MATATIZO YA MATUMIZI YA LUGHA KATIKA VYOMBO VYA HABARI: MIFANO KUTOKA KENYA 1 KITULA KINGE'I. 1. Utangulizi. AAP 64 (2000): Swahili Forum VII 45-56

Similar documents
Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

Information for assessors (do not distribute this page to participants):

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Kiswahili, utandawazi na umoja wa Afrika

N09/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q

Usimulizi wa Riwaya ya Nyongo Mkalia Ini E. S. MOHOCHI University of Egerton, Kenya

DHANA NA MATKTIZO YA TAFSIRI:

Hati ya Kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya.( K.C.S.E)

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

ATHARI ZA KIMOFOFONOLOJIA ZA KIOLUSUBA KATIKA MATUMIZI YA KISWAHILI SANIFU KAMA LUGHA YA PILI

KUSHUKA KWA HADHI YA LUGHA ZA JAMII NCHINI TANZANIA YOHANA P. MSANJILA University of Dar es Salaam, Tanzania

Ufundishaji wa lugha nyingine

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

Human Rights Are Universal And Yet...

Haja Ya Dini. Author(s): Publisher(s): Translator(s): Category: Topic Tags: Featured Category: Published on Al-Islam.org (

UCHANGANUZI WA NOMINO-MKOPO ZA KIGIRYAMA KUTOKA KIINGEREZA NANCY JUMWA NGOWA

NAFASI YA MUZIKI ULIOPENDWA KATIKA FASIID YA KISWAHILI PAMELA M. Y NGUGI. Inkisiri. M a kala. AAP 64 (2000): Swahili Forum VII

CHUO KIKUU CHA NAIROBI

MATUMIZI YA LUGHA KATIKA KANISA KATOLIKI: UCHANGANUZI WA UBADILISHAJI MSIMBO KATIKA MAHUBIRI

KENYA NATIONAL EXAMINATION COUNCIL REVISION MOCK EXAMS 2016 TOP NATIONAL SCHOOLS

MTIHANI WA MWIGO WILAYA YA BUTERE MUMIAS-2007 Hati ya kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya

Azimio lililopitishwa na Mkutano Mkuu tarehe 18 Desemba 2013 [juu ya taarifa ya Kamati ya Tatu (A/68/456/Add.2)]

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

Mwongozo wa Utamaduni Toleo la Kwanza

K. M a r k s, F. E n g e l s

LUGHA YA KISWAHILI KATIKA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA ELIMU SHULE ZA SEKONDARI

VITENDO USEMI NA ULINGANIFU WA MAANA KATIKA TAFSIRI: MIFANO KUTOKA TAFSIRI ZA KAZI MBILI TEULE ZA BARBARA KIMENYE

MAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II

MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA. Kwa Wanaoanza

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO

Kutetea Haki za Binadamu

TASFIDA KAMA MKAKATI WA UPOLE: UWIANO WA TASFIDA ZA KISWAHILI NA EKEGUSII

ATHARI ZA KIISIMU ZA LAHAJA YA KIMAKUNDUCHI KATIKAKISWAHILI SANIFU KINACHOTUMIKA SHULENI MAKUNDUCHI ZANZIBAR

Hakimiliki na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa TAFSIRI YA BIBLIA. Mwandishi. Jonathan M. Menn

Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara)

Pronunciation: Mä-hret Zäläke Ndal-ka-tscho Molla Mare Gebre-gzabiär 1/12

Utangulizi wa ugonjwa wa shinikizo la damu

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig

Sera ya Faragha. Upeo. Aina za Data na Mbinu za Ukusanyaji

MAKALA: USHAIRI WA KISWAHILI KATIKA NJIA PANDA: KUTUMIA AU KUTOTUMIA METHALI

Elimukombozi, Lugha na Upashanaji Habari nchini Tanzania, katika Muktadha wa Utandawazi

MARUDIO K.C.S.E KNEC KISWAHILI KARATASI 102/2 MASWALI NA USAHIHISHO

V\ FANI KATIKA USHAIRI WA HASSAN MWALIMU MBEGA: UHAKIKI WA UPISHO WA UMALENGA NA DAFINA YA UMALENGA DONALD OMWOYO OSIEMO

NAFASI YA MWANAMKE: JINSI INAVYOTETEWA KATIKA NYIMBO ZA TAARAB ZA ZANZIBAR ELIZABETH KANGOGO YEGO C50/68796/2011 IDARA YA ISIMU NA LUGHA

