Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Similar documents
Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI VIDOKEZO MUHIMU KATIKA UNUNUZI NA USALAMA WA CHAKULA

Information for assessors (do not distribute this page to participants):

Utangulizi wa ugonjwa wa shinikizo la damu

MTI KWA MATUMIZI YA KILA AINA HDRA

KILIMO CHA VITUNGUU MAJI NA VITUNGUU TWAUMU (SWAUMU)

Uwepo, Athari na Udhibiti wa Sumu-Suvu Kwenye Vyakula vya

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Mfumo na maelezo ya kina ya mpango wa kimataifa wa viwango vya chakula kwa wenye matatizo ya kumeza (IDDSI) Juni 2017

PYRINEX. 1 Liter INSECTICIDE

Picha ni hati miliki ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Watoto(PCD), Imperial College London. Maelezo

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees

2 Usimamizi wa Rutuba ya Udongo Tanzania Organic Agriculture Movement

Jamii. ,,,^mm^mmm-<^^^^ illli MA RH-EREN.CE CENTRE

AMMA KWA AFRIKA RATIBA/ITIKADI. Ratiba Maalum ya Kutibu Magonjwa Maambukizi na Hususan Fikra Zinazoleta Pooza Mwili na Akili

Siku ya kwanza. Mguso wa ngozi-kwa-ngozi (Ulezi wa kangaruu) Mtoto wako anaweza kuhisi mdundo wa moyo wako

Njia Bora za Ukusanyaji na Upimaji Maziwa

TIST HABARI MOTO MOTO

Uzalishaji wa mboga na matunda ni muhimu kwa afya na kipato

Bustani 10,000 Katika Afrika. Alberto Prina

Ni kwa nini mkulima awe maskini?

MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA. Kwa Wanaoanza

UMRI WA MAKAMO NA KUKOMA KWA HEDHI

Njia bora za ukusanyaji na upimaji maziwa

Kuwa na Ukimwi ni kama vile kutakiwa kuendelea kuuzima moto unaoniunguza bila kukoma.

4 WADUDU,MAGONJWA NA MAGUGU

Muongozo wa utatuzi. Kwa wasimamizi wa malaria RDTs 06/11/16. MALARIA Rapid Diagnostic Test

Teknolojia za Utayarishaji, Usindikaji na Matumizi ya Matunda na Mboga baada ya kuvuna

Shamba Darasa na Stadi za Maisha kwa Vijana (SDSMV) Tanzania. Kiongozi Cha Mwezeshaji. Jaap Van Pol na Francesca Dalla Valle

MTIHANI WA MWIGO WA WILAYA YA NANDI KASKAZINI 2013

Mwongozo wa Kitaifa wa Ujumbe wa Uzazi wa Mpango

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti

TIST HABARI MOTO MOTO MAANDALIZI YA MWAKA 2000 Y2K PREPARATIONS SASA NI WAKATI WA KUANZA KUPANDA MBEGU ZAKO

Uzio wa pilipili unazuia tembo kuvamia mazao shambani! Jinsi ya kujenga na kudumisha uzio wa pilipili Tanzania

Kuwawezesha wasichana kwa kuboresha kujikubali na kujithamini Hivi Ndivyo Nilivyo

pages/mkulima-mbunifu/

KUZALISHA MBEGU YA MAHARAGE KIJITABU CHA KWANZA

Kijitabu cha Maelezo cha Programu ya Famasia

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

Human Rights Are Universal And Yet...

Mwongozo huu wa ufugaji kuku wa Asilia umezinduliwa rasmi leo tarehe 1 Agosti 2009 wakati wa sikukuu ya Wakulima Tanzania mjini Mbeya

Makala ya Mshiriki wa Mafunzo

Yaliyomo. Kuhusu kitabu hiki. Hautakuwa peke yako. Mfumo wa msaada ni wa manufaa sana wazazi wote wanahitaji!

TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM)

Wewe Maisha Yako Ndoto Zako. Kitabu cha Vijana Balehe

Mukhtasari Wa Mabishano Kwa Na Dhidi Ya Vikombe Vingi Vya Ushirika

Utunzaji, Uhifadhi na Usafirishaji Bora wa Maziwa

Kubadili Sheria Za Mbegu Na Ulinzi Wa Aina Za Mbegu Na Mimea Nchini Tanzania

Palliative Care Toolkit

Wadudu na magonjwa ya mazao

Upande 1.0 Bajeti yako

JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI

TIST HABARI MOTO MOTO. Benefits of Loan Repayment. Faida za ulipaji wa mikopo U OTESHAJI W A M ITI Y A M ATUNDA

Njia za upimaji wa mpango wa kimataifa wa viwango vya chakula kwa wenye matatizo ya kumeza (IDDSI) VYAKULA VINYWAJI VYA KAWAIDA

Elimu Bora, lakini... C HakiElimu Elimu bora, lakini...

Usindikaji bora wa maziwa

Uhakika wa Mbegu kwa Uhakika wa Chakula MWONGOZO WA UZALISHAJI WA MBEGU ZA ASILI ZA MAHINDI

Vijana wanazungumza kuhusu ujinsia, maisha na uhusiano VIJANA WANAZUNGUMZA KUHUSU NGONO, MAISHA NA UHUSIANO. Training and Research Support Centre

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu WEMA

Usimulizi wa Riwaya ya Nyongo Mkalia Ini E. S. MOHOCHI University of Egerton, Kenya

USIMAMIZI MKUU WA UBORA WA MAHURUJI

International Labour Office. Kazi za Ndani Zenye Madhara kwa Watoto: Kijitabu cha Maelezo Mafupi

Ufunguo wa Kutaalamika Haraka

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

Muhtasari wa taarifa ya warsha ya wataalamu juu ya mfumo wa habari kwa njia ya ramani (PGIS), Morogoro, Juni 30 - Julai 1, 2014

Mwongozo wa Mwezeshaji

ONDOA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA AFYA YA WATOTO

Uzazi wa Mpango. Uzazi wa Mpango. Kulinganisha Ufanisi wa Njia za Uzazi wa Mpango. iwe na ufanisi zaidi. Zenye ufanisi.

Programu ya Uendelezaji Mifumo ya Maji Vijijini (PUMMV) katika Tanzania. Modeli wa Ukodishaji Mradi

ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA UCHUMI WA ZANZIBAR

MBINU ZA IPM KWENYE KILIMO CHA KAHAWA

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

Hatari, Haki za Usalama katika Bahari 03

Mwongozo wa Jamii juu ya Afya ya Mazingira

Ufundishaji wa lugha nyingine

MACHAGUO YA UZAZI KUFIKIRIA KUWA MZAZI

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO

Maoni ya Wananchi juu ya Huduma za VVU na UKIMWI Nchini Tanzania

Taarifa Kuhusu Hali ya Uchumi wa Tanzania

Miradi na jamii. 3.1 Utangulizi

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

Vyote Unavyopaswa Kujua Kuhusu Viazi Vitamu

KENYA NATIONAL EXAMINATION COUNCIL REVISION MOCK EXAMS 2016 TOP NATIONAL SCHOOLS

KUWEZESHA MBINU ZA UZUIAJI MIMBA KATIKA SUHULA ZA AFYA: MASWALI 10 KWA VIKUNDI VYA JAMII KUZINGATIA

HAKI NA TARATIBU ZA AJIRA, KAZI NA HIFADHI YA JAMII

Kiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

Early Grade Reading Assessment for Kenya

HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA. Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo. TOLEO Na.

