Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

Similar documents
Azimio lililopitishwa na Mkutano Mkuu tarehe 18 Desemba 2013 [juu ya taarifa ya Kamati ya Tatu (A/68/456/Add.2)]

Kutetea Haki za Binadamu

MAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1

TAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF) KUHUSU HAKI ZA WATOTO KATIKA KATIBA MPYA

MAPENDEKEZO YA MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA TANZANIA

KUHUSU AFRODAD. Dira ya AFRODAD. Dhamira ya AFRODAD. AFRODAD inalenga mchakato sawa na endelevu wa maendeleo kuelekea Afrika yenye mafanikio.

Information for assessors (do not distribute this page to participants):

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara

JAMHURI YA KENYA. Mkakati wa Ushirikiano MUKHTASARI FY Public Disclosure Authorized. Public Disclosure Authorized

MWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI

Songa kwenye kilele cha upeo. Masuala ya Msingi na Ujuzi juu ya Uendeshaji wa Serikali za Mitaa

UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU VIKWAZO VYA KULINDA MAISHA KATIKA USAIDIZI WA KIMATAIFA WA AFYA KWA MSAADA WA KIMATAIFA UNAOFADHILIWA NA MAREKANI

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU

Kubadili Sheria Za Mbegu Na Ulinzi Wa Aina Za Mbegu Na Mimea Nchini Tanzania

Miradi na jamii. 3.1 Utangulizi

MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA PRO-ROUTES. Ombi kwa ajili ya fedha za umma wa mradi wa ziada

Kitabu Cha Mafunzo Ya Uongozi Kwa Wanawake

JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI

MAADHIMISHO YA MIAKA 15 YA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

RIPOTI YA WARSHA KUHUSU HABARI KWA AJILI YA UWAJIBIKAJI

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi

KUSHUKA KWA HADHI YA LUGHA ZA JAMII NCHINI TANZANIA YOHANA P. MSANJILA University of Dar es Salaam, Tanzania

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

Mwongozo wa Kutathimini mifumo ya Ugawanaji wa faida na Mapato Katika Miradi ya Jamii ya MKUHUMI

Kimesanifiwa na:- E.D.Kissuu ECOMM TANZANIA S.L.P ,Dar es Salaam. Simu:

HISTORIA, MAENDELEO NA MABADILIKO YA KATIBA TANZANIA TANGU UHURU HADI MIAKA HAMSINI YA UHURU 9 DESEMBA 2011.

TANZANIA MARKETS PAN Sera zinazoboresha masoko

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO

KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA

Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara)

Kiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika

TAARIFA YA MWAKA YA UTENDAJI KAZI IDARA YA UTAWALA BORA 2013/2014

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

ORDER NO BACKGROUND

Kuuelewa Mchakato wa Bajeti Tanzania Mwongozo wa Asasi za Kiraia

KIJARIDA JUU YA HAKI ZA RAIA KATIKA MFUMO JINAI

Na Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake Toleola4

Dibaji ya Mwenyekiti wa Kamati ya Pamoja ya Uongozi

KAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI TANZANIA

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

In the matter of an Application by the KIGOMA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (KUWASA) For a Tariff and Charges Adjustment

RIPOTI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI

Unyanyasaji wa Watoto & Kutelekezwa

Mipango ya miradi katika udugu

Mwongozo wa Utamaduni Toleo la Kwanza

Human Rights Are Universal And Yet...

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU

Waandishi: wa Toleo la 5. Scholastica Jullu Athanasia A. Soka Safina Hassan Mary Njau. Toleo la 5: 2008 ISBN

HAKI NA TARATIBU ZA AJIRA, KAZI NA HIFADHI YA JAMII

TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM)

Uhakika wa Mbegu kwa Uhakika wa Chakula MWONGOZO WA UZALISHAJI WA MBEGU ZA ASILI ZA MAHINDI

AZAKI PIGA KURA UCHAGUZI MKUU TANZANIA OKTOBA. #TanzaniaTuitakayo OKTOBA 2015 ILANI YA UCHAGUZI YA AZAKI TANZANIA.

