UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO

Similar documents
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II

Information for assessors (do not distribute this page to participants):

Kufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007

KITEGO CHA MAREKEBISHO NA HAKI ZA MTOTO

Tufundishane! Mwalimu Bora In this issue: Issue 6, December Do you want to be in our next issue?

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

Nilikua na Ndoto ya Kumaliza Shule Changamoto za Elimu ya Sekondari Tanzania

Ufanisi katika Ufundishaji kwenye Shule za Msingi na Sekondari nchini Tanzania

Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA III VI

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

TANZANIA MARKETS PAN Sera zinazoboresha masoko

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU

Dibaji ya Mwenyekiti wa Kamati ya Pamoja ya Uongozi

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig

TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM)

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

Elimu Ina Umuhimu gani katika Jamii? Kuelekea Elimu Sahihi

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA. Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo. TOLEO Na.

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA

Elimu-Jumuishi Kwa Vitendo

JAMHURI YA KENYA. Mkakati wa Ushirikiano MUKHTASARI FY Public Disclosure Authorized. Public Disclosure Authorized

Songa kwenye kilele cha upeo. Masuala ya Msingi na Ujuzi juu ya Uendeshaji wa Serikali za Mitaa

Ufundishaji wa lugha nyingine

5. Mheshimiwa Spika, Bunge lako Tukufu lilijadili kwa kina Miswada ifuatayo:

Mwongozo wa Mwezeshaji

FOMU YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO

Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame M. Mbarawa (Mb.); Waheshimiwa Mawaziri na Wabunge wote mliohudhuria;

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

LUGHA YA KISWAHILI KATIKA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA ELIMU SHULE ZA SEKONDARI

Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara)

Makala ya Mshiriki wa Mafunzo

NGUZO KUMI ZA KILIMO KWANZA

Miradi na jamii. 3.1 Utangulizi

KUSHUKA KWA HADHI YA LUGHA ZA JAMII NCHINI TANZANIA YOHANA P. MSANJILA University of Dar es Salaam, Tanzania

MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA PRO-ROUTES. Ombi kwa ajili ya fedha za umma wa mradi wa ziada

HALMASHAURI YA WILAYA YA SUMBAWANGA

SautiElimu. Sauti Yako Isikike

Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA 2006/07

Human Rights Are Universal And Yet...

Sera ya Faragha. Upeo. Aina za Data na Mbinu za Ukusanyaji

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Mwongozo wa Utekelezaji wa Njia za S5-UUE (KAIZEN)-UUU Tanzania

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu WEMA

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara

Mazoezi yaliyofanyika wakati wa warsha kuhusu Elimu-Jumuishi kwa Vitendo. Zanzibar, 7-10 Februari 2006

UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU VIKWAZO VYA KULINDA MAISHA KATIKA USAIDIZI WA KIMATAIFA WA AFYA KWA MSAADA WA KIMATAIFA UNAOFADHILIWA NA MAREKANI

MAPENDEKEZO YA MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA TANZANIA

4. Kanuni za Petroli (Ushiriki wa Watanzania) za mwaka 2017 zilianza kutumika rasmi tarehe 5 Novermba Shughuli za Petroli za kwanza ni

Programu ya Uendelezaji Mifumo ya Maji Vijijini (PUMMV) katika Tanzania. Modeli wa Ukodishaji Mradi

MITAZAMO KUHUSU KISWAHILI MIONGONI MWA WAZUNGUMZAJI WA KIJALUO: KIFANI CHA SHULE ZA MSINGI KATIKA KAUNTI YA MIGORI. OWALA JAEL AKINYI C50/75493/2012

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

Draft 03 MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO MWENGE

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

UHUSIANO WA MIKAKATI YA UFUNDISHAJI WA FASIHI YA WATOTO YA KISWAHILI NA UMILISI WA KUSOMA KATIKA SHULE ZA MSINGI, KASARANI, KAUNTI YA NAIROBI, KENYA

MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2017/18

Kutetea Haki za Binadamu

KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA

RIPOTI YA WARSHA KUHUSU HABARI KWA AJILI YA UWAJIBIKAJI

Kitabu Cha Mafunzo Ya Uongozi Kwa Wanawake

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees

3. Mheshimiwa Spika, 4. Mheshimiwa Spika,

UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA)

KAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI TANZANIA

Kumb.Na.BSS/A.6/33 Tarehe: 18 Juni 2018 YAH: MAAGIZO YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2018/2019

