NAFASI ZA MASOMO MASOMO YA ASUBUHI

Similar documents
Information for assessors (do not distribute this page to participants):

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI-TAMISEMI HALMASHAURI YA WILAYA BUMBULI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA

HALMASHAURI YA WILAYA YA SUMBAWANGA

FOMU YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO

Kumb.Na.BSS/A.6/33 Tarehe: 18 Juni 2018 YAH: MAAGIZO YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2018/2019

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA IRINGA SHULE YA SEKONDARI TOSAMAGANGA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MANISPAA YA BUKOBA.

SHULE YA SEKONDARI KIBAHA S.L.P 30053, KIBAHA SIMU NA Kibaha

JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAGU

ARCHDIOCESE OF MWANZA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS - TAMISEMI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. OFISI YA RAIS- TAMISEMI.

YAH: MAAGIZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI KAREMA KIDATO CHA TANO MWAKA 2018

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA

JAMHURI YA MUUNGANO IVA TANZANIA

JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI-TAMISEMI

Kumb.Na.HVEMS/JI/BT/018 Novemba 17, YAH: MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE CHINI YA TAASISI YA ROCK MEMORIAL EDUCATION TRUST 2018

YAH: MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI WERUWERU HALMASHAURI YA MOSHI MKOA WA KILIMANJARO MWAKA 2018

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

KAWAWA JKT HIGH SCHOOL PO.BOX 213 MAFINGA IRINGA PHONE MOBILE, , , ,

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig

JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAMISEMI HALMASHAURI YA MANISPAA YA MPANDA SHULE YA SEKONDARI RUNGWA

2018/2019 OFISI YA RAIS-TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti

Ufanisi katika Ufundishaji kwenye Shule za Msingi na Sekondari nchini Tanzania

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Human Rights Are Universal And Yet...

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Hatari, Haki za Usalama katika Bahari 03

Mwongozo wa Familia wa Kujifunza

Tufundishane! Mwalimu Bora In this issue: Issue 6, December Do you want to be in our next issue?

Kifaa Maalum cha Kutazamia Jua: Maelekezo ya kutumia

TIST HABARI MOTO MOTO. Benefits of Loan Repayment. Faida za ulipaji wa mikopo U OTESHAJI W A M ITI Y A M ATUNDA

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

Early Grade Reading Assessment for Kenya

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees

JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1

Ellen White, waasisi wa Kiadventista,na Sabato Lunar

KANUNI ZA MAADILI MWONGOZO WA WANAFUNZI

SautiElimu. Sauti Yako Isikike

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO

Nilikua na Ndoto ya Kumaliza Shule Changamoto za Elimu ya Sekondari Tanzania

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

Adhabu ya jino kwa jino na Musitakabali wa imani zetu

Sera ya Faragha. Upeo. Aina za Data na Mbinu za Ukusanyaji

usudi la Maisha Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na kupishana usiku na mchana, kuna kweli ishara kwa wenye akili, ambaye mkumbuke-

Mhashamu Askofu Jude Thaddaeus Ruwa ichi, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania; Mwadhama Policarp Kardinali Pengo,

TIST HABARI MOTO MOTO

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

Ufunguo wa Kutaalamika Haraka

Upande 1.0 Bajeti yako

MACHAGUO YA UZAZI KUFIKIRIA KUWA MZAZI

MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA. Kwa Wanaoanza

TIST HABARI MOTO MOTO MAANDALIZI YA MWAKA 2000 Y2K PREPARATIONS SASA NI WAKATI WA KUANZA KUPANDA MBEGU ZAKO

Kijitabu cha Maelezo cha Programu ya Famasia

MTIHANI WA MWIGO WILAYA YA BUTERE MUMIAS-2007 Hati ya kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya

CGAP Smallholder Household Survey in Tanzania / Utafiti wa kaya ndogondogo Tanzania

4. Kanuni za Petroli (Ushiriki wa Watanzania) za mwaka 2017 zilianza kutumika rasmi tarehe 5 Novermba Shughuli za Petroli za kwanza ni

Utangulizi wa ugonjwa wa shinikizo la damu

5. Mheshimiwa Spika, Bunge lako Tukufu lilijadili kwa kina Miswada ifuatayo:

KIJARIDA JUU YA HAKI ZA RAIA KATIKA MFUMO JINAI

Roho Mtakatifu Ni Nini?

Kocha Mkuu. mabingwa. itakuwa INASTAHILI. Ili Kutoa mafunzo kwa wanafunzi wako kuwa. itakuwa ya kuumiza. Itachukua muda. Itahitaji moyo wa kujitoa.

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

ORDER NO BACKGROUND

In the matter of an Application by the KIGOMA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (KUWASA) For a Tariff and Charges Adjustment

KITEGO CHA MAREKEBISHO NA HAKI ZA MTOTO

Kufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007

Yaliyomo. Kuhusu kitabu hiki. Hautakuwa peke yako. Mfumo wa msaada ni wa manufaa sana wazazi wote wanahitaji!