MITAZAMO KUHUSU KISWAHILI MIONGONI MWA WAZUNGUMZAJI WA KIJALUO: KIFANI CHA SHULE ZA MSINGI KATIKA KAUNTI YA MIGORI. OWALA JAEL AKINYI C50/75493/2012

MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA PRO-ROUTES. Ombi kwa ajili ya fedha za umma wa mradi wa ziada

UCHANGANUZI LINGANISHI WA SINTAKSIA YA SENTENSI SHARTI YA KISWAHILI SANIFU NA EKEGUSII CHUO KIKUU CHA NAIROBI

Ufunguo wa Kutaalamika Haraka

FANI KATIKA NYIMBO TEULE ZA ANASTACIA MUKABWA MBURU JAMES MUNGAI TASNIFU HII IMETOLEWA ILI KUTOSHELEZA BAADHI YA

Mbinu za Ujenzi wa Wahusika na Usawiri wa Sifa Zao: Uhakiki wa Riwaya ya Dunia Uwanja Wa Fujo ya E. Kezilahabi

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

UFAHAMU NAME INDEX SCHOOLDATE UFAHAMU

JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1

Kimesanifiwa na:- E.D.Kissuu ECOMM TANZANIA S.L.P ,Dar es Salaam. Simu:

Na Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake Toleola4

MAPENDEKEZO YA MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA TANZANIA

Adhabu ya jino kwa jino na Musitakabali wa imani zetu

International Labour Office. Kazi za Ndani Zenye Madhara kwa Watoto: Kijitabu cha Maelezo Mafupi

Kiu Cha umtafuta Mungu

Shabaha ya Mazungumzo haya

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti

UJAGINA WA MWANAMKE KATIKA PANGO

Evaluation of Contextual Teaching of Kiswahili Proverbs in Secondary Schools in Kenya

MAP ISI YA KISW AHILI

JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI

UHUSIANO WA MIKAKATI YA UFUNDISHAJI WA FASIHI YA WATOTO YA KISWAHILI NA UMILISI WA KUSOMA KATIKA SHULE ZA MSINGI, KASARANI, KAUNTI YA NAIROBI, KENYA

TAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF) KUHUSU HAKI ZA WATOTO KATIKA KATIBA MPYA

Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2013

Hatari, Haki za Usalama katika Bahari 03

Kiinimacho cha mahali: kiambishi tamati cha mahali -ni. Ridder Samsom na Thilo C Schadeberg Chuo Kikuu cha Leiden

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara

Songa kwenye kilele cha upeo. Masuala ya Msingi na Ujuzi juu ya Uendeshaji wa Serikali za Mitaa

Nadharia za Uhakiki kama Mchakato wa Kutaalamisha Usomaji wa Fasihi

JAMHURI YA KENYA. Mkakati wa Ushirikiano MUKHTASARI FY Public Disclosure Authorized. Public Disclosure Authorized

Miradi na jamii. 3.1 Utangulizi

KIJARIDA JUU YA HAKI ZA RAIA KATIKA MFUMO JINAI

Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

(Hati ya kuhitimu kisomo cha sekondari Kenya (K.C.S.E)

ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA UCHUMI WA ZANZIBAR

KUCHUNGUZA MASUALA YA KISIASA KATIKA RIWAYA ZA SHAABAN ROBERT: MFANO WA KUSADIKIKA NA KUFIKIRIKA

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA

Kufafanua Upya Elimu Bora Tanzania: Kutoka Zana za Dufundishia mpaka Uwezo wa Wanafunzi 1 Oktoba 2007

Mukhtasari Wa Mabishano Kwa Na Dhidi Ya Vikombe Vingi Vya Ushirika

In the matter of Application by the TANGA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (TANGA UWASA) For a Multi-Year Tariff Adjustment

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

UFASIHI SIMULIZI KATIKA RIWAYA ZA SHAABAN ROBERT: Mifano kutoka Adili na Nduguze na Wasifu wa Siti Binti Saad. Khatib Khamis Saleh

