Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara

Similar documents
Information for assessors (do not distribute this page to participants):

Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu

SERA & TARATIBU YA YALE NEW HAVEN HEALTH

KUHUSU AFRODAD. Dira ya AFRODAD. Dhamira ya AFRODAD. AFRODAD inalenga mchakato sawa na endelevu wa maendeleo kuelekea Afrika yenye mafanikio.

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Muhtasari Rakesh Rajani na George Omondi

Azimio lililopitishwa na Mkutano Mkuu tarehe 18 Desemba 2013 [juu ya taarifa ya Kamati ya Tatu (A/68/456/Add.2)]

Songa kwenye kilele cha upeo. Masuala ya Msingi na Ujuzi juu ya Uendeshaji wa Serikali za Mitaa

NGUZO KUMI ZA KILIMO KWANZA

Jifunze kusimamia pesa zako nchini Uskoti

Uzio wa pilipili unazuia tembo kuvamia mazao shambani! Jinsi ya kujenga na kudumisha uzio wa pilipili Tanzania

MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2017/18

Kimesanifiwa na:- E.D.Kissuu ECOMM TANZANIA S.L.P ,Dar es Salaam. Simu:

GOVERNMENT NOTICE No... PUBLISHED ON THE ELECTRICITY ACT, (CAP.131) ORDER. (Made under Section 23)

JAMHURI YA KENYA. Mkakati wa Ushirikiano MUKHTASARI FY Public Disclosure Authorized. Public Disclosure Authorized

MAKUBALIANO YA 2005 YA ULINZI NA UKUZAJI WA VIELELEZO VYA TAMADUNI ANUWAI

MKAKATI ATHARI YA MAZINGIRA NA KIJAMII YA KAZI YA PRO-ROUTES. Ombi kwa ajili ya fedha za umma wa mradi wa ziada

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

MWONGOZO WA UTUNGAJI WA SHERIA NDOGO NA USHIRIKI WA WANANCHI

Miradi na jamii. 3.1 Utangulizi

TAARIFA FUPI KUHUSU SERA YA TAIFA YA ELIMU

RIPOTI YA WARSHA KUHUSU HABARI KWA AJILI YA UWAJIBIKAJI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA. Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo. TOLEO Na.

Huduma kwa wateja kupitia barua pepe na ujumbe mfupi Fig

Ripoti ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA 2006/07

KAMATI ZA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI TANZANIA

Misamaha ya kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?

TANZANIA MARKETS PAN Sera zinazoboresha masoko

TAMKO LA JUKWAA LA HAKI ZA WATOTO (TCRF) KUHUSU HAKI ZA WATOTO KATIKA KATIBA MPYA

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA MHESHIMIWA DKT

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU

In the matter of an Application by the KIGOMA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (KUWASA) For a Tariff and Charges Adjustment

TANZANIA OSAKA ALUMNI. Kitabu cha Mbinu Bora

HAKI NA TARATIBU ZA AJIRA, KAZI NA HIFADHI YA JAMII

Programu ya Uendelezaji Mifumo ya Maji Vijijini (PUMMV) katika Tanzania. Modeli wa Ukodishaji Mradi

UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU VIKWAZO VYA KULINDA MAISHA KATIKA USAIDIZI WA KIMATAIFA WA AFYA KWA MSAADA WA KIMATAIFA UNAOFADHILIWA NA MAREKANI

Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame M. Mbarawa (Mb.); Waheshimiwa Mawaziri na Wabunge wote mliohudhuria;

Kutetea Haki za Binadamu

RIPOTI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI

In the matter of Application by the TANGA URBAN WATER SUPPLY AND SEWERAGE AUTHORITY (TANGA UWASA) For a Multi-Year Tariff Adjustment

Kubadili Sheria Za Mbegu Na Ulinzi Wa Aina Za Mbegu Na Mimea Nchini Tanzania

MAADHIMISHO YA MIAKA 15 YA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

KITEGO CHA MAREKEBISHO NA HAKI ZA MTOTO

Ripoti Fupi ya Nchi kuhusu Kazi Zenye Staha TANZANIA (bara)

Dibaji ya Mwenyekiti wa Kamati ya Pamoja ya Uongozi

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )

Kuuelewa Mchakato wa Bajeti Tanzania Mwongozo wa Asasi za Kiraia

TAFSIRI RAHISI YA MPANGO WA MAENDELEO YA AFYA YA MSINGI (MMAM)

MKAKATI WA PILI WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI ( )

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA FEDHA

JHSPH MAADILI YA KUFANYA UTAFITI WA MASUALA YA BINAADAMU MUONGOZO WA MAFUNZO YA UTAFITI

UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA)

Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali ya Madini Ukanda

TAARIFA YA MWAKA YA UTENDAJI KAZI IDARA YA UTAWALA BORA 2013/2014

TIST (TANGA) HABARI MOTO MOTO. Kutunza miche yako. Take care of your seedlings. Take care of your trees

JUA HAKI ZAKO, SEHEMU YA 1

Waandishi: wa Toleo la 5. Scholastica Jullu Athanasia A. Soka Safina Hassan Mary Njau. Toleo la 5: 2008 ISBN

HOTUBA YA WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU: KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU MHE

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA,KWA WANANCHI, 30 SEPTEMBA, 2001

Sera ya Faragha. Upeo. Aina za Data na Mbinu za Ukusanyaji

UFUATILIAJI WA MIRADI NA TATHMINI

Dodoma ambako kikao cha Bunge kinaendelea kuja kushiriki japo sehemu ya uzinduzi wa mkutano.

MAPENDEKEZO YA MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA TANZANIA

ORDER NO BACKGROUND

Na Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake Toleola4

UTANGULIZI ANUANI NA MANDHARI YA CHUO

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAASISI YA ELIMU TANZANIA MTAALA WA ELIMU YA MSINGI TANZANIA

UNIVERSITY OF CAMBRIDGE INTERNATIONAL EXAMINATIONS General Certificate of Education Ordinary Level. SWAHILI 3162/01 Paper 1 May/June 2013

Elimu Bora, lakini... C HakiElimu Elimu bora, lakini...

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

Human Rights Are Universal And Yet...

Kitabu Cha Mafunzo Ya Uongozi Kwa Wanawake

4. Kanuni za Petroli (Ushiriki wa Watanzania) za mwaka 2017 zilianza kutumika rasmi tarehe 5 Novermba Shughuli za Petroli za kwanza ni

Mwongozo wa Kutathimini mifumo ya Ugawanaji wa faida na Mapato Katika Miradi ya Jamii ya MKUHUMI

Uhakika wa Mbegu kwa Uhakika wa Chakula MWONGOZO WA UZALISHAJI WA MBEGU ZA ASILI ZA MAHINDI

Taarifa Kuhusu Hali ya Uchumi wa Tanzania

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

KUSHUKA KWA HADHI YA LUGHA ZA JAMII NCHINI TANZANIA YOHANA P. MSANJILA University of Dar es Salaam, Tanzania

HISTORIA, MAENDELEO NA MABADILIKO YA KATIBA TANZANIA TANGU UHURU HADI MIAKA HAMSINI YA UHURU 9 DESEMBA 2011.