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )

HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE

Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA 2006/07

Sera ya Faragha. Upeo. Aina za Data na Mbinu za Ukusanyaji

KITEGO CHA MAREKEBISHO NA HAKI ZA MTOTO

Mwongozo wa Kanisa la Waadventista wa Sabato

Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame M. Mbarawa (Mb.); Waheshimiwa Mawaziri na Wabunge wote mliohudhuria;

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

Hakimiliki na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa TAFSIRI YA BIBLIA. Mwandishi. Jonathan M. Menn

MIONGOZO MIWILI KUPAA NA KUTUNGULIWA KWA AZIMIO LA ARUSHA

Afya Bora, Utu na Kinga. Ripoti ya Mashauriano ya Kiufundi Aprili 2009, Hammamet, Tunisia

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )

In the matter of Application by the TANGA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (TANGA UWASA) For a Multi-Year Tariff Adjustment

NGUZO KUMI ZA KILIMO KWANZA

UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA)

Kufanya Uwekezaji kuwa wa Manufaa kwa Afrika: Jibu la Mbunge kuhusu Unyakuzi wa Ardhi

USIMAMIZI MKUU WA UBORA WA MAHURUJI

MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2017/18

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig

ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA UCHUMI WA ZANZIBAR

Elimu Ina Umuhimu gani katika Jamii? Kuelekea Elimu Sahihi

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA MHESHIMIWA DKT

KIMAZINGIRA NA KIJAMII NA MPANGO WA UDHIBITI

LUGHA YA KISWAHILI KATIKA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA ELIMU SHULE ZA SEKONDARI

Kufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007

Afya Bora, Utu na Kinga. Ripoti ya Mashauriano ya Kiufundi Aprili 2009, Hammamet, Tunisia

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA III VI

wasiofaa. Naomba sana kila raia afanye bidii awezavyo kumkaribia Mwenyezi Mungu vile anavyoona inafaa, lakini asipitishe hukumu juu ya wengine.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II

Programu ya Uendelezaji Mifumo ya Maji Vijijini (PUMMV) katika Tanzania. Modeli wa Ukodishaji Mradi

Summaries of GC Reports 2012, Vol. 2, Sec. 1, Swahili

Elimukombozi, Lugha na Upashanaji Habari nchini Tanzania, katika Muktadha wa Utandawazi

Nilikua na Ndoto ya Kumaliza Shule Changamoto za Elimu ya Sekondari Tanzania

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA. Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo. TOLEO Na.

Mwongozo wa Utekelezaji wa Njia za S5-UUE (KAIZEN)-UUU Tanzania

SautiElimu. Sauti Yako Isikike

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Spika,

Ripoti hii ni kwa heshima ya wale wanaharakati wengi wa Tanzania ambao ndio binafsi wanaopitia hali iliyoangaziwa, na vilevile wale walioyapoteza

MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA. Kwa Wanaoanza

5. Mheshimiwa Spika, Bunge lako Tukufu lilijadili kwa kina Miswada ifuatayo:

KUCHUNGUZA MASUALA YA KISIASA KATIKA RIWAYA ZA SHAABAN ROBERT: MFANO WA KUSADIKIKA NA KUFIKIRIKA

Transcription:

The Human Rights Centre Uganda Azimio la Mkutano Mkuu 53/144 (8 Machi 1999) Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu AZIMIO KUHUSU HAKI NA WAJIBU WA MTU BINAFSI, VIKUNDI NA JUMUIYA MBALIMBALI KATIKA KUSIMAMIA NA KULINDA HAKI NA UHURU WA MSINGI WA BINADAMU Kiswahili The Human Rights Centre Uganda

Azimio la Mkutano Mkuu 53/144 (8 Machi 1999) Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu AZIMIO KUHUSU HAKI NA WAJIBU WA MTU BINAFSI, VIKUNDI NA JUMUIYA MBALIMBALI KATIKA KUSIMAMIA NA KULINDA HAKI NA UHURU WA MSINGI WA BINADAMU Hatimiliki 2009 Kitabu hiki kimeandikwa kwa faida ya watetezi wa haki za binadamu. Inaruhusiwa kunukuu au kunakili ilimradi chanzo na waandishi wanatajwa bayana The Human Rights Centre Uganda Plot 3327 (A) Kateeba Close Off Kironde Road, Muyenga P. O. Box 25638, Kampala-Uganda Telephone: +256 414 266186 E-mail: hrcug@hrcug.org Website: www.hrcug.org