Mazoezi yaliyofanyika wakati wa warsha kuhusu Elimu-Jumuishi kwa Vitendo. Zanzibar, 7-10 Februari 2006

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA III VI

Kilimo cha kiekolojia cha Wakulima Wadogo Hufanikisha Haki za Mazingira

TANZANIA MARKETS PAN Sera zinazoboresha masoko

SANIFU KWA SHULE ZA SEKONDARI KITABU CHA MWALIMU KIDATO CHA TANO

KUCHUNGUZA UJINSIA NA MATUMIZI YA LUGHA KATIKA METHALI ZA WAKURYA

Kitabu Cha Mafunzo Ya Uongozi Kwa Wanawake

Tora UTANGULIZI KWA TORA SOMO LA KWANZA

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

MADA MATUMIZI YA TAKRIRI NA SITIARI KATIKA UTENZI WA RASI LGHULI JUSTUS MAUNDU NDUMBU C50/65902/2011 CHUO KIKUU CHA NAIROBI IDARA YA ISIMU NA LUGHA

Transcription:

AAP 64 (2000): Swahili Forum VII 45-56 MATATIZO YA MATUMIZI YA LUGHA KATIKA VYOMBO VYA HABARI: MIFANO KUTOKA KENYA 1 KITULA KINGE'I 1. Utangulizi Mwandishi mawufu wa fasihi bwani Afiika, Chinua Achebe wnewahi kutoa maoni haya kuhusu matumizi ya 1ugha kama sanaa: "Imetwnbu1ikana tangu zamani kwamba 1ugha, kama ubunifu mwingine wowote wa wanadwnu, inaweza kutumiwa vibaya, inaweza kugeuzwa kutoka mahimizi yake ya asi1ia na kufaywa kitu kisicho na maana ua hata chenye madhwa (1975:17) (Tafsi1i yangu}. Kau1i hii ya Achebe inamaanisha kwwnba 1ugha inaweza kutumiwa kwa njia ya ubunifu wenye utasaha ufaao i1i kuwasi1iana au pia ikatumiwa visivyo na kwa njia potovu.. Ni nini hasa maana ya kuitumia 1ugha kwa njia potovu? Pengine ni rahisi kue1ezea kinynme chake. Mtumiaji wa 1ugha mwenye ubunifu huzingatia ras1mali zote za 1ugha. Y eye huitumia 1ugha kwna kitu ki1icho hai kinachokua na pia kuende1ea.. Katika juhudi za kuifanya 1ugha kumwezesha kutoa maoni, mae1ekezo, habwi na hisia, mtumiaji kwna huyu hutwnbua kuwa 1ugha ikitumiwa ipasavyo hu1eta uhai katika taaluma ya mawasi1iano (Luvai, 1991 :60) Hata hivyo, katika Kenya, kiwango cha ubora wa uandishi kwa jum1a kimeshuka sana katika miaka ishitini i1iyopita. Watafiti wanae1eza kwwnba "Kiwango cha 1ugha ya mazmjgumzo na maandishi kinaende1ea kuzorota ki1a mwaka Hati nyingi za nyw aka rasmi zinayo makosa yanayosababishwa na ujuzi duni wa 1ugha.. " (Senwnu na Williwns 1991: 5) (Tafsiti yangu}. Maka1a hii itachunguza kwa muhtaswi ushahidi wa matumizi yasiyofaa ya 1ugha ya Kiswahi1i katika vyombo vya habwi km. redio, te1evisheni na magazeti 1 Makala yaliyowasilishwa katika Kongomano La Kimataifa La Kiswahili, Fort Jesus, Mombasa, Oktoba 3-6, 2000.