Kijitabu cha Maelezo cha Programu ya Famasia

Elimu ya Msingi inaelekea Upande Sahihi? Kufikiri na Nyerere Rakesh Rajani

TANZANIA TAARIFA YA MWISHO WA UTEKELEZAJI

Deputy Minister for Finance

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI MTAALA WA ELIMUMSINGI DARASA LA I NA LA II

SautiElimu. Sauti Yako Isikike

Utumiaji Wa Kiswahili Na Lugha Za Jamii Kijinsia Nchini Tanzania Y.P. MSANJILA University of Dar-es-Salaam, Tanzania

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, MHESHIMIWA DKT. PHILIP I. MPANGO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO

3. Mheshimiwa Spika, 4. Mheshimiwa Spika,

KIMAZINGIRA NA KIJAMII NA MPANGO WA UDHIBITI

Ufundishaji wa lugha nyingine

Upande 1.0 Bajeti yako

Mipango ya miradi katika udugu

MATUMIZI YA FACEBOOK KWA BIASHARA. Kwa Wanaoanza

Unyanyasaji wa Watoto & Kutelekezwa

KUUNGANISHA VIZAZI KUPITIA RADIO MWONGOZO KUTOKA AFRIKA KWA WAANDAJI WA VIPINDI VYA RADIO WANAOFANYAKAZI NA WATOTO NA VIJANA

5. Mheshimiwa Spika, Bunge lako Tukufu lilijadili kwa kina Miswada ifuatayo:

TIST HABARI MOTO MOTO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Nilikua na Ndoto ya Kumaliza Shule Changamoto za Elimu ya Sekondari Tanzania

Draft 03 MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO MWENGE

Transcription:

Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara Umetayarishwa na Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania kwa Kushirikiana na Idara ya Maendeleo ya Ushirika - Septemba 2006

USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA Mwongozo kwa Lugha Rahisi wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sheria ya Vyama vya Ushirika Tanzania Bara Umetayarishwa na Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania kwa Kushirikiana na Idara ya Maendeleo ya Ushirika - Septemba 2006

YALIYOMO Dibaji......... ii Sera ya Maendeleo ya Ushirika 2002....... 1 Ushirika ni nini?...... 1 Kwa nini tunahitaji sera ya ushirika?...... 1 Serikali imedhamiria kukuza aina gani ya ushirika?...2 Ushirika na Maendeleo.... 3 Muundo wa ushirika.... 3 Nani watakaoongoza vyama vya Ushirika?.... 4 Elimu na Mafunzo ya Ushirika.... 5 Asasi za kiushirika za Fedha.... 6 Wajibu wa Serikali.... 7 Sheria ya Vyama vya Ushirika 2003 na Kanuni za Vyama vya Ushirika 2004... 8 Ni aina gani ya vyama vitakavyosajiliwa?...8 Chama cha msingi kitaanzishwaje?...... 9 Vyama vya Ushirika vya Msingi......... 10 Haki na Wajibu wa Mwanachama......... 14 Dhima za Wanachama...... 15 Usimamiaji wa Vyama vya Ushirika...... 16 Kazi za Vyama Vilivyosajiliwa...... 18 Shirikisho la Vyama vya UshirikaTanzania... 18 Taarifa zaidi na anwani muhimu...... 20 USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA i

DIBAJI Vyama vya Ushirika vimekuwa sehemu muhimu ya maendeleo ya Tanzania kwa miaka 75. Ni kweli kwamba vimepata mafanikio mengi na matatizo, katika kipindi chote hicho hakuna taasisi nyingine yoyote zaidi ya Ushirika iliyowaunganisha pamoja watu wengi katika azma na lengo linalofanana.. Baada ya Azimio la Arusha, vyama vya ushirika vilipewa kipaumbele katika kujenga moyo wa kujitegemea. Hata hivyo, kufuatia kuanzishwa kwa mfumo wa soko huru, vyama vya ushirika vimejitahidi kushindana na sekta binafsi na vingi havikuweza kuwapa wanachama wake huduma wanazozihitaji. Serikali imelishughulikia tatizo hili kwa kutunga Sera ya Maendeleo ya Ushirika (2002) ili kuvisaidia vyama vya ushirika kurudisha tena umuhimu wake katika maisha ya watu kiuchumi na kijamii. Sera inaeleza jinsi serikali inavyopanga kuwezesha maendeleo ya eneo maalum la uchumi kama vile kilimo, elimu au ushirika. Wakati ambapo sera zinatueleza mipango ya serikali ilivyo, sheria zinahitajika kuwezesha mipango hiyo kutekelezeka. Sheria zinaeleza jinsi ambavyo vyama kama vile vya ushirika vinavyopaswa kutenda katika njia ya kidemokrasia na ya kibiashara. Sheria: Zinataja haki na wajibu wa taasisi na watu binafsi. Zinaeleza mfumo wa utekelezaji wa maagizo. Zinaongoza mahakama katika kutekelezaji wake. Kwa hiyo, sheria zinawapa wadau haki na majukumu. Sera zinatoa tu mwongozo wa jinsi gani wadau wanavyoweza kuhusishwa. Kijitabu hiki kinaeleza hoja kuu za Sera ya Maendeleo ya Ushirika 1 na Sheria 2 na Kanuni 3 ambazo zimetungwa ili kuifanya sera hiyo itumike. Kimebuniwa kuzisaidia jumuiya kufanya maamuzi kuhusu maendeleo ya ushirika wao wenyewe. Aidha, kitawezesha jamii kuzungumza na wawakilishi wao waliowachagua kuhusu jinsi ambavyo serikali inapaswa kuzifanya sheria katika siku zijazo zitakazowasaidia kuwa na ushirika unaofanya kazi vizuri kwa wale wanaoamua kuwa wanachama. Wadau ni kina nani? Ni wale wote wenye nafasi katika sera, ikiwa ni pamoja na wale ambao: wanaathiriwa na sera wanatekeleza sera wanatoa fedha ili kusaidia sera 1 Sera ya Maendeleo ya Ushirika ya 2002 http://www.tzonline.org/pdf/cooperativedevelopmentpolicy.pdf 2 Sheria ya Vyama vya Ushirika 2003 http://www.parliament.go.tz/polis/pams/docs/20-2003.pdf 3 Kanuni za Chama cha Ushirika 2004 ii USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA

SERA YA MAENDELEO YA USHIRIKA Ushirika ni nini? Ushirika ni muungano wa watu ambao wanafanya kazi pamoja kwa hiari ili kufanikisha mahitaji yao ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni kupitia shughuli ya biashara inayomilikiwa kwa pamoja na kudhibitiwa kidemokrasia. Ushirika unazingatia maadili ya kujisaidia mwenyewe, jukumu binafsi, demokrasia, usawa na mshikamano. Wanachama wa ushirika wanaamini katika uaminifu, uwazi, uwajibikaji kwa jamii na kuwajali wengine. Kwa nini tunahitaji sera ya ushirika? Serikali na wadau wameamua kuunda sera na sheria mpya kwa ajili ya maendeleo ya ushirika kwa sababu: Vyama vingi vya ushirika havijafanikiwa katika uchumi wa soko huru. Matokeo yake vimeshindwa kutoa huduma za pembejeo, mikopo na masoko ya mazao kwa wanachama. Serikali inauona ushirika kuwa ni muhimu katika kufanikisha malengo ya maendeleo. Wachuuzi binafsi hawajaziba pengo lililoachwa na kuanguka kwa ushirika. Kwa hiyo, watu wanapaswa kuungana ili kutoa huduma kwa ajili ya jumuiya zao. Watu wanaofanya kazi pamoja wanaweza kutatua matatizo ambayo hayawezi kutatuliwa na mtu mmoja mmoja. Sera na Sheria za awali hazikushughulikia ipasavyo baadhi ya masuala ambayo ni muhimu kwa ushirika unaofanya kazi katika soko huru kama vile nafasi ya mwanawake katika Ushirika, kutunza mazingira na wajibu walionao wadau mbalimbali katika maendeleo ya ushirika. USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA 1

Serikali imedhamiria kukuza aina gani ya ushirika? Serikali inataka ushirika nchini Tanzania ufanye kazi kwa mujibu wa maadili yanayotumika katika nchi nyingi. Maadili hayo yanaitwa Kanuni za Kimataifa za Vyama vya Ushirika: Kanuni Uanachama wa Hiari na ulio wazi Wanachama na Udhibiti wa kidemokrasia Ushiriki wa wanachama katika shughuli za kiuchumi Uhuru na kujitegemea Maana Ushirika uko wazi kwa watu wote walio tayari kukubali majukumu ya uanachama bila ya aina yoyote ya ubaguzi. Wanachama wote wana haki sawa ya kupiga kura (mwanachama mmoja, kura moja). Wanachama wanachangia kwa usawa na kwa kidemokrasia wanadhibiti mtaji wa ushirika wao. Wanachama wanaweza kugawa ziada kwa moja au yote ya madhumuni yafuatayo: kuwekeza katika ushirika wao au kuwanufaisha wanachama kwa uwiano wa hisa zao katika ushirika. Vyama vya Ushirika ni vyombo huru na vinavyojitegemea chini ya uongozi na usimamizi wa wanachama. Endapo ushirika utafanya makubaliano na asasi nyingine, ikiwa ni pamoja na serikali, au kutafuta fedha nje ya ushirika, unafanya hivyo endapo tu wanachama wote wameamua kidemokrasia kuwa hivyo ndivyo wanavyotaka. Pia makubaliano yoyote lazima yahakikishe kuwa ushirika unabakia kuwa huru. Sheria na sheria ndogo za vyama vyote vya ushirika zifuate Kanuni za Kimataifa. Elimu, mafunzo na taarifa Ushirika unatoa elimu na mafunzo kwa wanachama wake na wafanyakazi ili waweze kusaidia maendeleo ya ushirika wao. naujulisha umma mzima kuhusu faida za ushirika. 2 USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA

Ushirika miongoni mwa Vyama vya Ushirika Ushirika kuijali Jamii Ushirika unaimarisha vyama vyote vya ushirika kwa kushirikiana kupitia mitandao ya wananchi, taifa, kanda na ya kimataifa. Ushirika unafanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya uchumi, jamii na utamaduni wa wanachama wake na jumuiya nzima. Pia unajali kutunza mazingira na vizazi vijavyo. Ushirika na Maendeleo Kwa miaka michache serikali ya Tanzania imekuwa ikitekeleza Mkakati wa Kupunguza Umaskini. Mchakato huu unatambua umuhimu wa asasi zinazowaunganisha pamoja watu maskini, kama ushirika. Kama sehemu ya programu ya kupunguza umaskini, serikali inataka kuwahamasisha watu kuunda ushirika ili kuboresha matarajio yao ya kiuchumi. Kuwahimiza watu kuunda Serikali ingependa kuona ushirika unapanuka aina tofauti za vyama vya katika sekta mbalimbali, kama vile fedha, ushirika, Serikali inaweza nyumba, viwanda, madini, mifugo, uvuvi, kutoa ushauri kwa watu ni ufugaji nyuki na usafirishaji. Ili watu wengi namna gani kila chama cha iwezekanavyo waweze kuhusishwa katika ushirika kinavyoweza chama cha ushirika, serikali: kuleta manufaa. Itahakikisha kwamba wanawake wanahamasishwa kuwa wanachama kamili wa ushirika. Itasaidia vikundi vyenye biashara ndogo ndogo vinavyohusisha vijana, wanawake, wahitimu wa vyuo wasio na ajira na walemavu kujiunga kwenye ushirika. Muundo wa Ushirika Katika kipindi kilichopita zimekuwepo na ngazi nyingi za ushirika nchini ikiwa ni pamoja na vyama vya msingi, vyama vikuu, vyama vikuu kilele na Shirikisho la Vyama vya Ushirika. Kwa nyakati tofauti vyama vikuu vimepoteza mawasiliano na vyama vyao vya msingi na vikaanza biashara ambazo hazikuhusiani na zile zilizokuwa zikifanywa na vyama vya msingi. Mpango uliopo sasa ni kukifanya chama cha msingi kuwa ngazi muhimu na ya msingi ya ushirika na kuhakikisha kuwa vyote vinajitegemea na vinadumu. Ushirika wa ngazi ya juu unawajibika kutoa ushauri na kujenga uwezo wa vyama vya msingi kibiashara. USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA 3

