Azimio lililopitishwa na Mkutano Mkuu tarehe 18 Desemba 2013 [juu ya taarifa ya Kamati ya Tatu (A/68/456/Add.2)]

Similar documents
Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

Kutetea Haki za Binadamu

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

KUHUSU AFRODAD. Dira ya AFRODAD. Dhamira ya AFRODAD. AFRODAD inalenga mchakato sawa na endelevu wa maendeleo kuelekea Afrika yenye mafanikio.

TAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF) KUHUSU HAKI ZA WATOTO KATIKA KATIBA MPYA

MAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU

Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi

MAPENDEKEZO YA MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA TANZANIA

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU

MAADHIMISHO YA MIAKA 15 YA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU VIKWAZO VYA KULINDA MAISHA KATIKA USAIDIZI WA KIMATAIFA WA AFYA KWA MSAADA WA KIMATAIFA UNAOFADHILIWA NA MAREKANI

Afya Bora, Utu na Kinga. Ripoti ya Mashauriano ya Kiufundi Aprili 2009, Hammamet, Tunisia

JAMHURI YA KENYA. Mkakati wa Ushirikiano MUKHTASARI FY Public Disclosure Authorized. Public Disclosure Authorized

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Dibaji ya Mwenyekiti wa Kamati ya Pamoja ya Uongozi

Songa kwenye kilele cha upeo. Masuala ya Msingi na Ujuzi juu ya Uendeshaji wa Serikali za Mitaa

Miradi na jamii. 3.1 Utangulizi

Afya Bora, Utu na Kinga. Ripoti ya Mashauriano ya Kiufundi Aprili 2009, Hammamet, Tunisia

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara

JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1

Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA 2006/07

Unyanyasaji wa Watoto & Kutelekezwa

Sera ya Faragha. Upeo. Aina za Data na Mbinu za Ukusanyaji

MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2017/18

MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA PRO-ROUTES. Ombi kwa ajili ya fedha za umma wa mradi wa ziada

Ripoti hii ni kwa heshima ya wale wanaharakati wengi wa Tanzania ambao ndio binafsi wanaopitia hali iliyoangaziwa, na vilevile wale walioyapoteza

HAKI NA TARATIBU ZA AJIRA, KAZI NA HIFADHI YA JAMII

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

Kitabu Cha Mafunzo Ya Uongozi Kwa Wanawake

HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )

NGUZO KUMI ZA KILIMO KWANZA

Information for assessors (do not distribute this page to participants):

RIPOTI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI

TAARIFA YA MWAKA YA UTENDAJI KAZI IDARA YA UTAWALA BORA 2013/2014

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Kubadili Sheria Za Mbegu Na Ulinzi Wa Aina Za Mbegu Na Mimea Nchini Tanzania

RIPOTI YA WARSHA KUHUSU HABARI KWA AJILI YA UWAJIBIKAJI

JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI

Programu ya Uendelezaji Mifumo ya Maji Vijijini (PUMMV) katika Tanzania. Modeli wa Ukodishaji Mradi

Kuuelewa Mchakato wa Bajeti Tanzania Mwongozo wa Asasi za Kiraia

Mipango ya miradi katika udugu

KITEGO CHA MAREKEBISHO NA HAKI ZA MTOTO

Mwongozo wa Utekelezaji wa Njia za S5-UUE (KAIZEN)-UUU Tanzania

KUSHUKA KWA HADHI YA LUGHA ZA JAMII NCHINI TANZANIA YOHANA P. MSANJILA University of Dar es Salaam, Tanzania

Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali ya Madini Ukanda

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara)

TANZANIA MARKETS PAN Sera zinazoboresha masoko

TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM)

Kufanya Uwekezaji kuwa wa Manufaa kwa Afrika: Jibu la Mbunge kuhusu Unyakuzi wa Ardhi

Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame M. Mbarawa (Mb.); Waheshimiwa Mawaziri na Wabunge wote mliohudhuria;

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA III VI

KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA. Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo. TOLEO Na.

KAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI TANZANIA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

USIMAMIZI MKUU WA UBORA WA MAHURUJI

AZAKI PIGA KURA UCHAGUZI MKUU TANZANIA OKTOBA. #TanzaniaTuitakayo OKTOBA 2015 ILANI YA UCHAGUZI YA AZAKI TANZANIA.