46 KITULA KING'EI 2. Sajala ya uandishi wa habari Katika sajili zote, lugha ya Kiswahili inakua, kubadilika na kusambaa kwa kasi. Sehemu kubwa ya mabadiliko hayo huchochewa na maendeleo katika nyanja kama vile sayansi na teknol()jia.. Mabadiliko hayo huzua haja ya ukuzaji wa lugha ili kuiwezesha kuwasilisha dhana mpya katika maisha ya kila siku (Ohly 1987:1) Makala katika vyombo vya habari, hugubika nyanja tofimti: habari, tahariii, michezo, makala maalum, burudani, uchambuzi, ripoti, mahojiano, maoni, matangazo na nyanja nyinginezo.. Nyanja zote hizi huzingatia mitindo mbalimbali na pia mbinu tofauti za uteuzi wa lugha Kwa hivyo, tunaweza kusema kuwa vyombo vya habari vina mtindo wake au sajala yake maalum.. Kulingana na Crystal na Davy (1969), Sajala ya uandishi wa habari hasa uandishi wa magazeti, inazo si fa zifuatazo: ( 1) Sifa zisizohusiana na lugha, km. (a) Vichwa vikuu na vichwa vidogo (b) Uzito au uhafifu wa chapa (c) Mpangilio wa makala- (nafasi na mahali pa makala yenyewe).. (d) Uakifishaji (e) Mpangilio wa aya (f) Matumizi ya visitari (2) Muundo wa sentensi usio wa kawaida (km. aya ndefu iliyounganishwa kwa Visitari na viunganishi).. (3) Matumizi ya istilahi hila maelezo.. ( 4) Msisitizo (mtindo wa mazungumzo na mafumbo ).. (5) Maingiliano kati ya maelezo juu ya maudhui na maoni halisi au mwelekeo wa mwandishi binafsi (Crystal and Davy 1969:187).. 3. Mtazamo wa kinadhal'ia Wanaisiinu kadha wameshughulikia uwanja wa matumizi ya lugha katika mawasiliano.. Matumizi ya lugha katika misingi yake asilia na kwa kuambatana na mikabala au kunga za jamii husika huwa na majukumu yafuatayo, miongoni mwa mengine:

MATUMIZI YA LUGHA KATIKA VYOMBO VY A HABARI 47 (1) Kusuluhisha migogoro miongoni mwa hadhira (2) Kuelewesha hadhira mielekeo sadifu au asi dhidi ya lugha na jamii kwa jumla. (3) Kudumisha uwiano na mapatano katikajamii (Leech 1974:xii). Kulingana na Searle (1969, 1975) umuhimu wa tamko lolote katika mawasiliano hutegemea mwasilishaji, hadhira, mahali na wakati.. Isitoshe, katika nadharia yake, Austin (1962), umuhimu huo hutegemea uteuzi wa maneno, nia ya mwasilishi na athari ya maneno hayo kwa hathira yake. Lugha ya kimagazeti inayochambuliwa katika makala hii hutekeleza kazi mbalimbali kama vile: maelezo, ufimanishaji au (ulinganishi), usisitizaji, ukinzani (utatanishi) na kadhalika Katika makala hii, mbali na maana za aina tofimti kama uelezaji wa dhana moja kwa moja (udhahiri), maana husishi (km. mkora, mwaminifu, mfisadi, mcha Mungu mk.), hasa aina ya maana inayozingatiwa ni ile ya kimtindo, yaani kisajili au kirejista.. Uandishi wa habari ni uwanja maalum wa kimatumizi. Kwa hivyo, uborawa makala za habari hutegemea "ujuzi" wa mtindo wa mwandishi mhusika.. Hata hivyo, dhana hii ya ujuzi wa lugha ni tata. Kama alivyodokeza Whiteley (1974:5); katika kuchunguza viwango vya ubora wa matumizi ya Kiswahili, vigezo vifuatavyo sharti vizingatiwe miongoni mwa vingine: (I) U gumu wa kitambua kinachomaanishwa na dhana ya "kujua lugha".. (2) Tofimti katika viwango vya 11iuzi ambao watumiaji wa lugha wanadai kuwa nao.. (3) Ukweli kwamba watu 'huijua' lugha kwa sababu tofauti kutokana na sajala zao za kazi km. biashara, mazungumzo, michezo nk. ( 4) Vigezo kama vile mahali pa kuishi, jamii, kazi na hata jinsia vimethibitishwa kuchangia au kuathiri "ujuzi" wa lugha.. (5) Vishawishi vinavyowavutia watu kl\jifunza lugha: Kwa sasa mvuto upo kwenye lugha za kigeni dhidi ya Kiswahili.