KATIKA KUSIMAMIA NA KULINDA HAKI NA UHURU WA MSINGI WA BINADAMU 03 MWENDELEZO /MWONGOZO Usanifishaji huu umetolewa na kupendekezwa na Taasisi ya Haki za binadamu Uganda pamoja na mchango wa hali na mali toka kwa shirika la TROCAIRE katika kuthamini kazi na juhudi zote zinazofanywa na watetezi wa Haki za Binadamu nchini Uganda kupitia uwakilisha kwa walengwa unaotekelezwa Moja ya changamoto inayowakumba watetezi wa Hakiza Binadamu ni ukosefu wa kupata /kupokea taarifa muhimu ambazo zingeweza kulinda,kutetea na kuheshimu misingi ya mfumo wa Haki za Binadamu pamoja na Kuwasaidia watetezi na usalama wa kutosha katika shughuli /kazi zao. Katokana na hayo,taasisi ya Haki za binadamu Uganda Umetafsiri Azimio la Umoja wa mataifa kwa Watetezi wa Haki za Binadamu katika Lugha tano za kitamaduni/kibantu ambazo ni Ateso,Kiswahili,Luganda,Luo (Acholi na Lango), Runyakitara(Runyankore Rukiga na Runyoro- Rutooro).Lengo Kuu la tafsiri hizi ni kutoa nafasi ya taarifa kwa Azimio la Umoja wa Mataifa kwa watetezi wa Haki za Binadamu Kuongeza matumizi sahihi ya lugha hizo na tafsiri zake ili kutoa ueleo sahihi kati ya watetezi wa Haki za Binadamu kuanzia kwenye mzizi katika Jamii mbalimbali.

04 KATIKA KUSIMAMIA NA KULINDA HAKI NA UHURU WA MSINGI WA BINADAMU Tafsiri hii inategemewa kuwapa nguvu watetezi wa Haki za Binadamu kujua haki zao na jinsi ya kujilinda wapanyapo shughuli zao.nijukumu kuwa tafsiri hii itakuwa na usahii wa pekee na jukumu Kubwa kwa kazi mbalimbali kwa wale wote wanaovutiwa na kufanya shughuli za kutoa changamoto na kulinda,kutetea ili kufanya haki za binadamu kutimiza malengo yake chini Uganda. Human Rights Centre Uganda Kituo cha haki za binadamu nchini Uganda.

KATIKA KUSIMAMIA NA KULINDA HAKI NA UHURU WA MSINGI WA BINADAMU 05 UTANGULIZI Mnamo tarehe 9 Disemba mwaka 1998,Baraza kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha Azimio linalohusu Haki na Jukumu la kila mtu/kilam moja,au kundi la watu na Mwongozo wa Jamii katika kuhifadhi, Kulinda na kutetea Haki za Binadamu zinazotambulika kutokana na uhuru wa msingi katika nukuu ya pamoja inayofahamika na kutambulika kama Azimio la Watetezi wa Haki za Binadamu. Azimio hili si chombo pekee kinachotambulika kama nukuu ya kisheria bali ni chombo kinachohusisha mfumo unaokwenda Sambamba katika misingi ya haki na kanuni zinazoelekeza katika wajibu wa viwango vya haki za kibinadamu kufuatana na shuguli za taasisi mbalimba kama vyombo vinauyohusika kwenye Azimio kisheria.kanuni hizi zinatoa mwongozo wa mshikamano na usalama/ulinzi kwa watetezi wa haki za binadamu katika mfumo wa mwenendo mzima wa shughuli zao husika. Azimio linatoa sura ya moja kwa moja kuhusu haki kama chombo cha kisheria katika kulinda haki za binadamu kwa mfano uhuru wa kushirikiana pamoja, uhuru katika baraza la amani, uhuru wa kutoa/kuchangia au kupokea taarifa muhimu,uhuru wa kuchangia na kutoa msaada unaofuata sheria na kanuni mbadala ili kuendeleza mfumo wa kutoa mawazo mapya yanayohusu haki za binadamu.

06 KATIKA KUSIMAMIA NA KULINDA HAKI NA UHURU WA MSINGI WA BINADAMU Takribani miaka 11 sasa ni idadi ndogo tu ya watu inayofahamu Azimio hili hasa tangu Uganda Imeanza kulitumia, Kuna malengo makubwa na ya dhati kabisa kwa wahusika kutoa elimu kwa Jami husika kuweza kupata ufahamu na kuelewa kwa undani katika kulitumia.hivyo Serikali na washirika wake wajulikanao kama watetezi wa Haki za binadamu wana jukumu hilo la kusukuma gurudumu hilo tangu kuanzishwa kwake.lengo la Taasisi ya Haki za binadamu nchini Uganda ni kusimamia na kuwekeza katika shughuli husika zinazofanywa na watetezi wa haki kwa pamoja kupitia tafsiri hizi ili kuhakikisha taarifa zinawafikia walengwa wote wa Azimio ambao ni kati ya wadau Jambo litakawongeaza mazingira yaliyo mazuri na bora kwa watetezi wa Haki za Binadamu nchini Uganda kufanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa. Tafsiri hii ni chombo kinachopaswa kutumiwa vizuri na mtu yeyote katika misingi ya kulinda na kutoa nafasi katika kazi na usalama kwa watetezi wa haki za Binadamu ili kujenga na kuweka misingi ya uelewo kwa walio wengi kujua na kufahamu kwa undani Haki za binadamu katika kulinda na kutetea Haki za binadamu nchini Uganda.

