizuu na magazeti. -Mkurugenzi Washiriki wa makundini wote Mikutano ya injili ya hadhara mitatu kwa mwaka, mmoja VOP wamejumlishwa ukifanyika kupitia radio ya Morning Star 105.3 FM. Uinjilisti kupitia shule ya sabato: -Mkurugenzi wa o S/Sabato o -Kiongozi wa o uchapishaji Vikosi vya shule ya sabato Sabato za wageni Kuanzisha matawi ya kujifunza biblia kwa kaya zilizo karibu na kuhusisha wasio washiriki pia. Elimu ya dini shuleni-vipindi vya dini (uinjilisti na malezi) o kufikia kila shule iliyopo katika eneo letu la kiutawala kuimarisha utaandaaji {kila idara/ chama knsn kuweka mkakati wa kuongoa roho} -Mkurugenzi wa Elimu -Kiongozi wa Champlensia -Sabato ya kwanza ya kila mwezi -Mwezi Aprili/Juni na Septemba/Okt. -Sabato ya 2 ya robo -kila Sabato -Mei/Oktoba Lengo 2: Kutenga makundi yaliyopo sasa kuwa makanisa ifikapo 2017 kuwaandaa washirki wa makundini kujitegemea kiroho, kiuchumi na kijamii. -Kiongozi wa Kundi/mzee wa kanisa -Sabato ya kwanza ya kila mwezi. (Zinga - 2013, Mabwepande - 2014, Kimele- 2015, Bumafa- 2016, na Vikawe 2017) Lengo 3: Kuimarisha na kuyawezesha makundi kujitegemea ifikapo mwaka 2017 au baada ya hapo. Kuyajengea uwezo wa wa kuimarika, makundi mapya yaanzishwe pale tu inapobidi. Hii itatupati fursa ya kuyahudumia vyema makundi yaliyopo sasa kwa kuyawezesha kuwa na nyumba za ibada zilizokamilika na zenye kuleta utukufu kwa Mungu. Wazee wa kanisa/mchungaji Mara moja kila robo 4

Lengo 4: Kuwa na 60% ya washiriki wanaosoma Biblia na Lesoni ifikapo 2017 Lengo 5: Kuhakikisha kuwa 70% ya washiriki wana ufahamu mpana kuhusiana na mtindo na mwenendo wa maisha ya kiadventista katika nyanja za afya, elimu, vyakula na vinywaji, na, maburudisho. kuwatembelea washiriki nyumbani. kila mshiriki atembelewe angalau mara moja kwa mwaka. kuimarisha mfumo wa ukusanyaji wa lesoni kwa njia tofauti,,,mpesa kwa fue [[kila idara/chama itengeneze mkakati itakavyohusika na mpango]] Semina, mafundisho, na mahubiri - semina mara moja kwa mwezi muda wa mchana Wazee wa kanisa /mashemasi/... / /SS, utandaaji/ huduma Wazee wa kanisa /Mchungaji/ Kila sabato kupitia vipindi vya mchana Kila sabato kupitia vipindi vya mchana 1.3.2 Rasilimali Watu MPANGO MKAKATI MHUSIKA MUDA Lengo 1: Kuelimisha wainjilisti walei 15 wanaoweza kutumwa kama wainjilisti ifikapo 2017. Kuimarisha mfuko wa uinjilisti hasa kwenye eneo linalohusu udhamini wa mafunzo ya uinjilisti. Mchungaji wa Mtaa N/A Lengo 2: Kusomesha mwanafunzi wawili elimu ya uchungaji ifikapo 17. Lengo 3: 90% ya wahubiri wawe na elimu ya homilia ifikapo 2017 Kutenga sehemu kidogo kutoka katika bajeti ya kanisa Kutumia washiriki wa kanisa kuchangisha pesa Semina ifanyike mara moja kwa mwaka Mchungaji wa Mtaa Mratibu wa mpango atakayechaguliwa na uongozi wa kanisa Mchungaji wa Mtaa N/A Mara moja au mbili kwa mwaka 5

1.3.3 Rasilimali Fedha MPANGO MKAKATI MHUSIKA MUDA Lengo 1 Kuhakikisha idadi ya washiriki wanaorudisha zaka na wanaotoa kwa mpango inaongezeka kwa Mafundisho/mahubiri/Semina za zaka na sadaka kila mwezi (wiki ya mwisho) Kiongozi/Katibu wa Uwakili na Maendeleo kanisani Mara moja kila mwezi. Wiki ya mwisho ya kila mwezi asilimia hamsini (50%) ya Mchungaji washiriki. Wazee wa Lengo 2 Kuwezesha 70% ya washiriki wasio na ajira wawe na elimu ya ujasiliamali na wale wanaopenda kuanzisha na kuendeleza biashara wawe na elimu ya ujasiriamali. Washiriki wa ndani watumike kufundisha mara moja kwa kila robo na utaratibu maalumu uwekwe kuratibu semina hizo. ATAP wahusishwe katika kufanikisha azima hii kanisa Kiongozi/Katibu wa Uwakili na Maendeleo kanisani Kiongozi wa ATAP Mara mbili kwa kila mwaka 1.3.4 Rasilimali Miongozo MPANGO MKAKATI MHUSIKA MUDA Lengo: 1 Mahubiri/mafundisho na semina zifanyike mara mbili kwa robo Mchungaji Kila sabato Kuhakikisha kuwa 100% ya Washiriki waelezwe kuhususiana na vitabu bora na vya uhakika Wazee wa kupitia vipindi washiriki wanafundishwa na ambavyo havikuchakachuliwa. kanisa vya mchana na kuelewa masomo muhimu Kiongozi wa pia kupitia yafuatayo : Roho ya unabii mahubiri ya misingi 28 ya kanisa ibada kuu. kufuata sera na taratibu za kanisa utumiaji wa vitabu vya Roho ya Unabii. 6

