JAZANDA YA NJOZI KATIKA BAADHI YA MASHAIRI YA EUPHRASE KEZILAHABI (ONEIRIC IMAGES IN EUPHRASE KEZILAHABI S SELECTED POEMS) 1

Similar documents
Hati ya kuhitimu kisomo Kenya (K.C.S.E)

MTIHANI WA MWIGO WILAYA YA BUTERE MUMIAS-2007 Hati ya kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya

Information for assessors (do not distribute this page to participants):

Ushindi ndani ya Kristo W. W. PRESCOTT

Agano Lililofunikwa Kwa Damu

MUNGU ANADHIHIRISHWA KUPITIA KWA YESU KRISTO.

Kifo Na Mbingu. (Death And Heaven) Ellis P. Forsman. Kifo Na Mbingu (Death And Heaven) 1

Roho Mtakatifu Ni Nini?

"ATATOKEA MARA YA PILI, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu." Waebrania 9:28.

Kiu Cha umtafuta Mungu

Theolojia Ujumla. Mike Taylor Semester Munguishi Bible College

Tora UTANGULIZI KWA TORA SOMO LA KWANZA

walozaliwa, si kwa damu, wala mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, mbali kwa Mungu. Sisi sio tena binadamu wa kawaida tu kwa sababu sisi ni w

Human Rights Are Universal And Yet...

Mafundisho Ya Msingi Wa Kikristo. Na Andrew Connally

Mutugi Kamundi. Jemma Kahn. Kiswahili. Demane na pacha wake. Author - South African Folktale

K. M a r k s, F. E n g e l s

BIBLICAL INSTRUCTION AND ENCOURAGEMENT FOR THE MAFUNDISHO YA BIBLIA NA HIMIZO KWA MISSION FIELD WORLDWIDE. KAZI YA KIMISHENI ULIMWENGUNI KOTE

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level

Ellen White, waasisi wa Kiadventista,na Sabato Lunar

Mukhtasari Wa Mabishano Kwa Na Dhidi Ya Vikombe Vingi Vya Ushirika

UTARATIBU WA KANISA. 2 Jambo la kwanza ninalotaka kusema ni kwamba mchungaji. 3 Sisi tunaamini katika Kanisa la kimitume, tukifundisha

Mbinu za Ujenzi wa Wahusika na Usawiri wa Sifa Zao: Uhakiki wa Riwaya ya Dunia Uwanja Wa Fujo ya E. Kezilahabi

Haja Ya Dini. Author(s): Publisher(s): Translator(s): Category: Topic Tags: Featured Category: Published on Al-Islam.org (

United Pentecostal Church June 2017

N09/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q

JE, YAWEZEKANA KUISHI BILA KUTENDA DHAMBI?

Ufunguo wa Kutaalamika Haraka

Ndugu na dada zangu wapendwa,

JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI

Hati ya Kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya.( K.C.S.E)

Kuzimu na Kurudi na Dr. Rawlings Documentary Video Transcript, TBN Films

MUNGU ALIUMBA ULIMWENGU 1 WETU NA VYOTE VILIVYO HAI

UJASIRI WA YOHANA MBATIZAJI

GRACE COMMUNION INTERNATIONAL KANUNI YA IMANI

Tafuteni Kwanza Ufalme Wa Mungu

usudi la Maisha Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na kupishana usiku na mchana, kuna kweli ishara kwa wenye akili, ambaye mkumbuke-

KWA NINI SISI SI MADHEHEBU?

Kifo Na Mbingu (Death And Heaven)

Adhabu ya jino kwa jino na Musitakabali wa imani zetu

Juni 3-9 Pata Manufaa Kamili kwakusomabiblia

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

MASWALI NA MAJIBU JUU YA KITABU CHA MWANZO

United Pentecostal Church April Kushangilia Kwa Sala

IMANI NA MATENDO ELLEN G. WHITE

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

UKUFUNZI WENYE NGUVU MMOJA-KWA-MMOJA

MSAMAHA NA UPATANISHO

WEWE NI NANI? Toleo X Toleo Ukweli wa Injeli Toleo 23

KUTAMBUA SIKU YA KO NA UJUMBE WAKE

KAMA MUNGU YU PAMOJA NASI, BASI YAKO WAPI MATENDO YAKE YA AJABU?