KATIKA KUSIMAMIA NA KULINDA HAKI NA UHURU WA MSINGI WA BINADAMU 07 AZIMIO KUHUSU HAKI NA WAJIBU WA MTU BINAFSI, VIKUNDI NA JUMUIYA MBALIMBALI KATIKA KUSIMAMIA NA KULINDA HAKI ZA BINADAMU NA UHURU WA MSINGI ZINAZOTAMBULIWA KIMATAIFA Azimio la Mkutano Mkuu 53/144 (Machi 1999) Mkutano Mkuu, Ulisisitiza umuhimu wa kulinda kanuni za Mkataba wa Umoja wa Mataifa kwa kusudio la kusimamia na kutetea haki zote za binadamu na uhuru wa msingi kwa watu wote katika nchi zote za duniani. Kuzingatia muhtasari wa azimio la Tume ya Haki za Binadamu 1998/7 la Aprili 1998, Angalia Kumbukumbu Maalum za Baraza la Uchumi na Maisha ya Jamii, 1998, Nyongeza No. 3 (E/1998/23), Sura ya II, kifungu A. ambacho Tume inathibitisha rasimu ya azimio kuhusu haki na wajibu wa watu binafsi, pamoja na jumuiya mbalimbali za kijamii katika kusimamia na kulinda kwa ujumla haki na uhuru wa msingi unaotambuliwa kote ulimwenguni, Kuzingatia pia azimio la Baraza la Uchumi na Maisha ya Jamii 1998/33 la tarehe 30 Julai 1998, Angalia Muhtasari Rasmi wa Baraza la Uchumi na Maisha ya Jamii, Nyongeza Na. 3 (E.1998/23, sura ya II, kifungu

08 KATIKA KUSIMAMIA NA KULINDA HAKI NA UHURU WA MSINGI WA BINADAMU A, ambamo Tume inapendekeza kwamba Mkutano Mkuu ukubali rasimu ya azimio katika muktadha wa kumbukumbu ya miaka hamsini ya Azimio la Dunia kuhusu Haki za Binadamu na Uhuru wa Msingi, Azimio 217 a (III). 1. Kukubali Azimio kuhusu haki za binadamu na wajibu wa mtu Binafsi na Uhuru wa msingi, lililoambatanishwa na azimio hili. 2. Kushawishi Serikali zote, wakala na asasi zisizo za kiserikali zilizoko katika mfumo wa Umoja wa Mataifa kueneza Azimio hili kwa kukuza heshima na uelewano ulimwenguni, pamoja na kumuomba Katibu Mkuu kuliingiza andiko la azimio hili katika toleo la Haki za binadamu: Mkusanyiko wa Vyombo vya kimataifa. 85 th plenary meeting(kikao cha themanini na tano) 9 December 1998

KATIKA KUSIMAMIA NA KULINDA HAKI NA UHURU WA MSINGI WA BINADAMU 09 KIAMBATANISHO AZIMIO KUHUSU HAKI NA WAJIBU WA MTU BINAFSI, VIKUNDI NA JUMUIYA MBALIMBALI KATIKA KUSIMAMIA NA KULINDA HAKI ZA BINADAMU NA UHURU WA MSINGI ZINAZOTAMBULIWA KIMATAIFA Mkutano Mkuu, Ulisisitiza tena juu ya umuhimu wa kutetea kwa makusudi kanuni za Azimio la Dunia kuhusu Haki za binadamu na Maagano ya Kimataifa ya kukuza na kulinda haki za binadamu na uhuru wa msingi kwa watu wote katika nchi zote za ulimwengu, Kusititiza pia umuhimu wa Azimio la haki za binadamu na Maagano ya Haki za binadamu Kimataifa 200 A (XXI), kiambatanisho kama msingi wa asili wa juhudi za kimataifa katika kukuza heshima ulimwenguni pamoja na kutetea uhuru wa msingi na umuhimu wa vyombo vingine vya haki za binadamu vilivyokubalika ndani ya mfumo wa Umoja wa Mataifa, na katika nchi za Umoja wa Mataifa, Kutilia mkazo kwamba jumuiya zote za kimataifa aidha kwa pamoja au binafsi zitimize wajibu wake kukuza, kutangaza na kuendeleza heshima kwa haki za binadamu na uhuru wa msingi kwa wote bila kujali

