Uzio wa pilipili unazuia tembo kuvamia mazao shambani! Jinsi ya kujenga na kudumisha uzio wa pilipili Tanzania

Similar documents
Information for assessors (do not distribute this page to participants):

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

TIST HABARI MOTO MOTO

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees

TANZANIA MARKETS PAN Sera zinazoboresha masoko

UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA)

Miradi na jamii. 3.1 Utangulizi

Mwongozo wa Kutathimini mifumo ya Ugawanaji wa faida na Mapato Katika Miradi ya Jamii ya MKUHUMI

JAMHURI YA KENYA. Mkakati wa Ushirikiano MUKHTASARI FY Public Disclosure Authorized. Public Disclosure Authorized

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU

TIST HABARI MOTO MOTO MAANDALIZI YA MWAKA 2000 Y2K PREPARATIONS SASA NI WAKATI WA KUANZA KUPANDA MBEGU ZAKO

Uhakika wa Mbegu kwa Uhakika wa Chakula MWONGOZO WA UZALISHAJI WA MBEGU ZA ASILI ZA MAHINDI

Human Rights Are Universal And Yet...

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi

ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA UCHUMI WA ZANZIBAR

MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA PRO-ROUTES. Ombi kwa ajili ya fedha za umma wa mradi wa ziada

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

KUWEZESHA MBINU ZA UZUIAJI MIMBA KATIKA SUHULA ZA AFYA: MASWALI 10 KWA VIKUNDI VYA JAMII KUZINGATIA

Kubadili Sheria Za Mbegu Na Ulinzi Wa Aina Za Mbegu Na Mimea Nchini Tanzania

HAKI NA TARATIBU ZA AJIRA, KAZI NA HIFADHI YA JAMII

NGUZO KUMI ZA KILIMO KWANZA

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

Bustani 10,000 Katika Afrika. Alberto Prina

Waandishi: wa Toleo la 5. Scholastica Jullu Athanasia A. Soka Safina Hassan Mary Njau. Toleo la 5: 2008 ISBN

TIST HABARI MOTO MOTO. Benefits of Loan Repayment. Faida za ulipaji wa mikopo U OTESHAJI W A M ITI Y A M ATUNDA

Upande 1.0 Bajeti yako

MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA. Kwa Wanaoanza

Na Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake Toleola4

Ni kwa nini mkulima awe maskini?

Hatari, Haki za Usalama katika Bahari 03

Programu ya Uendelezaji Mifumo ya Maji Vijijini (PUMMV) katika Tanzania. Modeli wa Ukodishaji Mradi

Muhtasari wa taarifa ya warsha ya wataalamu juu ya mfumo wa habari kwa njia ya ramani (PGIS), Morogoro, Juni 30 - Julai 1, 2014

JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1

Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara)

KUHUSU AFRODAD. Dira ya AFRODAD. Dhamira ya AFRODAD. AFRODAD inalenga mchakato sawa na endelevu wa maendeleo kuelekea Afrika yenye mafanikio.

In the matter of an Application by the KIGOMA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (KUWASA) For a Tariff and Charges Adjustment

RIPOTI YA WARSHA KUHUSU HABARI KWA AJILI YA UWAJIBIKAJI

Kimesanifiwa na:- E.D.Kissuu ECOMM TANZANIA S.L.P ,Dar es Salaam. Simu:

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

Kuuelewa Mchakato wa Bajeti Tanzania Mwongozo wa Asasi za Kiraia

KILIMO CHA VITUNGUU MAJI NA VITUNGUU TWAUMU (SWAUMU)

2 Usimamizi wa Rutuba ya Udongo Tanzania Organic Agriculture Movement

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA FEDHA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

Dodoma ambako kikao cha Bunge kinaendelea kuja kushiriki japo sehemu ya uzinduzi wa mkutano.

Mwongozo wa Jamii juu ya Afya ya Mazingira

UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU VIKWAZO VYA KULINDA MAISHA KATIKA USAIDIZI WA KIMATAIFA WA AFYA KWA MSAADA WA KIMATAIFA UNAOFADHILIWA NA MAREKANI

JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI

Kitabu Cha Mafunzo Ya Uongozi Kwa Wanawake

Utangulizi wa ugonjwa wa shinikizo la damu

MAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II

Summaries of GC Reports 2012, Vol. 2, Sec. 1, Swahili

International Labour Office. Kazi za Ndani Zenye Madhara kwa Watoto: Kijitabu cha Maelezo Mafupi

Kijitabu cha Maelezo cha Programu ya Famasia

Pronunciation: Mä-hret Zäläke Ndal-ka-tscho Molla Mare Gebre-gzabiär 1/12

Kifaa Maalum cha Kutazamia Jua: Maelekezo ya kutumia

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO

UFUATILIAJI WA MIRADI NA TATHMINI

Taarifa Kuhusu Hali ya Uchumi wa Tanzania

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

Siku ya kwanza. Mguso wa ngozi-kwa-ngozi (Ulezi wa kangaruu) Mtoto wako anaweza kuhisi mdundo wa moyo wako

MWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI

Tufundishane! Mwalimu Bora In this issue: Issue 6, December Do you want to be in our next issue?

Songa kwenye kilele cha upeo. Masuala ya Msingi na Ujuzi juu ya Uendeshaji wa Serikali za Mitaa

KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA

pages/mkulima-mbunifu/

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

Shamba Darasa na Stadi za Maisha kwa Vijana (SDSMV) Tanzania. Kiongozi Cha Mwezeshaji. Jaap Van Pol na Francesca Dalla Valle

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )

ONDOA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI: LINDA AFYA YA WATOTO

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA. Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo. TOLEO Na.