Elimu Bora, lakini... C HakiElimu Elimu bora, lakini...

Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA

PDF created with pdffactory trial version

Kuwawezesha wasichana kwa kuboresha kujikubali na kujithamini Hivi Ndivyo Nilivyo

MUONGOZO WA UTUNZAJI WA URITHI WA UTAMADUNI 1 SECURITY AT MUSEUMS

LUGHA YA KISWAHILI KATIKA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA ELIMU SHULE ZA SEKONDARI

In the matter of Application by the TANGA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (TANGA UWASA) For a Multi-Year Tariff Adjustment

Ufundishaji wa lugha nyingine

Vijana wanazungumza kuhusu ujinsia, maisha na uhusiano VIJANA WANAZUNGUMZA KUHUSU NGONO, MAISHA NA UHUSIANO. Training and Research Support Centre

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

Elimu Ina Umuhimu gani katika Jamii? Kuelekea Elimu Sahihi

MWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI

Siku ya kwanza. Mguso wa ngozi-kwa-ngozi (Ulezi wa kangaruu) Mtoto wako anaweza kuhisi mdundo wa moyo wako

UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU VIKWAZO VYA KULINDA MAISHA KATIKA USAIDIZI WA KIMATAIFA WA AFYA KWA MSAADA WA KIMATAIFA UNAOFADHILIWA NA MAREKANI

Uzio wa pilipili unazuia tembo kuvamia mazao shambani! Jinsi ya kujenga na kudumisha uzio wa pilipili Tanzania

Namba ya moduli 3 Kuangalia sanaa

Mazoezi yaliyofanyika wakati wa warsha kuhusu Elimu-Jumuishi kwa Vitendo. Zanzibar, 7-10 Februari 2006

Na Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake Toleola4

United Pentecostal Church June 2017

Mipango ya miradi katika udugu

Theolojia Ujumla. Mike Taylor Semester Munguishi Bible College

Banana Investments Ltd

KUWEZESHA MBINU ZA UZUIAJI MIMBA KATIKA SUHULA ZA AFYA: MASWALI 10 KWA VIKUNDI VYA JAMII KUZINGATIA

Transcription:

NAFASI ZA MASOMO Shule yetu, iliyoanza mwaka 1974, inazingatia taaluma na maadili kwa kufuata sera ya elimu ya Kanisa Katoliki. Ni ya mchepuo wa biashara. Inapokea wanafunzi wa kike na wa kiume, wa kutwa na wa bweni, bila kubagua yeyote. Iko katikati ya Manispaa ya Morogoro, kando ya barabara kuu ya zamani ya kwenda Dar es Salaam. Iko jirani kabisa na taasisi zote zinazotoa huduma muhimu (nyumba za ibada, hospitali ya rufaa, posta kuu, benki, shesheni ya reli ya kati, kituo cha mabasi ya mjini n.k.) Pamoja na kuwaahidia juhudi endelevu za kuboresha huduma, tunawatangazia nafasi zifuatazo za masomo ya sekondari. MASOMO YA ASUBUHI PRE-FORM I: Wanaohitaji kujiandaa miezi mitatu ili kujiunga na kidato cha kwanza mwakani katika shule yoyote, masomo yatatolewa kuanzia tarehe 13-9-2016 saa 2:00 asubuhi (darasa likijaa, wengine watasoma mchana). Ada ni Tsh. 90,000. Wanaohitaji kukaa bweni watapata nafasi katika vituo vifuatavyo: wavulana Malati Secondary School (mtaa wa Bigwa) tu - wasichana Savannah Girls Centre (Mzumbe) tu. Hao waongeze Tsh. 160,000. Jumla ni Tsh. 250,000. Inatakiwa kulipwa kwa mkupuo mmoja. FORM I: KUINGIA KIDATO CHA KWANZA (Civics, History, Geography, English, Kiswahili, Biology, Chemistry, Physics na Mathematics). Kutakuwa na masomo ya Book Keeping na Commerce pia. Wanaotaka kujiunga wawe wamezaliwa si kabla ya mwaka 2000 na kufaulu mtihani wa darasa la saba mwaka 2015 au 2016. Usaili utafanyika tarehe 3-12-2016 saa 2:00 asubuhi. Washindi watatangazwa baada ya siku tatu na kuanza masomo tarehe 3-1-2017. Ada yao ni Tsh. 600,000 kwa mwaka. Kwa kukaa bweni wataongeza Tsh. 600,000. Jumla ni Tsh. 1,200,000. Inaweza kulipwa kwa mikupuo minne. FORM V: KUINGIA KIDATO CHA TANO (History, Kiswahili na Language; au History, Geography na Kiswahili; au History, Geography na Language; au History, Geography na Economics; au Economics, Geography na Mathematics; au Chemistry, Biology na Geography). Wanaotaka kujiunga wawe: wamezaliwa si kabla ya mwaka 1995; wamefaulu (A, B+, B, C au D) English; wamepata credits (A, B+, B au C) katika masomo waliyoyachagua walipofanya au waliporisiti mtihani wa kidato cha nne; wamepata credit ya tatu mwaka 2015 au 2016. Usaili utategemea vyeti tu (cha kuzaliwa au cha kumaliza shule na hati za matokeo ya kidato cha nne). Washindi watatangazwa tarehe 12-6-2017 na wataanza masomo tarehe 4-7-2017. Ada ni Tsh. 700,000 kwa mwaka. Kwa kukaa bweni wataongeza Tsh. 600,000 (nafasi ni chache: watapewa watakaowahi kulipa). Jumla ni Tsh. 1,300,000. Inaweza kulipwa kwa mikupuo minne.