48 KITULA KING'EI 4. Uchanganuzi wa matumizi ya lugha Lugha ya kimagazeti iliyofafanuliwa humu imedhihirisha kwamba matatizo mengi - hutokana na utohozi wa msamiati wa kigeni, uundaji wa msamiati usio sanifu, ujuzi duni wa sarufi na tafsiri. 4.1. Utohozi Utohozi wa msamiati wa kigeni, hasa wa Kiingereza, hufanyika kwa utaratibu unaotofautiana sana. Kwa mfano, maneno kama 'Kocha' (Coach) hurejelea tu mtaalam afunzaye kandanda wala sio bogi au hehewa la kubehea shehena au ahiria katika gari la moshi.. Katika Kiingereza, neno hilo lina maana zote mhili. Hata hivyo, haieleweki vyema kwa nini haadhi ya maneno ya Kiingereza hutumiwa vile vile katika magazeti ya Kiswahili hila kutoholewa au kutafsiriwa.. Mifano ni kama: D.0. (District Officer) D.C. (District Commissioner) P C (Provincial Commissioner) Spt. (Superintendent) Pengine urahisi wa matumizi hayo ni kwamha yana kumhukika hila shida.. Isitoshe, Kunayo mifano ya msamiati amhao hutumiwa sana magazetini kila mara ambao umezoeleka sana hata ingawa ni wa kigeni, na umetoholewa.. Kwa mfano, Rt. Rev (Right Reverend) padri (Padre) kadinali ( Car dinal) dayosisi (Diocese) basi (bus)!'oil (lorry) hospitali (hopital) masikwata (squatters) tr ekta (tr actor) gazeti (gazette) ripoti (report)

MATUMIZI YA LUGHA KATIKA VYOMBO VY A HABARI 49 picha n.k (pictwe) Katika uandishi wa habari za michezo, msarniati wa kigeni uliotoholewa hupatikana kwa wingi. Sababu kubwa ya matumizi haya ni kwamba asili ya michezo inayosimuliwa ni utarnaduni wa kigeni. Pili pia ni kwarnba waandishi wanawasiliana na hadhira maalum arnbayo inatarajiwa kuelewa mazingira ya lugha na utarnaduni wa yale yanayoelezwa. Kwa hivyo maneno ya kutoholewa hutumika kwa wingi: kwa mfimo: soka gofu quota fainali nusu fainali pointi penati goli ligi re fa rali mechi (soccer) (goaf) (quarter) (final) (semi-final) (point) (penalty) (goal) (league) (referee) (rally) (match) Mbali na utohozi, maneno mapya yanayobuniwa kutokana na maneno mengine yaliyofaharnika tayari yanazua utata fulani. Kwa mfimo: Neno jipyl! Neno Sanifu Muingilio Maingilio M;jengo Ujenzi Madharau dharau ~jengo Jengo Mishughuliko Shughuli Ufahari Fahari Upanzi Upandaji

50 KITULA KING'EI Utumizi Usaidizi Ufadhi Matumizi Msaada Fadhili Haifahamiki iwapo maneno mapya kama haya yanatokana na athari gani. dhahiri kwamba maneno haya yamekuwa sinonimia.. K wa sasa, ni 4.2. Msamiati Mbali ya makosa yanayosababishwa na athari za lugha za kwanza kwa waandishi wa habari ambao sio wazalia wa Kiswahili, kunayo mifimo ya matumizi yasiyofaa ambayo hutokana na kiwango duni cha ujuzi wa msamiati miongoni mwa waandishi hao. Uandishi wa habari hujumuisha nyanja au sajili kadha tofimti kama vile: ripoti, sheiia, dini, michezo, sayansi na matangazo ya biashara Hii ina maana kuwa mwandishi stadi wa habari sharti aweze kumudu ipasavyo msamiati unaostahili kutumika katika nyanja zote hizi iwapo atahitajika kuandika makala asilia, kuhariri au kutafsiri makala kama hayo katika sajala mojawapo.. Ifhatayo ni mifano michache ya makosa yailotokfu~a na matumizi ya msamiati usiofaa katik.a uandishi wa habari. Neno mwafaka zaidi limeonyeshwa katika mabano.. (I) Wito umetolewa kuwa sekta ya sukari inastahili kuangaliwa (kuchunguzwa}. (2) Abdalla ni mwana mziki astahiki (stadi, malllii) (3) Taifa letu limejawa na uchu wa pesa (tamaa) ( 4) Abiria wawili waliuawa katika ajali (walifariki) (5) Watu waliqjipatia nyumba za umma kwa njia bandia watapokonya nyumba hizo. (magendo, zisizo halali) (6) Wafungwa sita waliuawajana walipojaribu kuheoajela.. (kutoroka) (7) Kingora chajela kililizwa (kilipigwa) (8) Kulitokea mkanyagano wakati askari walipotokea. (vurumai, rabsha, kukuru kakar a, pata shika}. (9) Majeshi yamepeleka vifaa vyao vya vita nchini Oman.. (zana, silaha)