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA

Kimesanifiwa na:- E.D.Kissuu ECOMM TANZANIA S.L.P ,Dar es Salaam. Simu:

In the matter of an Application by the KIGOMA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (KUWASA) For a Tariff and Charges Adjustment

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

SUALA NYETI NI VURUGU Mashambulizi dhidi ya Wana LGBT katika Pwani ya Kenya H U M A N R I G H T S W A T C H

TANZANIA TAARIFA YA MWISHO WA UTEKELEZAJI

MWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI

Mwongozo wa Kutathimini mifumo ya Ugawanaji wa faida na Mapato Katika Miradi ya Jamii ya MKUHUMI

Nilikua na Ndoto ya Kumaliza Shule Changamoto za Elimu ya Sekondari Tanzania

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA MHESHIMIWA DKT

In the matter of Application by the TANGA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (TANGA UWASA) For a Multi-Year Tariff Adjustment

Na Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake Toleola4

Hatari, Haki za Usalama katika Bahari 03

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO

Shabaha ya Mazungumzo haya

Mwongozo kwa familia zinazofanya kazi pamoja kwa maisha endelevu. Nyenzo ya Mafunzo

Mwongozo wa Mwezeshaji

International Labour Office. Kazi za Ndani Zenye Madhara kwa Watoto: Kijitabu cha Maelezo Mafupi

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II

UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA)

HUDUMA ZA AFYA KWA WOTE

KIMAZINGIRA NA KIJAMII NA MPANGO WA UDHIBITI

Mwongozo wa Utamaduni Toleo la Kwanza

Kufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007

Dodoma ambako kikao cha Bunge kinaendelea kuja kushiriki japo sehemu ya uzinduzi wa mkutano.

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

SautiElimu. Sauti Yako Isikike

Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2013

Waandishi: wa Toleo la 5. Scholastica Jullu Athanasia A. Soka Safina Hassan Mary Njau. Toleo la 5: 2008 ISBN

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

UFUATILIAJI WA MIRADI NA TATHMINI

Human Rights Are Universal And Yet...

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

Deputy Minister for Finance

3. Mheshimiwa Spika, 4. Mheshimiwa Spika,

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA FEDHA

HOTUBA YA WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA MHESHIMIWA DKT

Govt increases vetting threshold of contracts

Transcription:

This unofficial translation is provided by the International Service for Human Rights Umoja wa Mataifa A/AZI/68/ Ugaw Jumla Mkutano Mkuu 30 Januari 2014 Kikao cha Sitini na Nane Dondoo ya Ajenda 69(b) Azimio lililopitishwa na Mkutano Mkuu tarehe 18 Desemba 2013 [juu ya taarifa ya Kamati ya Tatu (A/68/456/Add.2)] 68/181. Uendelezaji wa Tamko la Haki na Wajibu wa Watu Binafsi, Vikundi na Vyombo vya Jamii Kuendeleza na Kulinda Haki za Binadamu na Uhuru wa Msingi Zinazotambuliwa Ulimwenguni: kulinda wanawake watetezi wa haki za binadamu Mkutano Mkuu, Ukiongozwa na Malengo na Misingi ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa, Tamko la Haki za Binadamu kwa Wote, 1 Mikataba ya Kimataifa ya Haki za Binadamu, 2 na vyombo vingine husika, pamoja na Mkataba wa Kutokomeza Aina zote za Ubaguzi dhidi ya Wanawake, 3 Ukikumbuka azimio lake na. 53/144 la Desemba 9 1998, ambapo kwa makubaliano lilipitisha Tamko la Haki na Wajibu wa Watu Binafsi, Vikundi na Vyombo vya Jamii Kuendeleza na Kulinda Haki za Binadamu na Uhuru wa Msingi Zinazotambuliwa Ulimwenguni, lililoambatanishwa kwenye azimio hili, na kusisitiza umuhimu wa msingi wa Tamko na uendelezaji na utekelezaji wake, Ukikumbuka pia maazimio yote ya awali juu ya suala hili, pamoja na azimio lake na. 66/164 la tarehe 19 Desemba 2011 na maazimio ya Baraza la Haki za Binadamu na.16/5 la tarehe 24 Machi 2011 4 na 22/6 ya tarehe 21 Machi 2013 5 Ukikumbuka zaidi Tamko la Vienna na Programu ya Utekelezaji 6, Mkataba wa Kutokomeza Aina zote za Ubaguzi dhidi ya Wanawake, 7 Programu ya Kazi ya Mkutano wa Idadi ya Watu na Maendeleo 8 na Tamko la Beijing na Jukwaa la Utekelezaji 9 na matokeo ya marejeo yao, pamoja na maamuzi na maazimio ya Tume ya Hadhi ya Wanawake yaliyokubaliwa, 1 Azimio na.217 A (III) 2 Azimio na.2200 A (XXI), kiambatanisho. 3 Umoja wa Mataifa, Mfuatano wa Mikataba, vol. 1249, Na. 20378. 4 Rejea Kumbukumbu Rasmi za Mkutano Mkuu Kikao cha Sitini na Sita, Nyongeza, Na. 53 (A/66/53), sura ya. II, seh. A. 5 Ibid., Kikao cha Sitini na Nane, Nyongeza Na.. 53 (A/68/53), sura ya. IV, seh. A. 6 A/SIRI.157/24 (Sehemu ya I), sura ya. III. 7 Rejea Azimio 48/104. 8 Taarifa ya Mkutano wa Kimataifa wa Idadi ya Watu na Maendeleo Cairo, 5 13 Septemba 1994 (chapisho la Umoja wa Mataifa, Sales Na. E.95.XIII.18), sura ya. I, azimio 1, kiambatanisho. 9 Taarifa ya Mkutano wa Nne wa Dunia wa Wanawake, Beijing, 4-15Septemba 1995 (chapisho la Umoja wa Mataifa, Sales Na.E.96.IV13), sura ya 1, azimio 1, kiambatanisho I na II.