TANZANIA MARKETS PAN Sera zinazoboresha masoko

TASFIDA KAMA MKAKATI WA UPOLE: UWIANO WA TASFIDA ZA KISWAHILI NA EKEGUSII

Pronunciation: Mä-hret Zäläke Ndal-ka-tscho Molla Mare Gebre-gzabiär 1/12

N09/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q

Kilimo cha kiekolojia cha Wakulima Wadogo Hufanikisha Haki za Mazingira

KUSHUKA KWA HADHI YA LUGHA ZA JAMII NCHINI TANZANIA YOHANA P. MSANJILA University of Dar es Salaam, Tanzania

Sera ya Faragha. Upeo. Aina za Data na Mbinu za Ukusanyaji

Haja Ya Dini. Author(s): Publisher(s): Translator(s): Category: Topic Tags: Featured Category: Published on Al-Islam.org (

SautiElimu. Sauti Yako Isikike

Transcription:

Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI C O U N S E N U T H I n f o rmation series No. 6 Toleo la Kwanza, March, 2004

Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI MATUMIZI YA VIUNGO VYA VYAKULA KATIKA KUBORESHA LISHE NA AFYA ISBN 9987-8936-7-8 C O U N S E N U T H, 2004 K i m e t aya ri s h wa na: Center for Councelling, N u t rition and Health Care (COUNSENUTH) n a Ku fa d h i l i wa na: M p a n go wa Ta i fa wa kudhibiti UKIMWI ( NACP) - Wi z a ra ya A f ya 1

Shukrani Kituo cha Ushauri Nasaha, Lishe na Afya (COUNSENUTH) kinatoa shukrani za pekee kwa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI (NACP) kwa kufadhili utayarishaji na uchapishaji wa kijitabu hiki. Shukrani za dhati kwa WAMATA, TAHEA, SHDEPHA+, NACP na watu binafsi walioshiriki katika kutayarisha na kuboresha kijitabu hiki. Asanteni sana. 2

UTANGULIZI Hali bora ya lishe huchangia katika kuongeza ubora wa afya na maisha ya mtu anayeishi na virusi vya UKIMWI. Pamoja na ulaji wa chakula mchanganyiko na cha kutosha, viungo mbalimbali vimeonekana pia kusaidia kuboresha lishe na afya. Hata kabla ya ugonjwa wa UKIMWI, viungo vimekuwa vikitumika katika mapishi mbalimbali ili kuongeza ubora wa chakula na hivyo kuchangia katika kuboresha lishe na afya ya mtu yeyote. Viungo hutokana na sehemu fulani ya mmea kama majani, mizizi, maua, mbegu au magome. Viungo huweza kuongezwa katika chakula ili kukipa ladha nzuri hivyo kuongeza hamu ya kula. Viungo huweza pia kusaidia uyeyushwaji wa chakula na usharabu (ufyonzwaji) wa virutubishi mbalimbali. Baadhi ya viungo huweza kutumika kuhifadhi baadhi ya vyakula ili visiharibike mapema. Wakati mwingine viungo huweza kutumika katika kutuliza au kutibu baadhi ya matatizo madogo madogo ya afya kama kichefuchefu, fangasi, kutapika, kuharisha, mafua au flu. Mtu anayeishi na virusi vya UKIMWI hukabiliwa na matatizo mbalimbali yakiwemo kukosa hamu ya kula, uyeyushwaji duni wa chakula na usharabu (ufyonzwaji) duni wa virutubishi. Matumizi ya viungo mbalimbali kwa kiasi yameonekana kupunguza baadhi ya matatizo hayo. Kijarida hiki kimeweka pamoja taarifa zilizopo hivyo kumpa mtu chaguo kubwa ili aweze kutumia vile viungo anavyovipata kwa urahisi. Kijarida hiki kinazungumzia matumizi ya kawaida ya viungo kama sehemu ya mlo na katika kupunguza makali ya baadhi ya matatizo. Baadhi ya watu baada ya kusikia kwamba viungo vinasaidia, wamekuwa wakivitumia kwa kiasi kikubwa mno na wakati mwingine kuwaletea matatizo. Ni muhimu kutumia viungo kwa kiasi, katika mapishi ya kawaida au katika vinywaji kama inavyoshauriwa. 3