MATUMIZI YA LUGHA KATIKA VYOMBO VY A HABARI 51 (10) Mfalme tito anauguzwa figo.. (anaugua) (11) Shughuli ya kupiga kura itadumu kwa siku tatu.. (itaendelea; itachukua}. (12) Dawa hii huondoa upepo tumboni (hewa). (13) Kutakuwa na mkutano wa kikosi cha wanakamati wa kuchunguza sheria.. (halmashauri, tume }. (14) Mshitakiwa alihukumiwa baada ya kupatikana na hatia ya makosa mbali mbali.. (15) Viongozi wote walikubaliana kuafiki msimamo wa pamoja.. (yote ni sawa). (16) Raslmali zetu zimeanza kuchakaa (kuadimika). Baadhi ya makosa ya aina hii hutokea pia kwa sababu ya marudio ambayo yanahusu sinonimia (km. sentensi 15}. 4.3. Sarufi Ingawaje ujuzi wa sarufi ndio uti wa mgongo wa matumizi ya lugha (Waihiga 1991:1), matatizo kadha yanayohusu muundo wa lugha hutokea sana katika magazeti na vyombo vingine. Makosa kama hayo hutokea katika viwango mbali mbali kama vile.. (a) Matamshi na tahajia (km. r badala ya!, his, f/v nk) (b) Muundo wa maneno na uwiano (km.. watu kumi na mbili (wawili) (c) Mpangilio wa maneno katika ngeli (km.. habari hiilhizi) (d) Sentensi changamano zenye utata. (e) Usemi wa taarifa (km.. Waziri alisema atarudi wilayani.. Sahihi ni angerudi) (f) Semi na mafumbo Ubadilishaji wa mpangilio wa maneno katika sentensi hutokea sana. Kwa mfano, katika ya sentensi zifuatazo, kiima kimeundwa kutokana na kifungu cha maneno yanayoonyehsa "umilikaji " (1) Wizi wake ulimfungajela (2) Ulaji njama wao umemfukuza kazi

52 KJTULA KING'EI (3) Tamaa Yill!lm iliniponza Kutotumia ipasavyo viambishi cha kudhihitisha mahali yaani ni pia husababisha kutokea kwa makosa ya kisamfi kwa mfano, (1) Mbunge aliambiwa aondoke chama (badala ya chamani) (2) Je, ungetaka kuingia siasa? (badala ya siasani) 4.3.1. Matamshi na tahajia Kulingana na Mbaabu (1995) na King'ei na Musau (2000), matatizo ya aina hii husababishwa na athati za lugha za kimsingi, hasa makosa ya kimatamshi. Rata hivyo, matatizo ya kifonolojia hutokea kwa nadra sana katika vyombo vya habati. Mifimo ya makosa kama hayo ni yale yanayotokana na fonimu zifuatazo: r/1 rinda na linda n/nd ndoanadoa hi hili na hii mb/b mbali na bali f/v faana vaa k/g kokonagogo t/d tatanadada p/b paana baa sh!ch shoonachoo s/z saanazaa Kwa upande wa tahajia, aina za makosa ya kimaendelezo ambazo hutokea hudhihitisha athati za kimatamshi za waandishi wenyewe. Hii hapa mifano michache: Makosa chokoraa Riadha filimbi medeli fimakisha Sanifu chokora riyadha ritimbi medali fimikisha