Aidha ushirika wa juu una jukumu la kuwa mwakilishi makini wa vyama vya msingi ngazi ya Taifa na Kimataifa katika kutetea haki, kutafuta masoko n.t. Kwa sasa Serikali ina mipango ifuatayo 4 : Kuhamasisha sekta mbalimbali za kiuchumi kuunda ushirika. Ushirika unapaswa Kusaidia vikundi vya biashara ndogo ndogo kuendeshwa kama biashara kusajiliwa katika ushirika. endapo utataka kudumu Kuhamasisha uanzishaji wa asasi za kifedha katika soko huria katika vyama vya Ushirika vya msingi. Kuwezesha vyama vya ushirika kujijengea uwezo wake wa fedha. Kusaidia vyama vya ushirika kupata mikopo kutoka benki. Kutoa udhamini kwa baadhi ya mikopo kutoka kwenye mabenki kwenda vyama vya ushirika. Kuhamasisha vyama vya msingi kuwa na biashara ya pamoja na vyama vingine vya msingi ili kuongeza ufanisi. Pia serikali kuendelea kutoa ushauri kuhusu baadhi ya vyama vya ushirika kuungana kila itakapoona inafaa. Serikali inatambua kuwa ushawishi mkubwa wa kisiasa katika kuendesha ushirika hapo zamani mara nyingi ulisababisha uendeshaji mbaya wa ushirika Nani watakaoongoza vyama vya Ushirika? Siku zilizopita vyama vingi vya msingi vilikuwa vikiongozwa vibaya kwa sababu: Baadhi ya viongozi walikuwa wakishika madaraka kwa muda mrefu sana. Hapakuwa na sheria za kuwabana viongozi kuwa watendaji wazuri na kufanya kazi kwa maslahi ya wanachama. Wanasiasa wameingilia mara kwa mara katika masuala ya vyama vya Ushirika. Kumbukumbu sahihi na taarifa za utendaji havikuwekwa na hesabu zilizokaguliwa hazikuwasilishwa katika Mkutano Mkuu wa Mwaka. Viongozi wamekuwa wakitoa maamuzi bila ya kuwahusisha wanachama katika Mkutano Mkuu wa Mwaka. Ili kuboresha hali hii serikali inataka kuhakikisha kuwa viongozi wa vyama vya Ushirika: Wanazo sifa za kufanya kazi za uongozi Watiifu kwa wanachama wa chama cha Ushirika Wanawajibika kwa wanachama wao kupitia uwasilishaji kwa bodi na mikutano mikuu ya mwaka wa taarifa za ukaguzi wa hesabu, makisio, mipango ya shughuli na taarifa za utendaji 4 Kupitia mabadiliko ya ushirika na mpango wa kufanya ushirika uwe wa kisasa (CRMP), mpango wa miaka kumi, ambao ulianza Januari 2005. 4 USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA

Wanachaguliwa kidemokrasia na wanachama Hawana maslahi ya nje ambayo yatakiathiri chama cha Ushirika. Ili kufanya hivyo, sera iliyopo inaainisha kwamba serikali ina mpango wa: Wafanyakazi lazima wawe na ujuzi unaofaa ili kuhakikisha ushirika una faida kwa wanachama. Kuunda kamati imara za usimamizi katika vyama vya Ushirika. Kuweka ukomo wa muda wa uongozi katika Vyama vya Ushirika Kuanzisha kanuni za maadili ili kuwafanya viongozi wawajibike kwa wanachama na kwa kamati. Pia serikali itahakikisha kuwa wafanyakazi ambao wanaajiriwa wanafanyakazi kwa uadilifu, uaminifu na uwajibikaji kwa wanachama. Kwa sababu hii, serikali itahamasisha ushirika kuwavutia wafanyakazi wenye sifa kwa kuweka mazingira mazuri ya kazi. Elimu na Mafunzo ya Ushirika Serikali inaamini kuwa ni muhimu kuwaelimisha watu katika maadili ya ushirika. Wakati soko huru lilipoanzishwa, mafunzo yasiyotosheleza yalitolewa kwa ushirika kuhusu namna ya kujiendesha katika mazingira mapya. Matokeo yake biashara ya Ushirika imeshuka kwa zaidi ya asilimia 50 Ushirika unashughulikia kiasi kidogo cha biashara ya wananchi ikilinganisha na hapo awali. USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA 5

Sera inasisitiza kusisitiza umuhimu wa ukuzaji wa elimu ya ushirika, ambayo italenga: Kuwa na viongozi wa ushirika walioelimika na wanaowajibika ambao wanaweza kudumisha maadili ya ushirika na kuendesha shughuli za biashara kwa ufanisi. Kuboresha usimamizi, biashara na ujuzi wa ujasiriamali wa wafanyakazi wa ushirika na wajumbe wa kamati. Kuhakikisha kuwa wanaushirika wanaarifiwa na kufahamu hali halisi ya shughuli za uchumi wa ushirika, kazi na majukumu yao na manufaa yanayotokana na uanachama wao katika ushirika. Kuuarifu umma kwa ujumla kuhusu hali halisi ya ushirika. Kuingizwa kwa Elimu ya Ushirika kwenye Mitaala na mfumo wa Elimu. Kuhakikisha kuwa ngazi zote za uongozi wa kiutawala wana hamasishwa kuhusu maadili na umuhimu wa ushirika. Asasi za Fedha za Ushirika Baada ya kuanzishwa kwa soko huru, Serikali ilipunguza kusaidia Vyama vya Ushirika moja kwa moja. Kwa kuwa ushirika haukuweza tena kupata fedha kutoka benki, ina maana ilikuwa vigumu kutoa huduma zinazofaa kwa wanachama. Wachuuzi binafsi waliweza kuchukua nafasi na kujinufaisha na hali hiyo, lakini matokeo yake yamekuwa ni huduma duni kwa wazalishaji wadogo. Serikali inazichukulia asasi za fedha za ushirika kama mbadala muhimu kwa mfumo wa uendeshaji benki kibiashara. Sababu ni kwamba ushirika unaweza kuhamasisha kuweka akiba na uangalifu katika kutumia fedha. Pia mikopo inaweza kutolewa kwa 6 USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA

wanachama kwa masharti nafuu kuliko ile itolewayo na benki za biashara. Asasi za kiushirika za fedha ni muhimu kwa sababu benki za biashara zinavichukulia vyama vya Ushirika kuwa havikopesheki. Mikopo inapaswa kupatikana kwa urahisi kwa wanachama wa SACCOs katika vipindi muhimu vya mwaka. Hivyo, Serikali inataka kuhamasisha uundaji wa asasi za fedha za ushirika kama vile: Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) Serikali inatambua kuwa kasi ya ukuaji wa SACCOS imekuwa ndogo, hususan katika maeneo ya vijijini. SACCOS nyingi zimeanzishwa mijini na maeneo ya kazi. Matokeo yake wanachama wa vyama vya msingi vijijini wameshindwa kupata mikopo. Mfumo wa zamani wa Serikali kujihusisha katika mambo yote ya uhai wa ushirika ulikuwa na gharama kubwa kwa nchi. Ili kuboresha hali hiyo, serikali inahamasisha uanzishaji wa SACCOS katika maeneo ya vijijini. Ushauri utatolewa katika ngazi ya chini kuhusu kuanzisha SACCOS na msaada wa kitaalamu pia utapatikana kwa SACCOS zote zilizopo ili ziweze kuboresha huduma zao na kuwa endelevu. Benki za Ushirika Uanzishaji wa benki za ushirika utakuwa ni sehemu muhimu ya uanzishaji wa asasi za fedha za ushirika zilizo imara. Serikali imeazimia kuhamasisha na kusaidia uanzishaji wa benki za Ushirika ili baadaye kuwa na benki ya Ushirika ya kitaifa iliyo imara. Katika ngazi ya Wilaya Ofisa Ushirika wa Wilaya atamuwakilisha Mrajis. Jukumu la Serikali Siku za nyuma serikali ilikuwa na jukumu kubwa katika ushirika. Ilijihusisha kwa kiasi kikubwa katika kutoa pembejeo, fedha na mafunzo. Kwa siku zijazo Serikali itawajibika katika uandaaji tu wa mazingira mazuri ya ushirika kustawi. Mihimili mikuu ya kukua itakuwa wanachama na menejimenti ya ushirika wenyewe. Lengo ni kuwezesha vyama vya ushirika kujenga uwezo wa kujitegemea kidemokrasia na kujimudu kiuchumi. USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA 7

SHERIA YA VYAMA VYA USHIRIKA Na. 20 YA 2003 NA KANUNI ZA VYAMA VYA USHIRIKA ZA 2004 Sheria na kanuni hizi zinaelezea jinsi ushirika unavyopaswa kuanzishwa na kuendeshwa nchini Tanzania. Zinakusudia kutekeleza kwa vitendo sera ambayo tumekuwa tunaizungumzia hapo juu.. Sheria ya Vyama vya Ushirika inaeleza kwamba ushirika unapaswa kuanzishwa na kuendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za Kimataifa za vyama vya Ushirika zilizotajwa mwanzoni mwa kijitabu hiki.( Ukurasa wa 2-3) Serikali na Waziri mwenye dhamana ya Ushirika wana wajibu wa kuunda sheria ambazo zinahamasisha uanzishwaji wa ushirika nchini. Aidha Rais kumteua Mrajis wa Vyama Vya Ushirika ambaye ndiye Afisa msimamizi wa utekelezaji wa Sheria na Kanuni zake. Kazi za Mrajis ni pamoja na: Kusajili, kuendeleza, kukagua na kuvishauri vyama vya ushirika. Kumshauri Waziri wakati vyama vya ushirika vinapohitaji msaada. Kuhamasisha uanzishaji wa vyama vya ushirika mbali mbali katika maeneo yote ya uchumi. Kwa sasa sera ya Serikali ni kuhamasisha ukuaji wa kujitegemea wa ushirika kwa kuwapa watu taarifa na ushauri ambao ni rahisi kuufuata na ambao unapatikana kwa urahisi. Kadri ushirika utakavyokua na kukomaa ndivyo ambavyo Mrajis wa Vyama Vya Ushirika atakamilisha majukumu yake (ya mafunzo, ushauri n.k.) kwa vyama vyenyewe, na kubakia na majukumu ya lazima ya usajili za usimamizi wa Sheria. Ni aina gani ya vyama vinavyoweza kusajiliwa? Kwa sababu serikali imepania kuhamasisha uanzishwaji wa ushirika katika sekta zote za uchumi, Mrajis anaweza kusajili ushirika katika maeneo kama vile: Kilimo, mifugo, uvuvi au ufugaji nyuki Uchimbaji madini Akiba na kukopa, Biashara ya jumla au rejareja miongoni mwa wanachama Viwanda Ushirika wa Nyumba unaojishughulisha na ujenzi, majengo na programu za nyumba kwa wanachama wao Ushirika wa ujuzi maalum n.k. 8 USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA

Chama cha msingi kitaanzishwaje? Chama cha msingi kinaweza kuanzishwa na: Watu 50 au zaidi kama ni chama cha kilimo Watu 20 au zaidi kama ni ushirika wa kuweka na kukopa Watu 10 au zaidi kama kinahusisha watu wenye ujuzi maalumu Watu 10 au zaidi kwa aina nyingine za Vyama vya ushirika Nani anaweza kuwa mwanachama? Umri wake haupungui miaka kumi na nane na mwenye akili timamu Yuko katika shughuli inayohusu chama cha msingi Ana mahitaji yanayofanana na ya wanachama wengine Anaweza kulipa ada na kununua hisa Hata hivyo Kijana mwenye umri Chama cha Ushirika cha Mwanzo ni asasi ya uchumi au kijamii inayoanzishwa kwa hiari na watu binafsi wenye maslahi sawa na kufanya kazi pamoja kama chama. usiopungua miaka 15 anaweza kuwa mwanachama na haki zote za kuwa kiongozi katika chama cha Ushirika cha shule. USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA 9

Vyama vya Ushirika vya awali, na jinsi ya kuanzisha Chama cha Ushirika kama huna wanachama wa kutosha Serikali itavitambua na kuvilea vikundi vya watu wenye muelekeo wa Ushirika hatimaye viwe vyama vya Ushirika kamili. Ili kuanzisha Ushirika lazima pawe na angalau watu watano. Ili kuweza kutambuliwa, kikundi kinatakiwa kwanza kuandika barua kwa Ofisa Ushirika wa Wilaya kuelezea nia yake na hivyo kuomba kutambuliwa. Mwombe msaada Ofisa Ushirika wa Wilaya wakati wa kukamilisha kazi hizo. Uandikishwaji wa chama utakuwaje? Wanachama wa Ushirika wa awali wapange kukutana chini ya uenyekiti wa afisa Ushirika wa wilaya ili kuchagua Bodi ya uundaji yenye Mwenyekiti na Katibu. Bodi ya uundaji itabidi ikamilishe majukumu yafuatayo: Kuamua ni aina gani ya chama kitakachoundwa Kutayarisha sheria ndogo za chama; Kutathmini kiwango cha shughuli cha wanachama waanzilishi Kutabiri chama kitakuwa na wanachama wangapi wa siku zijazo na viwango vya shughuli ambazo chama kitafanya Upembuzi yakinifu utajumuisha taarifa kuhusu idadi ya wanachama muhimu ambao chama kinaweza kuwa nao na viwango vyao vya biashara. Pia utazungumzia uwezo wa uongozi wa chama ili kuhakikisha chama kinapata faida na kuendeshwa kwa maslahi ya wanachama wote. 10 USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA

Kuandaa taarifa ya upembuzi yakinifu Kuandaa orodha ya wanachama waanzilishi na kurekodi mtaji wa hisa zao na michango Kuandaa orodha ya wanachama wanaotarajiwa na kurekodi mtaji wa hisa na michango wanayoweza kutoa Kuandaa mfumo mzuri wa utunzaji wa hesabu na nyaraka mbalimbali. Kuteua mwakilishi mfawidhi wa kuwakilisha kikundi katika mambo yote ya kiraia USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA 11