010 KATIKA KUSIMAMIA NA KULINDA HAKI NA UHURU WA MSINGI WA BINADAMU tofauti za aina yoyote, utaifa au asili ya mtu, rasilimali (mali), uzawa au hadhi, na kusisitiza umuhimu wa pekee kufanikisha kimataifa katika kutimiza wajibu kulingana na Mkataba huu, Kukubali dhima/wajibu muhimu wa ushirikiano wa kimataifa kwa kazi muhimu kwa mtu binafsi, vikundi na jumuiya katika kuchangia, matokeo halisi ya kuangamiza uvunjaji wa haki za binadamu na uhuru wa msingi wa watu, ikiwa ni pamoja na aina zote za ubaguzi wa kabila na rangi, ukoloni, utawala au uvamizi wa kigeni, uchokozi au vitisho kwa utawala wa taifa, umoja wa wa kitaifa au utawala wa himaya na kukataa kutambua haki za watu kwa kujiamulia wenyewe na haki ya mtu yeyote kutawala na kuwa na maamuzi juu ya utajiri na maliasili, Kutambua uhusiano ulioko kati ya amani na usalama wa kimataifa na kufurahia haki za binadamu na uhuru wa msingi, na kujali kuwepo kwa amani na usalama wa kimataifa na kutokubaliana kwa kutokuhalalisha au kutoafiki, Kurudia tena kusema kwamba haki zote za binadamu na uhuru wa msingi ni za ulimwengu mzima, hazigawanyiki, zinategemeana na kuhusiana hivyo ni lazima zikuzwe na zitekelezwe kwa njia ya haki na usawa, pasipo upendeleo katika utekelezaji wa kila haki na uhuru wa msingi, Kutilia mkazo kwamba kazi na wajibu wa kukuza na

KATIKA KUSIMAMIA NA KULINDA HAKI NA UHURU WA MSINGI WA BINADAMU 011 kulinda haki za binadamu na uhuru wa msingi upo mikononi mwa dola, Kutambua haki na wajibu wa watu binafsi, vikundi na jumuiya mbalimbali katika kuendeleza heshima na kuendeleza elimu ya haki za binadamu na uhuru wa msingi katika ngazi ya kitaifa na kimataifa, Iinatamka: Ibara 1 Kila mtu anayo haki ya, kipekee ama kwa kushirikiana na wengine kukuza na kupambana kwa ajili ya kulinda na kutekelezwa kwa haki za binadamu na uhuru wa msingi katika ngazi ya kitaifa na kimataifa. Ibara 2 1. Kila dola inayo wajibu na kazi kubwa kulinda, kukuza kutetea na kutekeleza haki zote za binadamu na uhuru wa msingi, pamoja na mambo mengine kwa kuzikubali hatua hizi kadiri zilivyo muhimu kwa kutengeneza mazingira muafaka katika maisha ya jamii, uchumi, siasa na katika medani zote pamoja na sheria za halali zinazohakikisha kuwa watu wote walio chini ya sheria hizo, mtu binafsi ama kwa ushirikiano na watu wengine, wanaweza kufaidi haki zote na uhuru wa msingi kwa vitendo. 2. Kila dola haina budi kukubali sheria, utawala na hatua zingine kadiri ya umuhimu wake ili kuhakikisha kwamba haki hizo pamoja na uhuru