1.3.5 Mradi wa kusambaza kitabu cha Pambano Kuu MPANGO MKAKATI MHUSIKA MUDA Lengo: 1 Kuhakikisha vitabu 20,000 vitanunuliwa na kusambazwa. Uhamasishaji na kila mshiriki ahakikishe amechangia angalau vitabu 5 kila mwaka kwa miaka mitano hadi 2017. Mkurugenzi wa Uchapishaji kanisani Mara moja kila robo ya mwaka. 1.3.6 Miradi mikuu ya ujenzi MPANGO MKAKATI MHUSIKA MUDA Lengo: 1 Kufanya ukarabati mkubwa wa jengo la kanisa na kukamilisha Kukusanya michango kutoka kwa washiriki au familia hadi 200 watakao kuwa tayari kuchangia shilingi 1,000, 000 kila mmoja kwa mwaka. Kiongozi / kamati ya majengo ujenzi wa majengo ya ibada Kwa kutumia michango kutoka kwa washiriki wote Mzee wa makundini. Changizo kutoka kwa watu mbalimbali ndani na nje ya kanisa kanisa Lengo: 2 Kukarabati nyumba ya mchungaji Lengo: 3 Ujenzi wa nyumba ya mkurugenzi makao makuu mapya ya ETC. Lengo: 4 Ujenzi wa Jengo la Ustawi wa Jamii Kutumia sehemu ya bajeti ya kanisa kadri itakavyoamuliwa na baraza la kanisa na, au mashauri ya kanisa kulingana na mgawanyo wa mtaa Michango ya washiriki Kutumia sehemu ya bajeti ya kanisa kadri itakavyoamuliwa na baraza la kanisa na au mashauri ya kanisa Michango ya washiriki Kukusanya michango kutoka kwa washiriki au familia hadi 200 watakao kuwa tayari kuchangia shilingi 1,000, 000 kila mmoja kwa mwaka. Ramani ya jengo na michoro yote iwe tayari ifikapo Septemba 2013 (Architectural drawing, Structural drawing, Plumbing drawings, Electrical drawings) Kamati ya uwakili- (Maendeleo) Kamati ya majengo Mzee wa kanisa Kamati ya majengo Mzee wa kanisa Kiongozi / kamati ya majengo kanisa la Mwenge Mzee wa kanisa Endelevu hadi lengo lifikiwe kwa kuanzia na mwaka 2013 Wakati wowote itakapohitajika Wakati wowote itakapohitajika Endelevu hadi lengo lifikiwe 7

2. DHIMA, DIRA, NA KAULI MBIU 2.1 Dhima (Mission) Dhima yetu ni kutekeleza agizo kuu la utume wa Yesu la Mathayo 28:19,20 na kushuhudia ujumbe wa malaika watatu wa Ufunuo 14:6-12 kwa watu wa mataifa yote ili wampokee Yesu kuwa Bwana na mwokozi wao na waweze kujiunga na kanisa la Mungu la masalio kuhudumia jamii na kujiweka tayari kwa marejeo yake mara ya pili. 2.2 Dira (Vision) Kuwa kanisa la mfano nchini Tanzania na duniani lenye kumpenda Mungu na kushuhudia upendo wake kwa ajili ya wokovu wa kila mmoja kabla ya marejeo yake mara ya pili kuwachukuwa wateule wake mbinguni (Mathayo 22:37-39). 2.3 Kauli mbiu (Mission Statement) Kutangaza injili ya milele kwa watu wote katika muktadha wa ujumbe wa malaika wa tatu wa Ufunuo 14:6-12. 3. MPANGO MKAKATI WA MIAKA MITANO KUANZIA 2013-2017 3.1 Mfumo wa uongozi Kanisa la Mwenge linaongozwa na Mchungaji anayesaidiana kwa karibu na wazee wa kanisa ambao wanawajibika kwa baraza la kanisa katika kuongoza shughuli za kila siku za kanisa. Kikao kikubwa cha maamuzi ya mwisho ni mashauri ya kanisa ambayo ndiyo kikao kikubwa chenye kufanya maamuzi muhimu kwa ajili ya kanisa. Muundo wa uongozi uko kama ulivyoonyeshwa kwenye mchoro hapa chini. 8

Baraza la Mashauri ya Kanisa Baraza la Kanisa Wazee wa Kanisa Mchungaji Maofisa wasimamizi (Karani mkuu, Mhazini, Shemasi mkuu Maofisa watendaji (Wakuu wa Idara za Kanisa) 3.2 Idadi ya washiriki na Makisio ya ukuaji wa kanisa kuanzia 2005-2020 Kwa mujibu wa taarifa ya mwezi June 2012 kanisa la Mwenge lina washiriki wapatao Katika kipindi cha miaka mktano iliyopita idadi ya washiriki ilikuwa kama ifuatavyo: Mwaka Idadi ya washiriki 2007 2008 2009 2010 2011 June 2012 Kwa kuzingatia ukuaji wa kanisa kwa ongezeko la watani wa washiriki.. kwa mwaka. Matarajio ya ongezeko la washiriki ifikapo mwaka 2020 ni washiriki wapatao Hii inaleta changamoto ya miundo mbinu hasa jengo la ibada kukabiliana na ongezeko hili. 9