Ukitambua uangalifu unaotolewa na Baraza la Haki za Binadamu kwa umuhimu wa wanawake watetezi wa haki za binadamu na wa kuhakikisha ulinzi wao na kuwezasha shughuli zao kupitia maazimio yao ya karibuni, na kutambua mjadala wa jopo juu ya wanawake watetezi wa haki za binadamu uliofanyika tarehe 26 Juni 2012, Ukitambua pia kuwa wanawake wa rika zote wanaojishughulisha na undelezaji na ulinzi wa haki zote za binadamu na uhuru wa msingi na watu wote wanaojishughulisha na utetezi wa haki za wanawake na usawa wa kijinsia, binafsi na au kwa kushirikiana na wengine, hutekeleza jukumu muhimu kijamii, kitaifa, kikanda na kimataifa, katika kuendeleza na kulinda haki za binadamu, kwa mujibu wa Tamko la Haki na Wajibu wa Watu Binafsi, Vikundi na Vyombo vya Jamii Kuendeleza na Kulinda Haki za Binadamu na Uhuru wa Msingi Zinazotambuliwa Ulimwenguni, 10 Ukizingatia kwa hofu kuwa katika nchi nyingi watu na mashirika yanayojishughulisha na undelezaji na utetezi wa haki za binadamu na uhuru wa msingi, wakiwemo wanawake watetezi wa haki za binadamu, mara kwa mara hukumbana na vitisho na usumbufu na hawana usalama kutokana na shughuli hizo, ikiwemo kunyimwa uhuru wa kushirikiana au uhuru wa kujieleza au haki ya kukusanyika kwa amani au matumizi mabaya ya taratibu za kesi za madai au jinai. Ukiwa na hofu kubwa kuwa wanawake watetezi wa haki za binadamu wamo hatarini na wanateseka kwa usumbufu na unyanyasaji, ikiwemo usumbufu kimfumo na unyanyasaji wa zao za msingi za kuishi, uhuru na usalama wa mtu, uadilifu kimwili, na kisaikolojia, faragha na heshima kwa maisha ya faragha na ya kifamilia na uhuru wa kutoa maoni na kujieleza, ushirikiano na kukusanyika kwa amani na zaidi ya hayo wanaweza kukumbana na ukatili wa kijinsia, ubakaji na aina nyingine ya vurugu za kijinsia, usumbufu na matusi ya mdomoni na kushambulia tabia, kwa mitndao au nje ya mitandao, yatendwaayo na watendaji wa Kitaifa, wakiwemo wanaohusika na usimamizi wa utekelezaji wa sheria na vyombo vya usalama, na watendaji wasio wa kitaifa, kama wale wenye uhusiaano na familia na jumuia, katika mazingira binafsi na ya umma, Ukiwa na hofu kubwa zaidi kuwa tofauti za kihistoria na kimfumo katika uhusiano wa kimadaraka na ubaguzi dhidi ya wanawaake, pamoja na aina mbali mbali za ukereketwaji wa kupindukia, zina athari za moja kwa moja kwa hadhi na jinsi wanawake wanavyotendewa na kuwa haki za baadhi ya wanawake watetezi wa haki za binadamu zinakiukwa au kutumiwa vibaya na kazi yao inanyanyapaliwa kutokana na desturi za kiubaguzi na desturi za kijamii au mielekeo ile inayotumika kuhalaisha ukatili dhidi ya wanawake au kudumisha desturi zenye vurugu kama hizo, Ukiguswa sana kuwa kutoadhibiwa kwa ukiukwaji na unyanyasaji dhidi ya wanawake watetezi wa haki za binadamu unaendelea kutokana na mambo mbali mbali yakiwemo ukosefu wa taarifa, nyaraka, upelelezi na upatikanaji wa haki, 10 Azimio 53/144, kiambatanisho. 2