NAFASI YA MUZIKI ULIOPENDWA KATIKA FASIID YA KISWAHILI PAMELA M. Y NGUGI. Inkisiri. M a kala. AAP 64 (2000): Swahili Forum VII

MAKALA: USHAIRI WA KISWAHILI KATIKA NJIA PANDA: KUTUMIA AU KUTOTUMIA METHALI

Uponyaji Wa Laana. (Kumb. 28:1-14).

Mzabibu Na Matawi. (The Vine And The Branches) Ellis P. Forsman. Mzabibu Na Matawi (The Vine And The Branches) 1

Kiumbe Kipya Katika Kristo

2 LILE NENO LILILONENWA

Kuiponya Picha Tuliyonayo Kuhusu Mungu

Maisha Ya Mkristo Ni Nini?

# 18 Uponyaji Kutokana na Kukataliwa

Usimulizi wa Riwaya ya Nyongo Mkalia Ini E. S. MOHOCHI University of Egerton, Kenya

Mwongozo wa Utamaduni Toleo la Kwanza

Uongozi Siri Na Larry Chkoreff. Version 1.2 Desemba 2010

B. Wanafunzi watapata ufahamu mkubwa wa kitabu hiki, na jinsi kinavyofundisha kuhusu kanisa.

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

wasiofaa. Naomba sana kila raia afanye bidii awezavyo kumkaribia Mwenyezi Mungu vile anavyoona inafaa, lakini asipitishe hukumu juu ya wengine.

Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya Tanzania

Kanuni. Muhimu za Kujifunza Biblia. Mchungaji Drue Freeman. Dan Hawkins & Joseph Brown. General Editors.

JE! MUNGU ANAMPA MWANAMKE HAKI YA KUTOA MIMBA IWAPO NI MHANGA WA UBAKAJI?

WAFUNAJI WA NAFSI ABC By Vagn Rasmussen Translation by Lydia Madsen

VITAMBULISHO VITA NO DHA HIRI VYA KA NISA LA KWELI LA MUNGU ALIYE HAI

V\ FANI KATIKA USHAIRI WA HASSAN MWALIMU MBEGA: UHAKIKI WA UPISHO WA UMALENGA NA DAFINA YA UMALENGA DONALD OMWOYO OSIEMO

Rahisi. Mabingwa kwa ajili ya tunda la Roho Mtakatifu. Kitabu cha mwanafunzi. Rahisi

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC)

Kifaa Maalum cha Kutazamia Jua: Maelekezo ya kutumia

Tazama Yuaja. Kuhusu Toleo Hili. Umuhimu wa Mafundisho ya Biblia. Nguvu katika neno la Mungu.

Yaliyomo. Kuhusu kitabu hiki. Hautakuwa peke yako. Mfumo wa msaada ni wa manufaa sana wazazi wote wanahitaji!

MIAKA 500 YA MATENGENEZO YA KANISA NA USHUHUDA WETU Na Askofu Dr. Abednego Keshomshahara

Hatari, Haki za Usalama katika Bahari 03

Inavyodaiwa na wanaochanganya Biblia. Ellis Forsman. Inavyodaiwa na Wanao changanya Biblia (Alleged Bible Contradictions) 1

Oktoba-Desemba

Watumishi Wa Kristo. Ellis P. Forsman. Watumishi Wa Kristo (Servants Of Christ) 1

Aina Tatu Za Ibada. Ellis Forsman. Aina Tatu Za Ibada (Three Kinds Of worship) 1

YEHOVA-YIRE 1. 2 Baba yetu wa Mbinguni, tunakikaribia Kiti Chako cha. 3 Tunakushukuru kwa kutuzuru jana jioni. Tunaomba

UNABII WA HABARI ZA BIBLIA

Mwabudu Yehova, Mfalme wa Umilele. Miaka 100 ya Utawala wa Ufalme Inakuhusuje? UKURASA WA 12 NYIMBO: 97, 101. Kufanya Maamuzi ya Hekima Ukiwa Kijana

KUMBUKIZI YA MAREHEMU MWALIMU EDWIN SEMZABA

Maisha Yaliyojaa Maombi

RISALA FUPI YA KUMUWEZESHA MTU KUPAMBANUA NI IPI DINI YA HAKI MWANDISHI: SALEH M. KYAMBO

Deutsche Welle, Learning by Ear 2009 Seite 1 People Who Make A Difference Liberia: Anita Varney Health Facilitator, Fishtown/Liberia

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees

SANIFU KWA SHULE ZA SEKONDARI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Nia Dhidi Ya Kristo Je Unamheshimu?