Mwongozo wa Utamaduni Toleo la Kwanza

Vijana wanazungumza kuhusu ujinsia, maisha na uhusiano VIJANA WANAZUNGUMZA KUHUSU NGONO, MAISHA NA UHUSIANO. Training and Research Support Centre

Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA 2006/07

Deputy Minister for Finance

TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM)

Kiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika

Dibaji ya Mwenyekiti wa Kamati ya Pamoja ya Uongozi

4 WADUDU,MAGONJWA NA MAGUGU

NGUO MPYA ZA UKOLONI. Mikataba ya Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Umoja wa Ulaya na Afrika. Agosti 2017

KAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI TANZANIA

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA MHESHIMIWA DKT

Kutetea Haki za Binadamu

MAADHIMISHO YA MIAKA 15 YA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

Mukhtasari Wa Mabishano Kwa Na Dhidi Ya Vikombe Vingi Vya Ushirika

5. Mheshimiwa Spika, Bunge lako Tukufu lilijadili kwa kina Miswada ifuatayo:

Mwongozo wa Familia wa Kujifunza

Ufanisi katika Ufundishaji kwenye Shule za Msingi na Sekondari nchini Tanzania

In the matter of Application by the TANGA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (TANGA UWASA) For a Multi-Year Tariff Adjustment

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu WEMA

TAARIFA YA MWAKA YA UTENDAJI KAZI IDARA YA UTAWALA BORA 2013/2014

Transcription:

Uzio wa pilipili unazuia tembo kuvamia mazao shambani! Jinsi ya kujenga na kudumisha uzio wa pilipili Tanzania

Jinsi ya kujenga na kudumisha uzio wapilipili Tanzania Wildlife Division, Tanzania Wildlife Research Institute, Tanzania National Parks, World Animal Protection, Aage V. Jensen Charity Foundation, TUI, RESOLVE, Biodiversity & Wildlife Solutions, Mikumi & Tarangire Tembo-Pilipili Teams, Honeyguide Foundation Imetafsiriwa na Raphael Omondi Wahariri: Alex Chang a, Raphael Omondi, Jonathan Konuche, David Olson, Nick DeSouza Arusha, Tanzania June 2015 Migogoro kati ya wanadamu na tembo ni swala la kitaifa nchini Tanzania, na ina madhara kwa tembo na maisha ya wanajamii wanaozunguka hifadhi za wanyamapori, kwa hivyo ina athiri juhudi za uhifadhi wa wanyamapori na mipango ya upunguzaji umaskini nchini Tanzania.

Uzio wa pilipili huzuia tembo kuvamia mazao mashambani! Jinsi ya kujenga na kudumisha uzio wa pililipili Kwa nini tunatumia uzio wa pilipili? Tembo wanapenda sana kula mazao. Wanaweza kuharibu eneo kubwa la shamba na kusababisha uhaba wa chakula na kupunguza kipato kwa mkulima ambacho ni hasara kubwa kwa wakulima. Tembo pia wanaweza kuwa hatari kwa binadamu, wanapokwenda kula mazao wakati wa giza, wanaweza kuuwa au kujeruhi watu. Wakulima wamejaribu mbinu mbali mbali za kuwazuia tembo wasivamia mashamba na kuwafukuza kutoka vijijini kwa kutumia moto, kelele, mitego ambayo inaweza kuwajeruhi tembo, kupanda mimea kama uzio na uwa wenye miba mikali. Lakini tembo ni waerevu na wajasiri na pia wanazoea haraka mbinu mbalimbali zinazotumika, baadaye hupuuza na kuingia shambani. Wengine wamejaribu uzio wa mizinga ya nyuki, mizinga ya nyuki iliyofungwa pamoja kwenye mstari huzuia tembo, lakini uzio wa mizinga ya nyuki una kazi ngumu na gharama kubwa kuweka na kudumisha kuzunguka mashamba makubwa na mara nyingi mizinga ni vigumu kuingia nyuki. Wakati mwingine tembo wanachomwa mikuki, kunaswa kwenye mitego, kupigwa na mishale na kupewa sumu, mbinu hizi ni kinyume cha sheria na zitachangia kutoweka kwa tembo kama rasilmali na urithi wa taifa la Tanzania. Tembo waliojeruhiwa ni hatari sana kwa wanadamu. Uzio wa kamba ya makonge wenye oili machafu na pilipili umethibitishwa kufanya vizuri kuwazuia tembo kuvamia mazao. Uzio huu haufanyi kazi wakati wote kwani baadhi ya tembo wamebuni jinsi ya kuingia kwenye mashamba kwa kutembea wakirudi nyuma ama kuvunja uzio kwa kutumia matawi ya miti, lakini kwa muda wa miaka sita sasa hutajashuhudia hata tukio moja ya uzio kuvunjwa Mikumi. Uzio wa pilipili unafanya kazi vizuri sana ukilinganisha na gharama ya kujenga na kudumisha wakati mazao yanakaribia kuvunwa na wakati wa mavuno. Pia, uzio wa wa pilipili unaweza kugharamiwa na kudumishwa na wakulima wenyewe bila msaada wowote kutoka serikalini au asasi zisizokuwa za kiserikali. Uzio wenyewe si ghali kujenga na kudumisha ikilinganishwa na baadhi ya mbinu zingine za kupunguza uvamizi wa

tembo kwenye mazao. Uzio wa pilipili unafanya kazi usiku na mchana, hivyo wakulima hawatakesha usiku kucha. Hapa tunaonyesha jinsi wakulima wanavyoweza kuweka uzio wa pilipili na kuudumisha msimu wa mavuno. Pia tunapendekeza njia ambazo wakulima wanavyoweza kuunda vikundi vya kijamii (Community Based Organization CBO) ambavyo vitawezesha wakulima kulima kwa pamoja na kuendesha mradi wa kuweka na kukopa, mikopo hii inawezakutumika kununua vifaa vya kuzuia tembo kuharibu mazao na kuwalipa fidia wanachama wa kikundi ikiwa mazao yao yataharibiwa na tembo baada ya kutumia uzio wa pilipili. Vikundi vya wakulima vinavyo tumia uzio wa pilipili vimekuwa vikifanya kazi katika maeneo ya hifadhi zaa Mikumi na Tarangire kwa miaka kadhaa sasa. Tuna imani kwamba mbinu hii au taratibu huu utafanya vyema kwa wakulima wengine Tanzania. Tembo wanauwezo mkubwa sana wa kunusa na hawapendi harufu ya pilipili. Kwa hivyo, hawawezi kuizoea mbinu hii kama mbinu nyingine ambazo zimekwisha jaribiwa za kuwaondoa mashambani. Ili uzio wa pilipili ufanye kazi kikamilifu, inahitaji kujengwa na kudumishwa msimu unaofaa wakati mazao yanaiva na wakati kuna uwezekano mkubwa wa tembo kuvamia. Vifaa gani vinahitajika kujenga Uzio? Uzio wa pilipili unatengenezwa kwa kamba mbili au tatu za mkonge/katani zilizofungwa kwenye nguzo zinazozunguka mazao.