MASOMO YA MCHANA A. KWA WASIOWAHI KUFANYA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE Ni kwa wale watakaofanya mtihani wa maarifa (maarufu kama Q.T.) na mitihani mingine ya taifa kama watahiniwa wa kujitegemea. Masomo yao yataanza tarehe 10-1-2017. Ni kuanzia alasiri (Jumamosi kuanzia asubuhi). Ada ni Tsh. 400,000 kwa mwaka. Inatakiwa kulipwa kwa mkupuo mmoja. Bweni halina nafasi kwa ajili yao. P I: KUJIANDAA MIAKA MIWILI KWA MTIHANI WA MAARIFA (Civics, History, Geography, English, Kiswahili, Biology na Mathematics; au Civics, History, Geography, English, Kiswahili, Commerce na Book Keeping). I-II: KUJIANDAA MWAKA MMOJA KWA MTIHANI WA MAARIFA (Civics, History, Geography, English na Kiswahili). P III: KUJIANDAA MIAKA MIWILI TENA KWA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (Civics, History, Geography, English, Literature, Kiswahili, Biology na Mathematics; au Civics, History, Geography, English, Literature na Kiswahili). Wanaotaka kujiunga wawe na elimu inayolingana na ile ya kidato cha pili. III-IV: KUJIANDAA MWAKA MMOJA KWA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (Civics, History, Geography, English na Kiswahili). Wanaotaka kujiunga wawe wamefaulu mtihani wa maarifa. B. KWA WALIOKWISHAFANYA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (HATA KAMA WAMEFELI) Ni kwa wale wanaotaka kurudia mtihani wa taifa wa kidato cha nne. Masomo yao yataanza tarehe 10-1-2017. Ni kuanzia alasiri (Jumamosi kuanzia asubuhi). Ada ni Tsh. 400,000 kwa mwaka. Inatakiwa kulipwa kwa mkupuo mmoja. Bweni halina nafasi kwa ajili yao. T (= TARATIBU): KUJIANDAA MIAKA MIWILI KURISITI MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (Civics, History, Geography, English, Kiswahili, Biology na Mathematics; au Civics, History, Geography, English, Kiswahili, Commerce na Book Keeping; au Civics, History, Geography, English na Kiswahili). H (= HARAKA): KUJIANDAA MWAKA MMOJA KURISITI MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (Civics, History, Geography, English na Kiswahili). C. KUJIANDAA MWAKA MZIMA KWA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA V-VI (History, Kiswahili na Language; au History, Geography na Kiswahili; au History, Geography na Language). Wanaotaka kujiunga wawe wamepata credits (A, B+, B au C) walau tatu katika masomo yoyote walipofanya au waliporisiti mtihani wa kidato cha nne. Wawe pia wamepata walau D katika somo la English. Masomo yao yataanza tarehe 23-5-2017. Ni kuanzia alasiri (Jumamosi kuanzia asubuhi). Ada ni Tsh. 600,000 kwa mwaka. Inatakiwa kulipwa kwa mkupuo mmoja. Bweni halina nafasi kwa ajili yao. MAELEZO MUHIMU KWA WOTE Wakristo wa madhehebu yote wanatakiwa kusoma pia Bible Knowledge au Divinity; kwa wengine ni hiari. Mbali na fomu, malipo yoyote yanatolewa risiti katika ofisi ya mhasibu; nje ya hapo malipo si halali, na shule haihusiki nayo, hata kama aliyepewa pesa ni mwalimu. Jihadhari sana. Ada inatakiwa kulipiwa benki; akaunti zenye jina la shule ziko MKOMBOZI C.B., namba 00111507671101, pia K.C.B., namba 3300977908. Ukishindwa kulipia huko, unaweza kutumia pia akaunti ya N.B.C., namba 026201160913, jina T.E.C. Mchikichini. Zaidi ya ada hakuna mchango unaodaiwa na shule. Uijaze fomu vizuri na kuitunza hadi utakapoirudisha imeambatana na kivuli cha hati ya matokeo ya mtihani wa kidato cha nne (pamoja na ya kurisiti). Ulete pia vocha ya ada uliyolipia benki ili tuweke kumbukumbu na kukupa risiti yetu. Ukipenda, ujitengenezee kwanza kivuli cha vocha hiyo.