vikwazo vya kijamii na vipingamizi katika kushughulikia ukatili wa kijinsia, pamoja na vurugu za kijinsia na unyanyapaaji vinavyoweza kutokana na ukiukwaji huu na unyanyasaji, na ukosefu wa kutambua jukumu halali la wanawake watetezi wa haki za binadamu, yote hayo hudumisha au kurasimisha ubaguzi wa kijinsia. Ukihofia kuwa aina zote za ubaguzi, ikiwa ni pamoja na ukabila, ubaguzi wa rangi, chuki dhidi ya wageni na ukosefu wa uvumilivu unaotokana na hali hiyo, unaweza kusababisha kulenga au uwezekano wa kuwasumbua wanawake watetezi wa haki za binadamu, ambao hukabiliwa na aina mbali mbali za ubaguzi mbaya zaidi na zinazokingana. Ukutambua kuwa usumbufu, unyanyasaji, ubaguzi na ukatili unaotokana na teknolojia ya habari na mawasiliano dhidi ya wanawake, wakiwemo wanawake watetezi wa haki za binadamu, kama usumbufu kwa njia ya mtandao, mazungumzo ya kisaiba, kuingilia faragha, kudhibitiwa na kuingiliwa barua pepe, simu za kiganjani na vifaa vyake vingine vya kieletroniki kwa lengo la kuwafedhehesha na/au kuchochea usumbufu na unyanyasaji zaidi dhidi yao, yanaongeza hofu na inaweza kuwa dalili za ubaguzi wa kijinsia kimfumo, inayohitaji hatua madhubuti zinazozingatia haki za binadamu,, Ukizingatia kuwa sheria za nchi na masharti ya kiutawala na utekelezaji wake sharti viwezeshe wanawake watetezi wa haki za binadamu kufanya kazi, kwa kuepuka ubaguzi wo wote au unyanyapaaji wa shughuli muhimu na jukumu halali la wanawake watetezi wa haki za binadamu na jamii wanamoishi au wanafanya kazi kwa niaba yao, na kuepuka vizuizi, vikwazo, udhibiti au utekelezaji wa kuchagua kinyume na vipengele husika vya sheria ya kimataifa ya haki za binadamu, Ukikumbuka kuwa jukumu la msingi la kuendeleza na kulinda haki za binadamu na uhuru wa msingi ni la Taifai, na kusisitiza kuwa sheria za kitaifa zinazokubaliana na Mkataba wa Umoja wa Mataifa na majukumu mengine ya kimataifa ya Taifa katika suala la haki za binadamu na uhuru wa msingi ni mfumo wa kisheria ambamo watetezi wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na wanawake watetezi wa haki za binadamu, hufanya shughuli zao, Ukiguswa sana kuwa, katika baadhi ya masuala, sheria za usalama wa taifa na kupambana dhidi ya ugaidi na hatua nyingine vimetumiwa vibaya kulenga watetezi wa haki za binadamu, wakiwemo wanawake watetezi wa haki za binadamu, au zimezuia kazi yao na kuhatarisha usalama wao kwa njia ambazo ni kinyume cha sheria za kimataifa, Ukitambua haja ya kushughulikia na kuchukuliwa haraka hatua madhubuti za kuzuia na kukomesha, matumizi ya sheria kuzuia au kuweka ukomo visivyo kwa uwezo wa watetezi wa haki za binadamu, wakiwemo wanawake watetezi wa haki za binadamu, kufanya kazi yao, pamoja na kupitia upya na panapohitajika, kurekebisha sheria husika na utekelezaji wake ili kuhakikisha utekelezaji wa wajibu na masharti ya Taifa kwa mujibu wa sheria ya kimataifa ya haki za binadamu. 3