Mwongozo wa Mafunzo Yaliyochanganywaya K4Health

MAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI

Azimio lililopitishwa na Mkutano Mkuu tarehe 18 Desemba 2013 [juu ya taarifa ya Kamati ya Tatu (A/68/456/Add.2)]

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI-TAMISEMI HALMASHAURI YA WILAYA BUMBULI

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, MHESHIMIWA DKT. PHILIP I. MPANGO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO

YAH: MAAGIZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI KAREMA KIDATO CHA TANO MWAKA 2018

Elimukombozi, Lugha na Upashanaji Habari nchini Tanzania, katika Muktadha wa Utandawazi

Kumb.Na.HVEMS/JI/BT/018 Novemba 17, YAH: MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE CHINI YA TAASISI YA ROCK MEMORIAL EDUCATION TRUST 2018

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

HAKI NA TARATIBU ZA AJIRA, KAZI NA HIFADHI YA JAMII

TAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF) KUHUSU HAKI ZA WATOTO KATIKA KATIBA MPYA

Bustani 10,000 Katika Afrika. Alberto Prina

Kimesanifiwa na:- E.D.Kissuu ECOMM TANZANIA S.L.P ,Dar es Salaam. Simu:

ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA UCHUMI WA ZANZIBAR

Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali ya Madini Ukanda

Mwongozo wa Familia wa Kujifunza

International Labour Office. Kazi za Ndani Zenye Madhara kwa Watoto: Kijitabu cha Maelezo Mafupi

Evaluation of Contextual Teaching of Kiswahili Proverbs in Secondary Schools in Kenya

Vyote Unavyopaswa Kujua Kuhusu Viazi Vitamu

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MANISPAA YA BUKOBA.

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA. Kwa Wanaoanza

KUHUSU AFRODAD. Dira ya AFRODAD. Dhamira ya AFRODAD. AFRODAD inalenga mchakato sawa na endelevu wa maendeleo kuelekea Afrika yenye mafanikio.

Yaliyomo. Kuhusu kitabu hiki. Hautakuwa peke yako. Mfumo wa msaada ni wa manufaa sana wazazi wote wanahitaji!

USIMAMIZI MKUU WA UBORA WA MAHURUJI

JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI

Kubadili Sheria Za Mbegu Na Ulinzi Wa Aina Za Mbegu Na Mimea Nchini Tanzania

HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE

Mwongozo wa Kutathimini mifumo ya Ugawanaji wa faida na Mapato Katika Miradi ya Jamii ya MKUHUMI

BUNGE LA TANZANIA MKUTANO WA NANE. Kikao cha Ishirini na Nane Tarehe 16 Julai, (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A

NAFASI ZA MASOMO MASOMO YA ASUBUHI

Transcription:

UTANGULIZI International Montessori Teachers College (IMTC), ni chuo kilichoanzishwa hapa nchini Tanzania mwaka 2012 na kinatoa kozi ya kimataifa ya ualimu wa watoto wadogo (yaani child care and nursery school teachers), kwa ngazi ya cheti na diploma. Chuo hiki kimeanzishwa hapa nchini, ili kukidhi hitaji la upatikanaji wa walezi wa watoto na waalimu bora wa elimu ya awali wenye viwango na ubora unaokubalika kitaifa na kimataifa. ANUANI NA MANDHARI YA CHUO Chuo kimejengwa katika eneo tulivu na salama lililopo katika kijiji cha Mapinga, jirani na Daraja linalotenganisha Mkoa wa Dar es salam na Wilaya ya Bagamoyo. Aidha, chuo kina mazingira yaliyoandaliwa maalumu ili kumwezesha mwalimu mtarajiwa kupata ujuzi unaoendana na aina ya ujuzi anaoupata chuoni na kazi atakayoifanya mara baada ya kuhitimu mafunzo yake. KUTAMBULIKA KWA CHUO CHA IMTC International Montessori Teachers College (IMTC), tunatambuliwa na kushirikiana na Serikali jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuhakikisha tunaandaa walezi wa watoto na walimu wa elimu ya awali wenye elimu, ujuzi na viwango vya kitaifa na kimataifa katika stadi za malezi na ufundishaji wa watoto. Pia, tunao usajili wa kudumu wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (National Council for Technical Education). Naomba yetu ya usajili ni NACTE No. REG/TLF/012. Usajili huo unatuwezesha kutoa mafunzo ya ngazi ya cheti na diploma kwa walezi na walimu wa elimu ya awali kuanzia ngazi ya NTA Level 4 hadi NTA Level 6. Pia, chuo hiki kimesajiliwa na kinashirikiana na Wizara ya afya na Ustawi wa jamii kutoa mafunzo ngazi ya cheti, kwa kozi ya huduma ya malezi ya watoto.