Kamba yenye vitambaa vya pamba vilivyochanganywa na kunyweshwa kwenye oili iliyotumika ya gari yenye pilipili na kufungwa kwenye Kamba za katani katitaki ya nguzo mbili. Vitambaa vya pamba na kamba za mikonge vinachanganywa kwanza kwenye oili iliyotumika ya gari iliyochanganywa na pilipili ambayo imekaushwa na kusagwa. Nguzo inafaa iwe kubwa kiasi cha kuweza kusimamisha uzio imara ambao utasimama ikiwa itasukumwa na upepo au wanyama kama ng ombe n.k. Nguzo pia iwe na ubora wa hali ya juu ili isioze wakati wa mvua. Nguzo inaweza kutumiwa kila mwaka ikiwa itawekwa kwenye sehemu kavu. Kamba ya mkonge/katani, vitambaa vya pamba, na oili ya injini ya gari iliyotumika na pilipili iliyosagwa ni baadhi ya vitu vinavyohitajika kujenga uzio wa pilipili. Ni shamba la namna gani linatakiwa kuwekewa uzio, mashamba yapi yanafaa kuwekwa Uwa? Ni shamba aina gani linatakiwa kuwekwa uzio wa kuzuia tembo? Aina fulani ya mazao inawavutia tembo kuliko nyingine na nyingine inaweza kuliwa na tembo kwa muda mrefu kuliko aina nyingine. Wakulima wanaelewa vyema kama mazao yao yapo kwenye hatari ya kuvamiwa na tembo. Ni sharti wakulima washirikiane kwa karibu na Afisi

Wanyamapori wa Wilayani, Kikundi Maalum cha Kuzuia Tembo vijijini (Village Game Scout), Maafisa wa jamii wa hifadhi (community outreach officer) na Maafisa ugani wa Kilimo ili kubaini mpango bora zaidi ya kutumia uzio wa pilipili kulinda mazao. Vikundi vya wakulima wanaweza kufanya kazi pamoja kwa kuweka uzio mashamba kwa pamoja ili kupunguza kiasi cha vifaa vitakavyotumika kuzunguka mashamba yao. Wakati mwingine, mashamba vinayopakana na hifadhi za wanyamapori wanakoishi tembo au kwenya njia wanakopitia ndiyo wanaweza kufaidika na uzio wa pilipili. Ikiwa shamba lina uzio wa pilipili, tembo mara nyingi ataelekea sehemu ambako ni rahisi kupata chakula, kwenye shamba ambalo halina uzio au atarudi hifadhini. Aina ya mazao inayohitajika kuwekewa uzio wa pilipili inategemea tembo walivyozoea kula mazao na thamani ya mazao kwa wakulima. Wakati mwingine, wakulima hupanda pilipili kuzunguka mazao yao na kuweka uzio wa pilipili kusaidia kuzuia tembo kupitia harufu ya mimea ya pilipili vilevile pilipili iliyolimwa itatosha kujenga uzio wa pilipili na pilipili ya ziada itauzwa ili kujiongezea kipato.

Unahitaji vifaa kiasi gani ili kujenga Uzio? Kadiria nguzo ngapi na kiasi gani cha vifaa vingine vinahitajika ili kujenga uzio kwenye shamba unalotaka kulinda. Unahitaji kukusanya vifaa na kuomba wenzako au marafiki au wanachama wa kikundi kukusaidia kuweka uzio. Kuweka uzio katika ekari moja ya mazao, tunahitaji kama lita kumi (10) ya mafuta ya injini ya gari yaliyotumika, kilo mbili na nusu (2.5 kg) ya pilipli iliyosagwa, vipande thelathini na mbili (32) vya nguo ya pamba (futi 2 kwa1.5), kilo tano (5) za kamba ya mkonge/katani, na nguzo thelathini na sita (36) za zenye urefu wa mita tatu ( 3m) na unene au kipenyo cha kati ya inchi mbili na tatu (2-3). Tunakadiria gharama ya vifaa vya kuweka uzio katika eka saba (7) ya shamba ni kama (dola arobaini ($40) za kimarekani au shilling elfu themanini na sita (86,000) kwa pesa za Tanzania), kwa mashamba yaliyo limwa pamoja au karibu karibu unaweza kutengeneza uzio kwa pamoja kama mraba ili kufanya uzio kuwa mfupi na kupunguza ngarama. Ni wakati gani unafaa kujenga uzio kuzunguka mazao? Baini lini uzio utajengwa na kubomoa uzio. Ni bora kujenga uzio wakati mazao yanaiva na yanakaribia kuvunwa. Kufanya hivyo husaidia kuzuia tembo kutozeoa uzio. Wakulima tofauti wanaweza kuweka uzio kwa wakati unaofaa kwao kutokana na aina ya mazao na jinsi ya uvamizi wa tembo kwa mazao katika eneo lao unavyofanyika. Uzio unatakiwa kubomolewa mara baada ya mavuno. Kuweka Uzio wa Pilipili Tahadhari! Pilipili iliyosagwa inaweza kuwasha macho, pua, na koo la mtu kwa hiyo kila moja anahitajika kuwa maakini kusafisha mikono na vifaa wakati wa kujenga na baada ya kujenga uzio. Watu wengi wanafunika nyuso zao kwa kutumia nguo wakati wanafanya kazi kwa kutumia pilipili. HATUA 1: KUWEKA NGUZO KWENYE ARDHI Nguzo inatakiwa kuwa kubwa kiasi gani? Nguzo zinatikiwa kuwa kati ya sentimita tano (5) na kumi (10) au inchi 2 3 kwa unene au kipenyo na angalau mita mbili na nusu mpaka tatu

kwa urefu (kutoka juu ya ardhi, kumbuka kwamba sehemu ya nguzo itazama kwenye ardhi kwa hivyo bora upate nguzo ya mita tatu (3) kwa urefu. Nguzo zinafaa ziwe ngumu (siyo hafifu na zisizo oza upesi) ili iweze kushikilia kamba ya mkonge na vitambaa vyenye mafuta ya engine ya gari yaliyotumika yenye pilipili, zisirahisi kuanguka zikisukumwa. Nguzo za uwa iliyohai inaweza kutumika yaani nguzo ambazo zitaweza kuota mizizi na kunawiri baada ya kuwekwa kwenye ardhi, na inaweza kutumika siku za usoni nyakati mbali mbali za mavuno. Nguzo zinatakiwa kuwa mbali kiasi gani? Nguzo zinafaa ziwekwa upana kati ya mita saba (7) na kumi (10) kutoka nguzo moja hadi nyingine. Nguzo mbili zinaweza kuwekwa karibu kama mlango ili iwezeshe watu kuingia kwa urahisi.