Sheria ndogo? Kila kikundi chenye mwelekeo wa Ushirika na chama cha Ushirika kinapaswa kuwa na masharti ili kuhakikisha kuwa vinaongozwa katika njia ambayo inawanufaisha wanachama wote kwa usawa. Masharti haya yanajulikana kama sheria ndogo. Aina mbalimbali za vyama zinaweza kutunga sheria ndogo ndogo za aina mbalimbali. Kwa mfano, chama cha ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) kitakuwa na sheria ndogo tofauti na za chama cha ushirika wa kilimo. Inaweza kuwa muhimu kupata msaada kutoka kwa Afisa Ushirika wa Wilaya au mtu mwingine mwenye sifa husika wakati wa kutengeneza sheria hizo ndogo. Kuna idadi ya sheria ndogo ambazo zinapaswa kutungwa na aina zote za vyama. Sheria hizo ndogondogo zitafafanua: Jina la chama na mahali pa kufanyia shughuli zake. Lengo la chama. Madhumuni ya kuomba fedha kwa ajili ya chama na jinsi fedha zitakavyotunzwa, kutumiwa au kuwekezwa. Kanuni za uanachama ikiwa ni pamoja na masharti ya kuingia, hisa na ada ya kuingilia. Kanuni kuhusu malipo, kama yapo, iwapo mwanachama atafukuzwa au kuacha. Hisa zitahamishiwa kwa nani endapo mwanachama atafariki. Kiwango cha madeni ya mwanachama katika kikundi na jinsi kitakavyoamuliwa. Jinsi mikutano mikuu itakavyoendeshwa na nini kitakachoamuliwa katika mikutano hiyo. Kanuni kuhusu kazi za wajumbe wa Bodi, jinsi watakavyochaguliwa, watakaa madarakani kwa muda gani na wataondolewaje kama itabidi kufanya hivyo. Kanuni kuhusu kazi za wajumbe wa Bodi, jinsi watakavyochaguliwa, watakaa katika nafasi hizo kwa muda gani na wataondolewaje kama itabidi kufanya hivyo. Kumwidhinisha ofisa kutia saini nyaraka kwa niaba ya chama. Vyama vya aina tofauti vitakuwa na masharti mengine tofauti. Kwa mfano, chama cha ushirika wa Akiba na Mikopo kitahitaji masharti ya ziada kuhusu viwango vya riba, masharti ya mikopo, dhamana ya mikopo na kanuni za kushindwa kulipa deni. Chama cha ushirika wa biashara kitahitaji sera ya kupanga bei kuongezea katika kanuni zilizopo. 12 USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA

Faini: Ni muhimu kutambua kwamba vyama vinaweza kuunda masharti ambayo yanaweza kumtoza faini mwanachama endapo atakiuka kanuni za chama. Faini hizo zitakuwa kama faini za kisheria kwa mujibu wa Sheria ya Ushirika na zinaweza kulipwa mahakamani kama ni lazima. Pindi wanachama wa kikundi chenye muelekeo wanapotaka kuwa chama cha ushirika cha awali watakamilisha taratibu zote za uanzishwaji wa chama, wanapaswa kutuma maombi kwa Mrajis au mwakilishi wake. Wawakilishi wa Mrajis ngazi ya mkoa (Mrajis Msaidizi) na ngazi ya Wilaya (Afisa Ushirika wa Wilaya). Ni kitu gani kinachohitajika kwa ajili ya Maombi ya usajili? Nakala iliyothibitishwa ya azimio lililopitishwa katika mkutano wa kwanza wa kikundi na Afisa Ushirika wa Wilaya Nakala nne za masharti za chama zilizopendekezwa Nakala nne za taarifa ya upembuzi yakinifu Hati nyingine zozote zitakazoombwa na Mrajis Ada ya Usajili Mrajis au Afisa Ushirika wa Wilaya pia wanaweza kuomba barua kutoka kwa watu wanaokusudia kujiunga, taarifa zaidi kuhusu kuwepo kwa mtaji au taarifa zaidi kuhusu uwezo wa chama kinachotarajiwa kusimamia biashara yake vizuri. Kama maombi yatakubaliwa Mrajis atatoa barua ya utambuzi. Barua hiyo inakiruhusu kikundi kufanya shughuli kwa miaka miwili kama chama kilichopo katika majaribio mpaka kitakapotimiza masharti yanayotakiwa ili kuwa chama kamili cha ushirika. Kama chama hakikutimiza masharti baada ya miaka miwili, kwa mfano hakikupata wanachama wa kutosha, basi barua hiyo itabatilishwa. Endapo Mrajis atakataa kusajili chama, wanachama wana haki ya kukata rufaa kupinga uamuzi huo kwa Waziri wa Ushirika na Masoko ndani ya siku 60. Uamuzi wa Waziri ni wa mwisho. USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA 13

Haki na Wajibu wa Wanachama Wanachama wote wa vyama vya ushirika mara wanapolipa kiingilio, hisa, na malipo mengine wanakuwa na haki zifuatazo: Majina na saini zao kuingizwa katika Daftari la Wanachama Kupiga kura na kupigiwa kura. Kila mwanachama ana kura moja bila ya kujali idadi ya hisa anazomiliki Kupewa hati za hisa mara tu wanapolipia hisa zao Kushiriki katika nafasi za uongozi Kuitisha mikutano kwa mujibu wa sheria ndogo Kuteua mrithi-kufuatana na masharti ya chama. Kupata taarifa kuhusu masuala yote ya chama na kuweza kukagua nyaraka za chama Kuarifiwa kuhusu masuala yote ya chama na kuweza kukagua nyaraka za chama Kupata kipato kutokana na shughuli za biashara ya chama Kushiriki katika kuandaa sheria ndogo za chama Kujitoa katika uanachama Kufanya uchunguzi katika masuala ya chama Kushiriki katika kuandaa na kurekebisha masharti ya chama Kukata rufaa Kwa vyama vya Akiba na Mikopo,mwanachama ana haki ya kulipa kwa kuzingatia mwanachama ana Akiba na amana za kutosha Tahadhari Ili kuhakikisha kuwa hakuna mwanachama hata mmoja anayekuwa na udhibiti mkubwa katika chama, ni kinyume cha sheria kwa mwanachama mmoja kumiliki zaidi ya moja ya tano ya hisa za chama. Kwa sababu kama hizo, ni kinyume cha sheria kwa kampuni iliyosajiliwa kuwa mwanachama wa chama cha ushirika mpaka Mrajis aandike barua inayoidhimisha kuwa kampuni hiyo itakuwa na manufaa kwa chama. Pia ni kinyume cha sheria kwa mtu kuwa mwanachama wa vyama viwili vinavyojihusisha na aina moja ya shughuli (katika eneo moja) kwa kuwa hali hiyo italeta mgongano wa kimaslahi. Wanachama wana Wajibu ufuatao: Kufuata masharti na taratibu za chama. Kulipia hisa zao, stahili na madeni mengine yoyote wanayodaiwa na chama Kushiriki katika shughuli za chama Kuhudhuria mikutano ya chama na kufuata maamuzi yaliyotolewa 14 USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA

Kuteua warithi wao Kulinda na kutetea mali ya chama Ukomo wa uanachama Mtu anaweza kukoma kuwa mwanachama wa chama endapo: Ataacha kumiliki hisa au kutoa michango iliyowekwa katika masharti ya chama. Atahama na kwenda mbali na eneo la chama Atafukuzwa au kusimamishwa baada ya kufanya kosa Kutunza na kulinda sifa na heshima ya chama Kifo Wanachama wote lazima wafahamu kuhusu biashara ya chama. Kushindwa kushiriki katika shughuli za kiuchumi za chama kufuatana na masharti ya chama Kurukwa akili Kuacha uanachama kwa hiari. Atakuwa hashiriki katika shughuli za chama. Dhima za wanachama Wanachama wanaweza kubeba dhamana ya madeni ya chama katika moja ya njia mbili: Dhima kwa hisa Hiki ni kiwango cha kawaida cha dhima na kinamaanisha kuwa mwanachama anawajibika kulingana na uwiano wa hisa zake za chama. USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA 15

Dhima kwa dhamana Kama masharti ya chama yanaruhusu, mwanachama anaweza kukubali kuwajibika kwa kiasi kikubwa kuliko hisa yake. Hii inajulikana kama dhima kwa dhamana. Usimamizi wa Vyama vya Ushirika Mikutano Mikuu Udhibiti wa jumla wa chama cha ushirika unafanywa na wanachama katika mikutano mikuu. Mikutano Mikuu inapaswa kufanywa angalau mara moja kwa mwaka. Masuala yote ya chama yanaweza kujadiliwa, yakiwemo; Uchaguzi, kusimamishwa au kuondolewa kwa Bodi Kuteua Mkaguzi wa Hesabu Kuzingatia na kuridhia hesabu zilizokaguliwa Kuamua kuhusu mgao wa ziada Kuamua kiasi cha posho itakayotolewa kwa wa wajumbe wa Bodi na maofisa wasiolipwa mishahara Kuzingatia bajeti na mipango ya kazi Kuzingatia marekebisho ya masharti ya chama Kuamua kuhusu ununuzi au uuzaji wa mali za chama Kubadili wajumbe wa Bodi mara kwa mara kunahakikisha kuwa hakuna mtu au kikundi kinachoweza kuwa na mamlaka zaidi katika chama. Angalizo Ili kutoa maamuzi katika mkutano lazima pawepo na angalau nusu ya wanachama, au wanachama 100, wowote walio wachache. Wanachama wote lazima wapewe notisi ya wiki tatu ya tarehe, mahali na muda wa mkutano. Bodi Kila chama cha ushirika ni lazima kichague Bodi ya wajumbe wasiopungua watano na wasiozidi tisa Ili kuhakikisha kuwa hakuna mwanachama au kikundi cha wanachama wanaojaribu kuwa na sauti zaidi katika kuendesha chama, hakuna mjumbe wa Bodi atakayeshika nafasi ya ujumbe kwa zaidi ya miaka tisa mfululizo Kwa kuongeza, Mrajis au mwakilishi wake, Ofisa Ushirika wa Wilaya, anapaswa kwanza kuwapima Viongozi na watendaji wote kabla ya kuwaajiri. Katika miaka ya kwanza ya chama, theluthi moja ya Wajumbe wa Bodi wanapaswa kubadilishwa kila baada ya miaka mitatu ili kuendana na sheria 16 USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA

Hakuna mwanachama atakayechaguliwa kwenye Bodi kama anamiliki, anasimamia au ana ushawishi katika biashara inayofanana na shughuli za chama Kila mwaka, kila mjumbe wa Bodi lazima ajaze fomu akitaja mali na biashara alizonazo, anazosimamia na lazima wakabidhi fomu hizo kwa Mrajis. Bodi inawajibika kuhakikisha kuwepo kwa uongozi mzuri wa chama kwa mujibu wa masharti ya chama. Ili kusaidia katika kazi hiyo Bodi inaweza kuajiri watu wanaofaa kusimamia uendeshaji wa kila siku wa chama. Kwa mujibu wa sheria, hakuna mtu atakayeajiriwa na ushirika kama hana elimu na ujuzi wa kufanya kazi iliyotangazwa. Kwa mfano, ni kinyume cha sheria kuwaajiri wafanyakazi kwa misingi ya uhusiano wao na mjumbe wa Bodi, rangi yao, kabila au utajiri wao. Pia ni kinyume cha sheria kwa mtu kutoa malipo ili kushawishi uamuzi wa kuajiriwa. Aidha, kila mfanyakazi wa chama cha msingi anapaswa kudhaminiwa na mdhamini. Mdhamini atawajibika endapo mfanyakazi atahusika na upoteaji au kushindwa kulipa deni. Mikutano Mikuu Maalumu Kama theluthi moja au zaidi ya wanachama wanataka kujadili jambo maalumu wanaweza kuitisha Mkutano Mkuu Maalum. Ili kufanya hivyo, wanachama husika wanapaswa kuandika barua inayoelezea dhamira yao na ni lazima watume nakala ya barua hiyo kwa Mrajis. Inatakiwa watoe notisi ya siku saba. Mrajis (au Afisa aliyemteua), ana mamlaka ya kuitisha Mkutano Mkuu Maalumu wa chama kama anaona ni lazima. Hii inaweza kutokea kufuatilia ukaguzi wa mambo ya chama. Katika mkutano huo Mrajis au Afisa aliyemteua ana mamlaka ya kuisimamisha Bodi iliyopo na kuweka Bodi ya muda kama itaonekana kuna ulazima wa kufanya hivyo. Anaweza pia kutoa amri ya kukivunja chama. USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA 17