012 KATIKA KUSIMAMIA NA KULINDA HAKI NA UHURU WA MSINGI WA BINADAMU wa msingi kama inavyotajwa katika Azimio hili/ lililopo zinatekelezwa kwa uhakika. Ibara 3 Sheria za kila nchi zinazoshabihiana/kukubaliana na Mkataba wa Umoja wa Mataifa na masharti mengine ya kimataifa ya Dola katika medani ya haki za binadamu na uhuru wa msingi ndivyo mfumo wa msingi unaotegemewa kwa utendaji wa yote yanayotajwa katika Azimio yaani katika kukuza, kulinda na kutetea utekelezaji wa haki za binadamu na uhuru wa msingi. Ibara 4 Hakuna kitu chochote katika Azimio hili kinachowezakutafsiri au kudhoofisha ama kupinga makusudio na kanuni za Mkataba wa Umoja wa mataifa au kuzuia/ kuwekea mipaka ama kuushushia hadhi zinazotokana na Tamko la Dunia la Haki za Binadamu, Maagano ya Kimataifa kuhusu Haki za Binadamu, na vyombo vingine vya kimataifa pamoja na ahadi zingine zote zinazofaa kutumika kwa makusudio haya. Ibara 5 Ili kukuza na kulinda haki za binadamu pamoja na uhuru wa msingi, kila mtu anayo haki, binafsi na katika ushirikiano na wengine, kutekeleza wajibu huo katika ngazi ya kitaifa na kimataifa kwa: a) Kukutana na kukusanyika kwa amani. b) Kuanzisha, kujiunga na kushiriki katika asasi zisizo za kiserikali, vikundi vyaushirika.

c) page KATIKA KUSIMAMIA NA KULINDA HAKI NA UHURU WA MSINGI WA BINADAMU 013 Kuwasiliana na asasi zisizo za kiserikali na za kiserikali. Ibara 6 Kila mtu anayo haki binafsi, na kwa ushirikiano na wengine: a) Kufahamu, kutafuta, kumiliki, kupokea habari kuhusu haki za binadamu na uhuru wa msingi, ikiwa ni pamoja na kuwa na haki ya kujua jinsi haki na uhuru vinavyopewa kipaumbele katika sheria za nchi husika, mahakama na mfumo wa utawala. b) Kama ilivyo katika sheria ya haki za binadamu na katika vyombo vingine halali vya kimataifa kila mtu anayo haki ya kuchapisha, c) Kuelimisha au kutoa mawazo kwa wengine, maelezo na elimu kuhusu haki za binadamu na uhuru wa msingi. Ibara 7 Kila mtu anayo haki, binafsi au kwa ushirikiano na wengine, kuanzisha na kujadili dhana na kanuni mpya za haki za binadamu na kuzitetea ili zikubalike. Ibara 8 1. Kila mtu anayo haki binafsi, au kwa ushirikiano na wengine, kushiriki katika serikali ya nchi yake na katika shughuli za umma.

014 KATIKA KUSIMAMIA NA KULINDA HAKI NA UHURU WA MSINGI WA BINADAMU 2. Hii ni pamoja na mambo mengine, haki binafsi ama pamoja na wengine, kutoa changamoto zinazohusu umma kwa serikali na taasisi zake ili kuboresha utendaji wake na kubainisha udhaifu wowote unaoweza kuzuia au kukwamisha, kuendelezwa, kulinda na kutekelezwa kwa haki za binadamu na uhuru wa msingi. Ibara 9 1. Katika zoezi la haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na kukuza na kulinda haki za binadamu kama inavyotajwa ndani ya azimio, kila mtu anayo haki, binafsi na katika ushirikiano na wengine, kufaidi marekebisho yenye kufaa na kulindwa katika matukio ya ukiukwaji wa haki. 2. Kwa mantiki hiyo, kila mtu anayehisi kwamba haki zake zimekiukwa anayo haki ama yeye binafsi ama kupitia mwakilishi halali, kulalamika na bila kuchelewesha malalamiko hayo kusikilizwa mbele ya umma kabla ya chombo huru adili na cha kisheria ama chombo kingine kilichowekwa kisheria. 3. Chombo cha sheria kutoa uamuzi, kulingana na sheria, kutoa fidia ama marekebisho, ikiwa ni pamoja na fidia inayostahiki, pale ambapo pamekuwa na ukiukwaji wa haki na uhuru wa msingi wa mhusika, pamoja na utekelezaji wa sheria na uamuzi wa mwisho na fidia, pasipo ucheleweshwaji usio wa lazima.