Ukisisitiza haja ya kuchukuliwa hatua stahiki kubadilisha mielekeo ya kijamii na kiutamaduni ya mwenendo wa wanaume na wanawake kwa lengo la kutokomeza chuki na mila na desturi nyingine zinazotokana na wazo la uduni au ubora wa mojawapo ya jinsia au mawazo mgando kuhusu majukumu ya wanaume na wanawake, kwa kuzingatia wajibu wa na masharti ya nchi kwa mujibu wa sheria za kimataifa, na kwa njia hiyo kushughulikia mitazamo hatarishi, mila, desturi na mawazo mgando ya kijinsia yanayodumisha na kuendeleza ukatili dhidi ya wanawake, pamoja na wanawake watetezi wa haki za binadamu, Ukisisitiza tena kuwa uwezeshaji, kujitawala na maendeleo ya wanawake na uboreshaji wa hadhi yao kisiasa, kijamii, kisheria na kiuchumi ni muhimu ili kuheshimu haki zote za binadamu, ukuaji na ustawi wa jamii na mafanikio ya serikali na taasisi za kidemokrasia za uwakilishi, uwazi na uwajibikaji na maendeleo endelevu katika nyanja zote za maisha, Ukitambua kazi yenye thamani ya watetezi wa haki za binadamu, pamoja na wanawake watetezi wa haki za binadamu, katika kuendeleza haki za kiraia, kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni na haki ya maendeleo, Ukipokea fursa iliyotolewa na ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015 kwa jumuiya ya kimataifa ya kuendeleza haki za binadamu na uhuru wa msingi kwa watu wote, pamoja na usawa wa kijinsia na kukutokuwepo na ubaguzi, na ushiriki wa kweli na wenye kuleta lengo lililokusudiwa, pamoja na ushiriki sawa kisiasa, kwenye michakato ya utoaji maamuzi, Ukipokea pia hatua zilizochukuliwa na baadhi ya Mataifa katika kupitisha sera za kitaifa au sheria za kulinda watu binafsi, vikundi na vyombo vya jamii vinavyoshughulika na kuendeleza na kutetea haki za binadamu, pamoja na kama ufuatiliaji kwa utaratibu wa Baraza la Haki za Binadamu wa kupitia yote upya kwa vipindi, 1. Unatoa wito kwa Mataifa yote kuendeleza, kutafsiri na kutekeleza Tamko la Haki na Wajibu wa Watu Binafsi, Vikundi na Vyombo vya Jamii Kuendeleza na Kulinda Haki za Binadamu na Uhuru wa Msingi Zinazotambuliwa Ulimwengu,10 ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua stahiki, kali na zenye kutekelezeka kulinda wanawake watetezi wa haki za binadamu, 2. Unatambua na kuthamini kazi ya Katibu Maalum juu ya hali ya watetezi wa haki za binadamu, ukitambua uangalizi maalum wanaopewa wanawaake watetezi wa haki za binadamu, 11 3. Unasisitiza kuwa heshima na msaada kwa watetezi wa haki za binadamu, pamoja na wanawake watetezi wa haki za binadamu, ni muhimu kwa kufurahia kwa ujumla haki za binadamu, na kulaani aina zote za ukiukwaji wa matumizi mabaya ya haki za binadamu ufanywao dhidi ya watu 11 Rejea A/68/262, A/67/292 na A/HRC/16/44 na Corr.1. 4