P. O. Box 677 MOROGORO www.kigur.com SHERIA ZA SHULE 1. Sheria za kiutu 1.1. Uwahi shuleni muda uliopangwa. 1.2. Uimbe kwa heshima, hali umesimama pamoja na kundi linalokuhusu, wimbo wa taifa unaotumiwa na shule kama sala ya pamoja kila siku kabla ya kuanza masomo. 1.3. Uwepo muda wote wa masomo na wa kazi ukifuata ratiba ya shule ndani na nje ya darasa ulilopangiwa. 1.4. Uheshimu picha takatifu, bendera na picha za viongozi wa nchi. 1.5. Uwe na tabia njema na utiifu kwa walimu, wafanyakazi na majirani wa shule, wanafunzi wenzako na binadamu yeyote. 1.6. Ukifikiwa au kukutana na mwalimu au mtu yeyote anayekuzidi umri usimame kumsalimia. 1.7. Ukiitwa na mwalimu yeyote umuitikie mara. 1.8. Uwe daima safi (mwili, nguo na vitu vyote unavyotumia). 1.9. Uwe na nywele fupi; usifuge ndevu. 1.10. Usijirembe kwa kutia nywele dawa, kujichora, kutia wanja n.k. 1.11. Usiache kucha ndefu wala kupaka rangi au hina. 1.12. Usivae kofia, jaketi, viatu vya ghorofa wala mapambo yoyote (herini, bangili, mikufu n.k.). 1.13. Uvae daima sare ukiwa shuleni (hata wakati wa likizo), ukitoka kwa shughuli za kishule, ukienda hospitalini, ukisafiri kufika shuleni au kurudi nyumbani, n.k. 1.14. Usionekane katika mazingira ya wasiwasi (klabu, kumbi za starehe, nyumba za wageni n.k.). 1.15. Usijihusishe na ulevi na uvutaji wa aina yoyote. 1.16. Usiwe na urafiki wa kimapenzi; hata hivyo ukipata mimba utakubaliwa likizo ya uzazi, usije ukaua mimba. 1.17. Ukae mahali pako katika darasa ulilopangiwa, pasipo kuhamahama wala kuchanganyikana na jinsia nyingine. 1.18. Ufanye kwa bidii kazi za aina zote, ukishirikiana na wenzako katika usafi na utunzaji wa mazingira. 1.19. Ulinde mali yako binafsi na ya shule (majengo, madawati, vitabu na vifaa vingine utakavyopewa). 1.20. Usitoe dawati nje ya jengo lake pasipo agizo au ruhusa. 1.21. Utambue ni marufuku kuiba, kugombana, kupigana, kutumia lugha chafu, kuchonganisha, kuchochea vurugu na kufanya mgomo. 1.22. Usitembelee nyumba za walimu na wafanyakazi wengine wala bweni la jinsia tofauti. 1.23. Usitoroke shule, bali utoe taarifa kama utashindwa kuhudhuria masomo. 1.24. Usilete shuleni simu, redio n.k. la sivyo utafukuzwa mara moja. 1.25. Uombe ruhusa ukitaka kuleta shuleni magazeti, majarida, vitini, vitabu n.k. 1.26. Ukubali mamlaka ya wanafunzi viongozi katika kushauri, kuonya na hata kuadhibu kabla tatizo lako halijaufikia utawala wa shule. 1.27. Usikatae adhabu. 2. Sheria za kitaaluma 2.1. Uwe msikivu na mtekelezaji wa maagizo na mashauri ya walimu. 2.2. Ukamilishe kazi zote zinazotolewa na walimu kwa wakati unaotakiwa. 2.3. Uwe mtulivu muda wote darasani, mwalimu awepo au asiwepo vilevile. 2.4. Ushirikiane vema na walimu pamoja na wanafunzi wenzako ili kupata msaada wa kitaaluma. 2.5. Ujitahidi kufanya vizuri mitihani ya mara kwa mara, usije ukaondolewa shuleni kwa kutoifanya mara tatu mfululizo (hata kama umeruhusiwa kwa shida maalumu) au kwa kutofikia mara mbili mfululizo wastani wa alama 45 kwa jumla ya masomo yote. 2.6. Utambue ni kosa kubwa kuibia, kusaidiwa au kusaidia katika mtihani wowote. 3. Sheria za nyongeza kwa wanaokaa bweni (hata la nje) 3.1. Uvae sare ya bweni muda wote, bila ya kuichanganya na vazi lingine wala urembo wowote. 3.2. Uombe ruhusa ukihitaji kurudi bwenini wakati wa vipindi darasani. 3.3. Uzingatie muda wa chakula kwa sababu huruhusiwi kukipeleka bwenini. 3.4. Usiwasiliane na mtu yeyote bila ya mkuu wa bweni kujua. 3.5. Usimpokee mgeni yeyote tofauti na walioandikwa na mzazi, wala nje ya siku za kutembelewa, tena upate kwanza ruhusa ya mkuu wa bweni na usimuingize bwenini. 3.6. Usiende nje bila ya ruhusa maalumu; ukienda kwenye ibada uvae sare na kurudi shuleni mara, bila ya kupitia sehemu nyingine. 3.7. Usipige pasi ndani ya majengo wala kutumia vibatari au mishumaa. 4. Adhabu 4.1. Ukikosa kufika shuleni siku 30 mfululizo bila ya taarifa utaachishwa masomo. 4.2. Ukikwepa mtihani wa somo lolote, na vilevile kwa kuibia, kusaidiwa au kusaidia wakati wa kuufanya, utaandikiwa alama sifuri (0%) katika matokeo yako. 4.3. Kwa baadhi ya makosa utapewa kwanza maonyo mawili, ambayo yataandamana na adhabu shuleni na kudai uandike barua ya kukiri kosa na kuahidi hutalirudia. 4.4. Kwa makosa makubwa zaidi hutapewa maonyo, bali utasimamishwa kwa siku au wiki kadhaa, kama si kufukuzwa shule. 4.4. Ukifukuzwa bweni hutaruhusiwa kuendelea na masomo kama mwanafunzi wa kutwa. 4.5. Ukipoteza au kuharibu kitabu au kitu chochote cha shule utatakiwa kununua kipya na kurejesha, la sivyo hutarudishiwa fedha za tahadhari. 4.6. Vitu visivyotakiwa shuleni vikinyang anywa na uongozi hutarudishiwa.