Kusajiliwa, kutambulika na kushirikiana na taasisi za Serikali zinazosimamia elimu na malezi ya watoto kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, kunamhakikishia mhitimu katika IMTC mambo makuu matatu kama ifuatavyo:- (a) Ubora wa elimu inayotolewa, (b) Uhakika wa nafasi ya ajira mara baada ya kuhitimu katika shule za Serikali au katika shule zinazomilikiwa na watu binafsi ama taasisi na mashirika, (c) Fursa na uhuru wa kujiendeleza kwenye chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali kwa ajili ya masomo ya digrii, nk. MIFUMO YA UFUNDISHAJI Tunao wakufunzi wa ngazi na viwango vya kimataifa, wanaotumia mbinu na stadi zinazomwezesha kila mwanachuo kujitambua, kujiamini na kujipatia ujuzi wa malezi na ufundishaji wa watoto wadogo. Aidha, ufundishaji wetu unazingatia nadharia na vitendo kama ifuatavyo:- (a) Mafunzo ya nadharia ya Darasani Ufundishaji wa nadharia unaambatana na utumiaji wa mifumbo mbalimbali ya teknolojia kama vile powerpoint, video na oudio. Aidha, walimu wanatumia mbinu shirikishi na mijadala ili kuhakikisha kila mwanafunzi anafikiwa, anajifunza na kufikia malengo. (b) Mafunzo kwa vitendo ya namna ya kutumia vifaa kufundisha watoto Tunalo darasa maalumu lenye vifaa mbalimbali, tunalolitumia kufundisha kwa vitendo. Lengo likiwa ni kumwezesha kila mwanafunzi kujua namna ya kutumia vifaa mbalimbali kulea na kufundisha watoto. Aidha, uwepo wa darasa hilo unatoa uhuru kwa mwanachuo kutumia muda wake wa ziada kufanya mazoezi kwa vitendo kadri anavyoweza ili kuhakikisha anatimiza malengo yake ya kujizoeza, kupata ujuzi na kufaulu vizuri majaribio ya kitaaluma. (c) Mafunzo kwa vitendo ya namna ya kutengeneza vifaa vya kufundishia watoto Chuo kinaendesha mafunzo kwa vitendo kwa kuwafundisha wanafunzi jinsi ya kutengeneza seti za vifaa mbalimbali vya

kufundishia watoto. Vifaa hivyo ambavyo vina thamani ya zaidi ya milioni tano, mwanachuo uondoka navyo mara baada ya kuhitimu mafunzo ili aweze kujiajiri au kuvitumia mara anapokuwa ameajiriwa. Vifaa hivyo vyenye thamani ya zaidi ya milioni tano vimegawanyika katika makundi yafuatayo:- (i) (ii) (iii) (iv) (v) (vi) (vii) (viii) Vifaa vya kumjenga mtoto ili aweze kujitegemea katika maisha yake Vifaa vya kutafiti na kuchochea ukuaji wa milango ya fahamu ya mtoto Vifaa vya kumfundisha mtoto stazi za lugha na mawasilino Vifaa vya kumfundisha mtoto stadi za Hisabati Vifaa vya kumfundisha mtoto stadi za jiografia Vifaa vya kumfundisha mtoto stadi kuhusu mazingira Vifaa vya kumfundisha mtoto stadi za sayansi Vifaa vya kumfundisha mtoto asili na utamaduni (d) Mazoezi kwa vitendo shuleni Chuo kinamiliki na kuendesha shule ya awali ambayo uwawezesha wanachuo kujifunza kwa vitendo tabia, mienendo na malezi ya watoto. Pia, kwa kushirikiana na shule za awali washirika, chuo uwapangia wanachuo kufanya mafunzo ya mazoezi kwa vitendo chini ya uangalizi maalumu. Mazoezi hayo uwawezesha wanachuo kuimarisha ujuzi wao kwa vitendo kuhusu malezi ya watoto, mfumo wa ufundishaji wa watoto wadogo, utaratibu wa uendeshaji wa vituo vya kulea watoto na shule za awali, n.k. Utaratibu huu wa mazoezi kwa vitendo kwa wanachuo, pia ufungua milango ya uhakika wa fursa za ajira mara baada ya kuhitimu. Kwa