2

UZAO WA NYOKA. 2 Basi, usiku huu, tuna malimbuko tu ya utukufu huo mkuu. 3 Kwa uchaji tunasimama kwa imani yetu katika Uwepo

KUCHUNGUZA MCHOMOZO KATIKA FASIHI YA KISWAHILI: UTAFITI LINGANISHI WA USHAIRI KATIKA DIWANI YA USTADHI ANDANENGA

KUCHUNGUZA UJINSIA NA MATUMIZI YA LUGHA KATIKA METHALI ZA WAKURYA

UFASIHI SIMULIZI KATIKA RIWAYA ZA SHAABAN ROBERT: Mifano kutoka Adili na Nduguze na Wasifu wa Siti Binti Saad. Khatib Khamis Saleh

maombi, kabla tu hatujalifungua Neno hili la Kiungu.

Transcription:

SWAHILI FORUM 11 (2004): 69-73 JAZANDA YA NJOZI KATIKA BAADHI YA MASHAIRI YA EUPHRASE KEZILAHABI (ONEIRIC IMAGES IN EUPHRASE KEZILAHABI S SELECTED POEMS) 1 GRAZIELLA ACQUAVIVA This article is based upon the following concept: Poetry is a chain of representation of the sub-conscience that is the creative source. We can read the poetic text in many ways, but if we imagine the text as the stage of images, we can understand the fundamental abstraction of the conscience. In this sense, oneiric images in some of Euphrase Kezilahabi s poems will be analysed by using insights from psychoanalytic theory. Euphrase Kezilahabi amejulikana sana katika fasihi ya Kiswahili ya siku hizi kama yule mshairi aliyetumia sana zaidi kuliko washairi wengine ushairi huru ulioleta mgogoro mkubwa katika miaka sabini na themanini. Katika diwani zake mbili zinazoitwa Kichomi (1974) 2 na Karibu Ndani (1988) 3 tunakuta maswala mbalimbali ya kijamii, ya kisiasa na ya kisaikolojia ambayo ni ya kawaida katika fasihi ya Kiafrika ya siku hizi, lakini mshairi huyu ni mtunzi wa pekee kwa jinsi yake ya kutumia sitiari na mafumbo. Njozi za ulimwengu zinazojitokeza katika ushairi wa Kezilahabi zinafanana sana na zile za mtu anayeweweseka akiwa usingizini. Njozi hizi ni kama maonyesho ya fujo ya kutoka ndani, na ukengeuko wa binadamu. Katika shairi la Wimbo wa Mlevi tunasoma: Kama Mungu angewauliza wanadamu Wanataka kuwa nani kabla ya kuzaliwa, Hilo ndilo lingekuwa swali gumu maishani. Na watu wangeishi kujutia uchaguzi wao. 1 Makala yalitolewa katika kongamano la kumi na saba la Kiswahili, Chuo Kikuu cha Bayreuth, tarehe 30 Mai hadi 1 June 2004. 2 Euphrase Kezilahabi. 1974. Kichomi. Nairobi Lusaka Ibadan: Heinemann. 3 Euphrase Kezilahabi. 1988. Karibu Ndani. Dar es Salaam: Dar es Salaam University Press.