OMBI LA KUANDALIWA MIEZI MITATU KWA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2017 EBU, JAZA SEHEMU ZOTE KWA UKAMILIFU, SI KWA KUBAHATISHA. UONGO WOWOTE HAUTASAMEHEWA! JINA LA KWANZA JINA LA MWISHO JINA LA KATI JINSIA TAIFA KABILA ULIMALIZA LINI DARASA LA SABA? ULIMALIZA KATIKA SHULE IPI? KAMA HUKAI NA WAZAZI, ANAYEKULEA NI NANI KWAKO? JINA LA HUYO MLEZI TAMKO LA MWANAFUNZI: Kisha kusoma sheria za shule, nimezikubali kwa moyo. Basi, naahidi kuzizingatia kwa makini muda wote nitakaokuwa shuleni na kwamba nitashirikiana na viongozi wake kwa kupokea malezi watakayonipatia kama mwanafunzi, nisidai mambo ya pekee kwa msingi wa umri, asili, kabila n.k. Nikihitaji kuhama darasa, bweni au shule.nitatoa kwanza taarifa. TAMKO LA MZAZI/MLEZI WA MWANAFUNZI ASIYEJITEGEMEA: Mimi,, nikiwa mzazi/mlezi wake, nathibitisha kuwa ameelewa na kukubali sheria za shule. Kwa jinsi ninavyomfahamu naamini ataweza kuzishika vizuri. Isipotokea hivyo, niko tayari kukubali uamuzi wowote ambao uongozi wa shule utachukua juu yake. Kwa kumuandikisha katika shule hii naomba Kanisa Katoliki linisaidie kumlea mwanangu, ambaye ni mfuasi wa dini ya., madhehebu ya. Uijaze vizuri na kuitunza hadi siku utakapoturudishia imeambatanishwa na vocha ya ada uliyolipia benki (akaunti ziko MKOMBOZI C.B., namba 00111507671101; pia K.C.B., namba 3300977908. Ukishindwa kulipia huko, unaweza kutumia pia akaunti ya N.B.C., namba 026201160913, jina T.E.C. Mchikichini) ili tuweke kumbukumbu na kukupa risiti yetu. Ukipenda, ujitengenezee kwanza kivuli cha vocha hiyo. Ada ya masomo ni Tsh. 90,000 tu. Wanaohitaji kukaa bweni watapata nafasi katika vituo vifuatavyo: wavulana Malati Secondary School (mtaa wa Bigwa) tu - wasichana Savannah Girls Centre (Mzumbe) tu. Hao waongeze Tsh. 160,000. Jumla ni Tsh. 250,000. Inatakiwa kulipwa kwa mkupuo mmoja. Masomo yataanza tarehe 13-9-2016.