Nguzo inatakiwa kuwekwa kina gani ndani ya ardhi? Nguzo inahitajika kuzama kina cha wastani kwenye ardhi ili iweze kusimama imara, baada ya kusindilia mchanga (unaweza kuongezea mawe au kokoto katika shimo ili kuongeza uthibiti au kuimarisha kwa kutumia vijiti) ili isiangushwe na ng ombe wakisuma (tembo wanaweza kusukuma na kuangusha nguzo yeyeto kwa urahisi ikiwa wataamua kufanya hivyo). Uzio unahitajika kuwa umbali gani kutoka kwa mazao? Vifaa vingi vitahitajika ikiwa uzio utakuwa mbali sana na mazao. Wakulima wengi wanapanda uzio wa pilipili kama buffer/kinga mita tano (5) hadi kumi (10) kwa upana ukizunguka mazao halafu huongeza uzio wa pilipili kuzunguka mazao. Hatua ya mita nne ( 4) kutoka kwa mazao utasaidia kupunguza mazao kuvutia tembo.

HATUA 2: KUSAGA PILIPILI NA KUCHANGANYA NA OILI YA INJINI YA GARI ILIYOTUMIKA Kiasi cha kama kilo mbili na nusu (2.5 kg) za pilipili (pilipili iliyo kaushwa ni lazima isagwe iwe unga), ni kama mikono kumi na miwili (12) hadi kumi na mitano (15), inachanganywa na lita kumi (10) ya mafuta ya injini ya gari yaliyotumika. Mchanganyiko huo unakorogwa kwa kutumia kijiti.

HATUA 3: NYWESHAJI AU UCHANGANYAJI WA KAMBA ZA MKONGE/KATANI NA VITAMBAA KWENYE OILI YA GARI ILIYOTUMIKA NA PILIPILI

HATUA 4: KUFUNGA KAMBA YA MKONGE/KATANI YENYE PILIPILI NA OILI ILIYOTUMIKA YA INGINI YA GARI KWENYE NGUZO KATIKA UREFU SAHIHI Urefu wa Kamba ya mkonge wa chini iwe mita moja na nusu (1.5) hadi mbili (2) juu ya ardhi na urefu wa Kamba ya mkonge ya pili iwe juu ya ardhi kama mita mbili na nusu (2.5). Uzio ni lazima uzunguke shamba lote kabisa bila kuacha pengo. Ikiwa tembo wanawatoto, inashauriwa kuongeza kamba ya ziada ya tatu mita moja (1) juu ya ardhi ili kuzuia tembo wachanga kutoingia. Baadhi ya wakulima huongeza miti ya miba kuzuia ndama na wanyama wengine kuingia kwenye uzio. Tumesikia kwamba uzio uliwahi kubomolewa na tembo jie ilikumwondoa ndama aliyeingia chini ya uzio wa pilipili.

HATUA 5: KUFUNGA VITAMBAA VYEENYE OILI YA INGINE YA GARI ILIYOTUMIKA NA PILIPILI KWENYE KAMBA ZA MKONGE/KATANI Vipande vya vitambaa vilivyonyweshwa kwenye oili ya engine ya gari iliyo tumika na pilipili vinafungwa katikakati ya nguzo mbili kwenye kamba mbili za juu. Vitambaa vinafaa viwekwe hatua sawa katikati ya nguzo mbili.

Kudumisha uziowa wa Pilipili HATUA 6: MPANGO WA KUIMARISHA UZIO, MUDA GANI UZIO UTAKAA SHAMBANI, NAAMNA YA KUHIFADHI NGUZO, VITAMBAA NA KAMBA ZA KATANI BAADA YA KUVUNA MAZAO Baada ya muda fulani, harufu ya ya pilipili iliyowekwa kwenye uzio iliyokuwa ikiwazuia tembo itapungua na haitafanya kazi kikamilifu kama ilivyokuwa hapo awali. Ni muhimu kuongeza oili ya gari iliyotumika na pilipili (tumia mchanganyiko kama ilivyoelezwa pale mwanzoni wakati uzio ulipowekwa) kwenye kamba za mkonge/katani na vitambaa, ukitumia ndoo, nguo au brashi, kwa utaratibu maalum, rudia baada ya siku ishirini (20) kama hakuna mvua na siku saba (7) kama mvua inanyesha. Pia ikiwa mvua imenyesha wakati wa mavuno, ni jambo bora kuweka oili na pilipili mpya. Ingawaje ni kazi ya ziada kuweka pilipili na oili, lakini ni muhimu. Vikundi vingine vinaajiri au hutafuta mtu maalumu wa kujitolea ili kufanya kazi ya kupaka oili na pilipili kwenye uzio wa pilipili unaomilikiwa na kikundi.