sababu waajiri na wamiliki wa shule upata fursa za kujua uwezo wa waajiriwa watarajiwa kabla ya kuingia katika soko la ajira. Pia, sifa na uwezo wa kila mwanachuo wa kumudu majukumu yake utambulika na kujulikana. UTARATIBU WA KUJIUNGA IMTC Mtu yeyote anayetaka kujiunga na International Montessori Teachers College (IMTC), anatakiwa kufika chuoni ili aweze:- (a) Kupata maelezo, kujionea na kujiridhisha (b) Kuchukua fomu ya maombi, kuijaza na kuirejesha kwa wakati (fomu inapatikana chuoni tu) (c) Kufanya mahojiano na majaribio ya kupima uwezo wa uelewa na mapenzi kwa watoto (d) Kukamilisha taratibu za kiutawala VIGEZO MUHIMU VINAVYOHITAJIKA Vigezo muhimu vinavyozingatiwa ili uchaguliwe kujiunga na International Montessori Teachers College (IMTC), ni:- (a) Kuwa mhitimu wa elimu ya sekondari, kidato cha nne au zaidi, (b) Mtu yeyote mwenye elimu ngazi ya cheti au zaidi (cheti kilichotolewa na taasisi au chuo kinachomilikiwa na Serikali au chuo kilichosajiliwa na kutambuliwa na Serikali), (c) Au mwenye cheti cha kuhitimu mafunzo ya malezi ya watoto kinachotolewa na Idara ya Ustawi wa Jamii, (d) Mwenye wito wa kulea na kufundisha watoto, (e) Kwa wanafunzi wa kigeni:-

Chuo chetu ni cha viwango vya kimataifa, hivyo kinatoa fursa kwa raia wa kigeni kujiunga na kozi zinazotolewa. Utaratibu wa kujiunga kwa raia wa kigeni umefafanuliwa katika kurasa za website yetu. Hata hivyo, ni muhimu pia kufahamu kwamba mhitimu katika chuo chetu anakuwa na misingi ya viwango, vigezo na uwezo wa kufanya kazi katika nyanja aliyoisomea popote duniani. KOZI ZITOLEWAZO Chuo kinatoa kozi za ualimu wa watoto wadogo kama ifuatavyo: 1. Diploma ya ualimu na malezi ya watoto Kozi hii ni ya muda wa miaka miwili (2), na ina masomo yafuatayo:- Child Development Teaching Methodology School Management Safety And First Aid Communication skills Education philosophy General knowledge Nutrition Mathematics Arts and raft Language- English and Kiswahili Leadership Health Civics Moja ya faida za kusoma kozi hii ni kuwezeshwa kuwa na ujuzi kamili wa kutengeneza vifaa vya kulea na kufundishia watoto. Pia mwanachuo akihitimu umilikishwa na kuruhusiwa kuondoka na vifaa vyote alivyovitengeneza wakati wa mafunzo. 2. Cheti cha ualimu na malezi ya watoto Kozi hii ni ya muda wa mwaka mmoja (1), na ina masomo yafuatayo:- Child Development

Safety And First Aid Communication skills Education philosophy Montessori philosophy General knowledge Health & Nutrition Arts and raft Language- English and Kiswahili Civics Kozi hii haiambatani na utengenezaji wa vifaa vya kulea na kufundisha watoto. MFUMO WA KUPIMA UWEZO NA UELEWA - MITIHANI Mitihani ya kupima uelewa na ujuzi ni asilimia 100%. Asilimia hizi hupatikana kwa njia mbili, nazo ni jumla ya mazoezi na majaribio yote ya nadharia na vitendo ni 80% na mtihani wa mwisho wa mwaka ukamilisha alama 20% ili kutimia 100% UJUZI MWINGINE UNAOTOLEWA CHUONI Mafunzo ya ICT Chuo kinatoa mafunzo ya matumizi ya kompyuta bure kwa kila mwanachuo. Mafunzo haya yanalenga kumpa ujuzi wa ziada na kumwandaa mwanachuo kutumia ICT katika mfumo wa ufundishaji na kujifunza. Aidha, utaratibu huu unamwezesha mwanachuo kuwa ni mlezi na mwalimu anayekwenda kwa wakati kwa kuzingatia mifumo ya kisasa ya elimu, habari na mawasiliano. Pia, mfumo huu unatoa fursa kwa kila mwanachuo kutumia rasilimali hizo kutafuta taarifa mbalimbali zinazohusiana na masomo yake. Ujasiliamali na stadi za maisha Kwa kuzingatia mahitaji ya ajira na kujiajiri, chuo kinaendesha mafunzo maalumu yanayomjengea uwezo mwanachuo ili aweze kujiajiri mara baada ya kuhitimu. Utaratibu huu maalumu unamwezesha mwanachuo kujitambua,