Kazi za Vyama Vilivyosajiliwa Kuweka Kumbukumbu Vyama vyote vya ushirika vinapaswa kuweka kumbukumbu ambazo zinaweza kukaguliwa na wanachama na Mrajis au mwakilishi wake. Kumbukumbu hizo ni pamoja na: Orodha ya wanachama na hisa zao Maelezo ya hesabu za biashara zinazohitajika kwa wanachama zinazoonyeshwa kwa umma. Hesabu zilizoidhinishwa na Mkaguzi wa Hesabu aliyechaguliwa na Mkutano Mkuu na kuidhinishwa na Mrajis Nakala ya Sheria ya Ushirika 2003, Kanuni za Vyama vya Ushirika 2004 na masharti ya chama chenyewe Marekibisho ya Masharti ya Chama Marekebissho ya masharti ya chama ambayo yameidhinishwa na mkutano mkuu yanapaswa kupelekwa kwa Mrajis kwa ajili ya kuidhinishwa. Hilo linafanyika ili Msajili aweze kuhakikisha kuwa mabadiliko hayo ni kwa mujibu wa sheria. Taarifa ya Hesabu Kila chama cha ushirika kinapaswa kutunza taarifa sahihi za hesabu. Mkaguzi wa Hesabu aliyesajiliwa anapaswa kukagua hesabu hizo angalau mara moja kwa mwaka. Hesabu hizo zinapaswa kuidhinishwa na Mrajis na wanachama katika Mkutano Mkuu wao na baadaye kutumwa kwa Mrajis. Kama chama kitashindwa kutayarisha hesabu katika miezi mitatu ya mwisho ya mwaka wake wa fedha, Mrajis atakuwa na uhuru wa kuondoa Bodi ya Uongozi iliyopo madarakani na kuweka nyingine. Wajumbe wa Bodi wanaoondolewa kwa jinsi hiyo, hawawezi kuchaguliwa tena kwenye Bodi kwa miaka sita.. Endapo Mrajis anaona ni muhimu, anaweza kukagua akaunti za chama zilizopo benki au mahali popote na anaweza kutoa amri ya kukielekeza chama kuchukua hatua ya kurekebisha kasoro zozote zitakazoonekana. Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC) TFC ni nini? Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC) ni asasi mama ya ushirika kitaifa ambayo inakuza, kuhudumia na kuratibu maendeleo na ustawi wa vyama vyote vya ushirika Tanzania bara. TFC ni asasi isiyo ya Kiserikali inayojitegemea na isiyo ya kisiasa inayomilikiwa na wanachama na kusimamiwa kwa mtazamo wa kanuni na maadili ya ushirika yanayotambuliwa kimataifa. Ni mwanachama wa Muungano wa 18 USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA

Vyama vya Ushirika Duniani (ICA) na linashirikiana na mashirika mengine kadhaa ya kitaifa na kimataifa yenye muelekeo unaofanana. TFC lilisajiliwa tarehe 8 Desemba 1994 (Namba ya usajili 5503). Wanachama wa TFC ni nani? Wanachama wake wa sasa ni: Vyama vikuu vilele vya ushirika vinavyosimamia mazao ya pamba na tumbaku; Vyama vikuu maalum vinavosimamia Ushirika wa viwanda na Akiba na Mikopo nchini TICU na SCCULT 5 ; na Vyama vikuu vya Ushirika wa mazao vitano ambavyo ni Karagwe District Cooperative Union (KDCU), Kagera Cooperative Union (KCU), Tandahimba-Newala Cooperative Union (TANECU), Mtwara-Masasi Cooperative Union (MAMCU) na Kilimanjaro Native Cooperative Union (KNCU). Uanachama wa Shirikisho ni wazi kwa Vyama vyote vya Ushirika kuanzia ngazi ya Msingi mpaka Ngazi ya Vyama vikuu vilele ili mradi chama hicho si mwana chama wa chama kingine ngazi ya kati. Mfumo mzima wa TFC unafanyiwa rejea ili kubaini maeneo muafaka ya kufanyia maboresho kwa manufaa na maendeleo ya wanachama. Uanachama wa jumla wa TFC unajumuisha Vyama vya msingi 5,700 vyenye wanachama binafsi zaidi ya 700,000. Maarubu ya TFC Shirikisho litajitahidi kuwa asasi mama ya ushirika ya taifa yenye uhai ambapo aina zote za ushirika zitaunganishwa katika kuvutia na kuhamisha maadili ya ujasiriamali na utawala bora. Madhumuni yake ni kuimarisha uendelevu wa ushirika ili wanachama wafaidike moja kwa moja kutokana na kupambana kwao dhidi ya umaskini kupitia ushirikishwaji kiuchumi katika ujenzi wa uchumi. 5 TICU Tanzania Industrial Cooperative Union Ltd; and SCCULT Savings and Credit Cooperative Union League of Tanzania. USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA 19

Malengo ya TFC Malengo yake ni kujenga msingi imara wa ushirika kwa: Kuwezesha na kuratibu uanzishwaji, maendeleo na ukuaji wa ushirika endelevu na wa kidemokrasia; Kufanya utafiti na kutoa huduma za ushauri kwa vyama vya ushirika wanachama katika maeneo ya masoko, biashara, fedha, bidhaa na huduma mpya; Kukusanya takwimu na taarifa kuhusu hali ya ushirika, masoko na bei na kuvisambaza kwa wanachama; Kuanzisha elimu shirikishi ya ushirika na programu za mafunzo miongoni mwa wanachama wake; na Kutangaza na kuhamasisha kuhusu aina zote za shughuli za ushirika nchini. Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi: SHIRIKISHO LA VYAMA VYA USHIRIKA TANZANIA Ghorofa ya 9, Ushirika Building, Barabara ya Lumumba, S.L.P 2567, Dar es Salaam. Simu: 255 (0) 22 218 4081 5 Faksi: 255 (0) 22 2184081 Baruapepe: ushirika@ushirika.co.tz 20 USHIRIKA NA MAENDELEO TANZANIA

SHIRIKISHO LA VYAMA VYA USHIRIKA TANZANIA LINGEPENDA KUPATA MAONI YAKO KUHUSU KIJITABU HIKI. TAFADHALI ANDIKA KWA: Katibu Mtendaji, Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania, Ghorofa ya 9, Jengo la Ushirika Mtaa wa Lumumba S.L.P. 2567 Dar es Salaam Simu: 255 (0) 22 218 4081 5 Nukushi: 255 (0) 22 2184081 Barua pepe: ushirika@ushirika.co.tz Tovuti: www.ushirika.coop TAARIFA ZAIDI Kwa taarifa zaidi kuhusu sheria, kanuni na taratibu zinazoongoza vyama vya ushirika kuna nyaraka kuu tatu za kusoma: Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 20 ya 2003 Kanuni za Vyama vya Ushirika 2004 Sera ya Maendeleo ya Ushirika 2002 Inawezekana kupata nyaraka hizi kutoka kwa: Ofisa Ushirika wa Wilaya wako; - Mrajis Msaidizi wa Mkoa wako; - Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (anwani ya hapo juu); au Mrajis wa Vyama Vya Ushirika, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, S.L.P. 201, Dodoma.