ARCHDIOCESE OF MWANZA Bukumbi Girls Secondary School P.O.Box 561 MWANZA. Tel: No. 0756312183/0755280924/0767643605/0732981368 Email: bukumbigirlssec@gmail.com Website: www.bukumbigss.weebly.com YAH: MWONGOZO WA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO MWAKA 2017 Amani na Baraka ya Mungu viwe nawe. Mpendwa.Ninafurahi kukutaarifu kuwa umechaguliwa kujiunga na Kidato cha.. katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Bukumbi. HONGERA SANA! Unatakiwa kufika shuleni tarehe.. ili uanze masomo. Mwanafunzi atakayechelewa kufika shuleni zaidi ya wiki moja hatapokelewa. TAARIFA YA SHULE Sekondari ya Wasichana ni Shule ya Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza. Inaendeshwa na Masista Wabenediktine wa Mtakatifu Agnes. Shule hii iko katika Wilaya ya Misungwi umbali wa kilometa 34 kusini mwa Jiji la Mwanza karibu na Kanisa Katoliki la Bukumbi. Ni shule ya bweni kwa wasichana tu. Katika shule hii tunachukua wanafunzi ambao wamefaulu mtihani wetu NA WENYEE SIFA ZA KUJIUNGA NA Kidato cha Tano. MALEZI YETU ni katika MISINGI YA KIKRISTO (KIKATOLIKI) kama vile kusali pamoja kabla ya vipindi, Misa kwa wote siku zilizopangwa (yaani JUMATATU, JUMATANO, IJUMAA NA JUMAPILI) Mafungo na kadhalika. Mzazi/Mlezi ahakikishe kwamba kiambatanisho No. (i) na (ii) vinajazwa kikamilifu. DIRA YA SHULE Kwa Neema ya Mungu Baba, Munguu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu, wanafunzi wetu wakue kama watumishi wa kuwahudumia watu. 1. MWONGOZO WA KUJIUNGA NA SHULE Soma kwa makini sana mwongozo wa kujiungana shule hii na kama unakubali, tafadhali jaza fomu iliyoambatanishwaa na uje nayo. 2. USAFIRI KUFIKA SHULENI Kwa kutokea Kigongo Ferry unaweza kutembea kwa miguu mpaka shuleni. Kwa kutokea mjini Mwanza kuna magari ya daladala.haya magari husimama katika kituo cha mabasi cha BUHONGWA. 3. TAARIFA YA AFYA YAKO Unatakiwa kupeleka Medical History Sheet kwa Mganga wa Hospitali (isiwe zahanati) yoyote inayotambuliwa na serikali. Fika shuleni na Medical History Sheet hiyo ikiwa 1 Tarehe
imejazwa na kusainiwa na mganga aliyekupima. Uthibitisho wa mganga wa kienyeji au mganga yeyote asiyetambuliwa na serikali hautakubaliwa na itabidi upimwe katika Hospitali ya Bukumbi kwa gharama yako. Ni vema magonjwa ya kudumu, ulemavu ubainishwe na uongozi ukaelewa. Shule haitapokea malalamiko yoyote ya kiafya ambayo hayana uthibitisho wa Mganga anayetambuliwa na serikali (Tumia medical History Sheet iliyoambatanishwa nyuma). 4. SARE YA SHULE Shule hii ina sare za aina mbili ambazo hutumika kwa nyakati tofauti kama ifuatavyo i. Sare za darasani wakati wa masomo: Sketi mbili zitakazoshonwa hapa shuleni ili kuondoa utata wa rangi na mtindo wa mishono. Hivyo njoo na shilingi elfu kumi na nne (Tshs. 14,000/=) kwa ajili ya sketi mbili. Njoo na mashati (Blauzi) mawili meupe ya mikono mirefu ambayo hayabani na wala si mapana sana. Ni marufuku kujishonea sare za shule nje ya utaratibu huu. ii. Sare za nje ya darasa wakati usio wa masomo Njoo na shilingi elfu ishirini (20,000) kwa ajili ya gauni mbili kwa sare ya nje ya darasa. Nazo sawa kama sketi mbili katika No. 4 (i) zitashonwa hapa hapa shuleni. Pia njoo na shilingi elfu saba kwa ajili ya T-shirt ya shule (7,000). iii. Mavazi ya michezo a. Bukta zenye mipira miguuni na gauni fupi (rangi nyekundu) b. Raba za michezo jozi moja. iv. Viatu Njoo na viatu vyeusi vyenye visigino vifupi jozi mbili na soksi nyeupe ndefu jozi mbili. Ndala (kandambili) rangi yeyote jozi moja. v. Aje na shilingi elfu kumi na tano (15,000) za sweta. Ni marufuku kuvaa sweta au jaket tofauti na hilo litakalonunuliwa hapa. vi. Aje na underskirt 2 na shimizi 3 vii. Aje na nguo za ndani za kutosha 5. VIFAA VINGINE Unatakiwa uje na : i. Bakuli, sahani, kikombe na kijiko sio vya udongo ii. Ndoo 1 ya lita kumi itanunuliwa shuleni ( sh.3,500 ) na beseni 1 (sh.2,000) litanunuliwa hapa shuleni. iii. Galoni nyeupe ya plastiki ya lita tano iliyo na mfuniko iv. Mifagio ya chelea 2 kwa usafi wa nje. v. Faili 1 vi. Bunda mbili (2) za ream za karatasi za Photocopy A-4 moja kwa kila muhula vii. Tochi ya betri 2 au taa ya solar, na saa ya mkononi (aina yoyote) kwa ajili ya kutunza muda. 6. MATANDIKO i. Godoro la mpira ft 2½ ii. Mashuka 2 ya rangi ya blue bahari iii. Chandarua 1. 7. VIFAA VYA DARASANI 2