kujiamini na kutumia fursa za ujuzi anaopewa ili kuwa chachu ya mabadiliko katika mfumo wa maisha yenye changamoto ya kukosekana kwa ajira. Aidha, mfumo wetu wa ufundishaji ni wa aina ya pekee na unazingatia mbinu ya elimu ya kujitegemea. Pia unamjenga na kumwezesha mwanachuo kuwa na ujuzi wa kutengeneza vifaa vya kufundishia ambavyo ni nyezo na mtaji wa kuweza kumudu kuanzisha kituo kwa ajili ya kutoa elimu ya awali kwa watoto. Vile vile mwanachuo anapewa mafunzo maalumu yanayomwezesha kutoa huduma ya ushauri nasaha kwa watoto na wazazi kuhusu ustawi na maendeleo ya watoto. Mafunzo ya upigaji picha kwa njia ya video Kila mwachuo anafundishwa ujuzi wa kutumia vifaa vya kisasa ili kuchukua na kuhifadhi kumbukumbu za watoto kwa njia ya picha, video na sauti. Utaratibu huu unazingatia ukweli kwamba, kila aliyefanikiwa hapa duniani amepitia katika mikono ya walezi na walimu walipo katika shule hasa za awali, ingawa kumbukumbu za walio wengi hazikuwekwa au kuhifadhiwa. Hivyo ili kukidhi hitaji hilo la kuweka kumbukumbu za watoto, chuo kimejenga studio za kisasa zenye vifaa vinavyotambulika kwa ubora ulimwenguni kwa lengo la kufanikisha utoaji wa ujuzi huo na kumwandaa mwanachuo kuweza kuchukua na kuhifadhi kumbukumbu za matukio muhimu ya watoto wanaopita mikononi mwake katika mchakato mzima wa malezi. Matuki hayo ni kama vile kumbukumbu za siku za kuzaliwa za watoto wa shule yake, kumbukumbu za mahafali, n.k Sanaa na ubunifu Moja ya misingi na aiba ya mlezi na mwalimu wa watoto wadogo, ni kuwa na vipaji vya ubunifu na sanaa. Ubunifu katika ufundishaji wa watoto unaoambatana na michezo na sanaa mbalimbali, urahisisha mfumo wa uamishaji wa maarifa na ujuzi kutoka kwa mwalimu kwenda kwa watoto. Hivyo, mkakati wa IMTC ni pamoja na kumwandaa mwanachuo kutumia michezo, sanaa na ubunifu katika kulea na kuwafundisha watoto. Lakini pia

unamjengea mwalimu na mlezi mtarajiwa uwezo wa stadi za kutambua vipaji vya watoto na mbinu za kuviendeleza. Huduma ya kwanza na usalama wa watoto Moja ya mafunzo yanatolewa katika mtaala wa masomo ni suala la ulinzi wa watoto, huduma ya kwanza na uokoaji. Mafunzo hayo humjengea mwanachuo stadi za tahadhari. Lakini pia umjengea uwezo wa kiufahamu wa hatua za kuchukua katika kukabiliana na ajali au majanga mbalimbali. ADA International Montessori Teachers College (IMTC), kwa kutambua mahitaji ya jamii kulingana na kipato cha Watanzania walio wengi, tumeweka utaratibu wa ulipaji wa ada unaozingatia uwezo wa kila mwanafunzi. Hivyo, ulipaji wa ada kidogo kidogo unajadiliwa na kuruhusiwa. HUDUMA NYINGINE MUHIMU ZINAZOTOLEWA NA CHUO Chuo kinamiliki hosteli nzuri yenye hadhi iliyojengwa katika mazingira ya chuo na huduma hii hutolewa bure kwa kila mwanachuo. Aidha, mazingira ya vyumba vya kulala ni mazuri na yenye vitanda na magodoro na huduma nyingine muhimu kama vile:- Maji safi na salama Umeme wa uhakika Ulinzi Viwanja vya michezo Chakula, nk.