GRAZIELLA ACQUAVIVA Wote wangetamani kuwa kinyume cha walivyo. Sijui nani angekuwa nani. Lakini mimi mlevi ningependa kuwa ye yote (Kezilahabi 1974: 64) Katika utafiti wake wa kishairi, Kezilahabi anayatazamatazama mazingira na mambo ya dunia, na tena kwa makini picha zake za malimwengu na ubinadamu zinaeleza, kwa upande mmoja, mambo yalivyo na, kwa upande mwingine, mambo yajitokezavyo ndotoni. Mshairi huyu anatuonyesha picha zake akitumia vitu, miti na mengineyo kama mambo yenye hisia, vile vile mambo haya yanapatikana katika fasihi ya simulizi. Mfano halisi ni Ngoma ya kimya: Lakini labda miti hii michache yakumbuka Nao upepo ukinifundisha lugha ya kimya (Kezilahabi 1988: 43) Jinsi hiyo ya kutunga ushairi inatuonyesha pia mtu-mshairi ambaye anajua vizuri mambo ya dunia na mahali anapokaa, lakini, wakati ule ule anaendelea kutafutatafuta Ego yake kwa busara kama katika shairi la Wanadamu Tunawajueni anapoandika: Mimi ni nguo ya ulimwengu Huvuliwa nikawekwa pembeni Mimi ni sabuni ya Ulimwengu Nimepapasa miili ya watu wengi Mimi ni chakula cha Ulimwengu Nimepapaswa na ndimi nyingi, nimeumwa. Nimekaa ndani ya matumbo kila aina Yaliyokwanyuka na pengine nilielea Mwenye bia pengine hukumbana na tegu. (Kezilahabi 1974: 61) Inawezekana kutambua ulinganifu fulani kati ya ushairi wa Kezilahabi na utafiti wa Ego ambao amefanya Carl Gustav Jung wakati alipokuwa akisikia upweke maishani mwake: yeye hakuwakimbilia watu wala dini, lakini aliangaliaangalia picha za kibinadamu zinazojitokeza katika njozi 70

JAZANDA YA NJOZI KATIKA MASHAIRI YA EUPHRASE KEZILAHABI zake. Kwa hiyo alianza safari yake ya kutoka ndani, kama inavyodhihirika katika wasifu wake Jung. Humu tunasoma: Kwa ajili ya kuelewa mazingaombwe yangu, nilijikuta mara nyingi kwenye mteremko mkali Ilikuwa kama safari ya kwenda mwezini, au nilikuwa kama nikiteremka hadi pangoni, ilikuwa inaonekana kama nipo ahera (Jaffé 1978: 223) Katika shairi la Kezilahabi linaloitwa Hii Moja Hadithi upweke unaomsumbua mshairi unarudi nyuma ukipita njia zote za roho yake kama ndotoni ambamo picha na kumbukumbu za maisha ya kibinadamu kama, kwa mfano, wakati wa kuzaliwa, zinachanganyika na picha za kifantasia: Ujana wangu ulianza kwenye ua waridi fumbo, Ukaishia kwenye gamba kandokando ya mto, Baada ya kisu kutokata kamba niloning inia. Nimepanda vilima na kushuka hadi pangoni, Nikaselea magofuni karibu na kisima cha uzima. (Kezilahabi 1988: 45) Maji yamekuwa kama kioo kinachotupa mambo mbalimbali ya Ego iliyobadilika, kama tunaweza kuona vile vile katika shairi la Mto wa Haki: Pole pole alianza kujiona mjinga kwa kuogopa Maji yaliyokuwa yakimtakasa mwenzake. Alisikia sauti ya haki na usawa wa binadamu: kwa mda wa dakika moja alielewa ukweli Ambao vitabu vyote vilikuwa vimeshindwa kumweleza. Alikuwa ameona kivuli chake majini. Unafanya nini? Sauti iliuliza. Hakuweza kujibu: mwili wake ulikuwa umeganda (Kezilahabi 1974: 17) Tena katika shairi hili, binadamu anaonekana kama mtu aliyeshikwa na mashurutisho ambayo hayaeleweki, hayaonekani au yale yaliyo dhahiri na yanayomhangaisha sana; binadamu huyo hayakimbii mashurutisho hayo kwa sababu anajua vizuri kwamba utakuja wakati ambapo kila binadamu lazima akabili haja ya kupata kujua Ego yake binafsi akizingatia kila kitu kinachotoka ndani yake. 71