3.3 Mambo muhimu (Key issues) Ili kujiweka katika mazingira ya kujitambu na kuweka malengo na mbinu za kusonga mbele, mambo muhimu yameainishwa hapa chini kuonyesha uwezo wetu, udhaifu na fursa tulizo nazo. Hii itatuwezesha kupanga na kutekeleza maeneo ya vipaumbele. Uwezo tulionao Washiriki Kanisa lina idadi kubwa ya washiriki wa jinsi zote za na rika zote Kanisa lina washiriki wengi wenye taaluma na ujuzi mbalimbali Kanisa lina washiriki wenye uchumi mzuri kwa maana ni waajiriwa na wafanya biashara Kanisa lina washiriki wenye mwitikio wa kujitoa kufanya kazi ya Mungu na kuchangia maendeleo ya kanisa katika nyanja mbalimbali Mali za kanisa Kanisa lina mali kadha ikiwemo viti, meza, vyombo vya meza ya Bwana, na vyombo vya mawasiliano. Pia lina Majengo ya kanisa japo yanahitaji kukarabatiwa na viwanja vya kanisa Uzoefu (kuanzia mwaka 1981) Kanisa linauzoefu wa muda mrefu wa kuanzia mwaka 1981, hii ni takribani miaka 31 Tuko mjini kijiografia Kanisa liko sehemu nzuri kijiografia na linafikika kwa urahisi kutoka pande zote za jiji la Dar es Salaam. Udhaifu na changamoto Kanisa halina mipango endelevu Utunzaji hafifu wa kumbukumbu mbalimbali za kanisa Mawasiliano hafifu kunasababisha muingiliano wa majukumu Mahudhurio hafifu sana katika vipindi vya mchana Udhaifu katika utunzaji wa wakati kwenye ibada Udhaifu katika makabidhiano ya kazi mwisho wa mwaka, Udhaifu katika kutayarisha na kuwasilisha taarifa kwa wakati hasa za kila robo Mabadiliko ya mara kwa mara ya uongozi kwa mujibu wa taratibu zilizoainishwa na kanuni ya kanisa. Kushindwa kufahamu washiriki walipo, wanapoishi na uwezo wao kiuchumi Kufuatilia michango mbalimbali itolewayo na washiriki hususani ahadi Mahudhurio hafifu ya washiriki katika vikao vya mashauri ya kanisa 10

Fursa zilizopo Kuweka miradi ya kanisa kwenye maeneo tuliyonayo Kuweza kutumia rasilimali watu tulionao na rasilimali walizo nazo washiriki Tunao marafiki wetu wengi wanaoweza kutuchangia na kutusaidia Changamoto Kukusanya rasilimali fedha kutoka ndani na nje ya kanisa (zaka, sadaka, na michango mingine) Kuwafikia washiriki wote na kuwetambelea Urasimu uliopo - tukitaka kufanya mambo yetu kwa wakati tunahitaji kupitia utaratibu wa kirasimu kiuongozi Mfumo wa uchaguzi inaonekana kuwa washiriki wanachaguliwa katika nafasi mbalimbali za uongozi ni walewale karibu kila mwaka. 3.4 Mikakati ya kukabili changamoto zilizoainishwa Ili kukabiliana na changamoto zilizoainishwa, mambo yafuatayo yanapendekezwa: Kutumia madarasa ya shule ya sabato kuwafikia washiriki kwa njia ya kutembeleana Kuboresha mfumo wa uwekaji kumbukumbu wa kanisa (Database) Kuboresha mikakati ya ukusanyaji wa fesha za kanisa hasa katika maeneo ya majengo na uinjilisti. Semina zitolewe kuhusiana na uchaguzi wa maofisa wa kanisa Tuweke sehemu ya kutunza vitu na tuwaelemishe watu jinsi ya kutunza kumbukumbu Kutoa mafunzo ya utawala kwa maofisa wa kanisa Ili kuongeza na kuhamasisha utoaji wa zaka, sadaka na michango mingine, tangazo kuhusiu utoaji liwekwe kwenye jalida la matangazo (Bulletin) muda wote wa mwaka Washiriki watembelewe kuhimizwa kutoa zaka na sadaka na kufundishwa somo la uaminifu. Washiriki wote kuanzia kwa wachungaji, wazee wa kanisa na maofisa wote kuhimizwa kuzingatia uwakili wa muda katika utendaji. 4. MAENEO YA UTEKELEZAJI KIMKAKATI Kanisa litatekeleza mpango wa maendeleao unaohusisha idara zake zote za kanisa, na pia kuweka kipaumbele maeneo maalumu ya kimkakati. 4.1 Uwakili Uwakili ni eneo muhimu sana kwa ukuaji wa kanisa kiroho na kiuchumi kwa kuwa unahusisha kila kitu katika maisha ya mkristo. Baadhi ya mambo muhimu katika uwakili ambayo kanisa linapaswa kuboresha na kuongeza juhudi ni pamoja na: Uwakili wa wakati Kuwahi katika ibada za siku ya Sabato Kufuata muda katika ratiba za siku ya ibada Uwakili wa mali za bwana 11

Majengo ya kanisa, viti, mazingira Zaka na sadaka Uwakili wa uwezo alionao mtu/mshiriki mmoja mmoja. 4.2 Huduma za Kanisa Hudama za kanisa zinahusisha mipango inayolenga ukuaji wa kanisa kiroho na kuunganisha baadhi ya idara katika majukumu na utendaji, hii ni pamoja na kupanga: Mipango ya uinjilisti hususani mikutano ya hadhara Semina za malezi ya kanisa (kiroho) Uelimishaji kuhusiana na mambo mbalimbli ya uhai wa washiriki na kanisa kwa ujumla. 4.3 Elimu Katika kukabiliana na changamoto za elimu kwa watoto na vijana wetu, kanisa halina budi kuwa na mipango madhubuti kwa ajili ya kuanzisha shule za awali hadi za sekondary. Hivyo basi, kanisa azimia kuweka mipango ya elimu kama ifuatavyo: Kuanzisha shule ya chekechea Kuanzisha mfuko wa maendeleo ya elimu Kutoa huduma za elimu ya dini mashuleni 4.4 Vijana Vijana ni nguzo kubwa ya kanisa katika nyanja zote, hivyo wanapaswa kuandaliwa kulitumikia na kuliwezesha kanisa kupitia raslimali watu na fedha. Kwa hiyo, kanisa linakusudia kuwaimarisha vijana katika maeneo yafuatayo i. Kutoa mafunzo ya ujasiriamali ii. Kuongeza mafundisho ya kiimani ili kutengeza/kuandaa kanisa la kesho iii. Kuhamasisha vijana wengi zaidi washiriki kwenye vyama na shughuli zinazowahusu iv. Kuimarisha vyama vya vijana v. Kutumia vyama vya vijana kuwapa mafundisho ya ujuzi ili kukabiliana na changamoto za maisha 4.5 Shule ya Sabato Shule ya Sabato ni moyo na uhai wa kanisa. Kanisa linakusudia kuendelea kuboresha shule ya sabato kama ifuatavyo: i. Kuimarisha vikosi vya madarasa ya shule sabato ii. Kutembeleana na kufanya uinjilisti kule mitaani kwetu na uhamasishaji wa kusoma lesoni na biblia iii. Ualikaji wa wageni-liwe jambo la kudumu 12