Ni muhimu kukagua uzio kila siku ili kuhakikisha kwamba hakuna sehemu uzio umekatika au nguzo imeanguka kwa kuangukiwa na mti au tawi la mti, kusukumwa na mifugo au tembo. Baada ya mavuno, ni lazima uzio ibomolewe mara moja na nguzo kuhifadhiwa katika sehemu kavu kwa matumizi ya musimu ujao, kamba na vitambaa zihifadhiwe ili zitumike mara nyingine mwaka ujao. Picha na Randy J Braun

Tofali la pilipili Pilipili iliyosagwa inaweza kuchomwa na kutoa moshi wakati wa usiku ili kuwazuia tembo wasivamie mazao. Matofali ya pilipili yanatengenezwa kwa kuongeza maji kwenye machanganyiko wa nusu kinyesi cha ng ombe na nusu pilipili iliyosagwa. Mchangayiko unafinyangwa ili kutengeneza tofali lenye sentimita kumi na sita (16) kwa urefu na ishirini (20) kwa upana.tofali litaanikwa kwenye jua ili likauke kwa muda wa siku mbili (2) hadi tatu(3). Wakati wa jioni, tofali linawashwa moto ili kutoa moshi. Tofali lililowashwa huwekwa kwenye njia wanazotumia tembo kuvamia mazao mashambani.

Vikundi Vya Kijamii (Community-Based Organization CBO) vya kusaidia jamii kuweka uzio wa pilipili na kujikimu kimaisha Ili wakulima na jamii ya wakulima waweze kutumia na kugharamia uzio wa pilipili kila mwaka, bila ya kutegemea msaada kutoka serikalini au taasisi zingine wanaweza kuunda kikundi cha kijamii (Community-Based Organisation CBO) ambacho kitawawezesha wakulima kusimamia kikamilifu rasilmali zao. Vikundi vya kijamii vinaweza kuazisha mfuko wa kuweka na kukopa ambao utawasaidia kusimamia rasilmali ya fedha, kupata mikopo, na kuwa na bima au kupata msaada ikiwa kuna janga litampata mwanachama. Vikundi vya kuweka na kukopa vijijini zinaweza kutoa mikopo kwa wanachama ili kuwawezesha kununua vifaa vya kutengenezea uzio wa pilipili na kununua pembejeo za kilimo wakati ambao upatikanaji wa fedha ni mgumu. Baada ya Kikundi cha kijamii kusajiliwa rasmi serikalini, kinaweza kupokea misaada na huduma mbali mbali kutoka serikalini na taasisi nyingine. Serikali ya Tanzania hufanya kazi na wakulima kupitia vikundi vya kijamii vilivyosajiliwa rasmi na halmashauri za wilaya. Ili kuunda kikundi cha kijamii, kunahitajika wanachama wasiopungua kumi (10) kuitisha mkutano rasmi, kuandika mhutasali ukiwa na sahihi za wajumbe, pamoja na kutunga katiba inayoelaza kwa uwazi mahali wanapo toka, malengo ya kikundi, namna ya usimamizi wa fedha na maswala mengine yanayo husu kikundi na kupeleka halmashauri ya wilaya. Wakati mwingine, vikundi vinaomba msaada kutoka Maafisa wa Maendeleo wa Wilaya au Mashirika yasiokuwa ya Kiserikali ili wawasaidie namna ya kuunda katiba na kuunda kikundi.

Faida mojawapo ya kuunda kikundi cha kijamii ni kwamba kikundi kinaweza kuwakutanisha wanakikundi na taasisi za serikali na taasisi zisizo za kiserikali. Serikali, mabenki, taasisi za kifedha, sekta binafsi na mashirika yasio kuwa ya kiserikali hupenda kufanya kazi na vikundi vilivyosajiliwa kisheria. Shirika moja la Tanzania linalofanya kazi na vikundi vya wakulima vilivyosajiliwa ni (MVIWATA) yaani Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA). JINSI MPANGO WA KUWEKA NA KUKOPA UNAVYOFANYA KAZI Hapa tunaelezea namna ya muundo wa kuweka na kukopa unavyofanyakazi Mikumi, Tanzania. Pamoja na kikundi kuweza kufanya kazi na serikali na taasisi za kifedha, vikundi vya kijamii vinaweza kuazisha mpango wa kuweka na na kukopa utakaoisaidia jamii kiuchumi.

Utaratibu wa kuazisha kikundi cha kuweka na kukopa unaazishwa na wanachama wanaojichangua wenyewe kwa hiari yao kuazisha mpango wa kuweka na kukopa. Fedha zinawekwa kwenye mfuko wa mikopo ambao wanachama watakopa na kulipa mikopo ikiwa na ziada ya mkopo Umoja wa kuweka na kukopa ni kama Savings Credit Cooperative Society (SACCOS), vikundi hivi ni mfumo mdogo wa kifedha wa kijamii. Madhumuni: Dhumini la mhimu sana la mpango wa kuweka na kukopa ni kusaidia jamii kuweka fedha na kupata mikopo mahali ambapo hakuna huduma za kifedha kutoka kwenye mabenki na taasisi nyingine za kifedha na kuwasaidia wanajamii ambao kipato chao ni kidogo sana na hawawezi kuweka fedha benki. Mikopo inawezakuwa aina ya kinga fulani kwa mwanachama ikiwa pamoja na mfuko wa jamii unaotoa msaada kwa mwanachama anapopata matatizo au janga ambalo halikutarajiwa. Wanachama wa kuweka na kukopa wanafanya maamuzi yao wenyewe bila kuingiliwa na mtu. Uwazi: Shughuli zote za kifedha zinafanyika kwenye mikutano mbele ya wanachama wote, ilikuhakikisha kuna uwazi na uwajibikaji. Ili kuhakikisha kwamba shughuli zote hazitekelezwi nje ya mikutano ya kawaida, sanduku la pesa gumu la bati lenye kufuli na funguo tatu hutumika, funguo hutuzwa na watu watatu tofauti waliochanguliwa na kikundi ili kuzuia fedha zisitolewe bila idhini ya mkutano na kuzuia uwezekano wa kubadilisha kumbukumbu. Mzunguko wa kuweka na kukopa una muda maalum. Mwisho wa mzunguko, fedha zilizowekwa na ziada ya mikopo inagawanywa kwa wanachama kulingana na fedha (hisa) alizoweka kila mwanachama. Mwisho wa mzunguko ni muhimu sana, ni wakati wa kutatua matatizo yaliyojitikeza, kuweka uwazi na kuongeza imani kwa wanachama. Inashauriwa mzunguko usizidi mwaka mmoja. Kijitabu cha kumbukumbu cha mwanachama: kila mwanachama atakuwa na kitabu cha kumbukumbu cha fedha anazoweka na mikopo anayochukua. Hakutakuwa na leja kwenye kikundi cha kuweka na kukopa. Kiazio na salio la fedha la mfuko wa jamii na mfuko wa mikopo linatakiwa wanachama washike kichwani na kutamukwa wakati mkutano unaaza.