JIMBO KATOLIKI LA MOROGORO Amekubaliwa tarehe... OMBI LA KUINGIA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2017 Ajiunge na darasa la Form I, mkondo... EBU, JAZA SEHEMU ZOTE KWA UKAMILIFU, SI KWA KUBAHATISHA. UONGO WOWOTE HAUTASAMEHEWA! JINA LA KWANZA, LA KATI NA LA MWISHO (KAMA KATIKA CHETI CHA KUZALIWA) JINSIA TAIFA KABILA ULIMALIZA KATIKA SHULE IPI? KAMA HUKAI NA WAZAZI, ANAYEKULEA NI NANI KWAKO? JINA LA MLEZI WAKO ULIMALIZA LINI DARASA LA SABA? TAMKO LA MWANAFUNZI: Kisha kusoma sheria za shule, nimezikubali kwa moyo. Basi, naahidi kuzizingatia kwa makini muda wote nitakaokuwa shuleni na kwamba nitashirikiana na viongozi wake kwa kupokea malezi watakayonipatia kama mwanafunzi, nisidai mambo ya pekee kwa msingi wa umri, asili, kabila n.k. Nikihitaji kuhama darasa, bweni au shule. nitatoa kwanza taarifa. NYONGEZA KWA MWANAFUNZI MKRISTO: Naahidi kufanya bidii katika masomo ya Bible Knowledge na Dini. TAMKO LA MZAZI/MLEZI WA MWANAFUNZI ASIYEJITEGEMEA: Mimi,, nikiwa mzazi/mlezi wake, nathibitisha kuwa ameelewa na kukubali sheria za shule. Kwa jinsi ninavyomfahamu naamini ataweza kuzishika vizuri. Isipotokea hivyo, niko tayari kukubali uamuzi wowote ambao uongozi wa shule utachukua juu yake. Vilevile naahidi kumhamisha ikiwa atakosa mara mbili mfululizo kufikia wastani uliopangwa na kikao cha wazazi (45% kwa masomo yote). Kwa kumuandikisha katika shule hii, naomba Kanisa Katoliki linisaidie kumlea mwanangu, ambaye ni mfuasi wa dini ya, madhehebu ya Fomu hii inakupa haki ya kushiriki usaili tarehe 3-12-2016; mahali ni shuleni hapo, muda ni saa 2:00 asubuhi. Uijaze vizuri na kuirudisha siku ya usaili pamoja na picha yako ya hivi karibuni katika chumba cha mtihani. Usaili utafanyika kwa lugha ya Kiswahili kulingana na elimu ya shule za msingi (Kiswahili, Kiingereza, Hisabati, Sayansi na Maarifa): kila mara watachaguliwa waliofanya vizuri zaidi. Matokeo yatapatikana baada ya siku tatu hapa na katika tovuti ya shule (www.kigur.com). Kuanzia hapo maelekezo ya kujiunga yatapatikana ofisini mwa mhasibu na katika tovuti hiyo. Baada ya kujaza hivyo mikondo minne usitegemee kupata nafasi hapa kwa njia nyingine, ila baadhi watachaguliwa kusoma katika shule nyingine za mtandao wetu: Malati na Askofu Adrian Mkoba.

OMBI LA KUJIUNGA NA MASOMO YA JIONI (P I, I-II, P III, III-IV, P IV) Ajiunge na darasa la..., mkondo... EBU, JAZA SEHEMU ZOTE KWA UKAMILIFU, SI KWA KUBAHATISHA. UONGO WOWOTE HAUTASAMEHEWA! JINA ULILOTUMIA KWA MITIHANI YA TAIFA JINSIA TAIFA KABILA KAMA ULIANZA SEKONDARI, ULISOMA MPAKA KIDATO CHA NGAPI? ULIMALIZA LINI DARASA LA SABA? JE, ULIFANYA MTIHANI WA MAARIFA (=Q.T.)? JE, ULIFAULU? KAMA UMESHAFANYA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE, ANDIKA A, B+, B, C NA D ULIZOPATA: CIVICS... HISTORY... GEOGRAPHY... ENGLISH... KISWAHILI... PHYSICS... CHEMISTRY... BIOLOGY... MATHEMATICS... BIBLE KNOWLEDGE... MENGINEYO (UYATAJE) 1)... 2)... 3)... KAMA UNAJITEGEMEA, UNAFANYA KAZI GANI? KAMA HUJITEGEMEI WALA HUKAI NA WAZAZI, ANAYEKULEA NI NANI KWAKO? JINA LA MLEZI WAKO TAMKO LA MWANAFUNZI: Kisha kusoma sheria za shule, nimezikubali kwa moyo. Basi, naahidi kuzizingatia kwa makini muda wote nitakaokuwa shuleni na kwamba nitashirikiana na viongozi wake kwa kupokea malezi watakayonipatia kama mwanafunzi, nisidai mambo ya pekee kwa msingi wa umri, asili, kabila n.k. Nikitaka kuhama darasa, bweni au shule, nitatoa kwanza taarifa. NYONGEZA KWA MWANAFUNZI MKRISTO: Naahidi kufanya bidii katika masomo ya Bible Knowledge na Dini..... TAMKO LA MZAZI/MLEZI WA MWANAFUNZI ASIYEJITEGEMEA: Mimi,, nikiwa mzazi/mlezi wake, nathibitisha kuwa ameelewa na kukubali sheria za shule. Kwa jinsi ninavyomfahamu naamini ataweza kuzishika vizuri. Isipotokea hivyo, niko tayari kukubali uamuzi wowote ambao uongozi wa shule utachukua juu yake. Kwa kumuandikisha katika shule hii, naomba Kanisa Katoliki linisaidie kumlea mwanangu, ambaye ni mfuasi wa dini ya, madhehebu ya... Uijaze vizuri na kuitunza hadi utakapoirudisha imeambatana na kivuli cha hati ya matokeo ya mtihani wa kidato cha nne (pamoja na ya kurisiti). Ulete pia vocha ya ada uliyolipia benki ili tuweke kumbukumbu na kukupa risiti yetu. Ukipenda, ujitengenezee kwanza kivuli cha vocha hiyo. Akaunti yenye jina la shule iko MKOMBOZI C.B., namba 00111507671101; pia K.C.B., namba 3300977908. Ukishindwa kulipia huko, unaweza kutumia pia akaunti ya N.B.C., namba 026201160913, jina T.E.C. Mchikichini. Masomo yataanza tarehe 10-1-2017: watapata nafasi watakayowahi kuleta vitu hivyo ofisini mwa mhasibu hata kabla ya tarehe hiyo. Baada yake usilipe benki kabla hujawasiliana na ofisi hiyo ili kuhakikisha kama nafasi ipo bado.