Kinywaji cha viungo: MSAMIATI Hiki ni kinywaji chochote ambacho kimetengenezwa kwa kuwekwa viungo. Kinywaji hiki kinaweza kuwa cha moto au cha baridi. Kinywaji cha baridi kinapotengenezwa, yatumike maji yaliyochemshwa. Chai: Hiki ni kinywaji ambacho hutengenezwa kwa kutumia maji ya moto na majani ya chai. Wakati mwingine sukari na maziwa huongezwa. Mara nyingine watu wanapotengeneza vinywaji vya viungo huviita chai hata kama havina majani ya chai. Ukweli ni kwamba chai ni yale majani ya chai. Katika kijitabu hiki vinywaji vya viungo havikuitwa chai. BAADHI YA VIUNGO, MATUMIZI NA FAIDA ZAKE Kitunguu saumu (Garlic) Kitunguu saumu ni kiungo ambacho kimekuwa maarufu kwa matumizi mbalimbali. Vipo vitunguu saumu vya rangi nyeupe ambavyo mara nyingi huwa na tumba kubwa ambazo ni chache. Vingine ni vile vyenye rangi ya zambarau au pinki ambavyo huwa na tumba ndogo na nyingi. Vitunguu hivi vina ubora sawa. Kitunguu saumu hufaa katika matatizo mengi kama kusaidia kuzuia maambukizi yatokanayo na bakteria, baadhi ya virusi na fangasi hasa katika utumbo, mapafu na sehemu za ukeni. Vilevile husaidia katika uyeyushwaji wa chakula, kuzuia kuharisha na pia hupunguza fangasi za kinywani, maambukizi katika koo na hata mkanda wa jeshi. 4

Kitunguu saumu kinaweza kutumika katika mapishi ya chakula, chai au kinywaji chochote cha baridi au cha moto. Mtu anapotumia vitunguu saumu atumie kwa kiasi. Inashauriwa kutumia vitumba visivyozidi sita kwa siku hasa kama vitatumika vibichi. Tangawizi (Ginger) Tangawizi ni kiungo ambacho kinatokana na mizizi ya mmea wa tangawizi. Kiungo hiki huweza kutumika kikiwa kibichi au kikiwa kimekaushwa na kutengenezwa unga. Ta n g a w i z i inaweza kutumika katika vinywaji vilivyochemshwa. Pia huweza kuongezwa kwenye vinywaji vingine au kwenye chakula. Tangawizi husaidia kuongeza hamu ya kula, kupunguza kichefuchefu, kutapika, kuharisha, maumivu ya tumbo na gesi tumboni. Pia husaidia uyeyushwaji wa chakula tumboni. Vilevile husaidia wakati wa matatizo ya mafua au flu. Iliki (Cardamom) Iliki ni mbegu zinazotokana na mmea wa iliki ambazo hutumika kama kiungo. Mbegu hizi huweza kusagwa au kutwangwa na kuongezwa kwenye chakula au katika vinywaji. Iliki ni nzuri katika kusaidia kupunguza maumivu, kichefuchefu au kutapika. Pia husaidia uyeyushwaji wa chakula na huongeza hamu ya kula. Mdalasini (Cinnamon) Mdalasini ni kiungo kinachotokana na magome ya mmea wa mdalasini. Kiungo hiki huweza kusagwa au kutumika bila kusagwa. Vilevile mdalasini h u weza kuongezwa kwe n ye chakula au katika vinywaji vilivyochemshwa au baridi. 5