MATUMIZI YA LUGHA KATIKA VYOMBO VY A HABARI 53 tikisha tikiza.. 4.3.2. Uwiano Uwiano wa majina na vitenzi huwatatiza baadhi ya waandishi wa habari Matatizo karna hayo hutokea katika uarnbishaji, urejeleaji na kadhalika. Mifano: (1) Mahakarna yalitupilia mbali kesi yake (5/6 au 9110)? (ilitupilia) (2) Mahakama kuujmearnuru kura zihesabiwe. (9/10) (3) Ghuba ~ uajemi au Ghuba la Uajemi. (Majina karna goli, K.labu na kocha huingizwa katika ngeli tofauti}. Wingi na Uchache Hali kadhalika dhana ya wingi na uchache husababisha makosa.. Waandishi kadha huchanganya dhana za wingi na kuzieleza kwa uchache. Km (1) Alieleza huzuni wake (112 badala ya 9) (2) Mvua!!llanyesha Nakuru (U2 badala ya 9/10) Majina kama hasira hutumika kwa wingi na pia uchache. Hata hivyo, majina karna taabu au pesa hukosewa yanapoelezwa kwa uchache.. Km Pesa chache Taabu chache Mvuachache Maumivu chache Maoni chache Uwezo mchache Faida chache 4.3.3. Tafsiri (badala ya kidogo) " " " " " " Makosa mengine ya tafsiii yanaweza kusababisha kupotoka sana kwa habari Hali hii hutokea pale arnbapo mwenye kutafsiii anakosa kuielewa dhana fulani katika lugha asilia. Kwa mfimo, kifungu: (1) "The leader of prosecution regarded the accused as a first offender.:

54 KITULA KING'EI kilitafsriwa kuwa: "Kiongozi wa mashitaka alimchukulia mshitakiwa kama mkosaji wa kwanza.." (Taifa Leo, Sept. 5, 2000:2) "first offender" linamaanisha mtu aliyevui1ja sheria mara ya kwanza sio mkosaji wa kwanza.. (2) "The woman was dressed in a skirt and a tight-top.. " Kilitafsiriwa: "Mwana.mke alikuwa amevaa sketi na kitopa cha kubana Neno kitopa halijasanifishwa wala halijulikani na watumiaji wa Kiswahili. Y amkini mwandishi alilitohoa ili kusadifu maana aliyoikusudia katika tafsiri yake.. Kwa kuzingatia mahitaji ya hadhira yake, mwandishi wa habari anala.zimika kubadilisha mtindo na hata uteuzi wa maneno na semi.. Kwa mfimo, katika tahariri na ripoti, lugha huwa sanifu na mtiririko wake huwa mkavu na rasmi. Hata hivyo, mwandishi anayewasiliana na hadhira ya vijana hutumia lugha yenye madoido mengi na wingi wa huchanganyaji wa ndimi. Mfano wa natumizi hayo unaonyesha kuwa sifa kuu za lugha hii huwa ni msamiati wa kukopwa kutoka kiingereza na usemi wa kitamathali..kadha. Mfimo: "Mrembo aliyedunga taiti na kitopa-mkato (tunk-top) aliponea tundu ya sindano kuvuliwa nguo ba.ada ya kupandisha manamba tempar echa (temperature) katika steji ya Mwembe Tayari. Kasheshe na hoi hoi ilizuka punde tu mrembo huyo alipopita katika steji inayopakia abiria wa kwenda Kaloleni, Mariakani na Voi." Kimaumbile, mrembo mwenyewe alikuwa katunukiwa "figa" (figure - eight) inayotatanisha wanawake wengi wanaotamani kuwa "Model" (Taifa Leo, kama hapo juu:3}. Mafunizi ya maneno na misemo ya aina hii mar a kwa mar a huishia kukubaliwa kama lugha sanifu lakini sharti yatumike kwa, hadhari na katika muktadha (Wamitila 1999: xi) Utata mwingine unaweza pia kusababishwa na matumizi ya vifungu virefu ambavyo hutinga uelewaji.. Matumizi ya viunganishi hurefusha sana kifungu k.m.