wanaojishughulisha na uendelezaji na utetezi wa haki za binadamu na uhuru wa msingi, 4. Unatambua kuwa haki zote za binadamu ni kwa wote, hazigawanyiki na zinategemeana na kuwa jumuiya ya kimataifa sharti ishughulikie haki za binadamu ulimwenguni kote kwa haki na hali sawa, katika hali moja na kwa mkazo na msisitizo sawa, na unatilia mkazo kuwa, pamoja na kutilia maanani, umuhimu wa tofauti za kitaifa na kikanda na asili mbali mbali kihistoria, kitamaduni na kidini, ni wajibu wa Mataifa, bila kujali mifumo yao ya kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni, kuendeleza na kulinda haki zote za binadamu na uhuru wa msingi, 5. Unaeleza wasiwasi wa pekee juu ya ubaguzi na usumbufu wa kimfumo na kumuundo wanaokumbana nao wanawake watetezi wa haki za binadamu wa rika zote, na unatoa mwito kwa Mataifa kuchukua hatua zote zinazohitajika kuhakikisha ulinzi wake na kuunganisha mtazamo wa kijinsia na jitihada zao za kujenga mazingira wezeshi ya kutetea haki za binadamu, 6. Unasisitiza tena haki ya kila mtu, binafsi na kwa kushirikiana na wengine, kutetea haki za binadamu za wanawake katika vipengele vyake vyote, na kusisitiza jukumu muhimu la wanawake watetezi wa haki za binadamu katika kuendeleza na kulinda haki za binadamu na uhuru wa msingi, ambazo ni haki ya kila mmoja bila ubaguzi wa aina yo yote, pamoja na kushughulikia aina zote za ukiukwaji wa haki za binadamu, kupambana na kutoadhibiwa, kupambana na umaskini na ubaguzi na kuendeleza kupata haki,, demokrasia, ushiriki kamili wa wanawake ndani ya jamii, uvumilivu, hadhi ya kiutu, na haki ya maendeleo, ikikumbukwa kuwa kufaidika na haki hizi kuna wajibu na majukumu yaliyobainishwa kwenye Tamko, 7. Unayasihi Mataifa kutangaza hadharani umuhimu na uhalali wa jukumu la wanawake watetezi wa haki za binadamu katika uendelezaji na ulinzi wa haki za binadamu, demokrasia, utawala wa kisheria na maendeleo kama sehemu muhimu ya kuhakikisha ulinzi wao, pamoja na kulaani hadharani vurugu na ubaguzi dhidi ya wanawake watetezi wa haki za binadamu, 8. Unatoa wito kwa Mataifa kuhakikisha kuwa watetezi wa haki za binadamu, pamoja na wanawake watetezi wa haki za binadamu, wanaweza kutimiza wajibu wao muhimu katika muktadha wa maandamano ya amani, kwa mujibu wa sheria za kitaifa zinazoendana na Mkataba wa Umoja wa Mataifa na sheria za kimataifa za haki za binadamu, na kwa hili kuhakikisha kuwa hakuna matumizi ya nguvu nyingi au zisizokuwa na mpango, kukamatwa au kuwekwa kizuizini kiholela, kuteswa au matendo au adhabu nyingine za kikatili, kinyama au zenye kudhalilisha, mtu ye yote, kutoweka kwa nguvu, matumizi mabaya ya taratibu za kesi za jinai na kiraia au vitisho vya vitendo kama hivyo, 9. Unatoa wito pia kwa Mataifa kuwa makini katika kuzuia usumbufu na unyanyasaji dhidi ya watetezi wa haki za binadamu, pamoja na hatua kimatendo za kuzuia vitisho, usumbufu na ukatili dhidi ya wanawake watetezi wa haki za binadamu, ambao ukumbana na hatari za kipekee, na katika kupambana na 5

kutoadhibiwa kwa kuhakikisha kuwa wale wahusika wa ukiukwaji na unyanyasaji, pamoja na ukatili wa kijinsia na vitisho dhidi ya wanawake watetezi wa haki za binadamu, yanayotendwa na watendaji wa kitaifa au wasio wa kitaifa, pamoja na kwa mitandao, wanashtakiwa mara moja kwa upelelezi unaofuata haki, 10. Unatoa wito zaidi kwa Mataifa kuhakikisha kuwa uendelezaji na ulinzi wa haki za binadamu hauwi wa kihalifu wala kuwekewa ukomo kinyume cha wajibu na masharti yao kwa mujibu wa sheria za kimataifa za haki za binadamu na kuwa wanawake watetezi wa haki za binadamu hawazuiliwi kufurahia haki za binadamu wote kutokana na kazi yao, pamoja na kuhakikisha kuwa masharti yote ya kisheria, hatua za kiutawala na sera zinazoathiri wanawake watetezi wa haki za binadamu, pamoja na zile zinazolenga kuhifadhi maadili ya umma, zinaelezwa vizuri, zinaweza kuchunguzwa, zisizorudisha nyuma na zinazoendana na masharti ya sheria za kimataifa za haki za binadamu, 11. Unasisitiza kanuni ya msingi ya uhuru wa mahakama na kuwa tahadhari za kiutaratibu ziwepo kwa mujibu wa wajibu na masharti ya Kitaifa chini ya masharti ya sheria za Kimataifa za haki za binadamu ili kuwalinda wanawake watetezi wa haki za binadamu dhidi ya vitendo vya kiuhalifu visivyoidhinishwa na vikwazo kutokana na kazi zao zinazozjngatia Tamko. 12. Unasisitiza pia kuwa wanawake watetezi wa haki za binadamu wanahaki ya kufanya kazi au kutumia taaluma zao kihalali na kuwa kila mtu ambaye kwa utalamu wake anaweza kuleta hadhi ya binadamu, haki za binadamu na uhuru wa msingi wa wengine anatakiwa kuheshimu haki hizo na uhuru huo na wafuate viwango vya kitaifa na kimataifa vya maadili na tabia za kikazi na za kitaalamu. 13. Unatilia mkazo kuwa, wakati wa kutumia haki na uhuru vilizotajwa au kuainishwa kwenye Tamko, wanawake watetezi wa haki za binadamu binafsi au kwa kushirikiana na wengine watahusishwa na ukomo kama huo kwa mujibu wa masharti ya kimataifa yanayotumika na yamewekwa wazi kisheria kwa lengo la kutambuliwa ilivyo na kuheshimu haki na uhuru wa wengine na kufikia mahitaji ya haki kimaadili, usalama wa umma na ustawi kwa ujumla kwenye jamii ya kidemokrasia. 14. Unayasihi Mataifa kuimarisha na kutekeleza hatua za kisheria, kisera na nyinginezo kujenga usawa wa kijinsia, kuwezesha wanawake na kuendeleza upekee wao na kuendeleza na kulinda ushiriki sawa wao, uhusikaji kikamilifu na uongozi katika jamii, pamoja na utetezi wa haki za binadamu; 15. Unawakaribisha viongozi wa sekta zote za jamii na jumuia zao husika pamoja na viongozi wa kisiasa, kijeshi, kijamii na kidini na viongozi wa biashara na vyombo vya habari, kuelezea uungaji mkono wao kwa umma katika jukumu muhimu la wanawake watetezi wa haki za binadamu na uhalali wa kazi yao; 16. Unatoa wito kwa Maitaifa kutekeleza kwa ufanisi na haraka, maazimio ya Baraza la Usalama Na.1325 (2000) la tarehe 30 Oktoba 2000, 1820 (2008) la tarehe 19 Juni 2008, 1888 (2009) la tarehe 30 Septemba 2009, 1889 (2009) la tarehe 6