Mdalasini huweza kusaidia kupunguza matatizo kama mafua au flu, vidonda vya kinywani na hata fangasi za ngozi. Vilevile kiungo hiki huongeza hamu ya kula, pia husaidia kupunguza baadhi ya matatizo katika mfumo wa chakula kama kichefuchefu, kutapika au kuharisha. Kinywaji kilichochemshwa chenye mchanganyiko wa mdalasini na tangawizi kinaweza kutuliza kikohozi. Giligilani (Coriander) Giligilani ni aina ya kiungo ambacho majani na mbegu zake huwez a kutumika kama kiungo katika mapishi ya vyakula mbalimbali kama nyama, supu au mchuzi. Kiungo hiki husaidia kuongeza hamu ya kula na kupunguza gesi tumboni. Pia husaidia kuzuia maambukizi ya bakteria na fangasi. Kotimiri (Parsley) Kotimiri ni aina ya mmea ambao majani yake na mbegu zake huweza kutumika kama kiungo katika vyakula. Majani ya kotimiri husaidia kupunguza msokoto wa tumbo ambao mara nyingi hausababishi kuharisha. Vilevile kiungo hiki huchochea vimeng e n yo tumboni na hivyo kuongeza hali ya kuhisi njaa. Mbegu za kotimiri huweza kusaidia kuondoa maji ya ziada katika mwili. Kiungo hiki huweza kuongezwa katika chakula wakati wa kupika au wakati wa kula. Karafuu (Cloves) Karafuu hutokana na mmea wa mkarafuu. Kiungo hiki huweza kutumika peke yake au kwa kuchanganya na viungo vingine. Kiungo hiki husaidia kuleta hamu ya kula na kubore s h a 6

uyeyushwaji wa chakula tumboni. Vilevile karafuu husaidia kupunguza kichefuchefu, kutapika na kuharisha. Ni nzuri ikitumiwa katika supu, mchuzi, juisi ya matunda yenye uvuguvugu au vinywaji vingine vilivyochemshwa. Binzari (Turmeric/Yellow Root) Binzari halisi hutokana na mizizi ya mmea wa binzari manjano ambao hufanana na ule wa tangawizi. Mizizi ya binzari huweza kukaushwa, kusagwa na kutengeneza unga wa binzari ya manjano ambao hutumika kama kiungo cha chakula. Vilevile binzari mbichi inaweza kutwangwa na kutumika kwenye mapishi mbalimbali. Binzari ikitumiwa katika chakula, hukifanya kuwa na rangi ya njano. Binzari inaweza kutumika kwenye mapishi ya wali au vyakula vingine vya nafaka, pia kwe n ye mchuzi au maharagwe. Binzari husaidia katika uyeyushwaji wa chakula na pia husaidia mwili usiharibiwe na kemikali mbaya. Ni vizuri kuwa waangalifu tunaponunua binzari ile ya unga kwani wakati mwingine wauzaji huuza binzari ambayo si binzari halisi. Binzari hii ambayo si halisi hutengenezwa kwa kutumia aina za unga wa nafaka ambao huchanganywa na rangi ya manjano na binzari kidogo. Limau (Lemon) Limau linaweza kutumika kama kiungo katika chakula na vinywaji kama chai au vinywaji vingine. Limau husaidia kuboresha uyeyushwaji hasa wa protini na mafuta. Limau pia huweza kutuliza vidonda vya kooni, kikohozi, homa na kuondoa msongo. 7