Uje na: i. Daftari kubwa Counter Books za kutosha kadiri ya Tahasusi aliyoichagua ii. Kalamu za risasi mbili au zaidi iii. Kamusi ya Kiingereza(Dictionary). iv. Rula ya sentimeta 30 au 50 v. Kalamu za wino bluu bic zisizopungua tano vi. Mkebe wa vifaa vya hesabu (mathematical set) vii. Aje na vitabu aina vinavyoendana na Tahasusi yake. viii. Aje na Scientific Calculator ( kwa wenye Tahasusi za Sayansi tu yaani CBG NA PCB) 8. KARO YA SHULE i. KARO YA SHULE NI SHILINGI 1,500,000(Milioni moja na laki tano ) tu kwa mwaka. MALIPO YOTE YAFANYIKE KWENYE AKAUNTI ZA SHULE NA SI PENGINEPO, NA UFIKE NA STAKABADHI (BANK PAY-IN-SLIP) ORIGINAL. UNAWEZA KULIPA ADA HIYO KWA AWAMU MBILI,TATU, AU ZOTE ( yaani Tsh.750,000, 500,000 na 1,500,000). ii. AKAUNTI ZA SHULE ZIPO KATIKA BENKI ZIFUATAZO: A. BENKI YA BIASHARA (NBC). TAWI LA NYERERE-MWANZA au sehemu yoyote yenye Tawi la NBC JINA LA AKAUNTI: BUKUMBI SEKONDARI AKAUNTI NAMBA; 015103004258. B. BENKI YA BIASHARA YA MKOMBOZI (MKOMBOZI COMMERCIAL BANK) TAWI LA MWANZA JINA LA AKAUNTI: BUKUMBI GIRLS SECONDARY SCHOOL NAMBA YA AKAUNTI: 00311401611001 Mkombozi Commercial Bank ipo katika jengo lililokuwa zamani Catholic Bookshop, Barabara ya Nyerere Mkabala na Benki ya CRDB iliyoko karibu na Benki Kuu ya Tanzania. Wazazi, walezi wanaoishi Mwanza na yeyote anayeweza kuifikia Benki hiyo kwa urahisi, kuanzia sasa alipie ada (karo) ya shule kwa kutumia AKAUNTI NAMBA iliyopo hapo juu (AKAUNTI NAMBA YA MKOMBOZI COMMERCIAL BANK) iii. Uje na shilingi elfu nne (Tshs. 4,000) kwa ajili ya kitambulisho na picha iv. Uje na tahadhari (caution money) shilingi elfu tano (Tsh. 5,000) v. Uje na sh. 3,000 kwa ajili ya Tai (Tie). vi. Unashauriwa uje na fedha kwa ajili ya matumizi yako binafsi, Ukipenda unaweza kutunzia fedha hiyo kwa Matron au kwa Mhasibu wa shule. vii. Uje na sh.15,000 za Taaluma viii. Uje na sh. 35,000/= za maabara (vifaa na kemikali ) kwa wanafunzi wanaosoma masomo ya Sayansi ix. Uje na sh. 10,000/= za matibabu. 9. MAWASILIANO Mzazi/mlezi atapata taarifa kuhusu mtoto wake kupitia UONGOZI WA SHULE NA SI VINGINEVYO. Ni marufuku mwanafunzi kuwa na simu ya mkononi hapa shuleni. 3
HUDUMA YA KIROHO WAKIWA HAPA SHULENI TANBIHI: Wanafunzi wote wakiwa hapa shuleni watasali katika Kanisa Katoliki ambalo lipo karibu na shule. 1. Kila kifaa kilichoagizwa ni muhimu. Hakikisha unakileta. 2. Mwanafunzi aletwe shuleni siku za kazi au Jumamosi na siyo Jumapili 3. Kutembelewa wanafunzi (visiting day) hakupo kabisa. 4. Ni marufuku kwa mwanafunzi yeyote kuleta au kuletewa aina yoyote ya chakula 5. Mwanafunzi anayejiunga na shule hii anatakiwa:- A. KITAALUMA Kuonyesha juhudi (bidii) katika masomo.elimu anayoipata imsaidie kujikwamua na adui ujinga, maradhi na umasikini. Mwanafunzi itabidi afaulu mitihani yake yote ya mihula miwili yaani mwezi wa Juni na Desemba kwa kiwango cha 50% ili kumruhusu kuendelea na darasa lingine. B: KIMAADILI Kukua katika maadili mema akifuata maelekezo ya walimu na walezi wake, na hatimaye kuwa raia mwema atakayefaa kuishi katika jumuiya yoyote na kujenga moyo wa kuwa tayari kutumikia na siyo kutumikiwa. 6. Mwanafunzi atakayekiuka sheria za shule ataondolewa shuleni mara moja. Tunaomba mzazi/ mlezi uwe na ushirikiano na uongozi wa shule hususani maendeleo ya mwanao kitaaluma na kinidhamu 7. Mwanafunzi yeyote atakayesimamishwa masomo kwa utovu wa NIDHAMU HATARUDISHIWA FEDHA YOYOTE ILE. 8. Mwanafunzi vile vile ataongozwa na sheria/kanuni za shule zilizotungwa kwa kuzingatia maelekezo ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kama zilivyoambatanishwa kwenye fomu hii. Nakutakia maandalizi mema na unakaribishwa sana kusoma katika Sekondari ya Wasichana Bukumbi.. Sr. Yovina F. Haule OSB Mkuu wa shule 4
5