Uanachama: Kikundi cha kuweka na kukopa kinatakiwa kuwa na wanachama 10 30 ili kuwa na idadi ya kutosha ya kuweka hisa za kutosha kwa ajili ya mikopo na idadi inayokuwa rahisi kufanya mkutano kwa urahisi na kwa muda mfupi. Wanachama wanajichagua wenyewe (watu majirani na waaminifu) wanaweza kuwa wanaume na wanawake pamoja. Inatakiwa angalau wanawake watatu kwenye kamati ya uendeshaji yenye watu watano. Mtu ambaye ni mfanyakazi wa uma hafai kuwa kwenye kamati ya uendeshaji. Mikutano: Kikundi kitakutana kila baada ya muda fulani watakaojipangia wenyewe, inashauriwa kwenye mzunguko wa kwanza wakutane kila baada ya wiki au wiki mbili au baada ya wiki nne kama watakavyo amua wanachama. Kwenye mizunguko ya siku za baadaye wanaweza kupunguza mikutano. Muundo na Vyeo: Kikundi cha kuweka na kukopa kina mkutano mkuu na kamati ya uendeshaji. Wajumbe wa kamati ya uendeshaji wanachaguliwa na mkutano mkuu. Wajumbe wa mkutano mkuu wanakura moja. Kamati ya uendeshaji ina wajumbe watano, mwenyekiti, mtunza kumbukumbu, mtunza sanduku na watu wawili wa kuhesabu fedha. Kila mzunguko mpya unapoanza kamati mpya ya uendeshaji inachanguliwa. Katiba: Kila kikundi kinatakiwa kiandike katiba yao inayowekwa sahihi na kila mwanachama. Katiba inakazi kuu mbili, kazi ya kwanza ni kutoa maelekezo ya namna ya kuendesha kikundi, kutatua migogoro ya kikundi na kueleza namna ya kuchukua hatua za kisheria kwa wanachama waliokwenda kinyume na utaratibu wa kikundi au kinyume na katiba. Kazi ya pili ya katiba ni kutoa kiwango cha hisa au fedha za kuweka kwenye kikundi, kiwango cha kuweka kwenye mfuko wa jamii na manufaa au faida za mfuko wa jamii. Kila mwanachama lazima ajue sheria moja au zaidi ambayo ataitamka wakati wa mkutano. Hii inafaida kubwa sana kwani baada ya miezi kadhaa kila mwanachama atajua sheria kutoka kichwani kwake. Kikundi kinakubariana muda wa mzunguko mmoja na kundikwa kwenye katiba. Mzunguko usiwe chini ya miezi sita na zaidi ya mwaka.

Mpango wa kuweka na kukopa: Wanachama wote wa kikundi cha kuweka na kukopa wataweka fedha zao kwenye kikundi kwa kununua hisa. Hii ndio kazi mhimu sana ya kikundi. Tofauti kati ya mwanachama mmoja na mwingine italeta kujiamini na maendeleo baina yao. Hisa zinazonunuliwa ni kati ya moja na tano, hisa zinanunuliwa wakati wa mkutano. Thamani ya hisa inapangwa na kikundi, inapangwa kwa kuzingatia uwezo wa wanachama, inatakiwa hata mwanachama asiyekuwa na uwezo aweze kununua wakati wa mkutano wa kikundi angalau hisa moja. Idadi ya hisa isipungue tano, pungufu ya hisa tano hazitauwezeshesha mfuko kukua na kutimiza malengo yake. Wakati wa kuanza mzunguko mpya wanachama wanaweza kukubaliana kuongeza au kupunguza thamani ya hisa. Kikundi kinaweza kuruhusu mwanachama anayeweza kuwa hana fedha wakati fulani kuacha kuweka fedha (kununua hisa). Kipindi fulani cha mwaka hali inaweza kuwa ngumu kumwezesha mwanachama kuweka fedha au mwanachama anaweza kuwa hana muda wa kuhudhuria mikutano. Pamoja na kuhakisha kunakuwa na nidhamu ya fedha na kunakuwa na ununuzi wa hisa wa mara kwa mara, ni ukweli kwamba vipato vijiji sio vya kudumu na haviaminiki. Pamoja na kwamba kikundi kitakuwa kimesimamisha ununuzi wa hisa au kuweka fedha waliokopa lazima waendelee kulipa mikopo yao na mikopo lazima iendelee kutolewa. Kikundi kinaweza kuruhusu uwekaji wa fedha wa kila siku kwa muda fulani. Wanachama wanaweza kuchangua mpango huu. Mpango huu unafanya uwekaji wa fedha kuwa rahisi, unaruhusu uwekaji wa fedha wa kila siku kwa kiasi kidogo cha fedha, hii itawafanya wanachama kutimiza kiasi cha fedha wanazotakiwa kuweka kila wiki. Mikopo inatolewa mara moja kila baada ya wiki nne. Wanachama wote wanayohaki ya kuchukua mikopo kutoka kwenye mfuko wa mikopo. Mfuko wa mikopo unatokana na fedha walizoweka wanachama kwa kununua hisa, ziada ya mikopo na faini. Kikundi kitapanga muda wa ulipaji mikopo ambao hautazidi miezi sita. Kwenye mzunguko wa kwanza isizidi miezi wiki kumi na mbili (miezi mitatu). Ukubwa wa mkopo unaopewa mwanachama usiwe zaidi ya mara tatu (3) ya hisa