Binzari nyembamba (Cumin seeds) Hizi ni mbegu nyembamba ambazo hufanana na mbegu za giligilani. Mbegu hizi huweza kusagwa na kutengeneza unga ambao hutumika kama kiungo katika mapishi mbalimbali mfano; supu, mchuzi, wali, n.k. Mrehani (Basil) Kiungo hiki husaidia kuongeza hamu ya kula, kupunguza maumivu ya tumbo na hata kuharisha. Mrehani ni aina ya kiungo ambacho huweza kutumika kwa kuongezwa katika chakula. Kiungo hiki husaidia kupunguza kichefuchefu na kusaidia uyeyushwaji wa chakula na kutuliza maumivu ya kichwa. Kwa vidonda vya kinywani mrehani unaweza kutumika kwa kusukutua. Calendula Vikonyo vya maua ya calendula vina kemikali inayozuia kukua kwa vijidudu kama bakteria katika jeraha, ngozi na pia kupunguza hali ya mwako wa moto (anti-inflammatory function). Vilevile c a l e n d u l a hupunguza maambukizi mbalimbali katika mfumo wa chakula. C a l e n d u l a inaweza kutumika kutibu vidonda. Vilevile inawez a kutumiwa kama kinywaji kilichochemshwa ili kuboresha uyeyushwaji wa chakula tumboni. Pilipili (Cayenne) Cayenne ni mchanganyiko wa aina za pilipili za jamii ijulikanayo kama capsicum. Pilipili hizi huwa ndefu na nyembamba, mara nyingi huwa ni kali na zina rangi nyekundu. Jamii hii ya pilipili huweza kukaushwa na kusagwa na hivyo kutengeneza unga laini ambao huwa na rangi nyekundu. 8

Cayenne huweza kuongeza hamu ya kula. Pilipili hii inaweza ikatumika kwa kuongezwa kwenye chakula wakati wa kupika au wakati wa kula. Pia huweza kuongezwa katika juisi au maji ya kunywa. Hata hivyo ni vyema pilipili itumiwe kwa kiasi. Shamari (Fennel) Shamari ni kiungo ambacho mbegu zake hufanana na zile za binzari nyembamba. Kiungo hiki husaidia kuongeza hamu ya kula na kupunguza gesi tumboni. Shamari inaweza kutumika kama kiungo kwenye chakula. Mbegu za shamari zinawez a kutumika kuandaa chai au kinywaji chochote cha moto. Ni vizuri ikitumiwa kwa kiasi. Nanaa (Mint) Nanaa ni majani ya mnanaa ambayo hutumiwa kama kiungo. Nanaa husaidia katika kuzuia hali ya mwako wa moto tumboni, kupunguza kichefuchefu, kuzuia kutapika na kuharisha. Pia huweza kupunguza maumivu ya tumbo na mkakamao wa misuli. Vilevile nanaa husaidia katika uyeyushwaji wa chakula tumboni. Nanaa iliyooshwa vizuri kwa maji safi na salama inawez a kutafunwa. Vilevile inaweza kutumika kutengeneza kinywaji cha moto au kusukutua wakati mtu anapokuwa na vidonda kinywani. Meti (Methi) Meti ni majani ya mmea uitwao kwa Kiingereza Fenugreek. Hii ni aina ya kiungo ambacho huchochea uvunjaji wa kemikali mwilini yaani umetaboli. Majani ya meti yanaweza kukaushwa na kutumika kama kiungo au kutumika yakiwa mabichi. Vilevile mbegu za Fenugreek huweza 9

kukaushwa, kusagwa na kutumika katika kutengeneza unga wa viungo yaani curry powders. Meti inaweza kutumika kama kiungo katika vyakula mbalimbali ikiwa ni pamoja na mboga za majani na vilevile katika mapishi mbalimbali ya samaki. Thyme T h y m e inaweza kuzuia maambukizi yanayosababishwa na bakteria au fangasi. Vilevile kiungo hiki husaidia kupunguza kikohozi na kulainisha koo. Zaidi ya hayo thyme husaidia ukuaji wa bakteria wazuri wanaosaidia katika uyeyushwaji wa chakula tumboni. Inaweza kutumika kama kinywaji cha moto au kusukutua. JINSI YA KUTAYARISHA BAADHI YA VINYWAJI VYA VIUNGO Kinywaji cha mdalasini Mahitaji: Robo ( ) kijiko cha chai cha unga wa mdalasini; Kikombe kimoja cha maji safi. Matayarisho: Chemsha maji vizuri, na kisha ongeza unga wa mdalasini; Baada ya hapo unaweza kuongeza asali au sukari kidogo ili kuongeza ladha; Na hapo kinywaji ni tayari; kinaweza kunywewa muda wowote. Kinywaji cha tangawizi Mahitaji: Kikombe kimoja cha maji; Kijiko kimoja cha tangawizi mbichi iliyopondwa; Sukari kidogo. 10