4.6 Huduma za watoto Huduma za watoto ni jambo muhimu kwa kanisa na kwa jamii nzima. Huduma kwa watoto zinalenga kukuza imani ya watoto wakiwa hawajazaliwa hadi wafikishapo umri wa miaka 14 wakiongozwa na kukua katika maadili ya Kikristo na kutambua mfumo wa kanisa. Hivyo, kanisa litaendelea kuwapa umuhimu unaostahili watoto kwa kuwapa huduma za kiroho na kijamii ili wakue ndani ya kanisa wakiwa na madili yanayofaa wakionyesha mfano mzuri wakiwa watoto wakristo wa adventista. Hii ni kwa kuwa watoto wana upeo mwepesi wa kushika mafundisho ya injili na wana uwezo wa kuyaweka katika vitendo maishani mwao. 4.7 Afya Kanisa lina amini katika wajibu wa kumfanya Kristo ajulikane ulimwenguni ni pamoja na wajibu wa kiroho wa kutunza utu wa binadamu kwa kuhakikisha usalama wa afya yake kimwili, kiakili na na kiroho. Kanisa linakusudia kuendelea kutoa huduma za elimu ya afya kwa uana wake wote kwa nia ya kuzuia magonjwa na kutoa elimu ya afya itakayowawezesha washiriki kuwa na afya njema katika maisha yao hasa kuhusiana na vyakula, vinyaji na maburudisho. 4.8 Kwaya za Kanisa na vikundi vya uimbaji Huduma ya kwaya au nyimbo ni muhimu katika ibada kwa kuongoa roho kupitia ujumbe wa injili unaoimbwa katika nyimbo. Kanisa litadumisha huduma za kwaya na uimbaji kupitia vikundi vilivyojiambatanisha na huduma za uimbaji ili kuhakikisha kuwa nyimbo, na aina ya muziki wa dini unaimbwa na kupigwa kanisani unafuata misingi ya kiadventista. Kwa kuzingatia mafunuo na mafundisho kuhusu muziki, kanisa litasimamia weledi katika muziki wa kidini unaoimbwa na kwaya na vikundi vyote kanisani, na kuhakikisha kuwa uimbaji na upigaji wa ala za muziki usiofaa au usioendana na Biblia unaachwa mara moja, mfano midundo ya ngoma na mchanganyiko wa manyanga kwenye nyimbo unaachwa mara moja. Mkazo utawekwa katika kufundisha elimu ya muziki kwa waimbaji wote pamoja na mafunzo ya vinanda ili waimbaji waimbe nyimbo zilizochezwa kwa weledi mkubwa kwa kinanda pasipo kutumia midundo kuongoza muziki, bali muziki uongoze nyimbo. 4.9 Ofisi ya Karani wa Kanisa Hii ni ofisi muhimu sana katika uendeshaji wa shughuli za kanisa na utunzaji wa kumbukumbu.. Ofisi hii inatakiwa iwezeshwe kwa kupatiwa vifaa vya kisasa vya kufanyia kazi. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo ofisi hi itawezeshwa kwa kupatiwa nyenzo zifuatazo: 1. Kompyuta mpya 2. Printer yenye kasi (high speed printer) 3. Machine ya kudurufia (photocopier machine) 13

4.10 Mawasiliano Mawasiliano ni nyenzo muhimu katika kufikisha ujumbe kwa walengwa. Ili kuwepo mawasiliano mazuri kanisani, hatuna budi kujizatiti kuwa na vifaa bora nyenye kiwango cha juu cha ufanisi. Hivyo, kanisa linakusudia kuboresha mfumo wa mawasiliano kanisani kwa kununua vifaa vya kisasa vya mawasialino vifuatayo: i. Mfumo mzima wa vipaza sauti na nyenzo zake (Complete PA system and accessories) ii. Kununua kinanda kikubwa kwa ajili ya ibada (Church Piano/Organ) iii. Kununua LCD screen 4 za dijitali iv. Kununua vifaa vya ukalimani (Translation equipments) 4.11 MIUNDO MBINU (Majengo ya kanisa, vyoo, viwanja) Kanisa linakusudia kuweka msisitizo mkubwa katika kuimarisha miundo mbinu ya kanisa hasa majengo, viwanja na huduma msingi kwa kanisa na makundi yake yote, ili kuweka mazingira mazuri ya ibada na utendaji mzuri wa kazi ya Mungu. 4.11.1 Hali ilivyo sasa Kwa sasa jengo la kanisa linachakaa na kuhitaji kufanyiwa ukarabati na marekebisha makubwa ya sakafu, kuondoa paa la Asbestos, kurekebisha madirisha na kuangalia uwezekano wa kuweka vipoza hewa (air conditioning) kwa ajili ya kukabiliana na hali ya joto la Dar es salaam. Pia kiwanja cha kanisa hakijafanyiwa landscaping na kupanga vizuri maeneo kwa ajili ya kuegesha magari. Kanisa lina choo cha kisasa ambacho kipo katika hali nzuri na kinahudumiwa vizuri kwa usafi muda wote wa wiki. Kanisa pia lina kisima cha ubatizo ambacho hakiko katika hali nzuri kiafya. Hii inaleta changamoto ya kufanya maboresho katika kisima hiki. 4.11.2 Maboresho ya Miundombinu (Majengo, Viwanja) Kwa kuzingatia mahitaji ya baadaye ya kanisa, na hali ya sasa ya uchakavu wa kanisa; ni njozi yetu kuwa na mpango mkakati wa kuwezesha kanisa kuwa na nyumba nzuri ya ibada. Njozi hii ni pamoja na kufanya ukarabati mkubwa wa jengo la ibada la sasa kwa kuliongeza (kulipanua) au kwa kwenda juu (vertical extension) au kwa kulipanua kiusambamba (horizontal extension). Hii itaendana na uandaaji wa eneo la kanisa kwa ajili ya kutengeza mandhari ya eneo la kanisa na maegesho ya magari (landscaping and car parking lots). Kwa upande wa makundi, ni kusudi letu kukamilisha ujenzi wa nyumba za ibada katika makundio yote na kuweka vifaa muhimu kwa ajili ya ibada. 4.11.3 Uboreshaji wa mandhari ya eneo na Jengo la Kanisa (Mwenge) Kanisa lina azimia kuweka jitihada ya kuboresha mazingira ya eneo la kanisa. Maboresho hayo yatahusisha mabadiliko makubwa kwenye jengo la kanisa na mandhari yote ya eneo la kanisa. Kanisa linakusudia kufanya ukarabati mkubwa na maboresho kwenye jengo la sasa 14