5 Oktoba 2009, 1960 (2010) la tarehe 16 Desemba 2010, 2106 (2013) la tarehe 25 Juni 2013 na 2122 (2013) la tarehe 18 Oktoba 2013 yanayohusu wanawake na amani na usalama, pamoja na masharti ya mafunzo yanayozingatia ujinsia kwa maafisa wa polisi na watumishi wanaohusika na usimamizi wa utekelezaji wa sheria, hususani juu ya vikwazo ambavyo wanawake watetezi wa haki za binadamu wanakumbana navyo katika kupata haki wakati na baada ya mapigano ya kijeshi, kuhakikisha ukatili wa kijisnia unaingizwa katika maana ya vitendo vinavyokatazwa na usitishaji wa mapigano na katika masharti ya ufuatiliaji wa usitishwaji wa mapigano na kuondoa kwa makosa ya ukatili wa kijinsia katika masharti ya msamaha katika mktadha wa michakato ya kutatua migogoro, kama hatua ya maendeleo katika kufanikisha ulinzi wa wanawake pamoja na wanawake watetezi wa haki za binadamu; 17. Unatoa wito wa nguvu kwa mataifa kujizuia na kuhakikisha ulinzi wa kutosha dhidi ya vitendo vyovyote vya vitisho au kisasi dhidi ya wanawake watetezi wa haki za binadamu wanaoshirikiana au wanaotafuta kushirikiana na taasisi za Kimataifa, pamoja na wanafamilia na washirika; 18. Unatilia mkazo haki ya kila mtu, binafsi na kwa kushirikiana na wengine, kufikia na kuwasiliana na vyombo vya Kimataifa hususani Umoja wa Mataifa, taratibu zake maalumu, utaratibu wa wote wa kuhakiki kwa vipindi na vyombo vya mkataba na taratibu za kikanda za haki za binadamu; 19. Unayasisitizia Mataifa kuandaa na kuweka sera za umma na mipango endelevu inayoeleweka na yenye kuzingatia ujinsia na inayounga mkono na kulinda wanawake watetezi wa haki za binadamu pamoja na kuwapatia rasilimali za kutosha kwa ulinzi wa papo hapo na wa muda mrefu na kuhakikisha kuwa yote hayo yanaweza kupatikana kwa njia zinazoendana na haki na kwa muda muafaka kuhakikisha ulinzi wa kimwili na kisaikolojia unaofaa, wakati zikitoa pia hatua za ulinzi kwa ndugu zao, wakiwemo watoto na vinginevyo kufikiria jukumu la wanawake watetezi wa haki za binadamu wengi kama watoaji pekee wa mafunzo muhimu katika familia zao. 20. Unatilia mkazo haja ya kushiriki kwa wanawake watetezi wa haki za binadamu katika kuandaa sera na mipango inayofaa inayohusiana na ulinzi wao, kwa kutambua uhuru na utaalamu wao kufuatana na mahitaji yao, na haja ya kujenga na kuimarisha taratibu za mashauriano na mazungumzo na wanawake watetezi wa haki za binadamu kama kuwa na kitengo maalum cha watetezi wa haki za binadamu katika utawala wa umma, kwa mfano, kwa kupitia taratibu za kitaifa za maendeleo ya wanawake na wasichana, zilipo tayari, au taratibu nyingine, kufuatana na muktadha wa kitaifa na mahalia;. 21. Unasisitizia Mataifa kupitisha na kutekeleza sera na mipango ya kuwawezesha wanawake watetezi wa haki za binadamu, kupata fidia pamoja na kuhakikisha: (a) Ushiriki wa wanawake watetezi wa haki za binadamu unaofaa katika hatua zote, pamoja michakato ya mpito.ya kupata haki, kuwajibishwa kwa ukiukwaji na unyanyasaji na pia kuhakikisha kuwa uhakiki wa kutorudia unajumuisha 7