Matayarisho: Osha tangawizi na ponda ponda; Changanya tangawizi na kikombe kimoja cha maji safi; Chemsha mchanganyiko huo ukiwa umefunikwa; Acha kwenye moto mdogo kwa dakika 5 hadi 10; Ongeza sukari kidogo (kama unapenda); Kinywaji ni tayari. Kinywaji cha kitunguu saumu Mahitaji: Tumba 3 hadi 4 za kitunguu saumu kilichopondwa au kukatwa vipande vidogo vidogo; Kikombe kimoja cha maji safi; Asali au sukari kidogo. Matayarisho: Chemsha maji vizuri; Ongeza kitunguu saumu kilichopondwa au kukatwa vipande vidogo vidogo, kwe n ye maji yanayochemka, funika na kisha acha mchanganyiko huo uchemke kwa muda wa dakika 10; Ipua na acha mchanganyiko huo upoe; Unaweza kuongeza asali au sukari ili kuongeza ladha; Kinywaji ni tayari. Kinywaji cha tangawizi na mdalasini Mahitaji: Nusu ( ) kijiko cha chai cha tangawizi mbichi iliyopondwa au kukatwa vipande vidogo vidogo; Robo ( ) kijiko cha chai cha unga wa mdalasini; Kikombe kimoja cha maji safi. Matayarisho: Chemsha maji kisha ongeza tangawizi, funika na acha vichemke kwa dakika 10; 11

Baada ya hapo ongeza unga wa mdalasini na acha mchanganyiko huo uchemke kwa muda wa dakika 5 zaidi; Ipua na kisha chuja kinywaji hicho. Sasa kinywaji ni tayari kwa kutumia; Unaweza kuongeza sukari kidogo ili kuongeza ladha. Kinywaji cha Limau Mahitaji: Limau moja; Nusu ( ) kikombe cha maji safi; Sukari kidogo. Matayarisho: Osha limau kwa maji safi kisha kamua ili kupata maji ya limau; Chemsha maji vizuri; Ongeza maji ya limau kwenye maji hayo; Ongeza sukari kidogo (kama unapenda); Ni vizuri kunywa kinywaji hiki kingali cha moto. 12 Kinywaji cha Nanaa (Mint) Mahitaji: Majani ya nanaa; Kikombe kimoja cha maji safi; Sukari kidogo (kama unapenda). Matayarisho: Osha nanaa vizuri na kisha katakata vipande vidogo vidogo; Weka vipande hivyo kwenye kikombe; Chemsha maji vizuri na ongeza maji hayo kwenye kikombe chenye nanaa; Funika vizuri na acha kwa dakika 5. Ongeza sukari kidogo (kama unapenda) na sasa kinywaji ni tayari. Kumbuka kutumia vyombo safi na maji safi na salama wakati wote.

HITIMISHO Inashauriwa kutumia viungo mbalimbali kwa kiasi ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na matumizi yaliyozidi kiasi. Hata hivyo bado hakuna ushahidi wa kitaalamu wa kutosha kuonyesha ni jinsi gani viungo vinaweza kutibu baadhi ya matatizo yanayoambatana na kuishi na virusi vya UKIMWI. Taarifa nyingi kuhusu namna viungo vinavyoweza kupunguza matatizo mbalimbali zimetokana na ripoti z i l i zo t o l ewa na watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI ambao wamejaribu kutumia viungo hivyo na kuona vinasaidia. Mtu anayeishi na virusi vya UKIMWI anapoamua kutumia viungo kama tiba anashauriwa kujaribu na kuona kama vinamsaidia. Baadhi ya viungo kama vile nanaa, kitunguu saumu, tangawizi, binzari manjano na vinginevyo vinaweza kuoteshwa nyumbani katika bustani ndogondogo au vyombo kama makopo, madebe au vyungu na hivyo kurahisisha upatikanaji wake. Ikumbukwe kuwa viungo vitachangia kuboresha afya na lishe ya mtu yeyote kwa kuboresha uyeyushwaji wa chakula na usharabu (ufyonzwaji) wa virutubishi mbalimbali vilivyomo kwenye chakula. Zaidi ya hayo viungo huongeza ladha nzuri kwenye chakula na hivyo kumwezesha mtu ale chakula cha kutosha ili kukidhi mahitaji ya mwili. Viungo vingi vinaweza kuoteshwa katika bustani za nyumbani. Baadhi ya vungo ambavyo mimea yake ni midogo huweza kuoteshwa katika vyombo kama makopo, madebe au vyungu. 13