ili kukidhi ongezeko la washiriki, na kuweka maeneo maalumu kwa ajili ya kinda na mafundi mitambo. Katika kutekeleza nia hii, yafuatayo yapaswa yatekelezwe: Kufanya upanuzi na maboresho ya eneo la kanisa utakaohusisha mambo yafuatayo: o Kuongeza nafasi kwa ajili ya office ya karani, mchungaji, mashemasi, wazee, na wahazini kwa kuongeza kwa mita tatu sehemu ya jengo la kanisa zilipo ofisi za sasa; o Kujenga ndani kisima cha ubatizo; o Kupanua kanisa ili kuongeza nafasi kwa ajili ya kuwezesha kuchukua watu wengi zaidi. upanuzi waweza kufanyika kwa kwenda juu (vertical extension) au kwa upanda upande (horizontal extension). Faida na hasara za kila kila chaguzi zimeainishwa katika kipengele 4.12.3.1 na 4.12.3.2 o Kuboresha sakafu kwa kuweka sakafu mpya ya kisasa na yenye kudumu muda mrefu; o Kurekebisha paa la kanisa na kuondoa asbestos; o Kutengeneza mandhari ya eneo la kanisa (landscaping); o Kujenga mfumo wa kutolea maji ya mvua; o Kuweka vipoza hewa kwenye ofisi zote za kanisa. Kufanya matengenezo ya uzio kwa kupaka rangi na kuweka bango elekezi la mawasiliano; Kutengeneza au kuboresha barabara ya kuingilia kanisani kwa kuweka moram na kushindilia; Kuweka uzio katika nyumba ya mchungaji. Kuweka uzio katika nyumba ya mlinzi (a) Sehemu ya kanisa ilivyo kwa sasa (b) Kisima cha ubatizo kinavyoonekana kwa sasa 4.11.3.1 Faida na Hasara za mapendekezo ya upanuzi wajengo la kanisa la sasa Upanuzi kwenda juu (Vertical extension) Faida zake Matumizi mazuri ya nafasi ya juu (good use of sky space) na eneo la kanisa halitapungua Jengo la kanisa litakuwa na mwonekano mzuri (aesthetics) 15

Changamoto zake Zinahitaji fedha nyingi kwa wakati mmoja ili kutekeleza Kanisa halitakuwa likitumika kwa ibada wakati wa ujenzi, hii itasababisha kanisa kuingia gharama kukodisha mahema ili kufanyia ibada nje wakati ujenzi ukiendelea kwa kipindi chote. Ujenzi lazima ufanyike wote kwa mara moja Upanuzi kwenda upende upande (Horizontal l extension) Faida zake Ibada wakati wa ujenzi zitaendelea ndani ya kanisa Haihitaji uwekezaji mkubwa sana na ujenzi unaweza kufanywa kwa awamu Changamoto zake Nafasi ya eneo la kanisa itapunguka Mwonekana wa kanisa hautakuwa mzuri (aesthetics) 4.11.4 Ujenzi wa Jengo la matumizi anuai Ujenzi wa jengo kubwa la kisasa kwa matumizi mbalimbali ya kanisa ikiwa ni pamoja na sehemu ya ibada kwa watoto unapaswa kutekelezwa ili kukabiliana na baadhi ya changamoto zilizoanishwa hapo juu. Kwa mfano, jengo hilo litakapokamilika litakuwa limepatia ufumbuzi tatizo la ufinyu wa ofisi za idara za uangalizi (Ofisi ya wazee, karani wa kanisa, mhazini) na store kwa ajili ya utunzaji wa vifaa vya kanisa. Hivyo, basi michoro na mipango ambayo ilikwishaanza miaka ya nyuma inapaswa iendelezwe. Gharama isiwe ni kikwazo cha kutokuanza kwa mradi huu. Kwa kuwa tayari kanisa lilishaingia gharama kubwa kusanifu michoro ya jengo husika, inapendekezwa kwamba michoro ya usanifu ujenzi wa jengo upitishwe rasmi na kanisa ili taratibu zingine za kutafuta vibali vya ujenzi kutoka mamlaka za manispaa ziweze kuendelea. Ni vyema mradi huu usikwamishwe kwa sababu za matumizi ya jengo kwani matumizi yanaweza kubadilishwa pasipo kukwamisha mradi husika. 4.11.5 Majengo Kanisa Makundini Ni kusudi la Kanisa kuhakikisha kuwa ujwnzi wa majengo ya ibada makundini unakamilika kwa ukamilifu ili ibada zifanyike katika nzuri na yenye utukufu. Hivyo, majengo ya kanisa katika makundi yaliyoainishwa katika vipengle hapa chini yatakamilishwa kwa kuwekewa sakafu, madirisha na viti ili yafae kwa ibada. Gharama za kukamisha ujenzi wa majengo haya zimeainishwa katika jedwali la gharama za utekelezaji mpango mkakati. 16