MATUMIZI YA LUGHA KATIKA VYOMBO VYA HABARI 55 Hitimisho "Msemaji wa kikundi cha Bw. Robert Mugabe cha Patriotic Front, kilichokuwa kikipigania ukombozi wa Rhodesia aliambia Barasa la Usalama la Umoja wa Mataifa jana kwamba, Uchaguzi mkuu utakaofanyika nchini humo kuanzia Februari 27 hadi 29 kwamba utakuwa wa haki iwapo wote wanaohusika katika usimamizi wake wataendesha shughuli zao hila woga, chuki au mapendeleo na hasa iwapo watazingatia maoni ya vyama vyote na wananchi kwa jumla ambao wana hamu ya kuwa na maongozi ya kidemokrasia baada ya kutawaliwa kimabavu kwa miaka mingi ya umwagikaji damu na mateso.. " (Taifa Leo, Feb. 2, 1980, uk.. 40) Waandishi wa habari wana wajibu mkubwa zaidi wa kuikuza na kuipanua lugha.. Wao ndio watarajiwao kuongeza msamiati, kuivuta lugha hivi na vile wakiinyoosha na kuiwamba kwa nia ya kuiendeleza na kuistawisha (Marshad 1993:ix) Ingawaje waandishi wanatarajiwa kutumia lugha sanifu, sharti ifahamike kuwa wao wana uhuru wa kiusanii kwa hivyo hawana budi kubuni na kuvyaza maneno na miundo mipya kila mara.. Hata hivyo, ubanifu hauwezi kuchukuliwa kama kisingizio cha kupuuza misingi yote ya lugha sanifu ingawa utaratibu wa usanifishaji hauna kikomo na daima unaendelea.. Licha ya uhaba na ugumu wa kupatikana kwa istilahi za nyanja ya waandishi wa habari, matumizi ya Kiswahili katika vyombo vya habari, katika sajala na viwango mbalimbali, "yanaendelea kushamiri licha ya mabadiliko na shida nyinginezo (Tumbo-Masabo na Mwansoko, 1992: 42). Makala hii imetalii kwa muhtasiri baadhi ya matatizo ya kimatumizi yanayodhihirika katika vyombo vya habari nchini Kenya Ukweli ni kwamba ingawa lugha ya Kiswahili haitumiki kwa wingi, hasa katika magazeti, vyombo kama redio na televisheni (runinga) vimepiga hatua kukuzaji, upanuzi na uendelezaji wa lugha hii Mfano mzuri wa juhudi hizi ni katika matumizi ya msamiati mpya kuelezea dhana mpya kama vile 'mtundao' (Internet). Marejeleo Achebe.. C. (1975).. Morning Yet on Creation Day.. London: Heinemann.. Austin, l. (1962).. How to Do Things with Words.. Cambridge: Cambridge University Press. Crystal, D. and Davy D.. (1969).. Investigating English Style.. London: Longman Giglioli, P.P. (1987).. Language and Social Context. Middlesex: Penguin Books

56 KITULA KING'EI Kingei, K. na Musau, (2000) P Utata wa Kiswahili Sanifo. Nairobi: Didaxis (Kitachapishwa hivi karibuni).. Leech, G. (1976). Semantics.. Middlesex: Penguin Books. Luvai, A. (1991) Poetry through a Popular Medium, in: Sanam, K. na Williams D. (1991). Mar shad, H. (1993) Kisw!J)!li au Kiingereza Nchini Kenya?. Nairobi: KKF.. Mbaabu, L (1995) Usahihishaji Makosa katika Kiswahili.. Nairobi: Longhom Kenya. Mdee, J. (1997).. Nadharia na Historia ya Leksikografia. Dares Salaam: TUKL Ohly, R. (1987).. Primary Technical Dictionary Swahili -English: Dar es Salaam: IPL Searle, J. (1969).. Speech Acts: An Essay in the Philosophy of Language. Cambridge: Cambridge University Press.. Senamo, K. na D. Williams (Wahariri) (1991).. Creative Use oflanguage in Kenya.. Nairobi: JKF. Ta..rnbo-Masabo na Mwa..11soko (1992)... l(iongozi cha Uundaji v;a lstilahi za.l(iswahili.. Dar es Salaam: TUKL Waihiga, G. (1999).. Sarufi Fafanuzi ya Kiswahili.. Nairobi: Longhom Publishers Wamitila, K (1999) Kamusiya Misemo Nahau: Nairobi: Longhom Publishers.. Whiteley WH. (mhariri) (1974). Language in Kenya: Nairobi: Oxford University Press.