Jina Nambari.. Shule... 102/3 KISWAHILI FASIHI KARATASI YA 3 JULAI / AGOSTI. 2007 MUDA: SAA 2 ½ MTIHANI WA MWIGO WILAYA YA BUTERE MUMIAS-2007 Hati ya kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya 102/3 KISWAHILI FASIHI KARATASI YA 3 JULAI / AGOSTI. 2007 MUDA: SAA 2 ½ MAAGIZO Jibu maswali manne Swali la kwanza ni la lazima Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja. Karatasi hii ina kurasa 4 zilizopigwa chapa 1
Watahiniwa lazima wahakikishe kurasa zote zimepigwa chapa sawa sawa na kuwa maswali yote yamo. USHAIRI Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. 1. Lau dunia nanena, tuseme si ati ati, Mauti kawa hakuna, katika wote wakati, Vipi tungelisongana, tunaoishi tiati? 2. Dunia ingetatana, na kizazi katikati, Huku kwazaliwa bwana, kule kwazawa binti, Vipi tungeliona, na kuzaa hatuwati? 3. Lau mauti hakuna, tungesongana sharuti, Kwa viumbe kukazana, wanadamu na manyati, Vipi tungelijazana, kwa kusitawi umati? 4. Walakini subuhana, kapanga sisi na miti, Ili tusizidi sana, si wengi na si katiti, Maisha ya kupishana, yule ende yule keti, 5. Ndipo dunia kufana, ikawa kama yakuti, Kwa uwezewe Rabana, kaipanga madhubuti, Maisha kugawiana, kayagawa kwa mauti, 6. Njia ingekuwa hapana, pembeni na katikati, Sote tungeambatana, pa kulima hatupati, Na njaa ingetutafuna, pa kulima hatupati, 7. Peleleza utaona, hayataki utafiti, Kama tungelikongana, ingelikuwa ni bahati, 2
Vipi tungelisukumana, katika hiyo hayati? 8. Mbele sitakwenda tena, hapa mwisho nasukuti, Yaeleni waungwana, shauri yake jabaruti, Yote tuloelezana, katenda bila senti, MASWALI a) Shairi hili ni la bahari gani? (alama 2) b) kwa kutoa mifano mwafaka onyesha jinsi mtunzi wa shairi hili alivyotumia uhuru wa utunzi (alama 2) c) Eleza muundo wa shairi hili (alama 4) c) Andika ubeti wa tano katika lugha nathari. (alama 4) d) Tambulisha mbinu zozote mbili za lugha zilizotumiwa na mshairi (alama 4) e) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika shairi i)katiti ii) yakuti iii) Hatuwati iv) Nasukuti (alama 4) SEHEMU B KIFO KISIMANI: KITHAKA WA MBERIA 2. Eleza jinsi utawala wa mtemi Bokono unavyodhihirisha udikteta. (alama 20) AU 3. --- kimoja hakipo tena kimenyakuliwa na kozi. Mheshimuni kozi. a) Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4) b) Taja na ueleze mbinu mbili za lugha zinazojitokeza katika dondoo hili. 3
(alama 4) c) Kipi kinachonyakuliwa na kina umuhimu upi? (alama 6) d) Fafanua sifa za mnenaji (alama 6) SEHEMU YA C MWISHO WA KOSA 4. Jadili jinsi mwandishi alivyoisawiri jinsia ya kike (alama 20) Au Ninajua hayo. Juu ya hivyo sidhani kuwa tunaweza kufanya lolote. Hatuwezi kuyaingilia, hayo ni maisha yao. Ni yeye tu Muna, atakayeweza kutenda lolote. a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4) b) Mzungumziwa alikuwa na nia gani. (alama 4) c) Kwa vipi msemaji anaweza kulaumiwa kwa kuchangia katika jambo analolishughulikia. (alama 4) d) Eleza visababisho vinne vya ugomvi kati ya Muna na Hasani. (alama 8) SEHEMU YA D HADITHI FUPI: MAYAI WAZIRI WA MARADHI 6. Eleza maswala yafuatayo jinsi yanavyojitokeza katika hadithi ya mayai waziri wa maradhi. AU a) Ukombozi b) Uongozi mbaya c) Elimu d) Ushirikina (alama 20) 7. Majuto ni mjukuu, Onyesha ukweli wa methali hii kwa kurejelea hadithi zifuatazo. a) Uteuzi wa moyoni. b) Ndimi za mauti. c) Pwaguzi d) Fumbo la mwana. (alama 20) SEHEMU YA E FASIHI SIMULIZI 8. a) Taja na ueleze aina zozote tano za Hadithi. (alama 5) b) Tofautisha kati ya (i) Mbolezi na Bembezi (ii) Vitendawili na chemsha bongo. (alama 4) 4
c) Eleza umuhimu wa vitanza ndimi (alama 3) d) Taja na ueleze sifa nne ambazo mtambaji anapaswa kuwa nazo. (alama 4) e) (i) Fafanua maana ya methali. (alama 2) (ii) Taja methali zinazohusu: a) Kilimo b) Kuliwaza. (alama 2) MWISHO 5