alizonunua. Hii inasaidia wanachama wengi kuweza kupata mikopo na kuzuia uwezekano wa mwanachama kuzidiwa na mkopo. Kikundi kitapanga asilimia itayotozwa kama ziada ya mkopo. Asilimia inayotozwa kama ziada ya mkopo inaandikwa kwenye katiba. Ziada ya mkopo inatolewa kila baada ya wiki nne. Ziada ya mkopo itafanyiwa hesabu kwenye kiwango cha mkopo uliobakia kila wiki ya nne. Ziada ya mkopo lazima itolewe ukifika muda wake hata kama mkopo hautalipwa. Mkopo unalipwa kila wiki ya nne. Kipindi ambacho mkopo utalipwa kinakubaliwa wakati wa kuchukua mkopo. Mkopaji anaweza kulipa mkopo mapema ili ziada ya mkopo isiwe kubwa. Sehemu ya mkopo ikilipwa, kiasi cha mkopo kinachobakia kinakuwa mkopo mpya. Ziada ya mkopo itapigiwa hesabu kwenye kiasi cha mkopo uliobakia ambayo itadumu kwa wiki nne. Mfuko wa jamii: Kikundi kitaazisha mfuko wa jamii, kikundi kitaamua muda wa kuchangia na kiasi cha kuchangia kwa kila mwanachama. Mfuko huu unatoa msaada kwa sababu maalum ili kutatua matatizo ya dharura kama mazishi na gharama za mazishi na kusaidia watoto yatima. Mfuko huu sio lazima uwe mkubwa sana ila unatakiwa uwe na kiasi cha kuweza kusaidia wanachama wakati wanahitaji. Mtu yeyote anayehitaji msaada kutoka mfuko wa jamii anaomba kwenye mkutano mkuu na uamuzi utafanywa na mkutano mkuu na fedha zinaweza kutolewa hapo hapo. Mfuko wa jamii ni tofauti na mfuko wa mikopo. Mfuko wa jamii hautahusika wakati wa kugawana fedha zilizowekwa kwenye mfuko wa mikopo mwisho wa mzunguko. Kugawana hisa: Muda wa mzunguko ukifikia mwisho wanachama watagawana fedha walizoweka kwenye mfuko wa mkopo (isipokuwa mfuko wa jamii). Inapokaribia mwisho wa mzunguko mikopo mipya isitolewe na urejeshaji wa mikopo ufanyike. Fedha zote zilizopo mikononi zichanganywe na mfuko wa mikopo na kugawia wanachama kwa kadri ya kila mwanachama alivyoweka hisa. Baada ya kugawana wanachama wanaotaka kutoka watatoka na wanachama wapya wataingizwa. Kwenye mkutano wa kugawana hisa wanachama wanaoendela wanaweza kuamua kuweka kiasi kikubwa cha fedha kwenye mfuko wa mikopo kama hisa anzia ili ziwasaidi kuaza kutoa mikopo mapema. Kama wataamua kufanya hivyo kila mwanachama ataweka kiasi

walichokubaliana kwenye mkutano wa kwanza wa mzunguko unaoanza. Kiasi kinachowekwa sio lazima kilingane na thamani na kiwango cha hisa tano. Baada ya hisa anzia kurekodiwa kwenye vitabu, kiasi kitakacho wekwa kwenye mizunguko inayofuata kitakuwa hisa tano kwa thamani waliyokubaliana. Mzunguko unapoanza wanachama watakubaliana thamani ya hisa, thamani ya hisa haitabadilishwa wakati wa mzunguko. UUNDAJI WA KATIBA Katiba inaweka utaratibu utakao saidia kukiongaza kikundi cha kuweka na kukopa. Katiba itawasaidia wanachama kutatua migogoro ya ndani na nje ya kikundi. Wanachama wote lazima washiriki zoezi la uundaji wa katiba inayo kubaliwa. I. HABARI MAALUM JUU YA KIKUNDI Jina la kikundi Anwani: Tarehe ya kuundwa kikundi II. III. Tarehe rasmi ya usajili MADHUMUNI YA KIKUNDI Madhumuni ya kikundi, kwa mfano, kikundi uhuru cha kutoa huduma za kifedha kwa faida kwa wanachama Huduma zinazotolewa na kikundi kwa wanachama ili wafikie malengo haya: MAHUSIANO NA VYAZO VYA NJE VINAVYO TOA HUDUMA ZA FEDHA Kikundi kinaweza kupokea au kukopa pesa kutoka kwenye taasisi za fedha baada ya kumaliza mzunguko wa mwaka moja. Itikadi taratibu zifuatazo zifuatwe wakati wa chukua fedha za ruzuku au mkopo kwenye taasisi za fedha:. o Kikundi lazima kiwe mkopaji sio wanachama

o Kikundi hakitaruhusu taasisi inayotoa mkopo kuchunguza mikopo ya wanachama o Fedha zilizowekwa na wanachama zisitumike kama dhamana ya mkopo. Mkopo unaochukuliwa na kikundi usizi jumla ya his azote za wanachama. o Mwisho wa mzunguko mkopo wa fedha za mikopo au ruzuku zitatolewa alafu zoezi la wanachama kugawana fedha walizoweka litaendelea IV. NANI ANAWEZA KUWA MWANACHAMA WA KIKUNDI? Umri Makao/makazi Vitu vingine vya kuzingatia V. KAMATI YA UENDESHAJII VI. Mwenyekiti Mtunza kumbukumbu Mtunza sanduku Wahesabu fedha wawili TARATIBU ZA UCHAGUZI Idadi ya mihula mtu anayoweza kuongoza Uchaguzi lazima ufanyike mwanzo mwa kila mzunguko Idadi ya chini ya wanachama wanaotakiwa kuwepo wakati wa uchaguzi ni Uchaguzi utakuwa wa siri Idadi ya chini ya watu wanaogombea itakuwa in watu wawili katika kila cheo Mgombea katika uchaguzi katika cheo fulani lazima apendekezwa na mwanachama mwingine VII. KUTOLEWA KWA MAAFISA KWENYE VYEO VYAO KABLA YA UCHAGUZI. Mwanachama wa mkutano mkuu anaweza kuitisha kura ya kutokuwa na imani na mwanachama wa kamati ya uendeshaji. Kama idadi kubwa ya wanachama wanaamua kwamba huyo mtu atolewe kwenye kamati ya uendeshaji, mwanachama lazima ajiuzulu na mtu mwingine achaguliwe ili kuchukua nafasi hiyo.