GRAZIELLA ACQUAVIVA Katika Hii Moja Hadithi, kama alivyofanya Jung zamani, Kezilahabi pia anazungukazunguka njia zote za nafsi yake: Nimeuona ule mji wenye lugha ya kimya, Nao huo mto wa damu ilimopotea miswada. Nimeshuhudia pia utapikaji wa roho, Na jinsi zilivyopotea kwenye maji ya uzima. Nimeicheza usiku kucha ngoma ya vurumai. (Kezilahabi 1988: 45) Ndoto ina maana ya mawasiliano kati ya wakati wa kale na ule wa kisasa, pamoja na kuwa kama tamthiliya ya maisha halisi; ndoto inaweka jukwaani ovyo nyakati na kumbukumbu mbalimbali ambazo nje ya ndoto zingetambuliwa na binadamu kama ishara za fujo. Wakati ambapo Jung alisafiri mahali palipoitwa naye ahera, aliwakuta babu zake wa kiroho, mmoja wao alikuwa Filemone. Kezilahabi pia anasikiliza sauti ya babu yake inayotoka ndani yake mshairi kama tunavyoweza kusoma katika shairi la Nimechoka: Ninaendelea kuning inia kama picha iliyotundikwa Katika shamba la mawele, na mwenye shamba Huvuta waya kutoka nyumbani, itingishike kuwatisha ndege. Sauti ya baba inasema kwa msisitizo Najua utafika wakati itakulazimu kudondoka, Lakini endelea kushikilia hiyo waya Kama unazo nguvu bado, na usikate tamaa, Ila usitegemee kusifiwa au kusaidiwa, Vichwa vyote hivi vilidondoka kutoka umbali huo, Nawe kudondoka, utadondoka! (Kezilahabi 1974: 34; 35) Tukiyafikiria maisha ya kibinadamu kama yanayoyumba kati ya kuwako na kutokuwako, maisha hayo yanaonekana hayana nguvu. Njozi zinafaa tuelewe, kwa maana ya kisitiari, zile nguvu za Uwezo ule uliokuwa unaonyeshwa na Kifo na Wakati. Mambo haya yanaweza kufahamika kwa lugha maalum ambayo Erich Fromm (1900-1980), mwanasaikolojia wa Kijerumani, aliita lugha maalum iliyosahaulika, yaani lugha ya sitiari. 72

JAZANDA YA NJOZI KATIKA MASHAIRI YA EUPHRASE KEZILAHABI Katika lugha hii, inawezekana kuupata uhusiano kati ya neno na ndoto. Tena, ndoto ni kama ile daraja ambayo washairi na wenye kuota wanasafiri ili wafike mahala pasipo mwanzo wala mwisho. Kuhusu picha mbalimbali zinazojitokeza ndotoni, Hillman 1988 anazishughulikia zile za wanyama. Yeye anaeleza kwamba picha za hawa wanyama ndotoni zinafasiriwa kama maonyesho ya sehemu ya silika ya tabia ya kibinadamu. Maelezo haya yanatokea nadharia ya Darwin ijapo inaonekana kwamba Hillman (1988: 139-141) anapenda zaidi kuzifikiria picha za wanyama kama totem au kama mizimu inayotusaidia wakati ambapo tupo kizani. Katika Kisu Mkononi tunasoma: Mbele chui mweusi, nyuma mwanga Nionako kwa huzuni vifurushi maelfu vya dhambi. Sasa kama Simba-Mtu shauri nimekata. Ya nyuma sana nisijali, ya mbele sana niyakabili. Kwa ujasiri na uangalifu nitazunguka Nikifuata kamba kama ng ombe aliyefungwa, Kila mpigo wa moyo wangu Huu mpigo muziki wa maisha. (Kezilahabi 1974: 13) Kwa makala haya nimechagua mashairi machache lakini ya kutosha natumai - kwa kuelewa maana ya mabadiliko na maendeleo ya ile lugha maalum iliyosahauliwa: kama tunavyoweza kuona, kila ishara inapata kuwa picha ya kila fikra ambazo zinajificha katika ukweli wa maisha na Kezilahabi ana nguvu na ujasiri wa kuzifunua fikra zake, lakini lazima tuseme kwamba kila kitu kinawezekana kwa sitiari na kwa ushairi. Marejeo Cancrini, T. 1981. Psicoanalisi Uomo e Società. Roma: Editori Riuniti. Hillman, J. 1984 [1983]. Le storie que curano [Healing Fiction]. Milano: Cortina. Hillman, J. 1988 [1979]. Il sogno e il mondo infero [The Dream and the Underworld]. Milano: Il Saggiatore. Jaffé, A. (Ed.). 1978. Ricordi, sogni, riflessioni di C. G. Jung. Milano: Rizzoli. Kezilahabi, Euphrase. 1974. Kichomi. Nairobi Lusaka Ibadan: Heinemann. Kezilahabi, Euphrase. 1988. Karibu Ndani. Dar es Salaam: Dar es Salaam University Press. 73