Bumafa Chivilikiti Mabwepande Zinga Amani Kimele Mnyambe Mpekeso 4.11.6 Ukarabati wa nyumba ya mchungaji Kulingana na sera za kanisa, mtaa unapaswa kumjengea na ama kukarabati nyumba ya mchungaji. Hivyo, Kanisa la Mwenge litachangia sehemu yake kwenye ukarabati wa nyumba ya mchungaji pale itakapohitajika kulingana na mgawanyo wa uchangiaji katika mtaa wa Mwenge. 4.11.7 Ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi makao mapya ya ETC Kanisa litachukua jukumu la kuchangia sehemu yake kwenye mchango wa mtaa pale gharama halisi za ujenzi huo zitakapokuwa zimeainishwa na kugawanywa kwenye makanisa ya mtaa wa. Mchungaji wa mtaa anapaswa kuulizia gharama hizi kutoka ofisi ya Konferensi. 5. MIKAKATI YA KUPATA FEDHA KWAAJILI YA MIRADI YA MAJENGO Ili kutekeleza mipango yote iliyoainishwa katika mpango huu, kiasi kikubwa cha fedha kinahitajika. Fedha hizi zinapaswa kutafutwa kutoka vyanzo mbalimbali, wahusika wakuu wakiwa ni washiriki wenyewe. Pia kunahitajika mikakati mahususi kuhakikisha yote yaliyopangwa na kukubaliwa na washiriki yanatekelezwa kwa ufanisi mkubwa. Mapendekezo ya kupata fedha ni yafuatayo: 1. Kuanzisha mfuko maalum kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya kanisa utakao hamasishwa na idara ya uwakili kwa kushirikiana na idara ya majengo 2. Kuwa na kikosi kazi cha washiriki wachache watakaoongoza changizo za ujenzi. 3. Kuwashirikisha washiriki wote katika kuchangia shughuli za maendeleo ya kanisa. 4. Kuendesha harambee za kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi 5.1. Kuanzisha mfuko maalum wa maendeleo ya kanisa Inapendekezwa kuanzishwa kwa mfuko maalum wa maendeleo ya kanisa. Mfuko huu utakuwa maalumu kwa ajili ya miradi mikubwa ya ujenzi wa makanisa na jengo la huduma kwa matumizi anuai. Washiriki wataombwa kuchangia katika mfuko huu kila wiki kwa kadri wanavyobarikiwa, na pia kuwe na changizo maalumu kwa ajili hiyo. 17

5.2 Kikosi kazi cha watu 100-200 Ili kuwezesha kazi ya ujenzi wa jengo la matumizi mbalimbali unafanyika, kuwe na kikosi ongozi cha watu au familia 100 hadi 200 zitakazoombwa kuchangia kila mtu/familia kuanzia kiasi cha shilingi 1,000,000 kwa mwaka; lengo ni kukusanya kiasi cha Shilingi 100,000,000 hadi 200,000,000 kwa mwaka kinachohitajika kwa kuanzia ili kutekeleza miradi mikubwa ya ujenzi ambayo itatekelezwa kwa kufuata kipaumbele kwa kuanzia na: 1. Maboresho na upanuzi wa jengo la kanisa, na 2. ujenzi wa jengo la matumizi mbalimbali. 5.3 Washiriki wote wa kanisa kuhusishwa Kwa kuwa ushiriki wa washiriki wote ni muhimu kwa kila kazi ya kanisa, washiriki wote watakuwa sehemu ya kuchangia kwa kutumia njia mbalimbali zifuatazo: Fomu za kuchangisha watu mbalimbali kwa kila mshiriki (wasio washiriki wa mwenge, na pia kwa watu wengine wa madhehebu mengine na kwa marafiki) kwa kuomba vibali vya kitaifa na kanisa. Uchangiaji kwa njia ya simu i.e. tuma neno Mwenge kwenda 15555 kwa kutumia mitandao ya simu iliyopo kama vodacom, airtel n.k. Uuzaji wa bidhaa za kanisa kwa bei ya juu kidogo kwa washiriki na watu wengine i.e Tshirts, Kalenda n.k. Washiriki wa mwenge wa zamani kuhusishwa (ndani na nje ya nchi). Kuweka Magoli kwa kila mshiriki/familia Kila mshiriki apeleke kadi maalumu zilizochapwa majina kwa watu watano wa karibu (wasiwe washiriki wa mwenge na au wawe ni marafiki, wafanyakazi wenzetu katika sehemu za kazi n.k) Kutoa matangazo ya changizo kupitia Morning Star radio 5.4 Changizo kutoka watu wa nje ya kanisa kwa njia ya harambee Kanisa halijatumia ipasavyo fursa ya kufanya harambee za uchangiaji zenye kuwahusisha watu wasio washiriki wa kanisa la waadventista wasabato katika kuchangia shughuli za maendeleo. Hivyo, inapendekezwa kwamba njia hii itumike pia kama sehemu ya mkakati wa kukusanya pesa. Harambee iliyotayarishwa vizuri kwa kuwaalika watu wenye nafasi kubwa serikalini na katika taasisi za umma na watu binafsi ifanyike, hii itakuwa katika mfumo ufuatao: Ifanyike nje ya eneo la kanisa Iwe ni katika mfumo wa chakula cha jioni (dinner) Michoro ya kanisa na model zake iwe tayari wakati wa harambee Kamati maalumu iundwe kuandaa harambee hii ili kuangalia sehemu ya kufanyia harambee, watu wa kualikwa, utaratibu utakaotumika unaozingatia misingi ya kanisa n.k 18