JIMBO KATOLIKI LA MOROGORO OMBI LA KUINGIA KIDATO CHA TANO MWAKA 2017 Ajiunge na darasa la Form V, kombi... EBU, JAZA SEHEMU ZOTE KWA UKAMILIFU, SI KWA KUBAHATISHA. UONGO WOWOTE HAUTASAMEHEWA! JINA ULILOTUMIA KWA MITIHANI YA TAIFA TAIFA KABILA ULIMALIZA LINI KIDATO CHA NNE? UMERISITI MARA NGAPI? ANDIKA A, B+, B, C NA D ULIZOPATA KATIKA KUFANYA AU KURISITI MTIHANI WA KIDATO CHA NNE: JINSIA CIVICS... HISTORY... GEOGRAPHY... ENGLISH... KISWAHILI... PHYSICS... CHEMISTRY... BIOLOGY... MATHEMATICS... BIBLE KNOWLEDGE... MENGINEYO (UYATAJE) 1)... 2)... 3)... 4)... 5)... ANDIKA SANDUKUNI NAMBA YA KOMBI UNAYOTAKA KUFUNDISHWA KATI YA HIZI ZIFUATAZO: 1) HKL (History, Kiswahili, Language) 2) HGK (History, Geography, Kiswahili) 3) HGL (History, Geography, Language) 4) HGE (History, Geography, Economics) 5) EGM (Economics, Geography, Mathematics) KAMA UNAJITEGEMEA, UNAFANYA KAZI GANI? KAMA HUJITEGEMEI WALA HUKAI NA WAZAZI, ANAYEKULEA NI NANI KWAKO? JINA LA MLEZI WAKO TAMKO LA MWANAFUNZI: Kisha kusoma sheria za shule, nimezikubali kwa moyo. Basi, naahidi kuzizingatia kwa makini muda wote nitakaokuwa shuleni na kwamba nitashirikiana na viongozi wake kwa kupokea malezi watakayonipatia kama mwanafunzi, nisidai mambo ya pekee kwa msingi wa umri, asili, kabila n.k. Nikitaka kuhama darasa, bweni au shule, nitatoa kwanza taarifa. NYONGEZA KWA MWANAFUNZI MKRISTO: Naahidi kufanya bidii katika masomo ya Divinity na Dini. TAMKO LA MZAZI/MLEZI WA MWANAFUNZI ASIYEJITEGEMEA: Mimi,, nikiwa mzazi/mlezi wake, nathibitisha kuwa ameelewa na kukubali sheria za shule. Kwa jinsi ninavyomfahamu naamini ataweza kuzishika vizuri. Isipotokea hivyo, niko tayari kukubali uamuzi wowote ambao uongozi wa shule utachukua juu yake. Vilevile naahidi kumhamisha ikiwa atakosa mara mbili mfululizo kufikia wastani uliopangwa na kikao cha wazazi (45% kwa masomo yote). Kwa kumuandikisha katika shule hii, naomba Kanisa Katoliki linisaidie kumlea mwanangu, ambaye ni mfuasi wa dini ya, madhehebu ya... Uijaze vizuri na kuirudisha pamoja na vivuli vya vyeti vyako vya kuzaliwa na kumaliza shule na hati ya matokeo (hati halisi, si matokeo yaliyopakuliwa kutoka tovuti ya NECTA). Usaili utategemea vivuli hivyo tu. Matokeo yatatangazwa tarehe 12-6-2017, saa 2:00 asubuhi. Watakaochaguliwa wataanza masomo tarehe 4-7-2017. Baada ya wiki moja, wale wa akiba wataweza wakapewa nafasi kama hao wa kwanza hawataripoti mapema.