VYANZO 1. Bijlsma, M., Living Positively: Nutrition guide for People with HIV/AIDS, Muntare City Health Department, Zimbabwe, Second Edition, 1997. 2. COUNSENUTH, Nutritional Care for PLHA: Training and Reference Manual (DRAFT), September, 2003. 3. Davidson S., Passmore R., Brock J.F., Truswell A. S,. Human Nutrition and Dietetics; Seventh Edition. Wilture Enterprises, (International) Ltd. 1979. 4. FAO, Living Well With HIV/AIDS, A manual on nutritional care and support for people living with HIV, 2002. 5. Food and Nutrition Technical Assistance (FANTA), HIV/AIDS: A Guide for Nutrition, Care and Support. Academy for Educational Development, Washington DC, 2001. 6. http://webhost.sun.ac.za/nicus/factsheets/hiv_alternative_diet_ therapy.htm 7. Ministry of Health, The United Republic of Tanzania. A National Guide on Nutrition Care and Support for People Living with HIV/AIDS, TFNC (DRAFT), May, 2003. 8. Morris, S. and Macklley, L. The Spice Ingredients cookbook. Lorenz Books. 1997. 9. The Netwok of African people living with HIV/AIDS (NAP+). Food for people living with HIV/AIDS, July, 1996. 14

VIJITABU VINGINE KUHUSU LISHE NA ULAJI BORA KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI VILIVYOTOLEWA NA COUNSENUTH 1. Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI: Vidokezo muhimu, COUNSENUTH Information series No. 2, Toleo la Pili, January, 2004. 2. Lishe na Ulaji bora kwa Watu Wanaoishi na Vi rusi vya UKIMWI: Maswali yanayoulizwa mara kwa mara, COUNSENUTH Information series No. 3, Toleo la Pi l i, January, 2004. 3. Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Vi rusi vya UKIMWI: Vyakula vinavyoboresha uyeyushwaji wa chakula na u f yonzwaji wa virutubishi mwilini, COUNSENUTH Information series No. 4, March, 2003. 4. Ulishaji wa Mtoto Mchanga kwa Mama mwenye Virusi vya UKIMWI: Vi d o k ezo Muhimu kwa Washauri Na s a h a, COUNSENUTH Information series No. 1, Toleo la Pi l i, January, 2004. 15

16

Kwa maelezo zaidi wasiliana na: M k u r u g e n z i Kituo cha Ushauri Nasaha,Lishe na A f ya ( C O U N S E N U T H ) S. L. P. 8218, Dar es Salaam, Ta n z a n i a Simu: (22) 2152705 au 0744 279145 Fax: (22) 2152705 Kijarida hiki kimetayarishwa na kutolewa na: The Centre for Counselling, N u t rition and Health Care ( C O U N S E N U T H ) United Nations Rd./ Kilombero Str. Plot No. 432, Flat No.3 P.O. Box 8218, Dar es Salaam Ta n z a n i a. ISBN 9987-8936-7-8 Kimefadhiliwa na: Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI S. L. P 11857 Dar es Salaam, Ta n z a n i a. Designed & printed by: Desktop Productions Limited P.O. Box 20936, Dar es Salaam, Tanzania 17