6. RAMANI YA UTEKELEZAJI 6.1 Ramani ya kila mwaka ya utekelezaji wa mpango mkakati A: RASILIMALI ZA KIROHO 2013 2014 2015 2016 2017 IDARA HUSIKA Lengo 1: Kuongeza washiriki kwa 100% ifikapo 2017 20% 20% 20% 20% 20% Wazee wa Kanisa Mchungaji Lengo 2: Kutenga makundi yaliyopo sasa kuwa makanisa ifikapo 2017 Zinga M'Pande Kimele Bumafa Vikawe Huduma Lengo 3: Kuimarisha na kuyawezesha makundi kujitegemea ifikapo mwaka 2017 au baada ya Shule ya Sabato Zinga M'Pande Kimele Bumafa Vikawe hapo. Lengo 4: 15% Wazee wa Kanisa i). Kuwa na 60% ya washiriki wanaosoma Biblia na Lesoni ifikapo 2017 10% 15% 15% 15% Huduma Shule ya Sabato ii). Kuhakikisha kuwa 70% ya washiriki wana ufahamu mpana kuhusiana na mtindo na mwenendo wa 10% 15% 15% 15% 15% Afya na Kiasi maisha ya ki-adventista katika nyanja za afya, elimu, vyakula na vinywaji, na, maburudisho. Elimu Uwakili B: RASILIMALI WATU Lengo 1: Kuelimisha wainjilisti walei 15 wanaoweza kutumwa kama wainjilisti ifikapo 2017. 3 3 3 3 3 Wazee wa Kanisa Mchungaji Huduma Wazee wa Kanisa Mchungaji Lengo 2: Kusomesha mwanafunzi wawili elimu ya uchungaji ifikapo 17 Hezron Mgwenya & Nathaniel Huduma Lengo 3: 90% ya wahubiri wawe na elimu ya homilia ifikapo 2017 15% 15% 20% 20% 20% Mchungaji 19

C: RASILIMALI FEDHA Lengo 1: Kuhakikisha idadi ya washiriki wanaorudisha zaka na wanaotoa kwa mpango inaongezeka kwa asilimia hamsini (50%) ya washiriki. Lengo 2: Kuwezesha 70% ya washiriki wasio na ajira wawe na elimu ya ujasiliamali na wale wanaopenda kuanzisha na kuendeleza biashara wawe na elimu ya ujasiriamali. D: RASILIMALI MIONGOZO Lengo1: Kuhakikisha kuwa 100% ya washiriki wanafundishwa na kuelewa masomo muhimu yafuatayo : misingi 28 ya kanisa kufuata sera na taratibu za kanisa utumiaji wa vitabu vya Roho ya Unabii. 2013 2014 2015 2016 2017 IDARA HUSIKA 10% 10% 10% 10% 10% Mchungaji Wazee wa Kanisa Uwakili 10% 15% 15% 15% 15% ATAP Uwakili Huduma za wanawake Mchungaji Wazee wa Kanisa Roho ya Unabii 20% 20% 20% 20% 20% Idara ya huduma E: MRADI WA KUSAMBAZA KITABU CHA PAMBANO KUU Lengo 1: Kuhakikisha vitabu 20,000 vitanunuliwa na kusambazwa 4000 4000 4000 4000 4000 F: MIRADI MIKUU YA UJENZI Lengo 1: Kufanya ukarabati mkubwa wa jengo la kanisa na kukamilisha ujenzi wa majengo ya ibada makundini. Lengo 2: Kukarabati nyumba ya mchungaji Lengo 3: Ujenzi wa nyumba ya mkurugenzi makao makuu mapya ya ETC. Lengo 4: Ujenzi wa Jengo la Ustawi wa Jamii Mwenge kukusanya 200,000,000 na kuanza upanuzi wa ofisi za kanisa Kuendelea kukusanya fedha za ujenzi Kuanza upanuzi na maboresho ya kanisa Kuendelea na ujenzi Kukamilish a maboresho na upanuzi wote Wazee wa Kanisa Roho ya Unabii Wazee wa Kanisa Majengo Uwakili Kwa kadri ya mahitaji kwa mwaka husika Wazee wa Kanisa Majengo Wazee wa Kanisa Kadri ya bajeti itakayoletwa na conference kwa kuzingatia mgawanyo Mchungaji wa uchangiaji kimtaa Kuandaa na kukamilisha michoro yote ya usanifu 20

6.2 Ramani ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi kwa mwaka 2013 F: MIRADI MIKUU YA UJENZI Lengo #1: Kufanya ukarabati mkubwa na upanuzi wa jengo la kanisa na kukamilisha ujenzi wa majengo ya kuabudia makundini Kutengeneza 3D model ya kanisa litakapokamilika (3D Physical Model) Kuandaa utaratibu wa kukusanya fedha kwa njia ya familia 100-200, na michango ya washiriki Kuandaa utaratibu wa kukusanya fedha kwa njia ya kuchangisha kutumia kadi kutoka kwa watu wa nje ya kanisa. Kuandaa utaratibu wa kukusanya fedha kwa njia ya "majengo day" ndani ya kanisa Kuandaa utaratibu wa kukusanya fedha kwa njia ya "majengo day" ndani ya kanisa na nje ya kanisa. Kuandaa utaratibu wa kukusanya fedha kwa njia SMS namba maalum. Ukusanyaji wa fedha za kutekeleza mradi Kuanza ujenzi wa upanuzi wa ofisi za kanisa Lengo #2 : Kukarabati nyumba ya mchungaji Lengo # 3: Ujenzi wa nyumba ya mkurugenzi makao makuu mapya ya ETC Lengo # 4: Ujenzi wa Jengo la ustawi wa jamii i). Kupitia upya michoro iliyopo kuona kama inakidhi haja za sasa na wakati ujao ili kufanya marekebisho pale inapobidi. ii). Kuandaa michoro mipya (kama kutakuwa na mabadiliko) iii). Kuandaa michoro ya kihandisi (structural engineering drawings). iv). Kuandaa michoro ya mfumo wa maji v). Kuandaa michoro ya mfumo wa umeme JANUARI FEBRUARI MACHI APRILI MEI JUNI Wk1 Wk2 Wk3 Wk4 W1 Wk2 Wk3 Wk4 Wk1 Wk2 Wk3 Wk4 Wk1 Wk2 Wk3 Wk4 Wk1 Wk2 Wk3 Wk4 Wk1 Wk2 Wk3 Wk4 Pale itakapohitajika Pale itakapohitajika 21