JIMBO KATOLIKI LA MOROGORO OMBI LA KUANDALIWA MWAKA MMOJA KWA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2018 Ajiunge na darasa la V-VI, mkondo... EBU, JAZA SEHEMU ZOTE KWA UKAMILIFU, SI KWA KUBAHATISHA. UONGO WOWOTE HAUTASAMEHEWA! JINA ULILOTUMIA KWA MTIHANI WA TAIFA TAIFA KABILA JINSIA ULIMALIZA LINI KIDATO CHA NNE? ANDIKA A, B+, B, C NA D ULIZOPATA KATIKA KUFANYA AU KURISITI MTIHANI WA KIDATO CHA NNE: CIVICS... HISTORY... GEOGRAPHY... ENGLISH... KISWAHILI... PHYSICS... CHEMISTRY... BIOLOGY... MATHEMATICS... BIBLE KNOWLEDGE... MENGINEYO (UYATAJE) 1)... 2)... 3)... ANDIKA SANDUKUNI NAMBA YA KOMBI UNAYOTAKA KUFUNDISHWA KATI YA HAYA YAFUATAYO: 1) HKL (History, Kiswahili, English) 2) HGK (History, Geography, Kiswahili) 3) HGL (History, Geography, English) KAMA UNAJITEGEMEA, UNAFANYA KAZI GANI? KAMA HUJITEGEMEI WALA HUKAI NA WAZAZI, ANAYEKULEA NI NANI KWAKO? JINA LA MLEZI WAKO TAMKO LA MWANAFUNZI: Kisha kusoma sheria za shule, nimezikubali kwa moyo. Basi, naahidi kuzizingatia kwa makini muda wote nitakaokuwa shuleni na kwamba nitashirikiana na viongozi wake kwa kupokea malezi watakayonipatia kama mwanafunzi, nisidai mambo ya pekee kwa msingi wa umri, asili, kabila n.k. Nikitaka kuhama darasa, bweni au shule, nitatoa kwanza taarifa. NYONGEZA KWA MWANAFUNZI MKRISTO: Naahidi kufanya bidii katika masomo ya Divinity na Dini..... TAMKO LA MZAZI/MLEZI WA MWANAFUNZI ASIYEJITEGEMEA: Mimi,, nikiwa mzazi/mlezi wake, nathibitisha kuwa ameelewa na kukubali sheria za shule. Kwa jinsi ninavyomfahamu naamini ataweza kuzishika vizuri. Isipotokea hivyo, niko tayari kukubali uamuzi wowote ambao uongozi wa shule utachukua juu yake. Kwa kumuandikisha katika shule hii, naomba Kanisa Katoliki linisaidie kumlea mwanangu, ambaye ni mfuasi wa dini ya, madhehebu ya... Uijaze na kuitunza hadi utakapoirudisha imeambatana na kivuli cha hati ya matokeo ya mtihani wa kidato cha nne (pamoja na ya kurisiti). Ulete pia vocha ya ada uliyolipia benki ili tuweke kumbukumbu na kukupa risiti yetu. Ukipenda, ujitengenezee kwanza kivuli cha vocha hiyo. Ada ya masomo ya mchana ni Tsh. 300,000 kwa mwaka. Inatakiwa kulipwa kwa mkupuo mmoja katika akaunti yenye jina la shule huko MKOMBOZI C.B., namba 00111507671101; pia K.C.B., namba 3300977908. Ukishindwa kulipia huko, unaweza kutumia pia akaunti ya N.B.C., namba 026201160913, jina T.E.C. Mchikichini.

FOMU YA KUKUBALI MASHARTI YA BWENI JINA LA MWANAFUNZI.. FORM.. TAMKO LA MWANAFUNZI: Kisha kusoma sheria za shule, nimezikubali kwa moyo. Basi, naahidi kuzizingatia kwa makini muda wote nitakaokuwa bwenini na kwamba nitashirikiana na viongozi wake kwa kupokea malezi watakayonipatia kama mwanafunzi, nisidai mambo ya pekee kwa msingi wa umri, asili, kabila n.k.... TAMKO LA MZAZI/MLEZI: Mimi,, nikiwa mzazi/mlezi wake, nathibitisha kuwa ameelewa na kukubali sheria za shule. Kwa jinsi ninavyomfahamu naamini ataweza kuvishika vilivyo. Isipotokea hivyo, niko tayari kukubali uamuzi wowote ambao uongozi wa shule utachukua juu yake. Kwa kumuandikisha katika bweni hilo, naomba Kanisa Katoliki linisaidie kumlea mwanangu, ambaye ni mfuasi wa dini ya..., madhehebu ya... Naomba aruhusiwe siku ya... aende kusali katika kanisa la... (au katika msikiti wa......). Kwa kumuombea ruhusa nachukua mimi jukumu la matendo yake akiwa nje ya shule siku hiyo. Wakati wa likizo atakuwa anakwenda... Asipoweza kurudi shuleni siku iliyopangwa au nikitaka ahame bweni, nitatoa taarifa mwenyewe. Ndugu wa karibu wanaoruhusiwa kumtembelea ni: 1)...... 2)...... 3)...... 4)........ Anwani.. Simu...... Tarehe...