VIII. MIKUTANO Mikutano ya kuhamashisha kuweka fedha itafanyika kila baada ya Kikundi kitatoa mikopo kila baada ya wiki nne (4) Mikutano katika mzunguko mmoja itafanyika kwa wiki 52 kabla ya kugawana fedha zilizowekwa na wanachama. IX. MWANACHAMA KUACHA KIKUNDI Kama mwanachama ataacha uanachama kwa sababu za msingi kikundi kitamlipa fedha zake kwa kutumia kanuni ifuatayo Kama mwanachama ataacha uanachama kabla ya kuisha mzunguko bila sababu ya msingi, kikundi kitamlipa kwa kutumia kanuni ifuatayo Kama kikundi kitamfukuza mwanachama kwa kushindwa kununua hisa/kuweka fedha, kikundi kitamlipa kwa kanuni ifuatayo: Kama mwanachama atafukuzwa kwa kushindwa kulipa mkopo, kikundi kitamlipa kwa kanuni ifuatayo: X. KUFUKUZWA KWENYE KIKUNDI XI. Sababu zitakazosababisha mtu kufukuzwa kutoka kwenye kikundi ni hizi: KIFO CHA MWANACHAMA Kama mwanachama akifariki, kikundi kitahesabu ni kiasi gani cha pesa kitakachopewa warithi wake kutumia kanuni ifuatayo: XII. FAINI Jedwali lifuatalo linaeleza kiwango cha faini kwa makosa atayofanya mwanachama.

Kosa Kutohudhuria mikutano kwa sababu ya kibinafsi isiyoidhinishwa na kikundi Kuchelewa kuhudhuria mikutano Kutokumbuka masharti ya kikundi Kupoteza kadi ya uanachama Kusahau funguo Kuvuruga mikutano Kudharau wanachama wengine Kutokumbuka maamuza na kazi zilizopangwa na mikutano iliyopita Kutowajibika mwanachama wa Kamati uendeshaji Kiasi XIII. KUBADILISHWA KWA KATIBA Theluthi mbili (2/3) ya wanachama lazima wakubaliane kubadilisha katiba Mtu yeyote anaweza pendekeza kubadilishwa kwa katiba SEHEMU YA 2: HUDUMA ZINAZOTOLEWA NA KIKUNDI I. KUWEKA FEDHA/KUNUNUA HUSA Wanachama wanaruhusiwa kununua hisa moja (1) hadi tano (5) katika kila mkutano Wanachama wanaweza changia kiwango ambacho wanakubaliana mwanzo wa kila mzunguko ili kukuza mfuko wa mikopo. Hii inawezakuwa zaidi ya hisa tano (5) kwa kila mwanachama kama wote watakubaliana. II. KUTOA MIKOPO Kiasi ambacho mwanachama anaweza kukopa ni Kiasi cha juu ambayo mtu anaweza kopa ni mara tatu ya thamani ya hisa zake Muda wa kulipa mkopo ni wiki ishirini na nne, kwenye mzunguko wa kwanza ni wiki kumi na mbili Mwanahama lazima alipe mkopo kabla hajachukua mwingine Ziada ya mkopo kwa wiki nne ni

Mwanachama akishindwa kulipa mkopo, utaratibu ufuatao utatumika Mikopo ambayo haitalipwa itajulika kama haiwezekani kulipwa baada ya muda ufuatao Mwanachama akifa mkopo wake hautalipwa Kipaumbele cha mikopo kitakuwa Kipaumbele cha pili cha mkopo kitakuwa: Kipaumbele cha tatu cha mkopo kitakuwa III. MFUKO WA JAMII : Kiasi cha kuchangia mfuko wa jamii kwa kila mkutano ni Kiasi cha fedha atakazopewa mwanachama baada ya kufiwa na mme au mke Kiasi cha fedha atakazo pewa akifiwa na mtoto Kiasi cha fedha atakazopewa akifiwa na mzazi Kiasi cha fedha atakazopewa nyumba yake ikiungua na moto au kuharibiwa kwa bahati mbaya ------------------------------------------------------------------------------ ------------------ Kiasi atakachopewa mwanachama ambaye mazao yake yameharibiwa na tembo, hata baada ya kutumia uzio wa pilipili Kiasi atakachopewa akiuguliwa na mwanafamilia ambaye ni mtegemezi wake itakuwa Muhimu: Kila kikundi kitatengeneza orodha ya matukio yanayoweza kulipwa na mfuko wa jamii ambayo wanachama wanaona ni mhimu zaidi. Kinachoonyeshwa hapa ni mifano ambayo inaweza kubadilishwa. Jina: Sahihi:

KUANZISHA MRADI WA KUJENGA UZIO WA PILIPILI VIJIJINI AMBAKO TEMBO WANAHARIBU MAZAO Mpango wa wakulima kutoka sehemu moja ambako wanatumia mbinu ya pilipili kwenda kwenda sehemu nyingine yenye matatizo ya tembo kuharibu mazao kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kufundisha namna ya kutumia uzio wa pilipili ili kupunguza uharibifu wa mazao, kuazisha vikundi vya kijamii vya kuzuia tembo kuharibu mazao (Community Based Organisation-CBO) pamoja na kuazisha mpango wa kuweka na kukopa kwenye CBO umeonyesha mafaniokio makubwa sana. Kwa miaka miwili sasa kuna timu za wakulima kumi (watano wanaume na watano wanawake) wa Mikumi na Tarangire zimekuwa zikitembelea na kufundisha wakulima sehemu ambazo tembo wanaharibu mazao na hawajui namna ya kuzuia tembo wasiharibu mazao. Wakulima wanafundisha namna ya kujenga uzio wa pilipili, uzio wa mfano unajengwa wakishirikia na wakulima, uzio utaangaliwa na wakulima waliofundishwa, ikiwa ni pamoja na kurudia pilipili na oili na kuimarisha uzio. Ufuatiliaji unaweza kufanyika ili kuazisha CBO na kuazisha mpango wa kuweka na kukopa kwenye CBO Kabla ya wakulima kutembeleana ni muhimu kutoa taarifa na kushirikisha taasisi zinazohisika na uhifadhi wa wanyamapori za Idara ya Wanyamapori, Hifadhi za Taifa, na Taasisi ya Utafiti ya Wanyamapori Tanzania, Halmashauri za wilaya, maafisa ugani ili washiriki wakati la wakulima wanafundishana