F: MIRADI MIKUU YA UJENZI Lengo #1: Kufanya ukarabati mkubwa na upanuzi wa jengo la kanisa na kukamilisha ujenzi wa majengo ya kuabudia makundini Kutengeneza 3D model ya kanisa litakapokamilika Kuandaa utaratibu wa kukusanya fedha kwa njia ya familia 100-200, na michango ya washiriki Kuandaa utaratibu wa kukusanya fedha kwa njia ya kuchangisha kutumia kadi kutoka kwa watu wa nje ya kanisa Kuandaa utaratibu wa kukusanya fedha kwa njia ya "majengo day" ndani ya kanisa Kuandaa utaratibu wa kukusanya fedha kwa njia ya "majengo day" ndani ya kanisa na nje ya kanisa Kuandaa utaratibu wa kukusanya fedha kwa njia SMS namba maalum Ukusanyaji wa fedha za kutekeleza mradi Kuanza ujenzi wa upanuzi wa ofisi za kanisa Lengo #2 : Kukarabati nyumba ya mchungaji Lengo # 3: Ujenzi wa nyumba ya mkurugenzi makao makuu mapya ya ETC Lengo # 4: Ujenzi wa Jengo la ustawi wa jamii i). Kupitia upya michoro iliyopo kuona kama inakidhi haja za sasa na wakati ujao ili kufanya marekebisho pale inapobidi. ii). Kuandaa michoro mipya (kama kutakuwa na mabadiliko) iii). Kuandaa michoro ya kihandisi (structural engineering drawings). iv). Kuandaa michoro ya mfumo wa maji JULAI AGOSTI SEPTEMBA OCTOBA NOVEMBA DESEMBA Wk 1 Wk2 Wk3 Wk4 Wk 1 Pale itakapohitajika Pale itakapohitajika Wk 2 Wk 3 Wk4 Wk1 Wk2 Wk3 Wk4 Wk1 Wk2 Wk3 Wk4 Wk1 Wk2 Wk3 Wk4 Wk1 Wk2 Wk3 Wk4 v). Kuandaa michoro ya mfumo wa umeme 22

7. BAJETI YA UTEKELEZAJI MPANGO MKAKATI 7.1 MAJENGO YA IBADA MAKUNDINI KUNDI LA BUMAFA Maelezo SHS. 1. Kuweka sakafu 2. Kupiga lipu (plaster) ndani na nje ya jengo 3. Kuweka grill kwenye madirisha 4. Kuweka milango 5. Kujenga choo Jumla ya gharama inayohitajika 11,403,700.00 KUNDI LA CHIVILIKITI 1. Kuweka lipu ndani na nje 2. Kuweka madirisha 3. Kuweka milango Jumla ya gharama inayohitajika 5,170,000.00 KUNDI LA MABWEPANDE 1. Kupiga lipu na kuziba nyufa 2. Kuweka umeme 3. Kufanya marekebisho ya mimbari Jumla ya gharama inayohitajika 1,300,000.00 KUNDI LA ZINGA Kufuatilia fidia kwa kuwa sehemu ya Kanisa iko katika hifadhi ya barabara. Hivyo kwa sasa hakuna shughuli za ujenzi zinazohitajika Jumla ya gharama inayohitajika 0.00 KUNDI LA AMANI 1. Kuweka sakafu 2. Kuweka lipu ya ndani na nje 3. Kufanya ukarafati wa choo kwa kuziba nyufa 4. Kubadilisha mlango mmoja wa choo 5. Kuweka milango Jumla ya gharama inayohitajika 4,361,500.00 23

KUNDI LA KIMELE 1 Kuweka lipu ndani na nje ya jengo 2 Kweka milango (frame na milango) 3 Kuweka madirisha 4 Kuta za ndani za kutenganisha 5 Kukarabati nyufa kwenye choo Jumla ya gharama inayohitajika 7,290,000.00 KANISA LA MNYAMBE 1 Ujenzi wa kanisa lenye uwezo wa kuchukua waumini 200 waliokaa vitini Jumla ya gharama inayohitajika 29,524,375.00 JUMLA KUU KWA MAKUNDI YOTE 59,049,575.00 NB: Mchanganuo wa gharama kwa kila kipengele utatolewa na idara ya majengo (Sehemu hii ni kwa ajili ya kuweka bajeti nzima ya kutekeleza mpango huu) 24

7.2 GHARAMA ZA MABORESHO YA MAZINGIRA YA KANISA LA MWENGE 25

8. VIELELEZO NA VIAMBATANISHI 8.1 Ramani ya upanuzi wa Kanisa (Sehemu za office) Picha 1: Sehemu ya chini (Ground floor) ikionyesha offisi ofisi za kanisa na kisima cha ubatizo 26

Picha 2: Sehemu ya juu (First floor) ikionyesha ofisi za mbalimbali za kanisa 27

8.2 Picha au mtazamo wa kisanifu katika picha za pande tatu (3D Views photos) Picha 3: Mwonekano wa Kanisa upande wa kuingilia kwenye ofisi mpya Picha 4: Mwonekano wa Kanisa upande wa mbele 28

Picha 5: Mwonekano wa Kanisa upande wa kushoto Picha 6: Mwonekano wa Kanisa kwa ndani 29