kuondoa vyanzo vya msingi vya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji katika maisha ya kila siku na kwenye taasisi. (b) Upatikanaji wa kutosha wa misaada ya huduma zinazofaa kwa wale watetezi wa haki za binadamu wanaokumbana na usumbufu, pamoja na malazi, huduma za kisaikolojia, ushauri, matunzo ya kimatibabu na huduma za kisheria na kijamii. (c) Kuwa wanawake watetezi wa haki za binnadamu waathirika wa vurugu za kijinsia na aina nyinginezo za vurugu wanahudumiwa na watumishi waliopata mafunzo ya kutosha na wenye mwamko wa kijinsia na utalaamu na wanaombwa ushauri kwa kila hatua ya mchakato. (d) Kuwa wanawake watetezi wa haki za binadamu wanaweza kuepuka mazingira ya vurugu, pamoja na kuzuia kutokea au kurudia kutokea kwa aina hizo za vurugu wakati wa kutimiza jukumu lao muhimu na halali kwa mujibu wa azimio hilo 22. Unayasisitizia pia Mataifa kuendeleza na kusaidia miradi ya kuboresha na kuendeleza zaidi uhifadhi wa nyaraka na ufuatiliaji, wa kesi za usumbufu dhidi ya wanawake watetezi wa haki za binadamu, na kuhimiza utoaji wa msaada wa kutosha na rasilimali kwa wale wanaofanya kazi ya kuwalinda wanawake watetezi wa haki za binadamu, kwa mfano mawakala wa serikali, taasisi za kitaifa za haki za binadamu na asasi za kiraia pamoja na asasi kitaifa na kimataifa zisizo za kiserikali. 23. Unahimiza taasisi za kitaifa za haki za binadamu kusaidia katika utunzaji wa nyaraka za vurugu dhidi ya wanawake watetezi wa haki za binadamu na kujumuisha mwelekeo wa kijinsia katika mipango na utekelezaji wa programu zote na shughuli nyingine zinazohusiana na watetezi wa haki za binadamu, pamoja na kushauriana na wadau husika. 24. Unahimiza taratibu za ulinzi za kikanda, zilipo, kuendeleza miradi ya kuboresha na kuendeleza zaidi uhifadhi wa nyaraka za kesi za vurugu dhidi ya wanawake watetezi wa haki za binadamu na kuhakikisha kuwa mipango ya usalama na ulinzi wa watetezi wa haki za binadamu zinajumuisha muelekeo wa kijinsia na kushughulikia hatari mahususi na mahitaji ya kiusalama ya wanawake watetezi wa haki za binadamu. 25. Unahimiza vyombo, wakala na vitengo vingine vya Umoja wa Mataifa, ndani ya uwezo wao wa kuwakilisha na kwa kushirikiana na Katibu Maalum na Ofisi ya Kamishna wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, kushughulikia hali ya watetezi wa haki za binadamu na kuchangia katika utekelezaji muafaka wa Tamko. 26. Unaomba wakala na mashirika yote ya Umoja wa Mataifa, ndani ya uwezo wao, kutoa misaada yote inayowezekana kwa Katibu Maalum ili akamilishe vizuri jukumu lake, pamoja na kwa muktadha wa ziara za nchi na mapendekezo ya kuhakikisha ulinzi wa wanawake watetezi wa haki za 8

binadamu; 27. Unaomba Katibu Maalum kuendelea kutoa taarifa ya shughuli zake kila mwaka kwa Mkutano Mkuu na Baraza la Haki za Binadamu, kwa mujibu wa jukumu lake. 28. Unaamua kuendelea kufikiria suala hili. Mkutano wa Wote wa 70 18 Desemba 2013. 9