KATIKA KUSIMAMIA NA KULINDA HAKI NA UHURU WA MSINGI WA BINADAMU 015 a) Kulalamikia kanuni na vitendo vya maofisa na taasisi za serikali kuhusiana na ukiukwaji wa haki za binadamu na uhuru wa msingi, kwa ombi la kisheria ama vyombo vingine halali vya kisheria vya ndani, utawala ama chombo kingine cho chote kilichoko katika mfumo wa Serikali na kinachoweza kutoa uamuzi bila ya ucheleweshaji usio na sababu ya msingi. b) Kuhudhuria usikilizaji wa mashtaka na uendeshaji wa mashtaka ili kuhakikisha kama maamuzi yanayotolewa yanapatana na sheria za nchi na kama zinalingana na kanuni au masharti ya kimataifa. c) Kutoa na kuandaa msaada stahili wa kisheria au ushauri mwingine wa kisheria na msaada katika kutetea haki za binadamu na uhuru wa msingi. 4. Kwa maana hiyo, kwa mujibu wa vyombo na taratibu za kimataifa zinazokubalika, kila mmoja anayo haki, binafsi ama kwa ushirikiano na wengine, kutozuia upatikanaji ama kuzuia mawasiliano ya mambo yote yanayohusiana na haki za binadamu na uhuru wa msingi. 5. Dola inapaswa kufanya kwa haraka na kwa uadilifu uchunguzi au kuhakikisha kwamba uchunguzi ufanyike wakati wowote ikiaminika kwamba ukiukwaji wa haki za binadamu na uhuru wa msingi umetokea ndani ya dola katika eneo lake lolote la kisheria.

016 KATIKA KUSIMAMIA NA KULINDA HAKI NA UHURU WA MSINGI WA BINADAMU Ibara 10 Hakuna mtu yoyote anayepaswa kushiriki kwa kufanya au kwa kushindwa kufanya anapopaswa, kwa kukiuka haki za binadamu na uhuru wa msingi wala mtu yoyote yule hapaswi kuadhibiwa au kufanyiwa kitendo chochote kisichofaa kwa kukataa kufanya hivyo. Ibara 11 Kila mtu anayo haki, binafsi na kwa ushirikiano wa wengine, kwa sheria halali kuwa na kazi na taaluma yake. Kila mmoja, kutokana na taaluma yake, anaweza kugusa (athiri) heshima ya ubinadamu, haki za binadamu na uhuru wa msingi wa wengine unapaswa kuheshimu haki na uhuru wa msingi na kuhusiana na viwango, mwenendeno wa kazi, taaluma na maadili ya kimataifa. Ibara 12 1. Kila mtu anayo haki binafsi na kwa ushirikiano na wengine, kushiriki katika shughuli za amani dhidi ya ukiukwaji wa haki za binadamu na uhuru wa msiingi. 2. Dola inapaswa kuchukua kila hatua muhimu kuhakikisha kwamba inalinda haki ya mtu binafsi na ya wengi dhidi ya vurugu, vitisho, ulipizaji kisasi, au ubaguzi, shinikizo au vitendo vya kidhalimu ambavyo ni kinyume na haki halali za mtu kama zilivyotamkwa katika Azimio hili.

3. page KATIKA KUSIMAMIA NA KULINDA HAKI NA UHURU WA MSINGI WA BINADAMU 017 Katika mfungamano huu, kila mtu anayo haki binafsi na kwa ushirikiano na wenzake, kulindwa kwa mujibu wa sheria ya nchi anapoonyesha hisia ama kupinga, kwa njia ya amani, mambo na vitendo, ikiwa ni pamoja na yale yasiyotekelezwa na Dola ambayo matokeo yake huwa ni ukiukwaji wa haki za binadamu na uhuru wa msingi, vilevile vitendo vya uvunjaji wa amani unaofanywa na vikundi ama mtu binafsi vinavyoathiri kufurahiwa kwa haki na uhuru wa msingi. Ibara 13 Kila mtu anayo haki, binafsi au kwa ushirikiano na wengine, kuomba, kupokea na kutumia rasilimali kwa kusudi ya kuelezea kusudio la kukuza, kuendeleza na kulinda haki za binadamu na uhuru wa msingi kwa njia ya amani, kama ilivyo katika Ibara ya 3 ya Azimio la sasa. Ibara 14 1. Dola ina wajibu wa kusimamia utungaji wa sheria, sheria za Kimahakama, kiutawala au hatua zingine zozote muhimu ili kukuza ueleo wa watu wote walioko chini ya mamlaka yake kiraia, kisiasa, kiuchumi, kijamii na haki za maendeleo ya jamii. 2. Hatua hizo ndani yake kwa pamoja na mengine kuhusu:

018 KATIKA KUSIMAMIA NA KULINDA HAKI NA UHURU WA MSINGI WA BINADAMU 3. a) b) Uchapishaji, upatikanaji na usambazaji wa maandiko ya sheria za kitaifa na kanuni na zitumiwazo na vyombo vya kimataifa vya haki za binadamu. Haki ya kupata bila pasipo kikwazo (upungufu) maandiko yote ya kimataifa yanayohusu haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na taarifa zinazotolewa kila baada ya kipindi fulani na Dola toka vyombo vilivyoanzishwa na vyombo vya kimataifa kuhusu makala za haki za binadamu ambazo ni wanachama; pamoja na majumuisho ya majadiliano na taarifa maalum zilizoko katika taarifa ya vyombo hivyo. Dola inapaswa kuhakikisha na kuunga mkono, pale inapoona inafaa, uanzishwaji na maendeleo ya asasi za kitaifa zinazojitegemea kwa kusudi ya kuendeleza na kulinda haki za binadamu na uhuru wa msingi katika eneo lake lote la utawala, hata kama ni mchunguzi wa haki za binadamu, tume ya haki za binadamu au asasi ya aina yoyote ya kitaifa. Ibara 15 Dola inao wajibu wa kukuza na kutoa mafundisho ya haki za binadamu na uhuru wa msingi katika ngazi zote za kielimu na kuhakikisha kwamba wote wanaohusika kuwafundisha mawakili, wasimamizi wa sheria, waajiriwa wa majeshi ya ulinzi na usalama

KATIKA KUSIMAMIA NA KULINDA HAKI NA UHURU WA MSINGI WA BINADAMU 019 na watumishi wa umma wanajumuisha mafundisho sahihi yanayohusu haki za binadamu katika taaluma husika. Ibara 16 Watu binafsi, asasi zisizo za kiserikali na asasi zingine husika zina dhima/wajibu wa kutoa mchango wa kuuelimisha umma ili ujue maswali yanayohusiana na haki zote za binadamu na uhuru wa msingi kupitia mambo mbalimbali kama vile elimu, utafiti na ufundishaji katika maeneo ili kuimarisha zaidi pamoja na mambo mengine, ueleo, uvumilivu, amani, na uhusiano wa kirafiki kati ya mataifa na kati ya jamii na vikundi vya kidini, kwa kuzingatia tofauti za kijamii na kijumuiya ambamo hufanya kazi zao. Ibara 17 Katika kutekeleza zoezi la haki na uhuru unaotajwa katika Azimio la sasa, kila mmoja, anayehusika binafsi au katika ushirikiano na wengine, atawajibika kwa kikomo kulingana na masharti husika ya kimataifa yaliyowekwa kwa mujibu wa sheria hizo kwa kusudi ya kuwa na hakika kutambuliwa na kuheshimiwa haki na uhuru wa wengine na matakwa ya uadilifu, utulivu na ustawi kwa ujumla katika jamii iliyo ya kidemokrasia. Ibara 18 1. Kila mtu anao wajibu ndani ya jamii ambamo ndani yake ndimo uhuru na maendeleo ya utu wake inapowezekana kukua kikamilifu.

020 KATIKA KUSIMAMIA NA KULINDA HAKI NA UHURU WA MSINGI WA BINADAMU 2. 3. Watu binafsi, vikundi, taasisi na asasi zisizo za kiserikali zinao wajibu muhimu katika kuchangia na kulinda demokrasia, kulinda haki za binadamu na uhuru wa msingi na kutoa mchango ili kukuza jamii za kidemokrasia, taasisi na utendaji. Watu binafsi, vikundi, taasisi na asasi zisizo za kiserikali zina wajibu muhimu pia katika kutoa mchango, kadiri ifaavyo, kuendeleza haki za kila mtu kulingana na utaratibu wa kitaifa na kimataifa, ambamo ndani yake vyombo vya haki na uhuru vinatambulika. Ibara 19 Hakuna kitu chochote kile katika Azimio hili la sasa kinachopaswa kutafsiriwa kumaanisha kwamba mtu binafsi, au kikundi au chombo cha kijamii au Dola yoyote kujiingiza kwa namna yoyote au kutenda tendo lolote lililokusudiwa kuleta uharibifu wa haki na uhuru wa msingi kama inavyotajwa katika Azimio la sasa. Ibara 20 Hakuna kitu chochote katika Azimio la sasa, kinachotafsirika kuruhusu Dola kuendeleza na kukuza vitendo vya watu binafsi, vikundi vya watu binafsi, taasisi au asasi zisizo za kiserikali kinyume na masharti ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa.